Search This Blog

Thursday 24 November 2022

NINGEFANYA NINI - 2

 

     



    Chombezo : Ningefanya Nini

    Sehemu Ya Pili (2)

     



    "Nitakutumia sikupata pesa, yule jamaa niliyemtegemea kanitumia nusu, nikifika tu nakutumia" aliniambia hivyo,



    Basi tulitoka nje na kuagana nikarudi nyumbani, kwa kipindi hicho sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, kwani niliacha kazi ambayo ilikuwa ni duka kubwa la kuuza simu, niliamua kuacha baada ya kuachana na boyfriend wangu ambae alikuwa ndo boss wangu, hivyo baada ya kunisaliti sikuona sababu ya kuendelea kubaki pale dukani kwake,



    Nilikaa nyumbani huku nikimuwaza yule mwanaume tu muda wote, ilipofika usiku nilimtumia msg kumuuliza kama amefika salama, hakunitafuta tena wala kunipa taarifa yoyote akanijibu ndio



    "Sasa kwanini umefika lakini hujanicheck" nilimuuliza maana kitendo kile kiliniudhi



    "Mambo mengi tu dear"

    "Sawa pole na uchovu"

    "Asante mpenzi"

    "Enhee mambo mengine vipi?"

    "Bado hajakaa poa nikiwa fresh nitakucheck tu" aliniambia



    Nilimtakia usiku mwema na kumuacha apumzike, asubuhi ilipofika hakunitafuta kwenye simu nami nilikuwa nategea ili kumuona kama atanijali tena, lakini haikuwa hivyo mpaka jioni ikafika hakunitafuta, niliingia fb nikakuta kapost pic, nikaona nimtumie msg inbox



    "Naona leo tangu asubuhi umeshindwa kunicheck lakini huku unachat tu"



    "Sasa sina pesa ya kukupa nitakucheck vipi, nimekwambia nikipata pesa nitakutafuta" alinijibu



    "Jamani sasa si ungekuwa unaniuliza hata hali yangu tu, kwani ndo tulivyokuwa tunaishi hivyo" nilihisi kupata tabu juu ya huyu mwanaume



    "OK nimekuelewa" alinijibu hivyo tu,



    Basi zilipita siku tatu mimi ndo nikiwa namuanza kumtafuta tu kila siku yeye wala hafanyi hivyo, nilihisi kuumia maana nilikuwa tayari nishaanza kumpenda vile vile alivyo, sikujali ufupi wake wala nini



    "Lini utanitumia nauli nije huko"

    "Kwasasa sina pesa kabisa" alinijibu hivyo

    ITAENDELEA



    HADITHI- NINGEFANYA NINI

    SEHEMU YA 7

    "Kwasasa sina pesa kabisa" alinijibu hivyo



    Nilishangaa sana amebadilika mno, wakati mwingine akiweka picha naona wasichana wakicomment mume, niliwaangalia ili kuona walichonizidi lakini hakuna kabisa



    "Naona watu wanatuma tu comment mume, nawe unachekelea tu, yule chausiku ndo nani" nilimtajia jina la mmoja Kati ya walio comment



    "Achana nao wanawake wengine wanapenda kujirahisisha tu, si umeona siwajibu kitu" alinijibu hivyo nami moyo kidogo ukapoa



    "Unajua nakupenda sana wewe mwanaume lakini sikuelewi"



    "Unielewi vipi mbona hata mimi nakupenda, hapa kwenyewe natamani nikuone mke wangu"



    Aliniambia hivyo nikajisikia raha sana maana tangu tukutane niliona amebadilika lakini leo amekuwa mkarim kwangu



    "Hata mimi natamani nikuone baby"

    "Sawa ila kwasasa sina pesa Habib wangu ningekupa uje huku, au kama una hela ya akiba njoo ukae japo siku mbili alafu mambo yakiwa mazuri nitakupatia hela"



    "Basi ngoja kwanza nitakwambia, itabidi nipambane nikipata pesa tu nakuja" nilimjibu

    Kweli nilikuwa na elfu 30 tu akiba lakini sikutaka kuitumia alafu nikawa sina pesa, hivyo iliniladhimu nipambane kutafuta pesa zaidi,



    Nilianza kwenda kushinda salun kwa dada yangu ili kumsaidia japo nipate pesa kidogo, siku zote sikuacha kuwasiliana na mwanaume wangu tuliongea vizuri na kuonyesha ananipenda sana, alikuwa akianza kunipost kwenye akaunti yake nilizidi kufurahi



    Siku hiyo nilipoenda salun kwa dada, aliniambia hatutofanya kazi bali tutatoka out, kuna rafiki yake alisoma nae hivyo amesema anataka kumtoa, nilikubali tulijiandaa na baadae tukafuatwa na gari, niliweza kumuona rafiki wa dada yangu, alikuwa mwanaume Mashallah mrefu pia amejengeka vizuri, kwa haraka umri wake alikuwa hapungui miaka 35, alitusalimia baada ya kuingia, dada akakutambulisha wote tukajuana, kisha akatoa gari na kutupeleka south beach iliyopo kigamboni, palikuwa pazuri Sana



    "Hamtaki kuogelea?" alituukiza yule mwanaume anaeitwa lameck



    "Wewe hukusema kama unatuleta beach tungejiandaa na nguo za kuogelea" Dada alisema



    "Kwani pale getin si wanauza nguo, twendeni tukanunue muvae, mi nataka muinjoy tu kama mnataka kuogelea twendeni mkachague"



    Basi dada alikubali, tulitoka na kununuliwa nguo, tukarudi na kwenda kubadilisha kisha tukaingia kwenye maji, tuliogelea dada alimpa simu atuchukue video, hakika tulienjoy, baada ya kutoka hapo usiku alitupeleka club bilcanas, alinunua pombe za gharama nami sikuogopa kunywa nilikunywa kwa umakini sana sikutaka kulewa nikatia aibu, nilikunywa hata chupa moja sikuimaliza, ilikuwa saa 7 usiku tulichoka, rafiki wa dada alitupeleka kwake alikuwa na nyumba nzuri ya kifaharii, tuliingia na kukaa ili kupiga story



    "Mwenzetu anasinzia ngoja nikamuonyeshe chumba alale" alisema Lameck na kumuacha dada yangu sebuleni, nikaonyeshwa chumba



    "Jisikie upo huru sawa" aliniambia



    "Na dada analala huku au nifunge tu mlango?" Nilimuuliza kwani nilihisi huenda dada asije na kulala na lameck ambae kanidanganya rafiki yake,



    "Anakuja tunapiga story kwanza"



    Basi aliondoka na kuniacha mimi, niliingia bafuni nikaoga na kujilaza, ilikuwa tayari ishafika saa nane, wakati usingizi ukininyemelea mlango ulifunguliwa aliingia Lameck



    "Nataka tuongee kidogo Aisha " aliniambia

    "Kuna nini?"



    "Nimekupenda sana natamani kuwa na wewe, nimekuangalia nimeona tunaendana kabisa"





    "Nimekupenda sana natamani kuwa na wewe, nimekuangalia nimeona tunaendana kabisa"

    "Mmhh mwenzangu naogopa"

    "Unaogopa nini, kwani dada yako amekwambiaje, kasema mimi malaya?"

    "Hapana hakuna alichoniambia kuhusu wewe zaidi ya kuniambia wewe ni rafiki yake tu"

    "Ndio mimi na yule ni marafiki tulisoma wote, nimeishi hapa kwa muda mrefu sina demu, nilipokuona wewe nikavutiwa nawe"

    "Nitakujibu siku nyingine"

    "Hapana kwani sasa unashindwa nini, nakupenda kweli na nipo tayari kwa chochote utakachoniambia nahitaji penzi lako tafadhali"

    "Tunaonana leo then unanitongoza na mapenzi unataka umekuwaje wewe?"

    "Nimezidiwa mwenzio wewe ni mzuri, ulipokuwa unaogelea ulinichanganya, usinihisi vibaya niambie unataka nini nifanye?" Aliniuliza nikabaki kimya

    Basi alifungua kabati na kutoa pesa akaniwekea mkononi, zilikuwa zote ni elfu kumi kumi, sikujua ni kiasi gani ila kwa haraka hazikupungua laki moja na nusu

    "Hizi pesa za nini?"

    "Chukua nimeamua kukupa kama zawadi hakika umeniteka haswa"

    Yaani nilishangaa yule kaka kanipa pesa zote hizo

    "Mi naenda kulala nipe namba yako ya simu najua kesho naweza nisiipate dada yako akiamka so nipe sasa hivi tutaongea zaidi"

    Nilichukua simu yangu na kumwambia ataje zake nikaisave, lameck alanibusu na kuninyonya mate kisha akaondoka

    Nilianza kuzihesabu zile pesa zilikuwa laki mbili, nilishangaa sana pesa zote zile

    "Kweli huyu mkaka ana pesa tena sio za mawazo" nilijisemea na kuweka kwenye mkoba wakati nikiwa pale niliamua kutoka sebuleni kumuangalia dada,

    Ile natoka ukumbini nilianza kusikia sauti za mahaba kutoka kwa Dada, nilishtuka na kuchungulia, niliweza kumuona dada akiwa amelala chali kwenye kochi huku lameck akiwa juu yake akimfanya, nilichukia na kurudi ndani

    "Kumbe ni waongo hawa," nilisema na kuamua kumtumia msg lameck

    "Umenidanganya kumbe unatembea na dada yangu" nilituma ikaonyesha imefika, baada ya dakika tano lameck alikuja kule chumbani

    "Mpenzi usiwe hivyo, rahma amelewa sana ananiforce kufanya vitu nami nimeshindwa kujizuia nisamehe, mimi sina mahusiano nae" aliniambia

    Nilijikuta nikihisi wivu, sikumjibu chochote kile, alianza kunibembeleza

    "Ipo siku utaamini ninacgokwambia kama nakupenda wewe tu, nitakupa kila ukitakacho na usisite kuniambia kitu chochote" aliniambia huku akinipapasa kisha tukaanza kunyonyana mate

    Sikuona hiyana kwani nilivyoona ule mchezo wakifanya nami nilikuwa kwenye hali mbaya hivyo nikajikuta nafanya mapenzi na lameck, bila kujali chochote, nilifanya na kumkatikia miuno ili kumchanganya haswa, mpaka wote tulipovunja madafu, lameck akatoka ili tusiweze kufumwa,

    Asubuhi dada akiniambia tujiandae kuondoka, kila mtu alijikausha, dada hakujua kama nilifanya mapenzi na lameck ila mimi nilijua alichofanya, lameck akanitumia msg

    "Ukitoka mtoroke uje tuyajenge basi" aliniambia hivyo nikamjibu ok

    ITAENDELEA



    CHOMBEZO- NINGEFANYA NINI?

    SEHEMU YA 9

    "Ukitoka mtoroke uje tuyajenge basi" aliniambia hivyo lameck nikamwambia OK

    Sikutaka tena mazoea nae, kwakuwa nilikuwa nishapata pesa ambazo ningefanya nauli za kunipeleka Moro kwa mwanaume ninayempenda, sikuona sababu ya kuanza kuhangaika na yule mwanaume, nilijiona nimekuwa Malaya kwa muda mchache niliapa kubadilika kabisa na kutulia na mwanaume mmoja,

    Nilipokuwa nyumbani nilimfahamisha mchumba wangu kuwa nishapata nauli,

    "Basi kesho uje sawa baby"

    Nikamuitikia, nikatoka chumbani na kuwaaga mama zangu kuwa nasafiri mara moja na sitokaa sana, waliitikia kwani hakuna hata mtu aliyekuwa na habari ya kunichunga, niliishi maisha yangu nikitaka kulala popote nalala ilimradi nimeaga tu,

    *****

    Siku ya pili nilikuwa tayari nipo ubungo nilipanda basi saa moja asubuhi mpaka saa saba nilikuwa nipo moro, bin mohd alifurahi kuniona alinichukua na kunipeleka gest

    "Mbona tumekuja hapa si unipeleke kwako"

    "Kuna mjomba wangu mgonjwa amefikia nyumbani lakini analala na mimi, sasa nilishindwa kukwambia mpenzi niliogopa utashindwa kuja nami nimekumiss" aliniambia lakini nikichukia sana

    "Kwahiyo na huyo mama yako je itakuwaje nitamuona au?"

    "Nitakupeleka kesho utamuona usijali"

    Basi tulioga na kula, kisha tukalala, usiku kucha tulikuwa tukifanya mapenzi tu, yule mwanaume alikuwa yupo vizuri sana, hakuchoka ila mimi ndo nilimuomba aniache maana sikuweza kuendelea, tulipumzika mara akapitiwa na usingizi, nilichukua simu yake na kuanza kuichezea niliingia fb moja kwa moja na kuanza kusoma msg zake, nilifanya hivyo kwaajili ya wivu ili kama ananisaliti nijue, niliweza kukuta msg za yule msichana Leila nilizisoma zote, aliweza kumlalamikia bin mohd kwa kumpotezea muda wake, alilalamika juu ya pic zangu alizoziona nimepostiwa, nilicheka kwani nilijua mohd ananipenda sana mimi, nilitoka na kuanza kusoma msg nyinyine,

    Niliona mwanamke akiwa amemtumia mwanaume wangu pic akiwa mtupu, kisha mwanaume wangu nae akamtumia sehemu zake za siri,

    "Umenitamanisha baby njoo home basi" iliandikwa hivyo niliangalia ili kujua imetumwa lini, ilikuwa msg ya siku moja kupita, nikahisi huyo mwanamke yupo kwa mohd bado ndo maana mimi kanileta pale gest, Mara nikaona msg WhatsApp zimeingia niliamua kuzifungua

    "Rajabu tambua nakupenda naomba usije kunisaliti" nilishangaa kusikia hilo jina rajabu,





    "Rajabu tambua nakupenda naomba usije kunisaliti" nilishangaa kusikia hilo jina rajabu,

    Nilianza kujiuliza huyu mwanaume ana wanawake wangapi jamani, maana nishasoma msg za wanawake sita tofauti

    Nikaendelea kupekuwa msg nikaona jina la Omar nilikumbuka ndo rafiki yake aliyekuwa akimwambia kuhusu mimi, niliona nifungue msg zake kwani niliamini lazima atakuwa amemtumia sauti yangu kama alivyomuahidi siku niliyokutana nae, niliona audio na kusikiliza, pia nikaangalia msg za muda, zilikuwa hivi

    "Unajua Aisha hajui kama Mimi ndo rajabu aliyeniambiaga hana hadhi ya kuwa na mimi"

    "Kwanini sasa hajui?" Omar alimuuliza

    "Kuna akaunti nilifungua nikajiita rajabu Mohammed alafu sikuweka picha, niliitumia kwaajili ya kuwatongoza madem tu wa fb hivyo sikutaka wanijue sura yangu, ila ile ya Bin mohd niliyotumia jina la baba ndo niliweka picha, lakini ndo imefanya demu akatoa namba, kumbe kuweka picha kuna faida anakusaminisha pale pale" alijibu hivyo nikaanza kukumbuka lile jina

    "Hhahaa, sasa utamwambia ukweli ukikutana nae?"

    "Simwambii nataka nimto**e maana aliniambia mimi sina hadhi, so nakula mzigo kisha nasepa"

    "Ila demu mkali unamuachaje?"

    "Amenidharau sasa siwezi kuwa nae, hapa nampanga ili niweze Kuonana nae ikiisha sikukuu tu" alijibu

    Nikajua kumbe mohd alinitafuta sababu ya kutaka kusex na mimi tu ili kulipiza kisasi kisa nilimjibu vibaya, kumbe hakunipenda huyu mwanaume

    Huwezi amini roho iliniuma sana, kumbe mtu ambae nimempenda kwa moyo wangu wote ndo yule niliyemchamba Facebook, alafu tayari nishafanya nae mapenzi na bado nilitoa nauli yangu kumfuata yeye, kibaya zaidi hakunipeleka anapoishi kanileta gest kisha ananidharau kwa marafiki zake, machozi yalinitoka sikujua nifanye nini,

    Mara simu ya mohd iliita jina lilisomeka habiba, nikajua kabisa ni mwanamke wake kwanini apige simu usiku, kutokana na hasira nilizokuwa nazo nilipokea ili niharibu kabisa yaani

    "Hallo mwenye simu yupo wapi?" Aliuliza habiba

    "Kalala ulikuwa unasemaje kwani?"

    "Wewe ni nani yake?"

    "Mpenzi wake"

    "OK poa vizuri sana utamwambia kuwa nilipiga"

    Yule msichana alikata simu na kutuma msg

    "Rajabu naomba unipotezee kuanzia leo sikutaki, mimi na wewe ndoa basi, bora ife" aliandika hivyo

    "Inamaana Rajab alitaka kumuoa huyu" nilijiuliza na kuamua kumpigia simu ikapokelewa

    "Mbona sielewi msg yako?" Nilimuuliza

    "Huwezi kuelewa kwasababu wewe sio mlengwa, akiamka raj mpe hiyo msg na umwambie asinisumbue tena" aliongea huku akilia

    "Sasa si uniambie wewe nani yake kwani"

    "Mimi ni mchumba wa roja baada ya miezi miwili tulipanga kufunga ndoa na taratibu zote zinaendelea mahari pia ameshatoa nusu, kumbe ananidanganya ana mke" alilalamika mara rajabu aliamka na kunipokonya simu

    ITAENDELEA



    CHOMBEZO- NINGEFANYA NINI?

    SEHEMU YA 11

    "Mimi ni mchumba wa roja baada ya miezi miwili tulipanga kufunga ndoa na taratibu zote zinaendelea mahari pia ameshatoa nusu, kumbe ananidanganya ana mke" alilalamika mara rajabu aliamka na kunipokonya simu

    "Unafanya nini sasa?" Aliniuliza akiwa amekasirika na kukata ile simu

    "Habiba alipiga, kumbe unataka kuoa alafu mimi unanidanganya kwanini lakini?"

    "Kwahiyo umemwambia nini?"

    "Nimemwambia ukweli wote kuwa wewe ni mchumba angu"

    "Hivi wewe una akili kweli? Ulichokifanya unaona ni sahihi? Mimi mchumba wako nishawahi kukutolea barua, unanijua vizuri mimi? Nishawahi kuja kwenu kujitambulisha au kukupeleka kwetu kukutambulisha? Kwanink unafanya vitu vya kipumbavu? Huyu uliyempokelea simu ni mke ujue natarajia kumuoa kwanini unaniharibia" aliongea akiwa amekasirika kabisa

    "Kwanini na wewe ulinidanganya, nishajua ukweli wote wewe ni rajabu, umenidanganya kwanini? Nimetoa nauli yangu nakufuata wewe lakini unajifanyia hivi mimi?"

    "Hiyo utajua mwenyewe, usiniambie upuuzi wako, napiga simu nataka uongee nae umuombe msamaha na umwambie kuwa mimi ni kaka yako binam hivyo ulikuwa ukimtania"

    Aliniambia hivyo, nilikataa na kuanza kulia, niliona ananionea alipaswa aniombe msamaha lakini ndio kwanza ananitolea ukali

    "Halo, habiba nisikilize tafadhali... Sikia basi mke wangu... Huyu Dada yangu anakutania tu mpenzi ... Embu sikiliza nakupa simu uongee nae..." Aliongea akiwa amechanganyikiwa hapakuwa na maelewano kati yao aliponipa simu nilikataa kuongea, alikasirika na kuvaa nguo kisha akaondoka,

    Nilibaki pekee yangu nikilia tu sikujua nifanye nini, nilijaribu kumpigia simu alinikatia na mwisho akaniblock kabisa, sikumpata tena, hiyo siku sikupata usingizi hata kidogo palipokucha nilijaribu kumtafuta rajabu lakini alikuwa bado ameniblock niliamua kumcheck fb, nikakuta kote kaniblock,

    Basi sikuwa na jinsi niliona nianze safari ya kurudi dar, kiukweli nilijuta kwanini nilimfuata rajabu safari yangu haikuwa na maana tena zaidi ya maumivu tu,

    Nilisafiri mpaka dar, nikiwa sipo sawa, nilikumbuka nilimblock lameck baada ya kunisumbua hivyo nilivyoenda Moro niliona anaweza kuniharibia tu, nikaitoa namba yake kwenye block, siku ya pili alinipigia

    "Aisha vipi Mbona ulikuwa hupatikani nikipiga simu yako inakata tu shida nini?" Aliniuliza baada ya kupokea

    "Simu yangu iliharibika hivyo nimeazima simu ya mtu na kuweka laini yangu"

    "Sasa baby unakaaje kimya ungeniambia, basi naomba leo tuonane"

    Aliniambia lakini sikutaka kuonana nae, bado nilikuwa na maumivu ya mapenzi toka kwa rajabu, hivyo sikuhitaji kuonana na mwanaume yoyote yule

    "OK nitakutafuta" nilimwambia lameck kumtia moyo







    "OK nitakutafuta" nilimwambia Lameck kumtia moyo

    Zilipita siku mbili sikuonana na Lameck, bado nilikuwa mtu wa mawazo, nilikuwa nikiingia kila siku Facebook ili kuona kama tayari rajabu amenitoa kwenye block lakini ilikuwa bado, basi niliamini ndo basi hanitaki tena,

    "Kumbe alinitamani tu, hakunipenda kabisa, niliamini nimepata mwanaume wa kutulia nae lakini hanitaki alinichukulia chombo cha starehe, anitumie kwa mara moja kisha anibwage" niliwaza na huzunika sana

    Mara simu iliita niliangalia na kugundua Lameck

    "Jamani eeh usinisumbue sikutaki kwanza wote ni wale wale tu" nilisema kabla sijapokea simu kwani nilianza kuhisi kuwachukia wanaume

    Kila nitakayempenda lazima tu ataniumiza, huyu nae kaniumiza sana, lazima nami nilipe kisasi nitawaumiza wanaume wote sasa hivi"

    Nilisema nikiwa na hasira sana, niliamua kuchukua simu na kumpigia Lameck kwani mwanzo sikuipokea

    "Hallo... Simu si nilikwambia sina? nimeweka laini kwenye simu ya mtu ndo sasa hivi ananiletea" nilimwambia baada ya kuniuliza kwanini sipokei simu yake

    Basi aliniambia tuonane, nilimwambia poa, nilijiandaa na kwenda buza kule kwa dada saluni niliposhuka kwenye gari nikasikia mtu akiniita niligeuka na kumuona mwanaume mmoja nikajiuliza nilimuona wapi, baadae nikakumbuka ni yule mwanaume ambae Dada aliniacha nae siku tuliyotoka club kwa mara ya kwanza kisha akaniingilia, aliitwa juma alinisalimia nikaitikia

    "Za siku nyingi, Mbona huonekani?" Alinuliza

    "Nipo tu" nilimjibu sikutaka story nae sana

    "Alafu nilikuwa nakutafuta ujue nilimuomba dada yako namba akasema huna simu lakini najua alininyima tu"

    "Ndio sina simu wala hajakunyima" nilimjibu vile ili asiweze kuniomba namba yangu

    "Basi sio mbaya twende home basi tukaongee"

    "Tukaongee kuhusu nini? Mimi sina muda huo kabisa"

    "Kwanini huna muda mbona mimi unavyovihitaji vyote nafanya nikiambiwa tu"

    "Vitu gani ambavyo nahitaji mimi, unavyovifanya"

    "Sikukuu ya idd dada yako kaniambia unataka pesa ya nguo nikampa laki moja na nusu alafu kasema unakuja sijakuona, akaniambia unaumwa umelazwa nikampa elfu 70 akuletee"

    "Wee vipi jamani, lini mimi nilimwambia Dada unipe pesa, atakuwa amekudanganya tu nawe unamuamini"

    "Lazima nimuamini kwasababu ile siku tuliyo onana mimi na wewe nilikuwa nishamtumia elfu 50 akasema atakuleta na ulikuja kweli"

    "Unasemaje mbona sikuelewi, mimi ulinijuaje mpaka ukaagana na dada anilete kwako?"

    "Nilikuwa namuonaga akikuweka status nikamwambia nimekupenda akasema nimpe elfu 60 ndo akulete, nikampa ile elfu 50, ndo ukaja lakini lengo lilikuwa kuongea n wewe kwanza nikutongoze, Ila tulivyofika ndani nikatamani pia penzi lako, kweli nimenogewa ndo maana alipo kuwa akiniambia unataka pesa nilitoa kwa kuamini ushakuwa wangu"

    Aliniambia hivyo, yale maneno yalinifanya nichoke, Kumbe Dada yangu kaniuza kwa yule mwanaume pasipo kujijua, alafu pesa nyingi anachukua

    "Yaani yule ana akili kweli? mimi hajawahi kunipa hata pesa iliyotoka kwako na sikubali atanikoma leo"

    Niliondoka kwa hasira mpaka saluni kwa dada

    ITAENDELEA



     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog