Search This Blog

Thursday, 24 November 2022

RATIFA & MWAJUMA (2) - 3

     

     

     



     

    Chombezo : Ratifa Na Mwajuma Season 2

    Sehemu Ya Tatu (3)

     

    Tulipoishia

    Jana

    Mama aliongea ghafla nikasikia

    Sauti ya kishindo kizito ikisika kutokea ukumbini

    Ikifwatiwa na sauti ya Nasra akiita Mamaaaa....

    Nilikurupuka na kutoka ndani mbio mbio

    Kufika ukumbini nilimkuta mama kalala chini

    Damu zikimtoka puani mdomoni na masikioni. Damu ilikuwa ikitoka kwa wingi

    Pale pale nikapotea......

    SONGA NAYO

    SASA

    Baada kupotea pale na kumuacha Mama yangu akiwa kalala pale chini huku damu zikimtoka nikaja kuibukia kwenye moja kati ya njia panda. Nikasimama hapo, niliangaza macho huku na kule ghafla nikaona michirizi ya damu ikipita kwa kasi utasema mfereji wa maji machafu uliofunguliwa baada vua kunyenyesha. Sikutaka kujiuliza sana kuhusu hiko nikionacho

    Nikainama na kuishika ile damu. Nikafanya kama kuikata mfano wa kukata kamba huku nikiongea Lugha za ajabu ajabu, ile damu ikarudi ilipotoka kwa kasi ileile niliyangalia kwa muda kisha nikapotea na kuibukia pale pale ukumbini

    Nilimkuta Nasra akihangaika kumwita

    “Mamaaa jamani mama yangu mimiii hiiiiii.

    “Nasra nini kimetokea?"

    Niliuliza huku nikiinama na kumshika Mama kichwani.

    “mi hata sijuiihiiiiii"

    “basi nyamaza usilie embu nenda kalete maji"

    Akainuka na kwenda kuleta maji hapo nikafanya kumpulizia kitu kwenye mdomo wake

    Mpaka akapiga chafya na kufumbua macho.

    “vipi mbona Niko hivi nini kimenitokea?"

    Mama aliuliza swali

    Sikumjibu kitu nikapokea kikombe cha maji na kumnywesha kisha nilimnyanyua na kwenda kumkalisha kwenye sofa pale sebuleni.

    “Vipi unajisikiaje na hali ewe Mama yangu?"

    “uwiii nahisi shingo inaniuma tu kwani nini kimenitokea?"

    “kiukweli hata sisi wenyewe hatujui sema tulishtushwa na sauti ya kishindo baada wewe kudondoka pale ukumbini"

    Nilimjibu huku Nasra nae akionekana kutaka kuongea kitu

    “sio hivyo kaka Mimi nilimuona mama akikugongea hodi wewe ghafla kuna mtu akatokea nyuma ya mama na kumpiga mtama!"

    “what? Nasra unasema kweli?"

    “ndiyo kisha yule mtu akapotea"

    “huyo mtu yukoje?"

    “sikuweza kumuona vizuri"

    “Wanangu"

    “naamu mama"

    Wote tuliitikia kwa moja mimi naamu Nasra abee.

    Mama akatungalia kwa zamu kisha akasema

    “kiukweli sitoacha kuwaambia kuhusu hiki niwaambiacho kiukweli sitoweza kuliona Jua la kesho,"

    “hapana Mama hutakiwi kuongea hivyo hiyo ni kufru kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu usijiombee kifo!"

    “Hafidhii"

    Nilipomwambia maneno hayo Mama akaniita na kunishika kwenye paji langu la uso

    “Naamu"

    “bila shaka utakuwa unafahamu kila kitu kuhusu matatizo haya tambuwa wewe si mtoto tena. Tuseme utakaa na kuanza kulia wakati familia yako inateketea. Nina Hakika utasimama imara na kupambana kiume

    Kuitetea familia yako!"

    “ndiyo mama sitoweza kukuacha tena nitasimama kushotoni na kulia kwako kuhakikisha nakulinda kwa gharama ya aina yeyote ile.

    Futa machozi usilie teenaa"

    Mwishoe tulikumbatiana kwa kupeana faraja

    Nilirudi chumbani kwangu na kupaza sauti kumwita Gogisu

    “Gogisuuuu"

    Ghafla nikaziba mdomo baada kujishtukia nimesikiwa huko nnje, kumbe sivyo

    Gogisu alikuja kwa heshima na taazima akapiga magoti kitendo cha kumwita vile alishafahamu nimekasirika.

    “Gogisuu"

    “naamu mkuu"

    “kwanini mlitaka kuniulia mama yangu?"

    “hapana sio sisi mkuu"

    “kama sio nyinyi kumbe ni kina nani?"

    “angalia pale ukutani"

    Niligeuza kichwa changu na kuangalia upande wa ukutani kulikuwa na kama tv aina protecta

    Niliikazia macho hapo ndipo nilipoweza kuona kikundi kingine kabisa cha Majinni kwa wachawi wakichezacheza na kuimba huku wakinywa damu pamoja na kula nyama mbichi.

    “ni kina nani hawa?"

    “hao ni Majinni ya Dar es salaam ni moja kati ya jamii hatari sana, kama uwonavyo mkuu"

    “unataka kusema kila Majinni wanakuwa na mikoa yao kama vile

    Makabila?"

    “ndiyo mkuu sema Majinni wote tunaongozwa na Lusifa"

    “Lusifa ndiyo nani?"

    “ni kiongozi wa Majinni wote!"

    “khaa! Sasa mbona kama unanichanganyia mada Mara mimi ndiyo kiongozi wenu mara Lusifa sasa niwaelewe vipi?"

    “kiukweli mkuu wewe ndiyo ni kiongozi tuseme kama Rais wa nchi si anakuwa na mawaziri wake sijui Wabunge madiwani na wengineo. Na kwetu ndiyo hivyohivyo!"

    “sasa mimi Mjumbe mwenyekiti au

    Nani?"

    “Mh! Mkuu mbona una maswali mengi hivyo?"

    “kudadeki jibu maswali sio kuuliza swali kwanza nahitaji kuonana na huyo Lusifa haraka iwezekanavyo"

    “hiyo haiwezekani mkuu"

    “kwanini isiwezekane yeye ni kama

    Nani katika dunia hii? Sasa iwe isiwe utanipeleka tu"

    “tatizo lako mkuu wewe unataka kulazimisha kufanya vitu ambavyo haviwezekani kamwe"

    “basi potea kuanzia leo sihitaji msaada wa mtu yeyote yule

    Kwanza nitaanza na hawa Kenge kisha nitadiri na huyo Lusifa sijui misifa"

    Niliongea kwa kujiamini nikatoka nnje nilitaka kupitia mlango wa uwani nikasita na kutokea mlango wa mbele. Hakika sikutakiwa kutulia kabisa nilitaka kufanya mambo yangu kwa haraka mno.

    Nilitembea mpaka sehemu ambayo kulikuwa na nyumba yenye Gorofa tatu ilikuwa ni nyumba nzuri iliyozungushiwa ukuta na kuwekwa Geti jeusi

    Niliizunguka ile nyumba na kujisemea imejengwa sehemu ambayo haikustahiri kuwepo hapo. Nikaenda kubisha hodi getini

    Dakika si nyingi mlango mdogo wa getini ukafunguliwa mlinzi wa Kimasai akachungulia kwa kutokeza kichwa

    “halloo wee mukijana taka nini saa hisi?"

    “Ahaa Masai mbona umeanza na maswali kabla ya salamu kaka!"

    “sina muda wa salamu embu elesea sida yako"

    Wakati anaongea mimi nikakuna kichwa nikifikiria sijui nimwambie nini

    Ghafla tukashtuka baada mlio mkali wa honi kutishtua nyuma yetu

    “embu pisapisa Bosi apate kupita"

    Aliongea na kufanya kunisukumiza kisha akafungua Geti

    Nilikaa pembeni na kuikodolea macho Gari iliyokuwa ikiingia ndani kwa kupita mbele yangu

    Nilipigwa na bumbuwazi baada ya macho yangu kukutana na sura ngeni mfano wa Malaika

    nae kama alishikwa na mshtuko fulani

    Akaniangalia huku gari ikiseleleka kuingia ndani.

    “ohoo Shit!"

    Nilijisemea hivyo na kuanza kuondoka eneo hilo

    “pseee! Wee mukijanaa"

    Nilimsikia yule Mmasai akiniita kwa kunipigia uruzi niligeuka kumtazama akanipungia mkono kuwa nimfate nikaenda kumsikiliza

    “oyaa unasemaje Yero?"

    “tulisa msuka basi nimeongea na Bosi kasema nikwite sasa usisahau kunipa hata ya soda"

    “kwenda zako huko unataka pesa ya soda kivipi?"

    “psiiiiii"

    Wakati naongea na mlinzi sauti ya

    Kuita ikasikika wote tukageuka na kutazama

    “embu nifate"

    Mlinzi aliniambia hivyo huku akiongoza njia. Nilianza kumfata mpaka tukafika sehemu ya kupaki Magari kulikuwa na yule Mrembo uzuri wake sijui niufananishe na nani. Nilishakutana na wanawake wakila aina sijui

    Mwajuma, Janeth, Ratifa, na wengineo hasa niliokuwa nikicheza nao Movie za ngono. Ni wengi aisee, lakini wako tofauti na huyu nimuonae mbele yangu. Nahisi nikianza kutaja sifa zake

    Wino utaisha na hata Daftari halitotosha maana ana sifa kemkemu

    Labda niandikie juu ya bahari.

    “Mambo vipi?"

    Jamani jamani hiyo sauti yake sasa mpaka nikahisi mwili ukinisisimka kwa raha.

    “Saengo huyu mtu wako ni kiziwi au?"

    Aliongea kumuuliza yule Mlinzi baada kuona nimekaa kimya pasipo kuitikia salamu yake.

    “hei Bosi salimia wewe mbona nauchuna?"

    “ahaa powa tu sister mambo vipi?"

    Nilikurupuka kuitikia baada Mlinzi kuniuliza

    “unaonekana una mawazo mengi sana kichwani

    Saengo embu muonyeshe kazi za kufanya kisha uingie naye ndani kwaajili ya makubaliano"

    Aliongea yule binti

    Akatembea kuelekea ndani hiyo tembea yake utasema Miriam Odemba

    “Sikia visuri kijana hii ndiyo ndoo ya kubebea takataka ukisamaliza kufagia koote kwa kuizunguka nyumba hii. Utafyeka majani na kumwagilisia maji"

    Nilimsikiliza tu Jinsi mlinzi wa kimasai

    Anavyonipatia maelekezo.

    “nasani umenielewa?"

    “ndiyo Bosi"

    “mimi apana ita bosi wakati bosi yenyewe ingia ndani sasa twende!"

    Tukaingia ndani mpaka Sebuleni ajabu hatukumkuta yule Mrembo zaidi ya Mama mtu mzima mwenye Asiri ya Kitasha.

    Nikamsalimia kwa heshima, nikakaa kwenye sofa pasipo kuambiwa nikae.

    Soengo wewe waweza kwenda kuendelea na kazi zako!"

    Aliongea yule Mama kumwambia mlinzi nae akatoka akiniacha mimi nikikodoa macho kwa kutalii pale Sebuleni hakika ilikuwa ni sebule nzuri sana yenye kuvutia.

    “ehee kijana unaitwa nani?"

    “James Jangoro ndiyo jina langu"

    “elimu yako?"

    “kidato cha nne"

    Nilimjibu hivyo baada ya hapo nilipatiwa mkataba wa kazi usitake kushangaa

    kazi ya Ushamba boy kuwa na mkataba. Kiukweli kabisa ujio wangu katika nyumba ni kwaajili ya jambo moja tu. Si lingine bali kuhakikisha

    Nampeleka kuzimu Bwana Suliya ni mmiliki wa nyumba hiyo usitake kufahamu kisa cha kutaka kumuuwa kama unawakumbuka

    Wahusika wa mauaji ya Baba yangu.

    Nilitoka ndani ya nyumba hiyo pasipo kumuona tena yule kimwana, nilitamani nimuone hata kwa sekunde mbili ikashindikana

    Nikarudi nyumbani na kumkuta mama akiwa anapika chakula cha usiku. Nilimsalimia na

    Kuingia ndani sikutaka kumwambia mama kuwa nimepata kazi, nilifahamu bila shaka ataniuliza maswali mengi tu.

    Nikakaa sebuleni nikawasha tv niliangalia kidogo tu nikaizima nikanyanyuka na kuingia chumbani kwangu. Nilipoingia chumbani tu nilianza kuhisi kichwa kikiniuma vibaya mno, nikaanza kuyumba huku nimejishika kichwani

    Kila sekunde iliyokuwa ikienda mbele ndipo maumivu yakazidi kuongezeka kwa kasi

    Nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada lakini sauti yangu haikutoka

    “mkuu pambana usizubae pambana. Huyo anataka kukuuwa"

    Ilikuwa ni sauti ya Gogisu akiniambia hivyo pale pale nikajivika taswila ya Kishetani na kujionea vitu vya ajabu vikitendeka ndani ya chumba changu

    Kulikuwa na Majinni takribani

    Kumi na saba baadhi yao walikuwa wapo kitandani kwangu wakifanya matendo ya Sodoma na Gomora

    huku wengine wakiwa wanashangilia

    mmoja alikuwa kanishika kichwani kwa kunibana. Sikutaka kuwauliza nikaongea Lugha ya kubadirika nikachenji mavazi.....





    -----------------

    Tulipoishia

    Jana

    Nilipoanza kubadirika vile viumbe wakaacha kila kitu walichokuwa wakikifanya mule chumbani na kuniangalia mimi. Kwa hali ya uwoga fulani,

    nilikuwa tayari nimekamatia fimbo aina ya

    Mkia wa taa, baadhi ya Majinni waliwahi kukimbia wale waliozubaa ikala kwao nilitembeza kichapo walipiga kelele kutokana na maumivu makali wayapatayo.

    Vilio ambavyo ni Mimi pekee ndiyo niliyeweza kusikia. Walijaribu kutaka kunizuia lakini wakashindwa mmoja kati ya Majinni akanirukia na kutaka kuninyonya damu.

    Nilimdaka na na kumbamiza ukutani akapotea.

    Ikawa kama kawaambia wenzake wote tukimbieni.kufumba na kufumbua wote walishasepa.

    Nilikaa kitandani nikiwa nahema huku hali yangu ikirejea kuwa kama awali dakika si nyingi nikatoka nnje na kwenda kukaa kwenye mkeka

    Sehemu ambayo Mama alikuwa kakaa yeye na Nasra wakicheza karata.

    “vipi hii last card au

    Albastini?"

    Niliuliza huku nikijiweka vizuri ili namimi niweze kucheza.

    “makonzi"

    “duhuu kumbe makonzi?"

    “ndiyo unacheza au?"

    “haya nacheza"

    Basi karata ziligaiwa tukaanza kucheza"

    “kiukweli kila nikiwaangalia wanangu basi nakumbuka mbali sana. Kipindi ambacho tulikuwa tukiishi kule nyumba ya juu

    Siku ambayo ilitokea ajali ya moto na kuambiwa kuwa Mwanangu kipenzi Hafidhi amefariki kwa ajali ya Gari niliumia sana mpaka kufikia hatua ya kupoteza fahamu zaidi ya Mara tatu.

    Sema nilikuja kupata nguvu baada Shekhe Ally aliponiambia kuwa Mtoto wako hajafa bali kachukuliwa kwa muda tu

    Na kikundi cha Mashetani ipo siku isiokuwa na jina tarehe mwaka wala mwezi mwanao atarudi. Japokuwa nilipata nguvu kwa kuniambia

    Hivyo sema sikutaka kuamini moja kwa moja kuhusu kauli yake kwani nilikusubiri kwa muda mrefu sana mpaka siku Ambayo Dada yako akachumbiwa na kuolewa bila wewe kuwepo. Siku zote harusi ni jambo la kheri ni siku ya furaha kubwa lakini ilikuwa tofauti kwa upande wetu ilikuwa ni majonzi na vilio.

    Nikaja kupata pigo lingine baada Shekhe Ally kufarik,

    “Mamaaa"

    “Abeee mwanangu"

    “unataka kusema kumbe Shekhe Ally amefariki?"

    “ndiyo tena yapata takribani miaka minne sasa"

    “uhuu mama umejinyea"

    Nasra akapiga kelele kwa kushangilia baada kuona makonzi kwa Mama nilibaki kucheka tu. Maana matendo na vituko vya Dada utasema mtoto mdogo

    Basi karata zikachangwa na kulazwa pale chini.

    Kila mmoja na kifungu chake

    “haya chagua"

    Yani Dada alikuwa na kimuhemuhe cha kumpiga makonzi mama tena yale

    Makonzi ya kubinjua mfupa na kuchovya mchanga

    Akachagua kwangu zungu,

    Nasra akanicheka ikawa zamu yake naye zungu akanuna

    Hakika tulizidi kufurahi huku mama akitusimulia hili na lile pia aliniambia kuhusu kifo cha

    Bibi ambaye ni Mama yake kama unakumbuka ndiyo ambaye nilijua ni yeye mwenye kunitokea usiku.

    Tukaingia ndani na kukaa sebuleni

    Chakula kikapakuliwa tukala na kwenda kulala.

    Ndani ya usiku huo hali ilikuwa shwari kabisa hakuna chochote kibaya kilichoweza kutokea.

    Kesho yake asubuhi na mapema niliamka nikafanya mazoezi mepesi

    mepesi na kumuaga mama kuwa natoka kidogo.

    “unaenda wapi tena asubuhi yote hii?"

    “kazi mama"

    “kazi imefanyaje?"

    “naenda kutafuta kazi ewe mama yangu"

    “sawa baba lakini ulihitajika upumzike kwanza. Kwani ni muda mrefu tokea uwondoke,

    Umerudi juzi juzi tu hata kupumzika hujapumzika, leo hii uingie kwenye pilikapilika kweli"

    Mama aliongea huku akiweka fagio pembeni na kuja kuchukuwa ndoo ya maji.

    “mmh!

    Niliguna pasipo kuongea kitu nikapiga hatua za taratiibu na kuondoka nikimuacha mama akiingia chooni nilitembea kwa mwendo wa haraka

    Nikafika kwenye ile nyumba ambayo jana yake nilikuja kuomba kazi.

    Nikabisha hodi pale Getini mlinzi akafungua mlango

    “mambo vipi Masai?"

    “powa aisee mbona umeselewa sana?"

    “huu sio muda wa kuulizana maswali

    Embu nipishe tusije kualibiana kazi"

    Niliongea kwa sauti ya ukali kidogo nikapita kibabe kwa kumpushi nikaenda Kuchukuwa vifaa na kuanza kazi. Nilifagia kwa kuizunguka nyumba yote kisha nikaingia Bustanini na kutoatoa Majani ambayo yalikuwa yamekauka. Huku

    Nikikusanya takataka zote nikaenda kuzichoma moto mpaka inatimia saa tatu kamili

    Nilishamaliza kila kitu. Nikaenda kukaa chini ya mti fulani hivi nikijifutafuta jasho. Kiukweli kazi ilikuwa ngumu mpaka kijasho cha Asubuhi ile ya Saa tatu kilinitoka.

    Nikiwa nimekaa pale nimejiinamia nikashtushwa na sauti nyororo misiri ya kinanda ikiniuliza

    “naona umechoka si mchezo"

    Nikainua kichwa changu kumtazama ni yule Mrembo wa jana akiwa katika mavazi ya mazoezi

    Chini alivaa kiatu aina ya Raba simpo sana na suruwali ya track suit

    Juu alivaa kibrauzi ambacho kilipanda kwa juu kidogo na kufanya kimstari

    Kile kinachopanda mpaka kitovuni kionekane vyema

    “vipi kule kwenye Swimming pool ulisafisha?"

    Nilishangazwa kutokana na lile swali kuhusu Swimming pool.

    “liko wapi hilo swimming?"

    “kwani ile jana Saengo hakukuonyesha?"

    “hapana hakunionyesha"

    “basi naomba unifate"

    Basi ikawa yeye mbele mimi nyuma kiukweli mtoto alikuwa na makusudi huyu yani hiyo tembea yake ilifanya makalio yake ya wastani si makubwa wala si madogo ni saizi ya katikati

    Japokuwa yalikuwa yapo ndani ya track suit

    Sijui kama alivaa na kitu kingine ndani yake. Yalitikisika kwa fujo na kufanya nipate mshawasha wa kutaka kuyashika japo kidogo tu.

    “huku mbona unaonekana kama ulifika kufagia inakuwaje Swimming pool usiweze kuliona upande wa kulee"

    Niliangaza macho kuiangalia hiyo sehemu

    “whaoo"

    Nilijikuta nikisema hivyo kutokana na mshangao nilioupata paada kuiona sehemu hiyo

    Kulikuwa na bwawa kubwa tu lenye maji masafii

    Huku kwa pembeni kukiwa na vile vitanda kwaajili ya kujipumzisha,

    Nikiwa naendelea kushanga nilipigwa na bumbuwazi baada kumuona yule Mrembo akivuwa

    Suruwali yake nilitaka kufumba macho akili ikaniambia uboya huo

    Akavuwa na brauzi yalaa mtoto wakike akabaki na

    Kisidiria na kichupi tu kisha akaniambia

    “kama hautojali tunaweza kwenda kuogelea"

    Nikataka kuvua nguo zangu

    “Hapana mkuu usifanye hivyo"

    “kwanini"

    “maji ya namna hiyo ni adui yako usiingie kabisa"

    Nikaacha kuvua na kubaki kumtazama yule binti aliyekuwa akinipungia mkono kuwa nimfate.

    Binafsi alinitamanisha tu, sema ndiyo hivyo nishapewa onyo kwa kuambiwa yale maji si mazuri kwangu. Mtoto wakike akapiga mbizi kwa kuzama chini, kisha akaibuka na kunitazama

    “vipi mbona huingii?"

    “siwezi kuogelea"

    “mmh! Mwanaume mzima kumbe hujui kuogelea?"

    “ndiyo sijui kiukweli sikuwahi kujifunza"

    “basi pole yako"

    “badala ya kuniambia nije unifundishe unanipa pole"

    “mmh! Usijali kesho kutwa nitajitahidi kufanya hivyo maana leo nahitajika kuwahi kazini"

    Aliongea huku akiniangalia akatoka kwenye bwawa nilibaki kula kwa macho tu. Mara ngapi nimsifie huyu binti kwa jinsi alivyoumbwa na kuumbika

    Ahaa wee acha tu,

    Akapandisha ngazi kwa mwendo wake uleule wa tetemente,

    Akaingia ndani na kuniacha mimi nikijiuliza maswali yasiokuwa na kichwa wala miguu.

    Nilifanya sikuweza kufanya kazi nyingi ilipotimia saa kumi Alasir nikarudi nyumbani.

    “karibu sana mwanangu kipenzi vipi kazi ulipata au?"

    “ndiyo"

    “mmh kazi gani na wapi?"

    “Shamba boy kule kwa mzee Arjun"

    “mh! Hongera sana mwanangu"

    Mama alinipongeza baada kumtajia sehemu ambayo nimepata kazi.

    Nilienda kuoga pamoja na kula chakula cha usiku niliingia chumbani kwangu kwaajili ya kulala. Mama na Nasra walibaki sebuleni wakiangalia tv

    Kiukweli sikukaa sana nilitoka na kuingia kitaani nikiwa kwenye taswira ya Kijinni.

    Nilifunga safari mpaka kwa Mwajuma niliingia mpaka ndani ya chumba chao na kukuta kuna

    Mzozo mkubwa sana. Mwajuma alikuwa akilalamika kuwa jamaa jogoo wake hapandi

    Mtungi anahitaji talaka yake. Jamaa nae akabaki kujitetea na kusema muda si mrefu ugonjwa wake utapata tiba nivumilie

    Ewe mke wangu. Niliumia sana kwa kauli ya jamaa kumwita Mwajuma ni mkewe

    Nikaondoka huku nikiacha ugomvi ule ukiendelea

    Ndani ya Baa ya Wazo iliyopo maeneo ya mji mwema ndipo nilipofikia baada kutoka kule kwa Mwajuma. Nnje ya baa hiyo kulikuwa na magari mengi sana.

    Nilienda kusimama kwenye moja kati ya magari yaliyopo hapo.

    Mahesabu yangu yaliniambia kuwa kile kikundi ambacho walihusika kwa namna moja ama nyingine kumuuwa Baba yangu wapo

    Kwenye Baa hiyo sikutaka kukurupuka kwa kuwavamia ndani. Nilifikia nnje na kwenda kuegemea Gari yao, nilikaa hapo takribani masaa mawili ndipo nikaweza kuwaona Wanaume walioshiba wakitoka ndani ya baa hiyo.

    Niliwaangalia kwa ghadhabu niliona kama wanachelewa kuja upande ule niliopo mimi nikajishika kiunoni na kuchomoa kisu. Nilianza kuwafata kwa kasi ya ajabu

    Nikawa nipo karibu nao.

    Nikachumpa na kuingia kati yao nikamkita mmoja kisu cha utosi

    Huku nikizunguka na kukata koromeo ya

    Mwingine wote walidondoka chini akabaki mmoja ambaye alitimua mbio kwa kukimbilia ndani ya

    Baa huku akipiga kelele za kuomba

    Msaada sikutaka kumuacha wala sikuwa na hofu. Mwanaume nilijiamini kupita kiasi

    Nikawa namfata humo humo ndani

    Nikakutana na kikundi cha watu wakitoka nnje huku mikononi wakiwa na silaha za jadi nikaruka juu na kuwapita nikaingia ndani

    Jamaa akakimbilia chooni na kujifungia kwa ndani.

    Nikagusa tu mlango na kuingia humo humo

    Hakuweza kuamini Aisee akabaki kutetemeka tu

    Sikumkawiza nikamkita Bisu la mdomo nikamkazia macho mpaka akakata roho kisha nikapotea





    Tulipoishia

    Jana

    Niliibukia chumbani kwangu nikapanda kitandani na kutulia kimyaa kama vile sio mimi niliyetoka kufanya mauwaji kwa watu watatu wale.

    Nilianza kumfikilia kipenzi changu Ratifa ambaye jamii nzima wanatambua kuwa amekufa kumbe sivyo. Ratifa bado anaishi. Yupo huko

    Mbagala Kiburugwa. Pia nilimfikilia Mwajuma aliyekuwa akipigizana kelele na mumewe kwa kuhitaji talaka. Jamaa jogoo hapandi mtungi.

    Si kwa marazi bali ni Vitimbi vya hawa

    Majinni. Bila shaka jamaa anahangaika sana kutafuta tiba lakini inashindikana kwa yeye kupona.

    Viumbe wameweka kigingi hawezi kuchomoka tena.

    Ukiangalia zimebaki siku chache atapoteza maisha.

    Niliwaza mambo mengi sana usingizi nao ukanichukuwa, niliota ndoto nyingi za kutisha.

    Nilishtuka zaidi ya Mara tatu, kutokana na ndoto hizo zenye kujirudia.

    Alfajir na mapema ilinikuta nikiwa kazini kwangu. Yote sababu ya kuota ndoto za ajabu nikashindwa kuendelea kulala nikakaa macho mpaka nilipoisikia Adhana ya swalati Subuhi nikaelekea kazini.

    Nilibisha hodi kwa muda mrefu kidogo lakini geti halikufunguliwa ilionyesha yero Masai hakuwepo hapo Getini, nikafikiria nini cha kufanya. Nisubirie mpaka kukuche au niruke uzio?

    Uwamuzi ukaja nikaruka juu na kuingia ndani nilipoingia kwa ndani. Yani nilitua chini bila kishindo chochote kile

    Nikatembea kwa mwendo wa haraka kuelekea sehemu ambayo kulikuwa na vifaa vyangu vya kazi nikaanza kazi mpaka kunapambuzuka nilishamaliza kila kitu.

    “heii wee mutu umekuja saa ngapi? Naulisa wewe pita saa ngapi pale getini?"

    “oyaa Saengo embu tulia bwana mi si nilipita pale mida yakama saa moja hivi"

    “hapana Mimi saa moja nilikuwepo pale mbona sija kuona ulisa tena wapitia wapi?"

    Nikaona anazingua nikakaa kimya

    “sasa naona wataka kujifanya wewe mwisi so

    Umeruka ukuta ehee"

    “nani karuka ukuta?"

    “si wewe hapo mi naulisa wewe nyamazia kimya namaanisha nini?"

    “hivi wewe kwaakili yako binadamu gani anaweza kuruka huu ukuta huoni umeme ule

    Kitu kingine ukuta ni mrefu!"

    Nilimuwelewesha Masai huku nikimng'ong'a"

    “Aisee wewe mutu mujanja yani umepita pale Mimi hata sijakuona"

    “si ulikuwa umesinzia"

    “basi usimwambie Bosi naweza fukuswa kasi Mimi"

    “siwezi kufanya hivyo ndugu wee nenda tu kaendelee na kazi zako!"

    Masai akaondoka huku akijisikitikia mwenyewe.

    Nilikaa pale mpaka ikatimia saa tatu kamili ya Asubuhi nikaletewa chai kwa chapati na binti

    Mdogo hivi.

    “karibu chai kaka yangu"

    Alinikaribisha binti yule kisha akageuka ili aweze kuondoka. Alipogeuka tu hapohapo nikagundua kitu baada kumuona akitembea kwa mwendo wa kuchechemea.

    “samahani ewe Dada yangu nakuomba Mara moja"

    Akageuka na kunitazama kwa mwendo wake uleule akajongea na kuja kalibu yangu.

    “bila samahani Kaka vipi ulikuwa na shida ya kitu gani?"

    Aliongea binti yule huku akijaribu kujenga tabasamu zito usoni mwake. Ni tabasamu la bandia

    Uso wake ulikuwa una mabaka mabaki fulani tuseme ni makovu

    “hapana sihitaji kitu chochote nilikuwa nataka ukae hapa ili tuweze kupiga story mbili tatu"

    “mmh kiukweli kwa muda huu haitowezekana maana nina kazi nyingi sana za kufanya na istosh....

    “wee Maida"

    Kabla hajaongea zaidi ikasikika sauti ya ukali ikiita Maida yule binti akaitikia huku akijitahidi kutembea haraka haraka kuelekea huko alipoitwa mwendo ule ukasababisha kitu kama matone ya Damu ya dondoke chini lakini hakujali. Sijui hakuyaona nilinyanyuka na kuchukuwa kitambaa nikachovya maji

    Na kuanza kufuta kila hatua niliona kuna arama ya Damu.

    “pumbavu zako ulikuwa unafanya nini kule?"

    “nilipeleka chai"

    Pahaa

    Sauti ya kofi ikasikika kuonyesha Maida kapigwa. Niliuma meno kwa hasira sikutaka kusikiliza tena nilirudi sehemu yangu nikakaa.

    Muda wa chakula cha mchana niliingia mpaka jikoni pasipo kuambiwa na mtu yeyote yule hata sikuelekezwa nilijikuta nishaingia. Nilimkuta Maida akilia

    “Embu lete hicho kisu nikusaidie kukata vitunguu"

    “hapana wee acha tu"

    “sio niache wee huoni kinakutoa machozi"

    Niliongea huku nikichukuwa kisu kingine nilianza kukata kitunguu yeye akamenya nyanya.

    “hivi wewe kibaraka wa shetani mwanaizaya mkubwa ulikuja hapa kuomba kazi ya kupika au?"

    Ilikuwa ni sauti tamu na nyororo kila nikiisikia sikosi kuisifia. Lakini kutokana na kuuliza kitu cha kipumbavu niliiona mbaya nikageuka kumtazama. Pasipo kumjibu kitu nilimfata pasipo kujiuliza au kujishauri kitu nikamshika shingoni

    “Sikia nikwambie kitu wee Mbwa wa Kihindi unapoongea kitu na kidume kama mimi unatakiwa uwe na adabu"

    Ghafla akanitoka na kunizungusha akanipiga teke nikadondoka chini puhuu kisu chenyewe kikaniponyoka Akakiokota na kunifata nikarudi nyuma nilisota nilipokuja kukaa sawa nikatoka mbio mpaka nnje. Ajabu alikuwa ananifata tu.

    Nilipofika nnje nikasimama na kugeuka nilimuona akija kwa mwendo wa mapozi huku kashikilia kile kisu mkononi

    “Siku yakwanza nilipokuona nilijuwa ni kijana mwenye akili sana ndiyo maana nikahitaji ufanye kazi ndani ya nyumba hii. Kumbe sivyo nilivyofikiria wewe ni mpumbavu kati ya wapumbavu niliowahi kuwaona.

    Unathubutu vipi kunishikia kisu mtu kama Mimi sasa leo utaondoka ukiwa na majeraha ili iwe fundisho kwa wengine!"

    Aliongea binti yule akiwa Sirius. Nikaona nikifanya uzembe wa aina yoyote ile anaweza kunifyeka pia nilitambua huyu binti ni mpiganaji hatari sana.

    “tafadhali Bosi nisamehe yalikuwa ni matani tu"

    Nilijitetea kwa kuongea hivyo

    Kiukweli hakutaka cha msamaha wala nini azma yake ilikuwa ni kunijeruhi tu. Akanifika na kunishika mkono wa kushoto akanivuta na kutaka kunikata nami nikazunguka kwa kasi nikampushi sikutaka kumpiga japokuwa nilikuwa na uwezo huo.

    Kisu kikaja mikononi mwangu, sikukishika sana nilimtumpia na kumwambia akichukuwe ili aweze kujaribu bahati yake kwa mara nyingine.

    Hapo ndipo akaghadhibika akaja kwa kasi huku akirusha ngumi za haraka haraka akapiga na mateke nilizitoa kwa dharau

    Alibadirisha kila style hakuweza kuambulia hata kofi moja kupenya mwilini mwangu.

    Akakiokota kisu na kuja nacho kwa kasi alitaka kunichoma hovyo hovyo nilimkwepa tu

    Nikaudaka mkono wenye kisu nikampiga pegani

    Akatoa ukelele wa maumivu nikampushi akadondoka chini nikamfata kwa kasi.

    Ghafla kuna njemba mbili zikashuka kutokea juu na kusimama mbele ya yule binti

    Nikainua kichwa changu kuangalia wapi walipotokea hawa watu

    Khaa! Kumbe kulikuwa na kikundi cha watu wamekaa kule juu wakiangalia kila kitu.

    Nilitamani kucheka nikajiuliza sijui nimwite Gogisu tumalize kazi au nicheze nao tu?

    Nikaona wacha nicheze tu nikajiweka sawa Washkaji wale wakaja kwa kasi mmoja alikuwa akipiga mateke kwa kutumia mguu wa kulia mwingine wa kushoto.

    Nilijitahidi kuzuia huku nikiwapa za chembe.

    Nifanya kama vile nakimbia nilipofika mbele kidogo nikadunda na kugeuka kwa kasi niliachia mateke mawili matakatifu mateke ambayo yalimpata mmoja kati yao akadondoka chini kwa kujibamiza kwenye sakafu

    Nilimfata yule mwingine akawa akirudi nyuma kwa uwoga

    “Hongera sana kijana binafsi sijawahi kuona kijana mwenye ngozi nyeusi mwenye kufahamu Mashowart kama wewe

    Nilishawahi kujionea kwenye movie za kina

    Michael J White

    Wesley Snipes. Bill Blanks na wengineo wengi tu sema zote zilikuwa ni movie. Lakini leo hii nimejionea moja kwa moja hongera sana kijana sijui unaitwa nani?"

    “naitwa James"

    “ohoo James ni jina zuri sana Mimi naitwa

    Arjun Putra ndiyo Baba mwenye nyumba hii huyu ni binti yangu anaitwa Karisma bila shaka alishakutajia jina lake karibu sana kwenye familia yetu"

    Aliongea yule mzee

    “nashukuru sana mzee wangu sema sihitaji tena kufanya kazi ndani ya nyumba hii"

    “ahaa usiongee hivyo kijana kwanini utake kuacha kazi wakati nataka kukutoa kwenye Ushamba boy ili uwe Bodigadi wa Karisma"

    Sikuongea kitu kama nimekubari au vipi nikatembea kuelekea getini kabla sijalifikia geti nikasikia sauti kitu kama bunduki hivi ikikokiwa kisha

    Nikasikia

    “kijana usitake kujifanya mjuwaji mbele ya watu wakubwa kama sisi hivyo vikarate vyako ndiyo vinakutia kiburi ehee. Sasa utaongea na chuma cha pua Malaya wee"

    Kwakuwa nilikuwa nimempa mgongo nikataka kufanya jambo ambalo kila mmoja litamshangaza sana nikazunguka kwa kasi na kumfata yule mzee ikawa kufumba na kufumbua Bunduki ipo mikononi mwangu huu unaitwa mwendo wa Kizuka yani ile faster kasi zaidi nishamfikia

    “sikia nikwambie mzee Mimi sijali kizito wala chepesi bali nakutwanga tu

    Nikafyatua risasi moja hewani.

    “Shenzi zenu nyote pigeni magoti"

    Nilitoa amri ya kibabe hakuna aliyebisha wala kukataa wakapiga magoti na kunyoosha mikono juu.

    Nikaachana na Mzee nikamfata Karisma.

    “hakika unaonekana ni binti mrembo sana tena sana tu kumbe urembo wako ni tofauti na roho yako.

    Wewe ni mnyama kupita hata wanyama niwajuao Mimi sasa basi usipobadirika ipo siku isiokuwa na jina nitakuchinja. Kuanzia leo nitakuwa nakulinda kila sehemu uwendayo na hii

    Bunduki nishapewa kama ulinzi juu yako

    Kesho nitakuja kuripoti kazini"

    Niliongea na kuondoka

    Wakati yote hayo yakitokea Maida alikuwa akifurahi tu maana nimetoa jambajamba kwa familia nzima kudadeki nikafungua geti na kutoka nnje sikutaka kuelekea nyumbani baada kugundua kuwa nafatiliwa kwa nyuma nikakata mitaa mengine na kuingia kwenye nyumba moja wapo iliyopo mbali na nyumbani







    Tulipoishia

    Jana

    Nilikaa kwa muda kwa kujibaza kwenye nyumba hiyo mpaka nilipokuja kuwaona wale watu waliotumwa kunifatilia wanaondoka.

    Nikatoka na kuelekea nyumbani.

    “whaoo kaka yangu huyoo anatoka kazini,"

    Nasra akanichangamkia na kuja kunikumbatia nikakaa kwenye mkeka nikavuta pumzi na kumuangalia mama aliyekuwa akichanja kuni

    “hivi Mama mbona Ratifa simuoni kuja hapa nyumbani?

    “mmh kwani huna taarifa kama kapelekwa Yemen"

    “what?"

    “ndiyo hivyo siku ileile uliyolala na Mama yake safari ilikuwa ishaandaliwa na babu yake. Alitaka mjukuu wake aende huko akasome na kujifunza tabia njema. Au wewe hutaki mwanao ajifunze kuwa na stara?"

    “nataka lakini mbona hajaniaga?"

    “yeye mwenyewe kashtukizwa tu wala alikuwa hajui"

    “lakini Mama wewe si ulikuwa unajua kila kitu. Kwanini usiniambie"

    “nilipitiwa mwanangu na kama ujuavyo kichwa chenyewe ni kibovu hiki

    Nisamehe sana baba pia usijali mwanao atakuwa akirudi kila likizo ikifika"

    Nikaingia ndani sikutaka kuendelea kumsikiliza mama niliona kama vile nimetengwa juu ya kutoa mawazo yangu juu ya binti yangu.

    “Gogisu"

    “naamu mkuu"

    Usiku wa leo kuna kazi moja kubwa sana nahitaji tukaifanye pia nilikuwa nahitaji uniitie Figisu"

    “sio aniite nipo hapa mkuu nimekusikia"

    Nilicheka kwanza baada kumsikia Figisu akidakia

    “kumbe nawe umekuja mpaka huku?"

    “ndiyo mkuu nipe kazi nikafanye mambo!"

    “sawa ndani ya usiku huu Gogisu atabaki hapa kwaajili ya kuilinda familia yangu. Kisha mimi na

    Figisu tutaenda kunyofoa baadhi ya roho za watu"

    “lakini mkuu kwanini Figisu asibaki hapa alafu Mimi nikaenda kuwajibika huko?"

    “Sasa hivi ni zamu ya Figisu kuonyesha uwezo wake wewe subiri kwanza"

    “ndiyo ndiyo mkuu mwambie huyu mzee"

    Figisu akashangilia kwa furaha.

    Nilikaa ndani kwa muda kidogo kabla ya kushtuliwa na sauti ya kelele za Dada akilia nikatoka mbio nilipofika mlangoni nikasimama na kuangalia nnje,

    Nilimuona jamaa mmoja akiwa kamshika

    Dada huku akimvuta sijui alikuwa akitaka kwenda naye wapi

    “Hafidhiiii mwanangu njoo umsaidie Dada yako huku wanamchukuwa,"

    Mama alipiga kelele kwa kuniita jina langu kitendo ambacho kiliwafanya baadhi ya watu waanguwe vicheko. Maana kila mmoja aliweza kufahamu huyo anayemwita mbona kashafariki muda mrefu tu.

    Nami sikutaka kujiuliza nilitembea kwa kasi

    Nilipofika kwa yule jamaa aliyemshika

    Nasra nilimshika na kumpiga kiwiko cha shavuni huku nikimpiga teke la kisogoni akadondoka chini.

    Si wakaitana

    “Nasra mchukuwe mama muingie ndani"

    Niliongea kwa sauti ya kiukakamavu

    Nikaingia kati

    “huyu ndiyo Hafidhi ametoka kuzimu a......yalaaa

    Nilichumpa na kumpiga ngumi ya mdomo yule aliyekuwa akiuliza maswali akashindwa kuongea zaidi. Nilitembeza kichapo mpaka wengine walikimbia nikamsogelea yule aliyekuwa akimvuta Dada nikaushika mkono nikauvunja kitu kikalia kohoo mfupa ukatokezea nnje

    Nikataka kung'oa kabisa mama akaja mbio na kunitoa huku akipiga kelele na kunitaka niache

    “Hafidhi achaa usifanye hivyo.

    Usiku huo watu walijazana polisi wakafika nikajikuta navishwa pingu na kupelekwa kituoni.

    Mmh sikuweza kuamini Aisee eti mkuu wa kituo ni

    Akida nilitamani hata kucheka.

    “embu vua mkanda vua viatu nyang'au wee unacheka cheka nini? Sasa leo utacheka kwa raha!"

    Akida aling'aka na kunipiga kibao kikali sana

    Nikavutwa na kuwekwa sawa

    “haya unaitwa nani?"

    Nikanyamaza kimya kama vile sijasikia chochote.

    “embu taja jina lako unaitwa nani mtoto wa haramu nini!"

    “naitwa Akida ukipenda niite Kid Master"

    “mmh!"

    Akaguna kisha akaandika

    “baba yako anaitwa nani?"

    “Halfani Mbondei"

    “khaa sasa mbona haya majina ni yangu Mimi?"

    Akasimama na kuniangalia kwa muda kisha akatoka nnje akaingia afande mwingine nikaandikisha nikaingizwa Selo

    “vipi mkuu tunaenda au?"

    “kama tayari ushajiandaa twenzetu hakuna kitu chochote ambacho kitaweza kuzuia

    Kazi zetu"

    Nilimjibu Figisu alafu nikapotea nilikuja kutokea

    Tandale maeneo ya kwa Bi mkali

    Usiku ulikuwa mkubwa sana nikatembea na kwenda kukaa kwenye Kibaraza cha nyumba ya Bi mkali nikaangaza macho huku na kule

    “sasa Figisu hii kazi nakuachia wewe ingia ndani nyumba ile pale kanifyekee Mzee Zodra"

    “ni huyo tu au kuna mwingine?"

    “mmoja tu!"

    Nilimjibu kimkato basi akaingia ndani alitumia sekunde chache tu akatoka.

    “tayari mkuu kifuwatacho?"

    “twenzetu kwa shemeji yako Ratifa si unapahamu ehee?"

    “ndiyo mkuu"

    “basi niongoze njia nifike mpaka pale alipo"

    Safari yetu ikaanza ya kuelekea Mbagala Kiburugwa njia nilianza kuingiwa na hofu. Yote sababu naenda kumuona mtu ambaye tayari alishakufa miaka

    Mingi kabla kumbe yupo hai mpaka leo hii kweli kwa hakika Majinni ni viumbe sio kabisa

    Bila shaka wengi wa maiti tunazoenda kuzika sizo

    Kabisa.

    “mkuu tushafika nyumba yenyewe ni hii hapa chumba chake ni kile pale!"

    Figisu aliniambia huku yeye akitoka akibaki nnje, nikazunguka nyuma ya nyumba mlangoni nilikuta kuna vikaratasi fulani vimeandikwa Quraan

    Bila shaka mwenye nyumba hiyo kaviweka kwaajili ya kuzuia viumbe wabaya wasiweze kuingia ndani ya nyumba yake.

    Lakini sio kwa kunizuia kiumbe kama Mimi nikapita na kuingia mpaka chumbani kwa

    Ratifa. Aisee sikuweza kuamini macho yangu baada miaka mingi kupita. Leo hii namuona tena.

    Nilikuwa na mpenzi ambaye alinienzi nusura nije kuwa chizi kwaajili ya lake penzi.

    Nilijikuta nikiwaza hivyo nikaenda kukaa kitandani.

    Ratifa, Ratifaa,

    Niliita kwa sauti ya kunong'ona huku nikikishika kichwa chake sehemu ya utosi.

    Nilianza kuongea maneno ya ajabu ajabu mpaka mwili wake ukaanza kuvabret mfano wa katapira,

    Nilizidi kuongea tu sikutaka kumuacha nilizidi kuongea mpaka alipotulia kisha nikatoka kwa kupitia mlangoni.

    Nilishtuka baada kupigwa na kitu kizito mfano wa kaa la moto. Niligeuka kwa kasi kuangalia. Nikarushiwa kitu kingine kilichonipata kifuani maumivu makali sana yalianza kunipata sema nilijikaza tu,

    “nani wewe?"

    Sauti nzito ya yule mtu aliyenipiga na vile vitu akaniuliza,

    Sikutaka kumjibu kitu maana alikuwa tayari kanitibua nilimfata kwa kasi, na kufikia kumkaba.

    Nilimshika shingoni ile kisawasawa, kisha

    Nikamnyanyua juu na kumbamiza ukutani,

    Nikamuangalia kwa muda alafu nikatoka na kumwambia Figisu twenzetu

    “vipi mkuu mbona kama umeumia?"

    “sio kama mwenzako mule ndani nimekutana na kizingiti hatari sana!"

    “Duhuu sasa mbona hukuniita nije kukifyeka hicho kizingiti?"

    “niliona haina haja Mimi mwenyewe

    Natosha kwa kila kitu embu nipatie Damu

    yako!"

    Nilimwambia hivyo Figisu basi akajikata sehemu na kunipatia damu nikafanya kujipaka kwenye yale majeraha ya moto

    Sekunde si nyingi nikawa safi nikarudi

    Selo na kutulia kimyaa

    Kesho yake Asubuhi na mapema mama alikuja akiwa kaongozana na Mwajuna pamoja na Nasra

    “Shikamoo Mama,"

    Nilimsikia Akida akiamkia sijui kama mama aliitikia au laa

    “vipi Mama ulikuwa na shida gani? Kuna ndugu yeyote aliyeletwa ndani ya kituo hiki?"

    “embu acha kuniuliza maswali ya kijinga unamaana hujui kama Rafiki yako Hafidhi kuwa yupo humu?"

    “what? Mama unamaanisha nini kusema hivyo kwanza unamzungumzia Hafidhi yupi?"

    “ni huyohuyo umjuae wewe"

    “inamaana bado anaishi?"

    “ndiyo maana yake alikuwa huko Uganda"

    Basi Akida alikuja mbiombio kuja kufungua geti la Selo akabaki kuniangalia kwa muda mwishoe akaja mbio kunikumbatia

    Furaha iliyoje marafiki kukutana tena

    Siku hiyo kikosi kizima cha Wabeba Lawama walipigiwa simu na kuhitajika kukutania nyumbani

    Ilikuwa ni bonge la Sapraizi kwao

    Kaunda aliponiona alikimbia huku akipiga kelele za mzimu mzimu jamani.

    Kina Othmani wakawahi kwenda kumshika na kuongea nae.

    Alirudi japo kwa shingo upande nami nikafanya sifa ya kumtisha kwa kumwambia Zombiee anakujaa.

    Mama alicheka si kidogo

    Nilikaa nao na kuanza kusimulia kila kitu pia nilihitaji kuwaonyesha kitu si kingine ni Video ya kwenye flashback niliseti kila kitu pale Sebuleni nikawasha kila mmoja akawa kimya kuangalia kile ambacho niliita ni tukio langu

    “Mungu wangu huyu si mume wangu jamani wanamuuwa hiiiihaa"

    Mama alipiga kelele na kuanza kulia baada kufika sehemu ambayo Baba akikabwa

    “Dahaa kumbe dunia sio mbaya walimwengu ndio wabaya, yani tulijuwa mzee wetu kafariki kutokana na ajari ya gari kumbe sivyo.

    Sasa basi tunaunda kikosi kuhakikisha kila aliyehusika anaingia kwenye mikono ya

    Sheria Wabeba Lawama tuunde nguvu moja kama zamani"

    Akida alieongea





    Jana

    Kila mmoja akapatiwa majukumu yake Akida akiwa kama mkuu wa kituo cha polisi cha Kawe yeye ndiyo aliyetoa mipango yote huku akinitaka mimi kutojihusisha kwa lolote juu ya watu hawa. Akasema kivyovyote vile watafanya juu chini mpaka kuhakikisha watu hawa wakiingia kwenye mikono ya sheria.

    “lakini mbona kama bwana Pundra amefariki usiku wa jana?’’

    Kaunda akauliza na kumfanya kila mtu aniangalie mimi lakini sikujari sana kwa kule kuniangalia, mipango ikaendelea kupangwa nilitulia kimyaa wakati kikao kikiendelea ghafla tukapokea ugeni. Ugeni ambao ulinifanya nishtuke si kidogo. Kilikuwa ni kikundi cha watoto wa Madrasa wakiwa wameongozana na Walimu zao. Mama aliwakaribisha kwa furaha sana

    “Mama kwani hawa watu wamekuja kufanya nini hapa?’’ Niliuliza swali huku nikiwa na hofu Fulani ndani ya moyo wangu, maana nilitambua muda si mrefu moto utaanza kuwaka,

    “wamekuja kupiga kisomo juu yako kama unavitu vibaya basi waondoke’’

    Mama akanijibu sikuwa na jinsi kukubari tu nitakataa vipi wakati kila kitu kilishaandaliwa.

    “Hafidhi ondoka haraka sana katika eneo hilo, kimbia kijana usishike ubani. Kimbia nasemaa!’’

    Bibi aliongea kwa sauti ya ukali sana na kunitaka niondoke, nikabaki kujiuliza sasa kati ya hawa watu msomi ni nani? Nilijiuliza hivyo maana sikuona hata mmoja mwenye kufanania na Shekhe Ally.

    “Sasa itabidi Shekhe Hafidhi tuanze kupiga Fatha kwa wewe kuweka ubani kisha tutamwita huyo mkuu wa Mashetani tuweze kuzungumza naye hapa alafu tutawaondoa mashetani wote. Maana mbele ya Mwenyezi Mungu muweza wa yote hakuna kinacho shindikana Takbir’’ Alianza kuongea mmoja kati ya watu wale na kumalizia kupiga Takbira wote tukaitikia Allahu Akbaru nikaweka ubani kisomo kikaanza alianza kusoma taratiibu mwishoe sauti ikapanda ikawa kila akifika Aya Fulani katika Surat Mulk anataja jina la Lusifa akafanya hivyo kama mara tatu hivi. Ghafla moshi mweusi tii ukaanza kutanda pale sebuleni taa zikazima na kuwa giza totoro kina Akida na Ukomando wao wote walianza kutetemeka kwa uwoga na kutamani kukimbia “msiogope tulieni vijana huyo ndiyo Lusifa mwenyewe mkuu wa Majinni’’ Aliongea Shekhe kwa sauti ya chini, ni kweli Lusifa alikuwa amefika akatanda juu angani yani alikuwa kama vile kaizua bati zote juu ya nyumba akatanda yeye tu. “nasikia nimeitwaa hiyo sauti yake sasa ilikuwa ni nzito na kali utasema mtu aliyechukuwa tarumbeta akakupurizia sikioni kwako. Tuliziba masikio.

    “ndiyo tumekwita Rusifa embu usipandishe sauti yako juu utaumiza masikio yetu. Kama ukikaidi nami nitaumiza watu wako!’’ Aliongea Shekhe kwa sauti ya kibabe. Lusifa akacheka kwa dharau na kusema

    “sawa nimeweza kukuelewa je ulikuwa na shida gani?’’

    “sina shida ila nilikuwa nataka mumuachie huru kijana wetu’’

    “embu acha kupindisha maneno mbona umesema hauna shida kisha useme tumuache huru kijana wenu kwani hiyo sio shida?’’

    “ndiyo hii sio shida maana si ombi ni amri na ni lazima mmuache’’

    “na kama hatujamuacha utatufanya nini?’’

    “Lusifa tambua kitu kimoja kuwa hatujaitana hapa kwaajili ya mabishano tumeitana kwa minajiri ya mapatano tu utamuachia kijana wetu au laa’’

    Lusifa hakujibu kitu akaondoka hali ikarudi kuwa kama awali vijasho vilitutoka sema mimi nikainuka na kuaga kuwa naelekea chooni mara moja nilipotoka tu nikaongea maneno yangu nilijikuta nipo angani nikisafiri kwa kasi sana. Nilikuwa katika safari ya kumfatilia Lusifa nilikata mawimbi na majangwa misitu na mapori, nikajikuta nikitokezea sehemu moja hivi yenye mkusanyiko wakila aina ya viumbe wa kutisha safari yangu ikakomea hapo nilishindwa kunyanyua hata hatua moja kusogea mbele nikasimama na kutua hapo,

    Sauti ya vicheko ikaanza kusikika niliangalia mbele yangu ndipo nikamuona Lusifa akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa mfano wa

    Nyumba pembeni yake kulikuwa na viumbe wengine walishika silaha. Nilimkazia macho kwa kumtazama nae akanikazia. Lakini sikuogopa ukali wa macho yake kama

    Makaa ya moto,

    “hakika unaonekana ni Binadamu wa ajabu sana kwanza umethubutu vipi kuja huku?"

    Lusifa alianza kuongea na kuniuliza hivyo,

    Sikumjibu kitu binafsi shida yangu kubwa ilikuwa ni yeye tu si vinginevyo. Sema nilishindwa

    Kujinasua pale, niliganda mfano wa Chuma kwenye Sumaku.

    “sikia nikwambie kitu kijana huu ndiyo utakuwa mwisho wako wa kurudi tena

    Duniani!"

    “Shatapu nyamaza wala usiongee chochote kuhusu Mimi kwanza huna uwezo wa kunizuia kivyovyote vile!"

    Niling'aka na kumkalipia Lusifa kitendo ambacho kilimshangaza sana yeye na Walinzi wake.

    “hivi unajiamini kitu gani wewe? Hivi unatambua kama upo mbali na Dunia huku ulipo ni kuzimu milango yote imefungwa huwezi kutoka

    Kamwe!"

    Lusifa akazidi kunitisha lakini sikutishika kwani nilijiamini Mimi kama mimi pia nilimtumainia Gogisu na Figisu pasipo kutambua kuwa huyo ndiyo mkuu wao. Nikajivuta na kufanikiwa kutoka pale,

    Nikazunguka kwa kasi na kuachia vitu kama

    Misumari midogo hivi niliirusha ikaenda kukita kwenye mioyo ya walinzi kama

    Watatu wakaanza kuungua na kupukutika

    Hapo sasa Lusifa akapiga kelele kuita Jeshi

    Wingu zito likatanda angati radi ikapiga umeta ukatokea

    Tarumbeta zikaanza kusikika kuonyesha Jeshi la Majinni wanakuja

    Nilibaki nimesimama tu.

    Lusifa akapotea na kuniacha nimezungukwa na viumbe wale wa ajabu

    Nikapiga kelele kumwita Gogisu na

    Figisu ajabu walikuja kwa kishindo na kujiunga nami

    “Nyie vipi mbona mnataka kumtetea kiumbe ambaye si jamii yenu?"

    Aliuliza kiongozi wa wale Majinni,

    “ndiyo sio jamii yetu lakini anatembea na nafsi yetu. Akifa huyu na sisi tutakufa pia. Sasa hatupo tayari kumuona akiuliwa wakati sisi tupo

    Hapa hakuna cha Lusifa wala nini. Ni kupambana tu"

    Aliongea Gogisu.

    Nikamuangalia Figisu kisha Gogisu na kuwaambia Tuanzeni kuwasha moto!

    Figisu akachumpa kwa kwenda hewani akaanza kutema mapande mazito mazito ya

    Moto huku Mimi na Gogisu tukipigana kwa chini.

    Ghafla ulisikika ukelele mkali huku Figisu akitupwa chini na kutawanyika vipande vipande

    Nilipiga kelele kuita Figisuu....

    Lakini ndiyo hivyo alishakuwa mavumbi. Ni kazi iliyofanywa na Lusifa kumuangamiza

    Figisu, kwa upande wa Gogisu akashikwa na Ghadhabu hasira zikampanda

    Akaruka juu kumfata kabla ya kumfikia naye akapanguswa tu na kuwa vumbi. Hapo ndipo nilipoamini mkuu ni mkuu tu.

    Yani kawaangamiza vijana wake kama vile sisimizi

    “Hafidhi usiogope jitahidi kupambana Mimi nipo pamoja nawe

    Umekiona hicho kisu kidogo kipo hapo juu ya kiti? Chukuwa hicho hakikisha unaenda kumchoma sehemu yenye moyo!"

    Sauti ya Bibi ilikuwa ikinipatia maelekezo

    Sikujiuliza sana nikakichukuwa hiko Kisu

    Tatizo la Lusifa ni Dharau sana pia akajiamini.

    Mshikemshike ukaanza baina yangu na Lusifa ilikuwa ni sawa na Tembo kupambana na Nzi. Nilikuwa nikimchenga huku na kule

    Sauti ya Bibi akishangilia ikazidi kunitia nguvu.

    Lusifa nia yake ilikuwa ni kunishika ili aweze kuniangamiza kama alivyofanya kwa

    Mabodigadi wangu nami nilitambua hilo.

    Nilifanya kupanda kwenye

    Mwili wake mkubwa mfano wa Gorofa

    Sabini elfu, nilienda kwa kasi ya ajabu

    Nikadunda na kukishikilia kile kisu kwa nguvu zangu zote nikamkita nacho pale pale kwenye moyo.

    Tetemeko si kishindo vilianza kutokea mpaka nilihofia kuwa Mbingu inaweza kudondoka.

    Ghafla niliona mabonde ya moto yakija upande ule,

    Mfano wa Tsunami.

    Lusifa akazidi kufoka na kupiga kelele alitapatapa na kuzunguka,

    “Kimbia kijanaa kimbiaa"

    Sauti ya bibi ikaniambia hivyo

    “nitakimbilia wapi wakati njia ya kutokea hakuna?"

    Niliuliza

    “tazama upande wa kuliani kwako!"

    Niliangalia ule upande ambao Bibi aliniambia. Niliona kitu kama duara Fulani hivi likiwakawaka sema lilikuwa mbali sana. “bila shaka umepaona sasa unaweza kwenda kwaheri kijana wangu kwaheri ya kuonana lakini ipo siku tutakuja tena kukusabahi. Siku isiojulikana nendaaa!’’

    Bibi aliongea kwa sauti ya ukali yenye kuambatana na kilio, bila shaka hakuweza kuamini kama siku moja nitakuja kutenda mambo makubwa kama yale. Joto la mwili likaanza kuongezeka ule moto uliokuwa unakuja ulikuwa ushakaribia karibu na pale nilishuhudia jinsi viumbe wengine wakisambaratishwa vipande vipande baada kukumbwa na ule moto. Muda wote huo Lusifa alikuwa akitapatapa na kuhangaika kukichomoa kile kisu akazidi kupiga kelele nikachumpa na kuanza kukimbia kwa kasi. Kiukweli mpenzi msomaji unaweza kusema kama vile ni ndoto, au ni movie Fulani ya kimarekani, lakini haikuwa movie bali ni uharisia mtupu uliokuwa ukinitokea mimi. Nilizidi kukimbia huku nyuma nikifwatwa na vile viumbe moto nao ulikuwa ukija kwa kasi. Viumbe vilivyokuwa nyuma yangu vikazidi kuteketea niliongeza kasi mpaka nikaweza kuifikia sehemu ile sikujiuliza wala nini nikajitosa. Nilidakwa na upepo mkali sana mpaka hapo sikuweza kujielewa tena.

    Maji ya bardiii yakanza kunimwagikia Usoni kwangu huku nikisikia kwa

    Mbaali sauti ya Quraan ikisomwa

    ????? ???????????? ??????? ???? ????? ????? ??????? ???????

    ???? ???????

    Hakika Shetani hupita (ndani ya mwili wa binadamu) kama ipitavyo damu (ndani ya mishipa ya binadamu).”

    Hii ni muhimu tukajua kua Shetani njia zake ndio hizo apitazo.

    ma katika Suratin Nisaa aya ya (119), akasema Mwenyezi Mungu (S.W.T) “

    ??? ?????

    ))* ?????? ????????? ???????????? ???????? ???? ????? ??????? ?????? ?????? ?????????? ????????

    ???? ?????? ?( 119 )

    Na mwenye kumfanya Shetani kuwa ni mlinzi (mungu wake

    badala ya Mwenyezi Mungu, basi yeye amekhasirika khasara iliyo dhahir.

    Kwahiyo tuwe makini na hilo ili tusiingie katika kundi la Hasara.

    ??? ?????

    ))* ?????? ?????? ???? ?????? ???????????? ????????? ???? ?????????? ?????? ???? ???????

    ?( 36 ?) ???? ??????

    Anayeyafanyia upofu maneno ya Mwingi wa Rehema Mwenyezi Mungu tunamwekea Shetani kuwa rafiki yake, (kuwa mwenziwe.

    Na hii ndio khatari kwa Mwanadamu kua Shetani kufanywa kwako ndio Rafiki yako mpenzi ,Jee ukifa na Shetani ni rafiki yako?

    Nikafumbua macho na kujikuta nikiwa nimelala chini huku watu wamenizunguka

    Niliangaza macho huku na kule ili niweze kuwatambua watu wale.

    “Uhu! Jamani mwanangu hatimae umefumbua macho ehe! Asante Mungu"

    Ilikuwa ni sauti ya Mama akiongea hivyo akaja kunishika nikajinyanyua kwa kusaidiwa

    “Mama niko wapi hapa?"

    Nilifungua mdomo na kuuliza

    Swali.

    “hapa upo nyumbani kwenu kijana kwanza hongera sana tena sana kwa kuweza kufanikisha hili swala.

    Ambaro kwa upande wetu lilikuwa zito sana"

    Aliongea mmoja kati ya wale watu

    Waliokuwa wamenizunguka. Nikamuangalia kwa sekunde kadhaa kisha nikainuka kabisa na kusimama

    “ahaa! Kaa kwanza kijana unataka kwenda wapi tena wakati kazi ishaisha?"

    “naenda kuwafata Wajomba zangu embu niacheni"

    “Hafidhi kaka embu tulia basi

    Shekhe amalize mambo kisha mengine yafate"

    Kaunda akanishika mkono na kuniambia hivyo. Basi nikakaa chini kisomo kikaendelea

    Yani mpaka inatimia saa tisa usiku

    Kisomo kilizidi kupamba moto mwishoe kila kitu kikaisha. Shekhe akasema sasa nipo

    Huru.

    Kesho yake Asubuhi baada kunywa chai

    Wabeba Lawama wakaniaga

    kuwa kila mmoja anaingia kwenye majukumu yake.

    Wakaondoka tukabaki familia tu

    Mimi Mama na Dada

    “mmh! Kiukweli Hafidhi wewe ni hatari sana yani umempiga Lusifa na Jeshi lake mpaka kumuua!"

    Nilishtuka kusikia ile kauli ya Mama

    “Mama unasemaa"







     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog