Search This Blog

Thursday 24 November 2022

MKE JEURI - 4

 

     

     

     

    Chombezo : Mke Jeuri

    Sehemu Ya Nne (4)

     



    "ngoja nikuseidie kuvua wifi yangu"

    Mwai alishangaa ni upendo gani wa ghafla mpaka kusaidiana kuvuana chupi, huezi amini rey alikuwa akivua huku akimshika shika mwai, kana kwamba rehema alikuwa akimtaka wifi yake kimapenzi, Lakini sasa wote ni wanawake......  Mwanaheri aliinama na kujiseidia haja ndogo kisha wakachukuwa vipimo kupitia mkojo, sasa wakati huo mwai anashtuka kwa kuona kipimo kimeonyesha kuwa ana ujauzito,.. Kumbe rey yeye tayari kesha data na wifi yake..

    "wifi nina mimba eti"

    Aliongea mwai huku akiwa na furaha ya hali ya juu,

    "unasemaje wewe"

    "siamini kama nina mimba"

    Kipimo kilionyesha ni kweli mwai ana mimba, je hio mimba ni ya nani?

    "waoooooo Jamani wifi yangu kumbe una mimba kweli"

    Aliongea rehema huku akiwa na furaha ya hali ya juu, lakini furaha hio haikuwa bure tu,.. Sasa mwai alishangaa kumwona wifi yake anamshika shika kama vile mwanaume anaetaka kuanza mapenzi kwa mkewe,..

    "wifi una nini tena"

    Aliongea mwai huku akimgeukia rehema na kumwangalia, alimwona rehema kalegeza macho kama mtu aliokula kungu,..

    "wifi, kwanza nina furaha ya kwamba una mimba ya mdogo wangu,.. Lakini utanisamehe kwa kile nitakachokwambia"

    Aliongea rehema huku bado akiendelea kumahika shika mwanamke mwenzie

    "usijali wifi yangu we ongea tu"

    Wakati huo mwai yupo mtupu kama alivyozaliwa yan.. Naye moyoni mwake anafuraha ana mimba lakini sio ya sheby

    "nakupenda wifi tangu... Yaani jinsi alivyokupenda mdogo wangu basi hata mimi Nimekupenda hivyo hivyo"

    "una maana gani wifi"

    Mwai aliuliza huku akidhani huenda akawa ni mwanamke mwenye jinsia mbili

    "nataka nifanye mapenzi na wewe Please wifi yangu nakuomba... Wewe una umbo zuri, limenivutia"

    "kwahio kumbe weww ni mwanaume"

    "hapana, mimi ni mwanamke"

    Rehema alijikuta akavua nguo zote ili kumhakikishia kuwa yeye ni mwanamke na sio mwanaume,...

    Mwai alithibitisha hilo, huku akiona aibu kwa kupendwa na mwanamke mwenzie,..

    Rehema alikuwa na tabia ya ulesbian (ufanyaji wa mapenzi wa jinsia moja kwa wanawake)

    "wifi wewe ulikuwa chuo ee"

    Mwai aliuliza, mana wasichana wengi wenye tabia hio ni wale wanaosoma shule za bweni, hua wanazipenda sana tabia kama hizo za kufanya mapenzi ya wenyewe kwa wenyewe..

    "ndio, nimerudi jana tu"

    Alijibu rehema huku akiendelea kumshika shika mwai... Sasa mwai nae alijikuta mwili wake unapata joto kwa kushikwa shikwa na wifi yake,

    "wifiiiiiiii... Twende chumbani"

    Aliongea rehema huku akimvuta ili watoke hapo bafuni

    "heeeeee nikupeleke chumbani kwa kaka yako"

    "kwani si mara moja tu"



    BAADA YA SIKU HIO KUPITA



    Hatukujua kama wawili hao walifanya chochote au laa, lakini dalili zote tuliziona kwao...  Sasa leo ikiwa ni siku nyingine,..

    "mama, ina maana yule ni mkwe wako lakini kwanini humpendi"

    Aliongea rehema huku akiwa kasimama kana kwamba anataka kumwambia mama yake ukweli

    "kwahio wewe umemuona ni mzuri"

    "ndio.. She is beautiful na ana umbo zuri tena mdogo wangu hajapotea pale"

    Mama alikasirika sana mana alitegemea yeye ndio atakwenda kuleta mbwembwe ili waachane, lakini matokeo yake ni kwamba ndio kwanza wanapendana...

    "ivi rehema una akili kweli wewe, lile gume gume nalipeleka wapi mimi"

    "mamaaaaa.... Sasa sikia, kama mwanao kakudanganya hawajawahi kufanya lolote sasa mkweo ana mimba tena ya wiki hio, moja tu"

    "unasemaje wewe"

    "mkweo ana mimba mama, jiandae kuitwa bibi"

    "ina maana sheby kunidanganya aliposema hamjui mkewe hata kidogo"

    "mamaaa yule ni mtoto wa kiume hawezi kukuweka wazi kwa kila kitu"

    "una uhakika ana mimba"

    "ndio"

    "hapana, sheby hawezi kunidanganya hata kidogo, yaani hio haingii akili mwangu kabisa, na hio mimba sio ya kijana wangu"

    Rehema baada ya kuona mama yake hataki kuelewa aliondoka zake na kumwacha hapo sebuleni,.. Moja kwa moja hadi kitandani kisha akampigia wifi yake simu

    "haloo wifi mambo"

    Alianza rehema kisha mwai akajibu

    "safi wifi yangu"

    "yaani wifi nashukuru kwa ulichonipa jana"

    Aliongea rehema huku akiwa anatabasamu sana tu

    "ila wifi unaonekana upo Addicted na haya mambo ee"

    Aliuliza mwai huku wote wakiwa kitandani

    "yaani nikuambie ukweli... Toka nianze chuo nimetembea na mwanaume mara moja tu,.. Yaani natamani nioe au niolewe na mwanamke mwenzangu"

    "heeeeeeeee, sasa hio ndoa itakuwaje jamani"

    "we acha tu, yaani kama sio mdogo wangu kukuwahi, i think ungeshakuwa mume wangu wewe"

    "ahahahahahahahahahaha acha kunichekesha wifi... Niwe mumeo tena"

    "ndio... Yaani natamani uivunje ndoa yako uje kwangu"

    "heeeeeeeeee.. We mwenzangu ntue shost"

    "kwaio vipi leo nije"

    "yes, njooo"

    Rehema alitamani na leo aende, na mwai nae hakukataa kumwita..



    Tukija huki Uswahilini katika nyumba za udongo

    "haya sasa kula kiazi cha leo leo hicho"

    Sheby anahangaika sana, na nia yake anataka kuoa jiko la pili yaani mke wa pili ndio mana anahangaika kutafuta mke bora kupitia hali ngumu ya maisha,...

    Sheby alifika katika boma alilopangisha, lakini hakukuta mtu, na wakati huo ilikuwa ni mida ya saa nne hivi

    "kula kiazi mbatata apo weweee"

    Alikuwa akifanya biashara kwa matangazo ya mdomo wake, mana biashara ni matangazo,..

    "aahhhhh hawa watu wamekwenda wapi tena"

    Sheby alijiuliza baada ya kukuta milango imefungwa na hakukuwa na mtu,...

    "aahh watakuwa wamekwenda kuteka maji tu..... Haaaaaaaaaya kula kiazi mbatata apo weweeeee"

    Sheby aligeuza mkokoteni wake ili arudi barabarani kuendelea na biashara yake...

    "Haaaaaaaaaaaaaaaya kula kiazi cha ch...."

    Ghafla Sheby alisita kutangaza biashara yake, kana kwamba kuna kitu kaona....

    "kula kia.... Kiaaaz.... Kiaaaz"

    Utangazaji ulimshinda na kujikuta akitangaza kwa muda mrefu kwa maneno kidogo tu...

    "kula kiazi u... Ut... Uta... Utamu... Ah ah No... Kula kiazi mbatata"

    Sheby alijikuta anakosea kutangaza bidhaa alionayo na kutangaza bidhaa ambayo hana..









    Wahenga walisema kuwa hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho, na hakuna kizuri kisicho na kasoro. Kijana sheby siku zote ni mtu wa kutafuta mke bora mana nia yake ni kuoa mke wa pili, mana mke alionae kwa sasa sii mke bali ni gume gume, kijana huyo alifika katika chumba alichopangisha huku uswahilini na kukuta chumba kikiwa na kufuli, maana yake hakukuwa na mtu,.. Sheby anaamua kutoka na mzigo wake wa viazi huku akitangaza biashara yake ya uongo na kweli,.. Lakini hamadi alishangaa kumwona zai na shadi wakiwa katika mavazi ya kupendeza sana kitu ambacho sheby alibaki mdomo wazi, haswa haswa vazi alilovaa zaituni lilikuwa vazi la kubana liliomchora umbo lake lote, yaani alipendeza mpaka alikera machoni mwa watu,..

    "zai? Ni wewe kweli?"

    Aliongea sheby huku akimfuata na kumshika, lakini zai alikuwa na wasiwasi sana huku akiangaliana na shadi, wakati huo shadi kaangalia pembeni huku akibofya simu yake...

    "ni mimi au umenisahau mchumba wako"

    Alijibu zaituni huku akijiskia aibu ya hali ya juu...

    "nimefika pale nyumbani sijakukuta ulitoka saa ngapi"

    "mbona nimetoka asubuhi tu"

    "aahhhhh basi nisamehe mke wangu mana nilijua umetoka jana"

    "heeeeee sasa jana nitakuwa nimelala wapi"

    "basi jamani mamy,... Nimeacha viazi pale utapika ule sawa mke wangu"

    "sawa baby"

    "shadi mambo"

    "safi tu hali yako"

    "salama"

    Lakini sheby alimwangalia shadi kwa jicho kali sana kana kwamba shadi kuna kitu kafanya ila sheby hajakipenda kabisa...

    "sasa zai narudi baadae wacha nikauze uze"

    "sawa mume wangu"

    Sheby aliondoka lakini kichwa kilianza kuwaza mambo mengi sana kuanzia hapo hakuwa na raha...



    Huku zai na shadi wakiwa wameshafika nyumbani

    "umeona eee... Mi najua haliwezi jua ulipotoka, ona lilivyopagawa kama sio mpenzi wake vile"

    Aliongea shadi huku akiwa kakaa kitandani

    "nakwambia niliogopa nikajua napigwa vibao pale pale"

    "acha uoga zai,... Hebu angali sasa hivi una shilingi ngapi"

    "mmmhhh shost.. Nakwambia yule boss unajua ilikuwaje, kwanza kanipa simu ya tachi hii hapa... Afu kanipa elfu 50 ya vocha na elfu 50 ya nauli, yqani hapa nilipo nina laki moja na simu mpyaaa"

    "umeona kazi ilivyo tamu eee"

    "mmmhhh lakini shadi? kwani ni lazima tuende kila siku?"

    "yes, . Ukiona dume hili linazingua unaliacha"

    "mmmhhhh sasa si ndio umalaya wenyewe huo au"

    "sasa waogopa nini zai... Ona sasa una simu na pesa taslimu, je ungelala ungezitoa wapi"

    "ni kweli shost lakini mmmhhh"

    Zaituni tayari keshajiunga na CCMT (chama cha malaya Tanzania)..



    Tukija huku nyumbani kwa sheby tunamwona mke wa sheby akitoka kuelekea hospitali,... Alichukua gari yake kisha huyoo kaondoka zake, yaani haamini kama kweli ana mimba

    Mwai anafika hospitalini akiwa na haraka ya hali ya juu mno,..

    "dokta, dokta"

    "habari yako mama"

    "salama tu... Nataka kupima dokta"

    "unapima nini sasa"

    "nataka kujua kama nina mimba, mana sijielewi elewi"

    "ok, punguza presha kwanza"

    Basi mwai alikaa kidogo kisha damu yake ikapoa kiasi, mwai alifanyiwa vipimo vyote

    "ni kweli, una mimba ya wiki moja"

    "mungu wangu weeeee, nitafanyeje mimi"

    Mwai alitoka hapo na kushindwa kuamini kweli ana mimba... Aliingia kwenye gari kisha akachukuwa simu yake... Alimpigia mpenzi wake ambae ni jemsi, mana kama unakumbuka ndoa ya yeye na sheby walilazimishwa ila sio hiari yao, hivyo kila mmoja ana mpenzi wake,..

    "haloo jemsi mambo"

    "poa niambie baby"

    "safi tu, nataka Nikwambie jambo zuuuri"

    "jambo gani tena"

    "we kubali basi jamani"

    "haya niambie"

    "wiki mbili zilizopita tulifanya mapenzi bila hata kutumia kinga... So, leo nataka kukwambia kuwa nina mimba yako"

    Aliongea mwai huku akiwa na furaha,

    "lakini mwai mpenzi wangu... Hali yangu si unaijua lakini.. Mimi sina uwezo wa kuilea hio mimba na pia siwezi kuikubali mana ulishawahi kuniambia umeolewa wewe"

    "James, nilishakwambia huyu mwanaume ni bwege tu hajawahi kunigusa yaani hata mwili wangu haujui ulivyo... Hii mimba ni yako kweli"

    "hapana bwana... Mimi siwezi kukubali"

    "lakini kama hofu yako ni kuilea, basi mimi naweza na sintokuagiza chochote kile, nitailea nwenyewe lakini we kubali tu mimba ni yako"

    "mmmhhh nitaamini vipi"

    "akizaliwa tutampima"

    "ok sawa"

    Mwai alifurahi kuskia james kakubali kua hio mimba ni yake....







     





    Sasa tukija huku kwa mama yake zaituni akiwa kakaa na mtoto wake zainabu ambaye ni pacha wa zaituni pamoja na jamila ambae ni dada yao mkubwa,

    "mama ivi jana yalikuwa macho yangu au nilikuwa naota"

    "kwani uliona nini na wewe"

    Mama aliuliza kwa mshangao,

    "nilimwona zaituni saa nane za usiku"

    "mschiuuuu... Nitolee ndoto zako za usiku mimi"

    "kweli mama nilimwona mwanao tena alipendeza huyo"

    "we zainabu, sasa huyo ndugu yako kama unavyomjua haoni, haya huko mjini saa hio anatafuta nini"

    Aliuliza dada yao ambae ni jamila,

    "heeeeeeeee ivi hujui kama sasa hivi anaona"

    "anaona???.... Kafanya nini mpaka kaona"

    "heeeeeeeee inaenda mwezi wa tatu huuu"

    Jamila yeye kaolewa hivyo mambo yanayofanyika huku yeye hayajui, hata alipokuja alishangaa sana kuona nyumba yao imezidi kuwa nzuri zaidi, na mbaya zaidi anaambiwa kuwa mdogo wake sio kipofu tena...

    "jamani nani katoa msaada mkubwa hivyo"

    "ni mpenzi wake huyo... Kamchukuwa na kwenda kumfanyia kazi"

    "inaonekana kapata mpenzi tajiri eee"

    "sanaaaaa, ila huezi amini hata zai mwenyewe hajui kama mpenzi wake ni tajiri"

    "kwanini sasa"

    "sijui"

    Walijikuta wanaongea mambo mengine na kusahau jambo la zai kutembea usiku alianza lini,... Mana huyu Zainabu ni mmoja kati ya CCMT hivyo kumuona pacha wake huko katika mitaa anayotembea...



    Tukija huku ofisini kwa kijana sheby ikiwa ni mida ya jioni hivi kila mmoja alikuwa akijiandaa kuondoka zake.. Ghafla mfanyakazi wake mmoja wa kiume kaja ofisini kwa sheby,.. Ni washkaji sana na wamezoeana sana japo ni boss kwa mfanyakazi,..

    "aaahhhhh boss naona bado upo na wakati tunaondoka sie"

    "aahhhhh mawazo mengi bwana"

    "sasa skia mzee.... Jana saa ngapi sijaingia mitaa ya kati nikakutana na toto bichiiiiii"

    "wapi uko"

    "mjini kati... Mtoto alitupia, mkali nikamwona piga mistari mingiiii kaingia laini... Ndani... Kichapo"

    "eeeehh mambo yako ayooo"

    "mtoto rangi ya chocolate shepu ya maana"

    Saidi alikuwa akiongea kwa kujisifu sana

    "sawa bwana kula ujana"



    Sasa tukija huku kwa akina rose wakiwa ndio wanafika nyumbani na kumkuta mwai kakaa kwenye gari yake akiwa anawasubiri rafiki zake wakubwa...

    "ooohhhh afadhali mumefika,.. Nilikuwa nawasubiria muda tu yani"

    "we nawe kwanini usingepiga simu sasa.."

    "mmmhhhh rose... Kwani vinapigika simu"

    "heeeeeee kwani vipi mwenzetu"

    "we acha tu, nina janga hilo sijui nilipeleke wapi"

    Aliongea mke wa sheby huku wakiingia ndani, kama kawaida yao wakikutana umbea mwingiiii...

    "enheee hebu nipe umbea mana wewe kwa umbea umo kweli"

    "yaani huu sio umbea.. Ni ukweli mtupu"

    "nini tena mwai... Au Umeachika nini"

    "bora hata ningeachika rose"

    Mwai alikuwa anawaza atamwambia nini sheby kuwa ana mimba yake na wakati hajawahi kulala nae hata siku moja japo ni mume wake,..

    "kwani una nini"

    "nina mimba rose"

    "heeeeeeee sasa cha ajabu ni kipi hapo"

    "nina mimba lakini sio ya mume wangu... Ni mimba ya james"

    "Eeeeehhh maakubwa ya jongo hayo"

    "nipeni ushauri basi jamani nifanyeje"

    "lakini mwai, kwanini mtoto wa watu hujawahi kumpa haki yake ya ndoa"

    "ni kweli... Lakini mi simpendi yaani hata kumpa mwili wangu naota kama vile nafanya na mbwa vile"

    Ghafla mary kadakia

    "we dada mwai, yaani ukifanya mapenzi na huyo unahisi kufanya na mbwa?"

    "we mary kwanza we bado mdogo yatakukuta haya"

    "sawa lakini sio hivyo dada mwai unamkufuru mungu"

    "atajua mwenyewe mi nakaona kama kambwa tu"

    Mary hakutaka hata kusikiliza akaingia zake chumbani mana wamepangisha dabo rumu....

    "sasa skia mwai mi nataka nikupe ushauri mmoja tu"

    "ushauri gani huo"

    "tembea nae.. Leo akirudi mpokee vizuri, mpeti peti... Mpe kitumbua chako, baada ya wiki unamwambia mimba ni yake... Hakatai ng'ooooo"







    Kiukweli sisi wanaume tumekuwa ni watu wa kuibiwa kila kukicha,.. Tena haswa haswa katika upande wa ujauzito, hua tunapewaga vitu ambavyo sii vyakwetu,.. Na kwa upande mwingine hatuna uwezo wa kupima DNA kwasababu ni gharama kubwa sana, wanaiweza matajiri peke yao.. Sasa kwa sisi wanyonge tunapewa damu za watu na kuzikubali... Kiukweli wanawake mnavyofanya sii vizuri kibinaadamu, mpe mtu haki yake aende... Hakikisha mimba ni yake kweli umwambie, sio uone tu kwasababu ana uwezo flani ndi9 umtupie mzigo.. Mana siku hizi ndio tabia ya wasichana wengi,.. Wakipata mimba hua wanajipitisha kwa wale wanaume wenye mwelekeo wa maisha na kutembea nao kisha kuwapa mzigo ambao haukuwa wakwake, na ndio maana baadhi ya wanaume hukataa mimba hizo...

    "sasa skia mwai mi nataka nikupe ushauri mmoja tu"

    "ushauri gani huo"

    "tembea nae.. Leo akirudi mpokee vizuri, mpeti peti... Mpe kitumbua chako, baada ya wiki unamwambia mimba ni yake... Hakatai ng'ooooo"



    Aliongea rose huku akimsihi sana mwai afanye hivyo,...

    "ati nini, yaani yule kinyago mi nimpe papuch yangu kweli"

    Aliongea mwai huku akijiangalia kuanzia chini mpaka juu

    "ok.. Kama hutaki acha,.. Ila mi nakuuliza hivi, endapo utamwambia una mimba yake, je? Yeye atakujibu nini na wakati hamujawahi kusex?"

    Mwai alikaa kimya kwa kuambiwa hivyo, kana kwamba ni lazima atembee na aheby kimapenzi japo ni mumewe na wanaishi nyumba moja lakini tendo la ndoa kwao ni ngumu mno kupatika, mana hakuna anaempenda mwenzake,.. Ghafla mary kaingilia kati

    "lakini ni kweli dada mwai, lazima umpe tu, mana hutoweza kumwambia una mimba na wakati hujawahi kumpa papuch yako... Afu usipomwambia mimba itaonekana na huenda akakuuliza au pia akatulia lakini anajua sio yake"

    Aliongea mary huku mwai akijiandaa kujibu

    "kwani hata akiiona na nikimwambia sio yake atanifanya nini"

    Aliongea mwai kwa kujiamini, lakini mary nae akamalizia kwa kusema kuwa

    "yeye hatokufanya kitu kwa uzezeta wake... Lakini je familia yake na yako vipi wakijua mimba sio ya mumeo?"

    Mwai alikaa kimya huku rose akisema

    "hilo nalo neno mary"

    "aaahhhhhhhh yaani anione uchi wangu kweli... Yaani simpendi yule kijana nyie acheni tu"

    "au kama vipi kaitoe utulie"

    "no, siwezi kuitoa kwasababu hata James nimeshampa taarifa hizo na kasema nimtunzie mtoto wake"

    "basi lazima uonewe uchi wako mama"

    "mmmmhhhhh"

    "sio mmmhhh tena, wahi nyumbani akukute ndio itakuwa vizuri"



    Tukija huku ofisini kwa akina sheby wakiwa ndio wanatoka,

    "lakini boss siku hizi unachelewa sana kutoka kazini"

    Aliongea mfanyakazi wake ambae ni Saidi,

    "aaahhhh amna lolote sema for now si unajua nimeoa sasa lazima nichelewe kidogo"

    "aaahhh ni kweli, lakini lazima uwahi ili ukampeti peti mama la mama"

    "hahahahaha yule anapetiwa usiku"

    Maskini kijana sheby anaongea tu, ili aonekane mwanaume ndani ya nyumba, lakini yupo kama mwanamke mbele ya mkewe, na sio kuwa hawezi kuwa mkali kama wanaume wengine, sema wazazi wake wamemsihi asimfanye chochote kile, hata akimtukana amuache tu..

    "ila boss nyie mlio oa mna raha eee"

    "aaahhh sanaaaa... Yaani raha za tanga si unazijua zile"

    "tena mtoto mwenye si mtanga kabisa yule"

    "haswaaa"

    Basi sheby na saidi wakiwa katika gari, sheby alikuwa akijioshea kwa kuoa lakini siri anaijua yeye mwenyewe,...

    "wewe si una mke wewe hotelini unaingia kufanya nini"

    "namnunulia mtoto mapocho pocho si unajua kuoa kulivyo"

    "ahahahahahahaha sawa bwana niosheee tu"

    Sheby anajua kabisa nyumba yao haipikwagi, mwanamke ni yeye na CHIPSI, yeye na KUKU au NYAMA yaani anataka vitu vya kukaanga kaanga tu.. Ila kupika hataki







     





    Walifika mahari sheby na saidi wakaachana kila mtu akaelekea sehemu yake,... Honi ilipigwa katika nyumba ya sheby mlinzi alikuwa na juhudu za kufungua... Alikuwa ni sheby ndie aliepiga hodi, sasa cha ajabu aliofungua alikuwa ni mkewe.. Sheby alitoa macho, kwanini afungue mkewe je huyo mlinzi yupo wapi, sheby alijua tu lazima mlinzi keshafukuzwa, mana sio kawaida na haijawahi kutokea mwanaheri au mkewe kufungua geti,..

    Sheby aliingia mpaka ndani na kuweka gari vizuri,..

    "kisoji... We kisoji"

    Sheby aliita kwa hasira kana kwamba kwanini alale afu mke afungue geti

    "jamani mume wangu, nae huyo pia ni binaadamu mwache apumzike tu"

    Sheby alibaki mdomo wazi huku akishikwa na mshangao wa hali ya juu, leo mwai kamwita sheby mume wangu,..

    "unasemaje mwai"

    "kwani ni vibaya kukuita hivyo"

    "ahahahaha hapana ni vizuri tu"

    Sheby alikuwa kabeba kuku wa kuchoma, mwai alipoona kamfuko keusi kakakimbilia ili kumpokea mumewe, wakati siku zote anamuangaliaga tu...

    "naomba nikupokee mume wangu"

    Kila kitendo au neno liliotoka kinywani kwa mwanaheri lilikuwa la kushangaza sana kwa kijana sheby,...

    Kijana aliingia ndani, humo ndani kwenyewe alishangaa kuona kule jikoni kunapikwa, tena kulikuwa kunapikwa vitu vinavyonukiaaa, sheby hakutaka kushangaa zaidi,.. Alipitiliza mpaka ndani, alikuta kitanda kimejaa mauwa ya kuvutia, afu shuka liliandikwa,.. KARIBU MUME WANGU... Sheby hakusema kitu pamoja na kuona vitu vyote hivyo, sheby alikuwa akivua viatu lakini ghafla alishikwa mkono na mkewe

    "naomba nikuvue viatu"

    Mshangao ulizidi kumuelemea kijana sheby na kushindwa kutoa hata neno moja,.. Mwanaheri alimvua mumewe kila kitu kisha akawa anampeleka bafuni,.. Sheby kufika bafuni kakutana na jambo lingine, leo haogi maji ya mvua au maji yanayotoka juu, leo anaoga kwenye ndoo, tena maji yalikuwa na mauwa kadhaa tena yaliokuwa yakinukia vizuuri kabisa.. Sheby mshangao ulikuwa mzito kwake.. Mke alitoka ili mume aoge mwenyewe,... Sheby alimaliza kuoga kisha akawa anatoka hapo sebuleni kuangalia taarifa za habari.... Mezani alikutana na chai safiiii iliowekwa viungo vyote, yaani sheby muda wote huo kabaki kua kimyaa,.. Hajatoa hata neno moja kwa mkewe..

    "karibu chakula mume wangu"

    Sheby alikuwa hakatai wala nini, kanawishwa maji kisha kala chakula alichopika mkewe...

    Sasa kuumbe kukaa kimya kwa sheby halikuwa jambo la kawaida,.. Mwanaheri aliangalia pembeni na kujichekesha kinafki huku akikumbuka kitendo alichokifanya kabla mumewe hajaja... Sasa alikumbuka saa ile akiwa kwa marafiki zake kule kwa akina rose na mary.... Sasa kumbe alipokuwa pale ilikuwa hivi.........









    "yeye hatokufanya kitu kwa uzezeta wake... Lakini je familia yake na yako vipi wakijua mimba sio ya mumeo?"

    Mwai alikaa kimya huku rose akisema

    "hilo nalo neno mary"

    "aaahhhhhhhh yaani anione uchi wangu kweli... Yaani simpendi yule kijana nyie acheni tu"

    "au kama vipi kaitoe utulie"

    "no, siwezi kuitoa kwasababu hata James nimeshampa taarifa hizo na kasema nimtunzie mtoto wake"

    "basi lazima uonewe uchi wako mama"

    "mmmmhhhhh"

    "sio mmmhhh, tena wahi nyumbani akukute ndio itakuwa vizuri"

    Aliongea rose huku akikaa kwa umbea,..

    "rose, unajua kuwahi sio tatizo, tatizo ni kwamba sheby hatokubali kulala na mimi"

    "ina maana nyie wote hampendani"

    "hilo ndio jibu rose"

    "duuuuuuu hapo unayo kazi shost, mimi nilijua yeye anakupenda ila wewe humpendi, kumbe ni hivyo.... Lakini hakuna shaka"

    Aliongea rose huku akiamka tena,..

    "kwanini nisiwe na shaka jamani rose"

    "skia, nina mzee huyo twende nikupeleke... "

    Sasa kabla mwai hajakubaliana na rose, ghafla mary kadakia

    "heeeeee rooose asa mambo hayo yanini... Kwanza penzi la kishirikina hua halidumu"

    "mary, mimi wacha rose anipeleke mana mi nataka nimpumbaze kwa siku moja tu basi"

    "mmmhhh haya safari njema"

    "kwaio we huendi"

    "akhaaa mi siendi"

    Mary alikataa kwenda kwa mganga,



    Dakika chache walifika kwa mganga huyo mana walikuwa wakitumia usafiri wa gari,..

    "karibuni sana"

    Sauti ya mganga ikiwakaribisha ndani, na wakati huo inakwenda kama saa 12 hivi jioni,.. Waliingia katika kibanda hicho na kueleza shida yao yote..

    "babu mimi nataka dawa ya kumpumbaza mwanaume kwa siku moja tu"

    Aliongea mwai huku akiwa kapiga magoti mbele ya babu huyo,..

    "kwahio huyo ni hawala wako au mumeo"

    Mwai aliwaza amjibu nini huyo mganga

    "ni hawala tu"

    Rose alishtuka kuskia mwai kasema ni hawala tu

    "we mwai, hata mungu hapendi,.. Mwaya babu huyo ni mume wake"

    "sasa kwanini anaficha"

    "anaficha kwasababu hampendi.. Hivyo hapo alipo ana mimba ya mtu meingine, sasa anataka ampumbaze ili alale nae amsingizie hio mimba"

    "kwani hajawahi kulala nae"

    "ndio"

    "mmmhh ok sasa... Kwaio wataka ulale nae siku moja tu"

    "ndio"

    Basi mganga alianza kufanya mambo yake, baada ya muda kidogo alikuja akiwa na kopo lililojaa mauwa,

    "unaona haya mauwa"

    "ndio babu nayaona"

    "haya ni moja ya masharti ya dawa hio.... Kwanza kabisa masharti ya dawa hio ni mazito ila ni mepesi kwa anaeyaweza"

    Mwai alishtuka baada ya kutajiwa baadhi ya masharti ya mzee huyo..

    "masharti gani babu"

    "kwanza kabisa unatakiwa kuwa na upendo wa kama mke... Weka maua kidogo kwenye geti, ila mtu asione.."

    Aliongea mganga huyo,.. Na sisi tunapata picha kuwa ndio mana kisoji alitolewa kwenye geti na kuambiwa akapumzike..

    "sawa babu"

    "akisha yakanyaga hayo mauwa ataanza kuwa mpole,.."

    "lakini babu... Mume wangu anakuja kwa gari sasa atayakanyaga vipi pale getini"

    Aliuliza mwai huku akiwa makini kwa masharti atakayopewa..

    "hata kama atapita juu ya geti kikubwa apite eneo lile, na kama ni gari basi dereva awe yeye... Afu geti ufungue wewe.... Kama kaja na chochote kashika mkononi, mpokee.. Afu akiingia ndani mvue viatu na nguo zake... Hakikisha hii dawa unainawa kabla ya kufanya hayo yote,.. Weka mauwa kotandani na ahuka jipya.. Mpelekee maji ya kuoga uyaweke hii dawa.. Mpikie chai muekee hii dawa... Pika chakula mlishe kama mumeo,.. Na mwisho kabisa nunua nguo ya ndani mpyaa, kisha inyunyizie hii dawa kisogo kisha ivae, na usiivue wewe, mwache aivue mwenyewe, ukiivua wewe utaharibu masharti ya dawa.. Na haitokubali tena kwasababu umechukuwa dawa ya mara moja.. Hivyo mizimu yangu haitokubali kukuseidia kama utataka kwa mara nyingine.."







     





    Babu alimaliza kuongea misha mwai akaanza

    "babu nina uhakika mimi nataka dawa ya mara moja tu, yaani sitaki hata kurudia nae tendo hilo"

    "sawaaa.. Shika dawa husika.. Shika na haya mauwa.. Jazi kwako"

    "ni shilingi ngapi babu"

    "weka kiasi chochote na uondoke bila kugeuka nyuma"

    Mwai alitoa pesa bila hata ya kuhesabu na kuzibwaga hapo kwenye ungo wa mganga huyo, kisha haooo wakaondoka zao yeye na rose wake..



    KUMBUKUMBU ILIISHIA HAPO



    "karibu chakula mume wangu"

    Sheby alikuwa hakatai wala nini, kanawishwa maji kisha kala chakula alichopika mkewe... Sheby kwa wakati huo hakuwa na la kusema zaidi ya kucheka cheka tu,..

    Mwai alinyanyua kijiko kilichokuwa na chakula cha saizi kisha akamlisha mumewe, tena wakati huo alikuwa akimshika shika katika kifua chake, sheby hua hakaagi na taulo baada ya kuoga, lakini leo kabakiwa nalo.. Wakati huo mwai katupia kanga na taiti ndani, yaani hapo mapaja yote yalikuwa wazi lakini huezi amini sheby hakuwa akimtamani hata kidogo yaani alimuona kama ng'ombe tu,.. Sema wakati huo tayari keshalegezwa na kila kitu, ila mapenzi tu ndio hataki.. Sasa mwai akashangaa mbona hata dudu ya mumewe haistuki hata kidogo... Mwai aligundua sababu kwanini hakuwa akimtamani.. Basi baada ya masaa mawili sheby alielekea katika kitanda chake mana hapo chumbani kwao kuna vitanda viwili, lakini kuna kimoja spesho..

    "hapana mume wangu leo tulale wote"

    Aliongea hivyo mwai huku akimshika mkono,..  Sheby hakutaka kwenda, ila mwai alijua sababu,.. Alimwacha kisha akaenda kwenye begi na kutoa chupi nyepesiiiii, tena ilikuwa mpyaaa alikwenda bafuni na kuinyunyiza vile vidawa kisha akaivaa..... Sasa alipofika tu chumbani sheby alihisi kuina mwanamke wa tofuati kaingia ndani,.. Ila kuangalia vizuri alikuwa ni mke wake,.. Mwai alifurahi sana kuona taulo la mume wake linavimba vimba kiaina,.. Kana kwamba tayari keshamtamani mkewe... Mwai hakutaka kumhamisha kitanda kingine, bali alimfuata pale pale, na kulala nae,... Mwai alivaa kanga Lakini aliifunua makusudi ili sheby aone chupi, mana ndio kivutio cha ngono katika dawa hio,.. Sheby alishangaa karukiwa mdomoni, mana mwai kaona kama vile mumewe anachelewa,.. Sheby kakubali kufanya mapenzi na mkewe,.. Lakini kabla hajaanza sheby ni mzee wa kuandaa mwanamke, alimfanyia mkewe maandalizi ya hali ya juu, huezi amini mpaka mwanaheri anatetemeka mwili mzima,... Sheby kanyonya kila kona ya mkewe, chupi ya mwai ililoa na kua chafu kutokana na ile dawa alioiweka,.. Mwai kalegea lege hata mlenda una nafuu.. Sasa mwai aliona mumewe anachelewa kumuingilia kimapenzi,.. Sasa mbaya zaidi mwai kasahau sharti la sheby avue chupi mwenyewe, kwa utamu wa mapenzi ya mumewe alisahau akajikuta anataka kuibua mwenyewe, kwasababu ilikuwa ikimuwasha washa katika sehemu fulani...







    Kiukweli mapenzi ni kitu cha ajabu sana, unaweza kutaamka neno bila kukusudia, yaani hata ukiambiwa muuwe ndugu yako kwasababu ya mapenzi, unajikuta unatekeleza jambo hilo bila kutarajia, yote ni kwasababu ya mapenzi,.. Hakika hakuna kitu kitamu zaidi ya mapenzi haswa haswa upate yule anaekupenda na kukutimizia kila utakacho,.. Mwanaheri na Sharbiny ni wanandoa waliotokea kuchukiana sana, kwasababu walifungishwa ndoa ya lazima, yaani hawakupendana, kila mmoja hakuwa akimpenda mwenzi wake, ila kwa lazima ya wazazi waliweza kuishi pamoja bila kufanya tendo la ndoa, yaani kila mmoja akimwona mwenzie anamwona kama takataka fulani hivi pale dampo,.. Na pia wawili hawakutegemea kama ipo siku watakuja kufanya mapenzi, japo wanatofautiana kiumri lakini kwenye mapenzi hakunaga mambo ya umri, kijana sheby ni mtoto mdogo sana kwa mwanaheri, lakini kitendo alichomfanyia kwa siku hii ya leo, hata mwanaheri mwenyewe kajiona kama yupo na mtu mzima mwenzie japo hawakupishana sana kiumri ni kama miaka 6 au 7 hivi ambayo kijana sheby kapitwa na mwai, hivyo mwai ana miaka kama 28 au 29 kitu kama hicho, na sheby yeye ana 22 hivyo ni namba tu za umri lakini kiuwezo, tunamuachia mungu....



    Sasa wakati huo mwai alikuwa hoi bin taabani, na katika upande wa masharti bado sharti moja ambalo lilitakiwa sheby avue chupi mwenyewe lakini sasa kutokana na kuzidiwa kwa mwai alijikuta anataka kuivua mwenyewe, wakati huo alikuwa kaishika kiunoni, lakini ghafla simu ya mwai ikaita, akajikuta anasita kuvua na kuipokea simu yake

    "nipo bize kidogo nicheki baadae"

    Leo mwanaheri hataki kuongea na rafiki zake kisa ni mapenzi yamemnogea... Alikata simu na kuendelea kumshika mume wake,.. Na hapo ndipo alipokumbuka sharti la kuvuliwa chupi

    "baby, nivue chupi"

    Aliongea mwanaheri huku denda likiendelea kuchukiwa nafasi yake,.. Kwakuwa sheby alikuwa kapumbazwa na asijue lolote lile, alijikuta anamvua mkewe chupi na kuiweka pembeni,.. Mwanaheri alisema kuwa sheby hatokaa kuuona uchi wake, yaani pale wakati wa kufanya mapenzi, mwai azime taa ndio sheby avue chupi, lakini wazo hilo halikuwepo tena,... Na huezi amini mwai kajianika mbele yake, tena bila aibu... Hapo ndio ujue kuwa mapenzi yana nguvu kuliko chochote kile,.. Wakati huo wawili hao walikuwa kama walivyozaliwa yaani hakuwa aliokuwa na nguo hata mmoja, mwai alikuwa akiiangalia Zakariya ya sheby jinsi ilivyokuwa na hasira, sheby alikuwa akipagawa kila anapoangalia mapaja ya mwai,.. Mwai bila kuchelewa alijitupa juu ya sheby huku akijitengenezea mwenyewe,... Kijana sheby akaona kama vile mkewe anacheza tu, sheby alimgeuza mwanaheri na kumweka chini,... Kisha akaishika babu yake na kuiweka mahari husika, Mwai alijikunja kiuno chake pale zakaria ya sheby ilipopiga hodi katika nyumba ya mwai

    "aaaaaaaaaiiiiiiiiii"

    Ni sauti ya mwai iliokuwa ikisikika baada ya shughuli kuanza,.. kama tunavyomjua kijana sheby mambo yake mazito mno katika sekta hio,..



    Baada ya usiku huo kupita Mambo yalienda vizuri kwa usiku mzima,... Sasa sheby alipoamka asubuhi anamkuta mwanaheri kamkumbatia, sheby alikurupuka, kabla hajauliza alishangaa kujikuta yupo uchi wa mnyama tena alikuwa akijihisi kuchoka mno...

    Wakati huo mwai kanyamaza tu, mana anajua alichokifanya mpaka sheby kukubali kufanya mapenzi nae,.

    "we mbwa umenifanyia nini hivi"

    Aliongea sheby huku akiokota taulo lake na kujifunga vizuri... Lakini huezi amini mwai alikuwa kimya na wakati siku zote hua wanatupiana maneno makali, sheby akiwa juu na mwai anakuja juu, sasa wanajikuta wote wakali, lakini leo mwai kimyaa hana hata neno la kuongea...

    "nakuuliza we bibi kizee... Umeshanifanyia uhanithi wako mpaka nimelala na wewe... Sijapata kuina bibi kizee malaya ivo"

    Yaani kwa jinsi sheby hampendi huyo mwanamke mpaka anadiliki kumwita bibi kizee kisa kapitwa miaka 6 tu ndio anamwita mwenzie bibi kizee, lakini pamoja na maneno yote hayo bado mwanaheri haongei kitu kakaa kitandani katulia kimyaaa, sheby aliongea sana kisha akaingia zake bafuni mana chumba chao ni hicho hicho sema kina vitanda viwili kwasababu ya kukwepana kimapenzi,







     





    Tukija huku uswahilini tunamuona zaituni akiwa ndio anavua viatu kana kwamba kuna mahari alikuwa akitoka kwa wakati huo,.. Na hata shadi pia alikuwa akivua nguo zake, lakini shadi yeye alikuwa hana pesa ila zaituni aliingia na pesa na kuzirusha kitandani... Lakini shadi hakuwa na pesa kana kwamba leo hajapata mwanaume,... Shadi alipomaliza kuvua nguo zake alikuja kwa zaituni

    "zai shost... Si unajua mwenzio leo nimetoka kapa"

    "tatizo wewe nawe unajitenga sana, wewe ndio umenifundisha kazi hii lakini mmhh umezidi kujitenga"

    "mi nimeanza muda sana hivyo bado aibu haijaisha zai"

    Aliingea shadi huku wakiwa wamekaa kitandani...

    "ok usijali... Chukuwa hii elfu 50 itakuseidia leo na kesho"

    Zai kampatia shadi elfu 50 ya matumizi kwasababu yeye leo hajapata katika mawindo yao

    "mmmhh Ahsante sana shost"

    "afu,.. hhhhhhmmmmm, yule jamaa kanipangishia nyumba, na leo ananinunulia simu ya tachi"

    Aliongea zaituni kitendo kilichomwacha shadi mdomo wazi,

    "we zai wewe, kuanza juzi tu"

    "heeeee, mimi nimemdanganya ni bikra, na ni kweli nilifanya mapenzi mara moja tu tena kwa kubakwa, hivyo juzi alivyoanza alinitoa vidamu kidogo vilivyodhihirisha kweli nina bikra"

    Zaituni alikua akiongea kile alichofanyiwa na mwanaume huyo

    "sasa na sheby nae"

    "huyu muuza viazi????"

    "sasa kwani yupi tena"

    "huyu nitamuacha taratibu bibie wala sina presha"

    "wewe zai weweeeee, kuwa na huruma wewe, si kakupeleka india mkaka wa watu"

    "sasa inahuuu... Si Kiherehere here chake, kwani kama ningekutana na huyu asingenipeleka"

    "nani angekupenda na wakati ulikuwa kipofu wewe"

    "lakini shdi, wewe si ndio umenifunsha hii kazi wewe, mbona kama tena unaniruka"

    "amna naona mwenzangu imekuwa too much kwa kazi hio mimi hata siendekezi hivyo"

    "afu sasa skia.. Kesho nampeleka kwa wazazi kumtambulisha"

    "we zaituni wewe,.. Kwani wazazi wako hawamjui huyu"

    "wanamjua sana tu, ila najua wazazi wangu wanapenda pesa"

    "mmmmhhhh haya mwaya kazi kwako"

    Aliongea shadi huku akiamka na kuondoka zake, lakini zai alijikuta kweli anafikiria kijana sheby ndie mwanaume peke yake aliompenda kipindi akiwa kipofu,... Zai alifungua mkoba wake na kumwaga hela alizohongwa na wanaume wa usiku huo, japo mmoja wao ndio kanogewa na kuingiza mzigo ndani..

    "laki mbili hizo.. Nikienda na leo tena nikipata kama hizi.. Nitaishiwa na nini? duka la nguo nililotamani kufungua sasa naliona mbele yangu"

    Aliongea zaituni akiwa peke yake, aliingiza pesa hizo katika kibegi chake na kufunga vizuri...



    Tukija huku kwa kijana sheby akiwa ofisini, alikuwa anawaza sana ilikuwaje mpaka akafanya mapenzi na mke wake, na wakati alishakula kiapo hatokaa kumgusa mana hampendi na hata mke wake pia hampendi mumewe,... Sheby alikumbuka ujeuri wa mkewe wiki za mwanzoni..



    WIKI ZA MWANZONI MWA NDOA YAO



    "lakini mke wangu, hio pesa ni nyingi sana"

    Aliongea sheby baada ya kudaiwa pesa ya mtaji wa lipustiki,..

    "kwaio we wataka nikae nyumbani tu nimekuwa paka mimi"

    Alijibu mwai huku akinyoosha mkono ili apewe pesa kiasi cha milioni 10 za mtaji wa lipustiki tu basi

    "mke wangu?... Milioni kumi duka la vipodozi tu... Au na duka la nguo hapo hapo"

    "weeeeeeeeeee duka la nguo linaghalimu milioni 50, jumla nipe milioni 60"

    Sheby kwa hali hio hakutaka kutoa pesa, mana ni pesa nyingi sana

    "siwezi kutoa hio pesa.. Ni kubwa sana"

    "ati nini... Wewe hebu njoo hapa, unasema hutaki kufanya nini"

    "we mwanamke, kuwa na adabu na mimi sawa.. Mimi sio mumeo kaa mbali na mimi"



    Siku hio walikwaruzana sana, lakini sheby akiwa ofisini kwake baba yake aliingia

    "we pumbavu umemfanya nini mkeo"

    Aliongea baba yake huku akiwa mkali sana

    "mzee kwanini usiulize vizuri"

    "nimepigiwa simu na baba yake sasa hivi anasema umemwambia wewe sio mkewe kisa kakuomba pesa hujampa"

    "ni kweli... Mzee yule mwanamke anataka milioni 60 za biashara"

    "kwani huna??... Nakuuliza hio pesa wewe huna??"

    "khaaaa mzee... Ina maana hata wewe upo radhi nitoe milioni 60 kwa yule mwanamke? Hapana mzee siwezi kutoa"

    Huezi amini baba yake sheby alitoa kadi ya benki na kumpa mtoto wake

    "shika hii kadi, nenda katoe milioni 60 umpelekee"

    Sheby alishangaa kuona baba yake anadiriki kutoa hio pesa kisa ni yule mwanamke,.. Kitendo hicho kilimfanya sheby kuwa mpole hata mbele ya yule mwanamke, mana ni kitu ambacho hakipo kabisa,...

    "basi mzee nitaitoa hio pesa"

    "tena nenda sasa hivi.. Alafu hutakiwi kumkwaza hata kidogo"

    Aliongea baba yake, huku kijana sheby akitoka kwa upole wa hali ya juu mno,.. Sheby alipanda gari yake na kwenda kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yake mwenyewe na sio ya baba yake kama alivyotaka,.. Alitoa milioni 60 kisha akanyooka moja kwa moja mpaka nyumbani,..

    "haya shika hio pesa"

    "waaaaoooo, asante"

    Sheby hakutaka kuingea wala kujibu chochote kile, alipanda gari na kurudi zake kazini,.. Baada ya wiki moja mwai kafungua duka la nguo pamoja na lipustiki,



    Sheby akiwa keshafika ofisini kwake na kutulia baada ya kupeleka pesa kwa mke wake,... Ghafla mzee wake kafika

    "vipi umeshampatia?"

    "ndio mzee, tayari nimeshampa"

    "yes, huo ndio upendo wa mke na mume, sio kukwaruzana kwa kitu kidoogo, milioni 60 ni kitu gani kwetu"

    Sheby alinyamaza tu na kumwacha baba yake aongee tu

    "tafadhali sana, usimkorofishe tena, mpe kile anachokita yani chochote kile mpe"

    "sawa mzee"

    Sheby alikuwa akijibu tu sawa lakini haikuwa ikiingia akilini mwake

    "kwahio hata akinikosea kama mume nimuache tu"

    "ndio.. Afu kwanza mwanamke hapigwagi"

    "ok sawa mzee"

    Kijana sheby alikuwa na hasira sana mpaka hakuwa na pointi ya kuingea zaidi ya kukubali tu...



    KUMBUKUMBU YA WIKI MBILI ZILIZOPITA BAADA YA KUOANA INAISHIA HAPO



    Sasa akiwa bado yupo ofisini ghafla saidi kaingia na furaha kubwa sana huku akiwa anacheeka sana

    "Hakiyamungu vile boss mi naoa... Yaani mtoto kakubali nimuoe eti"

    "sawa we oa tu, mana ndoa za siku hizi basi tu"

    "acha kunitisha wewe... Au unahisi naoa oa tu hovyo,.. Ngoja nikuonyeshe mtoto zaituni"

    Sheby alishtuka kuskia hilo jina japo zaituni ni wengi lakini mhhhh,...

    "hebu huyo zaituni... "

    "ngojaaa... Mtoto nilikuwa nae kitandani huyu hapa"









    Saidi ni mfanyakazi katika kampuni ya akina sheby, lakini katika pitapita zake aliweza kukutana na zaituni huyo huyo wa sheby, lakini saidi yeye hajui kama zaituni ni mchumba wa sheby,.. Zai alikutana na saidi katika moja ya starehe huko mjini kati ambako alipelekwa na shadi,.. Na saidi nae hakufanya makosa baada ya kukutana na mtoto mpole mzuri mwenye shepu amaizing,.. Saida ni mwanaume ambae hajaoa na anahitaji mke... Hivyo aliona kuchelewa chelewa huenda asikute mwana si wake....



    Jana ikiwa ni siku waliolala usiku kucha na kuongea mengi sana baina ya saidi na zai... Sasa leo asubuhi saidi akiwa na furaha ya kupelekwa kwa wazazi wa zaituni ili kwenda kutambulishwa zaidi... Saidi kaja ofisini kwa boss wake ambaye ni kijana sheby,...

    "hebu huyo zaituni... "

    "ngojaaa... Mtoto nilikuwa nae kitandani huyu hapa"

    Saidi alikuwa akipekuwa simu yake na kuziona picha walizopiga jana usiku,... Lakini kabla hajazionyesha ghafla baba yake sheby kamuita saidi

    "we saidi we"

    "naam boss"

    "kazi hujamaliza huki umekuja kufanya nini"

    Saidi alitoka mbio mpaka ofisini kwake, lakini hakuweza kumwonyesha sheby zile picha, hivyo sheby hakuona kitu,....

    "vipi mbona kama unaumwa hivi"

    Mzee huyo alimuuliza kijana wake huku akivuta kiti na kukaa,.. Wakati huo sheby anawaza tu ilikuwaje mpaka akafanya mapenzi na mke wake, na wakati hampendi hata kidogo..... Basi sheby alikaa na baba yake hapo waliongea mengi mengi



    Sasa Tukija huku nyumbani kwa akina sheby ambako ni kwao kule kwa wazazi wake, tunamkuta rehema akiwa na mama yake... Lakini ghafla simu ya mama sheby iliita... Kuangalia namba ilikuwa ni namba ya mama yake na mwai

    "haloo habari yako mama mwai"

    "salama tu mama sheby hali zenu huko"

    "nzuri tu, haya kulikoni simu mchana huu"

    "mwenzangu nimepata taarifa mwanao kainasa"

    "nini?"

    "mwenzangu watoto na nguvu zao, miezi mitatu tu kitu tayari kimejisoma"

    "una maana gani we mama mwai"

    Mama sheby alishawahi kuambiwa na rehema kuwa mwai ana mimba lakini hakutaka kuamini kwasababu sheby alishawahi kumwambia mama yake ukweli kuwa hajawahi kufanya mapenzi na mke wake,... Sasa leo anadhibitishiwa na mama mkwe mwenzie, kuwa watoto wameshanasana

    "ina maana we hujui"

    "akaaaaa sina taarifa mama"

    "basi jiandae kuitwa bibi"

    "what??????"

    "ndio.. Yaani mimi natamani hata ajifungue sasa hivi"

    "haya mama mwai hata mimi nataka iwe hivyo"

    Mama sheby aliongea hivyo ili asionekane kama hapendi ndoa hio,

    "haya bwana tuwaombee watoto wetu"

    "haya mama mwai"

    Simu ilikata huku rehema akiwa skio juu ili kujua kilichojiri

    "umeamini kuwa mwanao alikudanya ee"

    "kaa kimya, mimi najua sheby hawezi kunidanganya hata mara moja"

    "sawa mama ila ukweli ndio huo, mke wa sheby ana mimba"

    "sio yake"

    "sasa kivipi isiwe yake na wakati ni mke wake"

    "afu we mtoto mbina unamtete sana huyo mwanamke"

    "lakini mama"

    "hakuna cha lakini"

    Mama sheby alikuwa mkali kila alipotajiwa kuhusu mwanamke huyo ambae ni mke wa sheby,...



    Tukija huku ofisini kwa akina rose na mary wakiwa wapo kazini lakini mary bado mawazo yake yapo kwa sheby ambae ni boss wake

    "ivi rose, uliishia wapi ile ishu mana umekuwa kimya muda sasa"

    "labda niende sasa hivi, ila ujue mpenzi wako mgumu kama nini yani"

    Aliongea rose lakini rose hua anamruka mwenzie, badala ya kumsaidia anakuwa anamtaka yeye,..

    "fanya hivyo basi dada rose"

    Mary na rose mpaka leo hawajui kama sheby kaoa, na pia hawajui kama huyo huyo rafiki yao ndio kaolewa na sheby,.. Rose aliamka na documents flani hivi za kumpelekea boss wake

    Hodi ilipigwa na rose kisha sheby anaruhusu aingie,... Laaa haula rose alikuwa kavaa kisketi kifupi kilichomwacha boss wake mdomo wazi

    "za saa hizi boss"

    "salama tu"

    "boss kuna kazi hizi hapa"

    "mzee hayupo"

    "katoka kidogo"

    Rose alikuwa akiongea huku akijishika kifua chake kama vile anataka kuonyesha Matiti yake...

    "ok lete nizifanyie kazi"

    Sheby alizipokea zile documents kisha akawa anazikagua

    "unaweza kwenda tu"

    Lakini wakati huo hali ya sheby ilisha chenge kutokana maumbile alio yaona kwa rose...

    "sawa boss"

    Rose aliondoka kimadoido kwa kulitikisa kalio lake kana kwamba alikuwa akimtega boss wake, lakini sasa sheby aliooangalia vizuri katikati ya zile document alikutana na ujumbe...

    "mmmhhh huu ni ujumbe wa nini"

    Aliongea mwenyewe wakati akiwa anafungua, lakini wakati huo rose alikuwa hayupo keshaondoka...





    "BOSS, I KNOW UNA MPENZI, BUT NAOKUOMBA UKUMBUKE KUWA WAPO TUANAOKUPENDA... NI MAPENZI TU, BINAFSI NAOGOPA KUKUTAMKIA NAKUOENDA MANA UTANIONA MALAYA... I LOVE MY BOSS, HATA KWA PENZI TU NITARIDHIKA MIE..... BY WAKO ROSE



    "huyu mdada ana akili kweli"

    Aliongea sheby baada ya kusoma ujumbe huo,... Sheby alishika simu na kupiga

    "njoo ofisini"

    Alimwita rose huku akiwa kaishika ile karatasi,... Lakini wakati rose anakuja mary nae alikuwa kwa nyuma nyuma kana kwamba kuna kitu alitaka kusikia kutoka kwa boss akimweleza rose, mary aliishia nyuma ya mlango na kusikiliza...



    "yes boss"

    "nani kakuambia uniandikie huu uchafu"

    Rose alishtuka kwa kuona hio karatasi, na kushtuka huko kuliashiria sio yeye alioandika bali ni mary ili kujua boss atasema nini..  Lakini sasa rose baada ya kukataa kuwa huo haukuwa muandiko wake, ikabidi aunganishe na zakwake humo humo mana kajua huo ni muandiko wa mary na sio yeye...

    "lakini boss hizo ni hisia zangu boss"

    "hisia zako ndio uzilete ofisini kwangu"

    "nisamehe kwa hilo, ila sijapata nafasi ya kuongea na wewe zaidi ya hapa"

    "rose.... Staki ujinga na kazi, nataka kazi ifanyike maswala ya mapenzi kazini siyataki.. Naomba ufanye kazi"

    "boss, mimi sina mpango wa kuharibu kazi na pia Sihitaji hata senti tano yako... Penzi tu"

    "ebu toka bwana"

    Sheby alikuwa mkali lakini maneno aliyapenda,... Mary kakimbilia ofisini lakini ameshajua kumbe rose alikuwa hafanyi chochote badala yake alikuwa akimtongoza, hivyo hata huo ujumbe alioandika mary kama vile rose, umemseidia rose, mana rose hajawahi kumtaamkia boss wake kuwa anampenda...

    "dada rose boss kakuitia nini"

    Mary aliuliza kama vile hajui kinachoendelea

    "umefanya ujinga gani mary"

    "kwani mi nimefanyaje"

    "huu ujinga umeandika wa nini wakati wewe ndio unampenda"

    "kwani we humpendi??"

    "hata kama, lakini mimi niliacha hisia za kumpenda kwasababu ya wewe"

    "eti eeee"

    Mary aliitikia kwa dharau mana ananua kabisa anampenda....

    "ndio"

    "kumbe siku zote hizo nakutuma ukamwambie kumbe hata wewe unampenda, nyoooo yatakushinda"

    "mary naomba ujieshim"

    "wapi wewe unantongozea mpenzi wangu"

    "kwani ni mpenzi wako... Kwani keshakukubalia"

    Walikuwa wakirumbana kwa maneno ya hapa na pale,... Lakini kila. Mmoja keshamjua mwenzie



    BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA



    Masaa yalizidi kwenda, siku nazo zilikatika wiki nazo zilisogea na sasa ni miezi miwili baadae...

    Ikiwa ni mida ya jioni hivi kama saa kumi kasoro, saidi aliingia ofisini kwa sheby na kumkuta akiwa anaangalia tv,..

    "boss boss habari yako boss"

    "safi tu vp mbona una haraka hivyo"

    "boss, kuna kitu nataka nikuombe ndugu yangu"

    "nini tena"

    "gari yangu ipo gereji afu ndio nataka niende kwa wazazi wa yule mtoto"

    "kwaio ulitakeje wewe"

    "niseidie usafiri wako, yaani lisaa limoja tu"

    Saidi alikuwa akiomba gari kwa ajili ya kwenda kwa wazazi wa zaituni,

    "lakini si unajua saa hizi ni saa ngapi"

    "yes i know, but sintochelewa mana najua ndio miguu yako iyo boss"

    "ok poa chukuwa"

    Saidi alitoka mbio na kwenda kuwasha gari ya boss wake mdogo kisha akaondoka,... Lakini ile saidi anaondoka tu huku nyuma simu ya sheby iliita,...

    "haloo"

    "mchumba wako anakwenda kumtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake"

    Simu ilikata ghafla katikati ya maongezi

    "halooo, halooo.... Halooo"

    Simu ikata kabisaaa, sheby akaipiga ile namba lakini ikawa haipatikani tena,..

    "khaaaaa mchumba wangu nani anaenda kumtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake"

    Sheby aliniuloza sana bila kupata jibu, mana anajua fika kama ni zai hawezi kufanya hivyo,

    "inaonekana huyu kakosea namba huyu"

    Aliongea sheby huku akiiweka simu mezani na kuendelea kuangalia tv,..



    Tukija huku mjini zaituni wa sheby akiwa kasimama mahari akiwa anamsubiri saidi ili waende kwa wazazi wake wakamjue mpenzi wake mpya mana anaamini wazazi wake wanataka mwanaume mwenye pesa na sio upendo bila pesa...

    "piiiipiiii"

    Ni sauti ya honi iliokuwa ikipenya katika maskio ya zaituni,.. Kwa kero ya honi hio ilimfanya zaituni kuangalia inapotoka,.... Laaa haula alikuwa ni Saidi alioiteka roho yake kwa muda mfupi na kumsahau mtu aliomfanya kuona kwa mara nyingine tena,..

    "waaoooooo baby wangu kumbe ni wewe"

    "yes ni mimi...."

    "mbona leo una gari nyingine, ile nyingine ipo wapi"

    "ipo gereji mke wangu"

    Lakini sasa ile zaituni anaingia tu alikutana na picha ya sheby pale ndani... Ukumbuke kuwa gari hio ni gari ya sheby, sasa pale mbele ya dashboard kuna picha kubwa tu ya sheby, lakini alikuwa kavaa suti ya bei mbaya...

    "uuuuuuwiiiiiiiiiii"

    Zai alipiga kelele baada ya kuona hio pocha

    "nini teba baby? Umekalia nini"

    Saidi alijua zai kuna kitu kakalia lakini sivyo

    "huyu mtu ni nani hapa"

    Aliuliza huku akiwa hana hata raha mana anamjua sura yake

    "huyu hapa kwenye hii picha?"

    "ndio"

    "huyu ni boss wangu... Na hili gari ni lake"

    "boss wako???"

    "ndio,.. Kwani vipi unamjua"

    "huyu.. Anauzaga viazi na mkokoteni"

    Maneno hayo yalimchekesha sana saidi mpaka akapaliwa kwa kucheka

    "sasa unacheka nini na wakati mimi nipo siriasi"

    "yaani we na akili yako huyu ni mtu wa kuuza viazi kweli,.. Kama kusoma hujui hata picha huoni... Msuti wote huu auze viazi kweli"

    Kweli zaituni akafikiria kazi ya sheby mpaka aje kununua hio suti ni miaka kumi mbele,

    "aaahhhh basi wamefanana... Ama kweli duniani ni wawili wawili aisee"

    "kwani we ulimwona wapi huyo"

    "kule mtaani kweli kuna mtu mmoja anauza viazi kwa mkokoteni sasa nikajua ndio huyu"

    "aahhhhhh wacha wewe... Mtoto wa tajiri huyo aje auze viazi ana kichaa"

    "ok... Twende... Nyoosha happ mbele kisha utakuta barabara ya vumbi nyooka nayo"

    Ni maelekezo yaliotoka kwa zaituni baada ya kupanda gari mana Saidi hajui nyumbani kwa akina zaituni...

    Gari ya sheby ilikuwa ni gari ya gharama kubwa sana aina ya VX LIMITED lilikuwa ni toleo jipya kabisa na gari yenyewe ilikuwa mpyaaa... Sasa wakati wanakaribia kufika mana nyumba yao ipo sehemu kama vile kuna uwanja hivi,... Mama zai kaona gari ya mkwe wake,...

    "waooooo jamani mkwe huyoooo"

    Mama anajua fika anaekuja ni sheby mana hio gari sio ngeni machoni mwake,... Mama aliingia ndani na kupangusa masofa yakae safi palikiwa na watoto aliwatoa toa pale, hata zainabu pacha wa zaituni alikuwe hata dada yao mkubwa alokuwepo,...

    "mchumba wa zaituni huyo anakuja"

    Zainabu kwa umbea nae akachungulia

    "eeeee kweli.... Enheee dada kasema hamjui sasa ngoja amuone,.. Ni hensam haswa yaani zaitini kapata mume haswaaa"

    "nakwambia natamani nimuone"

    "nyie kueni na heshima.. Huyo ndie aliomseidia mdogo wenu mpaka sasa hivi anaona tena... Naomba mumpe heshma yake ni shemeji yenu huyo"

    Mama aliongea hivyo huku akitoka nje kwenda kumpokea mkwe wake ambaye ni sheby....







    Kweli ipo familia penda pesa lakini pia ipo familia penda fadhila za mtu, kusema kweli kijana sheby alifanya jambo kubwa sana katika familia hiyo, lakini mtendewa wala hakumbuki fadhila za mtenda, kijana sheby alijikuta akiilegeza akaunti yake ya benki kwa ajili ya zaituni,.. Lakini zaituni nae hakuwa mkweli katika mapenzi baada ya kuona kuwa waliishi maisha ya shida sasa kwanini achezee bahati kama ilivyo zamani, mana zamani ya zaituni alikuwa akikataa posa kwa kusema bado ni mtoto na istoshe hajafikia malengo yake,.. Sasa alipoona kwa mara ya pili aliona hawezi kuiacha bahati kwa mara nyingine tena.. Katika hatua za shadi kujiuza mjini kwa matajiri wakubwa wakubwa kutokana na uzuri wake, alijikuta anamteka zaituni nae kwenda kufanya biashara hio,... Kwa bahati nzuri zai kapata mwanaume wa kumpenda tofauti na ile ya kujiuza kwa kila mwanaume, sasa mwanaume huyo alimpenda sana zai na kutaka kuvuta jiko kabisa, na leo ndio ile siku ya kwenda kutambulishwa kwa wazazi, lakini mbaya zaidi ni kwamba wazazi wanamjua sheby na sio saidi,..



    "nyie kueni na heshima.. Huyo ndie aliomseidia mdogo wenu mpaka sasa hivi anaona tena... Naomba mumpe heshma yake ni shemeji yenu huyo"

    Mama aliongea hivyo huku akitoka nje kwenda kumpokea mkwe wake ambaye ni sheby,.....  Gari ilisimama na mama nae katulia kwa ajili ya kumpokea mkwe wake,... Lakini ghafla mama anashangaa anaetoka hakuwa sheby kama alivyotarajia,.. Lakini pia pamoja na hilo hakutaka kumuacha alimpokea kwa kudhani kuwa huenda alitumwa na sheby, kwani hio gari ilikuwa ni gari ya sheby

    "karibuni baba"

    Aliongea mama zai huku akimsalimia kwa heshima mana ni mgeni wa mkwe wake,..

    "heeeeee mbona kaja huyu mwingine kulikoni"

    Aliongea zainabu ambae ni pacha wa zaituni...

    "ebu tulia unawezakuta ni mshenga huyo"

    Aliingea amina ambae ndio dada yao mkubwa

    "karibu ndani baba"

    Mama alizidi kuwa mkarimu huku akichungulia nje kama sheby atatokea, kumbe maskini ya mungu sheby hajui hili wala lile...

    "shakomoo mama"

    "marahaba baba hujambo"

    "sjambo mama angu"

    Saidi nae alikuwa ana furaha sana kwa kuja ujitambulisha kwa mama mkwe,....

    "haya karibuni.... "

    Mama aliongea huku akiendelea kuchungulia nje kama vile anahisi sheby anakuja

    "mama mbona hutulii mama angu, nimekuja na mgeni"

    "nimemuona mwanangu, ngoja ndugu yako aandae chochote mle, huku mkimsubiria mwenzenu"

    Zaituni alimwelewa mama yake hapo aliposema mkimsubiria mwenzenu lakini saidi hajaelewa huyo wa kusubiriwa ni nani, mana mama anajua sheby yupo njiani anakuja... Zaituni alimtoa mama yake pembeni ili amwamnie ukweli



    "mama... Tumeishi kimaskini kwa muda mrefu, na mimi ndio nilikuwa na bahati ya kuolewa... Sasa kwanini tuendeleee kuishi maisha magumu hivi, mimi nimekuja kumtambulisha huyo kijana hapo ndani"

    Aliongea zaituni huku mama yake akishtuka na kubaki mdomo wazi,

    "unasemaje?"

    "ndio mama... Naomba umpokee tu, mimi sitaki sheby, maisha magumu kila kona nashindia kula viazi kila siku maisha magumu nyumba ninayoishi imetoboka magodoro yamechoka, mi nimeachana nae"

    "ama kweli yule kijana ana akili sana.. Yaani mungu amseidie katika maisha yake yote, sikutegemea kama ile akili yake ingelikuja kuzaa matunda"

    Aliongea mama huyo huku akitoa machozi ya uchungu kana kwamba alichokifanya mtoto wake ni ujinga usiokubalika hata kidogo....

    "ww mtoto ni mshenzi sana wewe... Yaani malezi yangu yote nikajua yatakuwa na faida kumbe unaniletea ushenzi tu... Umeacha mwanaume wa maana tena tajiri unakuja kunitambulisha mbuzi wako hao... Maisha mazuri kwa yule kijana, na namuombea apate mwanamke bora na sii bora mwanamke,... Ulipokuwa na yule kijana, nilijua maisha yetu tayari yameshakuwa mazuri lakini kumbe ni mjinga tu mshenzi wewe"

    Mama alikuwa akiongea huku akilia sana, mana mtoto karuka mkojo kakanyaga kinyesi...

    "mama, yaani yule muuza viazi ana kitu gani yule, au huko kukopa pesa na kunipeleka kwa wahindi ndio tatizo?? Si kama kamseidia mtu tu"

    Mama alinyanyua mkono na kumzaba kibao zaituni, tena kibao cha hasira kali

    "mshenzi wewe... Sasa kwasababu umeshaharibu ngoja nikuambie ili roho ikuume,... Yule kijana ndio alionunua hii nyumba na kuijenga upya, yote ni upendo wake kwako.. Yule kijana aliamua kuuza viazi ili ajue kama utampenda kutokana na hali yake alionayo ya kuuza viazi, yote hio ni kuangalia upendo wako, yule kijana kadiriki kukupeleka india ukapata kuona tena yote ni kwasababu yako wewe.. Haya muulize huyo mshenzi wako kama angekukuta kipofu angekupenda??... Nakuuliza angekupendaaa"

    Mama haachi kulia, na wakati huo zaituni ndio anafungukwa na maskio kumbe kaacha pesa kaufata umaskini,...

    "mama, ina maana"

    "ina maana nini?? mshenzi mkubwa  wewe, hata hio gari uliokuja nayo ni gari kama huamini angalia pale mbele ya gari kuna picha yake.. Na hio gari tulishwahi kuipanda mimi na wewe wakati wewe bado ni kipofu,.. Mtoto mbwa sana wewe, umechukuwa vya zainabu kuwa malaya wa mjinj, yaani nakuambia utakuwa malaya kama ndugu yako... Mbwa wewe.... Kijana wa watu kafanya yote hayo lakini humuoni, umeona huyo aliolegeza suruali mpaka miguuni ndio mzuri.... Eeehhh we kijana kama unanisikia nakuombea upate mke bora huko uliko"

    "kwanini lakini usingeniambia mama angu.."

    Mama kuskia hivyo kamzaba tena kibao

    "je angejuaje kama una upendo wa kweli... Eti umechezea mafungu 6 hili la saba siliachi.. Yaani mafungu saba yote umeshayamaliza mbwa wewe... Mtoto hananga sana wewe"

    Mama alikiwa akiongea huku akiondoka

    "mama ishia hapa hapa basi mama utaniharibia na hiko mama"

    Mama alikuwa akienda sebuleni huku akiongea kwa uchungu, ndipo zai akamzuia kuwa asiende huko sebuleni huku akiongea mana atamharibia kwa Saidi,.. Mama alinyamaza na kufuta machozi ili tu mtoto wake asikose bara na pwani, kama kakosa kikubwa basi wacha apate hata hicho kidogo alichoona kinafaa







     





    "Samahani baba, tumechelewa kidogo, nilienda kumwonyesha kwa dada yake"

    Aliongea mama zai baada ya kurudi sebuleni,...

    "pole baby"

    Zaituni alimwambia saidi lakini roho ilikiwa ikimuuma, kumbe sheby ni tajiri, na hata ile kazi ya kuuza viazi haikuwa yake bali alikuwa akimpima upendo

    "hakuna shida mama angu"

    Wakati huo saidi alikuwa anakunywa chai...

    "baba ongeza chai baba"

    Mama aliongea hivyo lakini moyoni mwake roho inamuuma sana mana myoto wake kafanya mistake kubwa sana....

    "tosha mama angu"

    Basi pale pale zaituni nae akaanza kuongea

    "mama... Huyu ndio mchumba wangu, nampenda na yeye ananipenda mama"

    "ooooohhhh karibu sana baba.. Na nashukuru sana kwa kukufahamu"

    "ahsante sana mama angu"

    "lakini mtafunga ndoa lini, mana isiishie kutambulishana tu"

    "mama... Yaani huu mwezi hauishi nataka mke mama angu"

    Mama aliona ndoa isipofungwa hapa kina kuachana tena hivyo anatamani wafunge ndoa,... Basi mambo yalienda vizuri mama kakubali lakini machoni mwake anamuona kijana sheby yaani haamini kama mtoto wake hajaolewa na yule kijana, mana kampenda sana yule kijana awe mkwe wake, lakini kwakuwa damu yake ni chafu basi watoto wake nao wamekaa kiuchafu uchafu... Basi saidi hakutoka bure nae aliacha kafungu chake kwa mashemeji na mama mkwe ili nae aonekane,.. Zaituni na mchumba wake walipanda gari kisha wakaondoka....



    "mama.... Huyu nae ni nani"

    Alikuwa ni zaituni aliomuuliza mama yake kuwa huyo mwanaume nae ni nani

    "ndugu yanu kaukimbia utajiri, yaani anamuacha mwanaume aliomseidia na kumfata huyu kijana, tena hata hio gari ni ya yule kijana kabisaa"

    "ina maana kaachana shemeji Sharbiny"

    "ndiooooo... Ndugu yenu mshenzi mmemuambukiza umalaya nyie, mtoto wangu hakuwa mtu wa kuchagua wanaume kiasi hiki"

    "mamaaaaa.... Sasa mimi nilikaa nae saa ngapi"

    "maskini ya mungu hii nyumba sjui atakuja kutufukuza"

    Mama aliongea huku akiangalia hio nyumba yake ambayo sheby aliinunua na kuijenga upya mana ilikiwa ni nyumba ya mama mkwe...

    "natamani nikutane nanyule kijana, nimuombe msamaha kwa niaba ya zaituni wangu jamani"

    Mama aliongea hivyo, lakini hana hata nguvu kwa kitendo alichokifanya zaituni.....



    Sasa huku ndani ya gari zaituni akiwa kaishika ile picha ya sheby huku akiuliza

    "kwahio huyu ndio boss wako"

    Aliuliza hivyo huku akiwa anamwangalia sana sheby katika ile picha

    "ndio, huyo ni kigogo haswa"

    "heeeee ivi kaoa huyu"

    "yes... Ana mke huyo"

    Zaituni alishtuka kuskia sheby ana mke,

    "ina maana alikuwa anifanye mke wa pili au"

    Zaituni alijiuliza kimoyomoyo maneno hayo huku asipate jibu la kuuridhisha moyo wake....



    BAADA YA MASAA MAWILI KUPITA



    Zaituni akiwa nyumbani kwake ambako amepangishiwa na mpenzi wake,.. Na wakati huo shadi nae anateremshwa na tax nje ya nyumba aliopangishiwa na buzi lake,... Lakini sasa ni sehemu ya kujiuliza kwamba kama shadi alikuwa malaya toka miaka hio mbona alikuwa akiishi nyumba za udogo, mpaka zaituni alipohamia kwake nae baada ya wiki nae akahamia, ni kwanini??.. Ukweli tutaujua hapo mbele.... Sasa wakati shadi anashuka kwenye tax, zaituni alikuwa na hasira na shadi mana shadi ndio kamfundisha kazi hio mpaka kakosa mwanaume wa maana na kutembea na mfanyakazi wake,.. Shadi alimpita zai na kumsalimia kisha akapita kwenda kwenye nyumba yake, mana wapo jirani kama walivyokuwa wakiishi kule uswahilini,... Zai aliingia kwa hasira nyumbani kwa shadi na kuanza kushikana tai...

    "we zai una nini lakini? Mbona una michezo ya ajabu bwana unanivurugia nywele zangu"

    Zai alimshika shadi tai huku akimtupia kitandani...

    "we malaya kwanini umenifundisha umalaya wako mbwa wewe"

    Zai aliongea hivyo huku akitaka kurusha ngumi kwa shadi, shadi nae alizuia na kumgeuza mwenzie

    "acha ufara wewe.... Wewe mwenyewe si akili zako zilivyo mbaya"

    Aliongea shadi huku akiwa kamkalia mwenzie kwa juu

    "shadi kwanini umenifundisha umalaya wako, mpaka namuacha sheby wangu kumbe ni tajiri kiasi kile"

    Shadi ndio anashtuka kuskia sheby ni tajiri

    "eti unasemaje wewe?? Sheby ni nani"

    Hapo sasa kila mmoja akamwachia mwenzie

    "sheby kumbe ni tajiri, anajifanya kuuza viazi kumbe ni tajiri ana hela"

    "we zai muongo wewe... Au katajirika kwa kuuza viazi"

    "mi sijui.. Ila nakulaumu wewe umenifundisha kazi yako mpaka nimemkosa"

    Aliongea zaituni huku akimnyooshea shadi kidole

    "weeee ishia hapo hapo... We ulifikiri mimi na wewe nani kamfundisha mwenzie??"

    Aliongea shadi huku akiwa kamshikia zai kiuno... Na wakati huo zai nae anashangaa kuskia kuwa hata yeye hakuwa malaya

    "una maana gani kusema hivyo we shadi"

    "tena unisikilize kwa makini.... Ulipokuwa malaya wewe mimi nilikuwa sio malaya, wewe ndio umenifanya mimi kuwa malaya"

    Zaituni alizidi kushangaa kuskia maneno ya shadi

    "we shadi unasemaje"

    "sasa skia ukweli mpaka nikakusababishia kiwa malaya... Mimi ndio chanzo lakini nyuma yangu kuna mtu mwingine alionituma kwako"

    "ati nini??.... "

    "unakumbuka siku ile ulipoanza kuja kule uswahilini ukiwa bado ni kipofu??"

    "ndio nakumbuka.... Kwani ilikiwaje"

    "sikiliza sasa ukweli mpaka wewe ukaanza umalaya.... Mimi wakati ule shadi mimi sijui mwanaume wala sijui hata kuvaa nguo fupi,... Ila ile siku nilipokuwa nje... Ilikuwa hivi"

    Sasa shadi anatoa ukweli juu ya kile kilichofanyika mpaka zai kuwa malaya,.. kumbe umalaya wa zai ulitafutwa, na sio kuwa alijikuta tu bali alikusudiwa, na huu ndio ukweli anaousema shadi....







    Katika maisha ya mwanadada shadi yeye hakufikiriga kabisa kama ipo siku atakuja kuuza mwili wake ili aweze kupata kipato cha kujikimu na maisha yake,... Lakini hutoweza kuamini kwamba shadi kajikuta akiingia katika kazi hio kutokana rafiki yake zai kufaidika kwa kupata mwanaume anaejiweza kimaisha.. Unaweza ukashangaa kwanini shadi kawa wapili kujiunga na zai wakati sisi tunajua shadi ndio wa kwanza... Siri nzito iliojificha siku zote lei ndio tunaijua na shadi mwenyewe ndio mropokaji wa siri hio....



    kumbe umalaya wa zai ulitafutwa, na sio kuwa alijikuta tu bali alikusudiwa, na huu ndio ukweli anaousema shadi



    KAMA UNAKUMBUKA SIKU ILE SHEBY ANAKUJA KUPANGISHA HIKI CHUMBA CHA USWAHILINI NA KUMKUTA SHADI AKIWA FUNDI CHEREHANI.... SASA KAZI ILIANZIA PALE.... NA ILI UELEWE VIZURI TUANZIE HAPA....... SIKU ILEEEE HATUKUJUA WALICHOONGEA AKINA SHASHA....



    "karibu ukae kaka"

    Yule dada aliongea hivyo ili hata kumshtua kijanja janja, mana anashindwa kumwambia asiangalie nguo yake,..

    "Ahsante dada angu"

    Sheby alikaa katika makochi yaliochakaa sana, yaani hata vitambaa vyake vimechanika afu yeye ni fundi,.. Mana hawezi kumaliza faida anayopata kwa ajili ya kushona vitambaa vya makochi yake,

    "ok ahsante dada yangu.... Aaaahh Samahani sana, nikiwa naendelea kumsubiria baba mwenye nyumba, kuna jambo nataka tuliongee mana umeshakuwa jirani yangu sasa"

    Aliongea kijana sheby huku nae akiwa na busara zake, sema busara hupotea pale anapoona nguo za kike,

    "sawa tuongee haraka nirudi kazini"

    Aliongea dada huyo huku akiwa kweli ana haraka ya kutoka hapo..

    "lakini bado hatujajuana hata kwa majina mama"

    "mmhhh.. Mimi naitwa Shadya ukipenda niite Shadi"

    "waoooo jina lako limeanza kama jina langu vile"

    "kwani we jina lako nani"

    "mimi naitwa Sharbiny, ni mtoto pekee kwenye familia ya kita... Nooo... Kwenye familia ya kimaskini"

    Sheby alitaka kukosea neno akajikuta anataka kuongea eti yeye ni tajiri... Basi shadya alipata kucheka kwa kigugumizi alichokipata sheby wakati wa kujitambulisha kwa Shadi (Shadya)...

    "unanicheka si ndio"

    "No, unajua nini? Ulitaka kujitambulisha hali za wenzako na wakati hali yako inaonyesha tu ulivyo"

    "kwani mi nipoje"

    "ulivyomalizia kujitambulisha ndivyo ulivyo, na ndivyo unavyoonekana"

    Shadi alimaanisha kwamba sheby alionekana maskini kabisa, lakini weeee heeeee balaa tu, pesa zimelala hapo..

    "sasa shadi, kuna kitu cha muhimu sana nahitaji kukuomba,.. Binafsi nahisi utanikubalia ombi langu"

    "mmmhh kaka unanitisha, kwani ni ombi gani unalotaka kuniomba"

    Maongezi yao hapa ndipo yanapoanza,



    MAONGEZI YALIKATISHWA HAPO.. SASA TUYAENDELEZE HAPA CHINI



    "nina mchumba wangu aitwae zai nataka kumleta aishi hapa,.. Lakini jirani mzuri atakuwa ni wewe"

    Aliongea sheby huku akiwa kakaa bila wasiwasi katika geto la mtoto wa kike,...

    "sasa kuna shida gani,.. Mana mimi sio mama mwenye nyumba kana kwamba nitakataa"

    "shadi.... Huyo mchumba ni kipofu,.. Kiukweli nampenda sana yaani tena sana, ila nina kapesa changu kidogo ambacho nilitaka kujenga kibanda changu huko mtaa wa chini... Lakini kutokana na hali alionayo mchumba wangu, nimesitisha kujenga ili nimpeleke india akafanyiwe matibabu ya macho"

    Aliongea hivyo kijana sheby, wakati huo shadi bado hajaelewa kitu chochote kile

    "mpaka hapo mimi sina kizuizi bado... Ila binafsi wewe ni mwanaume pekee ambae ndio kwanza nakuskia umempenda kipofu, Sipati picha mtaishi vipi"

    Aliongea shadi huku akichungulia kazi zake pale nje

    "enheeee.... Sasa hapo ndipo pazuri... Mchumba wangu huyo nataka nikukabidhi wewe uniseidie kumpikia chakula, kisha utampatia na pesa ya chakula mimi nitatoa, kumuogesha nitamwogesha mwenyewe,.. Nguo nitamvisha mwenyewe, kikubwa tu ninachokuomba ni kumpatia chakula na kumpeleka toilet tu basi na ni kitendo cha wiki moja tu"



    Shadi alichoka kwa hio kazi aliokuwa akipewa na kijana sheby, lakini sema shadi alikuwa ni mwanamke mwenye imani ya dini, hivyo kwake alihisi ni mitihani ya Mwenyezi Mungu,.. Shadi alikubali kupika chakula na kumpatia, na kumpeleka toilet...

    "kiukweli ni kazi ngumu sana lakini nitamwomba Mwenyezi Mungu anipunguzie mana nayo ni mitihani yake... "

    "nashukuru kwa kunielewa shadi.... Sasa nina ombi jingine"

    "lipi tena"

    "nataka hivi vitu vyako viwe kwake yaani haya makochi yako na kitanda chako viwe huko kwake atumie yeye"

    Shadi alishangaa kuskia hivyo

    "afu mimi nitalala wapi? Chini au?"

    "hapana... Nitanunua vipya utaweka afu hivi vilivyochakaa tuviweke huko kwangu"

    "mmmhhhh ivi unampenda mchumba wako kweli... Mana huezi kumuekea vitu vilivyochakaa ndani"

    "nina maana yangu na utaijua tu"

    "ok kwa hilo pia nimekubali, kwasababu una maana yako... Vipi kuna lingine"

    Shadi aliuliza kama kuna ombi lingine ambalo sheby anataka kuomba kutoka kwa shadi...

    "ndio ninalo ombi la mwisho kabisa"

    Aliongea sheby na kumwacha shadi hoi kwa maombi yake yalivyokuwa mengi,...

    "haya sema na hilo... Mana mwishowe utantongoza hapa mi sikuelewi eti"

    "kwani we si mwanamke tu, nitashindwaje kufanya hivyo"

    "we si una mchumba wako sasa untongoze wa nini tena"

    "kwani mchumba haachwi"

    "akaaa mi staki umuache mtu kwa ajili yangu"

    Shadi kumbe tayari alishaanza kumpenda sheby...

    "ok sasa skia... Ombi langu la mwisho ni hili... Baada ya kuona kwake, nataka uanze kumdanganya na mambo ya starehe, ili nijue kama kweli ataridhika na hali yangu au laa, mana nyie wanawake wa siku hizi mnapenda maisha mazuri sana na sijui ni kwanini"

    "aahhhh hebu ngoja kwanza... Unasema nimdanganye na mambo ya starehe kama yapi"

    "kwanza uwe unavaa vizuri na kumlingishia,... Afu akikuuliza unafanya kazi gani unamwambia nafanya kazi ya kujiuza"

    "whaaaat....hapana sheby hio mimi siwezi, siwezi mimi"

    "kwani unajiuza kweli??"

    "hapana mi siwezi kuvaa nguo za kujiuza"

    "sikiliza basi... Nguo unazivaa ukiwa nae lakini ukitoka unazivua au unavalia kanga kwa juu"

    "no, no sheby siwezi..... Yaani sasa mimi nianze kumkuadia sasa"

    "haswaaaaa... "

    "sasa si utakuwa unamuuza mchumba wako"

    "hapana.... Kama ana akili mimi ni nani na nilimtoa wapi na anataka awe nani yangu, basi kamwe hawwzi kukubali utakachomwambia... Lakini kama akili yake ni mbaya, atakubali unachomwambia"

    "mungu wngu shadi mie, kazi gani unanipa sheby"

    "naomba uniseidie shadi... Mimi siwezi kutambua mke wa kuoa, kuliko nioe ndio abadirike bora nimjue mapema"

    Aliingea sheby huku akiwa sirias kweli,

    "jamani sheby... Ok sasa hizo nguo mie nitatoa wapi"

    "ninachukuwa pesa kidogo kwenye mtaji wangu wa viazi, ukanunue nguo zile za kichangudoa zile... Afu nitakuwa nakupa pesa kwa ajili ya kumringishia ringishia,.. Kama ana akili basi hawezi kubali ujinga wako lakini kama hana akili atakubali huo ujinga"

    "sasa akisema na yeye anataka mwanaume kama mimi, haya nitampeleka au niamuache"

    "mpeleke kwenye mijumba ya starehe huko lazima watamuona, akishakuwa hivyo tu basi huyo sio mke wa kuoa... Kikubwa nataka kujua kuwa ataridhika na hali yangu ya kuuza viazi"

    "kazi ngumu sana.... Kazi ngumu sana.. Kwa mtu wa dini kama mimi kufanya hivyo,.. Hata kazi zangu zitakufa sasa"

    "nitakulipa elfu 10 kila siku"

    "ati unasemaje"

    "ndio..."

    "lakini mimi hata hayo majumba ya starehe siyajui hata moja"

    "nitakuonyesha baadhi ya majengo... Yaani wewe kazi yako ni kumringishia mavazi yako na pesa, akitamani mpeleke afu unijulishe"

    Maongezi kati yao yaliishia hapo lakini shadi alishampenda sheby hivyo kwa nafasi aliopewa ya kumringishia zai mavazi na pesa,.. Binafsi yake alisema atajiongeza zaidi

    "napenda mwanaume mchapakazi kama wewe,... Natamani unioe mimi.. Na kazi yako nitajiongeza mara dufu ili tu niwe na wewe"

    Aliongea shadi baada ya sheby kuondoka zake,....



    BAADA YA SIKU MBILI KUPITA







     





    sheby na zaituni walihamia katika nyumba hio, lakini wakati huo zaituni alikuwa bado ni kipofu,.. Kitanda kilichakaa makochi yalikuwa yameisha, na hivyo vitu ni vya shadi,..



    BAADA YA WIKI TATU KUPITA,..



    Wakiwa wamesharudi india, na zaituni alikuwa anaona vizuri kama zamani,.. Zai alikutana na hali ya mchumba wake kuishi kwenye nyumba ya udongo,... Sasa kazi ya shadi ndipo ilipoanza,.. Mara leo kavaa nguo mpya, mara kesha kaja na pesa, hivyo hivyo ikawa hivyo, nadhani tuliona vituko sema hatukujua tu... Ilifikia mpaka zaituni anatamani ile hali ya shadi kupendeza mara kwa mara bila kujua yeye ndio anategwa ili kujua ni mschana mwenye tamaa au laa.. Shadi na kazi yake alizidi kumdanganya zai,... Zai mwanzoni alikataa lakini mwisho wa siku alijikuta anatamani mavazi na pesa alizonazo,... Kumbe pesa alikuwa akipewa afanye hivyo, saa mingine anampa pesa kabisa ili kumwonjesha radha ya pesa.... Zai alijikuta nae anatamani ile hali, na kitaka kuunganishwa na kazi hio anayoifanya shadi... Kila hatua anayoifanya shadi alikuwa akimtaarifu sheby... Na kama unakumbuka kuna siku sheby aliwakuta njiani shadi na zai wakiwa wamevalia mavazi ya ajabu ajabu, wakati huo sheby akiwa na mkokoteni wake... Shadi alimpigia sheby simu na kumpa taarifa zote, mpaka zai akapata buzi la kumuoa kabisa na kumlipia kodi ya nyumba, uzuri ni kwamba hajajiuza bali alipata mwanaume aliopenda kabisa na kutaka kuweka ndani... Ilifikia mpaka hatua zaituni anahamia kwenye nyumba aliopangishiwa na buzi hilo.. Sheby alipata taarifa ya zai kuhamia nyumba mpya aliopangishiwa,..



    Sheby yote hayo alikuwa akiyajua lakini alikuwa anajifanya hajui pale anapokutana na zaituni,.... Sasa baada ya sheby kujua zai keshamuacha, akajikuta kuwa na mawazo mengi sana juu ya zai kupoteza pesa zake nyingi sana afu mwisho wa siku anakuja kuwa na mwanaume mwingine....

    "boss vp mbona una mawazo hivyo"

    Alikuwa ni saidi aliomkuta boss wake akiwa kajiegemeza kwenye ustelingi wa gari

    "we acha tu,... Ivi unaweza kugharamia kitu afu kikawa hasara tupu yani"

    Aliongea sheby huku machozi yakimtoka kwa uchungu,...

    "nini tena boss,.. Kuna mzigo umepotea"

    "bora hata kungepotea mzigo... Kuna demu nimemgharamikia mwili wake lakini huezi amini kaniacha hivi hivi yani"

    "aahhhhhh mbona kuna watu wanasomesha mademu zao lakini hawawaoi"

    "kweli?"

    "aahhhh wengi sana"

    Sheby kuskia mbona kuna watu wanasomesha na hawaoni ndani kidogo hapo akapata imani kuwa kumbe hakuwa peke yake....

    "aaahhhhh lakini mbona hata shadi ni mwanamke mzuri tu na anafaa kuoa yule"

    Sheby alikua akiongea hivyo baada ya kuona zaitini keshakuwa na tamaa ya maisha,...

    "kumbe ulikuwa na wengi vuta na huyo"

    Saidi alikiwa akisapoti, bila kujua huyo huyo saidi ndio aliomchukuwa zaitini wakati walipokutana matembezi huko mjini kati time za usiku,...

    "hawa wanawake hawaaminiki kabisa yani"

    "aahhhh mi wangu katuliaaaaa"

    "hebu ngoja nimpigie simu tukutane, na huyu staki kumsubirisha kama ni kunijua wacha anijue kuwa mi ni tajiri"

    Aliongea hivyo sheby huku akiwa anatafuta namba ya shadi ili ampigie



    Tukija huku geto kwa shadi ambako ni uswahilini, maskini kaachwa peke yake, zai keshahama kwenye jumba la maana,... Wakati zai akiwa anasubiria nguo za kushona mawazo yalimpeleka mbali sana

    "nyumba ya mwenzangu nzuri, kila nikienda natamani kulala kwa zai... Mimi ndio chanzo cha maisha yake... Kama yeye kaweza mimi nitashindwa vipi....tena kwa bahati nzuri kapata mwanaume wa kumuoa, kwanini mimi nisipate,... Nampenda sana sheby lakini lakini keshanisahau kwasababu kazi yake imeisha.... Hapana, hata mimi ni mwanamke mzuri naweza kupata mwanaume kama mwenzangu zaituni..."

    Shadya alikuwa akiongea mwenyewe huku nae akiitafuta namba ya zaituni. Wakati huo na sheby nae keshaipata namba ya shadi anataka ampigie ili amuite mahari wakutane.... Wakati huo na shadi nae keshapata namba ya zai ampigie wakutane ili amuulize kuhusu mwanaume ambae alishawahi kumuulizia...



    Kwa bahati mbaya sheby alipopiga aliambiwa simu inatumika,... Sasa shadi alikuwa akiongea na zaituni

    "eee shost mambo"

    "safi shadi mzima wewe"

    "salama tu... Nahisi upo nyumbani ee"

    "yes nipo hapa naangalia tv huku nikipata juice baridiii"

    Zai alikuwa akizidi kumringishia mwenzie na maisha mazuri, yaani sasa kule kwa shadi kumringishia mwenzie mavazi na pesa, sasa kumemgeukia yeye....

    "ok sasa skia zai... Ivi yule kijana aliokuuliza kuhusu mimi vipi? Ivi bado anaendelea kukusumbua tu"

    "yaani shadi umeikosa bahati wewe,.. Yule boy alinipigia jana, ila nikamwambia hutaki"

    "ooohhh shit, sorry naomba namba yake nimcheki"

    "ati nini"

    Zai alishtuka kwa kuskia shadi kakubali kuwa na huyo kijana wanaomsemea

    "nipe namba zake basi"

    "ok poa ngoja nikutumie"

    Zaituni aliitafuta namba ya huyo jamaa aliompenda shadi na shadi kukataa,.. Shadi alitumiwa namba ya huyo kijana na kuisevu kabisa,... Sasa akawa anasita kupiga, mana mwanamke kumtongoza mwanaume ni ngumu, sasa wakati huo huku kwa sheby nae akarudia tena kupiga, mana mwanzo aliambiwa kiwa namba aliopiga ilikuwa ikitumika,.. Wakati huo huku kwa shadi nae kabonyeza kitufe cha kupigia kana kwamba kaamua kumpigia huyo boy amwambie keshamkubalia.... Sasa hapo sijui kachelewa au kawahi, mana ikiingia simu ya sheby tu basi kapata bahati, lakini kama kawahi basi simu ya sheby hawezi kuipata tena... Sasa kila mmoja akawa anasikilizia kama itaita au vipi









    Katika maisha wahenga walisema kuwa kuna mafungu saba ya bahati kwa binaadam, na kila fungu huja kwa wakati maalumu na kwa miaka tofauti tofauti, ukichezea fungu moja basi jua yapo mengine yaliyobaki kwa ajili yako, hivyo usikate tamaa katika maisha,... Kijana sheby ni kijana ambae wengi tunamjua kuwa ana mke, lakini mke alienae pia tunamjua, hamtimizii haki za ndoa ugomvi haushi visa ndani ya nyumba haviishi, binafsi yake yeye alitaka kuoa kimya kimya bila hata ya wazazi wake kujua kuwa kijana wao kaoa, na ndio mana siku zote anakuwa mstari wa mbele kutafuta mke bora kwa kuibadiri hali yake kuwa hali ya watu wengine ili apate mke atakaeridhika na maisha anayoishi kijana sheby, lakini kila akijitahidi kutafuta hapati mke bora, mchumba aliomgharamikia macho leo kamuona hana maana kisa kapata mtu mwenye maana kuliko sheby,..

    Lakini kijana sheby hakukata tamaa, bado anaamini riziki ni mafungu saba huenda hilo lilikuwa sio fungu lake,... Zaituni ana rafiki aitwae shadi na ndio aliopewa kazi na sheby kuwa amdanganye kama ataweza kudanganyika ili ajue kuwa anampenda au laa,.. Mschana huyo aitwaye shadi nae alikuwa ni mtu wa dini hivyo kazi aliopewa na kijana sheby ilikuwa ni ngumu kwake kwasababu dini yake haikuruhusu kuvaa nguo fupi.. Ila ilimlazimu kufanya hivyo kwasababu nae alishaanza kumpesha sheby, hivyo hata kule kumkuadia zaituni, alikuwa akifanya kqa juhudi zote ili yeye awe na sheby.... Lakini sasa kosa la sheby alilofanya ni kumsahau shadi baada ya kujua zai keshaharibika na haambiliki tena... Sheby alikuwa hata simu kwa shadi hapigi mana hana kazi nae tena na hata shadi kama unavyojua maisha yake ni ya chini sana, na wakati huo zai keshahamia mjengoni tayari, kamwacha mwenzake kwenye nyumba za udongo, na sheby nae akasusa kuja uswahilini kwasababu hakukua na mtu wa kumleta huko, na alikua hajui kama shadi nae kampenda,.. Maskini shadi anakula msoto na kujikuta anairudia kazi yake ya kushona nguo, mana aliacha kwasababu alikuwa akipewa pesa na sheby... Lakini sasa kumbe kipindi wakati shadi anamtembeza mwenzie kwa wanaume yeye alikuwa pembeni na hataki tabia hio ila alifanya kwa kutumwa, katika moja ya wanaume walikutana na zai mana zai si keshakuwa mjanja wa mjini baada ya kujua utamu wa pesa,... Kijana huyo alimuuliza zai kuhusu rafiki yake ambae ni shadi,... Zai aliona shadi ni mtu wa mambo haya hivyo hawezi kukataa... Shadi alipoambiwa kuwa kuna mwanaume kampenda, shadi alikataa katu katu, mpaka zai akashangaa mtu aliomfundisha kujua wanaume leo anakataa mwanaume, ila hakutaka kujua sana wakaachana ila yule kijana alikuwa bado anamsumbua zai kuhusu shadi..



    Sasa leo shadi kaamua kumtafuta yule kijana mwenyewe mana hali ya maisha kwake anahisi imekuwa ngumu,... Lakini sasa huku shadi anawaza kumtafuta huyo kijana, na huku sheby anawaza kumtafuta shadi,... Na hapo ndipo simu zilipoanza kupigwa hivyo kila mmoja alikuwa akisikilizia kama itaita au vipi,



    "haloo Jackson mambo"

    Ilikuwa ni sauti ya shadi ikimsalimia Jackson ambae ndio kijana alimpenda sana kutoka moyoni,...

    "safi tu nani mwenzangu"

    "mmmh shadi hapa naongea"

    "aaahhhh rafiki wa zai si ndio eee"

    "ndio"

    "oooohhh mambo vip mrembo"

    "hahahahaha safi tu"

    "mbona wacheka kuna kipya"

    "i think kuna kipya"

    "basi tukutane mjini au vipi shadi"

    Wakati huo huku kwa sheby simu inamwambia kuwa namba aliopiga inatumika hivyo asubiri kidogo au akate apige tena... Sheby kwa hasira aliipigiza simu chini, alichoambulia ni laini tu, alichukuwa laini yake na kuondoka.... Sasa huki kwa shadi mambo yameiva

    "sawa nikukute wapi sjui"

    "aahhhh ebu chagua hoteli kubwa unayoipenda"

    "Novo hotel, panatufaa kiukweli"

    "eti eee"

    "yes"

    "basi njoo pale nami najiandaa kuja"

    "sawaaa"

    Jackson alifurahi sana mpaka akampigia simu zaituni na kumshukuru kwa kumpata shadi,... Shadi alikuwa ni mschana mzuri mwenye sifa kila kona ya mwili wake, yaani yeye na zaituni wametofautiana rangi tu lakini uzuri sheby yaani wapo vizuri kiukweli... Sheby alijikuta anakosa kila kitu... Mawazo kwake ndio chakula, mana hayaishi kichwani mwake...



    HAPO NDIO MWISHO WA KUMBUKUMBU KABLA YA MIEZI MIWILI ILIYOPITA.... NA KUMBUKUMBU HIO ILIANZA PALE ZAITUNI NA SHADI WALIPOSHIKA KWA KUPIGANA KISA KUKUADIANA







     





    "niachie sasa si nimeshakwambia ukweli"

    Aliongea shadi, mana zaituni alikuwa bado kamshika shadi...

    "lakini shadi ulichokifanya kwangu sio kizuri, umenikosea sana"

    "sikiliza zaituni... Unajua hata mimi nilikuwa nampenda sana sheby vile vile na umaskini wake, lakini hata mimi nimemkosa mana alishawahi kuniona nikiwa na Jackson"

    "weeeee wacha uongo shadi"

    "kweli, tena alinikuta sehemu za starehe tu"

    "mmmhhh basi ndio hivyo tumeshamkosa wote... "

    "lakini zai we mwongo kusema sheby ni tajiri"

    "kwani we ulivyokutana nae alikuwa katika hali gani"

    "alikuwa na mkokoteni wake"

    "ndio hivyo sasa, sheby sio muuza viazi wala nini, bali alikuwa anatafuta mke"

    "lakini wewe ndio roho itakuuma mana alikuwa mchumba wako yule"

    Zaituni alikasirika kuskia maneno hayo

    "shadi naomba tuepushe shari mana tutapigana hapa nikuuwe bure"

    "umuuwe nani bwana we nenda kwako bwana"

    "sawa... Lakini dhambi ulizonazo za kivunja uchumba wa watu, yaani utachomwa mpaka basi wewe"

    "nyoooo, utajiju bibie si umalaya wako mwenyewe"

    "sawaaaa"



    Wakati huo ni mida ya saa 12 kasoro sheby akiwa ofisini anasubiria gari ije aondoke, mana gari aliichukuwa saidi na kusema anakwenda kutambulishwa kwa wazazi wa mpenzi wake,.. Sheby akiwa kakaa zake ofisini kwake, tena alikuwa peke yake mana wafanyakazi wote walishaondoka mida ya saa 11 kamili za jioni,.. Hivyo yeye alikuwepo wakati wa kusubiria gari

    "piiiiiiii"

    Ilikuwa ni honi ya gari iliosikika nje ya geti la ofisini

    Sheby alichukuwa kibegi chake na kutoka nje mana gari hio iliopiga honi ilikuwa ni gari yake,...

    "aaahhhh sorry boss Nilikawia kidogo"

    "hakuna shida,... Twende"

    Basi saidi aligeuza gari kisha haoo wakaondoka zao



    Tukija huku kwa wazazi wa mwai waliokuwa na shamra shamra za sherehe juu ya kupata mimba kwa mtoto wao,.. Mana sasa mimba ya mwai yapata miezi miwili sasa na kila mtu anajua, lakini ukweli wa hio mimba sisi tunaijua sio ya sheby, bali ni mimba ya mpenzi wake mwai lakini kabebeshwa sheby kuwa ni yake,... Na shamra shamra hizo ina maana sherehe ni kesho, sheby kufika nyumbani alikuta nyumba imepambwa pambwa, na anajua fika kuna sherehe ya kupata mimba salama tena akiwa ndani ya ndoa yake, sheby siku zote yeye sio mtu wa raha kama ilivyo katika simulizi zingine ila hiii kachapika haswa...

    "mambo"

    Mwai alimsalimia mume wake kihivyo, lakini sheby hakuiyikia kabisa,.. Sasa huezi amini mwai toka siku ile afanye mapenzi na sheby, kwa sasa kidogo ana heshima kwa sheby yaani yale maujeuri JEURI hakuna tena siku hizi kawa mpole

    Sasa hivi sheby ndio kiburi, mana mwanzo kiburi alikuwa ni mwai lakini kwa sasa kiburi ni sheby haitikii wala nini... Sheby alioga kisha akaja zake sebuleni na kufungulia tv ili aangalie taarifa za habari,..

    "unawekaje michaneli yako na wakati mi naangalia chereko chereko, Ebu yoa ITV yako niwekee send off zangu niangalie mimi..... Afu kesho hakuna kwenda kazini,... Kesho ni sherehe ya mtoto wetu kufikisha miezi miwili tumboni"

    Sheby alimuangalia sana huyu mwanamke na asimpatie jibu.. Sasa sheby kuna CD alikuja nayo kutoka kazini, aliinunua mida ya mchana hivi sasa aliiweka kwenye gari sasa alipofika nyumbani akaitupia mezani

    "hiii ni cd gani.. Ya Bongo movie au ni ngumi zako tu"

    Mwai aliongea hivyo huku akiichukuwa hio cd na kuifungua kava ili atoe ile cd yenyewe,... Lakini sasa ile anafungua tu, kuna karatasi ilidondoka mezani, kana kwamba ilikuwa ndani ya lile kava....

    Sheby nae alishangaa mana aliponunua hio cd alifungua na hakukuwa na karatasi, yeyote sasa nani kaweka hio karatasi.. Lakini sheby hakuwa na wasiwasi sana kana kwamba huenda ni karatasi ya maelezo ya hio cd....

    "heeeee cd za siku hizi zina maelezo"

    Aliongea mwai huku akiifungua ile karatasi

    "mbona una Kiherehere we mwanamke, kwani nimekuletea wewe hio cd

    "hata kama, kwani si umeiingiza ndani... Haaaaaaaaaa"

    Sasa ghafla mwai anastuka kwa kusoma hio karatasi, hata sheby akapatwa na wasiwasi juu ya karatasi hio....

    "ina mana kumbe ulikuwa unatafuta mke mwingine???"

    Sheby alishtuka kuskia mwai kasema hivyo,..







    Katika maisha unaweza kufanya kitu bila kujua kuwa kinaweza kumuathiri mtu mwingine, kumbuka unapofanya jambo angalia na mbele kutakuja kutokea nini,... Kijana sheby mchana wa leo aliingia katika Library ya kuuza CD ili ile siku ya sherehe ambayo ni kwsho awe ndani tu anaangalia zake muvi, mana hajaipenda na hatamani kuhudhuria,.. Sheby alinunua cd moja iliomvutia sana iitwayo THE BEST WIFE... Aliiweka kwenye gari yake kisha huyo kaelekea kwenye mizunguko yake,... Sasa muda huu ndio anashangaa kumsikia mke wake anasema mambo ya kutafuta mke mwingine,..

    "ina mana kumbe ulikuwa unatafuta mke mwingine???"

    Sheby alishtuka kuskia mwai kasema hivyo, mana kwake analifanya kama siri na hataki hata wazazi wake wajue kama anatafuta mke mwingine, ili siku akimbwaga mwai aje mwingine,...

    "we umeikuta wapi hio karatasi"

    "si huku ndani ya cd uliokuja nayo"

    "yaani umekosa cha kuniongelesha sasa umeona uandike upumbavu wako afu ujifanye ilikuwa kwenye cd"

    Aliongea kijana sheby huku akiwa na hasira mno,

    "heeeeeeee ina maana mimi ndio nimeandika hivi"

    "hebu lete hio karatasi"

    Sheby aliichukua ile karatasi tena kwa kumpokonya mwai,... lakini sasa sheby anazidi kushangaa mbona mwai siku hizi kapunguza ukali, yaani ni tofauti na mwanzoni mwa ndoa yao mana kuna muda sheby anashikwa tai kabisa na kutaka kupigwa, lakini sasa hivi ukali umepungua,... Sasa sheby kuangalia ule muandiko ulioandikwa pale, ni muandiko anaoufahamu kabisaa...

    "ina maana yeye ndio kaandika hivi,.. Na nilimpakia lini"

    Sheby alikua anajiuliza huyo myu alimpakia lini mana hajawahi kumpakia kwenye gari hio

    "zaituni nilimpakia lini mungu wangu, mana huu ni muandiko wake kabisa huuu... Au ni huyo demu wa saidi ndio mwenye muandika kama wa zaituni"

    Sheby alizidi kujiuliza sana kimoyomoyo na wakati huo mwai ndio anaondoka kwenda kulala zake mana siku hizi kapunguza ukali na alijua tu huo ujumbe huenda haujui na ndio mana kaacha, na pia mpaka hapo sio tabia yake, kapunguza sana tu.... Sheby alijua kabisa huo ujumbe haukuwa ukimuusu yeye japo hata yeye anatafuta mke mwingine... Ujumbe uliandikwa hivi...



    SAWA NASHUKURU KWA KUNIFANYIA HIVYO,... KWANZA SIAMINI KAMA UNA MKE... ILA NISAMEHE SANA MANA HUENDA NIMEKUPOTEZEA MUDA NA PESA ZAKO,... HATA MIMI NILIKUWA NAKUPENDA SANA, ILA TAMAA YA MAISHA... BINAFSI NI KWAMBA TAYARI NIMEKUKOSA,.. LAKINI NAKUOMBEA KWA MUNGU UPATE HUYO MKE WA PILI,... MANA SIAMINI KAMA NINGELIKUJA KUWA MKE WA PILI.... SAMAHANI SANA, NAJUTA KUKUHISI FUKARA.... NAKUOMBEA UPATE MKE MWENYE HESHIMA KULIKO MIMI,.. NA PIA NAOMBA UENDELEE KUUZA VIAZI ILI UPATE MKE BORA...  AHSANTE SANA.... NAKUTAKIA BAHATI NJEMA



    Sasa sheby ndio kajua sababu ya mke wake kuachana na ujumbe huo ni kwasababu ya pale aliposema, usiache kuuza viazi ili upate mke bora.... Mwai akajua hio sms wala haimuusu mana sheby sio muuza viazi, lakini sasa sheby kajua fika huo ujumbe unamuusu yeye, sema alikuwa anazuga zuga tu... Ila kichwa chake kinatafakari sana, je huyu zai kapanda lini gari yake? Kila akifikiria juu ya zaituni kupanda gari yake hapati picha kabisa.... Sheby aliangalia simu yake haoni, akajua kaiacha chumbani,.. Aliamka na kwenda chumbani,... Alipofika alimkuta mke wake anachati Instagram yupo na laptop yake,.. Sheby kaka kwenye kitanda chake na kumpigia saidi...

    "oya saidi vp hali"

    "safi boss, vp saa hizi kuna nini tena"

    Saidi alipata hofu baada ya kuona simu ya boss mdogo usiku...

    "ivi mke ulioenda kutambulishwa kwao anaitwa nani"

    "hahahahahaha, mtoto wa Kiislamu mtoto anaitwa zaituni"

    Sheby alishtuka lakini hakuonyesha kama kashtuka... Ila akatumia maneno ya kawaida ya kumchombeza saidi ili atume picha ya huyo zaituni

    "waapi wewe usikute umeoa kimbaumbau hana hata nyama"

    "aaahhhh weweeee, boss ivi mi unanionaje vile... Ngoja nikuonyeshe mtoto,.. Nilimpiga picha akiwa kwenye vazi la kimjini mjini"

    Sheby hivyo ndivyo alivyotaka picha itumwe na ni kweli inatumwa... Sheby kwa uchokozi akamchokoza mke wake mana siku izi kapunguza ukali

    "vipi umeujua huo ujumbe ni wa nani, mana umeniacha ghafla tu"

    "niliposoma tu neno usiache kuuza viazi nikajua sio wewe wala haikuusu hio"

    Ghafla simu ya sheby ikaingia meseji, kuangalia alikuwa ni saidi kamtumia picha.... Laaaaa Haulaaaa alikuwa ni zaituni kweli, tena mtoto alivaa tishet kubwaa zile za kike ambayo imefika mpaka mapajani, tena ilikuwa imembana, hivyo umbo lake lote unaliona kwa ramani tu ya ile tishet mana ilimchora haswa,... Sheby alishikwa na hasira sana, yaani kumbe saidi ndio katongoza demu ambaye sheby alimtazamia kuwa mke, ila kwa mapepe ya mwanamke huyo ikashindikana,...



    BAADA YA USIKU HUO KUPITA







     





    Na leo ni asubuhi sheby akiwa anajiandaa kwenda kazini

    "hee hee hee, unakwenda wapi"

    Aliongea mwai huku akiwa kasimama mlangoni,...

     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog