Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE ISLAMIC WIFE - 4

 

     

     



     

    Chombezo : The Islamic Wife

    Sehemu Ya Nne (4)

     



    BAADA YA WIKI MBILI KUPITA



    Rahim akiwa nyumbani kwao, tena ukumbuke jamali alisema anapunguza kunywa pombe, na ni kweli toka alipo pona mpaka sasa anagusaga tu grasi moja moja,.. Huo ni mkakati wake na pia ni ushauri kutoka kwa hadija ambae ni mpenzi wake,.. Rahim yeye alikuwa anachati zake na simu... Lakini ghafla simu yake ikaita na namba ambayo ni ngeni kwenye simu yake,.. Aliipokea

    "haloo?"

    "eeehh habari yako ndugu"

    Mtu huyo alikuwa anahema sana kana kwamba kuna taarifa mbaya

    "salama nani mwenzangu"

    "aahhh ustake kunijua... Sikia.. Yule mchumba wako mweupe mweupe hivi yupo hospitali kalazwa"

    "Kalazwa??... Kapatwa na nini na jana usiku nilikuwa nae ghafla"

    "mimi sijui bwana... Nimepewa namba na bibi mmoja hivi nikupe habari mana simu zao hazina vocha."

    "ok..kalazwa hospitali gani"

    "bombo Hospital"

    Mara simu ikakatwa... Rahim kwa zena, kafa kaoza kabisaa, sema anapokunywa anakuwa na majibu ya shombo sana, na ndio mana zena hataki kukaa nae karibu pindi anapokuwa kalewa,... Rahim alichukuwa gari kisha akaondoka kuelekea hospitali,... Na uzuri ni kwamba hapo alipo bado hajagusa vitu vyake,... Kwahio kichwa kipo sawa,... Dakika kumi tu rahim alishafika hospitali huku akiwa na mawazo ya zena kapatwa na nini, na wakati jana jioni alikuwa nae

    Alipofika mlangoni kuna watu walimzuia asiingie, lakini rahim hakutaka kuelewa hilo,.. Kaleta tabu mpaka akaruhusiwa kuingia,... Laaaa haulaa.... Rahim alimkuta zena kazungushiwa madripu ya maji, yaani mipira imepita kila mahari, hata kupumua haqezi na hapo alikuwa akipumulia mashine,..

    "zena.... Zena... Jamani zena una nini na jana tulikuwa wote"

    Zena alikuwa hata kuona haoni, mana katika pua yake kawekewa kile kifaa cha Oxygen.. Cha kuingiza hewa, mana hawezi kupumua peke yake lazima aseidiwe na mashine... Rahim akiwa kapiga magoti chini akiwa anamjulia hali.. Mara dokta mkuu alikuja na kusema

    "ah ah, kijana.. Mgonjwa hatakiwi kusumbuliwa.... Jamani nani kumruhusu huyu mtu"

    Aliongea dokta huku akitaka kuita watu wamtoe,...

    "dokta... Naomba nikae nae... Mpenzi wangu, naomba niwe nae karibu"

    "unasemaje wewe"

    Mara familia ya akina zena inaingia, tena wote sio baba sio mama wala sio watoto,.. Wakati huo mama analia sana kutokana na ugonjwa wa mtoto wake zena.....

    Sasa rahim alipo waona wazazi wa zena, akasita kuongea mana anajua hua hawatakagi awe karibu na zena

    "nakuuliza unasemaje..."

    "kifupi ni kwamba, nampenda sana.. Na nataka niwe nae karibu"

    Sasa kabla dokta hajamjibu mara baba yake zena kadakia,...

    "dokta... Huyu ndio yule kijana tuliokuambia kuwa, yeye ndio mwenye uwezo wa kumuongezea zena damu... Na ikishindikana, mwanangu atapoteza maisha"

    Rahim alitoa macho kusikia kuwa kama itashindikana rahim kutoa damu, basi zena anaweza kufa

    "nitoeni basi jamani au mpaka afe"

    "ah ahhhh... Kijana.. Vuta subira kwanza.. Hatuendi haraka hivyo"

    "sasa nini shida dokta"

    "tukupime  kwanza...."

    "lakini dokta... Mbona Nilishawahi kumtolea damu mdogo wake... Tena huyu hapa... Nilimtolea kana kwamba damu ziliendana... Sasa kwanini huyu zisiendane??... Ebu nitoe bwana"

    "hapana... Tunataka tupime magonjwa"

    Basi mlolongo ulikuwa ni mrefu sana, kitu ambacho rahim hakukipenda....

    "unajua kijana.. Damu ya kununua kwa sasa hivi haifai... Mana damu nyingi hutolewa kwa watoto.. Sasa ukimuongeza mtu mzima kama yule na damu ni ya mtoto... Inakuwa sio vizuri, na hata kama ni damu ya mtu mzima.. Je? Tunajua alikuwa na ugonjwa gani... Kwahio huyu mchumba wako, hatutaki anunuliwe damu, ispokuwa wewe ndio umseidie"

    "kwani kapatwa na nini"

    "kapigwa na shoti ya umeme... Ila kwa bahati nzuri wamemuokoa mapema, hivyo hapo ni damu tu ndio inatakiwa"

    Aliongea dokta na wakati huo akiwa anaendelea kumpima rahim....

    "heeeeeeee we kijana unakunywaga pombe eee?"

    Dokta aliuliza baada ya kugundua kuwa damu ilikuwa na kemikali za pombe,...

    "ahh kidogo tu dokta"

    "basi.. Haitawezekana kutoa damu"

    "ati nini dokta??... Mbona nilishwahi kumtolea mdogo wake"

    "sawa lakini sio kwa ugonjwa huu.."

    "basi nitakaa hizo siku mbili bila kunywa... Kama vile vya siku ile"

    "hapana.... Hiii kemikali iliopo humu, sio ya siku mbili tatu... Kuna kemikali zaidi ya gramu 800

    "khaaaaaaaaa dokta... Gramu 800??..nimenywea wapi hizo pombe sasa"

    Rahim hajui mambo ya kidokta hivyo hata akiambiwa una kilo moja ya kemikali atakubali tu....

    "sasa.. Ili kemikali hizo zisafishike kabisa... Ili itoke damu yenye ubora... Basi ni lazima ukae mwezi mmoja na siku saba.. Bila kunywa pombe aina yeyote ile.. Yaani hata soda usiguse... Labda juisi ya kutengeneza mwenyewe"

    "khaaaaaaaaaaaaaaaa..... Ati unasema mwezi mmoja na siku ngapi vile"

    "siku saba"







    Dokta alihisi rahim anaweza kuacha pembe ndani ya siku hizo,... Na rahim sidhani kama atakubali, na hata akikubali je? Ataweza kukaa muda wote huo, ni kitu ambacho haiwezekani kwa rahim, japo kaka yake kwa sasa kapunguza kunywa pombe, mana aliponyeka ponyeka kufa, kaibiwa vitu vingi sana, kadi za benki, simu, yaani walichukuwa kila kitu, sema Kwenye mambo ya benki hawatoweza mana inakwenda kwa namba za siri, hivyo hizo kadi watazitupa tu hata kama zina pesa kiasi gani



    "khaaaaaaaaaaaaaaaa..... Ati unasema mwezi mmoja na siku ngapi vile"

    "siku saba"

    Rahim aliuliza na kujibiwa kama alivyosikia mwanzo,...

    "basi tununue damu mtu asije kufa bure"

    Aliongea rahim kuwa basi wanunue damu mana kitendo cha kukaa mwezi na siku saba hatoweza kabisa, mana siku moja tu kwake ni mateso makali mno,...

    "kijana, nilikwambia nini kuwa damu ya kununua siku hizi haiaminiki"

    "si utaipima kama ina tatizo"

    "hapana... Hatuwezi kufanya hivyo.. Na kama inashindika bora tumtolee mipira ya Oxygen afe, kuliko aendelee kuteseka bure tu"

    Aliongea dokta huku akimsogelea zena kutaka kung'oa ile mipira ya kupumulia,.. Rahim anampenda zena kutoka moyoni, akifikiria afe kweli,...

    "basi nitajaribu, ila nikishindwa basi bora afe tu"

    Aliongea rahim, huku akiwa haamini macho yake kama kweli anaweza kukaa muda mrefu bila kunywa pombe,...

    Zena hapo alipo anapumulia mashine yaani kama ni shoti ya umeme basi imempatia ya kisawa sawa,..



    Rahim alikaa hapo karibu na zena, mara bibi yake kafika hapo wodini

    "rahim, kwanini umekuja huku hata kula hujala umekimbilia hospitali"

    "kwani kuna tatizo gani"

    "hujala wewe"

    "lakini bibi, mimi ni mtu mzima, nikikosa kula nyumbani hata hotelini naweza kula tu... Wala usiniwazie katika swala la kula"

    "lakini chakula cha nyumbani ni kizuri zaidi"

    "sawa... Nitakwenda kula"

    Aliongea rahim huku akimfuata dokta na kumuuliza kuwa

    "dokta? Huyu mgonjwa kapata chakula kweli"

    Rahim aliuliza huku dokta akimjibu

    "ndio... Ila anakula kwa mipira, yani hata kuamsha mdomo hawezi.. Shoti ilimuumiza sana na kama sio kuwahi kumwokoa, basi angeshakufa kabisaa"

    "duuuuuuuuu.... Aisee dokta kuwa makini na mgonjwa,.. Yaani hakikisha anakuwa salama kwa gharama yeyote ile"

    "kijanaaaa... Huyu mgonjwa hapa hana gharama, ispokuwa gharama yake ipo kwako,.. Na ukinywa hata grasi moja tu, siku zinaongezeka... Na tutakupima kila baada ya siku tatu"

    "kwaio.. Hata kuonja pia"

    "yaani sio kuonja tu... Hata tone hutakiwi kuliingiza ndani ya mwili wako... Na ni vizuri umalize siku zako ili ukanywe pombe vizuri"

    Rahim akifikiria hizo siku ni nyingi sana kwake.... Basi rahim hakuwa na budi, kaenda dukani kisha kanunua kalenda na kuanza kuziweka alama kila siku ikipita, anaweka tiki,...



    BAADA YA WIKI MOJA KUPITA



    Rahim anaonekana kukimbizwa hospitali, yaani kawa mgonjwa kisa kukosa pombe,  na hapo yupo hoi, mishipa imemtoka kila mahala, yote hio ni mazoea ya pombe.... Madaktari walianza kumchangamkia mana wanamjua, sasa zena na rahim wapo hospitali moja tena wote wakiwa hoi,... Maskini zena ndio kabisaa mana anatumia mipira kila mahali, alipolala ni hapo hapo,... Toka alipolazwa sasa ni wiki imekwisha hajajigusa wala kutetereka,.... Sasa huku wodi nyingine, rahim anaumwa Kiukweli ukweli, yaani mishipa ilikuwa ikimbimba kila kona, alikuwa ni mtu wa kujikaza mara kwa mara... Sura yake ilibadilika,... Mchaka Mchaka wa madaktari ulikuwa sio mdogo, walifanikiwa kumtuliza baada ya kumpa vidonge vya kupunguza maumivu, lakini bado mishipa imemsimama, kana kwamba mwili umeshazoea kupata kemikali kila mara,...

    Sasa bibi anavyompenda mjukuu wake mana ni kweli rahim anaumwa haswaa, na hapo jamali yupo

    "jamani tumpeni hata grasi moja"

    Aliongea bibi yake huku akitaka kumtuma jamali,

    Lakini kabla hajafanya hivyo mama yake zena kaja

    "jamani mama?... Umpe pombe tena? Sasa mtoto wangu ataponaje? Au umesahau mama yangu"

    Mama yake zena aliongea kwa upole wa hali ya juu, mana akinywa pombe hapo kuna wiki nyingine inaongezeka mbele,..

    "lakini mama zena... Tunachokifanya sio sahihi, tutau mtu"

    "basi huko siriasi na jambo hili"

    "hapana mama zena... Huyu mtoto atakufa"

    "kwahio wakwangu kule atapo"

    Walikuwa kama vile wanabishana hivi, lakini ghafla simu ya bibi mzungu imeita, yaani bibi yake rahim...

    Kuangalia jina alikuwa ni mama mkwe wake, yaani mama yao hawa akina jamali na rahim,...

    "halooo mwanangu hujambo"

    "sijambo mama shikamoo mama"

    "maraha, haya uhali gani"

    "aahhh huku salama tu.."

    "basi ni vizuri mwanangu"

    "mama??... Mbona hao wajukuu zako hawarudi, na huyo mmoja bado anasoma mama... Wafukuze huko warudi"

    Sasa bibi hakuwa na cha kusema,.. Ikanidi aseme ukweli tu kuwa rahim anaumwa

    "kweli mwanangu, najua rahim bado yupo shule, lakini anaumwa"

    "ati nini??... Rahim anaumwa"

    "ndio... Yaani kashikika haswa"

    "mungu wangu, mtoto wangu... Haya cha zaidi ni nini"

    "ni malaria tu"

    "kwahio mpo nchi gani kwa sasa"

    Yaani familia ya akina rahim, hua haitibiwagi Tanzania, yaani mtu yeyote akiumwa, haijalishi homa ni kali au sio kali, wanapanda ndege kwenda kutibiwa nje ya nchi, mana hela ipo,... Sasa na mama yake nae anadhani kwa sasa rahim anatibiwa nje ya nchi, na ndio mana kauliza mpo nchi gani....

    "nchi gani.... Sisi tupo Bombo Hospital"

    "Bombo Hospital si hospitali ya tanga hio, au ni majina tu yamefanana"

    "hakuna cha majina kufanana wala nini, mtoto wako kalazwa Bombo Hospital ya mkoa wa tanga"

    "mungu wangu... Mama kwanini usingenipa taarifa kabla ya kumpeleka huko"

    "ndio imeshakuwa hivyo, na hapa anapata matibabu mazuri tu"

    "mmmhhh hapana... Ngoja nimpigie baba yake, tuje hapo tumchukue"

    Sasa kimenuka, na hapo mama rahim hajui kama anaumwa kwasababu ya kukosa pombe, na licha ya kukosa pombe bado atatakiwa kutoa damu kumwongezea zena,...

    "kuna nini tena"

    Aliuliza mama zena huku akiwa na shauku ya kujua

    "wanakuja kumchukuwa wampeleke huko kwa wazungu sijui wapi huko"

    "jamani... Ivi familia yenu ikoje? Yaani ugonjwa kidogo tu huu waende huko"

    "wacha waje wamchukue tu"

    "hapana... Kaza moyo tuongee nao... Mana mtoto wangu itakuwaje, na rahim akienda huko atakunywa pombe... Tuongee nao mana wewe ndio mama yao watakuelewa tu"







     





    Wakati huo sasa huku jijini Arusha, mama rahim kapandwa na presha sjui ni ya kushuka sjui ni ya kupanda hatujui... Kashika simu yake na kumpigia mume wake ambae ni mzee Rashidy,...

    "haloo baba jamali,.. Upo wapi"

    Aliongea mama bila hata salamu

    "kuna nini mbona kama unahema hema tu"

    "mtoto anaumwa"

    "nani tena"

    "rahim"

    "nini zaidi"

    "bibi yake kasema ni malaria"

    Baba alimuwa mkali kusikia mtoto wake anaumwa, tena yupo hoi,..

    "lakini kwanini umetoa ruksa ya hawa watoto waende tanga... Kule tanga kumejaa wachawi tu... Sasa nakuja arusha sasa hivi twende tanga"

    "sawa...wacha mi niwahi Airport sasa hivi"

    "haraka sana nikukute... Unatoa toa ruksa ya watoto kutoka, na shule zimeshafunguliwa sasa"

    "basi baba jamali yaishe"

    "hapana bwana... Mimi mwenyewe tanga ni kwetu lakini Naogopa kwenda"

    "sawa kata simu... Nami nijiandae"

    "haya twende.. Tukamchukue"

    Mzee kawaka, hataki utani na familia yake, yaani utani hataki kabisaa kwenye swala la watoto wake,.... Mzee ana makampuni mengi mno, sio Tanzania sio nje ya nchi, na ana watoto wawili tu wakiume, sasa wakianza kufa kufa nani anazuia mali zote hizo... Mzee alikuwa yupo dubai akiendelea kufanya kazi zake kama kawaida,.. Ila kaamua kuacha biashara zake na kuja Tanzania ili kufanya matibabu ya mtoto wake huyo,...



    Kesho yake mida ya saa tano hivi za asubuhi, paliingia gari moja ya kifahari, mpaka wauguzi walishangaa, na watu waliopo hapo hospitali, na sio mwingine bali ni wazazi wa rahim ndio wametia timu ndani ya hospitali

    Wazazi wa zena waliogopa sana mana kuumwa kwa rahim ni kwasababu ya mtoto wao,.. Hawakuwa wakitoa hata salamu kwa watu waliowakuta, ispokuwa kwa wale aliowakuta katika wodi aliolazwa rahim

    "za saa hizi jamani"

    "salama tu"

    "shkamoo mama"

    "Marahaba.. Haya haraka haraka za nini tena"

    Mama alimuuliza mtoto wake ambae ni baba yake rahim

    "mama... Huyu mtoto anasubiriwa na ndege aende Uingereza kutibiwa"

    "kwahio hapa hakuna matibabu"

    "mama... Matibabu ya Tanzania hayafai... Matibabu ya Tanzania hayatufai katika familia yetu,.. Na hapa tunapoongea tayari anasubiriwa Uingereza kwa matibabu zaidi"

    Na wakati huo baba rahim anaongea huku akimuweka rahim vizuri kwa kutaka kumbeba,.. Yaani hakukuwa na utani hata kidogo,...

    "mama... Fanya kitu hapo rahim ndio anaondoka hivyo"

    Aliongea mama yake zena, huku akimlazimisha bibi huyo amkataze mzee Rashidy kumchukuwa mjukuu wake,..

    "wacha amchukuwe mtoto wake... Mana sisi hatuna uchungu na huyu mtoto"

    "hapana... Usikate tamaa hivyo... Ina maana umesahau tunachokifanya kwa mjukuu wako... Wewe ukiwa kama mama mzazi wa huyu baba... Hawezi kufanya lolote kwako... Kwanini unamwogopa mwanao mno"

    Mama zena alikuwa akitamani kulia ili tu rahim asiondoke hapo hospitalini, mana akiondoka na mtoto wake ni basi tena,.. Na hakuna mtu anaweza kujitolea damu bure ispokuwa rahim tu, na ni kwasababu wanapendana.....

    "rashidi?... Naomba umuache huyu mtoto hapa hapa"

    Aliongea bibi mzungu, na hapo anatumia nguzo ya uzazi sasa na sio kauli, mana familia hii imeathiriwa na pesa hivyo haisikii cha mkubwa wala kiongizi, wakitegemea pesa ndio kila kitu kwao

    "mama.... Sio kusubiriwa tu,.. Na pesa za matibabu nimeshatuma ili akifika tu atibiwe.. Na ninakwenda nae mpaka Uingereza..... Hebu nifungulieni mlango nitoke nae"

    Aliobgea baba yake rahim ambae ndio mzee rashidi,....

    "sasa nasema hivi.... Kama hujakaa kwenye hili tumbo langu miezi 9, Thubutu kutoka nae... Na kama umekaa kwenye tumbo hili miezi tisa.. Naomba umrudishe alipokuwa"

    Wakati huo rahim keshawekwa begani, yaani kilichobaki ni kauli ipingwe waondoke nae





    Familia ya akina rahim ilijengwa na uzoefu wa pesa, ilijigamba kwa wingi wa pesa zao, kila mmuni mdogo kwao kutokana na pesa zao, hata Mwenyezi Mungu hawamjui kwasababu ya pesa, yaani pesa kwao ni kila kitu katika maisha yao, wanasahau kuwa kuna utu nao unahitajika, wao wanahisi kuwa na pesa ndio msaada mkubwa hapa duniani, hata wakubwa hawaeshimiki, dini haiheshimiki kwasababu ya pesa walizonazo..



    Haya leo mtoto wao anaumwa ugonjwa mdogo tu, lakini unaambiwa anatakiwa kwenda Uingereza kutibiwa na keshapiga simu na pesa kalipa, kilichobaki ni kumchukuwa rahim na kuondoka nae,...



    Sasa bibi wa rahim alikuja juu na kumweleza mwanae kuwa kama hajakaa katika tumbo lake kwa miezi 9 amchukue rahim na aondoke nae, lakini kama kakaa miezi 9 ndani ya tumbo lake basi na amuache rahim aendelee na matibabu....

    Baba yake rahim alifikiria sana na kutaka kweli kuondoka, lakini kabla hajajishauri, mama aliongeza neno lingine tena...

    "hata hizo pesa unazolingia... Kama sio baba yako kuzianzisha ungelikuwa wapi, mbona baba yako hakuwa hivi, na hata hayo malezi hatujakupa sisi, nashangaa hawa watoto mnawahiribu,... Mtoto mdogo kama huyu nalewa kiasi hiki,.. Hata kama huo upekee lakini sio kwa hali hii,... Pesa huendi nayo popote.. Haya leo anaumwa unampeleka Uingereza, sasa je kesho akifa utampeleka wapi?"

    Mama aliongea kwa uchungu huku akitaka hata kulia, lakini baba yake rahim ile kuangalia pembeni, hamuoni mkewe,.. Hatujui kaenda wapi,... Sasa ile bibi anataka tu kutupia maneno mengine, mzee kanyoosha mikono juu

    "basi mama inatosha... Kama unataka afie hapa sawa.. Mchukuweni"

    "sasa unamkasirikia nani... Taratibu zenu za kipumbavu kupelekana nje ya nchi kwa matibabu leo unanikasirikia mimi... Weww mshenzi kweli wewe.. Huna adabu mwehu wewe... Unaleta kiburi cha pesa, mbona baba yako mzee rahim alio anza nazo hakuwa hivyo??... Nyinyi watoto wa siku hizi ivi mkoje"

    Sasa wakati bibi mzungu anaendelea kumfokea mtoto wake, Ghafla mama yake rahim anatokea,...

    "baba rahim... Muache huyu mtoto... Nitakuambia kila kitu"

    "na wewe ushatiwa ujinga si ndio ee.. Nani anaweza kukupinga na pesa zetu"

    "lakini mama kasema"

    "hata yeye anaweza kupingwa, kwani ni nani"

    Mama kasikia hayo maneno akaja juu

    "thubutuuuuuuuuuuu... Hebu jaribu kunipinga kama hizo pesa hujaziona karatasi na ukaanza kuzichana sasa hivi"

    Bibi wa rahim hataki mchezo hata kidogo,... Lakini bwana Rashidy ambae ni baba yake rahim, alipokea simu pale pale



    "halo mr sandu habari yako"

    "salama bwana Rashidy.. Uhali gani"

    "hakuna matata, vp kuna jipya"

    "ndio... Gari zako zote zimeshafika bandari ya Dar es Salaam"

    "acha utani mr sandu"

    "aahhhhhh... We njooo na unatakiwa uje mwenyewe, si unajua ulipaji wa kodi wa safari hii"

    "najua, na nakuja kuzilipia zote, gari 100"

    "sawa ni wewe tu, na unatakiwa kufika hapa haraka sana"

    "sawa kaka nakuja hapo muda sio mrefu"

    Simu hio ilikata kisha akamgeukia mke wake na kumwambia kuwa...

    "mke wangu... Naomba uangalie usalama wa mtoto wetu"

    Lakini kabla mkewe hajajibu, mama yake akadakia

    "kwahio sisi uliotukuta nae hua hatupendi usalama wake.... Ivi rashidi mwanangu, hizi pesa zitakufikisha wapi... We ulizani ukifa utakwenda nazo... Mimi sitaki kiburi chako mbele yangu, shuuwain mkubwa wewe... Pesa za mume wangu unaniletea kiburi nazo.. Shenzi wewe... Na huyu mtoto hatoki hapa"

    "lakini mama? Mimi si nimeshamuacha mjukuu wako... Simchukui"

    "sasa maagizo. Mengi ya nini"

    "basi mama... Wacha niwahi pesa sisimwagike bure"

    Baba yake rahim alikuwa na dharau sana hata kwa mama yake, na ndio maana hata watoto hawana muelekeo mzuri wa maisha zaidi ya kuijua pesa,..

    "jamali... Jamali?"

    "yes daddy"

    "twende zetu.. Achana na Wasambaa hawa"

    "sawa mzee"

    Mzee rashidi alimuita jamali ili aondoke nae kwenda Dar es Salaam kupokea mzigo ulioingia muda huo... Kwahio hapo jamali na baba yake wameondoka kwenda Dar es Salaam

    , lakini mama yake rahim yupo hapo kabaki sasa na mama mkwe,.. Yaani mama wa mume wake,...

    "ivi wewe, hawa watoto mme waleaje?.. Mbona mumewapa malezi machafu kiasi hiki, watoto hawajui mkubwa ni nani.. Watoto hawajui maana ya dini.. Sio Mkristo wala sio. Muislamu yaani watoto wapo wapo tu kama wapagani vile.. Hata wapagani nao wana miungu yao wanayo ijua,.. Kama malezi ya kujua utu wa mtu mlishindwa kuwapa bora mngewaleta huku tuwaseidie kule... Hebu ona sasa, mtoto anaumwa kwasababu ya kukosa pombe, ivi kweli inaingia akilini hii??... We mwajabu si nakuuliza lakini"



    Mama yake rahim alikuwa akimfokea sana mke wa mtoto wake,...

    "mama... Lakini yote haya ni mwanao, mana mimi nikijitahidi kuwalea vizuri, baba yao anawatetea na kuwafundisha maisha ya pesa... Basi na mimi nikaacha, mana kuna siku nakataa rahim na jamali wasiende popote kwenye starehe, lakini baba yao akija anawachukuwa na kwenda nao, sasa mimi nina makosa gani mama"

    Mama yake rahim alikuwa mpole kuliko maelezo, mana mume wake nae kapewa vigongo vyake muda sio mrefu, hivyo naye hataki limkute hilo,.

    "mumewalea vibaya sana hawa watoto,... Malezi ya aina hii hayafai.. Je mkifilisika sasa wataishi na nani ni kila mtu walimuona pumba?"

    "tusamehe tu mama yangu"

    Pale pale dokta alileta bili ya mgonjwa wa kile, yaani zena,... Mana ana wiki nzima hapo hospitalini na hajalipiwa chochote, na rahim yeye kaletwa jana tu,..

    "kuna bili ya laki nne na elfu 60 inatakiwa kulipwa"

    "hakuna shida dokta... Hapa kuna ATM mahali"

    Mama yake rahim alikuwa tayari kulipia bili hio, japo haijui hio familia ina uwezo gani, mana ndio kafika leo hii,...

    "ndio, ATM ipo kwa pale mbele"

    Basi mama rahim alitoa kiasi kikubwa cha pesa kisha akampa dokta kile kiasi kinachodaiwa, na zingine akamkabidhi mama mkwe wake, ataendelea kulipa...

    "sasa mama, mimi naomba niwaache na mgonjwa... Mana nikiendelea kuqepo hapa mtahisi labda nawasimamia... Naombeni nirudi Arusha"

    "ina maana hata nyumbani hufiki"

    "hakuna shida mama... Nyumbani kupo tu, na kufika ni lazima.. Lakini wacha tukaangalie na biashara zinakwendaje"

    "aaahh sawa mmetukuta na mgonjwa wetu, kisha mnatuacha na mgonjwa wetu.. Sawa, nitakujulisha hali yake inavyoendelea"

    "sawa mama... Haya kwaherini jamani... Ila mama, akipata nafuu, unaweza kumruhusu aje, mana shule zimeshafunguliwa, akamalizie mwaka wake wa mwisho"

    "sawa mwanangu atakuja"

    Mama yake rahim nae hakutaka kukaa, kaona mama mkwe nuksi huyu hapa hapakaliki tena, kwasababu bibi yale rahim kesha chafukwa na roho, hivyo hataki kikaragosi chochote cha kutokea mjini,..

    "ufyyuuuuuuu... Afadhali wameondoka"

    Aliingea mama yake zena huku akishusha pumzi kubwa mno...

    "aahhh washenzi tu hawa... Wanadhani pesa ni kila kitu kwao, wamesahau kuwa kuna utu ndani yake"

    "alafu mama rashidi... Ina maana huyu mtoto bado anasoma"

    "ndio.. Si unajua mambo pesa,.. Sijui wanataka awe nani.. Wanashindwa kumpa malezi bora ya kuishi na kila mtu, wanampa elimu bora ya kumdharau kila mtu"

    "mmmhhh lakini... Mama umejitahidi"

    "we acha tu"



    BAADA YA WIKI MBILI KUPITA....







     





    Na sasa ni wiki ya tatu sasa rahim hajui pombe, na kila akiumwa anapelekwa hospitali,.. Wakati huo alikuwa sio wa kukaa mbali na hospitali, mana vikimuamka tu kuna dawa anapewa inayomtuliza kwa wakati huo,.. Hivyo muda wote yeye yupo na zena tu, na wakati huo zena kapata nafuu... Mgonjwa anapona bila kupewa dawa wala nini,.. Inashangaza sana,.. Lakini sasa licha ye zena kupata nafuu, pia rahim alikuwa akimtoa nje ya hospitali na kumpa mazoezi, mana naye rahim ni mgonjwa wa muda wowote ule,... Na uzuri sasa zena alipoanza kupata nafuu alikuwa anatamani kwenda madrasa,.. Na wazazi hawakuwa wakimkataza, ila mtu wake wa karibu alikuwa ni rahim kwa kumsindikiza taratibu... Yapata wiki moja toka waanze hilo swala,... Na hawaendi ule msikiti mkubwa,.. Mana kuna kaumbali kidogo... Sasa wiki hii wanapanda usafiri kabisa kwenda kule msikiti mkubwa,... Sasa leo ndio wamenza kwenda msikiti mkubwa kwa kupanda usafiri, na wakitoka huko ni hospitalini,.. Hata rahim alikuwa keshazoea mazingira ya msikitini, mana alikuwa akimsindikiza zena wiki moja iliopita, ila yeye hakuwa akiingia msikitini



    Sasa wakiwa jirani na msikiti huo, ule ambao rahim alipeleka jenereta, na kuleta shida,.. Na hapo alikuwa anamsindikiza zena akaswali,.. Na hio ni moja ya mazoezi na ndio mana rahim yupo nae, mana rahim ugonjwa wake ni wa kumjia tu pale mishipa inaposumbua kutaka pombe... Sasa njiani wakiwa hapo hapo maeneo ya msikitini,... Walikutana na fadhila

    "heeeeeee zena... Naona unapata nafuu kidogo, mpaka umekuja huku"

    Aliongea fadhila huku akimkumbatia rafiki yake,...

    "ndio.. Nimeona nifanye fanye mazoezi, ili nikija kuongezewa damu isinipe shida, mana ni damu ya kiume"

    "jamani zena... Ila umeumwa muda mrefu kweli, yapata mwezi sasa"

    "mmmhhhh bado bwana... Bado kama wiki moja ifike mwezi"

    Fadhila akikutana na zena akiwa na rahim, fadhila anajifanya hamjui rahim,...

    "rahim... Naomba niongee na fadhila dakika moja tu"

     Zena alimtaka rahim awaache kama dakika moja hivi waongee,... Rahim siku hizi ni mstaarabu sana, na hana makuu kivile... Aliondoka na kwenda kukaa pembezoni mwa msikiti, sasa hivi hasemi mambo ya uchawi tena..

    "fadhila, ivi kwa akili yako yooote, unadhani mimi naumwa"

    Fadhila alishangaa kuskia maneno hayo kutoka kwa zena,.. Na hata sisi wasomaji ndio kwanzaa tunalijua hilo

    "una maana gani zena"

    "sikiliza.... Huu ni mpango wa familia yetu na yao... Kinachotakiwa ni rahim aache pombe.. Hivyo mimi siumwi hata tone la ugonjwa,.. Sina hata mafua.. Mzimaaa na hata wazazi wake wanajua... We si unamuona alivyotulia, na hapa bado wiki mbili tu asahau pombe, mana zinatakiwa wiki tano, na hii ji wiki ya tatu"

    "zena unasema kweli?"

    "haaaaa... Sasa nikudanganyie nini.. Mimi siumwi, nilijifanyisha tu, na kwakua ananipenda, amekubali kutokunywa pombe ili aniongezee damu... Na mimi jinsi ninavyompenda na kumtaka abadirike, ndio sababu ya kuigiza kama vile naumwa hoi... Mpaka nawekewa mipira ya kupumulia lakini yote ni kumtaka rahim aache pombe na ni kweli sasa anaendea kusahau"

    Sasa kumbe zena alichokifanya sio sahihi, kutoa siri iliotunzwa ndani ya wiki tatu mfululizo,.... Ukumbuke kuwa fadhila anampenda sana rahim, hivyo kuambiwa maneno hayo, tayari na yeye keshapata njia.... Na haya ni maneno aliokuwa akijisemea kimoyo moyo akiwa hapo hapo na zena kuwa



    "kuuuuumbe... Sasa ngoja nimwambie rahim ukweli kuwa anateswa kutokunywa pombe bure tu, lakini zena haumwi wala nini... Hivyo nitamshawishi aendelee na pombe"



    Maneno ya fadhila hayo aliokuwa akijisemea mwenyewe katika moyo wake

    "kwahio zena... Yule akiacha pombe anakuoa au"

    "sasa swali gani hilo zena.... Pigia mstari tu,.. Mimi na rahim tunapendana sana tu"

    "Eti eeee... Kwahio akirudia pombe je? Utaendelea nae"

    "Kiukweli, hata wazazi wangu hawatompenda tena... Japo roho itaniuma lakink sina budi kuachana nae mana wazazi hawatotaka niwe nae"

    "kumbe??.... Basi jitahidi"

    Fadhila alikuwa akiitikia kinafiki tu, lakini. Alichokipanga katika moyo wake, ni pigo kubwa sana kwa zena

    "ndio hivyo.. Na bado wiki mbili tu"

    Zena yeye anaongea tu lakini hajui kuwa fadhila keshachukia, hivyo atamvizia rahim ampe ukweli wote, kumbe zena sio mgonjwa wala nini.



    "we jishaue tu na kujifanya kwako unaumwa... Na nita hakikisha anarudia pombe kama zamani.. Ili umkose"



    Fadhila aliendelea kujipangia mambo yake kimoyo moyo bila ya zena kujua chochote kile..... Masikini ya mungu zena kajikakamua kuwa mgonjwa ili rahim aache pombe, anaendea kufanikiwa,. Mara kidudu fadhila huyo kaja kuharibu mipango yote....







    Sasa leo ndio tunajua kuwa zena hakuwa akiumwa, bali alikuwa akijifanyisha ili kumfanya rahim aache pombe, na yote hio ni kwasababu ya upendo juu yao,... Zena alikubali kutungikiwa madripu bandia mipira iliompitia kila mahala, unaambiwa hata kula alikuwa akila kwa mipira, na ikifika muda rahim hayupo, anaamka na kula chakula kama kawaida, ila saa rahim yupo anakula kwa kutumia mipira, kitu kilichomfanya rahim aamini kuwa zena ni mgonjwa na kukubali kuacha kunywa pombe ili baada ya hizo siku atie damu amwongezee zena,... Lakinu kadri siku zilivyozidi kwenda, zena aliambiwa kuwa apate nafuu, ili aanze kumzoesha rahim katika nyumba za ibada, kwahio zena akajifanya anataka kufanya mazoezi lakini mazoezi yake hua anakwenda msikitini, na mtu wa karibu yake ni rahim, mana rahim sio mgonjwa ila ugonjwa wake ni mishipa kuvimba kwa ghafla pale inapotaka kupata pombe,... Kwahio mpaka sasa hivi rahim anajua, ana mpango wa kutoa damu, kumbe hakukuwa na lolote sema ni njia ya kumfanya aachane na vinywaji aina hio...



    Walipoanza mazoezi yao hawakuwa wakienda mbali, mana palikuwa na msikiti wa jirani na hospitali hio,.. Na rahim kazi yake ni kumsindikiza zena mpaka msikitini kisha rahim anakuwa anabaki nje, zena akitoka wanarudi hospitali, yaani ni msikitini to hospitali,... Lakini sasa leo wakabadili msikiti, wakaenda msikiti wa mbali, ambao wanautumia akina zena, ila ni mbali kwakuwa ni kutoka hospitali mpaka huko,.. Ila ni karibu sana kwa kule mtaani kwao.. Walipanda usafiri mpaka pale...



    Walipokuwa wanashuka walikutana na fadhila, zena akamwomba rahim aondoke ili zena na fadhila waongee, na hapo ndipo zena akatoa siri zote walizokuwa wanafanya, lakini sasa kumbuka fadhila anampenda sana rahim, hivyo alipoona kuwa fadhila anakwenda kufanikiwa jambo lake,.. Mana rahim akikubali kuacha pombe, ni kwamba atakuwa ni mpenzi wa zena, lakini akikataa kuacha pombe, basi zena hatompenda mana hata wazazi wake hawatompenda rahim.. Hivyo fadhila akabuni njia ya kumwambia rahim kuwa zena haumwi wala nini.. Nia yao ni kukutesa tu usijipe raha.. Mana fadhila yeye hajali hata kama rahim ana hali ya starehe, kikubwa ampate tu,...



    "we jishaue tu na kujifanya kwako unaumwa... Na nita hakikisha anarudia pombe kama zamani.. Ili umkose"



    Alijiongelea fadhila kimoyomoyo huku akiondoka baada ya kuswali swala ya Adhuhuri mana time hio ilikuwa kama saa nane hivi za mchana,... Lakini zena baada ya kuachana na fadhila alimfuata rahim na kumwambia kuwa

    "mimi nilidhani umeingia msikitini kumbe upo nje"

    Aliongea zena huku akikaa nae, na rahim sasa hivi mazingira ya msikitini keshayazoea mana sio mara ya kwanza kuletwa huku japo anaishia nje,...

    "sasa nitaingiaje na wakati sina kanzu"

    "heeeeeeee nani alikwambia msikitini lazima uwe na kanzu"

    "si nawaona haoooo wote wamevaa kanzu"

    "wamependa tu kwakuwa ni vazi muhimu zaidi lakini kama huna huezi kusema huingii... Hata mimi nikikosa hijabu naweza vaa hata kanga na nikaswali"

    "waaapi nakuona kila siku nguo nyeusi tu"

    "sawa.. Hili ni vazi la kunisitili na maungo yangu... Anaeweza kuniona ni wewe tu na sio mwingine... Twende tuingie"

    "mmmhhh zena we nenda tu... Mi sijui hata kuinama wala kuinuka.. Mi nawaona tu.. We nenda mi nakusubiri hapa"

    Sasa zena akawaza ni kweli rahim hajui chochote kile, anaweza kwenda huko akajikuta kakaa tu au kasimama tu,.. Hivyo aliona afanye jambo moja...

    "simu yako ina salio kidogo"

    Zena alimuuliza rahim kama simu yake ina salio... Mana zena hana simu

    "ndio..."

    "naomba tumpigie kaka sulesh aje hapa"

    "aje kufanya nini tena"

    "we andika hii namba"

    Zena hana simu na hajawahi kumiliki simu, ni wazazi wake na kaka yake tu basi, lakini yeye hajawahi na wala hatamani kabisa,.. Wakati huo msimu wa rahim ni dude kwelikweli, kubwaa hata mfukoni halikai vizuri,...

    Rahim aliandika namba za sulesh ambae ni bwashee wake, kisha akampa zena mana ndio anamjua vizuri kaka yake

    "haloo kaka.. As Salaam Aleykum"

    "waaleyku msalam nani mwenzangu"

    "zena"

    "aahhhh habari yako"

    "salama tu... Kaka nipo hapa nje ya msikiti sjui unaweza kuja"

    "sawa nafika hapo mara moja"

    Rahim alikuwa katulia tu hajui aanzie wapi aishie wapi kuingia huko msikitini, mana hata kuitikia salamu yenyewe hajui



    Punde sii punde sulesh kafika,..

    "hali yako ndugu"

    Sulesh alimsalimia rahim mana anajua hata ukimpa salamu ya dini hajui kuitikia

    "salama tu sjui wewe"

    "aahh tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa rekhema zake"

    Basi sulesh alimgeukia zena ambae ni ndugu yake



    "enhee Unasemaje"

    "kaka... Nadhani unajua kinachoendelea.. Sasa ndio tumeanza hivi"

    "aaaaaaaaaaa... Sawa sawa kabisa.. Inshallah... Mnaweza kuja pale bandani"

    Msikiti huo una majengo madogo madogo mengi tu, kwa ajili ya wanafunzi kujifunza Qur-aan, ila kuna majengo ya watu private, yaani kuna watu wazima walioona wamrudie Mwenyezi mungu, hivyo kabla hawajawa changanyikeni basi wanaanza kupigwa msasa kivyao vyao,... Hivyo rahim na zena waliingia katika jengo moja na sulesh akiwa kama mwalimu, na hapo rahim hajui kinachoendelea,... Walikaa kisha zena kamwambia kinachoendelea hapo

    "rahim... Mimi napenda uwe mpenda watu, nataka uwe mpenda dini... Nyumba hizi ndio sahihi kwako.. Na sio zile ulizokuwa unakwenda na kumwaga pesa zako bure na kufanya vitu vya ajabu ajabu... Mimi naomba tuwe tunakuja kusoma wote hapa, tujifunze mambo ya mungu... Ukumbuke hapo ulipo una pimzi wewe, hebu Jiulize hio pimzi umeipataje pataje... Ukumbuke duniani kuna maskini na tajiri,.. Na Mwenyezi Mungu akimpa mtu utajiri, maana yake ni kwamba amsaidie na yule masikini.. Kwakua hujui kitu chochote cha dini, naomba tuwe tunafundishwa wote hapa, utajifunza jinsi ya kuswali na taratibu zake, na dua zake,... Yaani kila kitu utakijua... Kikubwa ni kunikubalia tujiungea wote.. Fanya yalio mema rahim, pesa hutokufa nazo.. Utaziacha na watafaidi uliowaachia na wewe utakwenda kupata adhabu za kaburini.. Wakati wenzako wanatusua pesa zako tu... Kwanini usijijengee misingi ya maisha ya peponi, tumia pesa zako vizuri... Ondoa ule usemi usemao et TAJIRI NI VIGUMU KUPITA KWENYE TUNDU LA SINDANO... we ulifikiri kauli ile ina maana gani kama sio uharamia wanaufanya matajiri... Rahim, umejaaliwa elimu ya duniani... Rahim umejaaliwa kipato cha duniani, rahim umekosa elimu ya Mwenyezi Mungu.. Rahim amekosa hata kujua swala inaanza vp.. Hivi utakwenda kumwambia nini Mwenyezi Mungu.. Au wewe hutokufa??...pesa, Starehe, majumba, hizo meli zenu, magari yenu, makampuni yenu.. Yote utayaacha, je nani atakutengenezea maisha ya peponi?...jitengenezee mwenyewe ingali upo gai.. Zile nyumba unazokwenda sio sahihi kwa wewe... Pombe sio kinywaji chako, na kwa Mwenyezi Mungu hujachelewa, mpaka sasa bado una nafasi ya kurudi..... Nia yangu kuja hapa nataka ujue nini maana ya maisha ya duniani.. Na kesho peponi.. Na pesa yako ndio itakayo kuokoa na ndio itakayo kuteketeza jahanamu... Siwezi kuamini kuwa pesa zako ndizo zitakazo kuchoma kesho.... Rahim nakupenda sana, ila nataka ubadilike, nataka uwe mtu wa watu rahim, njia ulio nayo sasa sio.. Unapotea na bado ni kijana mdogo.. Ukumbuke kunyimwa kwa fukara, ni ili wewe uje umpe, na angapewa yeye, wewe ungekosa... Sasa kwanini hufanyi hivyo... Benki zenu zinafanya kumwagikia pesa.. Hata sadaka za Mwenyezi mungu hujawahi kutoa rahim... Rahim, nakuombea kwa mungu aweze kukuongoza katika njia sahihi, na sio hii ulioko nayo kwa sasa... Mi nao.. Mi nao... Naooo.. Naomba u..... Uba.... Ubadirike rahim"







     





    Zena aliongea maneno mengi sana mpaka hali yake ikaanza kuwa mbaya, lakini hapo sio kuwa hali ni mbaya, bali ni moja kati ya maigizo yake, ya kujifanya anaumwa,.... Lakini sio kuwa ana hali mbaya,...

    "zena... Pole"

    "uuuu... Umeniskia.. Nilichosema"

    "ndio... Nimekusikia"

    Zena alifurahi sana kuona bado rahim kawa mpole,...  Na hakujibu vibaya

    "sitaki tena unywe pombe rahim"

    Aliongea zena huku akijifanya kabanwa na mafua ile mbaya, lakini hakuna lolote,...

    "nitaangalia.. Wacha kwanza nikutolew damu, afu nitajua cha kufanya"

    Zena kuskia hivyo, alijua mpaka hizo siku ziishe, yaani hizo wiki mbili, lazima rahim asahau kunywa pombe,. Sasa sulesh alianza kazi yake mana hata sulesh anajua kinachoendelea, hawataki kumtasa mdogo wao zena, hivyo kama kapenda basi apende ila mtu huyo abadilishwe tabia,... Na uzuri ni kwamba hata mlevi anapenda, hivyo kupenda kwa rahim ndiko kulikomponza mpaka kujikuta akianza kuisahau pombe....



    BAADA YA WIKI MOJA KUISHA



    Imebaki wiki moja tu Rahim amtolee damu mpenzi wake,... Lakini tumeshajua kuwa zena haumwi na wala hahitaji damu,.... Huezi amini sasa hivi rahim wala hata hatamani pombe, na hata ile hali inayomjia ya kuvimba mishipa kwa kukosa kinywaji hicho,... Zena akiwa yupo kitandani akiwa anaendelea na hali yake ya kuumwa, aliulizwa mama yake, na wakati huo bibi yake rahim yupo hapo

    "we, huyo rahim anaendeleaje? Au bado anawaza ulevi tu"

    "hapana mama... Sasa hivi hata kuswali anajua... Na alikua hajui hata kufunga swala, yaani hata kuitikia salamu hajui... Lakinj sasa hivi, anaswali tena hata peke yake.. Na uzuri ni kwamba rahim ana kichwa chepesi sana sema pesa zilikuwa zikimharibu sana... Kiukweli mama, rahim sasa hivi ni mtu mzuri sana.. Na hata leo anataka nimpeleke mjini akanunue kanzu.. Mana anasema bila ya kanzu, haendi kuswali msikiti mkuu"



    "kwanini hataki kwenda huko"

    "eti kila anaemuona ana kanzu sasa yeye atatia aibu"

    "ina maana hujamwambia kuwa kanzu sio lazima"

    "nimemwambia kila kitu.... Ila anasema anaogopa kwenda pale msikiti mkuu"

    Zena alimwambia mama yake na bibi wa rahim kuwa rahim anaogopa kwenda msikiti mkuu..

    "kwasababu gani aogope kwenda"

    "eti kwasababu ya siku ile kukataa kuacha lile jenereta, sasa anaona aibu kwenda pale"

    "lakini si mnaendaga nyie"

    "ndio.. Ila tunaishia kule kwenye majengo madogo madogo"

    "akija hapa, umpeleke mkanunue hio kanzu, kisha umpeleke pale pale waumini wote wamuone na aombe radhi... Na atubu mbele za Waislamu wenzie"



    Wakati huo rahim yupo nyumbani, baada ya kuambiwa akalete matunda matunda ya mgonjwa,... Akiwa ndio anajiandaa kutoka ili aelekee mjini, na wakati huo anatumia gari yao ya kifahari,... Huezi Amini hata kwenye gari kaning'iniza kidani chenye maneno ya Qur-aan, yaani ni kweli rahim kaanza kubadirika haswa,..



    Lakini sasa alipokuwa njiani, alikutana na fadhila,

    "shemuuuuu..... Jamani shemuuuuu"

    Aliita fadhila, na rahim akasimamisha gari

    "aahhh fadhila? As Salaam Aleykum dada angu"

    "heeeeeeee Waleykhu msalam khaifah"

    "Allhamdulillah, namshukuru Mwenyezi Mungu anafanya wepesi"

    Fadhila haamini kama rahim ndio anajibu hayo maneno,... Yaani alijua rahim atakuwa mgumu kujua mambo hayo, lakini ndio kawa mwepesi ndani ya wiki mbili tu....

    "haya, mgonjwa wako anaendeleaje"

    Fadhila aliuliza kiunafiki, japo naye anajua..

    "ndio mana nikakwambia, Mwenyezi Mungu anafanya wepesi juu yake... Allhamdulillah kwa sasa hayuko mbaya.. Na hapa nakwenda kumchukulia matunda akaongeze afya... Mana kuumwa sio mchezo fadhila"

    Aliongea rahim huku akiwa na sura ya kufurahi tu, yaani ana furaha muda wote...

    "kwani anaumwa nini"

    "heeeeeeee fadhila??... Acha utani bwana ina maana unajifanya hujui kuwa fadhila anaumwa nini"

    Sasa nia ya fadhila anataka kumpa ukweli rahim kuwa fadhila haumwi,..

    "sikiliza rahim... Mimi binafsi nakupenda sana rahim... Na kuhusu zena sio mkweli kwako rahim"

    "una maana gani fadhila... Mbona sikuelewi"

    "kama zena ni mkweli kwako.. Asingekudanganya kuwa anaumwa na kukukatia starehe zako... Mi nashangaa pesa zako lakini unapangiwa matumizi.... Yule mtoto wa kisambaa, kakueka mkononi hujui tu.... Sasa kama huamini uliza vizuri zena anaumwa au anakuigizia tu wewe, ili akulie hayo matunda yako.. Hebu angalia sasa hivi kiduka chao kinaanza kujaa, lakini bado hushtuki tu kuwa pesa zako zinaliwa bila wewe kujua... Unaliwa pesa zako shituka rahim, zena haumwi anawalia pesa zenu tu... We uliona wapi kemikali ya pombe ikakaa mwezi na siku saba???....Shituka rahim wewe mtoto wa kiume, na hapo ulipo umewekwa kiganjani sema hujui tu.. "



    Fadhila alimaliza kuongea, wakati huo rahim, kavuta mdomo... Huku mashavu yakimtetemeka....

    "ina maana mimi nalipia matibabu kila kitu... Kwa siku karibia laki nzima inaisha, kumbe haumwi??"

    "Sasa unaniuliza au unapigia mstali... Hilo ndio jibu na sio swali tena"

    "kumbeee??"

    "yaani sasa hivi anachokifanya zena, ni wewe uwe mpole ili ale pesa zako vizuri mana utakuwa sio mkali tena.. Mana mwanaume akinywa pombe anakua mkali, sasa anakushawishi uache pombe ili uingie kwenye anga zake.. Mana hatoweza kukueka kiganjani ukiwa mlevi.... Na sasa ndio unaingia sasa kwenye kumi na nane zake... Utakoma baba, mwaka huu wako, nakupenda na nimediriki kukupa sehemu zangu lakini bado hunioni tu... Na ukiacha pombe, utajiju, anazichukua zote"



    "Fadhila.... Basi basi..... Nitakutafuta niongee nawewe vizuri... Lakini kumbe ulilijua hilo mapema kwanini usiniambie Fadhila??"

    "sasa we upo nae kila saa, mimi nitawezaje kukuambia?"

    "kwahio zena anataka kuniweka kiganjani mimi"

    "tena sio kidogo... Afu ana hasira na siku ile ulivyokuwa hutaki kuacha lile jenereta kule msikitini"

    "Alaaaaaaaaaaaaaa....  Acha utani fadhila"

    "Nakwambia usipokuwa makini, hata kufa utakufa jamani rahim wangu, si uachane nae, au kale kaweupe ka dukani ndio kanakuchanganya"







    Kwa maelezo ya dokta pale alipoulizwa kuwa binaadamu anaetumia kilevi kama chakula, ili aache kunywa atatakiwa kukaa kwa muda gani na aweze kusahau kabisa,. Dokta akasema kuwa, kumwachisha mtu pombe kwa haraka haraka ni kitu kigumu sana, ila pia ni kirahisi kwasababu ya kitu fulani,.. Kwa kawaida mlevi kuacha inabidi apunguze kunywa pombe taratibu, kwa mfano jamali kaka yake rahim, kataamka kupunguza, lakini ipo siku ataacha kabisa, kwasababu kuacha kitu kunatokana na nia ulioinuia moyoni mwako,.. Na pia mtu aliozoe pombe akija kukaa wiki moja bila kugusa kinywaji hicho, basi ni lazima viugonjwa vya hapa na pele vimjie kwasababu ile mishipa ilio zoea pombe inatoa zile kemikali zilizobaki hivyo lazima nguvu zikuishe... Na hapa naelezea walevi na sio wanywaji, mana kuna walevi na wanywaji... Na mtu akisema anapunguza kunywa pombe, basi nafasi anayoishika ni nafasi ya mnywaji... Kutoka mlevi,.. Kwahio hapa naelezea mlevi yaani wale walioshindikana, siku haiishi bila kupata, na akikosa ni maumivu kwake, lakini mnywaji anaweza kukaa hata siku tatu bila kunywa na akawa sawa tu.. Mana yeye sio kuwa anataka kila siku, bali wanasema kutoa loku tu basi...



    Sasa dokta alisema, rahim ili aweze kuacha pombe atatakiwa kuacha taratibu, lakini papo hapo familia ikadai kuwa kuna mtu anampenda sana, afu pia rahim ni mwepesi wa kutoa damu ili kumseidia mtu yeyote yule,.. Hivyo tukiitumia njia hio, huenda ikamseidia rahim kuacha pombe, hivyo waliianza kama kujaribu tu... Na dokta alisema akifikisha siku 37 bila kugusa pombe, basi hapo hatokaa kugusa pombe labda aanze upya, mana vile vimelea vinavyohitaji pombe mwilini vimeshakufa kwa kukosa taratibu zao za pombe, hivyo akinywa hapo kaanza upya, lakini kushawishiwa na mwili ni ngumu.... Jaribio hilo hawakuamini kama lingefaa, lakini wiki ilipoisha ndipo wakajua kumbe kweli rahim anampenda zena na yupo tayari kumwongezea damu,...



    Sasa rahim keshafikisha siku 30, kasoro siku 7 tu, anakutana na fadhila mwana izaya asiekuwa na haya na asiojua kibaya... Akaanza kumpa siri yote juu ya zena kuumwa kwake, kuwa hio ilikuwa ni triki ya yeye kuacha pomne na sio kuwa zena anaumwa,.. Tena fadhila hakuishia hapo aliongea na maneno mengi sana juu ya zena, mpaka akamuingiza mwenzie kwenye ushirikina kuwa anataka kumweka rahim kiganjani, mara anakula hela zake tuuu... Rahim yote hayo alikuwa hayajui, lakini leo ndio kayajua... Nani alikuambia wana ndoa huachana hivi hivi??????.... Lazima kuwe na mtu nyuma yake, hawawezi kuachana hivi hivi bila sababu...



    "Alaaaaaaaaaaaaaa....  Acha utani fadhila"

    "Nakwambia usipokuwa makini, hata kufa utakufa jamani rahim wangu, si uachane nae, au kale kaweupe ka dukani ndio kanakuchanganya?"



    Aliongea zena kuwa labda rahim anachanganywa na huo weupe wa dukani alionao zena, au inakuwaje..

    "fadhila, please please.. Naomba niwahi hospitali kwanza.. Yaani nikifika navuruga wote"

    Aliingea rahim huku akiwa na hasira ya kuua hata mtu,..

    "sawa, we wahi tu... Lakini jua nakupenda rahim"

    "tutakuja kuyamaliza... Sio kwa utamu ule nikuache aisee"

    Aliongea rahim huku akiondoa gari kwa haraka ya kuwahi hospitalini,.. Huku nyuma fadhila alikuwa akijisemea kuwa.

    "safi sana... Tayari nimesha mpasha moto, sasa zena imekula kwake, rahim ni wangu tu,.. Wacha ajishauwe kuwa mgonjwa, na sasa atakiona cha moto"

    Fadhila aliongea hivyo huku akiondoka zake....

    Sasa rahim alikuwa akielekea hospitali, Lakini cha ajabu, hakupitia huko, kitu cha kwanza alipitia sokoni kwanza akanunua matunda yaliohitajika, na hayo hayo matunda anataka yawe mtego kwa zena,..

    "Kwanini anifanyie hivyo mtoto wa mwenzie, pesa zangu, mdomo wangu, dhambi ni zangu, sasa yeye vinamuhusu nini, kama ni kunipenda angenipenda tu kwanini astopishe starehe zangu?? naumwa mishipa inanitoka nikitarajia kumseidia mtu, kumbe ni hewa"



    Aliongea rahim huku akikusanya matunda kwa hasira,... Alipomaliza kukusanya matunda, alilipia gharama zote,... Lakini sasa ujue kuwa kweli fadhila hakuwa mtu mzuri, rahim kapitia Supermarket kubwa mjini hapo, na kuenda upande wa vinywaji, kama kawaida yake, kachukuwa ile wine ya bei ghali, kisha akaenda pale kaunta...

    "bei gani hii dada yangu"

    Aliuliza bei ya wine hio, mana ilikuwa ni wine toleo jipya, mana ni nyeupe tofauti na zingine zilizo kama chai, sasa hio ni nyeupe inaendana kidogo na maji, lakini ni wine aina mpya...

    "hio ni laki tatu"

    "waoooo... Advantage Price for me"

    Rahim aliona ni bei rahisi sana kwake, kwani aliingiza mkono mfukoni na kutoa waleti kwa furaha, mana leo ndio kwanzaa anaanza kurudia starehe zake, baada ya kupewa ukweli wote...

    "brooo, unasema Advantage Price for You, wakati mimi nimeishindwa kuinunua"

    Alikuwa ni jamaa mmoja aliokutana nae hapo kaunta, nae pia alikuwa akinunua vinywaji vidogo vidogo kwa ajili ya nyumbani kwake,...

    "kwahio, unaniambia unapenda sana hii wine mpya"

    Aliuliza rahim huku jamaa akijibu kwa furaha

    "yes... Kwasababu ile wine ya zamani ndio Nilikuwa nagonga mimi.. Sasa leo nikaiona inatangazwa kwenye TV, nikasema siiachi hii.. Lakini huezi amini nimeiacha kutokana na bei"

    Rahim alicheka sana kusikia mtu anashindwa kununua kitu kwasababu ya pesa, alimuona yule jamaa ni masikini sana kwa kushindwa kununua wine hio... Sasa dharau za rahim ndio zinarudi upyaaaaaaaaaa







     





    Rahim akiwa barabarani, hata gari hakuwa akiendesha vizuri, tena wakati huo ule mchupa wa wine upo katikati, ina maana tayari keshaunywa nusu yake,... Macho ya rahim sio yale tena, yalikuwa kama yanataka kudondoka vile, wine mpya huja na mambo mapya,.. Rahim mpaka hospitalini, gari yenyewe kuisimamisha imekuwa tabu, mpaka anataka kukanyaga wamama wa watu,...

    "huyu mkaka vipi mbona anataka kutugonga"

    Aliongea mama mmoja aliokuwa mja mzito,

    "unasema we mwehu"

    Wenzake walivyoona rahim anamrudia yule mama, walimtoa mana rahim hapo kinachomfanya awe hivyo ni pombe, na ndio karudia upyaaa,.... Wakati huo akina zena hawajui hili wala lile, tena walikuwa wanapiga stori za rahim...

    "hizi zena... Kama rahim atatulia... Utakubali kuolewa nae"

    Aliuliza bibi yake rahim, huku mama zena katulia tu kimyaa

    Zena anajiskia aibu sana, mana hajaamini kama naweza kuolewa na mtu ampendaye na mbaya zaidi hata rahim anampenda zena,...

    "bibi, mimi sina pingamizi kama mama na baba watakubali"

    Aliongea zena huku akijificha kwa aibu, na ukumbuke zena haumwi wala nini,..

    "we zena wewe, hebu acha dhambi zako, kama sisi hatupendi uwe na rahim, tusinge kuruhusu kuwa nae hata kwa sasa... Kwa nafasi uliofikia kwa rahim basi sisi hatuna shida... Ruksa tu, na hata baba yako kakubaliana na hilo, mana kusikiliza ushauri wa sulesh kuwa huu sio wakati wa kuchaguliana waume, ilimradi wamependana basi"

    Mama zena aliongea hayo, na kumfanya zena atokwe na machozi ya furaha juu ya uamuzi wa wazazi wake kukubali kuolewa na rahim..  Masikini ya mungu wao wanapanga hili kumbe rahim anakuja na hili,... sasa zena alisikia sauti za wamama wanapiga kelele huko nje, tena walikuwa wakitukana sana juu ya mlevi huyo,...

    "mbwa wewe, unakunywa mipombe yako huko unakuja kutudondokea sisi.. Mshenzi wewe"

    Wakati huo rahim kudondoka chini, lakini chupa ya wine nzimaa na uzima wake, tena ina wine nusu..

    Sasa huku ndani zena anazidi kulaani walevi

    "yaani mama ninavyochukia walevi.. Hebu sikia huyo baba huko sijui kamfanyeje mke wake"

    Zena aliongea akizani labda ni mlevi fulani tu kaja hospitali kwa mke wake,.. Kumbe sio cha nani wala nani, ni rahim wake huyo huyo, aliomkalia ugonjwa ndani ya siku 30 ili aache pombe na leo kapata ukweli, karudia pombe upyaaa... Tena bora hata zamani, mana wine za zamani zilikuwa zikiuzwa laki moja, zingine laki mbili.. Sasa hii mpya ina ukali wake, inauzwa laki tatu...

    "we mama ntakutia teke la tumbo"

    Aliongea rahim huku akijitahidi kuamka,...

    Sasa kule ndani zena kasikia sauti ya rahim

    "mama, huyo sio rahim kweli, mbona ni sauti yake"

    Zena alimuuliza mama yake huku mama akicheka na kusema kuwa

    "hahahahah, rahim sio rahisi kulewa.. Kwa elimu ya dini alioipata kwa kifupi hawezi kuwa hivyo"

    "mamaaa... Atakuwa ni yeye tu"

    Wakati huo huku nje, rahim kakazana kutishia watu

    "ntaua mtu nyie... Tena ntaua wawili wawili, mama na mtoto wake... Njoo sasa"

    Macho haya amki kwa kuzidiwa na kilevi,.. Huku ndani zena anajikongoja kutoka, ili kama ni rahim basi aendelee kujua kuwa bado anaumwa, mana anajua rahim hajui mpango unaoendelea hapo...

    Masikini ya mungu zena hajaamini kumuona rahim ndio anadondoka na chupa ya wine... Zena alirudi wodini haraka huku akimlalia mama yake, na wakati huo rahim nae ndio anaingia katika wodi hio,.. Mama zena haamini, bibi yake mwenyewe haamini kwa kile alichokifanya rahim

    "mama... Naomba unisamehe mama yangu,.... Nilikuhakikishia kumfanya rahim aache pombe ili awe mume wangu,.. Lakini kumbe ilikuwa ni ngumu... Mama nisamehe mama yangu... Simtaki tena mama simtaki"

    Aliongea zena na wakati huo hatamani hata kumwangalia rahim,.. Bibi yake rahim aliamka na kumchapa rahim kibao, huku akisema

    "mtoto wa watu akupende vipi.. Siku 30 kazungushiwa mipira hapa ilimradi uache pombe,... Leo zimebaki siku 7, unakuja na chupa ya pombe"

    Aliingea bibi wakati huo rahim walaaa hata hasikilizi mtu

    "kwani hii si wine yangu... Matumda yenu nimeleta yapo Kwenye gari"

    Mara mzee mvungi kaingia kwa shangwe, lakini alishangaa kumkuta rahim ananing'inia na chupa ya wine, tena wakati huo rahim anapiga funda za kutosha mbele yao....

    "alafu nasema hivi.... Wewe dokta.. Nataka unipigie mahesabu ya huyu mtu kukaa hapa hospitalini,.. Nataka kuanzia siku ile ya kwanza mpaka leo... Naitaka pesa yangu,.. Mimi sijui utatoa wapi.. Nataka pesa yangu.. Unajifanya unaumwa kumbe huumwi,.. Mamilioni ya pesa yanatoka hapa kumbe huumwi... Sasa nataka pesa zanguuuuuuuu... Shenzi taipu.. Nyau wewe"

    Zena alimuangukia baba yake na kumuomba msamaha juu ya jambo hilo,... Baba haamini maskio yake kwa pesa inayotakiwa kulipwa... Ataitoa wapi, na maisha yao ndio hayo ya hali ya chini..

    "kachukueni yale Matunda muendelee kuongeza gharama"

    Aliongea rahim kisha akaketi kitandani na kukishika kile kitanda huku akisema,....

    "mgonjwaaaaaaaaa...... Mgonjwaaaaaaaaa...... Jamani mgonjwa upo wapi jamani... Jamani mgonjwa hutaki damu yangu tena "

    Sasa hapo rahim hata kuchizika kulikuwa kunakuja bila hata breki, mana anapiga funda moja la wine, huku akiita mgonjwa yupo wapi ampe damu....

    "sikiliza kijana wangu... Tupe siku mbili au tatu.. Tukauze mashamba na viwanja vyetu vyote... Tukulipe pesa yako"

    Baba zena aliongea maneno hayo kwa uchungu huku akiichukuwa familia yake na kuondoka.... Lakini kabla hawajaondoka,.. Rahim alisimama na pombe pombe zake kichwani kana kwamba kuna kitu anataka awaambie,... Lakini sasa kabla ya rahim kuongea lolote, kulisikika sauti ya kizibo kilicho dondoshwa makusudi na rahim, huku familia ya mzee mvungi inageuka na kuangalia kulikoni kwa kelele hizo...

    Zena ndio wa kwanza kuona kizibo kile,... Lakini sasa kumbe kizibo hicho hicho kina maana kubwa tu,.. Mana zena alipokiona alitikisa kichwa, kumaanisha kuwa hakubaliani na kizibo hicho....







    Rahim ni kijana mwenye akili nyingi sana, na ni msomi asieweza kusikiliza maneno ya mtu, kwasababu siku zote pombe hukatazwa, licha ya dini zote kukataza unywaji wa pombe, bali hata kiakili na kiafya hushauriwi kunywa pombe hata siku moja,.. Hivyo ni vitu vyenye athari katika mwili wako,..



    Rahim ni mlevi haswa na sio mnywaji, na ulevi wake hajauanza leo, yaani toka yupo shule za sekondari alikuwa ni mtu wa ulevi kwasababu kwao kuna pesa, walimu wamechapa mpaka basi, wazazi wake wameongea mpaka basi, wakaamua kumuacha kama anavyotaka,.. Lakini kumbuka kuna usemi uliosema kuwa ASIEFUNZWA NA MAMAE HUFUNZWA NA ULIMWENGU,.. Rahim alipokuwa shuleni alikuwa mzuri sana kwenye masomo, na kama sio pombe basi angelikuwa ni mwanafunzi bora sana jijini hapo,.. Alimaliza shule ya msingi akiwa hajui pombe, ila sekondari ndio kaanza kunywa pombe, mpaka sasa yupo chuo anakunywa pombe,.. Ni mwezi mmoja tu ndio hajagusa pombe kutokana na mapenzi ya dhati toka kwa zena,.. Zena anaumwa sana hivyo anahitajika kuongezwa damu,.. Rahim analivaa jukumu la kumwongeza damu mtu ampendaye, lakini kabla hajatolewa damu ilibidi akae ndani ya siku 37 ili damu yake itakasike kutokana na kemikali za pombe kujaa katika damu... Lakini rahim anakuja kugundua kuwa kumbe zena hakuwa akiumwa bali ni njia ya yeye kuacha pombe ili waishi wote....



    Kwa Muonekano wa rahim baada ya kugundua swala hilo, alionekana kurudia tena pombe upyaaa, mana alikua hanywi kwasababu ya mtu fulani, sasa leo kugundua kaamua kunywa kabla ya siku saba kuisha,.. Rahim aliingia katika wodi aliowaacha akina zena waliokuwa hawajui kama rahim keshagundua kuwa huo ugonjwa si ugonjwa bali ilikuwa ni njia tu... Rahim aliwataka wazazi wa zena walipe gharama zote toka wanaanza kuwepo hapa,... Wazazi wanakubali kwenda kuuza mashamba yao na viwanja vyao ili kulipa gharama hizo,.. Zena alijuta kitendo cha kumwamini rahim kwa kiasi kikubwa namna hio, mpaka anakuja kudai haki yake....

    "rahim unafanya nini?.. Kwa mtoto wa watu alichokifanya kinatosha... Maswala ya gharama achana nayo.. Rahim upendwe vipi mjukuu wangu.. Mtoto wa watu kajifanya mgonjwa ili uache pombe, leo umegundua sasa unataka kulipwa gharama zako... Shenzi wewe.. Nasema halipwi mtu hapa"

    Aliongea bibi huku akitaka kulia

    "mama... Wacha tumlipe mjukuu wako pesa zake... Tuna mashamba mengi, tuna viwanja kwa ajili ya watoto wetu, lakini wacha tumlipe tu"

    Mzee mvungi aliongea hivyo kisha akaichukuwa familia yake na kuondoka, lakini kabla hawajafungua mlango na kutoka... Kulisikika mshindo wa kizibo kilichodondoshwa na rahim... Kitu kilichowafanya wageuke ili kutazama nini kilicho dondoka chini....



    Zena ndio wa kwanza kuona kizibo kile,... Lakini sasa kumbe kizibo hicho hicho kina maana kubwa tu,.. Mana zena alipokiona alitikisa kichwa, kumaanisha kuwa hakubaliani na kizibo hicho....



    Kilikuwa ni kizibi cha kopo la maji ya Kilimanjaro,... Maana yake ni kwamba hapo alipo hanywi pombe bali ni maji ya Kilimanjaro,... Na ndio mana zena alitikisa kichwa kumaanisha kuwa hakubaliani na kizibo hicho kuwa rahim anakunywa maji ya Kilimanjaro,.... Itawezekana vipi na wakati tumeona rahim akinunua wine mpya kule supermarket.... Baada ya zena kukataa, rahim alimtaka zena anywe ili ajue radha yake,...

    zena anampenda sana rahim, na hata kuachana kwake ni kwasababu ya wazazi tu, lakini sio moyo wake kuamua hivyo... Na zena anajua sura ya rahim ikiwa ahaijalewa, japo sura aliokuja nayo ni ya ulevi, lakini aliibadirisha baada ya kuona familia ya mzee mvungi inakwenda... Na zena hajakataa kwenda kuonja kile kinywaji... Potelea mbali lakini kumwacha rahim hawezi...

    "we pumbavu anakunywesha pombe huyo"

    Aliongea baba yake zena huku akimzuia mtoto wake asinywe hata tone,... Lakini alichelewa mpaka zena akafanikiwa kunywa angalau funda moja la kinywaji hicho..

    "baba.. Ni kweli ni maji.. Sio pombe baba"

    Zena alimwelezea baba yake kuwa haikuwa pombe bali ni maji ya Kilimanjaro ndio aliokuwa akinywa rahim,...

    Wazazi wa zena hawataki kuamini lakini bibi yake rahim akaichukuwa ile chupa na kujaribu..

    "mbona kweli ni maji"

    Bibi nae alihakikisha kuwa ni maji,..

    "mama, unaweza kuta ni toleo jipya hilo"

    Aliingea mama yake zena kumtaarifu bibi yake rahim...

    "hapana... Ni maji, we jaribu tu"

    Bibi aliongea huku akimimina kwenye grasi,...

    "hapana mama zena usijaribu.. Labda tumuite dokta aipime"

    Aliongea mzee mvungi kuwa hataki mkewe ajaribu kama ni maji kweli ama ni pombe, mana hata mtoto wake hakutaka ajaribu, ila kwakuwa alichelewa basi akajikuta kaonja.. Dokta aliitwa na kuambiwa akipime hicho kinywaji

    "hii si wine mpya hii"

    Aliongea dokta kwa kuona chupa iliobeba kinywaji hicho...

    "we pima tuone"

    Aliongea bibi yake rahim, na wakati huo rahim katulia kimyaa hataki kusema hata neno, na sura yake ni ya kawaida tu haikuwa na hali ya ulevi wala nini... Basi dokta aliingiza kile kinywaji katika mashine zake,.. Ilichukuwa kama dakika tano hivi, kisha akatoa majibu

    "mbona haya ni maji?"

    Aliuliza dokta baada ya kupata vipimo vya kinywaji hicho...

    "na ndio maana tukakuita ukipime"

    "lakini hii chupa ni ya wine hii"

    Aliongea dokta huku akiikagua ile chuoa,

    "we rahim.. Una maana gani kuja na staili hio"

    Aliulizwa na bibi yake kwanini kaja kama anakunywa pombe







     





    "bibi?.. Nilikuwa sijui mipango yenu.. Lakini leo ndio nimejua,.. Fadhila kaniambia kila kitu,.. Kwa mara ya kwanza nilikasirika sana, lakini nilikaa na kufikiria kuwa kuacha kwangu pombe kuna faida sana, na pia zena hakuwa akifanya kama zena alivyonambia... Kiukweli fadhila kanijaza vitu vingi sana, lakini namshukuru Mwenyezi mungu kwa kutofatilia maneno yake... Na ukweli wote huu hapa nimeurekodi alipokuwa akiniambia... Aliongea mengi sana, lakini hakuna hata moja nimelifuata... Sikilizeni hii rekodi hapa, na ndicho alichosema fadhila... Wazee wangu.. Nisameheni kwa ujio wangu, nilikuwa nataka kudhibitisha ni kweli zena haumwi... Sikilizeni na nyie"



    Rahim aliongea kisha akatoka nje, na kuwaacha wakisikiliza ile rekodi.. Kumbe fadhila alipokuwa anaongea ujinga wake, rahim alirekodi kila kitu, tena mwanzo mwisho.... Na sasa wanasikiliza,....



    SASA NGOJA TUJUE KWANINI RAHIM ALIWEKA MAJI NA WAKATI TULIMWONA AKINUNUA WINE KULE SUPERMARKET....



    Sasa tuanzie pale rahim alipokuwa anaongea na yule jamaa aliemkuta pale supermarket baada ya jamaa huyo kushindwa kununua wine kwa ajili ya bei...



    "kwahio, unaniambia unapenda sana hii wine mpya"

    Aliuliza rahim huku jamaa akijibu kwa furaha

    "yes... Kwasababu ile wine ya zamani ndio Nilikuwa nagonga mimi.. Sasa leo nikaiona inatangazwa kwenye TV, nikasema siiachi hii.. Lakini huezi amini nimeiacha kutokana na bei"



    "ok.... Samahani dada... Unaweza kunioshea hii chupa"

    Alimuuliza yule mhudumu wa supermarket aliopo hapo kaunta,..

    "kwanini ufanye hivyo"

    "aahhh nina shida na hii chupa na sio kinywaji.. Hivyo naomba uioshe sana, tena sanaaaa.... Hakikisha hata harufu hakuna katika hii chupa... Afu hiki kinywaji mpe huyu jamaa"

    Yule jamaa kusikia hivyo alihisi raha ghafla.... Basi kikatolewa kile kinywaji kisha chupa ikaoshwa vizuri sana,...

    "tayari... Imeng'aa vizuri tu"

    Aliongea dada huyo huku akimkabidhi rahim chupa yake alioitaka, na kama ni hela kailipia pamoja na kinywaji chake, lakini yeye kachukua chupa tu...

    "nipatie maji ya Kilimanjaro baridi ya wastani"

    Rahim aliweka maji ya Kilimanjaro katika ile chupa, kisha akachukuwa na mfuniko wa kopo la maji hayo... Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kule supermarket... Kwahio rahim hajarudia pombe wala nini....



    SASA TUMEMALIZA SABABU YA KWANINI RAHIM KAJA NA MAJI.. SASA TUENDELEEE MBELE



    Huku hospitalini baada ya rahim kutoka,.. Aliwaachia kiredio kilichokuwa kikitoa sauti nzuri ya fadhila, na wakati huo rahim alienda toilet kujiseidia, ili akirudi akute familia ya akina zena, imepunguza hasira zao za kutaka kuondoka...



    Sasa rahim alipokuwa anarudi toilet, alisikia ile redio ikisema kuwa



    "Utakoma baba, mwaka huu wako, nakupenda na nimediriki kukupa sehemu zangu lakini bado hunioni tu... Na ukiacha pombe, utajiju, anazichukua zote"



    Hapo rahim alifanya kosa kuto kutoa hayo maneno,... Sasa hajakaa vizuri mara ikafikia mahali ikisema kuwa



    "tutakuja kuyamaliza... Sio kwa utamu ule nikuache aisee"



    Yaani watakuja kuingea na fadhila mana sio kwa ule utamu aliompa,... Rahim alikuwa anataka kufungua mlango lakini akasita,... Wakati huo huku ndani wazee wanatoa macho.. Huku wakisema

    "ina mana rafiki yako keshatembea na huyu kijana"

    Mama yake zena alimuuliza zena swali hilo, sasa zena nae pia ndio anashangaa, kumbe fadhila alishawahi kuwa na rahim kitanda kimoja,... Lakini sasa zena kabla hajamjibu mama yake, kwanza alikumbuka siku ile rahim alikuja dukani kwao na kumueleza mambo ya jana usiku ambayo zena hayajui... Pale pale zena akamjibu mama yake kuwa....

    "mama.. Ni kipindi kile alipokuwa mlevi... Na hata rahim mwenyewe hajui kama alikuwa na fadhila, mana alishawahi kuja kuniambia lakini mimi nikashangaa,.. Sasa hapa hata mimi ndio naamini kweli alikuwa ni fadhila,... Mama na baba... Nisameheni mimi... Naomba mnisamehe,..."

    "we mtoto mpumbavu sana... We si unasikia kasema watakutana waongee... Hatutaki mwanaume mwenye sifa za aina hii... Twende"

    Aliingea mama yake zena huku baba akitoka taratibu kabla hata rekodi haijaisha,.. Sasa huku nje rahim hajui kama baba yake zena anatoka nje, na rahim yupo hapo mlangoni anasikiliza maneno ya huko ndani... Lakini rahim akaona potelea mbali wacha aingie huko huko akaweke mambo sawa.... Sasa ile anafungua tu mlango, kakutana uso kwa uso na mzee mvungi, au baba mkwe....

    "heeeeee, mzee shkamoo mzee"

    Rahim kwa wenge akajikuta anasalimia kwa mara ya pili tena, mana hakutarajia kukutana nae hapo mlangoni.... CHEZEA BABA MKWE WEWE???









    Kabla hujafa hujaumbika, hakuna mtu alieamini kama rahim ipo siku atabadirika kutoka maisha ya starehe mpaka kufikia kwenye maisha ya kumjua mungu,... Lakini sifa zote anastahili zena, mana ndie chanzo kikubwa cha rahim kuacha starehe zote za kidunia,.. Licha ya wazazi wa rahim nao kujua kuwa anaumwa kwasababu ya kuachishwa ulevi, bado hawana imani kama mtoto wao angeacha pombe,..



    Zena kafanikiwa kumfanya rahim amrudie mungu wake, na yote hayo ni kwasababu ya upendo,... Baada ya zena kifanikiwa hilo. Kumbe nyuma yake kuna rafiki mnafiki aliokuwa akimla taratibu bila ya yeye kujua,.. Rafiki huyo alimjaza rahim maneno mazito mazito ili kuufarakanisha uhusiano wao,.. Lakini jua kuwa mungu sio asumani, rahim alipuuzia na licha ya kupuuzia, pia aliirekodi sauti ya fadhila alipokuwa akibwata maneno yake... Na ili zena aamini kweli rahim kaacha pombe,.. Basi rahim aliipeleka ile rekodi nzima mpaka hospitalini ambako familia yote ipo,... Rekodi ilikuwa na maneno machache yalioichafua furaha ya familia hio, kwani walikuwa hawajui kama rahim keshatembea na fadhila,



    Wakati huo rahim yupo nje anasikia kila kitu katika rekodi alioileta mwenyewe,... Sasa rahim akaona keshaharibu bora aingie akasuluhishe jambo hilo... Lakini ile anafungua tu mlango, alikutana na mzee mvungi mlangoni, rahim kwa wenge alijikuta anamsalimia mzee huyo aliotoka nje kwa hasira ya ile rekodi....

    "we mtoto mshenzi sana... Unataka kumchezea mwanangu.. Kumbe rafiki yake unae halafu unaaa.. Pumbavu"

    Rahim alijua kamkosea mzee, na uzuri ni kwamba rahim sasa hivi yupo ndani ya imani ya dini yake, hivyo hana dharau wala kiburi,.. Mwezi mmoja ulitosha sana kumfundisha mengi,..

    "mzee, sauti hio niliiacha makusudi ili muujue ukweli wangu kabla ya kuacha ulevi"

    "hakuna.. Mbona leo umemwambia mkutane"

    "mzee, kama kweli nilitaka kukutana nae, nisingekuja na sauti hio ili mjue, ingekuwa ni siri ya kukutana nae mzee wangu"

    Lakini mzee akafikiria mbona ni kweli, kama ni siri basi asingeileta, hivyo ni kama kaja kuujulisha uma ukweli wake, lakini ukweli ni kwamba rahim alikosea tu...

    "tena mzee, hata mimi sijui siku ile nilinanii na nani... Nikaenda kumbwatukia zena, kumbe sio yeye"

    Rahim alizidi kujitetea zaidi huku wakiingia ndani, zena na mama yake walikuwa nao wanatoka, lakini walipomwona baba anarudi, ikabidi na wao warudi, mana mama anatamani mwanae aolewe mapema, na zena anampenda sana rahim.. Hivyo bado wana wazo hilo hilo kwa rahim...



    Basi mambo yalikaa sawa, na haja ya kuendelea kukaa hospitalini, haipo tena, japo ilibaki wiki moja kumalizia dozi, mana rahim kuna dawa pia alizokuwa akitumia kwa ajili ya kuondoa hamu ya kunywa pombe,.. Kwa mara ya kwanza familia ya akina zena inapanda kwenye gari ya rahim,. Gari ya gharama kubwa dunia,.. Mama na baba ni furaha tu ndani ya gari,... Nusu saa mbele wanafika nyumbani kwao,.. Watu majirani wanashangaa akina zena wanateremshwa na gari ya thamani kubwa mno,... Watu midomo wazi,.. Lakini zena alishuka kisha akapanda tena kwenye gari, wakati huo ndani ya gari hilo bibi yake rahim yupo,

    "rahim, nataka twende tukanunue kanzu yako"

    Aliongea zena huku akitabasamu kwa mbali,..

    "sawa, ngoja nimshushe bibi pale nyumbani kisha twende Airport"

    "Airport kufanya nini"

    "si tunaenda dubai au"

    "kwani hapa hakuna kanzu nzuri"

    "lakini dubai kuna vitu original"

    "Hapana... Heshima ya kanzu sio lazima itoke mbali... Hata ya hapa hapa inafaa"

    Wakati wakiyaongea hayo na safari nayo ilikuwa ikisonga,... Walifika nyumbani kwao kwa akina rahim, wakamshusha bibi kisha rahim akapaki gari vizuri na kuanza kutembea mguu kwenda mjini, mana sio Mbali...

    "uwe unafanya mazoezi, sio kila mara gari tuuu... Utajinenepea bure tu"

    Aliongea zena wakati huo wanaelekea mjini, na vile rahim hakuwa na makuu toka mwanzo, mqtumizi yasio ya lazima alikuwa hana, kipindi hicho ni yeye na pombe, yeye na wanawake, lakini kwa sasa hayajui hayo,..

    "baba... Seidia baba... Naomba Seidia maskini"

    Ilikuwa ni sauti ya omba omba mmoja hivi akilia aseidiwe fedha...

    Sasa yule omba omba alipomwangalia vizuri rahim, aliomba msamaha

    "basi baba, pita tu... Sijakuomba wewe"

    Unajua kuna siku rahim alishawahi kupita hapa akiwa na zena.. Sasa akaombwa hela na huyu maskini, lakini rahim akataka kumpiga teke yule omba omba,.. Na kumwambia kuwa, asizoee kumuomba pesa mana sio za baba yake... Yaani sio za baba yake omba omba... Hivyo asizoee kuomba pesa kwake... Akamtishia teke sema zena akakemea hilo,... Sasa leo zena kampitisha tena rahim kwa makusudi kabisa, katika ule mtaa wa omba omba na ndio mana akamwambia awe anatembeaga ili asinenepe bure,. Lakini pointi ya zena ni kumleta rahim huku ili ajue kuna watu wanatamani kuseidiwa angalau hata shilingi mia tano,.....



    Rahim aliinama mbele ya omba omba yule, huku omba omba huyo akizidi kuomba msamaha mana aliponywa ponywa kupigwa teke la shingo,..... Huezi Amini rahim alitoa machozi kwa jinsi yule mzee alivyokuwa akilia kwa kuomba msamaha,...

    "Samahani sana mzee wangu... Ilikuwa ni maisha tu yalioniteka na pesa,... Ila kwa sasa Namshukuru mungu nimeanza kujua thamani ya mtu,... Mimi ndio nikuombe msamaha kwa nilichotaka kukufanyia siku ile..."

    Mzee omba omba kusikia maneno ya busara toka kwa kijana huyo, alinyamaza na kujisikia nae ni mtu mbele ya watu...

    Wakati huo zena katulia tu, hakusema lolote toka wafike hapo, tena zena ndio alionekana kuwa na haraka ya kuondoka hapo, yaani kama vile wanachelewa... Lakini haraka ya zena sio kuwa anachukia bali anamwangalia rahim kama atakubaliana na haraka zake au ataendelea kuwa na omba omba huyo,...

    "mzee, naomba uwaite hawa wenzie leo nitoe sadaka kwa ajili yenu"

    Rahim aliongea hivyo huku mzee huyo akiangaza macho na kuwaita wenzie,...

    Rahim bila kuchelewa alitoa noti ya elfu kumi kumi kila mmoja na walikuwa kama omba omba 25 hivi, kila mmoja kampa elfu kumi.. Kisha akaondoka zake na zena wake....

    "rahim sasa ulipofikia, hata mimi nafurahi... Na hio ulioitoa kwa hawa watu, ndio amali yako utakayoikuta Akhera"

    Rahim kweli alibadirika sana, na zena alifurahi kwa hilo







     



     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog