Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE ISLAMIC WIFE - 2

 

     

     



     

    Chombezo : The Islamic Wife

    Sehemu Ya  Pili (2)

     

     





    Wakati huo huku kwa akina zena, zena akiwa dukani akiuza bidhaa ndogo ndogo kama sehemu ya kujipatia riziki yake japo hana majukumu yeyote yale lakini kapewa kamtaji na baba yake hivyo kafungua kiduka cha bidhaa za kawaida tu...

    Mara alimuona rafiki yake dija,

    "heeeeee dija... Ulikuwa wapi wewe, siku hizi hata madrasa sikuoni kabisaa"

    Aliongea zena baada ya kumuona dija, mana wanajuana vizuri sana

    "we acha tu zena....  As Salaam Aleykum warahmatullah wabarakatuh"

    "Waleykhu msalam warahmatullah wabarakatuh.. Haya vipi hali yako"

    "aahh tunamshukuru mwenyezi Mungu anasaidia"

    "haya za wapi saa hizi mida ya kuswali hii"

    Zena alimuuliza hadija kuwa saa tisa hii anakwenda wapi na mida ya kuswali mana hata zena wakati huo alikuwa akitandika mswala (mkeka spesho wa kuswalia) ili aswali swala ya alasiri...

    "we acha tu zena... Huu mguu ni wako huu"

    Aliongea hadija huku akikaribishwa vizuri ndani

    "enhee haya karibu tuswali kwanza.. Kisha tuendelee na maongezi yaliokuleta"

    Basi zena na hadija waliswali hapo hapo mana mida ulishafika... Na kuswali ni popote pale kikubwa uwe na uzu (usafi wa mwili)..

    Baada ya kumaliza kuswali walipiga dua ya kumaliza ibada yao.. Dija alimisi sana vipengele vya kuswali, mana toka rahim aje, hajawahi kutoka nyumbani... Japo ni mfanyakazi tu



    "enheee niambie dija... Umesema mguu huo ni wangu"

    "ndio zena.... Kuna ujumbe nimekuletea kwako toka kwa kaka rahim"

    "heeeee yule si mtoto kwako yule, sa kwanini awe anakutuma"

    "najua sana, kale ni katoto sana kwangu... Yaani nalingana na kaka yake yule jamali, lakini rahim hanieshim tena ndio kwanza ananipeleka puta, nafanya mpaka kazi ambazo hazina ulazima"

    "mmmhhh pole sana... Najua ni haki yako mana ndio kazi yako"



    "sasa zena... Rahim kaniambia leo mkutane"

    "we, usiongee kwa sauti hivyo... Wazazi watasikia"

    "sawa, lakini ujumbe ndio huo alionipa"

    "hapana... Mwambie siwezi kukutana kafiri"

    Aliongea zena huku roho ikimuuma kweli

    "hapana zena... Hayo sio maneno ya kumwambia, nipe jibu zuri nikamjibu, yule ni boss wangu lazima nitoe maneno ya heshima hata kama ni mtoto kwangu"

    "sikiliza dija... Yule mkaka hata mimi pia nimejikuta tu nampenda... Yaani sio yeye tu,... Huezi amini madrasa kwetu kuna wavulana wengi sana, tena wenye hekima mbele za mungu na kwa wazazi wao... Lakini sijawahi kumpenda kijana wowote kati yao.. Nilishangaa sana kwanini nilijikuta nampenda yule... Tena nampenda sana tatizo ni tabia yake"



    "enheee hapo hapo... Yaani hapo ndipo unapoongea pointi ya msingi sana.... Sasa yule sio wa kumjibu hivyo,... Kikubwa wewe mkubalie tu"

    "dija wewe ivi nitaanzaje kumwambia nakupenda, vile alivyo mhuni, eti mimi mtoto wa Kiislamu nimelelewa na wazazi wangu wote... Leo nikamtaamkie nampenda... Haaaaaa labda abadilike"

    Aliongea zena huku akitaka kuamka kwa hasira

    "sasa we ulifikiri atabadilikaje bila kuwepo na mtu wa kumwambia?"

    "hata wewe pia unaweza kumwambia abadilike"

    "hapana... Mimi siwezi, ila wewe unaweza"

    "kivipi sasa"

    "sikia... Wewe mkubalie.. Halafu kaa nae chini kama mpenzi wako.. Mpe maneno makali, mi naamini atabadilika tu... Hebu ona... Toka aje mimi sijawahi kuja madrasa, toka aje mimi sijawahi kufunga ushungi, lakini leo kunituma kwako kaniruhusu kuvaa ushungi.. Yaani mpaka nimeshangaa jambo hili"

    Sasa zena akakumbuka kuna siku alimpa vigongo vyake kule hospitali alipokuja kumwona,..

    "sawa... Ila nenda kamwambie kuwa asije akiwa kalewa...."

    "sawa... Unajua zena mi nataka uwe wifi yangu, afu unaliinga"

    "sio hivyo dija... Tatizo kaka enu sjui kalelewa vipi yani"

    "sasa wewe ndio unatakiwa uwe mama yake.. Mana anaonekana kakuja moyoni mwake we acha tu"

    "kweli akibadilika,... Mimi sina tabu mana moyo wangu umetua pale ila tabia yake sasa ndio mbaya"

    Zena aliongea huku akimtoa dija kama kumsindikiza

    "sasa tabia hio wa kuikomesha ni wewe"

    Basi dija aliondoka zake kisha zena akarudi dukani kwao na kuendelea na mauzo kama kawaida,...



    Wakati huo hadija kafika nyumbani na kumkuta rahim anaangalia miziki kwenye TV, na alikuwa akiifurahia kweli miziki ya Bongofleva.... Ghafla hadija kaingia huku akicheka Cheka, rahim akahisi tu mambo yatakuwa mazuri huko

    "Enheee dada dija kuna nini"

    Heeeeee leo hadija kaitwa dada, haamini yaa saa hadi saa rahim anazifi kubadilika... Na hapo hajakunywa wiski zake wala wine, yaani toka alipokunywa jana ndio mpaka sasa hivi...

    "mambo safi tu... Ila.. Kasema kuwa, ili mkutane, hutakiwi kunywa pombe, hataki unywe pombe kuanzia leo"

    Hadija kaongeza chumvi, yeye kaambiwa akija aje akiwa hajalewa lakini hadija kaongeza chumvi kuwa, kuanzia leo asinywe pombe... Saa ngapi rahim hajaamka kwa hasira

    "ati nini... Anikataze pombe akiwa kama nani.. Yeye ni nani yangu"

    Sasa hadija kuona rahim kawa mkali, ikabidi anyooshe maelezo vizuri

    "ah ah, kasema hivi ukienda hio jioni usilewe, hajasema uache pombe"

    "sasa mbona ulisema, kasema niache kunywa pombe"

    "nilikosea kaka"

    Sasa kumbe jamali alikuwa ndani keshakuja, kusikia kila kitu

    "haaaaaaaa... Sasa itakuaje"

    Rahim aliongea hivyo huku akishika kichwa, kana kwamba ni kitu kigumu sana kwake

    "kwani huezi kukaa hata siku moja bila kunywa kaka"

    "kazi yako imeshaisha nenda kaendelee na kazi zingine"

    Rahim alimuamuru hadija akaendelee na kazi.... Sasa dija alipoingia chumbani kwake alimkuta jamali,....

    Kumbe jamali na hadija wana mahusiano,m ya kimapenzi wanapenda mno...

    "we jamali umekuja saa ngapi huku"

    "muda sio mrefu.. We ulikuwa wapi"

    "nilipeleka ujumbe kwa zena... Sasa zena kaniambia nimwambie rahim aende wakakutane akiwa hajalewa"

    Jamali alicheka sana kusikia hivyo, mana anamjua sana mdogo wake alivyo

    "sasa unacheka nini baby"

    "hadija.."

    "abeee"

    "unamjua bubu alivyo"

    "ndio... Bubu si mtu ambae hawezi kuongea"

    "sasa... Rahim asipokunywa pombe.. Yaani kuongea jambo kama hilo hawezi kamwe... Yaani hata mwanamke awe mzuri vipi... Kwanza hatoweza kumsalimia.. Cha pili anakuwa kainamiana kama kondoo.. Yaani asipokunywa anatia huruma huyo, we umuone hivyo... Hatokaa kwenda bila kunywa, hilo sahau, mana atakwenda kumchekea tu kama chizi"

    "ivi unasema kweli jamali??"

    "bila shaka huo ndio ukweli.... Na kama huyo mwanamke anampenda mdogo wangu... Basi nenda kamwambie kuwa amruhusu anywe hata glasi moja tu ya wine... Bila hivyo wataishia kusimama tu hapo walipokutana"







    Katika dunia wanaume tupo tofauti kabisa hususan katika upande wa kuongea na wanawake kwa nijia tofauti kabisa,... Kweli wapo watu hawajui hata kuongea na mwanamke mpaka azingue kichwa chake, sasa kumbe rahim ana tatizo hilo, ujanja wake woote, kumbe asipolewa anakuwa kama kondoo.... Dija alifikisha ujumbe kwa zena, na zena hakuwa na hiana, mana kaambiwa kama kweli unampenda basi wewe ndio ufanye kazi ya kumbadirisha... Heeee atabadirisha wote lakini sio rahim,....



    Wakati huo rahim anaumiza kichwa itakuwaje asipopata hata grasi moja ya wiski, ili mdomo uwe mwepesi wa kuongea,... Wakati rahim akiendelea kuumiza kichwa ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni baba yake

    "haloo dady, shkamoo"

    Alimsalimia baba yake huku akiwa na shauku ya kukutana na zena...

    "Marahaba ujambo...... Sasa rahim, hebu nenda hapo bandari ya Tanga kuna jenereta limefika ulipelekea sehemu husika"

    Aliongea baba yake, mana akina rahim wanadili na mambo ya usafirishaji wa mizigo au bidhaa za watu, hivyo kuna mzigo kutoka china unatakiwa kufika kwa wenyewe na kwakuwa rahim na jamali wapo tanga, basi ni rahisi kulifikisha kwa wahusika mana baba yao yupo kenya kuna biashara kaifuatilia....

    "sawa dady"

    Basi rahim alikubali kufanya kazi hio, na hapo hapo akawa anakwenda chumbani kwa kaka yake ambae ni jamali,... Lakini kabla hajaenda huko, alisikia sauti ya kiume kutoka chumbani kwa dija,... Saa ngapi rahim hajachungulia, alikuta kaka yake ananing'inia tu...

    Rahim alikuwa hajui kama dija na jamali kumbe wana mahusiano ya kimapenzi,... Ikabidi atumie simu kumpigia... Alimweleza jinsi alivyoambiwa na baba yake,.. Lakini kwa utamu wa mapenzi jamali alikataa kwenda,.. Rahim hakutaka kupoteza muda, alichukuwa gari kisha akatembea mbele kuelekea bandarini,.. Ikiwa ni time ya saa kumi hibi za jioni, rahim anafika bandarini kila mtu anamshangaa mtoto mdogo afu ni tajiri, lakini hawajui kama ni mtoto wa mzee Rashidy, mana gari alioingia nayo hapo, ni kichefuchefu kwa matajiri wengine walioko hapo bandarini,....

    Meli ilioleta mzigo ikiwa ndio kwanza inatia nanga,... Haraka haraka anapewa Documents za jenereta hilo ili kleni ianze kazi yake ya kulishusha,



    "boss, clan ipo tayari, sasa gari ya kutolea hapa mpaka msikitini litakuwa wapi"

    Rahim kusikia linakwenda msikitini, aliomba karatasi ya malipo

    "unasema ni jenereta la wapi?"

    "ni la msikitini boss"

    "limeshalipiwa"

    "aahhhh hapana ila litalipiwa mpaka likifika sehemu husika"

    "ebu lete karatasi ya charging"

    Akapewa karatasi ambayo ni Way Bill ya malipo,...

    "khaaaaaa.... Mbona wamechajiwa pesa ndogo hivi?... Nani kachaji hii mashine"

    "mzew wako"

    "hapana.... Hii pesa ni ndogo sana, haliwezi kitoka china mpaka hapa.. Afu lilipiwe milioni mia moja tu?... Haiwezekani"

    Rahim alimpigia baba yake simu, wakati huo mashine inashushwa kuingia katika gari

    "Eeenn haloo dady... Mbona hii mashine imesafirishwa kwa gharama ndogo hivi"

    "rahim.. Hio ni mashine ya msikitini"

    "lakini dady... Kwani kuna siku tulishawahi kula au kulala msikitini"

    Rahim alikuwa hajui kama kuna cha nyumba ya ibada wala nink, yaani yeye anachotaka ni hela tu,... Hajuagi neno msaada, hajui neno kutoa sadaka, yaani yeye yupo yupo tu

    "ok.. Ebu we fanya hilo unalohisi ni sawa"

    "eew hilo ndio jibu sasa.... Huu mzigo ni wa milioni 200 huu.... "

    "ok... Sawa.. Afu waambie hao vijana wakupatie pesa ya mwezi mzima.. Kisha uipeleke benki"

    "sawa"



    Sasa kule kwa pembeni kuna watu waliokuwa wakishangaa ni mtu gani huyu asiejua mambo ya dini, hajui hana jambo la kutoa sadaka kwa watu,...

    "huyu ni tajiri gani tena... Ama kweli wahenga walisema kuwa tajiri ni ngumu kuingia kwenye tundu la sindano...... Eti rehema huyu ni nani"

    Ni wanawake fulani waliokuwa nao wamejitanda Kiislamu wamevalia nikabu zao saafi Kabisa,

    "huyu si mtoto wa mzee rashidi.."

    "mzew Rashidy huyu huyu mwenye hio meli iliosimama hapo"

    "ndio... Huyu ndio mtoto wake wa pekee"

    Aliongea mwanamke huyo kuwa rahim ni mtoto wa pekee kwenye hio familia, hawajui kama kuna jamali,..

    "lakini mbona baba yake mkarimu sana kuliko mtoto... Hebu ona mashine inakwenda kufanyia kazi za ibada, lakini yeye halijui hilo"

    "sikili shamy,...huyu mtoto naskia amelelewa vibaya mno, yaani ana dharau huyo"

    "mmmhhh au labda atazikwa na pesa zao"



    Watu walikuwa hawaamini kwa kitendo anachokifanya rahim,.. Rahim alichukuwa kitabu cha kuandikia way bill kisha akaandika upya kuwa inatakiwa ilipiwe milioni mia mbili na sio milioni mia moja kama ilivyoandikwa awali..

    "alafu hashim... Mzee kaniagiza unipatie pesa za transport za mwezi mzima"

    "sawa boss"

    Hashim alikimbia haraka mpaka ndani ya meli hio ya mzee Rashidy,... Kweli akina rahim ni matajiri haswa lakini pesa zao hazina faida kwa jamii, tena ndio kwanza mtoto mtu ananyanyasa walala hoi...

    Begi la pesa lilitolewa utafikiri kuna nguo humo nfani, kumbe ni pesa zote

    "boss... Hizi hapa"

    "sasa unanipa nibebe mimi au? Peleka kwenye gari huko"

    Aliongea rahim, yaani rahim yupo kidikteta zaidi, na hakuna wakumsemesha mana yeye ndio mbadala wa baba yake, au kaka yake jamali,...

    "boss, huezi kuzihakikisha tu"

    "ivi we hashim una akili kweli wewe... Yaani begi lote hilo mimi niliesabu, huo muda anao nani... Peleka begi ndani ya gari.. We niambie ni kiasi gani"

    "ni bilioni 7 pointi 4"

    "sasa bilioni saba, naanzaje kizihesabu kw mkono.... Safari za maji zinakupunguza akili wewe"

    Basi hashim aliingiza begi hilo la pesa ambazo zimepatikana kwa njia ya usafirishaji wa mizigo au bidhaa mbali mbali za watu... Hivyo hizo ni ingizo la mwezi mmoja kwenye meli hio moja... Bado kwenye magari makubwa yanayosambaa mikoani na nje ya nchi... Bado hizo sheli walizonazo.. Bado wana supermarket mbili... Arusha na Dar es Salaam,.. Lakini sasa pesa zao zinajaa tu benki hazina hata faida, na mtu mbaya zaidi ni rahim anaetaka pesa zijae tu benki... Unaambiwa kwa Tanzania mzee Rashidy ndio anaongoza kwa pesa, lakini hatangazwi na wala hajulikani... Basi rahim aliondoka na mashine hio kuelekea sehemu husika







     





    Sasa huku kwenye makutano kati ya zena na rahim.... Maskini ya mungu zena yupo chini ya mti akimsubiri rahim aje, wakati huo ni mida ya saa 12 za jioni zena alikuwa anakwenda madrasa,... Sasa akaona akutane na rahim kisha aondoke,.. Lakini kakaa weee, haoni mtu,.. Mpaka zena akachoka kukaa, ikabidi aondoke lakini alikuwa kakasirika mno, na wala hataki kuskia jambo la rahim tena,..

    Sasa zena alipofika mbele alikutana na dija anatoka dukani

    "we dija wewe... "

    "heeeee zenaaa... Pole rafiki yangu, najua utakuwa umemsubiri eti eeeh"

    "sana tu yaani, yaani mpaka nimechoka"

    "mwenzangu weee... Kilichomfanya asije ni kwamba... Kumbe asipolewa hajui hata kuongea yaani ni kama bubu unaambiwa"

    "heeeee, yaani asipolewa hawezi kuongea"

    "yaani sio kuwa hawezi kuongea... Yaani namaanisha ukikutana nae naskia atainamisha tu kichwa chini kama kondoo"

    "mmmhhhhh, basi.. Na mimi kukutana na mlevi Kiukweli siwezi, tena mwambie anikome kabisaa"

    "heeeeeee zenaaa... Yamekuwa hayo tena"

    "lakini dija... We si unajua ukali wa wazazi wangu wewe... Hivi leo niwe na mahusiano na yule kaka yenu, itakuwaje, si nitauwawa mimi..."

    "basi humpendi kala etu"

    "dija Usiseme hivyo,.. Nampenda sana tu, lakini tabia yake hakuna mtu anaipenda Kiukweli"

    "mmmhhh we haya bwana.. Kwaheri, lakini kaa ukijua wakumbadirisha mi wewe na sii mwingine... Na kama unampenda mruhu ukutane nae hata kama kalewa, akutaamkie tu anakupenda we mkubalie.. Kitakachofuata hapo ni kumkataza yale yasio faa"

    Aliongea hadija kuwa zena akubali tu akutane nae hata kama kalewa kikubwa yu ni mataamshi yakamilike

    Zena hakumjibu kitu aliweka juzuu zake katika begi, mana alikuwa akijisomea pale alipokuwa akimsubiri rahim...



    Sasa kumbe ile mashine au jenereta linapokwenda ndio hapo hapo anapokwenda kisomea au kiswalia zena,.. Wakati huo zena wapo rosheni ya juu, mana ndio upande wa wanawake, na chini ni wanaume.. Ulikuwa ni msikiti mkubwa sana mkoani Tanga, na ndio ulioagiza jenereta kutoka china,.. Kweli palikuwa na mshekhe wakubwa, mawalii wakubwa wakubwa...  Mamufti wale wenye makarama yao, Waislamu wazito wazito hivi waliokuwa wakilisubiria jenereta hilo



    Mashekhe hao walimkaribisha rahim kwa furaha, wakizani ni. Mtu mwema kumbe ni kishetani cha duniani,..

    "As Salaam Aleykum warahmatullah wabarakatuh"

    Walimsalimia rahim karibia mashekhe wote... Tena huku akipewa na mikono ya baraka,...

    "safi tu, mambozenu"

    Heeeeeeee mashekhe walishangaa huyu ni kijana wa wapi, tena ni Muislamu lakini hata kuitikia salamu ya Kiislamu hajui,.. Tena mabaya zaidi anawaambia MMBOZENU? Mashehe walipiga astah khafirulah wote, lakini rahim haelewi kitu, Wakati huo zena anaona chini lakini hajui kama ni rahim, waumi walikuwa wakifurahi kwa jenereta hilo kufika, mana umeme unapozimika hua wanakosa mawaidha mazuri yatolewayo na Mashehe wao,..  Sasa rahim akawapa ile karatasi ya malipo, Mashehe walishangaa kuona kiasi cha malipo kimekuwa kikubwa zaidi,

    "shekhe jumaa, mbona milioni mia mbili badala ya mia moja"

    Mmoja wa mashekhe alimuuliza shekhe mwenzie, na wakati huo sasa kumbe hata baba yake na zena nae ni mmoja wa mashekhe hao... Alipomuona ni huyo kijana, aliona hapa ipo shuhuli pevu,...

    "huyo kijana ni mshenzi sana.. Yaani hapa hio mashine haitoshuka bila hio pesa kutolewa"

    Aliongea baba yake zena, aliokuwa kavalia kanzu yake saafi na kibaraka shehe,..

    "kwani we unamjua huyu kijana"

    Wakati huo rahim yeye yupo kwenye gari yake anasikiliza muziki wa Bongofleva, tena kwa sauti bila kujali kuwa hapo ni msikitini,.. Palitakiwa kuwa na heshima,..

    "ndio... Tena ndio aliowahi kunigongea mtoto wangu yule mdogo... Afu mbaya zaidi nikaanza kumuona analeta ukaribu na binti yangu"

    "mmhhhhh sasa hii pesa mbona ni kubwa,.. Pesa yenyewe tumeichangisha ndani ya miezi 6 ikapatikana hio milioni mia moja.. Haya hii mia moja ilio ongezeka hapa tunaitoa wapi"

    Mara rahim katoka ndani ya gari,

    "jamani vipi... Nipatieni pesa mchukuwe mzigo wenu... Mimi nikajua mnazihesabu kumbe mnang'aa macho tu"

    Baba yake zena alikuwa anatikisa kichwa tu, kana kwamba anayoyafanya huyu kijana, hata shetani hafanyi hivyo,... Sasa kule juu zena keshamjua kuwa ni rahim,.. Huezi amini zena alikuwa analia, mana rahim hajui umuhimu wa mashine hio,..

    "zena, ivi unajua kuwa rahim anakupenda sana"

    Aliongea fadhila huku akitaka kumshawishi akatoe neno pale chini



    Wakati huo mashekhe wanarudisha karatasi ya malipo, ikiwa na maana ya kwamba wameshindwa kulipia hizo gharama, japo na pesa yenyewe ya kulinunua imechangishwa ndani ya miaka mitano, na bado hawajamaliza kulilipia jenereta hilo, mana ni yale majenereta makubwa ambayo umeme ukikatika linajiwasha wenyewe,.. Majenereta yanayotakiwa kukaa katika hospitali zote, nyumba za ibada iwe kanisani au msikitini,... Rahim alimwamuru dereva ageuze gari waondoke zao,.. Wakati huo fadhila bado anazidi kumshawishi zena, akajaribu kumkubalia huenda akaliacha

    "fadhila... Baba yule pale chini, nitawezaje kufanya hivyo... Na istoshe rahim hakosi bunduki yule,.. Akiniua je?.. Hapana bora waondoke tu, kwanza simtaki tena"

    Aliongea zena kwa uchungu huku machozi yakimtoka kwa wingi sana,.. Na Wao walikuwa wakiangalia kwa chini, yaani akina zena wapo rosheni ya juu, sasa wanaangalia chini... Kweli rahim mtoto wa Kiislamu aliokosa utu, anadiriki kugeuza gari lake na gari ilioleta jenereta igeuze waondoke nalo mpaka watakapolilipia waje walichukiwe,... Kama unavyojua vilio vya wamama wanaoijua dini,...

    Sasa hapo hapo madrasa ya wanawake, pia mama yake zena yupo, mana hio ni familia ya Kiislamu, hivyo wote wanajua wajibu wao juu ya kujua maandishi ya Mwenyezi Mungu,... Fadhila alimkimbilia mama yake zena kule kwa wamama...

    "mama zena... Mshauri zena aende akamzuie yule kijana"

    "weeeee weee, unataka mwanangu aingie matatizoni... Yule mtoto nimesikia sifa zake ni mbaya"

    "mama... Kumbuka jenereta lina umuhimu sana hapa msikitini... Kwanini asifanye hivi"

    Aliongea fadhila na wakati wamama wanalalamika kweli kwa kitendo cha rahim kukosa hata ile staha ya ubinaadamu,...

    "sasa zena ni nani yake mpaka aweze kumzuia"

    "rahim, anampenda sana mwanao, yaani anampenda mno"

    "ati unasemaje wewe.... Yaani mwanangu apendwe na yule kafiri, tena kanigongea mtoto wangu kamtia kovu la maisha"

    Sasa fadhila kugeuka nyuma, hamuoni zena....



    Wakati huo huku chini magari ndio yanaondoka,... Ghafla mzee mvungi au baba yake na zena, anashangaa kumwona zena akiwa kasimama katikati ya barabara... Tena huku gari zikiwa na mqendo mzuri tu... Mzee alitamani kupaa mpaka pale,... Zena kapiga moyo konde, na rahim akisimama tu basi lazima kieleweke, lakini asiposimama basi mashine itakwenda na jinsi ya kuipata hakina, labda wajichange tena kwa mwezi 6 kama ilivyo ya awali.. Sasa mama ndio nae anashangaa kumuona zena kasimama katikati ya barabara, eti anazuia hizo gari zisiondoke... Sasa hapo kinachoangaliwa ni upendo bali sii kingine....







    Sasa tunataka tujue zena alikubali vp kwenda kufanya tukio lile, na wakati alibembelezwa na fadhila lakini akakataa katu katu,.. Sasa kama unakumbuka saa ile fadhila anakwenda kwa mama yake na zena kumwambia amwambie mwanae akajaribu kuzuia jenereta lisiondoke, mana anachokifanya yule kijana sio kitu kizuri katika nyumba ya ibada kama hio, ni mtu gani asiojua dini.. Sasa fadhila alipoondoka, kuna wamama watatu wenye heshima zao na wao walikuwepo madrasa hapo wakijifunza mambo mbalimbali ya qur-aan.. Walimsogelea zena huku wakimwambia kuwa

    "tumesikia kuwa yule kijana anakupenda sana, na sisi ni watu wa zamani.. Na kidini hairuhusiwi mwanamke wa Kiislamu kuolewa au kiwa na mahusiano na mwanaume kafiri... Yule kijana ni dhahiri kuwa ana imani ya kikafiri yule... Lakini kama nawe unampenda na yeye anakupenda,... Basi jaribu kufanya hili zoezi, na ukifanikiwa, basi kuna uwezekano mkubwa huyu kijana kutulia... Tunakuomba mtoto wetu yule ni shetani tu anampitia, hebu jaribu upendo wako"

    Aliongea mama mmoja mwenye busara zake,...

    "ni kweli,.. Kama mtu ana uwezo wa kubadirika basi basi hakuna tatizo katika dini"

    Aliongea mama mwingine mwenye busara zaidi

    "sisi kama watu wazima tutakuwa nawe bega kwa bega lakini kile kifaa kisiondoke hapa msikitini, hata Mwenyezi Mungu atakufungulia milango ya baraka juu yak"

    Huyu ni mama mwingine kana kwamba wote watatu jambo lao ni moja



    "mama zangu, kweli natamani kufanya hivyo, lakini wazazi wangu... Hawataki niwe na huyu kijana"

    "sisi tupo juu yako... Swala hili tuachie sisi"

    Zena akiwaangalia wale wamama ni watu wazima na hekima zao, afu msikiti mkubwa sana yaani tanga yote, msikitini mkubwa zaidi kuliko yote tanga nzima ni huo, ambao una kila kitu ndani yake... Kina madrasa ya watoto, kuna madrasa ya watu wazima, na pia kina madrasa ya bijana wakubwa kama akina rahim, kuna ukumbi wa kufungishia ndoa za Kiislamu, kuna sehemu kubwa sana za kuswalia,... Yaani ni jengo kubwa sana na linahitaji kifaa kama hicho kwa nia ya kutokatiza mawaidha au wakati wa kuswali pindi umeme unapokuwa umekatika.... Zena kweli aliwasikia na kunyanyuka, alikuwa juu ya ghorofa lakini alishuka na kwenda kusimama katika kati ya barabara, huku juu fadhila anageuka hamuoni zena,... Mama nae hamuoni mwanae, wote sasa wakawa macho chini kuangalia kile anachokifanya zena,.. Sasa huku chini baba mtu kaona mtoto wake anachokifanya, mzee mvungi hataki utani na familia yake,... Alinyanyuka katika kiti na kutaka kwenda kimzuia, lakini hawa mashekhe wengine, wanajua upendo ulivyo, kwahio walimzuia kwanza shekhe mvungi ili waone matokea juu ya mtoto wa kike.... Na hapo kinachoangaliwa ni upendo na sii kingine



    Rahim kweli alisimamisha gari yake, mana yeye ndio alikuwa mbele na lori lenye mashine lipo nyuma yake akiliongoza,...

    "we unataka kufa mbele za watu"

    Zena kuskia hivyo aliogopa mno, lakini akajikaza tu, mana mpaka kitendo cha kusimama ni dhahiri kuwa anamuheshim sana zena, mana uwezekano wa kumkwepa ulikuwepo mkubwa sana lakini rahim hakutaka kumkwepa...

    "bora uniue kuliko kuondoka na kitu kitakachoweza kusaidia umati wa watu.... Hebu angalia watu wote hao, wanatamani uache hilo jenereta, lakini kwa ulivyo na roho mbaya kqeli unaondoka nalo.. Huna hata aibu rahim, wewe ni Muislamu wa nchi gani wewe,... Kwani pesa ni kitu gani"

    Wakati huo zena akiyaongea hayo mama kule juu anatetemeka kwa woga, mana ni familia ambayo haina kitu lakini anakwenda kuongea maneno makali mbele ya mtu mwenye kitu, ni kuji risk maisha... Lakini sasa kumbe alichokisema jamali kuwa rahim asipolewa na kukutana na mtu ampendae hua haongei,... Sasa zena akawa anasubiri jibu,... Lakini kabla ya kujibiwa akakumbuka maneno ya dija kuwa

    "mmmhhh zena... Kumbe rahim asipolewa anakuwa kama kondoo mbele ya mwanamke anaempenda"

    Alipokumbuka hilo, zena alisogea karibu na rahim kisha akamshika mkono, rahim kumbe kweli anampenda zena, japo hatujui kama ana nia gani kati ya kuoa au kichezea tu,...

    "rahim.... Kama unanipenda kweli, utaiacha hii mashine... Lakini kama hunipendi basi ondoka nayo"

    Zena Aliongea hivyo kwa ujasiri huku akiamini kuwa hapa hakuna lolote,..

    "Samahani kaka, naomba mshushe hio mashine"

    Aliongea zena, lakini wale watu walishindwa kifanya hivuo mana wanasubiri kauli kutoka kwa boss,..

    "rahim, waamuru basi watu wako"

    Rahim alinyoosha tu kidole juu kisha akaonyeshea chini, maana yake jenereta lishushwe.... Waumini wote hawaamini, huezi amini hata zena alikuwa analia kwa furaha,..

    "rahim,... Naomba jioni tukutane kama ulivyotaka.... Lakini Please nakuomba ukija usije ukiwa imelewa sana, kidogo tu inatosha ili tu uongew na mimi.... Ahsante kwa kinielewa"

    Zena alimruhusu rahim aje akiwa kashtua kidogo, mana kama atakuja akiwa hajashtua basi hakuna atakacho ongea, yaani hata neno nakupenda kwake ni zito,.. Na hii watoto wa matajiri ndivyo walivyo asilimia chache kutongoza hawajui, wanajivunia pesa zao tu,... Sasa sehemu ambayo haitumii pesa, wanapata shida mno....

    Na zena kumruhusu ashtue haina maana anywe kila siku No, bali alimwambia ashtue ili aweze kumtaamkia hata hio nakupenda tu inatosha, mana asipokunywa hatoweza kuitaamka... Na rahim anakuwa domo zege mbele ya mwanamke anaempenda lakini kwa mwanamke ambae hana hisia nae,.. Doooohhh utasemwa wewe mpaka ukimbie... Zena aliondoka na kwenda kwenye ile mashine, wasichana wenzake walimpongeza, wamama walikuwa wakilia kwa furaha ya mashine hio, mana waliichangia kwa miaka kadhaa iliyopita mpaka pesa ya kununulia ikapatikana,... Na hapo bado haijaisha kulipwa sema wachina nao sjui waliona huruma kwa kuwauzia kwa pesa nusu...



    Mzee mvungi haamini kama mtoto wake ndio sababu ya mashine hio kubaki, tena sasa uzuri zaidi hata ile milioni mia moja ilioandikwa na baba yake haijachukuliwa, maana yake ni kwamba imesafirishwa bure mapaka hapo, lakini ni kwa nguvu za zena,..



    Akina rahim na timu yake ya kwenye meli waliondoka zao, ila rahim yeye alielekea benki kuweka maingizo ya meli,... Mashine imeletwa na ndege mpaka mahali fulani ndio ikapakiwa kwenye meli mpaka Tanzania,.... Wakati huo sasa huku madrasa mama mtu anafuta jasho utafikiri ni yeye ndio kafanya ile kazi,..

    "mama zena,.. Kweli pale kuna upendo wa hali ya juu... Kikubwa ni kwamba mwacheni mtoto wenu afanya atalo"

    "hapana mama salma,.. Yule kijana hawezi kuwa na mtoto wangu.. Sitaki"

    Zena akisikia hivyo anatamani hata kulia

    "hapana mama zena... Yule kijana kuna uwezekano mkubwa kubadirika.. Kikubwa mtoto wako ajitambue tu yupo katika hali gani"

    "sawa, lakini yule kijana sio Mtu eti"

    "hio kazi mwachie mtoto wako... Kikubwa tu we mpe ruksa"

    Mama yake zena hakujibu chochote kile na hata kule chini mzee katuliza mzuka baada ya mashine kubaki kwa nguvu za mtoto wake, rahim kweli ni ibilisi sio mchezo....







     





    Ikiwa ni mida ya saa mbili kasoro usiku, rahm akiwa nyumbani kwao, na wakati huo alikuwa anachapa grasi za kutosha, na kuambiwa ashtue tu, ili akataamke tu kuwa anampenda, mana mwanamke kuanza kumwambia mwanaume kuwa anampenda, ni jambo gumu sana kwao, na pia sio maadili ya mtanzania kwa mwanamke kumtaamkia mwanaume kuwa anampenda,... Lakini zena anampenda kweli sema tabia za rahim sio nzuri...

    "bibi, eti mjukuu wako anakunywa ili akakutane na mwanamke"

    Jamali aliongea hayo kana kwamba anamkandia rahim,

    "hata huyo mwanamke mwenyewe hana akili, kama ni mimi sikutani na mlevi"

    "bibi, afu huezi amini ni yule mdada mweupe pale mtaa wapili"

    "nani huyo.."

    "kuna kabinti keupe kanapita pata hapa nje"

    "au ni yule mtoto wa mzee mvungi"

    "atakuwa ndio huyo.. Anapenda kuvaa nikabu hivi"

    "sasa yule binti na huyu mwehu wapi na wapi"

    "nashangaa mimi"

    Jamali na bibi yake walikuwa wanamsema rahim

    "sasa wewe, na huo usharobaro wako na mtoto wa watu mshika dini... Unataka kumpotosha au... Hebu ona huona huo mkofia aliovaa..."

    "bibi, kila siku mi namuambia huyu mjukuu wako, haendani na yule binti hataki kusikia"

    Wakati huo rahim yeye anaongeza vigrasi vya wiski, wakati aliambiwa ashtue tu lakini anakunywa grasi za kutosha...

    Alipomaliza wala hakuongea na mtu, huyoo, tena hatumii gari wala nini, mguu wake, na wakati huo vinywaji bado havijamkolea vizuri katika mwili, mana kabigonga sasa hivi tu...

    Kweli alipofika mahali chini ya mti alimkuta zena akiwa kasimama... Mtoto kanyooka kila kona tukiongelea uzuri ndio kabisaa hatusemi kitu...

    "umevaa zile nguo zako tena.. Sa ntakuonaje"

    Aliongea rahim, na wakati huo sasa pombe imeanza kukolea ukilinganisha na vile alivyotembea, ndio kabisaa imempa joto

    "rahim... Mi sijakwambia unywe hivyo"

    "kwani kuna shida gani"

    "usiniguse... We ongea hapo hapo"

    "lakini si uliniambia wewe au hukumbuki"

    "rahim... Niamnie basi mi niende"

    "sa mbona uko mbali ivo"

    Zena hakuwa na hamu tena ya kukutana nae mana hakumwambia alewe hivi, sasa kaja kalewa sana, kana kwamba mpaka zena anaona kero,...

    "kwani wataka nini kwangu"

    Aliongea zena japo anajua kile anachokitaka rahim,

    "zena, ivi ni mwanaume gani utakaempata na anaekupenda kama mimi... Kiukweli nilikuwa nachukia sana watu wanaovaa mavazi ya kufunika macho... Lakini toka nikutane na wewe nimeona ni kawaida tu... Zena??... Nakupenda eti"

    Zena alisikia kwa masikio yake akitaamkiwa kuwa anapendwa,... Tabasamu zito lilimjia zena,.. Unajua kuambiwa unapendwa sio jambo dogo eti

    "rahim...  Nimekuelewa viziri tu... Na sio wewe tu, hata mimi Pia nakupenda... Lakini sasa kwa tabia yako ya kwenda baa, mi siwezi kuwa na wewe"

    "zenaaaa.... Mi nanywea nyumbani"

    "sasa sikia.... Kama kweli wewe unanipe..... "

    Sasa kabla zena hajamalizaa kuongea, alishangaa kumwona baba yake akiwa nyuma ya rahim,... Sasa rahim yeye hajui na kule kulewa ndio kabisaa haelewi,... Zena katulia tu wala hasemi,

    "yaani umevua mpaka nikabu kwa ajili ya huyu mtu....."

    Aliongea mzee mvungi na hapo rahim ndio akajua kumbe nyuma yake kuna mtu,...

    "aaahhhh dingi.. Mambo Vipi"

    Rahim aliita na kumsalimia mzee huyo, wakati huo zena anamkataza rahim asiongee lolote,..

    "ngoja niongee na baba mkwe"

    Wakati huo rahim pombe ndio zimemzidi kichwa

    "ivi mwanangu... Katika kutafuta kwako koote, umemuona huyu"

    Aliongea mzee huku rahim akidakia juu kwa juu

    "aahhhhh mzee, kwani mimi sio mtu?"









    Hakuna kitu kibaya kama ulevi, kwasababu ulevi hua hautambui umuhimu wa mtu aliopo mbele yako, kila mtu kwako ni sawa tu, sasa rahim kasimama na baba mkwe lakini anamuona kama mshikaji mwenzie tu, na hata majibu anayomjibu sio ya heshima kama inavyotakiwa,...

    "wewe kijana mbona ni mdogo sana lakini mambo yako ni ya kikafiri tu"

    Aliongea mzee mvungi, huku rahim anatikisika tu kwa ukali wa kinywaji alichokunywa,..

    "mzee, pesa.... Kuna kitu kinashinda pesa hapa duniani"

    Mzee aliona kusimama na huyu mtu ni sawa na kumsapoti tu

    "sikiliza we kijana.... Sitaki ufuate mtoto wangu, sema nimepunguza hasira kwa kile ulichokifanya kule msikitini japo ni kwa nguvu ya mwanangu, lakini... Sitaki tena nikuone nae"

    "ah ah, mzee kwani tatizo nini... Hela au?"

    "siuzi mtu"

    "mi nataka kuoa eti"

    Zena kuskia rahim kataamka neno nataka kuoa, alishangaa, mana walevi au masharobaro hua hawaoagi,..

    "kwa hali hii utamuoa nani.. Pumbavu wewe"

    "aahhh mzee ume mind sio"

    "kwenda zako... Zena... Sitaki kukuona na huyu mtu..."

    Zena hakujibu chochote kwa baba yake,... Rahim aliachwa peke yake pale chini ya mti, lakini ukweli keshauongea kwa zena, na zena keshajua kuwa anapendwa na rahim tena sana tu,... Sasa ile anataka kuondoka ghafla anakutana na fadhila nae alikuwa anatoka zake dukani, mana fadhila na zena hawapo mbali sana, fadhila alisharudi nyumbani na kubadili mavazi yake, na fadhila yeye ni mtoto wa Kiislamu lakini yeye malezi aliopewa ni malezi ya kawaida tu, yaani ni kama rahim, sema tu kidogo fadhila anaifuata dini, na fadhila yeye anawajua wanaume haswa,.. Wakati huo rahim kaachwa peke yake na fadhila yeye alikuwa akipita tu, na hakutegemea kumkuta ram maeneo yale,...

    "heeeee rahim mambo"

    Wakati huo rahim pombe imezidi kumkolea kichwani mana pombe za matajiri hua hazipandi haraka, ikiwa na maana kuwa kama mtu huyo kainywea mjini, hivyo kitendo  ha kutoka mjini kwenda kwake, kinawezekana hata kama anaendesha gari, hio sio kiroba wakati huo huo uko tilalila, sasa rahim huezi amini yani na ile pombe hata kusimama vizuri sio kivile, mana kanywa grasi nyingi sana,..

    "powa kwani we nani"

    Aliongea kwa sauti ya ulevi huku akipiga hatua moja mbele, hatua mbali nyuma, kana kwamba hapo haendi mtu,...

    "jamani ni mimi fadhila"

    "fadhila yupi Uyooooo"

    "mmmhhhh afu rahim umelewa wewe"

    "we unamjua aliolewaaaaaaa"

    Rahim alipomaliza tu kuongea alizidiwa na kuanguka chini,.... Mpaka hapo hakujua kilichoendelea







     





    Kesho yake asubuhi rahim anaamka nyumbani kwao,.. Alikuwa akijivuta sana afu kidogo kawa mwepesi lakini alikuwa kachoka mno,.. Ilikuwa ni mida ya saa nne hivi za asubuhi,..

    "vp broo"

    Alimsalimia kaka yake aliokuwa anaangalia tv huku akinywa chai

    "poa niaje"

    "freshi tu......daahhh sjui leo wachawi wamenilimisha leo"

    "wapi hao.... Hao wavaa kanzu na nikabu au?"

    Aliongea jamali mana rahim wachawi wake hua ni Waislamu, yaani Muislamu kwake ndio mchawi... Kweli pesa ina dharau sana...

    "ah ah, broo sijasema kuwa Waislamu ndio wamenilimisha, afu ilo swala naomba life, mana ukisema wachawi ni hao, basi hata zena wangu ni mchawi"

    Sasa rahim aliposema zena,... Jamali kuna tukio kalikumbuka

    "ahahahahaha kumbe yule aliokuleta jana ndio zena"

    "nani kanleta jana??...mimi si nilikuja mwenyewe"

    "we bwege nini... Si uliletwa hapa na mdada maji ya kunde hivi sjui mweupe mi sijui.. Kakuleta hapa saa saba za usiku"

    "saaa saba???.... We umeota wewe.. Siamini kumbe hata wewe unaotaga"

    Rahim alikataa kuwa jana aliletwa na mtu, tena mwanamke...

    "aahhhhh niache bwana nikaoge"

    Sasa alipokuwa anakatiza kona kwenda kuoga, alikutana na dija nae anatoka kuoga, si unajua wadada wakitoka kuoga wanakuwaje,.. Rahim katoa macho, macho nayo hayajatosheka, ikahamishiwa kwenye ubongo, ubongo nao haujatosheka, ikahamishiwa kwenye damu, damu nayo haijatosheka ikapeleka kule chini, kule chini nako hakujatulia,... Na hapo ndio rahim anagundua kiungo chake kilikuwa kikiuma baada ya kusachi network,...

    "sasa ram, unamwangalia dija humjui"

    Jamali aliongea kwa hasira mana dija na jamali wana mahusiano ya kimapenzi hivyo rahim alipokuwa anamwangalia dija, jamali alichukia sana kana kwamba labda rahim alimtamani...

    "Samahani broo... Ila mbona kiungo changu kinauma"

    "sasa unamwambia nani... Jana ulipokuja saa saba hapa afu unasema kiungo chako kinauma"

    "broo, mi sijafanya kitu jana... Afu jointi zote zinaniuma"

    "nennda zako kaoge uko, afu hujaoga kabisa jana"

    Rahim aliingia zake bafuni lakini kweli anajihisi kuchoka, japo kaka yake anamwambia jana kuletwa saa saba za usiku,... Na hata kama kaletwa muda huo kwani kuna ulazima viungo vyake vijiskie kuchoka

    Sasa alipoingia bafuni alivuta kumbukumbu ya jana, lakini kila akivuta inaishia pale pale zena alipo ondoka na baba yake, kwahio hakumbuki kuwa, baada ya hapo alikutana na fadhila,...

    "au zena alirudi nini... Mbona broo anakazania nililetwa na mwanamke"

    Rahim alijiuliza na asipate jibu sahihi,

    "huyu broo atakuwa sio mzima huyu.... Lakini sasa mbona nimechoka utafikiri nililala na mwanamke?"

    Rahim alijikuta hata kuoga anachelewa kwa kuwaza maumivu ya viungo vyake, na maumivu hayo ni dhahiri kuwa jana alikuwa na mwanamke

    "ahahahahhahahah... Zena mjanja sana, yaani kajifanya kaondoka afu karudi... Mmhhh lakini kanikwangua mno"

    Rahim alipata jibu kuwa ni zena ndie alie mpeleka nyumbani, lakini sisi wasomaji tunajua mtu wa mwisho kukutana na rahim ni fadhila, hivyo kama anahisi kitendo kama hicho basi ni fadhila

    Rahim alimaliza kuoga, kisha akarudi mezani kupata chai,.. Wakati huo inakwenda saa sita mchana, lakini wao ndio wanakunywa chai,... Ghafla simu ya rahim iliita,... Kuangalia jina alikuwa ni mama yake mzazi

    "haloo mamy, shkamoo"

    "Marahaba ujambo"

    "sijambo mama vp uko chuga"

    "safi tu... Naona umekuwa kimya sana hakumbuki kama kuna kurudi shule"

    "aaaaa mamy, mbona bado wiki nzima, acha nile bata kwanza"

    "sasa utajiandaa vipi jamani"

    "mamy, nitakuja baada ya siku hizi hizi"

    "sawa, ila hakikisha unakuja hapa siku mbili kabla ya kwenda shule sawa"

    "sawa mamy"

    Simu ilikata huku rahim akikasirika mno,...

    "uyu mza nae"

    Aliongea rahim huku akiitupa simu kochini...

    "kwani vipi dogo"

    "ah maza uyo"

    "kasemaje kwani"

    "anataka nirudi home eti mambo ya shule shule aahhh"

    "utaki sasa au?..."

    "aahhh bado bado"

    "lakini ukumbuke ni mwaka wako wa mwisho huu, tena unakwenda kumalizia tu"

    "najua... Au nawe wanikandia nini"

    "kunywa chai ujue swaga zingine"

    Basi rahim alikaa kitako na kugonga chai, baada ya kumaliza kunywa chai.. Alitamani sana kukutana na zena, ila kwa mida hio ya mchana hawezi kumpata mana yupo nyumbani, mida yake mizuri ni ile ya jioni wakati akienda madrasa, au akirudi madrasa, hua ndio mida mizuri ya kukutana nae,... Sasa rahim anapajua vizuri nyumbani kwa akina zena, basi akawa anatembea zake kwa mguu taratibu,.. Alipofika alipiga jicho kule kwao, kwa bahati nzuri zena alikuwepo dukani, mana hapo hapo kuna kaduka hivi na zena anapenda kuuza yeye, ila ikifika jioni anakwenda zake madrasa, ila kuswali hua anaswalia hapo hapo dukani,... Sasa rahim anatafuta gia ya kuendea pale dukani ili amuulize kwanini jana kaenda kulala nae wakati akiwa kalewa, hilo tu ndio swali kwake,... Sasa rahim akakaza moyo mpaka pale dukani, na hapo alikuwa hajalewa, na duka hilo lipo hapo hapo nyumbani, hivyo mzee akitoka tu atamuona rahim,...

    "mambo zena"

    "sema As salama Aleykum warahmatullah wabarakatuh"

    "mmmhhhhhh hio ndefu sitoweza kuitaamka"

    "afu umekujaje sa hii wazazi wangu wapo"

    Rahim mwanamke akishakuwa wake hua kuongea anaweza lakini ni kwa upole utafikiri kondoo,..

    "kuna kitu nataka nikuulize zena... Kizuri sana ila sijui kwanini umenivizia nikiwa nimelewa"

    "nimefanya nini"

    Sasa wakati huo huo fadhila nae anatokea nae alikuwa anakuja kwa zena, lakini alipomwona rahim pale dirishani, alibana mahali, na alikuwa akisikia yaliokuwa yakiongelewa na rahim....

    "mmmhhh eti unajifanya hujui... Jana ulinifanyia nini... Mpaka saa saba za usiku"

    Sasa zena yeye anashangaa maneno ya rahim,... Lakini sasa kule kwa fadhila nae alikuwa anajiuliza kuwa

    "khaaa... Ina maana rahim hakumbuki tukio la jana??.... Safi sana.... Wacha amwambie ili zena akasirike na waachane..... Rahim. Lazima awe wangu"









    Maneno ya fadhila aliokuwa akijisemea mwenyewe baada ya kusikia kuwa rahim hakumbuki mtu aliyekuwa nae mpaka saa saba za usiku,... Fadhila alifurahi sana kuskia hivyo kuwa rahim hakumbuki tukio la jana,... Na rahim wakati huo hajui kama fadhila yupo jirani na anasikia... Hivyo mpaka sasa tunajua fadhila ndio alikuwa na rahim jana usiku kucha, sasa ni pombe gani hizo mtu asijui

    "we rahim wewe, jana mimi si nilikuacha mwenyewe"

    Rahim ukumbuke ni mpole sana mana hajalewa, ila dharau za pesa zipo pale pale hata kama hajalewa,

    "sikiliza zena,.. Mi najua unaona aibu lakini unafahamu ulichonifanyia jana usiku... Afu kwani kulikuwa na haja gani unipeleke nyumbani saa saba hio.. Ungeniacha tu nimalize afu na asubuhi safi tu"

    Aliongea rahim kama tunavyomjua tabia yake, hua hachagui cha kuongea hata kidogo,... Lakini wakati huo zena anashangaa kwa kile anachokiongea rahim.... Kwahio kutokana na maongezi ya rahim, zena keshajua jana rahim kafanya nini.... Sasa zena ile anajiandaa tu kumjibu rahim, ghafla mzee mvungi huyo katokea kwa uwani

    "we kijana wataka nini hapa"

    Aliongea baba yake zena asiotaka zena awe karibu na huyu kijana

    "shkamoo mzee..."

    Rahim alimsalimia, na nilishakwambia kuwa rahim akiwa hajalewa, anakuwa mzuri sana ila dharau za chini chini kutokana na pesa zao, haziishagi siku zote... Na rahim hawezi kupitisha siku bila ya kulewa, yaani ni lazima,... Iwe kalewa tilalila au kagusa kidogo, lakini haachi hata siku moja,...

    "nakuuliza unataka nini hapa nyumbani kwangu"

    "Samahani mzee, nimekuja kununua kalamu"

    Rahim aliongea kwa upole, na hapo kidogo hata mzee akashangaa,.. Mbona jana kajibiwa kihuni na leo hali imekuwa tofauti,...

    "ina maana koote hakuna maduka umeliona hili tu au"

    "Samahani mzee... Zena, basi usinipe hio kalamu"

    Rahim akajifanya kasusa kabisa kuchukuwa hio kalamu, lakini pia sio kuwa aliitaka hio kalamu, ni basi tu gia zake za kuondokea baada ya kukutwa na mzee

    Rahim aliondoka zake taaratibu kisha huyooo, fadhila nae kuona hivyo akaamua kumfuata rahim kule kule alipoelekea,..

    Sasa huku dukani mzee alimfokea sana mtoto wake, lakini licha ya kumfokea, pia alimuuliza kuwa

    "mbona leo kaita mzee, na jana aliita dingi"

    "hapo bado hajanywa vitu vyake"

    "kumbe akiwa hajanywa ni kondoo"

    Mzee ndio anashangaa kusikia habari hio...







     





    Huku sasa fadhila kamkuta rahim kakaa mahari kwenye kivuli, wakati huo jua kali la saa saba hivi inakwenda saa nane...

    "mambo rahim"

    "poa nambie"

    "safi tu.... Naona leo umemfua umpendae mpaka dukani kwao"

    "ndio... Na jana kanipa vitu we acha tu"

    Sasa fadhila roho ilikuwa inamuuma, kitendo afanye yeye, afu sifa apewe zena,... Aliona ni kitu kibaya sana ambacho hawezi kukikalia kimya...

    "kwaio rahim unamaanisha jana ulipata utamu"

    "ahh we acha... Zena ata..."

    Sasa kabla rahim hajamalizia kuongea, fadhila kamstopisha

    "basi, basi basi... Inatosha.. Huyo zena na Uislamu wake ule aje alale na wewe ana kichaa...ulevi ulionae wewe, zena kweli asubutu kuja kulala na wewe na hali ile ya jana"

    Fadhila alivunja ukimya, mana sifa zote hizo zinamfaa yeye na sio zena..  Lakini sasa rahim nae anashangaa kuwa, fadhila kajuaje kama jana alilewa bwax,...

    "we umejuaje kama jana mi nililewa"

    "kwani uliolala nae jana ni nani kama sio mimi"

    Rahim alitoa macho kuskia kuwa jana kumbe alilala na fadhila afu keshaenda kusema ujinga kule kwa zena...

    "unasemaje wewe?"

    "jana ulilala na mimi, na sio zena... Ila nakushangaa sana kwanini hukumbuki"

    "fadhila? Ivi una akili kweli wewe"

    "ina mana mimi sistahili kuwa nawe.. Au mimi sio mwanamke"

    "hata kama.... Lakini unajua kabisa mimi nampenda zena, kwanini umefanya ujinga kama huo,... Fadhila sema asee we chalii umenikera kinoma asee"

    Rahim ameongea utafikiri anaongea na mwanaume mwenzake, kumbe ni mwanamke,.. Na kitu anachokililia rahim ni kwamba, kwanini asingesema mapema, mpaka akaenda kuropoka kule

    "kwahio hujapenda ram"

    "ndio... Kwasababu hukusema mapema mpaka nikaenda kuropoka kwa zena kule"

    "usijali.. Mimi nitalimaliza kwa zena"

    Unajua rahim ni mtoto wa kiume na mpenda starehe sana, hivyo kulala na fadhila sio kuwa kachukia, kufurahia sana mana ni moja kati sehemu ya starehe zake, lakini sasa kitu anachokililia ni kuwahi kumwambia zena na mbaya zaidi zena keshajua kuwa rahim kamaanisha nini...

    "hata kama lakini hawezi kuelewa hata kidogo... Afu umeniwekea nini?, yaani Sikumbuki kitu kabisa jana"

    Rahim aliuliza tena akiwa na hasira mno,.. Na fadhila alionekana kusita kuongea, kana kwamba kweli jana kuna kitu alimfanyia rahim mpaka kutokujitambua,...

    "utanisamehe rahim... Lakini na mimi ni mwanamke, nilishindwa tu kukuambia hata mimi nakupenda"

    "nataka nijue jana ilikuwaje"



    SASA HAPA FADHILA ANATUPA HISTORIA YA JANA JINSI ILIVYOKUWA



    Wakati ule rahim akiwa anamuuliza fadhila kuwa

    "wewe unamjua mtu alielewaaaaaa"

    Papo hapo akadondoka chini kwa ulevi kumzidia,.. Sasa fadhila akaanza kuogopa mana rahim ni mtoto wa tajiri mno, sasa akikutwa nae hapo ataambiwa kamfanya nini, roho ya kumuacha akawa hana,...

    "mungu wangu... Rahim.... We rahim... Ram... Jamani ram amka basi"

    Wakati huo rahim alikuwa akikoroma mno,...

    Yaani usingizi jumlisha pombe, yaani ni usingizi wa pono,... Sasa fadhila kwao hua hakuna jam sana, yeye ana chumba chake cha nje,.. Yani nyumba yao imeungana na chumba chake, kama vile nyumba iliojengwa mfano wa ( L ).. Lakini nyumba ni hio hio moja, sasa fadhila alifikiria ampeleke Kwao, yaani kwao huyu rahim, lakini sasa kwakina rahim ni mbali kidogo kuliko kwa akina fadhila..... Aliona kwa akina rahim ni mbali, Bora ampeleke kwao akampe hata huduma ya kwanza, mana ukiona mlevi kazidiwa na pombe basi ujue hajala akashiba au hajala kabisa



    Dakika tano mbele wakawa wamefika katika chumba cha fadhila, na hapo wazazi wa akina fadhila hawajui kwasababu hicho ni chumba cha nje, kama nilivyokwambia malezi ya fadhila ni ya kawaida tu, sio kama ya zena,... Hivyo mambo ya wanaume anayajua sana, ila sio kuwa kazidisha hapana yaani ni mtu ambaye keshawahi kuwa na mwanaume, simaanishi kuwa ni wengi,... Sasa alipomfikisha hapo chumbani kwake alimlaza vizuri kitandani kwake kisha akaenda nyumba kubwa yaani kwa wazazi wake, akakoroga uji saafi tena wa maziwa, huku ukiwa umejazwa nazi.. Kisha akaja kumnywesha rahim,... Dakika tano mbele rahim kapata fahamu, kumbe ni kweli alikunywa unywaji bila kula, na yote hayo ni kwasababu ya kumuwahi zena kule chini ya mti.. Sasa rahim kapata fahamu, lakini kuamsha macho au kuamka hawezi kwa kuchoshwa na kemikali za unywaji mana ni kali na ukali wake ni wa taratibu sana... Sasa kitu alichokosea fadhila, alijisahau kabisa kama rahim nae ni mwanaume,.. Kumbe alipokuwa anamnywesha ule uji, alikuwa kamkalia kwa juu katika haya maeneo ya flaizi,... Mwanaume hata kama hujaona lakini kuna hali lazima utahisi ni tofauti, sasa utofauti wa hali hio fadhila aliujua, kwasababu alimkali,.... Sasa fadhila aliipenda ile hali huku akijisemea kuwa

    "heeeeeeee.... Yamekuwa hayo tena?"

    Aliongea fadhila huku tabasamu zito likimshuka, lakini sasa aliwaza, mtu huyo kwa jinsi anavyompenda zena,hatokubali kulala nae,.. Fadhila ni mtoto wa kitanga, anajua aingie wapi atokee wapi,.. Kuna dawa alikwenda kuichukuwa, na rahim hawezi kujua kiwa ni dawa au ni tiba bado inaendelea,... Huezi amini rahim alijikuta anapatwa na usingizi wa pono, yaani bora hata mwanzo alivyozidiwa na pombe, sasa hivi ni zaidi ya mara tatu ya wakati uliopita..



    Ilipofika Saa saba za usiku,.. Fadhila alikuwa anafikiria alale nae mpaka asubuhi au inakuwaje,... Lakini akajua tu lazima rahim akasirike pale atakapogundua kuwa usiku mzima alilala na fadhila,... Huezi amini usiku huo huo alimkurupua... Kwa bahati nzuri alikutana na bajaji, aliiita kisha wakaseidiana na dereva bajaji,... Walipofika nyumbani kwa akina rahim, fadhila alikuwa hana hata shilingi tano,.. Fadhila alimsachi rahim na kuitoa pochi yake iliokuwa imejaa pesa nyingi sana Elfu kumi kumi zilizomtia uvivu fadhila kwa kuzihesabu... Fadhila alitoa noti ya shilingi elfu kumi moja tu, kisha akampa dereva bajaji aondoke zake,.. Fadhila aliirudisha ile pochi, lakini dereva toyo hakuridhika kuona pochi imerudi mfukoni na kuna burungutu la pesa

    "we vipi, unarudishaje pochi kirahisi hivyo"

    "sikiliza wewe, mimi nimekulipa ujira wako, swala la pochi halikuhusu sawa"

    "aahhh mbona unanikolomea sasa?.. Hawa ndio mafisadi wa nchi hawa, sio wa kuwaacha tu"

    "huyu kaka ni Mpenzi wangu sawa, naomba uondoke"

    Sasa dereva kuona huyu ni mwanamke tu kwanini ashindwe kuchukuwa pesa yote hio"

    "kwanza pesa ulionipa ndogo hii... Nataka nyingine"

    Ghafla dereva bajaji akatoa chuma katika bajaji yake... Fadhila alianza kuogopa, na wakati huo ni saa saba za usiku, kumetuliaaa

    "mtu mwenyewe fisadi tu huyu afu unamlegezeeea"

    Sasa wakati huo dereva bajaji anamsogelea rahim pale chini,.. Fadhila alikuwa tayari keshaogopa maskini ya mungu,.. Kajibana kwenye nguzo ya geti, na ubaya wa nyumba hio haikuwa na mlinzi, mana tanga ni raha tu...







    Fadhila alikuwa akiogopa sana kwa hali ile,... Lakini pale alipokuwa kaegemea fadhila ni kwenye nguzo ya geti, na hapo hapo kwenye nguzo hio palikuwa na swichi ya kengele ya kubonyeza ili mtu wa ndani aweze kuja kufungua...





    Fadhila alibonyeza kengele ya hapo getini, uzuri ni kwamba jamali na hadija walikuwa hawajalala, walikuwa sebuleni wakiangalia love stories moja ambayo wao waliipenda sana, na kutokulala huko ni kwasababu ya kumsubiri rahim... Mara moja jamali alitoka, na wakati huo dereva bajaji, kasita kuendelea kumfuata rahim kwasababu kengele ilishabonyezwa,..

    "we acha kelele ulichelewa wapi"

    Aliongea jamali huku akija kufungua geti,.. Sasa dereva bajaji kusikia hivyo, alirudi kwenye bajaji na kutimua mbio, mana hapakuwa na ujanja tena zaidi ya kuondoka... Hivyo ndivyo pesa ya rahim ilivyo okoka katika mikono ya dereva bajaji



    Jamali alipofungua geti, alishangaa kuona mdogo wake kashikwa na mwanamke na hakuwa akijitambua,

    "ana nini tena"

    Jamali aliuliza huku akimchukuwa mdogo wake, na wala hakuwa na time ya kumwangalia mdada alionleta

    "mdogo wako kalewa sana eti, kumbe anakunywa hivyo"

    Jamali kusikia hivyo wala hakutaka kuuliza mara mbili mbili, mana kqeli rahim kwa pombe humtoi hata kidogo,.. Basi jamali alimchukuwa huku akimwita hadija waje kuseidiana kumbeba,..

    "dada yangu nakushukuru sana kwa kumleta"

    "sawa kaka... Lakini mumpe maziwa freshi usiku huu"

    Aliongea fadhila akijua kuwa dawa aliompa rahim, ili azinduke mapema na awe na kumbukumbu za leo, basi apewe maziwa fresh

    "sawa dada yangu tutafanya hivyo"...Basi Fadhila aliondoka zake kurudi nyumbani na wakati huo alikuwa na raha sana mana tayari keshamjua rahim jinsi alivyo na raha zake... Kweli fadhila anampenda sana rahim, sema sasa ana urafiki mzuri sana na zena.. Sasa akina jamali nao walipo mbwaga rahim walisahau kumpa maziwa, wakajikuta wanarudi kwenye TV na kusahau kabisaaa.....  Huku kwa fadhila keshafika nyumbani, yaani haamini kama masaa mawili yaliyopita alikuwa na rahim, tena sii kwa hali ya kawaida....



    HAPA NDIO MWISHO WA HALI ILIVYOKUWA JANA USIKU... SASA HAPA TUNAENDELEA NA HADITHI YETU, HAKUNA KUKUMBUKA TENA









     





    "hivyo ndivyo ilivyokuwa"

    Aliongea fadhila baada ya kumsimulia rahim jinsi alivyolala nae jana.... Rahim alikuwa hana hata neno la kuongea, kabaki kimya tu juu ya fadhila

    "sasa sitaki huu ujinga ujirudie tena"

    "heeee yamekuwa hayo tena rahim"

    "ndio, we si unajua nampenda zena"

    "sawa, lakini sio lazima ajue... Mi nakupenda ram,.. Kwanza zena sio taipu yako ram"

    Rahim alitoa macho kuskia fadhila kasema eti zena sio taipu yake

    "una kichaa eee?"

    Rahim alimwambia fadhila kuwa ana kichaa

    "kichaa cha nini sasa?... Hebu angalia rahim vile ulivyo... Kweli simsemei dhambi zena ni rafiki yangu.. Yule mtoto wa watu jinsi ninavyomjua... Na hii hali yako, nahisi unamwonea tu"

    "fadhila, mi naona huna jipya hapa... Naomba niondoke"

    "sikiliza sasa"

    "nisikilize nini"

    "zena kuwa nae kwa unavyotaka ni ngumu... Zena kazaliwa ndani ya dini ya kiislamu, zena kakulia ndani ya dini ya Kiislamu, zena kasoma juzuu zote za Kiislamu.. Zena sasa hivi anaendea msafu wa tatu sasa... Zena ni mtu wa dini, zena hapitwi na swala hata moja... Haya wewe na yeye wapi na wapi... Kwanza nimeshangaa sana kuwa hata yeye kakupenda, mana alivyokuwa anasema kuhusu mambo ya mahusiano, yaani siamini kama kakupenda wewe... Inashangaza sana"

    "ni hivyo tu au"

    "rahim, lakini kwanini hutaki kuelewa, hata wazazi wake wenyewe hawakupendi, kwanza kile kitendo ulichokifanya pale msikitini muda ule, ulishajitia doa katika uso wako, leo msikitini mzima uje kuwa wewe na zena mna mahusiano, hio familia si itasuswa"

    "umemaliza"

    "bado"

    "enhee, endelea"

    "rahim... Nakupenda sana, mimi sijali ulivyo, zena hutompata kwa hali hii ya usharobaro huu.. Hebu ona mkofia umeweka mpaka machoni,.. Hata wewe ukijifananisha na zena unakuja kweli"

    "fadhila, una njaa"

    "nimeshiba"

    "sasa wataka nini kwangu.. Au wataka pesa"

    "kama Nataka pesa zako, ningechukuwa ile jana, lakini sikuweza kuchukuwa hata senti tano zaidi ya elfu kumi ya bajaji"

    "kwaio wataka nini kwangu"

    "mi nakupenda"

    "na zena je"

    "zena wacha aolewe na Muislamu mwenzie"

    "kwaio mi mlokole si ndio"

    "kwa jinsi ulivyo huna tofauti na mlokole... Mana nimepiga tumba zooote hapa lakini hakuna hata kimoja kimekuingia kichwani"

    Rahim alikuwa anatamani hata akachape vibao, lakini alimuacha tu na kupunguza hasira zake....

    "fadhila... Cha kwanza kabisa, ebu nenda kwa zena... Mwambie kile nilichokuwa naongea ni pombe tu"

    Rahim yote na yote aliona njia sahihi ya kwenda kumpoza zena, ni fadhila aende kuongea nae,..

    "hilo swala niachie mimi... Lakini jua kuwa mimi nakufaa kwa lifestyle yako"

    "we nenda bwana"

    Rahim yeye anampenda zena, mtoto mzuri, mwarabu sio mwarabu yaani yupo yupo tu kama kimalaika sio kimalaika, na ndio maana rahim kafa kaoza...



     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog