Search This Blog

Thursday 24 November 2022

KIPAPATIO CHA NANI - 5

 

     

     

     



     Chombezo : Kipapatio Cha Nani Season 1

    Sehemu Ya Tano (5)

     

    “kwani mmetumwa na nani kuja kunikamata?"

    Madebe akauliza swali wakati huo

    Alikuwa anakata kachumbari

    “Mzee Abraham ndugu sijui umemkosea kitu gani?"

    ”yule Mzee fala sana Mamae zake nikitoka huko kituoni nitaenda kumuonyesha kwanini nikiamka Asubuhi natafuna kokoto

    Oyii karibuni tule"

    “ahaaa si tayari tushakula Mzee"

    Ispekta aliitikia kwa kubabaika



    Songa nayo

    Sasa



    “hivi huyu jamaa anajiamini kitu gani mpaka anafikia hatua ya kumtusi mtu mbele yetu?"

    Yule Afande akamuuliza Ispekta Seba kwa sauti ya chini sana

    “sikia ndugu nikwambie hapa hatuna budi kujifanya wajinga juu yake kwa maana tukimfikisha tu kituoni tutamuonyesha kwanini sheria ipo juu ya sheria"

    ”na tumfinye kweli"

    Wakati wanaendelea kuteta wakashtushwa na sauti ya Madebe akiwaambia

    “haya twendeni huko kituoni"

    Wakanyanyuka na kuianza safari

    Watu walioweza kumuona Madebe akiwa kaongozana na Maafande wale walibaki kujiuliza maswali mengi bila kupata majibu

    Walipofika tu kituoni yule Afande akamtandika Madebe zinga la kofi lililotuwa Shavuni kabra hajakaa sawa akamuongeza lingine huku akimfokea

    “pumbavu zako

    Yani kiroboto kama wewe unataka kujifanya upo juu ya Sheria unatusurutisha sisi tukusubiri vuwa mkanda vuwa viatu"

    Madebe akafanya hivyo kisha akaingizwa Selo

    Ispekta Seba akatikisa kichwa kumsikitikia yule Afande

    ”vipi mbona kama unasikitika ndugu? Na kwanini wewe hukumfinya kama ulivyosema tukiwa kule?"

    Ispekta Seba hakujibu kitu akatoka nnje ile anatoka tu pale nnje kuna Pikipiki ilikuja kwa kasi na kupaki maeneo yale akatelemka Mzee Kitwana akiwa ndani ya Kombati iliyosheheni nyota kadhaa kuonyesha ni jinsi gani ana cheo kikubwa sana Jeshini

    Ispekta Seba alijikuta akimpigia Saruti

    ”kwanini umemkamata kijana wangu?"

    “ni agizo Mzee kutoka kwa mkuu wa kitengo"

    Ispekta Seba akajibu kikakamavu

    Mzee Kitwana alimuangalia kwa kumkazia

    ”ni agizo sio?"

    “ndiyo Mzee"

    “niongoze njia"

    Ispekta Seba akamuongoza njia mpaka ofisini walimkuta Mkuu wakituo bwana Mwita akiongea na simu huku miguu kainyoosha na kuiweka kwenye meza alipomuona Mzee Kitwana pale akakata simu na kusimama kikakamavu

    ”karibu ukae Mzee wangu"

    Alimkaribisha na kumuonyesha kiti.

    “sijaja hapa kukaa ila nimekuja kukutahadharisha kitu kimoja naskia Umemkamata Kijana wangu sijui kwa kosa gani? Ila tambuwa kijana anaumwa yule tokea Asubuhi hayupo sawa kihafya sasa ikitokea akafia humu

    Mtamla nyama bila kupenda

    Msiniletee Maiti mimi, mi naenda"

    Mzee Kitwana aliongea kwa upole kisha akatoka

    “muwachieni huyo kijana"

    Afande Mwita akatoa Maagizo kuwa Madebe aachiwe maana ile kauri ya Mzee Kitwana kengere ya hatari ilishaanza kugonga kichwani kwake

    Mzee Kitwana anajulikana kama Mzee wa visasi. Madebe alipoachiwa alimuangalia sana yule Afande aliyempiga makofi mpaka Afande mwenyewe alianza kuingiwa na hofu

    “utalipa hivi kidogo"

    Madebe alitamka hivyo huku akiondoka

    “umemsikia alichokitamka yule Mbwa"

    “usimwite Mbwa ndugu kuwa makini sana"

    Ispekta Seba alimtahadharisha mwenzake na kumtaka awe makini.

    Madebe alishachafukwa alitembea huku akiwa kakunja ndita Akaelekea kutuoni na kukodi Pikipiki

    “wapi mkuu?"

    ”Mikocheni Jomba sijui utanifanyia kiasi gani?"

    “Mikocheni kubwa kaka"

    ”unampata Mzee Abraham?"

    “ahaa yule Mzee Tajiri anaeishi maisha ya kawaida?"

    ”ndiyo huyo ndugu"

    ”mpaka kule nitakufanyia Elfu mbili tu!"

    “poa haina shida"

    Madebe akapanda kwenye Pikipiki safari ya kuelekea Mikocheni ikaanza

    Dereva Pikipiki alichochea moto hatimae wakawasili mitaa fulani hivi Madebe akashuka na kumtaka Dereva amsubilie

    Akaisogelea moja kati ya Nyumba kubwa za kifahari

    Akabofya kengere ya getini dakika si nyingi mlango wa Geti ukafunguliwa

    ”habari yako kaka"

    Madebe alimsalimia mmoja kati ya Walinzi aliyefunguwa mlango

    “safi tu nikusaidie nini?"

    ”nilikuwa nahitaji kuonana na Mzee Abraham"

    ”wee nani yake? Je una miadi nae?"

    ”hapana sina miadi nae kama yupo nenda kamwambie kuwa Madebe Kitwana yupo nnje ya Nyumba yake"

    ”sawa subiri"

    Mlinzi akarudi ndani punde akatoka na kumtaka Madebe aingie ndani

    Madebe alipoingia tu akajikuta kazungukwa na Wanaume walioshiba kitu ambacho kilimshangaza sana nipale alipomuona Mzee Abraham akiwa kashika Bastola

    “ha! ha! ha! ha! Vizuri sana kijana kwa kujileta mwenyewe,,"

    Ikawa kufumba na kufumbuwa Mmoja kati ya wale watu kunyoosha mkono akapuliza Dawa iliyokuwa kwenye kopo kama la Dawa ya Mbu iliyompata Madebe usoni

    Akakinga mikono kufikicha macho huku akirudi nyuma

    Palepale walianza kumshambulia kwa kipigo.

    Madebe alihitaji kujitetea lakini kile kitu alichopuliziwa Kilimnyong'onyesha na kumdebwedesha

    Akapigwa ngumi mateke akadondoka chini.

    Wale watu wakazidi kumpiga

    “sasa mkuu unaweza ukamaliza kazi"

    Mmoja kati yao alitamka hivyo Mzee Abraham akafunga kiwambo cha kuzuia sauti yani mlio wa risasi usiweze kusikika

    Akamrenga Madebe kichwani

    Na kujiandaa kufyatua risasi...

    *****

    “hivi leo kwani ni zamu ya nani kufagia na kudeki choo?"

    “unauliza hivyo wewe kama nani?"

    “khaa wee vipi kwani ulitaka niwe nani?"

    “embu nipishege mie"

    “nikupishe kwani ni zamu yako kuingia au shobo tu!"

    “sasa kama ni zamu yako si ukajisaidie

    Kutusimamia mlangoni na kuanza kutuuliza maswali inahusu"

    “chooni kwenyewe kunanuka uvundo nani aingie"

    Walikuwa ni wadada wakikubwa wakitupiana maneno ya hapa na pale kuhusu swala zima la usafi wasiku hiyo

    Wakiwa wanaendelea kutupiana maneno Mara Ghafla kila mmoja alishtushwa na sauti nzito ya mtu akilia

    Kitendo kilichowafanya wakimbilie ndani makopo wakatupa kule maji mwaah

    “Mamaa nakufaa nisaidienii jamani mi sio mwizii"

    Zilikuwa ni kelele kutoka kwa kijana wakiume mwenye umri wa miaka kama ishilini hivi

    Alipiga kelele huku akijitahidi kuwakimbia watu takribani saba waliokuwa wakimkimbiza lakini hakuweza kufika mbali kwani alijikwaa na kudondoka chini kufumba na kufumbuwa wale watu walishaweza kumfikia

    “tafadhari msiniuwee jamanii,, mi sijaiba Mimi,,"

    Alijitetea kwa kuongea hivyo wale watu wakaangaliana mmoja akatoa ishara kumtaka mwenzake aweze kuandaa kinywaji maarumu

    Kinywaji chenyewe hakikuwa kingine bari ni Sument basi ikaandaliwa yule kijana akashikwa kwa nguvu na kunyweshwa kilazima kisha wakamtaka anyanyuke aelekee nyumbani kwao.

    Kijana hakuweza kuamini kama wale watu wamemuachia huru yani hawakumpiga hata kidogo akashukuru pasipo kufahamu kitu alichonyweshwa hatoweza kufika mbali

    Akanyanyuka na kuanza kukimbia tumbo lilianza kumuuma koo lilikauka akawa anapumua kwa Shida kizunguzungu kikamshika Mara akadondoka chini chali pale pale akapoteza maisha,,

    “wee Mwajuma kwani huko nnje kuna nini?"

    “Mwendo wa Neema wanapita"

    ”kwani hawa Mwendo wa Neema na Masakara wana ndugu?"

    ”mi hata sijui"

    “hivi Serikali itawafumbia macho Watoto kama hawa mpaka lini jamani?

    Watu hatuna amani kabisa juzi tu wamenivuwa chupi"

    “khee unataka kusema walikubaka?"

    “sio walinibaka bali nilibakwa na mmoja kama unakumbuka juzi si nilienda Kawe Beach sasa wakati narudi nikapitia sehemu ile ambayo Wamasai wanapochunga Ng'ombe nikiwa sina hili wala lile nikashtukia Sande akitokea kichakani bila hata kuniuliza akanishika mkono na kunivutia kichakani

    Akaniambia

    “ukitaka nisikuumize wala nisiwaite wenzangu nipatie penzi mwenyewe ukizinguwa utaona, sikuwa na jinsi kukubali,,"

    “duuh pole sana Shogaangu sema bola alivyokuwa mmoja maana usiombe wakiwa kumi au nusu ya kundi maana naskia wapo zaidi ya Mia mbili"

    “duuh mi wangekuwa watatu tu wangentoa roho sembuse hao

    Mia mbili"

    Unampata Irene?"

    ”unamsemea yule mdogo wake Agnes?"

    “ehee ndiyo huyo"

    “kafanyaje?"

    “juzi kati hapa si kabakwa na Watu sita kibaya zaidi alikuwa bikra"

    “Mtumee roho yangu na umri ule alikuwa na Bikra"

    ”ndiyoo"

    “basi makubwa"

    ******

    Wakati Mzee Abraham akijiandaa kufyatua risasi ghafla alishtuka baada kuona kitu si cha kawaida kikitoka mwilini kwa Madebe aliyekuwa kalala chini hajitambui akashikwa na taharuki zaidi Kitu kile kilivyotoka tu kilianza kuwateketeza watu wake,

    Ikawa kufumba na kufumbuwa Bastola aliyokuwa kaishika kupotea mkononi mwake

    Akashikwa na kiwewe akageuka ili akimbie

    Kiumbe huyu hapa mbele yake

    Shetani si Shetani Jini si Jini sijui yukoje akanyoosha mkono na kumkaba Mzee Abraham kisha akamnyanyua na kumning'iniza juu

    ”cheza uchezavyo neng'eneka uneng'enekavyo utajiri wako sikitu mbele yangu naweza kukutawanya sekunde yoyote ile

    Kaa mbali na Madebe usimguse usimghasi

    Kwa chochote atakacho kifanya Mimi nitakuwa nyuma yake

    Narudia tena kukuonya kaa mbali na Madebee"

    Kiumbe kikatoweka Mzee Abraham alidondoka chini kama vile Mzigo wa kuni

    Ziliweza kupita kama dakika tano hivi ndipo Madebe akarejewa na fahamu zake

    Kwanza alijishangaa kujiona akiwa kalala chini

    Akaangalia huku nakule aliona jinsi watu walivyopangaranyika wengine walikuwa wamelaliana

    Akaona mmh hii sasa ni kesi akanyanyuka na kutoka nnje mbio

    Alipotokezea nnje yule Dereva Pikipiki hakumkuta kitu cha ajabu kuna Pikipiki nyingine ilikuja kwa kasi na kupaki mbele yake huku Dereva wa Pikipiki ile akimtaka apande ili waondoke

    Madebe hakutaka kujiuliza sana

    Akachukulia kama ni kawaida ya madereva Bodaboda kuwachangamkia wateja akapanda

    Kitu kingine kilimshangaza ni kuhusu yule Dereva kumpeleka nyumbani kwao Lugalo kapajuwaje? Wakati hakuzungumza nae kitu chochote

    Alishangaa sana

    Tena kafikishwa mpaka mlangoni kwao

    Alipotelemka Dereva Pikipiki akaondoka tena hakudai hata pesa

    Madebe akachoka hoi na kukaa chini kwenye kibaraza cha Nyumba yao

    Akajishika kichwani alianza kukumbuka tukio lilitokea kule nyumbani kwa Mzee Abraham mara ya mwisho alipoliziwa Dawa kitu ambacho kilimfanya apoteze fahamu sasa nini tena kiliendelea

    Au ile Dawa iliwalevya na wao?

    Au yule Dereva aliyenipeleka kule alipigiwa simu na mteja mwingine ndipo akamuachia maagizo Dereva mwingine maana yule wa mwanzo anapajuwa hapa nyumbani?

    Sasa mbona ajadai hela yake?

    Madebe alizidi kujiuliza maswali pasipo kupata jibu





    MWISHO WA MSIMU WA KWANZA



    ENDELEA KUFUATILIA SEASON 2



    MWISHO

     



0 comments:

Post a Comment

Blog