Search This Blog

Thursday 24 November 2022

KIPAPATIO CHA NANI - 4

 

     

     

     



     

    Chombezo : Kipapatio Cha Nani Season 1

    Sehemu Ya Nne (4)

     

     

    Kikosi cha Masakara walizunguka huku nakule wasiweze kumuona mbaya wao

    ”aisee huyu Mshenzi kwa sasa haonekani kama vipi tutamuibukia kesho"

    “kesho mbali jomba kama vipi twendeni Pekasi huwenda akawepo kule"

    “duuh kweli nilitaka kusahau twenzetuni"

    Wakageuza na kuelekea Viwanja vya Tanganyika Pekasi jioni hiyo kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya Gwanta na Ukwamani Madebe yeye anashabikia Gwanta moja kati timu yenye vijana wapole sana wasiopenda makuu

    Nikweli Madebe alikuwepo maeneo hayo akiifatiria mechi kwa umakini mkubwa

    ”oyaa masela si niliwaambia mimi kuwa huyu mshenzi huku hawezi kukosekana si mnamuona yule kule"

    ”sema nini Cheche

    Itabidi tunyuti kwa mda maana jamaa yupo na Wajeda pale"

    “Wajeda kitu gani bwana twendeni tukalianzishe"

    ”kama vipi wee nenda tu maana una kiherehere kama mwanamke aliyevaa chupi mpya"

    ”so mnaogopa Wajeda sio?"

    ”ndiyo maana yake"

    ”basi haina shida tunyuti"

    Wakati wanabishana pale Madebe alishawaona kilichomfanya asiweze kuwafata ni kuhusu wale Wanajeshi watatu ni moja kati ya marafiki zake wakubwa sana aliosoma nao Shule ya Msingi Kawe (A)

    Mpaka walipoingia sekondari ya Makongo baada kumaliza kidato cha nne wenzake wakaingia Jeshini huku Madebe akikataa kufanya hivyo,

    “hivi Madebe unafahamu katika maisha ya sasa kupata ajira yenye kueleweka ni vigumu?"

    Mmoja kati ya marafiki zake alimuuliza hivyo

    “ndiyo nafahamu lakini kwa upande wangu kuna ishu moja hivi naikimbizia ikitiki tu nitafurahi sana"

    “ishu gani hiyo?"

    ”kazi ya ulinzi"

    ”hahahahaha Aisee kweli wee kichaa yani ukatae kujiunga na Jeshi yenye kuweza kukupatia Pesa na baadhi ya mahitaji muhimu.

    Leo hii ukubari kuwa mlinzi yani mwezi mzima ukaisubilie Elfu tisini kama sio laki moja na nusu kama sio uchizi basi ni utaila"

    “lakini kila mmoja na maisha yake"

    “hata kama ndugu huwezi kujishusha kwa kiasi hicho"

    “embu nisubilini kwanza nakuja sasa hivi"

    Madebe akanyanyuka na kujifuta vumbi kumbe tayari alishaweza kuwaona Masakara akapiga hatua kadhaa kuwafata Masakara nao walipoona wanafatwa wakatawanyika faster kila mmoja akashika njia yake na kutokomea gizani

    Madebe hata alipofika pale hakuweza kuwaona tena akabaki kuangaza macho huku nakule kisha akasonya

    Usiku wasiku hiyo

    Madebe akiwa amelala chali kuna kitu cha ajabu sana kilitokea kwenye pembe ya Chumba Moshi mzito ulitanda ndani ya chumba kile kilionekana kama kivuli cha Jini kikiambaa kukizunguka kitanda

    Madebe aliweza kufumbuwa macho lakini hakuwa na uwezo wa kujinyanyuwa wala kufumbuwa mdomo akabaki kupepesa macho kumuangalia yule kiumbe

    “Madebee,,Madebee,, Madebee"

    Sauti nzito iliyotetemesha chumba chote kama sio nyumba nzima iliweza kusikika ikijirudia zaidi ya Mara tatu,

    Madebe alionekana kuchezesha midomo

    “nimekuja kukupa nguvu kijana kuanzia leo nitaishi ndani ya mwili wako

    Mpaka mwisho wa pumzi yako"

    Baada yule kiumbe kuzungumza hivyo akapanda kitandani na kumsimamia Madebe kwa juu halafu akafanya kama kumdondokea

    kwa kasi akaingia mwilini mwa Madebe aliyeshtuka kutoka usingizini akiwa anatweta alikaa Kitano pale kitandani huku akisikilizia mapigo yake ya moyo kwajinsi yanavyopiga kwa kasi jasho jingi lilimtoka

    Akanyanyuka na kuusogelea mlango akaufunguwa na kuelekea sebureni hakika alionekana kuwa ni mtu mwenye mawazo kupita kiasi

    “nini hiki mbona kila nikilala huwa naota ndoto za ajabu ajabu kwanini lakini?"

    Alijiuliza hivyo huku akifunguwa jokofu na kutoa chupa ya maji akakaa kwenye Sofa na kuanza kunywa maji yale

    Akachukuwa rimonti na kuwasha tv hakuweza kuangalia sana akaizima na kujilaza pale kwenye sofa usingizi ukampitia yapata majira ya saa kumi na moja alfajir Mzee Kitwana aliamka na kujiandaa kwaajili ya kuelekea kazini wakati anatoka alishangazwa sana kumuona kijana wake akiwa kajikunyata pale sebureni akamsogelea na kumtikisa huku akimwita

    “Madebe, wee Madebe,,"

    Taratiibu Madebe akafumbuwa macho

    ”vipi mbona umelala hapa sebuleni? Unaumwa au?"

    Mzee Kitwana alimuuliza Madebe akafikicha macho na kujinyoosha akapiga muyao kwa sauti ya chini sana akamjibu Baba yake

    “hapana ewe baba yangu siumwi wala nini, sema najihisi kama vile nitaiaga dunia siku si nyingi"

    Kauli ya Madebe ilimshtuwa sana Mzee wake akamshika usoni na kumpapasa

    “kwanini unatamka hivyo kijana wangu? Nambie kuna mtu au watu waliokutishia maisha?"

    Madebe hakuweza kujibu chochote kwa mbaali machozi yalianza kumtiririka ilikuwa ni Mara ya kwanza Mzee Kitwana kumuona kijana wake akidondosha chozi kwani inavyosemekana Madebe alipotimiza Umri wa miaka Tisa hakuwahi kulia alianza ununda tokea akiwa mdogo hata siku ambayo Mama yake alifariki kwa ajari ya Gari kwenye msiba watu wengi walilia hasa ndugu zake isipokuwa yeye peke yake hakulia hata kidogo

    Hakuna aliyeweza kushangaa.

    Mzee Kitwana akawa anamfuta machozi kijana wake huku akimsihi aweze kumueleza nini tatizo lakini Madebe hakuweza kumwambia muda kidogo Milfat akatoka chumbani kwake na kumkuta Baba yake akimbembeleza Madebe bila hata kuuliza kuna nini naye akaanguwa kilio kwa sauti kubwa

    “uwiiiiii, jamanii weeee Mungu wangu,,"

    Mzee Kitwana akazidi kuchanganyikiwa binafsi hakuweza kufahamu nikitu gani kinachowaliza vijana wake

    Milfat akajitupa chini na kuanza kujigalagaza mpaka Madebe aliyekuwa analia akamshangaa

    ”na wewe kitu gani kinachokuliza?"

    Mzee Kitwana alipaza sauti kumuuliza Milfat aliyenyamaza ghafla

    “kwani kaka analilia kitu gani?"

    Naye akauliza

    ”inamaana kaka yako akilia na wewe ndiyo ulie sio?"

    ”mi nilidhani kuna msiba nikaona niunge tera"

    “pumbavu zako wewe huo msiba wa bibi yako"

    Milfat akaanza kulia tena huku akisema njooni mnibembeleze na mimi sasa

    Mzee Kitwana akaona kama vile binti yake kawehuka alichokifanya ni kumuaga Madebe na kumsihi awe makini sana kisha akaelekea zake kazini

    “ehee kaka nimekumbuka kitu"

    Milfat aliongea hivyo huku akijifuta machozi akakaa kwenye sofa

    ”kitu gani tena?"

    ”unampata Hashim?"

    “Hashim yupi maana wapo wengi?"

    “si yule ambaye Baba yake anamiliki Mabasi ya Nasset"

    “kumbe kale kajamaa Kisharobalo ehee kafanyaje?"

    ”yule mkaka ni msumbufu balaa kila akiniona haishi kunitongoz,,,,,

    Milfat hata hakumalizia kuongea Madebe alishanyanyuka na kutoka nnje alitembea kwa kasi kuelekea Stendi,,

    Milfat alijaribu kumwita huku akimkimbilia pasipo kufahamu kitakachoenda kumkuta Hashim huko ni kisanga





    **********************

    “kumbe kale kajamaa Kisharobalo ehee kafanyaje?"

    ”yule mkaka ni msumbufu balaa kila akiniona haishi kunitongoz,,,,,

    Milfat hata hakumalizia kuongea Madebe alishanyanyuka na kutoka nnje alitembea kwa kasi kuelekea Stendi,,

    Milfat alijaribu kumwita huku akimkimbilia pasipo kufahamu kitakachoenda kumkuta Hashim huko ni kisanga



    Songa nayo

    Sasa



    “kakaa,, kakaa,,"

    Milfat alimwita Madebe huku akimkimbilia Madebe akasimama

    “nini sasa Sister?"

    “sio nini bali nataka kufahamu unaelekea wapi?"

    “kwani wewe unavyohisi nitakuwa naelekea wapi?"

    “halafu tabia ya kuniuliza swali wakati langu hujanijibu sipendi ujuwe"

    ”basi samahani Sister"

    Madebe akaomba msamaha kisha akaendelea na safari

    “sasa mbona unaondoka wakati haujanijibu unaenda wapi?"

    “kwani wewe unataka nielekee wapi?"

    “mi sijui ila isijekuwa unamfata Hashim ili ukampige"

    “walaa sina niya hiyo"

    “siku zote unasemaga hivyo hivyo"

    “Sister wee rudi nyumbani wacha mi nielekee kwa Mamdogo"

    ”mmh kama kweli unaenda kwa Mamdogo basi twende wote"

    “haina shida nenda basi kavae viatu mi nakusubiria hapa"

    Milfat akajiangalia miguuni nikweli alikuwa pekupeku akakimbia mbio kufata viatu

    Aliporudi ile sehemu ambayo Madebe alimwambia anamsubiri hakumkuta Kitambo mwenzake alishaondoka akaishia kusonya na kurudi alipotoka

    Tukija upande fulani hivi kulikuwa na kikundi cha vijana wakubwa na wazee walionekana kila mmoja akiwa bize katika kufanya kazi yake huku wengine wakipiga Stori za hapa na pale

    “oyaa wee Jeff embu punguza kelele hizo"

    “acha ufala wewe kama unaona kelele si uwende ukalale na mkeo tambuwa Mwanaume hapa nipo kikazi zaidi"

    “katika kazi hiyo nayo kazi bwege wewe sasa kwataarifa yako naweza nikakuajiri kwenye kampuni yangu nikakulisha na kukuvisha wewe na ukoo wako wote"

    ”sasa hayo matusi ndugu"

    “matusi wapi wakati nakwambia ukweli embu acha kugongagonga hivyo vyuma njoo uchukuwe pesa hii ukalale"

    “ahaa Hashim mwana embu acha dharau za kiboya unamdharau mshikaji kisa wewe familia yenu ni matajiri sio!"

    “hapana mi wala sijamdharau bali nilimtaka tu aache kelele"

    “sasa tokea lini fundi magari akaacha kugonga vyuma hii ndiyo kazi yake unataka kunambia ukiingia Disco utataka DJ azime mziki kisa anapiga kelele

    Wakati makelele ndiyo ajira yake"

    “poa basi yaishe Jomba oyaa Jeff usimaindi wala nini matani tu kwani unadhani mi sijui kama hapa kijiweni kuna kelele zakila aina"

    Wakati Hashim akiongea hivyo Mara Madebe akawasili pale kwanza akasalimia baada kuitikiwa akakaa kwenye Benchi Mzee mmoja akaghuna na kunyanyuka akaondoka taratiibu

    “nakuona Mzee wakazi Madebe mwenyewe ngumi chuma chuma baba"

    Hashim alianza kujishauwa alishaweza kufahamu ujio wa Madebe pale ni kwaajili yake

    Hashim anajulikana kama mmoja kati ya vijana watukutu Mbabe mwenye kutumia pesa za Baba yake kuwaonea na kuwanyanyasa masikini pia ana kauli za dharau kupita kiasi akimuhitaji Mwanamke yoyote yule kumkosa kwake ni mwiko

    Mabinti ambao walidiriki kumkataa wakaishia kutekwa na kubakwa

    Hakuweza kufanywa chochote hata ukienda kushitaki polisi utaambiwa tu wee nenda nyumbani mtuhumiwa atakamatwa

    Licha ya ubabe wake wote kitaa lakini moyoni mwake alikuwa anamuhofia mtu mmoja tu si mwingine ni Madebe yani haogopi polisi hata wawe mia moja lakini kwa Madebe anakuwa mdogo kama vile kidonge cha pilitoni

    Madebe alimuangalia Hashim kwa kumkazia macho akakohoa kulainisha koo kisha akamuuliza

    “wewe ndiyo Hashim?"

    “ndiyooo,,ndiy mimi mkuu kwani nimefanyaje?"

    Hashim aliitikia kwa kubabaika

    ”una Dada?"

    ”ndiyo ninao kwani wamefanyaje?"

    “nikikuuliza swali jibu kama nilivyo kuuliza usiongezee neno lingine"

    “sawa kaka kwani Milfat kakwambiaje kuhusu mimi?

    Ghafla Hashim akapigwa kofi huku akikalipiwa

    “wee pusi nimekwambia jibu swali"

    Hashim alipepesuka na kutaka kudondoka chini

    Akadakwa na kuweka sawa

    “bila shaka umeweza kutambuwa kosa lako sasa basi nakupa onyo kuhusu Milfat sio dizain ya wanawake unaowachezea unakumbuka kuna siku ulisema Wanawake nikama choo ukijisia haja unaenda kukojoa ile kauli sio kwa Milfat Dada yangu sio choo Milfat yupo kwenye himaya ya Tiger

    Nitakularuwa na kukutawanya fala wewe"

    Madebe alifoka huku akimkazia macho kumuangalia Hashim aliyekinga mikono kuomba msamaha

    “wa kubwa mi naenda kama vipi amani au sio"

    “sawa mkubwa bila shaka ameweza kukusikia hatorudia tena"

    Madebe baada kutoa onyo kuhusu Dada yake akaaga na kuondoka huku nyuma Hashim alichekwa na kuzomewa kitu ambacho kilimfanya asiweze kukaa tena pale akaelekea nyumbani kwao

    Akiwa njiani aliitoa simu yake na kumpigia Baba yake

    “Baba mwanao leo nimepigwa nimeaibishwa mbele ya umati wa watu"

    Hashim bila kutoa salamu alianza kumlalamikia Baba yake

    “nani kakutendea hivyo?"

    “Madebe Baba"

    Alipojibu tu simu ikakatwa akaishia kusema haloo haloo hata alipojaribu kupiga tena akajibiwa simu inatumika

    Kitendo cha kijana wake kumshtakia kuwa kapigwa kilimchukiza sana bwana mkubwa Abraham mmoja kati ya Matajiri wakubwa katika ukanda wa Afrika inavyosemekana Mzee Abraham anashika namba tatu kwa utajiri Afrika Nzima yote sababu ya vitega uchumi alivyokuwa navyo

    Anamiliki Viwanda takribani ishilini vyenye kutengeneza vitu mbalimbali kwa mahitaji ya Nyumbani maofisini kama vile sabuni mavazi vifaa vya kielotronik tv pasi feni nakadharika

    Pia anamiliki visima vya mafuta idadi isiojurikana huko uwarabuni achilia mbali

    Licha ya utajiri aliokuwa nao lakini bwana Abraham alihitaji kuishi maisha ya kawaida sana sio

    Ajabu kumkuta kwenye vijiwe vya kahawa akicheza Bao huku akipiga porojo kitu ambacho alikirithisha mpaka kwa Watoto wake

    Waliokulia maisha ya Uswahilini

    “wewe ni Afande Mwita?"

    “ndiyo mkuu"

    ”sasa nataka uwandae vijana haraka sana mwende mkamkamate Madebe"

    ”Madebe yupi Mzee?"

    ”yule nyau wa Mzee Kitwana"

    Simu ikakatwa Afande Mwita kijasho kilimtoka japokuwa hapo ofisini kulikuwa na feni iliyokuwa ikipepea kwa kasi.

    Kiukweli aliona wamepewa kazi nzito sana yani waingie

    Lugalo kumkamata kijana mtukutu kama Madebe akavuta pumzi kwa ndani na kuzishusha akapiga simu sehemu fulani

    ”unataka kusema mida hii yupo maeneo ya Kawe?"

    ”ndiyo mkuu nimemuona kakatiza sasa hivi anaelekea maeneo ya Hipro"

    ”asante kwa taarifa"

    Afande Mwita alihitaji kufahamu kwa wakati huo Madebe atakuwa wapi?

    Akakata simu kisha akasimama na kuelekea nnje

    “aisee Sebastian kuna kazi moja nyeti sana imeweza kutufikia muda huu"

    “kazi gani hiyo?"

    “kuhusu kwenda kumkamata Madebe"

    ”mmh Madebe yupi? Isijekuwa yule jini mtu"

    “ndiyo yeye huyo"

    ”aisee Mwita bila shaka unajitafutia matatizo ndugu yangu tunaanzaje kuingia Kambi ya Jeshi?"

    “kwani tunaenda kumkamata ni Mwanajeshi au ni Raia wa kawaida?"

    “hata kama ndugu tambuwa yule Mtoto baba yake ni mkorofi sana"

    ”unataka pesa au hutaki?"

    ”kwanza hiyo kazi umepewa na nani?"

    “na Mzee Abraham"

    “daah kama ni yeye wacha nikamkamate"

    Baada kuambiwa kuwa kazi imetoka kwa Mzee Abraham mtu ambaye anamwaga pesa kama hana akili nzuri

    Ispekta Seba alijikuta akikubari kwenda kumkamata Madebe akamwita mmoja kati ya Maafande akazungumza nae kwa Uchache wakati

    Afande Mwita akiwapa maelekezo wapi wanaweza kumpata Madebe

    Kisha wakaondoka

    Nikweli Madebe alikuwa yupo maeneo ya Kawe kwa mama yake mdogo

    Alionekana kuweka mkaa kwenye jiko

    ”Madebe mwanangu shida yote ya nini embu acha Dada yako Khailat atakusongea huo Ugali"

    “hapana Mama nitausonga mwenyewe nyie endeleeni na kazi zenu"

    Siku zote Madebe huwa hapendi kupikiwa na mwanamke akidai vyakula vyao ni vilaini sana havimpi nguvu yeye anataka Ugali mgumu yani ukipigwa na tonge usoni lazima uchanike

    Sio ugali laini kama unamlisha kibogoyo

    Wakati anaendelea kupepea moto

    Ispekta Seba akiwa na mwenzake wakawasili maeneo yale

    Wote walikuwa wamevalia sale za kazi

    “bila shaka wewe ndiyo Madebe?"

    Ispekta Seba akauliza aliuliza hivyo sio kama amfahamu bali alitaka kuonyesha ukakamavu mbele ya kiumbe hicho

    “ndiyo Mimi niwasaidie nini wakubwa?"

    Madebe akaitikia na kuwauliza

    “unahitajika kituoni sasa hivi"

    Yule Afande mwingine akajibu

    “usiseme sasa hivi wakati mnaliona hili jiko hapa nakoleza moto nataka ninyong'orote

    Kitu cha Nguna sasa basi mnaweza mkakaa pale

    Mnisubiri nipike nile nioge halafu ndiyo tuelekee huko kituoni au vipi?"

    ”sawa haina shida kiroho safi tutakusubiria"

    Basi Madebe akaendelea na kazi zake huku Ispekta Seba na mwenzake wakipiga stori za hapa na pale

    “kwani mmetumwa na nani kuja kunikamata?"

    Madebe akauliza swali wakati huo

    Alikuwa anakata kachumbari

    “Mzee Abraham ndugu sijui umemkosea kitu gani?"

    ”yule Mzee fala sana Mamae zake nikitoka huko kituoni nitaenda kumuonyesha kwanini nikiamka Asubuhi natafuna kokoto

    Oyii karibuni tule"

    “ahaaa si tayari tushakula Mzee"

    Ispekta aliitikia kwa kubabaika





    **********************

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog