Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE ISLAMIC WIFE - 3

 

     

     



     

    Chombezo : The Islamic Wife

    Sehemu Ya Tatu (3)

     

    Sasa huku kwa zena... Alikuwa kakaa akifikiria yale maneno ya rahim...

    "ina maana jana rahim kuna mwanamke alikuwa nae?... Lakini mbona jana ilikuwa ni usiku sana, sasa alikutana na nani"

    Zena alikuwa hapati jibu juu ya mtu wake, yaani unaambiwa zena hakuwahi hata kumpenda wala kutamani ndoa kwa wale wana madrasa wenzake, yaani hata wale Waislamu wenzie, hakuwahi kuhisi kuwa nao hata siku moja... Lakini automatically tu kajikuta kampenda rahim, na rahim mwenyewe ndio huyu, mhuni wa kupitiliza

    "lakini... Nani kakutana nae muda ule.... Ooohhhhh yes.... Nina wasiwasi na fadhila, mana fadhila nilikutana nae anakwenda dukani"

    Zena alikuwa akijiongelesha mwenyewe, ili kujiuliza nani kakutana na rahim, na zena anajua kweli jana rahim alilewa sana,..

    "kwanini fadhila ananifanyia hivi"

    Aliongea zena tena wakati huo michozi ilikuwa ikimshuka mfululizo,.. Ghafla mama yake huyo, kamkuta mtoto wake analia

    "we zena kulikoni tena"

    "mama... Fadhila naona ananiingilia sasa"

    "fadhila yupi tena? Au Fadhila huyu huyu rafiki yako"

    "ndio Mama"

    "haya... Kunani tena... Au Usikute kapoteza ule mswaafu wako"

    "wala tu...."

    "sasa nini"

    "jana kaenda na rahim kwao"

    Mama kuskia jina la rahim, akahisi kama vile hajasikia vizuri...

    "unasemaje"

    "mamaaa.... Jana kaenda na rahim kwao"

    "ivi mwanangu,.. Ni kweli unampenda yule kijana?...mimi siamini kama zena wangu ni yule wa zamani"

    "mama... Baba atasikia"

    Mama anajua uchungu wa kupenda na anajua mtu akipenda anakuwaje...

    Lakini mpaka hapo mama hajaelewa maana ya fadhila kwenda na rahim nyumbani kwao... Hakujua maana ya hayo maneno

    "sikia zena. baba yako aliniambia zena umekuwa wa ajabu sana siku hizi... Unampenda mtu asiokuwa na dini"

    "mamaaa....lakini yule ni binaadamu na anaweza kubadilika"

    "kwa yule kijana... Haiwezekani... Yule Kaharibiwa na pesa zao"

    "mamaaaa... Mniruhusu tu basi.. Lazima akae sawa"

    "heeeeee baba yako akisikia atakutoa roho"

    "najua mama... Lakini kwanini usiongee nae"

    "weeeeeeeeee si unajua baba yako alivyo mkali"



    Sasa wakiwa wanaendelea kuongea mara fadhila katokea,... Alikuwa anafurahia kumwona zena, lakini hajui kuwa zena keshajua kuwa yeye ndie alilala na rahim jana usiku,..

    "zena si huyo hapo"

    Aliongea mama yake zena huku akiamka na kwenda zake jikoni,.. Mama zena hakutaka kusikiliza mambo ya watoto wa kike hao..

    "As Salaam Aleykum zena wangu"

    Alisalimia fadhila huku akikaa kitako ili wapige story, lakini zena hakuitikia wala nini,... Tena kamkazia macho ile. Mbaya

    "heeeee zena toka lini ukaninyamazia jamani zena"

    Zena alianza kulia, yaani uyu mtoto zake ni kulia tu hana maongezi mengi

    "heeeee mbona unalia zena??... Lakini mimi sikuwa na rahim wako siku nzima"

    "kwani nimekuuliza??"

    "amna zena.. Nimeona tu umenuna"

    "sasa umejuaje kama nimenuna kwa ulivyokwenda na rahim kwenu..."

    "heeeeeee zenaaaa....rahim si shemeji yangu kabisa yule"







    Zena alipomwona fadhila alikasirika sana, tena sana... Na fadhila asijue hili wala lile, kaja mpaka ndani dukani kakaa bila kujua zena ana hasira nae ile mbaya...

    Zena alimsalimia zena lakini zena alikaa kimya, fadhila hakukata tamaa mana anakijua alichokifanya kwa rahim, hivyo anajua kununa kote huko ni kwasababu ya rahim



    "kwani nimekuuliza??"

    "amna zena.. Nimeona tu umenuna"

    "sasa umejuaje kama nimenuna kwa ulivyokwenda na rahim kwenu..."

    "heeeeeee zenaaaa....rahim si shemeji yangu kabisa yule"



    Aliongea fadhila huku akitabasamu vizuri tu...

    "shemeji yako kwa nani?"

    "heeeeee yamekuwa hayo tena"

    "yaani uwe nae wewe usiku kucha leo uje uniambie si shemeji yanguuu.. Nyooo muone vile"

    "zenaaaa, kwani mimi nimefanyaje lakini"

    "hujui eee... Nakuuliza hujui ulichokifanya jana mpaka saa saba za usiku"

    "nilichokifanya jana?... Nilifanya nini"

    "fadhila... Usinifanye mimi ni mtoto mdogo.. Kwanini jana umeenda na rahim kwenu na ukakaa nae mpaka saa saba usiku"

    "haaaaaaaa zeeeena, yaani mimi nikakae na rahim mpaka saa saba"

    "fadhila... Mimi sio mtoto mdogo... Rahim kaja hapa na kuanza kunisifia mambo ya jana... Na wewe jana nilipishana na wewe unakwenda dukani, na kama ungerudi mapema basi ungenikuta pale kwenye myi, mana nilikuwa namsubiria rahim"

    "hapana zena... Unavyofanya sivyo.. Mimi jana nilienda kwa kaka juma, na sikurudi mimi nililala kule kule"

    "muongo fadhila.. We muongo"

    "kweli vile... Unanihukumu bure tu... Halafu huyo rahim kakuambia saa ngapi"

    "si muda huu huu tu"

    "mbona mimi nimekutana nae hapo kalewa, japo sio sana lakini kama kalewa"

    Sasa zena akakumbuka kuwa, rahim akiwa hajalewa hua haongeagi mbele ya mtu ampendae,.. Anakuwa kimya, hivyo kwakuwa kaambiwa kalewa kidogo, basi huenda ilikuwa ni pombe zake tu.. Mana mlevi hanaga neno zuri pale anapokuwa chakali.....

    "ina mana umekutana nae kalewa"

    "ndio... Tena ilibaki kidogo tu ani dondokee"

    "jamani rahim... Sasa jana alikuwa na nani jamani"

    "we muulize vizuri... Atakuambia"

    "ngoja jioni nikutane nae, nitamuuliza"

    Basi zena na fadhila wakawa wamesha sameheana na urafiki unaendelea kama kawaida







     





    Huku kwa rahim, maskini ya mungu hajanywa hata tone la pombe siku hii ya leo, lakini fadhila kasema karibia adondokewe na rahim... Wakati huo rahim yupo zake nyumbani anaangalia mpira, mana naye ni mpenzi wa mpira kama kaka yake jamali,... Ikiwa inakwenda time ya saa tisa hivi, mpaka hapo rahim bado hajagusa, kitu na siku haitopita bila kugusa lakini ana muda wake,...



    Walikaa hapo mpaka mpira ukaisha, rahim alitoka zake kwenda kwenye viwanja vya mpira, tena kaenda kwa miguu tu, hapendagi kutumia gari mara kwa mara,... Alipotoka hapo ni mida ya jioni sana, basi akawa anatembea zake taratibu kurudi nyumbani, lakini papo hapo akapigiwa simu na kaka yake

    "haloo broo vp"

    "poa upo wapi"

    "aahhh natoka mpirani huku"

    "njooo hapa gaden baa... Zile wiski zako ndio zimeingia sasa hivi"

    Sasa kumbe rahim kukaa kote huko mchana zilikuwa zimeisha ndani mana wana tabia ya kuweka ndani, sasa kapigiwa simu huko gaden baa ndio zimekuja... Rahim alitoka mbio kuelekea gaden baa ili kutoa loku, wenyewe wanaita hivyo,...



    Wakati huo kagiza ndio kanaingia, kule kwa jamali ndio anapata unywaji tena wakati huo alikuwa kazungukwa na watoto wa kitanga nguo zao sasa mmmhhhh... Havisemeki, basi ilikuwa ni burudani kwa kwenda mbele,...

    "mambo mkaka"

    Alisalimia dada mmoja huku jamali akiendelea kukandamiza kinywaji cha gharama kubwa,

    "poa niambie mdada"

    "safi ti.. Vp upo peke yako leo, mbona simuoni yule mkaka mwingine"

    "ah yule... Yule anakuja... Sasa hivi utamwona, mana kinywaji chake kimekuja sasa hivi"

    Mara ghafla kamekuja kaschana kengine kadogo dogo hivi kazuri sana,

    "we rukiya... Usikute unakataka kale kakijana kadogo"

    "nani.. Yule ni saizi yako sio mimi...eti mkaka, mi naendana na wewe au yule"

    Kiukweli wasichana walikuwa wakijigonga sana kwa akina jamali,..

    "basi mimi namsubiri yule mdogo mdogo"

    Kaliongea kale kaschana kadogo kuwa yeye anamsubiri rahim... Basi yule rukiya akawa anakunywa pombe na jamali,... Baada ya dakika kadhaa, Rukiya alielekea chooni... Lakini sasa kumbe rukiya na na kale kasichana hawakuwa watu wazuri, kumbe kule chooni kuna mjidude ya wanaume haswa...

    "we broka.... Kasema dogo lake linakuja"

    Aliongea rukiya, huku ile minjemba inatoka katika uchochoro wa chooni ili ikae tayari,

    "lakini nyie mna uhakika ni watoto wa tajiri"

    "aahhh... Yaani kwao pesa godoro"

    "acheni utani nyie"

    "si ndio tunawaambia sasa... Wanakujaga hapa kila siku, na hawajawahi kununua bia za elfu mbili mbili... Wao wanakunywaga wine, wiski zile.. Mambo ya amarula midompo, angel wine,... Yaani wanahakikisha laki mbili imeisha kila siku"

    "nyieeeee"

    "aahhh sasa huyo. Anaekuja ndio balaa, ni Mdogo lakini anazimwaga... Waleti yake yenyewe imevimba namna hii"

    Jamali wakati huo hajui hili wala lile,. Ghafla anashikwa na haja ndogo akawa anaelekea chooni... Masikini wa mungu kule anakoelekea sio kazuri kabisaa.....

    "enheee... Huyo anakuja Jiandaeni"

    "amna... Huyu hafai kukaba peke yake, sisi tunamtaka huyo aliemuita, mana huyo pesa zake zitakuwa bado hazijaguswa"

    "lakini bonge.. Yule pia ana kiburungutu namna hii"

    "amna.. Yumsubiri huyo... Mana tukianza na huyu afu tikimwachia atamtaarifu huyo asijec

    "ok... Hapo nimekusoma mkubwa... Watoto wa mafisadi wanakula nchi yetu tu"



    Wakati huo huku kwa rahim sasa, anakimbia mno, ili kuwahi kutoa loku, na hapo alipo ana hamu na kinywaji ile mbaya,.. Mana toka asubuhi hajagusa hata kidogo..... Sasa mungu sio asumani, saa ngapi hajakutana na zena...

    "heeeeeeee haya kukimbia kote huko waenda wapi wewe"

    Zena alimuuliza rahim, mana rahim alikuwa spidi na anahema mno...

    "kuna mtu namuwahi hapo njiani"

    Rahim alipomaliza tu kujibu, akapiga hatua ya kukimbia kuelekea baa alipoitwa,...

    "hebu wewe, mbona hunisikilizi"

    "zena... Tutakutana kesho"

    Wakati huo rahim kakabwa kooni yaani anataka wiski tu...

    "ebu ngoja kwanza... Huyo mtu unaemkimbilia ni mwanamke au mwanaume"

    "mwanaume"

    "rahim?"

    Zena alimwita rahim na rahim bila hiana aliitikia

    "ebu fanya haaa"

    "mi sijanywa bwana alaaaaa"

    "we fanya tu"

    "zena... Nimeacha kunywa mimi, kweli vile sasa hivi sinywi na kuna mgeni namuwahi hapo njiani"

    "fanya haaaa"

    "ina maana huniamini au? ..... Haya Haaa"

    Rahim alifanya kama alivyoambiwa, zena alifurahi sana mana rahim siku hio yote hakugusa kitu,... Sasa hapo rahim alikuwa kama anapotezewa muda..

    "siku ya leo nimeipenda sana... "

    Aliongea zena huku akimshika rahim mkono wake, kana kwamba kufurahia kitendo cha rahim kutolewa siku yote hii...

    "haya niachie basi nimuwahi mgeni asije kupotea njia"







    Rahim alikuwa kashikika haswa, yaani chukulia kama wewe unapokuwa unahisi kiu, yaani unajikuta unasema kuwa ukipata maji utayanywa kwelikweli,.. Sasa ndio hivi vya rahim, kashikika mbaya afu jinsi anavyomheshim zena, huezi amini ndie aliekuwa akimchelewesha, zena alimtaka rahim afanye haa, ili ajue kama kanywa au laa mana sana sana unywaji wake ni wa jioni, na kama zipo nfani basi hata mchana anaweza kunywa, lakini stoku ya ndani imekwisha, na sasa wanazifuata katika mabaa makubwa makubwa,...

    "siku ya leo nimeipenda sana..."

    Aliongea zena baada ya kumnusa na kugundua leo hajalewa

    "haya niachie basi nimuwahi mgeni asije kupotea njia"

    Rahim aliongea huku akiwa kashikwa mkono wake,... Zena alifurahi sana kugundua kuwa leo rahim hajatupia vitu vyake,.. Hata kumkumbatia alimkumbatia bila wasiwasi... Rahim haamini kama leo kakumbatiwa na zena,.. Yaani zena anampenda kupitiliza, sema sasa kinacho mkwamisha zena ni tabia za rahim kuwa mbaya, kalelewa vibaya mno..

    "kwani unakwenda wapi ram"

    "kuna mgeni kashushwa hapo mbele sasa namuwahi"

    "kwani huku kuna stendi ya mabasi"

    "alipitilizwa na basi, hivyo kanipigia simu yupo hapo mbele"

    "ok.... Sawa ila usiende kufanya mambo yako ram"

    "mimi nimeacha kunywa... We niachie niende"

    Zena alimwachia rahim aende, rahim kuachiwa alichomoka mbio,..

    Lakini rahim alipokuwa anaanza kukimbia, zena alisisimkwa na nywele, kana kwamba kuna kitu hakiendi sawa... Unajua ukiwa unampenda mtu kweli kutoka moyoni, basi kuna ishara nyingi sana utaziona na huezi jua kama zinamhusu umpendae lakini ishara zitakuwepo tu,.. Sasa zena alipopata ishara kama hio, alimwita tena rahim







     





    "rahim... We rahim wewe"

    Alipaza sauti mpaka ram akasikia na kusimama, lakini alikuwa kakasirika mno, yaani atajikuta anamchukia zena,...

    "nini tena jamani"

    "ningoje hapo hapo... "

    Rahim alikubali kusubiri lakini hatulii kabisa yani, wakati huo tamaa ya wiski ndio inapamba moto...

    "kuna nini tena zena"

    "unakwenda wapi?...niambie ukweli"

    "naenda kwa mgeni"

    Zena aliingiza mkono mfukoni kisha akatoa ule mpochi uliojaa miburungutu ya pesa... Akawa anachambua pesa ndogo ndogo,

    "sasa kama ni hela si ungesema tu nikupe.... Aisee zena unanichelewesha eti"

    "nina wasiwasi unakwenda kwenye nanii wewe"

    Zena alitafuta pesa ndogo lakini akawa hajapata, mana rahim katoka benki muda aio mrefu, hivyo pesa iliopo hapo ni elfu kumi kumi tu...

    "hamna bwana mi naenda kumpokea mtu"

    "sasa akia... Wewe nenda, hii Pochi utaikuta nyumbani kwetu"

    "unasemaje we zena"

    "rahim... Mimi sitaki unywe pombe, na kama unanipenda mimi, kuanzia leo staki kusikia ulevi juu yako..."

    Zena aliongea hivyo kisha akaondoka na ile pochi ya rahim,...

    "zena?... unajua utani mwingine tutakuja kuuwana hivi hivi eti"

    Zena alikuwa hana utani wala nini, tena aliihifadhi ndani kabisa huku kwenye kipochi chake ambacho kawekea miswahafu yake huko...

    "zena?... We zena.... Jamani baby"

    Rahim alijaribu hata kuita baby ili hata zena ageuke lakini wapi, zena alikuwa anakata barabara utafikiri hana akili nzuri,...

    "sasa nauli ya kuja nao hao wageni nitatoa wapi"

    Kwa maneno hayo yalimfanya zena asimame....

    "shida ni nauli tu?"

    "ahahahaha ndio, nauli tu"

    Rahim alifurahi mana pochi inarudi mfukoni kwake....

    "shika hii hapa... "

    Rahim alitoa macho,... Kama vile haamini kwa pesa aliopewa, yaani ana muda hajui kushika pesa ndogo kiasi hicho

    "mbona umenipa elfu mbili sasa... Mi napandaga... VX"

    "toka rahim wewe? Hebu mwogope mungu... Toka lini VX ikawa gari ya abiria?"

    Zena alimuuliza huku akisubiria jibu

    "lakini si udigitali huu... Nipe pochi langu bwana"

    "sikiliza... Hii pochi nitakupa keshooo"

    Zena hakuwa na utani... Lakini ghafla simu ya rahim iliita

    "haloo broo"

    "dogo vp, unazingua ujue."

    "aaahhh broo, naenda benki kutoa pesa"

    "achana na hizo pesa... We njoo mimi ninazo za kutosha"

    "Eti eee... Aina noma broo"

    Sasa zena akahisi kuna msaada rahim aliupata,...

    Basi simu ilikata kisha rahim akamwambia zena

    "nipe basi kadi zangu za benki"

    "yaani hapa hupati kitu"

    "eee... Haya basi mama nenda"

    Rahim alitoka mbio, yaani kwenye pochi kaacha kama laki 7 au 8 na hio ni pesa taslimu, bado kwenye hizo kadi za benki zimejaa zote humo ndani, si unajua pochi za matajiri hua zinavimba tu, sio hio yako ikijaa sana ujue ina laki tatu...

    Zena alihisi labda kafeli, mana alitegemea rahim hatokwenda kabisa, lakini kaenda... Ghafla fadhila nae huyo, wakati huo rahim keshatembea saa mingi sana...



    Sasa huku baa, wale majambazi wamesikia jamali akiongea na simu kuwa rahimu aje tu, hata kama hana pesa, wakaona huo ni ujinga, kuliko waje wawe wengi afu hawana faida bora wamkabe huyu huyu,... Alimfuata dada mmoja aitwaye rukiya,..

    "jamali mpenzi... Nisindikize chooni, mi Naogopa"

    Jamali ni mwanaume anaejiamini sana, hivyo hakuwa na shaka kwa hilo



    Sasa huku kwa zena... Aliokuwa akishangaa tu rahim alivyomkosa kumrudisha na alijua lazima akalewe hakukuwa na cha mgeni wala ninj, zena aliotea kweli...

    "heeee zena, toka saa zote bado hujafika nyumbani"

    Aliuliza fadhila huku akimshangaa zena kwa kutofika nyumbani mpaka saa hizi,...

    "fadhila... Saa ngapi nisikutane na ram hapa.. Kukuru kukuru.. Sijui alikuwa anakwenda wapi"

    Aliongea zena huku wakitembea kuelekea nyumbani,..

    "heeeee mwenzangu na huyo ram wako, mmmhh... Kweli siamini zena kama kweli umempenda sharobaro kama yule"

    "fadhila... Yale ni mavazi ya kidunia tu, shida yangu aache pombe tu basi"

    "aah wapi... Kwa rahim ni ngumu... Rahim kuacha pombe, hilo sahau zena"

    "mi nakwambia lazima aache"

    "sasa utawezaje kumkontroo mtu na pesa zake zena"

    "heeeeeeee.... Mbona sasa hivi nimemnyang'anya pesa zake zote"

    "Whaaaat... Unasema umefanyeje"

    "Mpochi wake wake huu hapa... Nimempa elfu mbili tu, tena nilikuwa nayo mimi, mana nimetafuta hela ndogo hapa sioni, nimempa elfu mbili tu"

    Zena aliongea hayo huku akimwonyesha fadhila ule mpochi wa hela,.. Na fadhila anaujua huo mpochi mana kuna siku aliufungua na kutoa pesa ya bajaji,... Hivyo sio mgeni nao

    "we zena wewe una dhambi jamani"

    Fadhila aliongea hivyo huku akiwa kashika kiuno na kumshangaa zena kwa kile alichokifanya....

    "fadhila naomba uniache na dhambi zangu.... Rahim nampenda sana, na sijui ni kwanini.. Sijatokea kumpenda kijana yeyote yule hata awe katoka Uarabuni... hata awe anajua Qur-aan kama mtume.. Sijawahi kupenda... Lakini nimeshangaa nampenda mtu kama huyu... Fadhila we niache tu niuruhu moyo wangu uende unapotaka, hata kama wazazi wangu hawataki, lakini nitajitahidi mpaka wamtake"

    "heeeeeeeee zena"

    "kweli fadhila,... Nipo tayari kwa lolote.. Lakini nihakikishe rahim anakuwa sawa"

    Fadhila akisikia hivyo ndio anazidi kuumia mana hata yeye anampenda sana rahim, na yeye haoni haja ya kumfanya rahim aache kunywa kikubwa wapendane tu...

    "lakini zena rahim kakupendi hata kidogo.. Yule anataka kukuchezea tu"

    Fadhila aliongea hivyo ili kumkatisha zena tamaa

    "fadhila... Una maana gani kusema hivyo"

    "yule bishoo tu, wala haendani na wewe... Mtu hamjui mungu hajui hata neno moja la Qur-aan, eti unampenda.. Utajidhalilisha bure rafiki yangu"

    "fadhila, hebu twende kila mtu kwao mi staki kuongea sana... Mana hunielewi"

    Zena alikuwa hataki kusikia lolote lile kutoka kwa fadhila...



    Sasa huku kwa rahim, alikimbia mpaka kachoka, na hua hapendelei kupanda gari, na ndio mwili wake ni kimbaumbau siku zote,... Alikuwa anatembea taratibu tu, mana ilikuwa kama mida ya saa mbili usiku... Na hapo kurudi ni saa 6 usiku... Lakini sasa alipokuwa anapiga hatua, ghafla alijikwaa, kana kwamba kuna kigogo kilikuwa njiani,.. Alijiangalia hajaumia kisha akaamka, lakini sasa alipofika mbele, alijiuliza kile ni kigogo gani kilaini vile, mana alipojikwa hakuhangaika na kigogo hicho, lakini mbele ndio akahisi mbona kigogo kilaini,.. Ndipo alioorudi ili kukitoa mtu mwingine asidondoke,... Lakini sasa kuangalia vizuri mbona alikuwa ni Mtu, na wakati huo kuna giza

    "mbona ni kiatu hiki"

    Alijiuliza rahim, mana mtu huyo katupwa porini lakini mguu umetokelezea pembeni mwa barabara, na ndio mana rahim akajikwaa... Sasa rahim kufatilia akagundua ni mtu, saa ngapi asitoe simu yake na kumulika..... Laaa Haulaa kumbe alikuwa ni jamali,.. Kiu ya pombe ilimuisha kwa kuuona mwili wa kaka yake..

    "brooo.....broo....kaka..... Kaka jamali?"

    Rahim alikuwa akiita kwa sauti kubwa mno... Na hapa tuombe mungu isiwe ni Mtego, mana hata rahim nae ni mmoja kati ya wawindwaji...







    Unajua waswahili walisema mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni,... Kiukweli zena anampenda sana rahim, kitendo cha kuotea anakwenda kulewa, sio kitu cha kawaida, ni upendo uliopitiliza, na kama hakina upendo wa kweli basi asinge otea chochote, japo hana uhakika kama kweli alikuwa anakwenda baa, ila kwa muonekano na haraka zake, ndizo zilizo sababisha kujulikana kuwa anakwenda baa,...

    Zena alijitahidi kumzuia, na pia hakuridhika kwa hilo akachukua na pochi yake, ambayo ilikuwa na pesa taslimu shilingi laki nane mpyaaa, zilizokuwa zinakwenda kuchezewa baa zote au hata nusu yake..

    Lakini zena baada ya kumwacha aende na kiasi cha shilingi elfu mbili, hapo zena akaridhika, mana alishasikia kuwa vilevi vyao ni vya gharama sana, hivyo kuondoka na Pochi yake ilikuwa ni nafuu kwa kiasi fulani.....rahim aliondoka zake kwenda baa, mana alipigiwa simu na kaka yake kuwa aje tu, kama ni pesa ipo ya kutosha... Lakini sasa rahim alipokuwa anatembea taratibu kwa kuchoka kukimbia,.. Alijikwaa kwenye mguu wa mtu, na kwa bahati mbaya alikuwa ni kaka yake



    "brooo.....broo....kaka..... Kaka jamali?"

    Rahim alikuwa akiita kwa sauti kubwa mno... Na hapa tuombe mungu isiwe ni Mtego, mana hata rahim nae ni mmoja kati ya wawindwaji...



    Rabim aliita sana bila mafanikio ya kaka yake kushtuka,... Na uzuri ni kwamba palikuwa ni karibu na barabara kubwa... Bajaji tanga zimejaa mno, kama baiskeli zilivyo.. Kaita bajaji wakaseidiana na dereva huyo kisha moja kwa moja mpaka hospitali kuu ya mkoa wa tanga BOMBO HOSPITAL,... ikiwa ni mida ya saa tatu hivi za usiku, wakiwa ndio wanapokelewa hospitali hapo,.. Mchaka mchaka wa madaktari ulikuwepo, mana wanamjua rahim alishawahi kuuguza mgonjwa hapa hospitali hii hii.. Ambaye ni mdogo wake na zena aitwaye Bakari... Hivyo madokta wanajua mitoto ya matajiri kama hawa hua wana midomo sana ya kuongea.......

    Kule nyumbani kwao, bibi hana hili wala lile, na hana wasiwasi kwasababu anajua wajukuu zake wanarudigi saa tano au hata sita... Kwahio saa tatu hio anaona bado mampema sana kurudi...



    Kesho yake asubuhi bibi anazunguukia vyumba vya wajukuu zake kama walirudi salama mana kuwasubiria usiku kucha hawezi, ila kwakuwa hadija yupo, basi anaweza kuwafungulia,...

    "hadija... We hadija"

    Aliita bibi baada ya kugundua vyumba vyote havikuwa na watu

    "abee bibi"

    Aliitikia hadija huku nae akiwa na shauku ya kumuuliza bibi kuwa mbona akina rahim leo hawajarudi

    "hivi akina jamali wameondoka saa ngapi leo"

    Aliuliza bibi kumaanisha ya kwamba, labda walitoka asubuhi subuhi sana,

    "hapana bibi, hata jana nilikaa mpaka saa 8 usiku, lakini hakuna aliekuja hata mmoja"

    Bibi alianza kupatwa na wasiwasi juu ya wajukuu zake, mana anawapenda sana na wala hataki yawakute mabaya,...

    "hawa watoto ina maana wamelewa mpaka wameshindwa kuja?"

    Bibi alimwambia hadija, labda wamezidiwa nanunywaji lakini haikuwa hivyo

    "mmmhhhh hapana bibi, mi najua jamali hawezi kunywa mpaka ashindwe kutembea, labda rahim"

    "sasa mbona hawajarudi... Au we ulilala mapema wajukuu zangu wakakosa wa kuwafungulia"

    "hapana bibi, mimi nilikaa mpaka saa 9 usiku"

    Hadija ni mfanyakazi tu, hivyo kuwalinda watoto wa tajiri ni haki yake japo sio mlinzi,.. Hadija ni mschana mzuri na mpole sana, tena anapendelea sana kwenda madrasa, sema rahim alipokuja, ndipo alipoacha kwenda, mana anamuita mchawi kila mara...

    "hawa watoto watakuwa wapi"

    Aliongea bibi huku akishika simu yake na kutaka kupiga,... Lakini kabla hajapiga, ghafla simu yake ikaita, alikuwa ni rahim akimpigia bibi yake, bibi alipokea kwa utani mwingi sana

    "nyie washenzi mmelewaaaa chakali na wanawake zenu mpaka mkaamua kulala huko huko si ndio eee"

    Aliongea bibi huku akitabasamu

    "bibi... Jamali kavamiwa na majambazi, mpaka sasa tupo hospitali toka jana"

    "unasemaje wewe?"

    "bibi... Kaka jamali ana hali mbaya sana huku"

    "mungu wangu watoto nyie... Uuuuuuuwwwiiiiiiiii"

    "sasa bibi walia nini sasa"

    "mpo hospitali gani"

    "Bombo"

    Bibi kuskia bombo hakutaka hata kusikia maelezo mengine, mana anapajua vizuri...

    "hadija, wewe baki na nyumba"

    "bibi kwani kuna nini"

    "jamali kavamiwa huko.."

    Hadija alianza kulia baada ya kusikia ni jamali ndie mwenye matatizo,... Bibi hawezi kuendesha gari, lakini kama angeliweza angeondoka nalo,..







     





    Tukija huku hospitali, tunamwona rahim kaegemea kitanda cha mgonjwa, kana kwamba kalala hapo hapo toka jana,... Na mpaka sasa hivi kaka yake hajapata fahamu,..

    "kijana, ungelikwenda nyumbani tu"

    Aliongea dokta wa zamu, huku rahim akimwangalia kwa hasira mno

    "yaani sijajua hali ya kaka yangu, afu niende nyumbani"

    Rahim alimjibu dokta huyo huku akiendelea kulala katika kitanda,... Rahim hakuwa na raha kabisa kwasababu, toka jana hajaambiwa hali ya kaka yake, kila akiwauliza madaktari hawasemi lolote,.. Hivyo rahim kabaki tu kama zuzu hospitali hapo,..

    "lakini kaka yako yupo salama, na mapigo yake ya moyo yanadunda vizuri tu"

    "sasa mbona hukuniambia toka jana"

    "tuliacha kukueleza mana kuna vitu vilihitajika na tusingeliweza kukupa taarifa usiku ule"

    "na kaka yangu angekufa je?"

    "tulishampima na tukagundua ni kipigo kizito alichokipata... Na pia ni damu nyingi sana zimemtoka mana amekatwa panga katika mshipa mkuu wa damu"

    "ayaaaaaa..... Sasa itakuwaje dokta?.. Nitoeni damu basi"

    "hakuna shaka... Wacha tuendelee na matibabu mengine kwanza.. Kisha tuanze kuwapima afya zenu kwa ujumla"

    Wakati bibi alikuwa bado hajafika hospitali hapo



    Tukija huku nyumbani kwa akina zena, wakati huo zena alikuwa dukani akihudumia wateja wake,.... Ikiwa imefika saa 6 hivi za mchana, mzee mvungi alikwenda kutawadha ili aelekee msikitini kuswali,.. Lakini kwa kawaida yake kabla hajakwenda hua napenda kusoma mswaafu angalau mistari miwili au mitatu,.. Mswaafu anaopenda kuutumia ni mswaafu wa zena, yaani mswaafu wa mtoto wake,... Wakati huo mzee kaketi katika kochi, alimwita bakari

    "bakarii"

    "naam"

    "njooo"

    Bakari alikuja haraka hapo sebuleni,..

    "hebu mwambie dada yako anipe mswaafu wake nichukue mbili tatu"

    Aliongea mzee mvungi na wakati huo keshatia kanzu yake safi kwa ajili ya kwenda kuswalia,...

    Lakini kabla bakari hajakwenda, aliona mkoba wa dada yake upo pale pale sebuleni katika kochi, afu ukumbuke ndani ya mkoba huo kuna lile lipochi la rahim,... Bakari hakutaka kuingiza mkono bila kumtaarifu dada yake

    "dada, baba anataka mswaafu wako"

    "utoe tu hapo kwenye kibegi"

    Basi bakari alirudi na kuufungua mkoba wa dada yake... Alitoa tu kile alichoagizwa, lakini baada ya kutoa ule mkoba ukadondoka toka juu ya kochi mpaka chini, na haukuwa umefungwa zipu,... Sasa kitendo cha kudondoka ule mkoba, na lile pochi lilivyo limbea saa ngapi halijatoka,..

    "tatizo lako unachukua vitu kwa haraka... Sasa ukipasua vitu vya dada yak.... Ni nini hilo"

    Mzee alisita kuongea baada ya kuona mpochi uliovimbiana... Yaani pochi limefinuka kwa kujaa pesa,.. Mana laki nane kwenye pochi, lazima ivimbe kiuhakika...

    "baba, hii ni pochi afu ina hela baba"

    Sasa huku dukani, zena ndio anakumbuka kuwa kule kwenye mkoba kuna pochi ya rahim,... Na wakati huo alikuwa akiongea na mteja... Zena aliacha kumhudumia mteja na kuja mbio kwenye ule mkoba wake, mana Pochi hilo lina kiasi cha laki nane keshi... Mbaya zaidi ni hizo kadi za benki zilizobeba mamilioni ya pesa... Sasa zena ile anafika tu sebuleni alipo baba yake..... Laaa Haulaaaaa... Zena alikuta pochi limeshikwa na baba









    Maisha ya familia ya akina zena ni ya hali ya chini sana, na hata duka wanalouza ndilo linalowalisha, zena hana kazi, mama hana kazi, baba baba ndio huyu ni shekhe mkubwa tu, na sulesh ambaye ndio kaka mkubwa katika familia hii, yeye ni mwalimu wa madrasa, hivyo vile vi mia mbilimbili vinavyotolewa na wanafunzi kama shukrani ya elimu yake, ndivyo vinavyowaseidia, na licha ya kufundisha, suleshi ana kigenge chake maeneo ya sokoni, anauza dagaa kwa muda fulani kisha anakwenda madrasa kufundisha....



    Familia hiii ina watoto watatu akianza suleshi akifuatiwa na zena kisha akamalizia bakari mwenye umri wa miaka 12 hivi,.. Lakini kitu cha kufurahi ni kwamba familia hio imeridhaka na maisha wanayoishi, tena ukizingatia na ucha mungu wao, ndio kabisa hata mwenyezi Mungu huwapa riziki zao ndogo ndogo kila siku,....



    Sasa ukumbuke kuwa zena alimnyang'anya rahim pochi yake, na leo baba kaiona pochi hio.... Zena kukumbuka kuwa kuna pochi ipo ndani ya mkoba wake, ikabidi aache kutoa huduma na kukimbilia ndani



    Sasa zena ile anafika tu sebuleni alipo baba yake..... Laaa Haulaaaaa... Zena alikuta pochi limeshikwa na baba



    Zena alikosa cha kuongea zaidi ya kukaa kimya ili kumsikiliza baba atasemaje,.. Hawajakaa vizuri mara sulesh huyo,.. Mara na mama huyo

    "heeeee baba zena... Hizo si pesa hizo"

    Aliuliza mama zena, na wakati huo

    Zena alikuwa anatetemeka sana mana alishakatazwa kuwa na huyo mtu,

    "hata mimi ndio naiona hii pochi, na imetoka kwenye begi la zena"

    Kaka kusikia hivyo, alimgeukia mdogo wake wa kike na kumuuliza

    "zena, umetoa wapi hizi pesa zote hizo"

    Zena kabaki kimya huku akitaka hata kulia mana nia yake kwa rahim ni nzuri lakini wazazi kumwelewa ni ngumu...

    "baba na mama.... Hizo pesa ni za rahim.... Na nilimyang'anya jana... Mana nilihisi anakwenda kunywa pombe, ndio nikaichukuwa ili asiende huko hakufai"

    Kaka kuskia tu kuwa ni pesa za rahim, wala hakutaka kuingilia sana, alijua tu kuwa hapo kuna upendo, hivyo aliona awaachie wazazi wake waongee na mtoto wao,...

    "kaka unakwenda wapi sasa"

    Zena alitamani kaka yake aendelee kuwepo, mana ndio mtetezi wake kwa wazazi hao,.. Na hata siku akiadhibiwa basi sulesh ndio wa kwanza kusuluhisha,..

    "usijali hakuna tabu"

    Baba na mama walikaa kimya kwa muda,.. Huku wakitafakari jambo fulani... Mama zena alianza kuondoka kisha akamuita baba zena huko chumbani kwao... Baba akaiweka ile pochi mezani na kumtaka zena airudishe kwa mwenye hio pochi, baba kaona kila kitu ndani ya pochi, yaani pochi imeenea utajiri wa nguvu... Zena aliichukua ile pochi na kuiweka katika begi lake,.. Zena haamini kama leo hajagombezwa



    Walipofika chumbani wazazi hawa wawili walianza kuchuja akili zao juu ya swala hilo, mana waliliona la utani lakini kama linakuja kuwa kweli

    "baba zena?.... Ivi unajua inashangaza sana?... Mi naona tumuachie mwenyewe huenda akamueka sawa... Hawa watoto wanapendana kweli baba zena"

    Mama aliongea hayo kana kwamba tayari keshaona hapa kuna upendo wa kweli,..

    "lakini mke wangu... Ukumbuke kuwa yule kijana hana adabu, nitaiweka wapi sura yangu, eti yule mpuuzi aje kuwa mkwe wangu kweli"

    "najua... Ni bora lawama kuliko fedheha mme wangu... Ivi mwanamke kuthubutu kuchukuwa pochi ya mwanaume, ili asiende kufanya madhambi na kweli mwanaume akakubali, ivi huoni ni upendo upo hapo... Hata mimi mwenyewe sijawahi hata kuchukuwa mia mbili yako kwa kutoa na mkono wangu... Mi naona tuwape nafasi, na uzuri ni kwamba mtoto wetu tumemlea vizuri na anajielewa, anajua baya na zuri... Wacha tuwaangalie na huyo kijana sioni sababu ya kumchukia mana najua kile ni kiburi cha pesa zao tu"



    Mama aliongea sana kwa mume wake,...

    "lakini siwezi kumwambia mimi... Ongea nae wewe... Alafu umwambie amwambie huyo kijana awe na adabu mbele yangu... Nitamtoa shoo yule"

    "heee yamekuwa hayo tena"

    Basi zilikuwa ni mbwembwe za mzew mvungi, ni watu wanaoishi kwa furaha sana licha kuwa na maisha ya kawaida mno....



    Sasa huku dukani zena kashika begi lake hataki tena likae mbali,.. Anasubiri tu mida mida ifike ampelekee pochi yake,..

    Ghafla zena anaitwa na mama yake, wakati huo baba keshatoka kuelekea zake msikitini,... Lakini zena akawa anaingia kwa uoga,... Wakaenda mpaka chumbani kwa zena,... Sasa mama akaanza kumwagia lisala mwanae,..







     





    "zena mwanangu... Kwanza mimi nafurahi mana nahisi ni bahati yako, japo nia ya huyo kijana hatujaijua... Kifupi ni kwamba hata baba yako kakuruhusu,.. Lakini sasa je?  Mabadiliko ya huyo kijana yanahitajika,.. Nyumbani kwetu hatutaki watu wa aina ile... Na kama hatobadilika,... Baba yako kasema hataki kukuona nae tena, kwahio fanya juu chini huyo mtu ajielewe yeye ni nani na anakwenda wapi, na anatakiwa kupata nini katika maisha yake.... Zena mwanangu fanya unachokijua kwa huyo mtu.. Ila... Choonde chonde mama... Ukijilegeza yule hakuachi, mana tunatarajia utuletee faida juu yako.."



    "mamaaaa...faida gani mnaitaka kwani... Mi nataka niolewe tu"

    "sasa we jifanye wampendaaaa afu umuachia... Na baba yako anasema anataka ng'ombe saba madume ya nguvu"

    "haaaa mamaaaa.... Sasa hivyo ni kumkomoa mtu au??... "

    Mama zena alianza Kukasirika baada ya zena kukataa kutoza mahari kubwa kwa mume atakaempata,..

    "mama, nipewe mswaafu tu basi"

    "ngoja baba yako akusikie na hizo kauli zako"

    Mama aliondoka na kumwacha zena hapo chumbani kwake,..



    Ghafla zena anaitwa kule dukani... Kufika kumbe alikuwa ni fadhila, rafiki yake kipenzi,...

    "fadhila.... Siamini macho yangu."

    Zena alimwambia fadhila huku wakikumbatiana kwa furaha,

    "huamini nini zena"

    "nimeruhusiwa kuwa na rahim"

    "ati nini??... Wazazi wako hawa hawa au"

    "ndio... Wamegundua mimi na rahim.. Tunapendana sana.. Na ndio mana wakakubali... Ila wamesema asipobadilika hawamtaki tena.. Sasa ndio nawaza nitaanzaje"

    Fadhila roho ilikuwa ikimuuma, mana alikuwa hatamani zena na rahim waendelee kuwa pamoja, mana hata yeye anampenda,...

    "utaweza tu kikubwa uwe makini rafiki yangu"

    "sasa fadhila,... Naomba unipeleke kwao, mana toka jana bado sijampelekea hii pochi yake"

    "ok twende... Ila tutapitia na madrasa kabisa.. Kwahio huku haturudi tena"



    Basi zena na fadhila waliondoka kuelekea kwa akina rahim,.. Hakuna umbali sana..... akina zena walifika mpaka hapo kwenye hilo jumba la kifahari ambako ndiko kwa akina rahim au jamali...

    "mmmhhh bibi mzungu anavyoishi kwa raha kwenye hili jumba"

    Aliongea fadhila huku kama akimkebehi mwenzie kana kwamba labda nae anatamani kuishi kwenye jumba hilo,... Bibi mzungu ni bibi yake na jamali, na wamempa jina hilo kutokana na jumba analoishi bibi huyo,... Hivyo mitaa hio ukiuliza tu bibi mzungu, unapelekwa mpaka ndani,... Akina zena walikuwa wamesimama nje ya geti wakisubiri wafunguliwe baada ya kubonyeza kengele iliopo getini... Hadija alikuja lakini wakati huo hadija alikuwa akitiririkwa na machozi, kana kwamba alikuwa akilia....

    "heeeee hadija kulikoni tena"

    Zena alimuuliza hadija aliokuwa na michirizi ya machozi,... Hadija na fadhila na zena wanajuana sana mana ni watu waliokuwa wakisomea katika madrasa moja,...

    "we acha tu"

    "mmmhhh hadija si useme.... Ok rahim yupo"

    "wamevamiwa jana usiku, na sasa hivi wapo hospitali"

    Zena kusikia hivyo alipiga kelele kubwa ya mshtuko, mpaka majirani walisikia sauti hio

    "hadija.... Nani kakumia"

    "mi sijui"

    Hadija alikuwa hata kuongea hawezi mana hadija na jamali, ni watu waliopendana mno... Sasa zena na fadhila walichukuwa tax mara moja kuelekea hospitali....



    Tukija huku hospitali,... Bibi alikuwa keshafika muda mrefu tu,.. Na hapo alikuwa yupo na mjukuu wake mmoja, bibi analia tu mana mpaka sasa jamali hajazinduka,..

    "dokta... Toka jana mpaka saa hizi saa kumi hii"

    "sikiliza kijana... Huyu mgonjwa anatakiwa kuongezwa damu... Na hapa hospitali damu zimeisha.. Hivyo tumeagiza zingine"

    Rahim alikasirika, alitamani hata kumpiga kibao huyo dokta, sema akatuliza munkari wa kisambaa,..

    "yaani we dokta ni mpuuzi kweli wewe.. Yaani mimi nipo hapa ndugu yake, unashindwa kuniambia nitoe damu... Hebu mpime njoo unitoe damu mara moja"

    Aliongea rahim huku akielekea chumba cha kutoa damu,...

    "rahim.... We rahim"

    Bibi mzungu alimuita mjukuu wake

    "bibi subiri kwanza... "

    "rahim usitoe damu tafadhali sana usitoe damu"

    Heeeee rahim hakutaka kusikia

    "rahim jamani... Juzi juzi tu hapa umetoa damu mjukuu wangu, hata nguvu haijarudi unataka kutoa tena... Usitoe wacha tusubiri hio inayokuja"

    Bibi aliongea lakini rahim ndio kwanza anazidi kwenda katika chumba cha kutolea damu... Bibi yupo nyuma akitaka kuzuia jambo hilo lisifanyike...

    Dokta alianza kumfunga rahim mkono wake ili aipate mishipa ya damu,...

    "ngoja tukupime kwanza"

    Aliongea dokta huku akitafuta bomba la sindano,..

    "unipime ya nini bwana yule ni kaka yangu"

    "sawa kijana... Tunapima magonjwa kwanza.. Usije kumwambukiza mwenzio"

    "aahhh ok sawa... Pima"

    Bibi mzungu alitokea mpaka hapo huku akitaka kuzuia jambo hilo lisifanyike,... Na ni kweli, rahim katoa damu mwezi uliopita Kwa kumwongezea damu yule mdogo wake zena... Afu leo tena anataka kutoa,....

    "bibi... Wacha atoe hata lita moja tu, ili kaka yangu azinduke kwanza... Najua najihatarisha maisha... Lakini wacha ikamzindue kala yangu"

    Aliongea rahim huku dokta akimwita rahim

    "we kijana?... Yule alielazwa pale ni kaka yako"

    "bwana dokta una maswali mengi bwana... Hebu pima"

    "nakuuliza kwasababu damu zenu haziendani kabisa"

    Rahim alitoa macho huku akiamka kwenye kitanda alicholazwa ili atolewe damu

    "Ati unasemaje dokta??.... Yaani mimi na jamali damu zisifanane.... Hapana... Dokta umekosea"

    "kajana.. Ni kweli... Wewe ni Group O na yule ni B+ yaani huezi kumwongezea damu yule mgonjwa"

    Rahim kichwa kilianza kumuuma, inawezekanaje ndugu wa damu moja, afu ziqe sio sawa...

    "dokta hapana... Rudia tena"

    Dokta alikwenda tena kuchukuwa vipimo vya jamali, kisha akachukuwa tena vipimo vya rahim... Tena rahim akiwa sambamba na dokta...

    "si unaona.... Wewe una Group O... Na kaka yako ana Group B+, hivyo mpo tofauti kabisa"

    Rahim alianza kuchanganyikiwa... Inawezekanaje kitu kama hiki.... Rahim alimfuata bibi yake huenda anajua kitu.... Wakati huo bibi katulia tu tena hata hata nguvu kabisa

    "bibi... Kumbe ulikuwa hutaki nitoe damu mana unajua kila kitu.... Sasa Naomba uniambie ukweli... Kwanini mimi na jamali damu zetu hazifanani na ni ndugu???... Nani mtoto wa kweli katika hii familia??"









    Hakuna kitu kibaya kama kuwa ndani ya familia ya yenye hadhi ya aina hii afu mwiaho wa siku ndugu hamuendani hata kwa damu, hivyo wasiwasi lazima ukujie,... Rahim anampenda sana kaka yake hivyo alikuwa tayari kudhurika kwa kitu chochote kile ilimradi kaka yake apate unafuu kwa mara nyingine,... Lakini bibi wa rahim alikuwa akikataa kutoa damu kwa kumwongezea jamali ambae ni kaka yake wa kuzaliwa tumbo moja yaani toka ntoke, na baba mmoja... Sasa rahim anakuja kushangaa yeye na kaka yake damu haziendani hata kidogo yaani rahim yeye ni Group ( O ) na jamali yeye ni Group ( B+ ) yaani ni tofauti kabisa,.. Kushangaa kwa rahim hakukuwa kimya, alimfuata bibi yake na kumuuliza ukweli juu ya familia hiii....

    "bibi... Kumbe ulikuwa hutaki nitoe damu mana unajua kila kitu.... Sasa Naomba uniambie ukweli... Kwanini mimi na jamali damu zetu hazifanani na ni ndugu???... Nani mtoto wa kweli katika hii familia??"



    Bibi alikaa kimya kwa muda huku akiwa na mawazo sana katika kichwa chake,.. Rahim anawaza usikutw yeye kawa hana lolote, mana jeuri ya pesa itamuisha pale atakapojulikana sio mtoto halisi wa familia hio,..

    "kamuulize mama yako... Mimi najuaje sasa... Mbona mnanipa mawazo nyie watoto... Mimi mwenyewe ndio nashangaa kwanini damu zenu zinatofautiana na wakati ni watoto wa mzazi mmoja"

    Rahim alikosa cha kuongea, lakini mawazo yalimjaa sana,.. Nani mtoto wa hii familia

    Sasa hapo ukumbuke rahim toka jana hajapata pombe, sasa ukijumlisha na haya mawazo, sitaki kuamini hio pombe itanywewa kiasi gani...



    Wakati huo akina zena na fadhila ndio wanafika hospitalini hapo huku wakiwa na shauku ya kujua kinachoendelea,... Ghafla wanakutana na rahim akiwa anatoka katika chumba cha kutolea damu, zena akajua tayari rahim keshakamuliwa damu, mana alitoka akiwa kashika mkono pale palipotobolewa kwa ajili ya damu kupimwa

    "jamani ram... Pe sana kwa matatizo"

    Zena alimkimbilia rahim na Kumkumbatia kabisa, kitendo hicho kwa rahim kilikuwa ni kigeni sana lakini hakuwa na raha tena, mana keshaona utofauti wa familia yao ipo wapi,... Hivyo kama ni watoto wa mama mmoja basi baba ni tofauti,.. Sasa je? Nani mtoto wa mzee rashidi

    "zena??... Naomba utulie kidogo, siko sawa"

    Aliongea rahim huku akimtoa zena kifuani kwake... Mana zena kafa kafia kaoza, hasikii haambiwi...

    "I know... But atapona tu"

    Zena alijua rahim ana mawazo juu ya jamali, kumbe kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo,..

    "pochi yangu ipo wapi"

    Aliuliza rahim, huku zena akiutoa mkoba wake,

    "lakini rahim, mimi sitaki uendelee na hizo starehe zako.. Sizipendi mimi"

    Zena aliongea huku akitoa pochi hio, lakini rahim hakumjibu kitu,

    Sasa tukio lile la zena kutoa pochi ya rahim, bibi alikuwa akiliona live bila chenga,...

    "Ahsante... "

    "sasa si ukague"

    "kwani unaweza kuniibia?"

    Rahim alimuuliza zena kuwa kwani anaweza kumuibia,.. Zena alitabasamu tu mana kaaminika kwa asilimia zote,.. Fadhila roho ilikuwa ikimuuma sana wawili hao wakiendelea kupendana,...

    "twende basi nikamwone kaka yako"

    "hajaamka bado"

    Basi walikwenda mpaka wodini kumwangalia jamali,...



    Baada ya siku hio kupita,...  Jamali akiwa kapata ahueni kidogo, baada ya kuongezewa damu ambayo ni ya kununua, mana ile ya rahim imeshindikana, Rahi akiwa yupo karibu na kaka yake, lakini kwa wakati huo alikuwa yupo njwiiiii, yaani keshatupia vitu vyake,... Hata hadija alikuepo eneo hilo, akiwa karibu sana na jamali,... Sasa rahim yeye hajuagi kama hadija na jamali wana mahusiano, leo ndio anajua ukaribu wa hadija kwa jamali,...

    "broo vp hali kwa sasa, unajiskiaje"

    Aliuliza rahim huku wakiwa wanakula matunda matunda ili kumsapoti mgonjwa ale kwa wingi,...

    "aahhh sio mbaya sana... Ila kwanini umekunywa mchana huu"

    Jamali alimuuliza rahim baada ya kumjibu swali lake

    "aahhh broo, wacha nilewe tu... Mana nina mawazo mengi sana yaani we acha tu"

    "wazo gani tena... Mbona mimi niko sawa ru"

    "najua... Ila nina wazo tofauti na hilo"

    "basi usijali, nikitoka hapa... Utaniambia ili nikupe ushauri juu ya wazo lako,.... Ila kwa sasa nataka nipunguze kunywa... Mana hali hii imetokana na kwenda baa mara kwa mara"

    "heeeeee unasema unataka ufanyeje"

    "nataka nipunguze rahim... Sasa nataka niwege nashtua tu lakini sio kulewa tena"

    "duuuuuuuu....maajabu haya... Mmmhh haya mimi mwanzo mwisho.. Hachi mtu, wala hapunguzi mtu"

    "sasa na kale katoto kawatu... Nako katakunywa pombe au"

    "nani uyo"

    "si kale keupe"

    Rahim alijua jamali anamsemea nani... Lakini hakutaka kuendelea kuongelea jambo hilo... Ikiwa ni mida ya saa saba wakiwa ndio wameleta chakula, ghafla zena alikuja, tena akiwa peke yake,... Yaani sasa hivi walikuwa wakimtaja

    "As Salaam Aleykum Warahmatullah wabarakatuh"

    Alisalimia zena lakini wote hakuna anaejua kuitikia hio salamu zaidi ya hadija peke yake

    "Waleykhu msalam warahmatullah wabarakatuh.. Hali yako zena"

    "aahhh tunamshukuru mwenyezi mungu.... Jamali habari yako"

    "salama tu... Za siku shem?"

    "nzuri.. Unaendeleaje kiafya"

    "aahhhh kidogo najiskia safi... Ila shem hutajwi, muda huu tu tulikuwa tunakuongelea"

    "ahahahaahah... Basi mlikuwa mkiongea mazuri zuri"

    "ndio"







     





    Wakati huo Zena alishajua rahim hapo alipo tayari keshatupia vitu vyake, mana jicho la rahim lilikuwa limelegeaaaa.. Akajua hapa basi lazima tayari keshakunywa

    "rahim, habari yako"

    "safi tu"

    "naomba tuongee mara moja"

    Zena alimtaka rahim waongee mara moja, na rahim hakuwa mkaidi alinyanyuka alipokaa na kwenda mahari kwa ajili ya maongezi zaidi..

    "ivi rahim... Nataka kukuuliza.. Hivi ina nia gani na mimi"

    Aliuliza zena tena kwa upole wa hali ya juu

    "kivipi yani.. Sijakuelewa"

    "ivi u ajua kiwa nahitaji kuolewa"

    Rahim alitoa macho ya vile yalivyolegea kwa kulewa

    "yule mume aliosema baba yako ndio keshakuja nini"

    Zena alichoka kuskia hivyo

    "sikiliza rahim... Baba yangu alisema vile ili wewe usinifuate... Lakini sio kweli kama mimi nina mchumba... Sina"

    "sasa mbona unasema wataka uolewe"

    "ina maana wewe hutaki kuoa"

    "aahhhh mimi muda bado.... Starehe nitamuachia nani.. Nikishaoa ujue ndio basi tena yani... Skia... Mi nataka niwe na wewe kawaida tu, sitaki kuoa wala nini"

    Aliongea rahim bila kujua anauumiza moyo wa zena, mana umri wa kuolewa ndio huo,...

    "sawa bwana... Ahsante"

    Zena alikasirika sana na kuondoka zake, ila sasa tukio lile bibi aliliona tena, yaani bibi mzungu anafaa kuwa Shilawadu mkuu... Yaani kila tukio yeye yumo... Bibi leo hakulifumbia macho hili

    "sasa nauli je hutaki"

    Aliongea rahim huku akitaka kumpa nauli

    Lakini zena hakutaka kugeuka wala nini,... Bibi alimfuata zena, mana sio kuwa hamjui anamjua haswa kuwa ni mtoto wa mzee mvungi, ila hajui kama ana mahusiano na rahim,.. Rahim yeye aliingia zake ndani lakini bibi hakumuacha zena, ile zena anachukuwa tu bajaji, ghafla anasikia sauti ya kuitwa

    "mjukuu wangu subiri kidogo"

    Zena anamfahamu bibi mzungu,.. Ni bibi yake na rahim,...

    "shkamoo bibi"

    "Marahaba hujambo"

    "sijambo bibi"

    Bibi akimvuta zena mahali ili wakaongee zaidi...

    "nilikuwa natokea mjini, sasa nikaona nipitie hapa... Lakini mapozi ninayo kukuta na mjukuu wangu,.. Yananipa mashaka... Mana hata jana niliona ukiwa unampa sjui nini kile... Na leo nimekuona nae.. Sasa nilikuwa nataka tu kukuuliza"

    Zena hakutaka kumficha bibi yake rahim, alimpa ukweli wote kuwa, anatamani awe mume wake, kiufupi anampenda sana rahim

    "kwahio... Wewe unampenda rahim"

    "bibi?... Yaani asikwambie mtu... Yaani sijatokea kumpenda hata mtu wa aina yangu.. Lakini nimeshangaa moyo wangu kutua kwa rahim,na ni kitu cha ajabu sana na watu wananishangaa mno"

    "na wewe una uhakika anakupenda"

    "nina uhakika wa asilimia 100, rahim ananipenda lakini sasa nitawezaje kumfanya aache tabia ya kunywa mapombe hayo"



    Bibi yake rahim ni mtu mzima.. Na unaambiwa mkubwa dawa,... Bibi aliomba wakakutane wazazi wote washauriane,...

    "naweza kwenda nyumbani kwenu tukashauriane na wazazi wako"

    "sawa.. Mana hata wao wameniruhusu, ila hawataki tabia zake"

    "wewe niachie mimi... Hata sisi sio kuwa tunapenda rahim awe mlevi.. Ila mama yake kamlea vibaya sana huyu mtoto"

    Basi bibi na zena haoo wakaondoka kuelekea kwa wazazi wake,....

     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog