IMEANDIKWA NA : MOONBOY
*********************************************************************************
Chombezo : Mtoto Wa Hayati
Sehemu Ya Kwanza (1)
SIMULIZI HII INAMHUSU KIJANA MMOJA AMBAE ALIISHI NA WAZAZI WAKE KATIKA MAISHA MAZURI NA YENYE FURAHA, LAKINI KADRI MAISHA YANAVYOZIDI KWENDA, NA WAZAZI WAKE NA HUPOTEZA MAISHA KAMA KAWAIDA, WAZAZI WALIACHA MALI NYINGI KWA AJILI YA MTOTO WAO HUYO MMOJA TU KAMA WA DAWA, LAKINI KUMBE NDUGU WA FAMILIA HIO HAWAKUA WAKIHITAJI UWEPO WA FAMILIA ILE IKIENDELEA KUISHI KWA FURAHA NA UPENDO, MTOTO YULE ALIZURUMIWA MALI ZILE NA NDUGU WA MAMA YAKE, YAANI BABA AU MAMA WADOGO WA UPANDE WA MAMA YAKE, MTOTO ALIISHI KWA SHIDA NA TABU KATIKA NYUMBA HIO, HUKU AKIWA KAMA MFANYAKAZI KATIKO NYUMBA HIO, NA MWISHO WA SIKU WALIAMUA KUMFUKUZA MTOTO YULE......
JE UNAJUA NINI KILIENDELEA BAADA YA KUFUKUZWA?..... USIKOSE HATA KIPANDE KIMOJA CHA SIMULIZI HIII.... ILA KAMA UNA ROHO NYEPESI USIISOME MAANA INASIKITISHA SANA,
TWENDE KAZI, NA HAPA NDIPO INAPOANZIA RASMI SIMULIZI HIII
Ikiwa ni mwaka 1999 nikiwa mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne, maana nilizaliwa mwaka 1995, Nilikua nikitoka shule ya vidudu, almaarufu kama NURSARY SCHOOL, wazazi wangu walikua wakinipenda sana tena kwa uzuri ni kwamba nilikua nao wote, maisha kwetu yalikua ni mazuri kiasi kwamba baba alikua ana mkoko wake wa kutembelea, huku mama akifanya biashara ya kuuza nguo katika duka lake lililopo maeneo ya stendi jijini arusha, Kama kawaida mama yangu aliitwa MWAJABU na baba yangu aliitwa RASHIDY na mimi mwenyewe niliitwa SHARBINY au ukipenda niite SHEBY,..... Unaweza kujiuliza sana kwanini napenda kuyatumia hayo majina, ni kwasababu hayo ni majina ya wazazi wangu kabisa, yaani mbali na story zangu, basi hayo ni majina yao na sio ya kutungwa, na hilo jina la sharbiny ni lakwangu kabisa mimi muandishi wa simulizi hizi, hivyo usishangae kila story kuyasoma majina hayo, maana ni majina asilia na ya kweli kabisa......
Siku zilizidi kwenda na hatmae ni miaka mingi imepita mpaka nimemaliza shule ya msingi na sasa ndio naingia kuanza elimu yangu ya secondary kidato cha kwanza katika shule za international, maana wazazi wangu walijiweza kunilipia, maana baba yangu alikua akifanya kazi katika kampuni za kusafirisha wazungu, iitwayo LEOPARD COMPANY LTD ARUSHA kwahio kiukweli maisha yalikua sio mabaya sana,
"sheby?"
"yes dady"
"coming"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliitwa na baba yangu sebureni, na baba yangu alikua akiangalia mpira kwenye tv ilio kubwaa ya inchi 40,.... Kipindi hicho nilikua nina umri wa miaka kumi na nne (14), nilikua ni mtu mzima japo nilikua bado sijakomaa kiutu uzima, yaani kwa umri huo kama wewe unaakili basi nilikua bado ni mdogo sana kwani hata kubarehe yenyewe ilikua bado kabisa, na pia kutokana na malezi ambayo nimelelewa na familia yangu, basi ni ngumu sana kujua jua nambo ya kijinga jinga yasio na msingi wowote ule, kwani kawaida nikirudi tu shule hua nakimbilia madrasa au msikitini kusali..... Simulizi hiii inaendana kidooogo na ile ya SECONDARY SCHOOL ila hii ni balaaa, maana huko mbele mi sisemi ila ukiikosa mi simo
"yes dady"
"umerudi shule mwanangu"
"ndio baba, ila leo hujaleta zawadi dadiii"
"usijali, nitampigia mama yako simu akuletee chipsi kuku na kilo ya nyama, si utamaliza ee"
"ndio, tena nitakula afu sili usiku"
"mmmhhh mtoto muongo wewe, unaweza kumaliza kuku mzima na kilo ya nyama"
"vilete uone navipiga chap chap"
"sawa, tupinge usipomaliza sileti tena zawadi"
"haaaaaaaaa dadiiiii basi simalizi"
"uyoooo ahahahaha nilijua tu"
Nilikua nikifurahi na baba yangu mzazi kana kwamba tunaishi kwa amani na upendo tena kwa furaha ilio ya juu kuliko yeyote yule,.... Sasa we imagen upendo wa baba ni huo je huyo mama itakuaje, yaani ilikua ni familia ya kuigwa na watu wengine kupitia familia,
"vp unataka uangalie katuni zako"
"amna dadii mi nipo chumbani nafanya homework zangu"
"haya bwana"
Kwa upande wa shule kiukweli nilikua kichwa na ndoto zangu ni kuja kua dokta mkubwa katika tanzania hii, hio ndio ilikua ndoto yangu ya baadae,
Maisha yalikua ni mazuri sana juu yangu, kwani wazazi wangu wote walikuepo na walikua wakinipenda sana, maana nilikua nipo peke yangu katika familia yetu,...... Ila siku moja mamkubwa wangu alikuja kutusalimu huku mjini, akitokea kijijini, huyo ni mamkubwa kwa upande wa mama angu,.... Tulimpokea huku tukiwa na furaha juu ya ujio wake huo, ila siku moja nikiwa naenda msalani kujiseidia, usiku wa saa nane, nilishangaa kuona mtu kakaa nje kwenye kiti na usiku huo, hili lilikua ni jambo geni sana kwangu, niliwaza sana na kujua kua labda huenda akawa ni mama yangu anapunga upepo hapo nje, japo haikua tabia yake ya kupunga upepo mida hio, maana mama yangu anakaaga nje mwisho saa tatu usiku tena ni mpaka kuwe na mwezi ndio anatoka, sasa iweje leo aamke saa hizi,... Lakini nilipoangalia vizuri, ni kama hakua mwenyewe yaani walikua wapo kama watatu afu kuna mtu wamemzunguka katikati, na siku kwa bahati mbaya hakukua na umeme, walikua kama kuna kitu wanamfanyia huyu mtu waliomueka katikati, ila hakuna niliomuona sura kati yao,
Nilizidi kua na hofu huku nikinyata nyata ili niweze kuwasogelea karibu, lakini wazo langu lililopo kichwani ni kwamba, mimi najua ni baba na mama watakua wanacheza bao na jirani, hivyo nilikua nawamendea ili niwashtue, maana mama na baba wana tabia ya kucheza bao usiku, japo sio usiku mkubwa kama leo hiii, niliendelea kuinama huku nikijificha kwenye gadeni na maua yaliopo hapo, nilikua nahisi baridi sana, kwani nilitoka na boxer tu,...... Lakini nilipofika karibu nilishindwa kuelewa hawa wazazi wangu wanacheza bao gani, mbona sioni hata wakirusha rusha mikono zaidi ya kuona mikono ikiwa juu juu tu....... Nilijipa moyo kua huenda ni mchezo mpya waliougundua watu hawa, maana si wazee wa zamani hivyo watakua wakijua michezo mingi mno,..... Nilizidi kusogea mpaka nikakaribia karibu yao huku nikiwa nimejificha kwenye shina la ua moja kubwaaaa, lakini baridi ndio ilikua inanisumbua hivyo nikawa natetemeka sana huku, nikiwa nataka niwashtue baba na mama kama vile tunacheza kombolela,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikua sio mkubwa kama unavyofikiri, kana kwamba labda michezo ya kitoto nimeacha lahasha, bali nilikua ni mtoto mwenye umri wa miaka 14 tena umbo langu lilivyokua dogo unaweza kusema nina miaka 10 au 11, yaani nilikua nipo kidato cha kwanza lakini akili ya kiutu uzima ilikua bado haijanijia, hivyo ukiniangalia tu utanichukulia kama mtoto kabisa, japo miaka kumi na nne kwa msicha ni mdada mkubwa tu, na hata mimba anapokea vizuri tu, ila kwa wakiume mwenye unri wa miaka 14 hawezi kutungisha mimba, kataa kubali lakini ukweli ndio huo,
Sasa nilipokua nazidi kusogea maeneo yale, nilishangaa kuona mtu katikati tena walikua wskimwagia unga, huku wakimpiga vibao vya kichwa, tena cha ajabu zaidi ni kwamba wale watu watatu ambao wamemzunguka huyo mtu ambae sikumjua kwa sura, walikua wapo uchi wa mnyama, sasa nikajiuliza kua, huu ni mchezo gani ambao wameugundua watu hawa, tena mchezo wa usiku mida ya saa nane,.... Sasa nikiwa naendelea kuangalia, ghafla niliona kisu kilichojikunja ambacho kilishikwa na mama mmoja ambae nilikua namuona kwa nyuma, maana nilikua nyuma ya mgongo wa huyo mama, Nilishangaa kila kisu kikinyanyuliwa na kumpata yule mtu aliekua pale chini tena, sasa kilivyompata yule mtu aliguna, na kugundua kua alikua ni wa kiume,... Sasa nilipoona anarudia tena kumpiga na kile kisu, mimi niliamka na kuanza kukimbia kana kwamba niliogopa sana kwa kuuona ukatili ule uliokua ukifanyika maeneo hayo,
Sasa kile kitendo cha kukurupuka na kukimbia kiliwashitua wale watu, ila sikua nimeangalia nyuma kwa haraka ila nilipofika karibu na mlango niligeuka huku niliwa naingia ndani, lakini cha ajabu sikuweza kuona mtu maeneo yale, yaani sijui walipotea poteaje maeneo yale, sasa hicho ndicho kilichonifanya nizidi kua muoga zaidi kuliko mwanzo, nilifunga mlango na kuingia chumbani kwangu kisha nikalivuta shuka kwa uoga huku nikitetemeka kwa uoga, Nilijifunika brangeti huku nikiwa nimejikunja utafikiri mtu anaesikia baridi, Hata usingizi haukua ukija kwa urahisi,
Kesho yake asubuhi nilikua nipo zangu chumbani nikijiandaa kwenda shule, Tulikua tuna housegirl ambae alikua akinisambazia chai ili ninywe niende shule, Mtoto wa kiume nilipiga chai mida hio huku nikiwaza kupewa pesa ya kula sambusa shuleni,... Nilipomaliza nilichukua begi langu kisha nikaliweka begani kisha huyoo nikawa natoka zangu,
Sasa nilipokua natoka mlango mkubwa, ili niende nikasubirie school bus, niliskia sauti ikitokea chumbani kwetu huku ikiita
"dada, dada"
Ilikua ni sauti ya mama angu ikimuita mamkubwa ambae alikua ni mgeni tena mgeni wa jana tu,
"abeeeee"
"jamani baba sheby sjui ana nini kazidiwa"
Niliposikia tu hivyo nami sikutaka kuendelea kwenda shule bali niligeuza na kwenda chumbani kwa akina baba,
Kwwli nilimkuta baba yupo hoi, tena alikua hata kuongea hawezi.... Chapuchapu mama alienda kuwasha gari uwani na kuliweka sawa kisha tukamuingiza ndani ya gari, nami sikua nyuma kabisa, nililiacha begi langu nyumbani kisha nami nikaingia kwenye gari, safari kuelekea hospitalini japo mama alinikataza lakini niligoma kukaa nyumbani,............ Nyumbani aliachwa housegirl tu, na kwenye gari tulikua mimi mamkubwa na mama angu, mama alikua akilia sana huku mamkubwa nae akiwa analia kwa uchungu,....... Tulifika hospitalini kisha manesi walileta machela na kumuingiza wodini, sisi watu watatu tulibaki nje tukisubiria taarifa sahihi kuhusiana na huko ndani kunaendeleaje,
Tulikaa nje zaidi ya masaa mawili, huku madokta wakipita pita na madripu ya damu na maji kwa ajili ya kumuudumia baba anfu, mama alikua hakai kila akimuona dokta, tuliendelea kukaa hapo hospitalini bila majibu yeyote yale ambayo yangeturidhisha kwa namna moja ama nyingine,. Na muda huo nilikua nipo na yunifom za shule,
Ilipofika saa tano na nusu asubuhi, ndio dokta anatoka huku akiwa anavua gropsi zake, mimi na mama angu tulikurupuka na kumfata dokta,
"dokta vp, mume wangu anaendeleaje?"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"aaaaa Anaendelea vizuri na mnaweza kwenda kumuona"
Lakini baada ya dokta kusema hivyo, nilimsikia mamkubwa akiuliza huku akitoa macho
"unasemaje dokta? Mungu wangu afadhali shemeji yangu apone"
Sikua nikiwaza chochote kile bali mimi ndio nilikua na spidi ya kuingia katika hio wodi ambayo ndio alilazwa baba yangu,
"baba, unanini baba angu"
"mwanangu sheby, hata mimi mwenyewe sijui, kwani vilinijia gafla tu bin vuu"
Mara mama nae alifika na kumkumbatia baba pale pale kitandani, huku akimuuliza juu ya hali yake hio aliokua nayo, Pia mamkubwa alikua akiongea nae kwa uchungu sana huku huku akimshika shika, lakini mimi sikua na wazo lolote lile linaloendelea,
Sasa nikiwa nimekaa pembeni ya baba hapo hapo kitandani, niliikumbuka ile ndoto ya jana, sasa nikawa najiuliza kua
"ivi ile ilikua ni ndoto au kweli"
Sasa niliposema hivyo mamkubwa alidakia juu kwa juu huku akisema kua
"hio itakua ni ndoto mwanangu"
"heeeee kwani wewe unaijua hio ndoto"
Nilimuuliza hilo swali huku nikimuona akijibalaguza balaguza na kucheka cheka,
"unajua wewe ni mtoto wangu, hivyo ukiota tu lazima namimi nijue maana damu ni moja na wewe"
Aliongea hivyo huku akicheka cheka kinafiki, na mama pia alikua akimsapoti, wakati huo baba alikua akinywa chai ya maziwa kwa sambusa na chapati za mayai,
"lakini hapana, kama ni ndoto tu nisingechubuka goti"
Sasa kile kitendo cha kusema kua nisingechubuka goti kilimshtua sana mama angu na kumfanya aniulize huku akinipandisha suruali amvayo nilikua nimevaa ili aone hilo jeraha ambalo niliumia wakati wa ndoto,
"sheby, umeumia wapi baba"
"nimeumia kwenye goti hili la kulia"
"jamaaani we mtoto umefanyaje, hebu twende kwa dokta mara moja"
Mama alinivuta pale nilipokua nimekaa huku akitaka kutoka kwenda kuniripoti kwa dokta ili nipate matibabu, na huo ulikua ni mchubuko kidogo tu yaani haupaswi hata kwenda hospitali wala kupewa dawa, lakini kwa jinsi wazazi wangu walivyokua wakinipenda, waliona mchubuko ule ulikua ni bonge la kidonda kwa upande wao,
Sasa nilipokua natoka nilimuona mamkubwa akiniangalia kwa jicho baya kana kwamba kama vile kuna kitu ananionya,.... Huezi amini nilijikuta nasita kwenda kumuona dokta, afu hapo hapo nikakumbuka kua katika ule mkono uliokua umenyanyua kile kitu usiku ule ulikua una bangili flani aina ya waya kopa yaani bangili iliokunjwa ila haikua ya kununua dukani kama tulivyozea kuona wadada zetu wakizivaa, na bangili hizo hua zinapendwa sana kuvaliwa na watu wenye asili ya uganga, kwani niliwahi kuziona siku moja tulipoendaga tanga kusalimia, mmoja wa ndugu zetu alikua ni mganga, na ndipo nilipoanza kuziona, sasa leo ndio nimeiona moja katika mkono wa kushoto wa mamkubwa na bangili hio niliiona hata jana usiku katika wale watu watatu waliokua wamemzingira yule mtu,.... .
Sasa baada ya kuona ile bangili pamoja na vile alivyonikazia macho nilisita kwenda huko kwa dokta, maana tulikua tunamuacha baba na mamkubwa wenyewe, hivyo kuna akili ikanijia ghafla ya kutokwenda....
"sheby, twende dokta akapaone jamani"
"mamaa hapo hapana shida turudi tu"
Mara mamkubwa akadakia juu kwa juu
"mwanangu sheby, we nenda ukapewe dawa mwanangu"
Sasa nikiwa navutana na mama, nilimponyoka na kukimbilia kwa baba kisha nikaanza kumkagua kichwa kama ana alama ya yeyote ile kichwani, lakini hakua na alama yeyote ile,
"we sheby unanikagua nini"
Baba aliniuliza hivyo huku akijishika kichwa chake na yeye akijikagua,
Sasa kile kitendo kilimchukiza sana mamkubwa, kwani nilimuona akikasirika ghafla na kuniangalia kwa jicho baya, ilibaki kidogo tu nimuulize kua kwanini ananiangalia sana,
Mama angu alinirudia tena na kunishika mkono kwenda kwa dokta, Mara na mamkubwa nae akaamka, sasa tukawa tunaenda wote kwa dokta, kwani roho yangu iliridhika baada ya kumuona nae katoka pale wodini, maana roho yangu ilikua haitaki kabisa kumuacha mamkubwa na baba pale wodini na sijui ni kwaniniCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulipofika kwa dokta mama alitoa maelezo kuusu mimi goti langu lilivyochubuka,
"mmmhh mama kweli unamjali mwanao, yaani mchubuko huu unataka apewe dawa?"
"dokta, kidonda ni kidonda hata kama ni kidogo"
Mara mamkubwa nae akasapoti kua
"ni kweli, maana kinaweza kua kikubwa baadae"
Basi dokta akaanza kunitaftia dawa huku wakiongea mengi kuusu mimi, dokta aliniuliza kua nimechubuka na nini, nikamwambia nilikua nacheza mpira ndio nikachubuka, lakini haikua kweli, bali nilichubuka jana usiku pale nilipokurupuka na kukimbia baada ya lile tukio la usiku ambalo mpaka sasa bado sijalipatia jibu kua ilikua ni ndoto au ni kweli, na kama ni ndoto mbona nimechubuka goti, au nimejigonga ukutani nilipokua naota, nilijiuliza maswali mengi sana juu ya swala kama hilo,
Sasa nikiwa naendelea kupewa matibabu ya goti, mara mamkubwa alimuuliza dokta kua
"dokta, choo chenu kipo wapi"
"aaaa choo kipo kulia ukishapita hio kordo hapo mbele yake kuna vyoo"
"ok asante"
Nilimwambia mama kua tuondoke zetu
"mama, twende kwa baba"
"hebu subiri utibiwe we mtoto"
"mama mi staki matibabu tena"
Mara dokta akadakia juu kwa juu
"dogo tulia namalizia kukufunga bendeji tu"
Yaani kile kitendo cha mamkubwa kuondoka roho yangu ilikua ikidunda mno,
"sheby kwani una nini lakini"
"mamkubwa anaenda wapi"
"si anaenda msalani, kwani hujasikia hapo akiulizia uwani"
"mamaaa we twende bwana"
"nitakuchapa sasa pumbavu wewe, kikiwa kikubwa hiki utamsumbua nani? Hebu tulia mwehu wewe"
Nilitulia lakini sikua na amani kabisa juu ya mamkubwa kuenda uwani,
Basi dokta aliendelea kunifunga bendeji huku, akiipakia dawa ili mchubuko ule usilete shida, kweli familia yangu ilikua ikinipenda sana, kana kwamba yaani mchubuko kidogo tu tayari napewa matibabu, na hapo ni mama, kama ngekua ni baba ungekuta hata kutibiwa nisingetibiwa hapa, maana karibia magonjwa yangu yote hua napelekwa nje ya mkoa wa arusha, yaani sitibiwi arusha, basi zoezi liliendelea mpaka mamkubwa akarudi kutoka uwani huku akimuuliza dokta
"mmmhh dokta bado tu"
"aaaaaa mama si unajua watoto hawa tunaenda nao taratibu mno"
"ni kweli baba"
Mara ghafla nesi kaja resi huku akimuita dokta kwa uharaka zaidi
"dokta dokta njoo haraka yule mgonjwa kazidiwa"
Dokta hakutaka kuuliza ni mgonjwa gani aliezidiwa, badala yake aliniacha na kukimbilia huko, ila sisi hatukushtuka sana maana hapo ililua ni hospitalini, hivyo sio kila mgonjwa ni wako tu,
"vinauma"
Mama yangu aliniuliza huku akipashika shika kwa kuangalia kama kuna maumivu ambayo naweza kuyasikia,
"haviumi, mi niliwaambia hakuna shida lakini mkanileta tu"
"mwanangu, kidonda ni kidonda tu hata kama kiwe kidogo kiasi gani"
"mmnhh sawa"
Mara dokta alirudi huku akiwa mnyonge mnyonge kiasi,
"poleni sana jamani"
"poleni? Pole ya nini dokta"
Mama ndio alimuuliza dokta huku wote tukimtumbulia macho dokta huyo, ili atueleze hio pole anampa naniCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"aaaa kiukweli, mume wako ametutoka mama"
Nilimuona mama nae akalegea pale pale, huku mamkubwa akiangua kilio, Mimi nilitoka na kuelekea kwenye hio wodi ambayo baba yangu alikua kalazwa, Sikuamini macho yangu baada ya kukuta baba yangu akiwa keshafunikwa shuka jeupe, lililomfunika mpaka kwenye macho, Sikuweza kuvumilia juu ya lile, nami nilianza kulia kwa uchungu mkubwa huku mamkubwa akija huku na yeye akilia, Nilimlilia baba yangu huku nikigala gala hapo chini kwa uchungu wa kumpoteza baba yangu mzazi, Mamkubwa alikuja kuniamsha huku akinibembeleza kwa maana mimi ndio niliokua nalia kuliko wote, nilimuona baba yangu akichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha watu walio na hali hio, yaani MOCHWALI yaani sikua nikiamini macho yangu kwa kile nilichokua nikikiona juu ya hali ile,
Baada ya hapo nilianza tena kumtafuta mama angu maana toka alivyolegea pale ofisini kwa dokta, sikujua kaeleka wapi tena,
"dokta dokta, mama yangu yupo wapi"
"usijali, we tulia na mamkubwa wako maana mama yako nae hali yake sio nzuri"
"naomba nikamuone mama yangu dokta"
Nilikua nalia kwa uchungu mno huku nikimsumbua dokta anipeleke alipo mama, yangu ili nimuone,
"mama yako, yupo wodi namba 9 palee"
Niliwahi kwenda kumuona mama ambae na yeye hali yake ilikua mbaya baada ya kusikia kua baba au mumewe amepoteza maisha, na hapo hapo mama yangu akalegea akiwa kakaa kwenye kiti, nilimkuta mama yangu nae kalazwa tena huku madripu yakiwa yamemzunguka kitandani kwake,
"mamaaaaaaaaaaa, ooohhhhh mama, mamaaaa baba hayupo tena mama, uuuuuwiiiiiiiii"
"sheby mwanangu nyamaza, mama ako anaumwa muache kwanza"
"sitaki niache nikae na mama angu"
"twende nyumbani ukale"
"sitaki hata kula...... Iiiiiiiiiiiiiiiii oooooooooooojjujj uuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhh nnnnnnnnnnhhhhhh uuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhh uu uuuwiiiiiii"
"sheby baba, unampigia mama kelele"
"sitaki niacheee"
Mamkubwa alikua akiniamsha kwa nguvu eti nitoke hapo wodini lakini sikua tayari kutoka,
Nilitoka tena na kuelekea mochwali kumuangalia tena baba yangu, Nilizuiwa kuingia mochwali, nilirudi tena kule alipokua mama yangu na kuendelea kukaa nae karibu maana najua kilichomuua baba yangu, ila hata nikisema sintosikilizwa na mtu yeyote hivyo bora nitulie tu,
Baada ya siku mbili kupita, hali ya mama ilikua nzuri, na alikubaliana na matokea ya kifo cha baba, tulikodi gari la kusafirishia maiti, huku sisi tukiwa ndani ya gari yetu ndogo aina ya vx nyeusi mayai mayai hivi, tulikua tukielekea tanga kumzika baba, kiukweli nilikua nina huzuni sana juu ya baba yangu,............
Tulifika kijijini hapo maeneo ya pongwe kunako makazi ya mzee, yaani ndio nyumbani, Basi kama kawaida maandalizi yaliandaliwa kwa ajili ya mazishi, kiukweli sikua na raha kabisa.....
Baada ya siku mbili kupita, tulishamzika baba katika nyumba yake ya milele, Nilikua nina uchungu mkubwa sana juu ya kifo cha baba yangu,....... Sikutaka kulala nyumbani maana kesho yake ilikua tunarudi arusha, aisee huezi amini nilienda makaburi usiku kukaa kwenye kaburi la baba huku nikilia sana, yaani sikuridhika kabisa kwa kifo cha baba yangu, nilijikuta usingizi ulinipitia pale pale makaburini, maana nilitarajia ifikapo saa 3 usiku nirudi nyumbani, lakini usingizi ulinipitia pale pale makaburini, kwakua ilikua ni usiku na nisingeweza kutembea na giza hivyo niliingia kwenye kichaka cha karibu kisha nikawa nimejilaza, maana tanga kuna joto kwa wakati ule,.... Kiukweli mimi ni muoga sana ila kwa kifo cha baba yangu, aiseee huezi amini uoga uliniisha kabisa
Sasa nikiwa pale kichakani, ghafla niliona watu kwa mbaali, tena wakiwa wamevaa kanzu, lakini tembea yao hawakua wakitembea kama kawaida, yaani walikua kama wamekaa afu wanakuja huku nilipo, nikaona bora niende nao nyumbani, maana huenda nikawa nimepata kampani ya kunisindikiza, hivyo nilikua nawasubiria wafiki karibu ili niwasimamishe, basi na mimi nikaamka na kusimama ili niwafuate, lakini kabla sijaanza kuwafwata, ghafla niliona wengine kwa upande mwingine tofauti na wale wa mwanzo, nikajua daaaahh kampani imekua kubwa, maana ilikua ni mishale ya saa 6 hivi kwenda saa 7 usiku,..... Niliona nikojoe kabisa ili nikianza safari nianze kabisa...... Nilitamani wafike haraka ili niniunge nao kwenda nyumbani, maana wanaonekana ni mashehe wanatoka kwenye shughuli. Hivyo nilitoka ndani ya kichaka kile na kuanza kuwapungia mkono japo ilikua ni usiku wa kutisha......
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikua nimekua mtu mjasiri sana, nisieogopa kiza wala nini, ulikua ni usiku mbaya sana, lakini mimi nilikua siuogopi hata chembe,
Sasa nikiwa nawapungia mkono ili wanione, ghafla nilivutwa mkono kichakani na mtu nisiemjua wala kumuona, kisha papo hapo nikapatwa na usingizi wa ghafla, hivyo nilishindwa kujua wale watu waliishia wapi na walipita njia gani, niliuchapa usingizi utafikiri nilikua kwenye godoro vile, Lakini kwakua kulikua kuna joto sana,... Niliweza kuzinduka usiku huo huo mida ya saa kumi usiku, Lakini sikuamini macho yangu kwa kuona watu waliovaa kanzu wakiwa wamelizunguka lile kaburi la baba angu, nilishindwa kuelewa juu ya jambo hili, sasa nikajiuliza au watakua ni mashekhe wamekuja kupiga dua, itakua wanapiga dua ya kumuaga baba yangu, lakini sisikii hata msomaji wa dua hio, nilianza kupatwa na mashaka juu ya watu hao hivyo nilikaa kwanza ili niwaangalie wanachokifanya juu ya jambo hilo,
Nilitulia kimyaa, lakini baada ya muda nilishangaa kuona kaburi limebaki peke yake yaani halikua na shekhe hata mmoja, na sikujua hata jinsi walivyoondoka maana nilikua nasinzia sinzia,... Wakati huo tayari ni saa kumi na moja alfajiri tayari kumepambazuka, niliamka taaratibu na kuelekea, nyumbani ambako ndio mama yangu alipo,.. Kiumri ni mdogo sana ila nina ujasiri wa kiutu uzima na kukosa maamuzi kama mtu mzima, Nilifika nyumbani ambapo nilikuta mama analia kwa kuto kuniona usiku mzima
"jamani sheby mwanangu ulikua wapi baba"
"mamy, nilikua makaburini"
"haaaaaa we mtoto, ulikua na nani huko"
"mwenyewe tu"
"mungu wangu asante kwa kumuona mwanangu tena"
"kwani hatuendi leo"
"tunaondoka, tena hebu kalete begi lako tunachelewa"
Niliingia ndani na kumkuta shangazi ambae ni ndugu yake na baba yangu, nilimsalimia huku nikiwa na furaha juu ya yeye maana shangazi halima hua ananipenda sana, hivyo nami ilikua ni furaha kubwa ya kumuona yeye, Mama nae alikuja huku akiwa sambamba na mamkubwa jasu, mama alimuomba shangazi namba ya simu kana kwamba alikua nayo ikapotea,... Baada ya kumsalimia shangazi nami sikutaka kuyasikia yakwao, bali nilienda zangu ndani ya gari tayari kwa safari ya kurudi arusha....
BAADA YA MIEZI SITA KUPIA
Nikiwa nipo zangu nyumbani naangalia katuni, mama yangu aliniita chumbani kwake, huku mamkubwa nikimuona anaanua nguo, maana mamkubwa ndio tunaishi nae kwa sasa baada mama kumpa nafasi ya kuishi hapa kwetu,
"naam mamy"
"afu mbona leo hukuenda madrasa, nini shida"
"amna mamy leo ni ijumaa"
"aaaaahhh ok nilisahau,.. Sasa kesho nataka nataka nikupeleke shoping mwanangu"
"haaaa kweli mama"
"ndio, nataka ukachague mwenyewe nguo"
"iiiiii safi sana mamy, duuuu"
"umefurahi eee"
"ndio mamy, tena kama vp tusipitie popote mpaka tufike shoping"
"no lazima nipitie benki nikaweke hizi pesa, au nikupe upeleke"
"akuuuuu peleka mwenyewe je nikiporwa"
"mmmhhhh milioni 25 nani achukue"
"weeeee buku tu wanachukua washindwe na hio"
Basi ilikua ni furaha kubwa baina ya familia yetu, yaani mama alikua ananipenda sana,
"uuuwiiiiiii mamaaaaa"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nini tena mamiiii"
"mmmhhhhhhh uuuwiiiiiii tumbo limeanza kuniumaaa"
"jamani ngoja nimuite mamkubwa basiii"
"ngoja kwanza, hebu chukua hii kadi ya benki na hili begi la pesa, viweke kabatini kwangu afu kasogeze gari karibu"
Nilifanya kama alivyoniagiza, kisha nikaenda kuwasha gari na kulileta hadi karibu na mlango, kisha nikaenda kumuamsha
"mamy, tumbo tu ushindwe hata kutembea"
"mwanangu we acha tu, limenishika kwenye kitovu aaaaauuuuuuuuwiiiiiiiiiiiiiii nakufa mie3"
"mamy huezi kufa bwana"
Sasa nikiwa namkokota kuelekea kwenye gari, mara mamkubwa jasu katokea huku akiwa kashinga nguo alizokua akianua nje
"we mwajabu nini tatizo"
"mmmhhh dada nashangaa ninaumwa na tumbo la ghafla tu"
"jamani we mama sheby, lilianza lini hilo tatizo"
"sasa hivi tu dada"
"sheby hebu fungua geti mara moja"
Nilikimbia kufungua geti huku mamkubwa akiendelea kumpakiza mdogo wake kwenye gari, yaani mama yangu na huyu mamkubwa wamezaliwa tumbo moja ila mkubwa ni huyo mamkubwa jasu, ndio mkubwa wao, nilipomaliza kufungua geti niliingia ndani ya gari kisha nikawasha gari,
Lakini cha ajabu na cha kushangaza gari ilikua haiwaki, yaani kila nikipiga start wapi, nikashuka na kuangalia betri kama imeisha chaji, nikaitilia mashaka na kuitoa, kisha nikaenda uwani kunako gari ingine nikaitolea betri na kwenda kuiweka kwenye gari tuliokua tumempakia mgonjwa, kisha nikaenda ndani kumuita mfanyakazi aje kufunga geti baada ya sisi kutoka,... Basi nikaingia tena kwenye gari na kuiwasha kwa mara nyingine, lakini huezi amini gari haikuwaka, na wakati muda sio mrefu niliitoa uwani na kuileta hapa mlangoni, sasa kwanini ikatae kuwaka? Niligeuka nyuma na kumuangalia mamkubwa huku huku nikiwaza kuhusu yeye,
"hata ndugu yako pia"
Niliongea hivyo huku mama akiuliza
"kwani ni nini sheby? Hebu washa twende bwana"
Nikajaribu kwa mara nyingine tena, ikakubali, kana kwamba lile neno nililoliongea lilimgusa, basi mtoto wa kiume niliikimbiza gari mpaka hospitalini kisha fasta fasta tukamuingiza kunako wodi,.. Ila tatizo la mamkubwa sina uhakika nalo kwani ninamuhisi tu kuwa hivyo,
Baada ya kumkabidhi kwa dokta, mimi na mamkubwa jasu tulikua tupo nje tukisubiri majibu, baada ya muda dokta alitoka katika wodi ile nasi tulikua wepesi kumfuatilia,
"dokta dokta vp mama angu anaendeleaje"
"kiukweli hebu subirini kwanza maana hata ugonjwa hatuuoni, hivyo kuna dalili za kumpelekea kijijini kwa waganga"
"tena? Duuuuu"
"ndio hivyo"
"hapana dokta jitahidi kadri ya uwezo wako mama angu apone"
"nitajitahidi usijali, ila inahitajika pesa zaidi"
"hakuna shida dokta"
Niliposema hakuna shida, mamkubwa aliwahi kuniuliza kwa haraka kua
"we hakuna shida hizo pesa umeziona wapi"
"tutauza gari moja mama apone"
"weeeeeee mali haziuzwagi"
"dokta fanya mama angu apone ipo pesa"
"inahitajika pesa kwa sasa ili matibabu yaanze, we mama vp mbona upo kimya na wewe ni mtu mzima kuliko huyu mtoto"
"ni kweli dokta ila kwa mimi sina pesa"
Nilidakia juu kwa juu na kumuambia mamkubwa kua
"mamkubwa? Mi najua anapoweka pesa mama"
"unasemaje wewe"
"ndio, najua"
"unasema kweli, hebu twende ukanionyeshe.... Dokta anza kumtibu"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliona bora nimpatie mamkubwa ili aweze kumuuguza mama, kwasababu bila pesa matibabu ya mama hayawezi endelea,
"mamkubwa, ungekaa na mama mi nikazilete"
" sawa, wahi mara moja uje"
Niliingia kwenye gari na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kuchukua lile begi la pesa lenye Tasilimu million 25 za kibongo, ambazo mama alikua azipeleke benki baada ya kuzivuna katika duka lake kubwa lililopo mjini kati, na duka hilo linauza nguo kuliko maduka yote hayo, na hio pesa ilikua ni pesa ya wiki, (faida ya wiki) hivyo alikua azipeleke benki kuzihifadhi kwa ajili ya familia yake hapo baadae,...... Nilifika nyumbani ambapo nilimkuta mfanyakazi wetu akiendelea na majukumu yake ya kikazi zaidi,
Niliingia chumbani na kufungua kabati la mama ambapo muda si mrefu aliniagiza kuziweka pesa hizo pamoja na ile kadi ya benki, nilivikuta vyote vipo lile begi lenye million 25 pamoja na kadi ya benki ambayo siijui ina kiasi gani ndani yake,... Sasa nilipotaka kuondoka navyo vyote ili kuvipeleka hospitali kwa ajili ya matibabu ya mama angu, nilipata wazo moja ambalo niliwaza kumpelekea hio kadi ya benki badala ya hili begi, maana hio kadi siijui ina kiasi gani japo nazijua mpaka paswadi zake,..... Nililificha lile begi juu ya daling kisha nikatoka na ile kadi ambayo sikua naijui kiasi chake cha pesa kisha nikachukua na simu ya mama ambayo aliiacha mezani pale tumbo lilipomuanza..... Niliondoka kwa spidi sana ili niweze kuwahi hospitali ili matibabu yasisitishwe kwasababu ya pesa,.... Huezi amini nilikua nalia huku nikiendesha gari, maana miezi sita tu iliopita baba yangu aliumwa na kupoteza maisha, tena leo mama nae anaumwa duuuuuu,... Sasa nikiwa njiani, nilipungiwa mkono na trafiki niweke gari pembeni, kwasababu nilioneka kutembea kwa spidi sana,
"shkamoo"
"marahaba, we mtoto wewe? Ivi kwanza una leseni"
Kiukweli sikua na leseni kwasababu umri wangu haukua ukiruusu kumiliki leseni, ila gari nilikua naweza kuendesha tena nilikua naendesha vizuri tu lakini umiliki wa leseni nilikua siwezi kuimiliki maana ndio kwanza nilikua nina miaka kumi na nne,
"sina baba"
"we pumbavu kweli, utaendeshaje gari na wakati huna leseni, afu mbaya zaidi unalia. .. Askari askariii, hebu njoo"
Alimuita askari mwenzie na kuanza kunipiga maswali ambayo sikuweza kuyajibu,
"we mtoto usitutanie wewe"
Nilikua nalia kwasababu nilikua nachelewa kupeleka pesa hospitalini, na dokta alisema bila pesa hawezi kuifanya kazi yake,...
"aiseee we mtoto hebu twende kituoni"
"baba, nisamee mi nakwenda hospirali mzee"
"nimesema twende kituoni mshenzi wewe, unafanya hii nchi ni ya baba ako"
"mzeee nisamee mzee, au naomba basi tupitie hospitali kisha unipeleke unapotaka"
"we mtoto, unataka makosa yaongezeke"
Sikua na jinsi maana ni kweli sizijui sheria za barabarani, japo kuendesha najua... Basi niliwasha gari kuelekea kituoni ambako ndipo ninapokwenda kusomewa mashtaka yangu, lakini muda huo kichwa changu kilikua kikiwaza kwa mamkubwa kule hospitali, maana hata mamkubwa simuamini sana kama mseidizi wa mama yangu,
"we mtoto, tunakaribia kituoni sasa, vp huna chochote uwahi unapokwenda"
"sasa kwanini usiniambie toka saa hizo mi nimechelewa"
"usijali utawahi tuuu"
Niligeuza gari na kuelekea benki maana sikua na keshi ambayo ningeweza kumpa huyu askari,
Nilifika ATM kisha nikaingiza kadi ambayo paswadi zake ninazo, na pia akaunt hii inatumiwa na wote, yaani wazazi wangu walikua wakitumia akaunti moja kwa kuhefadhi pesa,...... Sikuamini kama akaunt hii ilikua ina pesa nyingi ambozo sikutegemea kuzikuta, ilikua ina million 145 .6, yaani nilishukuru kwa huyu askari kunipitisha huku, maana nilikua nampelekea mamkubwa hii kadi na kumpa paswadi zake,.... Sasa nilichokifanya ni kutoa ile milioni 5 .6, ambapo nilimpa yule askari elfu hamsini, kisha nikabakiwa milioni tano na laki 5 na nusu,.. Baada ya hapo nilitoka hapo atm kisha moja kwa moja niliishika simu ya mama na kumpigia shangazi yangu ambae ni ndugu na baba..
"haloo shkamoo shangazi"
"marahaba ujambo baba"
"sijambo"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"vp mbona unalia baba kuna tatizo"
"shangazi, mama anaumwa"
"jamani ni nini cha zaidi"
"mi sijui, ila alishikwa na tumbo la ghafla tu hadi hospitalini"
"jamani wifi yangu, poleni sana, sasa amepata nafuu"
"bado, kwani dokta alisema bila pesa hawezi kumtibu, na ndio nataka nipeleke pesa"
"hebu wahi basi haraka, kisha unijulishe kinachoendelea"
"lakini mi nataka uje shangazi"
"sasa sheby, mimi nikija na huku nitamuachia nani, maana huku kijijini nipo mimi na mume wangu tu, ila ngoja niongee nae nije sawa"
"sawa shangazi fanya hivyo haraka na kama tatizo ni nauli sema tu nikutumie"
"sawa usijali, lakini mamkubwa wako si yupo"
"shangaziiiii mi nakutaka wewe umseidie mama"
"ok hebu wahi basi hospitalini"
Nilikata simu kisha nikawasha gari na kuelekea hospitalini
Nilifika hospitalini nimiwa na spidi kubwa kuelekea kwenye hio wodi ambayo mama angu ndipo alipolazwa, kwanza nilikutana na mamkubwa akiwa mlangoni huku akiwa kama anatokwa na machozi na huzuni mno, nilimuuliza huku nami machozi yakinianza kunitoka
"mamkubwa mbona unalia"
"mwanangu sheby, umechelewaa"
Sikutaka kumsikiliza mamkubwa bali niliingia ndani ili nikahakiki mwenyewe, nilimkuta mama yangu katoa macho huku akirusha miguu kana kwamba labda ndio alikua anakufa,.... Nilikimbia na kwenda kumuita dokta
"dokta mama yangu kapatwa na nini"
"we mtoto toka hapa sisu tuendelee na matibabu"
Mara ikatoka sauti kutoka kwa mama ikimuamuru dokta aniache niendelee kuwepo huku akiniita kwa mkono,
"mamy usiniache, mamaiiiii"
"sheby mwanangu, naomba usome, soma kwa bidii baba, elimu yako ndio msaada mkubwa sana kwako,... Ulie nae usimtegemee mpigie simu shangazi yako aje uishi nae, maana kuna dalili mbaya juu yako mwanangu,... Naomba usome, soma kwa bidiiii,... Hebu niahidi baba utasoma kama nilivyokuambia"
"mamy, nitasoma mama, ila usiondoke mama iiiiiiiiii uuuwiiiiiii"
"sheby, mwanangu usilie, ila kaa ukijua kikulacho kipo nguoni mwako.... Naomba maji ninywe mwanangu"
"hapana mama, usinywe maji"
Mara mamkubwa akadakia juu kwa juu huku uso umemkauka kau
"we pumbavu mpe mgonjwa maji anywe"
Kwakua nilikua ni mtoto hivyo nisingeweza kubishana na mtu mzima, ila nikimuangalia dokta alitikisa kichwa kuashiria nisimpe maji,... Hivyo nilipoacha kumpa maji mamkubwa alikichukua kile kikombe cha maji kisha alimpa mdogo wake maji tena kama vile anamlazimisha.
"mamkubwa, basi yanamtosha hayo"
Mama alipomaliza kumeza yale maji, aliangalia juu kisha akaniangalia mimi,
"sheby mwanangu, usimpe mtu ile kadi na naomba uitunze itakuseidia baadae.... Shangazi akijana mkabidhi nyumba... Na uishi nae...... Soma mwanangu Elimu ndio msaa mkubwa kwako.... "
" mama, mama, mama usiniache mama"
"mwanangu, kwa mateso ninayo yapata kiukweli siwezi kuponaaa, ila nakuomba usome kwa bidiiii... hebu sogea karibu"
Nilimsogelea karibu, kana kwamba kuna kitu cha siri anachotaka kuniambia mimi peke yangu... Hivyo niliweza kusogea kisha mama akaniambia
"pale kwenye kabati langu droo ya chini kuna..............
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikua ninatokwa na machozi muda wote huku nikifiria kuusu wazazi wangu, maana kila nilupokua nikitegemea panavunjika, hebu ona na mama yangu haonekani kua na dalili za kupona ili aendelee kuishi na mimi, mama yangu aliniita nimsogelee karibu ili aweze kuniambia hilo neno analotaka kuniambia kwa wakati huo, basi nilisogea sikioni kwake na kuanza kumsikiliza kwa umakini sana... Ila alikua akininong'oneza kwa skio hivyo hakuna mwingine alieweza kusikia zaidi yangu
"pale kwenye kabati langu droo ya chini kuna kibegi kidogo kilicho jaaa nyalaka za mali zetu zote, hivyo hakikisha unamkabidhi shangazi yako akija, na pia usimuamini mamkubwa wako, maana ndio ndio, ndio ndio ndiiiii ndiooooo ndii"
"mama, mamaaaaaa, mamaaaaaaaaaa, mamiiiii amkaaaaaa, mamaaaaaaa uuuwiiiiiii maaaaaaaaaa.... Mamkubwa mama kafanyaje uuuuuuuwiiiiii mamaaaaa"
Kiukweli nililia sana huku mamkubwa nae akiangua kilio baada ya kuona mama angu anafunikwa shuka jeupe ambalo lilimfunika hadi usoni, kana kwamba mama yangu ndio nisingemuona tena katika upeo wa macho yangu ya kawaida, kiukweli nilikua nikilia sana mpaka macho yalikua mekundu, sikuweza kuamini kama ni kweli mama yangu amefariki, yaani nimebaki yatima sina baba wala mama, tena mbaya zaidi nimeachwa na mtu ambae sijamzoea katika maisha ambayo nilikua nikiishi, mamkubwa alikua ni mtu mwenye maamuzi magumu tena asiependa ujinga, sasa mimi kwa jinsi nilivyozoea kuishi na wazazi wangu sikui kama nitaweza kuishi nae,.... Basi mama yangu alichukuliwa na kupelekwa mochwari ili kuhifadhiwa mpaka tutakapoamua kwenda kumzika nyumbani, Nilikua nikiwafuata manesi mpaka mochwali muda huo nilikua nikilia bila mpangilio huku nikigala gala chini kwa uchungu, Lakini manesi walinitoa nje na kusema tukaandae mipango ya usafiri ili tuweze kumsafirisha kwenda tanga, nami nikaona ni sawa bora nifanye hivyo, wakati huo ile pesa shilingi milioni tano bado nilikua nayo, hivyo kwa muda huo nilikua naweza kumsafirisha mama yangu, kwenda kumzika, nilikua bado ni mtoto sana hivyo kuna mawazo mengine napaswa kuyaomba kwa wakubwa..... Nilichokifanya kwanza ni kurudi nyumbani huku nikiwa nimemuacha mamkubwa hospitalini akimlilia mdogo wake, nilifika nyumbani nikamkuta mfanyakazi katulia anaangalia tv, nilipitiliza hadi chumba cha mama na kufungua ile droo ya chini, kweli nilikuta nyalaka za kampuni yetu moja, na nyalaka ya nyumba hii ya kwetu, pamoja na kadi mbili za gari ambazo zipo ndani ya himaya yetu, nilivirudishia vitu hivyo katika kibegi kimoja kisha kisha nikavirudisha huko huko kwenye kabati, na kufunga vizuri, kisha nikaufunga na mlango wa chumbani ili mtu yeyote asije akaingia....
Nilipotoka mpaka sebureni mfanyakazi wetu aliniuliza
"sheby, mbona macho yako ni mekundu kuna nini"
Aliuliza hivyo lakini nilikua naskia uchungu kila nikitaamka kifo cha mama yangu, huezi amini machozi yalianza kunitoka tena kwa mara ya pili huku nikimwambia kua
"mama ameshafariki dunia"
Dada wa kazi nea kumbe ana presha zake za kushuka sijui kupanda, alizimia pale pale kwenye sofa, nami ndio nikazidi kulia, ila nikaona kulia haitoseidia kitu chochote, nilimlaza chini kisha nikaanza kumpepea ili aamke, maana yeye na shangazi ambae anakuja, ndio tegemezi langu, maana mimi binafsi sikua naweza kujiendesha mwenyewe kimaisha hata kama tunazo,.. Niliona ngoja nimpigie simu shangazi, Niliitoa simu mfukoni na kumpigia shangazi ili nijue kafikia wapi katika swala la kuja mjini,
"haloo shangazi"
"eee halo baba hujambo"
"sijambo shangazi, upo wapi"
"nipo mombo baba, nisubiri unipokee hapo stendi maana sipajui huko mnapoishi kwa sasa"
"sawa nakuja kukusubiri"
"sawa baba"
Sikutaka kumuambia kilichotokea huku ili nisije kumshitua na yeye akaukata maana ndio tegemezi kwa sasa,.... Basi fatuma au housegirl aliamka na kutulia vizuri tu
"vp unajiskiaje"
"sheby, ivi ni kweli mama kafa"
"usiseme ivyo, dada"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sheby, tutaishije sasa, maana hata huyu mamkubwa wetu simuelewi"
"mi mwenyewe hata sijui kwakweli"
Tulikua tukiongea mimi na dada fatuma, ambae ni mfanyakazi wetu wa ndani, ila tunaishi nae kama ndugu, hivyo nikimuona simuoni kama mfanyakazi bali namuona kama dada yangu, maana kanipita miaka mitano, mana kwa sasa ana miaka 19 na mimi nina miaka 14 hivyo ni kama dada yangu, na niliusiwa nisimdharau wala kumuita housegirl, bali awe kama dada yangu, na pia licha ya kua mfanyakazi, bali halipwi kama wafanyakazi wengine, bali atanunuliwa kila anachokitaka na pia familia yake tumeiwezesha huko kijijini kwao, hivyo hapa kapewa uhuru na mama yangu kua kama ndugu, na asijibague na wala tusimbague, hivyo toka aje mpaka sasa tunezoeana kiasi kwamba dada huyu ananipenda sana kama mdogo wake wa kuzaliwa nae, nami pia nampenda sana kama dada yangu wa kuzaliwa nae, kifupi tulikua tukipendana sana,...... Sasa nikiwa hapo nilikumbuka zile pesa zilizokua kwenye begi, ambazo mama alitaka kuzipeleka benki kabla hakuumwa, nilienda chumbani kwa mama na kulichukua lile begi, ambalo lilikua lina shilingi milioni 25 za kitanzani, hilo lilikua ni kusanyo la wiki, katika duka lake la nguo lililopo mjini kati, nilipozichukua mara moja niliondoka na kuelekea kwenye gari
"sheby, sheby unaenda wapi"
"dada, napeleka hizi pesa benki"
"sawa, ila uwahi kurudi ili tujue tunafanyaje kuusu mazishi ya mama"
"sawa"
Mtoto wa kiume nilikua sina leseni lakini kwenye kuendesha nipo vizuri,... Nilifika benki na kuziweka pesa zile, na akaunti ikasoma milioni 165, ukumbuke kua kulikua kuna milioni 145.6 baada ya kuto milioni 5.6 ndio ikabaki milioni 140, sasa nimeleta milioni 25 ikasoma milioni 165, nikatoa kadi yangu na kuiweka mfukoni, kisha nikaelekea stendi, nilikua najizuia kulia maana nikionekana nalia huenda nikazua maswali mengi machoni mwa watu, nilijikaza kiume japo havikaziki lakini ilinibidi nijikaze,........
Baada ya masaa kadhaa shangazi alikuja kutoka kijijini, tena alionekana kua na haraka ya kuja kumuuguza wifi yake, lakini ukweli ni kwamba hajui kama wifi yake keshafariki dunia, ila nilimficha tu ili akajionee mwenyewe,. Hivyo nilimpakia kwenye gari kisha nikampeleka nyumbani ili akaweke mizigo yake, na kupata msosi, dada alifurahi kumuona shangazi maana ahueni kidogo ilionekana..... Baada ya shangazi kumaliza kula tuliondoka sasa tukielekea hospitalini ili akamuone wifi yake....
Sasa cha ajabu na cha kushangaza tulipofika hospitalini, sikumkuta mamkubwa, ila sikushtuka sana maana labda huenda kaenda kujiseidia, hivyo tulinyooka moja kwa moja hadi kwenye ofisi ya dokta, kisha nikamtambulisha shangazi kwa dokta ili akienda kumtazama asije akamzuia,....... Lakini nilishangaa dokta akiniuliza kua
"dogo, wewe si ndio ulikua hapa na yule mama mnene hivi"
"ndio ni mamkubwa wangu yule"
"sasa nyie mumekuja kufanya nini tena"
"dokta, unauliza maswali gani hayo"
"hapana sio maswali gani maana mtu wenu keshatolewa masaa mawili yaliopita, na kwa sasa usikute hata kuzikwa keshaazikwa kitambo"
"Whaaaaaaaat, dokta, au umetusahau dokta"
Mara shangazi akadakia juu kwa juu
"sheby, ina maana wifi mwaju amefariki"
"ndio shangazi, na niliweza kukuficha kwakua ulikua safarini, naomba unisamee shangazi"
Shangazi alianza kulia kwa uchungu huku akitaka amuone wifi yake,
"dokta hebu twende basi kule mochwali ili shangazi amuone mama"
"we mtoto usituchezee hapa, nimekwambia hivi, mama yako kachukuliwa masaa mawili yaliopita na yule mwanamke unaemuita mamkubwa, na neno lake aliloacha kasema hivi, anaenda kumzika mdogo wake katika makaburi ya manispaa ya arusha, hivyo kama ni mama yako wahi kwenye makaburi hayo ili uyawahi mazishi, tena kama huamini ona sahihi ya yule mama baada ya kuichukua maiti"
Huezi amini nilianza kuchanganyikiwa juu ya swala hilo, ila sikua na jinsi ya kufanya bali nilimchukua shangazi na kuingia kwenye gari huku akilia mno, niliwasha gari kuelekea kwenye makaburi hayo kana kwamba huenda nikawaona wakizika, lakini kwanini mamkubwa anakua hivi, kwanini mama asiende kuzikiwa nyumbani........ Mungu si asumani kweli tuliona watu wengi wengi kiasi wakiwemo maostadhi, hivyo nasi tulisogea ili kuhakiki ni yeye kweli, maana huenda ikawa sio mama ndio anazikwa maana hapa ni makaburi ya watu wengi kwa wale ambao hawana maeneo ya kuzikia, hivyo unakuja kuzikiwa hapa kwenye makaburi ya manispaa ya jiji la arusha..... Nilipoangalia kwa mbali nilimuona mamkubwa akiwa anafuta futa machozi,.... Kweli alikua ni mama ndio anazikwa, nilikimbia na kuingia mbele za watu na kuktaza mchanga usiwekwe maana nimekuta ndio kwanza wanamuingiza katika shimo, sasa mimi nilipofika nilizuia zoezi lile la kumwaga,........ Mara nikaskiaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"we mshenzi unafanya ujinga gani apo, hebu toka haraka"
Niligeuka haraka na kuangalia huyo mtu anaenifukuza, huku watu wakisemezana kua
"huyu ni mtoto wa nani, mbona anavuruga mazishi"
"jamani mtoeni huyo mtoto huenda ni kichaaa"
"mpigeni, hawezi kuzuia mazishi ya mtu"
"watoto wengine sijui wana vichaa vya wazazi wao"
Wakati huo shangazi ndio kwanzaa analia kwa uchungu baada ya kuona tukio lile la kushangaza, la kukodi watu wa kuzika kisa maiti hatakiwi kuwekwa katika jokofu kwa muda mrefu, na hizo ni itikadi za kiislam..........
Sasa ile naangalia mtu alieniambia mshenzi, nilishtukia nimepigwa bereshi la kichwa huku nikisikia sauti zikisema,
"huyu mtoto huenda ni kichaa kinamuanza, hebu ona hata mama yake pale analia kwa kugala gala, hawa sijui ni vichaa wa wapi hawa"
Ilikua ni sauti niliokua naifahamu kabisa ndio iliotaamka hayo maneno....
Kwa wakati huo sikua na fahamu juu ya kipigo kile, maana yule alienipiga alinipiga utafikiri alikua akiua nyoka nyumbani, yaani utafikiri hana mtoto,.......
Nilipokuja kuzinduka nilikua nipo hospitalini, maskini ya mungu sikumzika mama yangu hata kidogo, tena mbaya zaidi nimeitwa kichaa mbele ya mwili wa mama angu, kisa ni kuzuia usizikiwe pale,
Nilipocheki pembeni nilimuona shangazi akiwa analia huku akiniangalia tu, na nilipocheki tena pembeni ambapo ni kushoto kwangu, nilimuona mamkubwa nae, akijifanya analia, nilipomuona mamkubwa tu nikajihisi na mimi huenda ndio siku yangu ya kufa, maana kila mgonjwa atakaeletwa hospitalini hapa hatopona kama mamkubwa yupo karibu, nilipojigusa kichwani nilikua tayari nimeshawekewa piopio la kichwa, kana kwamba lile bereshi niliopigwa la kichwa limenitoa kidondo kikubwa, nilikua nahisi maumivu makali mno,.... Shangazi aliniwahi na kuanza kunibembeleza huku mamkubwa nae alinyanyuka kwa aibu na kuja kunishika shika kujifanya ananijulia hali, wakati yeye ndio sumu kabisa ya familia hiii, ila kwa upande wangu mimi bado ni mtoto hivyo siwezi kumpa maneno makali yanayomstahiki kumpa,
"sheby mwanangu, usilie utapona tu"
Ilikua ni sauti ya shangazi ikinisemesha huku na yeye akilia kisiri ili mimi nisijue kama analia, kiukweli inatia uchungu sana, na kitu kinachoniliza ni kumzika mama yangu katika makaburi ya manispaa ya arusha na wakati pesa ilikuepo ya kumsafirisha kwenda nyumbani, Nilikua ninalia mtoto wa kiume huku nikijihisi kuzaliwa bahati mbaya na kuishi makusudi katika ulimwengu huuu, kipindi kifupi tu cha kuja mamkubwa kimezua maisha magumu juu yangu, mpaka sasa tegemezi langu ni shangazi peke yake, hivyo yeye ndio baba na yeye ndio mama..... Shangazi ni ndugu yake na baba, na mamkubwa ni ndugu yake na mama, hivyo hawa watu kila mmoja ana upendo wake juuu yangu,
BAADA YA SIKU MBILI KUPITA
nikiwa bado nipo hospitalini tena kwa uwezo wa mungu nilishatolewa lile piopio na hali yangu haikua mbaya sana japo usiku wa kuamkia leo niliona vimbwanga mbwanga vya kutisha,
"sheby baba umeamkaje"
Ilikua ni sauti ya shangazi yangu mpendwa ndio ilikua ikiniuliza, wakati huo mamkubwa ndio alikua anakuja kutoka nyumbani, wakati shangazi kalalia hapa hapa hospitalini kwa ajili yangu,
"shkamo mamkubwa"
"marahaba ujambo"
"sijambo"
"haya waendeleaje"
"aaaaa bado nahisi maumivu kidogo"
"pole mwanangu utapona tu"
Baada ya kunijulia hali mimi alimgeukia shangazi na kusalimiana, ila shangazi anajua kua mamkubwa ni fisadi kiwembe, tena sio kiwembe sema viwembe, maana kapiliza zaidi ya kiwembe huyuCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi walisalimiana pale na kuulizana habali za mimi na kuulizana habari za nyumbani,
Walitoana nje kitu ambacho kilinishtua sana kwa upande wangu, kwanini watoane nje tena anaemtoa mwenzie ni shangazi, daaahhh kweli mimi sina bahati ya maisha, maana kila tegemezi kwangu linakua shetani kwangu, je nimuamini nani na je nani ataniendeleza katika maisha haya...... Nilikua ni mtu wa kulia kila mara nifikiliapo wazazi wangu, ama kweli mzazi ni mzazi na ukipata mwingine basi jua hilo ni jinamizi,.... Swala la kulia kwangu liligeuka kama ndio furaha kwangu yaani furaha ya mwanzo sasa imeshatoweka.... Niliona bora ninyamaze ili nijue nini cha kufanya
Nilijisachi mfukoni kuangalia kiasi cha pesa nilichonacho, nilikua nina pesa kidogo tu kama laki 4 hivi tena nashukuru sikupigwa tero pale makaburini,..... sasa nilipokumbuka makaburini nilikumbuka kua tulienda na gari, afu ndani ya gari kulikua na brifkesi yenye pesa kiasi cha shilingi milioni 5 zile nilizodroo benki kwa ajili ya matibabu ya mama, Nilikurupuka hapo kitandani na kutoka nje, maana nina siku kama mbili hivi sijatoka hapo hospitalini, nilipocheki kwenye paking ya magari sikuona gari yetu, nilitoka nje na kuita toyo kisha ikanipeleka maeneo yale ya makaburi, lakini kufika mungu wangu sikukuta gari wala nini, lakini uzuri ni kwamba ufunguo nilikua nao lakini gari ndio silioni, gari yetu ilikua vx nyeusi, maana tunazo mbili vx na gari flani hivi ndogo, sasa hio iliopotea ni vx,..... Sasa kuona lile kaburi la mama nilijikuta nikianza kulia huku nikilifuata taratiiibu kabisa, nilikwenda kulishaka kaburi la mama yangu, mama yangu amezikwa katika maeneo ya kutupwa yaani hakuzikwa kiuhalali kabisa yani,....
"oyaaa we dogo twende bwana"
Alilua ni dereva toyo ndio aliokua akiniita tuondoke zetu, ila nilikua nina uchungu kuliko hata mwenye uchungu unaojua wewe,......
Nilitoka pale kaburini nikiwa nimechafuka vumbi la kaburi, maana nilikua nikilia kwa kugala gala juu ya kaburi la mama angu,
Basi nilienda kwenye kijiwe kimoja hivi kilichopo karibu na makaburi hayo, niliwakuta mabraza kadhaa wakiwa wanafanya kazi ya kutengeneza kacha,
"shkamoni wakubwa"
"maraaba vp dogo"
"poa sana kaka zangu, aaaa samaani naombeni kuwauliza"
"uliza tu dogo, hakuna shida"
Mara kuna mmoja akaropoka kitu
"aaa ras uyo dogo sio chizi uyo"
"nani, chizi awe uyu"
"eeee mbona kama nilimuona anacheza na kaburi pale"
"ebu jieshimu bwana, dogo yupo fresh uyu, ebana dogo ebu uliza kacha wangu, ulikua unasemaje"
"aaaa juzi juzi hapa kulikua kuna mazishi maeneo haya, ila kuna ugomvi ulitokea kidogo tu na kulikua na dogo alipigwa bereshi siku ile,... Kwahio kutokana ile fujo kuna bwana mmoja alisahau gari nyeusi maeneo haya"
"aaaaaaa yule dogo aliepigwa bereshi kwa kusadikiwa kua kichaaa,... Eeee bwana afu hata hio gari ilichukuliwa jana na brek daun, nadhani itakua polisi hio gari"
"oookee ni gari kubwa hivi"
"ndio tena aina ya vx nyeusi tiiii"
"enhee hio hio"
"we nenda police utaikuta, maana ni mapolisi ndio waliibeba na break down"
"ok poa sana wakubwa, ngoja niwaache na chai kidogo, hii hapa mtapata chai wakubwa wangu"
"daaahh asante sana dogo, ebana we nenda polisi tu, yaani nyooka moja kwa mojaaa"
"poa poa"
Nilipanda toyo kisha tukaelekea huko police,... Kweli nilipofika polisi nilifanikiwa kuiona ile gari,.... sasa tabu inakuja hivi je? Wataaminije kua gari ni yangu, japo funguo ninayo na kadi ya gari ipo ndani,.... Nilinyooka moja kwa moja hadi kaunta kwao na kutoa maelezo ya hio gari,
"sema shida yako"
"shkamoo broo"
"maraaba ujambo"
"sijambo...... Aaaa brooo samaani, kuna gari aina ya vx nyeusi nimeiona pale, hio gari ni ya kwangu na niliiacha pale makaburini baada ya kupigwa bereshi ya kichwa"
"heeeeee we mtoto unasemaje, yaani wewe uweze kumiliki gari kama ile, wewe umetumwa eeeeee? Afande, afande,"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"ndio afande"
"mwizi kajileta, na atawataja wenzie ni akina nani"
"broo gari ni yakwetu broo"
"pumbavu zako kimya, uwe na gari kapurwa mkubwa wewe, hebu kaone kalivyo chafuka, kwanza umri wako hata leseni hupati leo uwe na gari nani atakusajiria"
"brooo"
"kelele wewe"
"afande, tia sero huyu, halafu kesho ukatuonyeshe hao wanaokutuma, pumbavu zako"
"broo naomba unisikile kaka"
"nimesema vua viatu na mkanda huo, na kama una chochote mfukoni utakiacha hapa na utakitilia saini"
Daaaahh nilivua viatu na mkanda tayari kwa kuingia sero, tena muda huo tayari nilishachezea faru kama mbili hivi, nilikua nalia na mungu wangu tu, maana kila ninapogeuka hakuna msaada zaidi ya kukandamizwa tu, afu nikicheki huko sero kuna minjemba inatoa macho khaaa,..... Nilianza kulia huku nikiwakumbuka wazazi wangu,....... Ukiambiwa kuna mnaetukana wazazi wenu inshanlah mungu awasamehe katika hii dunia,..... Nilijisachi na kutoa kile kiasi cha laki tano pamoja na ile simu ya mama angu
"haaaaaaaaa pumbavuuuu huyu mtoto ni jambazi, yaani na umri huu unamiliki simu ya gharama namna hiii, afu bado unatoa na vibunda vya pesa........ Sasa utaniambia na hivi uliibia wapi.... Si nakuuliza we mbwaaa"
Faru ilipita mgongoni kwangu nikiwa nimevaa tisheti nyepesi iliokua ikipenyeza maumivu makali mno....... Sikua nikilia kwa maumivu ya faru, bali nilikua nikilia kwa kuwakumbuka wazazi wangu, huku nafsi yangu ikisema kua
"kama ni kuwakumbuka wazazi wako utawakumbuka sana tu, na bado huo ni mwanzo tu"
Machozi yalizidi kunidondoka mfululizo kwa kukosa utetezi wa maisha yangu,....
Niliona nimeonewa sana katika haya maisha maana kila nipitapo nakutana na vikwazo tena vigumu mno, hebu ona mtoto mwenye umri wa miaka 14 leo naingizwa kwenye sero ya mijitu mizima,
Nilikua nabubujikwa na machozi kwa kitu nisichokijua, maana chozi la kumlilia mama lipo, la kumlilia baba lipo, la kuonewa lipo, yaani sijui nini hatma ya maisha yangu, kwani sioni hata thamani ya kuishi tena hapa duniani,
Lakini mungu si asumani ghafla nilimuona rafiki wa baba yangu, nae alikuja hapo kituoni ila sikujua kua alifuata nini kwa wakati huo, maana alikua kashika brifkesi nyeusi,
Nikajipendekeza kumsalimia ili anione nipo maeneo hayo
"shkamoo mzee"
"marahaba, haaaaaa sheby? Unafanya nini huku"
"mzee, ni matatizo tu yananiandama kila kukicha mzee"
"nini tena, hebu vaa viatu vyako kwanza"
Yule askari aliposikia nimeambiwa nivae viatu alidakia juu kwa juu,
"mzee huyu mtoto ni jambazi"
"hebu tulia wewe mtoto mdogo kama huyu ujambazi autilee wapi"
"haiwezekani atoke sasa"
"kwani watuhumia si ruksa kuwekewa mzamana, sasa mimi namuekea mzamana"
Nilinusurika kuingia sero maana nilikua bado sijaingia, nilivaa viatu vyangu kisha nikavaa na mkanda wangu, na kuchukua simu pamoja na pesa zangu, kisha tukakalishwa chini na mkuu wa kituo ili tuyamalize,
"mbona umechafuka kijana"
"mzee nilikua kwenye kaburi la mama muda si mrefu"
"sasa huku nako umefikaje"
"mzee, nilifuata gari ya mzee, maana kwenye mazishi kulitokea fujo za hapa na pale na mimi nilijeruhiwa hivyo nikachukuliwa pale na ambulace nikaacha gari pale makaburi, sasa katika kuuliza nikaambiwa gari ipo kituoni, na kweli gari ipo nimeona.... Sasa hawa nao wakaanza kusema mi ni muizi na ndio walikua wanisweke ndani mzee"
"haaaaaaa yaani anakuja kudai haki yake mnamuita ni mwizi, ivi hii sheria nyinyi mnaichukuliaje nyie"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"sisi tulimhofia huyu huenda katumwa"
"sheby, fungu si unayo"
"ndio ninayo"
"sasa kumbe mtu mpaka funguo anayo mumeshindwaje kumuelewa"
Basi yaliongelewa pale kisha tukatoka nje na kuambiwa nikalitoe lile gari, na ndani ya gari kuna brifkesi ya pesa niliiweka humo,.... Kweli niliitoa ile gari na uzuri zaidi pesa niliikuta ipo pale pale haijaguswa,
"ndio hii afande"
"ala, hii gari si ile mpya hiii, baba ako anatunza"
"lakini mzee ivi huna taarifa zozote kuusu baba"
"taarifa gani, maana mi nakumbuka siku alikuja kwangu ni miezi kama sita hivi, nami nilisafiri nilikwenda uturuki na nimerudi juzi tu"
"baba alifariki mzee"
"unasemaje, amefariki lini na kwanini"
"mi mwenyewe ata sijui mzee wangu"
"mungu amlaze mahari pema peponi rafiki yangu"
"na mama nae ndio kazikwa juzi"
"mungu wangu, mumefanyaje nyie, au kuna mtu kazulumu"
"mzee, mi mwenyewe nina maswali mengi lakini sijui nikujibu vp"
"kwaio sasa hivi unaishi na nani nyumbani"
"nipo na shangazi"
"eeeeee mungu akuseidie tu, soma kwa bidii sheby"
"asante mzee, ila mzee kama utaihitaji hii gari, useme tu maana nahitaji kuiuza mzee"
"sheby, usiuze mali zako mwanangu, zitakuseidia baadae"
"sasa kama hii gari hata leseni yanyewe sina, litakaa ndani tu, nipe milion 30 tu mzee maana bado jipya"
"najua, maana tulienda kununua nae siku hio, nakumbuka alilinunua kwa dhilingi milioni 60,.... Ok nikikupa 30 nitakuonea wacha nikupe 40 sawa"
"sawa mzee wangu"
Nililifanyia mnada pale pale na kuliuza kabisa maana halina faida kwangu, shangazi na mamkubwa ndio hao wanatoana nje kisiri siri,
"ila nakushauri mwanangu, uza vyote lakini usiuze nyuma kabisa, yaani hata mtu akupe kiasi gani usithubutu kuuza nyumba"
"sawa nimekuelewa,"
Basi mtoto wa kiume nilitoka hapo na brifkesi yangu mkononi pamoja na cheki yangu mfukoni... Niliita tax na kunipeleka benki niliweka zile pesa kwenye akaunzi yangu, ambayo mwanzo ilikua na kiasi cha shilingi milion 165 kwahio nilipohamisha hii milion 40 kuja kwenye akaunti yangu, ikasoma shilingi milion 205 nikatoa kadi yangu na kuiweka mfukoni, kisha nikarudi nyumbani
"we sheby ulikua wapi we mtoto"
Alikua ni shangazi ndio aliniuliza swali hilo
Nilifata gari baada ya kuliacha makaburini kule"
"likuapi sasa hilo gari"
"sijaliona, mara niambiwe limeibiwa mara niambiwe lipo kituoni yaani hakuna muelekeo kabisa"
"lakini bora umerudi mzima, maana nilikuacha hospitalini nikamchukua mamkubwa wako na kumpa vigongo vyake, sasa kurudi wodini nikashangaa sikukuti mwanangu"
"usijali nipo hai na hakuna tatizo"
Basi mtoto wa kiume nikapitiliza hadi bafuni nikaoga vizuri kisha nikabali nguo safi, na kutoka sebureni ili kupata msosi, sebuleni nilikutana na mamkubwa akiwa anaangalia tv na wakati huo shangazi yupo chumbani kwa mama kapumzika, na dada fatu nae yupo jikoni....
"shkamoo mamkubwa"
"marahaba ujambo mwanangu"
"sijambo"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"unajiskiaje sasa, hebu njoo nikupakate mwanangu"
"najiskia vizuri tu"
Nilimsogelea mamkubwa huku akionekana kutabasam kwa ajili yangu,
"sasa mwanangu, hii nyumba nataka niipige rangi upya, sasa fundi kaniambia hapigi rangi bila kuona kadi ya nyumba (hati miliki)"
"aaaa okee"
"kwaio nenda kailete ili tupendezeshe nyumba yetu"
"sawa, ipo ndani"
"ipo kweli? Hebu Nenda basi kailete baba ee"
"sawa mamkubwa ila si utairudisha"
"ndio yaani tukimuonesha fundi tu, nairudisha maana ni muhimu sana sawa ee"
"sawa"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment