Search This Blog

Thursday 24 November 2022

PETE YA KIKE - 2

 

     

     



     

     

    Chombezo : Pete Ya Kike 

    Sehemu Ya Pili (2)







    Suria liingia bafuni akiwa na pete kidoleni, pete ambayo ina uwezo wa ajabu pindi uivaapo,... Kitu cha kwanza kwa surian baada ya kuivaa pete hio, kapigiwa simu ya kazi,... Hio ndio faida ya hio pete,... Na kingine ni kwamba kama kuna mapepo yanakuandama, ukivaa pete hio hakuna kiumbe yeyote atakaye kusogelea, na pia vile vile, ukivaa pete hio, hakuna kiumbe kitakachoweza kukudanganya kwa namna yeyote ile, hata kama ni jini mzuri, pia hawezi kukurubuni mana una pete kidoleni mwako,...



    Sasa surian alipogundua kuwa hajavua ile pete, aliivua kisha akaiweka kwenye kadirisha kalichopo hapo bafuni,.. Sasa kule maimati akapata ishara kuwa pete imevuliwa, maimati akajiandaa kupotea katika mazingira yao... Lakini kabla hajaruka, alipata ishara kwa mara nyingine kuwa pete imevaliwa... Hivyo akaahirisha kuruka, ikabidi akae kwa kutulia



    Sasa huku kwa asha,.. Kumbe asha ndio kaivaa ile pete,.. Baada ya kuwekwa tu kwenye dirisha, asha akaichukua na kuivaa... Sasa kule kwa maimati akapata tena ishara kua Pete imevaliwa, lakini imevaliwa na mtu wa jinsia yake, yaani mwanamke mwenzie, bila kupoteza muda maimati aliruka hapo hapo kuja kwa akina surian,... Lakini alipopita hapo nje alimwona shaimati akiwa katulia katika mti,... Akajua tu yeye ndio sababu ya surian kuvua pete,... Sasa hajakaa vizuri mara asha katokea huku akifurahi kwani mtihani aliopewa kaufaulu...

    Maimati aliweza kuiona pete aliompa surian ili imkinge,...

    "shit, shaimati... Umefanya nini"

    Maimati alikasirika na kumfuata shaimati huku akimwambia hayo maneno....

    "sasa mimi nimefanya nini"

    Sasa wakati huo wakibishana, maimati hakuwa akionekana (invisible), sasa asha anakuja anamshangaa shaimati kama anabishana na hewa, mana hakukua na mtu wa kitu mbele yake, lakini alikua akiongea....

    "lazima umemtuma huyu msichana akachukue pete"

    Aliongea maimati huku shaimati akijibu kua

    "hao ni ndugu, wajuaje kama wamepeana"

    "kama ni ndugu wamepeana, je wewe unafanya nini hapa"

    "napunga upepo tu, kwani huoni kuna kivuli kizuri"

    Sasa asha anazidi kushangaa, shaimati anaongea na nani...

    "we dada, kwani unaongea na nani"

    Asha alimuuliza shaimati ambao kwa sasa ni marafiki, lakini asha hajui kuwa shaimati ni jini...

    "aahhhhh mawazo tu... Wala siongei na mtu"

    Shaimati alimjibu asha kuwa ni mawazo tu lakini hakuwa akiongea na mtu

    "mmhh ok, ila punguza mawazo dada.. Afu kazi yako ulionipa nimeimaliza"

    Aliongea asha sasa shaimati bado anajibalaguza, mana aliambiwa na maimati kuwa yeye ndio sababu ya hio pete kuwepo kwa huyo msichana,

    "umeona eee, nilikwambia wewe ndio sababu ya hii pete kuwa kwa huyu mwanamke"

    Aliongea maimati lakini shaimati hakujibu kitu,... Pale pale maimati akaingia ndani chumbani kwa surian, na anae ona kuingia kwa maimati, ni shaimati peke yake, mana ni jini mwenzie...



    Sasa maimati ile anataka tu kuingia, alimuona surian akiwa anaitafuta ile pete,... Hapo ndipo maimati akajua ile pete ilichukuliwa wakati anaoga,.. Maimati aliumia sana mana hawezi kuichukua hio pete ikiwa kidoleni mwa mtu, ni mpaka aivue ndipo aichukue... Na hio pete ndio ilikua kinga ya surian ili asiende kule kwenye himaya yao,... Surian alitafuta pete mpaka kachoka,.. Alikwenda kuvaa vyema kisha akamfuata mama yake,.. Wakati huo maimati yupo nyuma lakini haonekani,...

    "mama"

    "abeee"

    "hujaona kijipete flani hivi"

    Aliuliza surian lakini kabla mama yake hajajibu ghafla asha akaingia...

    "mimi sijaona... Kwani nawe skuizi wavaa pete"

    Aliuliza mama yake, mana surian hajawahi na hua hapendelei kuvaa pete au cheni,...

    "hapana mama... Ni pete ya mwanafunzi wangu... Niliibeba kimakosa wakati machukua chaki kwa ajili ya kufundishia madrasa"

    "mmhh mimi sijaona, labda umuulize dada yako"

    Aliongea mama yake, kisha surian akamuuliza asha...

    "eti hujaona pete hapa kama ilidondoka"

    Suria alimuuliza asha ambaye ni dada yake kabisa

    "hio pete ni ya kike au ya kiume"

    "ni ya kike"

    "heeeeeee sasa wewe na PETE YA KIKE wapi na wapi"

    Asha alianza kumkandika wakati yeye ndio anayo hio pete na mkono aliovalia pete hio, kauficha ili surian asione

    "lakini si nimesema hapa kuwa ni pete ya mwanafunzi wangu"

    Wakati huo maimati katulia tu, mana hairuhusiwi kumnyang'anya mtu pete, mpaka aivue mwenyewe,...

    "mmmhhh mimi sjaiona nikiiona nitakwambia"

    Aliongea asha, na hapo hajui hio pete ina faida gani na uzuri ni kwamba pete hio haina ubaguzi, yeyote atakaye ivaa lazima aneemeke....

    "asha simu yako inaita huko chumbani kwako"

    Aliongea mama yake,... Huku suria akaamua tu kuwahi msikitini mana ilikuwa ni wakati wa jioni kwenda kuswali magharibi,... Sasa kwakua suria hana pete, hivyo maimati ana kazi ya kumfuata nyuma nyuma ili shaimati asije kumrubuni... Mana mwanzo suria alikataa kazi aliopewa na shaimati kuwa kwa wiki atalipwa milioni kumi,.. Lakini bado kakataa kwasababu alikua na pete, na pete hio haikubaliani na uongo,... Lakini kwa sasa suria hana pete hivyo akikutana na shaimati lazima akubali tu, hivyo maimati kaamua kuwa mlinzi badala ya ile pete.... Shaimati kweli hakua mbali, kana kwamba alijua tu suria atatoka kwenda msikitini hivyo atamvizia.. Lakini kwa bahati mbaya maimati yupo nae, hivyo akashindwa kwenda kumrubuni



    KESHO YAKE ASUBUHI MIDA YA SAA NNE



    Suria siku hio hakwenda kazini, kule shule kufundisha mana jana alipigiwa simu ya kwenda kupata kazi ya kulipwa milioni tano mpaka nane kwa mwezi,.. Sasa leo hakwenda shule, ili aende kwenye intaviu ya kazi hio aliopigiwa simu jana... Lakini kabla hajatoka akaitafuta ile namba iliompigia simu jana,...

    "hallo boss hali yako"

    Suria alimsalimia boss huyo wakiwa katika mazungumzo ya simu...

    "salama tu hali yako kijana"

    "Tunamshukuru mungu kwa rehma zake"

    Alijibu suria huku akitabasamu kwa mbaali

    "inshallah, sasa kijana mbona una haraka, sisi tulikwambia tutakupigia simu"

    "lakini boss, jana jioni mlinipigia kuwa leo nije saa nne"

    "hapana... Labda tulikosea namba tu"

    "boss, namba ni hii hii"

    "hapana bwana... Unataka kituuzi tena"

    "basi boss wangu, Nasubiri wito wenu"

    Aliongea suria kisha boss huyo akakata simu kwa hasira....



    "alaaaa.... Huyu si alinipigia jana huyu"

    Aliongea suria huku akiwa kama haelewi,... Mana Jana akapigiwa simu kuwa leo saa nne aende kwenye intaviu kwa ajili ya kazi, sasa leo anaipiga ile namba inamjibu tofauti,... Suria alichoka na kuchoka... Hata hamu ya kutoka tena ikawa hakuna,... Akarudisha baisikeli yake ndani na kukaa kwa kutulia,..



    Sasa kumbe ile pete iko hivi... Kama kuna mahali ulikwenda kuomba kazi,. Alafu ukaambiwa tutakupigia simu... Sasa kama ile nafasi ya kazi ipo lakini wahusika wanataka rushwa, basi ukivaa ile pete, inakuwa kama inamlazimisha yule mhusika kukupa kazi,... Mana nafasi ipo lakini unabaniwa kuipata... Lakini kama haipo basi haipo... Lakini kama ipo afu unabaniwa usiipate, basi ile pete inafanya kazi,.. Kwahio jana suria alipigiwa simu kwakua alikua kavaa ile pete, sasa hivi hana ile pete ndio mana boss hamuelewi...na suria hajui kuwa ile pete ni kwa ajili yake na ndio sababu ya kuitwa kazini... Yaani laiti angelijua kuwa pete ile ndio sababu,.. Angempokonya mtu ambaye yuko nayo... Mana suria au mtu yeyote anaweza kumpokonya asha ile pete, lakini kiumbe kama shetani au hawa hawa akina maimati na shaimati hawawezi kumpokonya asha ile pete, ni mpaka aiache mwenyewe,.. Kwahio hata kama ingelikua kidoleni kwa suria, pia hakuna kiumbe kitakacho weza kumpokonya ni mpaka aivue..

    "mama..."

    "abeeee... Ah bado hujaenda huko kwenye intaviu"

    Mama huyo Alimuuliza mtoto wake

    "ah mama... Ni mitihani tu... Jana kanipigia mwenyewe, lakini nashangaa leo ananigeuka"

    Aliongea surian huku akitamani hata kulia, mana ni kazi inayo endana na elimu yake, na anaipenda kwelikweli

    "pole mwanangu, labda sio riziki yako"

    "aahhh sasa si angesema toka jana.. Mana leo sijaenda kazini kule shule kwa kujua kuwa nakwenda kupata kazi"

    Aliongea suria huku mama akimuonea huruma mtoto wake

    "sasa kwanini usiwahi huko shule, ili usipoteze kote kote.. Wahi baba"

    "saa hizi mama ni saa nne hii, ni mwalimu gani anakwenda shule saa nne"

    "Sikiliza mwanangu, wewe ukifika useme nilipata dharura kidogo"

    Aliongea mama yake, ndipo suria akachukua baiskeli yake...

    "hivi dada asha yuko wapi"

    "si kaenda huko saluni kwake, eti watu wamejaa mlangoni wanataka kusukwa"

    "eeehh ndio katoka asubuhi hivyo"

    "kapigiwa simu toka jana"

    "eehh... Haya mi wacha niende"

    Basi suria alipanda baiskeli yake kisha huyooo....



    Sasa huku saluni kwa asha... Duuuu kumejaa wanawake,.. Wengine wanafumua nywele ili wasukwe na madraya... Wadada wanafanya kugombea anzee yupi amalize yupi, kiufupi leo asha alikua na wateja utafikiri soko... Hajawahi kuweka wasaidizi lakini leo kaweka wasaidizi kama watano hivi, tena kapandisha na bei ya kusuka sijui kushonea, ah mimi sijui misiko ya kile mnaitaje... Lakini asha siku hio mpaka yeye mwenyewe anashangaa, tena anafanya kuuliza kuwa huko mitaani umeme umekatila au vipi,.. Mana watu wanazidi kujaa saluni kwake..



    Sasa wale ambao wanamjua asha alivyo, leo wanashangaa...

    "kumbe mwenzetu ukivaa kiheshima unapata wateja hivi"

    Aliongea mmoja wa rafiki zake, mana hawajawahi kumuona asha kavaa hijabu,... Sasa leo kavaa afu ana wateja wengi mpaka hawataki Tena



    Lakini sasa mbali na hapo pia maimati yupo hapo habanduki, anasubiri asha avue ile pete ili aichukue, lakini asha havui wala nini anafanya kazi akiwa na pete, na yeye pia hajui kuwa hio pete ndio sababu ya wateja kuongezeka katika biashara yake, yaani ukiwa na hio pete riziki zako zote zinafunguka..



    Sasa huku barabarani, suria akiwa anakwenda zake shuleni kufundisha, japo kachelewa lakini ana kisingizio, japo uongo hapendi kuongea lakini leo itambidi ili alinde kibarua chake

    Lakini alipokua anawahi kwa kuchanganyia baiskeli yake ili ikimbie... Alipishana na mwanamke mmoja ambaye anamkumbuka lakini hamfahamu

    "samahani dada"

    Aliongea suria na yule dada akasimama bila tabu... Lakini sasa dada mwenye ni shaimati

    "bila samahani"

    Shaimati alijifanya hana mpango nae kabisa, wakati hata hapo kajipitisha makusudi tu ili suria amuite, na kweli ndivyo ilivyokuwa...

    "natumai jioni ya jana tuliongea tukiwa jirani na pumziko letu"

    Aliongea suria akimaanisha jana waliongea na huyo dada wakiwa jirani na kwao...

    "enhehehe, ni kweli, afu una kumbukumbu kweli.. Enhe niambie kaka yangu"

    "safi tu... Sasa ile kazi uliosema jana, inapatikana wapi mana sijakuuliza jana"

    Aliongea suria kana kwamba anajiingiza mwenyewe bila kujua...

    Sasa shaimati akachanganya kichwa haraka haraka na kusema

    "mimi naishi dubai, na hio kazi pia ipo dubai"

    Aliongea shaimati na aliamua kusema dubai kwasababu suria ni muislamu na anaipenda dini yake hivyo akiskia mambo ya dubai dubai, kidogo anaweza kushawishika mana ni sehemu iliotawala imani yake

    "ok safi sana... Aahh unajua jana nilikataa nikajua ipo ulaya huko, mana mimi sipendi kwenda ulaya"

    Sasa suria yeye anajua kuwa jana alikataa kwa akili yake, kumbe ni pete ndio ilikua ikimuongoza akatae, sasa leo anasingizia eti alikataa kwakua hapendi kwenda nchi ambazo zimekithili utandawazi na fasheni za ajabu...

    "ok poa"

    Sasa shaimati akajifanya kama hana muda nae

    "sasa dada... Mbona hunipi jibu sahihi"

    "jibu gani tena.... Kama upo tayari jiandae twende"

    "lini sasa tunakwenda"

    "kesho"

    "kwsho?"

    "ndio, kwani hujajiandaa bado"

    "ss.. Ss. Sawa tu, hata leo twende"

    "kesho mapema..."

    "sasa, twende kwetu basi ukapajue vyema, na wazazi wajue kuwa wewe ndio tajiri yangu"

    "usijali,... Tutakwenda"

    "lakini wazazi wangu wanatakiwa kufahamu hili"

    "kwani nimekataa?"

    "sawa"

    Shaimati aliondoka, lakini alipofika mbele akakumbuka kua mwenzake maimati kafuatilia pete yake, hivyo anaweza kuipata leo leo afu akampa suria na akisha mpa tu,. Suria haendi popote hata kwa kwa nini haendi... Shaimati akaamua kupanga safari siku hio hio,... Mana ilikua waondoke kesho ikiwa ndio siku yao ya saba toka waje duniani, sasa shaimati kaamua kuindoka mchana huo huo kabla maimati hajaipata hio pete...

    "mbona unarudi dada"

    Suria alimuuliza shaimati au shamimu. Mana kaenda mbele afu karudi...

    "nataka tuondoke sasa hivi"

    Aliongea shaimati huku surian akianza kutabasamu...

    "basi twende kwetu"

    Aliongea suria, lakini shamimu au shaimati alimsogelea na kumwambia

    "hapana... Twende leo, kesho tunarudi rasmi kuwaaga wazazi"

    Aliongea shaimati lakini suria hakupenda kuondoka bila kuwaaga wazazi wake...

    "lakini ni vyema nikawaage... Ili niweke na hii baiskeli yangu"

    "sikiliza we surian... Wazazi wako wamekusomesha kwa hali na mali ili upate kazi, sasa umepata kazi unaringa ringa... Sawa we nenda lakini ujue kazi ndio basi"

    Aliongea shaimati kisha akaondoka... Sasa suria na wazazi wake humtoi,.. Aliachana na shaimati kisha akapanda baiskeli yake mpaka kwao.. Lakini alipofika kwao geti lilikua limefungwa kuashiria mama yake hayupo, mana baba yake kaenda kijiweni... Ila mama yake hayupo hivyo huenda kaenda sokoni... Suria aliegemeza baiskeli yake kwenye geti lao la mabati kisha akawa anakimbilia kule walipo achana na shaimati, au shamimu kama anavyo mjua yeye. Lakini wakati huo shamimu anamuangalia tu huku akicheka.... Suria alikua anawahi huku akiwaza maneno alio yasema shaimati kua

    "hapana... Twende leo, kesho tunarudi rasmi kuwaaga wazazi"

    Aliyakumbuka maneno ya shamimu, na shamimu akatokea mbele yake kama vile hakumuona.....

    "dada? ... Dada?... Dada.?... Nipo tayari, twende sasa"

    Shaimati alifurahi sana huku akicheka katika moyo wake,... Leo ikiwa ni siku yao ya sita toka siku wanaingia duniani,... Lakini shaimati anailazimisha safari ili suria asije kupata kinga ya pete...



    Sasa huku kwa maimati kakaa kwa kutulia akivizia pete ivuliwe, ili ampe suria aivae... Na kesho wakiondoka waondoke bila mwanaume msafi, lakini bila kujua leo shaima anaondoka na suria... Mwanaume aliopendwa na jini mwenzie....









    Kila kiumbe kilicho umbwa kwa mikono ya Mwenyezi Mungu hapa duniani, kina hisia za kimapenzi kwani hata wadudu wenyewe wana hisia za mapenzi, sisimizi, viroboto, chawa, kupe, nzi, mbu.. Hao ni baadhi ya wadudu na wao wanafanya mapenzi kulinga na hisia ambazo wameumbwa nazo, sasa itakuwaje kwa upande wa majini?.. Ni jambo lisilo pingika kua maimuna alijikuta anampenda kijana surian ama suria,.. Na suria ndio mwanaume pekee ambaye katimiza vigezo ambavyo Murati sabaha anavitaka,.. Na maimuna na mwenzie shamimu wametumwa kuja duniani kutafuta mwanaume msafi, sasa mwanaume huyo waliompata na maimuna nae kampenda na hataki aende kwa Murati sabaha, lakini hapo hapo shamimu anataka surian aende kwa Murati sabaha,...



    Ikiwa ni siku ya sita toka kuja kwao duniani,.. Kesho ni siku yao ya saba siku ambazo hawatakiwi kupitisha, hivyo kesho ilikua ni safari yao ya kurudi ujinini, wawe wamepata au hawajapata, lakini leo shaimati yupo safarini na suria... Katika ufukwe mmoja mkoani tanga, shaimati alifika akiwa kavalia mavazi meupe, hayo ni macho ya shaimati, lakini kwa upande wa suria yeye anaona kama uwanja wa ndege, unaona sasa tofauti iliopo hapa... Shaimati yeye kama yeye, anaona yupo katika fukwe za bahari na ndivyo ilivyo, lakini suria yeye anaona kama yupo katika kiwanja cha ndege,... Hivyo suria kapigwa kiini macho mana akiona wanaingia katika maji atauliza huku ni wapi na hatakiwi kujua mana hata kule ujinini hutojua ni wapi, sasa shaimati na surian wanaingiza miguu kwenye maji, lakini surian yeye anahisi kupanda ndege ya kuelekea dubai,... Ndani ya ndege kweli kuna abiria lakini ni kiini macho ili surian asijue anakwenda wapi kupitia maji,...



    Sasa kitendo cha shaimati kugusa maji,.. Na kule maimati kapata ishara kuwa mbona jini mwenzie anarudi nyumbani ingali siku bado,... Pale pale akafanya mawasiliano na jini mwenzie...

    "shaimati, kuliko waenda leo"

    Aliuliza maimati huku shaimati akicheka sana....

    "hahaha, hahahaha... Ahahaha... Hahahah.. Hahahaha.... Nimeamua kuondoka leo"

    Aliongea shaimati, lakini maimati alipata mashaka kutokana na vicheko alivyokuwa akicheka shaimati

    Maimati hakutaka tena kusubiri pete ivuliwe na asha hivyo, ndani ya sekunde chache, maimati alionekana katika fukwe za bahari akiwa anafuata nyuma mana alihisi ni lazima shaimati anakwenda na surian....



    Kweli aliwakuta njiani kutokana na usafiri wao wanao utumia, lakini suria yeye anajua yupo katika ndege kuelekea dubai kufanya kazi,...

    "shaimaaaaaaaat"

    Maimati aliita kwa hasira kubwa baada ya kumuona suria akiwa sambamba na shaimati, na mbaya zaidi walishavuka mipaka ya ujinini na duniani,.. Kuna mahali binadamu hata uzamie vipi huezi fika.. Na hapo ndio himaya ya mipaka yao... Huko chini kuna viumbe vya kila aina, amaki wa ajabu ajabu.. Na pia kuna maisha mengine utafikiri ni duniani, lakini huku majumba yao yote ni ya kifahari, yaani yaliojengwa kwa matofali ya dhahabu, yaani nyumba imesimama kwa madini tu,... Kumbuka hata madini yote duniani yanamilikiwa na majini, na ndio mana kuna mahali mpaka mtu afe ndipo madini yatoke,.. Hapo ujue kuna jini mchafu, lakini mahali kuna jini msafi au mzuri, hapo hapahitajiki kafara lolote, zaidi ya juhudi za mchimbaji (nikimaanisha kwenye migodi)...

    "nilikwambia... Surian anakwenda lakini huamini"

    Aliongea shaimati wakati huo maimati yupo kwa mbele, lakini haonekani, hivyo suria pia hajui kama shaimati kuna kitu anaongea nacho, yaani anahisi maisha ni ya kawaida...

    "ni sawa, umeshinda... Lakini utajua kwanini sitaki suria aje huku... Najua ipo siku nawe utapenda,... Ahsante sana"

    Aliongea maimati kwa hasira sana, lakini pamoja na kukataa kwake surian asije huku, naye alijiunga katika safari hio ili Murati sabaha asijue kuwa maimati alikua tofauti nae, sasa hapo suria ndio anamuona maimati kama vile abiria ambaye amepanda ndege hio,.. Na kama unakumbuka kule duniani, suria alimuona maimati mara moja tu pale wakati alimkosa kosa kumgonga kwa baiskeli, kuanzia pale maimati hakuonekana mbele za suria, japo alikua nae sambamba kila hatua,



    Nani alikwambia safari ya majini huchukua muda,... Ndani ya dakika chache tu, wapo katika himaya yao, lakini surian yeye anajua safari ndeefu kumbe hata dakika mbili hakuna,.. Sasa kama kawaida shaimati hakutaka kuipoteza taswira ya mji wa dubai,... Hata mazingira yalikuwa kama dubai, hio yote ni kumfanya surian asijue lolote,.. Lakini wao wakiangalia mandhari yao, wanaona mapango makubwa makubwa... Lakini surian akiangalia mandhari hio, naona maghorofa makubwa makubwa tena ya thamani sana,.. Sasa kumbe macho yake yanapo ona ndivyo anavyo ona... Lakini nyuma yake surian, ni mapango makubwa wanayapita majani mzuri sana, miti, wanyama wa kila aina.... Lakini hata akigeuka haoni msitu wala mapango, na akigeuka kuangalia nyuma, na kule mbele yake ni msitu afu nyuma yake anaona jiji la dubai... Akirudisha macho mbele, anaona ni jiji vile vile, kwahio hapo macho yake yalipo angalia ndipo yanapo ona, hivyo anacho kiona mbele sicho kilichopo nyuma yake... Nadhani mumenielewa ndugu wasomaji wangu...



    Ndani ya falme ya majini Murati sabaha na wafuasi wake wengi sana, wakiwa katika hali ya kufurahia ujio huo,... Surian anashangaa kumbe dubai kuna warembo kiasi hicho, watoto weupe haoni mweusi hata mmoja, mpaka sasa surian anajua yupo dubai, kumbe yupo ujinini kwenye falme za majini huko chini ya bahari,...

    "hakika mumeifanya kazi vyema kabisa... Maimati na shaimati, hongereni sana"

    Aliongea Murati sabaha malikia mkuu wa kaya yao,.. Japo yupo kuu zaidi lakini katika jimbo hilo mkuu ni sabaha, na yeye ana asili moja tu ya ujini hana asili mbili.... Jamani kna aina 360 ya majini, na majini wengine ni watu kama akina maimati na shaimati, ikiwa na maana kuwa wapo majini walioshiriki tendo la ndoa na binadamu hivyo kupata mtoto mwenye asili mbili, na ndivyo ilivyo kwa wazazi wa shaimati na maimati

    "Murati sabaha? Sedutu potie santuu dubai rikati"

    Shaimati alimwambia Murati sabaha kuwa

    "Murati sabaha? Mtu huyu anajua tupo dubai kikazi"

    Hapo nimekutafsiria kwa lugha yao walio itumia ili surian asijue chochote, kwahio hata Murati sabaha kuskia hivyo akatumia njia hio hio kumkaribisha suria

    "waoooo kijana karibu dubai, hii ndio himaya ya Murati sabaha"

    Aliongea Murati sabaha huku surian akikaribia ndani, lakini hapo kwenye huo mtaa, kuna majumba ya kweli, hivyo surian hakuwa akiona kiini macho tena, ila akitoka mbali ya hapo ndipo ataona kiini macho.. Alishangaa nyumba nzima imejengwa kwa dhahabu, yaani hata kiti alicho pewa akalie kilikuwa ni dhahabu tupu, yaani hakuna mbao wala chuma hapo ndani.... Kama unavyojua majumba ya kifalme yalivyo, sasa hii ni falme ya majini... Wakili wenyewe wa madini yote yatokayo chini... Kama kuna dini linatoka juu, basi hilo sio lao... Ila yale madini yote yachimbwayo... Wamiliki ni hawa.. Sasa kwanini kila kitu kwao kisiwe dhahabu.. Surian alibaki kushangaa lakini yupo jini mmoja aliokua akiumwa na roho kwa kitendo cha suria kuja katika falme za majini.... Maimati hana raha kabisa kwani hakupenda surian aje huku kwani kampenda awe mume wake, na akija huku uwezekano hakuna na ndio mana hakutaka aje huku...

    Shaimati alitoka nje na kumsalimia maimati kama kumkejeli, lakini maimati alitulia tu kwani shaimati hajajua uchungu wa mapenzi...



    Huku duniani katika saluni ya asha, dada yake surian, akiwa bado anapiga hela kwa wateja walio miminika,... Marafiki wa asha wanajiuliza asha kagusa wapi,

    "hivi amina,.. Unajua bado sielewi"

    "ulizani ni wewe tu fatu... Jana si tulikaa pale wateja hakuna tena asha akawa analalamika kweli kodi inafika ajui atalipa na nini, hebu ona leo wateja walivyo wengi, afu huezi amini kapandisha bei ya saluni lakini ona wateja walivyo jaaa..."

    Aliongea amina ambaye ni rafiki wa karibu wa asha...

    "lakini amini.. Inaonekana hata mavazi yake yamechangia wateja kuja... Hebu ona toka afungue saluni, sikuwahi kumuona akiwa na hijabu... Leo kavaa"

    "enheee...danga lake lilee, linamfuata"

    "heee, sasa asha atatoka kweli"

    "asitoke kwa nini, mbona kila siku anatoka nae, anakwenda kubinjuliwa anarudi"

    Walikua ni marafiki wa asha wakiwa wanajadili mabadiliko ya asha, msichana mwenye mavazi ya kichefu chefu,.. Sio kichefuchefu kua mavazi yametoboka lahasha... Bali ni mavazi yasio stahili mbele ya jamiii, anaweza hata kuvaa kanga bila hata chupi, na akatembea mtaani, sasa imagen na umbo lake... Afu avae hivyo.... Ndio mana wengi hushangaa pale asha anapo vaa kiheshima mana sio staili yake ya uvaaji...



    Kwanza jamaa kashangaa kuona mavazi ya asha,... Duuuu.. Mpaka akasita kwenda pale saluni... Kisha akaamua kwenda

    "oohhh asalam aleykh"

    Alikuwa ni mpenzi wake na asha kaja kumtembelea kam ilivyo oda ya kila siku...

    "waaleykh msalam hali vipi"

    Watu walishangaa asha ndio wa kupokea salamu hio... Lakini pamoja na hayo asha aliitikia huku akiwa bize sana ikiwa ni mishele ya saa 11 za jioni lakini wateja hawakauki, yani mpaka asha kachoka sasa

    "vipi leo, naona upo bize sana mamii"

    "yes, kwa leo sina time na jambo lolote, labda tuangalie wiki ijayo"

    "wiki ijayo.... Asha ivi umetumia akili kwa kusema wiki ijayo"

    "sasa we huoni nipo bize"

    Asha alimjibu mpenzi wake kwa hasira, kwani alikuwa yupo bize sana

    "ni sawa, lakini wasaidizi si wapo"

    "nimesema siondoki hapa"

    Duuuuu asha leo alikua mkali hata kwa mpenzi wake,.. Yaani ukiwa na hio pete, utaanza kuvichukia vitendo ulivyokua ukivifanya,... Tena ndio utakua mstari wa mbele kufundisha wenzio ambao wana tabia za ajabu



    Baada ya masaa mawili akafunga saluni, huku wateja waliobaki wakiahidi kurudi kesho ili kufanya sevisi ya nywele zao... Asha akakaa chini na wasaidizi wake kisha akaanza kuhesabu hizo pesa....

    "eeehh mungu ahsante... Leo nimeingiza milioni na laki mbili"

    Aliongea asha huku akiwa haamini,.. Na hapo akili ya asha inawaza kuanza kufanya ibada, yaani hio pete ni kiboko unapata riziki na bado inakulazimisha kufanya yalio mazuri kwa mungu na kwa binadamu wenzako... Basi asha aliwalipa wale wasaidizi wake ile laki mbili yote na wasaidizi walikuwa watano... Kama unavyojua shughuli za saluni ya kike ina vitu vingi vya kufanya hivyo ukiwa mwenyewe utapata tabu pale wateja wanapokua wengi,... Leo asha hakupanda haisi, kachukua taxi kabisa mpaka nyumbani... Ikiwa ni mida ya saa moja hivi



    Alimkuta mama yake hana raha kabisa,

    "Shikamoo mama"

    Asha alimsalimia mama yake, lakini kabla mama hajaitikia... Mara baba yake suria kafika

    "mama asha, huyo suria bado hajarudi tu"

    Baba alimuuliza mkewe kuwa suria hajarudi...

    "kwani huko msikitini hayupo"

    "sijamuona na kule shule uliko sema kaenda, nimeenda nimeambia huyo mtu hajafika"

    Aliongea baba yake asha huku asha akiingilia kati na kusema

    "nyie mnamtafuta suria,... Yaani mtu mzima na akili zake mnamuwazia baba.... Sawa lakini baiskeli yake si ile pale"

    Aliongea asha lakini mama yake akasema

    "baiskeli niliikuta hapo nje..."

    "lakini mama na baba... Yule ni mtu mzima atakuja tu... Au mpigieni simu"

    "simu yake haipatikani, na hajawahi kuzima simu... Hapo ndipo tunapokua na mashaka"

    Aliongea baba yake asha huku asha akivuta kumbukumbu fulani anayo ijua...

    "enheeeeee, safi nimekumbuka"

    Aliongea asha huku mama na baba wakipumua kuona Afadhali asha kajua surian kaenda wapi...

    "kaenda wapi kwani"

    Aliuliza mama huku wakiwa makini kumsikiliza asha

    "jana nilimsikia suria kwa masikio yangu mawili...."

    Aliongea asha huku akiwashtua wazazi wake kana kwamba labda suria kabadilika tabia...

    "kasema nini mdogo wako? Hebu sema"

    "jana jioni suria aliiiii"

    Sasa asha kila akitaka kuongea uongo anashindwa, kwasababu ile pete haitaki uongee uongo bali inataka uongee ukweli,.. Sasa asha alitaka kumchomekea mdogo wake kisa anapendwa na wazazi, sasa pete haitaki uongo...

    "sasa aliiii aliii nini"

    Mama huyo alimwambia mwanae hivyo, kwani hajui hapo aliposema aliii kumbe hio pete ndio imemzuia kuongea uongo.. Sasa asha baada ya kuona anashindwa kuongea uongo, aliamua kuingea ukweli halisi ambao anaujua yeye kuhusu mdogo wake..









    Familia ya mzee Rashidi haipendani sana kwani wazazi hao walimpenda mtoto mmoja, kitendo ambacho mtoto mwingine amekosa elimu kutokana na upendeleo wa jinsia, wazazi hao walipenda kumsomesha mtoto wa kiume zaidi kuliko mtoto wa kike hivyo mtoto wa kike kujenga chuki katika moyo wake, hivyo hata ikifikia wakati wa kumuongelea mdogo wake, hujikuta akitaka kumchongea kwa kila jambo, kwani tayari alisha jenga chuki juu yake, kwakua kapendelewa elimu ya juu kuliko yeye, kwani yeye alipofeli tu wazazi wakaamua kumuacha, kutokana na mabadiliko yake ya kimavazi, hivyo kwa kitendo hicho wazazi wakaona watapoteza pesa bure, ni bora wamsomeshe mtoto wa kiume....



    Sasa leo suria haonekani nyumbani toka alipo aga kwenda shule baada ya kuchelewa kutokana na simu ambayo alipigiwa na kampuni fulani kwa ajili ya intaviu,... Hivyo alipoulizwa asha akajibu anafahamu ukweli wote, lakini asha alitaka kuongea uongo, ila pete alio nayo hamruhusu kuongea uongo.. Hivyo akaamua kusema ukweli ambao yeye anaujua



    "jana jioni suria alipigiwa simu kuwa anahitajika kwenye intaviu ya leo,.. Kwahio labda atakuwa kaenda huko"

    Ni kweli alicho ongea asha kuwa siku ya jana jioni suria alipigiwa simu na kampuni fulani....

    "lakini, ni kweli hata asubuhi alijaribu kupiga hio simu akaambiwa kuwa haikuwa simu yake walikosea tu,... Ndipo nikamwambie aende ahule tu ili asipoteze kote kote... Sasa ndio hajarudi mpaka sasa hivi"

    Aliongea mama yake surian huku mzee akishangaa

    "alaaa... Kumbe jana aliitwa"

    "ndio, aliitwa lakini ile simu ilisemekana sio yakwake hivyo kwa sasa hatujui kaelekea wapi"

    Aliongea mama huku huzuni ikizidi

    "mtaumia na presha bure wazazi wangu, tatizo mmezidi kumpenda mno, haya sasa masaa kadhaa tu mumesha anza kutaka hata kulia"

    Aliongea asha kisha akaingia zake ndani, huku wazazi wakimshangaa asha

    "huyu mtoto nae ana nini huyu... Badala awe nasi kupata habari za ndugu yake... Anataka kunanihii tena"

    Aliongea baba yake asha huku mzee akichungulia nje kana kwamba Anaweza kumwona mtoto wake kama atatokea kwa nyakati hizo,.. Lakini hakukua na lolote,...



    BAADA YA SIKU TATU KUPITA



    Katika falme ya majini, suria ali laani sana kwa kitendo cha kupewa kazi ya kuwa Gardener Boy (mtunza bustani) ikiwa ni kwenye mazingira mazuri mithili ya peponi, na ndio maana huku hawataki watu wachafu kwani wao wenyewe ni wasafi, hivyo wataishi na msafi vilevile kama wao



    Surian alilaani kazi hio kwani aliambiwa ni kazi za ofisini lakini mwisho wa siku anapewa kazi ya kunyweshea maua na kiti iliopo katika bustani hio,... Alikataa lakini alikubali baada ya kutajiwa malipo yake kuwa kila mwisho wa mwezi atalipwa dhahabu yenye ukubwa wa kidole gumba cha mguu wake,... Hakuamini kuskia hivyo, na ndipo akakubali kufanya hio kazi japo ni kazi za watu ambao sio wenye elimu kama yake,... Majini wote walipo hapo wakiwa wamevalia mavazi meupe mithili ya malaika,... Lakini suria yeye hajui kama anaishi na majini na yeye anajua yupo nchini dubai, kwani kawekewa kiini macho juu ya mazingira ambayo atayaona...



    Siku moja surian akiwa katika moja ya kazi yake hapo bustanini, tena alikuwa akiikatia bustani vyema sana

    Alikuja Murati sabaha kama kumjulia hali mfanyakazi wake,...

    "haha kumbe unaweza kukatia nyasi vizuri"

    Aliongea Murati sabaha huku akizidi kusogea katikati ya bustani,...

    "ndio dada, kwakua nalipwa, sina budi kufanya vyema katika kazi yangu"

    Aliongea suria huku akiwa bize, na unaambiwa hio bustani hua haina haja ya kuweka mfanyakazi, na sio lazima kuweka binadamu... Ila Murati aliamua kuweka binadamu badala ya jini mwenzie au kuacha kabisa...

    "ok ni sawa... Aaa kwa sasa nadhani utakuwa umechoka, kakoge upumzike sasa"

    Aliongea murati sabaha akiwa kama malikia wa eneo hilo,... Kweli suria aliacha ile kazi na kuingia zake bafuni ili apate wakati wa kupumzika... Toka surian afike huku hajui msikiti ulipo hivyo leo aliona ni vyema akimaliza kuoga aulizie msikiti ulipo..



    Kama kawaida majini hua sio wachafu hivyo kuanzia choo mpaka bafu hukaa nje kabisa tena mbali kwani wanajua madhara ya choo... Sio huku dunia ulipolala kuna choo... Kana kwamba unaishi na shetani karibu,... Ujinini hakuna kazi, majini walikua wakicheza na njiwa walio weupe mithili ya mavazi yao yalivyo, murati Sabaha nae pia alikua mpenda wanyama sana hivyo katika kuruka ruka na njiwa, akafikia kwenye dirisha ambalo surian anaoga... Jicho la kwanza lilitua katikati ya mapaja ya surian

    "Allahhitari (mungu wangu)"

    Murati sabaha alitahamaki kwa kushuhudia maungo ya suria akiwa anaoga, na hua kwenye huo mji wao hawa majini, hua wanaishi kama binadamu, hua hawatumii uhalisia wao, utmgusa mtagusana kabisa mtakula pamoja mtafurahi mapoja nao,... Yaani hawana uhalisia wa kijini ila wakiwa mbali na hapo ndio hutumia uhalisia wa kijini.. Ni kama mtu alio ishi mjini sasa akienda kijijini kwao anafanya kama pumziko mana kupo free hakuna bugza kama mjini, hivyo hata hawa majini wakiwa kwao, utawaona kama binadamu, hawatumii nguvu za kijini kama walivyo,... Hivyo Murati sabaha alipo ona maumbile ya kiume kwake ilikua kama ajabu, kwani hakuwahi kuona maumbile ya kiume ya binadamu,... Sasa akiwa kakaa kitandani kwake anahema sana,.. Huku akiyakumbuka maungo yale,..... Kwake ilikua kama ajabu kwani yeye na surian ni asili mbili tofauti, suria ni binadamu kamili, na Murati sabaha yeye ni jini kamili, na hana asili mbili kama maimati na shaimati...



    Sasa tukija huku duniani, ikiwa katika duka ambalo anauza faima... Akiwa kakaa kiunyonge sana kwani ni siku ya tano kwake hamuoni surian ambaye ni mchumba wake... Mana kamzoea sana....

    "shkamoo mama"

    Faima alikumbuka wakati alipokwenda kwa akina surian kumuulizia

    "marahaba mwanangu.. Tena Afadhali umekuja.... Hivi surian upo naye huko"

    Aliongea mama yake suria huku faima akishangaa, kwani yeye naye kaja kumuulizia suria sasa kabla hajauliza, anashangaa naye kuulizwa,

    "mama, hata mimi ndio nimekuja kumuulizia"

    Aliongea faima wakati yupo nyumbani kwa akina surian...

    "jamani, hivi mwanangu kaenda wapi"

    mama alianza kulia kwani kila mtu aliokua karibuni na surian hajui surian kaenda wapi,...



    Faima alimaliza kumbukumbu yake wakati wa asubuhi alipo pitia kwa akina suria,... Faima alikua hana raha kabisa katika moyo wake....

    "faima, una nini mdogo wangu... Mbona upo katika mawazo makubwa kiasi hicho"

    Alikua ni dada yake faima aliokwenda kwa jina la ZAMINA,...

    "dada zam, suria wangu simuoni, yapata siku ya tano leo, sijamtia machoni"

    Aliongea faima huku machozi yakimlenga na hapo ilikua ni dukani anapouzia nguo, na ikumbukwe kuwa, hata wale majini walikuja kununua nguo hapa kwa ajili ya kutembelea uraiani,...

    "yaani wewe sjui ukoje... Ina maana kumbe unawaza wanaume... Aahh tu umesha niuzi"

    Aliongea zamina, huku akipiga hatua za kuondoka

    "sasa niwaze nini... Surian ni mume wangu mtarajiwa... Leo ni siku ya tano... Nashindwaje kuwaza"

    "sawa, we wazaaaaa.. Wazuaaaa, kisha ukutwe na boss wako uikose hio kazi"

    Aliongea zamina huku akiondoka kabisa, na hio ni dhahiri kuwa zamina hakubaliani na mdogo wake awe mke wa surian...



    Huku kwa mama surian, kakaa katulia kimyaa kajiinamia huku asijue afanye nini...



    Huku kijiweni kwa baba yake, anatangaza kila mahali kuhusu kupotea kwa mtoto wake, yaani wanavyo mpenda suria, utafikiri ni mtoto mdogo, kumbe ni mtu anajielewa vyema...



    Huku kwa asha, kama kawaida anapiga hela tu... Wakati huo Pete ipo kidoleni inatoa riziki zake,...

    "hivi unajua siri ya wateja wa asha"

    Aliongea rafiki yake mmoja aliokuwa akiona umati wa wateja wakimiminika katika saluni ya asha, tena sasa saluni imekuwa na imeng'aaa, na pia kaongeza madraya ya kusukia sjui kushonea, aah mimi sijui



    "siri?? Siri gani tena nawe Fatuma"

    Aliongea amina na hao ni marafiki zake wakubwa wa asha lakini sasa hivi wanaanza kumfitinia baada ya asha kuanza kuneemeka kibiashara

    "acha uzoba amina.... Sasa hivi mdogo wake haonekani, na inasemekana keshamtoa mdogo wake"

    "weeeeeeeeee fatuma wewe... Maneno gani unaongea hayo"

    "sasa mimi ndio nakwambia sasa... Siku asha anaanza kupata wateja.. Na mdogo wake ndio akapotea poteeee"

    "mmmhhh we Fatuma mbona una makuu hivi"

    "ndio ujue sasa... Hivyo wewe waone tu wateja wamejaa pale.. Ila kuna damu ya mtu pale"

    Aliongea fatuma huku amina akibaki mdomo wazi kwa taarifa hizo ambazo fatuma anazitoa...

    "lakini mbona kama kweli"

    "sio kama kweli... Ni kweli"

    Marafiki hao walikua pembezoni mwa saluni hio, wakibwata umbea juu ya asha kupiga hela kwa wakati huu mdogo wake kapotea.....



    Sasa tukirudi huku katika ngome ya mjini, ikiwa ni usiku huku kwa majini, lakini kwa duniani ni mchana kweupe

    Suria akiwa kaketi mahali alikua akiskia harufu ya chakula kizuri sana lakini hakijulikani kinapo pikwa, mana hapo ni kama mji na kila nyumba imejengwa kwa vimiminiko vya dhahabu,... Wapo wafanyakazi wa kawaida ambao ndio wanamletea surian chakula,... Na hao sio wafanyakazi nao ni majini ila surian yeye anajua ni wafanyakazi, yaani yeye hajui kitu mpaka wakati huo...



    Sasa baada ya mfanyakazi huyo kuondoka, murati Sabaha alikuja...

    "aahh boss, karibu"

    surian alimkaribisha, na hata wao huvaa nguo za kawaida ila kwa mara chache sana na nguo zao zipo kama nguo za wahindi zile,... Mitandio mingii, gauni mpaka chini, yani ni heshima mwanzo mwisho..

    "ahsante sana, vp chakula unakionaje"

    Aliuliza Murati sabaha huku suria akijibu kuwa

    "ni kitamu kwakweli,..."

    Alijibu suria huku murati akikaa katika kiti cha kimalikia,... Sasa Murati kila akimuangalia suria, anakikumbuka kiungo alicho kiona bafuni, hakuwahi kuona kiungo cha binadamu..

    "numepika mimi"

    "waoooo safi sana"

    Aliongea suria huku murati nae akitabasamu,...

    "basi nikuache ulale kijana"

    "sawa boss"

    "kwani kuna ulazima uniite boss"

    "ndio, mana ndio unayeniweka huku dubai"

    "hapana, niite dada"

    "sawa dada"

    Suria alikubali kumuita sabaha dada, lakini Sabaha alikua akimchungulia kuwa suria alihisi nini baada ya Murati sabaha kuondoka... Lakini suria alikuwa wa kawaida tu...



    Saa kumi na moja alfajiri, ilisikika milio ya kimapenzi tena ilikua mikali sana hapo ndani,.... Huezi amini alikuwa ni Murati sabaha akiwa na suria... Kumbe Murati sabaha naye kampenda kijana surian... Hivyo usiku wa leo, hakutaka kuchelewa... Lakini sasa surian anajua yupo na faima, lakini hapo chumbani yupo na Murati sabaha....

    "faima mpenzi wangu... Nakupenda"

    Aliongea suria huku kiungo chake kikiwa ndani ya mwili wa Murati sabaha, lakini yeye suria anajua yupo na faima.... Sasa hii ni dhahiri kuwa ni ndoto na wala sio kweli... Lakini sasa maimati alihisi alfajiri ya leo kuna jini mwenzie katumia nguvu za kijini, mana wakiwa hapo hawatakiwi kutumia uhalisia wao... Sasa maimati anajua muda ambao wao majini huwaingilia wanadamu kimapenzi, akajua lazima surian yupo katika hatari ya kufanya mapenzi na jini....

    Na ni kweli,... Sasa maimati anakuja tena kwa kupaa, kwani alishajua kuwa kuna tatizo juu ya mtu ampendaye, lakini sasa mbaya zaidi aliokua na suria ni huyo malkia wao.. Sasa huku chumbani, murati Sabaha nae anashtuka kwa kuhisi kuna jini mwenzake anatumia nguvu za uhalisia wake,.. Wakati huo surian ndio anafika mshindo lakini Murati keshajitoa saa mingi sana katika mwili wa suria kana kwamba uchafu unaomtoka surian hautakiwi umguse jini yeyote na ndio mana mwanaume akiamka asubuhi, anakuta kajitandika bao la kisigino.. Sasa Murati anakuja kustuka anashangaa kuna jini mwenzie naye anakuja katika chumba hicho hicho... Murati akapotea na hapo hapo maimati anaingia, tena alikuja akiwa anaonekana live bila chenga.... Alimkuta surian anajikamua kumalizia utamu wake... Ndipo maimati akaamua ku...









    Katika ulimwengu huu kuna viumbe vingi sana, lakini tukija katika ulimwengu wa majini, kuna aina 360 za majini, na hapo hapo kuna wazuri na wabaya.. Majini wabaya ndio hao mashetani wenyewe, ambao huwatakia wanaadamu kufanya mabaya na kuacha kutii amri za Mwenyezi Mungu,... Lakini pia wapo majini wazuri ambao wao hawapo kwa ajili ya kumfanyia kibaya binadamu wala wanyama... Yaani hao wapo kimsaada zaidi pale wanapo kupenda kuwa nao,... Na wapo majini wa kike walio olewa na binaadam, lakini ndoa hizi hua zinajulikana ni za kawaida, hivyo hakuna atakae jua kuwa mwanaume fulani kaoa jini, ila yeye mwenyewe ndio anajua kaoa jini au pia hata mume huenda asijue kama kaoa jini, mana majini yana uwezo wa kuwa kama binadamu na hata maisha Anaweza kuishi kama binadamu... Yaani kila anachokifanya binadamu hata jini Anaweza kukitekeleza vilevile, hivyo upo uwezekano wa mwanaume kuoa jini bila ya yeye kujua... Lakini katika majini hao kuna majini wenye asili mbili, kuna majini wenyewe ambao hawana asili mbili... Yaani baba na mama ni majini.... Sasa kuna wale majini ambao walioshiriki tendo la ndoa na binadamu.. Wale ndio walituletea majini ambao wana uwezo wa kubadilika kuwa kama binadamu wa kawaida na usijue mpaka kufa kwako.. Na mwisho wa siku wakipata watoto, jini huchukua watoto wake... Hivyo kukawa na jamii ya majini wenye asili mbili... Ambao majini hao wakiingia duniani huezi jua kama ni jini.. Kwani utamuona ni mvulana mzuri tu... Utamuona ni msichana mrembo na mwenye tabia njema... Na pia hakuna mipaka juu ya kufanya mapenzi pale utakapo amua... Tuchukue mfano wa wanyama na binadamu... Hapo hakuna mipaka ya kufanya mapenzi na mnyama, lakini hairuhusiwi kufanya lakini pia hapo hapo unaweza ukafanya kwa akili yako jinsi ilivyo kutuma kufanya mapenzi na mnyama lakini hairuhusiwi lakini pia hakuna mipaka, kwahio ni hivyohivyo hata kwa majini wanaotaka kufanya mapenzi na binadamu hua hakuna mipaka sema sasa mtu akijua kuwa huyu ni jini ndio hairuhusiwi lakini hakuna mipaka juu ya mapenzi, Ilimradi jini mwenyewe kakubali kulala na binadamu, hapo hakuna mipaka....



    Lakini sasa hawa majini wenye asili moja wao hawana uwezo wa kuonekana kama binadamu pindi wawapo duniani,... Hivyo jini huyu akija duniani hawezi kuonekana... Na akionekana basi unaweza kumkuta ana mguu wa ng'ombe au farasi... Au ukamfunua katika sehemu za siri ukakuta hakuna njia, kote kuna nywele.... Kwasababu hana asili mbili, na wao wakitaka kuoana na binadamu, basi ni lazima binadamu akaishi katika falme za majini, kule ndio atakua kama binadamu, ila akija duniani atakua kituko.... Sasa na hawa wa asili mbili, wao wakitaka kuoana basi hawaruhusiwi kuishi katika falme za majini, hivyo wanatakiwa kuishi duniani na sio chini ya maji... Hivyo kwakua maimati alimpenda surian, hivyo hakutaka aje huku majini, kwani yeye maimati alikua tayari kwenda kuishi duniani kwa ajili ya surian....



    Sasa huyu Murati sabaha yeye ni jini mwenye asili moja,.. Na happ alipo hajawahi kufanya mapenzi live, na ili aweze kufanya mpenzi live na jini mwenzie au binadamu, ni lazima wafunge ndoa kwanza.... Lakini jini Murati sabaha alishikwa na tamaa ya mapenzi na kumjia surian katika ndoto kisha akafanya nae tendo la ndoa, lakini hapo haikutoa bikra yake kwani ndoto sio kitu cha uhalisia... Na hua sio akili ya mwanaume kufanya mapenzi pasina kutumia akili yake....



    Sasa kitendo hicho kilimkwaza sana maimati, kwani anampenda sana surian, sasa iweje awe anaingliwa kila wakati na Murati sabaha....



    NDUGU WASOMAJI,... NIMETOA MAELEZO MENGI KWANI SITAKI KUKUACHA NA MASWALI MENGI JUU YA SIMULIZI HIII.... HIVYO TUENDELEEE



    Maimati Alimkuta surian anajikamua kumalizia utamu wake... Ndipo maimati akaamua kuondoka katika himaya hio kwani asingeweza kugombana na mkuu wake,... Wakati huo surian anajiskia aibu kwani kuna mwanamke kamuona live akiwa anamalizia bao lake,... Hivyo alijiskia aibu hata siku hio hakutaka kutoka nje ili asije kuonana na maimati, na hapo surian hajui kama yupo katika falme za majini, bali anajua yupo dubai kikazi,.... Na hata hawezi jua nani kafanya nae tendo la ndoa katika nfoto kwani jini hapendi ajulikane hivyo akikujia hua anakuwekea taswira ya mwanamke yeyote yule, ili usijue wewe binadamu



    Surian aliingia bafuni na kufua nguo zake, ila jini aliomwingilia sio jini mbaya.....



    Maimati alimfuata shaimati na kumfokea sana kwani yeye ndio sababu ya surian kuja huku....

    "sasa umefanya nini?... Umeleta mtu afanye kazi au aingiliwe na Sabaha"

    Aliongea maimati huku shaimati akishangaa sana kuwa Murati sabaha kafanya jambo hilo ambalo hata wafuasi wake hawakuweza kulifikiri kabla...

    "unasemaje"

    "nakulaumu sana wewe... Nilikwambia, sitaki surian aje huku"

    Aliongea maimati kisha akaruka na kupotea,... Kumbe huku huku falme ya majini kuna wazazi wa kila jini, hivyo maimati alikwenda kwao,... Ikumbukwe kuwa kuna himaya yao ambapo ndipo ufalmeni kwao.. Na pia kuna kwao ambako ndipo alipo zaliwa.... Na kule kwao jini ni mama yake, ila baba yake ni binadamu wa kawaida na mtoto waliopata ni huyo maimati na mwingine mdogo alie itwa zubinati (zubeda) ... Majini ya majini bwana lazima yaishie na neno (ti)... Maimati alilalamika sana kwa wazazi wake, lakini wazazi walimshauri, kama kampenda kijana huyo basi ampe pete yake ili imlinde mana hawezi kugombana na Murati sabaha...

    "mamiii, pete ipo duniani"

    Aliongea maimati huku mama yake akishangaa kuwa pete kaiacha dunia wakati walipo kwenda kutafuta kijakazi wa kiume,...

    "unasemaje we maimati"

    "ndio mamii, dada yake suria ndio kaivaa pete hio, na toka aivae hakuivua"

    "akili zako haziko sawa muna... Unaachaje pete duniani"

    "nitakwenda kuichukua mamii"

    Alijibu maimati huku akilia kwani kitendo alicho kifanya Murati sabaha hakikumpendeza maimati....



    Siku zilizidi kwenda, surian kila siku asubuhi yeye ni kufua nguo zake baada ya kuingiliwa na Murati sabaha, hata suria anajiuliza ana inakuwaje, mana Amezoea kuwa hali hio humjia kila mwezi au miezi kadhaa kwa mara moja.. Lakini mbona huku dubai anachafuka kila siku,... Anasoma dua ya kulalia kila siku lakini wapi,... Na dua hio haiwezi kuzuia kwani tayari upo katika himaya yao,... Sasa yapata mwezi mmoja toka surian kuja katika falme za majini, lakini bado hajajua kuwa hapo sio dubai... Maimati kila siku anashuhudia jinsi surian anavyo fanya mapenzi na Murati sabaha... Na mpaka hapo kalipwa jiwe la thamani kama mshahara wa kazi yake,... Kwa sasa maimati yupo karibu sana na surian na hapo suria bado hajui kama maimati anampenda,

    "sasa hivi umezoea mazingira ya dubai"

    Aliongea maimati huku suria akijibu kua

    "ndio,... Sio mbaya sana"

    Alijibu suria lakini huku akiona aibu mana maimati alishamkuta suria kama mara tatu hivi akimalizia utamu wa ndoto... Lakini maimati akiwa hapo, ghafla alipata ishara ya kuvuliwa kwa pete, Kiukweli alishtuka sana mpaka suria naye akashtuka kutokana na sauti za mshtuko alizo zitoa maimati

    "mbona unanitisha dada maimuna"

    Aliuliza suria huku maimati akiwa hamjibu na badala yake alizunguka nyuma ya nyumba kisha akatoweka katika mazingira ya kutatanisha...



    Huku duniani, baada ya mwenzi mmoja kupita asha sasa anamiliki saluni kubwa,.... Sasa hapa ni kabla hajaivua pete,.. Kuna mteja aliokuwa akimuosha nywele baada ya kumpaka dawa zao wenyewe wanazijua... Sasa yule mteja alikuwa akilalamika kutokana na pete, kwani pete hio ilikua ikishika nywele za huyo dada hivyo kumsababishia maumivu wakati wa kuoshwa nywele, ndipo asha akadiliki kuvua pete hio na kuiweka pembeni... Hata kidole chake kilikua na alama ya pete kana kwamba pete hio haikuwahi kuvuliwa toka kuvaliwa kwake.... Sasa maimati yupo njiani kuja kuichukua pete hio mana hairuhusiwi kumpokonya ikiwa kidoleni, bali ni mpaka aivue



    Huku nyumbani kwa akina faima,... Faima kwa sasa hakua akiuza duka la nguo tena kwani mawazo juu ya surian yalizidi hadi kufikia hatua ya kuikosa kazi yake, mana kila wakati ni yeye na mawazo tu...

    "hivi faima... Huli, hulali... Kutwa kucha wewe ni mtu wa mawazo tu, hivi huyo suria ni mungu wako"

    Alikua ni dada yake na faima ndio aliemwambia faima maneno hayo,..

    "dada hujui tu, mimi naona uniache tu"

    "siwezi kukuacha.... Umeshapoteza kazi yako nzuri tu, kisa mwanaume"

    "dada ZAMINA, mbona unaongea sana... Mimi nampenda surian ndio mana sitaki akosekane moyoni mwangu"

    Aliongea faima huku zamina akirudia kwa kubana pua

    "eti nampenda staki akosekane moyoni mwangu... Kwa mwanaume gani, pamoja na elimu yake lakini kazi hapati... Akaona bora atoroke akaishi mbali na familia yake... Kama angelikua anakupenda hata simu si angekupigia?"

    Aliongea zamina huku wazazi wao wakiwasikiliza tu, mana hata mama yake hapendi mapenzi ya surian na fsima kwani wanapotezeana muda tu



    "asha atakuwa kamuua ndugu yake... Ona mjengo anao jenga"

    Hao walikua ni marafiki wa asha, wale akina amina na Fatuma ambao hawaamini mafanikio ya asha yalikujaje na hata asha mwenyewe pia hajui kuwa pete hio ndio sababu ya mafanikio yake...

    "heeee amina... Kamuuaje mdogo wake"

    Alishangaa fatuma baada ya maneno ya amina kumtoka

    "hivi wewe fatuma, huoni kabisa hizo ni pesa za haraka... Hebu ona ndani ya mwezi mmoja tu, saluni kubwaaa... Angalia ile nyumba anayo jenga pale bondeni, na ni mwezi mmoja tu"

    "lakini kama kweli Fatuma, ila we umejuaje"

    "kwani mimi si mtu mzima nimeweza kuchuja akili yangu"



    Katika saluni ya asha, maimati ndio anaingia,... Wateja walikua wamevaa nguo fupi sana kuliko asha kwani asha alibadilika kutokana na pete hio,.. Maimati alichukua pete yake na kuondoka zake, kwani alikuja kama upepo tu, hakutaka kuonekana... Sasa ile asha anageuka haoni pete,

    "hii pete imeenda wapi tena"

    Aliuliza asha lakini hajui kuwa pete hio ina thamani gani katika mafanikio yake,..

    "si uliiweka hapa"

    "ndio, niliiweka hapa kwenye kioo, sasa mbona haipo"

    "wewe niwashie mashine utaitafuta baadae"

    Aliongea mteja wake aliokuwa tayari katumbukiza kichwa chake katika draya wanayoitumia kuseti nywele...

    Sasa asha alijua ataiona tu, kwani haitokua mbali...



    Ilipofika jioni wateja hakuna hata mmoja, asha alianza kuitafuta ile pete kwani aliipenda sana kutokana na urembo wake, na ilimpendeza sana katika kidole chake,... Aliitafuta sana lakini hakuweza kuipata.. Hivyo yeye aliipenda pete hio kwakua ilimpendeza sana...



    Huku nyumbani kwa akina surian, wazazi wamesha kata tamaa juu ya ujio wa surian kwani ni mwezi sasa umepita toka surian kupotea...

    Ghafla asha katokea hapo nyumbani,

    "Shikamooni"

    Alisalimia asha huku wazazi wakiitikia na kumuuliza

    "asha mwanangu, hujasikia sikia hata fununu za ndugu yako huko"

    Aliongea mama yake asha huku asha akigeuka

    "mama,... Huyu mtu keshawatoroka tayari.... Alishapigiwa simu ya kazi anakwenda kulipwa milioni kumi,.. Aache kwenda kula na wanawake aje ale na nyie"

    Aliongea asha, ikiwa ni maneno ya uongo kwasababu ile pete inayo kataza uongo, hana tena katika kidole chake....

    "asha, mbona humpendi ndugu yako lakini"

    "mama, sio kuwa simpendi.... Mumemsomesha elimu ya juu, mimi mkaniacha, sasa ndio nataka niwaonyeshe kuwa hata mtoto wa kike ana uwezo.... Nyumba inakwenda kuisha, tutahamia... Na hata yeye akija ataishi tu... Pamoja na elimu yake kuwa juu lakini haniwezi kimaendeleo"

    Aliongea asha huku wazazi wakiwa kimya, mana kweli asha kaishia kidato cha nne tu,... Lakini mambo yake kwa sasa ni zaidi ya huyo aliesoma mpaka kumaliza maktaba nzima....



    Sasa tukija huku kwenye falme ya majini,... Surian alikuwa katulia ndani ikiwa ni asubuhi baada ya kufua nguo,... Ikumbukwe kuwa kule duniani sasa ni jioni, lakini huku ni asubuhi... Na sasa suria keshazoea katika swala la ndoto za mapenzi.... Yaani mpaka sasa kateua mpaka nguo ya kulalia iwe hio hio.... Lakini akiwa kakaa hapo, mara Murati sabaha akaja mbele zake

    "habari yako kijana"

    Suria alishtuka na kusimama kwa heshima, mana huyo ndio malikia wa eneo hilo,... Na huyo ndie anaye mwingilia suria usiku, lakini suria hajui

    "salama boss, Shikamoo"

    "ahsante, ila unaonekana kuchoka sana... Njoo upate supu"

    "hahaha hakuna shida boss"

    sasa wakati huo huo, maimati naye anatokea

    "usijali njoo utoe uchovu"

    Aliongea Sabaha mana anajua kweli ana uchovu mana kila siku anamuingilia....

    "hakuna tabu boss"

    "sawa basi, na kama unajiskia uchovu... Pumzika ndani"

    "ahsante boss"

    Sabaha aliondoka kisha maimati naye akaingia,... Lakini sasa Murati Alianza kuwa na wasiwasi na maimati kwani yupo karibu na suria muda wote... Murati aliingia chumba kimoja hivi,.... Lakini sasa kumbe Murati sabaha naye kuna jambo alikua akilifanya ndani ya chumba hicho.... Ni chumba chake, na juu ya Meza yake palikua na pete ya kiume, na hio pete ilikua ni spesho kwa ajili ya surian,... Murati kaichukua pete ile ya kiume kisha akaja nayo pale alipo surian, na hata maimati bado yupo na surian, alafu maimati kaja kumpa surian pete ya kike, na Murati sabaha naye analeta pete yake ya kiume ili surian aivae... Sasa wote nia yao ni moja, kinachotakiwa ni pete ivaliwe na pete ya mmoja wapo ikivaliwa na suria, basi hakuna atakaye msogelea

    "surian?.... Nina zawadi nataka nikupe leo"









    Sabaha aliondoka kisha maimati naye akaingia,... Lakini sasa Murati Alianza kuwa na wasiwasi na maimati kwani yupo karibu na suria muda wote... Murati aliingia chumba kimoja hivi,



    Wakati huo Murati akiwa ndani ya chumba chake,.. Huku sabaha anamsalimia suria, mana kwa sasa amekua mtu wa karibu sana na surian, kitu ambacho Murati sabaha anakitilia mashaka....

    "habari yako suria wangu"

    Alisalimia hivyo maimati huku suria akishangaa kwa kiasi fulani kwa kuitwa SURIA WANGU

    "salama tu dada muna, hali yako"

    "yangu safi... Vipi.. Leo pia umejichafulia?"

    Maimati alimuuliza suria hivyo mana ni mara nyingi anamkuta akiwa anamalizia kujichafua kupitia ndoto ambazo Murati sabaha ndio chanzo..

    Na hata suria haoni haja ya kumdanganya kwasababu anakutwaga akiwa anafanya tukio hilo kila siku alfajiri...

    "ndio, ila sijui ni nini kwakweli"

    "mimi najua... Ni kwasababu huna mwanamke"

    Aliongea maimati huku surian akisema kuwa

    "ni sawa, lakini mbona kule tanga kwetu, ilikuwa ikinitokea kwa mwezi mara moja tu... Au kwa miezi miwili mara moja... Lakini huku imekuwa ni kila siku"

    Aliongea surian tena kwa msisitizo wa hali ya juu kitu ambacho maimati alijiskia vibaya sana.... Mana ni jini mwenzie ndie anaye fanya kitendo hicho,...

    "ni rahisi sana hilo tatizo kuisha kama utakubali kuvaa hii pete"

    Aliongea maimati, mana kwa sasa ameona ni bora ampe kuliko kumtupia aivae mwenyewe, kwani hata akimpa haina madhara yeyote ispokua,.. Kuna tofauti ya kupewa na kuichukua kwa akili yako... Kuichukua kwa akili yako ndio kama vile alivyokua akitegewa kule duniani, na riziki zake hua ni nyingi kuliko ukipewa, kwahio hapa anapewa, maana yake hakuivaa kwa akili yake bali kafanya kuambiwa na akaivaa.. Kwahio hapa hakuna riziki,... Ila vitu vyote vipo lakini riziki kama vile alivyo itwa kwenye kazi, haitwi, na kama ana biashara basi itakuwa kawaida tu wala haito changanya, kama vya asha... Kwahio itazuia vyote vibaya lakini kile kizuri hakiwezi kuja mana umefanya kuambiwa... Na riziki siku zote haina taarifa...



    "hiii pete hii ni ya wanafunzi wangu, we umeipata wapi hii pete"

    Suria aliongea baada ya kuiona pete ile, mana anajua ni ya wanafunzi wake, kumbe alikuwa akitegewa yeye aivae, hivyo hapa maimati kaona bora ampe kwa mikono yake japo haina maendeleo ya kifedha lakini maimati yeye inamuuma mpenzi wake aingiliwe kimapenzi na mkubwa wake,... Japo hakuna uhalisia lakini ndivyo ilivyo...

    "hapana, hii haikuwa pete ya wanafunzi wako, bali ni mimi ndio niliokua nakuwekea ili uvae"

    Leo maimati alikua kama anataka kumwambia ukweli kuwa yeye ni jini na hapa yupo katika himaya ya majini

    "mbona sikuelewi dada muna"

    "sikia sasa nikuambie ukweli wa kila kitu,.. Na yote hii ni kwasababu nakupenda surian"

    Surian ana mwanamke mzuri sana duniani, lakini ikumbukwe kuwa majini wa kike ni wazuri kuliko mzuri yeyote unayemjua huku duniani...

    "ukweli gani huo?"

    "sikiliza surian. Hapa ulipo wewe"

    Sasa ile anataka tu kusema mara akasikia vishindo vya hatua kama kuna mtu anakuja.. Maimati aliirusha ile Pete kwenye mfuko wa shati la surian kisha akasima kama vile hakuwa karibu na surian



    Alikuwa ni Murati sabaha ndie aliekuja katika sehemu hio ambapo alimkuta maimati kasimama wima,

    "mati? Bado hujatoka kumbe"





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog