Search This Blog

Thursday, 24 November 2022

THE ISLAMIC WIFE - 5

 

     



     

    Chombezo : The Islamic Wife

    Sehemu Ya Tano (5)

     



    Walipofika katika duka moja kubwaa la kiarabu, si unajua mambo ya tanga, waarabu kama kwao yani...

    Basi rahim na zena waliingia, basi zena ndio aliokuwa akichagua kanzu ya rahim,..

    "hiii ya rangi ya bluu bahari inakufaa"

    Aliongea zena baada ya kuipenda kanzu hio, lakini rahim yeye alikuwa anataka kanzu za gharama kubwa...

    "kwanini tusichukuwe hii ya damu ya mzee"

    "hio achana nayo.. Nzuri hii bluu bahari"

    "eti kaka, hii.. Hii kanzu bei gani"

    Aliuliza rahim ile kanzu ya damu ya mzee

    "hio kanzu ni laki tano... Inakuwa na suruali yake na kofia yake na skafu yake"

    Kabla ya rahim kutaka kutoa pesa, zena kawahi kusema

    "sasa laki tano, unakwenda kumuonyesha nani kuwa una kanzu ya laki tano"

    Aliongea zena huku rahim akiguna na kusema

    "mmmhh haya bwana kama umeamua"

    Rahim aliiacha ile kanzu na kuchukua ile alioichagua zena

    "ok na hii aliochagua mwana mama ni shilingi ngapi"

    "hio ni laki mbili, nayo ni full kila kitu"

    Lakini zena alihisi kumkwaza rahim mana kamkataza kitu alichokipenda,..

    "basi nunua zote... Mana naona umenuna"

    "ila sio kuwa nanunua mimi tu, nawewe chagua hijabu zako..."

    Basi yalikuwa ni mahusiano yalio bora sana, na uzuri ni kwamba mmoja ana uwezo na mwingine hana uwezo wa kifedha, hivyo ni raha tu, kuliko wote kuwa na uwezo hua mnadharauliana mana kila mtu ana pesa,...



    BAADA YA MIEZI MIWILI KUPITA



    Rahim kwa sasa ni bonge la shekhe,.. Na kurudi shule kakataa kabisa, hakurudi tena, yaani hata Arusha hajarudi... Sasa hivi humuambii kitu katika mambo ya Qur-aan, anaongea kama ndege... Na muda wote yeye yupo msikitini,.... Ukumbuke kuwa jamali ambae ni kaka yake hayupo Tanga, aliondoka na baba yake kwenda kuangalia miradi yao, na jamali yeye anafanya kazi chini ya baba yake, na rahim yeye bado hajahusishwa na kazi kwasababu alikuwa ni mwanafunzi,... Wakati huo zena na rahim wakiwa wanarudi toka kuswali swala ya Ijumaa, wakiwa wote,...

    "rafiki yako siku hizi simuoni.. Kasafiri nini"

    Rahim alimuuliza zena, huku wakitembea taratiibu kabisa,..

    "unamuuliza wanini??... Hata mimi nina muda sijamuona, toka nilipokutana nae, na kumpa vigongo vyake, mpaka leo sijamuona, na hata kwetu hajaja"

    "we zena weee, ina maana ulikutana nae"

    "ndio... Tena alipobisha kua hajaongea na wewe, nikamsikilizisha ile rekodi.. Alitulia kimyaaa"

    "mmmmhh na wewe hugandishagi mmhh"

    "mbele ya mume nani agandishe"





    Sasa huku kwa akina fadhila,... Mtume simama weee. Kumbe fadhila ana kitumbo, tena kimetoka haswa,... Fadhila akiwa na rafiki yake mmoja hivi wakiwa wanaongea mambo yao

    "enheee, ile ishu ya zena na rahim umefikia wapi"

    Aliuzia dada mmoja ambae bado hatujamfahamu jina

    "minah,.. Mimi hata sielewi.. Nampenda sana rahim, na sasa hivi upendo wao ndio umezidiii"

    Aliongea fadhila, huku kitumbo kina miezi kama miwili hivi na nusu,..

    "kwa sasa huwezi tena... Umesha chelewa fadhila"

    "weeeee.... Unaiona hiii"

    "nini... Si mimba hio"

    "sasa huu ni mzigo wa rahim.. Atake astake lazima anioe"

    "we fadhila wewe... Unasema kweli hio mimba ni rahim"

    "tena sasa hivi.. Nataka nikawavizie wakirudi msikitini..."

    "Heheheeeeee haloooo... Hio kubwa bibie, lazima zena akae chonjo.. Heheeeee haaaaalooooo"

    Minah alicheka kicheko cha umbea huku akizidi kumjaza mwenzie upumbavu,....

    "tena kama tunachelewa vile.. Hebu nisindikize minah"

    Basi minah na fadhila waliamka walipokaa kisha hao kiguu na njia, mpaka kwenye barabara fulani hivi ya kutokea msikitini,.. Na ni kweli rahim na zena walikuwa wakitembea taratibu huku wakihadithiana hadithi za mitume waliopita, jinsi walivyokuwa wakiishi na wake zao.. Lakini sasa rahim alipofika mahari nywele zilimsisimka, kana kwamba kuna balaa mbele au kuna kitu fulani ambacho sio sahihi,..

    "zena, mbona nywele zimenisisimka hivi"

    "kuna nini kwani"

    "au kuna nyoka nini mbele yetu"

    "aah nyoka si ungemuona hapa"

    Basi waliendelea kutembea na ule msisimko wa nywele uliacha, na wakasahau, lakini walifika mahari rahim na zena wanaachana, yaani rahim anakwenda kwao na zena nae anakwenda kwao... Sasa kabla hawajaachana, mara ghafla fadhila huyo katokea...

    "Samahanini wana ndoa watarajiwa"

    Aliongea zena huku minah akifuata nyuma,... Wanafiki wakubwa hawa...

    Rahim alijua hapa hapako salama hapa, mana fadhila hakuja vizuri,...

    "fadhila, naomba uende ukampumzike, hivyo ulivyo na jua hili utadondoka bure"

    Rahim aliongea kwa upole japo yeye hajui kuwa kuna jipu kubwa haswaa linamhusu...

    "weeeeee naomba unyamaze hivyo hivyo... Kuna siku huyu mchumba wako sjui nani wako, kaja kunisuta kisa ni kukuambia ukweli.. Na ulivyo mjinga eti umenirekedi... Sasa nasema hivi umeyakanyaga babu weee"

    Fadhila aliongea huku vidole juu, yaani imani ya dini ilimtoka kabisa mwanamke huyu.... Wakati huo zena katulia kimyaaa

    "fadhila... Hebu Jihurumie ulivyo.. Unakitesa kiumbe cha watu kukiweka juani hivyo"

    Aliongea rahim kumaanisha kuwa fadhila yupo juani na hio mimba... Hivyo anamtesa huyo kiumbe aliopo tumboni...

    "heeeeeee... Kiumbe cha nani??... Yaani hapa naitesa damu yako na sii kiumbe cha watu"

    Zena alivaa nikabu usoni lakini macho yake yalionekana yalivyotoka kwa kusikia hayo maneno

    "unasemaje zena..."

    Aliuliza rahim... Huku zena nae akijiandaa kusema neno... Lakini kabla zena hajasema kitu.. Fadhila kawahi kuongea kuwa



    "sina shida na wewe rahim... Nina shida na huyu mke mwenzangu, alijue hili kuwa atake astake nyumba moja tutaishi,...... Wewe zena naongea na wewe,... Afu nadhani unazijua sunna za mtu.. Alioa wake zaidi ya mmoja... Nafurahi kuwa mke wa pili kwenye familia yenu"



    Aliongea fadhila huku nyuma minah akaanza kucheka kwa umbea...

    "heheheheheeeeee haaaaaloooooooo, Meseji sent hiooooooooooooo"





    Kiukweli Hakuna kizuri kinachokuja kiurahisi, lazima kuwepo na mabonde, milima, misitu, wanyama wabaya.. Katika mahusiano ya zena na rahim yamekuwa yakitawaliwa na vituko vingi,.. Walianza wazazi kumkataa rahim kwasababu alikuwa ni kijana wa starehe na mtoto wao ni mcha mungu, hivyo hawakutaka urafiki huo uendelee, na kipindi hicho rahim alikuwa anampenda zena kwa matamanio tu, yaani alikuwa apite kisha amuache, lakini kadri siku zilivyozidi kwenda ndipo mapenzi yao yakaongezeka mara dufu, na kujikuta anampenda kwelikweli,.. Lakini kumbe sio rahim tu kumpenda zena, bali hata zena alitokea kumpenda rahim, yaani zena anakwambia hajawahi kumpenda hata shekh au ostadh, lakini alijikuta tu anampenda kijana wa kihuni, sharobaro la mjini lisiojua hata herufi moja ya Qur-aan tukufu,



    Zena alipambana mpaka kuhakikisha rahim anakuwa mcha mungu, na yote hio ni upende, na alifanikiwa kumfanya rahim kurudi katika njia ya Mwenyezi Mungu,... Lakini licha ya kujitahidi huko, zena ana rafiki mnafiki ambae anampenda rahim kivyovyote vile, yaani fadhila yupo tayari hata kuwa mke wa pili ilimradi tu aolewe na rahim,... Fadhila alifanya vituko vingi sana lakini hakufanikiwa, sasa leo kaja na hili jioyaaaaa



    "Afu nadhani unazijua sunna za mtu.. Alioa wake zaidi ya mmoja... Nafurahi kuwa mke wa pili kwenye familia yenu"



    Aliongea fadhila huku nyuma minah akaanza kucheka kwa umbea...

    "heheheheheeeeee haaaaaloooooooo, Meseji sent hiooooooooooooo"



    Minah alikuwa ni zaidi ya mnafiki katika swala hilo,...

    "fadhila, hivi unasema hio mimba ni ya nani"

    Aliuliza zena huku machozi yakimtoka, yaani zena hasira zake ni kulia tu

    "muulize rahim sio mimi"

    "wewe fadhila wewe.. Acha ujinga wako huo.. Acha kumwongopea mwenzio"

    Aliongea rahim huku hasira zikimpanda kwa kasi...

    "rahim, sasa unabisha nini??... Wewe hujanigusa wewe.."

    Rahim ni mtoto wa kiume na hapendi ugomvi wa aina yeyote ile, wakati huo zena ni kulia tu mana rafiki yake kipenzi ndio leo anakuja kuwa adui yake kisa ni mwanaume tu...

    "naomba hapa hapa tugeuze twende hotelini tukayamalize"

    Aliongea rahim huku zena akikataa, mana rahim kwenda kuyamaliza huko ni jambo la kweli,...

    "rahim mpenzi wangu... Kumbe kweli mimba ni yako"

    Aliingea zena huku machozi yakimtoka kama maji

    "zena... Sio kweli, mimi nakumbuka mpaka tarehe alionibaka huyu bwana haramu... Ni siku ile mimi nimesimama na wewe pale tena uliniruhusu kunywa pombe ili niweze kukutaamkia nakupenda, mana nilikuwa naona aibu kama sijanywa pombe... Ulivyo ondoka tu, huyu ndio akaja kunichukuwa, na sikujua kama ni yeye na ndio mana kuna siku nilikuja kukuropokea pale kwenu lakini ukawa hunielewi... Na kutoka siku ile mpaka leo yapata miezi mitatu na siku za kutosha.. Lakini muone huyu kharamu la dampo anasema ina miezi miwili, hebu imagine miezi miwili iliyopita mimi nilikuwa nimesha acha pombe,.. Maana yake nina akili zangu timamu.. Sasa hio mimba nimempaje kwamfano yani"



    Sasa zena kufikiria vizuri akagundua mbona ni kweli, huenda fadhila ana wivu wake tu wa kimapenzi

    "naweza kuingiza hasira ikawa hasara"

    Zena alijisemea katika moyo wake, kuwa akiweka hasira zitakuja kuzaa hasara,... Hivyo alikubali kwenda hotelini kuyamaliza na fadhila,.. Na kitu anachotaka fadhila huenda ni pesa tu,



    Walifika hotelini watu wanne, fadhila na rafiki yake minah, rahim na mpenzi wake ambaye ni zena,...

    "fadhila, mimi ni mtoto wa kiume, kwa sasa naijua dini vilivyo, na sitaki malumbano na mtu haswa wewe... Ila leo nataka uniambie unataka nini kwangu, mana nina uhakika wa asilimia mia hio mimba sio yakwangu"

    Aliongea rahim kwa upole wa hali ya juu sana,... Sasa hata minah nae anaanza kutia mashaka, mana mtu ambaye ana imani ya dini, hawezi kuikataa mimba endapo amejua ni yake, sasa minah anashangaa mbona rahim anazidi kukataa tu,..

    "sikiliza rahim, mimi shida yangu uilee hii mimba.. Na baada ya kujifungua nataka niwe mkeo"

    Aliongea fadhila huku akiamsha mikono juu juu kama pembe za swala, na aliongea kuwa baada ya kujifungua ndio aolewe, kwasababu sheria ya dini ya kiislamu haruhusiwi kufunga ndoa na mwanamke mja mzito hairuhusiwi, hivyo hata fadhila analijua hilo na ndio mana kasema akijifungua tu aolewe... Awe mke wa rahim rasmi,...

    "fadhila, taja kiasi chochote cha pesa, mimi nitakupa, lakini sio kunipa mzigo ambao sio wakwangu, au hata kuilea nipo tayari, lakini useme tu sio yangu"

    Aliongea rahim huku rafiki yake fadhila ambaye ni minah, anazidi kushangaa, ina maana rahim kama mimba ni yake kwanini akubali kuilea ilimradi tu aseme sio yake... Munah alijua fadhila anamchomekea kaka wa watu,..

    "sitaki pesa zako.. Shida yangu uwe mume wangu...... Afu wewe zena.. Sasa sio rafiki tena... Mimi ni mke mwenzio, hivyo jishaueeeeeeee, lakini ujue mimi nitakuwa mke wa pili kwa mume wetu"

    Aliongea fadhila kisha akaondoka zake yeye na rafiki yake minah.... Sasa huku hotelini alipobaki zena na rahim, maskini zena ni kulia tu hana hata la kuongea,... Hata rahim hajui amwambie nini,...

    "zena?... Samahani sana kwa hilo"

    "kwahio umekubali si ndio?.. Kwanini usingeniambia kama umeshampa mimba, na sheria ya dini huwezi kutangulia kuoa mwanamke ambaye hajashika mimba, maana yake mimi ndio niwe mke wa pili... Rahim jamani Kwanini lakini"

    Zena aliongea sana kumaanisha kuwa yeye atakuwa mke wa pili badala ya kuwa wakwanza....







     





    Yaani kwamfano mwanaume ana wachumba wawili ambao bado hajawaoa kama hivi hapa kwa rahim, sasa kati ya wawili hao mmoja akapata uja uzito,... Kwahio kisheria unatakiwa kuanza kumuoa yule mwenye familia, afu yule ambaye hana familia yaani hajapata ujauzito ndio aje kuwa mke wa pili,... Hivyo zena ana uhakika wa hilo japo rahim ana uhakika kuwa ujauzito ule sio wakwake, japo kweli alishalala na fadhila na sii kwa hiari yake...

    "rahim... Yaani fadhila awe mke mkubwa kwangu"

    Aliongea zena huku akilia sana, akikumbuka tabu alizopata na rahim kumfanya aache pombe ili aje kuwa mume wake, eti leo anakuwa mke wa pili, mana hairuhusiwi yeye zena kuolewa ingali hana ujauzito, yaani haina maana kuwa hapati mimba, ila ni sheria ya dini ndivyo inavyosema, hata kama una wachumba wanne na unataka kuwaoa wote,.. Hivyo mmoja wao akipata ujauzito, basi huyo huyo ndio wa kwanza kumuoa, kama umekubaliana na ujauzito huo,...

    "nijibu rahim... Ni kweli sio yako.. Sema basi ni yako au sio yako"

    Uzuri ni kwamba zena ana busara, hivyo kuna mahari anakuwa mpole wakati wote, hasa sehemu kama hizi, hua anamtanguliza mungu kwanza..

    "sasa ili uamini kuwa ile mimba sio yakwangu... Wiki hii nafunga ndoa na wewe... Kwasababu hata nikikwambia hutoniamini,... Ngoja nipige simu kwa mama alijue mapemaaa"



    Rahim alitoa simu mfukoni na kutaka kumpigia mama yake, ili kama ni mipango ifanyike,

    "kwahio una uhakika sio kiumbe chako kile"

    "yaani asilimia elfu moja.. Sio kiume changu kile na ndio mana sina wasiwasi juu ya hilo zena"

    Rahim alipopiga simu aliambiwa simu aliopiga iko bize, inaongea na mtu...

    "iko bize.... Sasa sikia zena.. Naomba swala hili wazazi wako wasilijue, mana si unawajua walivyo??... Hili tulimalize wenyewe"

    Zena hilo sio tatizo kwake, Basi waliondoka kila mmoja akaenda nyumbani kwao... Mana bado ni wachumba wazuri tu....



    Sasa huku Arusha kwa akina rahim, mama yake alikuwa akigombezwa na mumewe kwa kitendo cha rahim kutorudi arusha kwa ajili ya masomo, na wakati huo baba yupo dubai, na hapo anagombezwa kwa njia ya simu na ndio maana rahim alipopiga aliambiwa simu aliopiga ipo bize

    "wewe upo Tanzania, lakini nashangaa mtoto haendelei na masomo kwanini... Ina maana mimi niache biashara zangu nije huko kumwambia rahim aende shule"

    "baba jamali, lakini si unamjua mtoto wako alivyo jeuri, na tumemlea wenyewe vibaya,.. Sasa mbona wanipa lawama"

    "sitaki kusikia maneno hayo... Nataka nisikie rahim yupo shule,.. Fanya ufanyalo mtoto wangu asome.. Alaaaa... Nimeshalipia shilingi milioni 5 za kumalizia shule.. Leo unaleta mchezo mchezo... Mtume jamali akamlete haraka, tena ikiwezekana leo leo hii"

    "sawa mume wangu... Wacha nimuite jamali akamchukuwe"

    Simu ilikata, mama presha juu, mtoto ni wao wote lakini anapelekeshwa ile mbaya,... Baba anajua rahim ndio jembe lake, sasa asiposoma itakuwaje kuhusu mali zilizopo nje ya nchi.... Sasa mama alipokata simu alikutana na missed call ya rahim.. Mama aliamua kumpigia mtoto wake

    "haloo... Rahim??.... Mshenzi wewe.. Kwanini unapenda mimi nigombezwe na baba yako... Hebu Rudi haraka huku, umeshapona muda mrefu kwanini umechelewa shule zimefunguliwa muda mrefu"

    Mama alianza kumfokea mtoto wake, na mama hajui kama rahim kwa sasa yupo katika hali gani, mana mara ya mwisho alimuacha kule hospitali, hivyo walikuwa wakiwasiliana kwa simu tu, na pia anajua ugonjwa wa rahim ni ili ache pombe, na mama anajua rahim hawezi kuacha pombe, hivyo mama hajui swala hilo japo anapoongea nae, hua rafudhi ya rahim imebadilika kwa kiasi kikubwa sana...

    "mama.. Shule imeshafunguliwa muda mrefu sana, yapata miezi mitatu sasa toka ifunguliwe... Afu sasa mama, hilo sio jambo zito sana.. Kubwa zaidi ni kwamba, mimi nataka nioe wiki hii.. Na ndio mana nilikupigia simu"

    "Ati Unasemaje we kiumbe?.. Hebu rudia sijasikia vizuri"

    "nataka nioe"

    "ivi una akili wewe? Haya na ukioa shule unamwachia nani"

    "mama, sasa shule imebaki miezi mitatu tu nimalizi chuo... Mimi sioni kama ina maana kwangu"

    Aliingea rahim bila kujua muda sio mrefu mama yake kagombezwa kwa swala hilo hilo analokataa rahim.. Lakini mama anajua kweli mwanae anastahili kuoa, na anajua rahim ana mchumba huku aitwae shakira

    "sasa, mimi ninachokuomba mwanangu, naomba uje uendelee na shule kwanza, na kama ni kuoa, ukimaliza tu, shakira wako yupo haendi mahari"

    "unasemaje mama"

    "nasema, shakira wako yupo.. Tena anakujaga kila siku hapa nyumbani.. Yaani sasa hivi kawa mwanamke bora sana, nimempenda bure"

    "eeti eee??.... Mama??"

    "nini tena"

    "uyo shakira uyo.... Mpe jamali.. Si unataka awepo kwenye familia yetu??, sasa mpe jamali anamfaa sana huyo"

    Rahim aliongea neno lililomuuzi mama yake, yaani mama achague mke kwa ajili ya rahim leo anaambiwa ampe mtu mwingine, Kiukweli rahim kila mahari alikuwa mpole lakini sio kwa kuchaguliwa mke,....

    "unasemaje we mshenzi.... Ivi rahim tanga imekupa wazimu eee??... Sasa utarudi Arusha taka usitake.. Mshenzi wewe huezi chezea akili yangu kiasi hiki"

    Mama aliongea kwa hasira huku akitaka kukata simu, lakini kabla hajakata, rahim aliingea neno

    "mama... Huku tanga, nina mchumba, tena ni bora kuliko unavyofikiria,.. Yaani kwa ubora wa shakira kwa zena anaingia mara elfu moja... Hivyo shakira sio chaguo langu"

    Mama kasikia mpaka jina la mchumba wa rahim huko Tanga...



    "huyo zena? Utajiri wao unasoma bilioni ngapi benki... Na nje ya nchi wana makampuni mangapi?"

    Mama alimuuliza mtoto wake, swali liliomuweka rahim kama sekunde kadhaa hivi na kujibu...

    "mama... Una maana gani kusema hivyo"

    "sikiliza rahim mwanangu.... Hatukatai wewe kuoa... Lakini baba yako na hata mimi hatutaki kusikia unaoa mwanamke wa kimasikini, sitaki uniletee kapuku ndani ya nyumba yangu..... Na nitamwambia baba yako, kuwa unataka kuoa mwanamke omba omba,... Afu si unamjua baba yako vizuri??... Sasa ili huyo nani sijui zena, ili aendelee kuishi katika hii dunia na huo umasikini wake... Ni lazima uachane nae, laa sivyo utahudhuria mazishi yake"









    Mahusiano yenye misukosuko ni kama haya, yaani hakuna penye unafuu hata kidogo, ukigeuka kwa wazazi wa zena, wao ni wafuata dini, rahim kabadilika kwa uwezo wa zena, leo hii anataka kuoa, wazazi wa rahim nao hawataki mwanamke masikini,.. Yaani ni tabu juu ya tabu, lakini mwamuzi mkuu ni rahim...



    Sasa mama baada ya kuongea hivyo kuwa, asipoachana na zena, ni kwamba uhai wa zena utakuwa matatani kwasababu wazazi wa rahim hawataki mtoto wao ateseke na haya maisha, hivyo hawataki kumuona na mschana wa kimasikini hata kidogo,...

    Sasa mama rahim alipomaliza kuongea hivyo alikata simu, kisha akampigia jamali, ambae nae ni mtoto wake sema ni mtoto wa kwanza katika familia hio,...

    "jamali??"

    "naam mama"

    "naomba uende Tanga ukamlete rahim, asiniletee ujinga wake mimi"

    "sawa mama... Lakini umeshamjulisha kuwa nakwenda kumchukuwa"

    "atajua huko huko jamali.. We nenda kamchukue aje aende shule, mana nashangaa ananieleza mambo ya kuoa tena"

    "anasemaje huyo bwege kweli.. Ngoja nifike huko nitamzaba mabao yule"

    "hebu nenda Airport mara moja ukamlete leo leo hii"

    Simu ilikatwa, kisha jamali kuanza mchakato wa kwenda tanga, mana jamali alikuwa ofisini kwao kikazi, sasa wacha akamchukue rahim...



    Wakati huo rahim kakaa sebuleni mawazo mengi yakimzonga kijana wa watu,.. Kila kona ya uhusiano wao ni tabu, sio wazazi sio marafiki... Na wakati huo ilikuwa yapata mida ya saa 8 za mchana,.. Hadija kaandaa chakula, rahim alikula lakini kama vile chakula hakipiti katika koromeo lake,... Na kweli anamjua baba yake akiamua kumfuatilia mtu, yaani atahakikisha mpaka anapata jibu sahihi juu ya mtu huyo......



    Kama unavyoujua usafiri wa ndege ulivyo, ndege sio basi.... Kwani ilipotimu saa kumi za jioni jamali keshafika tanga, na sasa kachukuwa tax kuelekea katika mitaa husika au kwao... Rahim wakati huo alikuwa akitoka msikitini kuswali swala ya saa kumi alasiri,... Tena alikuwa sambamba na zena, na hapo zena hajui chochote kuhusu uhusiano wao na hatujajua rahim kaamua nini kwa hilo,... Walikuwa wakifurahia uhusiano wao, zena kaamua kupotezea swala la fadhila kwani rahim kuamua kumuoa ndani ya wiki hii, basi ni dhahiri kuwa ule ujauzito sio wake,.. Rahim alikuwa akiongea huku akicheka lakini kila akimuangalia zena hapati picha itakuwaje,... Zena kila siku lazima aende msikitini na rahim.. Na mwanamke anaruhusiwa kuswali nyumbani kwa hizi swala za kawaida kasoro Ijumaa tu, hivyo zena kwenda msikitini kila saa, ni kwasababu ya kumpa rahim sapoti, mana akimuacha itakuwa sio vizuri,.. Mwanaume ndio anatakiwa akaswalie msikitini, ila mwanamke hata nyumbani ruksa,.. Na pia mwanaume nyumbani ruksa lakini kama nafasi ipo, basi we jongea msikitini... Rahim na zena walifika mahali wakakaa, ila rahim ana maana yake kukaa hapo, kuna kitu alitaka kumwambia zena, na hajui kama kitamuumiza kiasi gani...

    "zena??"

    "abee"

    "Nakupenda sana sana zena... Ila siamini kama naniii"

    Zena alianza kupatwa na wasiwasi juu ya maneno ya rahim,...

    "huamini nini"

    "wazazi wangu"

    "yaani huwaamini wazazi wako? au una maana gani"

    "zena.... Natamani sana uwe mk.."

    Lakini sasa kabla hajamaliza, ghafla kuna tax ilisimama mbele yao, kumbe ni jamali alikuwa anapita tu, hivyo kawaona ikabidi aamrishe tax isimame hapo....



    Jamali kashuka kwenye tax, anafikicha macho, kana kwamba haoni Vizuriiiiiiiiii au anaota,...

    Jamali alishangaa kumuona mdogo wake akiwa kama shekhe,....

    "ivi naota au"

    Aliongea jamali baada ya kumuona rahim akiwa amependeza katika vazi la kanzu, tena sio kanzu tu, na swala tano juu, kwani hata sigda ilishaanza kutoka kwa mbali...

    Jamali alitoa simu yake, na kumuita yule dereva wa tax...

    "eti ndugu... Hii sura hiii, unaweza kuifananisha na ile"

    Alimuonyesha picha iliopo kwenye simu yake...

    "unamaanisha huyu kwenye picha ndio yule... Mbona hapa ni sharobaro"

    "ndio nakuuliza.. Ili nisije kukosea njia"

    "ni yeye kweli"

    Jamali akamgeukia rahim na kujaribu kumuita kama ndio yeye

    "rahim??"

    "naam kaka"

    "haya kipi kimekukuta ndugu yangu"

    "aahh kwanza as Salaam Aleykum warahmatullah wabarakatuh"

    Jamali kabaki kutoa macho tu wala hajui aitikie vipi...

    "mmhhh haya safi tu.... Ivi we rahim wewe, ni wewe kweliiii au naota"

    "kaka, mi nadhani hakuna ndoto za mchana huu... Afu mbona umevaa mikofia ya ajabu ajabu kaka angu"

    "ati Unasemaje wewe???... Wewe hii si ndio ulinichagulia mwenyewe hiii??... Hakiyamungu wewe sio rahim wewe.... Dereva?? Endesha gari Twende nyumbani... Hapa nimekosea sio ndugu yangu huyu"

    Jamali alipanda gari kisha akaondoka zake...

    "jamani rahim huyu si kaka yako huyu"

    Aliuliza zena huku nao wakiondoka, na hata lile walilotaka kuongea wakaliacha

    "ndio, ni kaka yangu"

    "sasa mbona hakujui tena"

    "ni kwasababu nimevaa kanzu"

    "heeeeeeee ni hilo tu"

    "ndio"







     





    Sasa jamali alivyofika nyumbani, hadija alifurahi sana kumuona mpenzi wake, mana walikuwa wakiwasiliana kwa simu tu, sasa leo kaja...

    "hebu tulia kwanza hadija.... Naomba niitie rahim aje hapa"

    Aliongea jamali huku bibi akija na kicheko, si unajua mambo ya mabibi tena,...

    "heheheheheee... Halooooo... Bado wewe tu"

    "bibi unacheka nini?... Kwanza shkamoo"

    "Marahaba mjukuu wangu... Furaha nilionayo bado wewe"

    "mimi nifanyeje sasa"

    "sasa hivi rahim ni ostadh babu weye, yaani sasa hivi anasoma Qur-aan kama kichaa"

    "ina maana yule niliekutana nae kule kumbe ni yeye kweli"

    Alipo ongea hivyo mara sauti ilisikika mlangoni,

    "ndio mimi... Nimeamua kubadirika kaka.... Starehe hazina mwisho ila maisha yako yana mwisho... Jiulize ukifa sasa hivi kipi ulichokiandaa kwa mungu wako....mimi ndio rahim mdogo wako yule yule"

    Aliongea rahim huku akikaa katika kochi, yaani hata kaa yake imebadilika sio ile ya kujitupa kwenye sofa kama zamani, sasa kawa mstaarabu mno..

    "bibi... Ivi huyu ni rahim kweli"

    "kwani we wamuona ni nani"

    "ok sawa.. Yote tisa... Kumi anahitajika kwenda shule, hivyo nataka niondoke nae"

    "weeeeeeee pumbavu zako, ishia hapo hapo... Manataka mkamrudishe hali yake tena... Wewe ungejua kaachaje pombe huyu, usingesubutu kuongea ujinga.. Sasa kama umekuja kwa nia hio naomba urudi mwenyewe, staki shobo na mjukuu wangu sawa eee"

    Bibi wa kitanga nadhani unawajua wakicharuka, utatamani uzikwe mzima mzima kuliko usutwe na bibi yako....

    "lakini bibi, mama ndio kanituma"

    "hata kama... Nasema hapa haondoki mtu"

    "mmmhhh sawa"



    Jamali alitoka nje kabisa na kupiga simu kwa mama yake....

    "mama... Hali niliomkuta nayo rahim huku, yaani hata shekhe kasingiziwa"

    Aliongea jamali huku akizidi kusogea mbali na hio nyumba ili bibi au mtu mwingine asisikie maongezi hayo,...

    "kwani umemkutaje... Jamali sitaki ujinga... Hebu njoeni"

    "mama.... Sio rahim tu kukataa, hata bibi kakataa rahim aje huko"

    "shenzi kabisa... Ngoja nije mwenyewe huko... Na hicho kijimwanmke chake kitanitambua mimi ni nani"

    "sasa mama.. Ngoja nikupe nji... Nitawaambia waje kukupokea Airport, afu wewe njoo na wanajeshi wamkamate hapo hapo Airport muondoke,.. Yaani hata huku kwa bibi usifike"

    "yes... Jamali una mawazo mazuri wewe... Kesho saa nne nakuja... Waambie waje na huyo kimada wake"

    "sawa mama kazi yote niachie mimi... Rahim ni mdogo wangu hawezi tuumiza kichwa"



    KESHO YAKE MIDA YA SAA MBILI ZA ASUBUHI....



    Rahim alikwenda nyumbani kwa akina zena,...

    "heeee rahim, asubuhi hii vipi... Afu umeswali swala ya subuhi kweli wewe"

    "ndio.. Nitaachaje kwa mfano"

    "safi sana napenda sana tabia yako rahim"

    "mi pia...... Sasa zena... Leo naomba uvalie hijabu lako saafi kabisa.. Nami navaa ile kanzu ya bluu bahari ulionichaguliaga"

    Zena alipata wasiwasi, akajua labda ndoa imeshafika siku yake nini

    "kwani kuna nini rahim"

    "nataka twende tukampokee mama.. Anakuja leo"

    Yaani zena alifurahi kusikia mama yake rahim anakuja, na wanatakiwa kwenda kumpokea Airport... Zena alitamani hio saa nne ifike sasa hivi, mana hamjui mama mkwe wake,.. Na zena wakati wote huo anajua mama yake rahim anajua kuwa rahim ana mchumba aitwae zena.. Hivyo hana wasiwasi na hilo.... Hata rahim pia hana wasiwasi na hilo, mana hajui mipango ya wazazi wake ni ipi...



    Baada ya lisaa limoja kupita rahim na zena walisha jiandaa vizuri sana, rahim kavalia kanzu yake kisha akatupia na koti la suti kwa juu, bila kusahau kitambaa cha kanzu, na kofia yake... Tena kwa mbwembwe zaidi akashika kifimbo (bakora) mkononi, yaani ni bonge la shekhe sio ostadh tena...... Kama kawaida rahim na zena walipanda gari yao hio vogue ya gharama kubwa... Na jamali yeye alikataa kwenda Airport mana anajua ishu nzima itakayofanyika kule Airport,.. Zena ana furaha bila kujua nini kitatokea mbele yake,.. Kila mtu kapendeza kwa mavazi ya kujisitiri na miili yao.. Haswa zena,.. Tena zena hajataka kuvaa nikabu, kale kakitambaa ka usoni kama ninja, ili mama mkwe amjue kwa urahisi..



    Saa nne kamili rahim ndani ya airport na zena wake,... Kwa juu ndege husika aliopanda mama yake rahim ndio hio yaja... Rahim alishuka katika gari na zena nae alishuka katika gari,.. Sasa wakawa wanaelekea mapokezi ili kumsubiri mama... Ndege ndio inaanza kushusha watu,... Kweli mama yake rahim alikuwemo katika ndege hio, lakini sasa aliongozana na wanaume wa shoka kama watano hivi,... Na yote hio ni kuondoka na rahim...

    "jamali... Nikishaondoka nae nitakupigia simu uje ulichukue hilo gari aliokuja nalo, sawa"

    "sawa mama"

    Mama alimtaarifu jamali ili gari hio isije kupotelea Airport... Kweli rahim kamwona mama yake yulee, lakini watu aliokuja nao ghafla walipotea,.. Mana mama aliwaambia kuwa wakiona kasimama na kijana mdogo na mschana, basi ndio huyo, hivyo inaonekana hao jamaa wamemzunguka rahim japo bado hawajamjua, na hata mama bado hajamwona mwanae ila rahim keshamwona mama yake.. Rahim alisimama usawa wa mama yake anavyokuja..

    "zena??"

    "abeee"

    "unamjua mama yangu"

    "hapana simjui"

    "ndio huyo anaekuja hapo mbele"

    Sasa zena kuangalia, alijikuta anakunja uso...

    "rahim, huyu ndio mama yako"

    "ndio... Kwani vipi"

    "mbona kavaa sketi fupi hivyo"

    Zena aliongea baada ya kumwona mama yake rahim kavaa sketi fupi..

    "maamuzi yake"

    "hebu angalia pembeni rahim,. Usitoe macho mbele ya mama yako"

    Zena alimtaka rahim asimwangalie mama yake, kwakuwa alivaa sketi fupi,... Sasa mama alikuwa hajawaona,... Alishangaa usawa wake kuna Waislamu wawili wamesimama kama mtu na mkewe.. Na wakati huo rahim kaangalia chini afu zena ndio wa kwanza kutoa salamu kwa mama yake rahim



    "As Salaam Aleykum mama"

    Alisalimia zena huku akimpa mkono mama yake rahim,... Wakati huo rahim ndio anainua kichwa chake na kusema...

    "mama... Huyu ndio mchumba wangu.. Sasa mbona huupokei mkono wake"

    Aliongea rahim huku mama kashikwa na butwaa kwa jinsi alivyokuwa anamuona mtoto wake..... Masikini zena hajachoka kuunyoosha mkono wake, japo haukuwa na majibu ya kupokelewa na mama mkwe.... Na wakati huo sasa,.. Yale majamaa ndio yanakuja kwa nyuma nyuma taaratibu ili kumkamata rahim,... Sasa Mbaya zaidi kumbe wamempangia zena mabaya pale watakapo fanikiwa kuondoka na rahim wao....







    Ujio wa mama rahim sio wa kwenda kwa wakwe, bali alikuja kumchukuwa mtoto wake ili aende shule, mana baba yake anamfokea sana kwa rahim kuwepo Tanga huku shule zikiwa zimefunguliwa,... Na rahim ni mwanafunzi mzuri sana sema pombe ndizo zilizomharibu, na huu ndio ulikuwa mwaka wake wa mwisho ikiwa ni mwezi wa 9 sasa yaani ameshapitwa na masomo sana tu,....



    Sasa leo mama kaja kumchukuwa mwenyewe, na nia yake ni kumchukua hapo hapo Airport, na pia hakuja mwenyewe kaja na vijana wa nguvu kama watano hivi, na vijana hao tayari wamesha wazunguka akina rahim baada ya mama yake kusimama nao...



    Wakati huo zena kanyoosha mkono kumsalimia mama mkwe,.. Lakini mama rahim alikuwa kama hauoni mkono huo, yaani macho yake yalikuwa kwa rahim jinsi alivyobadirika....

    "ivi ni wewe rahim mwanangu ninaekujua au naota"

    "ni mimi mama...... Mama lakini zena anakusalimia"

    Aliongea rahim mana zena hakuchoka kunyoosha mkono kwa mama mkwe japo mama mkwe kama vile hauoni,..

    "nani kasababisha kuwa hivyo"

    Aliuliza mama rahim huku rahim akinyoosha kidole kwa zena, kumaanisha kuwa aliefanya yeye kuwa mtu wa dini, ni zena...



    Huezi amini mama aliona hata kuupokea ule mkono wa zena, bado haitoshi, mana kitu alichokifanya ni kikubwa mno.... Huezi Amini mama rahim alimkumbatia kabisa zena, yaani hata ule mkono aliona ni mdogo sana,... Mama hata machozi yalimtoka,...

    "mwanangu.. Ahsante sana kwa kunibadilishia mtoto wangu.... Sio kuwa nilikuwa sitaki uwe hivyo, ila upendo wetu kwako ulizidi mpaka tukawa tunakuacha sasa ufanye utakalo"

    Aliongea mama rahim huku akiwa kamkumbatia zena,... Sasa wale jamaa nao ndio walikuwa wanakaribia ili wamkamate rahim, lakini mama aliwazuia

    "jamani? Basi.... Nitawalipa pesa zenu, lakini basi msikamate mtu tena"

    Aliongea mama rahim huku akitoa pochi yake na kutoa burungutu la pesa na kuwapa wale majamaa waliokuwa tayari kufanya kazi ya kumkamata rahim.... Sasa wakati mama anatoa pesa, huku zena alitoa kitenge ambacho alikuwa nacho kwenye mkoba wake,.... Mama rahim alishangaa anafungwa kanga,.. Kana kwamba nguo aliovaa ni fupi mno.. Machozi yalizidi kumtoka huku akizidi kuingiwa na imani ya hutuma..



    "Ahsante mwanangu"

    Mama rahim alimshukuru zena kwa kumfunga kanga,... Sasa wale jamaa wakatafuta usafiri wao, na kurudi arusha... Ila mama Safari ya kurudi arusha ilikufa, na alikuwa hana nia ya kubaki tanga, lakini ilimghalimu aendelee kubaki...



    Wakati huo huku nyumbani bibi anamuulizia rahim kwa jamali

    "we jamali mdogo wako kaenda wapi"

    Aliuliza bibi mzungu huku akiwa na wasiwasi,...

    "aaahhhhh kwa sasa, nadhani atakuwa anakaribia kufika arusha"

    Bibi alitoa macho,

    "Unasemaje wewe??... Kaenda kufanya nini"

    "bibiiiii.... Yule bado ni wakusoma... Nashangaa mnakaa nae tu huku"

    "mungu wangu mjukuu wangu anakwenda kurudia pombe tena"

    "bibi... Hata mimi hapa Nasubiri tu simu ya mama aniambie nikachukue gari Airport"

    "kwahio mama yako nae alikuja"

    "tena kaja na wanajeshi ili wamkamate rahim"

    "mbona mimi sijui, na hamjaniambia"

    "sasa we si hutaki aende utaambiwa vip"



    Mara ghafla wanasikia sauti ya honi iliopiga nje ya geti,...

    Jamali alistuka, ina maana mama yake wamemshindwa kumkamata?? Mana alitegemea kupata simu ya kwenda kuchukuwa gari Airport,..

    Jamali haraka haraka anakwenda kufungua geti,.. Alishangaa kumwona mama yake, akiwemo rahim na zena..

    Jamali kashindwa kuelewa kwanini imekuwa hivyo,... Bibi alifurahi sana kumwona rahim karudi, mana tayari bibi keshaingiwa na wasiwasi juu ya mjukuu wake, kana kwamba kumtengeneza kote huko leo anarudi kuanza tena...



    Waliingia ndani lakini jamali bado haamini, kama rahim karudi tena hapa,...

    "shkamoo mama"

    Mama rahim alimsalimia mama mkwe wake, kisha wakaingia ndani...

    Walipokaa tu, jamali kaja na maswali yake

    "mama vipi tena... Huyu mtu shule zimefunguliwa tayari"

    Jamali aliongea hayo kwa kumwambia mama yake

    "jamali mwanangu.... Kweli nimejiskia raha sana rahim kuwa katika hali hii... Binafsi hata baba yako akilijua hili, litamfurahisha sana"

    "kwahio mama, Unasemaje kuhusu shule"

    Aliuliza jamali lakini mama hakumjibu,... Mama rahim alimgeukia mama mkwe wake na kumuuliza...

    "mama.... Rahim anatakiwa kwenda shule... Unaonaje nikaonana na wazazi wa huyu mschana tukaongea"

    Zena alifurahi sana kusikia hivyo,....

    "sawa nitakupeleka ukawaone"

    "rahim.... Nataka uoe, lakini Tuende arusha ukamalizie masomo yako huku ukiwa na mkeo, hilo nimeliona ni sahihi, kwasababu baba yako anagomba san kuhusu shule"

    Rahim kusikia aoe, alitamani hata muda huo huo

    "mama... Shakira je"

    Rahim alimuuliza mama yake kama mtego tu

    "hapana rahim.... Huyu huyu anakufaa"

    "lakini ni masikini hawa"

    "sitaki kujua...."

    Rahim aliongea hivyo kwa maana asije wakaenda huko wakakuta maisha ya ajabu wakaanza kuleta mambo ya Kiswahili...



    Jioni ilipofika, familia yote ya akina rahim, ilikwenda kwa akina zena,.. Na wakati huo na familia ya akina zena nayo yote ilikuwepo, mana waliambiwa kuwa kuna ugeni utakuja jioni,... Hivyo maandalizi ya kuwapokea wageni yalikuwepo,.. Mama yake rahim alijua anakwenda kwa wakwe wenzie, hivyo alitakiwa kuvaa kiheshima... Rahim hata yeye leo anamshangaa mama yake kavalia nguo ndefu ndefu,.. Hata jamali haamini kama leo mama yake kavaa hivyo....







     





    Maongezi yalianza... Baina ya wazee wazima, wazazi akina kaka.....

    "jamani wazazi wenzangu... Mtoto wetu kapenda kwenu... Hivyo anataka jiko... Na kwakuwa wanapendana,... Sioni kama kuna tabu"

    Aliongea bibi wakati huo bibi zake na zena pia wapo na ndio waliokuwa wanaongea wenyewe,...

    "sisi hatuna shaka... Ni nyinyi tu kukubaliana na matakwa yetu"

    Aliingea bibi yake zena, huku rahim na zena wanaomba mungu tu wakubaliane,... Mana wao hawaruhusiwi kuongea ispokuwa zena ataulizwa..

    "matakwa gani tena jamani... Tuwaozesheni watoto wakayaanze yakwao"

    Aliongea bibi yake rahim huku wakiendelea kunywa chai, si unajua vikao vya tanga vilivyo...

    "mtoto wetu katunzwa haswa... Ana kila kitu yule, hamjui mwanaume toka kuzaliwa kwake"

    Mama rahim alitoa macho kuskia zena alikuwa hamjui mwanaume toka kuzaliwa kwake,...

    "mnasemaje... Ivi karne hiii mabinti hao wapo kweli"

    Aliuliza mama yake rahim huku akishangaa kwa kauli hizo..

    "haaaaa mbona huku tanga wapo wengi sana... Kiukweli kwa mjini huko sidhani lakini huku tanga ndani ndani wapo weengi mno"

    Aliongea bibi yake zena huku akisubiri majibu toka kwa mume, yaani wazazi wa mume... Lakini mama hajaridhika ikabidi amuangalie mtoto wake amuulize.... Kwa macho macho, kuwa ni kweli zena ni bikra...

    Rahim alitikisa kichwa kuashiria hajawahi kumjua... Lakini pia bibi yake zena hakutaka kudhibitisha sana, hivyo alimuuliza zena kuwa

    "zena... Uko sawa au umeshaharibu"

    "bibi, nipo sawa... Fanyeni mnachojua tu ila mimi na rahim tunajuana vizuri"

    Aliongea zena, huku bibi yake zena akimrudia bibi yake rahim

    "unasikia huko.. Vijana wenyewe wanajuana wapo vizuri... Sasa kazi ni kwenu kwa kile tunachokitaka"

    "haya semeni mnataka nini"

    Hapo bibi yake zena akatulia na kumwachia baba mwenye mtoto wa kike..

    "kwa mimi... Nataka ng'ombe saba madume manne na majike matatu.. Hapo mimi nimemaliza"

    Alipomaliza baba, akaja mama yake zena

    "Kiukweli kwa mimi mama mtu... Ninachokitaka kwenu, naomba muishi na mtoto wangu vizuri,.. Anakwenda kuwa wenu, hivyo muishi kama mtoto wenu... Hicho ndicho kitu ninachokitaka kwenu"

    Sasa baada ya mama yake zena kuongea hayo... Mama rahim akamjibu kuwa

    "hilo umelipata mama.... Enhee kwa upande wa mabibi na mababu"

    Aliuliza mama zena,... Huku bibi akijiandaa

    "mimi nataka vitenge pea saba, na kanga zangu kama pea tatu... Nataka na hijabu,.. Hivyo tu vinatosha"

    Baada ya bibi kuongea,.. Alifuata babu yake zena,..

    "mimi bwanaaaaaaaaa..... Nataka kondoo wawili ili nichunge chunge kidogo... Nataka bakora... Mana nimezeheka sasa.... Kingine nataka koti... Bila kusahau kilo 50 za sukari.. Kuna baridi jamani"

    Sasa wale wakubwa wote waliisha kutaja matakwa yao, na yote hayo ni kwasababu zena amejitunza usichana wake na ndio maana wana uhuru wa kutaja watakacho... Jamani kujitunza usichana raha kweli,.. Sasa nyie hayeni

    Kaka mtu nae na mdogo mtu nae kila mtu alitaamka kitu akitakacho.... Sasa ikafika zamu ya zena kutaka kitu chochote kwa mume

    "mimi nataka mswahafu tu"

    Baba alitoa macho, mwanae kutaka mswahafu peke yake...

    Lakini baba ikabidi atulie tu mana ni maamuzi yake yeye mwenye kuolewa



    "ok, nadhani mumemaliza mambo yenu,... Sasa uwezekano wa kulipa pesa badala ya hivyo vitu si upo"

    Aliuliza mama rahim, ili kama uwezekano wa kulipa pesa upo, alipe pesa badala ya vitu,.... Familia ikakubali walipwe pesa zao zote, hivyo mahesabu yakapigwa, mama rahim hapo hapo akatoa pesa keshi, huku akisema

    "ndoa, nataka ifungwe kesho... Ili huyu aende shule"



    Kuanzia saa hio maandalizi yalianza,.. Walialikwa watu wengei sana na sehemu ya kufungia ndoa iliandaliwa vizuri sana, mpaka usiku saa nne watu wapo bize,... Kila kitu kilinunuliwa kasoro mavazi ya wana harusi yalikuwa bado,... Familia zote zilikuwa na furaha sana, lakini sasa mama yake rahim hakutaka baba yake rahim alijue hilo, kwasababu lazima ataleta pingamizi... Yaani mama rahim alimpenda zena kwa nusu siku tu, baada ya kumuona mtoto wake amekuwa Muislamu safi, na sababu ya kumrudia mungu ni kwasababu ya zena, hivyo mama alimoenda kwa kumbadirishia mwanae,.... Lakini sasa mbaya zaidi jamali yeye anataka mdogo wake amalize shule kwanza hivyo hajapenda kitendo cha rahim kupewa mke ingali bado ni mwanafunzi,.... Mama yake rahim, na bibi yake rahim, na rahim mwenyewe, simu zao zilikuwa zimezimwa kwa siku hio, ila kasoro jamali, kwani yeye alikuwa na simu ya pembeni tofauti na ile iliozimwa,... Jamali hakupenda mdogo wake aoe kwa wakati huo na istoshe jamali na baba yake vinaivana vizuri,.... Huezi amini usiku huo huo simu kwa baba yake, ambae kwa sasa yupo dubai...

    "haloo dady shkamoo"

    Alisalimia jamali huku akiangaza macho huku na kule ili asije akasikiwa na mmoja wao,....

    "Marahaba, vipi saa hizi"

    Baba yake aliuliza kuna nini muda huu,

    "mzee, huku unapatiwa mkwe"

    "mkwe Kivipi"

    "rahim anaoa kesho"

    "Whaaaaaat?"

    "ndio hivyo mzee... Na kesho saa saba ndoa inafungwa msikitini"

    "hivi huyu mtoto ana akili kweli... Na mama enu nae yupo wapi"

    "mama ndio kipau mbele mzee"

    "pumbavu sana.... Hebu ngoja nimpigie"

    "kazima simu, yaani hii yenyewe hawajui kama nina simu ndogo, mana tumezima wote simu zikawekwa mahali ili wewe usijue"

    "hapana.. Haiwezekani... Mimi nataka mwanangu asome... Yaani nitahakikisha hio ndoa haikamiliki"

    "sasa utafanyeje mzee"

    "kesho nakuja na ndege ya private... Nataka uje Airport na hio gari uje unichukue"

    "sasa watanishtukia wasiponiona mzee"

    "shiiiiit,... Ngaoja nina jamaa wangu hapo Airport nitamwazima gari yake, ila usizime simu.... Mama yako hana akili kabisa huyu"



    Kesho yake sasa mida kama saa tano za asubuhi akina rahim na zena walikuwa ndani, wakiangalia nguo za kufungia ndoa walizoenda kununua muda mfupi uliopita,... Katika viwanja vya ndoa, mashekhe walikuwa wamesha wasili eneo hilo,.. Wana madrasa walikuwa wakifanya yao kwa kupiga vidufu,... Palikuwa hapatoshi, kama unavyojua watu wa tanga kwa harusi usipime.....



    Sasa huku kwa fadhila kaanzisha balaa jipya, baada ya kusikia kuwa leo ndio ndoa ya akina rahim, na yite hio ni kwasababu ya rahim ili kumpa ukweli juu ya ujauzito ule kuwa sio wakwake,...

    "ivi unajua kinachoendelea fadhila"

    Minah alimwambia fadhila kama anajua kuwa rahim anafunga ndoa,...

    "ndio, si zena wanafunga ndoa"

    "sasa kwanini unaangalia tu na wewe ndio unastahili"

    "nastahili kivipi??.."

    "unajua fadhila wewe ni mwana madrasa, lakini hukuwa makini na hilo, ulikuwa bize na mambo mengine huzingatiii... Kisheria mwenye mimba ndio wa kwanza kuolewa kwasababu yeye ndio kaanza kuleta familia.. Sasa unaachaje nafasi kama hio"

    Sasa fadhila kweli ni mwana madrasa lakini swala hilo halijui...

    "unasemaje minah???"

    "we zubaa tu"

    "lakini pia sheria ya dini yetu inasema mwanamke mwenye ujauzito haruhusiwi kuolewa mpaka atakapojifungua"

    "wewe nenda kavuruge tu... Tena pale kuna watu wengi sana, ndio pazuri yaani kila mtu ajue una ujauzito wa rahim... Nenda wewe utapoteza haki yako.. Na sasa kumebakia nusu saa tu ndoa ifungwe"



    Kweli huku kwenye jukwaa, la ndoa wanandoa wakiwa wamependeza mno.. Rahim na kanzu yake ya kifahari, bila kusahau zena alivalia vizuri mpaka raha.... Jamali alikuwa mahali hivi, akampigia baba yake simu kuwa kila kitu kinakwenda kuisha

    "baba... Ndoa inakwenda kufungwa hivyo"

    Aliongea jamali huku akiwa na woga woga kiasi..

    "mbona mimi nimeshafika... Nipo jirani na msikiti mkuu"

    "ati unasemaje?? Tayari upo tanga mzee"

    "yaani hapa naulizia tu hilo jukwaa lipo wapi"

    "baba, jukwaa lipo jirani na msikitini.."

    "basi... Ngoja niulize hapa"

    Simu ilikata huku mzee akitafuta mtu wa kumuuliza....



    Sasa mbaya zaidi mtu anaemuuliza alikuwa ni fadhila aliokuwa na haraka ya kuwahi kuvuruga ndoa isifanyike... Mana yeye akisema tu kuwa ana ujauzito wa rahim, basi ni kweli ndoa itaahirishwa, mana kidini yeye ndio anatakiwa kuanza kuolewa yeye...

    "samahani mwanangu... Eti kwenye huu mtaa kuna kijana anaoa"

    Mzee rashidi au baba yake rahim aliuliza kama vile sio mzaliwa wa eneo hilo, na fadhila yeye hajui kama huyu ndio baba yake na rahim, hilo halijui kabisaa,...

    "ndio.. Ni hapo mbele tu"

    "unaweza ukanielekeza"

    Aliongea mzee ambae ndio baba mzazi wa rahim.. Ila Zena hajui

    "ndio... Twende"

    Fadhila alipanda kwenye gari huku akiwa na hamu ya kuwahi, na ni kweli watawahi mana bado hawajaanza lolote,... Fadhila ndani ya gari, na wote baba yake rahim na fadhila lengo lao ni moja kuistopisha ndoa isifungwe,... Ila sema hawajuani, fadhila anajua huyu mzee ni mualikwa tu... Na huyu mzee anajua huyu dada anamuelekeza tu.. Kumbe nia yao ni moja... Sasa kule jukwaani zena na rahim ndio wanaamshwa kwenye viti vyao, na kila Mtu kashika pete kwa ajili ya kumvisha mwenza wake..... Kwa mbaali gari ya mzee rashidi ilionekana,... Maana yake ni kwamba wameshafika eneo la tukio, na uwezekano wa ndoa kustopishwa ni mkubwa... Mana mzee na fadhila tayari wapo eneo hilo japo hawajuani kuwa lengo lao ni moja tu...







    Lakini sasa mzee alipofika karibu na eneo hilo, alistopisha gari na kuanza Kukasirika,...

    "we mtoto kwanini unanipoteza njia?"

    Fadhila alishangaa kuskia mzee anasema eti kampoteza njia na wakati anaona umati wa watu umejaa katika eneo la tukio,...

    "baba... Hapa ndipo kwenye ndoa ya kijana mmoja hivi"

    "sio hapa... Nipeleke sehemu nyingine"

    "lakini baba, mimi siwezi kwenda sehemu nyingine mana Nilipotoka kufika ni hapa na sio huko... Utanisamehe baba"

    Fadhila aliongea kwa heshima tu huku akishuka katika gari,... Mzee alipiga simu kwa jamali ambae ndie aliempa umbea wote huo....

    "halooo, we jamali, huyo mdogo wako anafungia wapi ndoa"

    Sasa fadhila kusikia jina la jamali, ndio akapata hisia kuwa basi huenda huyu ni baba yake na rahim, mana rahim ana kaka anaeitwa jamali...

    "mzee, ni mtaa ule ule wakwetu, sema ni pembezoni mwa msikiti"

    Mara simu ikakata,... Kumbe jamali keshafumwa na mama yake kuwa anaongea na simu,.... Sasa huku mzee hajui chochote kuhusu kukata kwa simu hio...



    "jamali mwanangu, ina maana humpendi mdogo wako mpaka uongee na baba enu"

    Jamali alikosa cha kuongea mana namba kweli ni ya mzee rashidi,...

    "mama... Rahim bado ni mwanafunzi, na natamani sana amalize chuo kama mimi"

    "sasa kama wazazi wake hawataki kwanini wewe uharibu... Jamali umesahau eee?"

    Aliongeq mama, kana kwamba jamali kuna kitu anatakiwa kukumbuka, na ndio mana mama kasema jamali umesahau,... Kuna jambo zito hapa katikati na halijulikani ni jambo gani

    "basi nisamehe mama angu"



    Sasa huku kwa mzee rashidi,.. Fadhila baada ya kujua kuwa huyu huenda ndio baba yake rahim, alimrudia na kumuuliza....

    "mtoto wako anaitwa rahim"

    Aliongea fadhila huku akitamani aambiwe ndio

    "umeshanipoteza.... Unanileta kwenye ndoa ya watu wa Kiislamu"

    "lakini baba... Mbona hata rahim ni Muislamu"

    "nitokee hapa...."

    "ni kweli baba... Rahim si yule pale anafunga ndoa na yule mwanamke mwingine, afu mimi nina ujauzito wake"

    Mzee akatoa macho kwa kumuangalia fadhila,...

    "unasemaje wewe??... Ati una nini yake"

    "hili ni tumbo lake"

    "ivi nyie mabinti wa huku mna kichaa eee"

    Sasa fadhila aliona kama mzee anampotezea pointi, na kazi yake haitoisha, mana mzee haamini kama kijana wake kazunguukwa na umati wa Kiislamu, Mashehe wakubwa wakubwa,.. Yaani wale watu wakubwa wakubwa katika ngazi za imani ya dini walikuwepo...

    "yule si shekhe ponda yule"

    Alijiuliza mzee rashidi na hapo bado hajaamini kama mtoto wake ndie anaefunga ndoa,... Akijaribu kupiga simu ya jamali, haipatikani tena...



    Sasa fadhila alifika katikati ya watu, na nafasi ya kufanya lolote ilikuwepo, lakini huezi amini roho ilimsuta kana kwamba kuna kitu anakijua yeye mwenyewe katika moyo wake, akaona hili jambo asilifanye yeye, ngoja ambandikie baba yake... Fadhila alirudi mpaka pale mzee alipo akiwa anahaha mwanae anafunga ndoa sehemu gani...

    "baba... Ivi unajua kweli yule ni rahim.. We mwangalie vizuri tu"

    "niache.. Toka hapa"

    Sasa mzee kugeuza macho... Alishangaa kumuona mbona kweli ni rahim mtoto wangu,...

    "mbona ni mtoto wangu yule"

    "ndio yeye... Muwahi ukamzuie si bado anasoma"

    Fadhila alitumia nafasi hio, ili mzee akaharibu badala yake... Na wakati huo rahim ndio anamvisha pete zena huku akifuata maneno ya shekhe ambayo ndio maneno tukufu na yenye uzito ndani ya ndoa yao...



    Mzee kujua kuwa yule ndio mtoto wake,.. Alitoka hapo na kuingia katikati ya watu, akitaka kwenda kustopisha jambo hilo,...



    Sasa huku Airport, kumbe mzee aliomba gari kwa rafiki yake ambae ndio meneja wa hapo Airport, sasa rafiki yake alipatwa na wasiwasi juu ya mzee rashidi mana alichukuwa gari kwa haraka kama vile anakwenda kuuwa... Sasa alipoondoka tu mzee rashidi.. Meneja na vijana wake nao wakafuata nyuma, ili gari yake isije kwenda kufanya mauaji halafu akachafuliwa jina lake, mana yupo kitengo kikubwa sana hapo Airport.... Na sasa ndio walikuwa wakiwasili eneo la tukio ambako ndipo ilipo harusi ya rahim



    "kumbe alikua anawahi ndoa... Nilijua anakuja kuua mana huyu nae, hakawii"

    Aliongea mr James, huku akishuka katika gari yake nyingine, na kuliona gari yake iliochukuliwa na mzee rashidi....



    Sasa mzee rashidi kufika karibu,.. Huezi amini alijikuta tu anatabasam, huku akipiga makofi,.... Mama kumuona mumewe, kapatwa na presha anahema kweli, mana ni Kosa kumpa mtoto mke bila baba kujua.. Lakini sasa uzuri ni kwamba baba nae kasapoti jambo hilo....



    Na hapa ndio naamini kuwa hakuna mzazi anaependa mtoto wake awe na tabia njema, sema sisi watoto wa siku hizi hatusikiii.... Mzazi yupi anaependa mtoto wake awe mlevi.. Mzazi yupi anaependa mtoto wake awe mvuta bangi, mzazi yupi anaependa mtoto wake awe changudoa au mwizi??...mi nasema hakuna mzazi wa aina hio.. Kila mzazi anapenda mtoto wake awe na heshima, awe mstaarabu aifuate misingi ya dini husika... Hivyo kitendo cha rahim kubadirika, kimewafurahisha wazazi wake wote, mzee hajaamini kama ipo siku mtoto wake atavaa kanzu, yaani hajaamini kabisa... Mzee aliweza kushuhudia ndoa ya mtoto wake, japo mwanzo hakuitaka... Mzee Rashidy alirudi katika gari yake, wakati huo fadhila keshanyong'onyea, na wakati huo kumbe minah nae alikuwa akimfuata nyuma, minah alitegemea kukuta timbwili timbwili la kuvunjika kwa ndoa hio, lakini ilishindikana, ila fadhila kuna kitu alifikiria ambacho kisingelikuwa kizuri mbele za Mungu.

    "sasa umeshindwaje na wewe"

    Minah alimwambia fadhila, na wakati huo walikuwa wakirudi zao nyumbani, minah hajaamini kama fadhila kashindwa..

    "minah... Nafsi imenisuta kweli... Unajua nimesoma Qur-aan tukufu, ila haijaniingia vizuri, lakini kwa yale machache yalioniingia... Nimeogopa kufanya hivyo"

    "sasa umeogopa nini... Au mimba sio ya rahim ulitaka kumbebesha tu"

    Fadhila hakumjibu kitu chochote, walirudi nyumbani kwao...







     





    Sasa huku kwa mzee rashidi kakutana na mr James..

    "alaaa, mbona nawe upo hapa"

    Aliuliza baba yake rahim kwa mr james

    "nilipata mashaka juu ya kuondoka kwako, nikaona wacha nikufuate nyuma... Mana zamani mtu akikuuzi wewe heeeee... Najua mwenyewe"

    "aaahhhhh bwana james, mbona nilisha achaga hayo mambo.. Sasa umri umekwenda si unaona mtoto wangu kapata jiko bwana"

    "alaah ivi aliokuwa anaona ni mtoto wako"

    "ndio... Tena mtoto wangu wa mwisho"

    "ila mtoto wako ni mtu wa dini... Lakini wewe baba mtu weweeee"

    "hahahahahahahaha... Mimi mwenyewe nilikuwa nakuja kumzuia.. Lakini nilivyoikuta hali halisi ya mwanangu.. Sikutegemea kabisa kama angeweza kuzungukwa na umati wa dini kiasi hiki"

    "sasa kwanini umzuie na kuoa ni jambo jema kwa mungu"

    Aliuliza James huku akitamani kujua kwanini rashidi alitaka kumzuia mtoto wake asioe...

    "unajua bwana james... Mimi nina mali nyingi sana, hasa hasa nje ya nchi... Hua napenda mtoto wangu asome ili aweze kuziendesha vizuri.. Na kutokana na uchakaramu wake wa kwanza.. Nikajua kitakacho mbadirisha mwanangu ni elimu ya juu.. Hivyo ndio mana nilikuwa napenda asome awe na elimu kubwa ili ajielewe kuwa yeye ni nani.. Lakini sasa nimefurahi sana kukuta kubadirika tena kawa mtu wa dini kuliko nilivyokuwa nikitaka... Mtoto wangu alikuwa anawaita Waislamu ni wachawi, ona leo yeye kawa kipaumbele"

    Aliongea mzee Rashidy Kingazi huku rafiki yake akimwambia kuwa

    "basi ulimlea vibaya huyu mtoto... Mpaka kuikashifu dini ya kiislamu"

    "sio dini ya kiislamu tu... Hata wakristo hakuwa akiwapenda hata kidogo.. Yaani mtoto wangu alijijengea kuwa pesa ndio kila kitu katika maisha.. Basi nasi tukamuacha afanye atakalo, ila nikajua lazima abadirike kwa elimu ya juu"



    Baada ya ndoa kuisha, james na mzee Rashidy walikwenda nyumbani, yaani pale kwa bibi mzungu,.. Ambapo ndipo alipozaliwa baba yake rahim... Wakati huo rahim ndio wanatoka msikitini kumalizia malizia ndoa yao.. Watu walikula sana, wanafunzi wa madrasa walifurahi mno, msikiti mzima ule ambao ulipelekewa jenereta ulimwagika kwenye harusi ya rahim, mana walisha msamehe kwa ile tabia alioileta pale msikitini....



    "mama rahim... Kwanini ulikuwa unifiche kuhusu ndoa ya rahim"

    Baba ndio anauliza sasa

    "hapana mume wangu... Sema ungeleta kompleni nyingi sana, hivyo niakaona wacha aoe kisha aje aendelee na shule, mana nilifurahi sana rahim kufuata misingi ya dini"

    Baba alijikuta hana la kuongea, mana ni kweli angejulishwa asingekubali rahim aoe..

    "kwani huyo kijana wenu anasoma kidato cha ngapi"

    Aliuliza mr James huku baba rahim akimjibu

    "yupo chuo, na ni mwaka wake wa mwisho huu.. Tena kabakiza miezi mitatu tu sasa"

    "aahhhh, sasa miezi mitatu, kuna haja gani ya kumsumbua... Mpe kipande chake cha mali akayaanze maisha yake na mke wake... Wacha mtoto afanye maisha, elimu haina mwisho... Na akipata elimu ya juu zaidi hata dharau za kuwazarau masiki itakuwa kubwa"

    "Eti eee"

    "mimi ndio nakuambia... Mtoto wangu anasomea digrii, sasa hivi ana nyodo hizo.. Yaani hata akiongea na mimi utafikiri anaongea mfalme fulani hivi"

    Mara rahim kaingia akiwa na mke wake,... Mzee keshaanza kumheshimu rahim, mana naye keshavuta jiko,.. Zena alipita moja kwa moja mpaka chumbani kwao, lakini rahim akabaki na wazazi hapo sebuleni.....

    "Assalam Aleykum wazee wangu"

    Waliitikia wote na james, ingawa James ni Mkristo,...

    "waaleykh msalam"

    Rahim alikaa chini ili kuwasikiliza wazazi wake wanasema nini kuhusu yeye,.. Na sasa rahim kawa na adabu ya kupitiliza kwani dini hua haitaki mtu mwenye kibri,..



    "rahim, hebu Niambie... Unataka nini sasa, mana nia yangu ni kukusomesha lakini naona umechagua maisha mengine tofauti na nilioyataka"

    Aliongea baba yake rahim, huku rahim akiwa tayari kumjibu baba yake

    "mzee, mi naona shule basi tena... Kwasababu muda uliobaki kwa sasa ni mchache,.. Mi naona niendelee kufanya kazi tu... Na ningependa kwanza nisimamie hii kampuni ya Tanga kwa muda kisha nitakuja Arusha"

    Aliongea rahim tena kwa kujiamini, lakini mzee Rashidy alishapewa ushauri na mzee James kuwa sasa keshakuwa hivyo amuache.. Na ni kweli bwana rashidi ana kampuni nyingi sana hivyo haoni tabu kwa hilo

    "kwahio hivyo ndivyo ulivyo amua"

    "ndio mzee... Ila pia nakuskiliza wewe"

    "kwa maoni yangu kwanini usirudi arusha, mana kule kuna miradi mingi sana kuliko huku tanga.. Mana meli yenyewe inakuja kila baada ya miezi mitatu"

    "mzee... Ni kweli... Ila kwa sasa nina mke, hivyo siwezi tena kuja kubanana nanyi kwenye nyumba moja... Nataka nijenge yakwangu ili nikija naingia kwangu moja kwa moja"

    Rahim aliongea jambo mpaka mr james akatikisa kichwa na kusema

    "good, sio wazo baya... Labda umsikilize mtoto wako"

    Jamali hatamani hata kuingia ndani mana yeye ndio alikuwa mchochezi mkuu wa mdogo wake ili asioe... Basi wazazi walikubaliana na kumuacha rahim huku tanga, na uzuri ni kwamba jumba la hapo tanga ni kubwa hivyo wanaweza kuishi bila tabu na bibi yao... Wazazi wa rahim walirudi arusha... Huku Tanga, rahim na zena waliyaanza maisha mapya ya ndoa.....





    MWEZI WA KWANZA......



    MWEZI WA PILI......



    MWEZI WA TATU.....



    MWEZI WA NNE....



    BAADA YA HIO MIEZI MINNE KUPITA



    Maisha ya akina zena yalibadirika sana, kwani hata familia yao nayo ina mafanikio, inaishi pazuri na imani yao ipo pale pale,... Zena alinenepa sana kwa kuyafurahia maisha ya ndoa,... Na wakati huo bado wapo jijini Tanga, mana rahim aliwaomba wazazi wake abaki tanga, walikuwa na maisha ya furaha sana, lakini zena hakuwa na furaha kama miezi miwili iliopita, hua ni mtu wa mawazo tu..



    Huku kwa fadhila sasa, bado ana ujauzito wake tena kwa sasa umekuwa mkubwa, na kila siku anaulizwa na mama yake mimba ni ya nani hasemi, kila akiulizwa hasemi sasa mimba ina miezi kama saba hivi yaani bado kama miezi miwili ajifungue,...

    "naona mke mwenzio ana nenepeana tu, nawe unakonda kwa ufara wako"

    Alikuwa ni minah rafiki yake wa muda mrefu, na kwa pembeni alikuwepo rafiki yake minah aitwaye Fatuma..

    "minah... Naomba uniache"

    "sio nikuache fadhila... Rahim alikuwa awe mumeo wazi wazi bila chenga... Lakini sijui ni ujinga gani umekuingia"

    Sasa huyu Fatuma yeye haijui vizuri hii ishu, ila alishawahi kudokezewa..

    "kwani nani aliompa mimba"

    Aliuliza fatuma huku akitaka kujua

    "we fatu, si nilikwambiaga yule mjukuu wa bibi mzungu ndio kampa mimba huyu... Na alistahili aolewe badala ya zena"

    "heeeeeeee.... Ivi ni yule tajiri tajiri hivi"

    "enheee huyo huyo ndio mwenye hii mimba.. Lakini shoti yangu kazubaa.. Mpaka kachelewa na ndoa ikafungwa"

    Sasa fatuma kuna jambo analijua... Hivyo akasema kuwa

    "mbona bado hajachelewa huyu"

    Fadhila kuskia mbona bado hajachelewa aligeuka na kusema

    "kwanini useme sijachelewa.... Hebu Niambie kama kuna njia niitumie, na sasa sitaki kufanya makosa... Hebu Niambie fatu"

    Fadhila ana hamu na kujua hio njia

    "sikiliza sasa njia nzuri.... Mimi nina urafiki na yule mfanyakazi wao... Juzi kuniambia kuwa... Zena hana raha ndani ya nyumba.. Na anatakiwa aachwe haraka iwezekanavyo"

    "heeee shosti huo ni umbe sasa, sasa aachwe kwa lipi"

    Aliuliza minah huku fadhila katoa macho tu

    "nasiki zena hashiki mimba... Na familia ya rahim inataka mtoto"

    "Yessssssss.... Fatu shika mkono wa asante huu hapa"

    Fadhila alifurahi kupita kiasi kwa kupata habari hio...



    Huku ofisini ambako rahim ndipo anapofanya kazi kwa sasa... Alikuwa bize sana, mara simu ya mama yake inaita, na wakati huo zena alikuwa akimuandalia mumewe chakula cha mchana hapo hapo ofisini, mana zena nae kuna kitengo kapewa katika kampuni hio hivyo wote wapo ofisi moja... Rahim alipokea simu ya mama yake...

    "haloo mama shkamoo mama angu"

    "Marahaba hujambo baba"

    "nipo salama tu... Na mkweo nae pia hajambo"

    Alisema rahim lakini mama hakupenda

    "kwani nilikuuliza habari zake.... Sikia rahim, mbona wewe ni mzito wa kufikiri... Unataka mimi nife ndio upate mtoto... Achana na huyo mwanamke tunataka mtoto sisi"

    "mamaaaa.... Hayo ni majaaliwa ya Mwenyezi mungu mama... Vuta subra angalau hata miezi kadhaa mama yangu"

    "nimechoka.... Ni miezi mingapi sasa mwanamke kazi ni kunenepa tu"

    "mama...kupata mtoto ni majaaliwa ya Mwenyezi mungu, sisi hatuhusiki kwa hilo"

    Rahim alizidi kumuelewesha mama yake, lakini mama ndio haelewi kitu na wala hataki kusikia kitu chochote kile...

    "Sikiliza mwanangu... Baba yako, kuna kitu aliniambia kuwa kuna siku alikutana na binti mmoja siku ile ya ndoa yenu... Yule binti alisema ana ujauzito wako na wewe umeukataa..... Sasa nasema hivi, kitanda hakizai haramu mwanangu... Hebu achana na urembo huo usio na faida,.. Nataka nimuone huyo mschana mwenye ujauzito wako... Nakuja tanga wiki hiii"









    Na wakati huo mama yake rahim akiongea hayo, hata zena alikuwa akisikia kila kitu mana iliwekwa laudi spika.... Zena ni wakati wake wa kulia tu, mana muda wote ni mtu wa kulia tu, hana raha na ndoa yake,... Simu ya mama yake ilikata kabla rahim hajamjibu mama yake, hivyo wakabaki na mawazo tu... Lakini zena ni mtoto wa Kiislamu na anaijua dini vilivyo, hivyo hawezi kuangalia ndoa yao inatetereka kiasi hicho..



    "mume wangu... Kwanini niumie namna hii... Kama vipi fuata sunna za mtume... Mtume wetu alikuwa na wake wanne... Fanya hivyo"

    Aliongea zena, yaani kwa moyo wake wote alikubali aletewe mke mwenza,

    "hapana mke wangu... Siwezi kufanya hivyo, abadani siwezi kuoa tena"

    "rahim.... Mama yako ataniua kwa maneno, roho yangu inaniuma rahim.. Nakupenda sana na sipendi uoe mke mwingine, lakini ruksa, oa tu uiridhishe familia yako"

    Aliongea zena huki machozi yakimtoka mfululizo katika macho yake,...

    "rahim mume wangu.... Nina wasiwasi na mimi mwenyewe.... Labda kuutunza usichana wangu kwa mada mrefu, labda ndio chanzo... Kutunza tupu yangu labda ni chanzo cha kutoshika mimba... Sihitaji kumkufuru Mwenyezi Mungu,... Naomba uoe mke wa pili... Mana najua tu ni lazima mimi niwe na tatizo... Kwasababu kama wewe una tatizo, mbona fadhila ana mimba yako.... Rahim mume wangu.. Nakuruhusu muoe fadhila, mana ana ujauzito wako"

    Zena aliyaongea hayo huku haishiwi kulia... Na rahim alimsikiliza mkewe, lakini bado hakubali kabisa...

    "hapana zena... Naomba tuongozane twende hospitalini"

    Zena hakukataa japo yeye ana mashaka kwakuwa aliitunza bikra yake mpaka anakuja kuolewa, sasa anahisi hicho ndio chanzo cha yeye kutoshika ujauzito.... Walikwenda hospitali wote wawili



    Sasa huku kwa akina fadhila, wakiwa wasichana watatu wabaya kama kutu yani... Ni watoto wa Kiislamu lakini ni waharibifu wa ndoa za watu,. Sasa mama yake fadhila alisikia yale maneno, mana kila siku anamuuliza mwanae hasemi...

    "Enheeee sasa leo ndio nimejua... Kumbe siku zote nakuuliza mwanangu mimba ni ya nani hio husemi,.. Kumbe ni ya mjukuu wa bibi mzungu,.. Kwanini usingesema"

    Mama yake fadhila aliongea hayo huku Minah akidakia na kusema

    "mama... Mwanao alikuwa na nafasi nzuri ya kuolewa na rahim... Lakini kazubaa"

    "haya... Hebu niambie.. Una uhakika hio mimba ni ya huyo kijana"

    Mama alimuuliza mtoto wake, huku akikaa chini... Fadhila alijibu kuwa

    "ndio mama.... Sema niliogopa kukuambia"

    "usije ukamsingizia kijana wa watu... Mana siku akija kujuaa... Heeeeee... Utakiona cha moto"

    Fadhila alitishika na maneno ya mama yake, mana wale ni matajiri, hivyo ukicheza na akili ya tajiri, siku akija kujua kuwa mtoto uliompa sio wake... Anaweza kukupiga Hata risasi na ukafa, hivyo maneno hayo yalimwogopesha sana fadhila,...

    "mama... Wacha nianze kumtafuta rahim, mambo yote yatajulikana mbele kwa mbele, kikubwa tu awe ni mtoto wake mama"

    "mimi sipo hapo, ukiletwa maiti hapa sintokukataa mana uliyataka mwenyewe"



    Sasa huku hospitali, baada ya kuchukuliwa vipimo vya wote wawili kama kuna mwenye tatizo na sehemu za uzazi, mana rahim yuko vizuri, ana nguvu haswa hivyo sidhani kama atakuwa na tatizo.... Sasa rahim yeye alitoka nje kidogo baada ya kuchukuliwa vipimo, na hapo wanasubiri majibu...

    "haloo, hadija Assalamu Aleykum"

    Rahim alimpigia hadija yule mfanyakazi wao wa pale kwa bibi mzungu,...

    "waaleykh msalam kaka, habari ya kazi"

    "aahhhh nzuri.... Ahh Samahani dija unaweza kunipatia namba ya fadhila"

    Rahim aliiulizia namba ya fadhila

    "fadhila???.... Fadhila huyu huyu mwenye mimba au"

    "ndio... Huyu huyu mwenye mimba"

    "mmmhh, sawa kaka ngoja nikutumie kwenye sms"

    "ok, Naisubiria sasa hivi"



    Sasa huku kwa hadija, baada ya kutuma namba kwanza, kaanza kumpigia fadhila mwenye kabla ya kutoa namba

    "haloo, fadhila.. Assalamu Aleykum"

    "Waleykhu msalam, za siku"

    "nzuri tu, vip hali yako"

    "aahhh we acha tu, namshukuru mungu"

    "mzigo umeutua nini"

    Hadija alimuuliza kwa utani kama tayari keshajifungua...

    "mmmmhhh mwenzangu weee bado"

    "heeeee hao pacha nini fadhila"

    "we acha tu, kwani najua basi"

    "sasa nataka nikupe jambo jipyaaa"

    "jambo gani tena hadija"

    "rahim anataka namba yako ya simu"

    "weeeeee hadija acha uongo"

    "kweli, ila bado sijampa"

    "sasa kwanini usimpe.... Hebu mpe bwana hadija"

    "sawa... Kata simu nimpe ila usiwe na papara shosti, sasa ni zamu yako kula raha"

    "mpe sasa jamani hadija"

    Hadija alikata simu yake kisha akamtumia rahim namba za fadhila..



    Kule hospitalini, rahim anasikia meseji inaingia... Kuangalia alikuwa ni hadija,.. Pale pale aliipiga ile namba, na wakati huo yupo nje ya hospitalini hapo, ila zena yupo Ndani anasubiri majibu yao...

    "haloo fadhila.. ASalaam Aleykum"

    "Waleykhu msalam warahmatullah wabarakatuh hali yako baba"

    Fadhila aliitikia kama vile mke wa rahim, yaani kwa heshima zote...

    "naomba tuonane sasa hivi fadhila"

    "no... Kwa sasa siwezi kutembea kwa umbali mrefu..."

    "ok... Chukuwa tax, nitalipia mimi"

    "tatizo huku mtaani hakuna tax"

    "basi naja kukuchukuwa hapo ulipo"

    "nipo nyumbani sasa hivi"

    "ok.. Ngoja nije"

    Fadhila haamini kama leo kapigiwa simu na rahim....

    "mke wangu... Naomba nitoke kidogo, nipe dakika tano nitakuwa nimesharudi hapa"

    "sawa mume wangu.. Lakini usichelewe, turudi kazini"

    "sawa"

    Rahim alichukuwa gari na kuondoka







     





    "we fadhila, nani kapiga huyo"

    Aliuliza minah, huku fatuma nae akiwa na maskio mbele ili kujua nini kinaendelea...

    "ni rahim, baba watoto wangu"

    "weeee, kakupigia mwenyewe kabisaaa"

    "ndio"

    Hajakaa vizuri, mara simu yake inaita tena,...

    "haloo rahim upo wapi"

    "nipo hapa barabarani, njoo kwa hapa"

    "sawa nakuja"

    Fadhila alikata simu, kisha akawaaga rafiki zake kwa mbwembwe zote

    "minah, fatuma... Narudi sasa hivi.. Ngoja tukayajenge na mme wangu"

    "weweeeee... Unariiinga kama nakuina vile ndani Vx yako mpyaa"

    "acha kunichawia wewe minah... Kwani changu si chako"

    "nenda bwana fadhila mbona kama unazidi kuchelewa"

    Walikuwa wakiongea maneno ya utani,... Kweli rahim kuangalia mbele, haamini kuona tumbo la fadhila limekuwa kubwa mno,.. Rahim alijiskia raha sana, mana kama kweli ni mtoto wake, basi hana budi kumuoa fadhila,...

    "hali yako fadhila?...pole"

    Alisalimia rahim huku akimpa pole kwa tumbo jinsi lilivyokuwa kubwa

    "Ahsante..."

    "fadhila... Nataka tuonge mambo ya maana kidogo"

    Rahim alishuka kwenye gari kisha akamshika mkono huku akisema

    "fadhila, naomba unisamehe kwa yale yaliyopita,... Nimekuja kukulipa malezi ya miezi yote ya hio mimba.. Na nitailea na pia naikubali kuwa ni mimba yangu"

    Fadhila haamini maskio yake kwa yale anayo yasikia toka kwa rahim...

    "rahim... Mimi sina chuki na wewe... Bado nakupenda,.. Na nipo tayari kukuzalia zaidi ya huyu... Niamini tu"

    Aliongea fadhila huku akilia ile kikudeka deka hivi....

    "fadhila.... Naomba ukubali nikuoe baada ya kujifungua mtoto wetu"

    "sawa... Ila kabla hujanioa... Na zena inakuwaje, mana staki tuwe wawili"

    Heeeeee fadhila nae kaanza Mashauzi, Eti anataka zena afukuzwe ndio aolewe...

    "una maana gani fadhila"

    Lakini sasa kabla fadhila hajasema, ghafla simu ya rahim inaita,.. Hivyo fadhila akastop kuongea kwanza, mpaka rahim amalize kuingea na simu.... Sasa rahim kuangalia namba, ilikuwa ni ya mke wake

    "haloo mke wangu, vp huko hospitali"

    Rahim alitaja mke wangu mbele ya fadhila, kana kwamba rahim kumuacha fadhila, labda mpaka kiama,... Wakati huo fadhila anasikiliza sauti ya simu, na anajua anaongea na mke wake ambae ni zena...

    "mume wangu... Majibu yametoka"

    Aliongea zena, huku rahim akiwa na shauku ya kutaka kuyajua kabla ya kwenda hospitalini

    "enhee, yakoje yakoje majibu"

    Fadhila alishtuka, kuskia swala la majibu hospitalini, alijua labda zena tayari kapata mimba... Hivyo fadhila akawa makini kuskiliza kinacho ongelewa...

    "si uje huku huku mume wangu"

    "hapana zena... Niambie tu"

    Zena aliona wacha amwambie ukweli wa majibu

    "majibu kwa upande wangu wangu, sina tatizo niko vizuri tu... Ila wewe sasa"

    "Unasemaje??.. Mimi nina nini"

    "majibu yanasema wewe una tatizo kwenye njia za uzazi mume wangu"

    "whaaaaaat.....yaani mimi ndio mwenye tatizo? Au kapima vibaya mke wangu... Mbona nachakalika vizuri tu sa kwanini nisiweze"

    "mume wangu.. Punguza hasira... Ila njoo kuna ushauri upewe na dokta"

    "oooooooohhhh mungu wangu weeee"

    "njoo mume wangu..."

    Rahim alikata simu lakini tayari kesha nyong'onyea mwili wote, kwa taarifa kama hizo.... Sasa ndio anakumbuka kuwa, kwahio fadhila alikuwa anamdanganya... Aligeuka na kusema

    "wewe fadhila hio mimba ni ya.... "

    Alishangaa hamuoni fadhila, mana alikuwepo nyuma yake... Yaani baada ya simu kuita, akampa fadhila mgongo ili aongee na simu... Sasa kugeuka haoni mtu tena... Sasa hapa ndio tunagundua kuwa hio mimba sio ya rahim...... Rahim aliwasha gari na kuondoka zake kwenda hospitali, mana ukweli umeshajulikana...



    Huku akina minah na fatuma wanamshangilia zena,.. Wakati huo zena mwili wake wote umeloa jasho utafikiri alikuwa akifanya kazi....

    "heeeeeeee mwenzetu vipi mbona jasho mwili mzima kuna nini"

    Aliuliza minah huku fadhila akiwa haamini

    "niacheni"

    "hee yamekuwa hayo tena... Imekuwaje? Au kaikataa tena hio mimba"

    Aliongea fatuma huku wakiwa wanamshangaa mwenzao...

    "si bora angeikataa"

    "sasa kafanya nini"

    "rahim, hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, nimesikia kwa masikio yangu"

    "ati nini???.... Sasa kama uwezo huo hana, na wewe alikupaje?"

    "hiii Mimba sio ya rahim... Ni mimba ya zuberi mtoto wa mzee bakari"

    "heeeeee, kwahio kumbe siku zote hizooopo ulikuwa unajishaua nini sasa"

    Aliongea minah, lakini fatuma akadakia na kusema kuwa....

    "sasa na wewe kwanini usingetafuta neno lolote la kusema ili aikubali"

    "heeeee wewe fatu wewe... Haya akakubali, na akaniona... Inafikia wakati anataka mtoto mwingine, haya nitamnyea wapi na wakati yeye hawezi"

    "wewe fadhila umesikia kwa nani"

    "mke wake huyo, kumbe walienda kupima, sasa rahim akaja kukutana na mimi,.. Kule majibu yametoka, zena kampigia mumewe... Rahim alitamani kulia.. Sasa nilipojua kuwa rahim hana uwezo, ndio nikaondoka kimya kimya bila hata kumuaga,.. Na ni kweli hii mimba sio yake, sema tamaa zangu tu"

    "yaani fadhila una hatari wewe.... Ivi unajua kuwa matajiri hawana utani na watoto... Ungekuja kufa bure wewe fadhila"



    Huku hospitalini, rahim anakutana na dokta,....

    "dokta, hizo taarifa ni za kweli au"

    Aliuliza rahim huku akiwa haamini macho yake kwa jinsi anavyoisoma hio karatasi ya majibu...

    "kijana... Tatizo lako sio kubwa... Ila sababu ya tatizo lako. Ni pombe.. Wewe ulikuwa unakunywa sana pombe, na pombe ni mbaya sana kwenye mishipa ya uzazi"

    "lakini dokta,... Mimi nilisha acha kitambo sana, yapata meizi saba sasa"

    "sasa sikiliza kijana... Una nguvu za kiume vizuri sana... Lakini mbegu zako zimethiliwa na kemikali za pombe... Hivyo nimefanya vipimo vyangu, inaonekana hapa una mwaka mzima mbele ndipo utaweza kupata mtoto... Kwasababu kemikali bado zipo katika mirija ya uzazi,.. Hivyo una mwaka mzima mbele"

    "aaahhh dokta.... Mwaka mzima mbele"

    "ndio... Mbona ni muda mfupi tu... Ila hapa katikati tumuombe mungu... Afu kula vyakula vya wanga sana, mana kwa mungu hakuna linalo shindikana, hata leo unaweza kushangaa mama ana hali nzuri"

    Aliongea dokta huku rahim akimwambia zena kuwa

    "zena.. Unasikia huko... Vyakula vya wanga niandalie sana"

    "usijali mume wangu... Ilimradi nimelijua hilo, utavichoka mwenyewe hivyo vyakula"



    Huku nyumbani kwa bibi mzungu ambako ndipo wanapoishi akina rahim,... Fatuma cha umbea kaja kuongea na hadija

    "dija, unajua kuna jipu zito linanikereketa rohoni"

    Aliongea fatuma huku akitaka kulijua hilo jipu

    "jipu gani tena"

    "nimesikia yule kaka yenu hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba"

    "weeeeee fatuma wewe... Umeyajuaje hayo? Wewe ni dokta"

    "heeeee muulize fadhila, kapigiwa simu na huyo kaka yenu, kaenda kuambiwa kila Kitu,.. Sasa hivi fadhila hana hamu na rahim tena, afu kumbe ile mimba sio ya kaka yenu, ni mimba ya zuberi mtoto wa mzee bakari pale juu"

    "weweeee fatuma unasema kweli"

    "aaahh muulize minah, au muulize fadhila mwenyewe akupe fulu data"



    Masaa mawili mbele, hadija nae hagandishi jambo,... Saa ngapi hajampigia jamali ambae ni mpenzi wake,... Ona sasa siri inavyo vuja yaani kama redio Mbao

    "haloo mpenzi hali yako"

    "safi hadija... Umenisusa we mwanamke khaaa"

    "umenisusa wewe au mimi"

    "ok basi yaishe... Niambie mambo ya tanga huko"

    "mmmhhh huku shwari tu, ni vijimambo tu"

    "vijimambo gani tena"

    "mdogo wako babu weye"

    "ana nini... Si ana mkewe wanakula raha tu, bado sisi"

    "mdogo wako, hawezi kumpa mwanamke mimba"

    "acha ujinga hadija"

    "heeeee... Tena wamerudi hospitali muda sio Mrefu, na sasa wameenda msikitini"

    "rahim huyu huyu mdogo wangu au?"

    "sasa kumbe nani"

    "heeeeeeeee.. Hebu ngoja kwanza"

    Jamali alikata simu huku akimuita mama yake,... Ona sasa redio za ajabu hizo...



    "mamaa..... Mamy"

    "kuna nini mbona unanishtua wewe"

    Aliongea mama baada ya kutoka chumbani kama vile alikuwa anaitiwa jambo kuubwa sana...

    "mwanao tasa"

    "we mjinga nini wewe... Unaongea maneno gani kwa mdogo wako"

    "nimepigiwa simu sasa hivi hapa na hadija, kasema wametoka kupima sasa hivi... Na rahim kaonekana kuwa na tatizo la kuto mpa mwanamke mimba"

    "Unasemaje wewe"

    "heeeeee... Yaani baba akilijua hilo, ataua mtu.... Yaani sijui itakuwaje"

    "we jamali unasema kweli au unatania"

    "mamaaa, kuna siku nilisha wahi kukutania mama angu"

    "mungu wangu, mwanangu rahim.... Hapana, lazima atakuwa kalogwa... Ndio mana sikutaka aende tanga, hapana wamenilogea mwanangu"

    Mama alianza maneno yake ya ushirikina kwamba kuna wachawi wamemroga rahim asipate mtoto..

    "lakini mama kama ni kweli... Mbona nilisikia rahim ana mwanamke mwenye ujauzito... Je huyo kampaje mpaje Kwa mfano"

    "si ndio hapo hata mimi najiuliza.... Hapana... Ngoja nimpigei baba yake, huenda ana madaktari wake wa huko Uingereza wataweza kumtibu rahim"

    Mama bila kudhibitisha jambo hilo, anaamua kumpigia simu mume wake... Na uzuri ni kwamba mzee rashidi alikuwa Arusha, mana asilimia kubwa yeye huishi nje ya nchi mana ndiko miradi yake mingi ilipo, hususan dubai,...

    "baba rahim, upo wapi"

    Aliongea mama rahim kwa kumtaka baba rahim afike nyumbani mara moja

    "kuna nini mama watoto... Shida nini"

    "ivi kuna taarifa nimezisikia sasa hivi kuhusu mwanao rahim"

    "taarifa gani tena... Mimi nimeongea nae sasa hivi hapa, kanipa mikakati ya kazi haya kuna nini tena"

    "mtoto wetu kaenda kupima na mke wake kujua nani ana tatizo la uzazi.... Lakini mwanao ndio ana tatizo"

    Mzee kusikia tu rahim ana tatizo, papo hapo akapoteza fahamu... Na huyo ni mwanaume lakini kapoteza fahamu,... Sasa tujiulize je? Kuna nini nyuma ya hapo?? Mbona swala la rahim kutopata mtoto ni gumzo katika familia hio... Je? Kuna nini kilichojificha juu ya rahim....









    Mzee Rashidy alidondoka tu ghafla baada ya kusikia taarifa za rahimu kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamke aina yeyote yule, hivyo hata akimuacha zena ni kazi bure,..



    Mzee Rashidy anakimbizwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya zaidi, na huku nyumbani mama kapatwa na wasiwasi juu ya ukimya na kishindo kikubwa,...

    "baba yako atakuwa na tatizo"

    Aliongea mama yake jamali na kumfanya jamali ashtuke kwa mshangao..

    "ati unasemaje mama"

    "nimesikia kishindo kama simu imedondoka chini"

    Jamali kusikia hivyo, alitoka nje kachukuwa gari yake kisha moja kwa moja mpaka ofisini,...



    Alipofika ofisini aliambiwa baba yake kakimbizwa hospitalini,... Jamali hakutaka kubaki hapo, moja kwa moja mpaka hospitalini,... Baba yake rahim hali ilizidi kuwa mbaya....

    "baba... Kwani kumetokea nini"

    "mu.. Mum....mu...muite mama yako, mwambie... Aje na karatasi zote"

    Jamali mara moja alimpigia mama yake....

    "mpigie na rahim aje"

    Baba alitaka na rahim nae aje arusha,



    Huku tanga ambako akina rahim na mke wake, wakiwa ndio wanarudi msikitini,.. Rahim yeye ni mtu wa furaha tu muda wote, hivyo hana anachokiwaza zaidi ya kufanya kazi..

    Mara simu yake inaita, kuangalia alikuwa ni jamali ndie anampigia simu

    "haloo kaka habari yako"

    "salama tu... Aisee unahitajika Arusha mara moja, mzee kazidiwa"

    "kuzidiwa???... Kazidiwa na nini na wakati muda sio mrefu niliongea nae"

    "we njoo Mount Meru Hospital,.. Na baba ana hali mbaya"

    Simu ilikata huku rahim akiwa haelewi chochote,...

    "kuna nini mme wangu"

    Aliuliza zena huku akiwa na shauku ya kujua

    "baba ana hali mbaya kule Arusha"

    "lakini si ulikuwa unaongea nae muda sio mrefu"

    "ndio, na hata mimi nashangaa"

    Basi rahim na zena waliwaaga wazazi na bibi mzungu kisha walikwenda Airport na kuchukuwa ndege ya private, ya jioni jioni hio, Moja kwa moja mpaka Arusha...



    Walifika mida ya saa kumi na mbili za jioni,.. Rahim na zena wanachukuwa tax ilio wapeleka mpaka Hospitali jioni hio hio,.. Yaani matajiri bwana raha sana, yani muda huu tu ulikuwa tanga, eti sasa hivi yupo Arusha,.. Duuu pesa kweli noma,... Rahim alifika hapo hospitali na kuonyeshwa wodi aliolazwa baba yake, kweli baba alikuwa na hali mbaya sana, na sababu haijulikani..... Alipofika tu pale alipolazwa mzee Rashidy,... Sasa familia yote ikawa imekamilika kasoro bibi tu alioachwa kule tanga,

    "rahim mwanangu... U... U... Umekuja"

    "ndio baba.... Nimefika mwanao"

    "mwanangu.... Nakukabidhi mali zote.. Kuanzia Tanzania mpaka nje ya nchi, nazani unaijua miradi yetu.. Hivyo sina hofu na wewe...."

    Aliongea mzee Rashidy huku akitoa hati miliki za makampuni yote walionayo,... Rahim anayapokea lakini wala hana hata hamu nayo,... Shida yake ni baba yake apone tu..

    "mzee, mbona unanikabidhi mali mzew na wakati wewe mwenyewe upo"

    "hapana rahim... Siwezi kupona kwani kuna ugonjwa wa moyo nilikuwa nao, hivyo mshituko nilioupata, ndio umekwenda kuutonesa ugonjwa huo... Hivyo, mali hizo hapo... Ila... Mali hizi ni za mtoto wako, na ndio mana tunataka uwe na mtoto mapema... Yaani kuanzia bibi yako, mimi, wewe... Hazikuwa mali zetu ila ni mali za mtoto wako wewe.. Aliwekewa na baba yake"

    Rahim alishangaa, yaani hizi ni mali za mtu ambaye hata dalili ya kuzaliwa hana...

    "baba yake nani"

    "ni stori ndefu... Ila muulize bibi yako atakupa ukweli wote kuhusu mali hizi"

    Rahim aliyakagua makaratasi yote, lakini hakukuwa na jina la jamali, ispokuwa yeye....

    "baba... Mbona hati miliki zote zina jina langu, na kaka jamali je vp"

    "hilo swali utamuuliza mama yako"

    "baba pole sana.. Ila utapona"

    "hapana... Naomba nimuone mkwe wangu"

    Baba alitaka amuone mkwe wake yaani mke wa rahim

    "mama.... Kwanza nikushukuru kwa kunibadirishia mwanangu.... Hakika nilitamani sana mtoto wangu abadirike,... Lakini tulishindwa kufanya hivyo... Na rahim ni mtoto wa pekee kwetu, hivyo tulimpenda mpaka kupitiliza na kwakuwa tunajua future yake ni ipi, na ndio mana tulikuwa tukimlinda sana.. Ahsante sana mama nakupa hongera zako"

    Aliongea mzee Rashidy huku akimuachia zena taaratibu,...

    "lakini baba, nitakuwaje wa pekee na wakati kuna kaka jamali"

    Aliongea rahim huku akitaka hata kulia...

    "rahim mwanangu, Nimekwambia swali hilo muulize mama yako"

    Mzee Rashidy alipomaliza tu kusema hivyo, alifariki dunia... Kilio cha watoto na mama yao hapo hospitalini.... Leo mzee Rashidy anapoteza maisha



    BAADA YA SIKU TATU KUPITA



    Familia yote ikiwa jijini Tanga, baada ya mazishi ya kumzika baba yao... Rahim akiwa kakaa katika sebule, haamini kama jana ndio wamemzika mzee Rashidy ambaye ni baba yake.. Na wakati huo, familia yote, iliitishwa kikao hapo sebuleni, yaani wote akiwemo, RAHIM, JAMALI, MAMA YAO, BIBI YAO, MKE WA RAHIM (ZENA) HATA HADIJA ALIKUWEPO..



    "mama kuna swali nataka nikuulize.. Mimi na jamali tupoje"

    Rahim alimuuliza mama yake, mana hili swala analijua mama peke yake,..

    "mwanangu... Jamali ni kaka yako.. Lakini baba yako sio baba yake... Nakumbuka... Baba yako aliniambia kuwa amehangaika sana kutafuta mtoto, na alihisi labda wanawake ndio wana shida,... Lakini kumbe ni mambo ya mungu.. Ndipo akamuacha mkewe wa kwanza.. Na kunioa mimi, ambae alinikuta nina mtoto mmoja ambaye ndio huyu jamali,... Kwahio jamali ni kaka yako tumbo moja kasoro baba tu"

    Aliongea mama huku naye akilia sana

    "lakini mama... Mbona ni mtoto wa familia kabisa, sasa kwanini kwenye mali hakupewa chochote"

    "rahim... Mali hizi.. Zinatakiwa zinyooke katika familia yenu tu.. Na historia ya hizo mali muulize bibi yako"

    Rahim kuskia hivyo hata hakuchelewa kuuliza kwa bibi...

    "bibi, hebu tupe ukweli... Mana swala la mali naona ni gumzo, na swala la kutopata mtoto pia ni gumzo, kwanini lakini"







     





    Sasa hapa bibi ndio anaanza kutoa ukweli wote kuwa....

    "kwa sasa unapaswa kujua kila kitu mjukuu wangu..... Nakumhuka miaka ya 40 nikiwa mschana mdogo sana.. Baba yangu mimi ambae ni baba mkubwa wako wewe,.. Alikuwa ni mchimbaji wa madini,.. Kule amani, baba mkubwa wako alifanikiwa kupata dini lenye ukubwa wa ngumi,.. Lakini kipindi hicho tulikuwa bafo tupo chini ya utawala wa Waingereza.. Hivyo walikuja kujua mzee KIVUYO kapata mali... Hivyo walianza kumtafuta kila upande na uzuri ni kwamba kule amani alikwenda kuchimba tu, lakini hawakuwa wakijua anapoishi mzee kivuyo,.. Baba yako huyo alikuwa na mtoto mmoja wa kiume, ambae sasa ndio mume wangu mimi na ndio babu yako wewe... Mzee kivuyo alimkabidhi mtoto wake huyo hilo dini,.. Lakini ni kwa sharti moja tu, kuwa mali hio ni maalum kwa ajili ya kilembwe chake, yaani kilembwe ni mtoto wako wewe rahim, wakati anapewa babu yako hilo dini, hata baba yako mzee Rashidy hakuwa hata na dalili ya kuzaliwa... Hivyo dini lile alipewa mume wangu mimi,.. Wakati anapewa wala hatukuwa tukijuana na yeye... Ila yeye ndio kanipa historia hio... Alipokuwa akimkabidhi dini lile, mzee kivuyo alijua tu ipo siku atauwawa na wakoloni waliokuwa wametutawala kimabavu... Na alisema mali hio ni ya mtoto wako wewe rahim, na hastahili kuimiliki mtu yeyote ispokuwa mtoto wako, yaani hata wewe sio zako hizi mali bali ni za mtoto wako.. Ambae ni kilembwekeza chake, na kama unavyojua sisi watu wa zamani, tukisema kitu fulani kisifanyike na kikafanyika, basi ni madhara makubwa yatatokea mana kuna maeneo yalitaamkwa, na zamani tulikuwa tukiheshimu neno kuliko vitendo, na toka mzee kivuyo ambae ni mkwe wangu, alipomkabidhi babu yako lile dini, hatukuwahi kumuona tena, na sisi tulijua keshauwawa na wakoloni waliokuwa wakisimamia migodi hio... Hivyo mume wangu ambae ni babu yako, alilitunza dini lile, mpaka tukaja kuoana na kupata mtoto wa kiume mmoja tu ambae ndio huyu baba yako mzee Rashidy.. Rashidy tulimsomesha mpaka akaja kuwa mtu mzima... Ndipo tulipompa dini hilo akaliuze ili tuanze kutumia mali, ila nae aliambiwa kuwa mali hizo ni za mjukuu wake ambae ni mtoto wako wewe... Kiukweli utajiri ulikuwa ni mkubwa kutokana na dini lile,... Baba yako aliweza kujiwekezea mali nyingi sana kampuni nyingi sana na ndio maana mpaka sasa hivi tuna kampuni nyingi sana.... Sasa baba yako nae akawa anatafuta mtot kwa udi na uvumba ili apate mtoto wa kumkabizi mali hizo... Baba yake ambaye ni babu yako alilia na baba yako apate mtoto mapema ili amuone mjukuu wake ambae ni wewe.. Baba yako alijikuta anaoa wanawake wengi bila mafanikio,.. Sasa ndipo akaenda kumuoa huyu mama yake, na yeye alimkuta ana mtoto wake ambae ni huyu jamali,.. Pia alikaa nae bila kupata mtoto... Mpaka babu yako anafariki dunia,... Rashidy bado hana hata dalili ya kupata mtoto.... Lakini mungu sio asumani... Allhamdulillah ukapatikana wewe,... Sasa mtoto wako wewe ndio anatakiwa kuchukuwa mali zake alizopewa na baba yake, na akaambiwa kuwa kitukuu atakapo oa atahesabiwa miaka miwili asipo pata mtoto, mali zote zitaanza kufilisika.... Hivyo ndio mana baba yako kafariki kwa kusikia kuwa huna uwezo wa kupata mtoto maana yake mali zitapotea kwasababu neno lililotaamkwa halijatimia... Na hio ndio historia ya mali hizi"



    Bibi alimaliza kuongea, kila mtu kashika shavu, mana story ni ndefu afu tamu... Sasa hapo kila mtu akajua siri ya mali hizo, hivyo sio mali mbaya na wala hazina shida kwa matumizi yeyote yale, ila mmiliki wake bado hajazaliwa.... Sasa rahim leo ndio anajua kuwa jamali sio mtoto wa baba yake, na ndio maana hata kule hospitali rahim alishindwa kumwongezea jamali damu kwasababu ni watoto wa baba tofauti na damu zao haziendani... Kuanzia hapo hakukuwa na maswali tena mana kila mtu keshajua kila kitu..





    BAADA YA MIEZI KADHAA KUPITA



    Basi familia yote iliamua kurudi arusha, na huku kijijini walimuacha bibi mzungu kama kawaida yake,.. Lakini jamali nae alitangaza ndoa kwa hadija, ila bado hajaoa... Kwa sasa Mama yake rahim hamchukii tena zena, mana atamchukia mtoto wa watu wakati mtoto wake ndio mwenye tatizo la mbegu zake kutoka zikiwa feki kwa kunywa pombe zenye kemikali za hali ya juu... Eti mambo ya kizungu... Rahim na zena wakiwa nyumbani kwao, katika nyumba mpya, mana hataki wabanane na mama kule nyumba kubwa,... Ghafla mlango ulisukumwa na kuingia mtu....

    "we nani kakuelekeza huku"

    Aliongea rahim, huku akitaka kumpiga mtu alioingia hapo ndani

    "rahim... Yaani umeona unitelekeze na kwenda kuoa hicho kimada chako"

    Sasa lile neno kimada lilimtia zena kichefu chefu na kukimbilia kutapika.

    "shakira, naomba uondoke nyumbani kwangu"

    "sawa, nitaondoka... Lakini utaukumbuka upendo wangu kwako"

    "shakira.. Mimi sio rahim wa zamani.. Kwanza hata huogopi kuingia kwenye nyumba ya shekhe"

    "shekhe wa mavi... Kwenda uko"

    Shakira aliondoka lakini hatamani hata kumuona rahim katika macho yake... Mara ghafla zena kaja

    "mume wangu.. Huyu mtu ni nani"

    "anaitwa shakira, eti huyu ndio mchumba nilioandaliwa kumuoa kabla ya kukutana na wewe"

    "na wao ni matajiri"

    "ndio"

    "mme wangu"

    "naam"

    "tumbo linaniuma eti"

    "tatizo lako unapenda kunywa maji baridi sana wewe... Haya ona sasa, ndio tabia gani hiii"

    "nimetapika chakula chote"

    Rahim alitoka nje na kuandaa gari kisha anampeleka mke wake hospitali,.... Lakini akiwa anatoka tu hapo getini anakutana na jamali ambaye ni kaka yake..

    "habari yako kaka"

    "safi tu... Vp tena wapi na shemeji"

    "aahhh nampeleka Hospitali hapo"

    "ok utawahi kurudi"

    "sina hakika kwa hilo"

    "sasa vp kuhusu dubai... Kwasababu toka baba alipofariki, hua tuna agiza tu, hatujawahi kwenda kutembelea hata wafanyakazi wa kule"

    "aahhh kaka umeongea jambo la msingi sana... Ila mimi ningekuomba kitu kimoja... Kwanini wewe usiwe kule dubai badala ya kutembelea,.. Yaani iwe ndio makazi yako.. Mana tukiwa tunatembelea tu, sidhani kama ni nzuri hio, afu mimi nitadili na hizi za Tanzania"

    "hilo nalo ni wazo... Ila unahitaji upate shemeji kwanza kutoka huku huku"

    Aliongea jamali akimaanisha kuwa basi anahita kuoa ndipo aende huko..

    "we panga ni siku gani tule kapilau uende"

    "hilo lipo wazi ndugu yangu... Keshokutwa tu"

    "basi kazi ni kwako tu"



    Rahim aliwahi hospitalini baada ya kuelewana na ndugu yake kuhusu mambo ya kugawana kazi... Rahim alimfikisha mke wake hospitalini, na alipokelewa vizuri tu na kufanyiwa vipimo....

    Baada ya kama robo saa hivi mkewe anaitwa kwenda kuchukuwa majibu

    "mama hongera, una ujauzito wa wiki mbili"

    Zena ilibaki kidogo tu apoteze fahamu,... Mana furaha ilizidi mpaka hata kucheka alishindwa.... Zena alilia kabisa, haamini kama leo ana ujauzito,... Rahim alivyoitwa na kupewa taarifa hizo, alikataa... Mana anakumbuka aliambiwa kuwa kuna mwaka mmoja mbele ndipo apate mtoto... Rahim alikataa kata kata.. Na ili akubali waliamua kwenda tanga mana waliona hospitali hio inatoa majibu ya uongo... Na kwakuwa usafiri wao ni wa ndege, basi Hawakuchukua muda walifika katika kama mida ya saa sita hivi za mchana, na siku hio ilikuwa ni ijumaa

    "zena mke wangu... Hii mimba itakuwa sio yangu"

    Aliongea rahim huku zena akianza kuingiza huzuni tena.... Na wala hakumjibu kitu na wasiwasi hana



    Walipofika walimwita dokta, wa hapo hospitali ya BOMBO HOSPITAL

    "aisee dokta, unanikumbuka vizuri"

    Aliongea rahim huku akijinyooshea kidole mwenyewe

    "ndio, tena nakukumbuka vizuri sana"

    "ivi vipimo vyako vilikuwa sahihi kweli.. Mana mke wangu kapata mimba kabla ya mwaka uliosema kuisha.. Au kachepuka huyu... Zena sema ukweli umechepuka wewe"

    "sikiliza kijana... Ukumbuke Nilikwambia hivi... Kwa vipomo vyangu vinavyo onyesha, una mwaka mmoja mbele upate mtoto, lakini kuna uwezekano pia kabla ya huo mwaka ukapata mtoto... Hivyo hapo kulikuwa na asilimia 50 kwa 50... Na nikasema tumuombe mungu.. Au sijasema hivyo kijana..."

    Rahim alipoambiwa hivyo alipunguza hasira

    "zena...nihakikishie kuhusu hii kitu"

    "rahim mume wangu..... Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu.. Siku nikijifungua tumpime huyu mtoto, na kama atakua sio mtoto wako... Nakuomba usiniache hai... Nifanye utakalo... Naapa mbele za mungu simjui mwanaume yeyote zaidi yako"

    Zena alipo Ongea hivyo, dokta alimchukua rahim na kwenda kuongea nae

    "wewe, mbona unashindwa kumuamini mkeo"

    Aliongea dokta huku rahim akicheka kicheko kikubwa...

    "hahahahahaha, sikia dokta,... Najua kabisa ule ujauzito ni wangu, sema nilikuwa nampasha moto tu... Usijali dokta namuamini mke wangu kuliko unavyo tegemea"



    Rahim alipotoka hapo alikwenda kwa mkewe, na kumjulisha kuwa alikuwa anamtania wala hakuwa siriasi..

    "kwanini lakini unanifanyia hivyo, mpaka naapa kwa jina la mungu... Yaani wewe haaaa"



    Sasa walipotoka hapo hospitali walikwenda moja kwa moja kuswali katika ule msikiti aliowahi kupeleka jenereta, na ilikuwa ni siku ya Ijumaa, sasa alipofika tu getini alikutana na baba mkwe, wakati huo zena yupo upande wa wanawake

    "kijana... Nataka leo unisaidie kuswalisha"

    Aliongea baba yake zena ambae ni mkwe wake...

    "sawa mzee... Lazima nifanye hivyo"



    Sasa kama unakumbuka katika sehemu ya kwanza, rahim aliota anaingia msikitini na kuswalisha watu zaidi ya 300, ile haikuwa ndoto bali alipewa maono kwa njia ya ndoto, sasa leo ndio anaitimiza ile ndoto alio ota akiwa anaswalisha watu zaidi ya 300 mana msikiti ulikuwa ni mkubwa sana,... Na ilikuwa ni siku ya Ijumaa...



    Baada ya kumaliza, alitoka msikitini, lakini alipoangalia kwa nje, alimuona mschana mzuri sana mbele yake, katika ile ndoto, iliishia hapa alipoona mschana.... Na mschana huyo hakuwa mwingine bali ni mke wake zena,....

    "nimeisikia sauti yako... Kumbe unaweza kuswalisha mume wangu"

    Aliongea zena huku akimpokea mume mswahafu aliokuwa kaushika,

    "aahhh nilikuwa napenda nikabidhie maiki, ila sio nichukue mwenyewe"



    Sasa wakiwa bado wapo katika eneo la msikitini, walisikika waumini wakisema mambo ya safari ya kwenda hija...

    "napenda sana kwenda hija, lakinj nauli shekhe"

    Rahim alisikia sauti hizo, zikamkuna katika moyo wake na kusogea karibu

    "As Salaam Aleykum ndugu zangu"

    "Aaahhh shekhe, rahim.. Waleykhu msalam warahmatullah wabarakatuh khaifah shekh"

    "Allhamdulillah tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehma zake... Ila shekhe kuna mada nimeisikia hapa ya kwenda hija"

    Aliongea rahim kama vile kuwauliza

    "ndio shekhe wangu... Hio safari inakaribia ila wengi wetu nauli zinatushida kwakweli"

    Rahim ana uwezo wa kulipia nauli hivyo hakutaka kujivunga na mali hizo

    "mimi naomba mjiandae tu, nipo tayari kulipia nauli kwa wale wenye nia na safari hio.. Mana ni jambo jema lenye kuhitaji nia katika moyo"

    Aliongea rahim huku akiwahakikishia safati hio

    "Shekhe... Tunakushukuru sana"

    "sasa nyie tafutaneni wote wenye nia na safari,... Haijalishi mtakuwa wangapi... Kikubwa muwe na imani na safari hio... Mimi nipo tayari kulipia kila kitu"

    Wakati rahim akiyaongea hayo, zena anatabasam tu kwa raha ya yale anayo yafanya mumewe, mana kulipia watu waende hija sio jambo la mchezo mchezo, kunahitajika fungu la uhakika, lakini kwa akina rahim, wana pesa nyingi walizolimbikiza huko benki....

    "basi shekhe wangu.. Tuta wataarifu na wengine... Na Mwenyezi mungu akijaalie kipato chako shekhe,.."

    "Inshallah ndugu zangu... Basi tutaonana panapo majaaliwa siku hio mkiwa tayari, mana kwa sasa narudi arusha"

    "Tunashukuru shekhe rahim... Tunakuombea safari njema.. Na maisha mazuri na mama yetu"

    "Inshallah nanyi pia"



    Akina rahim walitoka hapo na kwenda kwa bibi mzungu... Walipofika walishangaa kumuona jamali na mama yao wakiwepo hapo kwa bibi mzungu, na wakati aliwaacha arusha...

    "heeeee kulikoni tena"

    Aliuliza rahim huku mama akijibu

    "hutaki kaka yako aoe au?"

    "safi sana... Na sio kuoa tu... Natamani aache pombe"

    Aliongea rahim huku jamali akijibu kuwa

    "nina wiki sasa siijui pomne kinywani mwangu... Kifupi nami nimeacha"

    Hadija ambae ndie mke mtarajiwa wa jamali, alifurahi kweli....

    "zena??... Mpe mama hio karatasi"

    Zena alitoa ile karatasi ya vipimo na kumpa mama...

    "heeeeee.... Jamani.. Zena mwanangu una mimba??... Mungu wangu jamani asanteni sana"

    Bibi nae kasikia kuwa zena ana mimba... Saa ngapi hajaja na vigelegele kutoka huko ndani...

    "ururururururururururrurururrururururururururrurururururururuuuuuuuuu"



    MWISHO WA SIMULIZI HIII YA THE ISLAMIC WIFE (MKE MUISLAMU)



    JAMANI SIMULIZI HII ILIKUWA NI SPESHO KWA AJILI YA MWEZI WA RAMADHANI... MANA SIMULIZI ZANGU NYINGI NI ZILE ZA KWICHI KWICHI.. HIVYO ISINGEKUWA VIZURI KWA MWEZI HUO KULETA MAMBO YA KWICHI KWICHI.....







    MWISHO

     

     

0 comments:

Post a Comment

Blog