Chombezo : Ningefanya Nini
Sehemu Ya Tano
(5)
"Mtumeee" nilipiga kelele mikono nikaweka kichwani
nilianza kulia kwa sauti, Rajabu alikuja na kuniuliza vipi alijua
nimezidiwa
"Lameck jamanii Lameck, uwiiiii Lameck wangu
umepatwa na nini wewe" aisee asikwambie mtu nilikuwa kama chizi niliinuka
nikafungua kabati la nguo na kuanza kutoa natupa chini
"Wewe
vipi umechanganyikiwa au?" Rajabu aliniuliza
Sikumjibu nilikuwa
nikitafuta nguo gauni la heshima niweze kuvaa nitoke, nilipolipata nilivaa na
kutaka kutoka, Rajabu akaniwahi
"Embu niambie kuna
nin?"
"Lameck kafa! kafa! kafa jamani ameniacha" nilijikuta
naongea tu hapo nikaanza kuona umuhimu wa Lameck nikatamani hata nimuone ili
nimwambie yaishe nibaki nae asife,
"Sasa unataka kwenda wapi? Kwanza una
uhakika gani kama kafa?"
"Nimeona status niache niende kwao"
nilifanya fujo, nilihisi kuchanganyikiwa kwa wakati
ule
"Nimeona status niache niende kwao" nilifanya fujo
hizo, nikachomoka na kuondoka
Nilifika hadi alipokuwa akiishi Lameck
nilikuta watu wamesharudi kuzika, yaani jamani usiombe yakukute niliishiwa nguvu
hata za kutembea, nilipiga magoti na kuanza kulia, nilitamani kila kilichotokea
kiwe ndoto niamke tu mwenzenu, kufiwa kunauma kiukweli japo nilimkosea Lameck
lakini kilio changu kilitoka moyoni, watu walisogea na kunishika huku na huko,
wakaniingiza ndani
Niliwaona wazazi wake Lameck nao walinitambua kwani
tulikuwa tukijuana kupitia picha, nilivyolia ndo nilimfanya mama Lameck nae alie
upya, nilimsogelea akanikumbatia
"Mwanangu ajali imemchukua, alinipigia
simu akaniambia mama njoeni Tanzania na baba nataka kuoa kwa haraka msichelewe,
kumbe ndo alikuwa anatuita ili tuje kushuhudia kifo chake, ungetulia nyumbani
basi mwanangu labda yasingekukuta, Aisha yupo hapa umemuacha mwenyewe mke wako"
yule mama aliongea kwa masikitiko huku akilia, hapo nikatambua kuwa Lameck kafa
kwa ajali hapo nami nikazidi kulia
Basi tulibembelezwa tukanyamaza,
nilikuwa mpole sina hata raha nikajiinamia, mara nilihisi mtu kanishika mkono
niliinua uso na kumuona rafiki yake Lameck, aliniinua tukaenda nje pembeni
kabisa
"Pole kwa msiba lakini hutakiwi kulia tena, Lameck ameshaenda ila
tambua haya ni makosa yako Aisha, nilionana na lameck mara ya mwisho baada ya
kutoka kwako na kuniambia yote uliyomfanyia, wewe sio wa kumfanyia vile ndugu
yangu kiukweli umemuumiza sana, aliniomba nikupigie simu nimsaidie kukubembereza
lakini hukupokea, akasema basi muache kama hataki, kisha akaniaga, saa saba
usiku napokea simu na kuambiwa Lameck amepata ajali mbaya, ni kwasababu
yako"
Alinilaumu nikaanza kulia na kurudi ndani kiukweli niliumia
nikajiona nina hatia, sasa nitafanya nini maji yamesha mwagika
Siku hiyo
nililala hapo hapo matanga yakaisha watu wakaondoka, nami niliwaaga wazazi wa
Lameck kuwa nae
"Sawa ila tuna maongezi na wewe lakini ngoja kwanza
tukae kikao cha familia kisha nitakupigia simu uje" alisema baba Lameck basi
niliaga walinipa na pesa kidogo ambazo zilikuwa za rambirambi
nikaondoka,
*******
Nilirudi nyumbani nikiwa sipo sawa kivile,
Rajabu alininunia baada ya kukaa kule msibani
"Ushatoka kumzika bwana
ako ukaona ukae wee mpaka mmalize 40 kabisa" alisema hivyo kwa kunikejeli kwani
nililala siku mbili tu, hivyo hata 40 haijajulikana itakuwa
lini
Sikumjibu kitu niliingia bafuni nikaoga kisha nikachukua nguo
nyingine na kuvaa, mara simu yangu ikaita alikuwa mama Lameck nilipokea haraka
na kumsikiliza
"Mwanangu itabidi kesho uje tuongee, Lameck aliwahi
kutuambia kuwa wewe ni mjamzito sasa tushakaa kikao itabidi
tuzungumze"
"Sawa mama kesho nitakuja" nilimkubalia na nikapangiwa muda
wa kwenda
Ilipofika siku ya pili sikwenda kwani sikuona umuhimu ikiwa
mimba nilishatoa kwanza niliwaza nitaenda kusema nini, basi nilipigiwa simu
sikupokea, nikamwambia Rajab kuwa wazazi wa lameck wanataka waongee na mimi
kuhusu mimba akasema hakuna kwenda watumie msg waambie huna mimba, kiukweli
sikutuma msg niliogopa
Zilipita siku mbili nikabadilisha na laini ili
kukwepa usumbufu wao, nikiwa nimekaa sebuleni mlango uligongwa nilifungua na
kumuona rafiki wa Lameck na wazazi wa Lameck
nilishtuka
Zilipita siku mbili nikabadilisha na laini
ili kukwepa usumbufu wao, nikiwa nimekaa sebuleni mlango uligongwa nilifungua na
kumuona rafiki wa Lameck na wazazi wa Lameck
nilishtuka
Sikutaka kujua wamepajuaje kwani yule shemeji yangu
alipajua vizuri, niliwakaribisha na kuwasalimia
"Aisha upo sawa
wewe?" Baba Lameck aliniuliza
"Ndio baba"
"Tumepata
wasiwasi kwenye kikao hatujakuona, pia simu yako haipatikani, tukamuomba Denis
atulete kwako tulihisi una matatizo" mama Lameck aliongea kwa
upole
"Simu yangu imeharibika pia nilikuwa sipo sawa" nilijibu,
wakati huo Rajabu alikuwa chumbani anasikiliza kwani niliweza kuona kitasa cha
mlango kikicheza lakini baadae kikatulia, nilijua fika alitaka kutoka lakini
katulia
"Sasa mwanangu kama tulivyokwambia ile majuzi, taarifa
kuhusu kuwa na mimba tunazo, kwasasa wewe ndo faraja yetu pamoja na mtoto
aliyekuwa tumboni, tumeona tukuchukue ili twende wote London ukaishi huko,
uangalie hali yako mpaka utakapo jifungua" waliniambia hivyo, nilishtuka maana
sikujua niwaambie nini, nilitamani siku moja kwenda nchi kama hiyo lakini naona
ndoto zimefifia
"Mbona kimya kwani una hofu ya nini mkwe?"
Aliuliza baba Lameck,
Mara Rajabu alitoka na
kusalimia
"Nimesikia kila kitu mlichoongea huyu haendi popote
ni mke wangu, alishachana muda na mtoto wenu pia hiyo mimba ilishatoka kwahiyo
muacheni" aliongea na kuwafanya washtuke mimi nilihisi ganzi mwili
mzima
"Anachokisema ni kweli?" Mama
aliuliza
"Wee mama kwani huamini au? Haya nenda kampime kama
utakuta mimba nendeni, kwanza inukeni muondoke huyu mke wangu sitaki muongee
nae" alisema na kunitaka mimi niingie chumbani
Nilimuomba
asiwafokee watu wazima lakini hakuelewa, basi ikabidi wale waondoke na kuomba
samahani kwa usumbufu, walisema hawajajua kama mimi nimeolewa, walikuwa ni watu
wastaarabu na wapole nilijikuta nikiona aibu na makosa yote niliyabeba mimi,
walivyoondoka tu nikamsogelea Rajabu
"Kwa nini huna adabu wewe,
huoni kama umenidhalilisha? Unataka mimi niishi maisha gani, kila mtu unataka
anichukie?" Niliongea kwa hasira, basi hiyo siku tuligombana
sana,
Ulipita mwezi mmoja tukiwa watupatani kivile, pale kodi
iliisha akakataa kulipa nikatoa akiba zangu na kulipia,
Siku
moja nikiwa napika, mara nilisikia, simu ya Rajabu ikiita nilishangaa kwanini
haipokelewi kumbe hakuwepo ila aliweka chaji, nilitoka na kwenda kupokea
nikakuta ilishakata, niliangalia na kukuta msg, jina habiba nikalikumbuka lile
jina ni mwanamke wake wa muda mrefu alitakaga kumuoa aliandika
hivi
"Hupokei simu kwanini mimi Nina shida na pesa nataka
niende hospital"
Basi nikaingia na shauku ya kusoma na msg za
nyuma
"Mpaka sasa mimba inaingia miezi sita hutaki kuja hata
kuniona"
"Najua pia natamani kukuona lakini huku namalizia
nyumba yetu nikuchukue tukae wote usione kama mimi sikujali" Rajabu alijibu
hivyo
Huwezi amini nilianza kutetemeka mikono, sikutaka
kuendelea tena kusoma msg nyingine, nilirudisha simu pale
pale
Basi niliacha kusoma ile msg na kukaa kwenye
sofa, nilisikia harufu kama mboga inaungua lakini sikuweza kwenda kuishughulikia
nilikasirika haswa
"Wee Aisha usikii kama mboga inaungua au?"
Alisema Rajabu baada ya kuingia ndani
Nilikaa kimya akanifuata
na kuniuliza tena, nikampa bonge la Kofi
"Kwani kama unasikia
Mboga inaungua kwanini usiende kuiokoa, au mpaka niende mimi? Wewe huwezi au
umezoea kusumbua wenzio?" Nilimwambia kwa hasira huku nikimtolea
macho,
"Yaani kukwambia mboga inaungua ndo unipige kofi?"
Alijikuta nae akiniuliza kwa hasira huku akiwa ameshika shavu ujue kofi la
kushtukiza linauma jamani
"Sikia wee Malaya wa kiume, nishajua
kama umempa mimba huyo kenge wako, nimeona msg zote unanifanya mimi mjinga eh?
Hivi wewe unasahau nimekufanyia mangapi mimi? Mbona huna fadhila wewe? Kukupenda
kote nikakupa kila kitu alafu unanifanyia ujinga" nilizidi kupandisha
hasira
"Haya tufanye ushajua ukweli kwahiyo unaamuaje
tunaachana au?" Aliniukiza kwa dharau nilikasirika nikataka kumpiga kofi tena
akanidaka mkono
"Nitakupiga usinione mimi fala nitakuvunja
nalwambia" alisema na kunisukumiza kwenye kiti
"Nataka kuonana
na huyo kahaba wako anatoa hiyo mimba?" Nilisema kwa hasira akaanza
kunicheka
"Wewe umechanganyikiwa eeh mimi nimtoe mwanamke wangu
mimba? Utanitafutia mtoto wewe? Kwanza huna kizazi utanizaliaje?"
Aliniambia
"Na ile mimba uliyonitoa iliingiaje kama sina kizazi
labda wewe ndo huna kizazi kwasababu sikuwahi kubeba mimba yako hata siku moja"
nilimwambia na mimi kwa kumkashifu ili ajisikie vibaya,
akacheka
"Pole sana yaani wewe kuzaa sahau kabisa ushatoa mimba
na kizazi ushatolewa chote kama ulikuwa ujui ndo nakwambia na nilikuwa
nakufichia siri ila leo ndo nakupa ukweli maana jeuli" alivyosema hivyo
nilishtuka sana nilipiga kelele na kulia, nilianza kumtukana Rajabu akawa
ananipiga alinipiga mpaka nilihisi kuchanganyikiwa nilianza kupiga kelele nakufa
mara nyingi, nguvu ziliniishia kabisa sikujielewa tena
Jioni
niliamka na kujikuta nipo hospital pembeni yangu kulikuwa na wanawake wawili
wamekaa na mwanaume mmoja, nilipowaangalia nikagundua ni majirani zangu pale
nilipopanga, waliniambia kuwa walisikia kelele walipokuja ndo wakanikuta tayari
nimezimia Rajabu alitoka nje na beg lake la mgongoni akakimbia, mimi
wakanipeleka hospital
ITAENDELEA
CHOMBEZO- NINGEFANYA
NINI?
SEHEMU YA 31
Jioni niliamka na kujikuta nipo hospital
pembeni yangu kulikuwa na wanawake wawili wamekaa na mwanaume mmoja,
nilipowaangalia nikagundua ni majirani zangu pale nilipopanga, waliniambia kuwa
walisikia kelele walipokuja ndo wakanikuta tayari nimezimia Rajabu alitoka nje
na beg lake la mgongoni akakimbia, mimi wakanipeleka
hospital
"Asante kwa msaada wenu"
niliwashukuru
"Kwani ilikuwaje?" Mmoja aliniuliza hapo nilianza
kutoka na machozi
"Wanaume wabaya sana jamani" niliwahusisha
wanaume wote wakati aliyenitenda haswa alikuwa ni
Rajabu
Walinimbembeleza nikatulia, basi kwa kuwa yule jirani
yangu alikuwa polisi aliniambia atanisaidia kufungua
kesi,
Tangu siku hiyo sikuwa sawa, nilikuwa nawaza kila siku,
kilio ndo ilikuwa sehemu kubwa ya maisha yangu, kuweza kula vizuri nilianza
kukonda, homa zilikuwa haziishi, nikaenda hospital na kupima nikagundulika nina
virusi vya ukimwi, nilijua kabisa lazima niliambukizwa na Rajabu maana alikuwa
hajatulia, nililia sana siku hiyo, dokta akanishauri na kunitia moyo, alinitaka
niishi kwa matumaini pia nianze dozi
Nilitoka pale hospital na
kusimama nje, nikimkumbuka Lameck nikaanza kujuta kwa kila jambo nililomfanyia,
nilitamani nimuombe msamaha lakini nitamuombea wapi, Lameck ameshafariki tena
bila kunisamehe, nilianza kupiga kelele huku nakimbia ovyo kama mtu
aliyechanganyikiwa watu walinishangaa nikaanza kuwatukana
tu,
"Mnaniangalia hamnijui? Waone kwanza misura mibaya kama
ng'ombe" niliwaambia na kuendelea kukimbia tena,
Basi nilikuja
kupata akili ya kumtafufa Rajabu, niliamua kwenda kule tulipokuwa tunajenga
majohe, ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dining na jiko, choo
kilikuwa cha ndani, nilikuta nyumba ilishaisha kila kitu, ilibaki rangi tu nje,
lakini ilionyesha tayari kuna watu wamehamia, nilishangaa na kujiuliza nani
anaishi pale
Niligonga akatoka msichana mwenye mtoto mdogo,
sikuweza kumjua hata nilipomuangalia
"Wewe ni nani hapa?"
Nilimuuliza
"Mimi ndo mwenye hii nyumba"
alinijibu
"Umeinunua hii nyumba au? maana sikuelewi hii nyumba
ni ya kwangu alafu ilikuwa haijaisha vizuri nashanga nakuja nakuta mtu anaishi"
niliongea nikiwa nishaanza kuhamaki
"Jamani hii nyumba ya mume
wangu, yeye alinunua kiwanja na kuanza kujenga, sasa unavyosema yako
sikuelewi"
"Huyo mume wako yupo wapi, nataka kumuuliza nani
kamuuzia hapa" nilisema
"Ngoja nimuite" aliita akiwa pale pale
mlangoni, punde mwanaume akatoka, sikuamini macho yangu alikuwa ni
Rajabu
Yaani kama Mungu amenisaidia kunipa ile akili ya kwenda
kule majohe
"Baby huyu mdada kaja hapa alikuwa ana shida na
wewe anasema hapa ni kwake" alianza kumuelezea
nilivyomwambia
"Habiba nenda ndani" alisema
Rajabu
Hapo ndo nikagundua kumbe yule ndo habiba mwenyewe
niliyewahi kukuta msg zake, yule msichana
akatuacha
"Habiba nenda ndani" alisema
Rajabu
hapo ndo nikagundua kumbe yule ndo habiba mwenyewe
niliyewahi kukuta msg zake, yule msichana akatuacha
"Enhee
ulikuwa unasemaje?" Aliniuliza
"Unaniuliza nilikuwa nasemaje?"
Niliuliza na mimi
"Ndio maana umekuja kwangu sasa sijui shida
yako nini?"
"Hapa ni kwako wewe? Umesahau hiki kiwanja kanunua
nani na pesa za kujengea katoa nani? Unajisahaulisha, kwanza kwanini umehamia
kwenye nyumba yangu?" Nilimuuliza kwa hasira
"Wewe usiniletee
upuuzi wako hapa, pesa si ulinipa mwenyewe kwani uliniambia nikununulie kiwanja?
Ulinipa pesa nami nikaamua kununua kiwanja ili nikijenga niishi na wewe lakini
imeshindikana, sasa nini tena unachonitafutia?"
"Rajabu
usinitanie nakwambia, siwezi kukubali uniharibie maisha yangu kiasi hicho,
nataka nyumba yangu? Ona umenifanyia mambo mengi machafu, umeniambukiza maradhi,
wewe sio binadam" nilimwambia kwa hasira
"Sasa kama mimi sio
binadam kwanini unaniongelesha na hapa unasubiri nini? Ondoka mimi sina shida na
wewe tena tushamalizana" aliniambia mara yule mwanamke wake
akatoka
"Kuna nini mbona sielewi nasikia mnagombana tu?"
Aliuliza
"Huyu mwanamke amechanganyikiwa achana nae" Rajabu
alimjibu
"Mimi nimechanganyikiwa? Mwambie ukweli mwanamke wako
mimi nani?"
"Wewe si mbwa tu, ulitaka uwe nani?" Rajabu alisema
kwa dharau nikapata hasira
"Sawa mimi mbwa ila leo ndo utajua
kama mbwa koko au kichaa" nami nilijibu kwa kujiamini
"Jamani
embu wee dada ungeenda tu nyumbani kwako" habiba
alisema
"Niende nyumbani kwangu wapi wakati ndo hapa"
nilijibu
"Kwahiyo wewe unatembea na mume wangu na unataka ukae
hapa si ndio?"
"Sina shida na mwanaume wako, labda nikukumbushe
tu, tuliwahi kuongea kwenye simu zamani sana siku uliyopiga simu ya rajabu
nikaipokea mimi, ukasema wewe ni mchumba wake, sasa tangu wakati ule nilikuwa na
Rajabu akanifanyia mabaya mengi huku akikutuchanganya na kama alivyotoka Moro
alikwambia anakuja kutafuta maisha basi alikuwa amekudanganya aliishi kwangu na
hata hii nyumba ni yangu amejenga kwa pesa yangu, hivyo lazima aondoke na
kuniachia kila kitu" nilisema
"Anhaa kumbe basi mimi siwezi
kukutetea wewe uliniibia mwanaume wangu, hivyo kama ukimpa pesa huo ni ujinga
wako mwenyewe, acha kutupigia kelele kwanza hii nyumba imeandikishwa jina la
mwanangu hivyo siwezi kukubali kutoka hapa, wewe nenda popote" alisema habiba
wakawa wameungana
"Tena ondoka hapa kabla sijakupiga makofi
nikuumize" Rajabu alisema
"Haya nipige, nipige nasema, siwezi
kukubali unidhurumu" niliongea kwa hasira
"Basi nenda
unapotaka" alisema habiba nikataka kumzibua kofi Rajabu akawahi wakaanza
kunichangia walinipiga mpaka nguo zikachanika, watu wakaja na kutugombelezea,
wakanitoa mimi, basi nilistiliwa nguo nyingine na
kuondoka
Nilitafuta sehemu na kukaa pekee yangu na kuanza
kulia,
Yote ni makosa yangu, sikutakiwa kumuamini Rajabu ile
siku ya kwanza tu niliyokutana nae, niliona msg akimwambia rafiki yake kuhusu
mimi kuwa amenitamani lakini sikufanya lolote, ilitosha kabisa kumuona sio
mwanaume sahihi,
Haikuishia hapo bado Mungu hakuacha
kunionyesha ushetani wa huyu mwanaume pale nilipoenda kwao Moro na kunipeleka
gest ikiwa ana kwake alafu nikagundua anataka kuoa, kumbe mimi alinichezea
nilipaswa kumpotezea pale pale, lakini kwa ujinga wangu nikampa nafasi nyingine
wakati tayari nilishakuwa kwenye mahusiano na nilipendwa
sana,
Tamaa zangu za ngono na kutokuridhika kwa Lameck
kumenifanya niwe msaliti, hatimae nikaanza kufanya mapenzi kinyume na maumbile
bila kufikiria madhara yake, sikutakiwa kurudiana na Rajabu kabisa ikiwa
niliachana nae kwa tabia zake chafu, nilimsaliti mtu ambae aliweza kunisaidia
nilipokamatwa pia akanitoa kwenye maisha ya mateso na kunipa furaha, pamoja na
yote sikumlipa hata jema moja badala yake nikasababisha kifo, kiukweli najutia
kila kitu kilichotokea lakini maji
yameshamwagika
Haikuishia hapo bado Mungu hakuacha
kunionyesha ushetani wa huyu mwanaume pale nilipoenda kwao Moro na kunipeleka
gest ikiwa ana kwake alafu nikagundua anataka kuoa, kumbe mimi alinichezea
nilipaswa kumpotezea pale pale, lakini kwa ujinga wangu nikampa nafasi nyingine
wakati tayari nilishakuwa kwenye mahusiano na nilipendwa sana, tamaa zangu za
ngono na kutokuridhika kumenifanya niwe msaliti,
Hatimae
nikaanza kufanya mapenzi kinyume na maumbile bila kufikiria madhara yake,
sikutakiwa kuwa nae kabisa, nilimsaliti mtu ambae aliweza kunisaidia
nilipokamatwa pia akanitoa kwenye maisha ya mateso na kunipa furaha, pamoja na
yote sikumlipa hata jema moja badala yake nikasababisha
kifo,
Hatimae leo nimeachwa nikiwa sina thamani, sio Aisha yule
wa zamani hakuna aliyekuwa akitamani hata kunisalimia, nililia na kuomba Lameck
kama ananisikia anisamehe nilianza kuona umuhimu wake sikuacha kumkumbuka,
NINGEFANYA NINI?
Akili yangu ilikuwa ishabadilika, niliwaza
kufanya jambo moja kubwa na zito,
"Lazima wote wafe nitaua tu
Mungu atanisamehe, siwezi kukubali maisha yangu yaharibike kisha nikae kimya,
nitaua kisha nami nitajiua tu" nilisema na kuanza kutembea nilienda nilipokuwa
naishi na kuchukua pesa ilikuwa elfu 30 tu, nilienda kununua petrol, kisha
ilipofika usiku kama saa 3 nilitafuta boda boda ikanipeleka majohe hapo
nilitafuta sehemu nikakaa mpaka saa Saba usiku nilianza kumwaga ile petrol
dirishani mlangoni na iliyobaki nikazungusha kwenye nyumba, kisha nikachukua
mjiti nikawasha moto na kuurusha, moto ulianza kupamba nilisikia wakipiga kelele
na kutaka msaada nikaanza kuwajibu
"Kufeni washenzi nyinyi
mnajifanya dhuruma eeh sasa mufe tu, tutakutana huko mbinguni" nilisema kiukweli
sikutaka kufanya jambo baya kama hilo lakini moyo wangu uliuma yule habiba
alikuwa na majibu mabaya kwangu yalinifanya nipanic, unafikiri kwa maumivu na
mateso yote aliyonipa Rajabu NINGEFANYA NINI? kuua ndo niliona maamuzi sahihi tu
ili kuufanya moyo wangu utulie, wangenipa mali yangu basi tungemalizana
ningekubali kuendelea na maisha yangu lakini wote walijitia
majeuli,
Nilianza kusikia sauti ya mtoto nikamuonea huruma
sana, kwani hakuwa na hatia, nililia na kaunza kupiga mikelele kama mwehu, watu
walijaa na kuanza kuzima ule moto, wengine wakanikamata, nikawa nawapiga na
kuwatukana, nikasikia sauti za watu wakisema
"Hawa wamekufa
jamani hawaongei tena"
Basi nilikuwa nikitukana ovyo na
kuwapiga wale watu wasinishike nilianza kuongea ovyo
tu
**********
Nikiwa nimeamka usingizini nilikuwa
nimechoka sana, nilijiangalia na kujiona nimekonda mikono membamba nguo
nilizovaa ni chafu mno, nilishangaa imekuwaje, nilipoangalia vizuri palikuwa ni
hospital
Mara akaingia msichana mmoja nilianza kukumbuka
alikuwa ni rafiki yangu jesca niliyekuwa nikikaa nae jirani kule Lumo kwa mama
zangu, alikuwa ambadilika sana na kuwa mzuri haswa
"Aisha
unanikumbuka mimi?" Aliniuliza
"Ndio wewe si jesca"
nilimwambia
"Asante Mungu hakika umepona rafiki yangu"
alisema
Nilihisi nimepona ukimwi maana ndo ugonjwa niliokuwa
nao
"Kwahiyo sina virusi tena nimepona kabisa?" Nilimuuliza kwa
mshangao
"Mmhh hata nikikwambia huwezi kuelewa, ila kwa kifupi
ulikuwa chizi Aisha" aliniambia hivyo nikashangaa akaanza kunihadithia kila
kitu
Kumbe ile siku niliyomuua Rajabu na familia yake nikapata
uchizi kabisa, lakini nilikumbuka kuwa ile siku nilikuwa nikifanya fujo na
kutukana watu sikujielewa tena, Kumbe nilichukuliwa na kupelekwa polisi nikikaa
miezi sita na baadae sikupewa hukumu yoyote baada ya kuuwa kwani nilipimwa na
kuonekana chizi, nilitolewa na kuanza kuhangaika mitaani nikila ovyo na kulala
ovyo,
Akaniambia pia siku moja akiwa anatoka mini aliweza
kuniona k koo nikiwa natembea peku na nguo zikiwa chafu tena zimechanika,
aliingiwa na huruma na kupanga kunisaidia, baada ya mwezi alifanikiwa kunikamata
na kunifunga mikamba akanipeleka hospital,
Nilishangaa kwani
nilihisi ni jana tu ndo nimeua ila jesca aliniambia ndani ya miaka miwili
nilikuwa chizi na leo ndo nimeweza kupata akili zangu baada ya kutibiwa kwa muda
mrefu na kubadilisha mahospita
Nilianza kulia upya moyo
uliniuma, hakika nilidhalilika sana, tamaa zangu zimeniponza nimekuja
kusababisha mtu aliyenipenda kafa, pia nikajikuta nakuwa muuaji bila kutarajia
na kuua kiumbe kisichokuwa na hatia yule mtoto mdogo, nilitoa mimba na mwisho
nikapoteza uwezo wa kuzaa, nimepata maradhi makubwa kutokana na kuingiliwa
kinyume na maumbile sasa navakishwa pempas kama mtoto mdogo, uzuri wangu wote
umekwisha, hakuna mwanaume atakayenitaka tena sina
thamani,
Mpaka sasa jesca ndo mtu pekee aliyenipa msaada, nipo
kitandani siwezi kufanya chochote kile, niliweza kumuomba jesca aniitie mtunzi
anayeitwa Lissa wa mariam ili niweze kumpa historia ya maisha yangu na aweze
kuipost watu wajifunze wasiwe na tamaa kama mimi, ningetulia na Lameck pengine
leo ningekuwa mama mzuri na wa kuigwa ila nimekuwa mbaya sifai kuigwa na
jamnii
Kwasasa nasubiri siku yangu ya kufa tu ikaribie maana
hali yangu ishakuwa mbaya
*****MWISHO****
0 comments:
Post a Comment