Search This Blog

Thursday 24 November 2022

YOUNG PASTOR - 5

 

     



     

    Chombezo : Young Pastor

    Sehemu Ya Tano (5)

     



    “Mercedes, we mercy… “

    “abee”

    “chukuwa kila kilicho chako na uende”

    “kuna nini? Si ulisema tunalala wote”

    Aliongea mercy huku akiwa mvivu kutoka

    “mercy jamani… Mama na Jessica wanakuja huku eti mi naumwa”

    “sasa kwanini useme unaumwa jamani”

    Mercedes alikuwa hataki kutoka kabisa,…

    ” nakuomba mercy,.. Wanakuja na gari ya nyumbani watakukuta mama angu ondoka”

    Mercedes aliona bora atoke asije kumharibia mpenzi wake,.. Mercedes haraka haraka hata kuoga hajaoga, kakusanya kila kilicho chake na janaba lake, kisha kaitiwa bodaboda kisha hiyooo kaondoka zake….



    Adam akarudi ndani haraka akatandika kitanda kisha akaenda kuoga,.. Aliporudi alianza kumwaga marashi nyumba nzima, mana wanawake hua wanajuana harufu zao, alimwaga marashi mengi mpaka vinakera sasa…. Sasa akakaa kwenye sofa.. Ndio ghafla anaskia honi inapigwa huko nje… Adam alikwenda na kujifanya kama hataki kufungua hivi lakini hapo yupo free kabisa…



    “wewe fungua mlango… Afu si ulisema unaumwa wewe…. Hebu fungua mlango tumekuja na daktari”

    Adam haamini kwa ujio huo, ilimbidi tu afungue geti kubwa, waingie ndani



    SASA HAPA TUENDELEENI TULIPOISHIA..



    Adam alifungua mlango gari ikaingia mpaka ndani kwenye paking, kisha wakashuka kwa kumkimbilia adam..

    “we si ulisema unaumwa wewe”

    Aliongea mama yake adam baada ya kushuka kwenye gari,

    “ingieni ndani kwanza mbona mpo nje kama wezi…”

    Aliongea adam, hata mama haamini adam siku hizi kabadilika sana,… Basi wote na daktari waliingia ndani

    “daktari, hebu mpime huyu mtoto, anaweza kujifanya anajikaza tu hapa… Mana namjua huyu ni muoga wa sindano na dawa… Mpime”

    Mama Jessica aliongea huku dokta akifungua mikoba yake aliowekea zana zake,..

    “lakini mama, mimi mbona siumwi, nilikwambia tu mimi ni mchovu, sijiskii vizuri… Ndio simu ikakata mana mtandao ulikuwa unasumbua”

    “sasa kwanini usipige tena jamani…. Afu mbona huku ndani kuna marashi sana, unaishije na marashi mengi hivi… Utaumia wewe”

    Aliongea mama, baada ya kunusa marashi yaliokithili kiwango cha kupigwa,…



    Dokta alimpima lakini kweli hakuwa na ugonjwa wowote ule, ila ni uchovu tu ndio uliomsumbua…

    “basi baba,… Utarudi na mwanangu marha, akupeleke kisha atatukuta hapa”

    Aliongea mama huyo, kuwa dokta huyo apelekwe na martha, kisha atarudi hapa….

    Basi martha alitoka na dokta huyo kama vile kumpeleka mana walikuja nae na gari yao, hivyo wasimwache arudi kwa tax au bodaboda,..



    Sasa baada ya martha kuondoka na dokta, mama alianza kukumbushia ishu ya eva kubakwa ni ya kweli au inakuwaje,

    “mwanangu, kuna picha zimeanza kuzagaa mitandaoni, picha zinazoonyesha nguo za eva… Tumeziona, lakini eva anasema hilo swala unalifahamu, ndio mana nikakupigia muda ule ili nijue”

    Aliongea Rebecca au Joyce… Huyu mama yake adam ndio anaitwa Joyce au ukipenda mwite Rebecca..



    “ni kweli mama…. Alinipigia simu usiku ule, nikatoka lakini kabla sijafika nikakuta kelele, nikaona nitoe msaada kwanza kisha nifuate pale kanisani… Lakini kumbe huyo huyo ninaemfuata ndio aliokuwa anapiga kelele kichakani… Lakini kwa bahati nzuri, hawajafanikiwa kumgusa jpo nilimkuta kazimia… Sasa kutokana na ile hofu na haraka ya kumwahisha hospitali, nikasahau kukusanya zile nguo… Hivyo ndivyo ilivyotokea, lakini eva ni mzima na hajaguswa licha ya kusaminisha mimi mwenyewe, pia tulipofika hospitali alipimwa na daktari wa kike, na pia akamthaminisha na kugundua, bado hajaguswa… Kwahio kama kuna taarifa tofauti mlizo zipata ni uongo”



    Adam alimaliza kuongea, na mama hakuwa na la kusema tena,… Alimkumbatia eva kwa mara nyingine tena,…

    “pole mwanangu… Usiwe Unakwenda misa za usiku”

    Jessica nae hakuwa mbali kumwomba msamaha eva kwa kuwahi kumsemea mabaya bila kuchunguza,… Na adam Hujaogopa kusema ukweli wote mbele ya mama yake, mana akianza kuongopa, eva atachukiwa na familia ya adam…

    “Nisamehe wifi yangu… Unajua katika familia yetu, hatutaki mwanamke ambaye atanyooshewa vidole na watu… Nisamehe sana mana kwa dakika chache tu nimetokea kukuchukia ghafla tu kwa hilo… Nisamehe”

    Aliongea Jessica huku eva akimsamehe kila mmoja… Na sasa eva na adam wanasubiri siku waamue kuoana, mana ruksa imeshatoka kwa baba yake aliekuwa kizuizi cha ndoa hio.. Shida ya baba alitaka adam awe mhuni mana ana nguvu za upako wa kweli kuliko baba yake, hivyo akiwa mzinifu, mana yake keshatekwa na shetani, hivyo upako tena atakuwa hana… Na ni kweli adam sasa hata akihubiri sasa mahubiri hayana uzito wowote ni kama anapiga kelele tu,… Mwanzo akihubiri yaani mtu mwenye mapepo hata akiwa njia ya kanisa, anatetemeka, lakini sasa hivi hata awe nae karibu hatetemeki.. Ni kama ule usemi usemao, eti mwenye ndoa hawezi kushauriwa na mtu asie na ndoa… Sasa wewe ni shetani utawezaje kunishauri niache ushetani ingali wewe mwenyewe ni shetani…



    Siku zilikwenda na leo ni siku ya Jumapili adam akiwa anajiandaa kwenda kanisani,… Mana ni muda wa kwenda kutoa ibada kwa waumini wake,… Mtumishi alitinga suti yake saafi kisha akatoka, wakati huo ni mtu mwenye furaha sana,.. Mana mahusiano yao yeye na eva ndio yanazidi kupamba moto… Wambea Wambea wote walikaa kimya mana wazazi wakikubali sijui wewe mbea una nafasi gani,….



    Adam anafika kanisani kwa mbwembwe nyingi, na sasa kaacha mambo ya kuwa na wasichana mara kwa mara, sasa kupunguza kabisa… Na wapo baadhi ya wasichana keshagombana nao tayari, mana aliusikia umbea kuhusu mpenzi wake, adam anajua walikuwepo wasichana wengi waliotaka kuolewa nae,….



    Sasa adam anaingia kanisani, anashangaa anakuta waumini nane tu akiwa ni mama yake, dada zake watatu, Eva na mdogo wake pamoja na mama yake, na mwingine wa nane ni vero, yule mschana aliosema ana bikra na ataolewa na adam… Huezi amini adam alivua miwani na kuangali kanisa lenye uwezo wa kubeba watu 400 (mia nne)  na zaidi, leo limebeba watu nane,.. Wakati huo watu hao nane walikuwa wanajifariji kwa kuimba kwaya, yaani hata wale wasichana ambao keshatembea nao kimapenzi pia hawapo,… Hapa ndio tujue kuwa mungi hachezewi, unakuwa kiongozi wa dini afu unafanya ufuska,.. Adam hakutaka kuingia kanisani, mana kanisa lilikuwa likipunguza watu kila siku, sasa leo limefikia watu nane tena familia yake yote ndio iliokuja kumsapoti adam…



    “mbona anaondoka”

    Aliongea Veronica, baada ya kumuona adam anaondoka kwa hasira,… Mtumishi wa Mungu hutakiwi kuwa na hasira za aina hio, kama wenyewe wanavyosema kuwa MCHEZO HUU HAUHITAJI HASIRA



    Mama alitoka kuja kumwangalia mtoto wake kwanini haingii ndani, na katoka kwa hasira hivyo… Mama anatoka nje anakuta gari ndio inaondoka,…. Mungu hachezewi na maneno yake,.. Mnasema eti Yesu Kristo kaondoka na dhambi zetu, nani kasema…. Yaani ufanye dhambi zako afu umtegemee yesu, wewe na dhambi zako utachomwa peke yako, fanya yanayompendaza mungu wako kwa imani yako… Sasa familia kuona adam katoka na gari, na wao wakaingia kwenye gari kisha haoo,.. Vero na yeye hakukaa, akaondoka zake, mtu wa mwisho kutoka ni eva peke yake na mama yake na mdogo wake,… Wao walifanya maombi yao kisha eva akahakikisha kafunga kanisa kila mahali na ufunguo akawa nao,.. Alitoka zake taratibu mpaka nyumbani na hapo alikuwa na familia yake,…



    Mama wa adam na familia yake walikwenda moja kwa moja nyumbani kwa adam, mana walimfukuzia hawakumwona, sasa sijui kaamkwa na kichaa au vipi..

    Walifika nyumbani wakapaki gari nje mana rimoti hawana, ila funguo ya mlango mdogo anayo Jessica mana yeye ndie anaekuja kufanyaga usafi huku, hivyo ufungua anao,..

    Waliingia mpaka ndani lakini hawakukuta mtu,… Mama alichoka, nanni lazima achanganyikiwe mama huyu,…

    “hebu wewe baki hapa, ngoja mimi niende nyumbani huenda kaenda nyumbani”

    Aliongea Joyce kuwa Jessica abaki yeye aende nyumbani,… Aliondoka na watoto wake wawili akamwacha Jessica peke yake,.. Kisha mama akaondoka…



    Sasa huku mjini,… Mjini kumechafukwa,… Walikuwepo waumini waliomfahamu adam hata gari yake wanaifahamu

    “Angel, we angel”

    “nini bwana miriam”

    “sio nini… Ona hii si gari ya mchungaji adam hii”

    “mmmmhhh kama yake kweli”

    “sio kama yake kweli… Ni yake, mi najua mpaka namba ya gari”

    Aliongea miriam kuwa yeye anaifahamu gari ya adam,..

    “pasta adam hawezi kuja kupaki gari mazingira haya… We unamjua pasta vizuri kweli wewe miriam… Mtu aliosomea dini aje hapa”

    Sasa Angela akiwa anabisha, miriam alimuona adam mwenyewe,…

    “haya sasa ona anachokifanya adam pale…. Bisha sasa na yule sie”

    Aliongea miriam huku Angel akibaki domo wazi

    “haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa…. Adam ndio kawa vile… Maskini ya mungu, adam kakutwa na nini tena”









    Unapokuwa kiongozi wa dini hutakiwi kufanya mambo ambayo hayaendani na dini yako au imani yako, kwasababu unachokifanya ni dhambi afu licha ya shambi bado unaongoza au unaswalisha umati wa watu iwe msikitini au kanisani,… Watu wote wanakuskiliza wewe na kukufwata wewe, kumbe tabia zako ni mbaya hata waumini wako hawafanyi hivyo, ukishapewa wito na bwana mungu wako, fanya kadri inavyotakiwa



    Lakini kwa upande wa adam tunaweza kusema yeye kashinikizwa na watu mpaka kufikia hali aliokuwa nayo, adam ni mtumishi aliekuwa na msimamo mzuri, adam alikuwa akifuata sheria, kanuni na taratibu za dini kwa wito alio upokea, lakini nyuma ya kuharibikiwa kwa adam baba yake anahusika, licha ya baba, kuna atbishop wa mashetani nchini Nigeria bwana jehova, huyu ni mwalimu wa wachungaji wote afrika wenye imani ya kishetani,… Sasa hawa pia ndio sababu kubwa ya adam kupotea katika imani yake, japo adam akifikiria sana anahisi yeye ndie kajiharibu kwa kumwingilia Catherine kwa mara ya kwanza, lakini sivyo ule mchezo ulipangwa vizuri, kwani hata Catherine alikuwa hataki kuingia kqa adam mana anajua sheria za dini kwa mchungaji ambaye bado hajaoa…. Lakini Catherine akadanganywa kuwa hivyo ni bijisheria tu na havina kikwazo kwa hilo lililotakiwa kufanywa, tena akamwambia kuwa hata akiingia chumbani hatoguswa.. Kwahio kama sio Catherine kushauriwa kuingia ndani, basi hata adam asingelifanya ile tabia,… Kwahio kuharibika kwa adam kumechangiwa na watu kadhaa haswa baba yake mzazi… Na yote hio ni kwasababu kakiuka agizo la baba yake kwenda njia ambayo aliitaka adam badala ya ile alioitaka baba yake… Hilo ndio kosa, na sababu ya kumfanya mtoto wake awe kama yeye, mana akiendelea na upasta wa halali ipo siku atamdhalilisha, hivyo ndio mana baba alifanya juu chini adam awe shetani,.. Awe mdhinifu na kila kitu



    Adam aliwasha gari yake na kuondoka hapo kanisa baada ya kukuta watu hakuna zaidi ya familia yake tu, na kama angelikuwa na imani kama zamani asingeondoka lakini imani yake imesha momonyoka kwa kiasi kikubwa mpaka kukata tamaa ya uchungaji..



    Adam alikwenda mpaka kwenye baa moja hivi ili kutuliza akili,… Alikaa sana hapo, na hajui kashauriwa na nani kuja hapo kitu ambacho hakijawahi kutokea katika maisha yake,…

    “ebu nipe mbili za baridi nipunguze mawazo”

    Ilikuwa ni sauti ya jamaa mmoja hivi akitaka bia mbili za kupunguza mawazo, sasa adam yeye hajui kama pombe kumbe inatoaga mawazo,.. Sa ngapi nae hajaagiza, mana hapo alikuwa na mawazo mpaka kichwa kinamuuma

    “nipatie mbili baridi dada”

    Aliongea adam huku Muhudumu akichangamka kuleta bia hizo…



    Sasa huku nje ndio wakapita akina miriam na Angel, wakaiona gari ya mchungaji adam ikiwa katika mazingira ambayo, adam hawezi hata kusogelea… Walibishana sana kuhusiana na gari hio lakini ghafla miriam anaona trei la vinywaji vikishushwa katika meza ya aliokuwa kakaa adam…



    “haya sasa ona anachokifanya adam pale…. Bisha sasa na yule sie”

    Aliongea miriam huku Angel akibaki domo wazi

    “haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa…. Adam ndio kawa vile… Maskini ya mungu, adam kakutwa na nini tena”

    Aliongea Angel huku akishika mdomo wake mana ulikuwa wazi kwa kutahamaki adam anavyo shushiwa vinywaji katika Meza yake..

    “ina maana kumbe mchungaji ni mlevi”

    Aliongea miriam huku Angel asiamini kwa kile anacho kiona kwa wakati huo

    “hata mimi ndio kwanza naona wala sijuagi”

    “hebu lete simu yako.. Si una namba ya eva”

    “wala hata sina”

    “ngoja nimpigie dada yake”

    Miriam alimpigia simu Jessica na kumwambia kuwa adam yupo baa anakunywa pombe,… Adam wakati huo ndio anazidi kuziongeza afu kama unavyojua mgeni wa pombe jinsi inavyo mlewesha kwa haraka tofauti na mlevi aliozoea pombe,



    Jessica kwa haraka alipiga simu kwa mama yake, mama kuskia taarifa hizo kapatwa kichaaa, kachanganyikiwa ghafla huku akichukuwa gari,… Hawaamini adam kapatwa na nini…

    Mama akampigia simu mume wake

    “baba Jessica,.. Ivi una taarifa gani za mwanao”

    Aliongea mama huyo huku chozi la uchungu likimtoka mama huyo

    “taarifa gani tena… Na mtoto yupi huyo”

    “adam”

    “adam si yupo kanisani kwake”

    “hapana baba Jessica… Adam alikuja kanisani na kukuta kanisa lipo tupu halina waumini, adam akatoka mbio hatukujua anakwenda wapi… Sasa nimepigiwa simu na Jessica kuwa adam kaonekana baa anakunywa pombe”

    “ahahahahahahah, sasa hilo ni jambo la wasiwasi mke wangu… Anatoa mawazo tu huyo… Watu miatano ukute hakuna ai utakuwa kichaa… Mwache atoe mawazo, tena ana maamuzi ya kiume, angalikuwa na maamuzi ya kike, sasa hivi angeshakuwa kajitupia korongoni huko”

    Aliongea mr jacob huku mama kashika mdomo, yaani haamini kama kweli baba yake anaongea hivyo kuhusu kuharibika kwa mtoto wao,

    “ina maana bishop mzima unakubaliana na hali ya kijana wako”

    “kwani Bishop ni nani? Si mtu kama watu wengine”

    Mama alikata simu haraka,… Alibonyeza jina la Jessica na kumpigia

    “upo wapi Jessica”

    “ndio nipo njian hapa nakuja huko na bodaboda ili twende wote huko”

    Aliongea Jessica na wakati huo kila mtu kichwa moto mana ni aibu kubwa kwa mtoto wa kiongozi wa kanisa kuwa katika mijumba ya starehe,….



    Sasa huku baa, kama unavyojua baa hakukosi wanawake,… Sasa kuna wale makahaba baada ya kuona huyu ni kigogo, mana alikuwa bado ana suti yake,.. Makahaba hao walimzunguka adam na kuanza kumshika shika shika.. Kama vile wanamtaka kimapenzi, na adam wakati huo anajiskia raha kweli, kasahau kila kitu

    “wee.. Ee… We… We. Muuuuuuiduuuumiuuu.. Kuna vyumba”

    Adam aliuliza tena kwa sauti ya ulevi

    “ndio kipo”

    “sioooooo kiiipo.. Seeiiima viiipouuu”

    “unataka vingapi boss”

    “nataka gestiiiiiiiiiiii nziiiiiiiimaaaaa”

    “lakini boss… Ndani kuna wateja wengine”

    “nimeseimaaaaaaaa.. Watoeeeeee”

    Aliongea huku akimwaga mwaga pombe wakati huo hata kusimama yenyewe hawezi, mana hapo alipo kashikwa na wasichana kama watatu hivi wa hapo baa…. Sasa akina miriam, mama wa kufotoa mapicha picha, mama wa kituma picha za wasap,… Miriam angelisomea uandishi wa habari, duuuuuu… Angepiga bingo kwelikweli…. Mara simu ya miriam iliita wakati huo kesharidhika kupiga picha, sasa alikuwa anarekodi video kabisa

    “haloo Jessica, umefika wapi”

    “mpo baa gani”

    “hapa mjini kati… Kuna pub kubwa inaitwa CHOMBEZO PUB”

    Alitoa maelekezo miriam ili waweze kufika, maskini akina Jessica hawajui mabaa yalipo hivyo iliwapa shida sana hadi kufika hapo…..



    Walikutana na miriam kisha akawapeleka mpaka kwenye chumba ambacho adam kaingia na wasichana watatu,… Sasa Jessica anaogopa kuingia baa,…

    “mama… Huku ni baa eti”

    Mama alimwona Jessica ni mjinga kwa kuogopa kuingia baa, mama kaingia mkuku mkuku mpaka ndani na kuonyweshwa, chumba ambacho adam kaingia na wasichana watati, watu walijua huyo mama ni jimama la adam ambalo linammiliki adam, kila mschana aliogopa hapo baa mana inasemekana wamama wanaomiliki vijana wadogo huwa wakali na kutumia pesa zao kumpoteza mschana ambaye atakuwa karibu na kijana wake,.. Sasa mama haogopi kuingia mpaka huko gesti, mana ni mtoto wake ndio anakwenda kupotea,… Wakati huo Jessica kabaki nje huku akiwa na wasiwasi juu ya kaka yake huko alipoingizwa…



    “tokeni, tokeni… Mambwa nyie.. Tokeni, wapumbavu wakubwa nyie”

    Ilikuwa ni sauti ya Joyce au mama adam akiwa mkali juu ya wasichana aliowakuta wanamvua nguo adam tayari kufanya nae mapenzi… Mama alimkuta adam tayari suruali ipo chini kabakiwa na boxer tu,.. Mama ni mcharuko,… Kampandisha suruali kisha akafunga mkanda vizuri…

    “mbooooo…. Mboo.. Mbona mnafunga mkanda teeeena… Hamtaki sitarehe teeeena eeeeeeeee… “

    Adam aliongea huku akijua labda mkanda unafungwa na wale makahaba, kumbe ni mama yake mzazi,.. Mama kamuinua kidogo kisha akamnasa bonge la kibao

    “taaaaaaaaaaaaaaaassssss”

    “haaaaaaa…. Mamaaaaa”

    Adam kajua ni mama hapo hapo akakata moto mama sio haba, kamtia adam mgongoni kisha akawa anatoka nae… Kwa bahati ni kwamba alikuwa bado hajaibiwa

    “Samahani mama…. Huyo mtu bado hajalipa bili ya vinywaji alivyotumia na kununulia watu”

    Mama haamini macho yake, jinsi alivyo ona hizo chupa za bia alizotumia adam yeye peke yake…

    “sawa nakuja kulipa”

    Mama alimpeleka adam mpaka kwenye gari, kisha akarudi kulipa biashara ya watu

    “ni kiasi gani”

    “laki tatu na elfu 40”

    Mama hakuwa na jinsi ya kulipa, ilibidi alipe hio pesa yote kisha wakarudi kwenye gari na kuondoka wao wawili na adam wa tatu,… Akina miriam wao walibaki pale baa, na kuanza kitangaza….

    “ivi huyu kijana ni nani”

    Aliuliza mhudumu wa baa, sasa akina miriam wao ni wasichana wa kawaida sana, hata kanisani hua wanakwenda ile basi tu,… Walisogea pale na kuanza kutoa umbea

    “nyie hamumjui yule kiongozi mkubwa wa makanisa hapa jijini”

    Aliongea miriam hapo CHOMBEZO PUB baada ya watu kuuliza huyo kijana aliotolewa ni nani

    “nani huyo…. Huyu mr James”

    “kuacha mr james..”

    “sasa nani mana wakubwa zaidi na utajiri wao wapo wawili… Ni mr james na mwingine huyu wanamwita nani huyuuuuuu.”

    “mr Jacob”

    “yes.. Yes… Yes… Huyu mr Jacob.. Sasa huyu kijana ni mtoto wa nani”

    “huyu kijana, anaitwa adam… Ni mtoto wa mr jacob au Bishop Jacob”

    Aliongea miriam huku watu wakishanga, mana mr Jacob ni tajiri mkubwa na ni kiongozi wa dini hapa jijini

    “haaaaaaaaaaaaaaaaa….. Yaani huyu ni mtoto wa yule tajiri”

    Waliuliza mara mbili mbili, huku wale makahaba wakijuta kwanini hawaja mwibia adam huyo

    “yule mtoto pale, akili imelala… Pana shule pale acha mchezo”

    Aliongea Angel huku akiisifia elimu ya adam

    “sasa kapatwa na nini”

    Aliuliza Muhudumu wa hapo baa, na wakati huo pana kilinge kikubwa mno

    “kwanza adam kasomea huko kunakomilikiwa na malikia Elizabeth sjui ni wapi huko”

    “Uingereza au”

    “mi sijui kama ni huko… Lakini kasomea huko kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo, ni huko huko… Aliporudi hapa kakaa miaka miwili tu, kaenda Nigeria kusomea Biblia.. Aliporudi kakabiziwa kanisa… Kanisa lake linaingiza waumini miatano… Sasa leo nimepigia Vero simu, kuniambia mtumishi adam katoka hapo kama kichaaa… Kumbe sasa kaja huku baada ya kukuta kanisa liko tupu.. Chezea kukosa waumini wewe”

    Sasa watu wanazidi kushangaa kwa jinsi wanavyo hadithiwa historia ya kijana huyo,…

    “lakini ni kweli… Hata hapa CHOMBEZO PUB, pakikosa wateja, utapakimbia hapa… Lazima upaone hapafai, utatamani kutafuta sehemu nyingine”

    Aliongea miriam huku watu wakishika midomo.



    Sasa tukiachana na wambea hao tukija huku nyumbani kwa adam akiwa ndio analazwa kitandani akiwa hajitambui hata kidogo, eva maskini alishapa taarifa toka kwa marafiki zake mana sasa taarifa zilisha zagaa Jumapili hii, Karibia makanisa yote ya baba yake yameshajua taarifa hizi, picha alizopiga miriam tayari wengi wanazo hivyo ni ushahidi tosha….

    Eva alikuja mbio mbio nyumbani kwa adam hata ni kashfa kubwa kwa mchumba wake lakini bado hajatoka moyoni, tena kajaa tele…

    “hebu kaeni nae, msimpe chochote kwanza, naenda kumleta dokta”

    Aliongea mama huyo huku eva na Jessica wakiwa hapo sebuleni, na aliekwenda kumlaza ni mama yake peke yake,..

    “sawa mama uwahi basi”

    Aliongea eva huku akimtaka Jessica waingie kule chumbani, lakini Jessica ana maadili mazuri ya kutoingia chumbani kwa kaka yake akiwepo…

    “hapana eva…. Nenda kwanza wewe uli ujue amelalaje… Nikienda mimi sasa kama kalala vibaya?… Nenda kwanza wewe ili kama kalala vibaya umtengeneze afu mimi ndio nije”

    Eva alikubali ombi la Jessica, na hapo ndani wapo wawili tu mana mama katoka kwenda kumchukuwa dokta,… Eva kweli kafika kamkuta adam kalazwa vizuri tu na hapo hajitambui, chumba kizima kinanuka pombe tu…

    “wifi, hakuna shida njoo”

    Eva alimwita Jessica aingie wakae nae humo ndani… Basi wakawa wana mwombea adam kwa ibada yao fupi,… Baada ya hapo wakaona mmoja akapike mmoja akae nae,.. Jessica alikwenda kupika, huku eva akiwa na adam hapo chumbani,.. Sasa eva akaanza kupanga panga nguo ili hata dokta akija asikute pamekaa shagala bagala bila mpangilio,.. Wakati huo adam hajitambui hata kidogo mana kanywa bia nyingi sana, na huenda zikamletalea madhara mana wenzie wameanza taratibu lakini yeye.. Kazinywa nyingi kwa wakati mmoja..



    Sasa Jessica alimaliza kupika chakula, sasa akawa kachemsha maziwa analeta huku chumbani ili wanywe yeye na eva, mana mama kasema adam asipewe chochote kwanza, mpaka dokta aje mana hawajui huduma ya kwanza ya mtu aliolewa kupitiliza…. Sasa Jessica ile anaingia anamkuta eva analia,.. Alishtuka eva analia nini tena.. Sasa Jessica akawa anamwangalia adam kwenye uso, kisha anamwangalia eva kwenye uso,.. Eva analia huku akiwa kashika miguu ya adam…

    “eva nini ahida”

    Aliuliza Jessica huku akiweka vikombe vya maziwa lakini kabla ya kuviweka, eva akasema….

    “jamani adam wanguuuuu”

    Aliongea eva huku akitikisa miguu ya adam

    Jessica alipatwa na mshtuko mpaka akaachia vile vikombe vyenye maziwa vikapasuka…. Jessica alikosa nguvu, akadondoka na yeye, sasa kabaki eva peke yake,… Jessica kazimia hapo chini, adam hajitambui na eva hatujui analia nini…….











    Katika mambo yako pale unapoyafanya jaribu kuwa mkini yasijulikane na mtu mwingine iwapo yatakuwa ni mambo ya siri, adam alikuwa akifanya mapenzi bila umakini na kama unakumbuka kuna siku ilikutwa nguo ya ndani na dada yake, hio yote ni kukosa umakini na mambo yake,…



    Sasa leo eva akiwa anafanya fanya usafi wa hapa na pale, alifika mahali na kuanza kukung’uta nguo ili kama kuna vumbi litoke, saa ngapi katika zoezi hilo haijadondoka kondomu,.. Tena kondom iliovaliwa lakini haina uchafu, yaani haijamaliza kazi ikavuliwa….. Sasa bora hata ingelikutwa kwenye pakiti, ingejulikana bado haijatumika japo mpango wa kutumika upo… Sasa eva kuona ile kondomu alianza kulia maskini ya mungu na kujua kuwa kumbe adam alikuwa na mwanamke, na amemsaliti, sasa akawa analia huku akimshika adam miguu… Ndio Jessica akatokea pale pale akiwa na vikombe vya chai,.. Sasa Jessica baada ya kumwona eva analia huku kashika miguu ya adam, akajua labda adam kazidiwa na pombe hadi kufa, ndio Jessica akazimia papo hapo…



    Eva anashangaa tena Jessica kadondoshwa na nini tena,… Kazi ya kumpepea ilianza.. Alimpepea sana mpaka Jessica akazinduka na kuana kulia… Sasa eva nae anashangaa Jessica analia nini…

    “wifi, kwani kuna nini”

    Eva alimuuliza Jessica, yaani walio achwa apo wote walikuwa vichwa maji

    “wewe ulikuwa unalia nini”

    Jessica hakujibu badala yake akamuuliza eva, kuwa mwanzo alikuwa analia nini… Eva akanyoosha kidole katika ile kondomu,… Jessica alishagaa sana inawezekanaje jumba la mtumishi lionekane kondom,…. Lakini Jessica akakumbuka kuna siku alikutana na chupi humo ndani, akadanganywa na adam kuwa humo ndani kuna majini mahaba hua wanakujaga humo ndani… Nyumba ya mtumishi iingiliwe na jini mahaba toka lini…..



    Sasa Jessica akajua lazima adam alishakuwa shetani siku nyingi,.. Na lile swala la jini mahaba, alimdanganya, mana jini mahaba wanavaaje kondom, na hii imevuliwa kabla ya kazi,… Kama unakumbuka siku adam alivyozinguliwa na Mercedes kuwa avae kondomu ili itakapoishia kondom basi aishie hapo hapo,.. Sasa adam akakasirika na kuivua kwa kuitupa afu akasahau kuwa walitupa kondom…



    “aaahhhh hawa ni wale majini mahaba alioniambiaga siku zile”

    Sasa Jessica nae akamdanganya eva ili aondoe wasiwasi juu ya adam, lakini Jessica keshajua kuwa adam ni mchafu toka muda mrefu…

    “jini mahaba…. Jini mahaba ndio nini wifi”

    Eva aliuliza kuwa jini mahaba ndio nini, mana haya mambo ya majini mahaba haya… Sio ya upande huu… Hivyo ni ngumu kwa eva kutambua,

    “jini mahaba,.. Ni viumbe majini wanaokuja kufanya mapenzi kwenye mijumba ya watu usiku wa saa nane”

    Aliongea Jessica lakini anajua kabisa anamdanganya Jessica kama yeye alivyo danganywa na kaka yake…

    “sasa majini na nyumba ya mtumishi, mbona haviendani kabisa wifi”

    “hapana…. Majini hua wanapenda sana viongozi wa dini”

    “heeeeeeee jamaniiii… Bwana yesu awe karibu na adam wangu jamani”

    Eva alijikuta anakubali kwasababu hajui kitu kuhusu majini mahaba,.. Sasa akitajiwa hilo neno mahaba… Ndip kabisa anaamini ni kweli, lakini Jessica leo ndio kaujua ukweli, hata ile chupi haikuwa ya jini mahaba wala nini… Sasa waliishika kwa mti na kwenda kuitupa kwenye dastibin…



    Ghafla mama karudi akiwa na dokta, mama alikuwa hare hare sana,

    “dokta ni huku”

    Aliongea mama yake adam kwa kumuonyesha dokta njia…

    Basi dokta alifanya vipimo vyake vyote kisha akawapa ushauri nini cha kufanya baada ya adam kuamka…. daktari aliondoka zake na huduma kwa adam iliendelea, na hapo eva hajapata nafasi ya kwenda kwao. Mpaka pale adam alipopata nafuu..



    Siku zilizidi kwenda adam alizidi kuwa na tabia za ajabu, alikuwa ni mtu wa kushinda baa, kulewa, kutembea na wasichana haswa akina miriam, Angel, Vero, yaani karibia robo ya  wasichana ambao walikuwa ni waumini wake,… Eva alikuja kujua hilo basi akawa ni mtu wa kulia kila siku huku akimuomba mungu, ili adam aepushwe na starehe za kidunia…. Wakati adam akiwa baa mana pesa anazo hivyo anafnya starehe kwa kwenda mbele…..



    “mama joshua, ivi yule mtoto wa mchungaji jacob, Karogwa au ni akili zake”

    Aliongea mama miriam huku mama joshua akisema kuwa

    “yule kijana waliwahi sana kumkabidhi Biblia,. Bado ni kijana mdogo san yule,.. Bado ana akili za starehe, hebu ona anavyomdhalilisha baba yake akiwa kiongozi mkuu wa dini katika jiji hili”

    Aliongea mama joshua huku waumini wengine wakipokea pointi ya mama joshua… Na hapo ilikuwa ni mazingira ya kanisani kwa mr Jacob..

    “lakini mama joshua, mimi sioni kama kuna tatizo kijana kama yule kuwa mchungaji… Ni kutojielewa tu, tena ni sahihi vijana wadogo kuwa viongozi wa dini”

    “wewe mama eva unaongea tu kwakuwa ni mkwe wako… Yule kijana bado ni mdogo sana,…”

    Aliongea mama Joshua huku mama mwingine akija juuu



    “lakini alicho ongea mama eva, ni sahihi… Kweli ni kuto jielewa tu lakini ndio umri sahihi wa kijana kuwa mchungaji ili aweze kuhamasisha vijana wengine kutamani hali kama hio, na hat neno la mungu linapotangazwa na kijana lika lile, hua inapendaza sana”

    Aliongea mama Mercedes, na hapo walikuwa ni wale wamama na watoto wao wameshapitiwa na adam sema hawajui,…

    “unamkumhuka mama Jackson.. Alimkuta adam chooni kashika kiuno cha mwanamke, kule chooni kanisani kwake”

    Baadhi ya wamama walikuwa hawafahamu hio ishu haswa mama eva,

    “heeeeee chooni…. Yaani chooni kabisa”

    “sasa unabisha nini… Sasa hivi hatuna vijana, tuzaeni tu lakini.. Hakuna watoto karne”

    “haya wewe si mkweo… Una ushauri gani kwa mwanao eva”

    Mama Joshua alimuuliza mama eva, japo mama eva hakuwa na itikadi ya umbea, sema yupo na wanawake wenzie kanisani….

    “Kiukweli maamuzi anayo eva mwenyewe…. Akihitaji kuendelea nae mimi sina pingamizi juu ya hilo, mana sihitaji kumkwaza mtoto wangu”

    “kwanini sasa hivi anakwenda kwao”

    “hapana, hata yeye hataki kumuona japo anamuombea aache hio tabia”

    “mmmhhhh mama familia yako ina moyo, au kisa utajiri jamani”

    Aliongea mama Joshua, wakati huo kila mmoja akianza kuondoka zake taaratibu kurudi majumbani mwao



    “ongeza watoto biaaaaa wale maisha”

    Aliongea adam kumtaka Muhudumu aongeze bia kwa wasichana waliomzunguka,…. Mama akisikia mtoto wake yupo huko anawahi kwenda kumchukuwa… Kila siku ilikuwa ni kazi kwake kwenda kumchukuwa adam pale anaposikia kazidiwa kwenye baa fulani….



    “hivi baba adam, hili swala la mtoto wetu tunalichukuliaje… Kwanini usiite kongamano la viongozi wenzio tukamuombea… Ni wiki ya tatu sasa mtoto anashinda baa, anazungukwa na wanawake,…. Atakuja kupata magonjwa bure huyu mtu”

    Aliongea mama yake adam, huku baba akicheka sana kwa taarifa hizo

    “hahahahahh…. Mtoto wako, kaniuzi sana, nami ndivyo nilivyokuwa nataka, mtoto wako nilimwambia akasomee Biblia”

    Kabla baba hajamaliza, mama kaingilia kati,

    “si alikwenda kusoma”

    “hapana…. Mtoto wako kaenda kusoma katika chuo alichotaka yeye na sicho nilichotaka mimi”

    “kwahio tunamseidia vipi”

    “mwache amalize mwezi kwanza… Nitamshuhulikia mimi mwenyewe…. Mana nataka afuate njia zangu na nimkabidhi vitu vyangu vyote”

    Aliongea mr jacob lakini ghafla alishangaa glasi ya maji inatetemeka pale juu ya meza,… Bwana Jacob alijua kuna kitu hakiko sawa….

    “huyo adam yuko wapi nimshughulikie sasa hivi”

    Mr Jacob alimuuliza mke wake kuwa huyo adam yuko wapi ili amshughulikie sasa hivi, ingali punde tu hapa alisema adam aachwe mwezi uishe….

    “wewe si umesema tumuache mwezi uishe”

    “hapana…. Kamlete mtoto wangu nimkabidhi kila kitu”

    Mr Jacob amekuwa mkali ghafla tu… Lakini mama alishtuka jambo fulani hivyo hakutaka kufanya haraka kwenda kumleta adam…..



    Sasa huku nyumbani kwa adam akiwepo dada yake,… Mana adam kwa wakati huo alikuwa kalala ndani baada ya mama yake kwenda kumchukuwa baa na kumleta nyumbani kwake, sasa dada yake ndio mtu wa kumpa huduma…. Sasa simu ya adam ikaita,.. Kwa sasa anaekaa na simu ya adam ni Jessica mana ni ndugu yake,… Jessica alipoangalia namba kama haielewi hivi,….. Lakini aliipokea

    “hallow YOUNG PASTOR, be praise our Jesus”

    (Halo MCHUNGAJI MCHANGA, tumsifu Yesu Kristo)”

    Aliongea kwa lugha ya Kiingereza, na ilikuwa ni sauti ya kiume

    “forever Amen…. Mmhh sorry who Are you mr?”

    (Milele Amina… Mmhh samahani wewe ni nani ndugu?)

    Aliitikia Jessica kwa lugha ya Kiingereza, sasa hapa wacha tuandike kwa Kiswahili, ili tuepushe nafasi ya kutafsiri…..

    “Mimi ni mchungaji toka Nigeria, naitwa TB JOSHUA”

    Jessica anamfahamu huyu mtu mana ndio mchungaji mkubwa Afrika kwa wale wenye imani ya kweli, na ndio mwalimu aliomfundisha adam akiwa katika masomo yake, na ndio mmiliki wa chuo alicho somea adam na yeye mwenyewe ndie aliempokea Adam….. Hivyo Jessica anamjua mara mbili, kama mchungaji au kiongozi wa dini Afrika… Pili anamjua kama mwalimu wa mdogo wake…

    “waooooo thanks Jesus… Mimi ni dada yake adam… Na adam kwa sasa kapata matatizo”

    Aliongea Jessica huku akiwa na furaha,… Japo hajui kama mtu huyo yupo wapi,…

    “kapata matatizo??…. Matatizo gani”

    “hayasemeki kwakweli, laiti kama ungelikuja Tanzania… Huenda ikawa msaada mkubwa kwake”

    “ahahahahahh…. Mbona mimi nipo KIA AIRPORT hapa na ndio nimempigia aje kunipokea”

    “whaaat…. Ati upo KIA”

    “yes… “

    “nakuja kukuchukua mchungaji… Nakuja sasa hivi, nipe muda wa nusu saa natoka Arusha sasa hivi”

    “hakuna shaka mama… Ila usitembee mwendo kasi sana, usije kupata ajali mama sawa”

    “sawa mchungaji”

    “bwaaaana  yesu akuongoze katika safari yako”

    “amina mchungaji”

    Simu ilikata kisha akaingia chumbani kwa kaka yake na kumwangalia, alikuwa analia lakini alijipa moyo kupona kwake… Jessica alitoka mpaka kwenye paking, akachukuwa gari ya adam ambayo ndio ilikuwa na mafuta, mana hakuitembelea kwa muda mrefu,…



    Jessica anatoka na kupotelea mbali, lakini kabla hata vumbi halijaisha mama nae huyo na gari yake,… Sasa mama nae ana rimoti ya geti la adam, alifungua na kuingia ndani,…. Sasa mama amekuja kumchukuwa adam ampeleke kwa baba yake…. Na ni muda huo huo Jessica katoka kwenda AIRPORT kumchukua TB JOSHUA,… Mama hajui adam anachokwenda kukabidhiwa ni nini.. Na baba yake adam keshajua kuna mtu kaingia Tanzania…. Mama bila kujua kaja kumchua adam, na wakati huo adam hajitambui kwa ulevi….





    Wakati huo kule nyumbani baba anasubiria adam aje amkabidhi vitu vyake vyote, mana wameambiwa endapo unahisi kuna tatizo, basi achia mtoto wako itakuwa Afadhali, mana ukiachia mtu mpya, nguvu nayo inaongezeka hivyo yeyote hawezi kutikisa boma lako,… Mr jacob alipiga simu kwa mr yohana na wengine ambao wanaitumikia imani ya shetani,..

    “halo mr jacob habari yako”

    “huku sio salama sana”

    “sio kwako tu, nahisi hata kwangu… Mana kuna wakati nimepata tetemeko katika jumba langu, na mbaya zaidi nina mchungaji wangu kanipa taarifa hizo kuwa hata kanisani kuna matetemeko,… Sijui kuna nini hapa mr jacob”

    Aliongea mr Yohana huku kwa Jacob alikuwa akihaha kila kona ya nyumba yake,

    “kuna nini labda”

    Mr Jacob alimuuliza mr yohana,…

    “sina ufahamu sana labda tumuulize jehova”

    Aliongea Yohana huku Jacob akakata simu na kupiga simu moja kwa moja kwenda Nigeria kwa mr jehova, mwanadamu aliejipa jina la mungu



    “haloo mr jehova hali yako”

    Alisalimia mr jacob lakini jehova alicheka kisha akasema

    “hahahahaha,… Naona Tanzania inatetemeka… Ila msiwe na shaka, nadhani masharti yetu mnayafahamu vizuri,… Kikubwa wewe kabidhi mtoto wako vitu vyote na umwambie ukweli, hapo hawato weza kufanya chochote”

    Aliongea jehova huku jacob akibaki mdomo wazi kwa taarifa hizo

    “ina maana bwana jehova, wewe unafahamu kila kitu”

    “haswaaaaa…. Mr Joshua ametoka asubuhi ana inasemekana yupo katika iziala yake ya Afrika Mashariki, hivyo kwa wale wenye imani kama sisi, kama hawana watoto basi wajiandae kuachia mali, pesa, nguvu, na makampuni yote”

    Aliongea jehova tena akiwa Siriasi kabisa,…

    “sasa kwa ambae hana kijana, atarejeshaje mali”

    “ahahahhahhahah, mr jacoboooooooo…. Wewe una kijana sasa shida nini… Kama kijana wako atakataa, basi una wasichana hata wasichana inafaa, kikubwa aridhie mikoba yako… Na huhitaji kurejesha kama ulivyokuja kuchukuwa… Ukilala ukiamka, utajua tu hapa vitu vinarudi kwa wenyewe”

    Aliongea jehova huku jacob akiwa kumkatisha jehova kuongea

    “basi basi, kata simu mara moja”

    Mr Jacob alikata simu kisha akampigia mama Adam ambaye ni mke wake mana ndio kaenda kumchukua adam kule kwake..”

    “we mwanamke mbona huji,… Hebu wahi bwana… ”

    “nakuja baba Jessica, ndio namuweka kwenye gari, mana Jessica hayupo”

    “sawa, wahi mara moja bwana”

    Aliongea jacob huku akifoka sana, mana ukweli keshapewa sasa anasubiri nini, na sababu ya mitetemeko ni kuwasili kwa mchungaji joshua… Mana nguvu zinagongana, na karibu jiji zima lina wachungaji ambao sio wa halali, hivyo alipotua tu uwanja wa ndege, kila mwenye njia ya shetani alitetemeka mno….

    Sasa mara ghafla simu ya mr jacob inaita, alikuwa ni mr jacob amepiga tena…

    “mbona umekata simu mr jacob, hivi vitu havihitaji papara kama unavyo dhani, kuwa mpole….”

    “nilijua tumemaliza mr jehova, Samahani sana”

    “sasa sikia… Hakikisha kabla ya kesho uwe umeshamkabidhi mwanao wa damu mikoba hio”

    Aliongea mr jehova huku jacob akiuliza tena

    “mwanangu wa damu kivipi sasa, si mtoto wangu tu basi”

    “ndio ni mtoto wako… Nasemea pale mtoto wako atakapo kataa, Haruhusiwi kumkabidhi mtu yeyote ispokuwa damu yako tu”

    “nimekueleeeeewa mr jehova”

    “asifiwe bwana mwokozi wetu”

    “milele amina”

    Jacob alikuwa akitoka jasho,…



    Sasa huku KIA, Jessica keshafika, na wakati huo kashika simu yake anampigia mama yake simu,…

    “helo mama?… Nenda kwa kaka adam pale, ukakae nae mimi nipo kia, nimekuja kumpokea mchungaji joshua”

    Aliongea Jessica, huku mama akishangaa

    “mchungaji Joshua??….”

    “ndio”

    “yule wa Nigeria”

    “ndio mama… Nenda kwa kaka, kule yupo peke yake”

    Aliongea Jessica huku akiwa spidi hapo kwenye kona ya kuingilia KIA,

    “mwanangu Jessica, kwanini hujasema kabla”



    Sasa huku kwa mr jacob, alianza kumpigia Jessica simu… Lakini simu ikamjibu kuwa,.. Unaempigia anaongea na simu nyingine, mr jacob alikata simu kwa hasira huku akikaa lakini havikaliki, mana kufilisiwa na kuonekana kituko sio jambo la mchezo mchezo…



    “mama, kwani kuna nini mpaka unasema hivyo”

    Aliongea Jessica baada ya mama yake kumwambia, kwanini hajasema mapema

    “adam ndio nafunguliwa geti hapa.. Nyumbani, nimeshakuja kumchukuwa tayari”

    Jessica alishtuka sana kuskia mama yake kaja kumchukua adam, na sasa wapo nyumbani

    “mamaaaaa…. Kwanini lakini”

    “kwani huyo mchungaji, si aje moja kwa moja huku nyumbani”

    “aaahhh sawa, nitafanya hivyo mama”

    “sawa uwahi basi”

    Mama hapo hapo anapiga honi, kweli keshafika nyumbani,… Mzee jacob anachungulia dirishani, aaahhh mkewe ndio anaingia, lakini mzee hakuwa na mzuka tena, na hata mama pia kashtuka kwanini baba Jessica kamtaka adam kwa haraka hivyo,… Na alimwambia amuombee apone, lakini mzee akasema wacha mwezi uishe, papo hapo akabadirika na kusema, akamlete sasa hivi amuombee… Lakini ukweli ni kwamba mzee jacob anataka kumkabidhi adam mikoba yote, na adam keshafika tayari…. Wakati huo adam tayari kazinduka kwa ule mtikisiko wa gari, mana mama alikuwa akiendesha kwa haraka sana, kwahio adam alikuwa akitembea lakini kashikwa mana akili ya pombe bado anayo….

    “mtoto wako huyo hapo”

    Aliongea mama na kumkalisha adam kwenye sofa,.

    “hebu mpe supu kwanza, apate nguvu”

    Aliongea mzee jacob huku mama akifanya mpango wa supu nzito



    Wakati huo huku KIA, Jessica alishamchukua mgeni saa nyingi sana na walikuwa njiani kuja nyumbani, mr jacob hajui kama mgeni analetwa hapo hapo ndani kwake, yaani laiti angelijua sijui angafanyaje,….

    Jessica alimpigia simu eva

    “halo eva?”

    “Abee wifi”

    “asifiwe bwana yesu Kristo”

    “milele amina wifi”

    “sasa… Hebu nenda pale nyumbani”

    Aliongea Jessica huku eva kama akikataa

    “wifi, kwa matendo ya kaka yako.. Nitawezaje kwenda”

    “leo anaombewa, lazima uwepo pale”

    “anaombewa na nani sasa… Mana kama ni kuombewa na baba yake angesha ombewa muda mrefu tu”

    “no, hapa nilipo nipo usa riva, natokea moshi Kilimanjaro kumchukuwa mchungaji joshua”

    “mchungaji joshua…. Joshua huyu wa Nigeria au”

    “ndio”

    “yesu wangu, wifi… Naenda jamani wifi yangu, nakwenda sasa hivi”



    Sasa huku baba kila akijaribu kumpigia Jessica simu, anaambiwa inaongea na mtu mwingine, mzee anakasirika kuskia hivyo, anatamani hata kuipigiza hio simu chini… Lakini kavumilia tu

    “basi fanya haraka… Mana adam yupo nyumbani kabisa kule”

    “sawa wifi… Nashukuru kwa taarifa hizo”

    “ok Sawa”

    Eva alikata simu kisha akampa taarifa mama yake, wakabebana wote,



    “mwanafunzi wangu amekuwa nini kwani”

    Aliuliza bwana joshua huku Jessica akimjibu

    “baba mtumishi… Kwa sasa adam amekuwa mlevi, amekuwa mzinzi, amekuwa mtu wa ajabu kabisa”

    Aliongea Jessica tena bila kumficha mchungaji

    “asifiwe bwana mwokozi wetu alie hai, lakini kijana hakua na tabia hio… Sasa imekuwaje”

    Aliongea at Bishop joshua huku Jessica akisema yote

    “ni kweli,.. Sema walimchanganya sana… Mana ana mchumba wake, lakini baba akamchagulia mtu mwingine, ndio hapo adam akakataa, ndio mpaka sasa hivi hajaoa.. Lakini kapewa utumishi wa mungu”

    Aliongea Jessica, wakati huo ndio wanakaribia kuingia mjini Arusha, wapo kimandoru..



    Huku nyumbani eva na familia yake nae hao, wanaingizana… Adam kapiga supu nzito, kidogo pombe ikapungua makali, hivyo hata kuongea anaweza kuskilizana na watu… Lakini baba ule mzuka wa kumtaka adam uliisha kabisa

    “baba Jessica… Ulisema nimlete adam, ndio huyu sasa”

    Mara eva haooo

    “heeee mama…. Asifiwe bwana Yesu Kristo”

    Eva alimsalimia mama Jessica au mama mkwe wake

    “milele amina mwanangu, umetususa mno”

    “mama, kweli, lakini ni kutokana na hali ya mwenzangu sijaipenda”

    “najua….. Haaaaaa umekuja na mama”

    “ndio”

    Mama adam alisalimiana na mama mwenzie, wakati huo eva kapiga goti kwa baba mkwe

    “asifiwe bwana yesu Kristo baba”

    “milele amina mwanangu, karibu”

    Adam alishangaa kumsikia baba yake kamwitikia eva kwa heshima mno…

    “Ahsante sana baba”

    Sasa mama akamuuliza mzee jacob tena,… Tena mama alijua baba kamuita adam na huyu eva ili waje kutambulishana….

    “baba Jessica…. Watoto ameshafika hawa”

    Aliongea mama Jessica huku baba akisema

    “hivi Jessica yuko wapi… Ndio namsubiri hapa”

    “lakini ulisema unamhitaji adam”

    “hapana, nilisema Jessica”

    Baba alikataa kuwa alimtaka adam, sasa hapa kuna walakini wa hii familia hapa…. Tutajua huko mbele..

    “Jessica kaenda KIA”

    Aliongea mama huku baba akimuuliza

    “kaenda kia kufanya nini… Keshafata yule mzungu wake”

    Aliongea hivyo baba huku mama akishangaa

    “baba Jessica,… Sasa mzungu gani na wakati kaenda kumchunkuwa mchungaji joshua”

    Heeeee, heeeeee, heeeeee… Baba kusikia Jessica ndio kaenda kumchukuwa mchungaji joshua,.. Alitoa macho hayo heeeeeeee…

    “unasemaje we mama Jessica”

    “Jessica, kaenda kumpokea mwalimu wa adam wetu”

    Sasa hawajakaa vizuri, mara honi ilipigwa nje ya geti,… Sasa Baba anaijua honi ya gari ya adam

    “huyu si yupo hapa… Mbona gari yake inapiga honi huko nje”

    “nadhani ndio alioitumia Jessica”

    Baba kuskia hivyo, alianza kutetemeka huku akifunua pazia… Kweli alikuwa ni Jessica akiingia



    Sasa ile gari inaingia tu, nywele za mr joshua zilianza kumcheza cheza Kiduku,… Kuashiria kwamba anapoingia sio sahihi na hapako salama kabisa….

    “hapa ndipo anapoishi yule kijana”

    Aliuliza mr joshua, huku Jessica akipaki gari vizuri

    “ndio, mtumishi… Ni hapa”

    “kabisaaaa kaishi hapa na kuridhika kabisa”

    “ndio, na ndipo alipo zaliwa”

    “yesu wangu Kristo…. Hapa mbona kama jehanamu kabisa hapa”

    Sasa alipoongea jehanamu, Jessica alishangaa

    “jehanamu tena”

    “yes….”

    Jessica yeye hana upako wowote, na unaambiwa ukiwa unaishi humo huezi jua lolote, na ndio mana adam alivyo hama tu, akajua kuwa kwenye nyumba ya baba yake sio sehemu salama kabisa….

    Sasa mr joshua akaanza kushusha maombi hapo hapo nje,… Mzee Jacob saa ngapi asianze kutetemeka huku akikimbia chumbani kwake, mama Jessica na mama eva pamoja na watoto wake wanashangaa kukimbia kwa mr jacob,… Lakini na wao walianza kudondoka mmoja baada ya mwingine, na sio hao tu hata Jessica mwenyewe aliekwenda kumchukuwa pia alianza kugala gala chini,….. Eva, bite, mama yao… Na mama Jessica, na martha, na maria, na mfanyakazi wao… Na adam mwenyewe, wote wanagala gala chini.. Mr joshua aliingia ndani na kukuta hapo sebuleni ni mgalo galo wa watu, kitu cha kwanza alimkimbilia kijana wake, akamwombea haswa,.. Shusha maombi, sasa maombi yanashushwa kwa mmoja lakini wote hapo ndani wanatetemekana… Kule ndani mr Jacob ndio hutompenda, amebadilika na kuwa kitu cha ajabu sana,.. Mikono ilianza kujikunja,… Sura ilianza kubadilika kabisa, masikio yalianza kuzidi kichwa… Hayo ni yale mashetani yake, yanamrudia mwenyewe, kwahio hayajatoka bali yanarudi kwake… Adam alishushiwa maombi mpaka akazimia kabisa….



    Sasa mchungaji joshua akawa anatoa maombi kwa wote, sasa hayo maombi yanawatetemesha mpaka viongozi wengine waliopo karibu na mtaa huo, ambao wana imani ya kishirikina,… Mchungaji aliomba mpaka anatokwa na mchozi ya uchungu,… Baada ya muda akatulia huku akiomba taratibu katika moyo wake,… Wa kwanza kuzinduka alikuwa ni adam pekee….

    “tumsifu yesu Kristo YOUNG PASTOR”

    Adam kuangalia ni mwalimu wake, na ndio mchungaji mkuu Afrika kwa wale wenye imani ya mungu..

    “mwalimu…. Asifiwe bwana Yesu Kristo,…. Baba mtumishi Afadhali umekuja baba”

    Adam alimkubatia at Bishop Joshua huku machozi ya uchungu yakimmwagika,… Joshua alikuwa akiomba kimoyo moyo lakini adam kajua mwalimu wake anaomba nini, unajua adam ana upeo fulani anao, hivyo anaweza kukugundua unacho kinena kwa wakati ule, hivyo kuna maono fulani adam kabarikiwa na mungu, na adam ni kama mtu spesho katika watu waliochaguliwa kuwa watumishi wa Mungu,…. Sasa adam akaungana na mchungaji wake, wakaanza kuangusha maombi, omba sana….. Omba sana… Nje ya nyumba hio wale wenye matendo maovu ni kugala gala gani huko njiani, yaani kila aliesikia maombi hayo hata kama huyo nje ya hio nyumba, kama kayasikia lazima adondoke kama alikuwa hana upako wa kweli… Maomi yalivyo isha, wote wakawa wameamka, sasa kila mmoja anashangaa shangaa…. Mara Adam akasema….

    “mwalimu….. Kile chumba kile… Nataka leo tujue kuna nini mule ndani”

    Aliongea adam huku akinyoosha kidole

    “kwanini nimekufunsha karibia uwezo wangu wote, na umeshindwa kukabiriana na hili”

    Aliongea mr joshua kama kumfokea adam

    “niwie Radha baba mtumishi”

    “haya njooo…. ”

    Mr Joshua alimshika adam mkono na kuenda nae mpaka kwenye chumba husika, huku watu wengine wakifuata nyuma, karibu yumba yote

    “lakini funguo,…. Mama baba yuko wapi, atupe ufunguo”

    Adam alimuuliza mama lakini tb joshua akamgeukia adam

    “wewe, katika masomo kuna malango hukuwa nayo makini… Ulizani hapa panahitajika ufunguo?? Labda tutumie busara ya aliofunga ndio afungue, lakini tukiamua hapa… Huo mlango si kitu”

    Aliongea mr joshua huku, adam akiambiwa na mama yake kuwa baba yake yupo huko ndani,… Adam alikwenda na kumkuta baba yake kalala hapo chini,… Sasa yale mapepo yameshamtoka, mana yalikuwa yanarudi kwake na kumfanya kitu cha ajabu, lakini yalizidiwa na maombi, yakaondoka.. Wenyewe wanaita yamesafiri…

    “baba…. Mtumishi…. Mchungaji”

    “eeee… Wewe… Eee”

    Baba aliamka na wengi sana..

    “asifiwe bwana mwokozi wetu alie hai”

    “milele amina…. ”

    Sasa baba alianza kulia huku akitoa kisanduku kimoja ambacho kilikuwa uvunguni,… Alipokifungua alitoa funguo mana anajua kuna siku adam alimwomba baba yake fungua akamwambia kuwa huko hakuna kitu zaidi ya spea za magari… Sasa leo baba anampa funguo yeye mwenyewe,… Adam hakuondoka bure, alitoka nae mpaka sebuleni, lakini sasa kitu cha ajabu na cha kushangaza,… Baba yake adam alimpigia magoti mama yake eva…. Yaani mama yake eva ndio kapigiwa magoti, mpaka mama huyo akashangaa…. Sasa ile adam anataka kuchomeka ufunguo tu,.. Akakatazwa, mana anaetakiwa kufungua ni yule aliefunga mlango huo,… Sasa baba baada ya kupiga goti kwa mama na kuomba msamaha alikwenda kupiga magoti na kwa watoto wa mama huyo, yaani eva na bite…. Sasa kila mmoja anashangaa, ni kwanini anafanya hivyo???….

    “baba… Baba…. Basi inatosha… Shika ufunguo huu, tufungulie ule mlango pale”

    Aliongea adam huku mzee akikubali bila ubishi, mana hapo alipo kang’aaa hana ushetani wowote ule,

    “sawa mwanangu… Nakwenda kufungua”

    Baba kausogelea mlango wake, kisha akachomeka ufunguo…… Baba bila woga alisukuma mlango huo ukafunguka wote… Laaaaa haulaaaa..









    Katika hii dunia kuna watenda dhambi na kuna watenda mema, mr Jacob ni mmoja kati ya watu ambao bado hawajabarikiwa kupewa utumishi wa mungu, hivyo ni kama alijivika mwenyewe tu…



    Sasa leo mr Joshua katua Tanzania kwa ajili ya iziala yake ya kama mwezi hivi, ujio wake tu uliwatetemesha wengi wenye imani ya shetani,… Mr Jacob ndio mkuu wa wenzake katika jiji hilo, na vile mungu sio Asumani, mr Joshua kaingizana hapo hapo nyumbani kwake, kitu ambacho ni hatari zaidi kwa bwana Jacob…



    Maombi yalifanyika mpaka kila kitu kilikaa sawa, mr Jacob alikuwa akigeuka kiumbe cha ajabu, lakini maombi yalivyozidi kurindima wale mapepo walitoweka na kupotea.. Ilifikia wakati chumba muhimu ambacho adam alikitamani siku nyingi kujua hizo spea za magari huko ndani vipi, mbona hazitokagi ingali magari huharibika,.. Sasa leo baba kwa mikono yake mwenyewe anakwenda kufungua mlango wake alio ufunga mwenyewe



    Baba kausogelea mlango wake, kisha akachomeka ufunguo…… Baba bila woga alisukuma mlango huo ukafunguka wote… Laaaaa haulaaaa

    “haaaaaaaaaa, babaaaaaaa”

    Eva alitahamaki huku akiita baba, mpaka eva akazimia, mama yake nae akazimia,… Walitoka watu watatu, waliokonda sana tena licha ya kukonda, pia wamechafuka kama vile walikuwa wakiogelea kwenye unga,.. Mikono yao ilikuwa dhoofu sana, na mmoja wa watu hao ni baba yake eva,… Na ndio mana eva aliita baba na kuzimia,… Mr Joseph mzee wa kanisa la baba yake adam kumbe hakufa, bali alichukuliwa sukule ili wanavyo changanyikiwa huku ndani, kule kanisani mr Jacob anapiga hela tu, na nguvu kuzidi kuingia… Sasa wengine wawili walikuwa ni waumini wa kanisa la mr jacob,… Mmoja aliitwa Paulo, na mwingine aliitwa Emanueli, hawa wote walikuwa ni misukule wa mr jacob ili kujipatia kipato kupitia dini,… Mr joshua hakushangazwa na jambo hilo mana sio jambo la kwanza kuliona… Mr joshua aliwasogelea misukule wale ambao kwa wakati huo walikuwa tulivu mana mapepo yalisha watoka wakati wa maombi ya mwanzo… Mana wale mapepo walipo toka ndio waka waachia na hawa misukule…

    Maombi yalishuka juu yao,… Maombi yaliombwa kwa ajili yao, maombi yaliombwa takribani masaa mawili yalikuwa ni maombi tu…. Tena kwa kulia haswa…..



    Kesho yake mr jacob alitoka na gari wakati wa saa nne hivi kuelekea mjini, lakini alipotoka tu, alikutana na magari kama manne ya kiserikali…

    “habari yako mr Jacob”

    Alisalimiwa mr Jacob huku wakishuka wote katika gari

    “salama kabisa, haya nyinyi ni akina nani labda”

    Mr Jacob aliwauliza waungwana hao

    “sisi ni afisa wa mapato TRA, unatuhumiwa kwa makosa ya kujenga makanisa yako katika viwanja vya serikali na hukuvilipia… Mpaka sasa unadaiwa kodi bilioni mia mbili na pointi nne”

    “haaaaaaaa…. Kwanini lakini”

    “nadhani maelezo mengi tutayajua kituoni… Mana nimekuja na askari hawa hapa”

    “ok sawa sawa… Twendeni benki nikawalipe pesa zenu… Ni pesa ndogo sana hio…”

    Aliongea mr Jacob huku wakipanda katika magari yao, kuelekea benki kulipwa bilioni mia mbili, ama kweli mr Jacob ana pesa acha utani, bilioni mia mbili ni bajeti ya Tanzania nzima kwa kwa miezi kadhaa… Lakini yeye anayo,



    Mr joshua hakuhangaika kulala hotelini, wakati mwanafunzi wake ana jumba la kifahari ambalo anaweza kulala….

    Adam akiwa tayari keshajiandaa na hata mr joshua nae alikuwa keshajiandaa vyema,…

    Walitoka moja kwa moja mpaka kanisani kwa adam,.. Katika kanisa hili walimkuta eva na baba yake na mama yake, pamoja na mdogo wake, yaani familia nzima ipo hapo kanisani, katika maombi…waliomba sana….

    Mara mama yake adam pamoja na familia yake yote waliingizana nao hapo hapo kanisani, kasoro baba tu ndio hayupo kwa wakati, mana amekwenda benk na wale afisa wa mapato TRA mana kajenga makanisa kwenye viwanja ambavyo ni vya serikali na havikulipiwa hata mwezi mmoja,.. Viwanja zaidi ya 50 vyote ni vya serikali, na anadaiwa kuanzia alipoanzisha kanisa la kwanza… Na imepigwa mahesabu ni hizo bilioni mia mbili

    “tumsifu Yesu Kristo”

    Aliongea mr Joshua huku waumini wachache tena wana familia pekee wakiitikia

    “milele amina baba mtumishi”

    Kanisa lenyewe ni la kifahari, afu ndani ya kanisa kuna mchungaji mkubwa Afrika,… Inapendeza sana

    “aaahhh jamani, nadhani kijana huyu alishawatambulisha kuhusu mimi…. Mimi ni mwalimu wake toka Nigeria, ndie nilimpa elimu ya Biblia ingali wito wake anao,… Unaweza ukapewa wito lakini elimu ya Biblia ukawa huna, sasa mimi ndie niliempa elimu ya Biblia (Bible study)”

    Aliongea MCHUNGAJI huyo huku familia hizo zikimsifu bwana Yesu Kristo kwa neema zake,….

    “mama wa kijana huyu, yuko wapi”

    Mchungaji alimtaka mama yake adam

    “nipo hapa baba”

    “mmhhh natumaini leo baba atakuwa kabanwa na mambo yake yaliomsibu”

    “ndio baba mtumishi”

    “aahhh nimekuja Tanzania kwa niaba ya iziala yangu ya mwezi mzima… Na nilipendekeza kuanzia arusha, kwasababu najua kuna zao langu.. Akiwa ni mr adam jacob… Aaahh kwa kifupi ni kwamba, katika iziala hio nahitaji kitembea nae akiwa kama mwenyeji wangu… Lakini kabla sijaanza kutembea nae, nataka kwanza atafutiwe mchumba aoe”

    Eva kuskia adam atafutiwe mchumba alishtuka na kudhani labda huyo mchungaji ndio wale wale kama mr Jacob

    Lakini kabla mr joshua hajaendelea mama yake adam kanyanyuka na kuongelea swala la mchumba wa adam,… Mchungaji akaelewa…

    “kweli, hakika bwana Yesu kakuchagulia mke…. Nahitaji kesho nikufungishe ndoa mimi mwenyewe kijana wangu”

    Aliongea mr Joshua huku familia zote zikiwa na furaha… Lakini eva ni zaidi ya furaha mana alikuwa akilia kabisa…. Basi ibada ilikwisha na mr joshua alitaka kupumzika kidogo, hivyo alirudishwa nyumbani kwa adam…. Wakati huo nao akina Joyce au mama yake adam, tayari nao wapo nyumbani… Lakini adam alipigiwa simu na mama yake kuwa aje nyumbani mara moja…. Adam alimuaga mtumishi, au mwalimu wake kuwa anatoka kidogo….



    Huku benki mr Jacob kachanganyikiwa,….

    “kadi ya benki hii hapa… Unasemaje hakuna akaunti kama hio”

    Aliongea mr Jacob huku akitaka hata kurusha ngumi kwa muhudumu,…

    “mzee, hii kadi ni feki, na pia nimengalia akaunti namba huku haipo na wala hakuna namba kama hio”

    “acheni wizi nyinyi, trilion moja, afu leo unaniambia hakuna pesa hata kidogo”

    “mzee sio kuwa hakuna pesa… Bali hio akaunti huku hakuna”

    “mbona wiki hii iliyopita nilikuja kutoa bilioni moja, tena hapa hapa.. Sasa hio akaunti ilikuwa ni ipi”

    “samahani sana… Labda hukutumia akaunti hio, kumbuka vizuri baba… Huenda una akaunti nyingine”



    Mara wale maafisa wakajua huyu ndio wale wale akina mzee wa 900 Itapendeza zaidi…

    “mzee, hapa sasa tumekuvumilia tumechoka… Hapa ni moja kwa moja mahakamani usomewe vifungu vyako tujue cha kufanya”

    “lakini afande”

    “hatuna la zaidi… Wewe twende”

    Lakini ile anakokotwa kwenda kwenye gari, ghafla alikutana na mr Yohana, mchungaji mwenzie



    “vipi tena mr Jacob? Nini kimetokea”

    Aliongea bwana yohana yeye alikuwa bado hajakutwa na dhahama hio

    “samahani ndugu zangu… Nipeni dakika tano niongee na ndugu yangu huyu”

    Aliongea mr Jacob na kwakuwa mr Yohana anajulikana kuwa ni Bishop mkubwa hapa jijini…

    “hakika ni dakika tano… Bila hivyo utatuona wabaya”

    Ilikuwa ni sauti ya kamanda mmoja aliokuwa akitia mkwara kwa mr jacob, yaani sasa mr Jacob hana sifa yeyote na huezi amini ya kwamba sasa hakuna anaemjua mr Jacob na wakati alikuwa akijulikana kila kona ya Afrika, lakini leo hajulikani tena..



    Wakati huo huku nyumbani adam ndio anafika nyumbani kwao na kumkuta mama na dada yake Jessica peke yao, yaani adam ni mtu wa tatu kati yao…

    “kaa pale”

    Mama alimwambia adam akae mahali fulani, kwa maongezi zaidi…

    “haya mama, nimekuja… Na najua tu unataka tupange mambo ya harusi,.. Kiukweli nina furaha sana”

    Adam aliongea hivyo lakini sicho walicho muitia, mama kuna jambo alitaka kuongea na mtoto wake, na inaonekana hata Jessica analifahamu hilo…

    “hapana… Wala sijakuitia kwa swala la harusi…. Kuna jambo nahitaji ulijue mwanangu… Na nikuombe samahani kwakuwa sijakwambia kwa muda mrefu…”

    “mamaaaa….sioni haja ya wewe kuomba samahani… Wewe sema tu”

    Aliongea adam huku mama yake akijiandaa kusema jambo

    “mwanangu adam…. Wewe ni… Ni ni… Ni mtoto wangu wa damu, lakini sasa”

    Mama aliishia hapo huku adam akianza kuwa na wasiwasi juu ya jambo hilo



    Huku maeneo ya benki kwa mr Jacob na rafiki yake mr Yohana, ambaye bado hajakutwa na dhahama ya maombi, ila ujio wa joshua anaujua

    “bwana wewe…. Nimekutwa na dhahama hio sio ndogo…”

    Aliongea bwana Jacob huku yohana akiendelea kumsikiliza….

    “enheee dhahama gani tena”

    “jana unakumbuka tuliongea sana kuhusu tetemeko”

    “ndio nakumbuka vizuri sana”



    “sasa basi,.. Niliongea na jehova kuhusu swala hilo akaniambia kuwa joshua amekuja Tanzania kwenye iziala yake, hivyo msaada wenu ni kuwakabidhi watoto wenu hio mikoba… Kiukweli kwa swala hilo kwangu sikua na hofu nalo,… Na wakati huo nimeshamtuma mke wangu aende nyumbani kwa adam akamlete ili nimkabidhi mali zangu zoote na mikoba yote…. Saa ngapi jehova hajapiga simu tena… Akaniambia hakikisha unamkabidhi mtoto wako wa damu…. Nikamuuliza una maana gani.. Akasema ukimkabidhi mtoto ambae sio wako haiwezekani na haikubaliki…. Hapo bwana yohana, niliumwa kichwa ghafla”



    Aliongea bwana jacob kuwa aliumwa kichwa ghafla baada ya kuambiwa kuwa amkabidhi kila kitu mtoto wake wa damu

    “ahahahahahahaha, sasa wewe mjinga sana… Dume unalo, kichwa kikuume cha nini sasa…”

    “mr yohana?…. Mimi nilivyoambiwa kiwa nimkabidhi mtoto wangu wa damu, ikabidi nimpigie Jessica sasa..”

    “hebu ngoja kwanza nikukatishe maongezi yako….. Sasa utaacheje kumpa mikoba mtoto wa kiume afu ugeuke kwa mtoto wa kike”



    “mr yohana? Nakuelewa sana… Ila Naomba iwe siri yako…. Yule adam sio mtoto wangu… Niliwakuta yeye na mama yake wana maisha mabaya sana kipindi hicho mimi bado ni mwinjilisti nazunguka mtaani na supika langu nikitangaza neno la bwana… Yule mtoto alikuwa ana mwaka mmoja, na yule mama alikuwa bado binti mdogo… Afu nikiangalia mke wangu kanikimbia na kuniachia mtoto mmoja wa kike… Nikaona wacha nimchukue… Kama ni huyo mtoto wake nitamlea… Ndio ikawa hivyo mpaka leo yule mtoto hajui kama mimi sio baba yake… Na ndio maana jehova alipo niambia unatakiwa umkabidhi mtoto wako wa damu, ndio mana nikamgeukia Jessica, baada ya kuona adam hafai tena kukabidhiwa mikoba”



    “alaaaaaaaa… Kumbe ndio hivyo…. Sasa kwanini hujamkabidhi Jessica mikoba”

    Aliongea mr yohana, na kumuuliza hapo hapo, huku mr Jacob akajibu kuwa

    “sasa nilipohamia kwa Jessica, simu yake ilikuwa bize… Sasa nakuja kumuuliza mama yake kuwa Jessica yuko wapi, akaniambia Jessica kaenda KIA kumpokea mtumishi joshua…”

    “haaaaaaaa”

    “sikiliza sasa..”

    “enhee endelea”

    “sasa ile anamalizia tu kusema kuwa Jessica kaenda KIA… Ghafla honi ya gari inalia nje ya geti… Kuchungulia hivi ni Jessica anakuja na mr joshua.. Hapo ningekuwa na ujanja gani tena”

    “aaahhhh pole sana rafiki yangu… Poole sana… Ila huyo mtoto unapaswa umwambie ukweli kuwa wewe sio baba yake”

    “nitamwambia endapo hili likiniishia”

    “sasa hawa askari wanakutolea macho sana.. Wewe nenda, nitakuja kukushikia mzamana”

    “sio mzamana tu… Nilipie kodi yao, nitakulipa…. “

    “hio sintoweza… Mana ukumbuke wewe ndio mkubwa wetu… Nitakachoweza ni kukushikia zamana tu”



    Sasa huku nyumbani adam katega sikio ingalia sisi tayari tumeshajua kuwa adam sio mtoto wa mr Jacob, ila adam mwenyewe bado hajajua kuwa yeye sio mtoto wa mr Jacob na anadhani ndicho alicho itiwa na mama yake…

    “mama una maana gani kuongea hayo”

    Adam alimuuliza mama yake, wakati huo Jessica kakaa kimya hana la kusema na yeye pia anajua kuwa adam hakuzaliwa nae… Lakini hajawahi kumdokezea hata kidogo

    “adam…. Huyu baba yako… Sio baba yako mzazi…. Wewe umezaliwa katika koo za Kiislamu… Jina lako unaitwa Sharbiny Rashidi Kingazi”

    Aliongea mama huyo huku adam akishangaa na kitoa macho

    “Whaaaaaaaaaaaat????…. Unasemaje mama??”







    Adam alishangaa sana kuskia kuwa yeye amezaliwa katika koo za Kiislamu, kwahio adam ni damu y Kiislamu,… Adam alitamani kujua chanzo cha yeye kufika

    “hapana mama, mimi siwezi kuamini maneno yako mama,… Hebu mwogope mungu mama angu,.. Jana tu tumeomba hapa na sasa familia nzima tumetakasika kwa maombi toka kwa mchungaji alienifundisha Biblia, sasa kwanini unene uongo mama yangu”

    Aliongea adam kama vile hataki kuamini jambo hilo.

    “Jessica…. Hebu mwambie mdogo wako, kwanini hataki kuamini kwamba yeye sio mtoto wa mr Jacob”

    Mama alimwambia Jessica kuwa amwambie adam kuwa sio mtoto wa mr Jacob,

    “ni kweli mdogo wangu… Ulikuja kwetu ukiwa na umri wa mwaka mmoja…. Kwetu nilikuwa mimi peke yangu, mana mama yangu mimi aliachana na baba, hivyo hata huyu mama yako wewe, sio mama yangu mimi, mimi nina mama yangu japo hakuwahi kuja kunisalimia kama mtoto wake, lakini huyu ndio mama yangu mimi”

    Aliongea Jessica huku adam akianza kuamini, lakini kabla hajaamini ametaka kuambiwa kuwa ilikuwaje mpaka kufika katika falme ya kikristo, mama hakutaka kumficha kitu mtoto wake

    “mama?….. Kabla sija waamini nahitaji ukweli zaidi juu ya hili… Ilikuwaje”

    Aliongea adam huku mama akilia kwa kutoboa ukweli siku hii ya leo,

    “nitakwambia baba… Wala siwezi kukuficha”

    “halafu, Samahani kabla hujaendelea, umesema mimi naitwa nani”

    Adam aliuliza kwa msisitizo jina aliloitwa kipindi akiwa muislamu…

    “wewe uliitwa Sharbiny Rashidi Kingazi…. Babu yako mzaa baba anaitwa kingazi”

    “hebu ngoja kwanza… Pale ofisini kwangu,… Kuna bwana mmoja anaitwa Abdallah Rashidi Kingazi… Hili jina vipi hapa”

    “baba…. Nitakwambia yote baba yangu, utayajua tu”

    Sasa adam kumuuliza yule kijana mwenzie aliomwajiri pale kwenye kampuni yake,… Na anajua kuwa kuna mtu kamwajiri ana jina hilo… Lakini adam hakujua kwasababu hakuwahi kuambiwa kua ana baba wa Kiislamu na hata hilo jina amelijua leo, hii kuwa linamuhusu yeye



    SASA HAPA, TUPATE HISTORIA YA ADAM NA MAMA YAKE KABLA YA KUJA KATIKA NGOME HII YA KIKRISTO NA KUOKOKA KABISA



    ikiwa ni miaka ya nyuma kabisa miaka 22 iliopita kutoka sasa, katika jiji hilo la arusha maeneo yaitwayo Ngarenaro, uswahilini kabisa huko,..



    Sasa hapa mama anaanza kusimulia



    “kipindi baba yako ananioa, hakuwa na mke mwingine, zaidi yangu… Lakini ndoa yangu ikiwa bado mbichi, ina mwezi mmoja tu na siku kadhaa, bba yako akanitaarifu kuoa mke mwingine, kiukwe nililia sana, haswa ukizingatia maisha yalivyo magumu, kwani tulikuwa tumepangisha chumba kimoja tu,… Nililia lakini haikusaidia kitu, nilimkubalia baba yako aoe huyo mke wa pili, mana kwa imani ya dini ya kiislamu, mwanamke akikataa mumewe asio mke wa pili, anatakiwa aachwe na apewe talaka zote…. Kwakuwa nampenda mume wangu, nikakubali aoe lakini nikamuuliza…. Sasa tutaishi vipi katika chumba kimoja akanijibu kuwa atampangishia chumba chake na atatutimizia mahitaji yote, baba yako ni fundi wa magari,… Hakuwa na kipato chochote kikubwa cha kukidhi mahitaji ya wanawake wawili kwa pamoja… Basi nilimwacha baba yako, afanye anachojua, ilimradi tuishi kila mtu kvyake,… Kweli alioa lakini hata kwenye hio ndoa yao sikuenda mana sikupenda kuletewa mke wa pili,… Baba yako hakutaka kutuweka mbali sana, alimpangishia nyumba ambayo sio mbali na hapo nilipo mimi… Hivyo hata kuombana vitu, tulikuwa tunaombana… Mana ni kama nyumba ya kumi kutoka nilipokuwa naishi mimi…



    Maisha alikwenda, mimi na mke mwenzangu tulikuwa tukijifanya tu kupendana…. Lakinj kila mmoja alikuwa hampendi mwenzie…



    Kwa bahati nzuri tulishika ujauzito wote,… Ila tulipishana mwezi mmoja mmoja tu,… Mimi ndie wa kwanza kupata ujauzito, ambaye ni wewe,… Miezi ilisonga na hatmae nikajifungua, wakati yeye ndio ana miezi nane.. Huduma haikuwa mbaya sana, na labda ni kutokana na maisha magumu tulio nayo… Mana kilo moja ya nyama, nilikula siku nne.. Kitu ambacho hakitakiwi kwa mzazi.. Anatakiwa ale supu mpya kila siku.. Lakini kwangu haikuwa hivyo…. Lakini baba yako kila siku alikuwa akikushika anakuangalia sana usoni, mana ulikuwa ni mweupe,… Katika uso wako kuna kitu alikuwa akikiangalia lakini hakuwahi kuniuliza, miezi ilisonga… Hatimaye mke mwenzangu nae akajifungu,… Nakumbuka yule mtoto alikuwa ni wa kiume, na aliitwa Abdallah,…



    Lakini toka mke mwenzangu ajifungue, mahitaji kwangu yalipungua, nikaona labda mume wangu kazi sio nyingi,… Ilifikia mahali mpaka unga unaisha ndani… Yaani aliachana na mimi kabisa,… Hata uzazi sijamaliza… Na sijui kosa langu, siku moja nikasema ngoja niende kwa mke mwenzangu, mana baba yako ilifika mwezi sasa haji nyumbani, japo katusahau….



    Mwanangu, roho iliniuma sana pale nilipomkuta baba yako anafurahi na mke mwenzangu,… Tena alikuwa akinywa supu ya bata… Na hapo nje nikaona mabata kama matano hivi, na kila siku anachinjiwa bata… Naapa kwa mungi, mimi sikuwahi kuletewa hata kuku kwenye uzazi wangu… Nanunuliwa kilo ya nyama, naitumia ndani ya siku nne, maana yake kila siku natumia robo kilo,… Na bado hata sijamaliza uzazi baba yako akakata mawasiliano na mimi kabisa hata kulala haji, hata kuja kusalimia alikuwa Haji.. Roho iliniuma sana baada ya kukuta hali ile, tena alikuwa akimbembeleza mtoto wake aitwaye Abdallah,… Nililia sana pale nje ya ile nyumba, wakati huo mke mwenzangu anakula nyama ya bata,… Lakini mpaka hapo bado sikuwa na kinyongo na baba yako,.. Nikaingia ndani na kumsalimia,… Kisha nikamuuliza kuhusu sisi… Kabla baba yako hakunijibu, yule mwanamke alinicheka sana… Lakini bado nikamuuliza baba yako,… Ndipo akaniambia kuwa…. Unaona sura ya Abdallah, inafanana na mimi… Sawa wewe ni mweupe na mtoto wako ni mweupe,.. Sikatai kachukua weupe wako…. Sasa na hiki kidoti hapa… Mbona mimi sina kidoti.. Huyu mtoto ana kidoti hapa usoni… Mbona mimi sina…. Nilistaajabu sana kumsikia baba yako akiongea maneno yale,… Lakini hata yule mwanamke alishangaa kuskia kosa ambalo mimi nimesuswa nalo,… Kana kwamba kama mimi nimesusiwa mtoto eti kisa una kidoti cha usoni,.. Je yeye siku akiona tofauti pia si ataachwa.. Yule mke mwenzangu kuanzia siku ile aliacha kunicheka mana aligundua wanaume hawatabiriki… Nilimwambia baba yako huyu ni mtoto wako, lakini alikataa katu katu. Kumbe ndio mana pale alipokuwa anakushika alikuwa akikuangalia sana, sasa alikuwa anasubiri mtoto wa mke wa pili kama atakuwa na kidoti basi wote ni damu yake, lakini akikosa kidoti, basi wewe atakuwa sio mtoto wake… Baba yako alinikataa na kuniambia ameniachia kila kilicho huko ndani, nitajua mwenyewe kuanzia sasa hivi,… Nilirudi nyumbani, huku nikiwa nalia sana….



    Ilibakia mwezi mmoja kodi ya nyumba iishe, nilikuwa na kahakiba kangu kama elfu kumi, mana kipindi hicho kuwa na elfu kumi ni nyingi…. Basi nilianza biashara ya kuuza miguu ya kuku, utumbo wa kuku, bichwa vya kuku.. Uswahilini huko.. Wakati huo una miezi mitatu,.. Nakatazwa na wanawake wenzangu nisikutembeze juani, lakini nitafanyeje wakati kodi ya nyumba inaisha,… Basi nikawa nalipa mwezi mmoja mmoja hivyo hivyo siku zikazidi kwenda nawe ukakua… Nikaschana na miguu ya kuku nikaanza mtaji wa vitumbua… Hapo ulikuwa na miezi saba…. Maisha yalikuwa ni magumu sana… Hata afya ulikuwa huna,…



    Ilifikia hatua sasa baba mwenye nyumba anataka miezi sita sita… Na uwezo wa hata miezi miwili sina,.. Huo mmoja wenyewe najitahidi sana, najibana nashinda njaaa… Mana kipindi hicho kitumbua kinauzwa shilingi ishirini, hivyo hakukuwa na pesa…



    Ilifikia hatua mpaka tunadaiwa kodi ya nyumba, mana mtaji ulikufa pale ulipoumwa homa ya manjano, hapo ndipo kichwa kikaanza kuuma, nilimfuata baba yako anipe hata pesa ya hospitalini lakini hataki anasema nimpeleke mtoto kwa baba yake, kwani yeye sio baba yake….. Kuliko ufe mwanangu ilibidi niue mtaji wote, nikakupeleka hospitali, tena kulikuwa kuna redio la baba yako nikaliuza ili nizidi kupata pesa ya matibabu… Ulipona lakini niliporudi nyumbani, tumekuta mwenye nyumba kafungua nyumba yake… Alisema katuvumilia sana sasa imetosha, na ili tukomboe vitu vya ndani, basi tulipe kodi tunayo daiwa ya miezi minne bila kumlipa.. Nakumbuka ulikuwa na mwaka mmoja na ulikuwa umeshaanza hata kukimbia kimbia… Kweli sikua na la kufanya,.. Nilianza kuzunguka kwenye majumba na kutafuta hata kazi za ndani, mana nilikuwa bado ni msichana mdogo…. Nilikutembeza juani mwanangu,… Uliugua sana, nasaidiwa na watu… Nilikuwa nikilala kwenye vibaraza vya watu,.. Nalala kwenye majumba mabovu watu wamejisaidia lakini nitafanyeje,.. Nilitamani hata kwenda kuwa omba omba kule barabarani, lakini nilishindwa kwakua nina viungo vyangu vyote na naweza kufanya kazi.. Kiukweli mwezi mzima ulikuwa wa mateso ya kulala nje,…. Ilifikia hatua nikaamua kuvaa nguo chafu na kwenda kua omba omba pale safina.. Ili watu wakitoka katika maombi wanipatie angalau ya kula, mwanangu ulipigwa na jua haswa… Nilikaa pale takribani wiki… Na wala sikuwa nawakariri watu waliokuwa wakiniwekea hela katika bakuli langu,



    Siku moja nikiwa sijapata kitu,.. Bakuli lilikuwa jeupe sana… Nilishangaa kuona emedondoshwa elfu moja kwenye bakuli langu, na kijana mmoja wa makamo aliokuwa akibuliza redio lake akiwa anatoka kuitangaza injili ya bwana wao yesu,. Kiukweli nilimshukuru mpaka nikaamua kumsaidia kubeba lile redio lake, mana alikuwa kachoka, na hata viatu vyake vilikuwa vimeisha upande mzima kwa kutembea… Kijana huyo ambae alikuwa ni makamo yangu, lakini alinizidi umri kwa kiasi fulani.. Nilimbebea redio lake zito mpaka ndani safina,… Watu walinishangaa sana kuingia safina nikiwa mchafu, lakini pamoja na uchafu wangu wapo wanaume waliouona uzuri wangu…. Bwana yule aliniuliza kilichonisibu, lakini na yeye hakusita kuniambia matatizo yake,.. Aliniambia kuwa kaachwa na mke wake kwasababu amekuwa mtu wa kunuka jasho kila siku, mana alikuwa akiitangaza injili kwa miguu, yaani anatembea hapa na huko… Na redio lake yote ni kumsifu mungu wake,.. Baba yule alinionea huruma sana.. Na aliniuliza naishi wapi… Hapo ndipo alipochoka mana sikua na mahali pa kuishi…. Namshukuru mungu kwamba mwanaume yule hakua na subira hata kidogo… Aliniambia yeye ameachwa na mwanamke kwa kunuka jasho kila siku bila faida…. Hivyo mwanamke akaondoka na kumwachia msichana mdogo…. Sikuamini siku hio ananiambia twende nikapumzike kwake,.. Kiukweli sikusita kwakua nilikuwa nina shida…



    Nilifika kwake, alikuwa ana nyumba ya urithi wa wazazi wake… Kwani alifiwa na wazazi wake kwa ajali ya gari,.. Nilikaa nyumbani kwake ingali anajua mimi ni muislamu,.. Lakini kila anapofanya maombi yake nami nilikuwa nikiungana nae,.. Akiondoka kwenda kutangaza Injili aliniacha na mtoto wake wa kike aitwaye Jessica, alikuwa na mika minne hivi au mitano.. Basi nikawa namlelea mtoto wake,.. Nilimaliza mwezi nikiwa pale, hata afya yangu ilirudi, wewe ulikuwa na afya nzuri, kila ukiumwa alikuwa anakupeleka hospitali kama mtoto wake….



    Kuna siku alinishtua sana… Aliniambia kuwa, kwanini nisiwe mama wa watoto wake, yaani anioe.. Kiukweli kuolewa nae nilitamani toka mwanzo lakini nilikuwa nasubiria aanze yeye kusema…. Nilimwambia lakini mimi ni muislamu,.. Akasema najua kuwa ni muislamu… Na alisema kuwa mwanamke hana dini, ila kama nitapenda kuokoka sawa kama sintopenda sawa tuoane kwa ndoa ya kiserikali… Lakini alisema ndoa ya kiserikali, hua inachanganya watoto, wasijue waelekee dini gani… Kiukweli niliamua kuokoka moja kwa moja pamoja na wewe, kwasababu baba yako angekukubali basi usingeokoka, lakini kakukataa.. Na hata huyu mr Jacob nilimwambia baba yako kakukataa… Na yeye akasema kama kakataliwa na baba yake, basi nae aokoke na kuanzia siku unaokoka, akakupa jina la adam  na kumaanisha kuwa adam ni binadamu alioshushwa na mungu duniani, hivyo hivyo kwake akaona kama bahati kupata mtoto wa kiume,



    Lakini kabla hajaniona tulifuata taratibu za kuomba talaka kwa baba yako mzee rashidi,.. Mana usipopewa talaka, huruhusiwi kuolewa, na atakaenioa atafunguliwa kesi kwamba kaoa mke wa mtu…. Kiukweli baba yako alinipa talaka zote tena bila hata kufikiria.. Ndoa ya mimi na mr Jacob ilifungwa pale kwenye ukumbi wa safina nikiwa tayari nimesha okoka na kiwa Mkristo,…. Maisha yalienda, mr Jacob akajitahidi na maisha yake… Mpaka siku maisha yanakuwa makubwa, nikamzaa Martha, nikamzaa maria… Kwa upako wa baba yako alizidi kukua.. Na kila baada ya mwaka anaongeza kanisa moja au mawili… Maisha yalikuwa juu sana mpaka akaanza kumiliki kampuni nyingi na wewe ulishakua mkubwa,… Akakupeleka shule nchini Uingereza,.. Kisha ukasomea chuo huko huko… Uliporudi ndio ukakaa mwaka mmoja akakukabidhi kampuni ili ujikimu kwa mahitaji yako.. Na wewe ukawa na akili ukaanza kujenga nyumba na kanisa… Baada ya mwaka mwingine, ndio akakutafutia chuo cha Biblia huko Nigeria ndio ukaenda…..



    Sasa ulipoenda Nigeria, mimi ndio nilikuwa msimamizi wa kampuni yako, na nyumba yako, na kanisa lako



    Sasa Siku moja nikiwa ofisini kwako, nikasikia wafanyakazi wako wanaitana majina ya wazazi wao, sasa walikuwa wanamtania huyo mfanyakazi wa kiume alioitwa Abdallah, walikuwa wanamuita, kingazi cha kupandia… Niliwafokea wakaacha hio tabia… Nikasikia wakamuita mtoto wa rashidi kingazi, niliposikia hilo jina nikamuita yule kijana na kuanza kumhoji anapokaa na baba yake kila kitu nikamuuliza na documents zake, CV zake nikazisoma… Lakini yeye hakujua nimemuuliza kwa niaba gani… Alijua ni mambo ya kazi… Hapo ndio nikajua yule ni mtoto wa mzee rashidi ambaye ni mume wangu wa zamani, na sikutaka kukuambia… Lakini bora ujue…. Yule ni ndugu yako”



    HAPA NDIO MWISHO WA HISTORIA YA MAMA NA MTOTO WAKE….



    Adam alichoka baada ya historia hio, wakati huo mama analia sana tena jasho lilikuwa likimtoka kwa kuongea kwa muda mrefu….

    “kwahio mama? Mimi ni mtoto wa Kiislamu si ndio”

    Aliongea adam huku mama akimjibu kuwa

    “hapana.. Wewe sio mtoto wa Kiislamu, bali ulikuwa mtoto wa Kiislamu”

    Aliongea mama huku adam akiamka na kusema kuwa…

    “Samahani mama kwa maamuzi nitakayo amua… Naomba usinichukie mana siri hii umeniambia mwenyewe, hivyo uniache na maamuzi yangu…”

    Aliongea adam huku mama akikubali

    “sawa mwanangu… Sasa umeshakuwa sikuona haja ya kukuficha”

    Aliongea mama huku akilia sana tu mana hajui maamuzi ya mtoto wake yatakuwa ni yapi,.. Kurudi katika dini ya kiislamu, au kubaki kua Mkristo

    “mama…. Samahani sana…. Ila Kuanzia leo hii mimi sitaki ku….





    Adam hakuwa mtu wa mzaha mzaha hata kidogo, kwasababu ukweli wote kesha ufahamu, hivyo hakukuwa na cha ziada zaidi ya kuamua upande upi unamhusu zaidi, Jessica alikuwa na wasiwasi juu ya adam kuwa anaweza kubadirika kurudi katika dini yake ya mwanzo, mama mwenyewe hofu mana anampenda sana mtoto wake hivyo hawezi kupingana na maamuzi yake binafsi, na hakuwa na budi kulijua hilo…



    “mama…. Samahani sana…. Ila Kuanzia leo hii mimi sitaki kusikia jina la Sharbiny Rashidi kingazi,… Mimi naitwa adam Jacob Steven, na aimjui baba anaeitwa rashidi… Tena hata msingeniambia hili jambo lenu, nabaki huku ninako kujua,…. Baba ninaemjua ni mr jacob tu”



    Mama na Jessica kuskia hivyo kila mmoja alipumua kwa nguvu huku wakimshukuru mungu kwa maamuzi yake, mana mama hampendi tena mumewe wa zamani na hataki hata mtoto aende huko,…

    “naona sasa umekuwa mwanangu… Nashukuru kwa maamuzi yako juu ya kuchagua upande sahihi ambao wewe unaujua…”

    Aliongea mama huku akiwa na furaha ya hali ya juu, mana adam kaendelea kubaki Ukristo na haujui Uislamu mana hajakulia huko,…

    “mama, huyo mzee ni pepo, wala sitaki hata kumuona katika macho yangu,… Yaani kidoti tu ndio anikatae mimi sio mtoto wake… Leo nimtake wa kazi gani katika maisha yangu”

    Aliongea adam tena kwa msisitizo mkubwa ili kudhihirisha kuwa hahitaji kujua kama ana baba tofauti na mr Jacob, japo ni kweli baba yake ni muislamu lakini hataki kulitambua hilo,

    “Usijali baba, ni hilo tu ndilo nililokuitia hapa, hakuna kingine”

    “sawa mama,… Ila naomba mujiandae, kesho naoa…. Staki tena kuchelewa, taarifuni watu kuanzia sasa hivi hapa, na eva ndio yule, maandalizi yafanyike”

    Aliongea adam lakini wakati huo bado hajajua kuwa baba yake kapata balaa huko mjini…



    Wakati huo huo simu ya adam iliita kuangalia ni mfanyakazi wa adam, alipokea

    “tumsifu Yesu Kristo boss”

    “milele amina,… Habari ya kazi mama”

    “sio salama sana”

    “kwanini unaongea hivyo sesi?”

    “Boss… Wale watu wa mapato wamekuja tena, ila bili ya mapato imekuwa kubwa zaidi, mana inaonyesha kanisa, na nyumba pamoja na kampuni sasa sijui inakuwaje hapo”

    “Jackson hayupo”

    “yupo, lakini kashindwa cha kufanya mana ni pesa nyingi sana”

    “ok nakuja hapo”

    Adam alikata simu kisha akawasha gari yake na kuondoka,…



    Sasa huku kwa mr Jacob, alishapelekwa kituoni, lakini mr Yohana hakumwacha rafiki yake, alifika nae na kufuata utaratibu wa kumshikia mtuhumiwa zamana,.. Kwa bahati nzuri zamana yake ikakubalika, hivyo walikuwa katika hoteli moja hivi, yaani hapo mr jacob hana hata mia… Yupo kama alivyo hajui afanye nini kwa wakati huo,..

    “sasa mr Jacob, utafanya nini.. Mana sasa tayari upo uraiani sasa.. Tunafanyaje.. Mana bado kesi ipo pale pale”

    Aliongea bwana Yohana huku mr Jacob kichwa kikimuuma kwa kuambiwa kuwa akaunti yake haipo, yaani hakujawahi kuwa na akaunti kama hio katika benki hio,..

    “bwana yohana, we ulizani mimi nitafanya nini?, mana nategemea kulipa na pesa iliopo benki, sasa benki hakuna kitu, we ulizani nitafanyeje”

    “mi naona uuze ile nyumba yako”

    Aliongea bwana yohana huku mr Jacob akicheka

    “haheheheheh… Sasa Unauza nyumba na wakati na nyumba yenyewe imo… Tena wakaniambia kuna hii nyumba mpya, na kanisa jipya.. Ambayo ni kanisa la adam na nyumba yake, pamoja na kampuni… Nikawaambia hizo mimi sihusiki nazo, kwasababu tayari nilisha kabidhi kwa mtoto wangu, nyumba ile alijenga mwenyewe, kanisa kajenga mwenyewe… Kwahio hivyo haya majengo matatu mfuateni mwenyewe”

    Aliongea mr Jacob huku bwana yohana akicheka tu,.

    “kwahio sasa kwa upande wakp tunafanya nini ili tuziokoe mali zako”

    Aliongea mr yohana, lakini mr Jacob alikumbuka sauti ya jehova kuwa, endapo atashindwa kutekeleza matakwa yao.. Basi mali zote zitapotea na utabaki kama zamani,.. Hata pesa alizokuwa nazo benki hatozikuta tena mana hazikuwa pesa halali, ni pesa za miujiza

    “ahahahahahahahah… Aaaahhhh bwana yohana, wala usihangaike… Mana hapa naiona jela mbele yangu, kwasababu jehova alisha niambia kuwa nikishindwa kufuata matakwa yao kwa kumkabidhi mtu, basi hata nifanye nini hazitorudi”

    “skia, sio kuwa hazitorudi… Hapa hatuangalii kurudi kwa mali.. Bali tunaangalia uwepo wako katika uongozi…”

    “hebu ngoja, niwapigie simu… Niwaombe kitu”

    Mr Jacob alichukua na namba zao kabisa na kuwapigia…



    “hallo habari yako ndugu”

    “salama kabisa mr Jacob, vip… Una mwelekeo wowote juu ya malipo unayo daiwa”

    Aliongea huyo afisa wa mapato TRA,

    “hapana.. Ila ni hivi… Mnaonaje mkauza makanisa yangu yote mnibakishie moja, kampuni zangu pia mnibakishie moja.. Ili hizo zingine zilipe deni mnalonidai”

    Aliongea mr jacob tena kwa huruma ya hali ya juu, yaani kama upo karibu ni lazima huruma ikujie…

    “hapana ndugu… Sisi tunabinafsisha mali zako zoote, halafu tutaangalia umebakiza kiasi gani… Mana hata tukichukua mali zako zote, bado haziwezi kulipa gharama ya bilioni mia mbili point nne”

    “aaahhh ndugu,.. Nina kampuni saba… Nina makanisa 50,… Vyote hivyo mchukue na bado mnidai”

    “mpaka nyumba unayo ishi… Sio kampuni na makanisa tu, ni mpaka nyumba zako zote unayoishi na ulizo zipangisha… Tukishauza hivyo vyote, sasa hapo ndio unapigiwa mahesabu kimebaki kiasi gani cha pesa… Na hicho kama huna ndicho kitakacho kufunga”

    “mmmmmhhhh sawa bwana… Hembu fanyeni vile mnavyo ona”

    Aliongea mr Jacob huku akikosa nguvu kabisa

    “sawa,.. Sasa tupo kwa mtoto wako hapa… “

    “mmmhh sawa mheshimiwa”

    Mr Jacob amekuwa mtu wa kawaida Huezi mzania kuwa ni yeye… Yaani hapo alichobakiwa nacho ni hilo gari hapo na lenyewe lipo kwenye mpango wa kuuzwa na sio hilo tu bali ni magari yakw yote, yaani mashetani aliokuwa anayatumia yanaondoka na vitu vyake vyote, mpaka sifa alizokuwa akizipata nazo zinaondoka….

    “bwana hali ni tete… Kile kijumba chako ulichohama ai bado kipo”

    “ipi hio, ile ya kule mjini kati”

    “ndio, Hio hio”

    “mbona nilishauza tayari”

    Aliongea bwana yohana kuwa nyumba hio alishauza tayari,.. Huku mr jacob akimuona mwenzie mjinga kwa kuuza nyumba…

    “unauzaje nyumba za watoto sasa”

    “heeeeee si nimeamua”

    “aaahhhh sijui nitaishi wapi jacob mimi…. Hapa dawa ni kukimbia tu”

    “Kiukweli mr jacob mimi sina msaada na wewe, kwasababu mimi utajiri wangu ni mdogo kuliko wewe.. Pesa unayodaiwa, mimi sijawahi hata kuiingiza kwa miaka yote hio… Mimi na utajiri wangu wote, kwenye akaunti nina bilioni moja point saba… Wewe unadaiwa bilioni mia mbili… Haaaa”

    Aliongea me yohana huku mr Jacob akimlaumu kuwa

    “lakini kosa ni lako… Mr jehova alituambia tuuwe watu watatu, wewe umeua mmoja, ndio mana utajiri wako ni hafifu.. Sasa hivi ungenisaidia matatizo”

    “sasa mbona unanilazimisha kuua”

    “aahhh we pumbavu sana… Nilikuwa nakwambia ua muumini mwingine hutaki..”

    “wewe usiniite pumbavu wewe, kumbuka nimekushikia zamana ujue”

    “haijalishi”

    Walianza kugombana kwa kutupiana maneno ya hapa na pale,… Mr yohana alikasirika na kuondoka zake,.. Mr jacob nae kawasha gari yake na kuondoka, yaani hapo hata hilo gari likiisha mafuta Mara paaaaaap limeisha.. Hapo hana hata mia.. Chakula yenyewe kalipiwa na mr yohana, afu tayari keshamvuruga, na angelimsaidia siku mbili hizi kabla nae hajakutwa na dhahama…



    Huku kwa adam, maskini alikuwa akishika kichwa kwa gharama alioikuta katika listi ya mapato anayotakiwa kuyalipa,… KAMPUNI, KANISA NA NYUMBA… ila nyumba na kanisa kinachodaiwa ni biwanja tu, mana kampuni yale ni majengo ya serikali,… Sasa adam yeye kwenye kampuni anatakiwa kulipia mapato, japo alikuwa analiapa lakini kulikua na mkono wa shetani ndani yake, sasa hakuna tena mkono wa shetani.

    “lakini sawa, bilioni 19 sio kitu… Twendeni benki”

    Adam anadaiwa bilioni 19 vitu vyote anavyomiliki mpaka gari yake, yaani kila kitu ni gharama ya vitu vyote, ni bilioni 19, mana ana kanisa moja, kampuni moja… Nyumba moja.. Sasa baba yake, ana makanisa 50, kampuni saba… Nyumba tano, alafu makanisa yote hakuna hata kanisa moja liliolipiwa uwanja.. Yaani viwanja vyoye alipewa na serikali, kwa nguvu za shetani, sasa hio haipo kwa kisheria mtu mmoja kupewa viwanja vyote hivyo tena vikubwa afu mijini mijini tu….



    Adam kufika Bank,  ni vile vile vya baba yake, akaunti hazionekani hata moja,…

    “haaaaaaa… Nyie wahudumu… Pesa zangu zimekwenda wapi… Acheni utani nyie”

    Aliongea adam huku, akitamani hata kulia…

    “Samahani kijana,… Baba yako ilikuwa hivi hivi… Sasa naona hii ni janja yenu wewe na baba yako…. Afande??… Piga pingu huyu ataeleza kila kitu”

    “sasa jamani, muogopeni yesu jamani, kumbukeni yesu alisema atarudi kiutofaut sio kama zamani”

    Aliongea adam lakini haikusaidia kitu

    Lakini sasa, kuna afande aliona kitu kwa adam

    “halafu huyu kijana anatuchezea akili… Hapa mkononi ana ATM kadi tatu… na hapa kajaribu mbili… Hii moja mbona hakujaribu”

    Adam alikasirika kuskia wanataka kujua na hio akaunti nyingine…

    “mkanifunge tu, lakini akaunti ya kanisa, ni hazina ya watoto yatima…ambayo ni sadaka za waumini wangu, Sipo tayari kuitumia… Twendeni tu”









    Kweli Adam alikuwa ana akaunti tatu za bank… Akaunti yake binafsi, akaunti ya kampuni… Na akaunti ya kanisa… Sasa akaunti ya kampuni kuangalia hakuna akaunti kama hio,… Aligombeza watu lakini wale maofisa wakamwambia kuwa

    “wewe na baba yako mnatuchezea akili nyie, baba yako pia kachanganyikiwa hapa baada ya kuona akaunti hazina kitu”

    “lakini mimi hii akaunti ya kampuni ilikuwa ina bilioni 25…na hii akaunti yangu binafsi, ilikuwa na bilioni tatu tuu… Sasa nashangaa akaunti zote zinasema hakuna”

    Adam aliongea huku akiwa haamini

    “hapo mkononi una kadi ngapi.. Mbona una kadi tatu, angalia na hio mlipe kodi”

    Aliongea afisa huyo huku adam akikataa ile akaunti nyingine isitumike

    “hapana, hii ni akaunti ya kanisa… Ni sadaka za waumini hizi staki kuzitumia… Hizi ni kwa dharura tu”

    “sasa hii si ndio dharura”

    Mara simu ya adam ikaita.. Kuangalia ni baba yake

    “halo baba… Shalom”

    “shalom… Upo wapi”

    “nipo bank baba… Nashamgaa akaunti zangu hazipo.. Hizi benki zina wizi ndani yake”

    “hapana baba… Nisamehe bure mwanangu,.. Nilikuwa natumia mashetani kupata pesa, hivyo hata pesa zako pia ni za mashetani baba.. Nisamehe bure”

    “kwahio wewe je”

    “mimi nilikuwa na trillion moja… Nimekuta akaunti haipo kabisa”

    “sasa tunafanyaje”

    “najua huezi kosa… Fanya kitu mwanangu,.. Mpaka sasa sina hata kitu, yaani hata nyumba tunayoshi itabinafsishwa ili malipo yawatu yalipwe”

    “daaaahhhhhh, baba sasa nitafanya nini”

    “huna akaunti ya kanisa”

    Baba aliongea hivyo kwasababu anajua sadaka iliokuwa ikitoka kwenye kanisa la adam ni sadaka ya halali, tofauti na zile sadaka alizokuwa akichangisha yeye, zile zimetolewa na waumini sawa… Lakini ni msukumo wa kishetani, unakuta muumini ana nia ya kutoa elfu moja, lakini anajikuta anatoa hata elfu hamsini mpaka lakini… Yaani kasukumwa kilazima atoe ile pesa…… Lakini kwenye kanisa la adam hakuwa na mashetani, adam alikuwa mchungaji halali sema akili yake ilivurugwa na wanawake….

    “hebu ngoja nichomeke kadi nione kama ina kitu, lakini baba hii ni sadaka kwa ajili ya kusaidia watu mbalimbali wenye shida baba”

    “basi acha, tuanze upya kuzunguka na maredio kama zamani”

    Aliongea mr Jacob huku adam akikubali bila shaka

    “baba, mimi nipo tayari kuwa na kanisa hata kama nimezungushia majani ya mgomba,… Kuliko nitumie pesa ya sadaka za waumini siwezi”

    Adam aliongea kisha akakata simu, japo pesa yenyewe haijulikani kama ipo au haipo,…

    “sikiliza wewe… Kama wewe na baba yako hamuezi kulipa.. Tunabinafsisha mali zenu zote, na kama bado hazijafikia kiwango knachotakiwa kulipwa, basi kufungwa kutawahusu… Kwanza mpaka sasa upo chini ya ulinzi”

    “Yesu wangu na maria… Kumbe kuna kufungwa tena”

    “afande, tia pingu… Baba yako kashikiwa zamana, sasa wacha huyu akakae sero”

    Aliongea kama mmoja huku adam akifungwa pingu,… Yaani adam hakuogapa kabisa, lakini hataki kugusa hazina ya kanisa…. Lakini sasa alipopakiwa kwenye gari, akaikumbuka familia yake,.. Kwa sasa baba yake ndio huyo,.. Atataifishiwa mali zake zote, mana hatokuwa na kitu, akifikiria yeye ni mtumishi wa mungu, na yupo kwa ajili ya kulifikisha neno la mungu kwa wanadamu….

    “sawa… Hebu tuangalieni kama kuna chochote”

    Aliongea adam huku askari wakimfungua pingu na adam akarudi bank tena… Alichomeka ATM kadi, kwanza hio ilionekana kuwa inafanya kazi, sasa  akaangalia salio…. Kakuta kuna bilioni 20 tu…. Adam alijaza kanisa lake takribani miezi mitatu, kila siku watu mia nne, na kila mmoja anatoa sadaka…adam aliiona ile pesa lakini hakuwa na shauku ya kuitoa… Na deni lake analodaiwa ni bilioni 19….kabla hajatoa kwanza akawapigia simu wazee wa kanisa lake, aliwauliza kuhusu kutumia pesa ya kanisa… Alijibiwa vizuri tu kuwa

    “ni halali yako kitumia pale unapokuwa umebanwa kweli…. Yaani unaona kabisa hapa hakuna jinsi, basi unaruhusiwa kitumia… Mana unaambiwa kama una elfu kumi, Huruhusiwi kumsaidia mtu ingali familia yako italala njaa… Hakikisha familia yako hailii njaa ndipo umsaidie na mwingine”

    Kidogo adam akapata mwangaza… Na kuitoa ile pesa ambayo ni ya halali.. Hivyo mpaka hapo adam kafanikiwa kulipia mali zake zote, na yote hio ni kwasababu ya kumuamini mungu, laa zivyo wangeazilika mwaka huu…



    Baba aliposikia adam kalipa mali zake zote alijiskia furaha sana.. Na kujua kuwa mungu ndio kila kitu katika hii dunia, kwani njia aliotakiwa kupita adam sio sahihi… Ona adam kamtegemea mungu leo kaokoa moja ya mali na kanisa lake liliotakiwa kubinafsishwa na serikali



    “jamani mambo ni shwari, sasa pigeni kazi, acheni mchezo… Sawa”

    Adam alikwenda ofisini na kutoa amri kuwa wapige kazi kwasababu hali imekuwa tete, na adam hataki kitegemea kanisa japo ni halali yake litumia lakini yeye anataka sadaka za waumini zikawaseidie watoto yatima na wengine wenye kuhitaji misaada..

    “sawa bosa, ahsate kwa kututoa hofu”

    Waliongea wafanyakazi hao mana wameshasikia makampuni ya baba yake yameshafungwa….

    “Abdallah vp bwana”

    “safi boss…. Boss pole sana kwa matatizo”

    “wala sio matatizo, ni mitihani ya mungu tu”

    “Tunashukuru kwa kufanikiwa boss”

    “sawa kabisa.. Fanyeni kazi kwa amani”

    Adam alimwangalia sana Abdallah, mana ni ndugu yake kabisa…



    Sasa huku mjini mama na Jessica walikwenda benki nao kutoa pesa ili wafanye maandalizi, wanakuta akaunti hazisomi, yaani wote waliokuwa wanatumia pesa za mr jacob, yaani zinachukuliwa zoote,.. Walimpigia adam na adam aliwapa ukweli, kisha akawapa pesa.. Sasa pesa inayotumika kuanzia sasa, ni pesa kutoka kwenye akaunti ya kanisa la adam.. EDEN CHURCH,



    Kesho yake ikiwa imejaa shamra shamra za hapa na pale, pamoja na matatizo yao lakini lengo la adam kuoa lipo pale pale, mana pesa kidogo wanayo hivyo maisha yataendelea kama kawaida,… Adam alipigilia suti kali, huyo eva sasa ndio usiseme, katupia shela lake saaaafi, matron wake kapendeza, best man wa adam nae ndio usiseme… Anaefungisha ndoa ni Tb Joshua mwenyewe mana alisema…. Wakati huo bwana harusi na bibi harusi wanatolewa kwenda kuvishana pete



    “hivi wewe umekaa huku unajikwatua tu, hivi unajua kinachoendelea kwenye huu mji”

    Alikuwa ni rafiki yake Catherine, akimpa taarifa fulani

    “kuna nini”

    “adam anaoa leo”

    “unasemaje… Yaani adam anaoa leo”

    “ndio, mi nakushangaa na uzuri wako umeshindwa kuolewa nae.. Duuu”

    “halafu, ivi unajua adam kantoa bikra”

    Sasa marafiki ndio wanajua leo

    “haaaaaaa… Unasemaje Catherine”

    “ndio Herieth, kantoa bikra yeye”

    “sasa kama kakutoa bikra, hapa unasubiri nini…. Nenda kaolewe wewe, kisheria lazima uolewe wewe, sasa unazubaa nini..”

    “mmmmhhh we muongo jamani”

    “nakuambia kweli…. Pale mchungaji akisema nani mwenye pingamizi na ndoa hii, unatoka wewe.. Unasema ukweli kuwa ulitolewa bikra na adam,.. Lazima ugeukiwe wewe na ufunge ndoa”

    Catherine kichaa kimempanda, saa ngapi kweli hajawasha gari, na ni kweli ile anafika tu ilikuwa katika hali ile ile alioisema rafiki yake…. Catherine alishika breki kubwaaa, mpaka tairi za gari zikapiga kelele…. Watu wakageuka…

    Adam haamini kama Catherine kafika eneo hili,…. Walioyajua mahusiano ya Catherine na adam, walianza kupiga kelele….. Catherine alisogea mpaka pale karibu ya jukwaa, na kukaa kwenye kiti, anasubiri tu lile neno la nani mwenye pingamizi na ndoa hio, anyanyuke kisha aseme yake ya moyoni, na ni kweli Catherine akisema katolewa bikra na adam,.. Basi eva hana chake tena….









    Walio yajua mahusiano ya Catherine na adam walichekelea kisiri siri kana kwamba kuanzia hapo eva hana chake japo hawajui nini kitasababisha eva amkose adam,… Catherine alikaa hapo kwa hamu zote ili kuvuruga mapenzi ya adam na eva,… Basi mambo yaliendelea na mchungaji aliendelea kuwauliza wawili hao kuhusu kupendana kwao,.. Pete zililetwa kisha mchungaji akauliza swali kwa waliohuzuria hafla hiyo, haruawilikuwa ya kushtukiza lakini ilijaza watu wengi mno, Karibia kanisa lote la adam lilijaa, na sio harusi ilioandaliwa kwa muda mrefu,.. Ni jana tu na leo ndoa, lakini watu ni wengi mno,…

    “kabla wawili hawa hawajaanza kuvishana pete kama pingu za maisha yao…. Yupo mwenye pingamizi na jambo hili”

    Catherine alikuwa ni wa kwanza kunyanyuka, sasa kumbe walikuwa ni wengi waliotaka kunyanyuka, wale wote waliotembea na adam kumbe nia yao ni kumvurugia eva, ili waendelee kula starehe na adam, bila kujua mwenzao kwa sasa sio yule tena,… Sasa wale wa nyuma kuona Catherine kanyanyuka, wakabidi watulize mzuka wa kunyanyuka…. Watu walishangaa, adam na eva alitahamaki kumuona mtu mwenye pingamizi la ufungwaji wa ndoa hio,…

    “amepatikana mmoja mwenye pingamizi la ndoa hii, kuna mwingine?”

    Eva alinyong’onyea kabisa, mana anamjua pia alikuwapo katika moja ya wasichana waliotaka kuolewa na adam Jacob Steven,..

    “nadhani hakuna mwingine…. Haya mama tunaomba utuambie, kwanini unaipinga ndoa ya wawili hawa”

    Mchungaji aliongea hayo huku akimpa maiki Catherine aongee duku duku lake…. Eva wakati huo anatetemeka mno, mana ni kama anapokonywa tonge mdomoni

    “kiukweli naomba niongee ya moyoni ambayo hamkuyajua toka mwanzo…”

    Adam hana raha tena, na kumfokea mbele za watu haiwezekani, na Huruhusiwi kumkatisha maongezi yake…

    “adam alikuwa awe mume wangu mimi,… Lakini ilikuwa ni shinikizo kutoka kwa wazazi wetu…. Mimi binafsi niliamua kuachana na swala hili kwasababu adam hakuwa akinipenda…. Lakini wakati tunaagana, tuliambia kila mmoja ampe mualiko mwenzie katika harusi yake, na kwa bahati nzuri yeye ndie kaanza…. Nilishangaa sana kukosa mwaliko ingali tulipeana ahadi… Pingamizi langu mimi ni kwamba… Kwanini hakunipa mwaliko… Ila nawapongeza kwa hatua walioifikia”



    Watu hawajaamini kwa maneno ya Catherine, lakini marafiki wa Catherine walishangaa sana, kuona mbona Catherine kubadilisha mada,.. Basi mtoto wa kike alipongezwa sana mana kawa sapraizi ya nguvu katika ndoa hio,…



    Masaa machache baadae Catherine akiwa na rafiki zake katika gari wakiwa wanarudi harusini

    “ivi Catherine una akili wewe… Ni maneno gani umeongea wewe”

    Aliongea Herieth huku akiwa anamgombeza rafiki yake…

    “eh eh, Sikiliza heri, mimi sio mjinga… Hakuna maisha mazuri ya ndoa kama mkipendana wote,.. Kweli nampenda adam, lakini yeye hanipendi… Sasa nifanyeje… Atakwenda kunitesa bure… Na istoshe sasa hivi tayari nimesharudisha mahusiano na mpenzi wangu John, na karibu tutaoana… Leo nitangaze sina bikra we ulizani nitaolewa kweli”

    “kwahio sasa unataka kumuuzia John mbuzi kwenye gunia sio”

    “sio kuwa namuuzia mbuzi kwenye gunia… Bali nami nimeshamwambia na analijua hilo… Kitu nilichokataa ni kila mtu kujua kuwa adam ndio kanitoa bikra… Sikiliza Herieth, Mpende mtu akupendae, kama hajakupenda utakwenda kuteseka mpaka ujute”



    Adam na eva, ndani ya fungate katika hoteli kubwa, na hapo pesa inayotumika ni ile ya kanisani, ila ya kampuni sjui ya nini… Hio ilishatoweka na kurudi na mashetani yao…



    Wiki nzima ya fungate ya adam na eva,… Wanarudi nyumbani, kitu cha kwanza kaikita familia yake imejaa kwenye nyumba yake… Hajakaa vizuri mara baba huyo..

    “mchungaji adam, shalom baba”

    “shalom baba… Hali ya hapa”

    “salama, vipi mama mkwe hajambo”

    Aliongea baba huku eva akimsalimia baba mkwe kwa furaha ya hali ya juu

    “shikamoo baba…”

    “marahaba mama hali yenu”

    “salama tu”

    Basi eva aliingia ndani mana sasa kwake ndio hapo hana pa kwenda, chumba chao kilisha andaliwa, japo familia imehamia hapo…



    “mwanangu… Kwanza nina furaha sana kupata dume lenye maamuzi ya kipekee… Kama sio kufuata akili yako wewe mwenyewe, sidhani kwa sasa ningeiweka wapi sura yangu.. Nashukuru sana kwakuwa ulimtegemea mungu na sasa anafanya miujiza yake… Ahsante sana baba”

    Aliongea mr Jacob yaani sasa hivi huezi amini hata gari tena hana….

    “Usijali baba… Nadhani kila kitu kitakwenda sawa…”



    “sawa…serikali imechukuwa mali zangu zote, yaani kila kitu… Na Nashukuru ya kwamba ni kiasi kidogo sana kimebakia ili kuweza kumaliza deni… Nadaiwa bilioni tisa, kutoka bilioni mia mbili na pointi nne, sasa nadaiwa bilioni tisa…. Hata baiskeli sina mwanangu… Inauma sana”

    Aliongea mr Jacob huku akilia mbele ya mtoto wake

    “pole sana baba… Ila hutakiwi kujuta baba… Unatakiwa kumshukuru bwana mwokozi kwa kukuokoa na madhambi uliokuwa nayo… Kwa sasa nakuona mwepesi japo sijakupima… Mtumainie bwana Yesu atakubariki mali zingine… Ila usijaribu tena kuingia kwenye dhambi baba yangu”

    “siwezi tena mwanangu… Siwezi na Najuta kwanini nilijiunga na hiki kikosi”

    “najua zilikuwa ni tamaa tu baba yangu… Pole sana”

    “sawa…. Kwa sasa tumeshahamia hapa kwako,… Mana hatuna nyumba hata moja tulio achiwa”

    “hilo sio swala la kuniambia… Hapa ni nyumbani kwako mzee”

    Adam alimfariji baba yake kisha akaingia ndani na kusalimia,



    “mchungaji kaelekea wapi”

    Adam aliuliza, mana bado hawaja anza iziala yake rasmi ambayo atazunguka na adam mwanzo mwisho,..

    “heeeeee…. Baba… Sasa hivi kanisa letu, lina watu mpaka hawaenei”

    Aliongea mama yake adam huku adam akishangaa kuwa kanisa lina waumini mpaka hawaenei, misa zimekuwa nyingi mno….

    “wacha mama…. Ila kwa sasa hata nikute waumini watano, nitasonga nao mwanzo mwisho mama yangu”

    “sawa baba… Mchungaji joshua ndio analiongoza kanisa kwa sasa… Na keshakusafisha kwa yale ulio yafanya miezi ya nyuma… Sasa unasubiriwa kwa hamu”

    Aliongea mama huku akimsifu mtoto wake,…

    Adam kwa furaha aliwasha gari na kuelekea kanisani kwake,…. Kabla hajaingia kanisani aliona wacha aingie toilet kupata haja ndogo… Lakini alipokuwa akikaribia kuingia chooni… Aliskia sauti za watu zikiongea nyuma ya choo…



    “unamuona huyu pasta adam huyu…”

    “ndio..si huyu aliokwenda fungate toka juzi”

    “ndio.. Ila kesharudi…. Sasa, wewe unaweza kuamini kuwa pasta adam ni muislamu”

    Aliongea bwana mmoja akiwaambia wenzie, sasa adam ndio anashangaa, ina maana hii ishu imeshajulikana kwa kila mtu….

    “sio naweza kuamini… Kila mtu anajua karibia kanisa lote hili…”

    “lakini ana upako, utafikiri sio muislamu vile”

    “wewe… Mtumishi adam alikuwa muislamu, lakini kwa saaa sio muislamu tena… Jieshim wewe”



    Adam alitoka hapo chooni kisha akampigia simu mama yake,..

    “mama, mbona hili swala limevuja kiasi hiki”

    “swala gani tena baba”

    “mimi kuwa nilizaliwa kwenye koo za Kiislamu”

    “mimi hata sijui nani kusambaza huo ujinga, na nimemuuliza Jessica, kasema hajawahi kusema kwa mtu”

    “hapana mama, sio kuwa ni ujinga… Mimi nilitaka niwasapraizi waumini wangu kuhusu hili”

    “hapana adam usiliweke wazi”

    “Hapana mama, siwezi kuwa mtumishi wa Mungu ingali nami nina yangu yananisibu… Haifai kwakweli lazima wajue, na sema tu nilikuwa sijui toka mwanzo, lakini wangeshalijua mama”

    “mmmmmhhh sawa baba…. Kama umeshagundua hilo basi ni vyema”

    “sawa.. Ahsante mama”



    Adam alikata simu sasa kaingia kanisani, akiwa mpya, akiwa mume wa mtu,… Sasa ni mchungaji aliokamilika…. Na ilikuwa ni siku ya Jumapili iliojawa na furaha katika nyuso za waumini…

    “asifiwe bwana yesu Kristo”

    Aliongea adam huku akipunga mkono,.. Hakukuwa na pepo katika kanisa hilo, ilikuwa ni furaha kwa kila mmoja,…..

    “milele aminaaaaaaaaaaaa”

    Waliitikia waumini kwa furaha ya hali ya juu, akikumbuka mara ya mwisho kabla ya ndoa, alikuta waumini nane, tena familia yake na akina eva…

    Hapo ndipo kichaa kilipo panda… Sasa leo haamini kanisa limejaaa, mpaka baadhi ya wafanyakazi wake kwenye kampuni nao wamo…. Adam alifarijika sana, watu zaidi ya 500 wapo ndani ya kanisa lake… Inapendeza sana,..

    “leo….. sitaki muumini atoe ushuhuda katika kanisa hili”

    Waumini walishangaa sana, lakini mtumishi joshua alitabasam, kwani anajua kinacho endelea….

    “leo….. Nataka nitoe ushuhuda wangu mimi”

    Waumini wakapiga kelele za furaha, mana wamezoe kusikia ushuhuda wa watu wengine, sasa leo ni mchungaji mwenyewe….



    Alianza kuongea vile vile alivyo hadithiwa na mama yake,… Watu walianza kulia katikati ya ushuhuda wa mchungaji adam,.. Lakini alipofikia kulitaja jina lake la kuzaliwa akiwa muislamu,.. Baadhi ya wafanyakazi wake waliokuja ibadani, walishtuka kuskia jina la baba yake.. Basi ushuhuda uliendelea mpaka ukaisha…. Kisha adam akauliza



    “je? Hebu niambie nastahili kubaki wapi… Au nirudi kule”

    “hapanaaaaaaaaaaa…. Tunakuhitajiiii”

    Waliongea waumini tena kwa furaha sana

    “hata mimi nililiona hilo na ndio mana mpaka leo nipo hapa nanyi… Bwana Yesu asifiwe sana”

    “aminaaaaa”

    “Hallelujah”

    “ameeeeeeeeeeeeeeeeeen”



    Jumatatu kule kazini, sasa wale waumini waliokuwapo katika ibada ya jana jumapili, walianza kumtania Abdallah kuwa ana undugu na mtumishi adam…. Na Abdallah nae alikuwa ni mzuri katika imani yake, hivyo haoni shida kutaniwa kuwa ana ndugu Mkristo,… Swala hilo ni la kweli lakini Abdallah alijua ni utani tu

    “hivi unajua mtumishi adam kumbe alizaliwa akiwa muislamu… Na jina la baba yake ni kama lako”

    Aliongea dada mmoja aliohudhuria katika ibada ya jana….

    “aaahh bwana niacheni nifanye kazi..”

    “skia wewe… Mtumishi adam.. Alikuwa anaitwa Sharbiny rashidi kingazi… Sasa mbona wewe unaitwa Abdallah rashidi kingazi… Nyie sio ndugu kweli”

    Abdallah kidogo swala hilo lilimkuna mpaka akalifikisha kwa baba yake…



    Baba alikuwa kibarazani anatengeneza pikipiki yake,… Abdallah kafanya kazi kidogo.. Kwani wana kakibanda chao cha rumu tatu,.. Kujitahidi kuwajengea wazazi wake na ni kupitia kazi hio hio….

    “baba?”

    “nini tena Abdallah…. Wacha nitengeneze usafi wangu… Mana kuna gari imeharibika kule babati, sasa nimeitwa kwenda kuitengeneza”

    Aliongea mzee rashidi… Mana kazi ya mzee ni ufundi wa magari

    “baba.. Nina jambo nataka kukuuliza”

    “utaniuliza jioni”

    “lakini baba, huenda usirudi na mimi linaniumiza sana”

    “kwani ni jambo gani Hilo”

    Baba aliongea hivyo lakini hakuwa tayari kumsikiliza, si unajua wazee wa zamani hawa…

    “baba, mimi nina ndugu yangu”

    “we mtoto mjinga nini… Kwani asha sio ndugu yako”

    “hapana.. Sina maana ya huyu asha mdogo wangu,… Namaanisha, una mtoto anaitwa Sharbiny”

    Eeeeeeee, baba kuskia hilo jina aliacha hata kukaza nati kwenye pikipiki,

    “Unasemaje wewe”

    “boss wetu”

    “boss wenu ndio kafanya nini”

    “boss wetu kumbe ni alizaliwa kwenye koo za Kiislamu”

    “si uliniambia boss wenu ni Mkristo”

    “ndio… Ila alikuwa anaitwa Sharbiny Rashidi kingazi,… Sasa nimeshtuka sana kuskia hili jina”

    Mzee kuskia hili jina kamili, alijua ni mtoto wake, na mama yake anaitwa mwajabu….

    “hebu twende nikamuone”

    “kwa saaa huezi mpata… Yupo bize sana, we niambie ni mtoto wako”

    “ndio… Ni mwanangu huyoo”

    Abdallah alikuwa na furaha lakini pia alikuwa na maswali ya kumuuliza baba yake

    “sasa baba, kwanini ulimtenga mtoto wako”

    “wewe bwana huezi niuliza maswali mengi kiasi hicho… Wewe hujui kitu bwana”

    Baba aligomba kuulizwa maswali na mtoto wake, hapo ndipo Abdallah akagundua kuwa makosa makubwa anayo baba…

    “sawa mzee, Samahani lakini”

    “si umemuona ana kidoti hapa usoni”

    “ndio, ana kidoti hapa usoni”

    “hahahahahah ni mwanangu huyoo… Kumbe mwanangu ni bosi…. Mtoto mjinga sana huyu… Anapata hela hata kuniona baba yakw hataki… Mtoto laaana kum sana huyu”

    Aliongea baba huyo huku akitabasamu sana… Wakati huo Abdallah alishaondoka zake, lakini baba alikaa chini na kujiuliza…

    “kweli ni mtoto wangu,… Lakinj kama kaambiwa ukweli na mama yake… Basi hatoweza kunipokea hata mara moja…. Eeehh mwanangu, Nisamehe baba yako, ni tamaa za kimwili tu ndizo zilizofanya niwatenge wewe na mama yako…. Nisamehe sana… Nitakuja kukuona kesho”

    Aliongea baba yake Abdallah, huku machozi yakimtoka mfululizo….



    Kesho yake, mzee katia timu ofisini kwa mtoto wake wa kwanza, dume lake hilo, lakini keshalitenga… Ndio mana unaambiwa usitupe watoto wala usimkatae mtoto, tamaa za mwili zinapita tu…. Sasa baba kakaa hapo, kila mwanaume anaeingia anamwangalia uaoni ili aone kile kidoti, alikaa hapo mpaka saa tano za asubuhi…..



    Adam anakuja lakini ndani ya gari alikuepo mtumishi joshua,.. Anakuja kuangalia kampuni ya kijana wake, au mwanafunzi wake,… Mbali na uwanafunzi bado ni mchungaji mwenzake, sema joshua yeye ni mchungaji mkuu Afrika, kwa wale wenye imani ya mungu…. Sasa adam yeye hamjui baba yake,… Na hata huyu baba hamjui adam ispokuwa kidoti cha usoni ndicho atakacho kijua,…. Alishuka TB JOSHUA,… Mzee raahidi kuangalia, anaona ni sura ya kizee karibia alingane nae… Adam anashuka na kumuona mzee rashidi, lakini hamjui…

    “tumsifu yesu Kristo”

    Adam alimsalimia huyo mzee kwani alijua labda kuna kitu kufuata na hawezi kumuuliza, ni mpaka aletewe taarifa na Secretary…. Sasa baba kuangalia usoni,. Aliuona ule mdoti kwenye sura ya adam,… Baba haamini kumuona mtoto wake kabisa tena wa damu,…

    “Sharbiny mwanangu….”

    Adam aliskia akiitwa hilo jina tena likiambatana na neno mwanangu,.. Mr joshua analijua hilo jina mana jana aliusikia ushuhuda wa Adam… Sasa adam kageuka,

    “Nisamehe mwanangi…. Mimi ndio baba yako, naitwa Rashidi Kingazi… Nakujua kupitia hiki kidoti cha usoni”

    Adam alishangaa sana

    “samahani mzee, utakuwa umekosea… Mimi naitwa adam Jacob Steven.. Silifahamu jina la Sharbiny… Na pia sikuwahi kuwa na baba alieitwa hilo jina unalo niambia… Samahani sana mzee……”

    Adam aliongea hayo kisha akaelekea ofisini kwake, akiwa na mwalimu wake…..

    Hawajakaa vizuri mara mama yake adam huyo, katokea eneo la tukio, tena alikuwa pamoja na mr jacob ambaye ni mume wake,…

    Sasa mzee rashidi kumuona tu mkewe wa zamani,… Alikaa kimya mana mama ndio anajua ubaya, ila mtoto hajui ubaya…

    Sasa mama kutahamaki anaiona sura ya mume wake wa zamani, kama miaka 23 iliopita… Leo ndio anamuona kwa mara nyingine tena.. Mr Jacob anamfahamu kwa kile kipindi walichokwenda kuchukua talaka, ili amuoe mwanamke huyu…

    “habari zenu”

    Mama adam alisalimia kama vile hamjui

    “mama Sharbiny, yaani umenisahau”

    “kwani wewe ni nani mpaka nikukumbuke”

    Watu wanaojua dini wana maneno ya shombo acheni utani bwana, usiombe ukasutwa na mwanamke anaejua dini… Mana anakusuta kwa maneno ya busara na kukuchanganyia na ya mtaani

    “mama Sharbiny… “

    “weeeeee… Mimi ni mama adam, huyo Sharbiny mimi simjui… Sawa baba…….. Jackson”

    “yes boss”

    “msikilize huyu bwana ana shida gani, mumpatie shida yake na aondoke”

    “sawa boss”

    Mzee haamini mwanamke aliomtenga kisa mke wa pili leo anaitwa boss…. Na yeye bado ni choka mbaya vile vile… “

    “sawa, najua umesha mpandikiza mtoto chuki,… Lakini jua kuwa mimi ndio baba yake”

    Aliongea mzee rashidi kisha akawa anaondoka,… Mara adam na mwalimu wake huyo anakuja….

    “Unakwenda wapi nawewe?”

    Aliongea mama kama vile anamzuia adam….











    Kabla hatuja anza mahala tulipoishia kwanza tuanzie ndani walipo akina adam na mtumishi wake, au mwalimu wake…..



    “ni kweli kijana huyu ni baba yako”

    Aliuliza bwana joshua, na hapo wapo ofisini kwa adam

    “kwa muonekano ni kweli ni baba yangu,… Mana hata mama kanitumia meseji sasa hivi hapa,… Kaniambia huyu hapa ndio yule baba yako niliokwambia”

    Aliongea adam, kwahio kumbe wakati wanarumbana kule,… Mama alimtumia adam meseji kuwa huyo ndio yule baba yake aliemhadithia wiki mbili zilizopita…

    “sawa…. Kwa imani yangu mimi mpaka kufikia hapa, najua uchungu wa mtoto najua mzazi anajiskia vipi kwa hali kama hii… Binadamu hatujaumbwa kukamilika… Hivyo fanya kama vile baba yako alikosea..”

    Aliongea bwana joshua kama vile anamtaka adam amsamehe mr rashidi…

    “kwahio unanitaka nirudi kwenye imani ya Kiislamu”

    “hapana, sina maana hio… Kumsamehe sio kuwa lazima uwe huko… Bali umsamehe na umsikilize hitaji la moyo wake… Ikumbukwe kuwa hata kama aliwatenga wewe na mama yako… Lakini amekili kuwa ni kweli, msamehe… Binadamu tunakosea”

    “hapana mchungaji…. Hapana… Siwezi, roho inaniuma mama yangu alivyoteseka… Roho inaniuma… Simjui mimi huyu mzee simjui”

    Adam alikuwa akilia kabisa na kuapa kuwa hataki kumjua mzee huyo….

    “mimi ni mwali wako… Mimi ni kiongozi wako…. Mimi ni sawa na baba yako… Huyo ni baba yako, anapo sononeka kuhusu wewe, basi hakuna jambo zuri litakalo kunyookea…. Sasa mimi nasema hivi, kama wewe hujawahi kumkosea mungu, basi usimsamehe bwana huyu… Lakini kama ulishawahi kumkosea mungu, basi msamehe baba yako”

    Aliongea mr joshua kisha akanyanyuka

    “sasa Unakwenda wapi mtumishi”

    “nahitaji kuanza iziala yangu kuanzia sasa”

    “lakini ulisema tutakuwa sote kwanini unaniacha”

    “msamehe baba kwanza… Kisha tutakuwa wote… Utapata laana bure, msamehe tu.. Nakuomba mimi kama kiongozi wako,.. Msamehe baba”

    Adam alilia sana tena sana… Mpaka khanjifu yake ikaloa machozi matupu, lakini mwisho wa saa alikuja kukubali Kumsamehe baba yake….



    Adam alitoka pamoja na mtumishi joshua,.. Wakati huo anatoka machozi tu,… Sasa mama ndio ana uchungu zaidi mana yale mateso aliteseka yeye,.. Adam kahadithiwa tu, lakini alioteseka ni mama… Sasa mama kumuona adam anakuja akajua adam keshaamua Kumsamehe baba yake… Na mama hataki adam arudi katika imani alionayo baba yake…



    “Unakwenda wapi na wewe”

    Aliongea mama kama vile anamzuia adam….

    Lakini kabla adam hajajibu,… Mr joshua alijibu badala ya adam….

    “mama toto… Punguza hasira….. Ni kweli umeteseka sana na unastahili pongezi na sio pole… Kweli huyu ni baba yake na huyu kijana… Endapo huyu kijana hatomsamehe baba yake, kuna baadhi ya mambo hayatoenda sawa kwa mwanao,… Baba ni baba… Mpe mtoto nafasi”

    Aliongea mtumishi joshua… Wakati huo mama analia, yaani hakutamani kabisa kumuona mzee rashidi,…

    “mchungaji, inauma sana… Inauma sana…”

    “maumivu yako, mwachie bwana yesu… Mpe mtoto nafasi… Mchukie wewe lakini wacha mtoto amsamehe baba yake”

    Mama kwa maneno ya mtumishi adam, alikubali adam amuendee baba yake, wakati huo mr rashidi, anamalizikia kutoka getini tena huku akiwa na huzuni ya kufukuzwa kwenye kampuni ya mtoto wake,.. Na wakati huo Abdallah ndie aliekuwa akitoka nae nje….

    “baba?”

    Adam aliita…. Mzee rashidi kuskia neno baba, aligeuka haraka haraka,..

    “ndio mwangu….”

    Baba kumbe hakukata tamaa, alirudi mpaka kwa mtoto wake na kutaka kupiga magoti lakini adam kamzuia asifanye hivyo….

    “kweli wewe ni mwanangu…. Hiki kidoti ndicho nilichomfanyia visa mama yako mpaka kumtenga… Ni tamaa za mwili mtoto wangu… Nisamehe baba yako… Najua kweli mliteseka sana… Lakini nakili kuwa ni kweli, ila Nisamehe mwanangu.. Wewe ni damu yangu”



    Aliongea mr rashidi, wakati huo mzee analia huku adam na Abdallah wanamfuta baba yao machozi,…

    “baba… Mimi nimesha kusamehe..”

    Baba alishukuru sana,… Licha ya baba hata Abdallah nae alishukuru mno, mana adam ni ndugu yake…

    “Nimekusamehe baba yangu…. Lakini.. Naomba uniache kama nilivyo, baki na imani yako na mimi nibaki na imani yangu… Wewe ni baba na mimi ni mwanao… Nina baba alio yajali maisha yangu… Nampenda sana… Kuanzia sasa nimekusamehe…”

    “Ahsante mwanangu, mimi sina pingamizi juu ya imani yako… Najua kwa sasa wewe ni mchungaji… Na naifurahia nafasi ulionayo…. Baba Nashukuru kwa kunielewa… Nakutakia maisha mema, na kila gumu kwako liwe lepesi mwanangu… Huyu hapa… Anaitwa Abdallah… Ni mdogo wako… Na ndie alieniambia kuwa bosa wetu anaitwa jina kama lakwangu, ndio nikaamua nije kukuona…. Ni kweli ni wewe… Mungu akuongoze kwa kila jambo… Ahsante sana mwanangu…”

    “Nashukuru sana baba… “

    “naomba nikuache uendelee na majukumu mengine,.. Nisalimie mama yako… Mwambie anisamehe sana, nimekili makosa yangu”

    “sawa mzee wangu….. Ila… Ningeomba kuanzia sasa tafuta biashara ambayo utaiweza kuifanya.. Nikupe mtaji…”

    Baba kuskia hivyo, duuuuuuu hizo ndio neema za mtoto…. Mungu ampe nini

    “Ahsante sana mwanangu…. Nitalifanyia kazi swala hili… Mana mpaka sasa bado ni fundi tu kwenye magereji ya watu”

    “Usijali baba….. Naa, kuhusu Abdallah nadhani ninae hivyo hakuna kilicho haribika…”

    Aliongea adam huku baba akiwasihi wawili hao

    “najua imani zenu ni tofauti…. Wewe ni muislamu, na wewe ni Mkristo…. Nawaomba sana… Pendaneni wanangu, hizi ni dini tu, zisiwafanye mgombane… Tembeleaneni, peaneni ushauri wa hapa na pale…”

    Aliongea baba na kuwapa usia mzito juu yao…



    Lakini hawajakaa vizuri mara mr Jacob nae huyo,…. Adam alishangaa mr Jacob anampa mkono mr rashidi,

    “bwana rashidi…. Wewe ni mzee mwenzangu… Sasa tunatakiwa kifanya ibada na kuwaangalia watoto wetu kile wanachokifanya…. Binafsi yangu nimekusamehe kwa moyo mmoja,…”

    Aliongea mr jacob huku wakikumbatiana…

    “nami nikupongeze kwa malezi bora uliomlea mtoto wako…. Inapendeza sana..”

    Aliongea bwana rashidi kumaanisha kamlea adam katika malezi bora,..



    Mara ghafla mama nae huyo, pia kaja Kumsamehe mzee rashidi… Mana Mungu alisema, samehe saba mara sabini,…. Na kwakuwa wote ni wenye imani na mungu,.. Basi wote walimsamehe bwana rashidi… Na sasa kila mmoja ana furaha juu ya Kumsamehe mwenzake….



    Kesho yake mr joshua akiwa nyumbani kwa adam mana ndipo anapoishi, mana anapenda sana nyumba yenye familia kubwa na yenye furaha….. Adam wakati huo yupo kanisani kwake akitoa baadhi ya mahubiri, tena aliongelea swala lililotokea jana… Mana ukiwa mchungaji unatakiwa kuwa mkweli



    “siwezi kuamini ya kwamba lile neeno la SAMEHE SABA MARA SABINI jana limefanya kazi yake… Nani aliamini ya kwamba mr rashidi angelifika katika maeneo ya kazi yangu”

    Aliongea adam huku waumini wakitamani kujua nini kilitokea,…

    “haleluyaaaaaaaa”

    “aaaaaameeeeeeeen”

    “ilikuwa ni ngumu kutoa msamaha ule,.. Lakini nilipokumbuka lile lile neno la mungu katika Biblia Agano Jipya. Mathayo 6:14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi……. Nilipokumbuka haya maneno ya mungu…. Nikawa bado sijaridhika.. Nikafuata mstari wa chini yake uliosema hivi….  Mathayo 6:15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu……. Hapo nikaogopa na kumsamehe baba yangu mzee rashidi…. Ila ni kwa hekima ya maneno ya mungu pekee…. Haleluyaaaaaaaaaaaaaaaaa”

    “AaaaaaaaaaaaaaaMeeeeeeeeeeeN”

    “tumsifu bwana yesu Kristo”

    “milele amina”

    Waumini walikuwa na furaha sana mana kila analo liongea adam, basi kwa waumini kwao ni furaha na ndio mana kila ibada inawaingia moyoni

    “haleluyaaaaaa”

    “aaamen”

    “tumsifu bwana Yesu Kristo”

    “milele amina”

    Adam alikuwa akishuka mpaka madhabahuni kwa furaha ya mahubiri ya siku hio, yaani amejawa na imani kuliko siku zote….

    “Hallelujah”

    “amen”

    “ndio mana kuna siku nilisema kuwa, tusigombane jamani…. Sisi ni wamoja, hebu angalia hata hili neno HALLELUJAH, ni dhahiri kwamba sote Mungu wetu ni mmoja…. Angalia hili neno JAH….  Hili neno JAH, lipo mfumo wa Kiingereza, lakini ukija kwa katika imani ya wenzetu wanaita JA, mafano wakitaja Mungu kwa maandiko yao huwa hivi… DHUL-JALAALI

    WAL-IKRAAM, au kwa jina lingine huita hivi….. AL-JAAMI’…. yaani ile JAH na kwa wenzetu nao ni JA…. kwahio hizi herufi tu, zinatupa mwanga kuwa sisi ni wamoja, kasoro dini tu… Hivyo tupendane jamani… Haleluyaaaaaaaaaaaaaaa”

    “aaamen”

    “wale vijana wa chain player… Kama Kawaida, leo nitakuwa nanyi mwanzo mwisho… Lakini natumai kesho mungu akiniamsha salama.. Nitakuwa na iziala na mchungaji joshua… Kesho nitaanza kuzunguka Tanzania kuyatoa mapepo yooote yalioizunguka Tanzania yetu…lakini tutaanza na arusha….. Haleluyaaaaaaaaa… “

    “aaaaamen”

    Baba wa adam sasa ni muumini kama waumini wengine, sasa hana hamu na uongozi wowote kwani tamaa imempeleka pabaya… Na sasa kajifunza,.. Ni vyema kumtegemea mungu kuliko binadamu mwenzako… Binada hatokusaidia lolote, lazima mkono wa mumgu uhusike….



    Kesho mr Joshua alimtaka adam aanze kumuelekeza baadhi ya makanisa ili kutoa mapepo kama aliokuwa nayo mr Jacob,…. Kazi ilikuwa ni ngumu lakini kwa uwezo wa mungu walikuwa wakifanikiwa… Na mtu wa kwanza kuanza nae alikuwa ni mr yohana…. Catherine haamini hata zile pesa alizopewa na baba yake adam, hakuna hata sent, baba yake hana hata senti, na wao hakuna aliomfuata mungu…



    Adam akirudi nyumbani amechoka huku koo likimkauka,…

    “pole baba mtumishi wangu… Hakika hio ndio kazi yangu…. Au unataka kuacha”

    Aliongea eva ambaye kwa saaa ni mke wake wa halali…

    “weeeeee…. Usikute wewe tayari una pepo wewe, unaniambia niache… Shindwa kwa jina la Yesu”

    Aliongea adam huku akimnyooshea mkewe mkono

    “hehehehehheheheheeheh…. Bwana mimi sina pepo, nilikuwa nakupima tu baba mtumishi wangu…. Fanya kazi ya mungu iliokuleta duniani… Mungu akuongoze pale utakapo anza safari za mikoani”

    “amen…… Sasa nikianza safari za mikoani… Wewe ndio kila kitu kanisani… Wewe mama mchungaji”



    Baada ya miezi kadhaa, adam akiwa bado yupo mikoani, na mr joshua, mana kazi ya mumgu ilinoga mpaka wanafikisha miezi kadhaaaaa….. Adam akiwa katika maombezi katika mkoa fulani,… Alipata simu toka kwa mkewe….

    “haloo mama mchungaji, tumsifu Yesu Kristo”

    “milele amina baba mchungaji”

    “haya niambie za toka jana… Mana mama mchungaji, simu kila siku huchoki wewe”

    Aliongea adam akiwa pembeni ya jukwaa lililoandaliwa kwa ajili yao..

    “leo nina habari njema”

    Aliongea eva huku akiwa na furaha sana

    “najua kuwa, habari nyingi hua ni njema sasa sijui hio ina unjema gani”

    “baba mtumishi…. Yesu asifiwe sana.. Tena sana”

    “milele amina… “

    “baba mtumishi”

    “naam mama mtumishi”

    “hapa tumboni nina mr jacob anakuja”

    Aliongea eva akimaanisha kuwa hapo alipo, ana ujauzito kama vile mr Jacob,…

    “acha utani we mwanamke”

    “kweli vile huskii akilia”

    “waaaaaaaoooooo, Haleluyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa”

    Adam alipiga kelele mpaka wahudhuriaji wa semina hio wakashangaaa, mchungaji kapatwa na jambo gani huko la furaha…. Adam alipanda katika jukwaa na kusema…..

    “tumsifu mungu baba muumba mbingu na ardhi”

    “aaaaaaaameeeeeeen”



    SHUKRANI ZENU ZA DHATI KWA KUNIFUATILIA MWANZO MWISHO..





    MWISHO

     

0 comments:

Post a Comment

Blog