Search This Blog

Thursday 24 November 2022

YOUNG PASTOR - 2

 

     

     



     

    Chombezo : Young Pastor

    Sehemu Ya Pili (2)

     



    Sasa huku kwa akina eva,.. Alikuwa kujiandaa kawaida sasa alipo pata taarifa kuwa, kanisa la mchumba wake linafunguliwa,.. Alivua mavazi aliokuwa kavaa, kisha akavaa mengine, tena vazi safi na la heshima, hilo lilitakiwa kuvaliwa kwa siku maalum, si unajua familia ambazo hazijiwezi vizuri, hua wana mavazi ya kutokea na ya kawaida, tofauti na tajiri, yeye akitaka kutoka anakwenda dukani

    “we vipi hilo gauni kuna nini”

    Mama aliuliza kuhusu gauni hilo ambalo lilikuwa na kitambaa chake cha kichwa, kitambaa chenyewe kimetengenezwa kama kofia, unavaa tu, magauni ya kinaigeria hayo…

    “mama, hili ni speho kwa ajili ya EDEN CHURCH”

    mama alishangaa kusikia Eden Church, mana hilo kanisa anajua bado halijatengemaa….

    “Eden Church, si hili kanisa la mtumishi adam”

    “ndio mama…. Leo ndio linafunguliwa rasmi”

    Mama nae kuskia hivyo, anaachajwe sasa kwa mfano, kwenye kanisa la baba mkwe, japo mama anajua kuna fununu kazisikia lakini hakutaka kumwambia mtoto wake, mana anahisi atamvunja moyo…

    “nitakwenda ndio, lakini nitachelewa kidogo si unajua mambo ya nyumbani, ila mwambia mchungaji, nitakuja na hongera sana”

    “sawa mama”

    Eva siku hio alikuwa katupia mapak basi, yaani hapo ndio kavunja kabati, saa ngapi hata adam hajampita, mana kabadirika eva, anavaaga nguo za heshima lakini siku hio, kavaa nguo ya heshima mpaka imepitiliza,..

    Lakini uzuri ni kwamba eva analijua gari ya mchumba wake,.. Sasa lilivyompita eva hakutaka kumkimbilia au kupiga makelele… Eva alikaa usawa wa saiti mira kisha akapunga mkono, kwahio adam atamuona kupitia saiti mira.. Na ni kweli adam aliona kuna mwanamke anampungia mkono lakini hajamjua ni nani,… Adam alijua huyo mwanamke anaomba tu lifti, sasa adam akampa ishara kiwa anarudi amsubiri hapo… Eva akashika simu yake,.. Kumbe sababu ni vocha hana, na ndio mana alishindwa kumpigia..

    Eva alituma tafadhali nipigie, ili hata adam ajue kuwa aliompita ni eva,… Adam kuangalia kweli alikuwa ni eva, alicheka sana huku akisema

    “mama mchungaji ana haraka huyo,.. Nakuja mama subiri”

    Adam aliongea hivyo kumaanisha kuwa, eva yupo nyumbani,.. Hivyo hajampigia kwakuwa anakwenda huko kwao…



    “heeee eva, ivi ni wewe kweli”

    Alikuwa ni rafiki yake eva, aitwaye wini..

    “ina maana hujawahi kuniona na hili gauni au”

    “heeeee…. Eva? Shalom”

    “shalom.. Vipi, unakwenda wapi”

    “ndio nilikuwa nakwenda kanisani, tena nilikuwa nakuwaza sasa hivi kuwa tayari umetoka au bado”

    “ok Tuachane na hayo… Ebu nipe simu yako mara moja”

    “ya nini tena”

    “we nipe si ina dakika”

    “ndio”







    “nipe basi, haraka”

    Eva aliichukuwa ile simu ya wini, kisha akaingiza namba za adam na kumpigia… Adam alibakiza kama miguu 10 hivi kufika kwa akina eva, mara simu hio…

    “hallo”

    “eee, baba mchungaji… Umenipita hapa kwenye karavati”

    Kwakuwa adam anaijua sauti ya eva, hivyo hakuuliza wewe ni nani

    “what, ndio wewe ulionipungia mkono hapo”

    “ndio”

    “oooohhhh mama mchungaji Nisamehe sana sijakujua kwakweli, usitembee tena nisubiri papo hapo”

    “sawa baba mchungaji”

    Simu ilikata huku wini akiuliza

    “baba mchungaji nani tena huyo we eva”

    “wini, ina maana hujui kuwa adam keshakuwa pasta”

    “weeeeee… Kwahio uliompigia ni adam”

    “ndio, tena huyoo anakuja”

    Wakati huo wini keshapewa simu yake,…

    “ifute hio namba wini sawa”

    “wala Usijali eva, nitakaaje na namba ya mtu wa mtu”

    “ok sasa si tunaenda wote Eden Church”

    “kwani limeshafunguliwa hilo kanisa”

    “ndio leo”

    “lazima twende wote jamani mama mchungaji”

    “mmmmhhh nawe Ushaanza”

    “kwani si kweli”

    Mara adam kafika katika eneo walipo, lakini wakiwa wanaingia katika gari, simu ya adam iliita… Wakati huo eva alikaa mbele, na wini alikaa siti za nyuma

    “halllo, tumsifu yesu Kristo”

    “milele amina boss…. Aahh bosa ofisini kuna shida, mi naona ungekuja mara moja”

    “aahhhh hamuezi kuitatua hio shida”

    “hapana boss”

    “ok nakuja sasa hivi”

    Alikuwa ni sekretari wa kampuni yake huko mjini ndie aliempigia simu…

    “tumsifu Yesu Kristo”

    Wini alitoa salamu ya sifa kwa bwana mwokozi wao

    “milele amina… Hali yako”

    “salama”

    “aaahhh eva, samahani ofisini kumetokea shida… Sasa sijui twendeni au niwawahishe Eden Church”

    Aliongea adam ili kuwapa chaguo

    “mi naona twende huko huko ofisini kisha tutakwenda wote Eden”

    Alijibu eva huku gari ikiwashwa na safari ya kuelekea mjini ilianza,…. Hapakuwa na umbali na vile walitumia usafiri wao, hawakuchelewa kufika ofisini hapo…

    Adam alishuka mbio mbio huku eva nae akishuka mbio mbio yaani utafikiri ni kitu na mke wake.. Ilipendeza sana hali ile… Jinsi eva alivyo vaa kiheshima zaidi… Sasa aliobaki katika gari ni wini peke yake

    “enhee ulikuwa unasemaje Cecelia”

    Alimuuliza sekretari wake aitwaye Cecelia

    “Abdallah kaacha kazi”

    “heeeee yaani hilo ndip tatizo ulioniitia”

    “ndio boss… Samahani lakini kama sio tatizo kwako”

    “ok hakuna shida…. Ameacha kwasababu gani”

    “aahh bosa kama unavyojua, adam ndio muislamu peke yake… Hivyo hapendi sisi tunavyo fanya maombi kwa sauti”

    “lakini Cecelia… Huoni kiwa ninyi ndio mna makosa… Abdallah, yeye ana imani nyingine… Ombeni kwa ustarabu usimuuzi mwenzio ambae sio wa imani yako… Mumefanya makosa… Afu ofisini msiombe kwa sauti, panapokuwa hakuna kazi mnakwenda kwenye chumba cha maombi na kufanya maombi kistarabu, hata mungu hapendi maombi ya fujo, au ya kukebehi… Na kama unataka kufanya maombi kwenye meza yako ya kazi… Basi omba kwa utaratibu, sio lazima sauti itoke.. Sawa ceci”

    “sawa boss… Vp atarudi au”

    “Usijali, namrudisha kazini”

    Pasta Adam alishika simu kisha akampigia Abdallah

    “aahh bwana Abdallah, Assalam Aleykh shekhe”

    Hata eva na wini walishangaa kuskia salamu ambayo adam kaitamka kwa kumsalimia Abdallah ambae ni mtu wa imani tofauti na yakwake,…

    “haaaaaa boss,… Waaleykha boss habari za nyumbani”

    Hata amdala pia alishangaa japo anakumbuka pia kuna siku ila miaka ya nyuma, alishawahi kusalimiwa hivi na huyu huyu adam…

    “salama, aisee vipi naambiwa umetoka kazini ghafla”

    “ndio boss,… Naona wenzangu wanaomba kwa sauti sana… Na unajua mimi sio mtu wa imani hio.. Hawanikeri lakini Ati list wangeomba kwa ustarabu”

    “tayari limesha rekebishika, unaweza lirudi kazini”

    “Ahsante boss… Nafika hapo sasa hivi”

    Mchungaji adam alikata simu kisha akamwambia ceci kuwa

    “Abdallah anakuja sasa hivi… Msiudhishane tafadhali, kila mtu amuombe mungu kwa nafasi yake pasina kumkera mtu”

    Aliongea adam kisha akapanda gari

    “sawa boss”

    Waliondoka zao kuelekea Eden Church kwa ufunguzi wa kanisa… Eva alikuwa anatamani kumuuliza adam kuhusiana na ile salamu inaingiliana vipi na dini ya kikristo,….

    “baba mtumishi”

    “naam mama mtumishi”

    Aliitikia adam kwa heshima ya juu kwa kuitwa na mchumba wake

    “nilisikia salam pale,.. Nilitaka tu kujua, ila sina nia mbaya”

    Aliongea eva wakati huo gari ipo katika spidi ya kuwahi kanisani…

    “ni kweli, na mimi niliitamka makusudi sana tu ili mpate elimu…. Unajua sisi kwa sisi tumekuwa watu wa kufanyiana kufuru… Mkristo anamkufuru muislamu, na muislamu pia hivyo anamkufuru Mkristo… Nataka nitoe elimu hii nikiwa kanisani, ila salamu kama ile, kwa watu wenye imani tofauti… Kuna jinsi ya kuitamka, yaani kuna jinsi ya kuitoa salamu hio, na pia kuna jinsi ya kuipoea salamu hio.. Itategemea na nani kaanza.. Kwa mfano mimi pale nimetoa salamu yote,… Na alieipokea kwakuwa anajua, pia hakuipokea yote… Nitawafafanulia vizuri tuwapo kanisani sawa eva na wini”

    “sawa mchungaji”

    Adam alikatika hio mada baada ya kuwa wanakaribia EDEN CHURCH, yaani EDEN CHURCH ndio kanisa la adam.. Adam haamini pale anapoona umati wa waumini walipokuwa wanaanda mazingira, wake kwa waume wakiwa bize na mishuhuliko… Kulikuwa na watu wengi sana mpaka eva akashangaa, mana sio kawaida ya makanisa mapya kujaza watu kwa haraka… Majukwaa yalikuwa yakisimamishwa ili kupatikane kivuli kizuri sana mana kanisa hilo lina uwanja mkubwa sana

    Adam, Eva na wini walishuka katika gari, kuna pasta mmoja alikuja kutia baraka katika kanisa la adam.. Hivyo alikuwa kasimama mahali fulani huku akisalimiana na huyo pasta mwenzake….



    “ah ah, usilegeze hio kamba, kaza haswa”

    Ilikuwa ni sauti ya mwanadada Catherine, yaani yeye ndio alikuwa akiongoza mpangilio mzima wa maandalizi hayo, na nafasi hio alipewa na adam, kuwa kesho afanye hivyo mana aliiomba hio nafasi, sasa aliposema hivyo kuwa asiivute sana hio kamba, mana imezuia chuma moja kubwa ambalo ndilo chuma la katikati ya jukwaa… Sasa Catherine ikabidi aende pale akaikaze mwenyewe ili lile chuma lisije kudondokea watu pale litakapo fungwa vibaya… Sasa kwakuwa aliokuwa akimwelekeza haelewi ikabidi aende akaikaze mwenyewe ile kamba,… Catherine alifika pale kisha akawa kama analivuta vuta hivi lile lichuma lizito… Ili aliweke katikati kisha akaze,… Lakini sasa alipokuwa akifanya hivyo, Alijaribu kwamfano lile chuma lisipokazwa, litadondoka vipi kama akilegeza kamba kidogo… Sasa ile kujaribu kulegeza hio kamba, Aligundua kuwa kwa wakati huo akiendelea kulegeza kamba, lile chuma litamdondokea Eva….. Huezi amini Catherine alianza kuangalia kushoto na kulia na kugundua kuwa hakukuwa na mtu aliokuwa akimfuatilia hata kwa macho..

    “Irene? Naomba ukaniongezee kamba ili niikaze hii vizuri”

    Aliongea Catherine ili huyo irene asione kitu, mana ndio aliokuwa karibu nae,… Irene bila kujua kuwa katolewa ili Catherine atimize lengo lake

    “umekuja umependaza, ili uonekane mama mchungaji mtarajiwa…. Sasa ni maiti mtarajiwa…. Utanisamehe sana Eva, mungu akulaze mahali pema peponi… Amen”

    Aliongea Catherine huku akimuombea eva,.. Na baada tu ya kunena hayo maneno,.. Alianza kuiachia ile kamba huku akitabasamu,.. Mana Eva akifa hakuna mama mchungaji mtarajiwa zaidi ya Catherine… Kweli Catherine alinuia kumuua Eva, huezi amini kweli aliiachia ile kamba na lile chuma ni lizidi…. Yesu wangu jamani Eva hajui hili wala lile, kumbe juu chuma linakuja……

    “kwaheri eva…. Umama mchungaji wako ni huko huko ulikotoka…”

    Catherine Aliongea hivyo huku chuma linazidi kuteremka… Sasa Catherine alikuwa anafumba macho, ili akifungua macho akutane na maiti, sasa pale alipo adam, kumbe alikuwa akiongea na yule pasta na kumtambulisha mchumba wake, sasa kile kitendo cha kumtambulisha,.. Adam akamshika eva na kumsogeza kwa mbele ili pasta amuone mke mtarajiwa wa mchungaji adam,… Sasa lile chuma halimuelekei eva tena, bali ni adam… Sasa Catherine ndio alikuwa anamalizia kufunga jicho… Ghafla anashangaa alipokuwa kasimama eva, sasa hivi kasimama adam, kwahio kifo ni cha adam… Alafu mbaya zaidi sasa, kamba ya kuzuia hilo chuma ipo mbali, mana Catherine alisha iachia muda mrefu sana,..

    “pasta adam angalia juuuuuuuuuuuu”

    Catherine alipaza sauti kubwa, lakini haikufika mbali, mana kelele za hapa na pale kwa shamra shamra za ufunguzi wa kanisa la Eden Church, Catherine haamini kama adam hajasikia sauti yake…. Alijaribu kuita na kuita lakini wapi, na hapo kila mmoja na mambo yake yaliomleta hapo…. Maskini ya mungu mtumishi adam







    Wakati huo adam bado anaendelea kumtambulisha eva kama mke wake mtarajiwa, yaani huyo ndio mama mchungaji ambae anatarajia kumuoa, sasa wakati huo Catherine kashika kichwa huku akiwa kasumba macho ili hata asione kinachokwenda kufanyika katika mwili wa adam,….



    Lakini sasa kwa bahati nzuri, ukumbuke Catherine kuna mdada alimtuma kamba, ile ilikua ni njia ya kumtoa yule dada, sasa na dada huyo hakujua kama alitolewa kiujanja ili Catherine afanye mambo yake,.. Sasa alishanga kuona kamba aliokuwa akiifunga imefunga na ilikuwa ikiburuzika chini kama vile kuna mtu anaivuta… Sasa yule dada kuangalia… Laaaaa haulaaaa… Yaani chuma linakwenda moja kwa moja katika kichwa cha adam… Huyu dada hakujali kuwa ataumia kiasi gani, aliirukia ile kamba na alifanikiwa kuishika,.. Lakini sasa lile chuma lilikuwa ni lizito na istoshe lilishaongeza spidi ya kushuka chini sasa hapo ndio kila mtu anaona ila bado adam hajui kitu,.. Dada huyo alikuwa akiburuzwa na chuma hilo ilimradi tu lisifanikiwe kumkuta adam, sasa kwa bahati nzuri zaidi palikuwa na kibao cha zege, chenye jina la kanisa hilo… Hivyo yule dada alipofika pale akakumbatia nguzo moja ya kile kibao,… Lakini sasa kwakuwa lile chuma lilikuwa spidi,.. Lilikata kamba na kushuka sasa lenyewe lenyewe,… Lakini uzuri ni kwamba lilishapoteza muelekeo na halikuwa likimuelekea adam…  Sasa adam anakuja kushtuka chuma limeshafika jirani yake…iliskika sauti

    “paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa”

    Walio ona toka mwanzo walishikwa na kigugumizi juu ya kutoa sauti za kumwokoa adam,…

    “Catherine anakuja kufungua macho,.. Kwanza anakutana na irene akiwa kakumbatia nguzo huku kamba ikiwa mkononi,… Na hapo irene kachoka kaumia.. Catherine kuamsha macho kwa adam,… Gari ya adam ilikuwa haifai, lile chuma lilidondokea kwenye gari,.. Adam na Eva wapo salama salimini,… Kila mmoja anaangalia kiungo cha hilo chuma lilikuwa wapi,.. Wanagundua ni kule alipokuwepo Catherine,.. Wakati huo Catherine alikuwa akimuamsha irene pale chini,…

    “irene, irene… Rafiki yangu jamani amka”

    Catherine alikuwa akilia, mana bila irene, leo adam asingelikuwepo katika dunia hii

    Sasa adam alipoona kuna mtu kalala chini, gari yake haikuwa na thamani tena, adam alimkimbilia Catherine aliokuwa na irene pale chini… Sasa watu ndio wanaiona kamba ilioshika chuma kumbe irene ndiye aliekuwa akihangaika nayo, watu walianza kumuamsha irene,… Irene aliamka lakini alichubuka tumboni sana tu,..

    “hebu tumuwahisheni hospitali”

    Aliongea adam huku akimbeba kumpeleka katika gari ya Catherine,.. Adam hakusubiri mpaka Catherine aje kuendesha, aliingia mwenyewe na kuondoka kuwahi hospitalini,… Sherehe zote zikiishia hapo hakuna sherehe tena, mana kila mmoja ana wasiwasi muumini mwenzao kuumia, lakini mbali na hapo pia kuna watu walianza kutafsiri jambo lingine tofauti na ndio mana sherehe ikaahirishwa,…



    Adam huku hospitali, maskini irene yupo hoi, hajitambui kabisa, damu zilikuwa zikimtoka kwa wingi, ngozi ya tumbo ilikuwa ikining’inia… Yaani kama huna mayo mgumu huezi angalia mara mbili mbili… Irene alipewa huduma nzuri sana na gharama zote analipa adam…

    “dokta, tafadhali sana noamba mtu huyu apone… Yesu aishike roho yake, Israel akose nafasi”

    “amen…. Usijali ndugu, hapa ni sehemu salama kabisa”

    “nashukuru sana, naomba unipe dakika mbili”

    Adam aliomba dakika mbili, ili atoke hapo na kwenda kanisani kuangalia kinachoendelalea,… Lakini akiwa njiani nywele zake zilimcheza ghafla, kana kwamba kuna kitu kapishana nacho lakini hakionekani,.. Alisimamisha gari na kuangalia nyuma lakini hajafanikiwa kuona kibaya chochote kile,.. Aliendelea na safari ya kuelekea kanisani kwake



    Wakati huo adam ana wasiwasi sana juu ya irene, mana kaumia vibaya sana, japo uwezekano wa kupona upo, lakini kaumia vibaya sana katika tumbo lale,…



    Sasa ile adam kufika kanisani kwake, alitahamaki ghafla kwa kile alichokiona…..

    “heeeee, ni nini kimetokea hapa jamani, mbona hali imekuwa hivi”

    Adam aliongea hivyo baada ya kukuta uwanja mweupeeee, hakuna hata doa la watu, zaidi ya Catherine, Eva, Mama yake adam, Jessica, na Martha, pamoja na mdogo wake adam wa mwisho aitwaye maria… Yaani watu sita tu ndio ambao anawaona katika macho yake,.. Na hao ndio walikuwa wakikusanya vitu ili kuviingiza ndani na vingine kuvipeleka kwa wenyewe mana vilikuwa ni vya kukodisha…. Mama Adam alimkimbilia mtoto wake na kumkumbatia

    “mama, mbona sielewi mimi”

    “baba… Hata sisi hatuelewi, yaani tumeshangaa watu wanaondoka taratibu mpaka wakaisha… Yaani siamini mwanangu,…”

    Aliongea mama huku akilia, eva nae akafuatia kutokwa na machozi,… Watu zaidi ya 500 waliokuwepo hapo leo wamebaki watu 6 tu… Adam haamini macho yake,.. Basi nae ilibidi asaidie ili sasa kila mmoja akapumzike na hapo hakutokuwa na sherehe tena,.. Lakini sasa hata Catherine alikuwa kama vile haelewi nini chanzo cha ajali hio, wakati yeye ndio chanzo kikubwa sana….

    Adam na familia yake walimaliza ile kazi ya kutoa vile vitu,… Mafundi gereji walikuja kulichukuwa gari ya adam ambayo imeharibika sana,… Lakini papo hapo adam anapokea simu,..

    “haloo”

    Aliongea adam huku akiwa makini kwa kitega sikio

    “habari yako ndugu… “

    “salama, nani mwenzangu”

    “unaongea na daktari aliokuwa akimtibu mgonjwa wako aitwaye irene ndese,… Kiukweli tumejitahidi sana lakini hatukuweza kuyasaidia maisha yake…. Mgonjwa wako amefariki dunia”

    “Yesu wangu Uuuuuuuuuwiiiiiiii… Dokta unasema kweli au”

    Familia kuskia adam anapiga kelele na kutaja jina la dokta… Wakajua tu irene hatupo nae

    “halo dokta, halo.. Halo…. Yesu wangu weeee… Jamani binti wa watu mama”

    “nini tena adam”

    “yule binti amefariki dunia”

    Catherine kuskia vile alizimia pale pale mana ni rafiki yake kipenzi,… Hakuna ambaye hajatoa machozi kwakweli,…. Mana ilikuwa ni siku muafaka na yenye furaha kubwa duniani, lakini furaha yao imegeuka kuwa huzuni katika nyuso zao,… Basi walimbeba Catherine tena na kumueka katika gari,… Hakukuwa na muda wa kupepeana kwa wakati huo, ukizingua tu ni hospitalini…. Basi waliondoka wote katika eneo hilo walioachwa ni walinzi pekee,…



    Baada ya siku kadhaa kupita, wakiwa tayari walishamzika irene… adam akiwa kanisani kwake,.. Tena alikuwa kaketi mazabahuni akiliangalia kanisa lake,… Ghafla alianza kuteremsha maombi yalioambatana na machozi… Adam aliomba takribani masaa matatu tena akiwa peke yake katila kanisa hilo… Na ilikuwa ni siku ya Jumapili,… Sasa mama na watoto wake baada ya kuona mbona adam hayupo kule kanisani kwa baba yake, ndio wakakongojana sasa mpaka huku Eden Church na kukutana na sauti iliokuwa ikishusha maombi ya hali ya juu… Adam kweli alichagulia na mungu kulitangaza neno la Mungu,… Wakati huo eva nae yupo katika msafara wa familia ya akina adam.. Mama na watoto wake walinza kushika vifua vyao kwa maombi matamu yaliokuwa yakishushwa na mtumishi adam,… Ulishawahi kukuta pasta anaomba mpaka analia,.. Na sio kuwa analia bila sababu bali anawasikitikia waumini ambao wapo katika dini kama kebehi, wale wanaofanya madhambi ingali wakijua kila wanachokifanya si halali mbele za bwana…

    Maombi yalinza kuwaingia walioko nje,…. Ghafla Catherine nae huyu hapa, ikumbukwe kuwa Catherine ana kazi yake maalum wala hana kinyongo na mtu, shida yake aolewe na adam, anampenda sana kupita kiasi,.. Sasa Saa ngapi Hawajaanza kugala gala hapo chuni kwa ukali wa maombi, adam hajui kama nje kuna watu, maombi anayo yafanya ni makubwa, yale maombi ya ndani ya roho,… Familia nzima ilikuwa ikitakaswa kwa neno,… Inashangaza sana kuwa waumini wa mr Jacob wana mapepo ingali ni mtumishi wa Mungu, na anafanya kazi chini ya mungu lakini ilishangaza sana.. Adam anaomba mpaka analia…. Sauti yake ilikuwa ikitoka mpaka nje ya kanisa….. Sasa kelele zilipozidi ndipo akagundua kuwa nje palikuwa na watu,… Alitoka na kuendelea kushusha maombi juu yao thidi ya kile kilicho watembelea katika mili yao,….

    “huna mamlaka ya kuishi katika miili hii, achia na upoteee… Pepo tokaaa, mana hatupo kwa ajili yako, tupo kwa niaba ya mungu…. Damu ya yesu ihusike kuwatakasa watu hawa… Eee mungu pokea watu wako wakiwa wapyaaa… Na uwape upeo wa kutorudi walipotoka… Tokaaaaa…. Aaaamen”

    Adam alimaliza kufanya maombi yake huku wale waliokuwa wakigala gala, waliamka na kuanza kujipangusa,…

    “mungu wangu… Mbona nimekuwa mwepesi kiasi hiki”

    Aliongea mama yake adam…. Mara na wengine walifuata hivyo hivyo

    “yesu wangu…. Mama sio wewe tu, nimekuwa mwepesi na sio wepesi tu hata moyo wangu sasa mweupeee”

    Adam alifurahi sana baada ya kuskia maneno mazuri kama hayo,…

    “Ahsante sana baba mchungaji”

    Aliongea eva huku akilia machozi kabisa…. Maombi yaliwafanya kuwa wepesi katika nyoyo zao… Hakika adam ndio chaguo la mungu… Licha ya watu wengi kusema adam ni mdogo sana hakustahili kupewa wito mzito kiasi hicho… Baada ya maombi na ibada kuisha waliondoka zao nyumbani… Na hapo adam anatumia gari ya pale nyumbani kwao mana yakwake bado ipo gereji, hivyo kuna gari anatumia kwa muda japo uwani kwao kuna magari mengi lakini hatamani kuyatumia.. Lakini akiwa anaendelea na safari, ghafla simu yake iliita

    “yesu asifiwe fundi”

    “milele amina bwana mchungaji… Ah samahani gari yako ipo tayari huku gereji”

    “ooohhh unasema kweli fundi”

    “ndio.. Unaruhusiwa kuja kuichukuwa kwa wakati wowote mana hudaiwi bwana mchungaji”

    “Ahsante sana na yesu akubariki sana… Basi nitafika hapo wakati wa saa kumi ya jioni”

    “sawa bwana mtumishi… Mungu akutangulie katika ujio wako”

    “amen”

    Adam alikata simu na hapo alikuwa peke yake, mana gari anayotumia ni Vitz mayai new model… Hicho ni kigari cha maria, sema adam kaamua kutembea acho wakati gari yake ikiwa gereji… Sasa kwakuwa gari yake ipo tayari hivyo akanyoosha moja kwa moja nyumbani kwao,… Yaani anaongozana na familia yake mpaka kwao.. Ili kuirudisha gari na akachukue gari yake ilio tayari… Catherine kwa wakati huu mgumu aliacha kumsumbua adam, mana yupo katika mawazo toka ile ajali ilipotokea, mpaka leo adam hana raha, ni ile basi tu… Hivyo Catherine alipitiliza kwenda kwao,… Kisha adam na familia yake waliingia njia yao ya kwenda nyumbani….



    Mr Jacob alikuwa yupo ndani,.. Aliskia honi ya Vitz ikiwa nje, na anajua gari hio anatumia adam… Na kweli alikuwa ni adam akiingia katika nyumba hio,.. Adam alipofika kwenye parking ya magari aliona gari ya baba yake, hivyo akagundua kuwa mchungaji jacob yupo ndani… Adam aliingia ndani na kumsalimu baba yake

    “asifiwe bwana Yesu Kristo”

    “milele amina…… Mbona leo sijakuona kanisani”

    Aliuliza bwana Jacob huku adam akijibu

    “mchungaji… Kwa sasa nina kanisa langu, na linahitaji waumini… Hivyo sipaswi kuwa nalo mbali, kwa sasa nitakuwa nasalia kanisani kwangu”

    “oooohhh basi ni vyema… Ila kaa hapo nina maongezi na wewe”

    Adam alishtuka kuskia kaa hapo nina maongezi na wewe, mana siku zote maongezi ya mr Jacob na mwanae hua ni ya kukomandi kitu kifanyike…

    “kwanini ulikiuka agizo langu”

    Aliongea bwana Jacob huku adam akishangaa, kakiuka agizo gani

    “agizo gani hilo baba”

    “nilikwambia ukasome wapi na umekwenda kusoma wapi”

    Adam alishtuka kuskia hivyo, kana kwamba hapo ni kweli alikwenda tofuati na baba yake, na ndio maana hata sasa hivi huduma zao za kiroho ni tofauti kabisa… Kumbe shule aliokwenda kusomea adam huko Nigeria sio alioambiwa akasome.. Adam alichukuwa jukumu la kusoma shule nyingine tofauti na alioelekezwa na baba yake….

    “kweli baba, hapo naomba unisamehe, na sikujua kama utalijua hilo… Nisamehe sana baba”

    Mr adam alikasairika sana, hata kukubali msamaha wa mtoto wake kakataa kabisa….

    “we mtoto ni mjinga kabisa wewe… Kwanini unashindwa kuheshimu maagizo ya wazazi wako”

    “babaaa… Nimekuomba msamaha mzazi wangu, Nisamehe bure”

    “sitaki kusikia ujinga wako… Na ili nikusamehe ni lazima uoe mtoto wa mr Yohana”

    Bishop Jacob aliongea kisha akachukuwa koti la suti yake na kuondoka, hivyo msamaha kwa baba yake upo nje nje kama atamuoa Catherine,… Sasa baba katumia njia nyingine kama mzaz…. Mana radhi za wazazi ndio kila kitu hapa duniani.. Adam alikuwa na mengi ya kuongea lakini alikosa nafasi kwasababu baba yake aliondoka bila hata kumsikiliza mtoto wake.. Adam alinyanyuka pale sebuleni kisha akawa anakwenda upande wa nyuma ya hio nyumba ambapo huko nyuma ndipo jiko lilipo na ndipo mama yake alipo huko baada ya kurudi kanisani yupo huko kwa kazi za nyumbani.. Lakini sasa alipopita kwenye hio korido kuelekea nje,.. Ghafla nywele zake zilimsimama ghafla.. Lakini sasa kila kizidi kutafakari juu ya hilo.. Alikumbuka kuwa hii hii korido hii alishawahi kuiota,.. Hapo hapo kwenye hio korido kuna chumba ambacho toka kuzaliwa kwake hajawahi kukifungua wala kujua kuna nini… Kama vile ile ndoto ilikuwa ni ya kweli, ila hatujui… Adam kugeuza shingo, kweli alikiona kile chumba.. Alisita kwenda na kukirudia kile chumba,.. Alishika kitasa kama vile kwenye ile ndoto,.. Lakini kabla hajafanya hivyo aliangalia huku na kule na kugundua hakukuwa na mtu aliokuwa akimuona… Adam alirudi katika mlango na kuanza kuomba kabla ya kufungua mlango huo…… Alipomaliza alikishika kile kitasa, tayari kukishusha chini ili afungue… Sasa huku nje mama nae anaingia ndani, lakini ghafla akamuona mtoto wake kasimama katika mlango ambae hata yeye hajui….. Sasa kumbe hata mama mwenyewe pia hajui pale ndani kuna nini… Sasa mama hakutaka kwenda,. Hivyo nae akabana mahali ili mlango ukifunguliwa tu, aone humo ndani kuna nini… Mana hata mama mwenye nyumba hajui kuna nini humo ndani…. Adam bila kujua kuwa mama yake anamuona,.. Bila woga mtumishi adam Alishika kile kitasa na kukiminya chini, kisha akasukuma mlango mbele……





    Wakati huo kila mmoja, kati ya adam na mama yake wana hofu juu ya chumba hicho,… Yani nyumba nzima hakuna anaejua kuhusu chumba hicho,.. Licha ya watoto kutojua hata mama mwenyewe hajui chumba hicho kimewekwa nini.. Sasa leo kamkuta mtoto wake anataka kukifungua kile chumba, na mama hana hisia zozote juu ya chumba hicho, ila anataka kujua kuna nini… Na hata adam maisha yake yote kaishi hapo lakini wazo la kukifungua au hata kuuliza hana.. Kwa mara ya kwanza akiwa kwake ndio akapata ndoto ya hiki chumba,.. Sasa adam akashika kitasa cha mlango, wakati huo mama nae anaangalia kwa umakini kile anachokifanya adam, mana ana hamu ya kuona huko ndani kukoje



    Bila woga mtumishi adam Alishika kile kitasa na kukiminya chini, kisha akasukuma mlango mbele…… Lakini kwa bahati mbaya mlango ulikuwa umefungwa,…

    “yesu wangu… Kumbe pamefungwa”

    Aliongea adam huku mama ndio anakuja sasa baada ya kuona adam kashindwa kufungua, adam akaacha ili akamuombe mama yake ufunguo wa chumba hicho… Sasa ile anageuka tu, mara mama huyo

    “we ulikuwepo hapa jirani”

    Adam aliuliza mana anajua hakukuwa na mtu,…

    “nilikuwa pale nakuangalia tu”

    “sasa mama, ivi humu ndani kumewekwa nini… Hebu nipe ufunguo”

    Aliongea adam, mara mama akaanza kucheka sana… Kacheka sana mpaka akaenda kukaa kwenye sofa kwa kucheka…

    “sasa mama unacheka nini”

    “nacheka kwasababu huko ndani ya hicho chumba, utakutana na spea za magari humo”

    “spea za magari???….atawekaje spea za magari ndani”

    Adam alishangaa sana kuskia spea za magari ndio zipo humo,…

    “sasa kama nikimuuliza ndio anasema hivyo nifanyeje”

    “lakini hujawahi kuona”

    “we mwenyewe kwa macho yako”

    “baba wewe…. Mwisho wa kukiona hicho chumba, ni siku tunahama kutoka kwenye ile nyumba ya kule juu.. Ulikuwa bado hujarudi shule… Mlipofunga shule ndio ukaja ukakuta tayari tumesha hama na kila kitu kipo mahala pake”

    “kwahio wewe ulikionaje”

    “siku hio tunakuja kufanya usafi ndio nikakiona kilikuwa hakina kitu… Ila siku ile tunahama… Tulikikuta tayari kimefungwa na mpaka leo sijui kinafunguliwaje”

    “nipe huo ufunguo”

    Adam alimwomba mama yake ufunguo ili afungue

    “adam mwanangu, nirudie mara ngapi.. Nimekwambia sijui hata kinafunguliwaje, vile nina hamu ya kuona hata hizo spea za magari zikoje mana hata siku ya kuletwa hizo spea sijui zililetwa lini.. Kama ufunguo ninao sasa si ningeshaona muda mrefu tu”

    Adam hakutaka kumsumbua mama yake, alishika simu kisha akampigia baba yake

    “we unampigia nani”

    “baba”

    “weeeeeeeeee, unataka umwambie nini”

    “we subiri, Unaogopa nini mama… Yesu akutawale mama”

    Mama alitulia kimyaaaa na kusubiri adam ataongea nini na baba yake, mana walivyomaliza kuongea saa ile baba aliondoka zake…



    “haloo mchungaji”

    “vp adam.. Si nilikuwa hapo nimekuacha sasa hivi”

    “baba nataka ufunguo wa hiki chumba”

    Mzee Jacob alishtuka kuskia anataka ufunguo wa hicho chumba… Lakini baba akazuga ile kama hajui ni chumba gani

    “lakini adam.. Chumba chako mimi sijafunga,.. Na kama kimefungwa, mwambie mama yako”

    “baba mtumishi, sio chumba changu nilichokuwa nalala”

    “bali ni chumba gani?… Ina maana wataka kuingia chumbani kwangu”

    “eeeehhh basi baba, naona unawaza vingine, Samahani mzee wangu”

    Adam alikimbilia kuomba msamaha, lakini hakutaka kukata simu

    “kwanza fanya ninalotaka kwanza.. Oa”

    “sawa.. Ila shida yangu ni ufunguo wa hiki chumba cha katikati hapa”

    “Unasemaje?? Sasa spea zangu unataka kuzitoa za nini”

    “spea… Sasa baba mtumishi, spea za magari unawekaje ndani”

    “ni mpya”

    “eeeehhh… Sasa nipe basi niangalie hata piston moja kama itanifaa… Mana si unajua gari yangu ipo gereji”

    “sasa gari zangu mimi ni Benz za zamani na wewe unatumia Range Rover Discovery 4, wapi na wapi… Spea zake haziingiliani baba”

    “kwahio hata hio piston sipati”

    “kaulizie hio piston inauzwa shilingi ngapi nikutumie hela kama huna… Au hebu kata simu nikutumie milioni moja ukanunue hio piston”

    Mara simu ikakata kweli,… Huku adam akishusha pumzi nzito sana..



    “haya kasema ufunguo upo wapi”

    Mama aliuliza huku akicheka sana

    “we acha tu mama…. Ameniambia hizo spea hatakiwi kutoka hapo”

    Mara simu ya adam imeingia meseji, kuangalia, imetumwa milioni moja na laki tano, na wala hakuwa na shida na hio pesa..

    “eti katuma pesa nikanunue hio spea ninayo taka, ila sio kutoa kwenye hicho chumba”

    “lakini mwanangu, kama kweli kuna spea zake… Achana nae”

    “mamaaaaaaa… Huku ndani hakuna spea, huku ndani kuna kitu… Na ipo siku tu.. Damu ya Yesu itautaka ule mlango, ipo siku nitaona huko ndani kuna nini… Ila mwambie baba.. Sini haipelekwi hivyo”

    Aliongea adam kisha akawa anaondoka

    “weeeeeeee njoo umwambie mwenyewe, wewe ndio unamuweza baba yako.. Wataka nichezee makofi”

    Aliongea mama yake adam, huku adam akiondoka zake….



    Sasa kumbe baba alikuwa katika kikao na alikuwa akimuongelea mtoto wake, ndio ghafla akapiga simu, na hapo yupo kwenye kikao na mabishop wenzake, yaani matajiri wenzake ambao wanamiliki makanisa mengi, kila Bishop mmoja hapo hakosi makanisa sio chini ya 50, na ni matajiri haswa….

    “jamani uyu mtoto sasa atanitoa roho”

    Aliongea mr Jacob na hapa sasa ndio tujue silika yake ni ipi…

    “mtoto wako huyo”

    Aliongea kiongozi mwenzake huku akicheka

    “mimi mtoto wangu ananifuata mimi.. Yaani hana ubishi”

    Aliongea mwingine huku mwingine akisema kuwa

    “mpigie AT Bishop Jehova”

    Mmoja aliongea hivyo kuwa ampigie atbishop jehova, yaani kuna BISHOP  na ATBISHOP.. Huyu AtiBishop ni kiongozi msimamizi wa makanisa yote Afrika, anajiita Jehova,… Kajiita yeye mungu, kitu ambacho ni makosa kwa binadamu kujiita majina ya mungu,….

    “jehova nilimpigia juzi… Baada ya kumpa taarifa za mtoto wangu.. Kwanini kamfundisha mtoto wangu vitu tofauti na itikadi yangu”

    “alikujibu nini”

    “nilimwambia, kuwa kiukweli mtoto wangu, yupo tofauti na mimi.. Kiasi cha kwamba, siku anaingia kanisani kwangu kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Nigeria… Huezi amini nilikuwa natetemeka”

    “akakujibu nini… Alinipa njia ya kufanya, na ni kweli hio njia imefanikiwa… Lakini bado anazidi kiwa juu yangu, huyu mtoto atantoa roho jamani wenzangu”

    “ongea tena na jehova”

    Aliongea Bishop mmoja huku mr jacob akitikisa kichwa… Baada ya kikao kuisha, mr jacob akiwa katika gari yake… Aliwaza sana kuhusu mtoto wake…. Sasa hapa ndio tunapa fununu zote juu ya kilichotokea nyuma….



    TURUDI NYUMA KIDOGO KAMA SIKU NNE AU TANO ZILIZOPITA…. TUANZIE SIKU ILE ADAM AKIWA KANISANI KWA BABA YAKE…..



    Sasa ukumbuke adam alipoingia kanisani kwa baba yake, alipunga mkono kuwashukuru waumini kwa furaha walio nayo juu yake… Lakini upungaji ule ulimtetemesha mr Jacob, mpaka mama yake akaingilia kati na kusema adam akae chini, na hapo adam hakujua kuwa hata baba yake alikuwa akitetemeka…..



    Baada ya ibada, mr Jacob aliingia katika gari yake.. Na kuanza kuwaza sana juu ya adam

    “huyu mtoto ni nini hii… Inamana jehova kamfundisha zaidi yangu… Mbona kama ana upako zaidi”

    Aliongea mr Jacob akiwa peke yake katika gari lake,….

    “au huyu mtoto hakwenda kwa mr johova”

    Jacob alizidi kujiuliza na asipate jibu, alichukuwa simu yake ambayo anaweza kupiga hata nje ya nchi,.. Aliitafuta namba ya atbishop jehova wa Nigeria….

    “hallo mr jehova, asifiwe bwana yesu Kristo”

    “milele amina.. Hali ya Tanzania vipi huko”

    Aliongea jehova, ila hapo walikuwa wakiongea Kingereza, ila mimi naandika kwa Kiswahili,…

    “hakuna shida…. Ahh sasa mr jehova.. Kijana wangu mbona yupo tofauti sana, siwezi kuamini kwamba leo kaingia kanisani kwangu, kunyanyua tu mkono wake namna hii, nimetetemeka sana pamoja na waumini wangu… Ni uwezo gani umempa kijana wangu”

    Aliongea bwana Jacob tena kwa msisitizo sana

    “aaaahhh kwanza uniwi radhi,… Nimekuficha ndani ya mwaka wote huo… Kweli kijana wako alifika kwangu,… Lakini alinipa pesa za kusoma kwangu, lakini akaniambia kiwa hatosoma kwangu na niwe kimya kwa hilo.. Nilimuuliza unakwenda kusoma wapi, hakunijibu lakini baada ya kupeleleza nikagundua anasoma katika chuo kinachomilikiwa na TB JOSHUA na TB SOLOMON, huku Nigeria… na vyuo hivyo hufundisha bure bila malipo yeyote, na huko ndiko aliposoma mtoto wako… Chuo hicho ni chuo chenye imani ya kweli, ni chuo kilichojaa imani.. Ni chuo kilicho na upako… Hata mwanafunzi wa pale siendani nae kiuwezo”

    Aliongea jehova, kuwa hata mwanafunzi wa chuo kile haendani nae kabisa… Hivyo adam hapo alipo hafai, Biblia imejaa kichwani na matendo mema…

    “lakini kwanini unanifanyia hivi bwana jehova,… Ona sasa mtoto ananisumbua mimi”

    “keshaoa”

    “bado, tena kakataa kuoa kwa mana kuna mschana nataka amuoe lakini yeye hataki sasa kakataa kabisa”

    “fanya haraka, mpe nafasi ya kuwa pasta… Na akae tofauti na wewe, mana humuezi, mana sisi tunatumia nguvu za shetani… Yule humuezi mr Jacob”

    Aliongea mr jehova, yaani hata Jacob anaogopa mana anaweza kuumbuliwa hata mbele za watu…

    “kwahio nifanye bwana jehova”

    “itisha kikao cha viongozi, mpe heshima yake ya uchungaji… Si ulisema ana kanisa lake”

    “ndio”

    “mpe nafasi.. Itisha kikao hata leo mpe hio nafasi, inawezekana hata kama hajaoa… Mana kuoa hizo ni sheria za kutimizwa tu lakini panapo wito basi aitike tu”

    “sawa, wacha nifanye hivyo”



    Baada ya msaa kadhaa, ndio pale adam akaitwa kanisani na kukuta viongozi wengi sana akiwemo hata Catherine, japo Catherine hakuwa kiongozi ila baba yake alikuwepo hapo, na nia ya Catherine kuwepo ni kwamba adam anapokabidhiwa heshima ya uchungaji kama wito toka kwa mungu, basi akabidhiwe na mchumba papo hapo, na ndio mana Catherine siku ile alikuwepo… Adam alikubali kuitikia wito dhidi ya kulitangaza neno la Mungu mahala popote nchi yeyote….



    Sasa baada ya adam kukubali kuupokea wito,.. Siku hio hio akapanga kulizindua kanisa lake ambalo tayari limeshakuwa tayari kwa matumizi ya ibadaba… Kanisa la thamani kubwa, lenye kiwango kikubwa… Limetengenezwa kwa vioo tu basi,… Siku ile jioni akiwa na Catherine, adam ndio akamwambia Catherine kesho aje na wenzake, kwasababu ndio siku anazindua kanisa lake,…. Na siku hio hio ni siku aliohama adam toka kwao kwenda kwake,… Sasa kumbe ukikaa kule kwa baba yake, huezi gundua lolote kule kwenye ile nyumba mana unaishi na mashetani hayo hayo.. Ila ukiwa tofauti na hio nyumba ndio utajua ile nyumba haiko sawa.. Na ndio mana adam siku ya kwanza ya kulala nyumbani kwake, alipatiwa ndoto juu ya nyumba yao.. Na kesho yake hakufuatilia hilo, mana alikuwa na uzinduzi wa kanisa lake….



    Sasa mr Jacob alikwenda katika uzinduzi wa kanisa la mtoto wake, lakini siku ile hakufika mpaka pale kanisani, bali alikuwa kwa mbali kidogo na hakuna anaejua kuwa mr Jacob yupo…. Sasa mr Jacob alishangaa kanisa ni jipya, halafu limejaza utafikiri ni soko… Afu mbaya zaidi, watu wengi ni waumini wake.. Mr jacob aliona hio ni aibu kubwa, mana katika uzinduzi wa kanisa lake, yeye hakuwa na watu wengi kiasi hicho, palikuwa na watu kama miamoja na hamsini… Sasa hapa kwa adam ni soko la watu… Ni wengi mno… Mr Jacob aliona hii ni aibu kubwa, alimpigia jehova ambae ndio kiongozi msimamizi wa makanisa aina ya imani yake afika nzima…

    “jehova, jehova, jehova… Nakwenda kuaibika sasa, Bishop mzima sijawahi kujaza umati kiasi hiki… Aibu hii”

    “vp bwana jacob, hata salam imegoma… Kuna nini”

    “mwanangu anazidi kunipasua kichwa”

    “nini tena.. Si ulisema keshahama kwako, na tayari kaupokea wito”

    “ni sawa vyote hivyo vimefanyika… Ila leo anazindua kanisa lake…. Bwaaana weee… Naona kama soko vile, na mbaya zaidi Karibia waumini wangu wote wamenihama”

    “punguza presha bwana jacob”

    “nitapunguzaje presha na nakwenda kuaibika”

    Aliongea mr Jacob huku akilalamika sana mana heshima yake itashuka

    “sasa sikia…. Fanya kitu… Yaani hapo atabaki peke yake”

    Aliongea bwana jehova huku mr Jacob asijue afanye nini japo uwezo anao

    “nifanye nini.. Ukumbuke ni mtoto wangu,.. Mimi staki aibu”

    “sawa…. Hapo aulipo unamuona”

    “hapana…. Ooohhh yes, ndio anaingia namuona ndio anafika”

    “utaweza kufanya”

    Bwana jehova Alimuuliza bwana jacob kuwa ataweza kufanya…

    “una maana gani, mr jehova… Tafadhali sana naomba isije ikaleta madhara kwa familia yangu… Mana shida yangu ni kwamba mtoto wangu asinizidi uwezo wa uchungaji… Ila pasiwe na madhara… Nipe njia ya kufanya”

    Jacob alikuwa tayari kwa lolote litakalotakiwa kifanywa, kikubwa mtoto asimzidi…

    “hakikisha anakufa mtu mmoja katikati ya watu wa karibu wa mtoto wako”

    “aaaaaaaaaaaaaaa bwana jehova, nimekwambia mimi sitaki kufanya madhara… Sitaki”

    “basi, kama huezi basi… Ila mtoto wako hutomueza bila kutumia hio njea”

    “ahhhh…Ok Hebu niambie nitatumia njia gani, mana nipo mbali kidogo na eneo lenyewe”

    “ili mambo yaende sawa…  afe mtu wa karibu wa mtoto wako, na asipokufa wa karibu yake, lazima hilo jambo lirudiwe….. Laa sivyo hutomuweza kabisa”











    Aliongea bwana jehova ambae ndio atBishop kiongozi wa makanisa yote Afrika yenye kuitumikia imani yake, jehova akisema kitu kisipotekelezwa basi usije kulalama baadae,… Wakati mr Jacob akiwa jirani na kanisa la mtoto wake, alishangazwa na umati wa watu waliokusanyika kwa ajili ya kufungua kanisa hilo, kwake haijawahi kutokea toka alipoanza kulitangaza nrno la Mungu, ana makanisa 50 lakini yote hakuna liliojaza kama la mtoto wake,… Sasa kitendo hicho kwake ni aibu kubwa kwanini mtoto kamvua nguo kiasi hicho,… Aliwaza kuwa hapo ni siku ya uzinduzi, je? Siku za ibada itakuwaje??… Aliomba ushauri kwa mr jehova na kumpa ushauri ambao unaendana na imani zao,…



    “ili mambo yaende sawa…  afe mtu wa karibu wa mtoto wako, na asipokufa wa karibu yake, lazima hilo jambo lirudiwe….. Laa sivyo hutomuweza kabisa”

    Sasa alipoongea hivyo mr jehova, na Bishop Jacob alikuwa akiangaza macho, mara akamuona adam akiwa jirani na pasta mmoja hivi, halafu pembeni yake tena alikuwepo eva…

    “Enheee,.. Safi sana.. Nipe njia jinsi ya kufanya”

    Aliongea bwana Jacob, huku jehova akianza kumpa njia

    “pete yako si unayo hapo”

    Aliuliza bwana jehova kuwa pete yake anayo hapo alipo

    “ndio, ninayo”

    Alijibu bwana jacob, na kweli alikuwa na pete yenye rangi ya kijana katika mkono wa kushoto kidole cha pili kutoka kidogo cha mwisho,..

    “sasa angalia kitu cha hatari hapo… Kisha mnyooshee mtu ambae ataweza kusababisha ajali hapo.. Ili huyo mtu wa karibu afe… Na unapo nyoosha hakikisha unanuia manuio yako”

    “sawa.. Nimekuelewa bwana jehova”

    “nakutakia bahati njema”

    Alikubali bwana jacob huku simu ikikatwa,…



    Sasa huku kanisani hapo hapo,.. Irene ndio alikuwa anafunga lile chuma,.. Na kwakuwa Catherine ndio msimamizi wa maandalizi hayo,.. Alimkuta Irene akiwa anafunga lile chuma, na hilo chuma ndio kila kitu katika jukwaa linalojengwa,..



    “ah ah, usilegeze hio kamba, kaza haswa”

    Ilikuwa ni sauti ya mwanadada Catherine, yaani yeye ndio alikuwa akiongoza mpangilio mzima wa maandalizi hayo, na nafasi hio alipewa na adam….



    Sasa kule kwa mr Jacob akaangalia hatari ya kufanya,.. Mara akamwona Catherine,… Sasa alipoangalia ile nguzo ndio akagundua kuwa ikiachiwa pale itamdondokea Eva,.. Sasa wakati huo na Catherine nae hakuridhishwa na ufungaji wa irene katika lile chuma.. Hivyo akamwambia atoke amsaidie kulifunga,… Catherine anajua maandalizi ya kuandaa majukwaa mana ni mtoto wa pasta hivyo anajua mengi kwenye maandalizi ya sherehe mbalimbali,… Sasa alipoingilia kati swala lile la kufunga lile chumba, ndipo bwana Jacob akanyoosha pete yake akiwa mbali huku akinuia mambo yake katika moyo wake,.. Nia ya Catherine ni kulikaza lile chuma, lakini pale pale akili ikaanza kuvurugika… Alimuona eva ambae ni kama mke mwenzie lakini hakuna alio olewa bado,… Sasa kitendo kile kilimtia wivu, ila hapo haikuwa akili ya Catherine, hio ni akili ilimjia ghafla tu lakini hakuwa yeye… Sasa Catherine ndio akaanza kulivuta vuta na kujifanya kama anataka kuliachia lile chuma.. Ndipo akagundua kuwa akiliachia litamdondokea eva, sasa ili yeye aolewe na adam, basi eva hakutakiwa kuishi katika hii dunia na eva akifa tu,.. Basi mama mchungaji ni Catherine….



    “Irene? Naomba ukaniongezee kamba ili niikaze hii vizuri”

    Aliongea Catherine ili huyo irene asione kitu, mana ndio aliokuwa karibu nae,… Irene bila kujua kuwa katolewa ili Catherine atimize lengo lake…….



    Baada ya irene kuondoka, Catherine huku nyuma hakufanya makosa… Aliliachia lile chuma na likawa linaelekea katika kichwa cha eva,..



    Adam akamshika eva na kumsogeza kwa mbele ili pasta amuone mke mtarajiwa wa mchungaji adam,… Sasa lile chuma halimuelekei eva tena, bali ni adam….. Kwakuwa kifo hakikunuiwa kiwe cha adam, hivyo Catherine alipiga kelele lakini haikusaidia,…

    “pasta adam angalia juuuuuuuuuuuu”



    Ghafla irene aliotoka kuleta kamba, ndio akaona mbona pasta adam atakufa.. Hapo irene akajirusha na kuburuzika na ile kamba…



    Adam na Eva walipona wote, lakini irene aliumia vibaya katika tumbo,.. Lakini hakuwa mtu wa kufa, ni ngozi ya tumbo imechubuka sana wakati anaburuzana na kamba…. Adam alimpeleka irene hospitali…



    Sasa wakati adam anarudi hospitalini baada ya kumuacha irene akiendelea kupata matibabu… Akiwa njiani ghafla nywele zake zilimsimama, hajakaa vizuri mara kulipita kitu kama kimbunga,.. Adam alisimamisha gari na kuangalia.. Lakini hakuona kitu… Aliondoka zake



    Sasa huku hospitalini, kumbe kile kimbunga alikuwa ni baba yake adam anakwenda hospitalini kumalizia kazi yake… Kweli alionekana mr Jacob akiingia katika hospitalini hio bila kuonwa na mtu yeyote,… Aliingia moja kwa moja mpaka kwenye wodi aliolazwa irene.. Madaktari walikuwepo lakini hawakujua kama pembeni yao alikuwepo mtu… Juhudi za madaktari zikifanyika, na juhudi za Jacob zinafanyika…. Juhudi za Mr Jacob zilishinda kuliko za madaktari



    Huku kanisani alipo adam akiwa ndio anakusanya vitu baada ya sherehe kukatika ghafla,… Mara smu yake inaita, aliipokea simu hio

    “haloo”

    Aliongea adam huku akiwa makini kwa kutega sikio

    “habari yako ndugu… “

    “salama, nani mwenzangu”

    “unaongea na daktari aliokuwa akimtibu mgonjwa wako aitwaye irene ndese,… Kiukweli tumejitahidi sana lakini hatukuweza kuyasaidia maisha yake…. Mgonjwa wako amefariki dunia”

    “Yesu wangu Uuuuuuuuuwiiiiiiii… Dokta unasema kweli au”



    Sasa baada ya mr Jacob kumaliza kazi yake alirudi pale kanisani kwa mtoto wake adam… Nae alishangaa kukuta uwanja mweupeeee…

    “Ahahahahahahajahahahahahahahahahaha aaaaaaaaaaaa hahahahahahaaahahah… Safi sana jehova”

    Alicheka sana bwana Jacob huku akimsifu jehova aliompa akili hio,..



    Sasa ndio tunajua kwanini aliua… Maana yake ni kwamba… Muumini mwenye imani potofu, akiona kwenye umati wa watu pamekufa mtu tena kwenye nyumba ya ibada, huwa wanaogopa kwasababu wanajua huyo mtu katolewa kafara, yaani kanisa linafunguliwa kwa damu.. Hivyo umati wote ule, uliwaza hivyo kuwa kanisa limefunguliwa kwa damu ya mtu, yaani adam kaua mtu ili kanisa lake lijae… Hio ndio akili alioitumia jehova, kwamba waumini wengi wana akili potofu,.. Ni lazima wawaze ujinga huo… Na ni kweli na mdivyo ilivyotokea…..



    MWISHO WA KUMBUKUMBU YA MR JACOB, AKIWA KATIKA GARI YAKE BAADA YA KIKAO NA MABISHOP WENZAKE….



    mzee aliwaza sana kuhusu adam mana bado anamfuatilia katika mienendo yake, kana kwamba mpaka kufikia hatua ya kuulizia chumba chake cha siri nzito… Na tena alitegemea kumkabidhi mali na mambo yote akiwa kama mtoto wake wa kiume,… Kumbe kabadirika na ni mchungaji mchanga sana, lakini anawatikisa watu na ndevu zao, hakika imani ya mungu inaweza kuingia popote…



    Sasa adam alipotoka pale kwao alikuwa na hasira sana baada ya kuukosa ufunguo wa kile chumba, alimpiga baba yake lakini pia alishindwa kupata msaada,… Sasa kitendo cha adam kutoka kwa hasira, Jessica alimuona mdogo wake mbona ana hasira hivyo kuna nini.. Alimfuata na kumuuliza lakini alikuwa haongei kabisa kwa hasira.. Sasa adam akaona gari iliopo gereji atakwenda kuichukua kesho, hivyo aliendelea kuitumia ile gari ndogo ya maria… Sasa Jessica akaona mdogo wake ana hasira sana, hivyo hata gari hatoweza kuendesha… Ndipo Jessica akaingia kwenye gari na kumwambia…

    “wacha nikupeleke mchungaji… Mana haupo vizuri”

    Adam alikubali mana kweli hakuwa vizuri kabisa..



    Sasa huku nyumbani kwa wini,. Kama unamkumbuka wini, ni rafiki wa Eva, sasa wakati huo anaitafuta namba ya mtumishi adam,… Mana kama unakumbuka siku ile ya uzinduzi wa kanisa… Adam alimpita Eva mana alikuwa kavaa vizuri, hivyo simu ya wini ilitumika kumpigia adam arudi kwani amempita maeneo ya karavatini… Sasa ile namba ikawa imebaki katika simu ya wini, na Eva alimwambia wini aifute hio namba, na wini akakubali lakini hakuifuta na ndio sasa hivi anaitafuta katika namba zilizopigwa

    “eti, uifute hio namba… Nyooooo, labda sio pasta adam”

    Aliongea wini kwa kuibeza sauti ya rafiki yake eva pale alipomwambia aifute hio namba…

    “yes, hii hapa…. 0714419487… Yes Ahsante yesu, hii ndio yenyewe ilipigwa saa tatu na robo.. Ndio yenyewe hii, ngoja niisevu kabisa hapa”

    Aliongea wini huku akifurahi kupita kiasi,…

    “MTUMISHI… yes nimsevu kwa jina hili”

    Wini alimsevu kisha akawa anataka kuipiga na wakati huo ni jioni sana kagiza kanaanza kutanda… Wini alikuwa akihisi woga kupiga saa moja kasoro mida ya usiku,..



    Sasa huku kwa adam, wakiwa tayari wameshafika nyumbani, na hapo Jessica kwakuwa kafika nyumbani hivyo kaona ampikie kaka yake kabisa kisha aondoke… Walikuwa wamekaa sebuleni lakini Jessica alikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza kaka yake…

    “Samahani mtumishi kama nitakuuzi… Nina swali nataka kukuuliza”

    Aliongea Jessica ambae ni mkubwa kwa adam, sema kwakuwa adam tayari ni mchungaji hivyo ni lazima apate heshima yake…

    “uliza tu”

    “eti, baba yetu ana kiwango kikubwa sana katika imani yetu,.. Lakini nilishangaa siku ile unapunga mkono, baba anatetemeka, kana kwamba wewe umekuwa na upako zaidi kuliko yeye,… Kwanini imekuwa hivyo, na chuo cha Bibilia alichosoma yeye ndipo ulipokwenda kusoma wewe,.. Kwanini uwe juu yake”

    “swali zuri sana ila lina majibu marefu mno… Kwa sasa sipo vizuri, ningekuomba uje kesho mapema dada angu, nitakwambia kila kitu”

    Sasa ghafla simu ya adam inaita,..

    “simu yako inaita mtumishi”

    “aaahhh ni nani”

    “haina jina”

    “aahh nimechoka, mambie apige kesho”

    Bazi kwakuwa Jessica alipewa ruksa ya kuipokea, aliipokea simu ya kaka yake….. Sasa kumbe aliopiga alikuwa ni wini ndio kapiga afu inapokelewa na Jessica,

    “Hallo”

    Jessica alianza kisha wini akaendelea

    “hallo, tumsifu yesu Kristo”

    Alisalimia wini huku akiogopa sana mana hakutegemea kama itapokelewa na mwanamke… Na Jessica hajui wala hana namba ya wini ila akimuona atamjua mana anasaligi kanisani kwao..

    “milele amina… Samahani dada, mtumishi kachoka sana, labda umpigie kesho”

    Aliongea Jessica huku wini akikata simu,.. Wala hakutaka kuongea tena

    “ni nani huyo”

    Aliuliza adam, kuwa ni nani aliipiga

    “simjui, ila labda ni waumini wako tu hao…. Sasa. Chakula tayari ni wewe tu sasa kama unakula saa hizi nikupakulie”

    “hapana, niache ache kwanza”

    “sawa… Mi naondoka”

    “chukuwa gari nenda nayo”

    “sasa wewe utatumia nini”

    “nitamwambia fundi aniletee hapa nyumbani”

    “sawa… Usiku mwema kaka angu”

    “nawe,.. Yesu aiongoze nyumba yenu”

    Sasa Jessica akashtuka lwa kuskia hayo maneno, mana adam ndio mtu wa kwanza kugundua kuwa pale ndani kuna chumba kibaya.. Japo hata yeye alikuwa akiishi humo ila ili ujue utatakiwa usiishi humo ndani..

    “unasemaje”

    “yesu aiongoze nyumba yenu”

    “nawe pia”

    Lakini Jessica alikuwa na wasiwasi juu ya maneno hayo, ila hakutaka kumuuliza sana, kwasababu alikuwa kachoka sana….



    Kesho yake,… Huku kanisani kwa baba yake adam,.. Alikuwepo wini na Eva wakiwa kwenye gaden wakijisomea Biblia na kujifunza kuimba kwaya kwa kupitia Biblia,..

    “ngoja kwanza…. Iv Eva, jana umeenda kwa adam usiku”

    Wini alimuuliza eva kuwa jana alienda kwa adam usiku,.. Mana alipopiga alipokelewa na mwanamke

    “heeee adam tuliachana muda mrefu tu, toka saa kumi jioni”

    “sasa atakuwa ni nani aliokuwa nae jana usiku sanaaaa…”

    Alionhea wini, kitu kilichomshangaza eva

    “usiku sana…. Kama saa ngapi”

    “ustake kujua saa… Ila mchumba wako alikuwa na mwanamke usiku”

    “wewe umejuaje kama alikuwa na mwanamke usiku??”







    Ndugu yangu ukitaka kuwa mbea au mwongo, cha kwanza uwe na kumbukumbu ukumbuke jana au juzi ulidanganya nini, sio unakurupuka tu kua mbea ingali huna kumbukumbu

    Sasa kwa huyu wini alitakiwa kuwa na kumbukumbu kwanza ili akiulizwa umejuaje ajibu,… Juzijuzi wini aliambiwa afute namba ya mtumishi adam katika simu yake mana ilitumika kumpigia baada ya kumpita sehemu alipo simama… Sasa ile namba hakuifua na badala yake akaisevu afu jana ndio kapiga, na simu ikapokelewa na dada yake adam,… Sasa hakutakiwa kuja kusema, alitakiwa akaukie tu moyoni mwake, sasa kaja kusema afu Eva anamuuliza na yeye…



    “usiku sana…. Kama saa ngapi”

    “ustake kujua saa… Ila mchumba wako alikuwa na mwanamke usiku”

    “wewe umejuaje kama alikuwa na mwanamke usiku??”

    Hapo wini akakaa kimya mana kama hana namba ya simu basi alikuwa anamfuatilia nyuma nyuma,..

    “si nakuuliza we ulimkuta wapi na huyo mwanamke”

    Eva alirudia tena kumuuliza wini

    “Samahani Eva… Unajua juzi ulivyoniambia niifute ile namba yake, nilisahau kufuta… Sasa jana nikawa kuna namba naitafuta ambayo sikuisevu… Sasa nikajua ndio ile si ndio nikapiga, mara kapokea mwanamke… Sikutaka kuuliza sana ila akaniambia nimpigie kesho mana siku hio kachoka.. Sasa Eva? saa tatu za usiku pasta kachoka sasa je wameanza saa ngapi, si mapema sana”

    Wini Aliongea mengi kisha akaongeza tena na chumvi juu

    “sasa wini, nikuulize kitu.. Wewe umesema ulimpigia mtu namba yake umeisahau hujaisevu… Sasa wakati inapokelewa kwanini ulichukulia moja kwa moja kuwa ni mtumishi wakati namba huijui”

    “niliokuwa nampigia ni mwanamke, ila sauti sio ya mhusika, na baada ya kukata simu ile namba nikaikagua kwenye TigoPesa, ikaniletea Adam Jacob Michael, ndipo nikajua kumbe ni mchungaji adam ndio nilimpigia”

    Sasa Eva nae akaona mbona kama maongezi yake ni ya kweli,…

    “ina maana mtumishi alilala na yule mwanamke”

    Sasa Eva aliposema hivyo, wini akadakia

    “alaaa kumbe hata wewe unajua kuwa alikuwa na mwanamke”

    “nitajua tu… Tena nakwenda kanisani kwake sasa hivi”

    Aliongea eva huku akiondoka zake kuelekea kanisani kwa adam ambaye ndio mchumba wake,…

    “eeee mungu wangu umbea ungeniponza leo Uuuuuuuuuwiiiiiiii”

    Aliongea wini baada ya kuponea kwenye tundu la sindano kwa umbea,

    “basi twende wote”

    Wini na eva haoo wanaelekea Eden Church,… Ila nia ya eva ni kwenda kumuuliza adam kuhusu huyo mwanamke, mana adam hapo alipo haruhusiwi kuwa na mwanamke, na kam kuna mwanamke anatakiwa kufanya usafi kule kwa adam, basi anatakiwa adam asiwepo hapo ndani, labda awe dada yake au mama yake, lakini mwanamke tofauti na ndugu haruhusiwi kuingia kwa pasta adam afu awepo humo ndani, anatakiwa atoke na yule mwanamke akimaliza ampigie simu kuwa tayari na anaondoka.. Haitakiwi kabisa, sema mapasta wa sasa hivi ambao hawana wake wanaharibu sheria na miiko ya uchungaji



    Sasa huku kanisani,… Ah sasa hivi kanisa la mtumishi adam lina watu kiasi, tayari limeshaanza kuvuta waumini,… Mana mtumishi wa mungu anajulikana na mtumishi wa shetani anajulikana,… Ni wiki moja toka ajali ya ile nguzo kutokea, lakini waumini wameshaanza kusahau kilichotokea, mana dhumuni ni kuwapa wasiwasi juu ya kanisa hilo, ila mungu wa adam kaweka mkono katika kanisa hilo,.. Lilikuwa lina watu sio chini ya 50, n lenyewe lina uwezo wa kuingia watu 450 mpaka 500, na wote wanakaa vizuri, kwani kanisa lilikuwa ni kubwa mno….



    Adam mwenyewe akiwa mazabauni akilitangaza neno la Bwana kwa kondoo wake….

    “najua mpo mnaosumbuliwa na mapepo, mpo mnaosumbuliwa na ndoa zenu, mpo mnaochoka ingali hamkufanya kazi,.. Hayo ni mapepo na leo Unakwenda kuwa mwepesi zaidi ya karatasi… Haleluyaaaaa”

    “ameeeeeeeeee”

    Wakati huo eva na wini ndio wnaingia, Catherine alikuwepo hapo ndani, anapata maombi…

    “bwana yesu asifiwe sana”

    “ameeeeen”

    “baada ya mahubiri haya nitaomba tutengeneze kikundi ch kwaya… Tumsifu mungu kwa vipawa ambavyo kawapatia Haleluyaaaaaa”

    “ameeeen”

    Kiukweli kanisa la adam lilikuwa ni tamu sana, kwanza anajali muda wa kuingia kanisani, hii ni tofauti na baba yake anakuja muda anao utaka kanisani na akija haombi radhi kwa kichelewa,…



    Baada ya mahubiri kuisha pasta adam alikuwa na muda wa kupumzika…. Mama mchungaji alikuwa na gutu gutu moyoni mwake juu ya taarifa aliopewa….

    “tumsifu Yesu Kristo baba mtumishi”

    Alikuwa ni Eva huku akimsogelea mchungaji kwa heshima kubwa, wakati huo kanisani huko kwaya imepamba moto mana kanisa hilo lina kila aina ya chombo cha burudani kwa ajili ya kumsifu Yesu Kristo kwa njia ya nyimbo…

    “milele amina mama mchungaji”

    “baba mtumishi…. Jana usiku uliikuwa na nani”

    Eva hakutaka kukaa nalo rohoni alitaka kujua

    “jana usikuuuu… Yes, jana nilikuwa na dada Jessica, alikuwa akinipikia chakula cha jioni ia haikuwa usiku saana, ilikuwa kama saa mbili kasoro hivi… Kwani vipi”

    “aahhh nilihisi tu, mana kama niliota kuwa ulikuwa na mwanamke lakini sikuonyeshwa sura”

    “kuwa na amani mama mchungaji”



    Ilifika jioni sana, kila mmoja aliondoka zake, hata familia ya mr Jacob yote inasalia Eden Church,.. Wamemhama baba yao,… Wakati huo adam ana gari yake baada ya kuletwa na fundi nyumbani kwake,.. Ila Jessica kamganda kaka yake, anataka kujua kwanini adam yupo tofauti na baba yake kiuwezo, na ukiangalia baba yake ndio alitakiwa kumzidi adam yaani adam apite njia za baba yake lakini hapiti… Jessica alikwenda kwa kaka yake ili tu ajue nini kilitokea,….



    “we uoe tu bwana…”

    Aliongea Jessica huku akiingia jikoni kumpikia kaka yake,… Mana yeye ndio kajitolea kufanya usafi wa hii nyumba na pia pakiwa na uwezekano ampikie kabisa….

    “sufuria ikiendelea kuchemka nataka kujua utofauti wako wewe na baba”

    “mmmhhh kweli dada umedhamiria kujua duuu toka jana tu mi nilijua Umesahau”

    “hapana, unajua siku ile baba anatetemeka, nilikuwa na wasiwasi sana”

    “ahhhhh ni kweli dada Jessica,.. Mimi nipo tofauti na mr Jacob…. Kwasababu chuo cha Biblia alichonichagulia… Sikwenda huko”

    “ikawaje sasa”



    SASA ADAM ANATOA STORI ILIKUWAJE MPAKA AKAKATAA KUSOMA CHUO ALICHOSOMA BABA YAKE…. NA KUCHUKUA MAJUKUMU YAKE YEYE KAMA YEYE……



    “kwa sasa unaonekana una kipawa cha uchungaji mwanangu…. Mimi nataka nikupeleke chuo cha Biblia… Mana kanisa unalo lijenga linatakiwa kuwa na mchungaji muelewa”

    Aliongea mr jacob, wakati huo adam alikuwa akihudhuria vizuri katika makanisa ya baba yake, na waumini walikuwa wakimpenda sana,… Sasa baba kaamua kumtafutia chuo cha Biblia huko Nigeria….. Haikupita muda mrefu, adam aliondoka kwenda chuo na sasa akiwa juu ya ndege kuelekea nchini Nigeria kimasomo… Lakini kwenye siti aliokuwa kakaa alikuwa yupo na kijana mwenzie ambae ni lika lake…

    “habari yako ndugu”

    Alianza kusalimia adam kisha yule kijana akaitika

    “salama hali yako wewe”

    “namshukuru mungu…. Naitwa adam Jacob Michael”

    “ooohhh basi tumsifu yesu Kristo”

    “milele amina”

    “mimi naitwa Steven ayub”

    “ooohhh nice Name…. Haya safari ya wapi ndugu”

    Aliuliza adam huku wakionekana wote kuwa na furaha kwa kujuana kwao,…

    “nakwenda chuo cha Biblia kilichopo lagos Nigeria”

    “aaaahhh mbona hata mimi naelekea huko huko… Ashukuliwe bwana yesu, hata mimi nakwenda chuo cha Bibilia”

    “basi yesu atutangulie katika masomo yetu”

    “amen”

    Walipiga story nyingi sana hapo huku wakifurahia Safari yao ya kwenda katika chuo cha Biblia huko Nigeria..

    “mwenzangu wewe Unakwenda chuo gani”

    Aliuliza bwana Steven huku adam akijibu kwa kujigamba mana chuo anachokwenda kinasifika sana na kinalipiwa gharama kubwa sana juu ya masomo yake…

    “mimi nakwenda katika chuo anachomiliki atbishop jehova”

    Aliongea adam huku Steven akishtuka kuskia kuna binadamu anaitwa jehova,….

    “which name they called him (ni jina gani wamemuita huyo mtu)”

    Aliuliza Steven huku akishangaa sana kwa kusikia jina hilo ambalo adam alilitaja,

    “Heeeeeeee chuo kikubwa anachomiliki huyu bwana, yaani hakuna mfano”

    “sikiliza nikwambie mr adam… Sikujui hunijui… Kwanza kabisa hilo jina analoitwa huyo bwana ni makosa makubwa sana…. Jehova ni jina la Mungu… Hawezi kuitwa binadamu.. Afu pili hiki chuo nimekisikia sana, lakini siri ya hiki chuo ni kwamba… Hakitoi elimu ya Biblia bali unapewa nguvu za kuliongoza au kuyaongoza makanisa yako… Yaanii hapo hapo ni mwendo wa kishetani tu.. Hapo unakwenda kukabidhiwa mapepo ndugu yangu”

    Adam alishanaa kuskia hivyo kuwa anapokwenda sio sahihi, na kweli akifikiria hilo jina sio sahihi binadamu kuitwa jina la mungu….

    “wewe unakwenda chuo gani kwani”

    “mimi nakwenda katika chuo kinachomilikiwa na TB JOSHUA kiitwacho Jerusalem University Of Bible Studies”

    Adam kuskia hilo jina tu alikubali kweli Hicho ni chuo…..

    “duuuuu wanalipia kiasi gani”

    “Buuuure, ni wewe na imani yako tu”

    “waaacha bwana… Kwahio hakulipiwi kitu”

    “haswaaaaa”

    “shika mkono huu mr Steven”

    “una maana gani”

    “usiniache tafadhali, siko tayari kulitumikia jeshi la kishetani”

    “nipo pamoja nawe,… Na ukitaka kujua ni kweli… Basi mchunguze aliokuagiza kusoma pale, lazima nae amiliki shetani linalompa nguvu kila kuitwapo kesho”

    “basi yamekwisha hayo… Sasa ningeomba tukishuka Airport, nisindikize kwa mr jehova”

    “kufanya nini tena huko”

    “utajua tu”



    Baada ya masaa kadhaa wakiwa ndani ya nchi ya Nigeria mjini Lagos, walichukuwa tax iwapeleke mpaka katika chuo cha mr jehova…

    Adam alikuwa kachoka sana japo ni usafiri wa ndege,

    “we adam angalia usije kulala mana tunapokwenda unapajua mwenyewe”

    “silani nasinzia tu”

    ************************************



    Basi hapakuwa mbali sana, walifika katika chuo hicho, Walishuka na kutafuta jinsi ya kukutana na mkuu wa chuo hicho, ambae ni mr jehova,…. Kweli walifanikiwa kumpata mpaka ofisini kwake,… Wakati huo mr jehova nae keshapata taarifa toka kwa mr Jacob kuwa mtoto wake anakuja hapo hivyo awe beneti nae, ampe kila aina ya nguvu nae aweze kumiliki makanisa mengi na aweze kuaminika katika uongozi wake..

    “naitwa adam Jacob Michael…. Nmekuja katika chuo chako kwa maelekezo ya baba yangu”

    Sasa Steven anashangaa, mbona adam anajitambulisha sana, Steven aliona anaweza kushawishika kusomea hapo endapo ataendelea kukaa hapo,… Mana unaambiwa ukiingia hapo kutoka ni ngumu… Hivyo, Steven alianza kutia shaka juu ya hilo, na kweli kwa mtu mwenye imani utahisi nywele zako zinacheza cheza na ndivyo ilivyokuwa kwa Steven, mana yeye katoka kwenye familia yenye imani ya kweli, ina adam yeye katoka kwenye familia ambayo inaongozwa na mashetani japo hakuna anaejua hilo na ndio maana hapo hahisi kitu chochote kile

    “oooohhhh son of mr Jacob?, welcome to my university in Lagos (aahaaa ni mtoto wa bwana Jacob?, karibu kwenye chuo changu katika mji wa Lagos)”

    “Ahsante sana me jehova”

    Steven kuona adam keshaanza kukubali kusoma hapo, alianza kutoa mguu mmoja baada ya mwingine… Lakini ghafla mr jehova alicheka kisha akasema kuwa

    “hahahahahahahahhahah….. Kijana, umeshaingia hapa, kutoka sahau… Karibu katika chuo changu,… Mr adam Jacob kwanini unamwacha mwenzio nyuma..”

    Aliongea mr jehova tena kwa huruma kubwa kweli yan…

    Mara Steven karudi tena kwa furaha sana….

    “adam?.. Nimekubali kusoma na wewe hapa… Tutasoma wote, na baba yako kakuagiza chuo sahihi ni hapa”

    Aliongea Steven ambae alikiponda sana chuo hiki kuwa ni cha kishetani, lakini leo kakubali kusoma hapo pamoja na adam….

    “Steven, hayo ndio maamuzi ya kiume.. Hiki ndio chuo shihi”

    Aliongea adam huku Steven akitikisa kichwa kukubali

    “ndio… Nipo tayari tusome katika chuo cha mr jehova”

    Lakini wakiwa bado wamekaa hapo ofisini kwa mr jevova, mara bwana jevova akaagiza chakula…..

    “GUSTAVE DORÈ SATANÂS, lete chakula cha wageni”

    Adam na Steven wakaangaliana huku adam akimuuliza Steven

    “hilo jina vipi hilo… Mbona ni jina la Kigiriki, sehemu ya anguko la shetani”

    “wewe unauliza jina tu? Je hicho chakula kinacholetwa unakijua?”







    GUSTAVE DORÈ ni mji ambao alishukia shetani katika dunia hii, na hilo neno limetafsirika kwa Kingereza, lakini ukilikuta kwa lugha ya Kigiriki huezi kulijua…. SATANÂS ni kwa Kigiriki vile vile ambapo kwa Kingereza ni SATAN lakini kwa Kigiriki limeongezeka maneno kwa mbele na sio maneno tu bali kuna vikofia kwa juu kama unavyoona, na pia SATANÂS ni kwa Kigiriki… Alafu SÂTANAS ni kwa Kilatini, tofauti ya herufi hizo ni hivyo vikofia vya juu katika herufi za (A).. Hio ndio tofauti ya Kigiriki na kilatini… Wenzangu wa historia najua mtaanza kubisha hapo



    Sasa adam yeye anajua hilo jina, hivyo alipo lisikia ndipo akamtaarifu Steven kuwa analijua hilo jina, na Steven nae akamuuliza, we unauliza jina je unajua chakula kinacholetwa? Wote wakawa wametulia kimya kusubiri chakula kinacholetwa,… Kweli huyo Gustave Dore Satanas alikuja na sinia la chakula lakini walifunika kwa juu hivyo hujui chakula kinacholetwa…

    “karibuni waheshimiwa”

    Gustave aliwakaribisha akina adam kisha akaondoka,.. Adam akashangaa na mwalimu jehova nae akaondoka,…

    “mbona wameondoka”

    Aliuliza adam huku akifunua kile chakula

    “mi sijui”

    Alijibu Steven wakati huo hawana wasiwasi sana mana ndio tayari wameshafika chuoni…

    Sasa adam alipofunua.. Alishtuka huku akisema kuwa

    “Steven, huu si mkono wa mtoto huu”

    Steven nae katoa macho huku akisema…

    “tena havijapikwa bado vibichi”

    *************************************



    “oya… Oya adam, nilikwambia usilale ona sasa umelala”

    Alikuwa ni Steven akimuamsha adam

    “aaahhh Steven… Kwa mr jehova hapafai”

    Aliongea adam huku akifikicha macho yake, kana kwamba alikuwa usingizini….

    “kwanini hapafai”

    “nimeota tumepewa mkono wa mtoto eti kama chakula”

    Kumbe adam alikuwa anaota na hapo bado hawajafika kwa mr jehova, mmiliki wa chuo kinachosadikika ni cha kupatia nguvu za kishetani ili unapokwenda ufanikiwe, haswa haswa baadhi ya viongozi wa dini hupendelea sana ufahari huu….

    “mimi nilikwambia usilale, tupo kwenye miji ya watu hii”

    “Steven? Kuna jamaa anaitwa Gustave pale kwa mr jehova”

    “nani kakwambia bwana wewe”

    “nimeota”

    “izo ndoto bwana, we twende ukamalize mambo yako tuondoke, mr jehova hana chuo cha kutufundisha sisi”



    Haikuchukuwa muda mrefu walifika, wakamfanyia malipo dereva wa tax kisha wakaingia… Lakini adam aliingia mithili ya mtu anaepafahamu mahali hapo na wala hajawahi kufika kabla…

    “we adam Unakwenda wapi huko”

    “ww twende tu”

    Sasa Steven akajua labda mwenzie anataka kumpoteza nae akajikuta asome katika chuo hicho mana adam yeye kaelekezwa kusoma katika chuo kinachomilikiwa na atbishop jehova, mmiliki wa makanisa yote Afrika ambayo yanaendana na imani yake.. Sio makanisa yote Afrika, bali makanisa yote Afrika yanayoendana na imani yake ya kishetani, hivyo kama nchi fulani kuna kanisa na pasta anatumia nguvu za giza basi huyu jamaa ndio mfuasi mkuu…

    “adam,… Kumbuka tulielewana nini tukiwa katika ndege”

    Aliongea Steven huku adam akiendelea kwenda tu…. Lakini sasa cha ajabu, adam alinyooka moja kwa moja mpaka ofisini kwa mr jehova, yaani utafikiri kaja siku zilizopita..

    “adam rudi huko”

    Aliongea Steven huku akimfuata lakini kwa taratibu sana,.. Yaani adam hajakosea mpaka kaingia ndani

    “natumai wewe ndio mr jehova, mmiliki wa chuo hiki”

    “ndio, na karibu sana katika chuo changu”

    Adam akakutana na makaribisho yale yale alio yaota,..

    “sina muda wa kukaa…. Mimi ni kijana wa mr Jacob, nimeagizwa kufika hapa juu ya elimu nitakayo ipata hapa kwako…. Lakini nasikitika ya kwamba, sihitaji kusoma kwanza nahitaji kula raha za mji wa Lagos..”

    Adam aliongea vitu mpaka Steven akashangaa, ina maana adam kaja Lagos kustarehe tu,… Lakini kabla hajapata jibu adam alitoa vitita vitano vya pesa vikubwa… Kisha akaviweka mezani,…

    “hizi ni dola za kimarekani shilingi milioni hamsini (50 milioni) ambazo ni malipo ya elimu ambayo nitaisoma hapa kwako, lakini sintoanza kwa sasa… Mpaka nitakaporudi kwenye raha zangu,… Nakulipa kabisa peza zako… Ila simu itakapo pigwa na mr jacob,.. Jibu lake ni moja tu… KIJANA WAKO KUFIKA NA ANAENDELEA VIZURI… nafikiri tumeelewana mr jehova”

    Mr jehova alicheka sana kicheko cha ajabu kisha akaburuza zile pesa katika upande wake..

    “umeeleweka…. Ila utaingia lini chuoni”

    “nitakujulisha, ila nitakula raha miezi kadhaa kabla ya kufika hapa”

    “nitafanya hivyo, ila hakikisha unakuja, mana pesa hii haina thamani zaidi ya elimu ulioifuata”

    “sawa”

    Adam alipiga hatua moja kisha akageuka tena…

    “zingatia sana simu itakapo pigwa na mr Jacob”

    “ondoa shaka”

    Adam na Steven waliondoka zao… Ikumbukwe kuwa mr jehova ndio mmiliki wa chuo hicho, lakini yeye pia anamilikiwa na watu wengine, yaani nae ana wakubwa wake, sasa mr jehova ni kama mkuu au aliemikishwa chuo hiko ila wapo watu nyuma yake… Kwahio hata yeye pia anatafuta pesa hivyo haoni haja ya kuziacha pesa hizo…. Lakini wakati akina adam wanamalizia kutoka,… Jehova aliita…

    “GUSTAVE DORÈ SATANÂS….”

    “yes mkuu”

    Steven alisikia hilo jina, lakini kabla ya kulisikia hapo alisha ambiwa na adam kuwa yupo mtu anaitwa Gustave kule kwa mr jehova, Steven akabisha, sasa kalisikia kweli jina lipo

    “fuatilia hawa vijana wanaelekea wapi”

    Aliongea mr jehova huku Gustave Dore akifuata nyuma, wakati huo akina adam walishachukuwa tax inayo wapeleka katika chuo sahihi na chenye imani…. Lakini mpaka hapo inagundulika kuwa adam ana maono..





    “ivi adam, kwanini ulisema umekuja kwenye starehe”

    Steven aliuliza huku wakiwa safarini kuelekea huko Jerusalem University Of Bible Studies, chuo kikuu cha Bibilia Afrika nzima, sasa mkuu wa chuo hicho nae ndio atbishop wa mabishop wote Afrika wenye imani kama yake.. Ni TB JOSHUA…

    “najua ile ni sehemu ya kishetani.. Na ni ujanja ambao nimeutumia ili asijue kuwa nakwenda kusomea katika chuo kingine,… Na hua mashetani hupenda mambo ya starehe hivyo nilipoongea hivyo lazima achukulie moja kwa moja kuwa lazima niwe mfuasi wao”

    Alijibu adam bila kujua kuwa wanafuatiliwa nyuma na gari ya mr Gustave Dore,.. Jamaa mwenye jina la mji alioshukia shetani…

    “ok alafu kingine ulijuaje kuwa mr jehova yupo chumba kile”

    “kwani wakati nikiwa katika gari si nilikwambia nimeota tupo na mr jehova, na tukapewa mikono ya watoto kama chakula cha wageni…”

    “halafu pia jina ulioniambia nimeliskia likitaamkwa”



    Walifika katika chuo hicho, ambacho ni sahihi kwa masomo ya Biblia,… Hapa ndio mapasta wote hutokea, kuacha pale kwa mr jehova,.. Sasa bwana Gustave ndio anaona vijana wanapoingilia, hili swala hakuna anaejua kuwa wanafuatiliwa,… Hapo mr Gustave akarudi na kumwambia mr jehova kuwa vijana wameingia Jerusalem university….. Jehova hakusema kitu bali alishajua kiwa vijana wamejua hicho sio chuo cha uokovu, bali ni chuo cha maangamizi juu ya waumini



    Ndani walipokelewa na wahudumu wa chuo hicho,.. Kila wanapopita ni maneno ya Yesu kila mahala… Salamu na sifa kwa yesu hapo ndipo mahala pake,… Sasa Steven aliongoza moja kwa moja mpaka kwa mr Joshua,… Sasa kumbe baba yake Steven na mr Joshua wanafahamiana, hivyo kafika pale na kujitambulisha ila hakusita kumtambulisha adam… Steven aliongea yote jinsi alivyo kutana na adam mpaka kufika kwa jehova, mpaka kuja hapa… Mr Joshua alifurahi kwa kitendo cha adam kubadili mwelekeo wa kuifikia ndoto yake,… Lakini sasa kutokana na stori ya adam ilivyo,.. Mr Joshua alimtaka adam awe nae… Yaani mafunzo na elimu yote atafundishwa na mr Joshua,… Sasa tafakari wenzie akina adam wawepo darasani afu adam awe na mr Joshua,.. Ni sawa na uwe na urafiki na Head Master ahuleni alafu ufeli… Ni kwa ujinga wako…



    Baada ya mwaka mmoja kuisha adam akiwa keshamaliza masomo yake ya Biblia…. Alikuwa akisindikizwa na mr joshua ambae ndie alikuwa mwalimu wake yeye kama yeye, yaani alipewa ofa ya kipekee kua karibu na atbishop wa wa Afrika nzima… Tena ndie aliekupa elimu na mafunzo yote….

    “nakupongeza sana kijana… Mumgu akutangulie kwa kila utakacho kijaribu”

    Aliongea bwana joshua huku wakielekea Airport kwa ajili ya safari, na hapo yupo na rafiki ya Steven, wamekuja wote na wanaondoka wote

    “Ahsante sana bwana mchungaji”

    “natumai nitakuja Tanzania… Nahitaji uwe mwenyeji wangu… Kitendo cha kuachana na njia ya kishetani na kuja katika njia ya haki… Ni jambo jema sana, hukujua tu”

    “Yesu akuongoze katika safari yako ya kuja Tanzania”

    “lazima nitakuja hivi karibu… Nataka tuyatakase makanisa ya nchi yako.. Wachungaji walio katika imani potofu, tuwaponye na kuwatakasa kwa damu ya Yesu”

    “aaaameeeen”

    “basi nawatakia safari njema, na mfanya yalio mema…. Na Haruhusiwi kumkufuru mtu alio tofauti na dini yako… Weka kipaumbele swala hilo”

    “ameen, nitalifanyia kazi”

    Adam na Steven walipanda ndege tena kurudi nchini Tanzania



    HAPA NDIO MWISHO WA HISTORIA YA ADAM ALIPOKUWA NIGERIA KIMASOMO YA BIBLIA…



    “hivyo ndivyo ilivyokuwa dada… Na ndio mana mpaka sasa nipo tofauti na mzee”

    Ikumbukwe kuwa alikuwa anamsimulia dada yake jinsi ilivyokuwa mpaka kawa tofauti na baba yake,…

    “uuuufyuuuuuu…. Pole sana kaka angu,.. Ila nakupa pongezi sana juu ya hili, na yesu atakuongoza”

    “Ahsante sana”

    “nimechoka sana, wacha niende nyumbani mtumishi”

    Aliongea Jessica huku akinyanyuka na kuelekea nje, na wakati huo alikuwa akipewa stori huku akipika..



    Baada ya mwezi mmoja kupita…. EDEN CHURCH sio ile ya mwanzo, yaani kwa sasa ina watu wengi hata kuwahesabu huwezi,.. Ikiwa ni siku ya Jumapili adam akiwa ndani ya kanisa hilo anawahubiria kondoo wakw, lakini huezi amini mr Jacob yupo nje ya kanisa hilo… Yaani kaacha kuhubiri kanisani kwake yupo nje ya kanisa la mtoto wake, akiwa anakuna kichwa, haamini kama mtoto wake kamchukulia waumini wengi sana tena sio wa kanisa moja, karibia makanisa yake yote kwa sasa yamepunguza waumini kutokana na kanisa la mtoto wake,…. Simu sikioni

    “hallo mr jehova… Hali yako”

    Mr Jacob alimpigia mr jehova mana ndio suluhisho lake juu ya mtoto wake

    “hallo mr jacob Michael, hali yangu nzuri”

    “bwana weee, hapa nipo nje ya kanisa la kijana wangu… Yaani huezi amin makanisa yangu yamepungua waumini, siwezi kuamini kwamba nilikuwa siwezi kuwahesabu waumini wangu, lakini sasa naweza kuwahesabu… Siamini kuwa wanahamia kwa adam taratibu”

    “sasa watakaje wewe”

    “enheeeeeee, hilo ndio swali zuri kwangu…. Niambie sasa nifanye nini”

    “mtu mwenye upako wa kweli, kiukweli sisi hatumuezi…. Ila ipo njia moja tu na ndio itakayomwangusha mtoto wako”

    Aliongea jehova huku jacob akishangaa

    “njia moja tu… Na ndio ya pekee”

    “yes…. Hebu niambie… Mtoto wako kaoa?”

    Mr jehova aliuliza kuwa adam kaoa

    “hapana, bado hajaoa”

    “yeeeeees….. Hio ndio njia pekee iliobaki, na ikishindikana hio, basi mwache amtumikie mungu wake”









     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog