Chombezo : My Suzan
Sehemu Ya Tano (5)
Kama ungekuwa unawasikiliza jinsi walivyokuwa wanaimba, ungeweza kudhani mle ndani walikuwamo kweli Chris Brown na Jordin Sparks kwa jinsi walivyokuwa wakiwapatia, hakika ilipendeza kwa waliamba kwa sauti nyororo na za kuvutia utafikiri wao ndio walikuwa wenye wimbo… Walivyochoka kuimba walivuta shuka na kujifunika pamoja huku wakiwa wamekumbatiana na haikupita muda walipitiwa na usingizi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************* ********** **********
Ilikua siku ya jumamosi mida ya saa sita mchana ambapo kulikua na hali ya mawingu kiasi pamoja na hali ya kaubaridi kwa mbali, kwakua siku hiyo ilikua weekend, Michael hakwenda kazini, hivyo siku hiyo alipanga atoke out na mpenzi wake Suzan, mida ya saa tisa na nusu Michael pamoja na Suzan walikuwa ndani ya gari aina ya Mercedez benz wakiwa wanaelekea maeneo ya Coco beach kwaajili ya kufurahi na kumzisha akili zao, walikua wamependeza kweli, Michael alikua amevalia body nyeupe na chini alivalia suruali ya jinsi aina ya modo ya rangi nyeusi huku chini akiwa amevaa kiatu aina ya supermax na juu alikuwa kava cape(kofia aina ya chepeo) ya rangi nyeusi, hakika alipeneza sana, kwa upande wa Suzan yeye alikuwa amevaa kitop cha rangi nyeupe huku akiwa amevalia suruali ya rangi ya blue hali iliyofanya umbo lake namba nane lionekane vyema, hakika alipendeza sana, huku chini alikua amevaa viatu vya mchuchumio vya rangi nyeupe jambo ambalo lilimfanya azidi kuonekana mrembo na wa kuvutia zaidi katika mboni za macho za Michael… “Mmmh honey leo umependeza sana yani kama vile beyonce” alizungumza Michael huku akiibia ibia kumuangalia Suzan na muda mwingi alikua makini katika usukani.. Suzan muda huo yeye alikua akitabasamu tuu kutokana na maneno hayo ya mpenzi wake “Thank you honey, ila na wewe umetokelezea kama vile Chris brown” alizungumza Suzan kwa pozi huku akimtazama Michael usoni na Michael alipomtazama Suzan, Suzan alimkonyeza kwa kufunga jicho lake moja la kulia na kulifungua, Michael alitabasamu tuu na kumwambia… “Aaa love! Utoto bana huo” aliongea Michael huku akicheka.. “Ndio utoto kwani unaniona mimi mkubwa?” aliongea Suzan kumwambia Michael Michael alipaki gari pembeni ya barabara na kupandisha vioo vyake ambavyo vilikua na tinted na baada ya hapo alifungua ac (air condition) ya gari na baada ya hapo alimgeukia Suzan na kumwambia… “Babe hebu sogea hapa karibu kuna mdudu hapo kichwani nimtoe” alizungumza Michael akimwambia Suzan, Suzan nae pasipo kua na hiyana alisogea karibu kabisa na mpenzi wake Michael akiamini kwamba ni kweli alikua na mdudu kichwani na Michael alikua akitaka kumtolea, lakini alipokuwa karibu kabisa na Michael alishanga amedakwa shingo yake na hapo Michael alitoa ulimi wake nje kuonyesha kuwa alikua akitaka kubadilishana mate na mpezi wake, nae Suzan bila hiyana aliupokea vyema na kundendeka kwa muda kama dakika tano, hapo Michael alishusha mkono wake na kugusa maziwa ya Suzan kidogo ambapo Suzan alitoa kamguno cha kimahaba, baada ya kuridhika kubadilishana mate na mpenzi wake Michael alishuka katika gari na kumwambia Suzan akae katika usukani, baada ya Suzan kukaa katika usukani Michael alizunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari.. “Haya funga mkanda tuendelee na safari” alizungumza Michael akimuambia Suzan ambae muda huo alikua hajaelewa kwanini Michael alimuachia yeye usukani.. “Kwanini unaniachia nikuendeshe honey?” aliuliza Suzan “Amna nimependa niendeshwe na mpenzi wangu na pia niwe na wasaa mzuri wa kukuangalia jinsi ulivyopendeza” alizungumza Michael jambo ambalo lilipelekea Suzan atabasamu na kufurahi “Mmmmh sawa bana mi sina neno tena hapo” alizungumza Suzan huku akiingiza gari barabarani na safari ya kwenda beach ilianza… Mida ya saa kumi na mbili kasoro, Michael na mpenzi wake walikua maeneo ya Coco beach wakicheza michezo mbalimbali kama wapenzi wafanyavyo pindi wanapokuwa beach, lakini wakati wakiendelea na michezo hiyo Michael machale yalimcheza huku mwili ukimsisimka, kwakua Michael alipitia mafunzo mbalimbali kipindi alipokuwa nchini China alishaelewa nini maana yahali hiyo kutokea, kwamba chochote kibaya kinaweza kutokea kuanzia muda huo, hapo alimchukua mpenzi wake na kwa mwendo wa haraka alianza kutembea nae kwa hatua fupi fupi lakini za haraka akielekea sehemu aliyopaki gari, alifika na kufungua mlango wa gari na kumwambia Suzan atulie ndani ya gari mpaka atakaporudi kwani pale kuna kitu amekisahau maeneo yale waliyokuwa wakicheza, alirushia mlango wa gari na baada ya hapo alirudi kule alipokuwa akicheza na mpenzi wake…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******* ******** ********
Joel kitendo alichofanyiwa na Michael kwa kupigwa na kusababisha jino lake moja kung’ooka alihesabu ni kama kitendo cha kinyama sana ambacho hakuwahi kufanyiwa tangu azaliwe na ndiyo maana akaamua kupanga kuwa lazima amfanyie Michael kitu kibaya ambacho hatokuja kukisahau katika maisha, siku hiyo ya Jumamosi wakati Michael akipita maeneo ya mbezi mwisho na gari lake akiwa amempakia mpenzi wake Suzan kwa safari ya kuelekea beach Joel alibahatika kuliona gari hilo, hivyo aliamua kulifuatilia kwa ukaribu zaidi na mpaka Michael muda ambao anaingiza gari lake katika maegesho ya Coco beach Joel alikua akimfatilia bila ya yeye Michael kujua kuwa anafuatiliwa, alipohakikisha Michael ameshuka na mpenzi wake na kuelekea beach kwaajili ya kuogelea, hapo Joel alitoa simu yake na kubonyeza namba kadhaa ambapo baada ya sekunde chache simu upande wa pili ilipokelewa…
“Hello, njooni maeneo ya Coco beach sasa hivi ili tumalize kazi yetu, hakikisha mnakuja na silaha za kutosha na zana za kutosha za kufanyia kazi” alizungumza Joel na baad ya hapo akakata simu, hazikupita dakika kumi gari aina ya noa ilipaki karibu na gari la Michael huku kukionekana vijana wapatao wanne wakiwa ndani ya gari hiyo huku wakiwa na bastola katika viuno vyao… Wakati Michael akiwa katika harakati za kuondoka eneo lile la Coco beach, Joel pamoja na vijana wake walikuwa wakimtazama na kumfuatilia kwa kila hatua, kipindi ambacho Michael alimleta Suzan katika gari na yeye kurudi kule beach hicho ndicho kipindi ambacho Joel pamoja na vijana wake walikuwa wakikisubiri kwa hamu, kitendo cha Michael kuondoka eneo lile, vijana wawili wa Joel walisogea mpaka eneo lilipokua gari la Michael na walipofika walizunguka upande ambao Suzan ndipo alipokuwa amekaa na kugonga kioo cha upande huo, Suzan alifungua kioo ili kutaka kumsikiliza aliyekua akigonga kioo hicho alikua anashida gani, hilo likawa kosa kubwa kwani kitendo cha kufungua kioo alikutana na mdomo wa bastola ukimtazama usoni, Suzan alishtuka sana na almanusura ajikojolee…. “Toa lock za mlango wa nyuma” mmoja kati ya jamaa wale aliongea kwa sauti nzito na ya kukwaruza.. Suzan kwakua alikua katika hali ya uoga alijikuta akitoa lock za mlango huo wa nyuma, hilo nalo likawa kosa jingine, kwani yule jamaa wa pili aliingia katika mlango huo na hapo Suzan alistuka akiwekewa kitambaa puani na hazikupita hata sekunde tano Suzan alipoteza fahamu kutokana na ukali wa madawa ambayo yaliwekwa katika kitambaa kile, wale jamaa walimbeba Suzan na kumuingiza katika noah waliyokuja nayo na baada ya hapo waliliondoa gari hilo kwa kasi na safari ya kuelekea Bagamoyo ilianza, lakini wakati gari hilo likiondoka kwa kasi eneo hilo Michael nae alikuwa ndo anafika eneo hilo ambapo kwa haraka alipatwa na hofu na kuhisi kuna jambo baya limefanyika hivyo aliliangalia gari hilo kwa umakini wa hali ya juu…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TZ 750 CWK, hizo ndizo namba ambazo alizinukuu Michael katika diary yake ndogo ambayo muda wote alikua akitembea nayo, baada ya kumaliza kunakili namba hizo Michael aligeuka na kuelekea sehemu ambayo alikua amepaki gari lake, kabla ya kulifikia aliona milango miwili ikiwa wazi ilihali wakati anatoka alikua ameifunga na alikua amemuacha mpenzi wake mle ndani, Michael alianza kutembea kwa tahadhari kubwa kuelekea eneo lile ambalo ndipo alipokua amepaki gari lake, Michael alipigwa na butwaa baada ya kutokumuona mpenzi wake Suzan na wakati anaondoka alimuacha kwenye gari, hakika alipagawa, alivuta pumzi kwa nguvu na kuzitoa taratibu jambo ambalo lilifanya arudi katika hali yake lakini bado alikua na kitete, alivyoangalia vizuri katika siti aliyokua amekaa Suzan hapo alikiona kitambaa, alikichukua na kukikagua na kutokana na ujuzi aliokua nao aliweza kutambua kuwa kitambaa hicho kilikuwa kimewekwa dawa ya usingizi, hapo alishusha pumzi ndefu na baada ya hapo alibonyeza kitufe kidogo kilichopo katika dash body ya gari na baada ya sekunde kadhaa kiscreen kidogo mfano wa tv kilitokea kwa upande wa dereva, hapa alibonyeza kitufe ambacho kiliandikwa play na baada ya muda kile screen kikaanza kuonyesha matukio yaliyotokea…. “Oooh shiit!!” alizungumza Michael baada ya kuona tukio la kutekwa kwa Suzan lilivyokuwa, alitoa ili diary na kuangalia ile namba ya gari aliyoinakili, Michael alipoinua macho yake na kutazama mbele aliona kuna kijana ambae alikua akimuangali kwa kuibia ibia huku akibonyeza bonyeza simu yake, Michael alimtilia wasiwasi, hivyo alishuka katika gari lake na alipo hakikisha milango ameifunga vizuri alianza kusogea eneo ambalo alikuwepo yule kijana, lakini wakati amekaribia kufika lile eneo, yule kijana alikurupuka na kuanza kukimbia, Michael kwa kasi ya ajabu alichomoka kama mshale na baada ya hatua kumi tuu alimkaribia yule kijana.. “Tiii!!” ndicho kishindo kilichotokea baada ya Michael kumpiga ngwala yule kijana, na kabla hajakaa sawa ngumi nzito ilitua katika shingo yake hali iliyomfanya apoteze fahamu, Michael aliangalia kushoto na kulia na kuona hakuna mtu ambae alikua akimfuatilia, hapo alimbeba yule kijana ambae alikua hana fahamu na kuelekea nae sehemu ambayo alikua amepaki gari lake, baada ya kufika sehemu ambayo alikua amepaki gari lake alienda mpaka sehemu ya nyuma ya gari ambapo alifungua buti na gari na kumuweka yule
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kijana na baada ya hapo alilifunga buti la gari na kuingia katika usukani na safari ya kuelekea kwake ilianza. Mida ya saa mbili kasoro usiku Michael alikua akipaki gari lake katika nyumba yake ya siri ambayo ilikua maeneo ya kigamboni, kutokana na uzio kuwa mkubwa hakuna aliyejua ni kitu gani kimejengwa ndani ya uzio huo, ni Michael na Suzan pekee ndie waliokuwa wanajua eneo hilo, Michael alimtoa jamaa yule na kumuingiza katika chumba kimoja ambacho kilionekana ni chumba cha mateso kutokana na vifaa vilivyo kuwa humo ndani, hapo Michael alimkalisha yule kijana katika kiti ambacho kilikua kimesimikwa humo ndani na kumfunga kwa vyuma maalum vilivyokua katika kiti hicho,baada ya hapo michael alitoka na kufungua geti la jumba hilo la siri, alipotoka alielekea katika duka la karibu na kununua kiberiti cha gesi baada ya kununua alipita kwa street venders(machinga) na kununua taulo na baada ya hapo alirejea katika jumba lake na kuingia katika chumba ambacho alimfunga yule kijana, aliingia na kumkuta yule kijana bado amepoteza fahamu, alitabasamu kisha akachukua maji ya baridi ambayo aliyatoa katika fridge na kumwagia yule kijana, kijana yule alikurupuka na kutaka kukimbia lakini juhudi zake hazikufua dafu kutokana na vyuma ambavyo alikuwa amefungwa… “Tulia usiwe na papara, kuwa mpole” alizungumza Michael kwa sauti ya kukoroma Almanusra yule kijana azimie, nah ii ni baada ya kumuangalia aliyekua akimsemesha na hapo alikutana na mtu ambae alikua kavaa kininja, hakika alipagawa na asielewe mtu huyo ni nani. “Kupona kwako wewe ni kunijibu maswali yangu kwa ufasaha” alizungumza Michael kwa sauti ya kukoroma na yenye kitetemeshi kikubwa
“U… uu..likuwa un…a…se….m…a.je” alizungumza yule kijana kwa sauti iliyojaa woga “Unaweza ukaniambia mwanamke mliyemteka maeneo ya Coco beach mmemteka kwasababu gani?” alizungumza Michael kwa sauti isiyokua na masihara “Aaah!! Mimi sijui, unazungumzia kuhusu nini?” alijibu yule kijana kwa sauti kavu “Okay hamna tatizo.” Alizungumza Michael kwa sauti ya kukwaruza huku akiwa katika vazi la kininja kumaanisha kwamba alikua tayari kwa vita ambayo ipo mbele yake kwaajili ya kumtafuta mpenzi wake, alifungua kibox kidogo ambacho kilikua mezani na hapo alichukua kile kiberiti cha gesi alichonunua, alimsogelea kijana yule na kukiwasha kile kiberiti, alikisogeza mpaka karibu kabisa na uso wa kijana yule na hapo alimuuliza tena.. “Una hakika haujui ninachozungumzia? Aliuliza Michael kwa sauti ya ghadhabu.. “Ndio sijui unachozungumzia!!” alizungumza yule kijana kwa sauti ya kufoka, na hapo alicho kifanya Michael alikizima kile kiberiti, alichukua taulo alilokua amelinunua kwa machinga na kumfunga nalo yule kijana usoni na baada ya hapo alichukua maji ya baridi na kuanza kuyanyunyiza taratibu katika taulo lile, kadri muda ulivyokua ukienda ndivyo yule kijana alivyozidi kupata tabu katika upumuaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. “Koh koh koh..” alikohoa yule kijana baada ya kuona anaweza akapoteza maisha kizembe ingawa alikua hana hakika sana kama atatoka salama katika eneo hilo ambalo mpaka mda huo alikua hajafahamu eneo hilo liko wapi, Michael aliendelea na zoezi hilo na aliporidhika alilitoa lile taulo usoni mwa yule kijana “Koh koh koh” alikohoa yule kijana huku akitapika maji ambayo aliyanywa kipindi ambacho taulo lilikua usoni mwake “Nafikiri sasa unaweza ukaniambia kwanini mlimteka yule binti kule maeneo ya Coco beach” alizungumza Michael katika hali ya utulivu “Tulimteka kwasababu tuliagizwa na boss wetu.” Alizungumza yule kijana huku akipumua juu juu “Huyo bosi wenu ni nani?” aliuliza Michael “Ni Joel, yule muhasibu msaidizi katika benki ya CRDB tawi la Posta.” Alijibu yule kijana “Wewe unaitwa nani?” aliuliza tena Michael “Naitwa James, ni mdogo wake na Joel tafadhali usiniue!” alizungumza yule kijana aliyejitambulisha kwa jina la James katika hali ya uoga hasa alipomtazama mtu huyo aliyekua akimuhoji akiwa ndani ya vazi la watu hatari duniani, yani maninja.. Michael moyoni mwake alifurahi sana baada ya kuona kuwa alikuwa amemshikilia mdogo wa adui yake mkubwa Joel na aliapa kuwa kitu atakachomtendea Joel hatokuja kukisahau katika maisha yake.. “Mlivyomteka mlimpeleka wapi?” Michael alimuuliza James.. “Wamempeleka katika pori la Bagamoyo na huku ndipo ilipo kambi ya siri ya kaka Joel kwaajili ya kufanyia mambo maovu” alizungumza James kwa kirefu “Okay sawa wasalimie kuzimu..” alizungumza Michael na hapo alichomoa jambia lake la kininja ambalo alikuwa ameliweka mgongoni kwake na hapo alitenganisha kichwa na kiwiliwili cha mdogo wake Joel, Michael alishaamua kurudi katika hali yake ya zamani hali ya kuwa na roho ya kikatili, na hapo hakuna kingine alichokua akiwaza zaidi ya kuua tuu, aliubeba mwili wa James ambao ulikua hauna kichwa na kwenda kuutupa katika bwawa la mamba ambao alikua akiwafuga humo ndani na baada ya sekunde kadhaa James alikua tayari ameshaliwa na mamba wale, Michael baada ya kumaliza zoezi hilo alirudi mpaka katika kile chumba cha mateso na hapo alikichukua kichwa cha James na kukinyunyiza dwa flani hivi ambayo ilisababisha damu iliyokua ikitoka kuganda, baada ya hapo alikiweka kile kichwa katika mguko wa rambo na kukiingiza katika box na kulifunga box hilo vizuri, baada ya kulifunga vizuri box hilo, alilibeba na kwenda kulipakia katika buti ya gari, alirudi ndani na kuchukua silaha zake za kininja na kuingia kwenye gari ambapo safari ya kwenda katika pori la Bagamoyo kwenda kumuokoa mpenzi wake ilianza… *********** ********* *********** Mida ya saa tano kamili katika pori la Bagamoyo kulikua na vijana ambao walikua wakibishana kuwa nani aanze kumbaka mwanamke ambae alikua amepoteza fahamu huku akiwa amefungwa kamba katika mikono yake na miguu yake, naam hao walikua ni vijana wa Joel wakiwa wanabishana juu ya nani aanze kumuingilia Suzan ambae kwa muda huo alikuwa amepoteza fahamu na wakati huo Joel alikuwa yupo ndani ya jengo lililoonekana la kisasa katika pori la Bagamoyo mahali ambapo Suzan ndipo alipokua na hata amri ya kubakwa kwa Suzan ni yeye ndiye aliyeitoa, wakati huo yeye alikua amejilaza katika sofa lililokuwa sebuleni huku akitazama runinga aina ya flat screen nchi 32, muda wote ambao vijana wake walikua wakibishana juu ya nani aanze kumbaka Suzan yeye alikuwa akiwasikia vyema na alikua akitabasamu huku akiamini kwamba muda mchache ujao atakua amemvurugia Michael maisha yake kwa ujumla. Wakati vijana wale wakiendelea kubishana, ghafla walianza kuona upepo ukivuma kuelekea sehemu ambayo walikuwepo na wakati wakitahamaki kufunga na kufungua vijana nane tayari walikua wapo chini huku miili yao ikiwa haina uhai, hivyo kufanya idadi ya vijana wale kubaki wanne ambao nao ndani ya sekunde kumi, miili yao ilikua haina uhai, naam alikua ni Michael akiwa katika vazi jeusi la kininja huku mkononi akiwa kashika upanga wake wa kininja na vijana wale kumi wote aliwauwa kwa kuwachinja, baada ya kumaliza vijana wote, alirudi mpaka katika kichaka kimoja na kubeba lile box ambalo ndani yake kilikuwepo kichwa cha James ambae alikua ndie mdogo wa pekee wa Joel, alienda kukihifadhi sehemu salama kisha akaenda eneo ambalo mpenzi wake alikuwa amefungwa na alipofika alimpatia huduma ya kwanza na baada ya nusu saa Suzan alirejewa na fahamu.. “We ni nani?” aliuliza Suzan katika hali ya uoga baada ya kumuona mtu akiwa kavaa kininja “Ni mimi mpenzi wako, vipi unaendeleaje?” alijibu Michael huku akitoa kofia ya kininja kichwani mwake na sura yake ikaonekana vyema “Haa!! yani kumbe wewe ni ninja mpenzi, na kwanini ulinificha juu ya jambo hilo?” Suzan alishangaa na kuuliza katika hali ya masikitiko
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haina haja ya kuwa na hofu, sasa hivi yakupasa urudi nyumbani, mimi kuna jambo bado namalizia huku, tutakuja kuongea nyumbani, sawa mpenzi?” “Sawa mume wangu nimekuelewa, sasa nyumbani narudije?” Suzan alikubali kurudi nyumbani na kumuuliza Michael ni njia gani atatumia kurudi nyumbani “Usijali kuna gari ile pale nimekuja nayo, wewe nenda mimi nitakuja kesho” aliongea Michael huku akimuinua mpenzi wake na kumpeleka sehemu aliyoficha gari lake, na alipohakikisha Suzan ameshakaa katika usukani, alimbusu na kumtaki safari njema na hapo Suzan safari ya kwenda nyumbani Mbezi ilianza na muda huo ilikua yapata saa kumi na moja kasoro alfajiri.. ********** ************* ********** Mida ya saa kumi na mbili kamili asubuhi Joel aliamka katika chumba chake lakini alishangazwa na ukimya uliokuwa katika eneo lile, alipochungulia dirishani almanusra azimie, aliwaona vijana wake wote wakiwa wamekufa tena kwa kuchinjwa kama kuku, hakika alipagawa sana, alikurupuka na kuelekea sebuleni na hapo alipiga mueleka na kuinuka na kabla hajatoka nje alikuta kuna box limetengwa katika meza ya chakula, alilisogelea lile box kwa tahadhari akidhani kwamba ni bomu, alipolifungua alijikuta anakaa chini kutokana na miguu kushindwa kuhimili uzito wa kiwiliwili, aliona kichwa cha mdogo wake James huku pembeni pakiwa na kikaratasi ambacho kilionekana kuwa na ujumbe “Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti, na hiyo itakua zawadi yako ya mwisho kuiona katika dunia, nipo nje nakusubiri uje nikupe tiketi yako ya kwenda kuzimu, karibu sana” hivyo ndivyo ujumbe ulivyosomeka, Joel alipatwa na hasira kupita kiasi alisimama na kuelekea chumbani kwake ambapo alichukua bunduki yake aina ya SMG(Sub machine gun) ambayo ilikua ina risasi thelathini, aliikoki vyema na kisha kutoka nje, alivyotoka alikutana na mtu akiwa kasimama huku amempa mgongo, alichokifanya ni kuruhusu risasi mfululizo zitoke katika bunduke kuelekea upande aliokua yule mtu, lakini mpaka risasi zimeisha katika bunduki yule mtu alikua bado kasimama vile vile, ilibidi asogee mpaka eneo alilokuwa yule mtu na hapo alipigwa na butwaa baada ya kugundua kua alikua akimimina risasi kwenye kifusi cha majani ambacho kilitengenezwa na kuvalishwa vazi la kininja na huo ni moja ya uchawi ambao maninja hua wanatumia katika mapambano, wakati akitafakari alisikia sauti kutoka nyuma… “Hello Mr Joel, nafikiri ni muda muafaka wa wewe kwenda kuzimu” alikua ni Michael akiwa katika vazi la kininja huku akiwa amening’iniza upanga wake mgongoni Kwakua Joel alikua anahasira na mtu aliyemuua mdogo wake alijizoa pale chini na kuja kwa kasi sehemu ambayo yule ninja alikua amesimama, lakini kabla hajafika, kwa kasi ya ajabu yule ninja aliruka flight kick iliyotua vyema kwenye kifua cha Joel na kumrusha umbali wa sentimita kadhaa, na hapo joel alikua hawezi tena kusimama kutokana na pigo hilo, na kujikuta akiuliza.. “Wewe ni nani? na kwanini unafanya hivi?” aliuliza Joel huku akiwa katika maumivu makali “Naitwa Michael na huo ndio mshahara wa dhambi zote ulizozifanya” alizungumza Michael sambamba na kufua uso wake Joel alipigwa na butwaa baada ya kumuona Michael “Ni….n..i w..e…we. mwana..ha..r…” kabla Joel hajamalizia kauli yake upanga ulitua katika shingo yake na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, na hapo ndipo ukawa mwisho wa Joel “Watu kama ninyi hamstahili kuishi katika dunia hii ya watu wema” alizungumza Michael na kufunika uso wake kwa kofia ile ya kininja nahapo akaonekana kuwa full ninja, hapo alirudisha jambia sehemu yake na kuanza kutafakari jinsi ya kurudi nyumbani “Jamani muuwajiiiiii!! Muuuwajiiii!! Uwiiiiiii jamani wanakijiji!! muuwajiiiii!!” ni sauti ambayo ilimgutua Michael katika mawazo, walikuwa ni kuna mama watano wakiwa wamebeba majembe wakielekea shambani na hapo walijikuta wakipiga kele hizo baada ya kumuona Ninja akiwa amezungukwa na miili kadhaa ambayo ilikuwa imetenganishwa na vichwa vyao, Michael baada ya kuona hali hiyo akajua tayari lishakua tatizo hivyo alichokifanya ni kutupa bomu la kininja na baada ya sekunde kadhaa alitoweka eneo lile kimuujiza… Dakika nusu saa baada ya Michael kutoweka eneo, wanakijiji walikuwa wamefurika eneo la tukio na hazikupita dakika tano, ambulance tano pamoja na defender nne za polisi ziliwasili eneo la tukio, miili ilipakiwa na kwenda kuzikwa na halmashauri kutokana na ndugu wa marehemu kukosekana licha ya kutangazwa zaidi ya wiki nzima katika vyombo vya habari ************ ************* *************** Zilikatika siku,wiki na hatimae mwaka kupita huku Michael akiendelea vizuri na kazi zake katika benki ya CRDB tawi la posta, Suzan nae alizidi kunawiri na kunekana mpya mbele ya mboni za Michael kila siku, baada ya miaka miwili kupita Michael alipandishwa cheo na kuwa maneger wa benki hiyo ya CRDB tawi la posta kufutia kustaafu kwa Mr Alex ambae umri ulikua umeenda na aliomba kustaafu, ilifanyika tafrija fupi na hapo ndipo Michael aliamua kumvisha mpenzi wake Suzan pete ya uchumba huku zoezi zima likisimamiwa na Mr Alex ambae alimchukulia Michael kama mwanae. Ilikua imepita miezi miwili tangu Michael amvishe pete ya uchumba mpenzi wake Suzan, katika kanisa moja jijini Dar es salaam, Michael na Suzan walikua katika madhabahu huku mchungaji akiwafungisha ndoa, baada ya zoezi la kufunga ndoa kukamilika ambalo lilikua chini ya Mr Alex, Michael alikabidhiwa kipaza sauti ili aweze kuongea neno la mwisho…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndugu waumini wenzangu, napenda niwashukuru kwa wote mliohudhuria katika sherehe hii na kuhakikisha kijana wenu nakamilisha zoezi hili la kufunga ndoa, shukrani za dhati ziende kwa baba yangu mlezi Mr Alex kwa kuwa na mimi katika kila hatua ya maisha yangu, sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa Mungu kila la heri, shukrani zangu zingine ziende kwa mke wangu mpenzi kwa kuwa nami na kuhakikisha nasimama imara katika misukosuko yote na changamoto zote nilizokumbana nazo katika maisha, hakika “You’re my real SUZAN” Michael alizungumza kwa hisia na kanisa zima likafurika kwa shangwe huku wakisema “YES SHE DESERVES TO BE YOU’RE SUZAN”. Michael alimchukua mke wake na kuelekea nyumbani kwake Mbezi ambapo waliendelea na maisha yao kama kawaida na baada ya mwaka mmoja kupita walibahatika kupata mtoto wa kiume na walikubaliana kumuita “ZAWADI” wakiwa na imani kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu, kwapamoja walipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania mpaka hapo walipofikia.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment