Search This Blog

Thursday 24 November 2022

PETE YA KIKE - 5

 

     



     

     

    Chombezo : Pete Ya Kike 

    Sehemu Ya Tano (5)



    "Shikamoo mama"

    "marahaba mwanangu hujambo"

    "sijambo... Vipi, simu yako iko wapi"

    "nimeiweka chaji kule dukani"

    Aliongea mama huyo huku shadya akiwa haamini kama hajaonwa

    "vipi, boss hajakuona"

    Aliuliza shadya huku mama akishangaa

    "boss? Kwani kaja huku"

    "eeeh mungu wangu, Afadhali hata hajakuona"

    "kwani kaja"

    "ndioooo... Kafika mpaka hapa"

    "weeeeeeee shadya muongo"

    "ndio, yaani nilikuwa nishaanza kukusanya vitu vyangu mana nilijua kazi sina tena"

    "eeehh mungu wangu weeeee, Afadhali hajaniona jamani"

    Aliongea mama huyo, maskini ya Mungu bila kujua kumbe boss ni mtoto wake wa kumzaaa, yaani ilikua ni bahati juu ya bahati.... Basi ikawa ndio hivyo na hali ikaishia hivyo,... Mara ghafla simu ya shadya ikaita

    "yes boss"

    "uko wapi napiga simu ya mezani hupokei"

    "nakuja boss, Samahani"

    Shadya alikimbia kwenda ofisini, huku mama akiwa haamini kama boss kaja na hajamuona....



    Sasa huku kwenye ki restaurant Kimoja hivi, asha anamtolea nje sadiki

    "samahani sana kaka, nakueshim sana... Kiukweli Sitaweza kuwa nawe"

    Aliongea asha huku akimpa simu yake na uzuri hajawahi kumchuna...

    "asha, kwanini lakini,... Unautumiaje uzuri wako kunikosesha raha ya maisha namna hii"

    "Kiukweli siwezi, Utanisamehe.... Niache kwanza nina maumivu ya mapenzi hivyo sihitaji kuumia tena kwa sasa"

    "lakini asha, nimesha kwambia wanaume tupo tofauti asha... Nitakupenda mama"

    "hapana,... Niache niende kazini"

    Asha aliondoka huku sadiki akiumia roho,... Asha anataka kujipendekeza kwa boss mkuu japo hajui hata jina la boss huyo na hata sura hajawahi kumuona...



    Asha anafika ndani ya kiwanda anasikia kuwa boss mkuu alitembelea muda sio mrefu...

    "weeeee hadija... Unasema kweli"

    "weeee, afu ni kitoto kabisa kizuriiiiii"

    Asha roho ilimuuma mana ndio mwanaume ambaye anatamani kuwa nae hivyo moja kwa moja tunajua asha kaja kujipatia bwana ili amchune vizuri, lakini sasa anga anazo lenga ni mbaya sana... Hajui anampenda ndugu yake kabisa wa kuzaliwa naye..

    "nakwambia shosti asha umekosa uhondo,... Afu alipotoka hapa akaenda chooni kule kuangalia usafi wa vyoo"

    "mungu wangu jamani..."

    Asha kwa hasira alitoka kwenda mpaka chooni kwa mama yake...

    "mama, eti naskia boss katoka nje"

    Aliuliza asha huku mama nae akampa moto mwanae

    "ndio, kaja hapa na kundi la watu... Jamani kijana ni mzuri huyo"

    Mama nae anazidi kumuumiza mtoto wake ingali hata yeye mama hajamuona mtoto huyo, na ni mtoto wake...

    "mamaaaa... Namba zake hujapata"

    "mbona una haraka we mshenzi kweli, na ulikuwa wapi hujamuona"

    "nilitoka na Meneja kwenda kumpa simu yake"

    "kwahio humtaki meneja tena"

    "silitaki bwana... Nataka huyo saizi yangu, mi naona meneja mkuubwa"

    "ehehehehehehe, we mtoto acha kuchagua wanaume mwanangu"

    "booooo..... Mi naenda ndani,.. Ila fanya mpango wa namba mama"

    "hebu nenda tusije kuonekana tuna njama fulani"

    Mama alimfukuza mtoto wake ili wasije kuonwa kama kuna njama wanapanga hapo chooni....



    Ilipofika saa kumi na moja za jioni ikiwa ndio saa za kutoka kazini na kiwanda kufungwa, mabasi yalikuwa yakibeba wafanyakazi ili kuwapeleka,... Wafanyakazi ni wengi kana kwamba lazima mabasi yarudie wafanyakazi, ila wale wenye nauli au kwao ni karibu, hawana budi kuwahi..



    Mama surian akiwa ndani ya basi na mtoto wake, alishangaa na shadya nae huyo kwenye siti ile ile nae leo kaja kupanda gari ya wafanyakazi wa kawaida...

    "heeeeeee mwanangu, nyie si mna magari yenu nyie"

    Mama alimuongelesha shadya kuwa wao wana mabasi yao maalum

    "ndio, ila limejaa, sasa mpaka waturudie ni saa ngapi.. Bora nipande hili hili tu"

    Aliongea shadya huku wakibanana kwenye siti ya watu wawili akifosi wakae wawili ili awahi....



    "Uuuuuuuuuwiiiiiiii jamani nimesahau chaja yangu jamani"

    Aliongea shadya na kuacha mkoba kisha akashuka ili aende ofisini kuchukua chaja yake,... Sasa mkoba kawaachia mama surian na asha... Saa ngapi mama hajaingiza mkono kwenye mkoba wa shadya na kutoa simu kubwa ambayo ndio anayo itumia shadya....

    "we, hii ndio simu alipigiwa na boss, sasa tutapataje namba zake humu"

    Aliongea mama huyo huku basi likiwa sailensa kitaka kuondoka lakini kwakua mmoja kashuka hivyo limesimama kwa muda...

    "sasa kama ina loku itakuwaje mama"

    "hebu jaribu, wewe si unazijua kuzitumia hizi simu... Mana mimi sijui hata nagusa wapi hapa"

    Aliongea mama huyo huku asha akiichukua ile simu,.. Wakati huo wafanyakazi kila mmoja bize na simu yake mana huko kiwandani hawaruhusiwi kuingia na simu, sasa wakiwa kwenye basi, kila mtu bize na simu yake mana mchana kutwa hako nayo...

    "heeeee mama haina loku"

    "sasa mimi najua jamani... Angalia wewe si unazijua hizi simu"

    "ndio... Sasa nafanyaje hapa"

    "alipigiwa muda ule"

    Aliongea mama suria kisha asha akabonyeza sehemu ya namba zilizopigwa au kupiga...

    "sasa itakuwa ni ipi hapa mama, mana kapigiwa na watu wengi"

    Aliongea asha huku wakiangalia namba zilizopigwa muda sio mrefu

    "enheeee, kuna hii imeandikwa BOSS SURE"

    asha aliona namba ilioseviwa kwa jina la boss sure akiwa na maana boss suria, sema kaliandika kama kwa Kingereza fulani hivi kama swaga,...

    "itakuwa ndio hio... We ichukue sasa"

    Aliongea mama huyo kisha asha akasema

    "naichukua na nini sasa na sina simu"

    Aliongea asha huku mama akiwa haamini kuwa wanaikosa hio namba mana asha karudisha simu ya watu alio nunuliwa, na mama nae simu yake ipo chaji huko dukani kwa jirani yao... Afu mbaya zaidi shadya anakuja, na namba bado hawajachukua...

    "mama mi naona tuikariri tu"

    "hebu tujaribu, 0714419487... Mimi nitashikilia hio 071441....na wewe shikilia hio 9487"

    "sawa... Rudisha sasa huyo anapanda gari"

    Wakarudisha ile simu kisha wakafunga mkoba wake,.. Wakatulia kimya..



    Kiukweli familia ya surian imekumbwa na maisha magumu kana kwamba mpaka mama anakubali mtoto ajipendekeze kwa boss, tena mbaya zaidi mama ndio anampa msaada mtoto wake ili afanikiwe na maisha yao yaendelee kuwa mazuri zaidi, mana hapo mama kibarua chake kipo hatiani muda wowote anaweza kufukuzwa pale atakapo gundulika kuwa ni mzee asiotakiwa kufanya kazi kwenye kampuni hiyo... Hivyo anamtafutia mwanaye chansi kama Ataweza kumpa iwe rahisi katika maisha yao... Familia iliojaa dini lakini kutokana na maisha hawana budi kuwa watu wa aina hio,



    Huku ofisini baada ya wafanyakazi kuisha wote, surian ndio anatoka na kufunga milango ya ofisini, kwani yeye hutoka wa mwisho kabisa kama alivyo zowea kutoka kila siku,.. Aliwasha gari yake ya maana ambayo ndio wanaitumia yeye na mke wake,...



    Tukija huki kwa akina faima akiwa na tariki,... Mpaka leo tariki bado hajalubaliwa kwani faima alikumbushwa na shaimati kuwa surian yupo na yupo kwenye kiwanda cha nguo za Kiislamu,...

    "afu tariki mbona nimekuona umeshushwa na gari la STAFF BUS la Kampuni ya MICCO"

    Aliongea faima huku tariki akiwa haamini kama kaonwa, mana anajitapaga kuwa ana pesa chafu sasa leo kashushwa na gari la staff bus

    "ndio, kwani sijakwambia kuwa mimi ndio meneja wa ile kampuni"

    Aliongea tariki huku faima akijibu

    "aka, hata nikuulize ili iweje"

    "ok sasa lile jibu langu vipi, mana umebadilika ghafla"

    "naweza kukubalia, lakini nikupe mtihani mmoja,.. Nitafutie picha ya mmiliki wa kampuni hio yakwenu"

    Aliongea faima ili ajue kama kweli surian ndio mmiliki au vipi

    "mmiliki si unamaanisha boss wetu au"

    "ndio"

    "sasa fey jamani... Majibu yangu na huyo boss wapi na wapi jamani fey"

    "kwanza anaitwa nani"

    "aaahhh anaitwa sadiki"

    "sadiki??... Ni rangi gani"

    "mweusi hivi, mnene... Lakini fey, kwani ana nini"

    "nataka uniletee picha hapa"

    "haaaaaaa.. Feiiiiiiiiiiiii, sio kwa mtihani huu lakini"

    "kama unanipenda, utaweza, lakini kama hunipendi hutoweza"

    Aliongea faima kisha akamuacha tariki hapo hapo barabarani kisha yeye akapanda Bajaji kwenda zake nyumbani kwani giza lilikuwa likilindima kwa wakati huo.... Tariki kapewa mtihani mkubwa sana ambao hajui aanzie wapi na aishie wapi mana kweli anajua boss wa kampuni ile sio sadiki,.. Na kama sio sadiki je ni nani,.. Mana tariki hajawahi kumuona boss kwasababu mchana alipotembelea kiwandani, hakumaliza kiwanda chote, aliishia katikati na kwenda kukagua usafi wa vyoo... Hivyo hajafika kwenye idara ambazo tariki yupo... Hivyo hata tariki haijui sura ya boss....



    Sasa tukija huku kwa mama surian na mwanae asha...

    "wewe asha, tujaribu ile namba kabla baba yako hajarudi msikitini"

    Aliongea mama huyo huku wakiwa na shauku ya kupiga namba hio, na na waliishika nusu nusu....

    "sasa mama, tunapiga kwenye simu yako, kwani ina salio"

    Aliongea asha huku akiangalia salio kwenye simu ya mama yake...

    "weeeeeee tumia laini yako,.. Mana ukitumia yangu afu akapiga kwangu nitamjibu nini mimi"

    "sawa basi ngoja tutoe laini yako niweke yangu,... Ila yangu haina vocha ni sms tu"

    "nitakupa miatano ukanunue"

    Basi asha alimuachia mama yake aweke laini kisha akaenda kununua vocha, ili ampigie na usiku huo huo.. Ikiwa ni saa mbili kasoro, baba kaenda msikitini kuswali swala ya Ishah

    "hii hapa.. Lete niiweke"

    Aliongea asha huku mama akimpa mwanae simu ili aweke vocha ajiunge kisha ampigie....



    Wakati huo huku kwa suria katulia ndani anaangalia TV, na mkewe akiwa jikoni anapika, alikuwa akiangalia kipindi kimoja cha maigizo kinachoitwa MIZENGWE hivyo alikuwa akicheka sana, kana kwamba furaha kwake ilitawala sana



    Sasa huku kwa mama na mtoto,... Kumbe namba wamesahau, sasa wakawa wanabuni buni...

    "kwanini wewe ulishikaje jamani mama"

    "tatizo mimi nilishika namba nyingi ndio mana nimesahau mwanangu"

    Aliongea mama huku asha akiwa kashikilia namba zile za mwisho ambazo ni 9487, na mama kashika namba za mwanzo, afu kasahau...

    "jamani mama,... Bahati imepotea hivi hivi na mtu mwenyewe yule hatupandi nae gari mara kwa mara, leo ilikuwa kama bahati tu jamani mama"

    asha alilalamika sana kwa kitendo cha mama yake kusahau namba za mwanaume anayetamani kuwa naye kimapenzi ambaye ni boss wake, lakini bila kujua ni ndugu yake...

    "lakini kama vile kulikuwa na nne nne nyingiii"

    "aaahh bwana mama... Naenda zangu kulala..."

    "sasa njoo jamani"

    "sasa mama wewe unasema nne nne nyingi, ni namba gani inaanza na nane"

    Aliongea asha huku akitamani kulia, mana ndio basi....

    "heeeeeee uyoooooo njooo uko, nazikumbuka"

    Aliongea mama huyo huku akitabasamu kwani alimdanganya mtoto wake kuwa kazisahau,...

    "haya taja sasa jamani kabla hajalala... Mana ni tajiri yule analalaga mapema mno"

    Aliongea asha huku mama akicheka

    "mmmhhh jamani kupenda tabu,.. Heeee tu unalo mwanangu... Haya andika ni 071441 hizo ndio nimeshika mimi"

    Alipomaliza kutaja mama yake, kisha asha akamalizia kuzijazia zile alizokariri yeye,... Kisha akamuuliza mama yake kuwa...

    "sasa nimsevu nani"

    "we msevu vile vile boss sure"

    Asha alifanya kama alivyosema mama yake kisha akabonyeza kitufe cha kupigia

    "kohoa kidogo... Afu punguza uzito wa sauti yako... Bana sauti hata imtoe pangoni"

    Aliongea mama huyo kama kumfundisha mtoto wake jinsi ya kumteka mwanaume kwa sauti... Kweli asha kakohoa na kuseti sauti yake,... Mara simu inaita.... Na ni kweli ilikuwa ni namba ya surian, suria alikuwa bize na mchezo wa TV, lakini aliona bora apokee simu hio..

    Sasa alivyo pokea tu kabla hajasema hallo,.. Asha keshasema

    "Hellow, Samahani, naongea na boss sure"

    Aliongea asha kwa sauti ya kuvutia zaidi,..

    "samahani utakuwa umekosea namba... Mimi sio boss sure"

    Sasa huku kwa asha, ghafla alikata simu na kushtuka...

    "kasemaje? Ndio yeye au"

    Mama alimuuliza mtoto wake baada ya kukata simu

    "mama... Mbona ni sauti ya kaka surian"

    Aliongea asha kana kwamba kaijua sauti ya kaka yake,...

    "we mshenzi wewe, usinikumbushe machungu ya mtoto wangu, we niambie kakwambiaje"

    Mara simu ikaita tena,....

    "haya huyo kapiga yeye, pokea umsikie mwanao"

    Aliongea asha huku akimpa mama yake simu

    "asha mwanangu, mpokelee mwenzio bwana acha utani"

    "hapana mama... Ni sauti ya kaka surian"

    Aliongea asha huku mama akaichukua ile simu na kuipokea kisha akaiweka sikioni....







    Hakuna japo zuri kama siku kuongea na mtu uliopotezana nae kwa muda fulani,... Mama mwenye shida yake ni kusikia hio sauti ambayo asha anasema ni suria ambaye ni mtoto wake,... Mama kushika simu na Kutanguliza samahani, mana wamemsumbua mtu wa watu kumbe sio boss walio mtarajia... Mama kwa busara na hekima zake, aliipokea simu na kusema kuwa



    "Hallow baba, Samahani tulikosea namba tu"

    Aliongea mama huyo, lakini suria alishtuka na kujikaza kusema

    "hakuna shida mama angu siku nje..."

    Simu ilikata, lakini surian alishtuka kwa hio sauti, kwani kaifananisha na Sauti ya mama yake mzazi,....



    Surian hajavumilia kusubiri alipiga tena aongee na mwanamke huyo...

    "samahani, namba unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadaye"

    Surian alikasirika sana kwa kutopatikana kwa namba hio,...

    "nini baba Rashidi"

    Mkewe alimuuliza kwani alimwona akiwa na jazba ya ghafla tu...

    "skia muna,... Wiki ijayo nataka kwenda kuwaona wazazi wangu, na tutakwenda wote"

    Aliongea surian tena kwa hasira ili mke asije kuweka masharti mengine

    "lakini zile siku ziliisha, ni wewe tu mume wangu"

    Aliongea maimuna huku akimuuliza tena

    "kwani kumetokea nini"

    "kuna namba nimepigiwa nayo, nikasikia sauti ya mama yangu kabisa, sasa sjui ni yeye au zinafanana tu"

    "uaijali,... Wiki ijayo tutakwenda"

    Aliongea mwanamke huyo japo anajua kabisa mama yake alishawahi kuja kuomba kazi pale ila hana uhakika kama alipata au laah..



    Sasa huku kwa akina asha,... Ilionekana taxi ikibeba mgonjwa huku asha akilia sana, na aliokuwa akipakiwa katika gari ni mama yake... Kana kwamba sauti ya mtoto wake ilimshtua mno mpaka kupoteza fahamu.... Asha alikuwa akilia sana, sasa mbaya zaidi simu ipo kwenye ndoo ya maji... Kumbe wakati ule ilikuwa hivi... Wakati surian anaongea



    "Hallow baba, Samahani tulikosea namba tu"

    Aliongea mama huyo, lakini suria alishtuka na kujikaza kusema

    "hakuna shida mama angu siku nje..."

    Sasa wakati surian anaendelea kuongea, kumbe mama kaijua sauti ya mtoto wake, hivyo akapata mshtuko na kuachia simu ikaingia kwenye beseni la maji, ndio pale suria akaishia "SIKU NJE..." ni kwamba simu iiingia kwenye maji, sasa asha hakujali simu, kwani mama yake alikuwa na hali mbaya,.. Kwa bahati nzuri baba yao huyo kaja.. Ndipo akaita taxi ikaja kuachukua, simu bado ipo kwenye maji...



    Wakati huo huku kwa surian anazidi kupiga simu, lakini bado anapewa taarifa za kuto patikana kwa simu hio, sasa hatuliii hata kidogo, toka alipo ifananisha sauti ya mama yake...



    Huku hospitali mama yake akiwa katika matibabu, mpaka wakati huo hajazinduka wala kutoa neno lolote,.. Hio ni jinsi gani anavyo mpenda mtoto wake wa kiume, na imani ya kwamba surian alifariki alikuwa hana kabisa kwani anamuamini mungu kuliko maneno ya watu,



    Kesho yake ikiwa katika majira ya saa nne za asubuhi,... Shadya anahaha kwani Mwenye nafasi ya usafi wa vyoo leo hayupo,... Lakini ghafla asha katokea akiwa anakuja ofisini kwa Shadya...

    "samahani dada, habari yako"

    Asha alimsalimia Shadya

    "salama tu, ina maana wewe ndio unafika kazini"

    "ndio,... Kiukweli dada nauguliwa na mama yangu yule aliokuwa anafanya usafi wa vyoo"

    Aliongea asha huku Shadya akishangaa kusikia kua huyo ni mtoto  wa mama usafi,

    "ina maana yule mama ni mama yako"

    "ndio"

    "mmmmhhh ok, kwahio kapatwa na nini"

    "jana alianguka ghafla tu"

    "jamani poleni sana"

    "ahsante,.... Aahhh nimekuja kushika nafasi yake, japo yangu ipo kule idarani lakini nataka nishike nafasi yake"

    Aliongea asha kana kwamba kaja kumsaidia mama yake ile nafasi ya usafi wa vyoo,....

    "lakini ukumbuke nawe una nafasi yako asha"

    "ni kweli dada, lakini chooni ni sehemu muhimu zaidi, mana wakaguzi wakija itakuwa sio vyema wakute uchafu"

    Aliongea asha, na Shadya alimuelewa vyema kisha akamruhusu



    Tukija huku hospitali ambako mama yake surian kalazwa,. Alipata nafuu na ndio mana asha aliamua kufika kazini ili kazi zisiharibike, lakini mama surian kajua yule ni mtoto wake,. Nani kama mama... Yaani sauti tu inamfanya amjue mtoto wake aliompoteza katika macho yake ndani ya miezi mitatu kama sio minne, tena ni bora ijulikane kuna alipokwenda, lakini haijulikani mahali alipokwenda, na ndio mana familia ilipata mfadhaiko wa moyo kwa kumkosa kipenzi chao....

    "mama asha, haya tatizo ni nini"

    Mzee Rashidi alimuuliza mke wake sababu ya kuzimia siku ya jana usiku

    "mwenetu, jana kwa mara ya kwanza nimesikia sauti ya mwanangu"

    Aliongea mama surian huku mzee huyo akishangaa kwa maneno ya mke wake,..

    "mbona sikuelewi mke wangu"

    "suria,... Suria mtoto wetu yupo hai.. Nimemsikia jana kwa masikio yangu"

    Aliongea mama huyo huku mzee akisema

    "namba yake uliitoa wapi"

    "mume wangu, kuna ujinga tulikuwa tunafanya.. Lakini tunashukuru kwamba tumejua mapema"

    Aliongea mama huyo na wakati huo kapata nafuu vizuri kabisa....



    Huku ofisini surian ni wa kupiga simu, tena ile namba kaisevu kabisa kwa jina la LIKE MOTHER (kama mama) akiwa na maana ni kama mama, kwa ile sauti ambayo kaisikia ni kama ya mama yake, hivyo hakuweza kuisevu mama, bali kaisevu KAMA MAMA... Kila akipiga namba ile humjulisha haipatikani,.... Na laiti angelijua kuwa wanafanya kazi katika kampuni yake sijui ingelikuwaje,... Ndani ya ofisi yake akiwa kavua tai, yaani anatamani wiki ijayo ifike leo, mana leo ni Jumanne, sasa ni mpaka Jumapili ya wiki ijayo, sio hii inayokuja hapana... Sasa akifikiria ni mpaka wiki ijayo anaona ni mbali sana lakini kaipanga mwenyewe kana kwamba mpaka wiki hio atakuwa na asalio zuri la pesa yake, mana ikumbukwe kuwa hata maboss hujilipa wenyewe mishahara, unakuta boss anajilipa elfu 30 au hata 50 kwa siku, hivyo kapanga hio wiki kwa maana atakuwa ana fungu la jasho lake, mana kama mke kakataa na majasho yake haina haja ya kumbembeleza zaidi... Kwani masharti yake ni makubwa mno....



    Asha akiwa chooni, baada ya kufanya usafi, yeye hajifichi kwasababu ni umri sahihi ambao unahitajika katika kampuni hio,.... Alikuwa ana mawazo sana, namba ya boss sure ipo kichwani kwake,.... Akiwa anawaza sana kuhusu ile sauti kama ya mdogo wake kabisa,... Kiukweli ilimpa mawazo hata yeye,...

    "aahh mambo dada"

    "poa"

    Alikuwa ni tariki aliokua akiingia uwani kujisaidia,... Lakini kama unavyomjua tariki ni sharobaro anapenda kujipiga picha mara kwa mara,, sasa saa ngapi hajaanza kuji selfii kwenye sinki za kunawia.... Asha alimuona huyu mtoto ni mjinga kweli, mana anajipiga picha chooni

    "sasa ndio nini hivyo.... Hivi mnajua simu zitawaumbua hizo"

    Aliongea asha huku tatiki akicheka...

    "aahhh dada wewe ni mzuri na bado mdogo sana, nashangaa hujui mambo ya kidigitali zaidi"

    "digitali au ujinga"

    "aaahhh, hapa watanikoma wazee wa WhatsApp, natupia kama mbili Facebook, afu hii inafaa profile ya WhatsApp hiii"

    Alijiongelea tariki huku akicheka na simu yake,... Lakini asha kuna wazo lilimjia hapo hapo....

    "we mkaka, simu yako si ina WhatsApp"

    "ndio kwani vipi"

    "naomba nimuangalie mjomba angu kama yupo WhatsApp"

    Aliongea asha huku akijibalaguza mana alisha mtolea uvivu kwa kujipiga picha chooni...

    "we si umesema hazinifai hizi simu"

    "nisamee bure, naomba nimuangalie"

    "nyoooo, haya taja namba"

    Tariki alikubali kumsaidia ili asha amuone mjomba wake,...

    "ni 0714419487"

    "mmmhhh namba zenyewe kumbe tigo"

    "heeeee sasa hapa tanga kwani tunatumia mtandao gani zaidi kama sio tigo"

    Sasa tariki aliiweka ile namba kwenye simu yake, kisha akawa ana refresh ili itokee kwenye listi ya namba za wasapu asha aone picha ya mjomba wake, lakini sio kuwa ni mjomba wake, anataka kuhakikisha kama ipo WhatsApp, na je picha itakuwa ni nipi??... Kweli namba ilikuja na tariki aliisevu kwa herufi A hivyo ikawa ya kwanza kwenye listi ya namba zake za WhatsApp.... Lakini sasa kabla hajabonyeza ile picha ilioko kwenye profile ya hio namba, ghafla sadiki katokea hapo chooni....

    "riki? Saaa sita hii muda wa kazi unafanya nini huku"

    "apana boss, ni aisha kuna mtu alikuwa anataka kumbipu kasema hana simu"

    "ebu toka nenda kazini... Mwehu wewe"

    tariki aliondoka lakini asha hakuweza kuona ile picha,...



    "asha, sasa umefanya nini... Chukua simu yako, hata kama hunipendi lakini siwezi kukupokonya simu nilio kununulia"

    Aliongea sadiki huku akimpa simu, lakini asha aliikataa ile simu na kusema kuwa...

    "diki, hebu niache Kwanza, kwa sasa sipo vizuri kiakili kwani mama yangu anaumwa... Hivyo hebu niache Kwanza"

    Ameongea asha huku sadiki akisikitika sana,...

    "Shadya ameniambia hilo swala... Haya hali yake vipi na anaendeleaje"

    "kwa sasa ana nafuu kidogo"

    "nini tatizo kwani"

    "kichwa tuuu, na maumivu ya mwili, si unajua tena umri wake na hizi kazi sio sahihi"

    Aliongea asha na sasa hamjibu diki vibaya, mana kama kweli ile namba itakuwa ya ndugu yake, basi hana budi kumpenda diki, tena atampenda mpaka basi....

    "hebu ngoja mwezi huu uishe... Huo mwezi ujao nitajua cha kufanya"

    Aliongea sadiki huku akiondoka na kusema

    "lakini hebu tuliza kichwa chako,... Afu kuna deni kule hospitalini?? Manaaaaa.... Shika hii utakwenda kulipa kama anadaiwa matibabu na maradhi yote kwa ujumla"

    Sadiki alianza kujipendekeza kwa kutoa pesa, na asha nae hakutaka kuvunga kwani anatamani kupata mwanaume wa kumchuna zaidi afu sadiki alivyo na sifa alitoa bila kuhesabu kisha akampa kitu kama laki mbili au tatu hivi,... Sadiki aliondoka zake kwenda kiwandani kutembelea baadhi ya idara ambazo zinahitaji umaki wa hali ya juu katika uandaaji wa matirio,...



    Tukija huku ofisini kwa suria akiwa katulia zake hana kazi ya kufanya mana yeye ni kama anakuja tu ile kuambiwa boss yupo lakini hana kazi ya kufanya kwasababu wafanyakazi wapo wengi wa kuzifanya kazi hizo... Ghafla alimuona mke wake kaeti kwenye kiti, kana kwamba kaja sasa hivi tu...

    "pole kwa uchovu mume wangu"

    "ahsante mke wangu... Umekuja na chakula, mana nahisi njaa"

    "nimekuja twende lanchi"

    "aahhh sasa kwanini usije na chakula chako ulichopika wewe"

    Aliongea surian, na hapo mke kaja kimazingala sio kwamba kaja kwa miguu...

    "natamani kukupikia mume wangu, ila kingepoa bwanaaa"

    "kwaio"

    "twende hotelini tukale"

    "mmmhhh haya twende"

    "lakini hatuendi na gari"

    "heeeeee sasa tunakwendaje"

    "kwa mguu"

    "mungu wangu eeeee... Hayo ni masharti au tumeamua"

    Suria aliuliza kuwa hayo ni masharti au wameamua mana maimuna kwa masharti ndio mwenyewe...

    "hapana mume wangu, sasa hivi hakuna masharti yeyote amua utakaloweza"

    Aliongea maimati au maimuna huku wakichukuana, surian yeye hawezi kuwa invisible (kuto onekana) hivyo surian alionekana kutoka mwenyewe lakini yupo na mke wake wanakwenda kula hoteli kwa kutembelea kwa miguu,... Wakiwa wote muna katumbukiza mkono wake kwenye mkono wa surian, lakini mke haonekani ila yupo nae....

    "bwana mbona watu wananipamia bwana"

    Aliongea muna huku surian akicheka

    "nani kakwambia uwe invisible, na utakanyagwa mpaka ukome"

    "twende tukachukue gari bwana, mijitu kama haioni"

    "sasa wao wana makosa gani, mana wao wananiona mimi tu"

    "waambie bwana"

    "acha ukichaaaa"

    Sasa watu wakawa wanamshangaa surian akiwa anaongea, mana hakuwa akiongea na simu wala nini,.



    Walifika mahali husika mjini kati wakiwa wanapata chakula cha mchana, surian kakaa kwenye kiti, na kwa pembeni yake kuna kiti ambacho kakalia mke wa surian, lakini kiti hakionekani kukaliwa, yaani kipo kama hakina mtu lakini kina mtu... Basi walianza kula, tena huku wanacheka sana, ila sasa watu wanaona surian anacheka mwenyewe bila kuchekeshwa, mana watu wanamuona surian pekee,...



    Huku kiwandani tariki akiwa na simu yake aliweza kuona picha iliowekwa pale kwenye profile picha, ambayo ni picha ya surian lakini tariki yeye hamjui surian na wala hajui kama ndio boss wake, na mbaya zaidi hio ndio sura aliotumwa na faima, ila sasa hajui kama ni hio mana boss wake hamjui ana sura gani, na asha kamwambia ni mjomba wake,... Riki alifunga simu yake na kuendelea na kazi kwani hamjui mtu anaye mwangalia,... Sasa tariki akaona ngoja aombe namba za meneja sadiki mana ndio boss anaemjua, ili amuangalie picha kwenye WhatsApp faima amuone asije kukosa penzi juu yake... Tariki aliweza kuipata namba ya sadiki,..... Nyakati za jioni wafanyakazi wakiwa wanajiandaa kutoka, yeye riki alisha toka kana kwamba hakutaka kusubiri bus la wafanyakazi,.. Na yote hio awahishe kile alicho kitumwa na faima,... Lakini sasa alipofika mjini kati, alishangaa kumuona mjomba wake asha,...

    "heeeeee huyu si ndio yule kwenye picha"

    Tariki alijisemea kimoyo moyo huku akimsogelea surian...

    "kweli ni yeye mbona"

    Alijisemea tena huku akifungua ile picha na kuiangalia kwa mara nyingine tena, na kuhakikisha ni yeye mjomba wake,... Tariki alikimbia mbio mpaka kazini na kumkuta asha ndio anapanda basi kwenda nyumbani

    "asha asha.... Mjomba ako nimemuona kule mjini, twende ukamuone"

    Aliongea tariki na kumfanya asha atetemeke, mana sio mjomba wake kama alivyo mwambia tariki, bali ni mdogo wake kabisa....

    "unasemaje tariki"

    "twende sasa unapoteza muda"

    "tariki unasema kweli"

    "bwana wewe, twendeeeeeee"

    Asha alijikuta analia kabla hata ya kumuona mdogo wake wa damu aliosingiziwa kumuua,... Na lazima awe yeye kwasababu tariki asingelimjua kama sio ile namba alio mpa,....

    "sasa unalia nini asha... Twende ukamuone mjomba wako"

    Sasa asha akiwa anazidi kulia kwa furaha huku wafanyakazi wakimwangalia,.. Ghafla geti dogo linasukumwa, kana kwamba kuna mtu au watu wanaingia.... Wafanyakazi hawaamini kwa kile wanachokiona, hata asha mwenyewe haamini macho yake.......









    Wakati huo tariki akiwa anaingia ndani ya geti kuja kumpa taarifa asha kuwa kamuona mjomba wake ambaye alimpa namba ili amuone kupitia WhatsApp, lakini asha hakupata nafasi ya kumwona, hivyo riki alimuona kwenye picha na pia akamuona live bila chenga,...



    "unajua nini mke wangu"

    Aliongea surian huku wakiwa wanatoka kula lakini mke haonekani kama kawaida yake,...

    "sema"

    "sasa hivi pale getini patakuwa na watu wengi,... Nataka nisionekane nikiwa naingia"

    Aliongea surian mana anajua huo ni muda wa wafanyakazi kutoka kwenda majumbani, hivyo macho yatakuwa mengi sana kwake,

    "kwani unamwogopa nani babaa"

    "wewe mbona huonekani, kwani unamwogopa nani"

    Surian alimuuliza mkewe,... Ndipo mke akamshika surian sikio, hivyo wote wakawa hawaonekani, ila wao wanaona...

    "sasa kwakua wewe hawakuoni, nataka nawe usiwaone"

    "aaahhh sasa si nitajikwaa"

    "hapana, nami nataka usiwaone"

    Aliongea maimuna akimtaka surian afunge macho kwani kama haonwi basi naye asiwaone,... Sasa wakawa wanafanya kama mchezo wa mke na mume kufumbana macho yao kwa kutumjia mikono yao, hivyo walikuwa wakipeana zamu,... Ukimzima mwenzio macho basi hakikisha unamwongoza njia ilio sahihi asipaamie mtu.... Sasa walipofika getini wakiwa na mchezo huo huo, ikafika zamu ya surian kufumbwa macho,.. Na wakati huo hawaonekani wote,... Sasa wafanyakazi huku ndani walishangaa geti ndogo imefunguliwa kisha akafungwa, sasa wafanyakazi wakawa wanashangaa mbona geti imejifungua na kujifunga, na hakuna mtu alie ingia.... Hayo ni mawazo yao wao, lakini kumbe ni surian na mke wake ndio wameingia, na kwakua hawaonekani, wafanyakazi walistaajab mana hakuna alie ingia lakini wapo walio ingia ndani ya kampuni,... Surian na mkewe waliingia mpaka ofisini huku wakifanyiana baadhi ya utani wa hapa na pale,...



    Huki nje watu wakasahau swala la geti kujifungua na kujifunga....

    "twende ukamuone mjomba wako"

    Aliongea riki lakini asha hakutaka kwasababu juzi juzi aliitiwa kwenda kumuona surian kule TANGA BITES, lakini akapotea ghafla na kuto muona, hivyo anaona hata akienda huko hawezi kumuoa,... Na kama sio surian kushikwa sikio na maimuna, basi asha angemuona kwasababu alikuwa pale pale mlangoni, na kama sio mchezo wao wa kufumbana macho, basi surian angemuona dada yake,.... Asha hakutamani kwenda huko mjini kati kwenda kumwona ndugu yake,.. Mana hatomuona zaidi ya kuumia moyo wake,... Tariki aliondoka zake huku akiwa na hasira mana kachelewa kwenda kwa faima kisa kumwita asha akamwone mjomba wake,... Kampotezea muda mwingi sana...





    Huku ofisini mke na mume wanakusanya vitu vyao ili waondoke, lakini surian kwake mda bado kabisa

    "mi naona tangulia tu, nikute chakula kitamu"

    "afu mume wangu skuizi una kademu wewe"

    Aliongea maimuna huku surian akitabasamu

    "si bora ningelikuwa nako ningefurahi kwelikweli"

    "Jamaaaaani suri, ina maana ukipata kademu unaniacha"

    "weeeeeee, nikuache wewe, nani kasema"

    "mbona sasa unanitisha jamani... Yaani ndoa za utotoni zina tabu.. Bira tungelikuwa na umri mkubwaaa"

    Aliongea mke wa suria ambaye ni jini, lakini ndani ya ndoa na mume wake haruhusiwi kutumia asili ya jini, mana huyo mume wake ni binadamu wa kawaida,...



    Muda ulipofika surian na mkewe waliondoka ikiwa ni pamoja keshaondoka, yaani surian ni mfanyakazi wa mwisho kutoka, kana kwamba kesha zoea kuto onekana mapema hivi, yeye na ndani... ndani na yeye



    Asha akiwa nyumbani kwao akiandaa mambo ya usiku, mama haamini kama simu yake imeingia maji,... Lakini kila akiikumbuka ile sauti anajiskia raha lakini pia maumivu juu yake, kwani kaongea na mtoto wake na asijue alipo,.. Kwa sasa wote hawana simu, ni baba peke yake...

    "hebu nipeni hio namba nimpigie huyo mtu"

    Aliongea mzee Rashidi, mana kuumwa kwa mkewe kumetokana na sauti ya surian

    "hapana baba asha, acha kwanza akili yangu itulie, kama yupo yupo tu"

    Aliongea asha huku akipika chakula, na yeye anajua leo alikuwa amuone ndugu yake,... Sasa hisia za mapenzi hakuna kwani ana tetesi juu ya ndugu yake kuwa mmiliki wa ile kampuni



    Baada ya siku kadhaa kupita ikiwa ni siku ya jumatatu ya wiki nyingine, kazi ilikuwa ikilindima kama kawaida oda zilimiminika na kufanya wafanyakazi waongezwe mara dufu, kwani kazi Iliweza kwenda vizuri,...



    Siku hio ilikuwa ni mwisho wa wiki ya mwezi huo hivyo yupo kiongozi wa kike aliopewa kazi ya kuandika wafanyakazi ambao hawajafika, kwani kesho ni siku ya kupokea mishahara,... Na siku hio mama suria yupo kazini kama kawaida yake



    Tukirudi huku kwa faima tunamwona akiwa na dada yake

    "hivi dada? wewe ndio unampa nguvu tariki"

    Faima alimuuliza dada yake zamina, mana zamina Alianza tabia ya kumkuadia mdogo wake,....

    "kwani tariki ana ubaya gani, kijana wa watu ana hela, ina maana bado unampenda huyo mzimu wako"

    Aliongea zamina akimaanisha kuwa faima anampenda mtu aliofariki dunia,

    "skia dada, surian yupo hai na yupo mjini"

    "nani kakwambia kama surian yupo mjini, tayari kesha oza hata mfupa wake kuukuta ni bahati sana"

    "hata kama, lakini ipo siku surian nitamuona tu"

    "labda kwenye ndoto lakini sio kwa macho yako... Mkubalie tariki faima jamani"

    Aliongea zamina, kwani anamjua tariki ana hela kumbe nae ni choka mbaya,

    "kwanza hata sijamuona huyo tariki mwenyewe, kama siku nne hivi sijamuona"

    "sasa wewe si humtaki, kila akija mtoto wa watu unamkatisha tamaa, Angalia na uzuri wako Fey unapotea bure"

    "bwana weeee, nina mchumba wangu, hao wanaume wako utajua nao mwenyewe"

    "shauri yako... Kesho namwambia aje mara ya mwisho, na unapoteza mume hivyo"

    "yule sharobaro yule"

    "ana hela yule acha ujinga fey"

    "sitaki bwana, kwani si hata wewe ni mwanamke"

    "fey, unanitukana ivyo ujue"

    Zamina alishikwa na hasira kwa maneno ya mdogo wake kumwambia kuwa hata yeye ni mwanamke hivyo Anaweza kumkubalia vilevile...

    "dada, hebu nenda nyumbani, ukumbuke hapa ni dukani kwa watu"

    "sawa,... Ila ngoja tu"

    Zamina alikasirika sana, na hata fey kachoka kutongozeshwa kwa wanaume, mana dada yake ni mtu wa kudanga tu na wanaume hivyo anataka na mdogo wake awe kama yeye, na fey hapo alipo mzimaaaaaa ana bikra yake, na hio alimtunzia surian, lakini mpaka leo suria haonekani....



    Sasa tukija huku MICCO yule dada kiongozi alikuwa akipeleka zile documents ambazo kaambiwa aziandae kwa niaba ya kuwalipa wafanyakazi mishahara yao, hivyo amletee takwimu ya wafanyakazi wapo wangapo, kwa maana kuna walio ingia na walio toka kwa kuacha kazi, na idadi hio anaijua dada msimamizi mkuu wa idara zote,.. Sasa akiwa anatoka na documents hizo, haja ilimbana kana kwamba asingeweza kufika ofisini kwa boss kwasababu ana tumbo la kuendesha... Sasa kila akiangalia mtu ampe apeleke haoni,... Mara kamuona mama usafi ambaye ni mama yake surian,...

    "we mama hebu peleka hizi documents kwa boss"

    Aliongea dada huyo kisha akawa anaingia chooni haraka haraka

    "jamani mwanangu, kule siruhusiwi kufika"

    Mama surian alilalamika kuwa kule haruhusiwi kufika kwani hata kazi yenyewe kapewa kiujanja ujanja, leo aende mpaka ofisini kwa boss na umri huo ambao hautakiwi kwenye kampuni ya MICCO,..

    "we mama vipi, kama hutaki kazi useme, peleka haraka basi"

    Dada Aliongea kwa hasira mno kwani ana cheo kikubwa katika idara za ndani, hivyo ana sauti kwa baadhi ya wafanyakazi... Sasa mama kaona kuliko aharibu kibarua chake bora apeleke tu kama ni kukosa kazi basi



    Pale mapokezi shadya hayupo kaelekea kujisaidia katika vyoo vyao vya ofisini,.... Mama surian kaambiwa apeleke kwa boss, afu boss mwenyewe ni suria ambaye ni mtoto wake wa Kumzaa,.. Lakini hawajuani mpaka leo kuwa wanafanya kazi kampuni moja,... Sasa mama kafika mapokezi shadya hayupo, mana ndio alitegemea ampe shadya apeleke mana ndio kazi yake akiwa kama sekretari,... Sasa mama kila akitaka kiweka hapo mezani kwa shadya, nafsi inamsuta kwanini asipeleke mwenyewe, lakini kila akifikiria kibarua chake kimepatikana kwa njia ya ujanja ujanja, mana mwisho wa umri ni 35 sasa yeye ana miaka 58,..mbona atatukanwa na mtoto mdogo, na mbaya zaidi anaweza kumharibia shadya kibarua chake mana yeye ndio kafanya ile hali ya vyeti feki,.. Mama suria aliamua kupeleka, kama ni kufa kwa kibarua wacha kife kuliko kutopeleka documents za watu,... Sasa kwa mara ya kwanza mama anakwenda kukutana na mtoto wake wa kumzaaa,.. Mama hajui kama anafanya kazi kwenye kampuni ya mtoto wake, na hata mtoto hajui kama mama yake anafanya kazi hapo, na wote wamemisiana mpaka raha,... Surian akiwa ofisini kwake ghafla mlango unagongwa....

    "ngo, ngo, ngo, ngo, ngo"

    Ilisikika sauti kugongwa kwa mlango, na surian naye akajibu kwa kumkaribisha aliegonga mlango

    "karibu, ingia ndani"







    Mama surian alikuwa na uoga juu ya kukutana na boss uso kwa uso, kwani kanuni na taratibu za kampuni hiyo, hairuhusu mfanyakazi kuanzia miaka 36, yaani miaka 35 ndio mwisho wa mwajiriwa kuomba kazi, kwani sheria ya kampuni hio ni kuanzia miaka 18 mpaka 35 mwisho, hivyo ukiwa na umri zaidi ya miaka 35 basi kazi hutopata,.... Sasa mama surian ana miaka 58 na boss hajui kama kwenye kampuni yake kuna mfanyakazi mwenye umri mkubwa,



    Sasa mama surian akiwa hapo mapokezi anajishauri namna ya kuingia ndani ili kuweza kufikisha Documents hizo ambazo amepewa na kiongozi wa idarani apeleke kwa boss baada ya kiongozi husika kupata haja ya ghafla na kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo,...



    Mama surian alifikiria mno na kupata jibu, kwa namna nyingine....

    "ile namba, nilisikia ni sauti ya mtoto wangu, na ni namba ya boss huyu huyu, sasa hapa ndio nafasi yangu ya kwenda kumuona"

    Alijiongelea mama huyo huku akishika mafaili hayo na kuusogelea malango wa kuingilia ofisini kwa boss surian...



    Sasa ile anataka kugonga tu, mara shadya katokea...

    "heee heee heee we mama wewe, hivi umedhamiria kuingia huko ndani"

    Aliuliza shadya huku mama alijisikia kufanya kosa kubwa japo sio kosa lake,..

    "samahani mwanangu, ni kweli nimepewa hizi karatasi nilete huku kwa boss, sasa nimekuja sijakukuta, je ningefanyeje mimi jamani mwanangu"

    Aliongea mama huyo tena huku akilengwa na machozi kana kwamba alitamani hata kulia

    "yaani ungeingia,.. Sisi wote tusingelikua na kazi, mana mimi ndio nimefanya majambozi ukaingia, leo ikijulikana mimi nitakuwa sina kazi mama... Haya lete nikusaidie, wewe kaendelee na kazi"

    Aliongea shadya ama Cecilia kuwa mama huyo akaendelee na kazi tu,.. Lakini mama ilimuuma sana kwani kakosa nafasi ya kwenda kumuona huyo boss, mana unaambiwa hajawahi kuonekana toka kampuni kufunguliwa, zaidi ya juzi alipotoka na hakutembea sana akarudi ofisini kwake,..



    Sasa huku ndani ofisini kwa surian akiwa katulia hakuwa na kazi ni kama alikuwa akizisubiri tu hizo faili ambazo zilitakiwa kuletwa toka idarani,....



    ghafla mlango unagongwa....

    "ngo, ngo, ngo, ngo, ngo"

    Ilisikika sauti kugongwa kwa mlango, na surian naye akajibu kwa kumkaribisha aliegonga mlango

    "karibu, ingia ndani"



    Huku nje mama akawa anajivuta kuondoka ili asije kuonwa na boss,.. Lakini sasa ile anajivuta kuondoka, ghafla alishtuka kana kwamba kuna kitu kaona,.. Mapigo yake ya moyo alimwenda mbio ghafla tu huku akiwa kama haamini au ana hisia fulani hivi,... Mama surian aliondoka lakini kichwa chale bado kilikuwa na mawazo ya ghafla,... Alirudi kazini kwake na kuendelea na kazi, lakini kila wakati anarudisha picha ya kile alicho kiona..



    Sasa kumbe wakati ule shadya anaingia ofisini kumbe mama aliona kichwa cha boss kupitia ule mwanya wa mlango, pale pembeni kabisa kwenye vile vishikizo vya mlango,.. Mama surian aliona kisogo cha boss na kukifananisha na kisogo cha mtoto wake, hivyo ndicho kinacho muumiza kichwa, na kila akilinganisha matukio yote, ni kama anamuona surian, ila hana uhakika na hilo,....

    "yaani kichwa kama cha mtoto wangu"

    Alijisemea mma surian bila kujua kumbe kweli ni mtoto wake,... Lakini hajui na mtoto pia hajui kama mama yake yupo hapo kwani vyeti alivyotumia mama, vina mkanganyiko wa habari zake,... Wakati huo huo asha alikuja kwa mama yake kumjulia hali mana hakawii kupata mshtuko,.. Asha alimkuta mama yake akiwa katika dimbwi la mawazo mengi akikiwaza kisogo cha boss,...

    "mama mbona una mawazo hivyo"

    Aliongea asha huku mama akishtuka na kuendelea kufanya usafi

    "asha umefuta nini huku... Ukionwa na viongozi wako itakuwa tabu"

    Aliongea mama asha akiwa anapenda sana mtoto wake asichezee kazi kwani hawana wanacho kitegemea zaidi ya kazi hio,

    "mama nimekuja msalani tuu"

    "haya ingia basi kisha urudi ndani"

    "sawa, ila una mawazo sana mama angu"

    "asha?? Ni kweli kama ulivyo hisi... Unajua nilipeleka makaratasi yaliotoka huko ndani kwenu, nilipeka ofisini, lakini katika hali ya mlango kufunguliwa niliweza kuona kidogo cha boss... Asha?? kile kisogo ni kama cha kaka yako surian, yaani vile vile"

    Aliongea mama surian huku asha nae akiendelea kuchanganya matukio

    "sasa mama, ina maana kaka surian ndio mwenye hii kampuni? Mana ile namba ni sauti yake... Kichwa umesema ni chakwake... Atakuwa yeye mama"

    Aliongea asha huku mama akikataa..

    "hapana asha,.. Surian hawezi kuwa na utajiri huu ashindwe kuja nyumbani... Hebu ingia msalani uende kazini"

    "sawa, lakini mama... Nina wasiwasi na hilo mama"

    "asha, we humjui surian upendo wake kwetu?.. Leo awe na hali hii atuangalie kweli?? Hapana, mimi nina imani sio surian wangu"

    Aliongea mama huku asha akiingia ndani kujisaidia... Kwa sasa maisha yao sio magumu sana kwani wanafanya kazi, hivyo mahitaji kwao ni kama kawaida...



    Kesho yake ikiwa ni siku ya wafanyakazi kupewa mishahara yao, hivyo siku hio boss hua hakai kwani hakuwi na kazi kutokana na msongamano wa kila mmoja aingie ofisini kusaini mshahara wake,.. Hivyo mpaka wafanyakazi 500 waishe ni siku nzima itaishia hapo, hivyo siku ya leo bosa kaleta mishahara ya wafanyakazi wake kisha akaondoka, hivyo meneja akishirikiana na shadya wakiwa wanatoa mishahara kwa wenzao...



    "Leo nataka tutembee mjini unionyeshe mji wenu"

    Ilikuwa ni sauti ya jini maimati akimtaka mumewe amtembeze katika mji huo,

    "ila sitembei kwa mguu"

    Suria alijibu kuwa hatembei kwa miguu mana mkewe anapenda kutembea kwa miguu,..

    "sawa, mana hupendi kutembea kwa miguu"

    "sipendi kwasababu gari ipo, yanini tuumie"

    "sawa babaa..."

    Ikiwa ni majira ya saa sita za mchana



    Huku kwa faima akimalizia kuhudumia wateja wake... Tariki alionekana kuwepo nje ya duka hilo, na siku hio alikuwa na furaha sana kwani katoka kupokea mshahara muda sio mrefu, hivyo hapo alipo ana furaha ya hali ya juu na kila siku yeye humdanganya faima kuwa ana pesa, kumbe hakuwa na lolote juu ya hilo



    Baada ya faima kumaliza huduma kwa wateja, alitoka nje ili kwenda kupata lanchi kwani ilikuwa ni mchana wa saa sita,

    "umefuata nini hata riki"

    Faima alimuuliza riki kuwa alifuata nini hapo kazini kwake,...

    "faima? Mbona umebadilika ghafla? Wakati ulikuwa unaelekea vizuri"

    "haijalishi... Enhee nilikupa mtihani wangu na kukwambia ukiuweza basi naweza kukufikiria juu ya hilo"

    Aliongea faima kuwa kuna mtihani alimpa lakini bado hajautimiza, na mtihani alio mpa ni riki alete picha ya boss wake,....

    "skia faima... Kama wewe ni wangu basi ni wangu tu,... Namba ya boss wangu ninayo hapa wasap, japo sijui unataka ya nini... Kama ni pesa hata mimi ninazo, hivyo sioni haja ya kutaka namba au picha ya boss wangu... Mi najua hukutaka picha, najua ulitaka namba. Sasa simu yangu hii hapa... Chukua namba zake"

    Riki aliongea mengi huku akiwa hana amani kwani anajua faima anapenda wanaume wenye pesa, kumbe faima kasikia kuwa boss wa kampuni hio ni surian, hivyo ndio mana akamtuma riki alete picha ya boss wake....

    "riki unanikosea heshima... We huoni kuwa tunafanya biashara za nguo za dini, na hio kampuni inahusika na mavazi hayo"

    Aliongea faima huku akiwa kashika simu ya riki ambayo ina namba za meneja sadiki,...

    "basi yaishe... Tafuta hapo nimeandika boss sadiki"

    Aliongea riki kisha faima akafungua WhatsApp, na kuanza kukagua

    "mbona namba zako nyingi huku WhatsApp unasevu herufi tu"

    Aliongea faima baada ya kukuta herufi tu katika listi ya WhatsApp,..

    "umesema umesevu nani"

    "boss Sadiki... Angalia alfabeti za mwanzo baada ya Alfabeti A"

    Aliongea riki huku faima akianza mwanzo,... Lakini sasa akiwa anashuka chini,.. Ama kweli unambiwa chako ni chako tu,.. Faima alijikuta anabonyeza herufi A ambayo ndio namba ya surian,.. Lakini hapo hajajua kama ni surian,..

    "sio hio,... Huyu ni mjomba wake asha huyu"

    Aliongea kuwa huyo ni mjomba wake asha...

    "asha yupi huyo... Mtumeeeee.... Surian wangu jamani Uuuuuuuuuwiiiiiiii"

    Aliongea faima baada ya kifungua ile picha,... Sasa riki akashangaa

    "wewe huyu ni mjomba wake aisha, na hata juzi nilimuona mjini"

    Riki aliongea hayo lakini faima hakumsikiliza, kwani alikuwa akilia kwa furaha ya hali ya juu...

    "sasa unalia nini"

    Aliuliza riki huku faima akiichukua ile namba, mana picha tu ilitosha..

    "riki, ahsante sana... Huyu ndio mchumba wangu, na ndio inasemekana anamiliki hio kampuni... Na huyu ndio surian wangu huyu"

    Aliongea faima huku riki akibaki mdomo wazi kwani haamini kuwa kamletea faima mchumba wake...

    "ina maana, mbona sikuelewi faima"

    "huyu sio mjomba wake aisha, huyu ni mdogo wake kabisa... Shika simu yako, afu mazoea sitaki"

    Aliongea faima kisha akaingia zake dukani kuhudumia wateja... Riki haamini macho yake kwa alicho kifanya,... Sasa riki akaona ngoja arudi kule kampuni akapate uhakika kwa asha....

    Wakati huo riki anaondoka kwa hasira, faima alikuwa anahudumia huku machozi ya furaha yakimtoka...



    Tukija huku kampuni ambako baadhi ya wafanyakazi wanamalizia malizia kupewa mishahara yao,.. Watoa mishahara ni wawili, shadya anatoa mshahara, na Sadiki anasainisha... Kwahio mfanyakazi unapitia kwa saidiki unasaini kisha unakwenda kwa shadya kuchukua kibunda.... Sasa sadiki alilishangaa jina moja hapo kwenye listi....

    "ZUWENA RASHIDI SURIA analipwa laki nne"

    Alijisemea sadiki huku akimuangalia huyo mama.....

    "we mama si unafanya usafi wa vyoo"

    "ndio baba"

    Mama surian alijibu kwa huruma kana kwamba sadiki hajui kuwa kuna mgeuzano wa vitengo na mishahara yake...

    "shadya??"

    "abee boss"

    "huyu mama si anafanya usafi kule public toilets"

    "ye.. Ye.. Ye. yesi boss"

    "sasa inakuwaje analipwa laki nne, mshahara wa msimamizi wa idarani kabisa"

    Aliongea meneja huku shadya akitetemeka,... Mana meneja yuko juu na shadya ni sekretari tu..

    "labda boss ndio kampangia mwenyewe, mana mishahara yote kapanga boss mwenyewe"

    Aliongea shadya kana kwamba, Meneja hajaju kwanini mama mwenye umei huo anafanya kazi hapo,... Na hakuhoji ishu ya umri mana anaju kuwa hata boss anajua kuwa kuna mfanyakazi mwenye umri mkubwa....

    "hapana... Sidhani kama boss anaweza kulipa mfanyakazi wa usafi mshahara wote huu"

    Aliongea meneja huyo huku akiwa kama anakazia,.. Na anajua kabisa huyu ni mama yake asha hivyo anataka kufanya fitina kwasababu asha kamkataa kimahusiano....

    "lakini boss ndio kaamua kumlipa hivyo,... Hivyo mi naona tumpe tu boss"

    Shadya aliongea kumtetea mama surian, lakini sadiki akagoma huku akitoa simu na kusema..

    "hapana... Wacha nimpigie,.. Huu uchumi umebana sana hatuwezi kulipa mfanya usafi wa vyoo mshahara wote huu.... Ngoja nimpigie huu mshahara tuupange upya"

    Aliongea sadiki huku akilitafuta jina la boss surian.... Wakati huo mama surian analengwa lengwa na machozi kwasababu hana la kusema juu ya hilo, mana hakuingia kwa vyeti vyake, na mbaya zaidi umri wake ndio tatizo la kazi yake... Shadya haamini macho yake kwa kile sadiki anacho kwenda kukifanya...

    "boss sadiki, tumlipe tu mwezi huu kisha mwezi ujao tutampunguzia"

    "hapana... Afu wewe inaonekana unalijua hili swala... Ngoja boss apokee simu"







    Kiukweli familia hii imekumbwa na mitihani ya hapa na pale hususan katika upande wa kuyamudu maisha kwa kupata riziki,.. Mama surian aliokuja kuomba kazi katika kampuni ya mtoto wake ingali hajui kama mtoto wake surian ndie mmiliki wa kampuni hio,... Vigezo vya mama huyo viligonga mwamba kupata kazi katika kampuni hio, lakini alitokea dada mmoja alieweza kumsaidia kwa kumtengenezea vyeti feki ili mama huyo apate kazi katika kampuni hio,.... Jambo hilo liliwezekana na mama surian alipata kazi katika kampuni ya MICCO ambayo mmiliki wake ni mtoto wake wa kumzaa lakini hajui kama ni kampuni ya mtoto wake,...



    Swala hilo la vyeti feki alilijua shadya pekee, hivyo hakuna alieweza kujua ufeki wa vyeti hivyo,... Sadiki alimtaka asha kimapenzi lakini asha alikataa na kumtolea nje meneja huyo, hivyo meneja alipokutana na utofauti wa mshahara na kazi ya mama huyu,.. Kutokana na meneja huyo kukataliwa na asha, sasa akaamua kufufua jipu kwa mama huyo,...



    "boss sadiki, tumlipe tu mwezi huu kisha mwezi ujao tutampunguzia"

    "hapana... Afu wewe inaonekana unalijua hili swala... Ngoja boss apokee simu"



    Aliongea sadiki na wakati huo simu ya boss inaita, na sadiki anasubiri simu ipokelewe,...

    "eeh hallo boss"

    Aliongea sadiki baada ya boss kupokea simu,.. Mama surian alikuwa akitetemeka kwa woga kwani huenda asilipwe mshahara wake,..

    "ndio sadiki kuna shida gani"

    Aliuliza boss huyo kisha sadiki akaongea

    "kuna mfanyakazi mmoja hapa ananipa mashaka boss,... Anafanya usafi wa vyoo na analipwa laki nne na nusu boss"

    Aliongea sadiki huku boss akishangaa

    "hapana, mfanya usafi w chooni analiwa kitu kama laki mbili hivi na nusu,.. Sasa huyo vipi analipwa hivyo"

    "Kiukweli hata sielewi, na ndio mana nikakupa taarifa"

    "anaitwa nani huyu mfanyakazi"

    "aahhh anaitwa ZUWENA RASHIDI SURIA"

    Aliongea sadiki lakini surian akamjibu

    "ni kweli huyo mfanyakazi nilimpangia mshahara huo, lakini kitengo chake sio mfanya usafi bwana sadiki,.. Labda umechanganya tu, angalia vizuri"

    Aliongea boss surian huku sadiki akiwa hakati tamaa katika maongezi

    "sawa, lakini jina la huyu mama, lipo kwenye sekta ya usafi wa vyoo..."

    "mbona unasema jina la huyu mama ina maana ni mwanamke mtu mzima"

    Aliuliza surian huku sadiki akijibu

    "ndio, ni mama mtu mzima... Ina maana boss umeajiri mfanyakazi humjui boss"

    Aliongea sadiki kama kuchomekea fulani hivi ili tu mama huyo akose kazi,.. Na wakati huo mama surian analia lakini sadiki hata hana wazo la huruma kikubwa alipize kisasi cha kukataliwa na asha... Wakati huo asha yupo nje akisubiri foleni yake naye aje achukue mshahara wake,

    "namjua ila hakuwa mama mtu mzima"

    "hapana boss ni mama mtu mzima kabisa hakosi miaka 60 huyu"

    "what???, miaka 60?"

    "ndio boss"

    "amekujaje na kapateje kazi hapo kiwandani na nani kampa kazi"

    "boss, mi nadhani hili swala shadya analifahamu vyema mana ndio anawekea mkazo alipwe mshahara wake"

    "hebu mpe simu huyo shadya"

    Surian alikasirika mno kwa kuskia kuwa yupo mfanyakazi ambaye hajakizi vigezo vya kupata kazi,..

    "halo boss"

    "shadya, hivi huyu mfanyakazi kapataje kazi hapo"

    Aliongea surian tena kwa hasira kidogo

    "samahani boss, naomba nipate adhabu juu ya hili"

    "hebu mpe simu huyo sadiki"

    Shadya alimpa sadiki simu ili aongee na boss

    "Hallow boss"

    "sadiki"

    "naam boss"

    "mpe huyo mfanyakazi mshahara wake ila asirudi kazini tena... Sitaki kumuona mana nitachefukwa na kupiga mtu risasi,.. Sawa"

    "sawa boss"

    "mpe shadya simu"

    Surian alipata hasira kali kwa mfanyakazi huyo kuajiriwa katika kampuni yake,.. Surian bila kujua anamfukuza mama yake mzazi,

    "shadya?"

    "abee boss"

    "utawajibika kwa hilo, mishahara yote aliochukua huyo mfanyakazi utakatwa mpaka uishie... Na utaanza kukatwa mwezi huu"

    "sawa boss, ila usinifukuze kazi boss"

    "sitaki hili swala nilisikie tena... Shenzi taipu"

    Aliongea surian kisha akakata simu kwa hasira,



    "umeona sasa, unafanya vitu vyako vya ajabu ajabu tu... Haya jipigie mahesabu huyu mama kachukua mishahara mingapi"

    Aliongea sadiki lakini hizo ni kusudi zake kisa kakataliwa,...

    "lakini boss, ulichokifanya sio kizuri... Niliamua kumsaidia huyu mama aweze kuiisha familia yake,... Sawa nitailipa hio pesa"

    Aliongea shadya tena kwa huruma huku akijuta kumsaidia mama huyo kwani ni miezi mitatu kama sio minne toka kampuni hio ianzishwe, hivyo ni mishahara takribani mitatu kama sio minne atakayo takiwa kuilipa shadya ili iwe onyo kwa wafanyakazi wengine.....

    "mama, unapewa mshahara wako wote wa mwezi huu, lakini hutakiwi kuonekana tena hapa... Sawa mama"

    "sawa baba"

    "njoo usaini uchukue mshahara wako"

    Aliongea sadiki huku mama akikubali kusaini ili achukue mshahara wake wa mwisho baada ya kubainika kuwa ni mfanyakazi hewa katika kampuni hio



    Huku nje riki kafika na kakutana na asha pale kwenye foleni ta kwenda kupokea mshahara...

    "hivi wewe, kwanini unidanganye kuwa yule ni mjomba wako kumbe ni kaka yako"

    Aliongea riki, mana hasira zake ni kwamba kapewa namba akijua ni mjomba wa asha kumbe ni kaka yake na ni mchumba wa demu anaye mfukuzia, sasa anamlaumu asha kwa kuweka namba yake humo mpaka ikaenda kujulikana....

    "wewe nani kakwambia ni kaka yangu"

    aliuliza asha huku watu wakiwashangaa

    "si nimekwenda kwa mpenzi wangu, akasema eti ni mchumba wake"

    "aaahh bwana we niache nikachukue kibunda changu"

    "mi nakulaumu kwanini uniletee linamba namba lako bwana... Umenifukuzia ndege wangu bwana... Nunueni simu sio kudandia simu za watu.. Si umwambie kaka yako boss akununulie simu"

    Aliongea riki huku akiondoka,.. Lakini ghafla asha anamuona mama yake anakuja kwa huzuni sana...

    "mama? Una nini"

    Alimuuliza mama yake kuwa kapatwa na nini

    "mwanangu, nimejulikana kuwa nimeingia kazini kwa vyeti hewa, kwani umri wangu haukustahili kufanya kazi hapa"

    "jamani mama.... Boss hayupo sasa nani kajua hilo"

    "meneja sadiki, ndio kampigia boss simu akaambiwa kuna mfanyakazi ana miaka 60"

    "mama?? Sadiki huyu huyu anaye nitongoza au sadiki yupi mama"

    "huyo huyo mwanangu... Wala sio mwanaume wa kukuoa mama... Bora hata ulivyo mkataa... Wacha nirudi nyumbani, ila asha mwanangu, fanya kazi kwa bidii... Mimi sipo kazini tena kuanzia leo"

    Aliongea mama huyo huku asha naye akiangua kilio kwani haamini kiwa sadiki leo kamfukuzisha mama yake kazi,... Laiti wangelijua kuwa huyo ndio mama wa boss wao, sijui ingelikuwaje... Lakini wakati asha kamkumbatia mama yake kama kumfariji, ghafla alikumbuka maneno ya riki kuwa

    "Si umwambie kaka yako boss akununulie simu"

    Asha alizidi kupata mashaka juu ya hilo, mana riki kaambiwa na faima kuwa alisikia kuwa mtu huyo ndio mmiliki wa kampuni hio,...

    "mama, we Usijali, mpaka sasa nina asilimia 60 kuwa hii kampuni ni ya kaka surian, mana kila jambo lazima likae kwenye msitari"

    "mwangu, hizo ni ndoto za mchana... Mwanangu surian sijui yupo nchi gani, sijui amelufa au yupo hai... Japo nami nina asilimia 40 za kuhisi uwepo wake lakini sina uhakika"

    "mama? Acha nikachukue mshahara wangu twende nyumbani"

    "sawa, ila usiongee na huyo mbwa"

    Aliongea mama huyo kumuonya asha asiongee na sadiki jambo lolote lile

    "sawa mma, kwanza naanzaje kufanya hivyo"



    Ikiwa ni nyakati za mchana kweupeee surian akiwa na mkewe ndani ya gari...

    "mi naona tushuke twende pale restaurant tukapate lanchi"

    Aliongea jini maimuna au maimati huku suria akikubali swala hilo,...



    Huku ICC ambako faima Anauza nguo,.. Baada ya kupata namba ya suria amekuwa mtu wa furaha, lakini kila akitaka kuipiga anaogopa kufanya hivyo, mana amemmisi sana mchumba wake na haamini kama leo kamuona kwa picha,... Kila akitaka kupiga anaogopa, japo picha ni yeye lakini hana uhakika kuwa ni surian...

    "wacha nikale Kwanza,.. Nikirudi nimeshiba ndio nitapata ujasiri wa kuipiga namba hii"

    Aliongea faima huku akitoka kwenda kupata chakula cha mchana,.. Ikiwa ni eneo hilo hilo la mjini kati na hata akina surian pia hawapp mbali sana



    "afu mbona unapenda kujificha sana, tokelezea watu wakuone"

    Aliongea surian kuwa mkewe anapenda kuwa invisible (kuto onekana)

    "surian mume wangu, siruhusiki kuonekana kabla mama mkwe hajaniona"

    "duuuuuuu, kumbe ni masharti"

    "ndio"

    Alijibu maimuna huku safari ikiendelea, na wakati huo surian kavaa ile Bluetusi au Wayalesi (Bluetooth headset or Wireless).. Kile kifaa ambacho kinakaa upande mmoja wa sikio, ili ukipigiwa haina haja ya kutoa simu... Sasa surian kakivaa ili watu wajue anaongea na simu, mana hua watu wanamuona chizi kwasababu anaonekana anaongea mwenyewe, kumbe ana mtu kwa pembeni... Hivyo amekivaa ili aonekane anaongea na simu... Mana mke hataki kujionyesha kwa watu

    "pale pana chakula kizuri sana hivyo tulie pale"

    Aliongea maimuna huku wakielekea katika mgahawa huo... Lakini sasa mgahawa huo huo ndipo alipo faima akipata chakula cha mchana...



    Faima akiwa hana hili wala lile, anakula wali samaki kama kawaida ya wasichana kula wali... Surian akapita hapo hapo mbele ya faima, afu faima hajamuona.... Surian waliketi mahali ambapo pana viti viwili viwili ikiwa na maana mtu na mpenzi wake au mke wake,... Walikaa lakini kiti kimoja kilionekan kutokuwa na mtu lakini kina mtu..

    "samahani boss, nahitaji nikuhudumie lakini umekaa mahali pa V.I.P"

    Aliongea mhudumu wa mgahawa huo

    "una mana gani ukisema V.I.P"

    "nina maana kwamba wanaotakiwa kukaa hapa ni mke na mume au mtu na mpenzi wake"

    Surian na maimuna wakaangaliana kisha surian akamjibu

    "hakuna shida, nipo na mke wangu anakuja muda sio mrefu"

    Aliongea surian mana hakutaka kumwambia ana mke hapo alipo, kwasababu Muhudumu atashtuka kuskia kiti hicho kina mtu ingali anaona hakina mtu...

    "ok sawa, nikuagizie nini"

    "tuletee wali kuku"

    "sawa boss"

    Basi Muhudumu aliondoka kwenda kuleta chakula,... Punde si punde kafika na vyakula husika,... Basi mke na mume wakaanza kula tena surian analishwa na mkewe lakini hakuna anaye ona swala hilo zaidi ya kumwona surian akipanua tu mdomo na kutafuna...



    Sasa huku meza ya pili ambako kakaa faima,... Kumbe alimuona surian kama dakika moja iliopita, lakini sasa haamini kama ni yeye, mana kakaa kibosi bosi sana, ingali kasikia kuwa anamiliki kampuni

    "yule ni surian kweli"

    Alijiuliza faima, lakini papo hapo akapata akili... Alishika simu yake kisha akapiga,.. Kweli alikuwa ni surian wake, kwani alimwona akishika simu na kuipokea...

    "hallow"

    Alianza surian,... Faima kwa furaha aliitupa ile simu chini na kumkimbilia surian

    "suriaaaaaaaaaaaaaan"

    Sasa surian nae kuangalia, waooo ni mchumba wake faima,... Sasa faima anakuka kwa lengo la kukumbatiana, lakini sasa surian anakosa nguvu mana yupo na mkewe hapo alipo... Lakini huezi amini surian aliamka na kumkumbatia faima..... Faima alishindwa kuzuia machozi yaliokuwa mengi katika macho yake,.. Wakati huo maimuna anaangalia tu huo mchezo wa hao binadamu...

    "surian baba, ulikuwa wapi? Kwanini unataka kuniua baba"

    Aliongea faima huku kumbatia likiwa zito kutoka... Surian alikumbuka kuna mkewe hapo na surian anamuona mkewe yeye peke yake na si mwingine,...

    "nilikuwepo mbona"

    "surian mume wangu... Kiukweli leo nina furaha mpaka nalia"

    Aliongea faima, lakini surian alikuwa mpole kujibu kwani yupo jirani na mkewe,...

    "usijali faima, naomba nikutafute kwa wakati mwingine"

    Aliongea surian mana anajua pale hapafai kuongea mambo yao, ila sasa faima hajui....

    "hapana surian, kwa sasa siwezi kukuacha a abadan mpaka kufa kwangu, nitalala kwako nitakula kwako, aitaki nikuache tena baba"

    Aliongea faima kisha akakalia kile kiti ambacho maimuna au maimati kakalia... Surian alitoa macho mana yeye ndio anaona kuwa faima kakalia mtu, sasa atamtoaje pale...

    "mwambie mtu wako kanikalia"

    Aliongea maimuna baada ya faima kukalia kile kiti

    "ok... Faima, chukua kiti kile pale ukalie, hicho kitakudondosha"

    Surian aliongea hivyo ili faima asijue kitu

    "hapana,... Huku ni V.I.P, lazima uwe na mweza wako... Nashukuru tumekutana"

    Sasa kila neno analo ongea faima,.. Maimuna anaumia sana katika moyo na kujiona labda hana haki kwakua yeye ni jini...

    "surian mwambie mtu wako kanikalia bwana alaaaa"

    Aliongea jini maimati na hapo anaye sikia ni surian peke yake...

    "faima vuta kiti ukae"

    "mume wangu... Ina maana kwa sasa hutaki niwe karibu yako"

    "sina maana hio faima..."

    Sasa maimuna anazidi kuumia mana kakaliwa na mwanamke mwenzie afu ni lika lake, na vile faima ana umbo matata, basi na uzito umezidi...

    "surian, narudi tena mwambie kanikalia... Na asipo amka nitamuadabisha mana kaingia anga zangu vibaya"

    Aliongea jini maimuna kana kwamba kakasirika baada ya kujua huyo ni mke mwenzie ambaye ni binadamu kama surian.... Sasa surian naye anampenda sana faima, kuliko aumizwe ni bora amwambie ukweli

    "faima? nimekwambia uchukue kiti kingine mana hapo ulipokalia umemkalia mtu"







    Katika dunia hii kuna viumbe wengi sana lakini viumbe waliopewa uwezo wa hali ya juu huku duniani, ni pamoja na majini... Na majini hawa wapo wa aina nyingi kuna majini wazuri na majini wabaya, kuna jini maimuna mbaya na kuna jini maimuna mzuri, sasa huyu jini wa suria ni jini mzuri, na huyu maimuna ni jini mwenye asili mbili, na jini mwenye asili mbili ndio mwenye uwezo wa kuonekana na watu au asionekane, ni uwamuzi wake



    Sasa maimuna kila kifanya matembezi na mumewe hua hapendi kuonekana na binadamu kwasababu ya uzuri wake kupitiliza na kusababisha watu kumshangaa mwanamke huyo, hivyo ndio sababu ya yeye kuto onekana kwa jamii,... Na kuto onekana kwake hata alipokaa au kusimama pia haionyeshi kuwepo kwa mtu au hata kivuli,...



    Leo suria anakutana na mchumba wake wa zamani, akiwa na mkewe katika hali ya kuto onekana wanapata lanchi..... Faima aliweza kumuona mpenzi wake na kumfuata kwa furaha ya hali ya juu,... Bila kujua hapo alipo ana mkewe lakini faima hakuwa na uwezo wa kumuona zaidi ya mumewe ambaye ni surian,... Sasa faima alifikia mpaka kukalia kile kiti ambacho maimuna kakalia, hivyo kwa jinsi maimuna anavyo jiskia ni kuumia kwa kukaliwa kwa juu, na faima yeye anahisi kukaa kwenye kiti bila mashaka... Sasa maimuna anamwambia suria amwambie mtu wake kuwa anamuumiza kwa bile alivyo kaa kwa juu



    "faima? nimekwambia uchukue kiti kingine mana hapo ulipokalia umemkalia mtu"



    Aliongea suria huku faima akishtuka na kukiangalia kile kiti, alikiona hakina mtu, hivyo akakaa tena lakini wakati faima anakaa tena, maimuna alisha amka na kusimama,...

    "mbona hakuna mtu... Ina maana utani wako hujaachaga tu"

    Aliongea faima akizani labda ni utani wa surian,.... Na wakati huo maimuna anamuangalia faima kwa hasira mno, mana pia faima sio mgeni sana kwenye macho yake, na hata faima akifanikiwa kumuona maimuna basi pia hatokuwa mgeni katika macho yake yake, kwani walishawahi kuwa wateja wake katika kipindi fulani..



    "huyu mtu ni nani wako surian,... Ina maana kumbe ulikuwa na mchumba kabisa"

    Aliongea maimuna, kisha surian akajibu

    "hapana muna, kalikuwa ni kademu tu"

    Alijibu surian kisha faima akasema

    "unaongea na nani surian"

    Faima aliuliza, kwani alimwona surian anaongea pasina kumwangalia yeye,

    "fey, mi naona tutawasiliana kwa wakati mwingine"

    Aliongea surian baada ya kuona maimuna kakasirika na anaharakisha kuondoka

     "hapana surian, siwezi kukuacha tena, utaniua hapa hapa lakini lazima twende huko uendako"

    Aliongea fey huku akitaka hata kulia kwa jinsi surian alivyo taka,...

    Suria alimwangalia maimuna kavimba kwelikweli, licha ya kuwa ni jini lakini roho inamuuma kwakua kakutana na mke mwenzie ambaye alipenda kabla yake,...

    "surian, twende nyumbani basi mume wangu"

    Aliongea maimuna huku akitangulia kwenye gari na kuingia pale kushoto kwa dereva... Baada ya surian kuona hivyo, alitoa pochi na kutoa pesa kama laki moja na kumpa fey

    "shika hii, tutaonana"

    Surian alitoa pesa kisha akawa anaondoka..

    "sitaki pesa zako surian, nakutaka wewe tu"

    Fey alizitupa zile pesa kisha akatangulia kwenye gari ambalo surian alikuwa akilielekea na fey akajua hio ndio gari ya surian,.. Sasa surian akarudi nyuma kuokota ile pesa alio tupa fey,. Wakati huo fey naye kapanda gari na kukaa, hivyi kwa mara ya pili akamkalia maimuna, muna alishikwa na hasira sana..



    Surian yeye anaona kila kitu,.. Kiukweli hapo ana mtihani mkali juu ya wanawake hao,.. Suria aliingia kwenye gari na kuona hali halisi jinsi fey alivyo kaa juu ya maimuna...

    "muna, mi naona ujionyeshe tu akuone"

    Aliongea surian huku fey akisema

    "muna ndio nani surian, au unaongea na simu"

    Alijibu faima huku surian akiendesha gari kuelekea nyumbani akamwache maimuna kisha amrudishe fey kule alipo tokea...

    "siongei na simu, hapo ulipo umekalia mtu fey"

    "surian mimi staki utani wako"

    Aliongea fey akidhani labda surian anaongea utani, huku muna akisema

    "hivi surian, kwanini usingeniambia kuwa una mchumba"

    "muna, kukupenda nakupenda... Lakini hata ujinini nilikwambia mke wangu kuwa nina mchumba... Ukaniambia mchumba sio mke"

    "ni sawa,... Lakini mimi nilijua msha achana"

    "bado, sasa itakuwaje muna,.. Mana sina ugomvi nae"

    Aliongea surian huku fey akiuliza

    "surian, hio ni simu au unaongea na mimi"

    wakati huo wote walikuwa safari kwenda nyumbani, na hapo wamekaribia kufika,. Sasa maimuna akaona bora ajionyenye,... Sasa fey akajikuta anahisi kukaa katika mapaja ya mtu, ikiwa na maana kwamba muna kajionyesha,... Fey aligeuka nyuma na kukutana na msichana mwenzie mzuri kabisa... Ghafla fey alipata mshtuko na kuzimia baada ya kujua kumbe hapo yupo katika himaya isio sahihi... Muna hakumshusha fey katika mapaja yake kwani ingelikuwa ni kumnyanyasa mwanamke mwenzie hivyo fey alipakatwa kama jinsi alivyo kaa awali lakini akiwa kazimia,...

    Walifika nyumbani muna alitumia nguvu za kijini kumbeba fey mpaka ndani, na alimpeleka kwenye chumba kimoja kizuri kilichozungukwa na dhahabu, madini ya kila aina... Kitanda chenyewe cha dhahabu, yaani kila kilicho onekana hapo ndani ya mjengo ni pesa tupu...



    Huku ICC wateja wamejaa lakini mhudumu hakuna, muuzaji wa duka la jirani alijaribu kumpigia fey simu lakini haikuwa ikipokelewa,.. Ikabidi ampigie boss wake ambaye ndie alie mwajiri fey, mpaka hapo lazima fey aharibu kibarua chake



    Huku kwenye daladala mama surian na mtoto wake asha wakiwa na huzuni kubwa baada ya mama huyo kufukuzwa kazi kutokana na umri wake, yaani kilicho mfukuzisha kazi sio mshahara bali ni umri wake...

    "mama, wala usiwe na mawazo mama.... Mimi si bado nipo kazini"

    Aliongea asha huku akimtuliza mama yake.....

    Walifika nyumbani wakiwa na pesa zao na hapo ukichanganya wana kitu kama laki sita hivi na pointi,... Mama alimwangalia sana mtoto wake asha na kumsihi sana

    "asha mwanangu, kwa sasa mdogo wako surian tunamsikia tu... Sasa tegemeo letu ni wewe mwanangu... Mimi nilikuwa nina ombi moja kwako"

    Aliongea mama huyo, huku asha akimuuliza mama yake

    "ni ombi gani mama?, niambie tu"

    "asha,... Kwa sasa wewe ni mtu mzima... Unahitaji kuolewa, na katika wanaume wa sasa wanachagua sana aina na heshima za mwanamke... Mimi nakuomba ubadilike mwanangu.. Kua unavaa hivi ili upate mume bora mwanangu"

    Aliongea mama huyo huku asha akicheka sana.... Mana kwa sasa asha anavaa kiheshima kwakua pale kwenye kampuni ya MICCO hawahitaji mavazi ya ajabu, yena hususan mkoa wa tanga ulivyo miminika wingi wa imani ya Kiislamu, hivyo mama kamsihi mwanaye kuwa aendelee vivyo hivyo, yaani isiwe hivyo kwa niaba ya kazi, bali iwe ndio tabia yake na awe mwanamke mwenye heshima....

    "ahahaha mama, Kiukweli namshukuru mungu toka nilipojua kuwa ninaye mtaka kimapenzi ni ndugu yangu... Mama mpaka leo sitaki tena kudanga wala kutamani mwanaume,.. Mana naona tamaa yangu itanipeleka pabaya... Haya sasa kama sio kujua sauti ya mdogo wangu surian je si ningetembea naye?? Mama?? Mpaka leo nimekoma na sitaki tamaa"

    Aliongea asha na kumfanya mama yake kufurahi mara dufu zaidi,... Ni ukweli kua asha kaachana na hali ya kudanga,...

    "asha naomba uwe mtoto mwema kwetu, usitulize tena wazazi wako"

    "mama, nakili kulikubali hilo, nitawalea kuanzia sasa"

    Aliongea asha na wakati huo baba naye anaingia na kukuta mkewe anafuraha mpaka analia, yaani alipoteze ile huzuni yote ya kufukuzwa kazi,...

    "vipi jamani mbona furaha hivyo"

    Aliuliza mzee Rashidi ambaye ndio baba wa familia hio,....

    "we acha tu baba asha... Asalam Aleykh mume wangu"

    "waaleykh msalam mke wangu,.. Habari za kazi"

    "mmmhh Kiukweli kazi ni mbaya kwa upande wangu.. Kwani imegundulika kuwa nimeingia kinyemela"

    Aliongea mama huyo huku baba akishtuka kwa taarifa hizo,

    "mungu wangu, sasa itakuwaje mke wangu"

    "hakuna tabu, na hapa nilikuwa na furaha baada ya asha kukili kutulea kwani yeye bado yupo kazini"

    "asha mwanangu, ni kweli utakuwa nasi"

    Mzee Rashidi alimuuliza mtoto wake aliobaki baada ya suria kupotea takribani miezi sita sasa toka kupotea kwake, japo wapo waliosema surian amefariki dunia...

    "ndio baba, na naahidi kubadilika kuanzia tabia"

    "ahsante sana mungu, mana sikutegemea kama asha utakuja kubadilika mwanangu"

    "msijali wazazi wangu, na pia numepata tetesi kuwa ile kampuni anamiliki kaka surian"

    Aliongea asha, na swala hilo baba hakuwahi kulisikia kabla na hata asha hawana ule uhakika wa wazi

    "unasemaje asha.."

    "ndio baba, nimesikia tu, hivyo nitafanya upelelezi kwa hilo"



    Sasa tukija huku kwa surian, katika chumba ambacho kalazwa fey,... Faima alizinduka na kuanza kushangaa chumba ambacho kalazwa kikiwa na dhahabu kila kona, faima aliona mlango wa kutokea kisha akaufuata mlango huo, yaani alikuwa ni mtu wa kushangaa jengo hilo kwani lilijengwa kwa dhahabu, na kama mnakumbukwa kuwa jengo hili, lilishushwa tu kutokana na nguvu za maimuna,... Nyakati hizo ikiwa ni saa mbili usiku, surian alitoka hapo sebuleni na kuingia chumbani kuchukua laptop, hivyo ule wakati wa kuingia chumbani, faima alipita hapo sebuleni akitafuta wahusika wa jengo hilo,...



    Mke wa suria akiwa jikoni anaandaa maakuli ya jioni, faima alisikia hali ya mkaango katika chumba fulani,... Akafuatilia mpaka jikoni kaingia,... Maimuna akahisi kuwa yupo mtu anaingia na sio mumewe,... Na wakati huo faima bado hajafika jikoni, maimuna ni jini wazuri na hua hawazuru au hazuru mtu... Faima alishtuka kuona mwanamke anakaanga vitu vyake jikoni,...

    "shikamoo dada"









    Hakuna kitu kibaya mwanamke aolewe halafu akutane na mke mwenzie ambaye hata dosari na mume hawana,... Ila kwa kibongo Bongo hawa wanawake wangekutana hivi lazima ngumi zingerindima, lakini kwakua muna ni jini hivyo hatakiwi kuwa na chuki dhidi ya binadamu ambaye hana hatia naye,..



    Faima alifika jikoni na kumkuta muna ambaye ndio mke wa surian,

    "Shikamoo dada"



    Faima alimsalimia mwanamke mwenzie ambaye huenda akawa lika lake au kazidiwa kidogo....

    "safi tu, karibu"

    Huezi amini muna hakuwa na chuki na fey kwani kagundua ni msichana ambaye hana tabia mbaya na kitu kilicho mfanya muna asimchukie fey, ni kwamba fey bado ni bikra, hivyo ni msichan msafi kuliko wasafi wote, hivyo fey ana uwezekano wa kuwa jini kutokana na hali alio nayo mana kuna majini ambao hupewa nguvu kutokana na tabia na usafi wao,... Usafi sio usafi wa kuoga, bali ni usafi wa kuwa na bikra ukiwa mtu mzima, kana kwamba umeepuka ushetani mwingi sana katika dunia ya leo,... Hivyi hata surian angelikubali kubadilika kuwa jini, ingeliwezekana kwasababu alikuwa ni mwanaume Msafi,... Sasa kitu ambacho muna kampenda fey ni kwasababu ni bikra na hakumchukia kwa lolote lile...



    "ahsante dada,... Samahani wewe ni nani"

    fey alimuuliza muna kuwa yeye ni nani,...

    "mimi Naitwa maimuna au maimati.. Ni msichana mwenye asili mbili, ni binadamu na ni jini... Ni mke wa surian"

    muna hakutaka kumficha kwasababu hata yeye fey hakujificha baada ya kumuona surian,...

    Faima alishtuka sana baada ya kuskia kuwa ni mke wa surian,.. Yaani hakushtuka kuwa ni jini, bali kashtuka kuwa ni mke wa surian,... Muna alishangaa kuona fey anadondosha machozi mfululizo.

    "kuna tatizo fey"

    "lipo tatizo, dada"

    "unahitaji utatuzi juu ya hili"

    "sina jinsi dada... Nimesha kosa haki yangu,. Surian nampenda sana, nahisi hata nikifa nitakufa naye"

    Aliongea faima huku akilia,... Muna alishtuka sana kuskia hivyo...

    "kwanini msinge oana"

    "alikuwa anajipanga na maisha, ndio ghafla akapotea, toka siku hio ndio nimemuona leo"

    Aliongea faima huku akiendelea kulia

    "kahio bado unahitaji kumuona"

    "Kiukweli sio kumuona tu, hata kunioa nataka..... Dada? Nipe nafasi nami nijivunie kuwa naye"

    Muna alishtuka sana kuskia hivyo, mana ni ujasiri wa hali ya juu sana

    Mana fey keshaambiwa kuwa huyo ni jini lakini bado tu anatamani aolewe na surian angalau awe mke wa pili,

    "hapana, Utanisamehe fey.... Siwezi kuolewea mke wa pili... Kama unahitaji kumwona umwone tu, lakini kwa hilo, haiwezekani"

    Aliongea muna huku akiligeukia jiko na kuendelea kupika...

    "naomba unielekeze njia ya kumuona surian, niwe namuona tu"

    Fey aliumia sana baada ya kusikia kuwa haiwezekani kuolewa na suria kwa sasa, lakini fey hakukata tamaa mana hawezi kumuacha surian kamwe,. Hivyo fey akaomba awe anamuona tu,..

    "una maana gani kusema hivyo fey"

    "naomba hata niwe nafanya kazi humu niwe namuona tu"

    Aliongea fey kuwa apewe hata kazi za za ndani ili awe anamuona tu surian,... ni ujasiri wa hali ya juu ambao fey anao....

    "una maana gani kusema hivyo"

    "hata kunipa kazi hapa sawa tu"

    "hapana,.. Kukupa kazi ndani ni ngumu, labda kiwandani"

    Aliongea muna huku akiwa bize katika kupika,.. Fey alitoka jikoni hapo na kutaka kutoka....

    "Unakwenda wapi fey"

    Muna alimuuliza lakini fey hakujibu lolote,.

    Lakini fey alipokuwa anatoka, alimwona surian pale sebuleni... Waooo huezi amini alishindwa kutoka na kumkimbilia surian... Sasa suria kushtuka mara fey huyo,...



    Yalionekana machozi ya muna yakidondoka baada ya kuona surian kamkumbatia fey,... Kumbe muna naye roho inamuuma sana kwani fey ndio mwanamke wa kwanza katika moyo wa surian,...

    "we fey, tulia basi"

    Aliongea surian huku akijitahidi kumtoa, kana kwamba fey anafanya makusudi kwasababu keshakataliwa na hawezi kupata nafasi ya kuwa na surian,....

    "suri?? Hebu amua moja... Kama sipo moyoni mwako nijue kabla"

    Aliuliza faima huku suria akiwa hana jibu sahihi la kumpa....

    "fey, nina mke naaa"

    "najua, una mke na ni jini... Lakini jua kuwa moyoni mwako bado nipo nawe upo na hutokaa kutoka... Nimejitunza mpaka leo, na hata sinioe lakini naomba uitoe hii bikra"

    Muna alishtuka kuskia hivyo, kitu kilichomfanya aje mpaka pale walipo

    "fey, naomba ujieheshim tafadhali sana,.. Nimekuona ni mstarabu sana hivyo naomba uutumie ustarabu wako vyema"

    Aliongea maimuna huku akiwa Siriasi kweli,...

    "samahani dada... Lakini jua kuwa ni moyo ndio unanisukuma kulitaka hilo"

    "ni sawa, ila wanaume wapo wengi,.. Bikra alio nitoa basi inamtosha sana"

    Aliongea maimuna kisha akageuka kuelekea jikoni, ikiwa chakula tayari kimesha iva.. Muna alianza kuleta mboga, kabla hajatua fey kanyanyuka na kukimbilia jikoni kuleta chakula.... Kiukweli hakuta kitu cha raha kama kujiamini, na yote hio ni upendo wa kweli toka moyoni, hivyo muna kalenda mboga, na fey kaleta chakula

    Muna alijikuta anafurahi tu katika moyo wake, kwani ni ujasiri wa hali ya juu ambao fey anao..... Fey alimaliza kitenga kila kitu mpaka maji ya kunywa, na bila uoga naye akakaa na kula bila wasiwasi,... Yaani kaamua liwao na liwe kama muna ni jini muuaji basi auwawe tu kwa niaba ya penzi....



    Kesho yake fey kaamka asubuhi sana kabla ya muna kuamka,... Kawasha jiko kisha akawa anapika chai,... Yaani fey anaililia nafasi ya kazi ya hapo ndani, ili aweze kumwona surian hata kwa macho tu....



    Muna anaamka anakuta kila kitu kipo mezani, afu kakaa hapo akisubiri wenyeji waamke,... Yani muna alijikuta anampenda fey licha ya kumchukia kwakua analihitaji penzi la mume wake,..

    "kwahio ina maana kwamba unataka kuwa House Girl kwa nguvu"

    "dada? Nampenda sana surian, nipo tayari kufa kwa ajili yake... Na ukae ukijua kuwa dini yetu inaturuhu kuwa wake wawili kwa mume mmoja,.. Nitakuheshim vile utakavyo"

    Aliongea fey huku muna akiwa haamini maneno ya huyo msichana mwenzie,...

    "maneno yako wala siwezi kiyaweka akilini fey, mimi ni mke halali wa surian"

    "najua, na mimi pia ni mchumba wa kwanza wa halali kwa surian,.. Umeninyang'anya surian wangu"

    Mara surian alitokea akiwa kavalia kikazi, kana kwamba keshaoga, sasa hapo anywe chai aondoke, na wakatili huo ni saa 12 za asubuhi...



    Masaa kadhaa mbele ikiwa ni saa nne asubuhi surian akiwa kazini baada ya jana kito kuka kwakua ilikuwa ni siku ya kutoa mshahara, hivyo leo kazini kama kawaida.... Surian alipiga simu kwa shadya na kuwataka vikao kati yake na sadiki kutokana na hali ya jana kwa mfanyakazi yule mwenye umri mkubwa alipewaje kazi hapo MICCO, kikao kiliitwa na boss surian



    Tukija huku kwenye jumba la dhahabu, ambalo linamilikiwa na jini maimuna,...

    "afu wewe ulikuwa unauza duka la nguo"

    Aliongea muna baada ya kuachwa wote nyumbani na surian kajua hapo hakuna ugomvi mana muna anapenda sana mwanamke mwenye bikra kwani kaepuka vishawishi vingi mno,....

    "ndio, na hata wewe pia sio mgeni kwangu"

    "kama vile twajuana.... Ila kwa mume tafadhali sana"

    "sawa,... Ila mimi nataka kazi tu"

    Fey alikubali kumkosa surian lakini hio ni akili anaitumia,....

    "labda ujaribu kujitahidi sana"

    Aliongea muna tena kwa kucheka cheka kama watu walio marafiki zaidi, kumbe ni watu wenye kugombea mwanaume mmoja....

    "kikubwa nina furaha sana kumuona surian, na nitakuja kumuona kila wakati... Leo wacha na familia yangu ikajue furaha yangu juu ya kukutana na surian"

    Aliongea fey huku akiamka na kutaka kuondoka....

    "sawa karibu tena"

    Yaani kwa sasa wapo kama marafiki, lakini ni mahasimu wawili wakubwa sana....

    "na nitakuja tu"

    Aliongea fey kisha akaondoka, lakini alipofika nje, aliliangalia sana jengo hilo ili akija baadaye asilisahau,.. Yaani nje ni jengo la kawaida sana lakini ndani kumejaa dhahabu kila kona



    Faima kwa furaha kwanza akapitia kwa akina asha mbako ni kwa akina surian,....

    "yaani we mtoto nikikuona namkumbuka mwanangu"

    Aliongea mama yake suria baada ya kumuona fey, akiwa na maana hajui lolote juu ya mtoto wake,...

    "Shikamoo mama"

    "marahaba ujambo mwanangu"

    "sijambo... Asha kaenda wapi"

    Fey alimuuliza mama huyo

    "asha siku hizi ana kazi.... Kapata kazi kwenye kampuni moja hivi inaitwa MICCO"

    Aliongea mama huku fey akijibu kuwa

    "oohhh nilijua tu,..."

    "ulijua nini"

    "si anafanya kazi kwa ndugu yake"

    "unasemaje wewe"

    "ila mama.... Kwanini umekubali surian aoe jini, huezi amini mimi sina nafasi tena... Ila nina furaha kwa kumuona"

    "fatuma, una maana gani... Hio ndoto uliota saa ngapi"



    Wakati huo huku kazini, sadiki na shadya ndani ya kikao, siria ya surian kuwepo mjini imeanza kujulikana

    "shadya, sina maswali mengi sana kwa sadiki, mana hata yeye alipitia katika uchambuzi wako... Hebu niambie, huyo mfanyakazi alipataje kazi hapa"

    Shadya aliulizwa na boss wake,

    "ni kweli boss,... Kiukweli yule mama alilia sana, hivyo nikajikuta namuonea huruma,... Nilichokifanya nilitumia picha za mdogo wangu, na jina nikalitumia la huyo mama... Na pia ilishangaza kumpangia mshahara mkubwa.. Na pia kwakua hukutaka mfanyakazi mwenye umri mkubwa, nikafanya mabadiliko ya wafanyakazi, yule aliotakiwa kufanya usafi chooni nikamuweka idarani, na yule wa idarani nikamweka chooni kwakua huendagi kule, hivyo ni ngumu kumuona... Kiukweli naomba unisamehe boss na nitakubaliana na adhabu yeyote itakayo jitokeza"



    Shadya Aliongea kwa huzuni akionyesha ukweli juu ya huruma yake kwa mama huyo, bila kujua ndio mama wa surian, hivyo surian kamfukuza mama yake mzazi katika kampuni yake,...

    "kwahio umeleta huruma kwenye kampuni za watu"

    "samahani boss, sikujua kama itakuja kujulikana"

    "kwanini huyo mama asingeleta mtoto wake"

    "Kiukweli boss, mwanzo yule mama alisema hana mtoto... Na ana hali mbaya sana ndio nikashawishika kumsaidia,... Ila baade mtoto wake alikuja kuomba kazi, nakumbuka siku ile ulitoka... Hivyo mpaka sasa mtoto wake yupo idarani"

    Aliongea shadya tena kwa kujiamini kwani kama kazi inakufa basi ife, na kama ipo basi iwepo tu...

    Wakati huo sadiki katulia tu akisikiliza kwani hahusiki kwa jambo hilo,...

    "kwahio hii familia unaonekana umeipendelea sana... Haya na huyo mtoto wake analipwaje"

    "analipwa laki mbili na nusu"

    "elimu yake?"

    Surian aliuliza elimu ya msichana huyo

    "ni kidato cha nne felia"

    "haaaaaa... Yaani kidato cha nne felia analipwaje laki mbili na nusu??"

    "aliomsajiri ni boss sadiki"

    Aliongea shadya kuwa yeye hahusiki kumpangia mshahara mfanyakazi huyo...

    "sadiki?? Sasa kama mtu alio feli analipwa laki mbili je yule mwenye levo nzuri ya elimu alipwe kiasi gani.. Mana hio laki mbili analipwa mtu mwenye levo ya elimu nzuri, sasa kwanini unamlipa mshahara mkubwa kiasi hicho"

    Aliongea surian huku akiwa anaanza kukasirika kwani aliona wafanyakazi wanaongeza mishahara kwa mapenzi yao

    "samahani sana boss,... Nitalibeba jukumu hilo kama kosa langu, na nipo tayari kumpunguzia mshahara wake hivi punde"

    "sio kupunguza tu, pia kitengo abadilishwe... Akae kitengo cha mama yake,... Afu nasema hivi sitaki ujinga na kazi. Kama hamtaki kazi mseme"

    Aliongea boss surian huku akikasirika sana...

    "tusamehe boss, tunahitaji kazi"

    "haya mara moja nisiwaone hapa... Na huyo mfanyakazi apelekwe chooni, kulingana na elimu yake"

    "sawa boss... Sasa alipwe kiasi gani"

    "laki na nusu inamfaa kwake"

    "sawa boss"



    Sadiki alilichukua jukumu lile la kwenda kwa asha kisha akaanza kumtia Jamba jamba ya hapa na pale, wakati huo asha yupo bize na kazi...

    "mfanyakazi hodari... Haya niambie jibu langu lipo wazi"

    Aliongea sadiki huku asha akibinua mdomo,

    "mschiuuuuuiu (msunyo).. Huna hadhi ya kuwa nami, kama umeweza kumfukuzisha kazi mama yangu,.. Utawezaje kuwa nami"

    Aliongea asha huku sadiki akianza kusema

    "yaani unanisunya mimi.... Sasa kwa taarifa yako, kuanzia leo nakulipa laki na nusu, na kitengo chako, kuanzia leo ni chooni, kama hutaki acha kazi"

    Aliongea sadiki huku wafanyakazi wengi wakisikitika kwani idara aliopo asha ni kubwa kuliko...

    "sitaki kazi yako... Huezi kunipa kazi kwa kunitongoza..."

    Aliongea asha huku wafanyakazi wakiguna kuashiria kuwa kumbe sadiki ana tabia ya kitongoza Wafanyakazi,....

    "asha kwanini usiende kusema kwa boss"

    Aliongea mmoja wa wafanyakazi wenzake, waliompa ushauri huo...

    "hapana, wacha niache kazi"

    "hapana wewe... Nenda kashtaki kuwa sadiki kakushusha cheo kwasababu kakutongoza ukakataa, nenda acha ujinga wewe"

    Aliongea rafiki wa asha ambaye anafanya nae kwenye idara moja,... Kweli asha akashawishika kwenda kwa boss kusema, lakini sha nia ya kukubali swala hilo ni ili akamjue boss wa kampuni hio mana anasikia ni ndugu yake kabisa....

    "wewe Unakwenda wapi"

    "usiniulize"

    "we asha rudi huko hamruhusiwi kuingia"

    Aliongea sadiki kwani anaogopa kwa ushauri aliopewa na rafiki zake,...

    Asha alipata kichwa cha kwenda ofisini kwa boss...

    "we asha vipi tena"

    Shadya alimuuliza asha baada ya kumwona asha yupo mlangoni

    "nina shida na boss, haiwezekani boss sadiki anipeleke chooni kisa nimemkatalia kuwa naye"

    Aliongea asha huku shadya akishangaa

    "haaaaaaaaaaaaaaaaa, asha, unasema kweli"

    "ndio, nimemkatalia sasa amekuja kunishushia mshahara wangu na kunibadilishia kitengo"

    "lakini asha, hicho kitengo na mshahara, ni swala la boss mwenyewe na sio sadiki"

    Aliongea shadya huku asha akitamani hata kufungua ule mlango bila ruksa,...

    "sawa, lakini jua kuwa sadiki ana tabia ya kututongoza wafanyakazi wa idarani"

    "haaaaaaaaa, kweli asha?"

    "ndio... shadya"

    Shadya aliamka na kugonga mlango..

    "nani?"

    Boss aliuliza, lakini asha alishtuka kuskia hio sauti

    "ni mimi shadya... Yule dada anataka kukuona"

    "dada nani huyo"

    "yule mwenye mama yake aliokuwa mfanya usafi kule toilets"

    "ana shida gani"

    Suria aliuliza lakini asha akaona kwa hali hio hakutokuwa na ruksa.... Asha akapayuka kwa sauti na kusema

    "boss?? Boss sadiki kanitongoza"

    Aliongea asha, sasa sadiki alisikia sauti hio mbona ni kama ya dada yake.... Na ni kweli alikuwa ni yeye, hivyo surian kwa furaha alijikuta anatoka nje...

    "suuuuuuriaaaaan"

    Asha alipayuka na kumkumbatia mdogo wake kabisa.... Shadya kabaki mdomo wazi,... Mara sadiki katokea.... Alishangaa kukuta asha kakumbatiwa na surian

    "haaaaaaaaaa.... Uh nnh uuuh aahh uuun"





    Sadiki alipatwa na kigugumizi baada ya kukuta kumbatio zito baina ya suria na asha ambao ni mtu na dada yake baada ya kumisiana kwa muda mrefu,.... Asha wakati huo anaangua kilio, kwani haamini kama leo kamuona mdogo wake ambaye ameshukiwa kumuua kwa ajili ya mali,...



    Shadya na Sadiki wakiwa mashahidi wa kumbatio hilo, na wasijue watu hao wana uhusiano gani... Baada ya kumbatio surian naye machozi yalimtoka kwa kuto waona ndugu zake kwa muda mrefu,... Sadiki na shadya bado kimya kilitawala juu yao,.. Surian alimchukua asha na kuingia naye ofisini kwake,..



    "mbona sielewi"

    Aliuliza sadiki huku akiwa na wasiwasi,..

    "hata mimi sielewi"

    Shadya naye alimjibu sadiki, mana hakuna ambaye anafahamu hilo...

    "mungu wangu, isijw kuwa ni mpenzi wake"

    Aliongea sadiki huku akikaa kwa kalio moja kwa uoga wa hali ya juu

    "na asha kasema ulimtongoza, na kukukatalia kwake, ndio sababu ya kumfukuza mama yake... Sasa kama atamwambia mpenzi wake,.. Kazi huna boss"

    Aliongea shadya akidhani kuwa surian na asha ni mtu na mpenzi wake,

    "shadya usiseme hivyo jamani"

    Sadiki Aliongea huku akiwa kasimama mana kiti hakikaliki wala kusimama hakusimamiki,

    "sina maana kuwa ufukuzwe kazi, ila ulionyesha tamaa boss"



    Huku ofisini surian na dada yake walikuwa wakisimuliana maisha yalivyokuwa mpaka sasa

    "surian mdogo wangu, ulikuwa wapi... Dada yako naambiwa nimekuua jamani"

    Aliongea asha huku machozi ya furaha yakiendelea kumtoka kwa kasi mana haamini kama leo kamuona mdogo wake,...

    "dada, ni maisha tu... Mi nadhani utajua tu"

    Surian naye machozi ya furaha yalimtoka kwani ni miezi sita kama sio saba, toka kupotea kwake,.. Wakati huo huku mapokezi sadiki anajinyea nyea kwa kujua labda asha ni mpenzi wa surian,...

    "surian, hebu twende kwa mama, mana yeye ndio anaumwa kila siku juu yako... Japo naye kafanya kazi hapa na kafukuzwa juzi tu"

    Aliongea asha huku surian asiweke hata ubishi wa chembe moja...

    "ina maana kwamba mama ndio alikuwa akifanya usafi wa choo"

    "ndio, kwani ulikuwa hujui"

    "hapana.."

    "ndio hivyo, mama alikuwa akifanya usafi wa chooni na hajui kama wewe ndio mmiliki wa hapa"

    Surian alilia sana na kushikwa na hasira,

    "shadyaaaaaaa"

    Siku zote surian anapigaga simu kwa shadya, lakini leo kaita kwa mdomo tena kwa sauti kubwa,

    "abeee boss"

    "njooo"

    sadiki na shadya roho ziliwapasuka huku kila mmoja akichanganyikiwa juu ya uitaji wa boss kuwa mkali na wa hasira...

    "abee boss"

    "shadya?? Kwanini mama yangu umpangie chooni aisee"

    Alifoka surian huku shadya akitetemeka kwa uoga

    "bo... Bos.. Bos... Samahani sana,... Kwanza sikujua kama ni mama yako, na pia kigezo kikuu cha kampuni yetu, hairuhusu mfanyakazi mwenye umri zaidi ya miaka 35.... Hivyo yule mama aliniomba na kuniomba.... Boss? Niliingiwa na huruma kutokana na maelezo ya maisha yake yalivyo, hivyo nikaamua kumtangenezea vyeti feki ili apate kazi aweze kuilisha familia yake... Nilitafakari nitamueka wapi ili usimuone kwakua ana umri usiotakiwa hapa kwenye kampuni.... Boss? Nisamehe sana... Niliona huna muda wa kwenda public toilets, nikaona huko kunamfaa kwakua hutokwenda mara kwa mara.... Na jina lake ulilifanya kulipwa mshahara mkubwa sana, na sikuweza kuukata mshahara wake mpaka alipokuja kuacha kazi.... Boss? Nisamehe, sikujua kama ni mama yako"



    Shadya aliongea ukweli wote huku akilia kwa uoga wa hali ya juu.. Huko mapokezi sadiki anahangaika, moja haikai mbili haikai...

    Surian alimsikiliza shadya kwa umakini wa hali ya juu, alijua hana kosa....

    "rudi ofisini kwako"

    Aliongea surian huku shadya asiamini kuwa kaambiwa arudi kazini kwake....

    "ahsante boss"

    Alishukuru shadya huku asha akimtaka mdogo wake waondoke waende kwa mama yao....

    "twende kwa mama surian,.. Utamuua mama etu.."

    Surian alikuwa na mipango ya kwenda kwao wiki hio hio, lakini siku hio kakubali kwenda kabla ya siku husika ambayo kaipangilia kwenda...

    "twende dada...."

    Asha na mdogo wake surian walitoka na kupanda gari ya kifahari,... Wafanyakazi wanashangaa asha leo kapanda gari ya boss.... Waliondoka kwenda kwao



    "enheee... Mbona mimi hajaniita"

    Aliuliza sadiki baada ya boss kuondoka

    "we acha tu.... Ni kesi kubwa unayo"

    Aliongea shadya, sadiki nae presha juu...

    "shadya acha utani dada angu"

    Sadiki mpaka kamuita shadya dada, kwa uoga...

    "sasa skia balaaa... Kumbe yule mama ni mama yake mzazi, na huyu asha ni dada yake wa kuzaliwa naye"

    Shadya alimwambia Sadiki kuhusu asha na yule mama

    "ati unasemaje shadya??"

    "asha ni dada yake.. Na yule mama, ni mama yake mzazi"

    "mungu wangu weeee......kumbe nimemfukuza mama yake boss"



    Wakati huo huo huku nyumbani kwa surian, yaani kule kwa mke wake.... Kama ilivyo kwa viumbe ambavyo sio binadamu halisi hua wanajifungua kwa muda mfupi,... Binadamu hukaa miezi tisa... Jini wabaya (mashetani) hukaa miezi miwili mpaka na nusu... Na hawa majini wazuri, wao hukaa miezi minne mpaka mitano... Maimuna miezi mitano ilishafika, na ndio maana hakuwa wakwenda kazini japo mimba yake haionekani sana kwasababu ni miezi mitano tu, na pia wao sio binadamu kwamba atachoka kama ilivyo kwa binadamu.. Na hata kujifungua kwao hawaelekei hospitalini,... Bali hurudi ujinini kujifungua,.... Na siku hii ya leo shaimati alikuja nyumbani kwa maimuna baada ya maimuna kutoa taarifa ya kujifungua kwake, na hawa kama ilivyo wana ugomvi lakini hawapigani...

    "maimati twende sasa hivi"

    Aliongea shaimati kwani kisheria atatakiwa kujifungulia ujinini, na kama kuna kurudi kwa mume basi atarudi na mtoto wake...

    "hapana shaimati, wacha mume wangu aje ndio tuondoke usiku wa leo"

    "maimati, huyo ni binadamu tu, hawezi kuvuruga taratibu zetu"

    "shaimati, nenda nitakuja mwenyewe"

    maimuna kaamua kumfukuza shaimati kwani shaimati katumwa na uongozi wao aje kumchukua maimati lakini maimati kakataa kuondoka kwa siku hio mpaka surian aje...



    Tukija huku kwa mama yake surian akiwa na faima, mama alishtuka sana baada ya faima kumwambia mama mkwe wake kuwa surian kaoa jini....



    "ila mama.... Kwanini umekubali surian aoe jini, huezi amini mimi sina nafasi tena... Ila nina furaha kwa kumuona"

    "fatuma, una maana gani... Hio ndoto uliota saa ngapi"



    Aliuliza mama huyo huku akizani labda anadanganya kuhusu uwepo wa surian na kuoa jini...

    "mama, mbona surian yupo na hata asubuhi kaenda kazini..."

    "anaishi wapi kama umemuonac

    Mama aliuliza huki akilengwa na machozi mana ni miezi saba sasa hamuoni mtoto wake, na wala hajui yupo wapi kwa sasa...

    "kuna nyumba moja hivi anaishi, ila mkewe ni jini"

    Aliongea faima huku naye roho ikimuuma kwani atakuwa hana nafasi tena ya kuolewa na surian...

    "nipeleke nikamuone mwanangu.. Nina shida na mwanangu"

    "sawa mama... Lakini, na mimi vipi ina maana ndoto za kuolewa na surian zimeishia njiani mama"

    "wewe twende kwanza"

    Mama surian alivaa haraka haraka ili apelekwe huko ambako surian anaishi.... Mama keshavaa sasa akiwa anafunga mlango, ghafla aliona gari moja ya kifahari inasogelea jengo lao,...

    "enheee ndio huyo hapo... Hilo ndio gari analotumia"

    Aliongea faima kwakua anajua na alisha wahi kulipanda gari hilo...

    "we faima? Mbona sikuelewi"

    Mama akiwa katoa macho, aliona mtu wa kwanza kushuka ni asha... Mama katulia tu... Mara surian anashuka,... Mama haamini leo kwa mara ya kwanza toka kupotea kwake anamuona kwa macho yake...



    Mama surian anapoteza fahamu kwa kitendo cha kumuona mtoto wake,.. Haraka haraka surian na dada yake pamoja na faima wanambeba mama na kumueka kwenye gari, moja kwa moja mpaka hospitalini,....

    "dada? Baba kaelekea wapi"

    Surian alimuuliza dada yake, mana wakati akiingia pale kwao baba yake hakuwepo..

    "baba nadhani yupo msikitini, mana ndio mtunza hazina wa msikiti"

    "hebu nipe namba yake"

    Basi asha alimpa mdogo wake namba ya baba yake na kumpigia

    "Hallow mzee, Asalam Aleykh"

    Surian alimsalimia baba yake

    "heeee, wa.. Waleykh... Waleykh msalam, upo wapi mwanangu"

    "nipo hospitali hapa mama kapoteza fahamu"

    Aliongea surian na baba yake alijua tu sababu ya mkewe kupoteza fahamu kwani hata sauti ya surian tu ilimfanya apoteze fahamu,...

    "nakuja sasa hivi"

    Simu ilikata baada ya mzee Rashidi kutaamka ujio wake hapo hospitali..



    Ilipofika saa saba mchana mama asha alizinduka, jicho la kwanza lilipita kwa surian,... Mama Alianza kulia huku akiamka

    "mama, pumzika Kwanza mimi nipo tu"

    "surian mwanangu, ulikuwa wapi baba"

    Mama alimuuliza mtoto wake huku akilia sana,

    "mama? Ni stori ndefu sana..."

    Alisema surian huku akiwa kakaa katika kitanda alicho lazwa mama yake

    "ni nini tatizo? Dada yako kapewa kashfa nzito juu yako...."

    Wakati huo baba katulia tu nae furaha ilimjaa katika moyo, surian ni mtoto waliimpenda kuliko hata asha,

    "jamani, kama matibabu tayari, tuondokeni ili kusiwepo na gharama zaidi"

    Aliongea baba yake suria huku suria akisema kuwa

    "hakuna shaka baba"

    Basi baada ya baba yao kusema hivyo waliona ni bora waondoke, kwani mama huyo hakuwa na ugonjwa wowote zaidi ya kupoteza fahamu....



    "haya baba, nsikia umeoa jini"

    Alisema ZUWENA ambaye ndio mama mzazi wa surian na asha...

    "ati nini?? Mama asha?? Unasema suria kaoa nini"

    Baba alidakia juu kwa juu baada ya kusikia mtoto wake kaoa jini...

    "muulize mtoto wako si huyo hapo"

    Wakati huo surian anaendesha gari kurudi nyumbani...

    "wazazi wangu, mtajua hayo yote, wacheni tufike nyumbani, kisha nikamchukue mke wangu muje mumuone"

    Aliongea surian lakini mama na baba walisema kuwa

    "hapana, yaani kama huyo mwanamke ni jini sisi hatumtaki, hatuwezi kukupoteza kwa mara nyingine tena"

    Ni maongezi ya wazazi hao wakikataa ndoa ya wawili hao baina ya binadamu na jini... Wakati huo faima katulia kimyaaaaa...

    "tena kama inawezekana naomba twende sasa hivi huko kwa mkeo... Wewe ni binadamu huezi ukaoa jini.. Na umekubali vipi?"

    Aliongea mama yake asha huku mzee Rashidi akisema

    "twendeni huko huko... Mana hata leo hatutaki uondoke katika himaya yetu"

    Aliongea mama yake asha,... Lakini ghafla asha akadakia

    "surian, si uwasikilize wazazi lakini"

    Kiukweli suria alikuwa katika wakati mgumu sana kwa wakati huo... Mana anajiuliza Ataanzaje kumkana maimati, japokuwa kweli ni jini... Suria aligeuza gari kuelekea nyumbani kwake ambako mkewe ndipo alipo...



    "halafu na elimu ya dini ulio nayo, imewezekana vipi ukafanya ujinga kama huo suria"

    Mzee Rashid aliongea tena kwa hasira, kana kwamba pamoja na dini elimu zote alizopewa, lakini kakubali kuoa jini.

    "baba,... Labda niwaambie kwa ufupi kuhusu suala hilo"

    "sio kwa ufupi, nataka kujua sababu ni nini, kama ni magari rudisha gari za watu"

    Wazazi walikuja juu kwa tatizo la suria kuoa jini, kiumbe ambaye sio jamii yake,...



    "baba.... Siku hio nilichukuliwa na kuambiwa nakwenda kupewa kazi nchini dubai,... Kwa vile nilikuwa sina kazi nilikubali, na siku ile nilikuja kuwaaga lakini sikuwakuta, hivyo niliondoka na kutegemea kurudi.. Lakini kumbe haikuwa dubai bali ni ujinini,... Baada ya muda ndio nikafahamu kuwa nipo ujinini na sio dubai... Nilipendwa na jini kiongozi kwa tamaa, akawa na mimi kwa njia za ndoto, lakini yupo alionipenda kwa dhati kabisa na kunipa kinga... Hivyo yule jini akakosa uwezo wa kunifuata, hivyo akatumia njia ya kawaida ambayo kwao ni makosa... Jini yule aligeuka kuwa shetani kwa kuzini na mimi... Ndipo nikapewa taarifa ya kupendwa na jini huyo alionipa kinga,.. Nilishindwa kukataa kwakua nipo ndani ya himaya ya watu,.. Lakini nikaahidi nikija huku duniani nitaachana nae,.. Sasa nilipokuja huku nikamwambia nataka nije kuwaona, lakini yeye akasema katika masharti yao ni mpaka zipite siku saba ndio nije nae,.. Mara zikaongezeka tena,... Zilipoisha ndio nikapanga wiki hii nije nyumbani lakini kabla siku hazija fika ndio leo nikakutana na dada asha... Alafu pia  wazazi wangu?? Kwa hali ilivyokuwa ngumu, nikashindwa kumuacha kwakua alikuwa na mali nyingi sana.. Sasa nina kosa gani hapo wazazi wangu"



    Suria alimaliza kuongea lakini ghafla faima kadakia

    "kwahio mimi ndio basi"

    Aliuliza faima lakini wazazi wakasema

    "sisi hatumjui huyo jini.. Twende mkapeane talaka"

    Aliongea mzee Rashid huku suria akiwa na wasiwasi juu ya hilo...



    Walifika lakini suria ana wasiwasi kuingia ndani,....



    Sasa huku ndani shaimati bado yupo,

    "we maimati, nahisi nje kuna group la watu"

    Aliongea shaimati huku maimati akisema

    "najua toka wanaanza kuja... Na najua nia yao"

    "nia gani tena"

    "familia yake hainitaki"

    "na suria nae ana maamuzi gani"

    Kabla hajajibu, mama na baba na faima na asha waliingia ndani huku surian akiwa nyuma kabisa....

    Maimati na shaimati hawakutaka kujificha (kuto onekana)....

    "eti nyie jini ni nani hapa"

    Mzee Rashid Aliuliza huku maimati na shaimati wakiangaliana...

    "sisi sote hapa ni majini"

    Walijinu wote wawili maimati na shaimati.... Ghafla surian ndio anaingia huku akiwa mpole sana... Yani haamini kama leo anatenganishwa na mke wake... Sasa asha alishtuka kuskia ni majini mana asha ana urafiki na shaimati...

    "hata wewe pia ni jini?"

    "ndio"

    Ghafla mama akaingilia kati na kusema

    "sasa nataka nimjue mke wa mwanangu surian"

    "ni mimi... Shikamoo mama"

    Aliitika maimuna na kumsalimia

    "marahaba.... Kumbe majini manajua hata kusalimia"

    "mama, sisi hatuna tofauti nanyie, ni uwezo tu ndio tumekusudiwa nao"

    "sawa.... Sasa mwanangu,? Nimepata taarifa juu ya ndoa ya wewe na mtoto wangu wa kiume, tukiwa kama wazazi wa mtoto wake,... Tumekaa na kujadili swala hili kua, hatukubaliani na ndoa hio, kwani wewe ni kiumbe na huyu ni binadamu, hio ndio sababu ya kuikataa ndoa hio"





    Wazazi wa suria walijipachika roho ya ujasiri, kwa kumnusuru mtoto wao kwani kisheria katika dini, ndoa halali ya binadamu wote ama majini wote, na sio jini kwa binadamu, hivyo kwakua wazazi ni watu wenye kufuata dini hawakuhitaji mtoto wao aingie huko, kwani sio imani yao inavyo ruhusu,....



    Baada ya maimuna kusikia hivyo wala hakushituka, kwani swala hilo alisha lijua toka awali wakiwa nje ya jengo hilo,...

    "lakini mama, sisi tumefunga ndoa ya halali"

    Aliongea muna kama kujitetea kwa wakwe zake,

    "ni sawa, lakini hakuna dini inaruhu ndoa ya jini na binadamu, tafadhali sana mwanangu, hebu mpe uhuru mtoto wetu"

    Aliongea mama asha, tena kwa busara ya hali ya juu, kwani hapakuwa na ugomvi wa aina yeyote.

    Ni swala la kuelewana wazazi na maimuna,....

    "surian, toa maamuzi basi mume wangu"

    Muna alimwambia mumewe atoe maamuzi juu ya wazazi wake

    "mke wangu, kama wazazi wametia uwalakini, ulizani mimi nitafanya nini?? Ila nami sina raha na ndoa hii kutokana na masharti ya mali na hata ndoa kwa ujumla,... Nakupenda sana muna lakini umezidi kuwa na masharti mengi mno,... Hapa mjini nina miezi minne kama sio mitano, lakini umenipa sharti la kuto waona wazazi wangu,.. Tunamiliki kampuni wazazi wangu wanateseka mpaka mama yangu anakwenda kupewa kazi za vyooo... Mpaka nakosa raha na haya maisha mana nakosa uhuru wa maisha Kiukweli... Naona bora nibaki masikini mwenye uhuru na furaha nikiwa na familia yangu"



    Alimaliza kuongea surian kisha shaimati akadakia kwa kumwambia maimati kuwa

    "sasa nawewe? Ni masharti gani ulimpa ambayo hayapo? Kumbe umejiharibia mwenyewe, ungeanza kuonekana na familia yake"

    Aliongea shaimati kana kwamba hata yale masharti yote hayakuwa ya kweli....

    "samahani mume wangu, nilikupa masharti ili kujua uvumilivu na upendo juu ya wazazi wako, na sikuwa na maana nyingine"

    "sawa... Lakini ndio hivyo, wazazi wangu wamekataa ndoa yetu"

    Aliongea surian kisha shaimati akasema

    "muna,.. Hapo ulipo una ujauzito... Na ili urudi katika hali yako ya zamani, huyo mtoto ni halali ya viumbe vya sayari ya mwezi"

    Aliongea shaimati akiwa na maana kwamba kuna viumbe ambao wao ni kuchukua viumbe walio tumboni na hawazaliwi kama ilivyo kawaida bali anatoweka ndani kwa ndani na kumfanya mwanamke alio jitolea kiumbe hicho kurudi kama alivyo zamani, yaani bikra... Ni ukweli usiopingika kuwa majini wamepewa uwezo wa kipekee na sio kama binadam.....



    Maimuna alipewa muda wa kufikiri mana surian yeye yupo tayari kuachana na maimuna,.... Lakini sasa wakati maimuna anafikiria jibu la kutoa, kumbe alikuwa akiwasiliana na mkuu wao wa majini kuwa ndoa inavunjika kutokana na matakwa ya wazazi kwani mtoto wao na yeye ni mili tofauti kabisa....



    "sawa, ila ujauzito huu hatokuwa halali yangu wala halali yenu, ni sadaka kwa viumbe wa sayari ya mwezi,... Kama mtaridhia basi nami nipo tayari kwa hilo"

    Maimuna aliona hakutokuwa na baraka pale wazazi watakapo weka mgomo juu ya ndoa hio, hivyi kakubali ndoa ivunjwe kisheria, ila mtoto ni sadaka ya viumbe wa mwezini....

    "sawa, hata sisi tumekubali"

    Aliongea surian kisha mzee Rashid akashusha dua mana ni mzee wa msikiti hivyo kuna taratibu za kuvunja ndoa kisheria,....



    Ndani ya dakika 15 kila kitu kilikubalika na sasa surian na maimuna hawana ndoa tena, na mabaya zaidi mtoto sio haki yao wote, na ili iwe haki yake huyu maimuna basi kuna upande atatakiwa kuishi kama mjane, lakini kwakua bado anauhitaji ubikra, basi hana budi mtoto huyo kumtoa sadaka katika viumbe waishio mwezini,.. Na sadaka hio hutolewa wakiwa ndani ya himaya yao wao majini wenyewe,... Lakini licha ya ndoa kuvunjwa, maimati alimchukua surian na faima akawatoa pembeni..



    "surian, Kiukweli Nilikupenda sana, lakini kwa bahati mbaya wazazi wako hawakuridhia... Lakini hakuna budi juu ya hili kwasababu wazazi ndio kila kitu katika hii dunia,.. Nimekubaliana na yote na sina kinyongo na wewe wala familia yako... Katika masharti ya mali, haikuwa kweli kwani nilikuwa nakupima juu ya upendo kwa wazazi wako,..."



    Aliongea maimati huku surian akisema kuwa

    "sawa nimekuelewa, na sina kinyongo juu ya hilo, japo nimekuwa boss bila kutoa msada kwa wazazi wangu, lakini hakuna shida nitapambana kadri ya uwezo wangu ili niiwezeshe familia yangu"

    Aliongea hivyo surian akiwa na maana kwamba mali zote wanazomiliki kwa sasa zitapotea kwasababu mwenye mali ndio huyo anarudi atokako

    "tuachane na hilo... Faima?? Pia wewe ni mmoja kati mtu ulio changia mimi kukubali ndoa hii ivunjike kwani una upendo na heshima ya kipekee,.. Kiukweli unastahili sifa... Ninachokuomba, mpende surian, mpe kila atakachokikosa kwangu,.. Mwisho kabisa, mlinde kama nilivyokuwa namlinda mume wangu, ila kwa sasa anakwenda kuwa wako... Inaniuma lakini sina jinsi"

    Maimuna aliongea huku akitokwa na machozi kana kwamba asili yake ya ujini ndio chanzo kikubwa cha kumkosa surian,

    "usijali dada,... Kwani surian nilianza kumpenda toka tukiwa wadogo na nikaendelea kumpenda hata mlipokua naye huko.. Na nitaendelea kumpenda mpaka kesho"

    "ahsante sana kwa hilo faima... Mimi nadhani tumemaliza... Na hapa tutajiandaa kisha saa nane usiku tunaondoka rasmi,... Aaaaaaaaaa.. Surian, nyumba hii haitokuwa ya halali kwako, ila kampuni ya MICCO nakuachia ikiwa kama faida yako ya kuwa nami kwa upendo.. Faima?? Nimeacha kampuni kwa ajili yenu,... Hakuna masharti ilimradi muwe mnasaidia watu na kutoa sadaka bila kujali dini wala kabila na wala dhehebu na bila kuchagua umri"

    Aliongea maimuna huku surian na faima wakiitika kwa pamoja

    "sawa sawa dada muna, tutafanya kama ulivyo agiza"

    "sasa wewe surian unaniitaje dada"

    Aliuliza maimuna huku surian akijibu

    "lakini kwa sasa hatuna mahusiano, hivyo ni mtu na dada yake"

    Alisema suria

    "Kiukweli inaniuma sana lakini sawa, mie ni dada yako.. Nitakuwa nakuja kuwatembelea.."

    Ni maneno ya maimuna, na hapo ndio mwisho wa ndoa ya surian na jini maimuna kwani ni mtu na kiumbe kitu ambacho sio sahihi kibinadamu japo wapo walio oa majini lakini hakukuwa na kipingamizi, na kama wazazi wa surian wangelikubali, basi ndoa isingevunjwa.....

    "muna?"

    Suria alimuita maimuna

    "abee kaka"

    "pete ya kike unaisahau"

    Alisema surian huku akiivua pete ile..

    "hapana surian, hii pete nakuachia kama zawadi, mana najua Murati sabaha bado anahitaji kuwa nawe, hivyo hakikisha hii pete ya kike haitoki kidoleni mwako, mana ukiiitoa tu, Sabaha atakuingilia na kukutesa atakavyo"

    "ooohhhh ahsante sana dada muna... Shukrani sana kwa hili"

    PETE YA KIKE ambayo ni pete ya maimuna lakini kaamua kumuachia surian kama zawadi na iwe mlinzi badala yake... Waliagana wote kwa roho moja na hakukua na mwenye kinyongo kati yao



    Surian aliichukua familia yake yote na kwenda Kuanza maisha mapya akiwa na mchumba wake faima.. Wakati huo faima ana furaha ya hali ya juu kwani surian karudi kwake kama ndoto zake zilivyo dai kuolewa nae..



    Suria aliifikisha familia yake nyumbani kisha yeye akaelekea kazini akiwa na faima.. Tena hata asha alikuwapo katika gari hio,.. Sadiki alitetema baada ya kusikia honi ya gari ikipigwa nje ya geti,.. Sadiki alikua akimalizia kula lakini ghafla tu chakula kilishindwa kupita kooni, mana kafanya kosa kubwa sana ambalo hana imani kama litasameheka,... Ikiwa ni nyakati za saa nane mchana,....

    "shadya?"

    Aliita boss surian, kwa sasa kampuni ni yake peke yake... Mana mwanzo haikuwa yake kwani mmiliki ni mwanamke..

    "abee boss"

    "njoo pamoja na sadiki"

    Aliwaita wote wakakaa kikao chao kidogo pale ndani, na nyakati zote hizo kiwanda kilikuwa kikifanya kazi kama kawaida..

    "shadya,??? Kwa huruma yako juu ya mama yangu,... Kuanzia leo utakuwa meneja mkuu wa kampuni ya MICCO,. Halafu huyu faima huyu ambaye ni ndugu yako, huyu ni mke wangu mtarajiwa, hivyo ni boss wa pili kwenu..... Sadiki??"

    "yes boss, yes boss"

    "Kiukweli mimi sina hukumu juu yako. Ila niliskia mashtaka kuwa ulimtongoza dada yangu, na ndio sababu ya kumfukuza mama yangu.. Hivyooo...... Dada asha??"

    "abeeeee"

    "wewe ndio utajua cha kufanya juu ya Sadiki mana wewe ndie ulie shuhudia yote hayo.... Toa hukumu juu yake"

    Aliongea suria huku sadiki akitetemeka mana anaamini dhahiri kabisa asha hawezi kumuacha kwa makusudi alio yafanya juu yake...... Lakini asha hakukumbuka mabaya pekee japo mabaya ndio makali zaidi katika moyo wake, likiwemo swala la kumfukuza mama mzazi wa boss..

    "Nisamehe asha,.... Na sikua na nia ya kukuchezea, nilihitaji kukuoa asha"

    Aliongea sadiki ikiwa ni msamaha kwa asha...

    "surian, mimi naona tumuache tu.. Mana hakujua atendalo ila mi najua kajifunza kutokana na hili, hatoweza kurudia tena"

    Alisema asha huku suria akijibu

    "ahhh kama umemsamehe wewe, mimi sina shida..... Sasa sadiki, utakuwa meneja masoko. Mana nafasi yako ya awali nimempa shadya"

    "sawa boss, ahsante sana boss.... Asha nakushukuru sana dada angu"

    "ok.... Mimi naona kazi ziendelee na kama kawaida,..... Dada asha... Wewe utakuwa mkaguzi wa kiwanda kizima, mnaweza kushirikiana hata na wifi yako hapa"

    "hakuna shida..."

    "sasa,....mimi wacha nitoke, nikanunue kiwanja nijenge wazee watulie wale matunda yetu... Naomba mfanye kazi kwa bidiiiii"

    "sawa boss"



    Saaaa nane usiku ikiwa ndio saa ya safari ya majini hao, kama ilvyo ada ya wao kusafiri kila saa nane......



    Saa kumi alfajiri, shaimati na maimati wakiwa ndani ya himaya ya majini,... Na anahitai kuwa na bikra hivyo kisheria ni lazima utoe sadaka ya mtoto kwa viumbe waishio katika sayari ya mwezi,... Hivyo kabla hajaingia katika himaya ya mabinzi bikra, pale pae mwezi uliwaka kwa kupitiliza,... Ndani ya sekunde saba tu.. Maimuna hakuwa na mimba tena,... N uzuri zaidi hata bikra anayo kutokana na uwezo waliopewa viumbe hao... Binadamu hata utoa watoto kumi,. Bikra hupewi ng'ooooo,.. Sasa kuanzia hapo maimuna sio mama na wala sio mke wala mchumba wala demu wa mtu,.. Ni msichana mpyaaaa.....



    BAADA YA MIAKA 250 (MIAMBILI HAMSINI) KUPITA...



    Ikiwa ni miaka mingi imepita,... Koo nyingi zilizaliwa katika koo za suria, lakini mpaka sasa hazipo.... Kuna koo kama tano zimepita na hata koo ya sasa haijui kama kuna tajiri alie itwa surian,... Baada ya miaka hio surian kufariki dunia, ndugu na watoto wa suria walio wahuni waligombea mali na kuzifilisi mali hizo, hivyo uzao uliofuata baada ya uzao wa suria ukaendelea kuwa masikini kwani baadhi ya watoto wa suria walikuwa wahuni, hivyo waliuza mali zao na kuzitumia vibaya......



    Uzo ulizidi kuzaliwa lakini ni koo hio hio ya mzee surian aliofariki miaka 220 iliopita, hivyo surian alifariki akiwa na miaka 55 na kuacha watoto wahuni waliofuja mali mpaka kuteketea zote......



    IKIWA NI MIAKA YA SASA.... JIJINI ARUSHA......



    Uzao ulizaliwa mara dufu mpaka majina yakajirudia, yakafa, yakajirudia yakafa... Takriban mizao mitano imepita na yote imekufa....



    SASA HUU NI UZAO WA SITA KUTOKA UZAO WA SURIA,



    ikiwa ni familia ya kifukara sana inayo ishi jijini Arusha,.... Familia hio au uzao huo ulifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, alie itwa SUHAIBU.......



    Lakini sasa katika msitu mmoja mzito

    ikiwa ni mida ya jioni, yapata kama saa 11.30, alionekana dada mmoja wa makamo akiwa anahema sana huku akikimbia, nikisema msitu namaanisha msitu kwelikweli,.. Dada huyo alikuwa akikimbia mithili ya mtu anaetaka kuepusha maisha yake, kana kwamba kuna mtu au kitu kilichokuwa kikimkimbiza katika msitu huo,....

    "uuuuuu nakufa jamaniiii"

    Ni sauti ya dada huyo mwenye umri mkubwa tu, akiwa kama anaomba msaada katikati ya miti, majani, migomba, miba, na vingine vingi vipatikanavyo msituni,.. Lakini Kiukweli hakukua na mtu wala kitu kilichokuwa kikimkimbiza,... Alisimama mahali na kujifanya kama kajificha katika migomba iliostawi mpaka kuweka kiza kinene katika msitu huo, haijulikani alikuwa akikimbizwa na nini,...



    Lakini ghafla anaanza tena kukimbia kana kwamba kamuona adui wake aliokuwa akimkimbiza katika msitu huo,

    Mdada huyo hakufika mbali alinyongwa na kamba za miguu na kudondoka chini, sasa akawa hawezi hata kuamka hivyo akawa anapiga tu kelele kana kwamba mtu anaemfukuza yupo jirani yake, ila kwa jinsi tunavyo ona hakukuwa na mtu.. Lakini ghafla akiwa katika hali ya kujinasua,.... Alifika huyo aliekuwa akimkimbiza,......

    "uuuuuuuuuuuuuwiiiiiii"

    Alipiga kelele kubwa kuashiria hatari ya kudhuriwa na kitu fulani kisicho julikana.....





    MWISHO WA STORI HII YA PETE YA KIKE.



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog