Chombezo : Wapangaji Wenzangu
Sehemu Ya Tano
(5)
Kuna wakati mwanaume unapofikwa na jambo
ni lazima ufanye maamuzi ya kiume,... Kiukweli Swalehe alimpenda sana Zahra
lakini kwa nyodo zake akahisi Swalehe sio mtu sahihi kua kama mume wake, Swalehe
hakukata tamaa alisota na kusota juu ya Zahra, mpaka ikafikia wakati anapewa
ushauri na baadhi ya kaka zake ambao ni mafundi wake, hivyo kuanzia siku hio
akaacha kumfuatilia Zahra.....
Zahra baada ya kufanyiwa uhuni
ndipo akajua kuna umuhimu wa kumpenda mwanaume aliekupenda na haijalishi ana
kazi gani... Kwasababu mpaka mwanaume kukutaamkia anataka kukuoa, tayari
keshajijua anaweza kukuachia pesa ya kula kila siku,...
Zahra
alipigana sana juu ya kumrudia Swalehe mpaka akafanikiwa kumpata, lakini Swalehe
hakua na upendo kama ule wa zamani hivyo hata kumkubalia kwake ni kama kishingo
upande tu,.... Na ilifikia hatua mpaka akataka kulala nae, sema kuna vikwazo
vilijitokeza mpaka akaamua kumuacha, lakini ilibaki kiduchu tu Zahra aliwe na
Swalehe,.. Na Swalehe akamuahidi Zahra kuwa akirudi watafanya mapenzi,.. Lakini
sasa Swalehe aliporudi kakutana na mtoto wa kitanda aitwaye Farida, hivyo hamu
na Zahra ikawa haipo tena....
Leo usiku walikutana getini,
Zahra akiwa anatoka dukani kununua mahitaji madogo madogo, na Swalehe alikua
akitoka katika mishe mishe zake... Zahra aliweza kumzuia Swalehe asiingie ndani
kwanza, wafanye mazungumzo yao hapo hapo nje
"swai... Kwanini
unanitesa hivyo.. Yaani unalala na mtu mshamba vile, hajui hata kuoga... Kwanini
lakini unanitesa?? Niambie kama hunipendi"
Aliongea Zahra huku akilia
sana na hapo anatoka dukani kununua vitu vya kupika...
"Zahra...
Kiukweli labda uniache tu kwa sasa... Yule msichana wa watu ana kosa gani...
Msichana wa watu hana pakulala.... Mwache"
"nimeshajua hunipendi swai...
Niambie tu usije ukanichezea"
Aliongea Zahra mana hamuelewi
swai, kwanini alilala na yule mwanamke,
"lakini zaru, hata wewe mwanzo
hukua ukinipenda.... Hata mimi naweza kusema tuwe kaka na dada
tu"
Aliongea Swalehe tena kwa kujikaza sana,.. Na wakati huo Zahra
kabaki mdomo wazi....
"ivi swai una akili wewe... Yaani mimi na wewe leo
tuwe kaka na dada"
"kwani ajabu... Mana mwanzo hata urafiki na mimi
ulikua hutaki... Lakini mimi sitaki kulipiza baya kwa baya.. Mimi nataka tuwe
kaka na dada tu"
Aliongea Swalehe, tena kwa kujiamini haswa,... Sasa
hatujui Swalehe anajivunia nini kwa hilo mana ana mpango wa kuoa... Na alio
mlenga ni Zahra...
"swai,... Yaani umeuchungulia uchi wangu afu
unaniambia mambo ya kaka na dada... Niambie huo ukaka na dada unakujaje baina
yetu"
Aliongea Zahra tena akiwa anatetemeka mno,.. Mana waliingiziana
mambo lakini hawakufanikiwa hata kukatika viuno vyao, kukawa na vikwazo, sasa
Zahra analia kwakua Swalehe alisha mchumgulia uchi wake afu sasa hivi analeta
mambo ya kaka na dada....
"Zahra, mi nadhani utaelewa tu huko mbele,..
Tafadhali sana, tafuta mwanaume mwingine... Sihitaji kuoa kwa
sasa"
Aliongea Swalehe huku Zahra akimuangalia swai kwa jicho la
hasira
"najua kisa ni huyo malaya wako mchafu kuoga... Sasa tutaona sasa
mimi na yeye ama zangu ama zake"
Aliongea Zahra kisha akaingia ndani kwa
hasira, tena huku akitetemeka sana.... Mana hakuamini kama Swalehe angelimjibu
hivyo kua kuanzia leo tuwe kaka na dada, yaani ndugu
kabisaaa...
Baada ya Zahra kuingia kwao kwa hasira,.. Swalehe
nae akawa anaingia kwake,.. Lakini ile anafika tu mlangoni akakutana na farida
kabeba safuria ya ugali tena ikiwa ina moto...
"we farida...
Unakwenda wapi sasa"
"ndugu yako kanifukuza"
"ndugu yangu??...
Ndugu yangu nani"
"yupo huko ndani... Sijui ni mama yako mdogo sjui ni
shangazi yako..."
Sasa farida aliposema hivyo, Swalehe akajua huyo ni
mama Mwajuma ndio kaanza visa...
"rudisha hio safuria
ndani"
"wewe, unarudi kufanya nini tena huku"
Aliongea
mama Mwajuma, bila kujua na swai yupo nyuma yake
"we mtoto hivi
wewe ni kiburi sana ee"
Mama Mwajuma alikwenda tena kuzima jiko...
Swalehe akaingia na kuliwasha tena,... Safari hii kawasha
Swalehe..
HAPO NDIPO TULIPO ISHIA JANA
Sasa
Swalehe baada ya kuliwasha jiko hilo, mama Mwajuma akapunguza mikwara.... Mana
kazima yeye lakini kawasha Swalehe, na ndio maana pale juu nikasema mwanaume ni
lazima muda mwingine uwe na maamuzi ya kiume, Swalehe aliona mbali sana hivyo
aliamua kama kuna ubaya wacha uwe ubaya tu....
"swai, kwani vipi tena
baba"
Aliongea mama Mwajuma tena kwa kitumia pua... Mpaka farida
alishangaa sana, kwanini mama mtu mzima anamlegezea mtoto sauti kiasi
hicho...
"aahhh Samahani mama mwaju,.. Kwa sasa atakua akinipikia huyu
msichana..."
Aliongea Swalehe huku akimshika farida
begani....
"kwanini sasa swai... Mimi ndio mwenye haki ya kukupikia..
Kumhuka huyu ulimpa hifadhi tu"
Aliongea mama Mwajuma kwa sauti ile ile,
na hata macho yake hayakua makali juu ya Swalehe....
"ni kweli, lakini
nikiwa kama binadamu... Huyu msichana hana pa kulala mpaka sasa,... Na dada yake
anaendelea kumtafutia kazi"
Aliongea Swalehe,... Sasa mama Mwajuma
akajua kuwa kuishi kwa msichana huyu, hapo kwa swai, kutaleta matamanishi ya
kimwili, bila kujua farida kaamkia hapo hapo tena kaliwa vizuri sana na
Swalehe....
"sasa swai, mimi nina mdogo wangu wa kike... Naomba
nimuombee akaishi nae, ni hapo jirani tuu"
Aliongea mama Mwajuma, mana
aliona kwa uzuri wa farida, yaani haingii hata tone, japo mkubwa dawa lakini sio
kitandani jamani.. Mtoto ni mtoto na utamu wa mtu mzima na mtoto, ni tofauti
kabisa... Ni kama nanasi na papai... We mwenyewe unajua kitamu ni kipi, lakini
vyote vina kazi zake mwilini, ila utamu ni tofauti kabisa...
"yupo wapi
huyo mdogo wako"
"hapo nyumba ya pili tu"
"tutajua kesho
tunafanyaje, lakini kwa leo wacha apate hifadhi hapa"
"sawa,.. Kwahio
nirudi na chakula changu"
"Samahani lakini... Huenda nimekupata hasara
ya mchele... Kiukweli ungerudi nacho tu"
Aliongea Swalehe huku mama
Mwajuma akibeba mabakuli yake ya vyakula,....
"mwanangu kesho utapata pa
kulala sawa mama"
"sawa"
Aliongea mama mwajuma kisha huyoo
akaondoka zake.... Swalehe akajitupia kitandani wakati huo
kachoka....
"maji tayari, wacha nikupelekee bafuni"
Duuuuuu
Swalehe haamini kuambiwa maji tayari,... Wakati yeye alikua akiwaza ataanzaje
kuoga maji baridi, sasa kayakuta yamesha pashwa.. Wakati huo hata ugali
umeshaiva,.. Basi farida alipeleka maji bafuni.. Alipokuja alianza kumvua
Swalehe shati... Eeehh mpaka Swalehe anajihisi kua na mke, wakati walaaa..
Farida kweli alikua na mbinu za kijijini, mbali na ushamba wake lakini aliweza
kumteka Swalehe.... Sasa Baada ya kumvua shati, Swalehe alishangaa kasukumwa
kitandani,.. Mara kavuliwa mkanda na suruali ikatolewa... Akabaki na boxer peke
yake...
"mbona haraka hivi"
Aliongea Swalehe huku farida
akiangusha jicho la mahaba, bila kumjibu kitu....
Farida aliishika ile
boxer na kutaka kuivua, lakini swai alikataa...
"Unakwendaje na kuoga na
boxer?... Hebu vua nitaifua kesho"
Aliongea farida,.. Sasa ile Swalehe
anataka kujibu tu.. Saa mingi sana boxer ipo chini, sasa zakhari imebaki wazi..
Farida akaishika shika kisha akamfunga taulo,...
"twende
bafuni"
Farida aliongea hayo huku akimvuta waende bafuni... Wakati huo
Swalehe kaduaaa, yaani haamini vitu anavyo fanya farida,..
"kuoga wote
au"
"kwani kuna ubaya"
"hapana farida ... Mi najiskia aibu kuoga
wote"
"mbona leo alfajiri hujaskia aibu kunipanua mapaja
yangu"
"ahh tuyaache ayo... Hii kuoga niache niende
mwenyewe"
Aliongea Swalehe, na farida ni msikivu...
"sawa
basi... Wacha nikuandalie kachumbari, au hupendi"
"napenda sana... Kiwe
na Pilipili kwa mbali"
Aliongea Swalehe huku akitoka kwenda bafuni,...
Ikiwa ni mida ya saa tatu za usiku...
Kesho yake asubuhi,
Swalehe anakuja kuamka, kakutana na maji ya kuoga.. Aliporudi kakutana na chai
ya nguvu,..
"swai??... Jana usiku ulifanya kazi ngumu sana... Pata supu
kwanza kabla ya vyote"
Aliongea farida akimaanisha kwamba jana usiku
Swalehe alikata viuno sana,... Hivyo aanze kugonga supu kwanza... Basi Swalehe
alipata chai nzito ya mtoto wa kitanga.. Msambaa mwenzie,.. Baada ya Swalehe
kumaliza chai alitoka kwenda kazini,... Kama kawaida kamuachia pesa ya mezani
shilingi elfu tatu,
Baada ya masaa kadhaa farida kampelekea
dada yake elfu moja, ili ampikie mtoto, mana shemeji yake hakuacha
kitu...
"farida.... Ahsante sana... Yaani hapa nilikua nawaza nalujaje
hapo ndani kwako hata nipate kikombe cha uji"
Aliongea Semeni huku
akilia kabisa, mana mume anamnyanyasa sana, yaani hata pesa ya matumizi haachiwi
hata kidogo,..
"dada, Usijali, kidogo tutakula wote..."
"haya
niambie,... Na leo kakukandamiza"
"heee, sasa hivi ni kama dozi dada...
Naliwa mpaka naskia raha yani"
"wacha weee.. Mama mwenye
nyumba..."
"mmmhhh dada, bado... Afu kuna yule mama kasema eti niende
kuishi kwa mdogo wake"
"mama gani tena"
"yule chumba
kile..."
"mama Mwajuma"
"ndio"
"kwanini.. Na siku wakati
namuomba, kwanini asikusaidie"
"mimi sijui dada"
"hakuna
kwenda... Akalale mwenyewe.... Wewe tayari umeshapata mume, mdogo wangu tulia..
Wanaume wa sasa ni wababaishaji tu.. Wewe ni mtoto wa kitanga, hata kama hujui
sana mpe yele ya kishamba shamba...sema jimwanaume langu ni lilevi tu... Lakini
ningempa mapenzi mpaka adate mwenyewe"
Aliongea Semeni huku farida
akicheka
"sasa kwanini hajadata"
"mmmmhhh mlevi?? Mlevi na
mapenzi wapi na wapi? Bora mnywaji kuliko mlevi"
Basi walimaliza kuongea
mtu na dada yake, sasa kaja ndani kwake kakusanya nguo chafu kisha akawa
anazifua
"enheeeeeee... Nilikua Nakusubiri sana kwa ham we
malaya"
Alikua ni Zahra, tena wakati huo kafunga Kibwebwe
kiunoni...
"heeeeee zaru, haya cha kuniita malaya mimi kwa kosa
gani"
"muone vile.. Eti kwa kosa gani.. Kwani hulijui kosa lako
wewe"
Aliongea zaru tena wakati huo ana hasira mno
"lakini mimi
sijui kosa langu... Na kama ni gesi, sikumwambia kua wewe ndio
ulitumia.."
Aliongea farida akidhani labda Zahra kaja kwa kesi ya gesi
kuisha...
"we msenge nini wewe... Mimi naongelea mambo ya gesi
hapa..."
"Zahra... Tafadhali sana, mimi sihitaji ugomvi na
wewe.."
"ila unahitaji ugomvi na nani"
"sitaki
kabisa"
"kwanini kupewa hifadhi tu unachukua waume za
watu"
Aliongea Zahra, sasa kule ndani... Leo mama Mwajuma hajaenda
kazini, saa ngapi hajasikia kuwa kwanini farida anachukua waume za
watu...
"we zaru? Kuna kitu nimesikia ukikiongea, kama kimenigusa
hivi"
Aliongea mama Mwajuma huku akisogea,.. Kama unavyojua wapambe
tena... Baadhi ya wapangaji nao wakaanza kitoka..
"heheheeeee
haaaalooooo...."
Kuna mpangaji kacheka cheko la
kishangingi...
"mama Mwajuma.... Huyu mdogo wake Semeni ni nyoka...
Anauma na kupuliza huyu"
Aliongea Zahra, huku mama Mwajuma nae
akisema
"we zaru... Kwani kaiba mume wa nani"
Mama Mwajuma
Alimuuliza Zahra kuwa kwani kaiba mume wa nani...
"kamchukua mume
wangu... Sijui kampa nyuma.. Mshenzi huyu natamani kumpiga mimi
huyu"
Aliongea Zahra huku akitishia kumpiga,.. Sasa zaru hajaolewa na
wapangaji wanashangaa kuskia zaru kaibiwa mume.. Mume gani huyo
asiojulikana....
"we zaru uliolewa lini wewe... Na huyo mume ni nani...
Au wataka kumpakazia mwenzio tu"
Aliongea mama Mwajuma bila kujua Danga
lake ndio huyo huyo mume anae gombewa...
"we mama wewe.... Ina maana
unavyonikuta na Swalehe kule ndani, unaona ni mgomba yule... Yaani na utu uzima
huo hujavuta tu picha kua nina mahusiano na Swalehe... Na huyo Swalehe ndio
analala na huyu malaya hapa..."
Aliongea Zahra, sasa mama Mwajuma leo
ndio anajua kumbe huyu Zahra ana mahusiano na Swalehe,... Sasa mama Mwajuma
kamgeukia Zahra...
"haya wewe huo uhusiano na yule kijana umeanza lini
na umalaya wako.. Hivi zaru utakuwa malaya mpaka lini.. We juzi si ulikua na
mwanaume wewe... Sasa kwa taarifa yako wewe ni mtoto sana kwangu... Sasa ama
zako ama zangu"
Mama Mwajuma anachimba mkwara kwa Zahra,... Sasa
wapangaji nao wanashangaa kwanini mama Mwajuma kaingilia ugomvi wa
watoto
Sasa farida anashangaa kua huyu mama na Swalehe wakoje,.. Japo
jana walibishana pia lakini bado hajajua... Sasa farida akavunja ukimya na
kumuuliza mama huyo..
"Samahani mama angu... Kwani wewe na Swalehe ni
mtu na mtoto wake, au ni mtu na shangazi yake"
Aliuliza farida mana yeye
hajuagi kuwa huku mjini mambo ni watoto kwa watu
wazima....
Farida yeye ni mtoto wa kijijini, hakuwahi
kusikia kuwa mjini kuna wamama watu wazima ambao wanapenda wavulana wadogo, tena
anampenda mvulana ambaye ni mtoto wake hata wa tatu,..
"we nawe
unauliza swali gani hilo... Swalehe ni kama kijana wangu"
Aliongea mama
Mwajuma, huku akiondoka
"kumbe wewe unampenda swai, heheheeeeeeee
haaaaloooo... Nilikua sijui kumbe unamegwa na kitoto kidogo vile"
Zahra
aliongea hayo huku akiweka vidole juu tena kwa kuruka ruka,.. Farida roho
ilimuuma sana japo haamini kama kweli mtu mzima kama huyo ana mahusiano na mtoto
mdogo kiasi kile,... Yaani kadiriki kumvulia mtoto chupi na kumpanulia
mapaja,...
Sasa mama akarudi mbio kija kupigana na Zahra,.. Mama Mwajuma
alikua na mwili wa unene kiasi, hivyo Zahra akamkimbia na pia ni mtu mzima, na
kama unavyojua ngumi za kike, kama hawajuvuana nguo ni bahati... Mana zao ni
kuvuana nguo ili anapozuia asivuliwe ndipo hapo anapokula kichapo... Sasa Zahra
akamuepuka mama mwajuma na kukimbia ndani
"mbona unakimbia, wewe si
msichana mwenye nguvu... Toka sasa nje"
Aliongea mama Mwajuma wakati huo
farida anaendelea kufua nguo za Swalehe pamoja na zake,....
"halafu na
wewe... Utakiona hiki chumba kigumu"
Aliongea mama Mwajuma huku
akimnyooshea farida kidole,...
"hehehehehehe wewe mama mwaju, haya
kumchukia mdogo wangu huko kisa nini"
Aliongea Semeni ambaye ni dada
yake farida,...
"huyu mdogo wako malaya... Kafuata kazi mjini au kaja
kutafuta wanaume"
Aliongea hivyo mama huyo huku mama abu akiongea
kuwa
"sasa mama mwaju.. Huyo mwanaume alie nae ni wako?"
"hata
kama sio wangu, lakini sio kwa kutembea na wanaume wa humu ndani na kujifanye ni
mumewe"
Aliongea mama mwajuma kisha akaondoka, lakini wapangaji wote
wameshajua kuwa mama Mwajuma ana mahusiano na Swalehe,.. Farida alianza kulia
pale pale chini,..
"farida, pole... Ina maana umempenda Swalehe kiasi
hicho"
Dada yake farida alimuuliza mdogo wake, mana kwa mara ya Kwanza
kumsikia kuwa anampenda Swalehe kutoka moyoni, alihisi ni janja ya wanawake kama
wanavyosema,.. Sasa Semeni leo ndio anashangaa kumbe farida anampenda Swalehe
Kiukweli ukweli na sio uongo, yaani hatanii...
"dada niache,... Ina
maana kumbe huyu mama mtu mzima anatembea na mtoto kiasi kile"
Aliongea
farida huku akilia, mara Zahra katoka
"we malaya, unamlilia nani? Kama
ni swai wangu utaishia kuchezewa tu"
Aliongea Zahra, mara Semeni kaamka
nae,... Semeni sio mama mtu mzima ni msichana tu na mtoto wake wa kwanza ana
miaka miwili,.. Hivyo bado ni mbichi mbichi, sema shida tu ndio zinamzehesha...
Sasa ikawa ni ngumi baina ya mama abu na Zahra,... Kazi iliopo ni ya wapangaji
kuwatetea wasiendelee kupigana,.. Na yote hayo sababu ni Swalehe,.. Mtoto wa
watu hana kazi ya maana lakini anagombaniwa kama mayai ya mbuni,.. Basi ugomvi
uliisha na kila mmoja katulia kwake,.. Kama kawaida farida humpatia dada yake
unga ili aweze kupata chakula mana mumewe haachagi pesa ya kula, kwani ni yeye
na pombe tu,..
Jioni Swalehe alirudi nyumbani, lakini alimkuta
farida anapika huku akilia,.. Yaani haamini kama mama mtu mzima kama yule
anampenda Swalehe mtoto mdogo sana kwake,..
"alaaa, we una nini... Kuna
msiba"
Aliuliza Swalehe, farida alimkumbatia Swalehe huku akiendelea
kulia..
"swai, nakupenda sana... Nakupenda, lakini nimeumia sana pale
nilipojua kuwa mama mwajuma una mahusiano naye.... Ina maana umetembea na yule
mwanamke?? Nijibu swai, ni kweli umetembea
nae?"
"ndio"
"swaaaaaiiiii.... Si kama mama yako yyle jamani,
ina maana umerudi ulipotoka swai kwanini lakini"
"we nani kakupa hizi
taarifa"
"kila mtu anajua"
"basi pole... Ila nimeachana
nae"
"umeachana nae gani wakati anatishia watu"
Aliongea farida,
na hapo Swalehe ndio anajua ivi kumbe farida anampenda, mana alijua anamtumia tu
kwakua hana pa kuishi...
"ebu pika chakula kwanza tutaongea"
"mi
nataka tuhame hapa... Sitaki kuumia kila siku"
Farida alitoa wazo la
kuhama hapo mana hatoweza kugombana na majirani zake kisa
mwanaume,....
"sasa huyo mama ndio anakutishia au"
"sio mama
Mwajuma tu.. Hata Zahra ananisumbua sana"
"basi we pika
kwanza..."
Swalehe aliona ni jambo la kawaida na uzuri wa Swalehe ni
muwazi, kama jambo ni la kweli anakubali mana hata akificha ni kazi bure... Sasa
wakati farida anachota unga,.. Swalehe aliona mbona unga wa juzi tu umepungua
kiasi hicho.. "
"huo unga si wa juzi tu kama sio jana"
Aliuliza
Swalehe, hapo farida akaanza kuogopa... Mana kweli unga hauna hata siku mbili,
lakini umefika katikati... Uzuri ni kwamba wote wamekutana wasema kweli,..
Farida alipoulizwa hivyo,.. Pale pale alimuangukia Swalehe na kusema ukweli wote
kuhusu yeye na dada yake.... Swalehe alimuelewa kisha akaenda zake
kuoga...
"Unakwenda wapi na panga"
Aliongea farida baada ya swai
kutoka na panga usiku kama saa tatu hivi..
"nipo hapa nje"
"na
hilo panga"
"tulia"
Farida aliogopa sana kwa kitendo cha Swalehe
kutoka na panga usiku...
Saa nne na nusu Swalehe anarudi huko
alipo kwenda,... Lakini shati alilovaa lilikua na damu damu.. Farida alizidi
kuogopa kabisa, yaani siku hio hakutamani kabisa kulala na
Swalehe...
"swai, umefanya nini lakini"
"tulia wewe.... Ulizani
dawa ya maumivu ni parasetam peke yake"
Aliongea Swalehe, lakini farida
hakiyaelewa maneno hayo,.. Swai alichukua maji ya baridi na kwenda kuoga kwa
mara nyingine tena,.. Aliofanikiwa kuona damu kwenye nguo ni
farida...
Wakati huo huo Swalehe akiwa bafuni, ghafla geti
kubwa likasukumwa,...
"mama abu... Mama abu"
Aliingia mtu na
kuita kwa nguvu akimaanisha Semeni ndie alieitwa
"abeee"
"mume
wako atakufa..."
Aliongea mtu huyo huku mama abu akianza kuchanganyikiwa
kwa kuskia mume wake atakufa,..
"Uuuuuuuuuwiiiiiiii mume wangu kafanya
nini tena"
Alipiga kelele mama abu huku mjumbe akisema
"chukua
majirani zako twende tukambebe tumuwahishe hospitali"
Aliongea mjumbe
huyo... Baadhi ya majirani wakatoka, lakini swai alikua bafuni anaoga...
Alipotoka bafuni akakutana na hizo taarifa toka kwa farida, swai nae hakukaa
mana ni jirani yake... Mkuku mkuku mpaka hospitali.... Mr jomo alipigika, kwani
pia kakatwa kwenye mikono na miguu kidogo tu, kapigwa mno hata kujitambua
hajitambui....
"kuna nini tena jamani"
Aliuliza Swalehe baada ya
kufika eneo katika wodi ya majeruhi,...
"shem, sijui ni nini jamani
Uuuuuuuuuwiiiiiiii"
aliongea semen huku akilia sana,..
"we mama
hatutaki kelele"
Aliongea dokta baada ya mama abu akupiga
kelele
"Samahani dokta, mgonjwa kapatwa na nini labda"
Swalehe
alimuuliza dokta
"mgonjwa kavamiwa na majambazi.. Na hatuwezi kumtibu
mpaka mlete PF3 ndipo atibiwe"
Aliongea dokta, hapo hapo Swalehe
akakimbia kituo cha polisi na kupewa PF3, ili mgonjwa apate matibabu... Pesa za
matibabu zilikua ni za Swalehe mana mama abu hana kitu, mume mwenyewe ndio huyo
kavamiwa na huenda pesa hana...
BAADA YA WIKI MOJA
KUPITA
Swalehe akiwa na mgonjwa karibu, mana yeye ndio mwenye
dhamana ya kukaa nae,... Lakini kwa wakati huo mgonjwa keshapona imebaki ruksa
tu warudi nyumbani
"vipi hali kaka"
Swalehe alimjulia hali baba
abu au mr jomo,
"safi tu ndugu yangu..."
"hali yako
unaendelea"
"aisee safi jirani... Kiukweli nakushukuru sana jirani,..
Umeniokoa kwelikweli"
"Usijali jirani... Sisi ni binadamu, lazima
tusaidiane"
"sijui nitakulipa nini... Mungu atakulipa tu
jirani"
"Usijali... Haya vipi, kwani ilikuaje usiku ule"
"weeee
jirani.. Kwani hata nakumbuka.. Nilishangaa tu mapanga ya kichwa, mara mtama..
Nilikua nimelewa sana nilikuja kuzinduka nipo hospitalini"
"walikuwa
majambazi wangapi"
"mmhhhhh wengi sanaaaa... Yaani kila mmoja alikua
anapiga upande wake"
"duuuu pole sana ndugu yangu"
"ahsante
sana, ila pole sana hata wewe.. Mana umenihudumia mpaka sasa nina
nafuu"
Aliongea mr jomo, wakati huo kakaa kitandani...
"ila
jirani... Hio ni laana ya familia yako... Mimi siwezi kuamini kua ulikua huachi
matumizi ya familia yako,.. Mtoto wako abu mdogo kiasi kile lakini unashindwaje
kumpa huduma"
Aliongea Swalehe ila ana maana yake mpaka kusema
hivyo
"ni kweli jirani... Nakili kwa hilo,.. Ila siwezi kufanya huu
ujinga... Kweli hii ni laana ya familia hii"
"jirani??.... Acha pombe...
Acha kulewa,... Jali familia yako"
Swalehe Aliongea kisha huyoo
akaondoka zake....
WIKI MOJA BAADAYE
Swalehe
akiwa zake ndani mida ya saa mbili za usiku,...
"siku hizi naona unga
unakaa kaa"
Aliuliza Swalehe huku farida akijibu
"ni kweli mume
wangu.. Sasa hivi shemeji anaacha hela"
Alijibu farida tena kwa kumuita
mume, ingali bado hawaja oana, kana kwamba tayari Swalehe ana mpango wa kumuoa
farida,... Kana kwamba mpaka anakubali kuitwa mume basi ndo
ipo....
"waacha weee, kwahio sasa hivi kama kawaida"
"ndio..
Toka apigwe na majambazi mpaka leo... Sasa hihi anarudi saa kumi na mbili jioni,
tena anakuja na mkate kila siku"
Aliongea farida lakini Swalehe
alikaukia kucheka ile mbaya, Mapaka farida akaanza kushangaa Swalehe anacheka
nini
"we swai jamani sasa unacheka nini"
"unakumbuka kuna siku
nilikwambia sio lazima dawa ya maumivu iwe parasetam,.. Unakumbuka ile
siku"
"ndio nakumbuka ila sikukuelewa kabisa ulikua na maana
gani"
Farida alikaa vizuri ili asikilize maana ya ile sentensi ambayo
Swalehe Aliongea siku ile
Huku kwa Semeni au mama abu,.. Huezi
amini baba abu yupo safi anacheza na mtoto na mama anapika,... Mama abu
anajiskia raha sana na kujihisi kama mdio kaolewa jana, kumbe kala msoto mpaka
basi,.
Yaani sasa hivi ndoa yake imekua tamu mpaka raha yani..... Kwani
kila akiangalia unga ni mwingi, mchele, yaani kila kitu kama mahitaji ya
nyumbani,.. Sasa ilikua ni ndoa na sio ndoano
Sasa huku kwa
Swalehe akiwa na mpenzi wake farida,.... Wakati huo Swalehe anacheka kwa kusikia
baba abu sasa hivi anarudi mapema tena na kitoweo kikiwa
mkononi....
"kwani siku ile ulimaanisha nini kusema sjui dawa ya
parasetam"
Aliendelea kuuliza farida kisha Swalehe akakaa vizuri na
kusema kuwa
"sikia farida, kwanza Utanisamehe sana kwa hilo.... Ukweli
ni kwamba, mimi ndie nilie mcharanga mapanga baba abu"
Aliongea Swalehe,
huku farida akishtuka na mapigo ya moyo kumwenda
bio
"whaaaaaaaaaaat???"
Farida
hakutegemea kwamba Swalehe ndie aliweza kumpiga mapanga shemeji yake,.. Na sio
yeye tu bali ni kila mmoja aliejua tukio hilo hakuweza kuhisi ya kwamba
msababishaji ni Swalehe,.. Sasa baada ya wiki kama mbili hivi kupita, Swalehe
aliamua kusema ukweli na ni baada ya jomo
kupona...
"whaaaaaaaaaaat???"
Alishangaa farida huku
akishika moyo wake,
"sasa unashangaa nini"
"ina maana swai
mpenzi wangu kumbe wewe ni jambazi"
Aliongea farida huku Swalehe
akicheka sana, kana kwamba sio kweli kwa yale anayo yafikiri
farida..
"skia nikwambie farida... Lile neno nililokwambia kuhusu
parasetam, nilimaanisha kwamba.... Sio lazima mlevi uzungumze nae.. Bali
muongeleshe kwa vitendo"
Aliongea Swalehe lakini farida bado alibaki
njia panda...
"bado sijakuelewa sentensi yako ina maana
gani"
"skia farida... Kwa kawaida, mlevi hua haambiwi
akasikia... Kitendo cha wewe kuniambia kua unapeleka unga kwa dada yako ingali
mwanaume wake yupo na bado ni kijana mwenye nguvu tena mwenye kazi inayo
muingizia pesa.. Kiukweli roho iliniuma, na haikuniuma kwakua umetumia chakula
changu, hapana... Bali imeniuma kwanini aitese familia yake??"
Aliongea
Swalehe huku farida akiuliza
"kwahio, baada ya hapo ukahisi kuongea
nae"
"ndio.. Na siku ile ilikua hivi"
SIKU ILE SWALEHE
KATOKA NA PANGA
alipotoka na panga alipitia dukani na kununua
mayai mawili, na kwakua anaijua kona ya jomo ambayo huitumia wakati wa kurudi
nyumbani,.. Alikaa mahali na kumwona jomo akija staili ya ulevi,.. Kana kwamba
alilewa sana,... Alichokifanya Swalehe ni kuanza kumziba mdomo kisha akatoa pesa
zake zote kama elfu 50 hivi,.. Na kuanza kumshambulia mr jomo,.. Swalehe alikuwa
peke yake, sema alikuwa akipiga sehemu tofauti tofauti na kumfanya jomo ajue
wako watu zaidi ya mmoja lakini alikua mmoja... Na Swalehe hakutaka kumuacha
bila kumkata... Ila Swalehe alikua anachagua sehemu za kukata kwelikweli,..
Ilimradi tu asikate mshipa wowote katika mwili wa baba abu,.. Alimpiga kipigo
kikali, kisha akamvua suruali na kumpasulia yale mayai.. Kana kwamba akija
kuzinduka anajua kaingiliwa na wenzake... Hicho ni kijuto moja wapo na ni lazima
aache ulevi,... Pesa ya jomo haikuliwa na Swalehe, bali ile pesa ndio iliomtibu
jomo kule hospitalini...
MWISHO WA SIKU ILE
USIKU
"haaaaaaaa... Swaaaaiiiii... Ina maana kumbe kweli
ulimkata kata shemeji"
Aliongea farida baada ya kuambiwa ukweli juu ya
kuvamiwa kwa mr jomo
"ni kweli ni mimi... Ila nilifanya hivyo kwa kusudi
moja tu"
"kusudi gani kama sio kumuua baba wa watu"
"sikiliza...
Mlevi, hua hawekwi kikao.. Wala hasemeshwi...na wala haambiwi acha pombe
akaacha.. Ila mtafutie kitu kitakacho mfanya ajute katika maisha yake, na ajue
kitu hicho kama sio kulewa asingelifanyiwa.. Hivyo atauchukia ulevi mpaka kufa
kwake"
Swalehe Aliongea mpaka farida akacheka...
"ina
maana kumbe ulikua una maana hio"
"ndio"
"sasa angekufa
je"
"najua asingekufa kwasababu hata sehemu nilizokua nakata ni sehemu
ambazo sio njia za mishipa... Na kitu ambacho atakuja kujuta ni yale mayai nilio
yapasua... Na toka atoke hospitali hajanigusia, kana kwamba kalimezea na kujua
kweli aliingiliwa,.. Na siri hii usimwambie dada yako, mana atamwambia na mwisho
wa siku tabia itarudi pale pale..."
Swalehe alimaliza kuongea kisha
akapanda zake kitandani
"Kwahio unasema mlevi haambiwi acha pombe
akaacha"
"ndio... Mjeruhi mahali ambapo anaweza kujutia ulevi wake...
Sasa ona sasa mr jomo ni baba mzuri wa familia"
"Duuuuuuu... Yaani kama
sio kinifafanulia,.. Hakiyamungu ningeondoka hapa"
"mmmhhh ona ulivyo
mwongo"
"kweli vile"
Basi ilikua ni usiku mzuri sana kwao, na
sasa Swalehe na farida wapo katika mbio za kufunga
ndoa...
Kesho yake nyakati za asubuhi, farida akiwa anaosha
vyombo,... Swalehe alishatoka kwenda kijiweni mana kazi zake ni za ujenzi hivyo
mpaka wapate saiti ya kazi..
"kaona sasa... Kanajifanya kanajua
wanaumeeeeeee"
Aliongea Zahra, lakini papo hapo dada yake
alitoka...
"we Zahra, kwanini una uchokozi lakini.. Huyo si mchumba wa
mtu haya chokochoko ya nini"
Aliongea fatuma au mama
saidi
"dada, Swalehe ni mpenzi wangu.. Na hata utamu wake naujua... Hili
lisambaa sjui lilitoka wapi"
Aliongea Zahra huku fatuma
akishangaa
"wewe zaru.. Haya huyo swai lini akawa mpenzi wako... Mana mi
ninachojua wewe na swai mna ugomvi mpaka mkaanikiana nguo za ndani mlangoni,
sasa huo uhusiano ni upi"
"dada... Swalehe keshanifanya sana hapa ndani
kwake"
Aliongea Zahra, mara mama mwaju nae katoka tena, yaani mama hana
hata haya huyu... Wakati huo farida yeye hana stori nao,. Wacha waongee wao ndoa
afunge yeye...
"we Zahra, nimekuskia toka nikiwa ndani... Oohh sjui
unajua utamu wake.. Hivi wewe na kishepu chako hicho unaweza kuwa na Swalehe
wewe"
Fatuma alishangaa mbona mama Mwajuma kaingilia hilo balaa... Mana
siku ile mama saidi yeye hakuwepo kwahio wapangaji wasiojua kuwa mama mwajuma na
Swalehe wana mahusiano ni huyu mama saidi peke yake...
"mama Mwajuma,
mbona sikuelewi"
"hunielewi nini... Swalehe toka amekuja hapa, anakula
juu yangu, kuvaa juu yangu... Kila kitu juu yangu.. Leo mnashoboka tu
hapa"
"lakini mama Mwajuma... Sawa ulikua ukimpa chakula nilikua naona,
mana alikua bado ni bachela... Lakini mbona kuna jambo umeingilia hapo, sjui
kashepu sjui nini, naona havihusiani na mada hapa"
Aliongea mama said au
dada yake Zahra,
"sikiliza dada... Huyu mama huyu, umuone tu na utu
uzima wake wa bure tu... Huyu ana mahusiano na Swalehe"
"ati nini??
Yaani yule mtoto ndio katembea na huyu mzee"
"weeeeee mzee mama
ako"
Zikaamka ngumi,.. Wacha wapigane mama said na mama mwajuma...
Farida yeye kimyaa mana anayajua yote hayo hivyo hana hofu
nao...
Ilipofika jioni, farida alizidi kumkazania Swalehe
wahame hapo kwenye hilo boma mana anaumia moyo wake pale wanapozidi kumtaja
Swalehe kama mpenzi wao, japo kwa sasa haendelei nao... Kweli Swalehe alifanya
michakato lakini hakutaka kuondoka hapo mpaka ahakikishe wapangaji wote wamejua
kuwa kaoa
Taarifa zilifika kwa dada mtu... Semeni hakuamini
kama mdogo wake ataolewa, mana alikuja mjini kibabe babe tu, na kakutana na
bahati ya kuolewa... Kuolewa ni bahati sana na ndio mana kwa sasa ndoa ni adimu
sana mitaani... Huezi kuta wapenzi wa miaka 23 kwa 25 wakioana ni kwa bahati
sanaaaaa....
Baada ya dada kujua, taarifa nyumbani,... Kama
unavyojua ndoa za kisambaa.. Sjui upeleke hiki mara kile, yaani muoaji anaweza
kukata tamaa, lakini swai alijipanga.....
Tanga Tanzania ndoa
ilifungwa tena ya haraka sana, mana katika sheria ya dini inasema MWENYE KUOA
/KUOLEWA BASI NA AOE / AOLEWE HARAKA SANA...
Sasa huku mjini,
Zahra anajua fika Swalehe wamekwenda tanga kufunga ndoa na
farida...
"dada, hivi mimi sina bahati ya kuolewa... Nina ubaya gani...
Hebu niangalie, yaani napokonywa mwanaume na mtu mshamba mshamba hajui hata
kuoga"
Aliongea Zahra lakini dada yake hakutaka kumsapoti kwa hilo kwani
Zahra halujijua kosa lake lilipo...
"kweli mdogo wangu wewe ni mzuri,
una shepu nzuri... Pia unavaa vizuri... Ila kosa lako moja,
hujiheshim"
Aliongea fatuma huku akiondoka...
"dada... Una maana
gani"
"skia Zahra, wasichana wa siku hizi.. Wengi mtazikosa ndoa..
Kwasababu mna tabia za kimjini... Kitu cha kwanza kabisa.. Mwanaume hua hapendi
mwanamke Mjanja, wewe mdogo wangu umekaa kijanja janja sana, mwanaume mwenye
malengo hawezi kukuoa kwasababu anahisi ataoa balaa ndani ya
nyumba,.."
Fatuma Aliongea hayo yote baada ya mdogo wake kupokonywa
mwanaume,...
"dada, ina maana na kuvaa kwangu vizuri bado sito
olewa"
"sikiliza Zahra, wanaume hawaangalii mavazi pale wanapotaka
kuoa... Wanaangalia tabia... Afadhali mwanzo ulikuwa ukivaa vizuri, lakini ukaja
kuiga mavazi ya mjini... Afu sasa kingine, mwanaume hapendi mwanamke muongeaji
sana... Kingine mwanaume hapendi mwanamke mjuaji sana"
"mmhhh
dada"
"ndio hivyo... Sasa hivi unatakiwa
ubadirike"
Baada ya siku mbili Swalehe walirudi kutoka tanga,..
Sasa farida na Swalehe ni mume na mke,... Zahra aliumia moyo lakini haikuwa na
jinsi labda haikuwa bahati yake, japo aliikataa mwenyewe kipindi cha
mwanzoni.... Huezi amini Zahra alimtafuta ayub yule yule aliowahi kumdanganya na
kujifanya tajiri kumbe aliazima vitu vya watu... Namba alishazifutaga lakini
kichwani kwake bado zipo japp ni muda mrefu sasa umesha pita
"hallo ayub
mambo"
"poa.. Nani mwenzangu"
"ina maana ulifuta namba yangu
ayub"
"sikukumbuki tafadhali, na sasa nipo bize kidogo ofisini... Labda
unikumbushe mana nina kikao na wafanya biashara wenzangu"
Aliongea ayub
huku akionekana kweli ni boss
"ni mimi Zahra"
"oooohhhh Zahra
mpenda pesa.. Habari yako mama"
"salama tu... Ila tafadhali sana
usiniite mpenda pesa"
"nakuita hivyo... Kwakua nina uhakika bila
kujifanya mwenye pesa, nisingelipata penzi lako... Na umenila pesa nyingi sana
kisa uzuri wako Zahra"
Aliongea ayub lakini kama vile alikuwa na dharau
fulani hivi...
"ok tuachane na hayo... Naomba tukutane mjini leo
jioni... Nitalipia dina na hata chumba pia ukitaka nitalipia"
Zahra
aliamua kurudiana na ayub
"hahahahahahahaha, Zahra... Kwa sasa
umechelewa.. Tayari nina mke,. Nimeshaoa... Na pia kwa sasa siishi Arusha bali
nipo BABATI nimejenga mji wangu huku"
"Babati??"
"ndio.. Na pia
nina mke na mtoto mmoja"
Aliongea ayub huku Zahra akianza kulia tena,...
Yaani kakosa kote kote
Zahra alikata simu kwa
hasira,...
Sasa huku kwa ayubu,... Kweli ayub kwa sasa ni
tajiri, na ndio yule yule tajiri aliojenga jumba la kifahari kule mjini Babati,
na mafundi alikuwepo Swalehe kama mmoja wapo kati ya mafundi 20...
"kuna
malaya mmoja nilitembea nae muda mrefu nikiwa mbeba mzigo"
Aliongea
ayubu kama vile kumhadithia rafiki yake...
"kwani ulikuaga unabeba
mizigo"
"heeee... Ndio, kabla sijaenda mgodini, nilikua nabeba mizigo
kule NMC"
"alaaaaaa"
"ndio... Na mungu nae hakunitupa mgodini...
Ndio kama hivi hali imekuwa njema"
"kwahio kakuambiaje huyo
mwanamke"
"naona ana nia ya kurudiana, ila nina mke... Ila
kazuri"
"ahhhh mzuri bila tabia ni mbaya"
"umeona
eee"
Sasa huku arusha,... Swalehe na farida walikuwa wakihama
katika chumba kipyaaa, mana wakiendelea kuishi hapo farida atateseka sana kwa
maneno ya mama mwajuma na Zahra,... Hivyo baada ya ndoa yao waliamua kuhama na
kuwaachia boma lao,.. Sasa wakatengeneze maisha yao mazuri wakiwa ndani ya
ndoa...
"Nashukuru sana mume wangu kwa kukubali kuhama pale... Nilikuwa
nahisi huto nielewa... Ahsante sana... Naapa kukupenda mpaka kufa kwangu,
sintosikiliza ya mtu kuhusu wewe... Nakupenda sana mume wangu, utakacho kula
nami nitakula.. Utakapo lala, nami nitalala.... Tumuombe mungu nasi tubarikiwe
maisha mazuri..."
Aliongea farida wakati huo kajilaza katika kifua cha
Swalehe, tena huku akichezea gaden love za mume wake
"nami pia nakupenda
sana mke wangu.. Ninacho kusihi, tafadhali sana usisikilize ya mtu... Na
usidanganywe na mtu... Mana kwa kawaida ndoa huharibiwa na mwanamke,... Na
mwanamke huyo sio wewe, bali ni mwanamke ambaye ataanza kukupandikiza umbea,
chuki, na dharau juu ya mume wako... Nakupa ujumbe wangu, lakini jieshim,
jichunge na ndoa yako.. Na uchunge maneno ya mashoga zako,.. Baya toa, zuri
hifadhi... Hapa ni mjini kila mtu hutumia akili yake,... Wengine hutumia akili
zao kupotosha ndoa za wenzao kwakua zao zilishaoza... Hivyo kua makini na
jiji"
Aliongea Swalehe kama kumsihi mke wake,....
"mume
wangu.... Masikio yangu, hayasikii neno lolote baya kuhusu ndoa... Mimi ni wako
wa milele,..na Kama sikupendi ni kheri nisingelikubali unioe.. Lakini nakupenda
nakuheshim na nakujali na ndio maana nimekubali kuolewa nawe... Mume
wangu...Kama umetafuta kitoweo Umepata rudi nyumbani tule... Umekosa pia rudi
nyumbani tule cha jana... Kama hakuna pia rudi nyumbani tulale"
Yalikua
ni maneno mataam yaliomtoka msichana huyo,. Swalehe alijikuta akitabasamu kwa
mbaaali
Tukijua huku upande mwingine, Hutaamini macho
yako
Wakati huo huku ndani.... Farida alikua akimpa maneno
rafiki yake...
"Zahra, kwa kawaida huwa kuolewa sio kazi.. Kazi ni
kuilinda ndoa yako... Usifuate maneno ya watu,... Kwahio usione ajabu kuolewa,
ila jitahidi kuiheshim ndoa yako... Usimjibu mumeo vibaya, mtengee maji pale
anaporudi kazini... Mpe vile vitu anavyopenda... Mimi sina cha kukuambia, mana
wewe mwenzangu ulikua na kungwi, hivyo najua kakupa somo vizuri... Ila nakuomba
sana, mpende mumeo mheshim mumeo... Hapo utaiona raha ya ndoa
yako..."
Aliongea farida huku Zahra akitoa machozi kwa kua.. Kumbe
alikua akimkosea sana farida kipindi kile.. Kumbe alikua anamkosea mtu ambae ni
nuru katika maisha yake...
"pia.. Mumeo akipata Shukuru, akikosa muombe
mungu kesho apate... Na hata akikosa tena, usikasirike... Zidisha kumuombea
mumeo,... Achana na utajiri wa majirani au watu wengine, huo hauwahusu... Mpende
mumeo, ipende ndoa yako"
"PIIIIII... PIIIIIII.
PPPPIIIIIIIII"
Ni sauti ya honi ya gari ikilindima huko nje, mume
aliingia ndani fasta na kumchukua mkewe, waliingia ndani ya gari wote ili
kumsindikiza mwenzao mpaka kwake.. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Zahra na
mumewe....
Yalikua ni
maneno matamu sana yaliomtoka Farida, wakati huo wametulizana katika pango
jipya, walilo hama hivi karibuni,.. Tena wamepangisha dabo rumu (rumu mbili
zilizo shikana) na maisha yao yalikua na furaha sana
Tukija
huku kwa akina Zahra akiwa katulia pembezoni mwa ukuta, sambamba na chumba
chao,.. Alikua ni mwanamke mwenye huzuni sana, na kujiona mwenye nuksi ya
wanaume katika dunia hio, alikua akijiangalia sana katika mwili wake...
Haikutosha, aliingia ndani na kuvua nguo zake zote katika kioo...
Dada
yake alikua akimuangalia tu mdogo wake kile alichokua akikifanya...
"we
Zahra, haya sababu za kukaa uchi mbele ya kioo ni nini"
Aliongea dada
yake huyo ambaye ni mama Saidi au Fatuma...
"dada, naumia sana kumkosa
Swalehe.. Najiangalia mwili wangu, labda nina kasoro dada"
Aliongea
Zahra huku akilia sana, mpaka dada yake alimwonea huruma mdogo
wake...
"Zahra mdogo wangu,.. Kasoro alio iona Swalehe, haipo kwenye
ngozi"
Aliongea Fatuma huku Zahra akiuliza
"iko wapi sasa,... Na
kama ni kumpenda nimempenda"
"tatizo sio kumpenda tu... Mwanaume
anahitaji vitu vingi vizuri toka kwetu... Busara na hekima ni moja ya vitu
wanavyopenda... Unaweza ukavaa chupi tu na ukatembea nayo mtaani.. Ila hekima na
husara unayo, ispokua mavazi ndio yatakutafsiri vibaya... Jirekebishe...
Ikiwezekana fuata nyayo za Farida, kama kweli unahitaji
kuolewa"
Aliongea dada yake huyo kisha akawa anaondoka, lakini Zahra
alimzuia dada yake...
"dada, hebu shika hili tako langu... Au ni gumu
ndio mana sipendwi"
Aliongea Zahra huku dada akicheka
sana
"Zahra, naona sasa unakwenda kua chizi kisa Swalehe... Alafu nataka
kuuliza,.. Hivi mahusiano yako na Swalehe yalianza lini? Mana mimi najua mna
ugomvi nyie.. Sasa nashangaa sasa ukisema alikua mchumba wako"
Aliuliza
fatuma huku Zahra akikaa kitandani na kusema...
"ni kweli dada,.. Mimi
na sheby ilikua hivi... Wakati anahamia hapa, sheby alikua akinipenda sana,..
Lakini kipindi kile, nilikua na ayubu, nikajua nimepata mume.. Sasa sheby nikawa
simuelewi, saa zingine namtukana.. Saa zingine namletea nyodo na maneno ya
kashfa juu yake na wakati huo alikua akinitaamkia kunioa... Ilifikia hatua
Swalehe akachoka kunifuatilia, mpaka akaaniacha kabisa,... Sasa nilipo achana na
ayubu, ndio nikaanza kumsumbua Swalehe, mpaka nikawa naanika chupi mlangoni
kwake kwasababu ndio udhaifu wake... Kiukweli Ilifikia hatua akanisamehe... Sasa
tukawa na mahusiano mazuri tu,.. Kuna siku alitaka kunilala (kufanya mapenzi)
lakini kila akitaka kuingiza, mara simu imeita... Kila akitaka kuingiza mara
mlango umegongwa, Kiukweli siku ile hakufanikiwa kuingiza uume wake kwangu... Na
baada ya siku ile.. Kesho yake ndio akapata safari.... Nakumbuka huko alikaa
miezi kama sita hivi.. Na ndani ya hio miezi sita ndio akaja farida.... Baada ya
Swalehe kurudi,.. Nilishangaa alilala na farida badala yangu... Basi ndio ikawa
bifu mimi na farida, mpaka ikafikia wameoana"
Dada alisikia
kila kitu toka kwa mdogo wake....
"sasa mpaka hapo bado hujaiona kasoro
yako"
Aliongea fatuma au mama saidi...
"Kiukweli sijaona dada,
labda ni kwasababu farida ana shepu kuliko mimi"
Aliongea Zahra tena kwa
kutia huruma sana...
"Zahra mdogo wangu, mbona wewe ni mzuri,.. Tena
mzuri kushinda mimi na una umbo kushinda mimi.. Lakini mbona mimi nina
mume.."
Aliongea fatuma
"sasa kasoro yangu iko wapi
dada"
"kasoro yako.. Hekima huna... Busara huna... Mavazi mazuri ya
heshima uliacha kuvaa.. Wewe na saluni kila kukicha... Angalia Farida, toka
amekuja hapa, anasukwa na dada yake msuko wa twende kilioni, haijui saluni...
Ulimsema Farida ana chupi zilizo toboka.. Haya wewe mwenye begi zima lenye chupi
mpya mbona hujaolewa.... Ulimsema Farida ni mshamba, haya wewe mjanja mbona
hujaolewa... Ulimsema Farida hajui kuoga.. Haya wewe unae oga kutwa mara tatu,
mbona hujaolewa... Kwahio usidhani kwamba kuvaa kwako vizuri na kunukia labda
mwanaume ndivyo anavyo vutaka... Mwanaume anahitaji mwanamke MPOLE, MNYENYEKEVU,
ANAEJUA SHIDA NA RAHA... MWENYE KUMHESHIMU MUME... MWENYE KUVAA MAVAZI YA
HESHIMA...MWENYE KUIFUATA DINI YAKE... wewe hivyo vyote, ulikua navyo ulipokua
kijijini.. Ulipokuja tu mjini ukaviacha.. Ona dada washamba wamekupita... Mtu
ana miezi mitatu tu kapata mume.. Wewe una miaka minne sasa.... Na
usipobadilika, utachezewa sana"
Aliongea fatuma au mama saidi
kisha huyoo akaondoka zake, Zahra alilia sana, mana maneno ya dada yake
yalimchoma na kumuingia haswa,.. Pale pale tabia yake mbaya akaacha, mana ndio
nuksi katika maisha yake,.
Huku nje kwao mama Mwajuma akiwa
anamenya viazi kama chakula cha usiku, alikua na watoto wake wakiwa wana andaa
chakula cha usiku.
Ghafla Zahra akatoka nje,.. Huezi amini
Zahra kairudia asili yake ya zamani...
"heeeee, Zahra, ni wewe au macho
yangu"
Aliongea mama mwajuma, lakini Zahra alikaa kimya.. Huku mama
mwajuma akisubiri jibu chafu kutoka kwa Zahra, lakini Zahra alikua kimya, kana
kwamba, hahitaji ugomvi na mtu...
"Samahani mama,... Kama nina kosa juu
yako, naomba unisamehe. Kwa sasa sina kinyongo na mtu.. Kwan mtu aliekua
akitugombanisha, keshaoa sio wakwetu tena. Hivyo sioni haja ya
kugombana"
Aliongea Zahra, hata semeni au mama abuu alitoka nje na
kumkumbatia Zahra, mana kaongea point nzuri sana... Hata mama mwajuma aliona
kweli haikua na haja ya kuwekeana bifu la hapa na pale...
BAADA
YA WIKI MOJA KUPITA
Swalehe akiwa kijiweni kwake,.. Na baadhi
ya marafiki zake..
"sasa hivi swai anang'aaa, kuoa raha
kweli"
Aliongea mmoja wa rafiki zake
"asikwambie mtu bwana, kuoa
ni raha"
Aliongea Swalehe huku rafiki yake mmoja akisema
"kwaio
sasa hivi unaoga maji ya moto"
"kama kawaida yangu"
"aaaaaaa
Hahahahahahahah"
Ilikua ni furaha juu yao,... Basi ilifika nyakati za
kurudi nyumbani, hivyo swai na rafiki yake mmoja walikua ni wapitaji wa njia
moja..
"unajua bwana swai, kitendo ulicho kifanya, ni kizuri sana, nami
natamani sana kuoa.."
"aliongea bwana Bakari huku Safar ya kurudi
nyumbani ikiendelea.
"ni kweli, na kama uko vizuri, kwanini usioe...
Kupata na kukosa ajuaye mungu.. Usiwaze kua, ukiwa na mke afu ukakosa
itakuaje"
Aliongea sheby
"enheeee.... Sasa kwa wewe ambaye
tayari umesha oa... Hebu niambie, siku umekosa, je inakuaje hapo ndani
kwenu"
Aliongea bakari kana kwamba hicho ndicho anacho ogopa sana... Na
yote hio ni kwasababu wanawake wengi wanajua raha tu, shida hawazijui, na ndio
mana wanaume tunatatazika sana katika swala zima la kuoa..
"Kiukweli
nisikudanganye bwana bakari... Mimi nimeoa juzi juzi tu.. Nina wiki ya pili
sasa, na Namshukuru Mwenyezi Mungu, kwani hakunikosesha riziki toka nimeoa.. Ila
kabla hamjaoana, ni vyema kuambiana ukweli wa maisha yenu.. Mwambie kabisa bwana
kazi yangu ni hii na hii.... Ila sio lazima ajue kipato, labda uamue ajue...
Kwahio cha kufanya, hakikisha unampa ukweli wa maisha yako, ajue kazi ya mume
wake ina kukosa na kupata, na siku mume kakosa basi walale... Unajua bwana
bakari, wanaume wengi tunakosea sehemu moja tu katika kuoa....
"
Aliongea Swalehe,.. Bakari hapo alikua makini sana kujua kosa
lilipo...
"tunakosea wapi sasa"
Aliuliza bakari... Wakati huo
safari inazidi kwenda
"unajua, swala la kutafuta mke ni tofauti na
kutafuta kahaba... Jinsi tunavyo tafuta kahaba wa kutumia kwa muda, ndivyo jinsi
tunavyotafuta mke wa kudumu... Niulize kwanini"
"haya nakuuliza
kwanini"
"ok safi sana... Wanaume hua tuna tabia ya kujikweza mbele za
wanawake,.. Unakuta kwa mfano kazi zetu hizi za ujenzi.. Wapo wanawake
ukiwatajia kazi hii hawakuelewi,. Sasa tunajikuta tunataja kazi ambazo sio
zakwetu, unajikweza kutaja kazi ambayo inaingiza kipato kikubwa kwa siku,... Hio
yote ni ili mwanamke akuelewe na uwe nae... Sasa jua kua anapokukubalia mwanamke
huyo,.. Kakubali kwakua unaingiza kipato kikubwa kwa siku, hivyo hakuna siku
atashinda au kulala njaa mana mume ana kazi nzuri,.. Sasa umeshaweka mtu ndani,
mara kazi zikaanza kuyumba... Mwanamke hatakuelewa hata kidogo, mana anajua kwa
kipato unachoingiza kwa siku, hata kazi ikiyumba, bado hakiba ipo kubwa tu...
Kwahio ukimwambia sina anakua hakuelewi, na hapo ndipo ugomvi unapoanza mara
mmepigana mara mmeachana... Kosa sio lake, kosa ni lako wewe mwanaume, mana
ulijikweza mbele yake... Na ikumbukwe kua, siku zote mwanamke hukarili maisha,
hivyo mkarilishe maisha yako halisi,.. Mwanamke hua haelewi bali anakarili...
Sasa ole wako umkarilishe maisha yasiyo yakwako"
Aliongea
Swalehe huku bakari akibaki kimya na kujikuta ni kweli wanaume wengi tunapenda
kujikweza mbele za wanawake, kana kwamba nawewe uonekane umo kwenye waliomo...
Usiige maisha ya mtu, fuata yakwako...
"aaahhhh kweli Swalehe
leo umenifungua masikio yangu... Ni kweli na sio mara moja hata mimi nimejikweza
sana kwa wanawake... Kumbe nilikua nakosea sana"
Aliongea bakari huku
Swalehe akijibu
"unakosea sana bakari... Tujikweze kwa wanawake wa muda
ila sio mwanamke wa kudumu"
"nimejifunza kitu.. Na inaonekana
hata wewe yalikukuta"
"ndio... Yaani ile kumtajia tu kazi yangu...
Daaahhh niliangaliwa juu mpaka chini.. Kisha akatema mate... Kana kwamba kazi
yangu imemtia kichefuchefu"
"Duuuuuuu, kweli kazi ipo kutafuta
mke"
Aliongea bakari, na hapo walifika eneo la njia ya panda katika
kuachana...
"sasa swai, lini nitamuona shemeji... Tusije kupigana
vikumbo mjini huko"
Aliongea bakari, ili kumjua mke wa
sheby
"aaahhhh, kesho kwakua ni Jumapili.. Utakuja kumuona
usijali"
"nitafrai sana rafiki yangu"
"basi poa, kama vipi
kesho"
"poa"
Basi waliagana kisha haooo kila mmoja na njia
yake.. Ikiwa ni mida ya saa kumi, mana hakukua na kazi siku mbili
hizo...
Lakini wakati Swalehe anatembea peke yake kwenda kwake,
alihisi kuna mtu anamfuatilia kwa nyuma....
Lakini kila akigeuka haoni
mtu, na hapo alipo na kwake hakuna umbali sana ni kama kilomita moja hivi.. Sasa
Swalehe akajifanya kasahau kua kuna mtu nyuma, ikafikia mahala, akaguka kwa
haraka... Aliona ni mwanamke, na hakua mwingine bali alikua ni Zahra.... Zahra
baada ya kuonekana, ilibidi ajitokeze tu... Wakati huo kashikilia fuko la nguo..
Swalehe alipata wasiwasi kua labda Zahra kafukuzwa kwao..
"ni wewe
tena?, ivi Zahra?? Kwanini hutupi uhuru wa ndoa yetu,.. Kwahio unataka tuhame na
hapa tulipohamia juzi tu"
Aliongea swai huku Zahra akiwa kimya, tena
kavalia vizuri sana, kana kwamba karudia hali yake ya zamani.... Zahra hakutaka
kumjibu, badala yake alishuka chini mwenyewe kwa kupiga magoti.. Swai haamini
leo Zahra ndio anapiga goti
"swai... Najua Mwenyezi Mungu hawezi
kunisamehe kama wewe na mkeo hamjanisamehe... Naanza nawewe.. Naomba unisamehe
kwa yote niliokufanyia.. Yote ilikua ni mapenzi yangu kwako... Ila kwa sasa
nimetua mzigo huo mana tayari wewe ni mume wa mtu... Sasa sitakusumbua tena, na
naomba unisamehe kwa kila jambo"
Aliongea Zahra, swai haamini
macho yake, basi swai kwa haraka alimuamsha zaru juu, kisha
akamwambia
"nimeshakusamehe, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu,
akujaalie mume bora katika maisha yako... Na pia umefanya jambo la maana sana
kama umebadilika"
Aliongea swai huku zaru akijibu
"ndio,
nimeirudia hali yangu ya zamani, kwakua sikuzaliwa na tabia hii, kwahio, nimesha
acha... Hata sasa hapa nimeshika nguo zangu ambazo nilizikunja, sasa nimetoka
kuzifanya kua ndefu"
Aliongea Zahra, na hata swai alifurahi sana kuskia
hivyo...
"nimefurahi sana kwa hilo, na nimesha kusamehe... Ila pia
nitakuombea msamaha kwa Farida, hilo ondoa shaka"
Aliongea swai lakini
Zahra alikataa
"hapana, sitaki uniombee msamaha"
"kwanini? Ina
maana unataka ugombane na mke wangu"
"hapana swai... Sina maana hio,..
Bali nataka nikamwombe msamaha mwenyewe... Naomba unipe nafasi
hio"
Aliongea Zahra, huku swai akiwaza vile jinsi Farida anavyomchukia
Zahra,.. Sijui itakuaje...
"hapana Zahra,.. Sitaki ujue nyumbani kwangu,
mana sitaki ugomvi wenu"
Aliongea swai
"swai... Nipo chini ya
miguu yako... Mkeo namheshimu mno, sitakaa kugombana nae.. Nimesha badirika sana
swai"
Aliongea Zahra huku swai akiamua moja tu...
"sawa
twende"
Swai alikubali kumpeleka zaru kwa
mkewe
Walifika mahali, nyumba ipo mbele yao... Swai hakutaka
kwenda nae,.. Alimpa nafasi yeye kama yeye..
"mlango ule pale ule...
Ndipo alipo Farida, nenda mwenyewe"
Aliongea swai huku Zahra akitamani
kwenda na swai
"kwanini tusiende wote swai"
"hapana... Nenda
mwenyewe"
Aliongea swai kisha akawa kama anarudi nyuma hivi, kana kwamba
anawapa nafasi waombane msamaha wenyewe na asihusike na lolote kati yao, mana
hata kugombana waligombana wenyewe bila ya swai kuwepo, hivyo wakapatane wenyewe
pia bila ya swai kuwepo....
Basi Zahra alifika katika mlango
huo, na hapo ndipo wanapo ishi Swalehe na mke wake.. Zahra alikua akisita
kugonga mlango,.. Lakini akapiga moyo konde,.. Aligonga
"ngo.. Ngo....
Ngo.... Ngo... Ngo.. "
Farida alikua akiandaa mboga za jioni,..
Alifurahi sana kuskia mlango umegongwa, kwani alijua ni mume wake anarudi
kazini, na hua kazoea kumchezea kwa kugonga mlango...
"karibu mume
wan....."
Wakati huo swai
yeye kaelekea zake mtaani, mana ni jirani na nyumbani hivyo hana wasiwasi na
hilo, na pia hakuwafuatilia akina Zahra na mkewe, kama wanapigana wapigane yeye
akiwa hayupo,...
Zahra alipiga moyo konde kwani alikua akisita
kubisha hodi, mana anajua ni kama atamkwaza, kuna wakati alitaka kurudi ili tu
asije kukwaza Farida, lakini akaona bado atakua hajasamehewa na watu hao japo
mmoja keshamsamehe, bado mmoja ambae ndio mlangwa haswa aliokua akiteseka kwa
ajili yake,...
Zahra aligonga mlango,.. Wakati huo Farida alikua
akiandaa mboga zake za jioni,.. Hivyo kusikia mlango unagongwa, alifurahi sana,
kwani alijua ni michezo ya mume wake, kugonga mlango....
"ngo.. Ngo....
Ngo.... Ngo... Ngo.. "
Farida kwa furaha aliamka na kwenda
kufungua mlango...
"karibu mume wang.... Ni wewe tena?... Umejuaje
nyumbani kwangu Zahra??.. Mimi sitaki ugomvi nawewe, nakuomba sana, tumehama
pale kwa ajili yenu, leo tena umekuja hapa... Kwahio unataka tuhame na
hapa"
Aliongea Farida tena huku akitamani hata kulia, mana Zahra ndio
adui wa ndoa yake, hivyo haoni shida kumchukia... Zahra hakuweza kumjibu,
alifanya kama vile alivyofanya kwa Swalehe... Alipiga magoti kumwomba Farida
msamaha.... Farida haamini leo Zahra kawa mpole juu yake, wakati ndie aliekua
akimdharau kupita kiasi...
"Farida, kwa sasa sina tabia ulio ijua awali,
unavyo niona ndivyo nilivyo kwasasa... Nimejifunza mengi kupitia wewe... Nina
hamu ya kuolewa lakini imeshindikana... Farida, naomba unisamehe kwa yote
niliokufanyia, ilikua ni akili ya mapenzi ya kitoto tu,.. Najua nilikuumiza sana
katika moyo wako.. Naomba unisamehe sana Farida, kuanzia leo mimi ni kama dada
yako, nitamheshim mume wako na hata wewe pia.. Nisamehe Farida"
Aliongea
Zahra huku akiwa kapiga magoti bado,... Farida alilia sana,.. Na kulia huko ni
kwa furaha, kwani anapenda sana kuona mtu akibadirika na kua mtu
mzuri
Haraka haraka alimnyanyua na kumkaribisha ndani... Zahra haamini
kama Farida kamsamehe, mana alijua Farida hatakaa kumsamehe
kamwe..
"wewe nu mwanamke mwenzangu,... Nimefurahi sana kuona
umebadirika kiasi hiki... Kama upo hivi basi kuanzia leo, nimekusamehe
Zahra"
Aliongea Farida huku Zahra akifurahi kwa kusamehewa na farida...
Kweli alimkosea sana, alimzalilisha sana.. Lakini karudisha moyo nyuma na
kumsamehe...
"kwa hali hii, nakuapia hutakaa utapata mume
bora"
Aliongea farida huku Zahra akishukuru kwa maneno
hayo....
"Ahsante sana wifi yangu.. Nakupenda bure, kumbe ushamba wako
ni dili kwa waume zetu.. Nilikua sijui"
Aliongea Zahra, na hapo sasa
ilikua ni stori za kucheka mana tayari wameshakua marafiki, au
mawifi..
"ahahahahaha, Usijali Zahra, tupo pamoja... Haya niambie
umepajuaje hapa"
Aliongea farida huku Zahra akijubu bila
kigugumizi...
"Shem ndio kanionyesha.... Unajua, nilikua natoka kwa
fundi, kuongeza nguo zangu zilizokua fupi... Nikaona mtu kama shemeji Swalehe
akiwa na rafiki yake.. Nikaona niwafuate nyuma ili nijue kwenu, nije kuwaomba
msamaha... Na kweli mpaka rafiki yake akaenda kule na shem akawa anakuja huku..
Ndipo akaniona... Nimemuomba msamaha nae kanielewa, nio akanionyesha kua mnaishi
hapa.. Ila baada ya kunionyesha, yeye akaondoka zake... Samahani kama nimekuuzi
kukutana na shemeji"
Aliongea Zahra huku akiwa kavalia vizuri mavazi ya
heshima mpaka raha yani daahh...
"wala Usijali, mimi sina wivu kiasi
hicho.. Japo nikiona ntaua mtu atari"
Aliongea farida kwa utani utani
fulani hivi..
BAADA YA MASAA KADHAA
KUPITA
Swalehe akiwa ndio anafika nyumbani, lakini wakati huo
Zahra alisha ondoka zake,..
"heeee karibu mume
wangu,."
"Ahsante, hali yako vp hapa"
"safi tu,.. Maji tayari
kaoge uje upate chai"
"eti eeh"
"ndio"
Basi ilikua ni
ndoa iliojaa furaha sana katika maisha yao....
Ikiwa ni mida ya
saa mbili, tukija huku kwa akina Zahra,.... Zahra akiwa na furaha sana kwani
wale watu aliowakwaza wamemsamehe wote...
"leo mbona kama una furaha
hivyo"
Dada yake alimuuliza, na wakati huo Zahra alikua akisonga
ugali...
"dada we acha tu, nina furaha sana"
"kwanini? Au
ushapata shemeji mpya nini"
"hapana dada,.. Kwasasa nataka nitulie
kwanza kwenye swala la mapenzi"
Aliongea Zahra kua kwa sasa acha atulie
kwanza katika swala la mahusiano
"sasa furaha hio ni ya
nini"
"nafurahia kwakua nimepajua wanapo ishi Swalehe na
mkewe"
Aliongea Zahra, lakini fatuma alikasirika sana kuskia
hivyo...
"hivi una akili wewe..."
"kwanini
dada"
"unataka ukavunje ndoa ya watu... Acha ujinga
wako"
Aliongea fatuma au dada yake
"hapana dada... Nina furaha
kwakua nimewaomba msamaha wote wamenisamehe"
Aliongea Zahra na hapo ndio
dada yake akafurahi kuskia hivyo
"aaaahhh ungesema hivyo
sasa"
"yaani dada,.. Wanaishi kwa furaha sana, mpaka natamani kuolewa...
Kwanza dada nikianza kua na mahusiano, staki mwenye pesa.. Mi nataka mwanaume
tuanze maisha yetu,... Tuwe matajiri nikiwa nae"
Aliongea Zahra huku
dada yake akiguna
"mmmhhhh wewe uyo"
"dada? Ina maana mpaka sasa
hujaamini kua nimebadirika"
"naamini hilo, ila kutopenda pesa, sijui
kwakweli"
"Kiukweli dada hutaamini kwa hilo, ila huo ndio ukweli
wangu"
KESHO YAKE, BAADA YA SIKU HIO
KUPITA
Swalehe akiwa zake barabarani kuelekea kwa rafiki yake
bakari, mana siku hio ilikua ni siku ya Jumapili, hivyo ni siku ya
kutembeleana... Sasa Swalehe akiwa njiani ghafla
aliitwa
"swaiiiiii..."
Aligeuka nyuma, kuangalia alikua ni mama
Mwajuma... Swai haamini kua kakutana na balaa la mama huyo... Sasa swai alitaka
kuendelea na safari kana kwamba hakutaka mazoea naye..
"we swai we
nisubiri"
Wakati huo mama Mwajuma ana rafiki yake, na kwa muonekano
walikua wanakwenda harusini,.. Mana hata mtaa aliohamia swai.. Sio kua ni mbali
sana, ni kama mtaa wa tatu kutoka mtaa waliokua wakiishi,.. Katoka mnara wa
voda, kaenda kuishi sombetini, hivyo ni kama mtaa wa tatu hivi kutoka walipokuwa
wakiishi...
"skuizi umepata kuma ndogo,.. Langu bakuli unalikimbia...
Ila jua mtu mzima dawa swai... Hata kama hutaki bakuli langu, basi nisalimie tu
inatosha"
Aliongea mama Mwajuma tena bila aibu kua ana mwanamke
mwenzie...
"shikamoni mama zangu"
Alisalimia Swalehe, lakini
mama Mwajuma akajibu kuwa...
"akuuu, labda huyu ndio mama
ako"
Aliongea mama Mwajuma,... Sasa na huyu mama mwingine akajibu
kua
"aaahh we koma,.. Sina mtoto mkubwa kama huyu,.. Tena nakushangaa
unalalamika.. Ina maana hujui kukaba mpaka penati wewe"
Aliongea mama
huyo mwingine... Swalehe alichoka... Mana alijua mama huyo atakua na busara
kidogo, kumbe ndio walewale...
"eeeeee mama suzy.. Penati haikabwi
jamani na ndio mana nimetulia baada ya yeye kuoa... Mana penati anaachiwa
mlengwa peke yake.. Wao wawili tu.."
"ila kama ni mimi mama mwaju...
Huyu mtoto sio wa kumuacha"
Aliongea mama suzy... Sasa Swalehe akaona
bora aondoke zake mana hakukua na la maana...
"naomba niende
jamani"
Aliongea swai kisha huyoooo
"we mama mwaju... Kijana
mzuri hivi, unamuachaje kwa mfano"
Aliongea mama suzy.. Kumbe nae mama
suzy ni mijimama ya mjini vilevile....
"hapana, watoto watamu kama hawa
hawahitaji haraka... Najua sasa hivi ana hamu na mke wake... Ila nampa miezi
mitatu tu... Atamchoka tu"
Aliongea mama mwaju huku mama suzy
akisema
"au kama huezi niambie...."
"weeeee,mi Nasubiri yule
mtoto wa kike apate mimba... Swai atakuja tu hapa..."
"ni kabila gani
huyu kijana"
"msambaa huyo"
Aliongea mama mwaju tena kwa
nyodo...
"kama ni msambaa, basi ni haki yake... Mana hata mimi nilikua
nae mmoja.. Weeee, mtoto anato***mba huyo... Yaani tena ndio kanifilisi yule
mtoto.."
"sasa huyo ni cha mtoto.... Huyu ni balaaa"
"mmmhhhh
ila mama mwaju,... Hii tabia tutaiacha lini? Mana umri unakwenda
eti"
"aku mwenzangu... Acha nitomb****we kamwisho mwisho, kama ni dhambi
ninazo nyingi tu, hata nikitubu sjui kama zitaisha... Acha watoto wadogo waje
kwangu"
Tukija huku kwa bakari akiwa na Swalehe, kwani alisha
fika kwa rafiki yake...
"Afadhali umekuja, mana najua wewe ndio mshauri
wangu"
Aliongea bakari huku akiweka chai ili wapate
kunywa,...
"mbona chumba chako kimesha kamilika.. Bado mke tu
hapa"
"ni kweli kaka... Ila kumpata huyo mke ni mtihani
shekhe"
"ni kweli kabisa, ila usiwe na haraka na hili"
"wala
sina haraka japo nataka"
Basi walifurahi huku wakipata chai,.. Masaa
yalisonga,.. Kisha waliondoka wote, ili na bakari nae akapajue kwa rafiki
yake.... Mana karibuni marafiki zake wote wanajua alipo hamia Swalehe, na hata
kaka yake anajua, mana ndio alimsaidia kuhama
"karibuni hapa
ndio nyumbani"
Aliongea Swalehe, lakini walikuta ugeni humo
ndani...
"aaahh shem karibuni"
Aliongea Zahra, kumbe Zahra ndio
aliokuja, kwani kwa sasa ni marafiki wazuri
"Ahsante
shem"
Aliongea Swalehe huku wakikaa katika kiti..
"we mama
Rashid, vp chochote huko"
Aliongea Swalehe huku mama rashid
akijibu
"mbona tayari mume wangu.. Ni nyie tu"
Aliongea farida,
huku akiandaa chakula, na Zahra alikua akiandaa maji, yaani Zahra kawa mwema
moja kwa moja, utafikiri wana undugu na farida...
Sasa bakari
bado hajajua mke wa swai ni yupi, mana wote wana hekima kama
mapacha....
"Swalehe, acha nivunje ukimya... Mkeo ni yupi
hapa"
Aliongea bakari lakini wale wanawake hawakusikia swali
hilo...
"mke wangu ni yule mfupi mnene na mweusi,.. Huyu mrefu mweupe,
ni ndugu yake"
"sasa kwanini hunitambulishi mapema"
Aliongea
bakari.... Kisha swai aliwaida wote
"mama rashid... Huyu ni rafiki
yangu, anaitwa bakari, ni fundi mwenzangu"
"ooohhh karibuni sana
shemeji"
"Ahsante sana shem, nimefurahi kukufahamu"
"na huyu..
Ni ndugu yake... Anaitwa Zahra"
Aliongea Swalehe huku Zahra na bakari
wakipeana mikono ya kutambuana
"nashukuru kukufahamu nami naitwa
bakari"
Aliongea bakari lakini papo hapo simu ya swai iliita...
Kuangalia jina alikua ni fundi wake...
Swalehe alitoka nje kwenda
kuongea naye...
"hallo fundi habari yako"
"salama swai, vipi upo
wapi"
"nipo nyumbani"
Wakati huo huku ndani, bakari na
Zahra, kama vile wanaangaliana kiwizi wizi flani hivi.. Zahra alitoka nje,
ghafla na bakari naye alifuata nyuma... Wakati huo Swalehe anaongea na fundi
wake
"Zahra?? Zahra??"
Bakari aliita baada ya Zahra
kutoka nje,.. Sasa farida yeye alikua chumbani, ikumbukwe kua wamepangisha
daborumu
Sasa farida kutoka haoni mtu hata mmoja
Hakua na
wasiwasi sana japo anamuona mume wake anaongea na simu ila wengine
hawaonekani....
"abeee"
"simama basi bibie"
Aliongea
bakari kisha Zahra akasimama
"unakwenda wapi"
Aliuliza
bakari,...
"unajua sijapenda... Umeniangalia sana mpaka najiskia aibu..
Na haileti picha nzuri kwakua ni hapo ni kwa watu"
"ni kweli, ila sio
kwa ubaya... Katika macho yangu, nahisi kuona kitu kizuri kwako"
"kitu
gani hicho shem"
Aliongea Zahra huku akijifunika funika.. Bakari kumbe
tayari keshapenda
"nilikua natafuta mtu wa kuishi nae katika maisha
yangu,.. Sijui kama nimekupata"
Aliongea bakari lakini Zahra kakaa
kimya
"Zahra?"
"abeee"
"unanifaa kua
mke"
Aliongea bakari, Zahra haamini kwa mara nyingine tena anataamkiwa
kua mke... Aliwaza sana mambo ya nyuma, na kujisemea katika moyo wake
kua
"Mwenyezi Mungu, ana makusudi yake.. Huenda huyu ndio
bahati yangu... Siwezi kumtupa kama nilivyo mtupa Swalehe... Mungu anisamehe,
kwani naweza kumringia na nikamkosa..."
Alijiongelea mwenyewe
huku akimjibu bakari...
"Samahani shem... Labda uende nyumbani kwanza
uonane na dada etu mkubwa, akikubali nami nipo tayari"
Aliongea Zahra,
bakari haamini.. Yaani kaona tu kwa muda mchache, kataka mke
"kuja kwenu
sio tatizo... Tatizo lipo kwako, kuridhia maisha yangu... Labda nikwambie ukweli
wa kazi yangu.. Na pia maisha yangu kwa ujumla"
Aliongea bakari lakini
Zahra alimkatisha na kumwambia...
"usijali.. Najua una kazi kama shemeji
Swalehe, na sijaipenda kazi yako, bali nitakupenda wewe.. Kama kweli umenipenda,
basi twende nyumbani wakakujue"
Aliongea Zahra kwani hataki tena kuwa na
mahusiano yasiojulikana kwa dada yake...
Na bakari ana haraka ya kuwa na
mke.. Alijikuta anakubali.... Sasa swai anashangaa watu wanasonga
mbele..
"we bakari?? Vp mbona sielewi"
"nakuja bwana kaka
nisubiri"
"skia basi ndugu yangu"
Aliongea Swalehe lakini ghafla
sms iliingia kwenye simu yake... Kuangalia ilikua ni namba ya Zahra, na sms
ilisema hivi
"shemeji Swalehe, naomba usimwambie tabia
ulizowahi kuziona kwangu... Amenipenda, nami nimempenda... Na sasa tunakwenda
kwa dada akamjue, nataka anione yeye... Tafadhali sana shemeji, nilindie heshima
yangu"
Aliandika hivyo wakati wakiwa wanakwenda,.. Basi Swalehe
hakutaka tena kufuatlia... Ila alibaki kucheka tu
"heeeee wale nao
vipi"
Aliuliza farida baada ya kuona watu wameshikana mikono kuelekea
huko
"washapendana wale"
"mmhhhh kwani walikua wakijuana kabla
ya hapa"
"hapana, ila bakari anataka mke.. Nadhani hata Zahra
vivyohivyo"
"lakini mbona mapema mno"
Aliongea farida kisha swai
akamjibu
"kwani mimi nawewe tuna muda gani?? Mbona nimekuoa??... Sheria
za dini yetu ya Kiislamu zinasema kuwa... ALIEKUFA NA AZIKWE HARAKA KWAKUA HANA
HAKI NA DUNIA TENA.... LAKINI PIA KWENYE NDOA DINI INASISITIZA KUA.. MWENYE
KUOLEWA AU KUOA NA AOLEWE AU AOE HARAKA SANA KABLA MMOJA WAO KUBADILI MAWAZO...
Hivyo tuyaache yale hayatuhusu sana.. Kama wamependana, acha
wakatambulishane..."
Aliongea Swalehe huku wakiingia ndani na mke
wake....
BAADA YA MASAA KADHAA KUPITA
Ikiwa ni
mida ya jioni hivi... Swalehe akiwa na mkewe, walishangaa ugeni,.. Walikua ni
akina bakari wanarudi....
Zahra alikua na furaha sana, kwani alimrukia
farida kwa furaha sana...
"Zahra una nini wewe"
"dada katupa
baraka zote juu yetu"
"ina maana umekubaliwa kuoana"
"yes... Na
sasa bakari ni mchumba wangu"
Aliongea Zahra... Na wakat huo Swalehe na
bakari wapo nje....
"ila bwana kaka una zambi sana
wewe"
Aliongea bakari huku Swalehe akishangaa
"kwanini sasa, na
zambi zangu zinakujaje apo"
"yaani mi natafuta mke, kumbe shemeji yako
yupo huniambii"
"aaaaaaaaaaaa, sasa mi najuaje kama mtapendana...
Tuachane na hayo.. Kesho tuna safari ya kwenda Mwanza, kuna jengo la kwenda
kujenga, litachukua miezi miwili"
Aliongea Swalehe, kwani alipewa
taarifa na fundi wake,...
"aaahhhh.... Sasa mi nitaoa lini
aiseee"
"acha haraka... Fanya kazi
Kwanza"
BAADA YA MIEZI MITATU
KUPITA
Ikiwa leo ni siku ya furaha kwa watu wawili baina ya
bakari na Zahra... Lakini mbaya zaidi Zahra alikua akilia sana,.. Wakati huo
kafunikwa mtandio maalumu wakati wa kufungishwa ndoa yao... Bakari alipata hofu
sana baada ya kuona Zahra analia bila sababu.. Hofu ilimjaa
bakari...
Baada ya ndoa kupita wakiwa wapo nyumbani kwa
Swalehe, mana pale kwa Swalehe pana kisehemu kikubwa kubwa
kidogo,...
"farida, hebu kamuulize mwenzio alikua analia nini wakati wa
ndoa, mana bakari mpaka sasa ana hofu juu ya hilo"
Aliongea Swalehe huku
farida akitekeleza alicho agizwa na mumewe....
"unaionaje siku ya
leo"
Aliongea farida kumuuliza Zahra...
"Kiukweli nina furaha
sana... Nalia hivi sio kua sijapenda... Yaani siamini kua nami nimekua mke wa
mtu... Siamini kama nimeolewa,.. Nilihisi mume wangu bakari ananidanganya
kunioa... Kumbe kweli... Farida??? Nampenda bakari..."
Aliongea Zahra,
na wakati huo bakari yupo na Swalehe nje wakijadili mambo ya kazi,, yaani
Swalehe muda wote ni mtu wa kazi, wakati mwenzie anawaza mke waondoke
zao....
"sasa, kwakua tumerudi Mwanza juzi tu... Sasa tusubiri kazi
zingine"
Aliongea Swalehe lakini bakari kama haelewi...
"aisee
mambo ya kazi tutaongea kesho.. Ita tax tuondoke
zetu"
"ahahahahahahahahahahahahahhaha... Aisee una haraka
wewe"
Aliongea Swalehe huku bakari akiingia ndani,.. Alikua anapenda
kumuona mkewe kila wakati...
"mume wangu.. Twende kwetu
basi"
Aliongea Zahra huku akimkumbatia mumewe... Wakati huo tax
inaitwa...
Swalehe alikuja ndani kumchukua bakari,
"njoo nje...
Achana nao wakae ndani hao"
Wakati huo huku ndani.... Farida
alikua akimpa maneno rafiki yake...
"Zahra, kwa kawaida huwa kuolewa sio
kazi.. Kazi ni kuilinda ndoa yako... Usifuate maneno ya watu,... Kwahio usione
ajabu kuolewa, ila jitahidi kuiheshim ndoa yako... Usimjibu mumeo vibaya,
mtengee maji pale anaporudi kazini... Mpe vile vitu anavyopenda... Mimi sina cha
kukuambia, mana wewe mwenzangu ulikua na kungwi, hivyo najua kakupa somo
vizuri... Ila nakuomba sana, mpende mumeo mheshim mumeo... Hapo utaiona raha ya
ndoa yako..."
Aliongea farida huku Zahra akitoa machozi kwa kua.. Kumbe
alikua akimkosea sana farida kipindi kile.. Kumbe alikua anamkosea mtu ambae ni
nuru katika maisha yake...
"pia.. Mumeo akipata Shukuru, akikosa muombe
mungu kesho apate... Na hata akikosa tena, usikasirike... Zidisha kumuombea
mumeo,... Achana na utajiri wa majirani au watu wengine, huo hauwahusu... Mpende
mumeo, ipende ndoa yako"
"PIIIIII... PIIIIIII.
PPPPIIIIIIIII"
Ni sauti ya honi ya gari ikilindima huko nje, bakari
aliingia ndani fasta na kumchukua mkewe, waliingia ndani ya gari wote ili
kumsindikiza mwenzao mpaka kwake.. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Zahra na
bakari....
MWISHO WA STORI HII YA WAPANGAJI
WENZANGU....
MWISHO
0 comments:
Post a Comment