Search This Blog

Thursday 24 November 2022

MKE JEURI - 1

 

     

     IMEANDIKWA NA : MOONBOY



    *********************************************************************************

    Chombezo : Mke Jeuri

    Sehemu Ya Kwanza (1)

     

    "we pumbavu wewe, nani mkeo... Yaani mimi ni mkeo mimi"

    Heeeee kumbe chidi alikuwa anaota

    "mamy,.. Mke wangu yupo wapi"

    "we mtoto ushakuwa chizi sasa, huyo mke we ulimuokota wapi"

    "mama.. Mimi nimeoa eti,.. Afu tukapigwa risasi"

    "hebu amka mi nataka niende supamaketi sasa hivi"

    "kwaio wataka nikupeleke au"

    "hapana... Usije ukaondoka"

    Aiseeee kumbe chidi alikuwa anaota, hakuwa na mke wala ndugu yake mke,.. Hakuna cha Mariamu wala Sarah,.. Mara ghafla mdogo wake wa kiume kaingia

    "kaka sheby, mpira umeanza twende"

    "nani na nani"

    "Man U na Arsenal"

    "ayaaaaa bonge la game hiloo ngoja naja"

    Kijana huyo aliamka na kwenda kuangalia mpira hapo sebuleni kwao, tena walikuwa ni matajiri haswa haswa... Tena haitwi Rashidi.. Anaitwa Sharbiny (Sheby).. Na mdogo wake aitwaye Rajabu...



    ENDELEA............



    Kijana sheby ni mtoto wa pili kwa mzee Rashidy, nq Rajabu ni mtoto wa tatu katika familia hio, lakini kuna dada yao ambae yeye bado yupo chuo akiendelea kujichukulisha shahada zake huko,.. Chidi yeye ni form four feliazi, na hakupenda kuendelea na masomo hayo,.. Mdogo wake rajabu nae yupo darasa la 5,.. Familia ya watoto watatu inakamilika, na Mwenyezi Mungu kaijaalia familia hio pesa za kutosha kwani wanafanya biashara nje ya nchi na hata ndani ya nchi,..



    Siku hio kijana sheby akiwa yupo nyumbani na mdogo wake wakiwa ni wapenzi wa mpira, yaani hawakutaka kupitwa na mechi kama hio kwa siku hio,.. Japo siku hio ilikuwa ni siku ya kazi lakini kijana huyo hakuenda kazini....

    "sasa wewe hizo ndoto za jioni jioni unazoota ni ndoto gani"

    Aliongea mama yake sheby huku akicheka kwa kumcheka mtoto wake







     





    JAMANI UKIKUTA MAHARI PAMEANDIKWA CHIDI BASI UJUE NI SHEBY, KWASABABU MWANDISHI ALIKUWA AKIANDIKA STORY YA MKE WA KAKA HIVYO KAZOEA KUANDIKA CHIDI BADALA YA  SHEBY.. HIVYO UKIONA CHIDI, FANYA KUICHUKULIA KAMA SHEBY VILE..... USIJE UKAANZA MASWALI YAKO... OOHHH MBONA NI CHIDI TENAAA SJUI NINIII.. AH AH... MUELEWE HILO KIJANA ATAITWA SHEBY.. UKIONA CHIDI IMEKOSEWA HIOOOOOO



    "mama hio ndoto hata mimi siielewi eti"

    Aliongea sheby huku wakizidi kuangalia mpira,,

    "hhmm haya mi naenda supamaketi mara moja"

    "lakini mama, kwanini nisiende mimi huko"

    "we si unaangalia mpira hapo"

    "aahh mama.. Ina maana kuangalia mpira na kukuseidia kipi bora"

    "aahhhh haya bwana nenda.. Ila angalia vitu muhimu, mana toka jana mungesema ningeleta"

    "usijali mama"

    "sasa una pesa"

    "ndio mama... Nitakosaje pesa"

    "haya safari njema"

    Basi sheby alitoka hapo na kuingia kwenye paking kuangalia gari ya kuondoka nayo kwa siku hio.. Palikuwa na gari kama tano hivi za bei ya kutisha..

    "kaka nami naenda"

    Alikuwa ni rajabu akimwomba kaka yake waende wote supamaketi,..



    Wakiwa barabarani kuelekea supamaketi, walifika mahari kuna jamu ya magari, hivyo kulazimika kutulia katika laini kama walivyo wengine,.. Lakini sheby kupiga macho pembeni aliona mschana mzuuri sana, lakini huezi amini alikuwa ni kipofu,.. Dada huyo alikuwa na umbo la kipekee sana alikuwa na sura ya kipeke, hata rangi yake ilikuwa ya weusi wa asili, yaani ile rangi ya chocolate,.. Sheby aliona huruma kuona yule dada kaketi juani na kibakuli chake cha kuombea pesa, sheby alijisachi mfukoni ili ampe rajabu ampelekeee, na hapo wapo kwenye foleni ya mataa,..

    "raja, hebu kampe hii elfu kumi yule dada pale"

    Alimwambia mdogo wake hivyo, lakinu kabla raja hajatoka mataa yaliruhusu hivyo akashindwa kufanikisha lengo,..



    NAKUMATI ndio supermarket alioingia kijana sheby, yeye na mdogo wake waliingia ndani na kuanza kukusanya vitu wavitakavyo, walichukuwa muda mrefu sana..

    "kaka...kaka"

    Aliita rajabu huku akimuonyeshea kaka yake kitu fulani

    "nini wewe"

    "ona yule dada uliotaka kumpa pesa si yule pale"

    Kweli yule kipofu alikua akionekana eneo hilo, ikabidi sheby amsogelee ili amuone vizuri,.. Lakini huyo alikuwa kama vile ni mweupe mweupe hivi na yule kule, rangi yake ni ya chocolate rangi nzuri sana kwa wasichana wazuri,...

    "mambo"

    Sheby alikuwa na heshma sana lakini alikuwa mchokozi afu akisha chokoza anashindwa kumalizia,...

    "poa"

    Aliitikia dada huyo lakini ni kwa nyodo sana mana nae yupo ndani ya supamaketi akichagua vyakwake

    "umefika huku"

    "kwani we uliniona wapi"

    Alijibu dada huyo huku akiendelea kuchagua vitu katika shelfu la mapilipili,

    Sheby alikuwa hapendi kujibiwa hovyo hovyo,.. Aliachana nae mana hakuwa akijibu vizuri, yaani alikuwa akijiskia sana



    Basi walimaliza na kuja pale kaunta kisha wakapigiwa mahesabu ya vitu walivyochukuwa...

    "ni laki tatu na arobaini"

    Aliingea mhudumu huyo, huku sheby akitoa pesa kwenye waleti,.. Ghafla yule dada kafika hapo na kupigiwa hesabu ya vitu vyake,..

    "ni laki moja na nusu dada"

    Aliongea huyo mhudumu kwa kumtaarifu huyo dada kiburi

    "heeeeeee we dada... Mbona vitu vichache afu pesa kubwa"

    "kwani we ulitaka vya shilingi ngapi"

    "mimi nilikuwa na elfu 50 tu"

    "sasa elfu 50 unakusanya tenga zima, au ulijua ni sokoni hapa"

    Mhudumu nae hakutaka kumchelewesha kumpa makavu,.. Sheby alifurahi sana kuskia nae anajibiwa vibaya... Basi sheby yeye hakutaka kuwa mbea, aliondoka zake na mizigo zao...



    Lakini walipofika yale maeneo waliomuona yule kipofu walishangaa sana kumkuta pale,.. Kana kwamba yule kule supamaketi sie,.. Au huenda akawa ndie ila Anachezea watu,..

    Sheby aliweka gari pembeni, mana toka mwanzo alitamani sana kumseidia dada huyo, yaani alitamani kumpa pesa kama wengine wanavyotoa, na sababu ya kuweka gari pembeni ni kujua kuwa, mbona kamuona kule supamaketi..



    "habari yako dada"

    "safi shkamoo"

    Alisalimia dada huyo, lakini ni kwasababu haoni, kwani laiti kama angelikuwa anaona basi asingesalimia shikamoo, lakini sheby kumuangalia vizuri aligundua huyu sio yule aliomuona supamaketi, ila wanafanana kwa kila kitu

    "marahaba... Aaahh Samahani dada kama vile nilikuona pale supamaketi, ila nimeshangaa sana kukuona hapa"

    Sasa swali la sheby liligeuka kuwa kilio kwa dada huyo



    SASA HAPA NAKUPA STORY MBILI KWA MOJA.... NAKUPA KIPANDE CHA KABLA YA KUWA KIPOFU HUYU DADA, AFU TUNARUDI HUKU KWENYE STORY YENYEWE...



    Ikiwa ni familia ya watoto watatu, ila wote walikuwa wakike tupu,... Akianza na dada yao aitwae Rehema aliozaliwa peke yake yaani sio mapacha,.. Na uzao wa pili ni wa hawa mapacha ambae mmoja wapo ni yule kipofu,...

    Watoto hao walizaliwa mapacha na wapewa majina ya ZAITUNI NA ZAINABU, watoto wote walikuwa kwa upendo kutoka kwa wazazi wao, lakini upendo wao ulikuja kuvurugika baada ya kuwa wasichana wakubwa walioitaka kuolewa,...

    Sasa ZAINABU akiwa na rafiki zake maeneo ya nyumbani kwao na familia hio ilikuwa ni ya hali ya chini sana hivyo wazazi wao walitamani sana watoto wao waolewe mapema kwasababu hali ya maisha ilikuwa sio nzuri.. Hivyo kwakuwa watoto wa kike walishakuwa walitaka waolewe ili wakaishi na waume zao... Lakini zainabu alikuwa ni mschana ambae hajatulia hivyo wanaume wengi walikuwa wakipita tu,... Yaani tabia za mapacha hawa zilitofautiana,.. Zaituni alikuwa mpole mpenda dini, lakini zainabu amekuwa mtoto wa mjini yeye na disco yeye na wanaume japo ni kwa siri sana,... Zainabu akiwa na rafiki zake maeneo ya nyumbani kwao wakiwa wanapunga upepo katika mti uliopo hapo kwao...



    Haikupita muda zaituni alipita akiwa anatoka msikitini,...

    "hhhhh ostadhati huyo umemuona"

    Aliongea zainabu kumwambia rafiki yake alioko nae hapo

    "ila we zai, mdogo wako mbona anapenda dini lakini wewe hhhmm"

    "heeeee shost,.. Kila mtu na mambo yake bwana"

    Alijibu zai huku akibinua mdomo kwa dharau, wakati huo zaituni alikuwa anaona vizuri sana...  Lakini chuki alizonazo zainabu ni kuwa posa zilizokuwa zinakuja zilikuwa ni za kumhusu zaituni, na ndio maana zainabu alikuwa na chuki na pacha mwenzake,.. Tena zaituni alikuwa akiletewa poza na watu wa heshima, lakini zainabu yeye hakiwa na posa wala nini, japo walikuwa wamefanana sana lakini tabia zao ndizo zilizowatambulisha wanaume kuwa huyu ndio anafaa na huyu hafai,

    "lakini zai, ina maana mpaka sasa wewe hujapata posa"

    "hhhhmmm shost, posa itoke wapi na wakati hilo kahaba lipo, naona kila anaekuja tu anaulizia zaituni, najipendekeza lakini wapi analetewa yeye tu, afu mbaya zaidi anazikataa"

    "heeeeeeee, anakataaa??... Kwanini"

    "eti anasema yeye bado wakati wa kuolewa, na wakati mama kasema kila mtu atafute mchumba wake aolewe"

    Aliongea zainabu huku akimuona ndugu yake kuwa kama gundu juu yake,

    "lakini zai, kwani hao watu wanaokuja wengi wao wakoje"

    "ni Waislamu tupu"

    "sasa huoni upo tofauti nae,.. Wewe ni muislamu lakini huta itikadi hio, hivyo tafuta wale ambao ni taipu yako"

    "sawa lakini hata hao nilio nao, pia nikimwambia swala la kuoana wanabaki kunichezea tu, ila zaituni analetewa posa tena kwa heshima ya hali ya juu"

    "Nikwambie kitu shost..... Badilika dada"

    "kivipi we ney"

    "sikiliza, ukishajua kuwa gari yako ni ya petroli, basi anza kuwa rafiki na muuza petroli"

    "una maana gani lakini"

    "kuwa kama mdogo wako"

    "aahhhhhh mi nashindwa kutwa kushinda msikitini yaani siwezi... Ila ili wanione kama yeye lazima nifanye kitu"

    Aliongea zainabu huku akipiga chini kwa hasira

    "ufanye kitu gani"

    Aliuliza neema ambae ni rafiki yake na zainabu,....

    "mpaka sasa hivi mdogo wangu zaituni ndio anapendwa kuliko hata mimi, yaani lazima nimfanyizie"

    Hata neema aliogopa sana huku akiwa kafumba mdomo, kana kwamba zainabu alikuwa katili wa kutisha

    "zai, unataka umuue ndugu yako"

    "simuuwi wala nini... Ila chamoto atakiona"

    "mungu wangu zai sio vizuri lakini.. Kumbuka ni pacha wako huyo"

    "pacha anaenifanya nikose raha mjini, nani kasema??.... Nakwambia nakupa siku tatu tu.. Na iwe siri yako wewe na mimi tu.. Utakula vingi kama utakuwa msiri"

    Aliongea zainabu na kumfanya neema kuwa na wasiwasi juu ya maneno hayo, ila neema hakuonekana kuridhika na kitu anachotaka kukifanya zainabu...







    Zainabu na zaituni ni mapacha waliozaliwa tumbo moja, baba mmoja mama mmoja, ila tabia zao zilikuwa tofauti tofauti sana ukilinganisha na mapacha wengine ambao asilimia kubwa hua hawaachani katika upande wa tabia, lakini kwa zainabu na zaituni wamekuwa wakiishi kwa kuchukiana,



    Tabia njema ndio iliomfanya zaituni kuwa kipofu hadi hii leo,...

    "pacha anaenifanya nikose raha mjini, nani kasema??.... Nakwambia nakupa siku tatu tu.. Na iwe siri yako wewe na mimi tu.. Utakula vingi kama utakuwa msiri"

    "lakini zainabu, kumbuka akipata ndugu yako nawe umepata, wacha aolewe tu"

    "skia neema,.. Tuyaache hayo, hebu nionyeshe dula linalouza tindikali ni lipi"

    Neema kuskia hivyo alishtuka huku akiziba mdomo kuashiria kuwa jambo hilo sio zuri kabisa kumfanyia mwenzio hivyo

    "zai unataka kufanya nini"

    "nataka asione, afu nione hao viherehere kama watakuja tena"

    Aliongea zainabu huku akiamka kutika kwenye kiti alichokalia,

    "lakini zai sio vizuri hivyo"

    "we nawe kama hutaki uniambie, mi staki mtu mnafki bwana"

    "kiukweli sijui duka lolote linalouza hicho kitu na hata kama ningelikuwa nalijua nisingekuonyesha hata chembe"

    Neema aliongea huku akiondoka zake huku zai akimuita

    "ney sasa unakwenda wapi"

    "sitaki kushiriki unachotaka"

    Kitendo hicho kilimfanya neema akae pembeni kabisa,...

    Zainabu alifanya jambo hilo peke yake pasina kushirikiana na mtu yeyote yule,...



    Baada ya siku kadhaa kupita, siku moja zaituni akiwa anatoka madrasa kupata elimu ya dini yake, ikiwa ni mida ya saa 12 hivi jioni sana na kagiza ka saa moja kalikuwa kakianza hivi,...

    Wakati huo zainabu akiwa kajificha katika kona moja hivi, maskini ya mungu zaituni akiwa hajui hili wala lile, anajikuta anamwagiwa tindikali ya usoni,.. Uzuri wa tindikali hio haikuwa ya kuchubua ngozi bali ilikuwa ni spesho kwa macho tu, mana kuna ya kuchubua ngozi na macho pia, lakini kuna ya macho peke yake,... Zaituni alihisi kamwagiwa maji machafu mana harufu hio ilikuwa ikiendana na maji ya ukoko hivi,..

    "sasa tuone hao vimbalala vyako kama vutakupenda tena"

    Aliisikia hio sauti lakini hakumuona mtu tena,.. Na uzuri ni kwamba sauti hio anaijui ni ya dada yake ambae ni kulwa na yeye ni doto, hivyo ni dada yake,.. Sasa baada ya dakika 5 zaituni kufumbua macho alijikuta haoni kabisa, yaani hapo hapo alipo ni hapo hapo... Mpaka wasamaria wema walipotokea na kumchukuwa kisha kumpeleka hospitalini,



    Badaktari bigwa wa macho walifanya kila liwezekanalo zaituni aweze kupona, walishindwa na kusema macho hayo yameharibika sana hivyo kwa hapa Tanzania bado hawana uwezo wa kulitibu tatizo hilo, kwani waliambiwa kuwa tatizo hilo labda waende nje ya nchi... Sasa nje ya nchi na hali ya familia hio itaweza wapi,..



    Wakati huo huku kwa zainabu akiwa na rafiki yake neema, alikuwa akichekelea sana kutokana na swala hilo

    "tayari siku nyingi mtu haoni"

    "lakini zai hivyo sio vizuri wewe"

    "sasa nataka nianze kuwa kama yeye,.. Natamani kuolewa sana neema"

    "kuwa kama yeye... Yaani uwe swala tano"

    "ndio"

    "huezi... Yaani huezi nakuapia huezi"

    "nitajaribu nikishindwa basi.. Lakini staki kuona vijidume wanakuja kwa ajili ya zaituni"

    Zainabu alikuwa akijiskia raha sana kwa kitendo alichokifanya kwa ndugu yake,

    Sasa kuanzia siku hio hakuna aliokuja nyumbani kwa ajili ya zaituni yaani ile sifa ya kuletwa kwa posa ikawa haipo tena,.. Zaituni alipotoka hospitli akiwa kapewa miwani maalum na kifimbo kwa ajili ya kumseidia matembzi,... Atafanya kazi gani familia yao yenyewe ina hali duni sana,.. Aliona bora we omba kama watu wengine,... Lakini licha ya  zainabu kumfanyia ndugu yake hivyo ili apate kuolewa yeye na sifa nyingi za kifamilia zimdondokee yeye.. Huezi amini mpaka leo hii hajaolewa wala kuchumbiwa tena ndio kwanzaa anatanga na njia, yaani kwa sasa kawa malaya wa kutupwa,...







     





    SASA TURUDI KWENYE SIMULIZI YETU, MANA HIO ILIKUWA NI STORY KABLA YA UPOFU WA ZAITUNI



    Sheby akiwa bado kasimama na dada huyo huku akilia sana kwa kutajiwa kuwa amekutana na mtu anafanana nae sana, ambae amemkuta supamaketi,...

    "mbona unalia dada, kwani yule na wewe mpoje"

    "ni stori ndefu sana kaka yangu"

    Aliongea dada huyo ambaye bado hajajitambulisha kwa kijana sheby..

    "pole sana dada yangu"

    Lakini muda huo huo kuna mama alitokea eneo hilo..

    "hujambo baba"

    Alisalimia mama huyo huku kama anataka kuondoka na yule dada,

    "sijambo shikamoo mama"

    "marahaba..... Zai mwanangu kumekuchwa twende nyumbani"

    Maskini kumbe yule aliokuja kumchukuwa alikuwa ni mama yake mzazi, tena hata mama yake alikuwa akilia kwa uchungu kutokana na hali aliofanyiwa mtoto wake,.. Na ndio aliokuwa akimpenda kuliko wote

    "mama, kwani ni saa ngapi sasa hivi"

    Aliuliza zaituni huku machozi yakimtoka, huezi amini hata sheby hakuweza kuvumilia, alitokwa na machozi mana ilikuwa inauma sana,..

    "mwanangu ni saa kumi na mbili hii giza linaanza"

    Zai hata muda unavyokwenda hajui, yapata miaka mitatu au minne toka afanyiwe unyama huo na dada yake,.

    "sawa mama twende"

    "leo umepata shing ngapi"

    Mama huyo alimuuliza mtoto wake mana hakuna mtu anajua pesa kama kipofu, yaani ukimpa noti yeyote akiifikicha tu lazima ajue hii ni shilingi ngapi, mana bila kuwa hivyo hatojua pesa anayopewa na wasamaria wema... Hivyo ni mjuaji wa pesa kuliko kitu chochote kile

    "leo nimepata elfu tano tu mama"

    Aliongea zaituni huku mama akifurahi kwa kiasi alichokipata mtoto wake...

    Sheby aliwaza kuwa yaani yeye katoka kulipia vitu vya laki tatu na arobaini, kumbe huku kuna watu wanasherehekea kupatikana kwa elfu 5 tu,... Chidi hajaamni macho yake,... Sasa mama akawa anamchukuwa mtoto wake ili kwenda nyumbani, mana anamleta asubuhi aombeeee afu jioni anakuja kumchukuwa,..

    "Samahani mama angu"

    Aliongea sheby huku akiwasimamisha, mama na mtoto wake

    "bila Samahani mwanagu"

    Alijibu mama huyo huku akigeuka..

    "mama ni nani huyo unaemuita mwanangu"

    Aliuliza zaituni kuwa ni nani aliomuita mwanae...

    "ni yule kijana uliokuwa nae saa ile"

    "haaaa kwani alikuwa bado hajaondoka"

    "ndio"

    Sheby aliwafuata wawili hao huku akitoa waleti na kutoa noti tano za shilingi elfu kumi kumi... Yaani jumla ni shilingi elfu 50,...

    "itawaseidia hiii"

    Sasa zaituni kuskia neno itawaseidia hii alimuuliza mama yake kiwa kijana huyo katoa shilingi ngapi

    "mama... Katoa shing ngapi huyo kaka"

    Sasa mama kabla hajasema, sheby akamnyamazisha na kumwambia katika skio kuwa

    "mwambie nimetoa elfu tano tu"

    Mama alishangaa kwanini kijana katoa elfu hamsini, lakini anataka amwambie zai kuwa imetolewa elfu tano tu

    "mama niambie katoa shilingi ngapi"

    "katoa elfu tano mwanagu"

    "ooohhh mwenyezi mungu akujaalie wewe kaka... Nakuombea ufanikiwe kaka angu"

    "ahsante dada"

    "baba tunashukuru mwanangu"

    "usijali mama"

    Sasa zai kasikia pafyumu nzuri ya sheby...

    "mama huyo kaka ndio mwenye huo mnukio"

    Sheby akawahi kumwambia mama yake kuwa amwambie sio yeye kuna mtu kapita tu...

    "hapana mwanangu kuna mtu kapita tu"

    Sasa mama anazidi kujiuliza mbona huyu kaka hataki ajulikane kwa zaituni.... Mama alikuwa hapati jibu kwa kijana huyo...

    "mama sasa hivi tuna elfu kumi si ndio eee"

    Zaituni aliongea hivyo huku akitabasamu vizuri sana...

    Yaani shilingi elfu tano tu katoa shukrani yote hio, sasa kama kajua ni elfu hamsini ingelikuwaje...  Basi mama huyo na mtoto wake walikuwa wakiondoka lakini mama alikuwa kama ana maswali mengi sana kwa kijana sheby, mana kila anachotaka kujua mtoto wake, sheby hataki ajue sasa sijui alikuwa na maana gani..



    Ikiwa ni mida ya saa 12 na dakika 45 sheby na mdogo wake wakiwa ndani ya gari kuelekea nyumbani,.... Akili ya sheby ilikuwa ipo kwa Zaituni tu, yaani Zaituni aliumbika yaani ni bonge la toto sio la kispoti spoti,...



    Dakika chache yeye na mdogo wake walifika nyumbani,

    "sheby mbona umechelewa hivyo lakini"

    Aliongea mama yake sheby huku baba yake akiwa yupo hapo sebuleni,

    "aahh mama, gari ilikuwa inasumbua kidogo, lakini hakuna shida mama"

    "hofu juu yako lazima niwe nayo mwanangu"

    "sawa basi nisamehe"

    Lakini ghafla simu ya baba yake inaita,...

    "eeehh halo mr magesh habari yako"

    Ni baba yake na sheby wakiwa wanaongea biashara na mfanyabiashara mwenzake aliopo india, na sheby anamjua mtu huyo

    "nzuri tu mr rashidi hali yako huko Tanzania"

    "aahhh huku swalama tu magesh"

    "sasa... Nina mzigo unatakiwa uende kongo,.. Ila utatakiwa uje india ili uueskoti mpaka huko"

    "aahhhh sawa kabisa,... Nitafanya hivyo"

    Sasa sheby kusikia ishu za india alijiskia raha sana mana anakuoenda sana huko,...

    "aaahhh sasa ngoja niweke mambo sawa, kisha nitakupa mwongozo"

    "sawa mr magesh"

    Sasa simu ilipokatwa tu sheby kadakia juu kwa juu,...

    "shikamoo mzee"

    "marahaba vp"

    "safi tu... Naskia kuna ishu ya kwenda india"

    "ndio, ila hio huiwezi we zako za kenya uganda, huko niachie mimi"

    Aliongea mzee huyo huku akiendelea kuangalia tv, lakini ghafla mama sheby anaingilia kati

    "lakini baba sheby, kwani mtoto akijua na huko kuna shida gani"

    "yes mamiii hebu mwambie baba... Kama vipi nitume nikauchukuwe huo mzigo"

    "wewe sheby huezi.. Ni mizigo ya thamani sana huko huezi wewee utahari kazi.. Nitakwenda mwenyewe"

    "babaaa, nipe nafasi hio moja tu basi yaani hio tu"

    "kwanza ulishawahi kwenda india wewe"

    "si tulishaendaga wote"

    "nasemea peke yako"

    "aahhhh peke yangu sijawahi kwenda"

    "sasa je"

    Sheby alikuwa anaitaka sana hio safari ya india na sijui ana ishu gani na huko

    "baba.... Niamini mi mtoto wako nitume niende huko..nitafanya vizuri"

    "mama sheby... Huyu mtoto mbona hanielewi... Hebu mwambie basi mwanao"

    "lakini Baba sheby naomba nikuulize swali moja tu... Baada ya wewe nani atamiliki hizi mali"

    "si hili jinga"

    "heeeeeeee kawa jinga tena"

    "ndio.... Leo nimeangalia kwenye akaunti ya kampuni, imepungua milioni 15, kazipeleka wapi? Leo nije nimuachie kazi kubwa kiasi hicho.. Hapana Siwezi"









    Baba yake sheby alikuwa ana hasira sana juu ya jambo hilo la sheby kuchukuwa milioni 15 bila idhini ya baba yake,.. Sheby alishangaa sana kuskia kuwa kachukuwa milioni 15 kwenye akaunti ya kampuni yao,..

    "mzee, si ulisema ile pesa nimpelekee mzee magese"

    "sasa kama umempelekea mbona kanidai tena na nimempa, kwanini asiseme kuwa ulishampa... Sheby staki ujinga na pesa eti"

    "mzee, kama huamini ebu tumpigie"

    "ngoja nimpigie mimi... Staki ujinga na pesa mimi, Alaaaa"

    Baba yake sheby alichukuwa simu yake na kupiga simu kwa mzee magese, simu iliita na hatmae inapokelewa

    "halo mr magese habari yako"

    "salama mr rashidi.... Sasa kumbe kijana wako alishanitumia ile pesa ila sikujua na hata sasa hivi nilikuwa nikkupigie baada ya kutoka kuoga"

    "aahaaa nami ndio niliokuwa nakupigia"

    "hakuna shida, nimeshairudisha kwenye akaunti yako"

    "ok Ahsante mr magese"

    Walimaliza maongezi yao kisha baba yake sheby akamgeukia mtoto wake,

    "una bahati sana... Mana naijua akili yako inawaza starehe tu"

    Alionge mzee rashidi huku akiwa anatabasamu kwa mbali,...

    "sasa nichukue pesa yote hio yanini"

    "basi yaishe.... nilijua umechukua"

    "ok... Sasa mzee, vipi nitaenda mimi au"

    "hebu ngoja kwanza, tutajua hio siku ikifika"

    Aliongea baba yake sheby huku akiendelea kuangalia tv kwa umakini wa hali ya juu mno,... Ikiwa ni mida ya saa 2 usiku sheby akiwa chumbani kwake ghafla mlango wake unagongwa, alikuwa ni mfanyakazi wa ndani ndio kaja..

    "kaka chakula tayari"

    Aliongea dada huyo huku sheby akiamka kutoka kitandani mana alikuwa kajipumzisha baada ya kurudi supamaketi....

    "sawa nakuja"

    Alijibu kijana huyo na kumfanya dada huyo aondoke baada ya kujibiwa kuwa anakuja

    "afu Samahani Jacqueline"

    Alimsimamisha dada huyo kana kwamba kuna kitu alitaka kuongea nae

    "abee kaka"

    Aliitika jack huku akiwa anafikicha mikono yake

    "hivi mbona kila ukija chumbani kwangu huji kiheshima"

    "kakaaaaaa"

    Jack aliita huku macho yake kama yakumtega sheby,... Na hapo alipo kavaa gauni refu afu jepesiiiiii, ambalo lilionyesha nguo ya ndani kutokana na uwepesi wa gauni hilo,.. Jack alikuwa akimpenda sana mtoto wa boss wake, lakini ile hali ya kuongea ndio anashindwa na ndio maana wanawake wengi huishia kutaamka kwa vitendo tu, mana akiongea ataonekana malaya, hivyo vitendo ndio kila kitu kwao..

    "jack, spendi hii tabia, naomba usifanye hivi tena"

    Sheby aliongea huku mkono wake wa kushoto upo mfukoni, kana kwamba Zakaria au babu juma kasimama baada ya kumuona jack... Hivyo kaingiza mkono mfukoni ili kumseti akae vizuri,

    "sawa kaka"

    Jack aliondoka lakini ni kwa mwendo wa kumsumbua mtoto wa kiume, sheby alifumba macho,.. Maana ndembetembe sio ndembetembe, tepetepe sio tepetepe,.. Sheby kabaki kushika kichwa huku macho akiwa kayafumba,..



    Baada ya siku kadhaa kupita na leo ni siku nyingine tena sheby akiwa zake ofisini kwake akiendelea kuandika baadhi ya karatasi za kikazi,

    Ghafla simu ya mezani inaita

    "halooo"

    "sheby njoo ofisini kwangu"

    Alikuwa ni baba yake ndie aliemuita mana mtoto ana ofisi yake na baba ana ofisi yake, ila jengo ni moja na kampuni ni moja, sheby alitoka ofisini kwa na kwenda kwa baba yake,..

    "ndio mzee"

    Alifika kijana sheby na kumsikiliza baba yake amemwitia nini

    "kuna wasichana wawili hujawaona hapo reception"

    "aahhh sijawaona.. Kwani wananidai nini, au wamesema nimewaita"

    Sheby alianza kuongea mambo tofauti tofauti, mana anajua hii hali ilishawahi kutokea kwa msichana mmoja aliekuja hapa hapa ofisini na kusema kaja kwasababu ya Sharbiny (sheby) na hakupewa ahadi ya kuja hapo lakini kaja sasa na leo wamekuja wawili sheby akaanza kuruka mapemaaa kabla hajajua kama wasichana hao wamemfuata yeye au..

    "mbona una haraka hivyo.. Kwani hawa wanawake wamekufanya nini wewe, mbona kama hupendi wanawake"

    "mzee, mimi sipendi kuharibu CV zangu kwako.. Mana nikiwa mchakaramu hutoniamini tena"

    "ni sawa, lakini unaonekana unawachukia sana"

    "mzee tuyaache hayo, hebu niambie hao wasichana wamesemaje kuhusu mimi"

    "hawakusema lolote kuhusu wewe, na wala hawakujui wala huwajui... Ila wameomba kazi, lakini sina muda wa kukagua vyeti vyao, hivyo nimewaambia wasubiri kwanza hapo reception kisha nitawaita"

    "ok nipe nikazikague kule ofisini kwangu"

    Sheby alichukua vile vyeti na kutoka navyo mpaka ofisini kwake,..







     





    Alianza kukagua cheti kimoja baada ya kingine, na cheti alichokishika kiliandikwa jina la MARRY JOHN KISUI... Alikuwa ni msichana mwenye miaka 22 mzaliwa wa jijini Dar es Salaam lakini kahamia jijini Arusha,.. Elimu yake ni kidato cha nne, lakini alionekana kufaulu ila huenda ugumu wa fedha ndio uliomkwamisha hivyo ndio mana alikuja kuomba kazi...

    Alipomaliza kukikagua chote kisha akakifuata na kile cheti cha pili, alikifuatilia kwa umakini kwa kukisoma vizuri, jina lake aliitwa ROSE EMMANUEL HAULE mwenye umri wa miaka 24 nae alizaliwa jijini Dar es Salaam na kuhamia arusha, elimu yake ni kidato cha sita na alifaulu vizuri...



    Baada ya kuvipitia vyeti vyote kwa umakini wa hali ya juu, sheby alinyanyua simu ya mezani na kumpigia Secretary..

    "walete hao wasichana"

    "sawa boss"

    Baada ya dakika kadhaa mlango uligongwa na kuingia ndani, walikuwa ni wasichana wazuri, wadada na maumbo yao, binafsi wao walihisi kupata kazi popote kutokna na uzuri wao,...

    "boss, ni hawa hapa"

    "ok unaweza kwenda kuendelea na kazi"

    Aliongea sheby kumuamuru Secretary aondoke akaendelee na kazi

    "rose ni nani hapa"

    Aliuliza kijana sheby huku akiwaangalia kwa umakini sana....

    "mimi apa boss"

    Alijionyesha dada huyo huku mioyo yao ikiwaenda mbio, kwa kuhofia kukosa kazi...

    "ok wewe rose kaa pale"

    "sawa boss"

    "na weweeee, nani vileeeee..... Marry"

    "abee boss"

    "mbona unaonekana imefaulu lakini umeishia elimu ya chini"

    "hali ya kulipia kalo ilikuwa ngumu boss"

    Aliongea marry tena kwa huzuni sana, lakini sheby yeye hakuwa mtu wa kuangalia mtu usoni, hua anafanyakazi kiufasaha kabisa,...

    "okeee... Sasa wewe rose, unajua kutumia kompyuta vizuri"

    "ndio.. Ila sijasomea kazi zake.. Yaani mifumo yenu ya hapa siijui"

    "wewe unaitumia kwa mfumo gani"

    "mimi natumia mfumo wa maintenance"

    "Prog Excel ulishawahi kuisomea"

    "hapana boss sijawahi"

    "mungu wangu weeeee... Sasa itakuwaje"

    Aliongea sheby huku akikuna kichwa, na akiangalia kwenye kampuni yao kuna nafasi mbili kama jinsi walivyo, ila sasa elimu zao zilikuwa ni za chini sana, na mbaya zaidi hawakusomea programu yeyote ile,...

    Marry alianza kuwa na wasiwasi juu ya kupata kazi, mana kama rafiki yake rose tu ni form six lakini anakutana na maswali ambayo hata huyo marry hayajui hata kidogo, tena kama hio Prog Excel ndio kwanza hata haijui, na kampuni ya akina sheby ni kampuni kubwa sana jijini hapo yaani ni kampuni ya usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya nchi na hata ndani ya nchi katika mikoa mbalimbali,..

    "kiukweli vyeti vyenu haviwezi kuwapatia kazi,.. Na mbaya zaidi hamuna hata Experience ya Prog yeyote ile,.. Mi nadhani sina kosa mpaka hapo, mana nilitaka niachane na hivi vyeti nihamie kwenye uzoefu, lakini hata uzoefu wenyewe hamuna"

    Aliongea kijana sheby huku akivikusanya vyeti vyao, kana kwamba aliwataka waondoke tu,..

    "boss, tuseidie.. Tuna shida na kazi"

    "kweli tuna nafasi mbili kama mlivyo, lakini nafasi hizo hamuziwezi kwasababu zinahiraji elimu ya kutosha, mbali na elimu bado mlitakiwa kuwa na Experience ya kazi hizo"

    "ni sawa, lakini boss, je tungesoma Experience ngapi ili kila mahari tupate kazi,.. Na hizo gharama za kusoma hivyo tungelitoa wapi kama hata elimu ya kawaida ilitushinda kutokana na hali za familia zetu"

    Sheby akisikia jambo la familia hua anajiskia huruma sana lakini haikuwa na jinsi,. .

    "tena bora hata wewe una form six nzuri tu, lakini sasa huyu mwenzio huyu, aisee sina mpango nae kabisa.. Yaani asitegemeee... Kwa wewe rose, hebu njoo kesho tujue cha kufanya lakini jua kuwa ni asilimia 50 za kupata na 50 za kukosa"

    Sheby aliongea hivyo kisha akatoka kuelekea uwani, na tayari keshawapa ukweli wao.... Mary alianza kulia kwa kukosa kazi,.. Wakati huo sheby kaelekea uwani

    "mary, lakini hata mimi sina uhakika, tena bira hapa tumepokelewa vyeti, kuliko huko tulipopita hata kuonyesha vyeti tu hawataki"

    "kama ni kukosa wacha nikose... Lakini mimi nikafanye kazi kiwandani kweli,.. Siamini kweli"

    Mary alilalamika sana kuwa yaani yeye akafanye kazi kiwandani, mana kakosa kazi karibia ni kampuni ya tatu hio, .

    "sikiliza mary,.. Kwa sasa hebu tuyaache maisha ya kuigiza, tulikuwa tunavaa nguo za maana lakini hazikuwa zakwetu,.. Nguo za mwana ndio zilizokuwa zikituonyesha kuwa sisi ni wasichana wa kitajiri,... Lakini sasa tuyaache hayo tufanye kazi"

    "rose.. Ni kweli kabisa lakini"

    "lakini nini??.... Sasa skia mary, mimi naondoka ila wewe baki hapa hapa.. Fanya juu chini mpaka akubali, wewe ni mwanamke bwana utashindwaje kutumia umwanamke wako"

    "rose,... una maana gani kusema hivyo"

    "usijifanye hujui mary, tuachane na kazi za kuigiza kuonekana matawi kumbe tunalingia nguo zawatu"

    "lakini sijakuelewa rose"

    "sikiliza... Hata ukimpa haondoki nacho, kikubwa upate kazi tu"

    Aliongea rose kumshawishi mwenzie kuwa ajirahisishe kwa sheby ili apate kazi

    "basi usiondoke rose.. Nijitahidi kufanya hivyo, lakini ni ngumu kwangu"

    "jitahidi tuuuu"

    Basi rose aliondoka na kumuacha mary pale ndanu ili sheby akija akutane na vimbwanga vya dada huyo,.. Haikupita muda sheby karudi, na rose yeye yupo pale reception anamsubiria rafiki yake amtege mtu huko ndani...

    "heeeeee bado hamjaondoka tu"

    Aliongea sheby huku akikaa kwenye kiti

    "boss, nina shida na kazi"

    Mary aliongea hivyo lakini kila akitaka kubinua matiti yake yatoke nje, anashindwa kufanya hivyo mana sio kawaida yake,.. Alichokiweza ni kulegeza macho tu peke yake, huku akijitahidi kupandisha suruali..

    "Bosiiiiiiiiii.... Nina familia kubwa, mama yangu anaumwa, nategemewa na familia yangu boss, nisaidie kupata kazi tu, na sio lazima iwe hapa, ila kampuni yeyote ile lakini uniseidie"

    Sasa chidi huruma ilimjia baada ya kusikia mambo ya familia,... Lakini kila akimuangalia mary anakuta kuna action anaziona zinaanza kufanyika..



    "huyu mtoto wa kike anata kazi, na ni kweli ana shida ya kazi lakini mbona anaonekana kunitega kimapenzi hivi..... Hebu ngoja nami nimtanie kama vile nimetegeka, ili nijua kuwa yupo tayari kuuza utu wake kwasababu ya kazi au laaa"



    Sheby alijiongekea mwenyewe kimoyomoyo huku akiamka na kumkamata mary mpaka ukutani,.. Wakati huo mary anatetemeka kwa woga mana hajawahi kumtega mwanaume bila kutongozwa,.. Hivyo hata mihemo yake ilionyesha dhahiri kuwa sio ridhaa yake bali ni shida ndio ilimfanya akubali hilo... Sasa sheby alipomfikisha mpaka ukutani, alijikuta anaipandisha sketi yake mpaka juuu,.. Mary alikuwa anatamani kuzuia ili asifanye hivyo lakini hakuwa na jinsi mana ni shida ndio iliomleta, hivyo ikamlazimu kutulia.. Sheby alipeleka lipsi zake katika lipsi za mary,.. Mary kuona vile alifumba macho kumaanisha kwamba yupo tayari anyonywe denda lakini moyo wake ulikuwa hautaki tendo hilo.... Wakati huo huku chini kijana sheby anaendelea kuipandisha ile sketi ya mary.... Laaaaa Haulaaaa sheby kakutana na chupi ya mary,.. Aliigusa na kumfanya mary afumbue macho kwa woga.. Sheby aliishika chupi hio na kuivuta kidogo...

    Mary alizidi kuogopa na kujua kuwa leo ndio siku ya kubakwa kisa kazi.. Alikumbuka maneno ya rafiki yake rose yakisema kuwa

    "mary rafiki yangu,.. Najua jambo hili ni gumu sana kwako,.. Lakini vumilia tu tupate kazi rafiki yangu, natamani nikusaidie lakini siwezi mana tutaonekana sisi ni malaya,.. Akitaka mkubalie tu ili tupate kazi"

    "rose,.. Lakini si unajua mi sipendi tabia hio... Kwanini usiwe wewe"

    "nina sababu mbili za kutofanya hili... Kwanza, kaniambia nije kesho, kana kwamba kuna uwezekano wa kupata kazi au kukosa... Afu pili.. Mi najua we ni mzuri kuliko mimi, na una umbo la kumchanganya mwanaume yeyote yule kuliko mimi... Sipendi tuachane mary,.. Mpe tufanye kazi, tuachane na maisha ya kuigiza mtaani"

    Mary Alipomaliza kukumbuka, alishangaa kuona chupi yake ipo nusu.. Ilionekana hata sheby hakuwa akitania tena kama alivyotaka kufanya utani juu yake,







    Wakati huo huku reception rose alikuwa hakai, yaani kiti kilikuwa kina moto, maskini wasichana wa watu hawajazoea tabia ya kutoa mwili kwasababu ya kazi,.. Rose alikuwa kasimama huku akiwaza juu ya rafiki yake,..... Na ni kweli mary ni mzuri kuliko hata rose, mary anavutia ana umbo zuri, ana sura nzuri.. Japo jinsi ya kumteka mwanaume ndio hajui,.. Ila ukiwaona unaweza sema ni machangudoa lakini wala tu, ni watu wa kujiheshim kiasi chao, mavazi hua wanavaa vazi lolote na hata kuja arusha kutafuta maisha walikutana na rafiki yao ambae kwao kuna noti, hivyo wakawa wanaishi kupitia rafiki yao huyo, hata nguo walikuwa wakivaa nguo za huyo rafiki yao aitwae mwana,.. Kwasababu kwao kuna pesa, lakini wakaona ni ujinga, watamtegemea mwana mpaka lini, watavaa nguo zake mpaka lini, watajishebedua kwa uwezo wake mpaka lini... Hivyo wakaamua kuchukuwa vyeti vyao kisha wakaanza kuzunguka mjini ili waweze kupata kazi, waliingia kampuni nyingi sana lakini vigezo vyao havikuwa vikiwapatia kazi,.. Na ni kweli kwa kazi walizokuwa wanaomba kiukweli hawana kigezo hata kimoja,.. Lakini wamejiamini na kuja kutafuta kazi.. Kwenye kampuni kubwa kama hio kuajiri mfanyakazi mwenye elimu ya kidato cha nne, ni kuidhalilisha kampuni, mana kitengo atakachokaa mtu huyo hakutokosekana uharibifu kwasababu hana uzoefu na kazi hio na hata elimu pia hawana vizuri.. Na ukikuta kidato cha nne yupo kwenye kampuni kubwa basi ujue kachomekwa kisiri siri tu...

    "dada kaa"

    Aliongea Secretary huku akimuonea huruma..  Rose badala ya kukaa alimfuata yule Secretary na kumuuliza

    "Samahani dada, eti boss we anapenda sana wanawake"

    Rose aliuliza ili kujua kuwa rafiki yake atapo au ataumizwa..

    "boss mdogo au mkubwa"

    "mdogo"

    "hhhhmmm kiukweli tabia hio hana, labda aanze hivi karibuni"

    Aliongea mwanadada amina ambae ni Secretary wa kampuni hio.. Lakini wakiwa wanaongea, ghafla simu ya Secretary ya hapo mezani iliita

    "haloo boss"

    Haikusikia sauti ya boss, lakini aliongea kuhusu rose

    "sawa boss"

    Simu ilikata kisha amina akamwambia rose kuwa

    "boss anakuita"

    Aliongea Secretary huku akiendelea na kazi zake

    "boss mdogo eee"

    "ndio"

    Rose alitoka hapo mpaka mlango na kugonga kwa heshima ya hali ya juu mno,.. Huku akiwa na wasiwasi juu ya rafiki yake mary kama tayari keshaumizwa nini...

    "karibu"

    Aliongea sheby huku rose anaingia kwa kuangalia masofa kama yamevurugwa vurugwa, lakini masofa ya watu yalikuwa yamepangika kama ilivyo,... Kana kwamba hakukuwa na ngumi za utu uzima eneo hilo, rose alikaa lakini macho yake yako kwa rafiki yake ili kupata hata hisia za kuumizwa kwake..

    Wakati mary kakaa kwenye kiti na rose kakaa kwenye kiti na yeye...

    "sasa, ninyi mnajua kingereza vizuri"

    Rose na mary waliangaliana,..

    "ndio"

    Aliitikia rose peke yake lakini mary alinyamaza, na rose kweli kwa kiasi fulani yeye amesoma mpaka kidato cha sita, hivyo kalugha ka kigeni kidogo bado kapo, lakini mary alioishia kidato cha nne alikuwa kimya,...

    "mary vipi mbona kimya"

    Aliuliza kijana sheby, huku akishika kichwa mana wasichana hao walikuwa pasua kichwa,...

    "boss, kiukweli mimi sikua makini sana shuleni, ba siwezi kuitika kwa kitu ambacho sikijui"

    Aliongea mary, huku akiwa na huzuni, lakini sasa rose yeye wasiwasi wake ni kutaka kujua mary kamegwa kweli au vipi.. Nadhani hata wasomaji mnatamani mjue hilo..

    "ok.. Na kupiga hesabu za haraka haraka bila kutumia kalukuleta si mnaweza... "

    "hapana boss"

    "mungu wangu weeeee.. Kweli hapa kazi ipo"

    Ghafla wote wakapiga goti chini kuomba msaada juu ya kupata kwao kazi,

    "ah ah sasa mbona mnapiga magoti.. Hebu amkeni bwana, msiwe hivyo, kama ipo ipo tu"

    Aliongea sheby huku akiendelea kucheki vyeti vyao tena...

    "ok... Sasa, heeeeee mtanipa kazi sana nyie... Ok... Sasa itabidi nitenge muda wangu sasa wa kuanza kuwafundisha kazi kuhusu kampuni hii, itabidi nidanganye mmepata msiba wa ghafla, ili ndani ya hio wiki mjifunze kazi.... Kiufupi ni kwamba vyeti vyenu haviwezi kuwapa kazi hata kidogo... Bado vipo chini sana kwenye kampuni kama hiii.. Vyeti kama hivi labda ukaombe kazi A to Z au Sun Flag... Lakini sio hapa... Nitawaseidia kazi lakini itabidi mnionyeshe kwenu ili nije niwape mafunzo mawili matatu mkiwa wote"

    Rose na mary kuskia hivyo walifurahi sana, walikumbatiana kwa kupata kazi.. Lakini ilikuwa ni kama kuseidiana hivi,...

    "ok nendeni mkanisubiri hapo nje"

    Aliongea kijana huyo huku akiwapa vyeti vyao nae anatoka kuelekea ofisini kwa baba yake,... Wakati huo akina rose wanapita hapo reception wanakutana na amina au Secretary

    "vipi jamani mmefanikiwa"

    Aliuliza amina huku akiwa na shauku ya kujua

    "ndio dada, lakini ghafla tu tumepata msiba, hivyo tuhudhurie kwanza"

    Aliongea rose mana ndio keshazoeana na amina,..

    "oooohhh poleni sana"

    Basi akina rose na mary walitoka nje na kumsubiri boss wao,...







     





    Wakati huo huo huku ndani kwa mzee akiwa na mtoto wake

    "enhee umeshawakagua vyeti vyao"

    Aliuliza baba huyo huku sheby bila kujing'ata ng'ata alimjibu

    "ndio, na wapo vizuri.. Vyeti vyao vinaruhusu kupata kazi na tayari nimeshawapatia.. Lakini kwa bahati mbaya wamepata msiba hivyo watahitajika waende"

    "ooohhhh wape pole sana.. Na kwakuwa tayari ni miongoni mwa wafanyakazi basi wapatie chochote kama rambirambi"

    "sawa mzee"

    "sawa kazi njema"

    Sheby alimdanganya baba yake kuwa wadada hao walifaa kazini na vyeti vyao vinaruhusu kufanya kazi hapa.. Lakini sio kweli bali sheby aliwaingiza kisiri siri.... Tena ni hatari sana kwa kampuni yao mana wasipokuwa waelewa na kile watakacho fundishwa, basi kuna uwezekano wa kuingia hasara kubwa tu...

    "ok twendeni.. "

    Sheby aliwachukuwa wadada hao mpaka nyumbani kwao,.. Wasichana hao walipangisha chumba kimoja tu wao wawili,.. Basi sheby alijua nyumbani kwao hivyo akitoka kazini saa 11 jioni, basi aje kuwafundisha masaaa mawili hawa wasichana ili wapate kazi na wafanye kazi kwa uwelewa mzuri..

    "naomba kila saa 11 niwakute, yaani fanyeni yenu mchana wote huo, lakini ifikapo saa 11 jioni mrudi ili niwakute hapa... Hilo zoezi tutalianza kesho"

    "sawa boss.. Ahsante sana"

    "msijali"

    Sheby aliondoka zake na hata hivyo muda ulikuwa umekwisha, hivyo alirudi kule kazini ili kuweka mafile sawa,.. Aliifanya kazi hio mpaka kagiza kalianza kutanda,.. Ilipofika saa moja kamili jioni ndio kamaliza kazi yake, hivyo alichukuwa gari yake kisha huyoo kaondoka zake.. Wakati huo kila mfanyakazi alishaondoka muda mrefu sana, sema sheby yeye kuna baadhi ya document hakuziweka vizuri hivyo ndio maana amechelewa kurudi...  Sasa Sheby kufika pale kwa yule kipofu alishtuka sana kuona yule dada mpaka saa hizi yupo kana kwamba hakuja kuchukuliwa na mama yake.. Sheby alipaki gari pembeni na kushuka,.. Lakini zaituni kunusa pua, aligundua karibu yake kuna mtu mwenye pafyumu ambayo alishawahi kuinusa kabla

    "hapa mbele kuna mtu namjua"

    Aliongea zaituni ambae alikuwa ni kipofu

    "anaitwa nani"

    "jina simjui..."

    "ok...iv unajua sasa hivi ni saa ngapi"

    "itakuwa bado ni saa 10 jioni"

    "hapana, sasa hivi ni saa moja usiku"

    Zaituni kusikia hivyo aliruka na kumlilia sheby amseidie,...

    "nini kwani"

    "watanibaka tena..... Kumbe ni usiku.. Kaka niseidie, nitabakwa tena"

    Heeeeeeee sasa sheby anashangaa, ina maana alishabakwaga,..

    Sheby alijikuta analia tu kwa kuskia hivyo, yaani watu hawana hata huruma, mtu ni kipofu lakini wanambaka,...

    "ulibakwa lini"

    "muda tu, kama miezi sita imeshapita walinibaka wanaume wawili,... Naomba unilinde kaka, mimi nakuja kwa harufu yako tu"

    Wakati huo sheby hisia za kimapenzi zilishamjia, afu kumbe sheby alishampenda huyo dada na ndio maana anang'ang'anua ile safari ya kwenda india ili aende nae kule kuna wataalam wa matibabu,.. Na hio ndio sababu ya sheby kutaka kwenda india,...  Wakati huo zaituni kamkumbatia sheby, mana anajua akimuachia tu atabakwa, na wakati huo sheby hisia za kimapenzi zimemjaa tele,.. Mana hilo toto sio toto la mchezo mchezo, ni bonge la msichana, yaani hata angelikuwa kuchaa, angebakwa tuu, mana anaita vilivyo..

    "unaitwa nani"

    "naitwa zaituni"

    "mmmhhh natamani kukuoa"

    Zai kidogo tu azimie kwa kusikia neno hilo, mana akikumbuka kipindi cha uhai wa macho yake alikuwa akiletewa posa kabisa, lakini leo anataamkiwa kuwa anamaniwa kuolewa...

    "kiukweli kaka yangu kwa sasa siwezi kuwa mke bora kwako, siwezi"

    "kwanini"

    "sababu nyingi sana ninazo... Lakini moja wapo ni kwamba nitawezaje kukuhudumia kama mkeo,.. Kiukweli siwezi"

    Sheby kweli alikuwa anatamani kumuoa huyu mtoto wa kike, mana ana ndoto za kumfanya aone kwa mara nyingine tena,....

    "utaweza tu..."

    Sheby aliongea hivyo huku akimtoa mwilini mwake, mana zai alimkumbatia sheby kwa kuogopa kubakwa... Lakini ghafla mama yake katokea huku akiwa anakimbia kweli kweli...

    "wewe mwanaume ni nani muachie mwanangu"

    Ilikuwa ni usiku kuna kagiza hivyo hata mama huyo hakumuona sheby,

    "mama huyu ni yule kaka wa juzi"

    Sasa mama kuangalia vizuri alimuona sheby

    "eeee baba nisamehe sijakuona... Una kuna binadamu sio watu, na wala sitaki kusema"

    "mama nimeshamwambia"

    Aliongea zai kumaanisha hicho alichotaka kusema mama huyo, tayari zai keshasema kuwa alibakwa

    "shkamoo mama"

    "marahaba baba habari za toka juzi"

    "aaahhh nzuri tu.... Sasa mama naomba niwapeleke"

    "jamani baba tutakuchelewesha"

    "hakuna shida"

    Basi sheby aliwaingiza katika gari na kuondoka nao mpaka kwao...



    Sasa walipikuwa wanashuka katika gari, zainabu alikuepo kwa pembeni tena alikuwa na rafiki yake neema,..

    "heeeeeeee mdogo wako leo kaletwa na gari kali"

    Wakati huo zainabu bado kazubaa tu, kwa kuona mdogo wake bado anaendelea na bahati zake,..

    Yaani zainabu na Zaituni wamefanana kila kitu, yaani kasoro rangi, tena rangi yenyewe sio sana mana zainabu keshaanza kujikoboa koboa, hivyo ana ngozi ya maji ya kunde hivi,. Sura wanafanana, shepu, kifuani, yaani kila kona ni wao..

    Basi sheby alimchukua zaituni na kumkokota mpaka ndani kwao,..

    "karibu baba"

    Mama alikuwa akimueshim sana sheby,..... Lakini kuna sauti iliskika kwa mbali ikisema

    "wewe si unajijua una ugonjwa lakini, sasa ukimuambukiza kaka wa watu"

    "potelea pote.. Liwalo naliwe, kwani ugonjwa ni nini bwana?, mi nataka nimuweke kiganjani kwa mapenzi tu,.. Wacha nikampe tunda langu hata kama lina ugonjwa atajijua mwenyewe"

    Iliskia hio sauti kwa nje... Ila huku ndani mama alizidi kumkaribisha sheby akae katika kochi.. Lakini sheby ghafla alishikwa na haja ndogo na kuomba kutoka msalani..

    "Ahsante mama angu... Ahh naomba niingie msalani kidogo"

    Aliongea sheby kuwa anaomba aingie msalani kidogo..

    "sawa baba, utazunguka tu hapo nyuma"

    Basi sheby alitoka nje na kuingia msalani, huku ndani mama anamuuliza mtoto wake

    "wewe mbona nilikukuta mmekumbatiana"

    "lakini mama mbona umechelewa kuja lakini, au nia yako nibakwe tena"

    "hapana mwanangu usiseme hivyo, kuna mteja nilikuwa nampelekea ndizi sasa ndio nikachelewa, nisamehe mwanangu"

    "sawa lakini sio vizuri mama.."

    "nisamehe mwanangu zai"

    "sawa mama.... Afu mama.. Yule kasema anatamani kunioa"

    "mmhhh kakudanganya, mwanaume nani wakati huu aoe kipofu"

    "mama kasema kweli"

    "hawezi kufanya hivyo"

    "mamaaaaaaa unanikatisha tamaa mwanao"

    "basi mwanangu kama kasema hivyo basi wacha tuangalie kinachofuata"



    Sheby akiwa anatoka msalani tena huku akiwa na furaha,.. Kila akilifikiria lile umbo la zaituni, anapata ukichaa, yaani ni mtoto wa haja,.. Afu heshima imejaa pale,..

    "yaani mtoto alinisisimua pale alipo nikumbatia"

    Aliongea sheby huku akitoka msalani,.. Lakini ghafla anakutana na zaituni akiwa kashika kamti kake na miwani yake

    "we zaituni unakwenda wapi huko"

    Aliongea sheby, huku akimfuata kwa kumkimbilia

    "nilikuwa nakutafuta wewe"

    "nipo hapa"

    Sheby kafurahi mno kuona zai katoka nje,..

    "naomba tuongelee ndani ya gari"

    Aliongea zaituni huku akimshika shika sheby sehemu za kifua...  Sheby kwa raha alimbeba mpaka kwenye gari,.. Sasa kufika kwenye gari sketi ya zaituni ilipanda juu, hivyo shepu lake likaonekana live,.. Sheby kuona mipaja ya zaituni, macho yalimtoka na kujikuta anayatetemekea,.. Na zaituni kwa makusudi anazidi kuipandisha sketi hio mpaka chupi ikaonekana bila chenga, tena zaituni kwa kusudi alijilaza kabisaaa, huku sheby akiona ni bonge la zari la mentali kutembea na mrembo kipofu,....



    Sasa zaituni akiwa anataka kuivua ile chupi, alikumbuka alipkuwa nje akiongea hivi...

    "neema, mimi nataka nimtege huyu mpenzi wa zaituni awe wangu... Nataka hata ikiwezekana anifanyie lolote lile"

    "heeeee we neema kumbuka ni kama shemeji yako huyo eti"

    "sasa usheji si kuzima taa... Hii hainaga ushemeji neema we tulia kama maji ya mtungi"

    "ina maana zainabu... Huyo kaka akitaka papuch yako unampa"

    "heeeeee nimnyimie nini sasa... Wacha ale ili anogewe aje kwangu"

    "Lakini we zainabu wewe si unajijua una ugonjwa lakini, sasa ukimuambukiza kaka wa watu"

    "potelea pote.. Liwalo naliwe, kwani ugonjwa ni nini bwana?, mi nataka nimuweke kiganjani kwa mapenzi tu,.. Wacha nikampe tunda langu hata kama lina ugonjwa atajijua mwenyewe"

    Kuumbe Huyo hakuwa zaituni,.. Mungu wangu weeee, afu mbaya zaidi ni kwamba inasemekana zainabu ana ugonjwa ila hatujui ni ugonjwa gani,... Na sheby wakati huo anaona chupi ya zainabu inashushwa, yeye anajua ni zaituni ndio anamshushia chupi, kumbe sie... Udenda ulimtoka sheby kila akiina maungo ya zainabu, ila hajui kama ni zainabu,... Zainabu aliiacha chupi katikati ya mapaja yake, kisha akaifuata zipu ya sheby iliokuwa nyepesi kuvuta.... Laaaaaa Haulaaaaa maskini sheby wa watu ndio huyo anakubali kuvuliwa suruali, tena sheby mwenyewe wakati huo ana moto wa kula tunda hilo... Kila akiona chupi ilivyoishia magotini ndio anazidi kupata joto la mapenzi...







    Kufanana kwingine kuzuri sana lakini ni kubaya sana katika mapenzi, zainabu anajua fika huyu ni mwanaume aliekuja na mdogo wake ambae ni pacha wake, lakini kwa wivu wa mapenzi anajikuta anamtaka mwanaume huyo,.. Na kijana huyo bila ya kujua alijikuta nae anamtamani kimapenzi... Sasa wakati huo chupi ya zainabu imeishia magotini huku kijana sheby joto likizidi kumpanda haswaa, aliishika ile nguo na kuimalizia kuivua, kisha akapandisha ile sketi tayari kwa kula tunda lq zainabu ila hajui kama ni zainabu,... Lakini sasa kumbuka kulikuwa na kiza hivyo walioongia kwenye gari kiza kilizidi kuwepo, mana gari ilikuwa ni tinted hivyo hata uwashe taa bado mtu wa nje hawezi kuona ndani ispokuwa kioo cha mbele peke yake, na aliopo mbele ya gari pia hawezi kuona kwasababu wao wapo siti ya nyuma wakiwa wamezuiwa na siti ya mbele... Sasa mtoto wa watu kila akiitafutia papuch ya zai ili aanze gemu, zai anasema sio hapo.. Kana kwamba zai kuna kona zake alikuwa anataka.. Mana shebt yeye alikuwa anataka kutumia njia ya kawaida lakini zai anakataa na kusema sio huko.. Sheby kwa hasira tu alijikuta anawasha taa ya hapo ndani,.. Sasa hapo ndio akamuona vizuri mwadada huyo, kitu cha kwanza macho ya sheby yalitua kwenye papuch ya zai,.. Kisha akamuangalia usoni.....  Laaaaa Haulaaa kumbe hakuwa zaituni bali alikuwa ni zainabu, sheby ndio anajua sasa hivi kuwa huyo hakuwa zaituni aliomtegemea, bali ni zainabu... Na hata zainabu alipomuona sheby alimkumbuka vizuri tu... Walishawahi kukutana supamaketi, lakini zainabu alimletea nyodo kaka huyo,... Zainabu kuona hivyo alishikwa na aibu, papuch yake imeshaonekana afu kumjua keshamjua...



    Mzee wa msimamo kaanza misimamo yake,.. Kama ulishawahi kusoma Love Story yangu iitwayo SECONDARY SCHOOL basi utaujua vyema msimamo wa sheby,...

    "haya vaa uende"

    Yaani mtoto wa kike jinsi alivyosimamia kucha lakini huezi amini kama sheby angeweza kumwambia kuwa avae aende zake

    Na zainabu hana la kusema mana keshamkumbuka na alishamleteaga nyodo kule supamaketi kisa kaulizwa mbona kama kafananishwa na kipofu, badala aseme ni ndugu yangu, kajibu maneno mabovu kwa sheby,.. Hivyo hata hapo sheby kafanya kisudi kumwambia avae ili ajue kweli kuna wanaume wenye misimamo yao...

    Zainabu kashusha sketi tu na kushika chupi yake mkononi kisha huyoo kaondoka zake... Sheby nae kaingia ndani akamkuta zaituni mwenyewe akiwa kaketi kwenye kochi,..

    "sasa mama naomba tuongee"

    Aliongea sheby kumaanisha alimtaka mama zai watoke pembeni kidogo wapate kuongea,

    "sawa baba"

    Mama alikuwa akijibu kwa heshima ya hali ya juu mno,...

    Basi mama zai na kijana huyo walitoka pembeni kisha wakaanza kuongea jambo fulani



    Tukija huku kwa akina mary na rose wakiwa nyumbani kwao rose alikuwa anaandaa chakula lakini mary alikuwa katika mawazo mazito sana

    "we mary chakula tayari"

    Rose Aliongea peke yake bila kujibiwa

    "mary?... We mary?... Mary, mary... We meriiiiiiii"

    "nini jamani rose, umenishtua eti"

    "una mawazo gani shost, kama ni kazi tumeshapata sasa mawazo ya nini wakati kama huu"

    "alionipa kazi ananiumiza kichwa sana rose"

    "nani.. Yule boss"

    "we acha tu, yaani sijui hata ni mwanaume wa dizaini gani yule"

    Mary alikuwa akimsifia sana kijana sheby kana kwamba kwa kitendo alichokifanya sheby ni kitendo ambacho wanaume wengi wasingeweza kukifanya...

    "Enheeee afu umenikumbusha.. Ivi saa ile pale nilipokuacha nae, alikuduu au"

    "ndio hicho kitu kinachoniumiza kichwa rose"

    "kivipi sasa... Amejaaliwa mkongomani au"

    "bora ingelikuwa hivyo"

    "au ni kibamia"

    "bora ingelikuwa hivyo"

    "we mjinga kweli, sasa ni nini kama sio hivyo"

    Rose alikuwa ana hamu ya kujua kilichojiri kwa rafiki yake mary, mana hata yeye hakuwa na uhakika wa kupata kazi, bali aliitwa tu na kupewa kazi baada ya mary kubaki na boss wakiwa wawili tu

    "rose, ivi ni mwanaume gani anaweza kukuvua chupi afu akakuacha"

    "kwa sasa hivi hakuna... Na hata huyo hawezi kua hivyo"

    Aliongea rose huku wakiendelea kula

    "sikia sasa... Hivi Unajua ilikuwaje saa ile uliponiacha nae"

    "najulia wapi sasa"

    "saa ile ilikuwa hivi"

    Sasa mary anatumalizia kile kipande pale tulipoishia sehemu ya tatu... Ilikuwa iendeleee hivi..





    *************************************



    Alikumbuka maneno ya rafiki yake rose yakisema kuwa

    "mary rafiki yangu,.. Najua jambo hili ni gumu sana kwako,.. Lakini vumilia tu tupate kazi rafiki yangu, natamani nikusaidie lakini siwezi mana tutaonekana sisi ni malaya,.. Akitaka mkubalie tu ili tupate kazi"

    "rose,.. Lakini si unajua mi sipendi tabia hio... Kwanini usiwe wewe"

    "nina sababu mbili za kutofanya hili... Kwanza, kaniambia nije kesho, kana kwamba kuna uwezekano wa kupata kazi au kukosa... Afu pili.. Mi najua we ni mzuri kuliko mimi, na una umbo la kumchanganya mwanaume yeyote yule kuliko mimi... Sipendi tuachane mary,.. Mpe tufanye kazi, tuachane na maisha ya kuigiza mtaani"

    Mary Alipomaliza kukumbuka, alishangaa kuona chupi yake ipo nusu.. Ilionekana hata sheby hakuwa akitania tena kama alivyotaka kufanya utani juu yake,



    Mary alikuwa anatetemeka mana anakumbuka amewahi kufanya mapenzi mara moja tu wakati wa kutolewa bikra yake, na ni muda mrefu umepita mpaka sasa, hivyo bado ule uoga wa mwanzo mwanzo anao..

    Sheby aliendeleza kuivua ile chupi mpaka magotini kabisa, kisha akaipandisha sketi ya mary,.. Wakati huo mary kafumba macho wala hataki kuona kitu anachotaka kufanyiwa na kijana huyo,.. Sheby alimsogelea na kumng'ata shingoni mwake (Love Bite) Kitendo kilichomsisimua mary mapaka kufumbua macho yakiwa yamelegea kisa love bite aliong'atwa na sheby,.. Kijana huyo alimwangalia sana mary mpaka mary akashusha macho chini kwa aibu, wakati huo chupi imeshafika chini ya miguu, yaani kazi ya mary hapo ni kunyanyua miguu nguo ivuke kabisaa mana alikuwa kasimama ukutani,.. Lakini Ghafla sheby akainama chini na kuishika ile nguo,.. Sasa kumbe mary nae tayari keshaanza kulegea kua alikuwa tayari kwa kufanya mapenzi na kijana huyo, na sababu ya kukubali ni lile kiss la meno lilimsisimua na kumueka katika nafasi ya matamanio ya kimapenzi,.. Mary alikuwa anataka kunyanyua mguu ili chupi itoke, lakini alishangaa mguu umezuiwa, kisha hapo hapo sheby akaipandisha ile chupi na kumvalisha vizuri.. Huezi amini sheby kamuacha mary nyakati za mwisho, tena hata muhusika mwenyewe alikuwa tayari kwa tendo hilo,.. Ila sheby kamvalisha mtoto wa watu nguo yake...

    "vp tena boss"

    Aliuliza mary huku akishu pumzi nzito kwa kuachwa mana kilichomsukuma mpaka kujikuta anakubali ni lile kiss la meno (love bute) ndio lililomchanganya mary,..

    "nimegundua unapenda kazi, na hupo tayari kwa jambo hili bali ni kazi ndio imekufosi kufanya hivyo, na hata kuja hapa sikuja kwa lengo hilo bali nilikuwa nataka kujua kama kweli upo tayari kuutoa mwili wako kwasababu ya kazi"

    "Ahsante boss.. Kweli sikua tayari ila ningelikubali tu kwasababu ya kazi"

    "ok mimi sitaki tena... Ngoja nimuite rafiki yako aje nijue cha kufanya"

    Ndio hapo sheby akapiga simu kwa Secretary kisha akamuagiza amina amwambie rose aje ofisini kwake.. Na hapo ndio mwisho wa mwendelezo wa sehemu ya tatu, ambayo tulifichwa tukio liliofuata



    ***********************************

    Kumbukumbu imeishia hapo sasa tuendeleee....

    "hhhmmmm mary wewe.. Hivi hajakuona papuch yako kweli"

    Aliuliza rose huku bado wanakula..

    "hhhmmm rose weweee, ataacha kuiona kweli... Mi najua aliiona pale alivyoinama, mana mi nilikuwa nimeshikilia sketi kwa juu afu nae kainama, hivyo hapo ndio nahisi kaniona, mana ni kuigusa papuch yangu kaigusa kabisaa"

    "hhhhmmm ila Ahsante mary, umejitahidi sana"

    "nimejitahidi??... Na wakati nimshukuru yeye kwa kughairisha mpango"

    "heeeeee kwaio hata wewe ulikuwa unataka"

    "mwanzo sikuwa nataka.. Lakini kuna Live Bite moja alining'ata shingoni, hio ndio iliniamsha kila kilicholala,.. Hapo hapo mwili wangu ukawa tayari kwa kufanya mapenzi, hivyo hata vile alivyositisha nilichukia sema sikutaka ajue tu"

    "mmhhh na uzuri wako huo kweli kakuacha... Siamini mary, wewe umefanywa sema unanificha tu"

    "kweli rose, hata nikuonyeshe we si unajua mwanamke aliofanya muda uliopita, haya ngoja nikuonyeshe ili uamini"

    "achana na hayo mambo bwana, tule tukalale zetu, utantamanisha bure"

    "iiiiiiii afu rose... Hatujamwambia mwana kuwa tumepata kazi"

    "achana nae kwanza"

    Aliongea rose huku wakiendelea kula,

    Katika chumba chao hicho walikuwa wakiishi wao wawili tu....



    Sasa tuje huku kwa wazazi wake na sheby wakiwa wamejawa na wasiwasi juu ya mtoto wao kuchelewa nyumbani mana muda huo yapata kama saa mbili za usiku na kazini kutoka ni saa 11 za jioni, sasa mpaka saa hio hawamuoni mtoto wao

    "huyu mtoto wako mi nakuambia ana wanawake huyu wewe husikii ona mpaka saa hizi yupo wapi"

    Baba yake yake sheby alianza kuwa mkali baada ya kutomwona sheby nyumbani,..

    "huezi jua mtoto kapatwa na nini huko"

    "unaona sasa unavyomtetea, ndio maana anazidi kuwa bogazi yule, kumbe wewe ndio chanzo"

    Mama alikuwa anatamani kumtetea mtoto wake lakini baba hawezekani kabisa kushaurika,

    "sio chanzo mume wangu,.. Kumbuka mtoto wetu keshakuwa sasa.. Kwanini umlinde, basi mwambie aoe ili ikutoke akili ya kuchelewa kwake kwasababu ya wanawake"

    Mama aliongea hivyo kwa hasira baada ya kuona mtoto wake anabebeshwa mzigo ambao hahusiki nao

    "Enheeee hilo nalo neno... Ili atulie inabidi aoe,... Safi sana"

    "yaani baba sheby kweli unakubali yule mtoto aoe na umri ule"

    "shida yangu atulie... Staki pesa zangu ziishie kwa wanawake wengi"

    "heeeeee baba sheby jamani... Mtoto wetu bado ni mdogo sana eti"

    "itawezekana tuuu... Tena kuna yule mtoto wa rafiki yangu anamfaa sana"

    "rafiki yako yupi huyo"

    "Mohamedy ana mtoto wake mzuri tu"

    Aliongea mzee rashidi huku akiangalia tv,..

    "wee baba sheby, yule Mohamedy si ana mtoto mmoja tu wa kike afu ni mkubwa yule"

    "Enheeee, huyo huyo, anamfaa sana mtoto wetu"

    "Ati nini.... Yaani unataka kumchagulia mke???... Haiwezekani baba sheby, patachimbika hapa... Mtoto wangu hawezi kuoa mtu mzima kiasi kile, haiwezekani labda niwe nimekufa"









    Mama sheby alikuwa ni mwanamke mwenye hasira za karibu sana, kwani hakutaka kujua huyo mwanamke yupoje au ana umri gani,...

    Kikubwa hataki mtoto wake aoe katika nyumba hio,.. Lakini wahenga walisema kuwa mwanaume ni mwanaume tu hata iweje, ila ngoja tuone hapa itakuwaje kati ya mama na baba nani mshindi wa juu ya mtoto wao,

    "Enheeee, huyo huyo, anamfaa sana mtoto wetu"

    "Ati nini.... Yaani unataka kumchagulia mke???... Haiwezekani baba sheby, patachimbika hapa... Mtoto wangu hawezi kuoa mtu mzima kiasi kile, haiwezekani labda niwe nimekufa"

    "wewe ndio umesema hivyo, lakini sio mimi"

    Aliongea baba sheby huku akiondoka tena hakutaka maneno mengine na mke wake huyo,..



    Tukija huku kwa akina zaituni, sheby akiwa yupo nje na mama zaituni akiwa kamtoa kwa ajili ya maongezi zaidi

    "mama, Samahani sana... Jambo hili lilihitaji mshenga lakini kwa dharura hii sidhani kama kuna haja"

    "una maana gani baba, sijakuelewa"

    "kifupi ni kwamba, nimevutiwa sana na mtoto wako.. Tatamani sana hata angelikuwa mke wangu"

    Mama zaituni alishangaa kuskia maneno hayo ambayo hayajawahi kuskika katika maskio yake toka zaituni apate upofu, lakini leo anayasikia

    "hehehehhee kijana wangu naona unanichekesha kweli... Sidhani kama litakubalika hili"

    Mama aliongea hivyo bila kujua kweli sheby alikuwa ana nia na zaituni na hataki tena akaombe kule barabarani, mana keshakuwa mchumba wa mtu..

    "kwani lisikubalike mama angu... Kweli mtoto wako ana sifa zote za kuwa mke,.. Namuitaji"

    "ivi baba hebu nikuulize swali.. Ivi mtoto wangu unataka kumfanyia nini haswa,.. Mtoto wangu ni kipofu.. Wewe utahitaji kufuliwa nguo zako, mtoto wangu haoni... Wewe utataka upasiwe nguo zako, mtoto wangu haoni... Wewe utataka utandikiwe kitanda, mtoto wangu haoni... Wewe utahitaji unyumba, mtoto wangu haoni... Na sio hivyo tu vipo vingi vinavyotakiwa kufanywa na mke, mtoto wangu haoni... Je? Unamtakia nini mtoto wangu na wakati hawezi kufanya chochote kile ukaridhika,.. Au pesa zenu zimekuagiza mwanamke kipofu"



    Mama alichafukwa, hata heshima kwa sheby tena ikawa hakuna, mana ukiangalia ni kweli... Mke anatakiwa kuwajibika na kila kitu ndani ya nyumba, lakini sasa kama haoni we ulifikiri atawajibika vipi,..

    "mama, Samahani sana mama angu, mimi sipo huko na sina hata hilo wazo unalofikiria... Kweli nampenda mtoto wako, lakini kwakuwa huhitaji basi.. Naomba nimuage tu niondoke, lakini tambua kuwa,.. KUOA AU KUOLEWA NI SHERIA...  Kwa kukataa kwako umemnyima mwanao haki ya msingi.. Kwani mi sijui kuwa ni kipofu? Kwani mimi sijui mke anatakiwa aweje ndani ya nyumba?... Mama pesa zetu hazina masharti kama unavyofikiria, na istoshe hata mtoto wako sitaki ajue hali yangu"

    "sasa si ndio mashetani yenyewe hayo, yaani mtu unaempenda hutaki ajue hali yako"

    "najua hujui mama yangu... Na kukujuza itachukuwa muda mrefu sana,... Nampenda sana mtoto wako.. Endelea kumueka ndani tu... Ngoja nimuage niondoke mama angu.. Ila Samahani sana kama nimekuudhi"





    Mama alikaa kimya kwa kuona maneno ya sheby kuwa makali,.. Sheby aliingia ndani na kuongea na zaituni

    "zai?"

    "abeee kaka"

    "Samahani sana zai... Sikutaka kukuambia wewe kwanza... Ila nimeongea na mama yako kakataa"

    "kakataa kufanya nini"

    "zai... Binafsi yangu mimi nakupenda sana na wala sitaki kujali hali ulionayo, nipo tayari kuwa na wewe kama mke wangu, lakini mama yako kakataa"

    Aliongea sheby huku akiwa kama anonyesha msistizo juu ya jambo hilo, na sheby hataki kutoa taarifa ya kumseidia kuona mana linaweza lisiwezekane jambo hilo..

    "lakini kaka yangu, mama yangu hana kosa,.. Nadhani anataka kukuseidia wewe na maisha yako usipate tabu.. Kiukweli mimi nitakuwa mzigo kwako, mana nitakuwa mtu wa kukaa tu, sasa hio sifa ya mke itatoka wapi kama sintojishughulisha na chochote..mkubalie mama yangu ili usipate shida katika ndoa yako"



    Sheby hakuamini kama atamkosa zaituni mana nia yake ni kumseidia na sheby anajua kabisa kweli hawezi kuishi nae, lakini yeye anataka kumseidia kuona tena,..

    "sawa, naona familia yote mpo pamoja.. Basi nakwenda.... Lakini pale barabarani sitaki kuluona tena, kama ni hio pesa unayopata pale mimi nitakupa mara mbili yake kila siku"







     





    Sasa kumbe wakati mama alikuwa anasikia kila kitu,.. Yaani mwanzo mwisho mama kasikia...

    "lakini kaka, kwanini nikupe kazi ambayo haikuhusu... Kama mama yangu kakataa basi"

    "kwasababu nilikuwa na nia ya kukuseidia, basi nitaendelea kukuseidia hata kama mumekataa... Kwaheli"

    Sheby alitoka lakini akiwa kakasirika sana, yaani hata hamu hana....



    Lakini sasa mama aliyasikia yale maneno na kumuingia katika moyo wake,..

    "sasa kama mtu kakataliwa lakini bafo tu ana nia ya kumseidia,.. Ni mtu wa aina gani huyu??... Zimetupita posa nyingi sana wakati wa uhai wa macho yake, lakini toka alipopata upofu, sijawahi kuona hata wale vijana wa kihuni wakimsalimia mwanangu.... Hakika huyu sio mtu wa kumuachia.. Kama ni pesa zao wacha iwe hivyo, lakini anastahili alichokitaka"



    Mama aliongea mwenyewe kimoyomoyo huku akimfuata sheby,..

    "baba... Baba Samahani sana naomba tuongee"

    Mama alijikuta anapiga magoti kumuomba sheby waongee tena, mana alimkashifu kuhusiana na pesa zao, kuwa labda ni hizo pesa zao ndizo zilizotuma mwanamke kipofu..

    "mama sidhani kama nitakuwa na muda tena"

    "baba nisamehe sana... Naomba unisamehe... Nimekubali awe mkeo, lakini sasa...... "

    Sasa sheby kuskia hio lakini... Akaona ngoja amsikilize mama huyo

    Sheby alimkubalia na kumsamehe..



    Tukija huku kwa akina mary wakiwa ndio wanalala, lakini mary huezi amini kumbe tayari keshampenda sheby wa watu, yaani kafa kaoza.. Hivyo kila mara yeye ni mtu wa kulikumbuka lile busu la meno alilopigwa na sheby,..

    "unajua sasa utakuwa chizi wewe"

    "bora niwe chizi rose... Kiukweli sijawahi kupenda toka nizaliwe, na ndio mana naiona tofauti ya kupenda na kutamani,.. Kiukweli yule kijana nimempenda dada rose.. Niseidie mwenzio"

    Aliongea mary kumaanisha amseidie, mana rose na mary, mkubwa ni rose.. Mana rose anaendea miaka 25 sasa, na mary yeye ndio kaifikisha miaka 22 mwezi uliopita hivyo ni rafiki yake lakini pia ni dada yake kiumri,..

    "sasa mimi nitakuseidiaje na wewe shost heeee"

    "Dada Rose, mi najua kidogo una umri huenda akakuelewa eti"

    "heeeeee mary siki hizi unaniita dada?? Ama kweli umependa kweli,.. Toka tuanze urafiki sijawahi kuskia hilo neno, lakini leo unalitaamka.. Basi nakuahidi nitajaribu nikishindwa basi"

    "Ahsante dada angu"

    Lakini sasa kumbuka hata rose ni mzuri na ana umbo la kuvutia sema anapenda kujishusha sehemu kama ile aliomuacha mary na sheby ofisini, sehemu kama zile rose hua hazipendi na ndio mana anamsukumia mwenzie ili wapate kazi kupitia mwili wa mwenzie, lakini hata rose pia ni kisu cha kukalia mbali kwa uzuri na umbo aliokuwa nalo...

    "yaani nimependa mpaka naumwa yani, na kitu ambacho sikukitarajia kabisa yani"

    "mapenzi ni upofu mama... Ndo ushapenda hivyo"

    Lakini sasa Rose akiwa anaongea hivyo huku alikuwa kama anabinua mdomo kana kwamba hajapenda ishu kama hio... Kuna kijiba roho kinaanza kati yao, na yote hayo kisa ni mwanaume tu... Ngoja tuone mwisho wao..



    Tukija huku kwa mama zaituni akiwa na sheby pembezoni mwa ukuta wa nyumba yao, wakati huo inakwenda mida ya saa nne hivi usiku, kijana sheby anazidi kuchelewa kwao bila kujua kule nyumbani wazazi wake tayari wamesha chafukwa juu yake,..

    "baba... Mimi nimekubali, lakini sasa utaishi ishi vipi nae"

    Aliongea mama zai huku sheby akicheka sana,

    "kikubwa ni ruksa yako tu.. Na tutafanya mipango ya ndoa kabisa lakini sio sasa hivi"

    "kweli una nia njema na mtoto wangu... Lakini sasa kabla ya hio ndoa yenu mtoto wangu ataishi wapi.. Mana akiendelea kuishi hapa kwangu atakufa"

    Mama aliongea jambo lililomshtua sheby...

    "Ati nini... Afe???... Auwawe na nani"

    "sio Auwawe na nani... Ivi kumbe hajakwambia"

    "aaakuuu mimi sijui... Kwani kuna nini"

    Sheby alikuwa tayari kuskia sababu ya kifo kwa zaituni pindi atakapoishi hapo

    "ivi unajua kiwa huyu zaituni kamwagiwa tindikali na dada yake ambae ni pacha wake"

    "Whaaaat"

    Sasa Sheby yeye alikuwa hajui hii ishu kama upofu wa zaituni ulisababishwa na zainabu.. Sasa leo ndio anatobolewa siri

    "ndio.. Na sababu ya kumwagia ndugu yake, ni hii hii ya mambo ya wachumba... Nakumbuka kuna kioindi nilikuwa sijiwezi, hivyo nikawaambia kila mmoja sasa atafute mchumba aolewe, lakini sasa zaituni ndio aliokuwa anapata posa nyingi kuliko zainabu,.. Na zaituni yeye hakiwa akitaka kuolewa hivyo posa zote akawa anazikataa eti mpaka afikie malengo yake... Lakini sasa kumbe dada yake zainabu anaona wivu na jambo lile, hivyo alifikia hatua ya kumwagia ndugu yake tindikali ili zile posa zimjie yeye.. Sasa na wewe ukiweka nia kama hio atauwawa kabisa, mana alifanya hivyo ili asiolewe, sasa kama wewe umejitokeza baba... Afu unasema tutafanya mipango ya ndoa baadaye huoni atamuua kabisa"



    "mungu wangu weeeeee....ivi una uhakika na yeye ni mtoto wako kweli"

    "baba, nimewazaa mwenyewe tumbo moja na walikuwa pamoja"

    "sasa si umfukuze... Kwanini ukae na mtu kama huyo.. Mtu katili kiasi hicho unaishi nae vipi sasa"

    Sheby alikasirika sana kuskia kuwa yule aliotaka kumbandua kwenye gari ndio aliosababisha upofu kwa ndugu yake,..

    "kumfukuza siwezi.. Kwasababu kuna vitu anafanya na bila yeye hatujui tutaishi vipi"

    "kwahio upo tayari familia iishe kwasababu ya hicho kitu mama... Kwani ni kitu gani hicho"

    "mmmhhhh baba,.. Tuyaache tu hayo"

    "we niambie mama angu, huenda nikaweza kukuseidia japo kidogo tu"

    Sheby alijikuta anaingilia majukumu mengine ambayo hayakuwa yakimuhusu kwa yeyote ile,... Mama anasita kuongea, kana kwamba jambo analofanya zainabu ni kubwa sana na hata sheby hatoliweza kulifanya...

    "baba, nakuonea huruma sana... Sidhani kama utaweza baba"

    Hata sheby mwenyewe alianza kuogopa kuhusiana na jambo hilo, alijikuta anarudi nyuma, kwani hata huyo mama alianza kumwogopa, mana ni jambo gani analoweza kufanya mwanamke afu mwanaume ashindwe???... Sheby aliogopa na kutia hofu kubwa sana ndani ya moyo wake.. Alihisi kuna jambo kubwa hapa...

    "basi mama usiseme tena.. Tuyaache hayo mambo"

    Lakini sasa kabla sheby hajataka kuondoka,... Ghafla zaituni alitokea na kusema kuwa

    "mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"







    Kijana sheby aliogopa sana kuhusiana na jambo hilo, kama mwanamke kaweza je huyo mwanaume atashindwa vipi kuliweza jambo kama hilo,.. Kijana huyo alitaka hilo jambo lisiongelewe tena mana huenda kweli likawa zito kwake, hivyo bora asiambiwe mana huenda ni jambo asiloliweza, lakini wakati mama zai anajing'ata ng'ata, mara zaituni katokea huku akiwa anapapasa pakupita,..

    "mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"

    Aliongea zaituni huku akiwa tayari kwa kuongea,..

    "zaituni mwanangu, kakae utulie nitaongea nae tu"

    Aliongea mama yake zai huku akimrudisha ndani.. Baada ya hapo mama na sheby walisogea pembeni zaidi ya pale walipokuwa na kuongea



    "ukweli ni kwamba, zainabu ndio anaelipa kodi ya hii nyumba, kwa mwezi ni elfu 70, na mimi sina kipato chochote cha kuingiza ili niweze kulipa"

    "ina maana ni hilo tu ndilo linalowafanya akae humu ndani"

    "ni hilo tu, mana kama ni zaituni akienda kuomba anakuja na hela ya kula tu, na tukifukizwa kwenye hii nyumba je tutaishi wapi, baba yao amefariki miezi kadhaa iliyopita... Hivyo zainabu ndie mlipa kodi ya nyumba hiii na ndio maana siwezi kumfukuza"

    "kwani anafanya kazi gani huyo mwanao"

    "hhhhmmmm baba,... We acha tu... Sasa hivi anajiuza tu na ndio maana anaweza kuilipa kodi ya nyumba hii"

    "kwahio hili ndio jambo uliokuwa unaona uzito kuniambia"

    "ni hilo tu baba yangu, siwezi kumgukuza kwa hilo, japo ni katili lakini nitafanyeje sasa"

    "ok unaweza kuniunganisha na huyo mwenye nyumba"

    "labda kesho niongee nae mkutane"

    Sheby alitaka kumaliza utata juu ya swala hilo, mana wahenga walisema kuwa, ukipenda boga basi penda na uwa lake, na sheby kweli kampenda sana zaituni, kuachilia umbo lake, bali hata heshima anayo yaani sifa zote za kuwa mke anazo, na sheby uwezo wa kumfanya aone tena anawo,...

    "sasa... Naomba usimuambie hali yangu,... Narudia tena, sitaki ajue kuwa mimi nina uwezo kifedha, akikuuliza kuhusu mimi mwambie ni kijana mchapakazi tu, anafanya kazi ya kuuza viazi kwa mkokoteni sawa mama"

    "sawa baba nimekuelewa.. Lakini kwanini unafanya hivyo"

    "utajua baadae mama angu, ila naomba uwe kimya kwa hilo"

    "mmmhhh sawa"

    Basi sheby na mama zai walielewana kisha akamwachia mama huyo kiasi kidogo cha pesa,..

    "sasa mama, utaniagia huyo ila umwambie ukweli kuwa naitaji kuwa nae, na sijali hivyo alivyo"

    "sawa baba nitamwambia"

    Sheby hakutaka kuooteza muda mana tayari ni saa nne usiku, hivyo kapenda kuwahi zaidi nyumbani.... Akiwa niiani alikuwa akiumiza kichwa sana jinsi ya kuongea kwa wazazi wake,...

    Sheby alifika nyumbani na kupaki gari katika paking ya hapo hapo kwao kisha akatoka na briefcase yake mkononi mana anatoka kazini..

    "wewe mtoto ulikuwa wapi mwanangu"

    Mama alikuwa mlangoni akimsubiri mtoto wake arudi

    "mama, gari ilipata pancha, hivyo ikabidi niipeleke kwa fundi mana kesho ningeenda na nini"

    Sheby aliwadanganya wazazi wake hivyo huku wakiamini hilo..

    "oooohhh pole sana baba"

    "Ahsante mama... Vp baba yupo ndani"

    "ndio, ila anataka kukupa mke.. Mi nasema usikubali"

    Sasa sheby kuskia jambo la kuoa,.. Heeeeee alifurahi kinoma

    "mamaaaaa, kwanini nisikubali sasa, tena nimefurahi kinoma mama angu, yaani we acha tu, yaani saa zote naumiza kichwa nitaanzaje kisema kumbe nyie mumeshalijua"

    "sheby, acha ujinga wewe, umri wako bado ni mdogo, kwanini unataka kujizehesha mwanangu"

    Mama anakataa mtoto wake asioe kwasababu mwanamke yenyewe anaetaka kumuoa ni mtu mzima kabisaa, lakini sasa sheby yeye alijua ataoa mtu amtakaye yeye mwenyewe, kumbe keshachaguliwa mke na baba yake... Yaani huu urafiki wa kijinga kuja kusumbua watoto wenu sio mzuri,..

    "yaani ungelijua unaozeshwa na mtu kama mama yako wala usingefurahi namna hio"

    Sasa sheby kuskia hivyo, hata furaha ilikata,..

    "unasemaje mamy"

    "utajua mwenyewe... Mi nakwambia kitu cha maana we unaruka ruka tu"

    "yaani nyie wazazi mna utani nyie"

    Aliongea sheby na kujua swala hilo ni utani, wakati huo mama yake anakwenda kulala,.. Lakini ghafla mzee kaja

    "we mwehu ulikuwa wapi mpaka saa hizi"

    Aliongea baba yake huku akiwa mkali

    "mzee gari ilinisumbua kweli, imepata pancha karibia mara mbili eti"

    "sasa kwanini usingesema tuite fundi"

    "sasa kama fundi nimemuona mbele ya macho yangu.. Ina haja gani nikupigie simu sasa"

    "ok upo salama lakini"

    "nipo fresh mzee usiwaze wala nini"

    "alafu hicho kihuni chako sikitaki.. Uhuni wako uko uko mtaani sio hapa kwangu"

    "basi mzee"

    Basi kijana sheby aliingia chumbani kwake kisha kaingia bafuni na kutoka, wala hakuhangaika kula wala nini... Kalala zake mpaka asubuhi...







     





    Baada ya siku hio kupita, na leo ni siku nyingine tena,.. Lakini ghafla tunamuona kijana sheby katika mavazi tofauti kabisa tena alikuwa katika mitaa ya uswahilini,... Alikuwa akitafuta chumba cha kupanga katika nyumba zile za miti,.. Si unajua mambo ya uswahilini yalivyo,.. Kijana sheby alivaa nguo za kimaskini na sijui alikuwa na nia gani,.. Ikiwa ni mida ya saa nne asubuhi hivi, alikuwa akiingia kila kijinyumba akiwa anaulizia chumba, sasa sijui ni chumba cha nini na wakati ana jumba la kifahari huko kwao,.. Uaikute mali za akina sheby ni zile zile za akina binzuluza... Kila anapoingia anaambiwa hakuna chumba, yaani ni vijumba vya miti lakini bimejaza watu balaaa...

    "za saa hizi dada"

    Alimkuta dada mmoja hivi ambae ni FUNDI CHEREHANI..  Alikuwa ni mzuri sana na mwenye umbo la kuvutia, tena alikuwa kajitanda ushungi wake vizuri,...

    "salama habari yako"

    "safi tu... Samahani dada, eti mtaa huu naweza kupata chumba dada angu"

    Yaani hapo sheby alikuwa kama mtu mshamba mshamba hivi, kama vile kaja mjini juzi tu, kumbe ni mtoto wa boss wa maboss,...

    "hhhmm hapo jirani kulikuwa na chumba sasa sijui kilipata mtu"

    "kipi hicho"

    "nyumba hio hapo"

    "jamani dada angu kwanini siniangalizie kama kina mtu au laa"

    Jamani huyo mtoto alipoamka, yaani sheby alibakia mdomo wazi, mtoto mzuri, mweupe, shepu ya maana, afu mpole, mbaya zaidi alionekana kuwa mtu wa dini sana, kazi yake ni kushona nguo hapo barani katika nyumba ya jirani alafu kwake ndio hapo hapo anapokwenda kuonyesha chumba,...

    Sheby aliomba tu apate chumba maeneo hayo,..

    Basi dada huyo alikifungua chumba hicho kisha na kukuta hakikuwa na kitu chochote ila kilikuwa kimebomoka kidogo katika ukuta

    "kaka, hakina mtu ila kimebomoka kidogo ukutani"

    "ebu nikione.... Ahhhhhh hiki hiki kinafaa, mladi watu wasione ndani.. Sasa mwenye nyumba yupo wapi"

    "labda nimpigie simu"

    "hebu fanya hivyo basi dada angu"

    Basi mtoto wa kike huyo mwenye uzuri wa kila kona,  japo alikuwa ni mtu wa kucheka cheka hivyo lakini katulia kiukweli,.. Kavaa hijabu lakini bado umbo limejichora tu,.. Yaani sheby alitoa macho kama mbwa mwizi.... Basi mwenye nyumba alipigiwa simu na kusema kuwa anakuja kuongea na mpangaji huyo mpya... Lakini sheby kaumiza kichwa sana kuhusiana na hio sehemu.. Lakini akapata wazo..

    "Samahani dada yangu naomba tuongee kidogo"

    Sheby alimwita mpaka kwenye chumba hicho hicho lakini mtoto huyo hakuta wakae kwenye hicho chumba ambacho hakikuwa na chochote,...

    "karibu ndani, kwani hapo hakuna cha kukalia"

    Mdada huyo alimkaribisha sheby ndani kwake,... Lakini sheby baada ya kukaa kwanza kenye kochi, alijikuta anaanza kushangaa mazingira ya hapo ndani yalivyo,.. Makochi yalikuwa yamechakaa, kitanda chenyewe ni tano kwa nne (5×4), alishngaa mrembo kama huyu ataishije kwenye mazingira kama hay, afu mbaya zaidi haoni hata aibu kumkaribusha mtu, kana kwamba kesharidhika na maisha hayo, yaani hapo anahisi ndio kafika na kazi yake ya kushona...

    "kaka karibu ukae"

    Dada alizidi kumkaribisha bila kujua kuwa sheby kuna jambo analiwaza kichwani mwake na huenda likawa faida kwake.... Lakini sheby ile kupiga jicho katika mguu wa kitanda kuna kitu kaona, kilichomfanya mapigo ya moyo kumwenda mbio.. Sasa dada kumwangalia sheby usoni aligundua alikuwa anaangalia nini... Maskini dada wa watu alijiskia aibu ya mwaka...







    Kama tunavyomjua kijana sheby tabia yake katika simulizi zilizopita hua hapitwi na matamanio ya kimapenzi, katika hisia za kijana sheby yeye hata ukae uchi, hisia zake hazitopanda kwa kasi kama ilivyo katika nguo ya ndani ya kike, yaani kila mtu anajua nini kinachompa hisia za kimapenzi,.. Kuna mtu mwingine akimuona tu mwanamke kavaa dera anachanganyikiwa mpaka basi, mwingine akiona hata wigi kichwani anaweweseka halali usiku kucha, mwingine hata akiona unyayo wa mwanamke yaani anafanya kutetemeka,... Hivyo kwa huyu kijana yeye hisia zake ni hizo, akiona nguo ya ndani tu hata kama ipo wapi yeye hali yake inabadirika na kujikuta anatamani mwanamke.....

    Sheby alizidi kuiangalia chupi hio iliokuwa imetundikwa katika tendegu la kitanda,.. Hisia za mapenzi zilimpanda ingali yupo ugenini kwa watu... Yule dada aliona sheby kaangalia wapi, lakini hakuta kumshtua kuwa kwanini alikuwa akiiangalia sana nguo yake,..

    "karibu ukae kaka"

    Yule dada aliongea hivyo ili hata kumshtua kijanja janja, mana anashindwa kumwambia asiangalie nguo yake,..

    "Ahsante dada angu"

    Sheby alikaa katika makochi yaliochakaa sana, yaani hata vitambaa vyake vimechanika afu yeye ni fundi,.. Mana hawezi kumaliza faida anayopata kwa ajili ya kushona vitambaa vya makochi yake,

    "ok ahsante dada yangu.... Aaaahh Samahani sana, nikiwa naendelea kumsubiria baba mwenye nyumba, kuna jambo nataka tuliongee mana umeshakuwa jirani yangu sasa"

    Aliongea kijana sheby huku nae akiwa na busara zake, sema busara hupotea pale anapoona nguo za kike,

    "sawa tuongee haraka nirudi kazini"

    Aliongea dada huyo huku akiwa kweli ana haraka ya kutoka hapo..

    "lakini bado hatujajuana hata kwa majina mama"

    "mmhhh.. Mimi naitwa Shadya ukipenda niite Shadi"

    "waoooo jina lako limeanza kama jina langu vile"

    "kwani we jina lako nani"

    "mimi naitwa Sharbiny, ni mtoto pekee kwenye familia ya kita... Nooo... Kwenye familia ya kimaskini"

    Sheby alitaka kukosea neno akajikuta anataka kuongea eti yeye ni tajiri... Basi shadya alipata kucheka kwa kigugumizi alichokipata sheby wakati wa kujitambulisha kwa Shadi (Shadya)...

    "unanicheka si ndio"

    "No, unajua nini? Ulitaka kujitambulisha hali za wenzako na wakati hali yako inaonyesha tu ulivyo"

    "kwani mi nipoje"

    "ulivyomalizia kujitambulisha ndivyo ulivyo, na ndivyo unavyoonekana"

    Shadi alimaanisha kwamba sheby alionekana maskini kabisa, lakini weeee heeeee balaa tu, pesa zimelala hapo..

    "sasa shadi, kuna kitu cha muhimu dana nahitaji kukuomba,.. Binafsi nahisi utanikubalia ombi langu"

    "mmmhh kaka unanitisha, kwani ni ombi gani unalotaka kuniomba"

    Maongezi yao hapa ndipo yanapoanza,



    Siku hio ilipita lakini hatukujua maongezi ya akina Shasha (Sharbiny na Shadya).. Ilionekana kuna siri kubwa tumefichwa baina yao,..

    Sasa sheby akiwa ndio anatoka kazini mida ya saa 11 hivi akielekea kwa akina mary, kama unakumbuka ana kazi ya kuwafundisha wadada hao ili wapate kazi katika kampuni yao,.. Mana vyeti vyao havina sifa ya kupata kazi popote pale labda viwandani,. Sheby alipiga honi nje ya geni lakini sio kuwa alitaka kuingiza gari, ila alikuwa anawaita waje wafungue mlango mdogo,.. Mana nyumba wanayoishi ni nyumba ya kupanga,... Haikupita muda mrefu akina mary na rose walitoka na kumpokea sheby, mana alikuwa ana laptop na kibegi chenye madocoment ya kumfunzia mfanyakazi,.. Na jukumu hilo baba yake halijui kabisa, ni sheby mwenyewe ndio kajitolea kufanya hivyo,...

    "karibu boss"

    Aliongea mary lakini mtoto wa kike haondoi macho yake katika macho ya kijana sheby,...

    "waaooo Boss karibu"

    Kiukweli walimueshim sana sheby kwasababu bila sheby wasingelipata kazi pale kampuni kubwa,..

    Basi walipoingia ndani sheby kafungua laptop yake na kuanza kuwafundisha wadada hao... Aliwapa kila njia inayotakiwa kufanya kazi katika kampuni hio

    "sasa wewe rose, utamfundisha mary Kingereza, mana muda wa kufanya hivyo kwa mimi sina"

    "sawa boss, lazima sasa hivi tuanze tabia ya kuongea Kingereza humu ndani"

    "enheee hapo mtajua, mue mnaongea Kingereza wenyewe humu ndani ndio mtajua kirahisi sana, na unapoona mwenzio kakosea, unamrekebisha tuu"

    "sawa boss tumekuskia"

    Lakini mary mawazo yake yalikuwa bize kwa kijana sheby, na wakati huo sheby hajui hili wala lile kama kuna mtu anampenda kupitiliza,...

    Lakini haikupita muda mrefu, mary katoka na kuelekea toilet,.. Lakini huko toilet haikuwa toilet, bali alishika simu yake na kumtumia rose meseji kuwa Aanze kazi aliomuagiza







     



     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog