Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE ISLAMIC WIFE - 1

 

     

     



     IMEANDIKWA NA : MOONBOY



    *********************************************************************************

    Chombezo : The Islamic Wife

    Sehemu Ya Kwanza (1)

     

    Inapoanzia Rasmi



    NDUGU WASOMAJI WANGU... SIMULIZI HIII... HAITOKUWA NA VIPENGELE VIREFU, KAMA ILIVYO KATIKA SIMULIZI ZINGINE... HII ITAKUWA FUPI FUPI, KUNA SABABU ZILIZOPO NJE YA UWEZO WANGU NA NDIO MAANA IMEKUWA HIVYO..



    HAYA TUANZENI RASMI HADITHI, SIMULIZI, STORY... AU VYOVYOTE UTAKAVYO IITA SAWA TU.....



    SIMULIZI yetu inaanza Katika Chuo Binafsi ambacho ni chuo kikubwa sana kilichopo jijini Arusha,.. Wanafunzi walikuwa ni wengi sana na leo ni siku yao ya kupata likizo ndogo, yaani ule mwezi wa sita.. Mana kuna vyuo vingine hufunguliwa mwezi wa sita au saba lakini pia vipo vingine hufungwa miezi hio,.. Inategemea na utaratibu wa vyuo binafsi, yaani sio vyuo vya serikali...



    Wanafunzi wengi sana walikuja kupokelewa na wazazi wao, walezi wao, au hata marafiki zao..



    Nje ya geti la chuo hicho kulisimama magari makubwa makubwa, yaani sio malori, namaanisha magari ya thamani kubwa na mmoja wapo alikuwa ni Jamali aliokuja kumpokea mdogo wake,.. Gari aliokuja nayo ni gari aina ya VOGUE DISCOVERY V807

    Gari yenye thamani kubwa sana duniani japo zipo zaidi ya hio lakini hizo ni babu kubwa na ukiona mmiliki wa gari hio usije kumdharau, sio tajiri wa mchezo mchezo,...



    "aahhh dogo langu la faida.. Niambie sasa"

    Alikuwa ni jamali aliomkumbatia mdogo wake wa kiume aitwae RAHIM, ukipenda unaweza kumwita RAM au RAMY... Ramy huyu ndio yule yule kijana tuliomzoe katika simulizi zilizopita na zinazokuja... Anaitwa Sharbiny Rashidy Kingazi, katika simulizi hii kutumia jina la Rahim,.. Ni mtoto wa kitajiri wacha mchezo, hata hiki chuo anachosoma hapa, ada yake ya mwezi mmoja tu unakula mpaka kufa kwako...



    "niaje broo"

    "nisalimie weweee, au kisa umepanda hewani tumelingana si ndio"

    Aliongea jamali kumtaka rahim amsalimie mana ni kaka yake, na ni kweli wamelingana utafikiri wamezaliwa siku moja, kumbe wamepisha kama miaka 7 hivi au 8, basi rahim aliingiza begi lake la nguo kisha wakaondoka zao...



    Walifika nyumbani kwao..... Hilo jumba lao sijui hata ulishawahi kuliona wapi, ni jumba haswa, yaani sio kijumba cha mchezo mchezo, yaani ni familia yenye pesa sana, ila kwa hasara zaidi ni kwamba hawaijui dini, wapo kama wapagani vile... Hua wao wanachojua ni pesa na starehe kwa kwenda mbele,... Geti lenyewe hakina mtu wa kufungua, bali kila mmoja kuna saa maalumu kaivaa hio ni spesho kwa familia hii,.. Na kama huna saa basi Utapiga kengele uje ufunguliwe, lakini kama una saa basi ni mwendo wa kuminya ukiwa humo humo ndani ya gari,..







     





    Mama mzazi wa watoto hao alipomwona mtoto wake wa mwisho alimkimbilia sana na kumhag, (kukumbatiana)... Mama alifurahi sana kumwona mtoto wake,..

    "weee ram umekonda mwanangu"

    Aliongea mama yake ram au ramy.. Na wala ram hajakonda ila si unajua tu mambo ya akina mama, kupenda sana watoto wao wa kiume hata akinenepa atasema kakonda, ni upendo wa wazazi tu...



    Basi waliingia ndani kisha akaandaliwa madiko diko ya maana, lakini ram alikuwa hatulii, moja haikai mbili haikai,....

    "mamy, gari yangu ipo wapi pale mbona siioni"

    Aliuliza ram, mana familia yote kila mmoja ana gari yake,

    "baba yako kasafiri nayo.. Alafu wataka uende wapi na hujala"

    Aliongea mama huku akimshika mkono kumzuia asitoke

    "mama nimewamisi sana machizi wangu"

    "kula kwanza"

    "mama nitakula nikirudi"

    Ram ni mtoto alielelewa katika mazingira ya kuachiwa sana kiasi cha kwamba ni yeye na starehe ni yeye na pesa... Hata mlango wa msikiti haujui toka kuzaliwa kwake,.. Hajui hata neno la Quran tukufu, yeye anajua starehe tu,..



    Ram alitoka na gari ya baba yake, na kuelekea zake mjini kwa marafiki zake,... Aliwachukuwa washkaji zake kisha haoo, mwendo wa kwenda katika club kubwa kubwa zenye starehe za kila aina,.. Vinywaji alivyokuwa akivinunua, ni vinywaji vya gharama kubwa sana, usishangae ram kuacha milioni moja kwa masaa mawili tu... Walikunywa sana na kila mmoja aliondoka na mschana wake anaemjua...



    Ram alirudi nyumbani usiku sana kama saa 6 hivi, kaingiza gari viziri na wakati huo alikuwa kalewa sana, mana kanywa vile vinywaji vya gharama kubwa ambavyo havileweshi sana kama utagusa gusa tu, lakini ukinywa nyingi hata kutembea utashindwa,..

    "mamaaaa"

    Ram aliita huku akishindwa hata kutoka kwenye mlango wa gari kwa kulewa,.. Mama yake alikuwa sebuleni hata kulala hajalala mana Mziwanda wake hajarudi,.. Japo ni tabia ya ram kila anapokuwa nyumbani kwa likizo hizi hua anakuwa mtu wa starehe sana na mama yake keshamzoea kihivyo yani,



    "rahim mwanangu, leo umekunywa sana kwanini lakini"

    Aliongea mama yake huku akimtoa katika gari

    "mamaaa... Gambe (unywaji) la leo tamu mno"

    "lakini umezidisha baba"

    Mama akaanza kumkokota mtoto wake mpaka ndani,.. Na kwakuwa alikuwa kashiba alipotoka, basi mama hakuhangaika na kupika, japo wafanyakazi wapo wengi sana lakini kwa watoto wake hua anawapikia mwenyewe, eti haamini kama wanaweza kuwapikia watoto wake, hivyo anawapikia mwenyewe....  Ndani ya jengo hilo kuna wafanyakazi wengi sana na kila mtu ana kazi yake... Yaani watoto wa hii nyumba wakiamka tu ni wao na kula na starehe kwa wingi, hawana kazi wanajua hawa... Tena hapo ndani penyewe kuna kaunta utafikiri baa,.. Kama mtu una hamu ya wine basi unaingia kaunta na kujisevia... Na hapo kaunta hakuna Serengeti, hakuna Eagle, hakuna Safari, hakuna Kilimanjaro, Hakuna Tusker,.. Yaani hakuna kinywaji cha elfu 3 au 5...yaani hapo ni mwendo wa wine, wiski yaani vile vinywaji vinavyo anzia na bei ya shilingi laki moja na kuendelea



    **************************************



    Ikiwa ni siku ya ujumaa, iliotukuka umma ulishangaa kumwona shekhe fulani leo akiingia msikitini,.. Kila mtu alishangaa sana kwa kumwona shekhe aliovalia ki Nigeria,.. Wapo waliofurahia ujio wake lakini hakuna aliochukia ujio wake na wapo walioshangazwa na ujio wake...

    "as Salaam Aleykum"

    Aliwasalimia watu wote waliopo msikitini, tena alifika muda muafaka, katika swala ya Ijumaa mchana kweupee

    "aahhh shekh rahim"

    Aliitwa na imamu wa msikiti huo kisha akapewa nafasi ya kuswalisha ijumaa ya leo...

    "naam mzee wangu"

    "nina furaha sana kuwa na kijana mtiifu kama wewe.... Leo sijiskii vizuri hivyo nipo nyuma yako leo"

    Aliongea imamu huyo huku rahim anajua maana ya kukaa nyuma yako, yaani kampa nafasi ya kuswalisha Al Ijumaa kareem,.. Huezi amini alikuwa ni rahim ndie mswalishaji wa Ijumaa ya leo,... Sasa hapa inakuwaje, mbona rahim tunaemjua sisi ni mtu wa starehe tu na hajui cha msikitini wala nini... Sasa mbona hapa anaonekana kuswalisha tena anaswalisha umati wa watu wasiopungua 300,... Sasa huyu ni rahim yupi na yule sharobaro mhuni ni rahim yupi?







    Kweli ram alikuwa ni kijana aliojawa na imani ya dini haswa,.. Kwani hata alipokuwa aki kim swala, ilikuwa inapendeza sana, kijana aliovalia kanzu yenye rangi bluu, kibarakashee chenye rangi ya bluu... Alipendeza sana,... Kama kawaida dakika chache tu mnamaliza swala ya Ijumaa,.. Baada ya swala, rahim alipongezwa sana mana ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuswalisha katika msikiti mkubwa sana uliopo mjini kati ila hatujui ni mji gani,.. Rahim alitoa mikono ya heshima kwa maostadhi wakubwa wakubwa huku akipongezwa sana, na wakati huo alikuwa akitoka nje kuwahi kitu fulani.. Lakini ile anafika tu nje, aliona mschana mweupe pee, kama malaika, mschana huyo alikuwa kapiga uchungi mzuri sana, nae alikuwa akitoka msikitini katika upande wa wanawake...

    *************************************



    "uuuuuuwiiiiiiiiiii... Mamaaaa"

    Rahim alizinduka usingizini usiku wa manane, huku akiwa anahema juu juu, mama yake alikuja chumbani kwa rahim huku akiita

    "rahim, mwanangu una nini"

    Aliuliza mama yake

    "mama... Huezi amini nimeota nipo msikitini, tena mbaya zaidi nilikuwa naswalisha watu zaidi ya 300 mama"

    Aliongea hayo ram huku akisema MBAYA ZAIDI yaani badala ya kufurahi yeye anasema mbaya zaidi

    "mwanangu, watakuwa ni wachawi hao.... Wewe huezi ota mambo kama hayo... Huo ni uchawi tu.. Pole sana mwanangu"

    Yaani nyumba ya kishetani ni ya kishetani tu,... Yaani badala waone ni jambo jema eti wanasema ni uchawi huo...



    Basi siku hio iliisha lakini ram bado anaiwazia ile ndoto ya kuingia ndani ya msikiti tena ameswalisha umati wa watu,... Lakini sasa kumbe yeye hawazii hilo, yeye anawaza mwisho wa ile ndoto kuna mwanamke kamuona.... Hicho ndicho anachokiwaza rahim....

    "we vipi, mbona umetulia huku uwani peke yako"

    Alikuwa ni kaka yake jamali, ndie alie muuliza

    "broo, we acha tu.. Yaani kirudi shule jana tu... Wachawi wameshaanza kinifuata..."

    "wachawi??...wachawi gani tena... Au ni yule mama nini?... Mi nakuambia yule mama balozi ni mchawi sana yule.. Alafu naskiaga anataka watoto wa mwisho mwisho tu"

    Aliongea jamali huku akitaka hata kuamka na kumfuata huyo mama

    "mi nadhani sio huyo mama"

    "ndie tuuu"

    "nimeota nipo ndani ya msikiti"

    Jamali kusikia hivyo aliruka mpaka akadondoka  hini

    "unasemaje wewe"

    "we acha tu broo... Tena mbaya zaidi nimeswalisha watu.. Nimevaa kanzu kubwaa"

    "weweeeeeee.... Ahh Kudadeki kweli huo uchawi babu kubwa.. Yaani wewe uingie msikitini wewe... Hakiyamungu vile lazima siku hio mtu afe.. Au huo msikiti lazima uvunjike"

    Aliongea jamali huku akicheza cheza kwa furaha ya ndoto ya rahim,...

    Mara ghafla mama yao katokea pale walipo

    "nyie kuna nini hapa mbona makelele tu"

    Aliongea mama yao huku jamali akimjibu kuwa

    "mama... Huyu balozi sasa ataniulia mdogo wangu.... Yaani mpaka kampeleka msikitini kweli"

    Aliongea jamali huku kijasho Chembamba kikimtoka, kwa maneno ya kuikashifu dini yao,.....

    "mi naona aende kwa bibi yake... Mana huyu balozi ataniulia mwanangu"

    Mama nae aliingiza hofu kuhusu swala hilo,...

    "ndio mama, kama vipi rahim aende akale likizo kwa bibi... Mana huyu balozi mimi nitamuua"

    Aliongea jamali lakini ram yeye yupo kimya wala hana hata neno la kuongea, yeye anawaza tu yule mwanamke aliemuona wakati akitoka msikitini,...

    "rahim mwanangu,... Si utaenda kwa bibi yako"

    "mmmhhh huko kwa bibi kwani kuna uzuri gani"

    "yaani ram mwanangu.. Bibi yako akuloge"

    "sina maana hio... Wewe unajua tanga kulivyo, kumejaa wachawiii"

    "sawa, lakini bibi yako ni mwenyeji wa kule, lazima watakuogopa... Afu kule kuna upepo mzuri.. Utainjoi."

    Aliongea mama huyo huku ram akikubali kishingo upande,..

    "kwanza kule ndio kwenu, nani anaweza kuloga mtu wa kijiji hicho hicho"

    Mama rahim alizidi kumweleza mtoto wake juu ya safari hio

    "sasa nitaenda na nini"

    "si utachukuwa gari la baba yako hilo"

    "aahhhh kila saa kuingia sheli, silipendi hilo gari mama"

    "ataendesha kaka yako jamali"

    "ina maana nakwenda na huyu bwege"

    "aahhhh sasa mbona wamuita kaka yako bwege"

    "huyu ni bwege huyu.. Hata kutongoza hajuagi"

    Mama kuskia hivyo aliondoka zake mana ni vijimambo vya watoto wake hivyo haoni haja ya kuvisikiliza...



    Baada ya siku kama mbili hivi rahim alipanga kila kitu  hake, na jamali pia alifanya hivyo,.. Walipakia mabegi yao kuelekea mjini tanga,..

    Lakini walipokua wakitoka nje ya geti, walikutana na gari ya kifahari hapo nje ya geti lao,... Alishuka mschana mrembo sana tena ni mtoto wa tajiri kama yeye alivyo,.. Na anamjua vizuri

    "rahim Mambozako mpenzi wangu"

    Alisalimia dada huyo lakini ram hakuwa na taimu nae

    "poa"

    "jamani rahim, toka urudi chuo, mpaka leo hujawahi hata kunipigia simu kwanini lakini"

    Aliongea mdada huyo huku, akifikicha vidole vyake....

    "oya ram... Si unasemeshwa huko"

    Aliongea Jimmy huku akimtaka kutoa gari....

    "aahhh achana nalo"

    "heeeew rahim, yaani unaniambia mimi hivyo kweli.... Rahim mpenzi wangu"

    "ebu toa gari tupite"

    Lakini mdada huyo alionekana kuvaa saa apeho kwa ajili ya geti, hivyo ni mtu wa karibu wa familia hii,...

    Ghafla mama katokea pale getini huku akisema

    "ina maana bado hamjaondoka tu"

    Aliongea mama huyo,....

    "waaoooo mama mkwe.. Shkamoo"

    "Marahaba mwanangu... Shakira hujambo"

    "sijambo mama... Nilikuwa naongea na ram"

    Aliongea Shakira kumaanisha ya kwamba, anamjali sana ram...

    "okeee... Ila utammisi kweli ndani ya wiki hizi"

    "kwanini mama nitammisi"

    "hapo alipo anakwenda kwa bibi yake tanga"

    "Whaaaat???.... Ram.. Yaani unaondoka hata kuniaga huniagi kwanini"

    "ram alifunga kioo kwa dharau"

    "ram jamani..... Mama mi lazima niende na ram... Siwezi kubaki mwenyewe hapa mjini"

    Ohoooooo Shakira nae Anataka kwenda na mbaya zaidi ram hampendi dada huyo, sema kwa shinikizo la wazazi kutaka kuoana kwasababu wote ni matajiri, na hataki mwanamke kapuku..

    "shakira mwanangu... Muache atarudi tu"

    "hapana mama... Lazima nikaishi nae huko huko"

    Ram kafungua kioo huku akisema









    JAMANI NDUGU WASOMAJI WANGU, KAMA KINA MAHALI UTAKUTA NENO ( SAM ) BASI UJUE LIMEKOSEWA TU, BALI NI ( RAM ).. KUNA SIMULIZI NYINGINE NAIANDIKA AMBAYO SHEBY AMETUMIA JINA LA SAM,.. HIVYO SAM NA RAM VINAENDANA,... KWAHIO UKIKUTA NENO SAM, HEBU LIFANYE KAMA VILE RAM... MANA LITAKUWA LIMEKOSEWA... SAM NI JINA LA KWENYE SIMULIZI NYINGINE SIO HIII... HII ANAKWENDA KWA JINA LA RAM.. NA SIO SAM



    Unajua kuna itikadi za kifamilia zinakuwa kama zinataka kuendana,.. Mtoto wa masikini anapenda sana kuolewa na mtoto wa tajiri, lakini wazazi wa watoto wa kitajiri hawataki mtoto wao aoe au aolewe na mtoto wa kimaskini,.. Familia ya kitajiri hua inataka inataka muunganiko wa matajiri wenzake, yaani hataki masikini, hivyo Shakira nae ni mtoto wa mfanyabiashara mmoja maarufu sana jijini Arusha, hivyo kwao nae ni tajiri na hata wazazi wa rahim pia wametazamia mwanae amuoe Shakira, lakini kwakuwa mapenzi ni sawa na ndege anatua mti aupendae,... Kiukweli rahim hana mapenzi ya kweli kwa Shakira na licha ya hivyo, pia hajawahi hata kumuomba penzi lake,  hivyo hana hisia nae kwasababu ni mschana wa kuchaguliwa tu, hajampenda yeye kama yeye,... Sasa shakira alipokuwa anang'ang'ania kwenda na rahim tanga,... Rahim akafungua kioo huku akisema

    "nisikilize kwa makini we shakira.... Usije ukahisi mimi nakupenda, kaa ukijua sina hisia na wewe hata kidogo... Waambie wanaotaka nikuoe wakuoe wenyewe, mimi sina hisia na wewe... Achia mlango wa gari yangu na uondoke... Afu mazoea na wewe sitaki"

    Mama yake rahim kasikia kila kitu alichokisema mtoto wake rahim

    "we ram wewe... Unasemaje?.... Yaani unasubutu kuongea ujinga namna hio mbele yangu.... Shakira njoo mama, tutayamaliza tu"

    Wakati huo shakira analia tu hana la kisema zaidi ya kulalamika tu

    Rahim alipoona mama anazidi kutangaza Injili aliondoa gari kwa spidi kali,... Ndio safari ya tanga imeanza hio, kawaacha watu wengine wakiwa katika huzuni...

    Mama yake ram akiwa katika hali ya kumbembeleza shakira aliopewa vigongo vyake muda sio mrefu,...







     





    "lakini rahim, hujafanya fea pale,.. Mwanamke hua haambiwi ukweli"

    Aliongea jamali ambae ni kaka yake na rahim,...

    "amna lolote, mwanamke ukimficha ficha ndio anazidi kukusumbua,.. Mpe makavu live atuloe mbele uko"

    "kiukweli imeniuma sana... Afu mtoto mwenyewe mkali vile unampa maneno hayo kweli"

    "hata mbwa ni mkali weweee,... Sio yeye tu"

    "ahhh... We kweli umelaaniwa"

    "acha swaga zako basi broo"

    Basi walikuwa wakiongea huku safari ikiendelea kwenda,... Walipitia supermarket na kununua zawadi nyingi sana kwa ajili ya bibi na babu kule kijijini,... Rahim alikuwa anafurahi sana mana hajawahi kwenda kula likizo tanga kwao, na leo ni kama mara ya pili au tatu, lakini mara zote hizo hakwenda kula likizo bali alikwenda kwenye misiba misiba tu...

    "bibi anapenda chocolate utafiki katoto cha kike"

    Aliongea ram huku akinunua chocolate za kutosha

    "yule ni binti wa zamani wewee

    Basi walikusanya bidhaa nyingi sana katika Mall mpya iliopo jijini Arusha iitwayo AIM MALL... Baada ya kujaza baadhi ya vitu katika VOGUE DISCOVERY V 807 ya baba yao,.. Safari ilianza rasmi ya kuelekea tanga, kama unavyojua umbali wa Arusha to Tanga ulivyo,... Iliwachukuwa masaa kadhaa huku wakibadilishana kuendesha,.. Walikuwa wawili tu katika gari hio,..



    Baada ya masaa kadhaa walifika tanga mjini,.. Sasa wanashika njia ya kwenda katika mitaa yao,.. Ambako ndiko jengo lao la kitajiri lilipojengwa,

    Mitaani watu ni kushangaa gari ilivyo new model, gari ya bei ghali zaidi duniani,.. Afu wanaendesha watoto wadogo tu,.. Bibi alipoona gari hio alijua ni mtoto wake mzee rashidi, yaani baba yao na akina rahim, lakini sivyo,.. Kumbe ni mijambazi yake ndio imevamia gari,... Sasa kama unavyojua maisha ya tanga, baiskeli nyingi sana, sasa katika pita pita wakati huo ram alikuwa anamwangalia bibi yake pale nje, mara ghafla kuna mtoto kapita mbele ya gari akiwa na baiskeli... Watu walishika vichwa tu... Ram alishuka haraka haraka na kumkomba yule mtoto aliokuwa akitokwa na damu nyingi sana kichwani,.. Ram alimpakia yule mtoto kisha wakamkimbiza hospitali..

    "we ulikuwa unaangalia wapi... Ona sasa mtoto wa watu akifa je"

    Alikuwa ni jamali aliokuwa akimfokea ram ambae ni mdogo wake,...

    "broo huu sio wakati wa kulaumiana.. Mcheki dogo uyo asizime"

    "aya yote umeyata wewe, ina mana humjui bibi mpaka uanze kumwangalia anavyokuja"

    "tulia basi broo mbona injili nyingi ivo"

    "sio ivo, tatizo lako ni msomi lakini hutaki kutumia akili zako kwenye vitu vya hatari kama hivi"

    Jamali alikasirika sana kwa kitendo kilichotokea hapo...

    Kwanza alipelekwa katika hospitali ya karibu na wao,.. Ili kupata huduma ya kwanza,.. Rahim kichwa chake kimechanganyikana yaani akileta utani anaweza kugonga mwingine tena mana alikuwa spidi sana ili kuweza kumwahisha kijana huyo..



    Walipofika hospitali mara moja machela ililetwa, mtoto huyo akaingizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi,.. Mana damu nyingi sana zilimtoka mtoto huyo na hata kutikisika alikuwa hatikisiki,... Akina rahim na kaka yake Jamali wakuwa katika mlango wa wodi hio huku wakiuzunguka kila mara,... Yaani hata kukaa hakukaliki,... Kuna viti lakini vilikuwa kama vina moto vile,... Baada ya kama nusu saa hivi mara dokta katoka huku akifungua kile kitambaa alichofunga puani,...

    "dokta hali ya mgonjwa vipi"

    Aliuliza rahim huku akiwa na wasiwasi juu ya mgonjwa wake,.. Kula likizo kumegeuka kula mateso ya moyo, mana kwa utajiri wao wanaweza kulizimisha swala hilo kama mtoto huyo atakufa... Lakini sasa roho ya mtu haiwezi kurudi... Wakati huo huo ndugu, wazazi ndio wanaingia... Ram ndio presha inazidi kumjia yani...

    "dokta... Mgonjwa wangu anaendeleaje lakini"

    Ram alirudia tena lakini dokta alikuwa mpole sana kwa hali isiojulikana...

    "samahani sana kijana... Kiukweli tumejitahidi sana kadri ya uwezo wetu,... Lakini tumeshindwa kumtibu mgonjwa wako"

    Ram machozi yalianza kumtoka huku akisema kuwa

    "una maana gani dokta,... Eeehh mungu wangu siamini kama nimeua mtoto asiekuwa na hatia"

    Sasa wale wazazi na ndugu waliokuja walikuwa hawajui kama hawa vijana ndio waliomgonga mtoto wao, sasa waliposikia tu ram akisema haamini kama kaua mtoto asiekuwa na hatia... Mama wa mtoto huyo nae kadondoka chini.... Machela nyingine ikaletwa kwa ajili ya mama....









    Rahim ni kijana mwenye roho ya huruma japo katawaliwa na mambo ya kidunia,.. Starehe ndio imemharibu rahim au familia yote wanaishi kistare tu, hawajui kama kuna mungu hawajui kama kuna kumswalia mtume Muhammad na Mwenyezi Mungu kwa ujumla, wao hawalijui hilo, dunia imewatawala kutokana na utajiri wao,... Rahim kila akirudi shule katika likizo ndogo yaani yeye hushinda kwenye maclub makubwa makubwa,.. Na wazazi wanalijua hilo, mana kuna siku familia yote inatoka auti, na hio ndio sababu mpaka watoto sasa hivi wanakuwa ni wachafu wa kupindukia, na yote haya yanasababishwa na wazazi wetu, katika hizi familia zenye unafuu wa maisha.... Wazazi tuwalee watoto wetu vizuri hata kama una uwezo kiasi gani, mlee mwanao vizuri



    Sasa rahim akiwa hapo hospitali ndogo ndogo tu ya mtu binafsi,.. Dokta alitoka huku akiwa na huzuni kwa kiasi fulani na kumwambia rahim kuwa, wameshindwa kumtibu mtoto huyo..



    "una maana gani dokta,... Eeehh mungu wangu siamini kama nimeua mtoto asiekuwa na hatia"

    Sasa wale wazazi na ndugu waliokuja walikuwa hawajui kama hawa vijana ndio waliomgonga mtoto wao, sasa waliposikia tu ram akisema haamini kama kaua mtoto asiekuwa na hatia... Mama wa mtoto huyo nae kadondoka chini.... Machela nyingine ikaletwa kwa ajili ya mama







     





    "dokta... Ina maana mumeshindwa kumponya huyo mtoto"

    Aliongea rahim huku akilia haswa, mana hakutegemea kuua na pia hajawahi kuua,..

    "lakini kijana.. Huyu mtoto bado hajafa.. Ni mzima tu"

    "we dokta una akili wewe... Sasa mbona umesema mumeshindwa, una maana gani"

    Wakati huo akiongea hayo kwa pembeni kuna jamaa mmoja ambae ni ostadhi,.. Na huyu jamaa ni kaka wa yule mtoto,.. Na yule mama aliozimia ni mama wa yule mtoto, halafu kuna kabinti kengine keupe pee ambako kwa sasa kapo na mama yake kule ndani baada ya kuzimia, nae huyo binti ni dada yake na huyo mtoto,..

    "hapana kijana... Nilikuwa na maana ya kwamba, hospitali yetu imeshindwa kumtibu, hivyo naomba muende hospitali kuu ya mkoa wa tanga"

    Rahim kusikia hivyo alitamani hata kuruka na huyo mtoto mpaka kwenye hio hospitali,... Sasa kabla hajauliza ni hospitali gani, yule binti katokea ili kumuita dokta,.. Wakati huo yule binti alikuwa analia ila machozi yake huezi kuyaona kwasababu kavaa kininja, mana ni mtoto wa Kiislamu,...

    "hio hospitali inaitwa na ipo maeneo gani"

    Rahim aliuliza huku binti akitaka kumuita dokta

    "huyu mtoto mpeleke Bombo Hospital, kule atapata matibabu mazuri tu"

    "Bombo Hospital ipo wapi hio hospitali"

    Sasa kabla dokta hajajibu, yule binti kamshika rahim mkono huku akisema

    "nitakupeleka kaka yangu, naomba mdogo wngu apone tu"

    Sasa kile kitendo cha binti yule kumshika rahim... Rahim alisisimkwa na mwili wake kama vile kapigwa shoti,... Sasa ram kuona vile alimkwapua yule binti mkono ili asiushike tena

    "niachie bwana... Na usinishike tena, una hadhi gani ya kunishika wewe"

    Lakini sasa kumbe sio rahim peke yake aliosisimkwa, kumbe hata huyu binti pia alisisimkwa na mwili wake baada ya kumshika rahim... Binti alibaki kulia tu muda wote, mana rahim aliongea maneno machafu sana katika kinywa chake, na hapo hajitambui kuwa yeye ni nani, bali anajijua tu kuwa ana pesa nyingi za baba yake,.. Sasa yule ostadhi aliokuwa nyuma ya rahim, yeye akasema

    "astah khafirullah"

    Baada ya yale maneno ya rahim kumwambia mdogo wake kuwa hana hadhi ya kumshika, mana wao ni matajiri na hawa ni masikini tena masikini haswaa,...

    "we nawe vipi huku nyuma yangu, au unaniloga nini na wewe"

    Aliongea rahim baada ya kusikia ile Astah Khafirulah...

    "Samahani ndugu yangu... Naomba tumtibu ndugu kipenzi... Samahani kama nimekuudhi ndugu yangu"

    Yule ostadhi aliomba tu msamaha juu ya tukio hilo,.. Rahim ana roho ya huruma kidogo sana, lakini ana roho ya dharau mno,...

    "Skia dokta, naomba unipeleke katika hio hospitali"

    "hapana mimi siwezi kutoka hapa, mana ndio mkuu wa matibabu hapa"

    "sasa nitapelekwa na nani"

    "lakini kijana... Hawa ni ndugu wa huyo mtoto, kwanini wasikupeleke"

    "wachawi hawa we huwaoni"

    Yule ostadhi akaruadia tena yale maneno

    "astah Khafirulah"

    "we vipi jamaa... Tueshmiane bwana"

    Rahim aliingia ndani na kumchukuw yule mtoto kisha akamueka pale ndani ya gari yao, wakati huo buti ya gari hio imejaa vitu vya kula kula tu.. Ndugu wa mtu huyo hawakupata hata nafasi ya kupanda katika gari hio kwasababu wanaonekana ni wachawi,... Rahim alichukuwa mtu mwingine ili aende nae huko hospitali



    Baada ya nusu saa gari ilifika katika hospitali kuu ya mkoa wa Tanga, iitwayo BOMBO HOSPITAL, mtoto alipokelewa vizuri kisha akapatiwa matibabu mazuri tu,... Na wakati huo mama, kaka, dada, baba, wote walishafika hospitali hapo kwa ajili ya mtoto wao,.. Lakini sasa likaja swala la yule mtoto kuongezewa damu, japo hali yake sio mbaya kiafya,.. Lakini damu inahitajika

    Ndugu walipimwa lakini nao damu zao zilikuwa ni chache mwilini, mana mtu anaetakiwa kutoa damu anatakiwa awe na damu nyingi, sasa kama ni chache afu ukatoa atajikuta nae anaingia kwenye matatizo,.. Damu iliomwagika ilikuwa ni nyingi sana, hivyo kunahitajika damu nyingi mno ili mtoto awe imara kama zamani,...

    "aaahhh jamani... Tumewapima wote hamuda damu za kutosha... Lakini damu ya kuuza ipo"

    Aliongea dokta huyo huku baba wa mtoto huyo akisema kuwa

    "ni kiasi gani hio damu dokta"

    Aliuliza baba mtu kisha dokta akajibu

    "lita moja inauzwa shilingi milioni 3"

    "mtume roho yangu... Yaani damu inauzwa kama nyumba.... Mungu wangu mwenetu atapona kweli"

    Lakini kama nilivyokwambia kuwa rahim ana roho ya utu, ila kajawa na dharau na kebehi, kwa ajili ya pesa zao....

    "dokta, naomba unipime mimi, kama itakuwa sawa utoe hata kama ni lita nne"

    Aliongea rahim yule yule mwenye kiburi cha pesa, mpaka anaikashifu dini yake kwasababu ya pesa, na yote haya ni malezi ya wazazi.. Basi dokta alimchukua ram mpaka ndani na kuanza kumfanyia vipimo...

    "jamani huyu kijana ana imani ya kuseidia watu"

    Aliongea baba mtu, huku mama akidakia kuwa

    "ni kweli.. Unajua mtu kujitolea damu sio kitu rahisi baba zena... Na hata kama kamgonga yeye, lakini haikuwa na lazima ya kutoa damu.. Lakini ona katoa.. Kiukweli ana malezi huyu mtoto"

    Mama na baba hawakuweza kushuhudia dharau za rahim lakini walio ona ni kaka na dada,... baba na mama hawajui

    "mama... Achana kabisa na huyo kijana,.. Dharau imelala hapo wacha kabisa... Zena alimshika tu mkono.. Huezi amini maneni alioyatoa huyu kijana.. Yanakera mno mama, nilitamani hata kulia"

    Sasa huku chini ya miguu, zena alikuwa akimkanyaga kaka yake kuwa asiendelee kusema,... Mara ghafla rahim katoka na dokta,..

    Familia ikanyanyuka ili kujua kinachoendelea,...

    "dokta, mtoto wetu kapata tiba"

    Mama aliuliza, huku baba mtu akitoa shukrani kwa kijana huyo japo hawajui kama wamefanikiwa

    "aahhhh.... Mtoto wenu atapata damu, na tumefanya vipimo vyote kwa huyu kijana, na damu yake inaendana vizuri tu... Ila sasa"

    Familia kusikia neno, ila sasa walianza kupatwa na wasiwasi juu ya kijana huyo.









    Akina jamali na mdogo wake ambae ni rahim, watoto wa mzee rashidi, tajiri mkubwa sana jijini arusha,... Jamali alishamaliza chuo na sasa anafanya kazi kwenye kampuni ya baba yake, na rahim yeye bado yupo chuo mwaka wa mwisho huu, na sasa yupo likizi mkoani tanga ambako amezaliwa baba yake,... Lakini sasa akina jamali walipotoka arusha waliingia AIM MALL (Supermarket) wakanunua vitu vingi sana mpaka vinywaji vile vya bei ghali,... Kama vile waini, wiski, dorodo wisk, Angel,... Na kila kitu,.. Na walikuwa wakinywa katika gari, na ndio maana ajali ilitokea kwasababu walikunywa wakiwa ndani ya gari..



    Sasa baada ya ndugu wazazi kupimwa, na kugundulika damu za wengine ni chache, na wengine ni damu za kizee, hususan baba na mama wana umri mkubwa hivyo huezi kutoa damu kumpa mtoto mdogo, mana ni damu za kizee hizo,



    Baada ya wao kushindikana kutoa damu, rahim alijitolea kutoa damu, aliingia ndani ya wodi na kupimwa vizuri,... Dokta alitoka pamoja na rahim, wazazi wote na ndugu wakasimama ili kujua hali ya kupata damu kwa ajili ya mtoto wao,

    "aahhhh.... Mtoto wenu atapata damu, na tumefanya vipimo vyote kwa huyu kijana, na damu yake inaendana vizuri tu... Ila sasa"

    Familia kusikia neno, ila sasa walianza kupatwa na wasiwasi juu ya kijana huyo...

    "dokta, una maana gani kusema Ila sasa"

    Aliuliza mama yake zena, kisha dokta akamjibu kuwa

    "huyu kijana, ana damu nyingi sana.. Lakini sasa, Damu yake ina kemikali za pombe,.. Amekunywa pombe muda sio mrefu.. Hivyo anapaswa kukaa masaa 48 mpaka kemikali hio iishe mwilini mwake ndipo tutoe damu"

    Zena aliposkia rahim kanywa pombe, alitamani hata hio damu isitoke tena, mana anahisi mdogo wake ataambukizwa damu ya pombe....

    "lakini dokta, sasa mtoto wangu itakuwaje, mana ni masaa mengi mno"

    "aahhh mtoto hana tatizo, na ataweza kufikisha siku hizo... Lakini kikubwa zaidi ni huyu kijana asinywe pombe ndani ya siku hizo"

    Jamali kuskia maneno hayo alishtuka sana, mana anamjua rahim hajawahi kupitisha hata siku moja bila kunywa hata grasi moja.. Mana hata kule shule, kuna ka Supermarket ka shule kwa ajili ya wanafunzi, na rahim alikuwa akiagiza wine kwa siri, hivyo hata kule ahule alikuwa anakunywa, na zilikuwa zikija kwa njia ya kuingiza bidhaa za Supermarket kwa ajili ya wanafunzi... Mana ni shule za Boding,...

    "sasa dokta nadhani wataka kuniulia mdogo wangu"

    Aliongea jamali huku akitaka kumchukuwa waondoke zao...

    "broo subiri... Mimi nataka nihakikishe huyu mtoto anapona,.. Nipo tayari kuvumilia hayo masaa"

    Aliongea rahim huku akiwafuata wazazi wa mtoto huyo...

    "Samahanini sana wazazi wa huyu kijana... Mimi ndie niliemgonga mtoto wenu, na nitahakikisha mpaka anapona,. Kwahio nyinyi kazi yenu ni kuja kumjulia hali tu... Lakini kila kitu kuhusu matibabu nitalipia mimi"

    Aliongea rahim kisha wakaingia kwenye gari,... Wazazi na ndugu waliingia katika wodi ili kumwangalia mtoto wao,.... Rahim alishalipa kila kitu hapo hospitali hivyo hakudaiwi kitu chochote kile...







     





    Safari ya kwenda kwa bibi ndio imeanza upya, mana hapo walikuwa Bombo Hospital....

    Ndani ya gari kumejaa vinywaji vile vya bei ghali mno, yaani ni vile vinywaji vya kitajiri, Rahim alikuwa akiviangalia tu huku akivitamani,... Bibi yao alikuwa nje ya nyumba akiwasubiria mana katika ile ajali bibi aliona hivyo wasiwasi ukamjia kuhusu wajukuu zake,... Jumba lao la hapo kijijini ni balaa,...

    "nyie mu wazima jamani"

    Bibi aliwauliza wajukuu zake kuwa wapo salama, wakati huo kuna mfanyakazi wa kike aliokuwa akiingiza vitu ndani pamoja na mapombe yale ya kitajiri, sio viserengeti vyenu vya elfu 2,... Mfanyakazi wa ndani alikuwa ni mschana mzuri sana lakini rahim hakuwa akiliona hilo, ni kumpelekesha kwa kwenda mbele,.. Rahim kitu cha kwanza alikimbilia kulala, ili kuweza kupumzisha akili yake, wakati huo jamali yupo sebuleni akitupia grass mbili tatu huku akitazama mpira katika tv..

    "wewe mshenzi, humu sio baa"

    Aliongea bibi huku jamali akicheka na kumjibu kuwa

    "we bibi Weeeee, pesa ipo, kila kitu kipo, kwanini tusifurahi... Hebu njoo upate mbili tatu"

    Jamali alikuwa akimtania bibi yake

    "we, hivi huyo mtoto wa watu ni mzima?"

    "bibi... Mtoto yupo salama, sema tabu kwa mjukuu wako"

    "kafanya nini tena"

    "kajitolea kutoa damu kwa yule mtoto, lakini alivyopimwa amegundulika kuwa ana kemikali ya pombe... Hivyo akae siku mbili bila kunywa pombe, kisha akatolewe damu"

    "kwanini kafanya hivyo"

    "kaamua mwenyewe"

    Bibi yake rahim hakupenda rahim atoe damu,.... Kule chumbani rahimu kasikia maongezi yote, akaamua kutoka

    "nasema hivi, hata kama nisingemgonga mimi, lakini damu ningetoa tu"

    Aliongea rahim huku akija hapo sebuleni na kumkuta jamali akinywa wiski moja ya gharama sana...

    "sasa broo baada unifariji ara nizifikishe hizo siku, afu ndio kwanzaa unanitamanisha"

    "kwani nilikutuma utoe damu"

    Yaani familia hii pombe kwa ni kama maji yaani hawalali bila kunywa, tena bora hata jamali kuliko rahim,...  Basi yalikuwa ni maongezi ya kawaida tu lakini bibi hajapenda mjukuu wake atoe damu

    "lakini rahim mjukuu wangu... Kwanini uendeshe gari na wakati imelewa... Afu huku kulewa kwanini huachi ingali bado ni mwanafunzi"

    "bibi tulia nawewe, au chukuwa zamu yangu hizi siku mbili... Mana unaongeea"

    "mshenzi wewe... Nitokeee hapa mlevi wewe"

    Utani wa bibi kama tunavyoujua ulivyo,...



    BAADA YA SIKU MBILI HIVI KUPITA



    Na leo ndio ile siku ya rahim kwenda kutoa damu, lakini huezi amini rahim mpaka kaumwa kwa kukosa japo grass moja tu ya pombe, na mbaya zaidi toka aje hajawahi kwenda sehemu yeyote ile ya starehe zaidi ya kutembelea hospitali,...

    "unaweza kulala na ulilax vizuri.. Yaani usijikaze"

    Sauti ya dokta ikimuamuru rahim asijikaze mana akijikaza ataizuia damu kutoka,... Damu ya rahim ilikuwa ni safi kupita maelezo, mana ana siku 2 na masaa kadhaa hajapata hata gras moja ya wine,.. Shukrani zilitoka katika upande wa familia, licha ya kumgonga yeye, lakini jambo alilofanya ni jambo zito mno, rahim alitoka mpaka pale nje na kumkuta yule dada yake na yule mtoto,... Rahim hua hapendagi mwanamke aliefunika uso, yaani wale wanawake wanaovaa kininja ninja, alimwangalia sana huku moyoni mwake anasema kuwa

    "anaonekana mtoto mdogo lakini mchawi"

    Yaani rahim imani ya dini hana kabisa, lakini anajua kuwa kuna mungu, ila anazidharau dini mno,..

    "As Salaam Aleykum Warahmatullah Wabarakatuh"

    Alisalimia yule dada, huku akiwa kainamiana chini japo haonekani sura lakini anaona aibu...

    "safi tu"

    Rahim alishindwa kuitika jinsi inavyotakiwa na badala yake ameitika salamu ya kidunia,... Na hata hio yenyewe ameitika huku akiangalia pembeni kana kwamba hajapenda kusalimiwa.... Yaani hapendi wadada wa aina hio hata kidogo,...

    "ivi ukivua huo mnguo wako utakufa"

    Aliongea rahim huku akiwa kashikilia mkono pale kwenye alama aliotolewa damu,..

    "haya ni mavazi ya heshima kwangu siwezi kuyavua"

    "waaapi nyie mnaloga watu nyie"

    "astah khafirulah... Usiseme hivyo we kaka"

    "umesemaje.... Umentukana nini?"

    "basi nisamehe, lakini sijakutukana"

    Mara mama na baba walikuja na kumshukuru sana rahim kwa kutoa damu, mana bila yeye sijui ingekuwaje....

    "Tunakushukuru sana kijana kwa msaada ulioufanya"

    Wazazi wa zena waliingia tena kule ndani ili kuwa karibu na mtoto wao,.. Lakini sasa cha ajabu na cha kushangaza, yule mschana aitwae zena, dada yake na yule mtoto alikuwa analia lakini rahim hajui mana hakuwa akimwangalia katika macho japo kafunga kininja,.. Na pia muonekano wa zena inaonyesha dhahiri kuwa mtu huyo anamjua vizuri sana, na hatujui sababu ya kulia kwake,.....







    Rahim ni kijana wa Kiislamu lakini hajui nini maana ya Uislamu,... Akiona mtu kavaa hijabu anamuona kama mchawi vile mana kavalia vazi jeusi mwanzo mwisho,.. Akiona mwanaume kavaa kanzu anamwona ni mchawi mwanzo mwisho.. Na hii yote inatokana na malezi ya wazazi wetu huko majumbani, mtoto haijui hata dini yeke, kisa kazaliwa kwenye kisima cha pesa basi hata salamu ya Kiislamu hajui hata kuitikia... Vijana tubadilikeni jamani, tumgeukieni mwenyezi Mungu, kwa Mungu sio kwa mzungu jamani.. Bila kifanya mema hapa duniani usije kitegemea utakuta pepo baada ya kifo chako.. Pepo yako ni hii hii unayoifanya hapa duniani, lakini moto wa jahanamu utaukuta ukiwa tayari kukuteketeza mana tayari umeshakula pepo yako toka duniani....



    TUENDELEENI NA STORY



    Wakati zena analia sana ila haonyeshi kama analia kutokana na uninja aliovaa, yaani kafunika mpaka uso mzima, kabakiza macho tu,.. Ghafla kaka yake kafika...

    "ndugu yangu... Nakushukuru sana kwa kitendo ulichofanya, tunakuombea"

    Sulesh ambaye ni kaka yake na zena alikuwa akitoa shukrani zake kwa rahim, lakini rahim kaangalia pembeni tena anatamani hata amtukane.. Mana ndio wachawi wake hao,...

    "sawa"

    Rahim aliitikia kishingo upande, na hata sulesh alijua kuwa kaitikiwa kwa dharau, lakini hakuwa na budi kutulia mana wao ni masikini na hawana lolote lile,.. Sasa sulesh kugeuka na kumwangalia mdogo wake, aligundua kuwa analia,.. Alimchukuwa ndugu yake na kwenda nae chemba

    "zena, unalia nini sasa... Kama ni bakari atapona mana tayari keshawekewa damu"

    Aliongea sulesh akidhani labda dada yake analia kwa ajili ya mdogo wake

    "hapana kaka sulesh,... Naililia dini yangu jinsi inavyo kashifiwa na huyu kijana... Kiukweli sijapenda kwakweli"

    Aliongea zena huku akizidi kulia kwa uchungu mno... Kumbe kilio chake ni kwa sababu ya rahim kuongea ujinga juu ya dini yake,...

    "zena... Pesa inawapoteza watu wengi sana katika hii dunia... Tena bora ya huyu anajua kuna mungu ila haijui dini yake, na uzuri wa huyu hana roho ya kuuwa... Kuna wengine wanasema hakuna mungu,.. Mungu ni yeye na pesa zake... Huyu kijana ni malezi tu hayajamkaa vizuri.. Kalelewa na pesa na ndio mana hajui dini.. Hajui imani yeyote ile kuhusu dini"

    Sulesh aliongea maneno hayo kwa uchungu wa hali ya juu sana,...



    "dogo, tayari umeshamaliza haja yako ya kutoa damu,... Twende tukatoe loku, mana una siku mbili hujagusa kitu"

    Jamali alimchukuwa mdogo wake na kupanda katika gari yao ya kifahari,.



    BAADA YA WIKI MOJA KUPITA







     





    Rahim akiwa zake nyumbani time za jioni hivi,.. Alikuwa akichati na rafiki zake katika mtandao kwa kitumia laptop,.. Huku simu kubwaa iko kwa pembeni,.. Rahim alikuwa nje ya nyumba kabisa, na jamali alikuwa ndani anaangalia tv,... Sasa rahim akiwa anafurahi kichati Instagram na friends zake tena wakiwa online LIVE CHAT,... Ghafla aliona mschana mzuri akipita mbele yake,... Yaani sio kwenye kompyuta, bali amepita mbele ya macho yake pale alipokaa... Lakini sasa mschana huyo ni wale wale wanaovaa mahijabu, sema huyu kaachia uso, yaani hajafunika uso wote, kafunga ushungi wa kawaida tu

    Rahim alikuwa akimtolea macho mno, alikuwa ni mschana mzuri sana mithili ya malaika,...

    "we vipi... Ushapenda nini"

    Alikuwa ni kaka yake jamali, ndio kamshtua kwa maneno hayo

    "broo hiki kitoto ni kizuri sio mchezo ndugu yangu"

    "sasa wewe na yeye wapi na wapi"

    "kivipi"

    "wale si unasemaga ni wachawi kwako, iweje leo awe mzuri"

    "mmmmhhh ni kweli... Lakini duuu"

    Rahim alibaki kumsindikiza kwa macho tu huku akitamani hata kuwa nae kimapenzi,..

    Lakini sasa mschana huyo kumbe alikuwa na rafiki yake anafuata kwa nyuma, waliachana kwa dakika kadhaa tu...



    "zena mbona umeniacha sasa"

    Aliongea yule rafiki yake huku akihema kwa kukimbia

    "nilijia huji sasa hivi.."

    "afu mbona imefungua kitambaa cha usoni"

    Alimuuliza rafiki yake mbona alifungua kitambaa cha usoni mbacho hicho kitambaa ndicho kinacho unganika na kingine ili kufunika uso wote kasoro macho tu.. Lakini sasa huyu mschana aitwae zena ndio yule yule mwenye mdogo wake aliogongwa na gari, yaani mdogo wake sulesh, au dada yake Bakari,.....

    "nina maana yangu tu"

    "ok sawa... Ila zena... Mbona yule kaka alikuwa anakuangalia mpaka unapotelea hapa"

    "mmmhh nani huyo"

    "si yule alikuwa kakaa pale kashika kompyuta ndogo"

    "yule mkaka wa kidunia"

    "ndio... "

    "mmmhhh atajua mwenyewe"

    Basi hayo yalikuwa ni maongezi yao baina ya fadhila na zena, watu hawa ni marafiki wa karibu sana, na wanaishi kama ndugu....



    Siku ya pili tena, rahim alitega muda kama ule ule, ili yule dada aongew nae hata kama ni mchawi,.. Mwenyewe anasema tanga kuna wachawi wazuri sana,... Na rahim hajui kama huyo ndio yule zena aliokuwa nae kule hospitali, mana zena alipokuwa hospitali alifunika uso wote kasoro macho, sasa jana alivyopita, kaachia uso wake ukaonekana, na hapo rahim ndipo alipomuona,... Ghafla akamuona yule ragiki yake zena aitwae fadhila,... Rahim Alimwita fadhila na fadhila hakukataa mana wahenga walisema, usikatae wito bali kataa neno...

    "As Salaam Aleykum Warahmatullah wabarakatuh"

    Fadhila alimsalimia rahim huku akimpa mkono uliofunikwa na hijabu, ikiwa na maana kuwa asigusane na mwanaume ngozi kwa ngozi mana hapo alipo ana uzu (usafi wa roho)

    "safi tu"

    Rahim hajui hata kuitikia salamu hio, mana hakuwa akiipenda...

    "hali yako"

    "nzuri tu... Aahhh Samahani dada.. Eti yule rafiki yako leo hapiti hapa"

    Aliuliza rahim huku akinyoosha vidole kwa ishara ya vitendo

    "rafiki yangu nani mbona hata simkumbuki"

    "mweupe hivi"

    "aaahhhh zena"

    "mmmhhh nadhani atakuwa huyo"

    "leo hajaingia madrasa... Anaumwa"

    "madrasa ndio nini.... Na anaumwa nini, mbona jana kapita mzima tu"

    "heeeeee we kaka, hata madrasa hujui.... Ok, madrasa ni darasa la kiislamu linalofundisha maadili ya dini, linafundisha Quran tukufu, linafundisha mambo mengi sana juu ya dini yetu ya Kiislamu"

    Rahim hapo hata haelewi kitu, anabaki hewani hewani tu

    "ok anaumwa na nini"

    "ni malaria ya ghafla tu yalimuanza jana"

    "hospitali gani"

    "hapo kwa MOHAJI HOSPITAL"

    Rahim alitamani kwenda hata jioni hio hio,... Lakini wamewekewa torati ya kuto toka usiku...

    "tafadhali, naomba kesho unipeleke"

    Aliongea rahim... Lakini fadhila alionekana kujigonga kwa rahim, ila hakupenda kusema,....



    Kweli zena alikuwa mgonjwa na fadhila leo alikwenda hospitali kumwona rafiki yake, ikiwa ni mida ya saa moja hivi, yupo nae katika kitanda cha wagonjwa...

    "As Salaam Aleykum Warahmatullah wabarakatuh"

    "Waleykhu Msalam Warahmatullah wabarakatuh... Hali yakl fadhila"

    "salama tu... Sjui wewe huku waendeleaje"

    "aahhh tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuendelea kunipa pumzi yake"

    "hata mimi nashukuru kukuona ukiwa hai.... Ila nina ujumbe wako zena"

    "ujumbe... Ujumbe gani tena fadhila"

    "yule kijana wa jana nimekutana nae leo"

    "Enheee... Kasemaje"

    "nimemwambia unaumwa... Akatamani hata kuja leo leo lakini kasema nimlete kesho"

    "sasa kwanini usimlete"

    Aliongea zena huku akitamani hata aje

    "lakini zena... Yote tisa, kumi yule kijana anaonekana kakupenda wewe"

    "mmmhhh fadhila Usiseme hivyo.. Yule ni mtu wa kidunia siwezi kuwa nae... Afu yule ni kama shetani... Yaani nimekosa kupata mume mwenye imani kama yangu mpaka nimfuate yule... Siwezi"

    "sasa mbona unatamani aje"

    "ivi unajua kuwa yule ndie aliemgonga mdogo wangu"

    "unasemaje...."

    "ndio yeye... Afu yeye ndio kamwongezea damu mwenyewe.. Yule kijana ni mtu wa starehe sana, ni mdogo lakini anakunywa pombe.. Simtaki... Kama ni kuniona tu aje lakini kama ni mambo hayo asije"

    "mmmhh Afadhali... Mana nilijua unampenda"

    Aliongea fadhila na kumshtua zena

    "kwanini useme hivyo fadhila"

    "mimi... Nitafanya mpango nimbadilishe,... Kiukweli ni kijana mzuri kwa sura.. Ila tabia yake nitairekebisha tu"

    Zena alishangaa kusikia hivyo

    "sasa wewe umrekebishe ili iweje"

    "nampenda... Natamani awe mume wangu"

    "fadhilaaaaaaaaaaaaaaaaaa"

    "nini?"

    Zena aliita kwa hasira huku akilia kana kwamba maneno ya fadhila yamemgusa vilivyo....







    Mapenzi ni jambo lingine, haijalishi dini wala kabila, damu zikishaendana tu yaani hakuna atakaezuia swala hilo, huezi kuamini kuwa zena na imani yake dhabiti ya dini ya kiislamu lakini katokea kumpenda rahim,.. Ila sasa kitu ambacho hakipendi kwa rahim ni ile tabia yake,... Ana tabia mbaya ya kuikashifu dini yaani pesa zao anaona ndio kila kitu



    "sasa wewe umrekebishe ili iweje"

    "nampenda... Natamani awe mume wangu"

    "fadhilaaaaaaaaaaaaaaaaaa"

    "nini?"

    Zena aliita kwa hasira huku akilia kana kwamba maneno ya fadhila yamemgusa vilivyo,

    "skia fadhila.... Hata mimi nina moyo wa kupenda, lakini tabia ya yule mtu, hata baba na mama hawatonielewa japo kumsaidia mdogo wangu ila sio swala la kuwa nae

    "zena... Mimi simpendi... Nilitaka kujua tu kama kweli unampenda... Nimeshajua"

    Fadhila kumbe hakumaanisha kweli kama anampenda, lakini moyoni mwake, kweli anampenda ila hataki kumuudhi rafiki yake...

    "Ufyuuuuuu... Basi mlete hata anijulie hali"

    "lakini zena... Kwanini umempenda yule kijana"

    Fadhila alimuuliza zena kwnini kamapenda na wakati ni mvulana wa starehe tu,.. Anakunywa pombe, ni mtu wa wanawake tuuu

    "fadhila.... Kabla ya kukutana na mtu huyu... Hii sura Nilishawahi kuiota akiwa kama mume wangu mtarajiwa... Lakini ndoto ile, niliota akiwa ni Muislamu mzuri tu.. Yaani alikuwa kaishika dini vilivyo... Lakini sasa nimekuja kishangaa ni mtu wa tofauti kabisa yani... Na mbaya zaidi kuna siku nilimshika mkono, kwa nia ya kumuomba nimpeleke Bombo Hospital... Lakini kitendo cha kumgusa tu, nilosisimka mwili mzima.. Na hata yeye pia ilikuwa hivyo mana alinisukima kana kwamba hakuupenda msisimko ule... Toka siku ile kaingia moyoni kakaa.. Lakini matendo yake sasa siyapendi hata kidogo.. Mtu mwenyewe unaambiwa hawezi kukaa hata siku moja bila kunywa hizo wine zao"

    Zena aliongea sana, mpaka anatamani kulia

    "sasa kwanini ulimpenda"

    "mimi sijui"



    Kesho yake mida ya mchana hivi rahim akiwa nyumbani kwao yeye na kaka yake

    "broo yule mtoto niliomuona juzi.... Kiukweli ni mkali mno"

    Mara bibi yake kasikia maneno ya rahim

    "wewe mjinga sana,.. Ulizani kina wahuni kama huko mjini kwenu... Huku uwe na adabu na wasichana wa watu"

    "bibi vunga basiiii"

    "nivunge nini"

    "mtoto mkali yule"

    "mkali amekuwa mbwa"

    Rahim alikuwa akiongea na bibi yake kwa utani,....







     





    "skia bibi... Huyu mjukuu wako ana dharau za pesa.... Huezi amini Waislamu wa watu eti anasema ni wachawi, ivi ana akili kweli huyu? Afu mbaya zaidi eti kaona binti wa Kiislamu afu anasema ni mkali... Mjinga sana huyu"

    "heeeeeeee unasema anawaita nani?... Hivi we mtoto pesa zitakupeleka wapi?... Kwanini huiheshimu dini yako"

    Rahim kuona bibi anaongea sana aliondoka zake,... Kachukuwa gari kisha akawa anaelekea zake mjini.. Lakini ghafla fadhila katokea,

    "enheee we mdada"

    Aliita rahim wakati huo fadhila kavalia nguo za kawaida tu

    Fadhila aliingia katika gari mana anakumbuka jana alimwahidi kumpeleka hospitali ambako zena kalazwa... Fadhila mwenyewe haamini kama kapanda kqenye hio gari, na anatamani sana awepo katika hii familia, lakini atawezaje?.. Gari ilitua mbele ya hospitali, kisha rahim akaingia ndani kwa kuelekezwa na fadhila kuwa ni wodi namba fulani... Rahim hajui lolote la kubisha Hodi hajui... Aliingia tu bila hata hodi

    "heeeeeee mbona umeingia kama chooni"

    Aliongea zena, tena bila kumuogopa mana alishadokezewa na fadhila kuwa rahim atakuwa anakupenda.. Hivyo ana uhakika hawezi kimfanya lolote,

    "kwani una nini"

    Ubaya wa rahim ana dharau sana yaani hataki umseme jambo limguse

    "basi yaishe"

    Rahim alikuwa ana Tabasamu tu, mana kumkuta zena akiwa kavalia mavazi ya kawaida, yaani sio hijabu bali alivalia gauni lake refu suruali ndefu, kisha kufunika nywele zake kwa ushungi... Alikuwa ni mzuri mithili ya malaika,....

    "kumbe unapendeza kiasi hiki"

    Na hapo rahim bado hajajua kuwa huyo ni yule zena waliokuwa wote katika ile hospitali ya bombo,.. Mana yule alifunika sura yote na kubakiza macho tu,...

    "tayari umeshaniona unaweza kwenda"

    Alionhea zena, lakini rahim ndio kwanza kakaa....

    "unakaaje bila ruksa yangu... Baba na mama wakikukuta hapa.. Naomba uondoke"

    Zena alizidi kuwa mkali zaidi

    "mwanamke mzuri kama wewe... Kuwa mkali haipendezi, tena ukali wako ni bora iwe kwa mwanamke mwenzio... Ila sio mwanaume"

    Aliongea rahim huku akikaa vizuri,



    "tatizo lako wewe una tabia mbaya... Wewe ni mtoto wa Kiislamu, unatakiwa ufuate misingi ya dini.. Lakini kwa pesa ulizo nazo unaikashifu dini yako kwa kuwaita watu ni wachawi... Nani alikuambia Quran inahusishwa na hayo mambo.. Wewe ni Muislamu,.. Sisi sio wachawi.. Zile ni nguo za heshima kwa wanawake,.. Kiukweli unapata dhambi kubwa sana kutuita wachawi, kisa tumejifunga vitambaa vya uso.. Hakika hata hizo pesa zako utaziacha hapa hapa.. Hata hilo gari lako hutoenda nalo... Unakosea sana kuita watu ni wachawi... Nani alishawahi kukuloga wewe,.. Kwanini unajibebea mizigo ya dhambi ambayo haikuhusu....... Nasema sitaki kukuona, naomba utoke nje"



    Zena aliongea mpaka analia,.. Sasa hapa ndio tunajua kweli zena anampenda rahim, ila sasa tabia yake,.. Rahim ni sharobaro mpenda starehe sana, ana dharau za kutupa..

    "yaani kulia kwako tu ni uzuri tosha"

    Aliongea rahim kisha akamuita dokta

    "dokta.. Huyu mgonjwa anadaiwa"

    "ndio... Lakini sio kubwa sana"

    Mara zena kasema kuwa

    "usilipe kiasi chochote kile... Mana haina maana kusaidia mtu wakati mungu wako humheshim.....pesa zako sii chochote mbele za Mungu.. Tutalipa wenyewe"

    Rahim, alikasirika sana mana hua hapendi kuambiwa ukweli juu ya maisha yake... Kweli rahim hakulipa ile pesa, alitoka... Lakini ghafla anakutana na baba yake zena na mama yake zena... Mbaya zaidi mpaka yule mtoto aliomgonga, mbaya zaidi na sulesh ambae ni kaka yake zena.... Sasa rahim anajiuliza, hawa wanamfuata nani tena huku..

    "shkamoni"

    "Marahaba ujambo"

    "sijambo... Mama vp kuna nini huku"

    "ni yule mtoto wangu wa kike... Kalazwa toka juzi"

    Wakati huo baba mtu kaingia ndani lakini bila ya salamu au kumjulia hali mtoto wake... Kaanza kuuliza

    "yule kijana kafata nini huku ndani"

    Mzee alimuuliza mtoto wake wa kike

    "alikuja kuniona tu"

    "nimesema hivi, sitaki tena kumuona huyu mtu... Kama keshatoa msaada kwa mdogo wako inatosha, lakini sio kwako tena... Naona unataka kinivunjia heshima yangu kwa bwana hamisi"

    "hapana baba"

    "sasa kesho... Nakwenda kwa bwana hamisi kuchukuwa ng'ombe wa kwanza.... Sasa ole wako"

    "babaaaaaaaa"

    "nini...."

    "basi sawa tu"

    Zena alianza kulia kwa uchungu huku mzee akitoka kwa hasira... Alimkuta rahim anaongea na mama hapo nje

    "we kijana... Naomba ukae mbali na binti yangu.... Usinitishe na pesa zako sawa... Binti yangu ana mchumba wake huyo... Maswala ya kumfata fata utakiona cha moto"









    Mzee Mvungi aliwaka moto alikuwa hana utani kabisa na mtoto wake, na kama unavyojua wazazi wa kijijini hua wanapenda kuwachagulia watoto wao wachumba wa kiwaoa,.. Kumbe hata zena ni mmoja wapo, na mzee unaambiwa anataka ng'ombe saba, kama mahari kwa mtoto wake, familia moja imekubali kulipia ng'ombe sana na leo mzee anakwenda kuchukuwa ng'ombe mmoja...



    Sasa kumbe mzee hakufurahiwa na rahim kabisa, na licha ya baba, hata mama pia hakumfurahia rahim, hata pale wakati Bakari anaumwa, walikuwa hawataki kompleni na huyu kijana,.. Na aliosababisha watulie alikiwa ni sulesh,... Mana hata damu hawakuitaka na hawakuwa na shida nayo,... Na siku ile ilikuwa hivi



    "baba, mtoto anaumwa na huyo ndie aliemgonga, acha presha mtoto apone mzee"

    Sulesh alimwambia baba yake siku hio aliotaka kuamsha tempa, kwahio hata zile shukrani zilikuwa ni za kuzuga tu

    "huyu kijana mchafu sana atawezaje kutoa damu kwa mtoto wangu... Hebu ona ana kemikali za pombe katika damu hio je itakuwaje kuhusu mtoto wangu.."

    "baba, kama ingelikuwa haifai, hata dokta angesema kuwa haifai... Lakini kwakuwa inafaa ndio mana akapewa siku kadhaa asinywe pombe"



    Sulesh alimtuliza baba yake huku mama nae akiwa hataki pia... Yaani hii familia imejawa na imani ya dini, hivyo hawakupenda rahim atoe damu kwa mtoto huyo licha ya kwamba yeye ndie alimgonga.... Wazee walikubali kishingo upande tu..



    Sasa leo kwenye ugonjwa wa zena rahim kakutana na mzee Mvungi

    "we kijana... Naomba ukae mbali na binti yangu.... Usinitishe na pesa zako sawa... Binti yangu ana mchumba wake huyo... Maswala ya kumfata fata utakiona cha moto"

    Rahim aligeuka kwa hasira huku akijiandaa kumjibu,.. Lakini kabla hajafanya hivyo alimwona zena katika dirisha akimwambia kwa vitendo kuwa asithubutu kufanya au kuongea lolote lile,.. Rahim alibakia kutulia tu, huku akiondoka zake kwa hasira, na hapo alikuja na fadhila,... Fadhila kasikia kila kitu,...



    Rahim hakukata tamaa alihakikisha tu mpaka zena anapona vizuri, na leo ilikuwa ni siku ya zena kutoka hospitali, rahim kapata nafasi hata ya kutoka nae nje ya hospitali...

    Na wakati huo zena alikuwa kavaa NIKABU anaonekana macho tu,.. Rahim hapendi hilo vazi lakini kwa maneno aliopewa na zena pale hospitali kuwa pesa zako magari yako, nyumba zako, utaziacha hapa hapa,...

    "we ram, si upande gari sasa"

    Aliongea jamali huku akifungua mlango,

    "wacha mgonjwa anyooshe miguu"

    Aliongea rahim, huku wakitembea pamoja... Lakini wakati huo zena hapendi kuwa sambamba na rahim, kwasababu mavazi yake, hayakuwa sahihi kutembea na zena..

    "ivi we kijana, unaweza kuniacha nielekee nyumba mwenyewe"

    Aliongea zena, na wakati huo fadhila yupo nyuma kama mita 20 hivi, ili kiwapa nafasi,..

    "kwanini"

    "mavazi yako hayastahili kutembea na mimi"

    "ok... Sawa nitakuacha"

    Zena anampenda rahim yaani ghafla tu alijikuta tu anampenda vile alivyo, lakini sasa hataki kuwa na mahusiano ya kificho, anataka wajulikane kwa wazazi na wazazi wenyewe ndio hao wameshaanza kumchukia rahim, we ulifikiri nini kitatokea hapo....







     





    Sasa wakiwa wanaendelea kutembea taratibu,...

    "ndugu zangu seidia.... Nisaidieni"

    Alikua ni omba omba aliokuwa kakaa pembezumwa barabara, na alikuwa hana mikono pia miguu, na mbaya zaidi hata kuona kwake ni kwa shida, kwasababu ya umri wake kuwa mkibwa, yaani ni mzee....

    "we vipi... Unaniomba pesa kwani kanipa baba ako.... Ntakutia teke la mbavu"

    Rahim aliongea hivyo huku kweli akitaka kifanya hivyo kwa kumpiga yule kilema wa watu, tena alikuwa ni mzee sana,...

    Zena alimzuia asifanye kile alichokifanya, afu zena kumbe alimpitisha makusudi sehemu hio,...

    Zena hakumsemesha kitu,.. Mzee wa watu katulia kimya huku akilia kwa umasikini aliokuwa nao, hana mikono hana miguu, lakini rahim kashindwa kumsaidia, tena mbaya zaidi kampa na vitisho vya kutaka kumpiga mateke ya mbavu... Zena ilimuuma sana lakini hakusema kitu alimwacha tu



    Baada ya siku kadhaa kupita,.. Rahim akiwa nyumbani kwao,..

    "ivi bibi... Eti yule binti ana mchumba yule"

    Rahim alimuuliza bibi yake,... Lakini jamali akamjibu

    "wewe umesha ambiwa kuwa ana mchumba sasa yanini ung'ang'anie.. Ujinga uo"

    Mara bibi kaingilia kati,...

    "ngoja... Licha ya kuwa na mchumba,.. Huyu ni kichaa sana huyu... Wewe na usharobaro wako huu ulitegemea utampata mschana kama yule... Watoto wa tanga wana imani ya dini.. Sasa wewe hivi ulivyo.. Kweli we ni mjinga kama alivyosema kaka ako"

    Bibi na jamali walikuwa wakiongea maneno makali sana ya kukatisha tamaa

    "lakini bibi.. Unaependa ni moyo au mavazi"

    Aliuliza rahim

    "na uliona wapi mavazi bila vitendo... Haya mavazi na vitendo vyako, kuna tofauti"

    "aahhhhhh broo, achana na bibi twenzetu club sisi"

    Aliongea rahim huku bibi akisema kuwa

    "umeona eeee..... Sasa yule ni mtu wa club yule... We ulifikiri utampata kwa staili hio"

    "kwani si atamfuata mtu wake"

    Jamali na rahim walichukuana haoo mpaka club, waliagiza wanavyojua wao mana pesa iko,...



    Wakati wanarudi, walikutana na zena na rafiki yake fadhila,...

    "zena... We zena wewe"

    Rahim aliita huku akimfuata mana walikuwa wanatembea kwa miguu, hua rahim hapendelei gari mara kwa mara,...

    "we, we, we,.. Ishia hapo hapo.. Yaani usinisogelee"

    "kwanini sasa"

    "we hujioni ulivyo... Tena staki mazoea na wewe"

    Aliongea zena kisha akaondoka zake.. Lakini fadhila yeye hakuondoka alibaki na rahim,.. Unajua hata fadhila anampenda rahim, lakini anamuogopa zena, mana zena anampenda kupita maelezo,... Sema tabia ya rahim ni mbaya mno, na zena haipendi... Sasa zena baada ya kuona fadhila haji,.. Ilibidi arudi taratibu mana kakata kona kadhaa hivi lakini fadhila Haji...

    Wakati huo fadhila ndio anaongea,...



    ************************************



    "rahim... Kwani wewe unampenda zena"

    Fadhila alimuuliza rahim wakati huo zena anachungulia tu mahali,...

    "kiukweli nampenda kwasababu ni mzuri, natamani kuwa nae"

    "sio.. Umuoe"

    "aahhhh wakuoa atakuwa mimi bwana"

    "sasa kwanini unahangaika na mtu ambae hakupendi.... Kwasababu mimi juzi nilimwambia kuwa rahim yule mjukuu wa bibi mzungu anaonekana anakupenda... Alichonijibu siwezi kuamini kwakweli"

    "kakujibu nini......"

    Fadhila anaharibu kila kitu kwa zena,

    "kwanza.... Zena ana mume.. Alafu alishawahi kutoa mimba tatu, usimuone vile, kamrudia mungu hivi karibuni tu lakini alikuwa kama wewe"

    "we muongo.."

    "ninao ushahidi wote??.... Ila usije kupaniki"

    "sawa.. Ebu Niambie"









    Fadhila alionekana kuongea maneno ya kumchafulia zena, mana rahim anampenda sana zena... Yaani anampenda mno toka alipomwona basi anatamani kuwa nae kama mpenzi wake,... Lakini pia sio rahim tu, bali hata zena katokea kumpenda rahim, lakini tatizo la rahim, ni hio tabia yake ambayo zena hatamani kuiona kwa rahim....



    "we muongo..."

    "ninao ushahidi wote... Ila usije kupaniki"

    "sawa.. Ebu niambie"

    Rahim alikaa tayari kwa kusikiliza umbea wa fadhila kuwa zena alishawahi kutoa mimba tatu, na alikuwa mhuni kama rahim alivyo kwa sasa



    ************************************



    Lakini sasa kumbe hayo yalikuwa ni mawazo ya zena pale alipokuwa anachungulia baada ya kuona fadhila haji, sasa ndipo alipohisi kuwa fadhila huenda anaongea hayo maneno,... Sasa kama zena kayawaza hayo basi ni kweli,..

    "fadhila anaongea nini na yule kijana"

    Aliongea zena kimoyomoyo kama vile anajiuliza mwenyewe,...



    Wakati huo huku fadhila alikuwa akimwambia rahim kuwa

    "sikiliza rahimu, hapa ulipo umelewa wewe, huezi kuongea nae hata kidogo"

    Aliongea fadhila huku nae akitaka kuondoka,...

    "kwani sasa hivi mtarudi tena huku"

    "hapana, ndio tumetoka madrasa sasa hivi"

    "sasa nitamuonaje"

    "labda uende dukani kwao"

    Aliongea fadhila, huku nae akipiga hatua za kuondoka....

    "sawa"

    Ghafla jamali katokea huku akicheka

    "tatizo mdogo wangu unajisumbua sana, hawa watoto wa watu wa Kiislamu unataka kuwafanya nini... Hawa si wachawi wako hawa"

    Aliongea jamali na hapo walipo walikuwa wameshapata moja moto moja baridi,...

    "ah ah broo, usiseme hivyo bwana"

    "heeeeeeee.... We si ndio uliokuwa unasema ni wachawi na nguo zao"

    "ndio, lakini sio zena"

    Waliongea kisha wakaingia zao ndani, rahim kwa sasa kidogo kapunguza kuikashifu dini... Toka alivyopewa darasa kule hospitali mpaka sasa hataki tena kusema wachawi,...



    Kesho yake mida ya mchana hivi, alimwita hadija ambae ndio mfanyakazi wa ndani hapo kwao,...

    "dija"

    "abee kaka"

    Rahim alimwita kwa upole, mana hua anamnyanyasaga sana dija au hadija, maskini hadija wa watu kaja kwa heshima anajua lazima apewe kazi ya ajabu ajabu tu...

    "abee kaka"

    Alifika dija huku akiwa kachuchumaa

    "hapana, kaa kwenye kochi"

    Hadija alishangaa sana mana rahim ni dikteta mzuri sana,... Sasa leo anashangaa anaambiwa akae kwenye kochi..

    "asante kaka"

    Aliongea hadija mtoto mpole, tena nae alikuwa anapenda sana kufunga ushungi, lakini rahim alipokuja tu hapo nyumbani, akamkataza kufunga ushungu, na akamwambia endapo ataendelea kufunga ushungi angemfukuza kazi,... Na hata dija alikuwa yeye na madrasa hawaachani lakini aliacha kwasababu ya rahim....

    "Samahani sana dada angu"

    Rahim leo kamuomba msamaha dija, mpaka dija alitaka kuanguka kutoka sofani,... Mana rahim hajawahi kumpumzisha dija yaani ni tabu tupu kisa wana hela,..

    "lakini kaka, hujanifanyia chochote kibaya"

    "hapana dija... Vipo nilivyokufanyia... Nimekunyanyasa sana, sikupi raha ndani ya nyumba... Na uzuri wako huo lakini sikuwa nikiuona"

    Dija alibaki kutabasamu tu,.. Unajua ukiwa mfanyakazi afu boss anakusifia vizuri lazima uachie Tabasamu mwanana..

    "lakini kaka mbona mimi nilishakusamehe tu"

    Wakati huo jamali alikuwa hayupo

    "sasa, kuna kitu nataka nikuombe"

    Dija ndio akajua kumbe misamaha yote hii kumbe kuna kitu anataka kuniomba,....

    "sawa kaka"

    "sasa sikia... Nataka uende kwa akina zena,... Ukamwambie jioni tukutane"

    "mmmhhhhh kakaaa....."

    Dija aliguna, mana swaga za zena na swaga za rahim, ni tofauti kabisa, yaani hawaendani hata kidogo.. Na dija aliguna kwasababu anajua tu rahim anataka kumchezea mtoto wa watu...

    "unaguna nini sasa"

    "hapana kaka... Sawa naenda sasa hivi"

    Dija alitoka kichwa wazi lakini rahim alimuita na kumwambia afunge ushungi,... Dija alizidi kushangaa, rahim kabadirika kwa kiasi kikubwa sana,... Basi dija aliondoka huku akifunga kitambaa chake kichwani,..







     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog