Chombezo : The Dom
Sehemu Ya Pili (2)
Wakati huo
General nyange akiwa ndio anaweka simu yake katika mfuko, kisha wakaingia ndani
wakiwa na makamanda wasiopungua 15,ambao alikuwa nao kwenye sakata lile la
kupakia silaha katika gari la kawaida,...
"sasa, kila mmoja afe na mzigo
wake, afu longo longo sipendi"
Aliongea general nyange, huku makamanda
ambao ndio walimu wa wanafunzi wote,...
"sawa kamanda,.. Lakini mkuu
mbona ishu hii tunayo muda mrefu na hakuna aliejua"
"nalijua hilo,
lakini bingo la leo,... Mtafurahi... Kuleni milioni kumi kumi kila
mmoja"
Aliongea general nyange huku akiweka briefcase mezani ili kutoa
vitita kadhaa kwa ajili ya kugawanya.. Kweli kila kamanda alipewa kiasi cha
milioni kumi, huku akiwataka waelekee katika nyumba zao za hapo hapo kambini,...
Kumbe wanafanya biashara ya uuzaji wa silaha za serikali
JAMANI
SIMULIZI HAINA UKWELI JAMANI, MSIJE MKAANZA KUSEMA KUWA NI KWELI.... MANA NYIE
DUUU
Sasa huku ndani kwa sahi, mwaju akiwa ndio kaishika ile
simu ya kijana BB,... Lakini ghafla alishangaa kuona picha moja ikiwa katika
screen sever, mwaju aliitupa ile simu mezani na kuzidi kujiuliza, huyu kijana ni
nani hasa, yaani licha ya kazi yake hii ya upelelezi, bado ufamilia wake una
mashaka, mana inawafanya watu kujiuliza mara mbili mbili,...
"huyu mkaka
ni nani haswa.. Na hii picha inamhusu vipi"
Aliongea mwaju huku
akiichukiwa ile simu na kutaka kumpelekea General ambae ndio mkuu wa
majeshi,...
Lakini kabla hajapeleka, kwanza
alijiuliza,...
"au General atakuwa ananichezea akili, mana naweza
kumlipoti mtu kumbe ndio najilipoti mimi mwenyewe"
Aliongea mwaju katika
moyo wake
"ngoja niiweke kwanza... Nikipata kitu kingine, itakuwa bora
zaidi..
Mwaju aliirudisha ile simu kisha akawa anaendelea kutafuta kitu
kingine, lakini ukumbuke kuwa sahi hakuja na begi lolote hapa jeshini, kwani
hakutarajia kuanza mafunzo siku hio hio, hivyo nafasi ya kwenda nyumbani kwao
kuchukuwa baadhi ya vitu, alikosa kabisa na ukizingatia leo ana siku ya pili
toka aanze mafunzo yake,.... Mwaju hakutaka kuipeleka ile simu kwanza kabla
mpaka apate kitu kingine tofauti na simu... Mwaju aliendelea kutafuta uvunguni,
funua makabati ambayo sahi bado hajayawekea kitu chochote
kile,...
Sasa huku msituni pembeni na eneo la jeshi palipokuwa
na kazi ya kupakia silaha za jeshi,...
Sasa Mwarabu akawasha gari
ikawaka, lakini kila akiingiza gia na kutaka kuondoka, inakataa alishangaa ni
kwanini gari imekuwa na hitilafu kabla ya kuondoka pembezoni mwa
jeshi,...
"hebu kaangalie au kuna jiwe"
Mwarabu alimtuma mtu
wake, na wakati huo kiza totoro, yaani hata tochi hazikuwepo eneo hilo, kutokana
na kazi waliokuwa wakifanya watu hawa... Yule kijana alitoka katika gari, na
kuanza kumulika mulika kwa siri sana, ili tochi isionekane na watu wengie,..
Sasa kijana akaona propela imefunguliwa,.. Akaona wacha akaifunge,... Kitendo
cha kusogea ni kitendo hatari mno kwa kijana huyo,...
Ukimya
ulitawala chini ya gari, hakuwa na mtu akicheza cheza wala
kuhema,...
"mbona harudi huyo,.."
Mwarabu Alimuuliza jamaa
mwingine aliokuwepo eneo la kibini, mana hamuoni akirudi baada ya
kuchungulia,...
"si unamjua jamali alivyo kalegea? Unaweza ukakuta
kalala huko ndani"
Aliongea jamaa mmoja huku akishuka naye kwenda
kumwangalia jamali, kweli alipofika chini ya gari alimkuta jamali akiwa kalala,
lakini hajajua kuwa ni mtego..... Wakati huo Mwarabu anachukuwa simu yake na
kuwapigia wanajeshi waasi ambao waliasi jeshi, ila sio kuwa ni wa kitanzania,
bali mwarabu huyu ni raia kutoka kenya, hivyo anawapigia makamanda wao
wanasubiri katika njia fulani ya chocho mana hawapitii njia ya moshi ya moja kwa
moja, watapita chochote na watapitia boda ya namanga,... Hivyo wanatakiwa
kusubiri upande huo huo wa Kenya,..
"eee halo jabir"
"yes
mkuu"
"maili tisa tusubirini"
"sawa mkuu, tupo ready kwa hali
yeyote ile"
"ok"
Mwarabu anakata tu simu, alishangaa anamulikwa
tochi ya macho kisha ikazima,.. Alijua ni watu wake, kumbe sio, ni sahi, jeshi
la mtu mmoja.... Mwarabu alitolewa ndani ya gari na wakati huo hakuwa na silaha
yoyote ile kutokana na mazingira walio kuwepo, yaani silaha wanazo katika viuno
vyao, lakini hazikiwa tayari kwa tukio, mana pembezoni ya jeshi, gaidi gani
anaweza kuja.... Sasa kumbe sahi alikuwa akiwavunja shingo mmoja baada ya
mwingine,... Hata mwarabu kwake alikuwa mlaini sana kitokana na kustukiza, yaani
hakutegemea kukutana na swala kama hilo....
"General nyange
umetusaliti"
Aliongea mwarabu huku akiwekwa vizuri,
"hakuna cha
General hapa.... Nataka uniambie, silaha mnapeleka wapi"
"kwani we
nani????.............aaaiiiiiii"
Sahi hatakagi kuulizwa wakati yeye
kauliza, Ajibiwe kwanza ndipo aulize,
"nakuuliza tena, silaha mlizipakia
mnapeleka wapi"
"hapana kamanda, sisi tumeagizwa tu, tuna wakuu wetu
nchini Nairobi"
"kwahio hizi silaha mnapeleka Nairobi?"
"ndio...
Tumeagizwa tu... Lakini wewe si nilikuwa na wewe hapa, mbona
umenisaliti"
Sahi kuona mwarabu anaropoka ujinga, zake ni kuvunja shingo
tu, mana mambi ya kutumia silaha kwa sehemu kama hio ni hatari sana,.. Sahi
baada ya kummaliza yule gaidi la kiarabu, aliingia katika gari na kuutoa
ufunguo, ila aliuweka humo humo kwenye gari ila sio kuupata kirahisi,... Baada
ya hapo alizunguka katika gari na kuimulika pleti number ya gari hio, kweli
ilikuwa ni gari ya kenya..... Sasa kumbe hio saa ikikumulika sio kuwa ni tochi,
bali ni flashi ya kamera, hivyo hapo kapiga picha vizuri
sana...
BB hakuwa na haja ya kuondoka wala kulisumbua gari,
alivua gropsi zake baada ya kazi kisha, akazificha mahali kana kwamba hazikufaa
kutumika tena, mana kama angewashika bila gropsi, katika upelelezi angejulikana
kupitia finger print,... Sahi taarabu anarudi kambini tena kwa umakini wa hali
ya juu, wakati huo ni mida ya saa nane za usiku,... Sasa saa ngapi mwaju
hajatafuta mpaka kachoka, kila kona ya makabati anakutakana na zana za kijeshi
tu, mana kila chumba cha mwanafunzi kinatakiwa kukaa na kila kitu cha kijeshi,..
Sasa mwaju baada ya kutafuta mpaka kuchoka, alijikuta kapitiwa na usingizi,..
Wakati huo sahi ndio anaruka ukuta na kuingia katika anga za jeshi... Yaani
ndani ya jeshi, huku akianza kukroo, taratibu... Kwa bahati mwaju anazinduka na
kujikuta yupo chumbani kwa sahi,.. Mara moja bila kuchelewa aliamka kwa haraka
haraka ili arudi
alipotoka
Sasa
ile anafika tu nje, ndio anakumbuka kasahau simu ya sahi, ili ampeleke general
nyange,.. Lakini alichelewa ilimbidi tu aendelee na safari yake ya kwenda
bwenini kwake, wakati huo sahi ndio anaingia chumbani kwake, yaani mwaju
angerudi tu, lazima angelikutana nae njiani..... Sahi alipoingia ndani, kwanza
alihisi harufu ya mtu aliotoka muda sio mrefu,.. Aliingia kwa umakini zaidi
lakini hakukuwa na mtu, kitu cha kwanza kwanza kabisa alikimbilia simu yake,
kisha akafungua na ile saa yake ikawa katika mfumo wa simu,... Kumbe sahi
alilirekodi lile tukio mwanzo mwisho walipokuwa wakipakia silaha, sahi aliituma
ile video iingie kwenye simu yake,.. Pia zile picha za magaidi pia alizikopi
katika simu yake ya kwaida, ila kwenye saa bado vipo
vyote,
Asubuhi kama kawaida ni mazoezi kwa kwenda mbele, sahi
hakutaka kumwambia mtu kitu chochote kile juu ya tukio la jana, mana hatakiwi
kujulikana kama ni yeye ndio kafanya hivyo,... Katika mazoezi kuna makundi
mawili, sasa sahi kachagua kundi la kwenda mbali kidogo kwa ajili ya mazoezi,
yaani sahi hana wasiwasi mana anajiweza kivyovyote vile,... Sasa hili kundi la
pili, katika mazoezi yao likaona kuna gari, ndani ya kundi hilo mwalimu anajua
kuhusiana na gari hilo, ila wanafunzi hawajui jambo kama hilo, na nia ya sahi ni
kwamba anataka wanafunzi wote wajue kuwa kambi yao inatoa silaha na kuwauzia
nchi jirani,.. Kwakuwa mwalimu hawezi kuifanya kuwa siri tena, alijifanya na
yeye hajui kisha akapiga simu kwa General nyange,
"mkuu, kuna gari hapa
imetelekezwa"
"gari??.... Gari gani"
"gari hii inaonesha
ilipakiwa silaha mkuu"
Sasa kamanda kusogea karibu, ghafla anawaona wale
majangili waliouziwa silaha....
"mkuu... Kuna watu watatu wanaonekana
kupoteza maisha"
Unajua huyu kamanda, anajua kila kitu, lakini hapo ni
mbele ya wanafunzi, ambao hawajui lolote, hivyo lazima ajifanye hajui chochote
kile kuhusu kupakia kwa silaha hizo..
Nusu saa mbele, gari
limesukumwa mpaka kambini, tena lina silaha zake zote, hakuna hata moja ambayo
imesafirishwa,.. Gari lilifikishwa katika kambi ya jeshi, huku maiti waliokutwa
katika eneo la tukio wakipelekwa hospitali iliopo hapo hapo jeshini, yaani
hospitali ya jeshi
"kamanda kuti??, haraka sana naomba upelelezi
ufanyike"
Aliongea general nyange huku akiwa na wasiwasi juu ya tukio
hilo mana wao ndio waliouza silaha za jeshi na kushindikana
kwenda,..
"sawa mkuu"
Kamanda kuti alikwenda katika ile
hospitali akiongozana na General nyange,
"dokta, tunaomba uangalie
finger print za muuaji katika hizo maiti"
Wakati huo kikosi cha pili cha
akina sahi bado kipo msituni na hakijui lolote kuhusu suala la kukamatwa kwa
gari yenye silaha, ila sahi mwenyewe kimyaa, nazidi kujifanya hajui
mazoezi...
Sasa katika hali ya kuwageuza wale maiti,... Kumbe
kuna mmoja alikuwa hajafa vizuri, saa ngapi hajatoa macho, na kumwona General
nyange uso kwa uso,...
"vp kijana... Habari yako... Nini kilitokea usiku
wa jana??"
General Nyange aliuliza kwa presha ya hali ya juu
mno,...
"eti, unamjua mtu aliowafanyia tukio hilo"
Yule gaidi
alitikisa kichwa kuashiria ni kweli anamjua mtu aliowafanyia hivyo, kwahio yupo
tayari kumwambia General nyange kwakuwa ni mtu wao,... Wakati huo sahi hajui
lolote lile kama huku kumbe kuna mmoja hajapatwa na umauti,....
"dokta,
tunaomba ututolee huyu kijana na kubaiskeli cha wagonjwa... Afu kamanda kuti,
naomba unikusanyie wanafunzi wote hapa kambini"
Aliongea general Nyange
huku akiwa na hasira juu ya tukio hilo,....
"lazima tufahamu.....
"
Nusu saa mbele, kundi la pili linawasili kambini kutoka
mazoezini, wakati huo kundi la kwanza lipo katika paredi ya utulivu,.. Mbele ya
paredi yupo yule gaidi alio tayari kwa kumtaja mtu aliohusika na tukio
hilo..
Sasa sahi hajui hili wala lile,... Alitahamaki kuona sura ya yule
gaidi ipo hai,..
"mungu wangu... Kumbe hili fara
halijafa"
Aliongea sahi huku wasiwasi ukimjia, kwani nia yake ni
kugundua mengi zaidi katika kambi hio, sasa endapo atagundulika mapema, itakuwa
tabu
General leo ndio aliokuwa akiwapanga line wenyewe, yaani mpaka
wanafunzi wote waka kaa sawa katika line zao,...
"gidi... Naomba
utuonyeshe mhusika wa tukio la jana"
Sahi pale alipo moyo ulikuwa
unakwenda mbio,.. Mana lazima ajulikane ni yeye,... Sasa kumbe huyu gaidi
ha......
Wakati huo gaidi akiletwa
hapo paredi, viongozi walikuwa makini sana na gaidi lile, mana ila General
nyange anawajua watu hao sema tu anajibalaguza na kuwa na ujasiri ili akamatwe
huyo aliewafanyia hivi, na licha ya hivyo, pia General ana wasiwasi sana na
kibarua chake kuota nyasi, mana lazima kajulikana uharamia ambao anaufanyaga
siku zote, sasa leo kabainika japo mtu aliombaini hajajulikana na ndio wanamsaka
kwa udi na uvumba,...
Yule jamaa aliletwa mbele ya wanafunzi
wote, mana hakuna aliefanya wa nje ispokuwa ni hawa hawa wanafunzi au walimu
ambao hawaijui hio ishu,...
Rahim alikuwa kakaa tayari tayari kwa
kutajwa mana ana kuna wakati alivyokuwa akiwanyonga alikuwa akiwapiga pocha
kupitia saa yake, sasa ule mwanga wa flash huenda akawa kaonekana na mtu huyo,
gani aliwekwa katika akiwa hajiwezi mana aliponea chupu chupu
kufa,....
Sasa kumbe huyu gaidi hawezi kuongea kutokana na kile
kinyongo alichokipata toka kwa sahi, sauti hana lakini kwa macho tu pia anaweza
kumtambua mtu,... Sahi alikuwa na wasiwasi sana juu ya kujulikana,... Lakini
sasa ujue sahi ni mpelelezi makini sana, tena ni mtu anaeipenda kazi yake,..
Alimwangalia yule gaidi alivyokuwa anapitishwa karibu lakini cha ajabu alikuwa
haangalii sura, yeye alikuwa anaangalia mikono, na hapo ndipo akagundua kuwa mtu
huyo alikuwa akiangalia saa za mikononi, mana ndio iliompiga picha, afu mbaya
zaidi walikuwa wakikaribia karibu na sahi, afu sahi na ule msaa wake upo
mkononi,... Kumbe gaidi hajaona sura ya mtu alio wanyonga, ila kile kitendo cha
kuoigwa picha kwa kutumia saa, huyu gaidi ndio kitendo alichokikariri katika
macho yake na sio vinginevyo.... Na wakati huo wanafunzi wote mikono mbele,
hivyo sahi kuivua hawezi mana mstari umenyooka afu wamesimama kwa utulivu
mkubwa, hivyo mtu mmoja akijigusa anajulikana....
Ghafla
alikohoa mwanafunzi mmoja, General kasikia, akauliza
"nani analeta
ujinga"
Aliuliza sahi mana hajui nani aliokohoa...
"samahani
mkuu, naona ni vumbi vumbi tu"
Kumbe aliokohoa alikuwa ni sahi, na kudai
kiwa amepatwa na vumbi, basi General ndiye aliekuwa anapointi macho ya gaidi
pale yatakapotua basi ndio hapo hapo... Huku gaidi akiendeshwa kwa kutumia
kibaiskeli cha wagonjwa.... Sasa walipofika karibu na sahi, General wasiwasi
wake ni sahi, yaani hata asipo pointiwa yeye lakini ana wasiwasi na huyo kijana,
japo ana kopi kopi za mtoto wake aitwaye Sharbiny ambaye nae alikufa katika
mazoezi ya kijeshi,.... Sasa walipofika pale walisimamisha kibaiskeli ili tu
gaidi apate muda wa kumkagua... Lakini pointi anayoitaka gaidi ni saa, lakini
sahi kwa wakati huo hakuwa na saa mkononi,.... Yaani ushapu ni kitu kizuri sana,
yaani kitendo cha kukohoa tu na saa imetolewa... Na alifanya hivyo kwasababu
akikohoa ni lazima atikisike hivyo upenyo wa kuivua saa ulikuwepo mzuri wakati
wa kukohoa... General alipitisha baiskeli mbele, lakini hawakufanikiwa kumjua
mhusika,... Sasa hapo General kichwa moto, wakati huo gaidi anarudishwa
hospitali, na General anaingia ofisini kwake....
Wanafunzi
wengine hawajui kinachoendelea hapo,... Basi sahi akavaa saa yake na hapo
wakaendelea na mazoezi ya hapo hapo kambini mana walishapoteza muda mwingi
katika sakata hilo la kumjua mtu aliohusika kuwauwa hawa magaidi na kuzifanya
silaha kurudi mikononi mwa kambi ya jeshi
Mazoezi yakiwa
yanaendelea, mwaju alikuwa akimtazama sana sahi,... Mwaju ni mwanafunzi lakini
ana muda mrefu hapa shuleni, hakosi miaka miwili au mitatu, na alikuwepo hata
kipindi cha mtoto wa General alipokufa huyu mwaju alikuwepo, hivyo hata yeye
anamshuku kuwa mtoto wa General, lakini tofauti yao ni sura, yaani sura
hawafanani hata chembe, mana Sharbiny alikuwa maji ya kunde afu ana Kidoti
kwenye sura upande wa kushoto chini ya jicho lake
Lakini hayu ni mweusi
afu hana kidogo, na oia hawafanani hata kidogo, na huyu anaitwa salehe, na huyo
anaitwa Sharbiny, ni watu wawili tofauti kabisa... Lakini mwaju kile alichokiona
kqenye simu, kinazidi kumpa mashaka juu ya kijana
huyo..
"mwaju"
"yes mkuu"
"nakuitaji
ofisini"
General nyange alimwita mwaju aje ofisini kwake huenda kuna
kitu anataka kumuuliza, ila mwaju nae ana ham ya kuongea na General kwa kile
alichokiona kwenye simu ya sahi,
Mwaju pasina uoga wa aina yeyote
aliingia ofisini kwa General na anajua kitu anacho itiwa
"hivi huyu
kijana umeshapata fununu zozote"
Aliuliza mr Nyange au general
Nyange
"yes, jana usiku nilikuwa katika chumba chake"
"enhee,
umemkuta anafanya nini"
"Kiukweli sikumkuta"
"what??....
Ulikwenda saa ngapi"
"ilikuwa ni mida ya saa saba mpaka saa nane za
usiku"
Sasa general Nyange kusikia mida hio ndio alikuwa porini kule
wanapakia silaha,...
"enhee, alirudi saa ngapi"
"Kiukweli
hajarudi, nadhani ni mpaka asubuhi mana nimetoka akiwa bado
hajarudi"
"yes,... Lazima atakuwa ni yeye tu.... Huyu kijana ni wa
kumuondoa"
Aliongea general nyange, maneno yaliomfanya mwaju kushtuka
sana
"General..... Kwanini lakini... Huenda yule ni mtoto
wako"
"ina maana mtoto wangu humjui wewe?... Mtoto wangu anafanana na
yule kweli... Yaani hata sura haziendani labda sauti tu"
"lakini mbona
kwenye simu yake nimekutaka picha ya mke wako"
"ati unasemaje?... Picha
ya mke wangu mimi"
"ndio... Ila ni picha ya mama sheby yule mke
mkubwa... Ambae ni mama yake sheby"
Sasa huyu mwaju, anaijua vizuri
familia ya General nyange....
"huyu kijana ni nani.... Hebu nenda
ntakuita kwa wakati mwingine"
General alijikuta mawazo yakizidi kumpanda
katika kichwa chake,...
"najua sio mtoto wangu, lakini kwanini awe na
picha ya mke wangu katika simu yake??.... Huyu kijana kuna kazi imemleta kwa
ajili yangu,.. Atakuwa hayupo kijeshi hapa kambini"
Mzee general alianza
kuhisi kuwa sahi atakuwa hajaja kimafunzo japokuwa kaletwa kwa ajili ya
mafunzo,...
Sasa mwaju alikuwa anakumbuka miaka ya nyuma
kipindi akiwa na sheby,... Kumbe sheby na mwaju walikuwa ni wapenzi waliopendana
sana, wakiwa hapo hapo kambini, lakini sheby alipofariki kwenye mazoezi ndipo
kupenda kwake kukaishiaga hapo,... Mpaka leo hajapenda tena mtu wa aina yeyote,
sasa anapomuona sahi anamfananisha na sheby mtoto wa General nyange, na wakati
mtoto wa General alishakufaga kwa mlipuko wa bomu, katika mabomu ya kufanyia
mazoezi kuna moja lilikuwa ni la kweli, hivyo
alikufa..
Sasa
huku kwa General alimwita mkubwa mwenzake ambae wanalingana vyeo kidogo tu, ila
nyange ndio kuu la majeshi....
"me deo? Unajua huyu kijana mgeni toka
aje yaani mimi sipati usingizi kabisa yani"
Aliongea mr nyange huku
akitamani hata kulia, mana wakimpangia njia za kumuua, chuo kitaonekana kina
matatizo, mana wanafunzi wanakufa tu, hivyo miaka inayokuja hakutokuwa na
wanafunzi, na miaka kadhaa mbele kutakuwa hakuna jeshi, hivyo kumuua hawawezi
kwa kubofia nchi kuingia hatarini kwa kukosa jeshi,...
"kwanza kabla ya
yote mi naona ule mzigo tumkabidhi mwenyewe kwanza... Mana huyu kinana akiuona..
Itakuwa tabu"
"lakini deo, kwanza tumjue huyu kijana ni
nani"
"wala haina haja sana bwana nyange,.. Huyu kijana ni mdogo sana
kwetu, na wala hajatumwa huyu.. Sema sisi ni wasiwasi wetu tu"
"deo
usichukulie jambo hili mzaha mzaha"
"sikiliza... Huyu mtoto ni wa kuwa
nae karibu, kama umegundua ana uwezo basi ni wa kukaa nae karibu"
"ukae
na hatari tena..."
"kwani una asilimia ngapi za kumhisi"
"aahhhh
nyingi sana, tena na vile kamanda alivyoniambia kiwa ni mtaalamu wa kuruka ruka,
ndio nahisi atakuwa mpelelezi huyu"
"hapana hisia zako tu... Sasa
mpelelezi hawezi kuja jeshini... Sasa sikia ngoja tumuite"
General Deo
alitoka nje na kumuita sahi, sahi bila kujua mipango ya mageneral hao alikuja na
kuingia, lakini sasa ile anaingia tu ile saa ikawaka taa nyekundu kuashiria hapo
ndani kuna kamera, sahi aliizima haraka haraka kabla hajashtukiwa na mageneral,
sahi alipiga saluti kubwa kuwapa heshima yao kutokana na vyeo vyao
"kaa
katika kiti"
Aliongea mr deogratias tena kwa kumbembeleza kwa utaratibu
wa hali ya juu, na hawa nao ni mageneral wa zamani wanajua jinsi ya kumteka
mtu,
"jana saa nane ulikuwa wapi"
Aliuliza mr nyange, huku sahi
akiwa na wasiwasi sana, mana anajua jana hajaonekana kumbe
kaonekana....
"nilikwenda msalani"
"msalani kwa masaa
mangapi"
General anauliza maswali yale yale ya kumkamata, mana kapewa
ifo zote kuhusu jambo la jana,.....
"nilikuwa nasumbuliwa na tumbo la
kuendesha"
Mara mr deo akaingilia kati,...
"sikiliza kijana....
Jana tumeona ulichokifanya kule porini,... Sasa endepo hutokuwa na sisi,
tunakutimua hapa jeshini... Na wala usitake kubisha, hana umeuwa watu wawili, na
mmoja ndio huyo yupo hospitali hoi hoi.... Hii ni kesi"
Sasa sahi yeye
alijua tu hapa anapelelezwa kichini chini...
"nilitokea wapi kwenda
huko"
"tunakujua, na aliekuleta tunamjua wala usitake kutuumiza
kichwa... Umeshajua sisi ni wauzaji wa silaha hapa jeshini... Sasa unachokifanya
hakitokuseidia lolote.... Ungana nasi.. Yule mgonjwa katuambia kila kitu sema
hatujataka kukudhalilisha mbele za watu pale paredi.... Yule mgonjwa kasema,
ulikuwa umevaa saa kubwa,.. Afu hio saa inawaka taa... Hapa jeshini waliovaa saa
ni walimu tu, sasa je? Wewe ni mwalimu"
Alipomaliza kuongea mr deo, mara
mr nyange akatoa briefcase ya pesa na kuiweka mezani huku
akisema
"kijana... Kabla ya yote... Kuna milioni 100 hii hapa... Yaani
ukikubali tu, chukuwa hizo pesa"
Mr Nyange
aliona hakina njia nyingine ya kumteka kijana huyo, ispokuwa pesa tu,... Lakini
sasa ubaya wao ni kwamba hawa hawajui kama sahi ni mpelelezi wa serikali, tena
mwenye kiwango cha hali ya juu mno,... Kwahio wanachokijua kwa sahi wao
wanadhani ni kijana tu ambae anapenda haki hapendi vitu viende tofauti, kumbe
sivyo, bali sahi ni mpelelezi tena aliepitia ujeshi nchini korea,.. Lakini hawa
hawalijui hilo kuwa sahi ni mpelelezi wa serikali, wanajua ni kijana mpenda haki
na ndio mana akazuia silaha kusafirishwa,...
Sahi alitoa macho
kuona lile briefcase la pesa taslimu shilingi milioni 100, na ni zake endapo
atakubali kujiunga nao,...
"sawa,... Ila kila kinachoendelea kwenu nami
napaswa kukifahamu"
Huezi amini sahi alikubali kujiunga nao, na
kadhihirisha kuwa yeye ndie alie wauwa wale magaidi kule porini,
"hilo
ondoa shaka kijana, kila kikao lazima tukuhusishe"
"sawa,...nipo tayari
kujiunga nanyi"
Sahi aliisaliti serikali yake, ila sahi alionekana
msaliti kabla, mana kabla hajaja jeshini alionekana na kifaa cha pesa kiitwacho
Discate of money (DOM).... Na kifaa hicho kinatafutwa na serikali yake na yeye
ndie aliepewa kazi, na yeye ndie anae kimiliki kifaa hicho,... Yaani sahi ni
msaliti kabla hivyo hapa kadhihirisha usaliti wake....
"ok... Ila kijana
kuna swali naomba kuuliza. Kuna picha nilishawahi kuiona katika simu yako... Ile
picha una uhusiano gani nayo"
Sahi kabla hajajibu aliitoa simu yake na
kuiweka mezani huku akisema..
"nina rafiki yangu mmoja nilisoma nae,
aliitwa Sharbiny... Alikuwa ni rafiki yangu sana, na yeye alikuwa jeshini, mimi
nilikuwa sipendi kujiunga na jeshi, lakini rafiki yangu alipofariki dunia, ndipo
nikaamua kumuunga mkono... Nakumbuka kabla ya yeye kujiunga tulikuwa tukienda
sehemu ya mazoezi ya mapigano,... Na yeye alikuwa akinisihi kujiunga na mafunzo
ya jeshi, na aliahidi kunisaidia kwakuwa baba yake alikuwa mkuu wa jeshi,..
Lakini pia sikutaka kujiunga... Nilikuja kujua umuhimu wake pale alipokufa,
ndipo nikaamua kujiunga na jeshi... Nilimpenda sana rafiki yangu na ili nimuenzi
na kumkumbuka, ndio nimeweka picha ya mama yake katika simu yangu, mana hata
mama yake alikuwa ana upendo nami kwakuwa nilikuwa rafiki wa mtoto
wake"
Sahi alimaliza kuongea ukweli wake wa hapo
awali,...
"je huyo baba yake unamfahamu"
"hapana, sijawahi
kumuona"
"mbona ndio mimi baba wa Sharbiny.. Na ndio mana nikakuuliza
kuhusu hio picha"
"waooooooo.... Kumbe nimefanikiwa kukutana na baba wa
rafiki yangu"
"ndio... Karibu kwenye ulimwengu wa
wanajeshi"
"Ahsante sana mzee wangu"
Sasa mzee kaamini moja kwa
moja kuwa sahi ni rafiki wa mtoto wake, na General Nyange na deo, wanajua kuwa
sahi ana wiki ya jeshi na ana wiki ya TSS, basi sahi aliondoka huku akiwa
kashika kibegi chake cha pesa akielekea chumbani kwake,
Wakati
huo mageneral wawili wakiwa hapo ofisini kwao, walikuwa wakigongesheana mikono
kwa kumjua kijana machachari kama huyu
"Deo, huyu kijana anafaa tumtumie
kwenye kazi zetu,... Tena uzuri ni kwamba kazi yake ina Options mbili.. Anafanya
hapa TMA na TSS, sasa urahisi wa kupata ule mzigo uliobakia kule ni mkubwa sana
kupitia huyu kijana"
"Nyange una akili sana, unajua kupata kijana jasiri
kama huyu ni ngumu sana"
"vijana wote tuliowaweka mbele, wamekwisha
kufa,.. Hawakuwa na uwezo, sasa kama huyu peke yake kauwa qale wajinga na silaha
zikabaki"
"deoooo.... Hapa tutawini, mana kijana ana kazi za Dar es
Salaam, hivyo ni rahisi kufanikiwa kwa urahisi"
Sasa wakiwa wanazidi
kuingea mara ghafla mwaju kaingia,...
"ooohhh binti karibu"
Mr
deo alimkaribisha mwaju
"sasa binti, kazi yako tuliokupa imekwisha, sasa
huna haja ya kumfuatilia tena, ila ukiona jambo lolote baya kwale, tunaomba
utudokezee.... Kwanza shika milioni tano hizi.. Ahsante kwa kazi nzuri, mana
bila wewe jana kwenda ndani kwake, imeturahisishia sana kumbana kijana mpaka
akakubali"
"Ahsante sana generally, nitafanya kama ulivyosema, na
nitazidi kuwa nae karibu pia"
Aliongea mwaju huku, akiziweka pesa zake
vizuri.. Na pesa hizo ni zile walizouza silaha na hazijakwenda.. Sasa hizo pesa
ndio hizi wanazogawa gawa mpaka sasa,...
Sasa huku nchini
Kenya, katika kambi ya waasi waliokuwa wakisubiri silaha toka Tanzania, lakini
mpaka sasa ni hewa..
"mbona hawa watu hawafiki na watakuwa wamepatwa na
nini"
Aliongea mkuu wa kikosi hicho, kila wakipiga simu hazipatikani...
Na gari lao huku Tanzania limetelekezwa porini hivyo hakuna hata wakisema
wafuatilie watashindwa kujua kilichoendelea, na maiti zimesha zikwa muda mrefu
sana... Na yule mgonjwa alishauwawa kwa kauli ya sahi, mana sahi ni mpelelezi na
anajua jangili akiwa hai ataleta athari gani... Sasa huku kenya wamechafukwa
wanataka silaha na watu wao,...
Baada ya wiki moja kupita, sahi
akiwa anawasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo ya Tss, sasa huku
ndipo kazi inapomhusu yeye,. Sahi aliingia katika jumba lake la kifahari, huku
akiwa na briefcase ya pesa taslimu shilingi milioni 100,...alizopata kule kambi
ya jeshi baada ya kukubali kujiunga na mageneral wauza silaha,... Jumba hilo la
serikali ambalo ni maalum kwa maisha ya sahi, lina kamera kila kona lakini
kasoro chumba chake cha kulalia ndio hakijawekwa kamera,... Basi alitoa pesa
zake na kuzipangilia vizuri katika begi maalum linaloweza kufichika kwa urahisi
mzuri... Alitafuta sanduku lake na kuitoa ile DOM (Discate Of Money).. Na
kuiangalia kwa kucheka...
"lazima imjue mwenzake alipo"
Aliongea
sahi akimaanisha kuwa ni lazima ajue codes Number zake zilipo, mana bila codes
number haiwezi kuchapa pesa hata kidogo..
Kesho yake asubuhi
akiwa katika gari yake yenye Number za usajili wa usalama wa taifa,.. Kwanza
transmission ya sikioni ilikuwa hewa,
"GU naongea..."
"ndio mkuu
hali yako"
"salama.. Nakuona umeingia mjini"
"ndio mkuu na sasa
naelekea TSS"
"ok... Kuwa mpole na kazi yako"
"sawa
mkuu"
Rais GU ana mawasiliano na sahi kwa kitumia transmission za siri
sana, lakini sasa transmission nyingi huonekana katika sikio, sasa mbona ya sahi
haionekani, je imeunganishwa vipi mpaka isionekane, mana sikio jeupee, halina
kinasa sauti lakini sahi anasikia... Katika geti la TSS, sahi anafunguliwa kama
mgeni katika kitengo hicho... Mpaka akaingia katika kile kibanda kilicho kama
gereji lakini ukifika hapo hio sehemu inabonyea chini na kukushusha chini,
ambako ndio makao makui ya
tss,...
Sasa kuna
wakuu wa kitengo hicho, kama mageneral, na General mmoja anamjua sahi, ila kuna
general mwingine huyo kijana kijana sana, aitwaye JJ huyu ni mtoto wa rais
kapewa cheo kutokana na elimu yake, lakini sasa kijana huyo alipo mwona sahi,
alishangaa sana zile hatua anazopiga sahi,.. Yaani huyu JJ alikuwa akimshangaa
sana BB...
"mkuu vp mbona unamtazama sana huyu mgeni"
Aliulizwa
na kijana mmoja aliopo katika kitengo cha computer,...
"huyu mtu ana
hatua kama rafiki yangu,.. Yaani anatembea hivyo hivyo"
Aliongea JJ huku
akizidi kumtazama sahi,... Sasa saho nae kajua kuwa anaangaliwa sana na General
JJ...
"habari yako generally JJ"
Sasa JJ alizidi kutaharuki pale
aliposikia sauti ya sahi,... Yaani vinafanana na rafiki yake kasoro sura tu ndio
havifanani kabisa...
"salama tu hali yako"
"nzuri... Ahh mimi ni
mgeni, naitwa salahe Rashidy, nilikuja juzi hapa lakini kwa bahati mbaya
sijaweza kuku kuta General wangu"
"sawa kabisa.... Hakuna shida na hiki
ndicho kitengo husika"
JJ alikuwa akiongea lakini hisia zake zinahisi ni
rafiki yake tu, hata iweje, japo rafiki yake alifariki dunia akiwa mazoezini,..
Yaani JJ au Joseph John alikuwa na urafiki mkubwa sana yule mtoto wa General wa
jeshini, yaani yule mkuu wa majeshi kule kambini....
Sahi yeye
alipitiliza mpaka katika computer yake, mana siku ile ile, alipatiwa kisehemu
chake chenye computer, na sio yeye tu bali ni watu wote wa vitengo hivyi, ni
lazima ajue maswala ya computer, na kazi kubwa hufanywa na computer, hivyo
lazima uijue computer,....
Sasa sahi alipofika katika computer
yake, aliingiza program ya ile DOM kisha akaanza kuichambua kwa undani wake,..
Ipoje na inafanya kazi vp, na mashine yake ni ipi... Lakini akiwa anaendelea
kufanya hivyo mara alibanwa na haja ndogo, hivyo akaacha kile alichokuwa
akikifanya kisha akaelekea toilet, mana hapo ni ofisi moja lakini imegawanywa
vijichumba vidogo dogo kusudi kila mmoja akae sehemu yake apeleleze kitu
chake,.. Sasa sahi yeye kaja kama mwanafunzi lakini kitu alichokiacha katika
computer yake, ni kitu kikubwa sana ambacho kilitakiwa kufuatiliwa na mageneral
wakubwa ila sio mwanafunukama huyo,... Sasa JJ akawa anakuja katika ofisi ya
BB,... Alishangaa sana kwa kile alichokikuta katika skrini ya
sahi,...
"hii si DOM hiii??... Huyu anaitafuta kama
nani"
Aliongea JJ lakini alikuwa kama anajiuliza mwenyewe,.. Joseph
hakuridhika na jambo hilo alitoka na kuelekea chooni kule kule alipo sahi ila
Joseph hajui kama sahi yupo huko,.. Sasa JJ ndio anapiga simu lakini haijulikani
alikuwa akimpigia nani ila ilionekana ni simu ya siri sana... Na huyu ni mtoto
wa rais,..
"halo habari yako mkuu"
"salama.. Vp mbona kama una
wasiwasi hivyo"
Sasa sahi anasikia ishu nzima ya JJ anavyoongea na huyo
mtu... Kama kawaida ya saa yake kurekodi,..
"kuna kijana ananipa mashaka
sana hapa kitengo"
"ana nini"
"Naona ana program ya DOM sasa
huyu ni nani na ni mwanafunzi"
"whaaaat?? Unasema ana program ya
DOM??.... Kaipata wapi?"
"siwezi kufahamu, ila mkuu nina wasiwasi na
wewe, mana kijana huyu ni mgeni katika kitengo hiki, iweje ajue siri hii....
Kwanza niambie hio DOM ipo"
"ndio ninayo... Na yule mnunuzi anakuja
kuichukuwa mwezi ujao sasa DOM Codes ndio inatakiwa haraka
sana"
Maongezi hayo yalikuwa yakiendelea
pasina kujua kuwa palikuwa na mtu akisikia, yaani sahi ana bahati ya kujua vitu
kuliko uwezo wake, sasa kitu anachokitafuta na asijue angeanzaje leo anapata
njia jinsi ya kukianza... Hapo alipo sahi alikuwa anajiskia furaha sana kwa
kujua dom ilipo,... Ila sema hakujua nani aliekuwa akiongea nae
"kwahio
sasa mkuu, huyu kijana tumfanye nini, mana tayari anaifuatilia ishu
yetu"
"huyo hana shida, tayari yupo upande wetu"
Sasa hapa ndio
kama tunapata ufumbuzi juu ya mtu ambe anaongea naye katila simu, ni baada ya
kusema kuwa kijana huyo yupo upande wetu
"sasa mbona hujaniambia
kabla"
"hapo ndipo nilipofanya makosa, lakini.. Kuhusu ishu ya dom
hatujamgusia hata kidogo"
"sasa kwanini anayo programu ya
dom"
"hebu mshirikishe, huenda ana elimu zaidi au anaweza kuipata codes
za dom"
"hebu ngoja nijaribu kuongea nae mana katoka
kidogo"
"sawa... We mshirikishe mwambie mimi na wewe ni kitu
kimoja"
"sawa mkuu, nimekuelewa... Afu unaonaje tukamfanya kipaumbele
akailete hio codes, na akifa huko atajua mwenyewe"
"sawa pia, ila kuwa
makini na hilo"
"usihofu mkuu, tulikuwa tukifikiria chambo tutakitoa
wapi sasa ndio hichoo kimejileta"
"na huyo ataiweza kazi mana ni
majasiri mno"
"basi tuyaache mkuu"
"sawa"
Simu
ilikata kisha Joseph akarufi katika ofisi ya sahi na kukaa, mana tayari keshajua
kuwa wana ushirikiano mzuri na sahi,... Sasa hapa tunagundua kuwa hata huyu
mtoto wa rais sio mwema, na ndio anaeiumiza nchi kwa cheo alichopo.. Mana hiki
kitendo ni zaidi ya CIA (Criminally International Army).. Na kitengo hiki
kinaingia sehemu yeyeote ile ndani ya nchi husika, yaani ni kitengo
kisichojulikana lakini kinapoingia mahala hakiwezi kukataliwa kutokana na
utambulisho wake...
Sahi akiwa ndio anafika katika computer
yake lakini alishangaa kumkuta Joseph akiwa kaketi katika kiti cha pembeni, sasa
sahi akajifanya kama kakosea sana kuiacha ile programu pale kwenye
skrini,...
"Samahani mkuu, ni programu ya kawaida tu"
Aliongea
sahi kujifanya ni muoga kama panya, kumbe hakuna mtu mbaya kama
yeye,...
"wala usijali... Ila nina maswali kadhaa kuhusu hii programu
yako hapa"
"sawa mkuu hakuna shida"
Hawa watu wawili ni lika
moja, lakini Joseph yeye ana cheo kikubwa sana cha ugeneral, ila hata kama awe
nani hawezi kuukuta uwezo wa sahi,... Sahi kasomeshwa na mtu binafsi na sio
serikali, hivyo hapo anaifanyia serikali na sio mtu binafsi,.. Mana mtu
aliomsomesha mpaka sasa yupo madarakani,.
"hii programu uliipata
wapi"
Aliuliza Joseph huku sahi akijifanya hajui saaana kuhusu hio
kitu
"aaa... Hii programu mbona niliikuta hapa hapa kwenye hii
computer"
"unasemaje??... Ni kweli, na hata mimi nimeshangaa kwanini ipo
hapa, na pia nimeshtuka sana kuiona hapa"
"sio kuwa umekuja
nayo"
"hapana, mimi ni mgeni nitawezaje kuja na kitu kama
hiki"
"unakijua hicho kifaa"
"yes... Hio ni dom"
"hii
dom ainatafutwa sana,.. Na nitakuwa nawe mstari wa mbele"
Aliongea
Joseph huku akiangalia pembeni kama hakuna mtu anaesikia, kisha akamuinamia sahi
na kumwambia
"sisi sote tupo pamoja... Hio dom sisi tunayo... Ila codes
zake ndio hatuna"
Sahi akajifanya kushtuka sana huku nae
akisema
"aahhh kwani hizi dom zipo ngapi... Mana mimi ninayo yenye codes
zake kabisa"
Joseph alishtuka kuskia hivyo, ilibaki kidogo tu adondoke
kwa mshtuko...
"unasemaje"
"ndio... Ninayo dom ina codes zake..
Ngoja nikutafutie programu yake"
"wewe si ulisema hio programu uliikuta
hapa wewe"
"nilikudanganya, hii program ni yangu na hapa nilikuwa
nacheki information yake ipoje"
Sasa sahi akafanya vitu vyake kwenye
computer, kachapia chapia hapoo kisha akamwonyesha codes za
dom..
"unaziona hizi... Hizi ndio codes za dom... Alafu dom yenyewe
ninayo hapa kwenye begi"
Sahi aliitoa ile dom kisiri siri, na
kumwonyesha Joseph ambae ni mtoto wa rais aliopo madarakani,.. Hivyo mtoto
anaihujumu nchi ya baba yake,..
"we hii kitu umepata
wapi"
"unanitisha tena"
"hapana, nataka tu kujua umetoa
wapi"
"niliikuta chumbani kwa baba yangu"
"baba yako anafanya
kazi gani serikali"
"Alikuwa ni mtumishi wa BOT"
"sasa, tupe hio
dom na hizo codes zake... Tutakupatia bilioni moja tasilimu"
Sahi
kusikia neno Bilioni moja, sio pesa ndogo hio, unakula mpaka ucgakae, sasa hapa
wamekutana wapelelezi wote, hivyo kikubwa ni kumjua mshindi ni nani na wote ni
lika moja, yaa hata umri wa hawa watu ni sawa... Sasa sijui kwanini imekuwa
hivyo
"hio ni pesa kubwa sana mkuu... Lakini, nikikupa hii baba yangu
ataniletea shida... Sasa tufanyeje ili nisiletewe shida"
Aliongea sahi
huku akiingiza dom katika begi lake,...
Joseph alikuwa akiutamani sana
mana huenda kule bank alichezewa mchezo siku ile na kuwekewa feki,... Afu mbaya
zaidi ile walionayo haina programu,
"huyo baba yako alistaafu mwaka
gani"
"mwaka jana"
Sasa kusikia mwaka jana, Joseph akajua lazima
huyu baba yake sahi aliondoka na Original kisha akaacha dom feki,.. Na ndio hio
wanayoitafutia codes zake, kumbe sio Original...
"sasa sikia,
nitakupatia hio tulio nayo.. Kisha utupatie hio"
"sawa... Mimi kitu
ninachokitaka ni baba yangu asijue kama dom haipo"
Joseph aliona kapata
Zezeta lao la mwaka, yaani bonge la Zezeta... Wasipoangalia watafanywa mazezeta
wao...
Joseph hakuchelewa kuoiga simu kwa General
Nyange,..
"haloo mkuu..."
"kuna nini tena
Joseph"
"mkuu... Huezi amini kumbe sisi tunamiliki dom
feki"
"ati unasemaje wewe"
"hio dom ni feki mkuu, yaani
tumeingia choo cha kike"
"kama hii ni feki, hio Original iko
wapi"
"huyu kijana anayo, tena ina codes
zake"
"Whaaaaaat???..... Ati unasema nini"
"ndio hivyo
mkuu"
"sasa si umwambie akupe, huyo ni mtu wetu"
"tatizo ni
kwamba, anahofia kwa baba yake atajua kuwa dom haipo ndani.. Hivyo angalao tumpe
hio feki akamdanganyie"
"una uhakika hio ni yenyewe"
"ndio mkuu,
na nimeziona codes zake"
"basi ngoja niitume hii dom nilionayo huku,
kisha nawe itume hio... Nampiga simu yule mzungu aje aichukuwe sasa hivi, mana
haifai kukaa
nayo"
Sasa huku
kambini kwa General aliekuwa ofisini kwake pamoja na mr deo General
mwenzie
"deo, hatimae dom original yapatikana"
"unasemaje
nyange"
"kumbe yule kijana baba yake ni mtumishi wa BOT, na ndie
alieondoka na dom original"
Aliongea mr Nyange huku wakiwa na furaha ya
hali ya juu,... Na wao wakiipata wanaiuza kwa mzungu mmoja ambae yeye ndie
anamiliki mashine ndogo ya kuchapia pesa, hivyo mzungu huyo akifanikiwa kuwa na
dom hio atachapa pesa ya Tanzania ambayo ni laki moja ya noti moja, ni hatari
sana mtu binafsi kuachia pesa tofauti na serikali...
"kwahio, yule yule
kijana tuliekuwa nae jana ndio mmiliki wa dom Original?"
"ndio, na ni
dom iliokuwa ndani kwa baba yake"
"anhaaaa, sasa tutaipataje hio
original"
"lazima tumpatie hii yakwetu ili baba yake akaendeleee
kudanganyika"
"sasa unasubiri nini, ita helikopta hapa uitume
haraka"
Harakati za kutuma dom zilianza huku wakijua kuwa watakapo ipata
tu wanaiuza yaani hawataki kukaa na mzigo tena, na hata sababu ya kukaa na mzigo
kwa muda mrefu ni kwamba hawaku ukamilisha mzigo huo,....
"lakini mr
nyange, angalia sana uwepo wa huyo kijana.... Mana kuipata dom sio kitu cha
mchezo eti"
"aaahhh hakuna tabu, kama kasema baba yake alikuwa mtumishi
wa BOT sasa kuna maswali gani hapo"
"basi haya,
itume"
Huku TSS sahi alikuwa akiendelea kumwonyesha kazi ya hio
dom, unajua wengi wanaitafuta lakini hawajui inafanyaje kazi, japo wanajua ndio
kichapisho cha pesa lakini hawajui kinafanyaje kazi,... Sahi akazidi kumpa
Joseph jinsi dom inavyofanya kazi katika mashine...
"sahi, hii mashine
upatikanaji wake vipi"
Aliuliza Joseph baada ya kuoneshwa mashine
hio
"hii mashine, kuipata sio rahisi, unapaswa kuwa tajiri mkubwa sana
katika dunia... Na hata serikali binafsi haiwezi kuimiliki mana kuinunua kwake
inaweza kufilisi nchi"
"duuuuuu,... Kwahio yule mzungu ana mashine
sio"
Aliongea Joseph, maneno yaliomshtua sahi mana hajui hio dom inauzwa
wapi,..
"mzungu??...mzungu gani huyo"
"kuna mzungu anataka
kuinunua kwa thamani ya shilingi bilioni 500"
Sasa sahi ndio anajua kuwa
hio dom inauzwa kwa mzungu na gharama ni Bilioni 500,...
"sasa
mnachelewa nini nanyi"
"wewe si ndio unayo"
"walete hio feki
basi nika mdanganyie mzee kama ipo kumbe ni feki"
"inakuja
usijali"
Wakati huo helikopta ipo angani kuelekea jijini Dar es
Salaam, kuipeleka dom feki,...
"sahi, tutoke nadhani dom inakaribia
Airport"
"Twende"
Basi sahi na Joseph walitoka pamoja lakini ni
kila mtu na gari yake,...
Sasa wakiwa wapo njiani, sahi alipokea simu ya
Mheshimiwa rais GU,
"haloo mkuu"
"habari yako
kijana"
"salama tu Gu"
"vipi kazi inakwendaje"
"nakwenda
kuchukuwa dom original"
"sawa... Angalia usije haribu mipango, wasije
kukushtukia"
"usijali mr GU"
Mazungumzo yao hua sii ya simu ya
kawaida, huwa wanatumia transmission iliounganishwa automatically katika sikio
la sahi, lakini hio transmission haionekani katika sikio la
sahi,...
Sasa sahi alipokuwa barabarani, kuna gari aliiona, na
anaijua hio gari, wakati huo Joseph yupo nyuma ya sahi, na sahi yupo mbele, sasa
sahi kaona gari ya mama mmoja hivi anamjua vizuri,... Sasa ile gari ya yule mama
ikapaki pembeni,... Sahi alishindwa kuvumilia kumpita huyo mama,.... Sasa hata
Joseph pia anaijua hio gari ya huyo mama,... Lakini yeye hakutaka kusimama...
Ila hofu ilimjia mr Joseph, kwanini sahi kasimama kwa ajili ya huyo mama... Mama
huyo ni mke mkubwa wa General Nyange, yaani mama wa yule marehemu itwae
Sharbiny,... Sasa Joseph anashangaa, huyu sahi amemjuaje huyu mama.... Sasa sahi
anaharibu kila kitu,.... Lakini sasa huyu mama ndio yule alie onekana kwenye
simu ya sahi, ndio huyu hapa
"shkamoo"
Sahi alimsalimia mama
huyo, mama kwa mshtuko wa sauti ya mtu huyo alijikuta akilia mwenyewe,... Sasa
swali linakuja hivi, kwanini sahi anafanana sauti na huyo kijana... Sasa je,
hata huyu mama pia hamjui sahi??....
"huyu sahi, anajuana vipi na huyu
mama,... Hapana lazima nimtaarifu General Nyange, je huyu ni
nani?"
Aliongea Joseph huku akichukuwa simu yake na kutafuta jina la mr
Nyange,...... Sasa sahi keshaharibu swala la kwenda kuchukuwa dom
original....
Hatimaye Dom original
yapatika kirahisi sana, kumbe ile dom tuliokuwa tukiiona kwa sahi ile dom
feki,.. Hivyo kwakuwa sahi ni mpelelezi japo kajiunga na watu hao sasa katika
hali ya kwenda kuchukuwa dom original, wakiwa barabarani na askari mwenzie
aitwaye Joseph John (JJ) sahi kina gari aliiona kitu kilichomfanya nae
asimamishe gari baada ya gari hio alio iona kusimama katima sehemu za paking...
Sasa kumbe hata Joseph anamjua mama huyo ambae sahi kasimamisha gari kwa ajili
yake,
Joseph aliona hili nalo ni tatizo, hivyo alichukuwa simu
na kumpigia mr Nyange wa kule kambini, na mama huyo ni mke wa mr Nyange, ambae
ni mkuu wa jeshi
"haloo mkuu"
"Enheee vp umeshaipata hio
dom"
"hapana, ndio tunaelekea huko... Lakini tupo hapa njiani tumemwona
mama, ila kinachonishangaza ni kwamba mbona huyu kijana anafahamiana na mkeo
ambae ni mama yake sheby"
"ni kweli... Ila huyo pia alikuwa ni rafiki wa
sheby, hata mimi huku niliona picha ya mke wangu kwenye simu yake, nikamuuliza
ndio akanipa huo ukweli"
Aliongea mr Nyange na ni kweli hata kule
kambini sahi aliulizwa kuhusiana na hio picha katika simu yake, je wana
mahusiano gani na mama huyo, na sahi alijibu vizuri tu.. Basi Joseph akawa
kaupata ukweli kuwa kumbe nae huyu alikuwa rafiki yake, lakini Joseph bado
haamini amini kwasababu yeye ndie rafiki mkubwa wa sahi, na anamjua sahi hakuwa
na rafiki mwingine zaifi yake, sasa iweje leo ana rafiki
mwingine...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment