Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE DOM - 5

 

     



     

    Chombezo : The Dom

    Sehemu Ya Tano (5)

     



    "we leah utaumia wewe, unapeleka wapi domo lako ilo"

    Aliongea sahi wakati akikusanya chupi,.. Sasa leo kumbe yalikuwa ni mawazo yake, kuwa keshakuwa mke wa sahi, sasa wakati wanalambishana, huku upande wa kweli, leah anapeleka mdomo mbele, ndio sahi akamuona na kumstua...

    "twende ukaoge basi upate supu"

    Sahi haamini kama tayari keshapikiwa supu, yaani ile nyama mbichi ya jana, leo imepikiwa supu,

    "shika michupi yako"

    Sahi alimpa nguo zake huku akifunga taulo, kuelekea bafuni,...

    "sasa unaendaje peke yako jamani"

    Aliongea leah wakati huo sahi anazidi kwenda tu,.. Leah alizitupa zile nguo na kuwahi bafuni ili aoge nae, yaani hampi chansi, kikubwa leah azoeleke kwenye akili ya sahi,..

    "kwanini tuoge wote, afu jacuzzi dogo hili"

    "nawe kqanini ulale na mimi usiku kucha ushindwe kuoga na mimi"

    "leah unajua tutachelewa kwenda"

    "ndio tuoge sasa tuondoke"

    "ivi we kabila gani"

    "msambaa"

    "duuuuu kumne ndio mana upo kama chizi yan"

    "sawa haina shida, lakini nataka nikuogeshe leo"

    Sahi ana shida sana na huyo mwanamke hivyo hataki kumuuzi kwa wakati huo, ila wakimaliza kazi tu, asepe zake tena wasitake mazoea kabisaa... Basi leah nae ndani ya jacuzzi utoto kwake hauishi, sasa sahi anajikuta anazidi tu kumzoea taratibu sana,... Leah na lile umbo, ukijumlisha na jinsi vile alivyo jipakalia povu, yaani kawa mlaini hata mtoto mchanga kasingiziwa...







     





    Kuoga kulinoga mno, sasa ile kushika shikana mara leah kamgusisha kalio mara wanashikana sehemu fulani, sasa saa ngapi sahi asianze ushetani,... Sahi katamani mkia wa leah, NADHANI NIKISEMA MKIA MNAELEWA NI NINI.. Leah akiwa kainama katika jacuzzi huku povu likimjaa mwilini, sahi alimsogelea karibu na kuanza kumshika shika upya, lakini safari hii sahi anataka mkia,.. Sasa leah yeye anajua sahi keshamtamani hivyo wacha ageuke ili ampe utamu wake, kila akigeuka sahi hataki agauke, mana kashikwa

    "jamani sahi, ngoja basi nikurahisishie baby"

    Leah keshaanza majina yake ya kimapenzi,..

    Lakini sahi kakaza tu hataki leah ageuke, akae vile vile kama mbuzi,..

    "leah, please naomba kichwa tu"

    Sasa leah anashangaa, mtu anaomba kichwa tu na wakati jana aliliwa mwili mzima

    "sawa ngoja basi nigeuke jamani"

    "Nooooo,... Si unajua thamani ya kondoo hutokana na nini"

    "najua, hutokana na mkia"

    "basi mteja kapenda mkia"

    Sasa leah ndio anajua kumbe sahi anataka kinyume na maumbile,.. Masini leah hajwahi hata kutaamkiwa hilo tendo, sijui kama alishawahi kufanya,...

    "sahi, unamaanisha unataka huku"

    "yes, kidogo tu leah"

    "hapana... Sahi, siwezi kufanya hivyo.. Sijawahi hata siku moja yaani hata kutaamkiwa hilo jambo"

    "kichwa tu"

    "No, No, Siwezi sahi.... Sijawahi... Nitapata shida kupata mtoto.. Naomba endelea huku tu"

    "leah, kwani hunipendi"

    Leah kusikia hivyo, mmmhh alinyamaza kwanza,... Kisha akasema

    "jamani sahi, nitaolewa na nani mimi nikifanya huko, wanaume wengi hawapendi wanawake wenye tabia hio"

    "nitakuoa mimi"

    Leah alitoa macho kama paka mwizi

    Ila kama unavyojua wanaume tulivyo waongo

    "Sahi unasema kweli?"

    Leah aliongea hayo huku akikumbuka kauli ya mama yake mzazi ikisema kuwa

    "MWANANGU, UNAKWENDA MJINI, LAKINI NAOMBA UJITUNZE MANA RAHA YA MWANAMKE NI KUOLEWA MAMA, SAWA"

    alipomaliza kukumbuka kauli ya mama yake,.. Alimwambia sahi kuwa

    "lakini mimi sijawahi jamani sahi, ntaumia"







    Yaani leah kwa fundisho alilolipata kwa siku jana na yule mama, akichanganya na kauli ya mama yake mzazi aliomwambia siku wakati ndio anakuja mjini,...

    Aliona kuolewa ndio ishu ya mjini, tena anaitamani ndoa sana tu sema uchangudoa alio nao ndio balaa kwa wanaume waoaji,.. Kweli ni mzuri na ana umbo zuri lakini kazi yake jamani umalaya tupu,..



    "lakini mimi sijawahi jamani sahi, ntaumia"

    Aliongea leah huku kweli akimgeuzia sahi mkia, kweli leah alikubali kitoa mkia ili aolewe na sahi, sasa uliona wapi mwanaume akaoa mwanamke mtoa mkia,.. Sahi kila akiingiza mtoto wa watu anashtuka kama kwamba ni kweli hajawahi kufanya tendo hilo,.. Kila akiguswa leah hatulii,..

    "nini leah"

    "nimekwambia sijawahi sahi, nionee huruma basi taratibu"

    "sawa..... Ayaaaaa... Kalete kondom kwenye mkoba wako leah"

    Sahi aliongea hayo huku akikumbuka zinaa bila kondom haifai,... Sasa sahi kasahau jana kamla mtoto wa watu nila kondom, na mbaya zaidi leah ni changudoa, tena member haswa,...

    "mimi sina kondom jamani sahi"

    "sasa kazi yako unaifanyaga vipi,.. Inamaa wanakukula bila kondom"

    "sahi, mimi sio malaya kama unavyofikiria sema sina cha kujitetea kwakuwa umenikuta katika mazingira yale"

    "aaahhh we malaya mi siwezi kukufanya bila kondom"

    "sasa sahi jamani, mbona jana umenibabadua raundi nne nzima bila kondom"

    "leah unasemaje we malaya"

    "jana hatujavaa chochote"

    "mungu wangu leah ushaniua aisee,.. Leah ujinga gani umefanya lakini we malaya??... Kutwa kucha una wanaume afu unakuja kunipa mdude wako bila kondom kwanini lakini leah"

    "sahi mimi nipo salama"

    "salama ya baba ako.... we fara nini wewe, ivi una akili wewe bwege"

    "sahi... Nipo tayari tukapime uhakikishe, mimi sio malaya sahi"

    "sitaki uniambie usenge wako"

    Sahi alikasirika sana hata hamu ya mkia hakiwa nayo tena, yaani hatamani mkia wala wa masikio,...

    "nisamehe basi"

    "yaani kama sio kuitafuta dom wewe ningekuchapa risasi ufilie mbali hiko"

    Unajua jana sahi alidatishwa na mtoto wa kitanga, kadata mpaka kasahau kuulizia kondom,.. Akajikuta anafanya kavu kavu, mbaya zaidi leah ni changudoa tena member kabisaa.....

    Leah alimaliza kujisuuza sahi kwani hata anakumbuka hilo,.. Katoka na povu lake akajifuta tu

    "njoo ujisuuze basi jamani"

    "afu wewe, sitaki mazoea na wewe.... Tena lazima tukapime,... Ole wako ukutwe nao, yaani leo nabeba bastola, yaani ukisemekana unao tu.. Sikuachi"

    "sawa, beba hata bastola mbili, unipige kote kote"

    Aliongea leah kwa kujiamini mno,...

    "nenda kavae twende mbwa wewe,..."

    "supu je"

    "aiseee wewe, ivi unanijua vizuri"

    "basi yaishe"

    Leah kaingia chumbani kwake ili kubadili nguo,.. Sahi hana hata hamu na supu tena, haaa mtu anaejiuza leo utembee nae kavu kavu, heeeee sahi haamini macho yake, yaani haamini kabisaa... Masikini supu iliwekwa mezani inaachwa ivyo ivyo ilivyo, leah akiangalia supu alioipika ikapikika, leo hainyweki tena,.. Waliiacha hapo mezani kisha wakapanda gari wote kulekea hospitalini,... Anaetakiwa kupima ni leah mana sahi akipima hatoonekana kuwa nao kama kaambukizwa... Mana ni leo tu, ila leah ndio wa kupima,.... Walitoka nje ya geti na kulifunga kwa rimoti,...



    Sahi alikuwa na hasira ya ukweli ukweli, yaani leo kitaumana huko hospitalini.... Haikuchukuwa muda wakawa wamefika katika hospitali moja hivi ndogo iliopo jirani na ostabei,.... Waliingia hospitali hapo na kumuona dokta mkuu,

    "za saa hizi dokta"

    Alisalimia sahi wakati huo sahi ana hasira lakini alionyesha sura ya bashasha

    "salama kijana hali yako"

    "nzuri tu"

    "Enhee niwasaidie nini na mama"

    Dokta aliongea hivyo akizani ni mkewe, kumbe ni kahaba fulani tu..

    "aahhh tumekuja kujua afya zetu"

    "ooohhh vizuri sana kijana, uamuzi mzuri sana... Yaani kwa jinsi mlivyo naanza na nyie, mana mumenifurahisha sana"

    Aliongea dokta huku akichukuwa zana za kazi kwa ajili ya kuanza kuwapima wawili hawa,.. Leah hakuwa na wasiwasi kabisa yani utafikiri alikuja kupima jana,...

    Basi walipimwa wote kisha wakapewa dakika chache wakae mahali,



    Huku Ikulu kwa Mheshimiwa rais aliokuwa akipiga simu kwa General wake mkuu wa majeshi,..

    "hallo, nyange"

    "ndio mheshimiwa rais"

    "nakuhitaji uje ikulu kesho"

    "kuna nini mr President"

    "amri yangu hua haina maswali"

    Raisi alikata simu kisha akatafuta namba nyingine, hatujui ni nani







     





    Sasa huku kambini, TMA wakiwa wamekaa watu watatu,.. General nyange, General Deo, na Joseph John ambae ndio mkuu wa pili wa kitengo cha TSS kule jijini Dar es Salaam, sasa hapa yupo arusha..

    "baba yako kanipigia sasa hivi tu"

    Aliongea General Nyange kwa kumtaarifu Joseph ambaye ndio mtoto wa rais GU, huku akiwaonyesha wenzie namba za mkuu wa nchi,....

    "amesemaje"

    Aliuliza Joseph, huku akiwa na wasiwasi kuwa tayari wameshajulikana... Lakini kabla Nyange hajajibu, ghafla simu ya Joseph inaita...

    "aaahhh mbona ananipigia"

    "nani huyo, ni raisi"

    "ndio, ni baba"

    "mpokelee"

    Joseph aliipokea simu ya baba yake, wakati huo ni uoga mtu aliokuwa nao

    "haloo mr daddy"

    "sitaki cha Daddy wala konyagi... Nataka kesho saa tatu kamili nikuone Ikulu mara moja"

    Kabla Joseph hajauliza simu ilikata kisha ikaita kwa generally deo,... Yaani kila mmoja alio onekana kwenye ushahidi lazima apigiwe simu, kasoro wanafunzi tu, mana anajua hawa wamekokotwa tu... Wote walipigiwa simu wafike Ikulu, na mbaya zaidi walikuwepo wote wakati wanapigiwa kila mmoja...

    "mzee nyange, hili ni jipu hili, yaani hapa hatuna chetu tena"

    Aliongea Joseph ambae ni kijana mdogo sana, ila ana cheo kikubwa mno,... Yeye mavazi yake ni suruali nyeusi na shati jeupe, kisha na tai nyekundu, huyo ndio Joseph hata kwenye kava tunaona picha hio,.. Ila sahi yeye ni mzee wa nguo nyeusi tu, na ndio mana akaitwa BB (Black Boy)

    "ni kweli, yule kijana ni hatari sana"

    Aliongea mr deo, huku Joseph akidakia kuwa

    "mbaya zaidi yule ni mtoto wa General nyange"

    Aliongea Joseph huku General nyange akiwa kimya

    "ndio, mtoto wake ndio katuchoma"

    Kwa sasa sahi keshajulikana kiwa sio sahi, bali ni sheby ambae ni mtoto wa General nyange,..

    "lakini huu sio wakati wa kulaumiana, hata mimi sijui kama ni mtoto wangu, nyie ndio mnaniambia hivyo"

    "sasa kama sio mtoto wako ni nani"

    "mimi najua mtoto wangu alishakufa"

    "ok Tuachane na hayo,... Mzungu wa dom anasemaje"

    Aliuliza Joseph mana yeye ndio kiungo mkabaji kwenye dom

    "mzungu amesema dom ni feki, na anahitaji dom original, nami najua tu ile tuliompa yule kijana ndio dom original, na ni lazima awe nayo tu"

    Aliongea general nyange, huku akitamani hata kulia yani,...

    "sasa atatupatiaje hio dom"

    Aliuliza Joseph Wa John huku General nyange akiumiza kichwa jinsi ya kuipata dom....

    "yes, nimepata wazo... Lazima tuipate, na tukisha mkabizi mzungu, sioni haja ya kuwepo Tanzania tena"

    Aliongea general nyange huku general deo katulia tu,... Joseph akauliza

    "ni wazo gani umelipata mzee"

    "tulia kijana... Sasa wewe pambana kuitafuta Codes za dom original, mana tumeshaipata tayari"

    "tumeipata kivipi general"

    "we kalete codes zake kama ulivyoleta dom"

    Aliongea mr nyange kwa kumbembeleza Joseph.... Sasa hapa ndio tunapata picha kuwa Joseph ndio alioiba ile dom kule BOT, mana ana cheo kikubwa na istoshe ni mtoto wa raisi,...

    "sawa, nitaifanyia mpango hio codes, lakini kuwa makini General"

    "usijali"

    Sasa katikati ya maongezi mara General deo kauliza swali

    "ivi huo wito wa ikulu inakuaje jamani"

    Aliuliza mr deo, lakini nyange akamjibu kwa utaratibu....

    "nani aende,... Yule kijana tayari keshatuchomea, yaani tunakwenda kitumbuliwa hadharani mbele ya wananchi,... Siendi ng'ooo"

    "hata mimi siendi"

    "basi hata mimi siendi"

    Wote walikataa kwenda ikulu hapo kesho, na hapo ndio wamesha asi jeshi, tayari wapo kinyume na amri ya  mkuu wa nchi,...

    Mpaka hapo tayari wako nje ya utumishi wa nchi...



    Huku hospitalini sahi akiwa na wasiwasi juu ya vipimo walivyopima pinde tu hapa hospitalini,...

    "leah umeshaniua eti"

    "mimi mwenyewe nina wasiwasi na wewe sahi"

    "tena usinijibishe ujue, ntakuzaba bao sasa hivi eti"

    "basi yaishe"

    Sahi ana hasira na leah sema kwakuwa tu ana kazi nae hivyo anamstahi tu,...

    "mnaweza kuja wapendwa"

    Leah ndio wa kwanza kuamka baada ya kauli ya dokta kuwaita waingie ndani

    "kwanza nawapa pongezi kwa uamuzi mliouchukuwa"

    "Ahsante sana dokta"

    Alijibu leah wakati huo sahi moyo juu juu, yaani changudoa kama huyo kukosa gonjwa ni kitu kisicho wezekana,..

    "labda mnaweza kuniambia nani kawapa ushauri wa kuja kujulia hali afya zenu"

    "dokta, naona maswali mengi sana, ebu tupe hayo majibu tukafie mbele uko"

    "ok.. Samahanini sana,... Kiukweli afya zenu ni nzuri, hakuna mwenye gonjwa hata mmoja... Ila mjitahidi kula vyakula kama matunda matunda hivi, ili kuziboresha damu zenu, mana damu ya huyu dada ni damu yenye kupatwa na magonjwa kiurahisi, hivyo kuleni matunda kwa wingi,.. Ila msiache kuja kupima kila baada ya miezi mitatu"

    Sahi haamini yani, mana uzima wa leah ndio uzima wake yeye,...



    Waliondoka hapo na kupanda katika gati

    "umeamini sasa mimi ni mzima"

    Aliongea leah, huku akimrembulia sahi

    "sina haja na mcho yako.... Sasa sikia hapa tupo kikazi zaidi,.. Safari inaazia hapa hapa"

    "kwa muda huu, hatutofika leo, ni bora tulale tuende kesho"

    "gari ni yangu, tutakapofikia nitakupangishia gest ukalale mi nitalala kwenye gari"

    Leah roho ilimuuma sana, mana tayari keshampenda sahi, yaani anatamani hata kuolewa nae,..

    "sahi, kwanini ulale mbali na mimi... Nimeshaujua utamu wako, kwanini tusilale wote"

    "mapenzi na wewe sitaki tena"

    "sahi, nakubaliana na maneno yako... Lakini nakuomba pale unapota nafasi ya kuoa mke wa pili, naomba unioe mimi,... Najua nyie Waislamu mnaruhusiwa mke zaidi ya mmoja, nipo tayari kukutumikia kama mkeo, na shivaz siendi tena... Naomba uwe mme wangu sahi, hata mimi nahitaji kuolewa jamani,... Please, niwe mke wa pili hata watatu, lakini nihakikishe nina mume ambae ni wewe"









    Wahenga walisema kuwa UOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO, na wengine pia wakasema kuwa KUJARIBU NI KUZURI KULIKO KUACHA KABISA, hii ikiwa na maana ya kwamba unapokuwa na shida ya kitu fulani basi acha uoga, na ustake kuacha ni bora kujaribu ili ijulikane umeshindwa au imeshindikana, lakini UMEJARIBU,



    Kwa upande wa mwanadada Leah alijaribu kutupa karata yake ya mapenzi kwa sahi, yaani kukaa na sahi kwa siku moja tu, kumempa mafunzo aliotakiwa kuyapata mwaka mzima, lakini kayapata kwa siku moja tu,....

    Kila kona anapokwenda anaonekana kuwa mke wa mtu, na hata hapo walipo ni hospitalini walipokuja kupima pia dokta aliwaona ni kama mke na mume, hivyo kwa muonekano huo leah kaitamani sana hio nafasi japo haiwezi kuja kwake... Masikini ya mungu hapo leah kavaa kiheshima yaani ile kimama mama kabisaa, hata wenzake wakimuona watashangaa, mtu aliokuwa akivaa vinguo vya kutega wanaume leo kavaa kimama mama kabisa, ni kitu cha utofauti katika macho ya watu waliomzoea leah....



    "heee, ivi unaongea pumba gani wewe,.. Mi sijawahi kusikia changudoa anaolewa"

    Aliongea sahi huku akifunga mkanda tayari kwa kuianza safari,...

    "kwasababu mimi sio mwanamke si ndio"

    "wewe ni mwanamke ila kazi ulionayo ndio itakayokunyima haki ya kuolewa"

    "ni kweli, lakini mimi siku hivyo unavyfikiria sahi"

    "bwana wewe, funga mkanda twende, kwanza sina hata wazo la kuoa hata huyo mke wa kwanza"

    Aliingea sahi huku akiwasha gari yake tayari kwa safari,... Kweli safari ilianza lakini leah anajutia sana kutotulia kimaisha na kujiingiza katika kazi ya ajabu inayomnyima haki za kuolewa... Mana hakuna mwanaume atakae oa mwanamke changudoa... Tena wanaume wenyewe ndio hawa wa sasa hivi, wana dharau kama mbuzi dume alionusa mkojo... Safari ya kuelekea Magima ndani ndani huko ilianza, ikiwa ni majira ya saa tano za asubuhi, na uzuri ni kwamba wana gari yao... Lakini leah alishngaa mbona sio njia wanayokwenda

    "mbona unaelekea Airport sahi"

    Aliuliza Leah huku akitaka kumwambia sio njia hio

    "we ulifikiri tunakwenda kwa gari,.. Hapa ni mwendo wa kupaa tu"

    Aliongea sahi huku akiingia katika njia ya airport,...

    Leah kusikia wanapenda ndege, alijisikia raha sana mtoto wa kitanga tena ndani ndani huko, hajawahi kupanda ndege hata siku moja, hua anazionaga tu,.... Sasa alishangaa wao na gari yao wanaingia kwenye ndege, yaani walipanda ndege ya abiria ya kawaida lakini haikuwa na watu, sahi aliikodisha mwenyewe kikubwa waende na gari yao ili watakaposhuka basi ni safari moja kwa moja,... Waliingiza gari katika upande husika wa kuingilia magari, kisha wakatoka na kupanda upande wa abiria, yaani wanasafiri na gari yao, pipa linachanganya miguu tayari kwa safari ya kwenda tanga, kutoka jijini Dar es Salaam,



    Huku nyumbani kwa General Nyange, ambako ni kwa mke mdogo,.. Akiwa mezani na familia yake tena ni jijini Dar es Salaam, alikuwa hana raha kabisa, sasa General ana mtoto wa kike, aliokuwa akiangalia Video fulani hivi alioirekodi,.. Yaani huyo mtoto wa kike chakula kinapoa mezani lakini yeye ni kuangalia video katika simu,..

    "we aneth, mbona huli"

    Aliuliza baba mtu ambae ni General nyange,.. Lakini kabla aneth hajajibu mara mama yake kajibu

    "heeeee kumbe we unamuona leo, huyu mtoto ana wiki ya tatu sasa, kula kwake ni kwa uvivuu eti kisa kampenda huyo kijana anaemuangalia katika simu yake"

    "ameshaanza mambo yake ya Facebook"

    Aneth kuskia hivyo akaacha kuangalia kisha akamwambia baba yake kuwa

    "baba, wewe si unapenda niolewe na shujaa wewe?, sasa nimempenda huyu shujaa"

    "ahh peleka utumbo huko"

    "baba si unamuona anavyo wapiga hawa wanajeshi"

    Sasa aneth akawa amemuelekezea baba yake simu ili amuone huyo shujaa,...

    Cha ajabu mr Nyange anavua miwani na kumwangalia vizuri shujaa huyo,.. Sasa aneth kuona baba yake anamuangalia kwa makini, akamwambia mama yake kuwa

    "mama, unaona baba mwenyewe kamkubali"

    Sasa kumbe shujaa mwenyewe ni sahi, masikini mtoto wa mr Nyange kumbe alikuwa akimuangalia sahi,.. Na video hio aliirekodi yeye pale Airport, kama unakumbuka sehemu ya kwanza sahi alipiga pale Airport, sasa huyu aneth nae alikuwa akitoka safari za nje huko, hivyo alipoona mapigano kama yale akarekodi,... Afu pia ukumbuka mlinzi wa rais alimpa taarifa rais kuwa, yeye alimwona mtoto wa General nyange pale... Kama unakumbuka ilikuwa ni kipande hiki hapa chini...



    __________________________________

    "mkuu, nimemwona mtoto wa General, yule wa kike na alionekana nae anatoka korea"

    Aliongea askari huyo huku safari ikiwa inaendelea,....

    "hakuna tatizo, hatojua lolote"

    Aliongea raisi huku safari ikizidi kwenda

    _________________________________



    Sasa huyu mtoto waliomuona ndio huyu hapa sasa ambae hataki kula, yeye na kuangalia video tu

    "we hii video,..."

    Kabla mr nyange hajamaliza kuongea, mara aliona raisi akitokea huku akipiga makofi,... Sasa nyange ndio akaamini kumbe kweli yule kijana ni spy, mana kitendo cha kupigana na makomando watano wale hatari, ni dhahiri kuwa hata wanajeshi hawa wa kawaida hawafui dafu,.. Sasa General nyange akarudisha ile video nyuma,... Sasa baba ndio kageuka mtoto, hali chakula tena kagandana na simu ya mtoto wake kuangalia video

    "heeeee na wewe pia umekuwa kama mtoto wako"

    "kuleni tu,... Mimi naangalia vitu vya maana hapa"

    Mara mama na mtoto wakacheka sana kwa kitendo cha baba kukaa vizuri ili aangalie video vizuri,...

    "baba mkweo jamani mi napenda kuolewa na shujaa kama huyo"







     





    Sasa general nyange aliporudisha nyuma video ile, kuna mahari sahi akatoa kitambulisho, lakini ile anatoa tu kikachukuliwa na askari wa rais, kama unakikumbuka hiki kipande hapa chini



    __________________________________

    Sasa ile anatoa tu kile kitambulisho ghafla kilinyakuliwa na askari wa rais,

    "unafanya ujinga gani... "

    Aliongea askari huyo huku akikificha kile kitambulisho, inaonekana huyu ndio mgeni wa raisi, lakini wale askari walitamani sana kujua kitambulisho cha kijana huyo

    ____________________________________



    General nyange alicheka sana baada ya kukiona kile kitambulisho japo ni kwa mbali sana lakini alikiona, mana alirudisha nyuma kama mara tatu tatu hivi huku akiweka pozi ili aone vizuri, aliivuta ile video wakati sahi anatoa kitambulisho....

    "ahahahahahahahahahahah, mtoto mshenzi sana huyu,..... Haya mama shika simu yako"

    General alimrudishia mtoto wake simu, huku akicheka sana....

    "baba umemuona shujaa wangu"

    Baba kuskia hayo maneno akamfuata mtoto kwa hasira huku akisema

    "acha ujinga aneth, yule ni kaka yako"

    Heeeee wote walishangaa, kaka yake Kivipi, mama ndio mwenye maswali mengi, kwanini awe kaka wa aneth, ina maana ana mke mwingine wa tatu, mana mama huyu anajua wapo wawili, yeye ni mke wa pili, ila kuna mke wa kwanza lakini mke wa kwanza mtoto wake alifia vitani, sasa huyu nae katoka wapi...

    "baba aneth, ina maana una mke mwingine"

    "hapana mama aneth, huyu ndio yule mtoto wangu sheby"

    "mtoto wako sheby"

    "ndio"

    "kivipi na wakati alikufa"

    "hapana... Yupo hai, sema ni rafiki yangu mr President ndio kanichezea kamchezo juu ya mwanangu, na mpaka sasa nina vita vikali sana na mtoto wangu"

    "mbona sikuelewi baba aneth"

    "mr President kamtorosha mtoto wangu kwa kutumia akili yake... Mimi namjua yule tumesoma wote, tumeingia jeshini wote, sema mwenzangu akajitosa kwenye siasa na ndio mana sasa ni raisi, lakini alikuwa ni mwanajeshi kabla ya kuwa waziri wa ujenzi"

    Aliongea mr nyange au generally wa majeshi yote Tanzania,..

    "hahahahahahah, siamini kama kweli mtoto anamsumbua baba yake.. Hahahahahah, dom lazima ikae mikononi mwangu"

    Aliongea generally Nyange huku akifurahi sana na kumpigia simu General deo ambae ni generally mwenzie, lakini huyu ndio General mkuu kuliko deo,...



    Sasa huku kwa sahi anaesemekana ndio mtoto wa General nyange, lakini haijulikani kama ni kweli....

    Sahi na leah walishafika tanga siku nyingi tu na sasa wameshika njia ya magoma huko ndani ndani,... Mana Dar es Salaam na Tanga hakuna umbali kama arusha mpaka tanga,.. Dar es Salaam to tanga ni karibu sana, hivyo akina sahi walisha shuka katika ndege na sasa wapo katika njia ya magoma,... Wakati huo saa zao zinasoma time ya saa 12 za jioni, sahi mwenyewe hajui hio njia afu mbaya zaidi leah kalala kwa uchovu wa safari kuwa ndefu,... Sahi hakutaka kuendelea na safari mana anaejua njia analala, sasa atelekezwa na nani,... Walifika kwenye kakijiji fulani hivi, wakaamua kupaki gari, na kutafuta nyumba ya kulala, almaarufu kama gest...



    Dakika kumi mbele wapo ndani ya gest...

    "duuuu gest haina hata maji khaaa"

    Aliongea sahi huku akitafuta maji ya kuoga,

    "maji yapo ukitaka, ila unaletewa"

    "sasa tukitaka kuoga je"

    "unaita maji, mtu analeta"

    "duuuu... Kazi kweli kweli yani"

    Sahi nae alichoka sana, hivyo walipata chakula ambacho kwa bahati nzuri kilibaki wakati wanakula mchana,...

    "yaani sahi unalala kama gogo jamani"

    "sasa wataka nilale vipi"

    "hujui kama una mwanamke hapa"

    "basi wacha mi nilale chini we lala hapo kitandani"

    Walifanikiwa kupata chumba kimoja tu, mana vyote vimejaa japo ni kijijini,

    "sina maana hio"

    "ila"

    "ina mana hunigusi leo"

    "acha ujinga, kwanza kufanya na wewe jana niliteleza tu"

    "eti eee"

    "tena ngoja nikalale kwenye gari"

    Sahi aliamaka na kuvaa suruali yake kisha akawa anatoka,... Leah alikwenda kumzuia huku akiwa kashika kanga moja kifuani,..

    "we unataka makofi sasa"

    Sahi aliongea hivyo huku leah akaiachia ile kanga na kudondoka chini,....

    "ivi sahi, na uzuri wangu wooote, bado huvutiwi na mimi tu"

    "leah naomba unipishe mlangoni"

    "nami nasema hivi... Nakupisha, ila kwenda huko utakwenda mwenyewe, au lazima nikupoteze njia... Sawa, toka ukalale kwenye gari"









    Sahi anaipenda sana dom, na asipoipata ana adhabu isiojulikana toka kwa mheshimiwa raisi, yaani adhabu haijatajwa na itatajwa pale atakapo shindwa,....



    Huezi amini sahi hakutamani tena kwenda kulala katika gari, mana kuhangaika kote huku ni ili aipate dom,...

    "siamini kama leo tena nafanya mapenzi na wewe"

    Aliongea sahi huku akiwa kweli hana nia ya kulala na leah yaani ni kama anamlazimisha kufanya nae mapenzi kisa tu anatafuta dom...

    "kwani mimi sio mtu sahi"

    Aliongea leah huku akiivua chupi yake tayari kwa kuupokea mtalimbo wa sahi,..

    "tena leo bila kondom leah"

    "lakini sahi jamani si tumepima asubuhi na hakuna mgonjwa kati yetu"

    Sahi hakiwa na ujanja juu ya hilo, yaani kikubwa aipate dom,..



    Asubuhi na mapema gari ikiwa njiani tayari ilisha anza safari toka saa kumi na moja za asubuhi, na uzuri ni kwamba walikuwa wakikaribia kufika,

    "yaani leah siamini kama umenifanya kuwa Sex machine yako eti"

    "kwa ulivyo mtamu, bila kukutishia siwezi kukupata... Natamani kuolewa nawe, ila sio mbaya hata ukioa nipo tayari kuwa mchepuko wako"

    "sawa"

    Sahi yeye anaitikia tu, yaani akipata dom, hataki mazoea na mtu tena, yaani hataki kuskia cha leah wala tunza, yaani hataki tena,...



    Leo huku jijini Dar es Salaam palikuwa na semina ya akina mama katika ukumbi uliopo mlimani City, na mgeni rasmi alikuwa ni mke wa rais, yaani mama yake Joseph,.. Sasa tukiachana na hii semina



    Huku nyumbwkwa generally, sasa huku ndio kule kwa mke mkubwa sasa ambae kafiwa na mtoto wake wa kiume,.. General akiwa na watu wake wawili Joseph na General Deo, wote wapo jijini Dar es Salaam,..

    "heeeeee mwanangu Joseph, karibuni"

    Mama alimkimbilia sana Joseph kwakuwa alikuwa ni rafiki wa mtoto wake aitwaye sheby, yaani wamezaliwa siku moja tena wodi moja na wamesoma pamoja, wamekua pamoja,... Lakini Joseph hakuwa akifurahia kukaribishwa kule na mama na pia kati yao hakuna aliekuwa akicheka,...

    "kwani kuna nini jamani... We baba sheby si nakuuliza"

    Wote hakuna aliokuwa akiongea, kila mtu alikuwa kimya tena wamenuna mnoooooo



    Tuje huku tanga walipo akina sahi,... Kwa bahati nzuri wamefika mapema mno kama majira ya saa tatu hivi za asubuhi,.... Walifika mahali gari halifiki katika hizo nyumba, hivyo walishuka na kutembea kwa miguu,..

    Walifika kwanza kwa akina sauda na kumuulizia... Kwa bahati nzuri leah anajulikana mana ndio vischana vya kipindi hicho kabala hawajaja mjini,...

    "leah jamani umekuwa mzuri... Hakika mama yako akikuona atafurahi sana eti"

    Aliongea mama yake sauda, na wakati huo sauda alikuwa hayupo, sahi anatamani ampate huyo sauda

    "Ahsante mama"

    "shkamoo mama"

    "marahaba baba huyo jambo"

    "sijambo mama"

    "karibuni jamani"

    "Ahsante... Mama sauda yupo wapi"

    Leah aliuliza huku mama akicheka

    "hahaha, mwenzio maisha yamemshinda mjini karudi sasa kaenda shamba"

    Sasa kabla leah hajaendelea kuongea mara sahi kadakia,

    "shambani kwake ni wapi"

    Sahi aliuliza kitendo kilichomtia wasiwasi mama wa sauda,...

    "leah, kwani kuna nini"

    Mama aliuliza kuwa kwani kuna nini, mana sahi kauliza haraka haraka mpaka mama akaogopa....

    "hakuna kitu mama, sema si unajua sauda ni rafiki yangu hivyo nilikuwa nataka nimtambulishe rafiki yangu mpya"

    Leah aliokoa jahazi kwa njia hio ya kujifanya sahi ni mchumba wake, sahi alikua anaharibu kwa uharaka wake mana mama akitia hifu tu, utashangaa sauda hatokei alipoenda

    "jamani leah hongera sana mama angu"

    Mama sauda alimpongeza leah kwa kitendo cha kupata mchumba...

    "karibuni kwanza jamani hata mpate chai"

    Mama alitoa viti huku sahi akikaa lakini hakutaka kukaa kabisa,... Alikaa kishingo upande tu hivyo hivyo,

    Chai ililetwa na mihogo ya kuchemsha wakaanza kunywa ila sahi hajazoea maisha hayo,.. Lakini sasa atafanyeje mana yupo kazini hapo....



    Sasa uzuri wa wamama wa kijijini, hua wana taarifiana kwa matukio mbalimbali,.. Sasa mama sauda kuona ugeni huu unakwenda kwa mama leah, aliona achepuke kwenda kwa mama leah ili ajiandae na ugeni,

    "mama leah ivi una taarifa gani wewe"

    Mama sauda alimuuliza mama leah aliokuwa kakaa kwenye mkeka huku akifuma vitambaa vyake,...

    "sina taarifa yeyote ile mama sauda, kwani kuna nini"

    "heeee, mama unaletewa mkwe mama"

    "mkwe, naletewa mkwe na nani"

    "leah kaja na mchumba wake, hivyo nimekuja kukushitua ili ujiandae usije ukakutwa shagala bagala hapa"

    "mungu wangu, Afadhali umeniambia mama sauda... Hebu nijiandae"

    Mama leah kaanza presha avae nguo gani impendeze, si unajua kijijini kule, wanavaa nguo nzuri mpaka siku ya tukio, sasa leo mtoto wake kamletea mkwe,... Laiti wangejua kilicho waleta, hata wasinge jisumbua kiasi hicho,..



    Huku kwa mama sauda, akina sahi wakiwa wamemaliza kunywa chai,.. Mara mama sauda katokea na kuwapa taarifa,

    "leah, mama anawasubiri kule"

    Sasa leah akashangaa, huyo mama yake kapewa taarifa na nani kuwa yeye kaja,...

    "haya mama tunakwenda"

    Sahi yeye anaangalia ile njia ya kutoka shambani kama sauda anaweza kutokea hata kwa dawa tu,..



    Leah anajua sahi wala haitaji hata kuwajua wazazi wake,.. Hivyo alimuacha sahi pale na kwenda kwa mama yake kumsalimia, mana angekwenda lakini ni mpaka ahakikishe sahi kampata mtu wake,. Sasa leah alipofika kwako, alikuta maandalizi ya viti, mkeka umetolewa ule mpyaaa, tena ule wenye mapambo, mama mwenyewe kavunja kabati ile mbaya... Sasa leah anashangaa upambaji huo veepe,.

    "shkamoo mama angu"

    "marahaba mama hujambo"

    "sijambo mama"

    "pole na maisha mwanangu"

    "Ahsante mama angu, poleni na nyie huku"

    "usijali mwanangu"

    Laiti wamama wangejua kazi za watoto wao huku mjini, wasingesema kitu. Lakini sasa mama anashangaa mbona leah kaja mwenyewe kwanini, na wakati kaambiwa kaja na mwanaume

    "we leah, huyo mkwe wangu yupo wapi"

    Aliuliza mama huku akiangaza macho, sasa leah ndio akavuta picha Anhaaaa kumbe kupambwa kote huku ni kwasababu ya mkwe sio... Alijua ni mama sauda ndio kaja kuubwaga umbea huku kwa jirani yake,... Leah kichwa kinauma, mama yake kavunja kabati, katoa vitu vipya kwasababu ya baba mkwe,... Afu leah akifikiria yeye na sahi wakoje, ndio anachoka kabisa

    "ahahahah mama, si unajua wanaonaga aibu, nilianza kuja mimi kwanza"

    Aliongea leah huku akiwaza atamshawishi vipi sahi aje aonekane kama mchumba wake ili wazazi waridhike tu,... Alipata wazo moja,







     





    Wakati huo sahi kaikodolea macho ile njia ya shambani, yaani sahi anawaza dom tu na sii kingine,... Mara leah katokea mbele yake, huku akiwa mpole,

    "kaka sahi, nakuomba mara moja tuongee"

    "aahh niache bwana... Mi stoki apa, mpaka nimuone sauda hapa"

    "sahi... Nakuomba tu dakika moja tu"

    "ongea tu nakuskiliza"

    "hapana... Twende huku.. Ikiwezekana twende moja kwa moja mpaka shambani kwa sauda"

    "acha utani leah, unapajua shambani kwa sauda"

    "ndio.. Ila tupitie njia hii"

    "twende sasa tusichelewe"

    Sahi aliamka na kumshika leah mkono, lakini leah ana akili yake binafsi,.. Walifika mahari pana kagiza giza ka mahindi, yaani mahindi yametanda kwenye hicho ki njia.... Ghafla sahi anamuona leah kampigia magoti kabisa,...

    "kaka sahi, nakuomba tafadhali sana... Japo swala hili wewe ndio umelisababisha wewe, nimemwambia yule mama sauda kuwa wewe ni rafiki yangu, ikiwa na maana mchumba wangu.... Lakini mama sauda kashindwa kuvimezea, kaenda kuwaambiwa wazazi wangi.. Sasa hivi nafika nyumbani nakuta kumepambwa, kuuliza naambiwa leah anamleta mchumba wake kumtambulisha.... Kaka sahi, nakuomba nitoe aibu kwa wazazi wangu, Please nakupigia magoti,.. Nakuomba uwe kama mchumba wangu jamani sahi Please"

    Wakati huo leah analia kweli kweli huku akimshika miguu,... Lakini sahi yeye kanuna tu wala haongei,..

    "kaka sahi, simaanishi uchumba kweli, nitolee aibu kwa wazazi wangu waliojiandaa kwa ajili yako... Naomba unisaidie sahi... Na kama ni hayo malipo ya wewe kunilipa mimi usinilipe tena, nilipe kwa kujifanya mchumba wangu"

    Sahi aliinama chini na kuyaangalia machozi ya leah,... Sahi ni mwanaume, na ni mpelelezi mzuri, ni myu aneujua fikra za mtu kwa kumwangalia usoni,.....

    Leah alikuwa akilia sana ili amuombe sahi akubali kiwa kama mchumba wake, ili tu wazazi wake waridhike kuwa mwanae kaja na mchumba,.. Yaani ni heshima kubwa kwa mschana wa kijijini kumleta mchumba kwa wazazi wake,... Yaani wazazi hua wanajisifu sana kwa kuzaa mtoto aliewatoa aibu,...

    "kaka sahi, nakuomba... Na kama kunilipa huko haitoshi, basi nitakupa chochote ukitakacho sahi, nipo tayari hata kuwa kijakazi wako na usinilipe, lakini nitolee aibu kwa wazazi wangu,... Nakupigia magoti sahi, na miguu nakulamba baba nakuomba uwe mchumba wangu kwa dakika tano tu"

    Leah aliongea huku akilia machozi, tena wakati huo anaangalia huku na kule Ghafla leah anamuona sauda kabeba jembe lake kichwani,.. Leah akajua sahi akimuona sauda hapa ishu yote itavurugika, na sahi ana hamu na sauda ile mbaya,... Sasa mama sauda nae hamezei jambo,.. Ile sauda anafika tu kwao anapewa taarifa za ujio wa rafiki yake

    "rafiki yako leah kaja, yupo kwao sasa hivi... Tena mwenzio kaja na mchumba"

    Sauda kusikia hivyo katupa jembe kule, kisha kaanza mbio za kuja nyumbani kwa akina leah, na njia wanayoombana akina sahi na leah ni hio hio anayokuja nayo sauda,.. Ukumbuke sauda nae alisha lala na sahi hivyo sijui patakuaje hapo....









    Sahi ni mwanaume anaejali hisia za mtu,.. Kweli leah ni changudoa, ila nae ni mwanamke na anastahili kuolewa kama wengine,.. Na hakuna mtu mzuri duniani kama yule anaechukia kazi yenye dhambi au chafu kwa jamii,... Kitu kizuri ni kwamba leah keshaonyesha dhahiri kuacha kazi hio, yaani iwe isiwe ni lazima kuacha,...

    Kabla ya sahi kukubali au kukataa kwanza alikumbuka maneno ya mama yake mzazi kipindi hicho kabala ya kwenda korea,...



    "mwanangu sheby, natamani sana upate mke mapema mwanangu... Ila baba ndio huyo ni komando anataka nawe uwe komando, yaani sijui itakuwaje mwanangu"

    Aliongea mama yake sheby,.. Na hapa ndio tunapata ukweli kuwa huyu sahi ndio sheby aliozaniwa kufariki dunia, sasa mbona sura sio yakwake kama kweli ni yeye,...

    "mama, licha ya mimi kufanywa kuwa komando na baba, lakini kuna mwanamke gani wa kuia mama katika dunia hii,... Hakuna mwanamke katika hii dunia, wote ni wachafu hawafai"

    Aliongea sahi lakini mama akawa hajamuelewa maana ya maneno yake hivyo mama amesema kuwa



    "SHEBY MWANANGU, DUNIANI HAKUNA MWANAMKE MBAYA,.. DUNIANI HAKUNA MWANAMKE MCHAFU,... ILA HAKIKISHA ANAKUPENDA, ATAKULINDA, ANAKUHESHIM, ANAWAHESHIM WAZAZI WAKO, ANAIHESHIM NDOA YAKE,... MWANAMKE KAMA HUYO SIO WA KUACHA,... HATA KAMA WEWE SIO WA KWANZA KWAKE"



    Hio ni kumbukumbu ya maneno ya mama yake na sheby ambaye kwa sasa ni sahi,... Sasa sahi baada ya kukumbuka maneni hayo, alimwangalia sana leah huku akitokwa na machozi ili akubalia kuwa mchumba feki mbele ya wazazi wake,..



    "Leah,... Sihitaji kuwa mwongo kwako,.. Na sihitaji kuwa mchumba feki,.. Wacha nijitoe sadaka kuoa changudoa... Twende kwa wazazi wako nikawe mchumba wa kweli"

    Leah ni kama vile alipatwa na mshtuko wa ghafla, mana alikuwa kimya kwa muda, sio mchezo kitu ulichokipenda kiwe afu kimekuwa vile vile ulivyotaka, sijui utafurahi kias gani, sasa kwa leah ilikuwa ni zaidi ya furaha,.. Alimkumbatia lakini kama vile haitoshi, wakaanza kunyonyana denda, lakini leah akaona kama vile haitoshi

    "sahi nikupe nini ili ujue nimefurahi sahi, naomba useme nikupe nini"

    Leah alimuuliza sahi ampe nini ili ajue kweli kafurahi kupita maelezo,

    "ninachokitaka ni wewe kuiheshim ndoa yako, kuwaheshim wazazi wote, kuniheshim mimi kama mume wako... Ila cha kwanza uiheshim ndoa yako"

    "twende baba, hayo yote yamejaa katika moyo wangu,.."

    Aliongea leah huku wakikokotana kwenda kwa mama mkwe, na sasa sio utani tena, yaani leah kaokota EMBE DODO kwenye shamba la minazi, ni bahati ilioje kwa mwanamke kama huyu aliojikatia tamaa juu ya kuolewa kwake...



    Lakini ile wanaondoka tu, sauda nae huyo,...

    "leah jamani mambo"

    Ilikuwa ni sauti ya sauda ikimsalimia leah

    "heeeee sauda jamani Mambozako"

    "safi tu za huko"

    "nzuri,... Heee nawe ukiwa kijijini unapendezaga"

    "mmmmhhh mwenzangu, nami sina muda narudi mjini mana nimeshapata mchumba mwenzio"

    Sasa wakati huo sauda bado hajamuona sahi, yaani sura bado hajaiona mana anajua ni mwanaume mwingine tu, afu istoshe sahi ni mzee wa nguo nyeusi na kofia, hivyo kwa haraka haraka huezi kumuona...

    "weee sauda acha utani"

    "ndio, na keshantumia nauli yaani ni mimi kwenda tu"

    "ok, basi shem lako ilo apo"

    Leah alimtambulisha sauda, wakati huo sahi anafurahi sana kwa kumuona mtu wake.. Sasa ile sauda anamwangalia vizuri, mbona ni yule askari aliomwibia ile dom,... Ila sauda hajui kama ile inaitwa dom na hajui kazi yake, yeye aliiba tu,...

    "za saa hizi shem"

    "salama tu hali yako"

    "safi tu"

    Sauda aliogopa sana mana anamjua

    "aahhh nadhani unanikumbuka vizuri eee"

    Aliongea sahi huku akimshika bega

    "ndio"

    "tafadhali sana, sikuhitaji wewe, wala sihitachi chochote toka kwako, ispokuwa kile kifaa tu,.. Ulikiuzia wapi tukakikomboe"

    Aliingea sahi, wakati huo sauda anatetemeka, mana anamjua huyo ni askari,.... Sauda hajui ajibu nini, hajui atamwambia nini... Lakini alishaona kuwa kitu anachokitaka sahi kinaonekana ni cha gharama kubwa sana, hivyo wacha amchombeze kwanza

    "honey, naomba twende kwa wazazi kwanza,.. Wanatusubiria pale nje"

    Aliongea leah huku sahi akimsikiliza leaha kama mkewe mtarajiwa,..

    "sauda, kama hukumbuki, nakupa robo saa tu, ukumbuke hilo suala"

    Sahi aliongea hivyo kisha akaelekea kwa wakwe zake,...



    Sauda anarudi kwao, hata hamu hana, kaiba kitu sasa leo kaletwa na kajulikana mpaka anapoishi

    "umemuona rafiki yako"

    "ndio mama..... Ila kuna kitu niliibaga mama, na huyu kaka ndio kanifuata mimi"

    "uliiba??... Uliiba nini"

    "mimi hata sikujui hicho kidude... Na nilikitupa kule kule Dar es Salaam"

    "mungu wangu sauda wewe, yaani najuta kukuruhusu uende mjini mwanangu"

    Aliongea mama yake sauda huku nae akitamani hata kulia

    "mama, afu mbaya zaidi huyu mwanaume mi askari"

    "uuuuuuwiiiiiiiiiii, yaani mapaka hapo siko na wewe tena"

    Aliongea mama sauda huku akilia sana,....

    "mama, sina budi kumpeleka nilipokitupa"

    "mungu wangu mwanagu huenda usirudi tena sauda"

    "mama, nisamehe sana mama angu"



    Huku kwa akina leah na sahi, ndio wanamalizia Malizia kubarikiwa uchumba wao na wazazi wa leah....

    "leah mwanangu, sasa umeshakua mchumba wa mtu, utulie mwanangu"

    Aliongea mama kumwambia mtoto wake, na wakati huo sahi yupo na mzee ambae ni baba yake leah,.. Yaani mwanaume kwa mwanaume na mwanamke kwa mwanamke... Kwahio kila mmoja anamshauri kijana wa jinsia yake,..

    "mama, hilo ninalo kichwani,.. Siwezi kumdharau mume wangu, siku zote nitakuwa chini yake"

    "halafu kingine ni kwamba,.. Mwanamke hanaga dini, huyu kijana ni Muislamu na sisi ni wakristo,.. Ni lazima uende upande wake"

    "mamaaaaa.... Hilo kwangu ni jambo rahisi sana,.. Kubadili dini kwa ajili ya mume wangu, nipo tayari mama"

    "basi lazima ndoa yako idumu mwanangu"

    "afu mama, tuna haraka sana eti tunataka kuwahi mambo ya mjini, mana si unajua kazi kazi hizi"

    "ni kweli mwanangu, basi mimi nawatakia Safari njema.... Ila saa hizi mtapanda basi gani jamani"

    "mama, tumekuja na usafiri wetu"

    Aliongea leah huku akimfuata sahi kule kwa baba yake mkwe,.. Mana alikuwa anaongea na mwanaume mwenzie

    "kijana wangu, mimi nadhani wewe ndio unaanza kuingia katika ndoa... Kitu kikubwa cha kuzingatia... Mwanamke ni kama ua, mmoja wenu akiwa chini basi ndoa yenu itadumu sana, hivyo jitahidini sana mnapokwazana mmoja ajishushe kikauli"

    "sawa sawa mzee wangu"

    "ila sio wewe.... Wewe hutakiwi kushuka sana kijana,... Wanawake wa siku hizi ukijishusha tu, nae anapanda kichwani, hivyo kuwa makini sana kijana, Mana sasa umeshakuwa mkwe wangu"

    Baba yake leah alikuwa akimpa sahi lisala juu ya kuishi na mwanamke,...

    Basi leah alifika pale na kuaga kwa baba yake,... Ila walipo piga hatua kama mbili hivi lea alimwomba sahi pesa kidogo

    "sahi mme wangu,.. Hapa nina elfu 15 tu hii hapa... Natamani niwaachie wazazi kiasi kidogo, lakini sasa haitoshi mme wangu"

    Aliongea leah tena kwa upoleee, mana keshafundwa na mama yake huko kuwa mume hahitaji sauti ya juu hata siku moja... Basi sahi alitoa waleti na kutoa kiasi cha laki mbili,

    "wape hii, hio yako achana nayo"

    Leah alirudi nyuma na kuwapa wazazi wake ile pesa aliopewa na sahi...

    Basi wazazi ni furaha gani hio, na hio ndio faida ya kuwa na mtoto wa kike,







     





    Wakati huo huku sauda keshajiandaa mana swala la kurudi mjini lilikuwa na ulazima ila sio ombi, yaani ni lazima arudi mjini kuonyesha kifaa cha watu,.. Kwani palikuwa na cha kusubiri,.. Walitoaka hapo mpaka walipoacha gari yao, mama sauda anajua mtoto wake kurudi ni ndoto tu

    Kwa jinsi sahi anavyoitamani kuipata dom, yaani hataki mchezo kabisa.... Basi safari ya kuja mjini jijini Dar es Salaam ilianza, na uzuri ni kwamba ilikuwa ni mapema sana,..... Sauda hana raha kabisa yani, mana ni wiki mbili zimeshapita toka akitupe kifaa kile,... Sasa je? Watakiona.....



    Sasa huku jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Mheshimiwa rais,.. Mzee akiwa sebuleni anaangalia tv, alishangaa kusikia sauti ya kilio huko chumbani kwake,.. Akatilia mashaka hurnda ni mke wake,... Na ni kweli alikuwa ni mke wake aliokuwa akilia

    "we vipi tena, chato kuna msiba"

    Aliuliza mr GU huku akimuamsha mkewe,...

    "siamini kama mtoto ndie aliekufa"

    Aliongea mke wa rais huku raisi akishangaa kwa maneno ya mkewe,..

    "huyu mtoto sintomuua bi ni lazima nimtumbue, mi nikajua unamlilia mtoto nani kumbe ni huyu fara... Lazima nimtumbue jipu, afu na vile kakataa wito wangu.. Yaani sipati picha"

    Aliongea mzee GU huku akiondoka chumbani taratibu..

    "mimi simsemei Joseph"

    Aliongea mke wa rais huku rais akigeuka kwa mshangao na kuuliza

    "unamsemea mtoto gani, na sisi tuna mmoja tu"

    Sasa mama kabla ya kumwambia mumewe, kwanza alikumbuka siku ya jana wakiwa kwenye semina ya akina mama....



    Wakati semina hio inaisha na mgeni rasmi alikuwa ni mke wa raisi,.. Lakini ile mke wa rais anaingia tu ndani ya gari, kuna mama mmoja hivi akamuita...

    "mwanangu, mwanangu samahani sana"

    "bila Samahani mama shkamoo"

    "marahaba... Mwanangu kama nakukumbuka"

    Aliongea mama huyo wa makamo sana tu,

    "mmmhhh labda, ila mimi sikukumbuki"

    Aliongea mke wa rais huku akiwa na shauku ya kukumbushwa

    "miaka kadhaa ya nyuma, mimi nilikuwa ni dokta,.. Nakumbuka mlikuja kujifungua katika hospitali moja, mlikuwa wanawake wawili afu wote waume zenu ni wanajeshi"

    Sasa mama Joseph au mke wa rais akakumbuka ni kweli

    "waoooo wewe ndie yule dokta ulietuseidia"

    "haswaa.. Ilikuwa ni zamani sana... Halafu waume zenu wajinga sana yaani wanakuja kufanyia mazoezi hospitalini"

    Aliongea mama, mana kipindi hicho rais GU na General Nyange walikuwa ni marafiki wakubwa sana, walisoma wote, wakajiunga na jeshi wote, kwa furaha hata ndoa zao zilifungwa siku moja... Kizuri zaidi hata wake zao wote wakashika ujauzito kwa wakati mmoja,... Ila siku ya kujifungua, alianza huyu mke wa rais, sasa mke wa General ndie alikuwa karibu sana na mke wa rais, hivyo alivyosikia mwanamke mwenzie atajifungua kwa operesheni,.. Mke wa General alishtuka na kuanza kuskia uchungu ghafla, lakini yeye hakuwa wa siku hio ila kwa mshtuko, ikawa siku hio hio na wakajifungua siku mbili tofauti, yaani walifuatana... Sasa vitoto vyao vikawa vimelazwa katika kitanda kimoja....  Sasa kumbe majamaa akataka kuwakaribisha watoto wao kijeshi jeshi.. Saa ngapi wasije na mabunduki hospitalini,.. Mlinzi kuona mabunduki, akatangaza vita imeanza, basi viashiria hatari vikawashwa, ili mwenye kujiseidia ajisaidie.. Sasa wale wazazi wawili wakakurupuka na watoto wao... Kumbe wakati wanachukuwa watoto wao, walijichanganya na kila mmoja kuchukuwa mtoto wa mwenzie... Na hivyo ndivyo ilivyokuwa...



    "hahahahaha bwana mama unanichekesha sana... Unajua wao walikuwa wanajeshi kweli, na walitaka kuwakaribisha watoto wao kijeshi jeshi na ndio mana wakaja wanajeshi wengi pale hospitalini"

    "sasa kama unakumbuka siku ile mlikuwa watu wawili mlijifungua chumba kimoja na yule mwenzio yule unamjua... Lakini wakati ile vita inatokea, wewe ulichukuwa mtoto wa rafiki yako,.. Nikatamani kukuambia lakini nikaikosa nafasi"

    "ati unasemaje??... Yaani nilichukuwa mtoto wa rafiki yangu"

    "ndio... Mimi nakumbuka wewe ndio wa kwanza kujifungua,.. Na mtoto wako ana alama hapa chini ya jicho la kushoto"

    Sasa mke wa raisi ndio anakumbuka mtoto mwenye alama ni yule mtoto wa General nyange ambaye ndio sheby, au sahi wa sasa hivi, lakini mke wa raisi anajua kuwa yule mtoto alikufaga...

    "we mama acha utani"

    "mimi nakuambia sasa, ulichukuwa mtoto wa rafiki yako.. Umelea mtoto sio wako"

    Pale pale mke wa rais akaanza kulia, lakini mama akamuuliza

    "unalia nini sasa, yaani kukupa ukweli ndio ulie"

    "hapana... Nalia kwasababu huyo mtoto keshafariki dunia.."

    "ooohhh pole sana"



    Kumbukumbu ya mke wa rais baada ya semina iliishia hapo...

    "baba Joseph, kumbe yule kijana ni mtoto wetu"

    "kijana gani huyo"

    Hata mheshimiwa GU hajui kama sahi ndio mtoto wake,.. Yaani Joseph ndio mtoto wa Generali nyange, sema haijulikani....

    "yule mtoto wa rafiki yako"

    "unasemaje"

    "ndio.. Jana nilikutana na dokta akanipa ukweli wote, na sababu ni ule ujinga wenu wa kuja na mabunduki hospitalini, mpaka watu wakachanganyikiwa"

    "ahahahahahahahahahaha saaafi sanaaaa"

    "sasa unacheka nini baba Joseph"

    "hahahahahaha kama ni hivyo basi safi sana... Huyu sahi unaemuona anakuja kuja hapa ndani... Ndio yeye huyo.. Hahahahahaha saaafi sana"

    Mzee GU alifurahi sana kwa taarifa hizo, mana amepata kijana shujaa

    "unasemaje baba Joseph"

    "weee koma, mimi sio baba Joseph wewe"

    "heeeee mara hii umeshamkana mtoto uliomlea"

    "sina mtoto jambazi mimi"



    Baada ya siku hio kupita, kesho yake sahi na sauda wakiwa katika dampo, yaani sahi haamini kama dom imetupwa dampo, yaani haamini macho yake Kiukweli...

    "yaani sauda unatupa kifaa kama kile dampo?"

    Aliongea sahi huku akitamani hata kulia, lakini sasa mbaya zaidi taka taka zilishachukuliwa na kwenda kumwagwa dampo kuu.. Hivyo hapo ni peupeeeee....



    Sahi alikimbia manispaa ya jiji hilo na kupewa mamlaka ya uongozi wa mtaa ule,...

    "takataka zilichukuliwa jana"

    "tafadhali sana ndugu, naweza kujua aina ya gari inayochukua takataka hapa"

    "ndio.. Na dereva yupo ndani"

    Mara moja kumfuata dereva, kaongea nae sana kuwa takataka alizochukuwa upande huu, alizitupa upande gani kule dampo kuu... Dereva akawa anasita kuingea, sahi kavuta waleti katoa laki Mbili

    "haya niambie"

    Wakati huo wapo dampo kuu hapo

    "nilizimwaga pale, na ni jana tu"

    Sahi alipo onyeshwa tu hajapoteza muda, si unajua dampo kuna wale watoto wa mtaani wale,... Akawaita na kuwaonyesha kitu watakachokitafuta... Jamani pesa inaweza kufanya lolote lile,.... Sasa sahi anaona wanachelewa kutafuta, nae akaingia kwenye kazi, sahi alivaa nguo zake nyeusi safiii,... Alichafuka hata kichaa ana nafuu, lakini mungu sio asumani kweli DOM hio hapo keshaiona, haamini macho yake kama kweli kaiona dom, yaani alichokifanya ni kuibusu hata kama ilikuwa chafu,... Aliwalipa wale watoto pesa nzuri sana... Sasa ile anaondoka na furaha zake, mara simu mbili zinaita, simu ya mkononi na simu ya sikioni,... Ila simu ya sikioni ananua nani anaepiga ila simu ya mkononi hajui nani anapiga.. Kwanza aliipokea simu ya sikioni ambayo ni ya mr GU,...

    "hello"

    "Mjerumani amekuja anataka dom, sasa sijui upo wapi sasa hivi"

    "nakuja nayo sasa hivi mzee"

    "harakisha"

    Sahi aliachana na ile simu, na hua haikatagi hio simu, sasa baada ya kuongea na hio simu ya siri, sasa katoa simu ya mkononi... Lakini alishangaa jina liliopiga....

    "MAMA"

    aliongea sahi huku akitabasamu kwa kuona simu ya mama yake, wakati huo kachafuka, ananuka kila kona ya mwili wake...

    "hallo mama yangu mzazi shkamoo"

    Aliipokea kwa furaha kubwa sana lakini ghafla anasikia

    "sheby mwanangu, usije huku na usilete hicho kitu wanachokitaka... Baba yako kaniteka huku ananitesa sana... Usije tafadhali sana baba"

    Ilikuwa ni sauti ya mama yake,.. Lakini ukweli wa mama wa sahi ni mke wa rais GU, hivyo huyu ndio ndio mama wa Joseph...

    Mara ghafla sauti ikabadilika

    "kama unampenda mama yako, utaileta hio dom,.. Nadhani unanijua mimi baba yako, siangalii huyu ni mke wangu au laaa,... Naua kama usipoleta hio dom hapa... "

    Aliongea general Nyange lakini kwa mbali sahi akasikia sauti ya mama yake ikisema

    "mwanangu usijeeeeee, acha nife tu"









    Sahi aliisikia hio sauti,... Lakini sasa kumbe ile simu ya siri ambayo ni simu ya sikioni, ina uwezo wa kuvuta sauti ya simu nyingine ya upande wq sikio lingie, hivyo mheshimiwa rais GU kasikia kila kitu,.... Sahi alipotaka kukata simu ghafla General akasikika akisema kuwa

    "na kama unakuja, njoo katika msitu wa sentago mbele ya kambi ya TMA haraka sana laa sivyo mama yako hutomwona tena"

    Sahi alikataka simu, kisha akapanda gari mpaka Airport,... Sahi hawezi kuacha mama yake afe kwasababu ya dom,.... Huezi amini sahi anaipeleka dom kwa general Nyange ili mama yake aachiwe...



    Huku msituni,... Huezi amini Joseph ndio wa kwanza kumwazibu mama yake sahi, lakini bila kujua anamwazibu mama yake mzazi,..

    "Joseph mwangu, leo wewe ni wa kunipiga kibao mimi... Ahsante sana baba"

    Aliongea mama huyo ambae ndio mama Joseph originally,...

    "mimi nataka kupiga pesa, sasa nitaonaje haya kukupiga makofi... Tena usinisemeshe (tasi)"

    Joseph alikuwa ni katili wa kimya kimya,... Mama alikuwa akilia sana na yupo tayari kufa lakini mtoto wake asije...



    Sasa je mama kajuaje kama yule alikuwa ni sheby wake... Kama unakumbuka siku ile sahi alipokuwa katangulizana na Joseph kwenda Airport kubadilishana dom, walikutana na mama huyo njiani.. Sasa sahi alipoingia ndani ya gari ya yule mama alimwambia kila kitu, kiwa yeye ni sheby, ila hapo alipo amefanyiwa plastic surgery katika uso wake, lakini baada ya kazi atavuliwa sura hio na kubaki na sura yake originally,... Hivyo kumbe kweli Joseph alichokisema kuwa sahi ni sheby ila kafanyiwa plastic surgery katika uso wake na ndio mana hafanani na mtu ispokuwa sauti na mwendo ndio mana wengi walimdhania kuwa sheby, ila ni kweli ni Sharbiny Rashidy,...



    Usafiri wa ndege sio wa mchezo mchezo,.. Kwani alichukuwa muda??.. Dakika kadhaa tu tayari yupo ndani ya eneo alilo agizwa,... Sasa tunamjua kama sheby na sio sahi,.. Alipofika kwanza alichungulia katika hio kambi mpya,.. Aliona mama yake anateseka sana ila hajui kama huyo sio mama yake,...



    Sahi alijitokeza huku akiwa kanyoosha mikono juu,... General alipoona dom imefika, alimchapa mkewe kibao cha mwisho mwisho... Hajakaa vizuri Joseph nae akamchapa mama sahi kibao cha mwisho mwisho, hio sahi aliiona,..

    "haaaa Joseph, yaani hata wewe unadiliki kumpiga kibao mama... Joseph tumelelewa na huyu mama leo unampiga kofi"

    "haikuhusu we fara nini, tupatie dom hio"

    "mfungulieni mama kwanza.. Laa sivyo naipigiza chini tuikose wote"

    General anakijua kichwa cha mtoto wake, hashindwi kweli kuipasua hapo chini,.. Basi mama akafunguliwa na kumkimbilia mtoto wake na kukumbatiana,... Sasa kumbe walishapanga sahi auwawe baada ya kutoa dom,... Sahi akawarushia dom yao,... Sasa nyuma ya dom kuna target imemlenga,.. Mama si kaiona, akamgeuza sahi ile risasi ikampata mama, sasa kile kitendo cha General kuzubaa, sahi saa mingi sana keshachukuwa bastola ya baba yake, kitu cha kwanza alianza na wapambe waliozunguka eneo hilo, utamu ni kwamba kila risasi alioitoa haikuwa ya hasara... Wakati huo. Mama yupo. Chini,... Mara bastola ikaisha risasi General anacheka tu kwa kuiona dom, sasa sahi mikono juu kwa kuguswa na ubaridi wa bunduki katika shingo yake,.... Sahi hakuwa mjinga mjinga, alionyesha umahiri wake juu ya uwezo wake,... Aliinama chini huku mguu akiuzungusha kwa nyuma kana kwamba alikuwa akimpiga mtama huyu aliekuwa nyuma yake,... Sasa jamaa aliposhangaa mtama chini, kumbe juu anapokonywa silaha yake,.. Na si mwingine bali ni Joseph,.. Sahi alipoimiliki silaha ile, cha kwanza alivunja miguu, sahi hajakaa sawa mara nae kapigwa za miguu, kuangalia ni nani, ni mwaju.. Kumbe mwaju aliungana na mr general,...sahi akawa hana ujanja tena, dom inakwenda na kutekwa katekwa...



    Lakini mungu sio asumani, gharama kunatua helikopta kubwa sana ilioshusha makomando wapatao 15 ndani yake dokta alikuwepo, sasa hatuji dokta ni wa nini.... Sasa kumbe mr gu alikuwa akiifuatilia ile simu, mana alisikia mazungumzo,.... Viwanajeshi vyote vilivyodanganywa na generally Nyange vilipukutishwa vyote, sasa wamebaki watatu tu General nyange, General Deo, na Joseph ambae kavunjwa miguu na sahi,,.. Mara ghafla dokta anashuka na mke waraisi,.. Dokta kitu cha kwanza alimpa huduma ya kwanza mama yake sahi, uzuri ni kwamba risasi haikupiga sehemu mbaya,.. Hivo huduma alipatiwa... Sasa mke wa raisi alipofika tu, aliita

    "mwanangu sheby umzima"

    Mr Nyange anashangaa, mwanae sheby,... Kivipi... Sasa Nyange hakushangaa mwenyewe tu hata mama yake sheby pia alishangaa,... Na sio mama sheby tu hata sheby mwenyewe alishangaa,...

    "unashangaa nini sasa jipu mkubwa wewe"

    Aliongea rais GU kwa kumwambia General nyange,...

    "ivi nikuulize mr President... Kijana wangu imekuwaje mpaka sasa yupo hai"

    "kijana wako?? Kijana wako ni huyo hapo chini, huyo ndio mtoto wenu"

    "unasemaje mheshimiwa rais"

    Mama sheby alipata hata nguvu ya kuongea

    "huyu hapa chini ndio mtoto wenu"

    "kivipi"

    "siku ile tunaingia hospitalini na mabunduki, tumesababisha wake zetu kuchukuwa mtoto wa mwenzie... Mke wako akachukuwa mtoto wangu na mke wangu akachukuwa mtoto wako... Sasa hivi ndio tunajua hili swala, mtoto wako yule pale chini"

    Aliongea raisi GU, huku akinyoosha kidole kwa Joseph,...

    "afu kwanini hafanani na sura ya mwanzo"

    Aliuliza generally Nyange huku akimuangalia sahi,... Sasa yule dokta aliokuja na mr GU, kumbe alikuja kwa ajili ya sahi, kwani sahi ana nini.... Dokta alimtaka sahi au sheby aje karibu yake,...

    "vua shati kijana"

    Dokta alimtaka sahi avue shati lake,.. Sasa kumbe sahi alishonwa nyuzi maalum katika shingo yake, na ukiangalia kwa umakini utaona kuna kiungio ila usipokuwa makini huoni kitu,.. Sasa dokta alianza kumpaka sahi mafuta fulani katika kile kiungo,.. Dakika 5 mbele, ile sehemu ilionekana kuvimba na nyuzi zilionekana, dokta ndio anajua zinatolewaje nyuzi hizo..... Dakika 10 mbele, damu zilianza kutoka katika shingo ya sahi,... Mama sasa wamama wote wanamlilia sahi, kila mtu

    "jamani mwanangu unamfanyaje"

    Hata mke wa rais hamtaki tena Joseph, yaani baada ya kujua huyo ndio sheby wake, hataki kusikia neno Joseph tena,... Sasa sahi ana wamama wawili...

    "tulieni nyie wanawake, mnalia lia nini"

    Aliongea dokta, wakati huo sahi damu zinamtoka baada ya nyuzi hizo kutolewa...



    Sahi alianza kulivuta lile lingozi alilovalishwa nchini Korea, wakati alipokwenda kusoma,... Plastic surgery zipo aina tatu, kuna ya kuvaa kama likofia tu hilo halina haja ya dokta, na kuna ya kushonwa nyuzi maana yake hio sio ya kutolewa mara kwa mara na ndio hii ya sahi, afu kuna ya kufanyiwa operesheni ya usoni yaani sura yako ndio ifanyiwe operesheni ili ije sura nyingine, hio ni ya milele kabisa.... Sahi alifanikiwa kulivua lile likofia, kila mmoja haamini kama kweli alikuwa ni sheby, na ni kweli ni Sharbiny aliosadikika amekufa,..  Mwaju aliokuwa taabani kwa kuchakazwa risasi za mbavu leo anashuhudia kumwona mpenzi wake kwa mara ya pili,.. Haamini macho yake, lakini wakati huo hali yake inazidi kuwa mbaya,... Na yeye ndie aliempiga mama sahi risahi ya mgongoni....

    "amaizing boy, siamini kama ni mtoto wangu aiseee"

    Aliongea generally nyange ila wakati huo wapo chini ya makomando, hivyo hawakuwa na ujanja hapo walipo.. Mama sheby anajua kuwa ni mtoto wake mana alishampa taarifa kiwa hapo yupo kazini na sura nyingine...

    "haya niambie, kwanini ulimfanya mtoto wangu mfu kumbe ni mzima"

    Mr Nyange alimuuliza raisi GU, kuwa ilikuwaje mpaka sahi akaonekana mfu,....

    "kwanza nimeshakwambia huyu sio mtoto wako, huyu ni mtoto wa Tanzania"

    Aliongea rais GU huku akitoa kumbu kumbu juu ya kifo sa sheby miaka mitatu iliyopita,...



    SASA HAPA NI MIAKA MITATU ILIOPITA....







     





    Kipindi cha uchaguzi mkuu Tanzania, marais walikuwa wengi sana waliogombea nafasi hizo,.. Katika hoteli moja ya kifahari walikutana viongozi wawili, ila wakati huo hawakuwa viongozi wakubwa... Ila mheshimiwa rais alikuwa ni Waziri wa ujenzi,.. Na huyu mwingine sijui alikuwa nani lakini kwa sasa ni Waziri mkuu,..



    "niambie bwana mzee wa kujaaliwa na mwenyezi mungu"

    Aliongea waziri wa ujenzi, ambae kwa sasa ni rais,...

    "safi tu ndugu yangu,.. Naona umeshachukuwa fomu ya kuwania urais mwaka huu"

    "ni kweli... Ila nahitaji nipate vijana kama wawili watatu hivi, niwasomeshe ili nikipata urais wanisaidie kazi ya kuniletea majipu"

    "aaahhh yaani unaandaa vijana kabla hujapata"

    "ndio"

    "ukikosa je?"

    "nikikosa urais nitamuuzia mtu aliofanikiwa kupita"

    "ok.. Sasa mi naona tuangalie kule jeshini, kule hatutokosa vijana"

    "enheeee, umetoa wazo zuri sana... Sasa tunachukuaje kijana pale, mana sihitaji serikali ijue mipango yangu"

    Aliongea waziri GU, huku mwenzie akitafakari jinsi ya kufanya,...

    "mi naona tuanze na kijana mmoja kwanza"

    "sawa, je ni yupi pale jeshini"

    "yule mtoto wa General nyange hafai yule... Mana atakuwa na mazoezi mazuri kwasababu namuonaga sana baba yake anampa mazoezi ya private sana"

    "mmmhhhh nyange ataua mtu,.. Ataua mtu nakwambia"

    "sikiliza bwana mr GU,.. Hatumchukui kama tunachukuwa kuku"

    "tutafanyeje sasa"

    "sikiliza... Hata sisi ni wanajeshi wa kale, na unamjua vizuri General nyange ni rafiki yako... Tumchukue mtoto wake"

    "sawa sikatai, ila tutamchukuaje yule"







    "njia rahisi sana.... Sisi tutafute mtu wa pale kambini, awalete wanafunzi wengi sehemu tunayotaka"

    "kuna.. Jamaa mmoja pale ni mwalimu wa mafunzo ya mabomu,.. Anaitwa mr deo... Tuongee nae huyo mtu"

    Aliongea mr GU wakati huo bado hajawa raisi,..

    "sasa akishawaleta wanafunzi pale tunapo pataka, aanze kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kurusha mabomu, afu amtangulize yule tunaemtaka"

    "una akili wewe,... Sasa huyo deo atakubali kufanya hivyo"

    "tumuahidi kumpandisha cheo kutoka kwenye ualimu kuja kwenye ugeneral"

    "sawa, hebu fanya hivyo... Lakini sasa huyo kijana utampataje"

    "wakisha anza kurusha mabomu, sisi tutakwenda na bomu la kweli, tunalifunga funga kwenye nguo za kijeshi, kisha tunalirusha... Baada ya bomu la kweli kulipuka mahali ambapo hakuna watu, basi huyo deo kazi yake ni kumzimisha huyo kijana, afu atatukuta sehemu tutakayomwagiza... Kwakua ni msituni hakutakuwa na atakaejua zaidi ya huyo mr deo,...na hawatoana mwalimu wao alipopita kwasababu patakuwa na wingu la moshi wa mabomu... Afu wakienda kuangalia watakuta vipande vipande vya nguo za jeshi huku kijana mmoja haonekani... Hio ndio akili yangu"

    "ndio mana ukatwa majaliwa, kumbe una akili kiasi hicho"

    "aahhh sisi wajeshi wa zamani bwana"



    Baada ya siku tatu kweli zoezi lilifanikiwa na kweli sheby akafanikiwa kuletwa kwenye nyumba ya Mheshimiwa Waziri GU,.. Ila sheby hata yeye hakuwa akijitambua mana alibonyezwa mshipa wa fahamu ili asijue kilicho endelea kule msituni

    Sasa muda huo ndio anazinduka akiwa katika chumba maalum.....

    "kuanzia leo umekufa kijana sawa..."

    "nini??.. Afu we si waziri wewe, mbona umeniteka"

    "sikiliza kijana, nataka nikusomeshe uwe ripota wangu hapo baadae"

    "kwahio ndio nimekufa"

    "ndio, na pia utakwenda korea kufanyiwa plastic surgery ya sura yako, na ukirudi sitaki utambuzi wako uhusike, utabadili jina baada ya kumaliza mafunzo ya kijeshi nchini korea, na pia utakwenda kusomea upelelezi, utakwenda kujifunza mbinu za mapigano, yaani kuna option tatu zinazokupeleka kule... Gharama zote za kwenda mpaka kuishi kule ni zakwetu sisi, hivyo tunachokihitaji kwako uthubutu wa kukubali kuishi kama mtu aliekufa"

    Aliongea waziri GU huku sahi akiwa kaketi katika kiti,...

    "Na pia utakaporudi utakuta nyumba yako ipo tayari"

    "sawa, nimekubali"

    Sahi au sheby alikubali kujulikana kuwa kafa ili akasomeshwe nje ya nchi...

    "sasa nataka nikutengenezee vitanzi kadi za bank, ili usiteseke kwa utambulisho"

    "sawa"

    Mipango ya sheby kusafirishwa kwenda nje ya nchi iliisha na sheby alikwenda,...



    BAADA YA MIAKA MIWILI NA MIEZI 9 NDIO DOM IKAIBIWA BOT, NA HAPO SHEBY KABAKIZA MIEZI MITATU KUMALIZA MAFUNZO YAKE, NDIO RAIS GU AKAKUMBUKA KIJANA YUPO KULE KOREA, HIVYO AKAITWA KABLA YA KUMALIZA MIEZI YAKE MITATU ILI AFIKISHE MIAKA MITATU KAMILI.....



    Siku ile sheby anarudi nadhani tunajua, mpaka akapambana na makomando,...



    Walipofika Ikulu sheby alitakiwa kutoa vitambulisho vyake (VITANZI) alivitoa vyote, kisha rais GU akavichukuwa vile vitanzi (KAMA UMESAHAU KASOME SEHEMU YA PILI) Kitu alichokwenda kukifanya kwenye vile vitanzi, ni kuchapisha jina jipya katika vitanzi vile, kisha sheby akaitwa akapiga picha upya.. Kesho yake sheby anakuja akavishangaa sana vitanzi vile,... Kumbe vilikuwa vimebadilishwa majina.. Kutoka Sharbiny Rashidy Kingazi (Sheby), mpaka kuja kwenye jina, Salehe Rashidy Mohammed (sahi),.. Lakini pale pale alionywa kutosema chochote na kutomwambia mtu yeyote yule, ispokuwa mama yake tu, mana mama ni mama jamani roho inauma kumdanganya mama....



    SASA HUO NDIO UKWELI JUU YA SAHI AU SHEBY....



    sasa pale kila mtu anashangaa, ila rais GU akamuuliza mr deo

    "wewe nawe tumekupandisha cheo kwa kazi nzuri ulioifanya, lakini sasa nawe kumbe ulikuwa na mambo yako unayafanya"

    Aliongea raisi GU huku akiwaamuru makomando wawachukuwe watu hao

    Sasa mr deo yeye ndio anashangaa nae, kumbe huyu ndie yule kijana aliomteka na kumpeleka kwa raisi.. Kumbe hata yeye deo hajui, mana deo anajua mpango wa kumteka na kumpeleka kwa Waziri baada ya kuahidiwa cheo, sasa ishu za kijana kubadirishwa sura hajui na ndio mana hata alivyokuja kambini hakumtilia shaka mana haijui hio sura



    "lakini rafiki yangu ulichonifanyia sio kizuri ndugu yangu"

    Aliongea general Nyange,

    "tena nyie mna haki ya kunyongwa kwa ujinga mliokuwa mnaufanya kambini"

    "sawa, umeshika mpini sisi tumeshika makali.... Mana hata mtoto wako humtaki tena"

    "ebu watoeni hapa... Sitaki kujua ni General au nani, peleka sero, kesho niwatolee habari kwa wananchi wangu"



    Basi mama sheby aliwahishwa hospitalini japo alikaa kwa muda kwasababu risasi haijaingia  sehemu mbaya sana katika mwili wake,...



    Sasa hivi leah anaishi kwa sheby ambaye ni sahi, mana tayari keshakuwa mchumba wake sasa,.. Lakini sasa alipofika nyumbani leah hamjui tena sahi, ila sauti ni sawa kasoro sura tu, mana sheby kavua lile lingozi alioshonwaga nalo usoni, sasa ana sura Original... Sheby aliingia na gari yake, ukumbuke geti linafunguka kwa remote control, sasa leah kwa furaha anatoka ndani na kwenda kumpokea baba watoto wake... Lakini alishangaa kuona mtu alioingia ni tofauti na mchumba wake anaemjua

    "we ni nani mwenzangu"

    Aliuliza leah huku akirudi nyuma, mana ni sura ngeni kwake

    "vp baba nanii yupo"

    Sasa leah aliposikia hio sauti ni ya sahi kweli lakini sura sio sahi tena,..

    "wewe ni nani"

    "mimi mdogo wake na sahi.... Sikia mi nataka nikuoe nitakumilikisha mali zangu, achana na sahi"

    Sheby alikuja na ka njia ka kumdanganya leah ili aone bado ana tamaa au kaacha,... Kweli mwanamke ataamkiwe umilikishwaji wa mali akatae? Sijui ni nani

    "ondoka zako apa,... Kwenda nitampigia simu huyo ndugu yako"

    Aliongea leah huku akishika simu kweli tayari kwa kupiga, kana kwamba hajakubaliana na maneno yake... Lakini leah alishangaa simu inaitia kwa huyo huyo mtu...

    "kivipi iitie kwako"

    "leah, acha presha.. Mimi sahi original, ile sura ilikuwa ni sura ya kazi, sasa huyu ndio mimi, kama huamini ngoja niivae hapa uone"

    Sahi kweli alilivaa lile lingozi na kumfanya leah kuamini

    "waaooo lakini mbona wewe ni hensam kuliko hata hilo lingozi"

    Aliongea leah huku wakiingia ndani







     





    Kesho yake sahi na leah wakiwa hospitalini, walimkuta mama kapata kaunafuu kidogo, haijapita muda msafara wa rais unafika hospitali hapo...

    "sahi si raisi yule"

    "ndio hana shida"

    "mmmmhh isije kuwa kuna jipu humu hospitalini"

    "hapana hatumbuagi hovyo pasina sababu"

    Sasa mke wa rais alipofika hapo, cha kwanza alimkimbilia sahi,..

    "mwanangu hujambo"

    "sijambo shkamoo mama"

    "marahaba baba hali yako"

    Aliongea mke wa raisi huku akimkagua shingo, mana jana ilitoka toka damu,... Sasa mama sheby aliopo kitandani, nae ana hamu ya kumuona mtoto wake,...

    Sasa sheby kumuona tu mama yake kaamka akamkimbilia

    "shkamoo mama, hali yako vp"

    "salama tu,.. Vp baba shingo yako imepona"

    Sasa mama sheby alipouliza hivyo, mke wa rais akadakia

    "nimeshamuuliza mtoto wangu kuhusu shingo yake, mfuate mtoto wako kule jamani wewe mama Joseph"

    Yaani huyu huyu mama Joseph ndio anamuita mwenzie mama Joseph, yaani kila mtu anamtaka sheby kuwa mtoto wake.... Hata mheshimiwa rais akaona hapa kuna utata, bora ukweli unge endelea kuwa siri...

    "hebu nyamazeni, nyie si marafiki toka zamani nyie? Sasa mnagombania nini... Wacheni ujinga"

    Aliongea rais huku sheby akiwa zaidi upande wa mama aliomzoea,...

    Hata leah anashangaa sheby ana wamama wawili, hajui nini sababu

    "huyu ni mtoto wangu"

    Aliongea mama sheby, huku mke wa rais nae akasema

    "mimi ndio mtoto wangu, kama huamini tumuite dokta aje"

    "mimi simtaki huyo dokta wako"

    "utamtaka tu hata kwa lazima"

    Sasa majibizano yakawa mengi sana hapo hospitalini,... Rais kavuta kibao na kumpiga mkewe

    "mke wangu angalia usije ukawa jipu, huyu mtoto kamzoea mama yake... Sawa huyo kijana ni mtoto wetu kwa ukweli unavyo dhihirisha, lakini nae ana uchaguzi wake... Mbona mimi sipigi kelele"

    "sawa mheshimiwa rais, lakini huyu ni mtoto wetu"

    "sawa najua, lakini hawawezi kuachana hao wameshazoeana"

    "baba sheby, uje nyumbani sawa baba"

    Aliongea mke wa rais huku wakiondoka... Sasa walipo ondoka leah akamuuliza sheby

    "we baby, ina maana una wamama wawili"

    "hapana, mama yangu ni huyu hapa"

    Leah alishindwa kuelewa kitu hapo.. Basi walitoka nje kwenda kumnunulia mama matunda,

    "sheby mpenzi wangu? wewe ni mtoto wa rais"

    "ndivyo inavyosemekana"

    Basi zoezi la kununua matunda sokoni liliendelea,... Lakini ghafla leah kawaona wale rafiki zake huku sokoni,... Leah kwa heshima akamwangalia sheby, kama vile anamuomba akawasalimie, sahi alimruhusu



    "heeee leah umekuwa wa tofauti siku mbili tu"

    "we acha tu jack,.. Mwenzio sasa hivi ni mchumba wa mtu"

    "weweeee muongo"

    "kweli"

    "afu yule mkaka jana tulimuona kwenye tv, tukasema nawe huenda tukakuona"

    "weeeee, Bado sijajulikana kwao, ila kwetu tayari"

    "mmmhhhh umefanya haraka nawe"

    "nampenda hata hivyo"

    "tunajua, mana toka siku ile ulikuwa unameza mateeee"

    "ni mtoto wa raisi yule, hivyo nina kibarua cha kumlinda"

    "Whaaaat, ati ni mtoto wa nani"

    "ina mana hujaskia au"

    "leah wewe umeokota dodo kwenye shamba la miwa leah"

    "bwana jack, baadae, spendi kumuuzi naombeni Niende, ila nawasihi sitaki tena muendeles na hio kazi, kuanzia leo... Nitamuomba mpenzi wangu anifungulie biashara yeyoye ile, nitakuwa nanyi pamoja.. Ila acheni hio kazi, na kuhusu kula niachieni mimi na kodi ya nyumba niachieni mimi, staki muende shivaz tena"

    "leah we nenda, sisi tumekuelewa... Nenda usije kuandikwa kwenye magazeti mke wa mtoto wa rais kakutana na machangudoa.. Nenda wewe, shilawadu hawakawiii"



    Hospitali wakiwa wanafikisha matunda ya mama, yena leah ndie aliokuwa akifanya kazi hio,..

    "sheby mwangu... Mbona hunitambulishi"

    Aliongea mama yake, kuwa mbona hamtambulishi huyo mschana

    "ahahahahaa mama bwana... Bado mapema mno, ila wacha ujue tu,... Anaitwa Leah"

    "najua mwanamke hana dini, lazima awe mkwe wangu huyu"

    Basi ilikuwa ni furaha, lakini ukweli ni kwamba mama yake sheby ni mke wa raisi, na baba yake ni raisi GU,.. Sema keshamzoea mama yake, na mama pia kamzoea mtoto wake hivyo kukubali tu kuwa sawa ni mtoto wa raisi, hapo ndipo mahali pagumu mno.... Hawezi, hivyo ataendelea kuishi na mama yake huyu lakini wazazi wake wa kweli wapo...



    Hospitalini Joseph anauguza miguu mana ilivunjwa kwa risasi, na akipona ni gerezani,.. Mr nyange yupo ndani ya kifungo cha maisha mana alikuwa akihujumu mali ya serikali na General mwenzie mr deo, hivyo wana kifungo cha maisha tena ikiwezekana kunyongwa kabisa..



    Dom imeshapelekwa Germany, tusubirie noti ya laki moja ya Tanzania..... Subira huvuta kheri shekhe... Tusubirini tu



    MWISHO WA SON OF PRESIDENT GU



    MWISHO

     

     

0 comments:

Post a Comment

Blog