Search This Blog

Thursday, 24 November 2022

PETE YA KIKE - 1

 

     

     



     

     IMEANDIKWA NA : MOONBOY



    *********************************************************************************

    Chombezo : Pete Ya Kike 

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    MWANAUME MSAFI



    Simulizi yetu inaanza rasmi katika mji ambao bado hatuja utambua vyema,.. Lakini ni katika mkoa wa tanga,... Ikiwa ninkatika bustani nzuri sana tena sana,.. Kwa namna moja ama nyingine, ni kwamba bustani hio imetunzwa vyema mpaka kufikia katika hali hio ya kupendeza,.. Alikuwapo malikia mmoja mdogo sana, ila cheo chake ni kikubwa kuliko wote walioweza kumfuata nyuma,.



    Malikia huyo ni mzuri hakuna mfano, lakini sasa kumbe malikia huyo ana wafuasi wake ambao ni wasichana na wana uzuri kama wakwake, yaani kuanzia umri wako pamoja na sura hawakupishana kabisa, ispokua kwa cheo ni yeye peke yake,... Sasa kama kuna malikia basi hata mfalme wao yupo,...



    Malikia alikaa katika kiti chake cha umalikia, nyuma ya kiti kumezungukwa na njiwa wengi sana haswa weupe peee,.. Kwani hata hawa viumbe waishio hapa, hakuna mweusi, bali wote ni weupe mithili ya wazungu lakini hawa hawakuwa wazungu,...

    "nadhani mmekamilika"

    Aliongea malikia huyo ambaye bado hatujajua jina lake na wafuasi wake..

    "Yeeeeeeeee Murati Sabaha (ndio mkuu Sabaha)"

    Waliitikia wale wasichana wapatao wanne kwa idadi ya uwingi wao, hivyo pamoja na malkia wao wanatimiza idadi ya viumbe watano







    "shaimati (shamimu) na maimati (maimuna)... Nime waiteni hapa nina shida moja nanyi"

    Aliongea malkia huyo huku wawili hao wakiitika

    "yeeeeeee Murati sabaha"

    "katika himaya yetu, tunahitaji KIJAKAZI kwa ajili ya kutunza mazingira yetu"

    Sabaha aliongea hiyo lakini wengine walishtuka kwasababu kwa kawaida mazingira yao hujitunza wenyewe, sasa kwanini kuhitajike kiumbe kingine kwa ajili ya utunzaji?

    "yeeeeeee Murati sabaha"

    "shaimati na maimati, nawatumeni duniani mkaniletee kijakazi huyo"

    Aliongea malikia huyo, akimaanisha anawatuma wawili hao kwenda duniani,.. Kwahio inavyo onekana hapo walipo sii dunia... Sasa haijulikani ni wapi hapo walipo...

    "yeeeeeee Murati sabaha (ndio mkuu wetu sabaha)"



    "ila, nahitaji kijakazi msafi"

    Sasa sabaha alipo ongea hivyo, wale wasichana wote wakashtuka... Waliposikia anahitajika kijakazi msafi,

    "Queen sabaha? Huyo kijakazi anahitajika wa kiume ama wa kike"

    Aliuliza msichana mmoja kati ya wale wanaotumwa na mkuu wao

    "nahitaji KIJAKAZI WA KIUME kwa niaba ya mazingira yetu"

    "Queen sabaha, dunia ya sasa sii ya zamani... Kwa sasa kupata kijana msafi ni mtihani kwetu,... Sasa hakuna wasafi duniani"

    Aliongea shaimati ambaye ni mmoja kati ya anaetumwa wakati huo maimati kakaa kimya,...

    "wapo vijana wasafi wengi duniani... Nawapa siku saba, nahitaji kijana mmoja tu, na hio ni kazi nawatumeni mkaifanye"

    Alimaliza malkia sabaha kisha akanyanyuka katika kiti chake, kisha akaingia katika jumba la kifahari ambalo ndilo limezungukwa na bustani nzuri iliopo katika eneo hilo..



    Wasichana hao wanne wakiwa ndani wakiendelea kujadiliana kuhusu swala la Murati (mkuu) Sabaha kwenda duniani kutafuta kijana msafi

    "shaimati, dunia ya sasa imekuwa chafu sana... Tutapata wapi kijana msafi kwa ajili ya mazingira ya himaya yetu"

    Aliongea maimati huku shaimati akimjibu kuwa...

    "hatuna budi kukubali agizo lake, ni vyema kutekeleza.... Hivyo usiku wa saa nane, tuianze safari yetu"

    Aliongea shaimati, wakati huo Saudati na Suariti wapo kimya mana wao hawapo katika safari hio,...



    Sababu ya Saudati na Suariti kuto jumuishwa na safari ya kwenda duniani, wao ni majini ambao hawana asili ya kibinadamu, hivyo wakienda duniani wao wanakua Invisible (hawaonekani)... Lakini hawa wawili Shaimati na maimati wao wana asili mbili, asili ya jini na ubinadamu na hawa wana familia zao huku huku waishio wao, na wazazi wao pia wana asili mbili... Sasa hawa saudati na Suariti wazazi wao ni asili moja tu ya ujini... Hivyo duniani hawato onekana, hususan kwa kazi hio inatakiwa waonekane...



    Shaimati na maimati kwa majina ya upande wa kibinadamu wanaitwa MAIMUNA NA SHAMIMU (maimati na shaimati) haya majina ya Maimati na shaimati wamepewa wakiwa huku kwenye himaya yao japo wamezaliwa huku huku lakini bado wazazi wao wana asili mbili,... Na kila mmoja wao ana wazazi wake.... Ispokuwa sio wote kuwa wazazi wao wana asili mbili... Na hata Sabaha pia yeye hana asili mbili, na ndio maana akawatuma wale wenye asili mbili, mana yeye akienda hato onekana kama wengine, bali atakuwa upepo tu



    SASA TUACHANE NA HUKO KWA MAJINI... TUJE HUKU DUNIANI



    Alikuwepo msichana mmoja mzuri sana alieumbika, yaani mwili wake umegawanyika vizuri,.. Hii ni mkoani tanga katika mtaa uitwao UZUNGUNI, na hapo ni katika duka moja la nguo za Kiislamu alizokua akiuza msichana huyo mwenye umbo na uzuri wa kipekee,.. Mambo ya tanga hayo....



    Kama unavyojua wasichana wengi wa tanga ni wao na mahijabu,.. Ukimkuta ndani na hicho kipande cha kanga, utafurahi mpaka upasuke, mlioishi tanga nadhani sio mageni kwenu,... Sasa wakati msichana huyo anapanga nguo, ghafla kuna gari ilisimama katika duka hilo... Alikuwa ni mwana mama mmoja ambaye ndio boss wa duka hilo...

    "Faima Asalam Aleykh"

    Alisalimia mwanamama huyo kan kwamba huyo msichana muuza nguo anaitwa faima au ukipenda muite (Fei)..

    "waaleykh msalam mama karibu"

    "ahsante, nimekuja kuangalia mzigo ulio isha"

    "ok.. Hapa naona kanzu zimekwisha ipo pisi moja tu"

    "ooohhh, aah mzigo umeenda enda kiasi"

    "ndio mama, sasa kidogo biashara sio mbaya"

    "ni kweli, sasa wacha kesho nielekee dubai kuleta mzigo"

    "ni vyema, mana sio mpaka ziishe kabisa"

    "sawa, wacha nikafanye utaratibu wa safari mapeema mno"

    Aliongea mama huyo huku akipanda gari yake na kuondoka,... Huyo ndio boss wa faima au fei,...



    Sasa tukija huku katika mtaa mwingine uitwao PONGWE, alionekana ostadhi mmoja aliovalia vyema kabisa kwa mavazi yalio mjulisha kuwa yeye ni ostadhi ama shekhe... Aliingia katika nyumba moja ya kizamani sana kana kwamba ndipo wanapo ishi katika jengo hilo,.. Tena linaonekana ni yale majengo ya kiserikali... Yale majengo ya mkoloni

    "Asalam Aleykh baba"

    Kijana huyo alimsalimu baba yake

    "waaleykh msalam mwanangu hali yako"

    "aahh swalama tu"

    "mbona wasema Aah, kunani tena"

    "baba? Tuyaache hayo mana ni masala ya kazi tu... Mama yuwapi"

    "mamayo kaenda teka maji kisimani huko"

    "wacha nikamsaidie basi"

    Aliamka kijana huyo na kuvua kanzu yake kisha akachukua baadhi ya ndoo ambazo zipo tupu, kisha akaelekea kisimani ambako mama yake naye kaelekea huko... Alikua ni kijana mwenye kujielewa na kuijua thamani ya wazazi wake,... Inashangaza sana kuwa wapo vijana wasiojua thamani ya wazazi....



    "suria? Haya nini kukuru kukuru na ndoo za maji"

    Alikua ni mama yake suria, kana kwamba kijana huyu anaitwa suria...

    "Asalam Aleykh mama"

    "Waleykh msalam,.. Haya kwani wabeba ndoo kwenda kisimani"

    "mama, kwani mimi sipaswi kukusaidia? Tena hio iwe ndoo ya mwisho wewe enda na ukae usirudi, kama ni mapima nitajaza mie"

    Aliongea suria, ila kwa rafudhi ya tanga, mchanganyiko na Pemba hivi

    "ni sawa lakini umeshachoka weye,.. Haya vipi kazi uliofuata huko yapo mafanikio"

    Mama yake suria alimuuliza mtoto wake mana kwa sasa suria hana kazi kabisa toka amalize alimu yake ya chuo...

    "mama we Enda tu takuja ongea nyumbani, lakini hali ya kazi bado mbaya mamy"

    Suria aliposema hivyo mama alinyong'onyea sana, mana furaha yake ni mtoto wake apate kazi...... Basi mama aliendelea na safari yake ya kurudi nyumbani toka kisimani...



    Ilipofika usiku mida ya saa mbili,.. Suria akiwa na baba yake toka msikiti kuswali,..

    "baba, kuna mahali nilikwenda mchana, walinambia hawawezi kunilipa mshahara kutokana na elimu yangu"

    Aliongea suria, huku baba yake akisikitika sana kwa taarifa hizo, mana suria ana elimu kubwa sana, kaomba kazi serikalini lakini bado hapati kwasababu ya elimu yake imebezi sana katika upande wa dini,.. Ila serikali humfanyia fitina kwasababu ana elimu ya juu, yaani suria amepiga kitabu vibaya mno,.. Elimu ya dunia humwambii kitu... Sasa hio elimu ya dini ndio kabisa usiseme,... Quran imejaa kichwani mpaka basi... Vyeti vyote anavyo lakini ana mwezi wa sita sasa hapati kazi...

    "lakini suria mwanangu... Kwanini usiachane na taasisi za serikali... Hebu angalia kwenye makampuni binafsi"

    "baba, huko ndio kabisa wanasema hawawezi nilipa kutokana na elimu yangu... Wanasema kutokana na elimu yangu napaswa kulipwa milioni nane mpaka kumi... Lakini wao hawana uwezo"

    Aliongea suria na wakati huo walishafika nyumbani kwao... Wakiwa mezani wakivuta subra ya chakula cha usiku

    "kwanini usingekubali tu kwa huo mshahara wao"

    "niliwaambia kuwa nipo tayari kwa mshahara wao.. Lakini wakasema, siku serikali ya haki za kazi ikija kukagua mishahara ya wafanyakazi ikakuta wangu ni mdogo.. Watafunguliwa mashtaka... Hivyo hawawezi kunipa kazi"

    "aahhhh, lakini Usijali baba, utapata kazi.. Muamini mwenyezi Mungu kwa kila jambo.. Na hakika hata ukikosa sema alhamdulilah"

    Aliongea mzee huyo ambae yeye alikua akifanya kazi katika vituo vya reli hapo tanga,.. Na inasemekana ya kwamba mzee huyo alitakiwa kuwa tajiri mkubwa lakini pesa zake zote alimsomesha suria, sasa suria ana elimu ya juu lakini hapati kazi kutokana na figisu figisu za hapa na pale... Mama aliandaa chakula kisha akawa anatoka nje kwenda kumwaga maji machafu.... Lakini ghafla alimuona mtoto wake wa kike aitwaye ASHA

    "heee asha mwanangu, ulikuwa wapi mpaka saa hizi weye"

    "mama nilikua kwa rafiki zangu"

    Aliongea asha huku akitaka kuingia ndani, lakini vazi aliovaa ni fupi mno kana kwamba hawezi kupita mbele ya baba na mdogo wake wa kiume

    "hebu subiri kwanza... Hii nguo ni sahihi kuivaa asha... Mbona unantia aibu mwanangu, hebu muone mdogo wako alivyo.. Mbona havaagi suruali za ajabu"

    Aliongea mama huyo wakati huo huku ndani baba na mtoto wanakula

    "nyie si mmemsomesha suria,.. Sasa tutaona mtu aliosoma na ambae hajasoma nani wa muhimu... Yeye kasoma sana ndio mana hana tabia mbaya, mimi nimeishia kidato cha nne, ndio mana nina tabia mbaya"

    Aliongea asha huku akitaka kuingia ndani,... Sasa hapo kuna vita kali kati ya asha na wazazi wake... Kana kwamba wazazi walizidi kumsomesha mtoto wa kiume sana tena kwa kumpenda mno huku wakiamini ya kwamba mtoto wa kike ni wa kuolewa tu...

    "asha, hebu vaa hii kanga.. Baba yako yupo hapo ndani"

    Mama alimvalisha mtoto wake kanga ili aweze kupita mbele ya baba yake

    "Shikamoo baba"

    Asha alimsalimia baba yake huku akipita

    "marahaba mama.. Haya saa hizi saa tatu kasoro hii ulikua wapi"

    "nilikua kwa rafiki zangu"

    "saa hizi.. Rafiki zako wametulia kwao wewe umewafuata"

    "ndio, sasa nitakaa na nani"

    Aliongea asha huku suria akidakia

    "dada asha, hayo sii majibu ya kumjibu baba... Hebu kuwa na heshima kwa nyakati zingine dada"

    "we nawe sijaongea na wewe.... Siongei na watu wa vuo vikuu mimi"

    Aliongea asha kitu kilichomfanya suria kukaa kimya mana hawezi kubishana na dada yake....

    "basi mama nenda ndani tu"

    Aliongea baba lakini ni kishingo upande tu...



    Ilipofika usiku wa saa nane, kandokando ya bahari walionekana wasichana wawili warembo sana wakiwa na mikia ya samaki, yaani mithili ya nguva,.. Lakini walipopigwa na hewa ya duniani, ile hali ya unguva iliwatoka na kuwa na miguu ya kawaida,.. Kwa kawaida majini hutoka saa saba za mchana lakini sio wote wenye uwezo huo...  Wale wanaotoka mchana ni wale wenye asili moja tu,... Ila hawa wenye asili mbili wao hutoka muda wowote, iwe mchana au usiku... Ni maamuzi yao wenyewe... Ila kwa hawa wameamua kutoka usiku... Ni sekunde chache kutoka baharini mpaka barabarani wakiwa wamevalia nguo nyeupe mithili ya malaika, ila hawa ni majini wema, mana kuna majini wabaya na wazuri, sasa hawa ni wale wazuri..



    "shaimati, naskia sauti za miziki usiku huu... Kweli kutakua na wasafi kweli??"

    Aliongea maimati ambaye ni maimuna, (muna)...

    "Afadhali waliopo katika muziki... Ona wale wasichana... Wamevalia mavazi ya aina gani... Ile si nguo ya ndani kabisa ile"

    "haaaaaaa Kiukweli haifai hata kuangalia... Shaimati, mimi naona turudi tulipotoka... Wacha tukamweleze Murati sabaha kuwa katika dunia ya sasa hakuna wasafi"













    Katika dunia hii kuna viumbe wengi sana ambao wengine hawana asili ya binadamu,.. Lakini katika simulizi hii inaelezea viumbe aina ya majini, lakini wanaoelezewa hapa ni wale majini wa baharini, sio majini wote wa baharini ni wazuri, ila hapa tutaelezea wale wazuri, mana wabaya ndio hao mashetani.. Hivyo hapa hatuelezei mashetani... Mana simulizi ilio elezea mashetani tayari ilishatoka inaitwa THE MEAT OF MY MOTHER, hivyo hapa tunaelezea wale majini wema, wazuri, wanaopenda kusaidia watu...



    Murati sabaha ni jini mkuu katika himaya yake, sio kuwa bahari nzima ni yeye mwenyewe, lahasha, bali zipo himaya nyingi ndani ya bahari.. Mfano ni kama tukisema Jiji la Dar es Salaam ndio kama mfano wa bahari nzima,... Sasa himaya zipo nyingi mfano wa Majimbo au kata vitongoji vya jiji hilo au bahari hio...



    Sasa katika himaya nyingine ndani ya bahari, wanamiliki binadamu ambao wameamua kuwasaidia kwa kuwapa kazi za kutunza bustani, Sasa Murati sabaha na yeye anataka KIJAKAZI WA KIUME kwa ajili ya kutunza bustani iliopo kwenye himaya yake au jimbo lake... Wanaotakiwa kuja huku Haijalishi jinsia, awe wa kike au wa kiume, kikubwa awe msafi,



    Je unajua usafi huo ni upi??.. Haimaanishi msafi wa nguo, au msafi wa roho... Au msafi wa kuoga kila mara.. Bali anahitajika msafi ambaye toka kuzaliwa kwake hajawahi kufanya mapenzi,.. Na hahitajiki mtoto, bali ni kuanzia umri wa miaka 20 kwenda mbele, ilihali ule umri wa balehe umeshapita bila ya mhusika kutamani mapenzi... Hivyo wakisema neno msafi.. Yaani ambaye hajawahi kufanya mapenzi, huyo ndio msafi....



    Murati sabaha baada ya kupata wazo la kuhitaji kijana wa kazi,.. Aliwatuma wafuasi wake ambao wana asili mbili katika mili yao,... Shaimati na maimati, hayo ni majina yao ya upande wa baharini, ila huku dunia wanaitwa Shamimu na Maimuna,... Wao wana uwezo wa kuonekana au wasionekane, ila Murati sabaha na wale wengine waliobaki, wakija duniani hawaonekani kwasababu asili yao ni moja.... Hivyo kawatuma maimuna na shamimu wamtafutie mfanyakazi wa kutunza bustani yao..



    Saa nane za usiku shaimati na maimati wanafika katikati ya mkoa wa tanga,... Kitu cha kwanza walisikia sauti za muziki ukilindima katima katika tundu za masikio yao



    "Afadhali waliopo katika muziki... Ona wale wasichana... Wamevalia mavazi ya aina gani... Ile si nguo ya ndani kabisa ile"

    "haaaaaaa Kiukweli haifai hata kuangalia... Shaimati, mimi naona turudi tulipotoka... Wacha tukamweleze Murati sabaha kuwa katika dunia ya sasa hakuna wasafi"



    Aliongea maimuna au maimati kuwa ni bora warudi kule walipotoka, kwasababu hali walio ikuta hawawezi kupata binadamu alie msafi,...

    "hapana muna,... Ukumbuke kuwa Murati sabaha tulimweleza ya kuwa, kwa dunia ya sasa hatuwezi kupata binadamu msafi tofauti na watoto chini ya miaka kumi... Lakini alikataa na kudai kuwa wapo wengi sana.. Hivyo kwa mimi kurudi ni ngumu maimati"

    Aliongea shaimati kumsihi maimati asirudi walipo toka,.. Kwani watagombezwa na mkuu wao ambae kawatuma kuja kutafuta kijana msafi

    "lakini shaimati, wewe unaonaje hii hali? Na ukumbuke tumepewa siku saba tu ndani ya dunia hii"

    "ni vyema tumalize siku saba turudi tukiwa hatuna, kuliko leo leo turudi"

    "sawa, nimekuelewa... Sasa haya mavazi meupe vipi"

    "ni lazima tupate nguo za kibinadamu"

    Majini hao walishauriana juu ya upatikanaji wa nguo na kupata muafaka juu ya hilo...



    *************************************



    Tukija huku kwa akina surian au suria akiwa na mpenzi wake... Sasa hapa inashangaza kisogo kwani hapa yupo na mpenzi wake tena walikuwa wakilifaidi tunda la msimu wa siku hio... Ila usiku wa jana kabla ya kulala kwake alikuwa kwao na familia yake, lakini usiku anaonekana yeye na mpenzi wake,... Ila sauti ilikuwa ni ya suria pekee...



    Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, mzee Rashidi ambaye ni baba yake suria ama sua, alifika katika chumba alicholala suria kwa niaba ya kumwamsha ili waelekee msikiti kufanya ibada ya Subuh...

    "suriaaa"

    Aliita mzee Rashidi huku akigonga mlango

    "naam baba"

    "swalaaa swalaaa swalaaa"

    Mzee Rashidi alimwamsha kwa maneno hayo ambayo hutaamkwa kwa nyakati za swala ya asubuhi... Basi suria aliweza kukurupuka, lakini ghafla anaanza kukasirika bila sababu... Aliusogelea mlango na kuufungua bila wasiwasi wa mzee kumwona mwanamke aliekuwa naye usiku wa leo....

    "haya twende basi... Mana unatakiwa uka adhini wewe"

    Aliongea mzee Rashidi akiwa na maana ya kuwa, suria ndio mpiga adhana wa siku hio.... Lakini suria hakutaka kumficha baba yake....

    "Assalam Aleykh baba?"

    "waalekh msalam,.. Vipi kheri?"

    "aahhh baba, sii kheri sana"

    Suria alijibu kuwa hakuna usalama sana....

    "nini tena"

    "jana nilipitiwa na usingizi hadi kusahau kusoma dua ya kulalia"

    Aliongea suria huku mzee wake akiwa kasimama nje ya mlango wa chumba cha suria...

    Sasa baba yake kuskia hivyo tu, akajua suria kuna jambo limemkuta usiku wa leo

    "basi we kakoge utanikuta nje hapa"

    "kwanini usitangulie baba.. Mana nataka zifua nguo hizi.. Mana dada aisha akijua atancheka kweli yule"

    "sawa pia.. Mimi nitakusubiri baba.. Wewe enda kakoge kisha nikute nje"

    Aliongea mzee Rashidi, huku akitoka nje,... Hawa wanaongea rafudhi ya pemba hivi.. Hivyo hio Enda kakoge ni rafudhi yao... Basi mzee Rashidi alitoka nje na kuanza kushika udhu (kujisafisha ili aweze kuswali)... Wakati huo suria aliingia bafuni na kuvua nguo zile ambazo alilalia leo..

    "daahh uyu mwehu leo kaniweza kweli huyu... Yapata mwezi wa sita sasa hajaja.. Kaona nimejisahau tu usiku kaja..."

    Aliongea suria huku akifua nguo hizo ambazo amezichafua baada ya ndoto ya usiku akiwa na mpenzi wake,... Na hio ni mbinu ya jini mahaba ambaye tabia yake ni kuchafulia watu bila sababu....



    Jini mahaba ni mmoja wa majini ambao ndio mashetani, wao hawana jema nawe binadamu... Na jini mahaba hua anawafuata wale wanaume ambao hawana wapenzi, au wana muda mrefu bila kufanya mapenzi, na hata hawa jini mahaba wao pia hawataki mwanamume mchafu ambae ana zini kila wakati.. Na hua hawataki zile mbegu zinazo mtoka mwanaume... Mana kwao ni uchafu, hivyo anamfuata mwanaume na kuanza kufanya nae tendo la ngono, sasa pale mwanaume anapokaribia kufika mshindo, huyu jini mahaba yeye hujitoa ili zile mbegu za kiume zisimguse... Hivyo shida yake ni kukuchafua wewe na sio yeye.. Na ndio maana hataki uchafu wako,... Uchafu ubaki nao mwenyewe, kama ni raha keshapata sasa wewe jichafue mwenyewe.... Ndio asubuhi unajikuta tayari umeshaloa... Na pia wapo majini mahaba wa kiume ambao huwafuata wanawake,.. Ila kwa wanawake sio sana... Ila majini mahaba wa kike, hupenda kuwafuata wanaume wasio na wapenzi au wenye muda mrefu bila kufanya mapenzi....



    Saa moja za asubuhi, suria na baba yake wana tabia ya kufanya mazoezi baada ya ibada ya asubuhi... Hukimbia kilometa kadhaa kwa ajili ya kuilinda miili yao, na hio ni faida moja wapo ya kidunia kwa wale wanaoswali swala za asubuhi... Wakati huo wanaingia nyumbani ili waweze kuoga....



    Ilipofika saa tatu wakiwa mezani wanapata chai,... Wakati huo suria kaweka vyeti vyake mbalimbali katika meza... Mzee Rashidi akiangalia hivyo vyeti, anajua hio ndio pesa yake iliipotea miaka yote hip... Unaambiwa mzee huyo alimuwekezea sana mtoto huyo aweze kusoma kwa bidii kwani ndie mwokozi wao,... Na kweli kamsomesha suria vizuri sana, ila ukubwa wa elimu yake unamkosesha kazi katika baadhi ya kampuni binafsi, kwani akienda serikalini anaambiwa aambatanishe vyeti vyake na karatasi inayo muonyesha uzoefu wa kufanya kazi kwa miaka mitatu... Sasa mwanafunzi katoka shule mwaka huu, je huo uzoefu wa miaka mitatu kautolea wapi... Hicho ni kikwazo ambacho anakutana nacho suria katika ngazi za serikali.... Na huko binafsi wanamwambia, kwa ukubwa wa elimu yake hawawezi kumlipa...



    "sasa mwanangu... Mimi nikushauri jambo moja kama utalikubali"

    Aliongea mzee Rashidi, mana suria akimaliza kunywa chai anaondoka zake kwenda kutafuta kazi...

    "ushauri gani baba..."

    "kwanini usitafute kazi ya ualimu tu..."

    Aliongea baba yake suria,

    "baba,... Yaani elimu nilio nayo, kila sekta hawaitaki... Nilikwenda katika shule moka kubwa hapa mkoani Tanga,... Tena ni shule ya sekondari ya mtu binafsi,.. Shule kubwa sana katika mkoa huu... Lakini mkuu wa shule hio alipo ona vyeti vyangu.. Alinuna hapo hapo... Nilipotoka ofisini kwake, nikakutana na head master... Akaniuliza kama nimefanikiwa... Mana yeye ndie alienielekeza kwa mkuu wa shule hio.. Nikamwambia kuwa mkuu nimemwonyesha vyeti vyangu lakini hakunijibu zaidi ya kuniambia hakuna nafasi.... Yule head master akaniambia, nafasi zipo lakini elimu yangu ni kubwa kumzidi yeye.. Hivyo naweza kumpindua katika kiti chake"



    Aliongea suria kama kumpa stori baba yake aliotaka akaombe kazi ya ualimu,...

    "daaaahh pole sana mwanangu... Ila mimi nilikua na maana uende kufundisha shule za dini"

    Aliongea mzee huyo akimaanisha kua suria akaombe kazi ya ualimu wa shule za Kiislamu, akafundishe somo la ISLAMIC KNOWLEDGE, na hilo ni somo la kiislamu na ni shule ya sekondari inayofundisha masomo yote lakini ni shule ya Kiislamu... Ila hata za kawaida zipo ila mpaka uongozi uamue kuweka somo hilo..

    "labda nijaribu huko kama nitapata"

    "ah ah, usiseme kama... Sema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nitapata"

    "sawa baba"

    "ila, kama unakwenda huko... Punguza hivi vyeti.. Nenda na vyeti husika.. Hivyo vingine acha"

    Aliongea mzew Rashidi, mana suria ana vyeti vingi... Yaani kasoma vyuo vingi sana na kila chuo ana cheti chake alicho somea jambo fulani,..

    "sawa baba"



    Sasa ikiwa ni nyakati za saa nne asubuhi, katika duka la nguo za jinsia zote.. Waliingia wale wasichana wawili ambao wametokea katika dunia nyingine ya chini ya maji.. Na duka walilo ingia ni duka ambalo anauza Faima...

    "karibuni, karibuni"

    Faima alikuwa mkarimu kwa wateja wake, japo walikuwa wamevalia mavazi meupe peee...

    "nipatie hijabu lile pale"

    "lile jeusi"

    "ndio"

    Aliongea maimati huku faima akitungua hijabu hilo na kumkabidhi maimati... Papo hapo na shaimati nae akaagiza hijabu lake lenye rangi ya ugoro ugoro hivi...

    Walielekezwa mahali pa kubadilisha nguo mana wamedai kuzivaa kwa nyakati hizo... Faima hana wazo lolote kuwa wasichana hao ni majini,.. Shaimati na maimati walilipa bidhaa zile kisha wakaondoka... Faima alishangaa sana pesa zao kuwa mpya kuliko mpya za benki... Ila aliona ni wateja tu....

    "maimati..."

    "yeeeeeee"

    "toka jana usiku tuingie duniani,.. Kwa mara ya kwanza nimeona msichana msafi"

    Aliongea shaimati kuwa leo kaona msichana msafi....

    "shaimati... Nadhani sisi tumetumwa mvulana, sasa wasichana wanini? ... Najua yule msichana alietuuzia hizi nguo ni msafi.. Lakini sifuatilii hilo"

    Aliongea maimati huku wakiendelea kutembea kwa hatua kubwa kubwa,..

    "sawa, lakini niliongelea tu"

    Shaimati alikubali huku maimati akisema kuwa

    "sasa hapa mimi naona tujibague... Kila mmoja apite njia yake"

    Aliongea maimati huku wakilifanya jambo hilo, yaani majini wakijadili jambo, ni wakati huo huo linafanyika..



    Shaimati na maimati kila mmoja na njia yake,... Na wao hawana uwezo wa kugundua moja kwa moja kuwa mtu huyu ni msafi,... Ila ugunduzi wao wana uwezo wa kuongea na kiumbe kiitwacho QARENA, kiumbe hiki huzaliwa na kila binadamu... Na kiumbe hiki sio salama sana katika maisha ya binadamu... Na hakuna binadamu anaweza kuongea naye, ispokuwa viumbe ndivyo vinaweza kuongea na QARENA, ambaye ni pacha wa binadamu.... Huyu kiumbe kazi yake ni kitoa taarifa za binadamu kwa viumbe wengine au wanadamu wenye upeo wa kweli kama vile waganga wa kienyeji wale wa kweli,.. Watu wenye majini marohani pale majini yanapo wapanda watu.. Ndipo mtu huyo ana uwezo wa kuongea na QARENA,... Sasa majini hawa wanapata taarifa za mtu kupitia QARENA, na QARENA ndio kazi yake kitoa umbea wa binadamu, ila kama binadamu hajui kitu, basi hata QARENA pia hajui, hivyo wewe ukijua tu unakwenda kukojoa basi hata QARENA anajua unakwenda kukojoa....



    Wakati huo suria yupo mbio mbio kwenda katika shule moja ya Kiislamu ambayo baba yake kamwelekeza akajaribu hapo kama ataweza kupata kazi,.. Hivyo alikuwa ana haraka mno,...



    Sasa huku kwa shaimati, ukumbuke wamegawana njia, kila mmoja apite njia yake ili kuweza kupata kile walicho tumwa... Mana majini ndio wanatumwa ila binadamu huagizwa..

    Shaimati alikutana na dada yake suria akiwa kavalia vazi la kanga moja, sasa shaimati yeye anajali sana wasichana wenzake... Vazi hilo la kanga moja lilimfanya aisha awatoe wanaume udenda, kwani vazi hilo lilikuwa likionyesha dhahiri vazi la ndani (chupi)... Hivyo vidume macho kwa aisha ambaye ni dada yake na suria,... Na nyakati hizo alikuwa akitoka sokoni... Shaimati alikuwa hana kitenge lakini ghafla tu kaonekana kashika kitenge na kumvisha aisha... Lakini aisha hakujua kama kavishwa kitenge, ila akijiangalia anahisi kuwa na ile ile kanga moja.... Shaimati hio kazi yake, anapenda sana kujali wanawake wenzie... Hivyo aliendelea na kazi iliomleta duniani.... Unajua mwanamke anafanyaga makusudi kuvaa nguo fulani,.. Na anajua lazima wanaume wampigie mbinja na wengine kumuita wengine kumsifia kutokana na muonekano wake.. Sasa alifika mahali alishangaa mbona sifa alizokuwa akipewa awali sasa hazipo.. Na alikuwa kila kipishana na mwanaume lazima ageuke, lakini sasa hivi hakuna anaemuangalia... Chezea kitenge wewe... Sasa alipofika nyumbani alishangaa kupewa sifa na mama yake...

    "heeeee, aisha mwanangu... Kweli mungu mkubwa, siamini ulivyotoka na jinsi unavyorudi"

    "una maana gani mama"

    "kile kikanga ulicho toka nacho.. Kiukweli sikukipenda kabisa... Lakini nimefurahi umevalia kitenge kwa juu"

    Aliongea mama yake aisha lakini aisha akijiangalia, anajiona ana kile kikanga ila watu wanaomuangalia wanaona bonge la kitenge tena kipyaa... Aisha hajaelewa kabisa mama yake ana maanisha nini, hivyo walikua ni watu wasio elewana



    Sasa huku dukani kwa faima,.. Kumbe shaimati karudi huku dukani tena, yaani hana mzuka wa kutafuta KIJAKAZI WA KIUME, bali kafurahi sana kwa kuona msichana ambaye hajawahi kuguswa kwa namna yeyote ya kimapenzi,..

    "ooohh karubu tena"

    Faima alimkaribisha shaimati kana kwamba labda kapenda kuja kuongeza nguo nyingine, kumbe yeye ndio kapendwa kwa usafi wake...

    "usijali,... Kiukweli wewe ni mrembo sana"

    Aliongea shaimati huku faima akisema

    "ni kweli ila sijakuzidi wewe"

    "mmmhh urembo wangu ukiujua, hutokula siku nzima"

    Aliongea shaimati akimaanisha kuwa akimweleza jinsi alivyo uhalisia wake, basi hatokula siku nzima...

    "kwanini nisile siku nzima"

    "ah tuachane na hayo.. Vipi umeolewa wewe"

    Shaimati alimuuliza swali hilo ilihali anajua faima ni bikra...

    "ndio, nimeolewa na nina mtoto mmoja"

    alijibu faima, huku shaimati akicheka na kusema kuwa

    "inaonekana unapenda kuolewa sana"

    "nimekwambia nimesha olewa na nina mtoto"

    "ila uaijli, hivyo vyote vina wakati wake... Utaolewa na utapata mtoto"

    Aliongea shaimati, lakini faima alishtuka mana anamdanganya mtu, wakati mtu mwenyewe anajua ukweli wake....

    "sawa Nashukuru kwa ushauri wako dada"

    faima alishukuru kwa kupewa ushauri

    "ila nimependa kwa jinsi ulivyo jitunza... Hebu niambie, umewezaje hadi kufikia miaka 21 bila kujichafua"

    Aliongea shaimati na kumfanya faima azidi kushtuka... Yaani mpaka miaka yake kaitaja...

    "umejuaje kuwa nina miaka 21 na nani kakwambia mimi nina bikra"

    "usijali faima... Sisi ni sote ni wanawake hujuana sana jinsi tulivyo"

    "na jina langu nani kakuambia ingali ndio mara ya kwanza nakuona"

    Aliuliza faima ila hapo hofu ilianza kumjia... Mana mtu anajua siri zake zote

    "alafu kumbe una mchumba, mbona sioni pete ya uchumba"

    Yaani shaimati yeye hapendi kujibu maswali, wewe ukiuliza na yeye anauliza, hio ndio tabia ya majini, wao kutoa majibu ni ngumu ila wao wanataka majibu pale wanapo uliza

    "ndio, ninae... Na huyo ndio atanioa"

    "na yeye pia hajawahi kama wewe"

    "ndio,.. Tuko sawa na yeye pia hawajawahi kufanya mapenzi"

    Sasa shaimati kuskia hivyo, alishtuka na kumuuliza faima kuwa

    "yuko wapi huyo mwanaume msafi... Anaishi wapi na anaitwa nani"



    Sasa tukija huku kwa suria, akiwa katika harakati zake za kwenda shuleni tena kwa kutumia usafiri baiskeli aina ya sehewa,... Mbele ya kitenga cha baiskeli kaweka vyeti vyake... Alikuwa na haraka mno... Sasa alifika kwenye kona fulani almanusura amgonge dada mmoja kwa haraka zake...

    "ooohhh samahani dada yangu... Kwanza Assalam Aleykhum"

    Suria alimsalimia mdada huyo ambaye kavaa baibui au hijabu, wengine huita nikabu.. Japo kilabu ni kile kininja...

    "waaleykh msalam, haya mbona wataka nigonga na usafiri wako"

    Aliongea dada huyo huku suria akiomba radhi

    "niwie radhi dada yangu... Nipo katika upesi kuwahi mambo yangu"

    Aliongea suria, kisha dada huyo akasema kuwa

    "sawa kaka... Unaweza kwenda"

    Aliongea dada huyo, lakini suria alisisimkwa na nywele zake, ikiwa na maana kuwa aliopishana nae sio binadamu wa kawaida....

    lakini sasa kumbe huyu dada ndio maimati mwenyewe, mmoja wa wale majini waliokuja duniani kutafuta MWANAUME MSAFI











    Qarena ni kiumbe ambaye huzaliwa na kila binadamu alioko duniani, na kiumbe hiki hakionekani na mtu yeyote, hata jini mwenyewe hakioni hiki kiumbe... Lakini kwa sauti unaweza kukisikia ila sio kwa binadamu bali ni kwa viumbe kama vile jini, wanyama na vitu vingi ambavyo viko tofauti na binadamu



    Binadamu ana malaika watatu, MBELE, KUSHOTO NA KULIA... Sasa Hawa Malaika wako wa kushoto na kulia na mbele ni wazuri wote ila kila mmoja ana kazi yake.. Malaika aliopo upande wa kulia, yeye huandika matendo mazuri ambayo unayatenda duniani... Na huyu wa upande wa kushoto, yeye huandika matendo maovu ambayo unayatenda duniani hivyo hakuna tendo lako linalo potea na yote utayakuta kwa mungu... Sasa huyu wa mbele,. Kazi yake yeye ni kukuongoza njia ilio sahihi... Ila ukikataa hakulazimishi... Yeye anakupeleka kwenye nyumba ya ibada wewe unakwenda disko, huko haendi... Atakusubiri utoke ajaribu tena kukuongoza mazuri mana ndio kazi yake... Na hata hawaa waandishi wa kushoto na kulia wakiona unaingia sehemu chafu hata wao hawaingii... Sasa unaye ingia nae disko au baa, au danguro... Ama sehemu yeyote yenye starehe... Pale unaingia na Qarena, huyo ndio unaingia nae.. Afu unakutana na shetani huko huko mana nyakati hizo malaika wapo nje wakikusubiri...



    Sasa huyu Qarena ndio ana urafiki na mwandishi wa kushoto ambaye anaandika matendo mabaya... Hivyo wewe ukitoka disko,.. Mwandishi wa kushoto anamuuliza Qarena yale ulio yafanya ndani, kisha anaandika mabaya ulio yafanya huko ndani... Na huyu Qarena yeye anakaa nyuma.. Ukumbuke nimetaja MBELE, KUSHOTO NA KULIA... sasa huyu Qarena yeye anakaa nyuma.. Na yeye anatunza kumbukumbu zako zote tofauti na hawa wa kushoto na kulia.. Qarena yeye anakusanya takataka zako zote ambazo unazijua,... Hakuna anayeweza kumuona Qarena ispokuwa wao wenyewe tu ndio wanaweza kuonana... Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kuona viumbe vyake.... Labda kama nawe una nafasi ya ukiumbe ndio utaweza kuona au kusikia sauti za viumbe wenzako... Au kiumbe aamue kuonekana mbele za wanadamu... Kwahio Qarena yeye anatunza kumbukumbu zako unazofanya na ulizofanya toka kuzaliwa kwako.. Na ukifa sio lazima na yeye afe, anaweza kubaki na kuendelea kuishi kwenye ukoo wenu...



    SAMAHANI SANA NDUGU WASOMAJI WANGU... MIMI HUA SIPENDI MSOMAJI WANGU AWE ANAJIULIZA MARA KWA MARA NA NDIO MAANA NIKAANZA NA UFAFANUZI WA HIKI KIUME KIMBEA MBEA... HIVYO MSAMAHA MNISAMEHE, ILA NI KATIKA HALI YA KUWAELEWESHA VYEMA ZAIDI... KAMA KUNA KOSA HAPO NIMETELEZA



    "sawa kaka... Unaweza kwenda"

    Aliongea dada huyo, lakini suria alisisimkwa na nywele zake, ikiwa na maana kuwa aliopishana nae sio binadamu wa kawaida....

    lakini sasa kumbe huyu dada ndio maimati mwenyewe, mmoja wa wale majini waliokuja duniani kutafuta MWANAUME MSAFI



    JANA TULIISHIA HAPO, SASA TUENDELEE



    Wakati suria kesha panda baiskeli yake na kuendelea na safari yake ya kuwahi shule ambayo anakwenda kujaribu kuomba kazi,..



    ILANI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO



    TAHADHARI SANA KWA WEWE UNAYE UZA KAZI HII KATIKA MITANDAO YAKO YA KIJAMII...



    HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA KIFUNGU CHA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MITANDAO, KWA KOSA LA KUHUJUMU KAZI ISIO YAKWAKO..



    NDUGU MSOMAJI, HAKIKISHA ANAEKUUZIA SIMULIZI HII NI MMILIKI HALALI MWENYE NAMBA HII, +255714419487... LAA SIVYO NAWE NI MMOJA KATI YA WAHUJUMU WA KAZI ZA WATU, KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.....



    KWA WALE NDUGU ZANGU WA KUPOSTI KWENYE KURASA ZAO,

    HAKIKISHA, UNAPATA IDHINI KUTOKA KWA MMILIKI HUSIKA KWA SIMU NO, +255714419487 WhatsApp

    ILI UPEWE MAELEZO, VIGEZO, NA MASHARTI YA KUPOSTI KWENYE UKURASA WAKO WOWOTE ULE..



    JIEPUSHE KUKOPI KAZI HII BILA IDHINI YA MMILIKI HUSIKA



    TAFADHALI SANA HATUPO KWA AJILI YA KUPELEKANA PABAYA KISHERIA.....



    TUWE MAKINI NA KAZI ZA WATU KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII



    Sasa pale kwenye kona maimati alisita kuendelea na safari, kwani kuna kitu kahisi kwa kijana huyo..

    "mkarimu, mpole, mnyenyekevu.. Atakosa kuwa msafi kweli?"

    Alijiuliza maimati, bila kuchelewa papo hapo akawa invisible (isio onekana) yaani kawa upepo ghafla kisha akaanza kumfuatilia suria kule ambako anakwenda,... Yeye hatembei bali anaruka tu... Yaani anapotelea hapa anaibukia mbele.. Sasa ili maimati amfahamu vyema suria, alianza kuzungumza na Qarena



    "Qarena?"

    Maimati aliita japo waliitika Qarena wa watu wengine lakini maimati alikuwa jirani na suria hivyo, Qarena wa suria alijua fika anaitwa yeye

    "ndio"

    "pacha wako anakwenda wapi"

    "anakwenda shule"

    "anakwenda kufanya nini"

    "kuomba kazi"

    Yaani Qarena hafichi kitu,... Ukiwa na uwezo wa kuzungumza na Qarena basi utajua siri nyingi sana za watu,.. Mana qarena anajua mpaka unachotaka kukifanya..kile usichokijua basi hata yeye hajui, ila ukikijua tu na yeye keshakijua...

    "pacha wako ana mke"

    "hana"

    "kwanini"

    "sijui"

    "ana mpenzi"

    "hana"

    "kwanini"

    "sijui"

    "ana mchumba"

    "ndio"

    "wameshafanya mapenzi"

    "hapana"

    "ana mchumba wa ngapi toka kuzaliwa kwake"

    "ni wa pili"

    "wa kwanza yuko wapi"

    "sijui"

    "kwanini waliachana na mchumba wa kwanza"

    "waliachana kwasababu mchumba alitaka mapenzi na pacha wangu hataki"

    "kwanini hataki"

    "kwasababu hataki hakutaka kuchanganya mapenzi na masomo"

    "pacha wako kafanya mapenzi mara ngapi toka kuzaliwa kwake"

    "hajawahi"

    "kuna siku anapataga shida kihisia"

    "ndio, hata jana usiku kuna shetani kaja"

    Yaani qarena ni mbea mpaka basi... Yaani anasema vyote,.. Mpaka jana suria kajiwa na jini mahaba, qarena kasema vyote... Maimati aliumia sana kuskia suria anatembelewaga na jini mahaba pale anapo jisahau kuomba dua...

    "huko anapokwenda atapata kazi"

    "sijui"

    "kwanini hujui"

    "yeye hajui na mimi sijui"

    "anakwenda shule gani"

    "SADAQ SEMINARY SEC SCHOOL"

    Maimati alipotea ghafla na maeneo hayo na suria ndio alikuwa akiinga katika geti la shule hio,.. Baada ya kuingia akapaki baiskeli yake vyema kisha akaingia ofisini,.. Kitu cha kwanza alishangaa kukaribishwa utafikiri alikuwa akisubiriwa yeye...

    "karibu... Karibu mwalimu"

    Alishangaa mpaka akatukuzwa kwa cheo na kuitwa mwalimu,.. Alimshukuru mungu katika moyo wake, japo hajui kama atapa kazi, lakini kwa uchangamfu huo ulimpa matumaini ya kupata kazi,..

    "ahsanteni sana ndugu zangu... Habari za kazi jamani"

    "aah salama tu sjui wewe huko utokako"

    "aahh namshukuru Mungu ni salama sana tu"

    "basi in sha alah, karibuni sana"

    "ahsante sana... Aahh naweza kumuona mkuu wa shule"

    "ndio, bila shaka ni ofisi ile pale"

    "Maashalah.. Kumbe ni pale tu"

    "ndio Waweza kwenda kumuona"

    "basi niwashukuru kwa hilo"

    "haya haya"

    Basi suria alitoka pale staff kisha akaenda kwenye ofisi ya mkuu wa shule hiyo,...



    "hodi hidi"

    Suria alibisha hodi huku akigonga mlango kiaina hivi"

    "karibu"

    Alikaribishwa na sekretari, kisha akaketi...

    "ahsante"

    "Samahani, nikusaidie nini"

    "aahh Samahani dada.. Nina shida na mkuu wa shule"

    "ok una miadi nae"

    "mmhh hapana.. Kiukweli ni binafsi zaidi"

    "ok wacha nimpigie simu"

    Basi dada yule alipiga simu kwa mkuu wa shule, ambaye yupo chumba cha pili, ila huezi kumwona mpaka uwe na miadi nae..

    "amesema ingia"

    Suria alifurahi kuruhusiwa kuingia,... Lakini sasa ndani ya hicho chumba, alionekana maimati kasimama katika kona ya ukuta,.. Lakini hakukuwa na mwenye uwezo wa kumwona pale alipo...

    "Shikamoo mzee wangu"

    "marahaba kijana habari yako"

    "salama tu... Aahh Samahani mzee wangu,. Nimekuja katika shule yako, ili niweze kupata nafasi ya uwalimu"

    Aliongea suria akimaanisha kuomba kazi,..

    "hebu tuone vyeti vyako"

    Suria bila wasiwasi alitoa vyeti vyake,.. Mkuu wa shule kuangalia, duuu suria ni bonge la msomi, yaani ni msomi atari...

    "aahh kijana.. Familia yako iliwekeza sana kwenye elimu yako"

    "ndio mzee wangu... Kiukweli nawashukuru sana wazazi wangu kwa hili"

    "ni kweli, pongezi zao... Lakini kijana.. Kiukweli hapaaa... Nafasiiii ha.."

    Mkuu wa shule alitaka kusema nafasi za kazi hakuna, lakini kabla hajasema hivyo.. Maimati alimulika mwanga mkali katika kichwa cha mkuu wa shule...

    "hebu subiri kidogo..... Batuliiii"

    "yes boss"

    "njoo"

    Aliitwa batuli ambaye ndio sekretari wake, na huyo ni sekretari wa mkuu wa shule, na sio sekretari wa shule

    "ndio boss"

    "hivi mwalimu saidi toka alipotoka juzi alirudi kweli"

    "hapana.. Tena aliondoka kwa matusi sana,.. Kiukweli hawezi kurudi"

    "anhaaa... Basi kaendelee na kazi zako"

    "sawa boss"

    Batuli aliondoka na kwenda kuendelea na kazi zake,.. Kisha mkuu huyo mwenye umri mkubwa sana akaanza kuzungumza na suria...

    "una bahati sana... Hebu barua yako ya maombi ya kazi"

    Suria alitoa barua ya maombi ya kazi, na kumpatia mkuu wa shule...

    "una hati nzuri sana..."

    Aliongea mzee huyo huku mlango ukifunguliwa na akaingia batulia

    "enhee nini tena"

    "boss..kipindi cha masomo ya dini kimefika"

    "mwalimu huyu hapa.. Mchukue ukamwonyeshe kila hatua na anaanza kazi leo leo huyu... Kijana.. Mfuate batuli akakupe mikakati ya kazi"

    Ilikuwa kama bahati japo maimati kahusika kwa namna kubwa katika swala la suria kupata kazi,.. Hii shule ina tabia, mwalimu akiacha kazi.. Basi ule mshahara wake huliwa na mkuu wa shule, sasa hakutaka kuleta mwalimu mwingine kwani walipo Wangeweza japo hawana taaluma ya kumudu somo la dini japo ni shule Kiislamu lakini sio kuwa inafundisha dini, bali na masomo aina yote yanayo fundishwa kwingine hata hapa yanafundishwa... Na kila mmoja ana kipindi chake kila darasa



    Suria hakurudi nyumbani siku hio kaanza kazi, tena kaanza katika darasa la wanafunzi wa kidato cha nne,... Hapo ni somo la dini, na akitoka hapo anakwenda kidato cha tatu vivyo hivyo mpaka afikie kidato cha kwanza ndipo anakwenda nyumbani... Na somo lake ni hilo tu

    Islamic Knowledge, mana suria emesoma na akasomea sekta hio...



    Katika darasa hilo, dawati la mwisho kabisa ambalo halina mwanafunzi.. Alikuwa kakaa maimati, lakini hakuna alie muona na wala hakuna atakae muona, mpaka aamue mwenyewe kuonwa na binadamu, na hata ukimuona utamuona kama binadamu wengine, hivyo bado hutojua ni jini..



    Suria akiwa yupo bize na ubao, tena hakaukwi na maneno mana sifa ya mwalimu ni kuwa mwongeaji na wanafunzi wako...

    "kamwalimu kadogo eee"

    Aliongea mmoja wa wanafunzi walipo jirani na maimati...

    "Afadhali huyu... Kuliko lile lizee"

    Aliongea mwanafunzi mwingine, na mwingine akadakia na kusema

    "afu ni hensam"

    Sasa mwanafunzi huyo aliposema kuwa suria ni hensam, maimati alishtuka sana..

    "ina maana hii shule haina maadili kwa wanafunzi?.. Inakuwaje wanafunzi kuanza kumtamani mwalimu wao"

    Aliongea maimati lakini ni katika moyo wake,...

    "haya sasa wanafunzi wangu, wadogo zangu,.. Nilianza na mbwembwe za ubaoni ili muone uwezo wa Mwalimu suria... Naitwa suria, ila nyie nitawajua taratibu.."

    Aliongea suria huku akitabasamu, sasa kumbe tabasamu lake limekuwa haluwa kwa maimati... Huezi amini maimati naye alikuwa akitabasamu zaidi...

    "mwalimu ana tabasamu zuri"

    Aliongea fadhila ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne,

    Saaa fadhila kumwangalia Mwanaidi, kamkuta amelegeza macho zidi ya suria....

    "we Mwanaidi"

    "nini bwana fadhila.. Tunakatiana stimu"

    Yaani walikuwa katika somo la imani lakini wao hawaelewi,.. Kisa uzuri wa suria..

    "Mwanaidi, ina maana ushampenda ticha suria"

    "pigia mstari... Now is your brother-in-law"

    "haaaaaaaaaa, mwanaiiiiiiiidiiiiiiii"

    Sasa maimati kawaangalia sana hawa wasichana, akajua hapa kamsaidia suria sehemu ambayo sio ya maadili yake... Akajikuta kakosea sana na anajuta kumsaidia suria kwenye hii shule... Lakini sasa hakukua na jinsi,.. Pale pale maimati kaivua pete yake ambayo ilikuwa na urembo wa kike na ni pete ya dhahabu ila ina urembo wa kike... Aliivua kisha akairusha pale mbele alipo suria... Na hakuna alie ona, na hata suria hajaona wala kusikia mshindo wa kitu kikidondoka.. Mara suria akadondosha chaki, sasa ile anainama tu, akaiona ile pete... Hakuigusa lakini akatoa tangazo...

    "wanafunzi wangu... Kuna mmoja wenu kadondosha pete yake hapa"

    Aliongea suria huku akiendelea kuandika, wala hana muda nayo mana anajua ni ya mwanafunzi wake

    "heee... Amesemaje yule hensam"

    "we fadhila, hebu Jieshim.. Ile pete anataka anipe mimi kwa njia hio.. Sasa wewe wataka kujua ili iweje"

    "kwani wewe umekuja na pete wewe"

    "si nimekwambia anataka anipe"

    "lakini Mwanaidi... Mwalimu kaanza kazi leo.. Ushaanza kumtamani jamani"

    "weeeee, najua hapa kuna mbwa mwitu, nikichelewa tu sina changu.. Si unakumbuka mwalimu Shabani.. Nilimpenda nikajifanya kuchelewaa.. Mpaka zaina akamchukua... Ina na hiyu nichelewe?? Hapana.. Wacha nikachukue Pete kama zawadi yangu toka kwake..."

    "mmhhj haya mwaya"

    "sio haya... Najua anaogopa kunipa mbele yenu mana kuna miaka 30 jela.. Hivyo ananipa kiujanja ujanja.. We si unaona hakuna aliotoka"

    Aliongea Mwanaidi huku akinyanyuka kwenye meza yake kuelekea mbele ili kuchukua ile pete... Na wakati huo maimati anaangalia tu, Mwanaidi anavyokwenda kuchukua ile pete













    Suria ni mtoto wa pili katika familia ya mzee Rashidi, mtoto wa kwanza akiwa ni mwanamke mwenye jina ASHA, mzee Rashidi alipenda sana uzao wa kiume kwani ndio anajua unaweza kumsaidia,.. Suria alipendwa sana na baba yake, na baba yake akaamua kumsomesha suria kwa gharama zake zote,.. Mzee Rashidi alikua na mifugo lakini yote ilikwisha kwa kumsomesha suria,.. Asha hakuipata nafasi hio kwani baba alipenda kuendeleza upande mmoja, asha aliishia kidato cha nne lakini suria alizunguka Tanzania nzima kuhakikisha anapata ilemu ya juu isio na mfano... Mana vyuo vyote vikubwa vikubwa kasoma ili hali tu kudokoa dokoa hapa na pale..



    Baada ya kuhitimu elimu yake yote, suria Anaanza kutafuta kazi ilio endana na elimu yake,.. Lakini anakutana na vikwazo vya hapa na pale katika hali ya kutafuta kazi...



    Suria hakukata tamaa, aliendelea kitafuta kazi, hasa ile alio shauriwa na baba yake... Lakini kwa bahati nzuri, suria anapata msaada kutoka kwa kiumbe mwenye asili ya ujini...



    Maimati aliweza kumsaidia suria mpaka kupata kazi, tena siku hio hio akaanza kazi rasmi... Lakini sasa maimati naye ni msichana na ana asili mbili, asili ya kibinadamu na asili ya ujini,.. Katika dunia hii hakuna binadamu wala kiumbe ambacho hakina hisia,... Sifa alizotaka murati sabaha, suria anazo lakini sasa mbaya zaidi hata maimati anataka mwanaume wa aina hio,... Hivyo moja kwa moja tujue jina maimati kampenda suria, na sio kampenda kwa niaba ya Murati sabaha,.. Bali kampenda yeye kama yeye...



    Kwakua suria yupo ndani ya moyo wa maimati,.. Basi jini huyo aliweza kuvua pete yake ambayo ni PETE YA KIKE, kwani ina urembo wa kike, japo ni pete ya gharama kubwa... Mana ni dhahabu tupu... Pete hio ina kazi Nne pale binadamu anapo ivaa...



    1). KUMLINDA BINADAMU ASIFUATWE NA SHETANI AU JINI MAHABA KWA NJIA YEYOTE ILE.... HIVYO UKIVAA HIO PETE, KAMA ULIKUA MALAYA UNASAHAU NA HUTOFANYA TENA KIPINDI UNAPO KUA NAYO....



    2). BINADAMU ANAPOIVAA PETE HIO, HUMUONGEZEA RIZIKI KATIKA KAZI YAKE,... YAANI KAMA NI DUKANI, BASI WATEJA UTAWACHOKA MWENYEWE



    3). BINADAMU ANAPOIVAA PETE HIO, HUMUONGOZA KUFANYA MAZURI TU... YAANI KAMA ULIKUA UNAZULUMU WATU, UKIIVAA HIO PETE HUWEZI KUZULUMU TENA.. LAKINI UKIIVUA UNARUDI KATIKA HALI YAKO ILE ILE YA UZULUMISHI



    4). BINADAMU ANAPOIVAA PETE HIO, HAWEZI KUKUBALI KISHAWISHI KIBAYA CHA AINA YEYOTE ILE, YAANI KAMA KUNA MTU ANATAKA KUKUSHAWISHI KUFANYA JAMBO, BASI HUEZI KUKUBALI..



    Sasa maimati kampa anampa suria pete kwa niaba ya wale wanaomtamani wasikubaliwe.... Afu pia anampa ili jini mahaba au shetani asiwezi kumsogelea pale anapo sahau kuomba dua,... Hivyo suria akiivaa hio pete, hakuna kibaya kitakacho mkuta yaani hata huyu maimati mwenyewe, hawezi kumwingilia kimwili katika ndoto mana wapo majini wema ambao nao huja usiku kwa wanaume wanao wapenda,... Hivyo hata yeye hatoweza kama akitaka kumjia katika ndoto...



    Sasa maimati alipoirusha pete ile suria aliona, lakini kwakua ni pete ya kike, aliwaarifu wanafunzi wake kua kuna pete hapo chini hivyo alio idondosha aweze kupita mbele aichukue...



    Ni shule ya sekondari inayosemekana kua na maadili mazuri, lakini kwa upande wa wasichana walikuepo ambao wanaweza kumtamani mwalimu wao, na hio ndio sababu kubwa ya maimati kutoa pete yake na kumpa suria... Fadhila na Mwanaidi wao walikua kipaumbele kumpenda suria, kitendo ambacho maimati alikasirika sana lakini hakuweza kuwafanya lolote...



    Sasa Mwanaidi alipofika mbele, alishangaa haoni pete,... Hivyo akamuuliza mwalimu tena kwa upoleee wa taratibu sana...

    "hensam ticha?.. Iko wapi hio pete"

    Aliuliza Mwanaidi lakini suria alishangaa kuskia anaitwa hensam ticha,...

    "umeniitaje"

    Suria alimuuliza kwa sauti kubwa

    "ticha, nimekuuliza taratibu, sasa mbona wapaza sauti hivyo"

    Aliongea Mwanaidi tena huku akijinengua flani hivi,.. Suria akashangaa ina maana kaingia choo cha kike, kapata kazi lakini kazi ina mitihani mingine juu yake.. Na achana na wanafunzi wa sekondari ni hatari kwa visura vyao na makusudi yao pale wanapo amua...

    "kama umeshachukua pete yako, rudi kaketi"

    Aliongea suria, na Mwanaidi akatii amri ya mwalimu... Lakini Mwanaidi alihisi hakukua na pete ila ni Janja ya mwalimu ili amuone vizuri... Yaani Mwanaidi bado anajipa matumaini juu ya suria.. Na ni leo tu hata siku haijaisha... Sasa jiulize hio ni shule au balaa..



    Maimati alitoka zake hapo shuleni baada ya kuona mambo ni shwari kwa upande wa suria... Alipotoka aliwasiliana na shaimati ambaye yeye shaimati yupo huku kwa faima



    Sasa tukija huku kwa faima akiwa na shaimati,.. Na faima bado hajajua kuwa hapo anaongea na kiumbe cha aina gani... Shaimati alikua akimbembeleza faima ampe muelekea huyo jini alipo,... Lakini faima hakutaka kusema kwani anajua ataibiwa mpenzi wake, na mpaka sasa hatujui mpenzi wa faima ni nani...sasa shaimati baada ya kujua kuwa faima hataki kusema,.. Alianza kumuuliza qarena wa faima

    "Qarena?"

    "ndio"

    "niambie anapoishi mchumba wa pacha wako"

    "anaishi pongwe"

    "nyumba namba ngapi"

    "namba 40 majengo ya mkoloni"

    Sasa papo hapo shaimati akiwa anazungumza na qarena,.. Aliweza kupata mawasiliano kutoka kwa maimati, hua wanasikilizana hata wakiwa umbali kiasi gani,.. Na hawatumii simu kama sisi binadamu, shaimati alisogea kwa pembeni ili faima asigundue, mana akimwona anaongea afu hana simu, itakuwa tabu



    "shaimati"

    Maimati aliita kisha shaimati akaitika

    "yeeeeeeeeee"

    "vipi, umefanikiwa kupata hata Msafi mmoja"

    "kuna ambaye namfuatilia sasa hivi, ili niweze kumfahamu"

    "wacha nije tumfuate wote"

    "sawa, tukutane pongwe majengo ya mkoloni"

    "sawa"

    Shaimati alimfuata faima na kumwambia,..

    "sawa umekataa kuniambia"

    "ndio, mana sikuamini... Wewe ni mzuri, je ukienda kumteka mchumba wangu"

    "siwezi.. Basi kwaheri"

    Shaimati alimuaga faima kisha huyoo akaondoka zake,.. Alitoka hapo kwa mguu lakini alipofika mahali pa Kujificha aligeuka kuwa upepo na kupotea papo hapo,...



    Jioni nyakati za saa kumi na moja, faima akiwa anapanga nguo ambazo ni mzigo ulio ingia sasa hivi, hivyi kachana beli kisha anazipanga... Hilo ni duka la ngu za Kiislamu tu, kama tunavyojua shamra shamra za mkoani tanga zilivyo za mavazi ya heshima, mana asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuvalia hijabu, na wanaume huvaa kanzu... Faima akiwa bize ghafla alimuona mchumba wake akiwa na furaha sana...

    "waoooooo, mume wa mie huyoo"

    Aliongea faima kwa furaha kubwa mno, kwa kumwona mchumba wake, na mchumba mwenyewe sii mwingine bali ni suria...

    "Assalam Aleykh mke wa mie"

    Suria alimsalimia faima, huku wakiitana mke na mume kama vile wameona, na hio ni ishara ya lazima waoane,.. Na mpaka sasa kinacho mkwamisha suria kuoa ni kazi, mana kuona sii jambo la mzaha.. Kwanza mungu anasema, kama huna uwezo wa kumlisha mke basi usioe mpaka pale utakapo pata uwezo wa kumlisha mke,..

    "waaleykh msalam, haz wangu"

    Faima anampenda sana suria, yaan hapo kasahau mpaka kazi kwa kumuona suria alio mtembelea kwa nyakati hizo...

    "sasa naona leo upo bize... Nikuache kidogo"

    "hapana... Wewe ndie unaenifanya mimi kua bize... Surian, nakupenda sana sua wangu"

    "nalijua hilo na kunipenda si tatizo tatizo dhumuni kutimia"

    "heeee hilo lazima kwa uwezo wa Allah"

    "kweli eee"

    "yes.... Afu Surian,.. Mbona leo kama una raha hivi, niambie Tufurahi sote"

    Aliuliza faima huku suria akitabasamu na kusema...

    "mwenyezi Mungu kaniwekea mkono wake... Nimepata kazi ya ualimu"

    Aliongea Suria huku faima akitabasamu mno kwa furaha

    "waooooo... Surian mpenzi wangu.. Sasa naona ndoa yetu hiiooo imefika"

    Aliongea faima huku akizidi kumkumbatia suria,..

    "hata mimi naona inakaribia.... Lakini?"

    "lakini nini tena haz wangu"

    "wale wanafunzi hawana maadili.... Kuna mwanafunzi kaniita hensam ticha... Kiukweli wananipa mitihani"

    Aliongea suria na faima akajua tu, wanafunzi wamesha anza kumtamani Surian wake.... Lakini faima hakuogopa hilo, tena alizidi kumpa nguvu

    "haz (Husband) wangu.. Najua uzuri wako umekua tabu kwa wasichana wengi hasa hasa mimi... Lakini hebu nikuulize... Toka umezaliwa, humjui mwanamke,.. Umediriki mpaka kuachana na mpenzi wako wa zamani aliokua anakufosi kufanya mapenzi, ukamuacha.. Umezunguka vyuo vingapi hapa Tanzania?.. Umeona wazuri wangapi huko vyuoni?"



    "wengi tu"

    "sasa iweje leo utikiswe na watoto wa juzi tu"

    Aliongea faima (fey) kama kumtia nguvu asiache hio kazi

    "unajua nimeshangaa kua.. Shule inasifika kua na maadili, iweje wanafunzi wanze tamaa kwa walimu zao"

    "nakuomba sana haz wangu.. Usiache hio kazi.. Jitahidi kuwakwepa na uwaambie ukweli ikiwezekana nenda kashtaki kwa walimu wengine"

    "mmmhhh Kiukweli nitavumilia lakini vikinishinda naacha"

    Aliongea suria mana hapendi kufanya kazi huku akitegwa,... Acha na tabia ya mwanafunzi pale anapo amua kufanya jambo lake,... Basi kwakua ni jioni suria alimuaga faima anaelekea nyumbani

    "chukua basi hii weka mfukoni"

    Faima alimpa suria elfu kumi na tano,

    "faima.. Kila siku unanipa.. Hii imezidi sasa.. Fanya kazi jiwekee fedha zako kulingana na kazi yako... Mimi bado nipo nyumbani"

    Aliongea suria huku faima naye akiongea

    "kwani mimi naishi peke yangu?.. Hata mimi naishi kwetu.. Nimeshakupa na nitakupa na sintochoka kukupa.."

    Aliongea faima kisha akaingia ndani kuendelea na kazi...



    Sasa huku mtaani kwa akina suria.. Maimati na shaimati wapo katika mti mmoja, wakimsubiria kijana mwenye sifa anazo zitaka Murati sabaha... Lakini sasa maimati yeye hajui kama wanae mtega ndio yule aliomsadia kupata kazi, na nzuri zaidi tayari yupo moyoni mwake... Shaimati nae yeye kapata muelekea kuwa mtaa huo una kijana ambaye wanamtafuta.. Sasa wamekuja kuweka kambi kwenye mti mmoja hivi.. Ila walikua wakionekana na kila mtu, lakini hata uwaone huezi jua kama ni majini.. Sasa shaimati yeye anaangalia nyumba namba 40, mana yeye ndie anajua kijana huyo anaishi nyumba namba ngapi...



    Punde sii punde suria akiwa anaendesha baiskeli yake kurudi nyumbani,... Sasa maimati ndio anamuona suria,..

    "kumbe huyu mwanaume Msafi anaishi huku"

    Alijiuliza maimati, japo hajui kua ndio mtu wanaye msubiria hapo... Mara shaimati akanyanyuka na kusema

    "yeeeeeee, itakua ni yule"

    Aliongea shaimati, lakini maimati alimshika shaimati mkono kua waondoke waachane na huyo mtu

    "maimati mbona sikuelewi lakini"

    "huyo kijana ni mchafu achana nae"

    Aliongea maimati ili shaimati aachane na suria...

    "hapana, niache niongee na qarena wake"

    Aliongea shaimati huku maimati akikasirika sana..

    "shaimatiiiiiiiii...."

    Maimati alimuita mwenzie kwa hasira, mpaka shaimati akashangaa leo ndugu yake ana nini....

    "wewe, mbona leo sikuelewi?... Hii ndio kazi tuliotumwa huku duniani... Leo nataka nimjue kama ana sifa.. Afu wewe hutaki una maana gani"

    Aliuliza shaimati na kuachana na suria.. Wakati huo suria keshaingia kwao...

    "ni kweli shaimati... Huyo mwanaume ni Msafi, ila nilisha mwona tokea asubuhi.... Ana sifa zote za kuishi ndani ya himaya yetu... Lakini sifa alizonazo huyo mwanaume, hata mimi nazitaka... Hivyo sipo tayari nimpeleke kwa murati sabaha... Tafadhali sana shaimati... Naomba tutafute MWANAUME MSAFI mwingine, ila sio Surian"

    Aliongea maimati tena kwa kumuomba shaimati

    "maimati, hivi una akili wewe... Hivi umejisahau kuwa upoje... Yule ni binadamu na wewe ni jini... Inawezekanaje kwa hilo"

    "nikifuata taratibu zote.. Naweza kuwa nae"

    "hata kama... Lakini huyu mwanaume ni lazima afike kwenye himaya ya Murati sabaha... Na nitampeleka mimi kama wewe hutaki"

    "sasa tutaona... Mimi na wewe nani zaidi.... Surian haendi popote"











    Katika dunia hii kila kiumbe kimeumbwa na hisia zake na matamanio yake, hata wadudu hutamaniana kama ilivyo kwetu sisi binadamu, na hisia za mapenzi anazo kila kiumbe kilichopo duniani.. Maimati akiwa nusu mtu, nusu jini amejikuta akiangukia katika penzi la mwanadamu, lakini rafiki yake alikataa juu ya swala hilo la maimati kumpenda binadamu ingali binadamu huyo ana sifa za kuishi katika bustani yao huko chini ya bahari ambako ndiko makazi ya watu hawa yaliko... Shaimati hakubaliani na maimati katika swala la kumwacha suria dunia,....



    "sasa tutaona... Mimi na wewe nani zaidi.... Surian haendi popote"

    Aliongea maimati kisha akapotea pale pale katika mazingira ya kutatanisha, shaimati alibaki pale akiendelea kumsubiri suria ili aweze kumshawishi waondoke wote, mana hairuhusiwi kuondoka nae bila makubaliano na kama hataki basi hatakiwi kuondoka, hivyo utumike uongo wowote ule ilimradi akubali, yaani kikubwa asilazimishwe kuondoka



    Shaimati alikaa sana hapo nje lakini suria hakutoka nje, kwani hanaga tabia za kutoka nje pale afikapo nyumbani.....

    "mwanangu? Mbona leo umechelewa sana kuja nyumbani"

    Mama yake surian alimuuliza mwanaye baada ya kurudi jioni sana mida ya saa kumi na moja..

    "mama? Mimi nimepeta kazi ujue"

    Aliongea surian ama suria au sua, vyovyote utakavyo mwita sawa tu..

    "umepata kazi?"

    Alidakia dada yake surian aitwaye asha

    "ndio dada, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake"

    Alimjibu dada yake kwa uzuri tu kisha asha akamuuliza mdogo wake

    "ni kazi gani umepata"

    "ualimu"

    "boooo, nikajua kazi ya maana kumbe ualimu?... Mama? Ina maana kumsomesha kooote huko Kapata kazi ya ualimu?"

    Aliongea aisha huku akibinua mdomo, kana kwamba kapata kazi ya kishamba ambayo haiendani na elimu yake alio nayo, na ni kweli surian ana elimu kubwa sana na hakupaswa kuwa mwalimu... Yaani alitakiwa kuajiriwa serikalini tena ngazi za juu sana.. Na kima cha mshahara wake kilitakiwa kiwe kuanzia milioni 5 kwenda mbele... Lakini kapata kazi ya ualimu ambayo analipwa laki tatu na elfu sabini...

    "asha mwanangu.. Mbona huna furaha na maendeleo ya ndugu yako"

    "sio sina maendeleo mama.. Mmemsomeshaaaaaaaaaa.... Sasa mbona hata ukimuomba hela ya vocha hapo hana"

    "sasa si alikua hana kazi hamani"

    "hana kazi eeee??... Mtajibeba na elimu zenu za juu... Mwana PHD"

    Aliongea asha kisha akaondoka zake mana alikua kashika chupa ya mafuta ya kula, kana kwamba anakwenda dukani....

    "surian mwanangu... Achana na dada yako si unamjua? Au bado hujamzoea tu"

    "wala tu sina shida nae... Afu mama? Ina maana vile alivyo vaa ndio anakwenda dukani vile"

    "heeeeee... Tena vile kavaa vizuri sana vile... Kuna saa nyingine mpaka nampa kanga hapa nje ili asipite mbele ya baba yake.. Vile?? Vile mbona kava vizuri sana pale"

    Aliongea mama yake asha huku suria akizidi kutikisa kichwa

    "mamaaaa.... Yaani vile ndio kavaa vizuri vile"

    "hebu nenda kaoge ule"

    "lakini mama, dada mnamleaje lakini mama"

    "surian?? Ina maana dada yako humjui wewe?"

    "mi najua unamwachia tu ni kwasababu anawapa wapa visent sent"

    Aliongea surian kana kwamba asha ndio anatoa pesa ya kula pale baba yao anapokua kakosa, mana asha anamiliki saluni hapo mjini mjini, hivyo hakosi pesa...



    Sasa huku barabarani, shaimati alimwona asha, akitoka kwenye ile nyumba,.. Shaimati anamkumbuka sana asha mana alisha msitili kimavazi bila asha kujua,... Na shaimati hapendi kuona hali ile.. Hivyo pale pale akamvisha hijabu katika mazingira ya ajabu... Hivyo watu wanaona asha kavalia hijabu lakini asha akijiangalia anajua ana kasketi kafupi...

    "Asalam Aleykh dada"

    Shaimati alimsalimia asha... Na wakati hua inakwenda saa 12 kasoro za jioni..

    "Waleykh msalamu mambo"

    "poa.. Naona Unakwenda dukani"

    "enheheh ndio, nakwenda kuchukua mafuta ya kula"

    Alijibu asha, na hapo bado hajui kama anazungumza na jini, na shaimati kavalia hijabu kisha kapiga ushungi wake,...

    "ila we mzuri"

    Shaimati alimsifia asha huku asha akitabasamu kusifia na mwanamke mwenzie.. Unajua wachilia mwanaume kumsifia mwanamke kuwa yeye ni mzuri... Kuna mengi yamemvutia au kaamua tu kumwambia ni mzuri.. Lakini mwanamke akimwambia mwanamke mwenzie ni mzuri basi inakua kuna ukweli kiasi na hata anae ambiwa mzuri hujiskia vyema, japo alitamani kuambiwa na mwanaume.... Sasa tabu ni kwa wanaume kuambiana ni mahensam,.. Utasubiri sana kuskia mwenzio kakwambia wewe ni hensam,.. Hatusemagi wanaume hua tunavungaga tu.. Huezi kumsifia mwanaume mwenzio eti ni hensam... Ila jamaa atajisemea mwenyewe tu kua DUUU JAMAA NI HENSAM YULE

    lakini haji kusema WEWE NI HENSAM..



    "kweli?"

    "haaaa... Sasa nikudanganye kwani mimi mwanaume"

    "kwani mwanaume akimwambia mwanamke ni mzuri, kamdanganya"

    "huenda asimdanganye au akamdanganya,.. Na pia huenda akamwambia ni mzuri kwa umbo... Au kifua, hivyo wanaume hawasemi mzuri mwili mzima.. Bali kuna kipande cha mwili kakipenda hivyo labda hawezi kusema una umbo zuri, au una kifua kizuri, au una sura nzuri... Hawezi kichambua lakini atasema kwa ujumla wewe ni mzuri, lakini kuna sehemu kailenga"

    Aliongea shaimati na kumteka asha kwa yale maneno yake...

    "haaaaaa, basi mimi sijuagi... Kumbe wanaume hawapendagi mwili mzima"

    "tena sio kupenda bali kutamani"

    "heeee dada unaniacha hoi"

    "usijali... Mimi natamani uwe rafiki yangu, sjui unaitwa nani"

    Shaimati aliongea hivyo na kumuuliza jina lake, lakini sio kuwa halijui bali kaamua tu kumuuliza...

    "haina shida.. Mimi naitwa asha.. Ni mtoto wa kwanza katika familia ya kawaida sana"

    "waooooo... Mimi Naitwa shamimu, ni mtoto wa tatu katika familia yetu.. Vipi kwenu mmezaliwa wangapi"

    Shaimati au shamimu alimuuliza asha kuwa kwao wamezaliwa wangapi...

    "Kiukweli tupo wawili tu.. Nina mdogo wangu wa kiume anaitwa surian"

    "waoooo... Kumbe una ndugu wa kiume"

    "yes"

    Aliongea shaimati, japo anajua kila kitu lakini hakutaka kumwonyesha kuwa anajua hilo.... Asha alifika dukani akanunua mafuta kisha wakawa wanarudi....



    "kaka yako ni mkubwa eee"

    Shaimati alikua na maswali mengi sana ili tu kujenga mazoea na asha kwa urahisi wa kumpata suria, ili huyo huyo asha amrubuni mdogo wake kwa njia yoyote ile...

    "yes, ni mkubwa.. Ana miaka 23 sasa"

    "waoooo, basi mwambie mimi nina 20"

    Aliongea shaimati ili kumwonyesha asha kua keshazimika na mdogo wake

    "mmmhhh shamimu, ina maana ushampenda mdogo wangu"

    "nikipata muda wa kuongea nae... Sitasita kumwambia"

    Aliongea shaimati huku akishusha tabasamu zito mno... Asha hajui kuwa huyo ni jini

    "waooo basi napenda pia uje kuwa wifi yangu"

    "eti eee"

    "ndio"

    Asha alifika kwao kisha akamuaga shaimati

    "shamimu? Nimefika na hapa ndio nyumbani... Afu subiri nikuitie surian"

    "ah ah Noo Noo... Mwache kwanza.. Nafikiria kachoka kwa kiasi fulani"

    "sawa wifi, kesho basi"

    "ok poa"

    Sasa ile asha anafunga tu mlango, huku nje shaimati kapotea pale pale...



    Sasa huku ndani,.. Surian katoka kuoga, sasa alikua akivaa saa yake, lakini kwa pembeni ya ukuta alikuwepo maimati akimtazama huku akizidi kumpenda surian... Wakati huo surian anaharakisha kuvaa ili awahi msikitini kuswali swala ya magharibi.. Suria alitoka na maimati akafuata nyuma... Kana kwamba hamuachi... Surian alipoingia msikitini, maimati alipotea mana kahakikisha anaingia sehemu salama kabisa....



    Sasa huku katika kambi yao ambayo wamefikia wao wawili..

    Maimati alimkuta shaimati akiwa katulia, tena kavalia mavazi meupee ambayo ndio waliokuja nayo toka baharini....

    "mpaka sasa nimefanya mawasiliano na Murati sabaha, nimemwambia kuna msafi tumempata"

    Aliongea shaimati kama kumwelezea maimati

    "lakini shaimati.. Mbona unafanya haraka hivyo? Mimi nimekuomba tutafute mwingine"

    Aliongea maimati kana kwamba bado anazidi kumwomba ili watafute mwanaume mwingine lakini sio suria

    "sikiliza maimati... Lazima twende na matakwa ya Murati sabaha..."

    "hapana...ivi wewe shaimati huna hisia za kimapenzi"

    "ninazo ila sihitaji mwanaume mana hakuna mwanaume atakaye timiza sifa ninazo taka"

    Aliongea shaimati kana kwamba naye anapenda lakini ana sifa zake ambazo anataka...

    "sifa gani wewe unataka"

    Maimati alimuuliza ili aweze kujua

    "nataka mwanaume ambaye hajasoma kabisa... Yaani kama kasoma sana, basi awe kaishia darasa la saba tu basi... Na awe msafi"

    Aliongea shaimati huku maimati akitikisa kichwa,...

    "Kwa sasa huezi kupata mwanaume kama huyo, labda zamani... Mana zamani watu hawakua wakisoma sana... Lakini sasa hivi watu wanataka mpaka PHD, leo unasema unataka ambaye hajasoma... Na kama kasoma basi awe kaishia darasa la saba"

    "ndio"

    "mmmhhh Masharti yako magumu sana... Lakini yote tisa.. Surian tumuache shaimati"

    Maimati alizidi kumwomba mwenzie kuwa suria wamwache kama alivyo...

    "maimati... Mimi sihitaji kuishi duniani... Kwanza duniani kunatia kichefuchefu... Wanawake wanasagana.. Wanaume ndio usiseme... Mimi sitaki kabisa. Sitaki kuishi huku.. Hebu tumchukue huyo aliopatikana tuondoke zetu"

    "kweli surian haondoki shaimati..."

    "mimi nasema hivi surian ataondoka"

    Walibishana lakini uzuri ni kwamba hawa hawapigani ila ili mmoja aonekane mshindi basi ni lazima wapimane nguvu kwa kutumia akili..

    "sawa.. Tutajua... Na nahitaji niwasiliane na Murati sabaha,.. Kua tunaona wanaume wasafi ambao wanajichua tu"

    "heeeee... Maimati?? Unataka kupeleka uchafu kwenye bustani yetu... Yaani hatakiwi mwanaume alio fanya mapenzi, au alio jitoa manii zake kwa njia ya mkono ama njia yeyote ile kama katumia akilia yake"

    Aliongea shaimati,... Shaimati Kiukweli hajui kitu kuhusu mapenzi japo wote hawajui.. Yaani hawa wasichana wawili wote ni mabikra, hawajui mapenzi lakini maimati kapenda, hisia zimemjaa kwa kumuona surian...

    "kwahio"

    "mimi naona usisumbuke kuwasiliana nae"

    Aliongea shaimati, jini asiejua kupenda, mwenzie kapenda lakini hataki kujua swala hilo...



    BAADA YA SIKU NNE KUPITA



    AFTER FOUR DAYS AGO



    Zikiwa ni siku nne zimepita lakini ni siku tano toka kuingia kwa majini wawili, yaani shaimati (shamimu) na maimati (maimuna).. Hivyo wamebakiza siku mbili warejee katika dunia yao, iwe wamepata au wamekosa lakini wanatakiwa kurudi baada ya siku saba walizo pewa na malikia wao Murati sabaha ambaye anataka KIJAKAZI WA KIUME kwa ajili ya Kutunza bustani yao,.. Lakini Murati sabaha anataka mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi mana hata wao wote hawajawahi kufanya mapezi...











    Wanaume ambao hawajawahi kufanya mapenzi duniani, ni wengi sana tena sana.. Lakini sasa wengi wetu hua tunajichua, yaani majini hawa hawataki mwanaume mpiga nyeto,.. Hata kama hajawahi kufanya mapenzi lakini hawamtaki mana kajichafua kwa akili yake... Ila kama umejichafua kupitia ndoto basi wewe wanakutaka mana sio akili yako... Hivyo kama yupo mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi toka kuzaliwa kwake na hajawahi kujichua.. Basi aje tanga huku anatafutwa kwa udi na uvumba



    Wakati huo surian yupo shuleni akifundisha wanafunzi wake katika kipindi chake cha dini, yaani masomo ya dini husika... Lakini katika lile lile dawati la mwisho alionekana maimati akiwa kakaa, lakini hakukua na mwenye uwezo wa kumwona...

    Surian kila akiokota chaki kwenye kiboksi anaona pete,... Na hio pete ndio hio suria anatakiwa aivae, lakini sasa tatizo ni kwamba pete yenyewe ni ya kike.... Na suria yeye anajua ni pete ya mmoja kati ya wanafunzi wake humo darasani,...

    "hii michezo yenu hii.. Sasa mumecheza mpaka mumesahau pete kwenye kiboksi cha chaki"

    Aliongea mwalimu surian huku akiendelea kuandika,.. Leo Pete haipo chini bali ipo ndani ya kiboksi cha chaki... Na hio pete ni maalum kwa ajili ya surian,... Baada ya kipindi chake kuisha, surian hua anafundishaga watoto wa madrasa kule msikitini pale anapo pata muda.. Hivyo akaona ngoja achukue chaki moja,.. Lakini katika hali ya kichukua alibeba na ile Pete lakini hakuona kama kaibeba ile Pete.. Akaweka katika mguko wake wa suruali akijua kaweka chaki, japo ni chaki kweli lakini imeambatana na ile PETE YA KIKE ambaye anatakiwa kuivaa mwanaume huyo alie onekana msafi katika mkoa wote huo wa Tanga...



    Ilipofika mida ya kutoka kazini, surian alipanda baiskeli yake kisha huyoo akaondoka zake,... Hapo sasa maimati karidhika kuona pete ile ipo mfukoni mwa surian... Maimati hakuendelea kumfuatilia, alielekea sehemu yao ambayo wamefikia na wala hahangaiki kitafuta mtu kwani nia yake ni kirudi mikono mitupu kwa Murati sabaha na kumwambia duniani hakuna mwanaume msafi



    Sasa huku jirani na nyumba ya akina surian katika mti mmoja ulio acha kivuli kizuuri sana alionekana shaimati akiwa katika hali ya kibinadamu na anaonekana na kila mtu anapewa salamu kama kawaida, na anaitikia kama kawaida, hivyo huezi jua kama ni jini..

    "leo lazima niongee na surian... Namshawishi kuna kazi nzuri nje ya nchi atalipwa milioni 10 kwa wiki... Lazima akubali, mana najua akifika kule hawezi kurudi hivyo ni lazima afuate sheria, kanuni na matakwa ya himaya yetu"

    Alijiongelea huyu jini shaimati huku akitafuta maneno ya kumrubuni.. Mana anao uwezo wa kumchukua bila kuongea naye, lakini Taurati yao ni hivi... Anatakiwa amrubuni kwa njia ya kibinadamu mana yeye ni binadamu, ila kama suria angelikua ni jini basi angerubuniwa kwa njia ya kijini jini..... Sasa shaimati anaandaa maneno ya kuongea pindi surian anapotokeza kwenye kona...



    Sasa huku surian kapitia msikitini kuweka ile chaki moja ambayo kaichukua kule shule kwa ajili ya kuja kufundisha watoto madrasa hapo msikitini.... Sasa alipotoa, alishangaa kuona pete...

    "ina maana hii pete ya mwanafunzi niliibeba"

    Alijisemea mwalimu surian huku akimpa mtoto chaki akaweke pale ubaoni kwao... Surian hakuona kama kuna tatizo, aliirudisha ile pete katika mfuko wa suruali yake.. Kisha akaanza kupekecha baiskeli na kuondoka, lakini kila akikaa kwenye kiti cha baiskeli ile pete inamchoma choma kana kwamba inamghasi kukaa vizuri katika kiti...

    "aahhhh jamani hiii pete.. Nitaitupa mimi aahh"

    Aliongea suria huku akiitoa pete ile

    "sema ni pete ya mwanafunzi wangu.. Wacha niivae ili kesho nimpe, japo sijui ni ya mwanafunzi yupi"

    Aliongea suria kisha akaivaa ile pete kwa hiari yake,... Lakini ni kwasababu imemghasi kukaa katika baiskeli.. Sasa lipo ivaa tu, maimati kapata ishara kuwa pete imevaliwa katika kidole cha surian,..





    Sasa shaimati bado kasimama kwenye ule mti.. Akamuona surian kwa mbaaali sana anakuja mbio huku akiwa anaendesha baiskeli.. Sasa shaimati akaona kwa ule mwendo wa baiskeli anaokuja nao surian hatoweza kumsimamisha... Hivyo alinyoosha kidole chake na kuifanya tairi ya nyuma kuwa na pancha...

    "ayaaaaaa... Misumari hii imetoboa tairi yangu aiseee"

    Aliongea suria baada ya kuona tairi ya nyuma haina upepo,... Sasa kwakua nyumbani sio mbali alianza kukokota baiskeli.. Sasa surian akaingiza mkono mmoja mfukoni ili watu wasione ile pete mana ni pete ya kike, watu wakiona itakua aibu..

    "samahani kaka.... Kwanza Asalam Aleykh"

    Shaimati alianza mambo yake, yaani hapo haruhusiwi kutumia nguvu za kijini...na ndio maana wakatumwa hawa kwasababu wana asili mbili...

    "waaleykh msalam dada kheri"

    "kheri, za kazi"

    "aahh salama tu"

    "inaonekana unafanya kazi nzuri eee"

    "kawaida tu dada yangu"

    Shaimati alianza kumsifia kiasi fulani

    "ni kazi gani kwani..."

    Kwa kawaida mtu ukiulizwa sana unaweza kushangaa lakini surian hakua mchoyo wa kusema...

    "mimi ni mwalimu..."

    "aahhh mi nikajua upo wizara fulani hivi ya fedha"

    "hahahha hapana dada yangu"

    "ila binafsi ningependa tuzungumzie swala la maendeleo... Vipi Naweza kupata walau muda tuongee"

    "hapana, sina muda"

    "ok.. Mana kuna kazi nje ya nchi.. Mshahara ni milioni kumi kwa wiki"

    Aliongea shaimati lakini Swalehe hakuonekana kushtuka kwa hilo

    "Kiukweli sihitaji kazi za nje.. Mana kwa sasa nina kazi hivyo nimetosheka na kipato changu"

    Aliongea surian kisha akawa anaondoka...

    "sasa kaka"

    Shaimati aliendelea, lakini surian aliutoa ule mkono wenye pete na kumwambia kwa vitendo huku akisema

    "Samahani dada nimechoka sana.. Naihitaji kukoga niwahi msikitini.. Hivyo utaniwia radhi"

    Aliongea suria kisha akawa anaondoka,... Sasa shaimati kaiona ile pete, ndio akajua kiumbe ndio mana alikua hataki ni kwasababu ya hio pete...

    "ina maana maimati kampa pete?? Shiiiit.... Ujinga gani huu, ina maana nimemkosa?"

    Aliongea shaimati lakini ghafla akitabasamu huku akiangalia chini..



    Sasa huku ndani surian anaingia, anapishana na dada yake... Mara simu ya surian ikaita

    "haalo habari yako"

    Ilisikika sauti ya mwanaume mmoja

    "salama nani mwenzangu"

    "naitwa shabani kisu, ni afisa mwajiri katika kampuni ya MOON VISION ENTERTAINMENT, wewe ndio surian Rashidi Kingazi"

    "ndio mimi mkuu... Vipi nimepata kazi"

    "acha presha kijana... Utaitwa kesho kwenye intaviu, na boss kasema atakulipa mshahara kwa Mwezi Ni shilingi milioni 3"

    Aliongea afisa huyo, surian alifurahi

    "haaaaaaa milioni tatu"

    "ndio... Kesho saa nne tutakupigia simu"

    "sawa boss"

    "haya, nikutakie siku njema"

    "nawe pia boss"

    Simu ilikata, wakati huo asha kashika kiuno akiskiliza swala la milioni tatu

    "dada.. Nimepata kazi mpyaa.. Naachana na kazi ya ualimu mimi"

    "hongera kwa hilo.... Sasa na hii pete ya kike vipi jamani we surian"

    Asha kaona ile pete

    "aahh achana nayo"

    Suria aliingia zake ndani, asha nae akaachana na ndugu yake.. Sasa ile asha kutoka akakutana na shaimati

    "Afadhali umetoka... Njoo njoo haraka"

    Shaimati alimwita asha na asha hakusita mana ni marafiki wakubwa kwa sasa...

    "kwani ulikuja muda sana..."

    "hapana... Sasa skia, mdogo wako nimeongea nae... Lakini nasikitika kua sintokua nae"

    Aliongea shaimati huku asha akiuliza

    "kwanini sasa jamani shamimu"

    "mdogo wako kumbe ni shoga"

    Shaimati aliongea hivyo, huku asha akikasirika

    "shamimu naomba tuheshimiane.. Kama umemtongoza kakukataa basi, isiwe sababu ya kumtukana"

    "hapana aisha... Mdogo wako kavaa pete ya kike... Kama sio shoga, basi inamletea sifa mbaya sana.. Wewe uliona wapi mwanaume akavaa PETE YA KIKE?"

    Aliuliza shaimati kisha asha akajibu

    "kweli sijawahi kuona.. Lakini sidhani kama ni sababu ya kumwita ndugu yangu hilo jina"

    "ashaaaa.. Labda kweli hana hio tabia.. Lakini ile pete... Inamfanya aonekane hivyo... Mimi naomba ukaichukue, mi nampenda mdogo wako... Watu wanamchukulia hivyo akiwa na ile pete... Hebu wahi"

    Aliongea shaimati huku asha nae akianza kukubali,...

    "lakini, mimi siwezi kuingia chumbani kwake"

    "ashaaaaa... Mdogo wako sio shoga lakini watamuona ni shoga"

    "sawa lakini pete ipo kidoleni mwake mimi naichukuaje"

    "sikia sasa... Hawezi kwenda kuoga na pete... Wewe mvizie kaenda kuoga, ichukue pale mezani kwake"

    Aliongea shaimati na yote hayo ni ili ile pete isivaliwe na surian tena..

    "sasa mimi sijawahi kuingia chumbani kwake bwana shamimu"

    Sasa shaimati kuona asha anazidi kuwa mgumu, alitoa kitita cha pesa kama laki mbili hivi kisha akampa...

    "nampenda sana mdogo wako... Chukua hii pesa, fanya hio kazi... Nampenda mdogo wako kweli asha"

    Aliongea shaimati huku asha akiwa haamini,... Na keshazipokea zile pesa

    "sasa ile pete nikuletee wewe au"

    "hapana, vaa wewe tu, mana ni ya kike ile"

    Aliongea shaimati kisha asha akaondoka muda huo huo kuingia ndani ili akaiibe ile pete ya suria..



    Sasa huku ndani, suria anaingia bafuni huku anacheza kaswida (nyimbo za Kiislamu).. Alikua katika furaha kubwa kwa kuitwa kazi, na wakati huo ana taulo tu.. Anaingia bafuni huku anacheza... Lakini sasa suria kasahau kuvua ile pete, sasa asha kuangalia anaona pete ipo kidoleni,.. Sasa hapo kichwa moto mana anapenda hela kuliko maelezo, suria aliingia bafuni, sasa ile anaanza kuoga anagundua ana pete kwenye kidole, na huezi kuoga na pete kidoleni mana itakuchubua chubua au kukugasi wakati wa kuoga... Sasa wakati huo asha kaduaa, mana kapewa hela lakini pete haipo, na huezi kumvua mtu... Sasa huku bafuni suria kaishika ile pete huku akisema...

    "ayaaaaa kumbe sijavua hili lipete"

    Aliongea kwa sauti mpaka asha akasikia,... Sasa asha huku anaomba hio pete ivuliwe mana hata akivua hawezi kuiacha huko bafuni, bali ataiweka mahali...



    Sasa huku kwa maimati akiwa katulia, ghafla akapata ishara kuwa pete imevuliwa,... Kwa ishara hio aliona kuna umuhimu wa kwenda alipo surian... Maimati akajiandaa kuruka ili akaangalie kulikoni pete ivuliwe,.. Lakini kabla hajaruka, akapata ishara tena kua, pete imevaliwa, hivyo akaahirisha kwenda









    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog