Search This Blog

Thursday, 24 November 2022

PETE YA KIKE - 3

 

     

     



     

     

    Chombezo : Pete Ya Kike 

    Sehemu Ya Tatu (3)



    "yeeeeeeeee Murati sabaha,... Nilikua namsalimia suria"

    "ok, nina maongezi na suria kwa sasa kuhusu kazi"

    "yeeeeeeeee, Murati sabaha"

    Maimati aliondoka kwa heshima ya mkubwa wake, lakini alipofika mbali kidogo alimwangalia surian kisha akamtikisia kichwa kua asikubali... Kwani maimati alishajua kuwa murati Sabaha anataka kumpa surian pete ya kiume...

    "mlikua mnaongea nini na mati"

    Murati alimuuliza surian huku suria akisema kuwa

    "hapana, tulikuwa tunaongea kuhusu mazingira ya dubai"

    Alijibu suria huku Sabaha akitoa pete na kusema kuwa...



    "surian?,......nina zawadi nataka nikupe leo"

    Aliongea Sabaha huku akimpa pete, ambayo kwa juu ina dini la kijani, (GREEN GAINET)... Surian akaona mbona hio ni pete ya kiume, na hio aliopewa ni Pete ya kike... Suria alikumbuka maimati alimwambia asichukue kwa ishara ya kumtikisia kichwa...

    "hapana... Mimi sipendi kuvaa pete"

    Aliongea suria huku akiwa kaangalia chini kuashiria heshima ya hali ya juu

    "kwanini, hii ni zawadi nakupa tu"

    "Kiukweli siwezi kuvaa pete"

    Sasa kumbe kwa sheria za hapo pia ni kweli ni lazima uwe na pete, kwani wote hapo kwenye falme yao wana pete, lakini suria hawezi kuziona kwasababu yeye ni binadamu... Labda kama ingelikua ni duniani... Sasa kwa kawaida binadamu alio katika falme hio akikataa pete, hua anapewa siku saba awe keshaondoka ndani ya eneo hilo, na ndio mana maimati akatumia njia ya kumwambia akatae ili apewe siku saba za kuondoka.. Kwasababu kakataa kuvaa pete alio pewa na mkuu wa falme hio... Sasa kwa kawaida Murati sabaha yeye mwenyewe hutoa amri hapo hapo kuwa ndani ya siku saba arudishwe alipo toka,.. Lakini cha ajabu Murati hakutoa amri hio badala yake aliondoka kwa hasira kali,... Kumbe maimati alikua akisikiliza kwa umakini sana,.. Na hata yeye alishangaa kwanini suria hakupewa siku saba za kutoweka hapo falme za kijini.... Maimati aliondoka zake kabisa huku surian akitoa ile pete ya kike na Kuivaa,.. Maimati akapata ishara kuwa pete yake imevaliwa, alijiskia furaha sana kwani kwa sasa hakutokua na kiumbe yeyote atakaye weza kumrubuni suria kwa lolote lile.



    BAADA YA SIKU HIO KUPITA



    Huku duniani ikiwa ni asubuhi na mapema, asha akiwa kadaamkia kazini, lakini alishangaa hakukuwa na wateja kabisa,.. Yaani imekuwa kama zamani kwani hakujua kuwa pete aliokua kaivaa ndio ilikua kila kitu katika biashara yake,... Alikaa sana hapo saluni kwake na hata baadhi ya watu walishangaa kuona saluni hio haikua na wateja kama zamani, na mbaya zaidi hata asha sasa ameendelea kuvaa vinguo vya ajabu ajabu kama zamani,... Wakati akiwa hapo mara faima alikuja,

    "ooohh wifi, habari yako"

    Faima alimsalimia asha kama wifi yake

    "safi tu zakwako"

    "aah salama tu,... Leo kidogo haupo bize sana"

    Aliongea faima mana amezoea kumkuta na wateja wengi sana, takribani mwezi mzima na nusu...

    "ndio, haya niambie wifi yangu"

    "salama tu,... Hivi wifi, suria hajapiga simu kabisa"

    Faima alimuuliza asha kuhusu suria

    "mmmhh Kiukweli ni mwezi na kitu hivi sijui sura wala sauti yake"

    "eehh mungu wangu, suria wangu kapatwa na nini"

    Aliongea faima huku Chozi likimtoka haswa, mpaka asha akashangaa ni mapenzi ya aina gani mtu mpaka alie

    "usijali wifi, labda atarudi... Hata wazazi wangu kila siku ni kulia kwa sababu ya mtoto wao"

    Aliongea asha, lakini asha hua hampendi sana ndugu yake kwani amependelewa na wazazi wake kuliko yeye..



    Sasa huku majini ikiwa ni usiku wa saa nane,... Sabaha akiwa chumbani kwake, yaani majini ukiwakuta katika falme yao, utafikiri ni binadamu kama sisi,... Lakini wakija duniani ndio tunawaona ni viumbe wa tofauti sana,... Sasa sabaha akakaa na kujisemea katika moyo wake...

    "kisheria, kiumbe ama binadamu atakaye kataa zawadi kutoka katika falme yetu,.. Hutolewa mara moja... Lakini suria nampenda, nipo tayari kuoana nae, je nitawezaje kutoa amri hio??... Katika ndoto suria ni mtamu sana,.. Je vipi nikijaribu kufanya nae mapenzi kwa hali ya kawaida? Hapana, surian haendi popote.. Na usichana wangu huu, nahitaji kuwa na mfalme katika eneo langu,... Wacha saa 11 ifike nikapate penzi la mwisho kisha nifanye taratibu za kuoana naye"



    Aliongea Sabaha huku akitabasamu, kumbe yupo tayari kuoana na suria kwani kampenda kupita kiasi, na anahisi huyo ndio mwanaume Msafi aliobakia duniani, hivyo akimkosa ajue hatopata tena mwanaume mwingine Msafi kama surian,....



    Huku alipolala maimati, alikuwa naye ana mawazo sawa sawa na Murati sabaha, naye hakuwa na usingizi kabisa....



    "nawezaje kuishi na surian ingali keshaingia katika falme hii,... Murati ameshampenda surian na ndio mana humuingilia kila siku,... Kesho ni lazima nikapate ushauri toka kwa wazazi wangu nifanyeje niweze kuishi na suria kama mke na mume"



    Maimati alijiongelea maneno hayo huku akilala kama binadamu wengine, yaani wakiwa huku huezi jua kama ni majini, labda uambiwe mana wapo kama binadamu wa kawaida kwasababu wapo kwenye falme yao...



    Saa kumi na moja alfajiri Murati sabaha alijiangalia katika kioo. Sasa hivi ndivyo inavyokuwa pale ndoto inapomjia mtu... Sasa jini kabla halijaja kumuingilia mtu, ni lazima ajiangalie katika kioo na ndio maana watu hukatazwa kujiangalia kwenye kioo usiku, kwani hata viumbe aina hii hutumia njia hio hio... Sasa alipojiangalia katika kioo, kile kivuli kilichopo kwenye kioo ndicho alicho kituma kwenda kwa surian, lakini kivuli kile alikipachika sura ya msichana mwingine... Kisha akakituma kwa surian, afu yeye akaendelea kulala, hivyo kama kivuli kitafanikiwa kumuingilia suria, basi huku yeye anapata raha,... Sasa binadamu anajua anafanya mapenzi na demu wake au msichana yeyote yule, Lakini sivyo, bali anafanya mapenzi na kivuli cha jini... Na ndio maana ukiamka hujikuta umechafuka kwasababu kivuli hakiwezi kuingiza mbegu, na mhusika wa kivuli hicho yupo mbali hivyo mbegu hukosa pa kwenda na kutoka hovyo hovyo....



    Sasa Murati sabaha anajishangaa mbona hapati raha kama ilivyo siku zote,... Akaamua kwenda mwenyewe mpaka kwenye chumba cha surian,.. Kwenda kwake ni kitendo cha kupepesa macho keshafika eneo husika,... Lakini alishangaa kuona kwenye kitanda cha suria kuna mwanga mkubwa sana ambao hawezi kwenda eneo lile,...

    "shiiiiiti, nani kampa pete"

    Aliongea Sabaha huku akiwa kakasirika mno,... Murati aliondoka huku akisema....

    "kesho naitisha kikao nijue nani hana pete"

    Aliongea huku akirudi chumbani kwake, lakini leo hajapata utamu wa suria kama ilivyo kila siku...



    Asubuhi surian anaamka, kitu cha Kwanza alijishika maeneo fulani kama leo kaharibu tena au laaa,.. Lakini ikawa hajachafua

    "heeee... Kumbe ni kweli hii pete imenisaidia"

    Aliongea surian huku akikimbia nje kumshukuru maimati kwa kumpa pete hio,... Lakini sasa alipofika nje, alianza kuona tofauti tofauti.... Kwanza kabisa kaweza kuona wasichana wote waliovaa pete kama hio, na mwanzo hakuweza kuziona kwasababu hakuwa na pete, sasa ndio anaona pete hizo zikiwa nimeshamiri kwenye vidole vya wasichana,... Na alikuwa akiona kuna wanaume lakini sasa haoni tena wanaume,... Kwani mwanzo aliwekwa kiini macho ili ajue ni kama dubai, sasa anashangaa haoni mandhari ya kidubai dubai,... Japo ni kuzuri na bustani na majengo ni yale yale.... Mara maimati kaja... Maimati alijua kuwa surian keshaona utofauti wa falme hio...

    "mbona sielewi, au tumehama usiku usiku"

    Aliuliza surian huku maimati akicheka na kumwambia ukweli

    "samahani sana surian... Hapa upo kwenye falme ya majini, na sio dubai kama ulivyo ambiwa awali"











    Katika falme za viumbe ambayo vimepewa uwezo wa hali ya juu, haswa majini ambao wana uwezo wa kumiliki kila aina ya thamani hususan upande wa madini,... Viumbe hawa unapokwenda katika falme yao, kwa mara ya kwanza huezi kuona mandhari yao au huezi kuona maisha yao ya uhalisia mpaka pale utakapo ambiwa au kupewa kifaa maalum cha kuweza kukuonyesha..



    Kwa mfano suria toka aje hapo ufalmeni hakuwahi kuona viumbe hao wamevaa pete vidoleni mwao, na pia alikua akiona wanaume lakini kwa sasa haoni mwanaume,... Hii ina maana kwamba falme hii inaongozwa na mwanamke hivyo hakuna mwanaume anayeweza kuongozwa na mwanamke, labda mwanamke huyo awe na mume ndipo wanaume watakubali kuongozwa na wote wawili, lakini sio yeye peke yake.... Yaani maisha yao yapo kama binadamu wengine, nao kuna wajeuri vile vile kama ilivyo duniani, ila majini hawa wakija duniani ndio hua tunawaona tofauti na Waziri kupita kiasi.. Lakini ukiwa huku kwao, utawaona ni wa kawaida tu, kwani nao wana maisha kama sisi tulivyo,...





    Sasa suria haelewi baada ya kuona baadhi ya mandhari ya kidubai dubai haoni,... Alikuwa akiona wanaume wengi sana pale anapotoka nje ye jengo, lakini sasa hivi haoni, zaidi ya kuona warembo tupu tena ni wazuri hakuna mfano, sema sio wanene wala wenye maumbile ya kichina,..



    "samahani sana surian... Hapa upo kwenye falme ya majini, na sio dubai kama ulivyo ambiwa awali"

    Aliongea maimati ili kumuweka wazi surian,.. Wakati huo huo shaimati naye kafika eneo hilo,...

    "ati unasemaje maimuna"

    Alishangaa surian huku akitoa macho kwa mshangao wa hali ya juu

    "huo ndio ukweli surian, na mimi sikutaka uje huku.."

    Aliongea maimati sasa shaimati ile kufika tu

    "na huyu naye ni jini"

    Suria alimuuliza maimati, lakini kabla maimati hajajibu, shaimati akajibu na kusema

    "hata huyo unaye muuliza mwenyewe ni jini"

    Aliongea shaimati, huku surian asiamini kile anachokisikia katika masikio yake,....

    "kwanini lakini mmenileta huku.. Wewe dada wewe kwanini umenileta na kuniambia kuna kazi... Yaani mimi nakuja kuishi na majini huku?.. Hapana, nataka nirudi nilipo toka"

    Aliongea suria huku akitaka hata kulia,... Lakini kabla hajajibiwa, ghafla likapigwa la mgambo, wanawake wote wajipange mstari mmoja kwani malikia ana maongezi nao,... Wapo waliokuwa tayari katika msitari na wale wengine kama akina maimati na shaimati, wakati huo hakuna anaye jua sababu ya la mgambo hilo kulia,... Malkia Sabaha anakuja akiwa katika kiti chake,...



    "nadhani kuna sheria inavunjwa katika falme yangu"

    Aliongea malkia huyo au Murati sabaha, tena akiwa kakasirika kupita kiasi

    "na tena kuna mwenzenu ananifuatilia katika njia zangu"

    Alizidi kuongea Murati sabaha huku majini wote wakiwa wanaangalia chini kwa heshima juu ya mkuu wao, wakati huo surian anaagalia kwani naye ana pete hivyo kila kinacho endelea katika falme hio naye anakijua kwakua anamiliki moja ya kifaa cha viumbe hao,....



    "nataka wote mnyooshe viganja vyenu"

    Aliongea Murati sabaha,. Na hapo ndipo maimati akagundua sababu ya kuitwa la mgambo,

    "yeeeeeeeeee Murati sabaha (ndiiioo malkia sabaha)"

    Walikubali kunyoosha viganja vyao na wote walikua na pete, lakini maimati yeye hakuwa na pete kidoleni kwake,....

    "maimati"

    "yeeeeeeeeee Murati sabaha"

    "nakuhitaji kandikuti (chumba cha mahojiano)"

    Malkia aliondoka zake kwani aliomtaka alimpa, na wengine wakaendelea na shughuli zao za kawaida,...



    Tukija huku duniani katika nyumba ambayo anaishi faima ambaye ni mchumba wa surian,.. Ikiwa ni suku wa saa mbili, lakini kule kwenye falme ya majini, ni saa mbili asubuhi, lakini huku duniani ni saa mbili usiku



    "mama unamuona mwanao, kula hataki, kulala hataki... Kisa ni yule mjinga jinga wake alie mtoroka"

    Aliongea zamina ambaye hakuridhika na upendo wa wawili hao,...

    "zamina, hebu heshimianeni basi... Wewe umeshakua na yeye keshakua, anampenda mtu wake, kwanini unamfuatilia mdogo wako"

    Mama alivunja ukimya baada ya kuona zamina anamsumhua faima

    "lakini mama... Jitu lenyewe hata kwao hawajui kaenda wapi, familia yake yenyewe inalia kila siku juu ya mtoto wao,.. Ina maana na huyu pia"

    Zamina aliongea tena kwa hasira sana mana anampenda sana mdogo wake, na hata sasa kazi hana kwa mawazo juu ya surian...

    "labda dada yake anajua"

    "anajua wapi, tena dada yake sasa hivi anafanya kazi mpaka anajenga nyumba kule bondeni... Asha atakuwa kamtoa mdogo wake mama sio bure, hivyo nataka faima atulie"

    Zamina aliongea lakini faima alijibu kuwa

    "dada zamina, Kiukweli nakuheshimu sana na kuuheshim mchango wako... Lakini katika swala la kupenda surian, naomba usiliingilie, niache kama nilivyo"

    Aliongea faima kisha akaondoka na kukimbilia chumbani kwake, na kujilaza kwa hasira



    Sasa tukija Huku kwa akina maimati na malkia wake

    "nani kakupa amri ya kutoa pete na kumpa binadamu ambaye huendani naye"

    Aliongea Murati sabaha huku maimati akiwa hana hata wasiwasi, kwani alifanya hivyo kwa niaba ya kulinda penzi lake

    "nimefanya hivyo kwa niaba ya kumlinda"

    Alijibu maimati huku Sabaha akiendelea

    "ivi huoni ulicho kifanya ni kinyume na sheria za asili yetu"

    "lakini ukumbuke hata wewe ulichokifanya kwake kila siku ni kinyume na taratibu za asili yetu, hio ni tabia ya mashetwaini, lakini inashangaza kuwa nawe waifanya"

    Aliongea maimati bila woga kwani yupo tayari kwa lolote na hakukuwa na kosa kama alilo nalo malikia Sabaha,....

    "mati? naona sasa umekuwa, mpaka kufuatilia hatua zangu"

    "ni kweli, na ni kwasababu unayemwingilia nampenda vilevile na sifa zake hizo hizo"

    Hapo Murati sabaha alishangaa, ina maana kumbe yeye hako peke yake ambaye kampenda surian kutokana na sifa alizo nazo..

    "sasa mulimleta wanini ingali unampenda, na unajua kuwa asili yako na asili yake haviendani"

    Aliongea Murati bila kujua kuwa hata yeye na surian haviendani, bali wakifuata njia sahihi wanawaza kuishi jini na binadamu kama mke na mume, ila ni mpaka pande zote waridhie hali hio...

    "lakini Murati, mbona hata wewe huendani na binadamu.. Tena ni kheri yangu mimi nina asili mbili"

    "sasa nasema hivi, ile pete ni kwa ajili yako, nataka uichukue haraka sana, kwani ipo yakwake ya kiume na sio ile ya kike"

    Aliongea Murati sabaha kisha akaondoka,... Lakini maimati alijisemea katika moyo wake kuwa

    "siwezi kumpokonya suria Pete, kama unamtaka fuata sheria"

    Aliongea maimati kisha naye akaondoka....



    BAADA YA WIKI MOJA KUPITA



    Ikiwa ni siku ya Jumapili katika falme ya majini,.... Murati akiwa katika kiti chake cha umalikia, alikuwa kakasirika mno, kwani toka majuzi hawezi kumfaidi surian kupitia ndoto, alimwita maimati sio chini ya mara tatu kumtaka aichukue pete hio, lakini hakutaka kuichukua.. Na pete hio surian hua anaivua mchana, kwani anajua msaada wa pete hio ni usiku tu,... Na hata Murati sabaha akiona pete ya surian imevuliwa hawezi kuichukua kwani hawaruhusiwi kushika pete ya jini mwenzie, na ndio mana hata siku ile kule duniani, asha alimuulisha shaimati kuwa akiipata hio pete amletee, lakini shaimati akakataa na kumwambia ukiipata we ivae,.. Hio ina maana hawaruhusiwi wao kwa wao kushikiana pete, yaani hata kuigusa hawezi,... Sasa surian yeye anaivua pete nyakati za mchana tu, wakati Murati anataka usiku...



    Siku moja surian akiwa katulia mahali na anajua kuwa hapo yupo katika falme ya majini,... Hivyo kitu cha kwanza ni muoga afu pia hatamani tena kuishi hapo,... Sema msaada wa kutoka hapo ndio hajui, akiwa katulia kwenye bustani ambayo huifanyia kazi ya kuitunza kila siku,... Murati sabaha alikuwa akimwangalia surian kwa mbali sana, tena wakati huo surian hakuwa na pete,... Sasa kitendo cha surian kutokuwa na pete, ni nafasi moja kubwa sana ambayo Murati anataka kuifanya,.. Na Murati sabaha sio kuwa ni mkubwa, bali ni binti mdogo sana sema cheo chake ndio kikubwa,



    Surian alijikuta anaamka pale alipo,.. Sasa kumbe Murati sabaha alikuwa akimuita kupitia kidole,... Hivyo Murati katumia nguvu za kijini kumuita surian, na yote hio ni kwasababu hakuwa na pete kidoleni,.. Mana kama surian angelikuwa na pete, hata Murati asingeweza kumuita... Sasa surian kawa kma zezeta na wakati huo anaingia moja kwa moja katika chumba cha Murati sabaha... Sasa Murati sabaha anakwenda kuvunja amri ya sita na surian na hio sio ndoto bali live bila chenga, na itakuwa ndio mara ya kwanza surian kufanya mapenzi, na pia itakuwa ni mara ya kwanza Murati sabaha kufanya mapenzi,.. Nyakati hizo kila kiumbe kilikuwa katika mazingira yake,... Hivyo ndani hawakujua kilichokua kikiendelea



    Lakini baada ya masaa mawili, kitanda cha Murati sabaha kilitapakaa damu chote,.... Na huku nje majini wanapata ishara kwa harufu ya damu ambayo inasikika katika falme yao takatifu....









    Kumbuka kila kiumbe kina maisha kama sisi binadamu tulivyo,... Hata sisi tuna nguvu zetu ambazo wao hawana, na wao wana nguvu zao ambazo nasisi hatuna, hivyo tumetengwa tusiishi kwa pamoja ispokuwa kwa matakwa ya viumbe husika, kwani vimependelewa zaidi kuliko binadamu, hivyo ili uweze kuishi navyo ni lazima kuwepo na makubaliano kati ya wewe na kiumbe husika,... Haswa haswa kiumbe kikubali kuishi na wewe,...



    Hivyo Mwenyezi Mungu kaweka mipaka juu ya tendo la ndoa liwe ndani ya ndoa pekee na sio nje au kabla ya ndoa... Na mipaka hii haikuwekwa kwa ajili ya binadamu pekee bali hata viumbe wana mipaka kama ya binadamu, na endapo wanapokiuka amri za mungu nao huadhibiwa au kutolewa nje ya utawala wa majini wema,... Tuchukulie kama shetani, shetani alikua ni malaika pekee wa mungu, lakini alikwenda tofauti na amri za Mungu hivyo akalaaniwa na kutolewa katika utawala wa malaika wa mungu



    Hivyo yeyote atakaye kwenda tofauti na amri za mungu ni lazima adhabu imshukie, japo adhabu za binadamu huzikuta baada ya kifo, ila viumbe huadhibiwa papo kwa hapo bila subira ya kifo chake



    Wakati surian anaingia katika chumba cha Murati sabaha, akiwa hana akili hata chembe... Mpaka hapo Murati sabaha kafanya kosa kutumia nguvu ndani ya utawala ambao sii lazima kutumia nguvu za kijini... Surian hakushangaa kumuona Sabaha akiwa kama alivyo zaliwa kwani akili haikuwa yakwake.... Pale pale suria naye alianza kupambua nguo zake kama Sabaha alivyo... Murati sabaha ni binti mchanga, sema alipewa cheo hicho na mkuu wa majini katika bahari hio, na wote hakuna alio wahi kufanya mapenzi kabla, hivyo hapo ni kutoana bikra kwa kwenda mbele...



    Mapenzi ya kulambana yalianza wakiwa watupu kama walivyo zaliwa,.. Jini akikubali ulale naye, basi hua katika mwili wake anakuwa binadamu kabisa, mana wapo majini ukiwafunua huni njia ya kupitishia uume, au ukakuta nywele nyingiii hata njia ya kike huioni,.. Yaani hua wanafanyaga vituko ili kukutisha au kukukatisha tamaa... Lakini kama kakupenda na yupo tayari kwa tendo, basi atakuwa kama alivyo binadamu mwingine,.... Murati alishikwa na kulegea kana kwamba yupo tayari kwa kuingiliwa na surian,.. Na hapo hatumii nguvu zozote zile, hivyo surian keshanogewa au huenda akahisi ni ndoto tena... Kati yao hakukua na aliekuwa akizungumza kwa raha ya mpapasano uliopo milini mwao,...



    Sabaha aliishika zakhari ya surian kisha akaiweka sehemu husika,..



    Nje ya jengo hilo na himaya yote ulitokea mtetemeko usiojulikana sababu zake ni nini, kwani haikuwahi kutokea tetemeko kama hilo... Ikiwa na maana kwamba toka kuzaliwa kwao hakuna alio wahi kufanya mapenzi ndani ya himaya hio.... Majini waliokua wanashauriana juu ya tetemeko hilo, na kuamua kwenda katika jumba la kifalme ambalo anaishi (Queen Murati sabaha) ambaye ndio kiongozi wao, hivyo wanakwenda ili kupata ushauri huenda akawa anafahamu juu ya tatizo hilo,...



    Huku chumbani viuno vilikuwa vikilindima, na wakati huo surian alikua anakaribia kufika kileleni,... Murati keshakojoa mara kadhaa kutokana na jinsi alivyo jiachia kama binadamu,.. Yaani akijiachia kama binadamu basi huridhika kama binadamu, lakini akiwa katika hali ya ujini, kumridhisha utakuskia kwenye bomba tu...



    Surian alikakamaa kwakua alikua akifika kileleni (anamwaga nye**).. Sasa ikumbukwe kuwa Sabaha ni bikra na kwa kawaida bikra ni lazima uchache wa damu kuonekana,.. Lakini sasa cha ajabu, damu za bikra zilianza kumtoka mdomoni badala ya kwenye uke wake...., sasa surian anashangaa mbona Sabaha anatoka damu mdomoni,... Sasa sababu alijua tayari kesha haribu, hivyo alijinasua kwenye mwili wa suria... Ile anatoka tu, Sabaha alianza kutapika damu hapo hapo kitandani, tena alitapika mfululizo na wakati huo tayari keshajinasua katika mwili wa suria baada ya suria kumaliza kujikamua, tena kakojolea ndani...



    Suria yeye kadua kwani kitanda chote kilitapakaa damu ambazo Sabaha alikuwa akitapika.... Ghafla sabaha alianza kuota meno marefu mithili ya shetani, mara kucha zake nazo zikabadirika na kuwa ndefu kupita kiasi,... Pale pale alianza kuzilamba zile damu alizotapika mwenyewe, hio ni ishara ya kwamba, murati Sabaha kesha laaniwa kwa kitendo cha kufanya mapenzi haramu, tena katika himaya takatifu...



    Huku nje majini walipofika katika jengo la Murati sabaha walianza kuhisi harufu ya damu iliokuwa katika jengo hilo na waliokuwepo hapo walikuwa majini wasiopungua 50, ni watoto wazuri kupita maelezo na wote ni bikra, lakini kati ya hao kuna wawili wenye asili ya kibinadamu, ambao ni shamimu (shaimati) na maimuna (maimati)... Na himaya ina majini wengi lakini kwenye ngome hio walionekana majini zaidi ya 50,...



    Lakini wakiwa hapo nje walisikia muungurumo mkali sana ukitokea ndani,... Wasichana wote waliamua kutumia nguvu za kijini ili kujua kulikoni ndani kwa malikia wao,.. Lakini walipozitumia nguvu zao, waligundua ndani kuna tatizo,... Maimati alijua surian yupo ndani hivyo alikuwa wa kwanza kuingia ndani,...



    Sasa huku chumbani kumbe Murati anataka kumbadilisha suria kufuata njia zake, mana sabaha keshakuwa shetani na sio jini mwema... Sasa ile anamsogelea suria, ghafla maimati alitokea na kuzuia swala lile, nyakati hizo, suria alikuwa kama alivyo zaliwa na maimati kajua hapa mapenzi haramu yamefanyika hivyo.. Sasa maimati alichukua shuka na kumzungushia surian ili wanaokuja wasiweze kushuhudia maungo yake..



    Pale pale Sabaha alitoweka akiwa kesha haribika sura mpaka mwili wake, uzuri wake wote uliisha miguu ilikuwa kama ya mbwa,... Majini wengine wanafika wanakuta Sabaha ndio anamalizikia kutoweka katika ngome hio, yaani ndio tayari kesha laaniwa na kuwa shetani moja kwa moja,...



    Nje ya jengo hilo, ghafla alikuja mkubwa, yaani huyo ndio mkuu wa wakuu wote,... Majini waliokuwa ndani walitoka pamoja na surian, wakati huo mfalme mkuu akiwa katika kiti chake cha kifalme...



    "Sabaha kalaaniwa moja kwa moja kitokana na uchafu alio ufanya... Na kuanzia leo, sihitaji kumuona huyu kijana katika ngome hiii"

    Aliongea mkubwa huyo huku majini wadogo wakishangaa, kwa kusikia kuwa Sabaha kesha laaniwa moja kwa moja....

    "na kuanzia leo, sitaki kuona binadamu katika himaya yetu... Hii ni himaya takatifu, na huyo kijana pamoja na usafi wake hatakiwi kuwepo hapa"

    Aliendelea kuongea mkuu huyo lakini maimati akaomba kuongea kidogo

    "tusamehe sana sisi... WAIRATI SARIKA (mfalme sarika)"

    Maimati aliomba radhi kwani wao ndio walimleta binadamu huyo katika himaya yao,...

    "hukumu kaitoa Allah subhanahu Wata allah"

    Aliongea wairati sarika ambaye yeye ndio mkuu wa majini yote mema katika bahari zote duniani...

    "yeeeeeeeeeee wairati sarika"

    Waliitikia kuwa wamekubali kutofuata njia aliopita Sabaha,

    "kesho na mapema, sitaki kuona binadamu kamili ndani ya himaya hii"

    "yeeeeeeeeeee wairati sarika"

    "na kuanzia leo, nateua malikia mwingine msafi kama mlivyo wasafi"

    Aliongea mkuu wao huku wengi wakiwa na furaha kwani kuna wengine hawakupenda uongozi wa Sabaha, haswa wale wenye asili mbili

    "maimati utashika nafasi ya sabaha"

    "Noreeeeeeeee wairati sarika (hapana mfalme sarika)

    Maimati alikataa cheo hicho cha umalikia

    "kwanini hutaki? Mana Sabaha alikuwa na asili moja, sasa nateua mwenye asili mbili kisha hutaki kwanini?"

    "yeeeeeeeeeee wairati sarika... Ni kwasababu, nami kwa sasa nahitaji mfalme pale nitako kuwa malikia... Na huyu kijana nilimpenda na Natamani awe mfalme wangu nami niwe malikia wake... Lakini kwakua humtaki awepo katika himaya hii... Basi naomba nikaishi naye duniani, hivyo kwa cheo unachonipa sitaweza kukifanyia kazi ipasavyo... Ni hayo tu"

    Aliongea maimati na kuwashangaza majini wenzake kwani walikua hawajui kuwa naye anampenda surian,.. Na wakati huo surian anashangaa, atapendwaje na jini, na atafunga nae ndoa kivipi na wakati ana mpenzi wake...

    "shaimati, nafasi ya sabaha utaishika wewe, na kila jambo nipate taarifa sawa"

    "yeeeeeeeeeee wairati sarika"

    "maimati, kwakua kijana huyo hakuwa mchafu na mpaka sasa bado ni Msafi, hivyo ruksa kuishi nae, lakini ndoa itafungwa hapa hapa ili wenzako tuweze kukusherehekea... Na unaruhusiwa kumiliki madini na malizo zote ukiwa duniani, ila huruhusiwi kurudi ujinini ukiwa bado upo ndani ya ndoa na mtu huyu... Na ukirudi utaishi katika himaya ya KAIRUTI, ila sio hapa tena.. Kwani hutokua msafi tena"



    Aliongea mkuu huyo na licha ya masharti yote hayo bado maimati kafurahi mno... Himaya ya KAIRUTI ni himaya ya majini ambao walisha olewa, na wana watoto.. Na ndio huko hata wazazi wa maimati na shaimati walipo... Ukishapenda kuolewa na binadamu huzuiliwi, Ilimradi awe Msafi.. Na hapa surian bado ni Msafi kwasababu alipofanya naye ni jini kamili na sio binadamu mwenzie,... Labda mbaya zaidi sabaha angelikua na asili mbili hapo ndio ingelikuwa mbaya..

    "yeeeeeeeeeee wairati sarika, na lini tunafunga ndoa"

    Maimati alikubali masharti na kuuliza lini wafunge ndoa

    "kwakua sihitaji kuona binadamu katika himaya hiii... Ndoa iwe kesho na hio hio kesho muondoke"

    Aliongea sarika lakini surian alitahamaki kwa sauti

    "haaaaaaa, ndoa ni kesho?"

    Majini wote waligeuka pamoja na wairati sarika, kwani imeonekana wawili hao hawakuambizana swala hilo,... Na ni kweli, surian anajua anapendwa na maimati, lakini hakuambiwa wafunge ndoa... Sasa hapo kazi ipo na ndoa haifungwi kama upande mmoja usipo ridhia, sasa je? Maimati atafanya nini pale surian akikataa kuoa jini











    Swala la kuoa jini sio tatizo, ila tatizo ni hayo masharti ya jini kuendana nayo jinsi yanavyo takiwa uendane nayo....



    "haaaaaaa, ndoa ni kesho?"

    Alitahamaki surian kuwa ndoa ni kesho?

    "maimati?, inaonekana hili swala unalazimisha"

    "Noreeeeee wairati sarika,.. Sikumjuza swala la siku husika"

    Alijibu maimati, huku suria akiwa katulia kimya kwani toka ajue hii ni himaya ya majini, basi kawa mpole na hataki kuongea sana kama ilivyo awali,...

    "shaimati? kuanzia leo utakuwa Murati shaimati"

    Aliongea sarika huku wasichana mabikra wakishangilia kana kwamba wamemkubali shaimati kuwa malikia wao,... Na shaimati naye alikikubali cheo kile bila pingamizi, ila siku naye akipata mwanaume wa kumuoa, kama ni binadamu kama surian, basi watakwenda kuishi duniani, lakini kama ni jini mwenzie basi wataishi hapa hapa ujinini,.. Hivyo sababu ya maimati kuambiwa akaishi duniani ni kwasababu surian sio jini bali ni binadamu wa kawaida,... Na kama surian angelikuwa ni jini basi wangeishi huku huku ujinini...



    Basi hali ilikuwa hivyo,... Wairati sarika aliondoka zake na kikosi chake cha majini hivyohivyo, kwani hua anakuja wakati wa tatizo tu,.. Sabaha sasa sio jini mwema, bali ni jini mbaya ambaye ndio shetani mwenyewe,... Kwa sasa tuna Murati shaimati, na sio Sabaha tena....



    Usiku wa siku hio maimati alikwenda chumbani kwa surian, kwenda kuzungumza naye, kwani kesho ndio ndoa yao ili wakaishi wote... Suria haamini kumuona maimati anamjia kwa magoti, kweli JINI MAIMATI kampenda surian tena kaoza kabisa



    "suria, nimekuja mbele yako ukiwa kama mume wangu mtarajiwa,.. Ni kweli mimi ni jini, ila nina asili mbili... Surian, nakupenda kesho tufunge ndoa. Nimekubali kujitenga na majini wenzangu kwasababu yako,... Surian, mimi ni jini, lakini nina mwili kama binadamu, nina upendo juu ya binadamu, nitakulinda wewe na familia yako, nitakuja na nitakuheshim ukiwa kama mume wangu, nipe nafasi surian"



    Maimati Aliongea maneno mengi na wakati huo machozi humtoka kama maji kuonesha kwamba yupo Siriasi na jambo hilo....

    Suria alipatwa na huruma huku akisema

    "lakini mimi nina mchumba"

    Aliongea surian, lakini maimuna hakushtushwa na hilo

    "sina uhakika na hilo, lakini pia mchumba sio mke... Surian, sidhani kama huyo anakupenda kuliko mimi... Nikubalie tukaishi duniani mimi na wewe, hebu ona, nimeacha majini wenzangu kwasababu yako... Suriiiiiiiii... Nipe nafasi, au unataka niwe kama sabaha"

    Aliongea maimati huku akiendelea kulia



    Kesho yake ikiwa ndio siku ya harusi, palikuwa na umati wa majini wote, wale waliozaa au walio olewa, na majini ambao ni mabikra... Bustani ilijawa na mavazi meupe tupu ikiwa ndio mavazi yao waliyo yavaa na ndio asili yao,..... Surian alikubali kumuoa maimati ambeye ni jini mwenye asili mbili,...



    Ilipofika saa nane usiku ikiwa ndio nyakati za kutoka ujinini kwenda duniani, wakiwa wanasindikizwa na majini wenzao mpaka duniani, familia ya maimati ilifurahi sana kwani hata wao kuna jini na kuna binadamu, ila wao kuna njia walitumia na kuruhusiwa kuishi ujinini kukiwa na binadamu ila kwa sasa hata huyo binadamu tayari keshakuwa jini kwani kaishi na jini miaka mingi mno, hivyo mama yake maimati sio jini, ila baba yake maima ndio jini, hivyo kuna matakwa ukiyatimiza basi unaweza kuishi ujinini bila tabu na ukubali kwa mabadiliko ya kutoka binadamu kuwa jini kwa kukabidhiwa baazi ya nguvu na kuzikubali kwa moyo wote, sasa kwa upande wa suria yeye hawezi kukubali kuwa jini wa kukabiziwa asili,... Kwani asili nzuri ni ile ya kuzaliwa nayo



    Saa nane usiku wawili hao wanatua duniani wakiwa ni wanandoa,.. Surian ana miezi kadhaa toka atoweke duniani na kupelekwa ujinini pasina yeye kujua kuwa anakwenda ujinini,..



    "sasa hapa, tunakwenda nyumbani kwetu"

    Aliongea suria huku maimati au maimuna akimjibu mumewe kuwa..

    "hapana mume wangu,... Ipo nyumba maalum kwa ajili yetu"

    "nyumba ipi hio"

    "usijali, hilo ni jambo dogo sana"

    Maimati alimshika mumewe mkono, ni kitendo cha kufumba na kufumbua surian anajikuta yupo ndani ya jumba la kifahari kama lile alilokuwa akiishi kule ujinini, ambalo kila kilichopo ndani ni dhahabu tupu,...

    "hapana ni wapi"

    Suria aliuliza kuwa hapo ni wapi, kwani walitua ndani moja kwa moja

    "hapa, ni tanga mtaa wa UZUNGUNI"

    "mmhhh huku kwa watu wenye pesa"

    "kwani wewe ni fukara?"

    "sina uhakika na jibu langu"

    "twende tukapumzike mume wangu"

    Aliongea maimati huku akimvuta mumewe mkono, ikiwa ni siku wa saa tisa...



    Wakiwa kitandani suria alikuwa na jambo la kuongea

    "muna?... Kesho nataka twende kwa wazazi wangu wakakuone na wajue nimekuoa wewe"

    Aliongea suria huku maimati akisema

    "ni sawa, lakini kwa sisi sheria za majini, mpaka zipite siku saba ndio tunaweza kutambulishwa na kuonwa upande wa wakwe"

    "duuuuuuu.... Mbona sheria kali hivyo"

    "samahani mume wangu"

    "alafu kingine, nguvu zako sizihitaji katika maisha yangu"

    "siwezi kutumia nguvu za kijini niwapo duniani, ispokuwa sinto onekana mara kwa mara"

    "kwanini sasa"

    "suria, sisi majini tuna uzuri uliokithiri, yani nitaangaliwa sana... Afu istoshe binadamu watakuja kunijua mimi ni jini"

    Aliongea maimati huku suria akichoka kwa masharti anayo pewa..

    "mmmhh kingine tena"

    "sharti lingine, chumba namba tatu kimejaa pesa na vitu vya thamani, tafadhali, pesa hizi huruhusiwi kumpa mtu mwenye pesa... Huruhusiwi kunywea pombe,.. Huruhusiwi kuzifanyia starehe yeyote ile,.. Mwisho haruhusiwi kuitumia mtu yeyote yule ispokuwa wewe na mimi tu"

    Aliongea maimati, wakati huo wakiwa kitandani na hapo ni mkoani Tanga,... Ikiwa ni usiku wa matisa,

    "tutaendelea na biashara gani hapa mjini"

    Suria aliuliza swali hilo huku maimati akijibu kuwa

    "tutafungua kampuni ili binadamu wasitutilie shaka, kwani hata tusipo fanya kazi, pesa haiwezi kuisha... Ila tutafungua kampuni ambayo itaendesha kiwanda cha kutengeneza nguo za Kiislamu"

    "kwahio hata tusipo fanya kazi pesa ipo"

    "miaka 10000 (elfu kumi) pesa ipo"

    "duuuuuu, ni pesa kiasi gani hizo zenye kuishi miaka elfu kumi na zisiishe"

    Suria alikuwa na maswali mengi mno, lakini maimati alimshika mkono mpaka kwenye chumba ambacho kina pesa na vitu vya thamani

    "haaaaaaaaaaaa..... We maimuna, hapa ni benki, au ni nyumbani kwetu"

    "hapa ni nyumbani kwetu.... Sikiliza, mimi ni jini... Sisi ndio wamiliki wa madini yote yatokayo ardhini"

    Aliongea maimati na hapo ndipo surian akatulia....

    "mmmmhhh sawa, kwahio kesho ndio tunafanya mpango wa hio kampuni"

    "hapana, kesho, tukanunue usafiri binafsi, kisha tununue mabasi matano kwa ajili ya wafanyakazi kupelekwa na kurudishwa majumbani"

    "ok basi, lazima nifike kwa wazazi wangu nikawaone kisha tuelekee kwenye manunuzi"

    "hapana... Yatakiwa umalize siku saba ndipo uende kwa wazazi wako"

    "munaaaaaaa... Mbona masharti makubwa hivyo, kumbuka wale ni wazazi wangu... Inatakiwa nikawaone angalao niwape chochote nao wainjoi maisha"

    Aliongea surian tena kwa hasira mno mana masharti ya huyu dada yalizidi mno...

    "nimesema hivi, pesa hii tutaitumia mimi na wewe tu,.. Na watakaopaswa kutumia pesa hii, ni wafanyakazi kwenye kampuni yetu mpya, hivyo tutasaidia watu kupitia kazi na sio kumpa mtu bila kazi"

    Aliongea maimati tena kwa upole kwani anajua thamani ya mume mbele za mungu hivyo atakiwi kumkemea ila ni anatakiwa kumtuliza



    Usiku huo huo faima hakulala kabisa, yaani kama alijua mchumba wake yupo duniani usiku wa leo,...

    "mi naona unataka kufa faima,. Yaani hulali wewe usiku kucha... Ni miezi mitatu toka surian afariki dunia kwa kutolewa kafara na dada yake... Lakini wewe hutaki kuamini hilo, weww ni mtu gani lakini mdogo wangu"

    Aliongea zamina kwani kwa sasa mji mzima kwa wale wanao ijua familia ya surian, wanajua dada yake suria ambaye ni asha kamtoa surian kafara ili biashara yake inoge,.. Lakini mchumba wa surian hakutaka kuamini hilo japo kweli asha alikuwa akipiga bingo la pesa katika saluni yake,..

    "dada, hebu niache... Mimi nawaza kesho nikaombe msamaha kwa boss nirudi kazini... Lakini pia siwezi kumsahau surian wangu, na pia Sintokaa kupenda mwanaume yeyote yule hapa duniani"

    "acha ujinga faima,... Hebu lala, kesho nikushauri kitu"

    "sina shida na ushauri wako, mana hauna msaada kwangu"

    "faima, kumbuka mimi ni dada yako"

    Aliongea zamina huku faima akivuta shuka

    "nyie washenzi, usiku wote huu mnaongea kwanini?"

    Alikuwa ni mama yao, baada ya kuskia sauti za watoto wake wakiongea usiku huo...



    Tukirudi huku kwa akina surian na mke wake maimuna (JINI MAIMUNA)

    "ok hao watu wengine sawa... Lakini je familia yangu je?"

    Suria bado alikuwa na hasira, na hapo ni siku moja baada ya ndoa, na ndio usiku wa kwanza duniani, na hapo hata tendo la ndoa bado hawajafanya toka wafunge ndoa.. Kwani hawaruhusiwi kufanyia kule, japo ni halali lakini wanatakiwa wakafanyie tendo huko wanapokwenda kuishi...

    "mume wangu, hebu vuta subra angalau hizi siku saba ziishe ikiwa ni sheria zetu"

    "sitaki kuskia kuwa eti mimi nina pesa na ni tajiri, afu wazazi wangu wanaishi kwenye kota za serikali tena zile za mkoloni.... Fanya ufanyavyo, ongea na wakuu wako... Ukitaka tuelewane katika hii ndoa,.. Nahitaji nineemeka na familia yangu, ila sio mimi peke yangu.... Ukumbuke kuwa bila wazazi hata wewe usingenijua...sasa sikia nataka kesho asubuhi nipate jibu sahihi, ili kesho hio hio nikawanunulie wazazi wangu nyumba inayo endana na hadhi yangu kama tulivyo"

    Aliongea suria huku akitoka nje kwa hasira,

    "Suriiiiiiiii, please subiri kwanza mume wangu... Jambo hilo sio rahisi kama unavyo fikiria wewe"

    Aliongea maimuna lakini surian haelewi la mwazini wala la mnadi swala.... Suria ana hamu na wazazi wake, yaani anatamani hata kwenda sasa hivi, afu anaambiwa mpaka siku saba ziishe ndio aende...

    "sawa,.. Jambo hili sio rahisi,. Sasa nihakikishie kuwa familia yangu itaishi maisha ya kitajiri kama mimi nitakavyo ishi,... Laa sivyo hii ndoa itakufa sasa hivi na usiku huu"

    "naweza kusema sawa... Ila endapo utajaribu kuwapa ama kuinunulia chochote familia yako, nami nitakufa.. Labda utumie njia nyingine waneemeke lakini sio kwa kuwapa pesa,..."

    Aliongea maimati huku akilia, mana anatamani kuitajirisha familia ya surian, lakini kutokana na sheria zao, inakuwa ngumu kufanya hivyo, na surian jinsi anavyo ona mipesa iliojaa chumba na madini, vitu vya thamani ambavyo wanavimiliki, afu wazazi wake waendelee kuishi maisha ya kimasikini,.. Roho inamuuma

    "kwahio haiwezekani"

    "hebu tuliache hilo... Twende ndani nikupe haki yako ya ndoa... Mambo mengine baadae"

    "maimuna, swala la wazazi lisikie tu, hivi watu watanionaje wazazi wangu kuishi katika hali ile"

    "najua sana,... Lakini wewe una dada, kwanini usimuajiri ili afanikishe swala la familia"

    "hapana.... Nataka nitumie nguvu zangu mimi kama mimi niwahudumie wazazi wangu..."

    "Kiukweli hapo ni pagumu mume wangu..."

    Aliongea maimati huku suria akitaka kusema jambo fulani.. Lakini kabla hajasema, ghafla ilisikika sauti ya kike ikisema

    "hapanaaaaaaaaaaaaaaaaa"

    Suria alishtuka lakini maimati alitulia kimya kama vile hajasikia chochote kile, na sauti hio imesikika nje ya nyumba hio waliopo wao





    Katika maisha hapa duniani hakuna kitu bora kama wazazi, tena surian kila akifikiria kuwa yeye ndio kamaliza pesa kwa wazazi wake kwani aliwekezewa yeye asome kwa bidii ili aje kusaidia wazazi wake, lakini kwa bahati mbaya alikosa kazi nzuri,.. Lakini pia bahati imemdondokea ya kupendwa na jini mwema na wameshafunga ndoa, kawaida ya majini wao humiliki mali nyingi sana hususan madini yote wao ndio wamiliki, hivyo kumiliki na pesa kwao sio jambo la kuuliza... Lakini pamoja na mali wanazomiliki hua kuna masharti ya kuzitumia kwa binadamu atakaye pendekezwa kuzitumia pesa hizo,... Suria alikubali masharti yote lakini sharti la kutowatajirisha wazazi wake hilo kwake hakulitaka... Ikiwa ni usiku huo huo waliotoka nao majini, na kuja duniani kwa maisha yao rasmi, walikuwa wakibishana sana ili maimuna aweze kukubali surian aifanye familia yake kuwa bora zaidi



    Lakini katika ya maongezi yao ilisikika sauti ya mwanamke ikisema



    "hapanaaaaaaaaaaaaaaaa"

    Suria alishtuka sana mana ni sauti iliosikika nje ya jengo hilo, japo jengo lenyewe limefanywa kuoteshwa kimiujiza na maimati, maimati hakushtuka kwa sauti hio kana kwamba anaifahamu vyema sauti hio



    "ni nani kasema hapana"

    Aliuliza surian huku akitaka kutoka nje

    "usitoke mume wangu, tafadhali sana"

    "nataka niangalie huyo dada kafanywa nini huko nje, utakuta anataka kubakwa"

    Aliongea surian huku akitoka nje,.. Maimati alimshika mkono na kumpigia magoti kwa kumuomba asithubuti kwenda nje...

    "huyo ni sabaha mume wangu, usiende"

    Aliongea maimati huku akilia, mana Sabaha keshaonja utamu wa huyu msambaa hivyo anamfuata kila aendapo...

    "Sabaha si kafa"

    "hakufa, bali amesha laaniwa na sasa ni shetani"

    "hapana bwana... Utakuta kuna mwanamke anabakwa huko nje"

    Aliongea surian, lakini maimati akaona wacha amuachie kwani haamini kama huyo ni sabaha, na kamuscha ili hata siku nyingine akisema ni kitu fulani, aamini kweli,..

    "sawa, nenda, lakini usithubutu kuvua hio pete hata kama unakwenda kuoga"

    Aliongea hivyo, kisha maimati yeye akarudi ndani mana anajua surian ana pete hivyo Sabaha hawezi kumfanya lolote,...



    Kweli huku nje alikuwa ni Sabaha, na wakati huo anachuruzikwa na damu mdomoni, kucha zake ni ndefu ana mapembe mithili ya ng'ombe, na mbaya zaidi alikuwa akinuka sana kwani kutokana na damu zilizomgandia katika mwili wake,...



    "hahahahahhahahaha, baba wa watoto wangu... Nimefurahi sana kukuona"

    Aliongea shetani sabaha huku akisima mita saba mara mbili, yaani mita 14, na hapo hawezi tena kumsogelea surian kwasababu ya ile pete alio nayo,...

    Na surian kwa sasa ni mjasiri kwa kiasi fulani kwani mpaka kukubali kuoa jini, ni ujasiri wa hali ya juu...

    "wewe ndio umepiga makelele eneo hili"

    Aliuliza surian huku sabaha akicheka

    "hahahahhah, unapimwa lakini pimika tu... Hahahahaha... Mtoto wako ninaye tumboni kwangu..."

    Aliongea sabaha akiwa na maana kuwa ana ujauzito, na ujauzito huo uliingia juzi tu hata siku mbili sidhani kama zimeisha toka sabaha afanye mapenzi na surian,

    "nani kakupa hio mimba"

    "hahahahahahh.... Surian baba wa mtoto wangu.... Nimekuja tu kukupa taarifa juu ya mtoto wako,... Natamani niijaze dunia kwa kuzaa watoto wenye asili ya kibinadamu lakini ndani yake awe na asili yetu... Ahahahahahahahahahaa... Huyu nitampa jina la TAMALA, mana ni mtoto wa kiume... Na ndani ya mwezi huu natarajia kujifungua dume hili,... TAMALA mwanangu? Baba yako ndio huyo hapo mbele"





    Sabaha aliongea mengi sana huku surian kabaki kuduaa

    "sabaha, Usifanye hivyo... Kiharibu kiumbe hicho sio salama kwa maisha ya binadamu"

    "hahahahahahh, BABA TAMALA, mtoto huyu ndio atakuja kuzaa mtoto atakayeweza kufanya kazi hio.... Hii ni taarifa tu... Nikipata muda nitakuona kwa nyakati zingine, ila ahsante kwa penzi tamu"

    Aliongea sabaha kisha akafungua mabawa na kuondoka, meno yake yalikuwa ni marefu mno, nguo nyeupe alizokuwa anavaa wakati akiwa jini wa majini, imeloa damu na kuchafuka bila kujua hio ni nguo nyeupe,... Surian alilia sana kwani hizo taarifa sio nje kabisa katika maskio yake, na itakuwa hatari dunia ikijaa binadamu wenye asili ya ushetani, na hio ndio maana ya sabaha, hivyo TAMALA hawezi kuzaa watoto hao... Ila mtoto wa Tamala ndio atakuja kuzaa watoto wenye asili ya kibinadamu lakini ndani yao ni mashetani, hivyo dunia itakuja kutawaliwa na mashetani...



    Suria aliingia ndani huku akipangusa machozi, na maimati kasikia kila kitu hivyo hakuwa na haja ya kumuuliza,.. Suria anaingia ndani kamkuta maimuna kajilaza mlalo wa mtego mtego, huku akiwa kavalia mtandio ulio onyesha chupi yake,... Yaani utafikiri binadamu, kumbe ni jini...



    Suria alitokwa na mate kwa tamaa, ikiwa maimuna ndio mara yake ya kwanza kufanya mapenzi toka kuzaliwa kwake,... Pete alioivaa surian haiwezi kumzuia maimuna kwasababu sasa wao ni mwili mmoja, ila pale mwanzo kabla hawaja oana maimati hawezi kumsogelea suria kwa ubaya wowote japo pete ni yake lakini hawezi, ila kwa sasa anaweza kwasababu ni mwili mmoja... Surian alisahau swala la wazazi wake na kujikuta anaingia katika swala la huba bin hububu, kilikuwa ni kitendo cha kuvuta ule mtandio, na kukuta na mchupi mweupeee, uliojaaa katika mwili wa maimuna, au maimati kwa jina la asili yake... Ikiwa ni saa kumi za usiku kwenda saa kumi na moja hivi alfajiri, kitanda hakikuwa kikifaa kwa kwa raha walizokuwa wanapeana wawili hao, ila kwa maimuna kwake ilikuwa ni maumivu kwasababu ndio mara ya kwanza...



    Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili,... Alionekana faima akiwa anaelekea katika duka la nguo alilokuwa akiuza awali, kwani alifukuzwa lakini hatukujua kosa lake

    "Asalam Aleykh boss"

    Faima alimsalimia boss wake aliokuwa akiuza mwenyewe kwani toka faima aachishwe kazi hakupa mfanyakazi mwingine,

    "waaleykh msalam,.. Haya kipi kimekuleta tena... Unataka kuja kunipa hasara tena"

    Aliongea mwanamke huyo mwenye asili ya kipemba,

    "samahani boss, naomba unisamehe, nimejifunza kutokana na makosa, sitarudia tena"

    Aliongea faima huku akiwa kapiga magoti,

    "hivi unajua kuwa ulinitia hasara kiasi gani"

    "Nisamehe boss"

    "sio Nisamehe,... Nataka kujua hasara yangu inarudi vipi"

    "fanya utkalo katika mshahara wangu"

    faima alikubali hata kukatwa nusu ya mshahara wake ili kuweza kufidia hasara alioweza kuitia katika duka hilo,..

    "mschiuuuuu (msunyo)... Ole wako urudie tena... Sitaki mtu mwenye mawazo hapa"

    "ahsante boss, siwezi kurudia tena"

    "haya nakuacha na wateja hao endelea nao"

    Boss wa faima alikubali kumsamehe faima kwa roho moja, kwani faima katia hasara kubwa katika duka hilo, wateja wanakuja hawahudumiwi kutokana na mawazo ya kumpoteza surian wake,... Laiti angelijua kuwa surian yupo mjini, sjui ingekuwaje.. Basi faima alirudi kazini upya, na duka hilo huhusika na nguo za Kiislamu pekee... Kama ujuavyo asilimia kubwa ya mavazi ya tanga, kukuta kimini mchana ni bahati sana, ila kanga na mahijabu... Kanzu na kibaraka shekhe, utaviona vingi sana



    Katika godauni moja lililokufa zama za wakoloni lilikuwa likifyatua mavazi ya Kiislamu, lilikufa kutokana na maslahi, hivyo walioneka wana ndoa wawili surian na mke wake maimuna wakiwa wanalikagua godauni hilo kwa niaba ya kuweka kiwanda kipya kwani, kwani cha zamani kilikufa na mashine zilisha tolewa.... Surian akiwa mwenyeji wa tanga, alifuata sheria zote za serikali ili kuweza kufungua kiwanda..., godauni liliwekwa mabati mapya siku hio hio, ikumbukwe kuwa maimuna ni jini, hivyo vitu vyake hua vya sekunde tu vimekaa sawa,... Godauni ambalo lilitakiwa kupigwa bati mpya kwa wiki nzima, lakini ilitumika dakika saba tu mpaka kumaliza.... Mashine ziliota ghafla tu godauni limejaa mashine na vitengo vyake,... Kwa pembeni wakaotesha ofisi maalum kwa ajili ya boss au wageni wanaokuja kuweka oda,...



    Ndani ya siku moja kampuni imekamilika, wakati ingelichukua hata miezi mitatu lakini imechukua siku moja, tena hapo kapunguza makali, kana kwamba vyote hivyo ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua iwe kila kitu kipo sawa,... Sasa imekamilika ni kampuni mpya imepigwa rangi vyema na kung'aa...

    Ila siku hii kampuni ikifa, linabaki godauni vile vile... Mana ni vitu vimeoteshwa tu,... Kasoro bidhaa ndio zitakuwa hai mana zimefanya kutengenezwa,...



    "hapa sasa tunafanya nini mke wangu"

    Surian alimuuliza mke wake huku wakiwa wamekaa hapo ofisini kwao wawili tu,

    "hapa mi naona tichapishe karatasi tuzisambaze mitaani watu waandike barua za kazi"

    Aliongea maimuna huku suria akisema

    "duuuuuu, hivi tutamaliza lini kuchapisha mikaratasi ya mkoa mzima"

    "ni kazi rahisi... Lete plan paper (karatasi tupu) moja nikuonyeshe"

    Aliongea maimuna huku suria akitoa karatasi na kumpa.....

    "hii hapa"

    Alimpa, lakini maimuna akamuuliza

    "sasa kampuni tunaiitaje"

    "tuiite MOON ISLAMIC CLOTH COMPANY"

    Aliongea surian kisha maimuna akaishika ile karatasi, ndani ya sekunde saba tu, palikua na mlima wa karatasi ambazo tayari zimesha chapishwa.... Surian alibaki kushangaa tu,.. Pale pale maimuna akazungusha mkono kumaanisha karatasi hizo zisambae mkoa mzima, na ni kwenda ndani ya muda mchache tu, meza haina karatasi hata moja.... Kana kwamba zinajigandisha zenyewe kwenye nguzo za umeme au kuta mbalimbali huko nje,.... Likiwa linaendelea hilo, huku barabara yaliongozana makontena yaliobeba material (nyuzi za kutengenezea vitambaa hadi kuwa hijabu au kanzu)....



    Siku ya pili suria na mkewe walitembelea show room (Sehemu inayouzwa magari



    Walinunua gari 51.... Gari 30 ni zenye makontena kwa kusafirisha bidhaa kwenda mikoa mbalimbali... Gari 20 zingine ni mabasi kwa ajili ya kupeleka wafanyakazi kwenye vituo vyao na kuwaleta kazini... Nangari moja ni maalumu kwa ajili ya boss,.. Awe surian au maimuna lakini gari ni hio hio moja wataitumia wao,.. Gari ya gharama sana.... Magari yote hayo yalifanyiwa utaratibu na kuingia kiwandani kwa kazi rasmi...



    Zile gari zilizoleta nyuzi kutoka bandarini zilifika na kila nyuzi ilikaa katika mashine yake, hapo wafanyakazi bado hawaja anza kuleta barua zao, kwani kesho ndio siku ya usaili,.... Kampuni imekamilika kasoro wafanyakazi tu



    Siku hio hio huku nyumbani kwa akina surian, yaani kule kwao...

    Alionekana asha akilia sana kwa kashifa ambayo anaipata kila akipita mitaani,... Kwani huambiwa kuwa kamuua mdogo wake na ndio maana alipiga hela wakati ana ile pete, sasa hivi hana pete, watu wanasema nguvu zimeisha anatakiwa kuua mwingine,... Majirani wote walio izunguka nyumba hio wanajua asha kamuua mdogo wake ndio mana alipata pesa mwezi uliopita,... Sasa asha yeye analia tu huko ndani kwani hata saluni hatamani tena kwenda,

    "asha mwanangu, umebakia wewe tu kama mboni.. Leo tena unatuliza na sisi wazazi wako"

    Alikua ni mama yake surian akimsihi asha asilie kwa anawaliza wazazi wenye uchungu zaidi kuliko yeye...

    "mama, inaniuma sana... Yani mimi nimuue mdogo wangu kisa pesa"

    Aliongea asha huku akizidi kulia...

    "usijali mwanangu, hao ni binadamu tuu ndivyo walivyo"

    "naona bora na mimi nife mama, sina raha na huu mji... Kila mtu ananitenga"

    "nyamaza mwanangu.... Hebu angalia hii hali tulio nayo kwa sasa,.. Baba yako ndio huyo hana kazi, mimi ndio kama unavyo niona, tegemeo letu ni wewe, leo unalia ivi unadhani nasi tunajisikiaje..."

    "mama,sina hamu ya kuishi kabisa, kama surian nimemuua mimi, basi bora na mimi nimfuate huko huko"

    "ashaaaaaaa.... Wewe ni mshenzi,... Sitaki kusikia huu upuuzi mimi... Hebu amka uenda saluni tupate chochote"

    Aliongea mama yake asha,.. Mana anamfokea huku akimpoza

    "mama.... Saluni nilisha iuaza yote... Mana pesa niliokua napata awali, Kiukweli kwa sasa inachosha sana... Nimesha uza kila kitu"

    "haaaaaaaaa.... Asha mwanangu... Sasa tutakula nini?... Kwanini lakini umeuza? Hata kama ni mali yako, lakini ilikuwa ikitusaidia"

    Aliongea mama yake asha, lakini wakiwa bado wanazungumza... Ghafla mlango ulisukumwa....

    "heeeeeeeeeeeeeeeee"

    Mama alitahamaki kana kwamba kuna mtu kaingia bila kutarajia







    Hakuna kitu kibaya katika hii dunia kama kuzushiwa jambo ambalo hujalifanya, hususan kwenye upande wa kifo,... Asha anaye nyooshewa vidole kwa taarifa za kumuua ndugu yake surian kisa ni pesa, na ukiangalia ni kama kweli, mana wakati surian anapotea, huku nyuma asha kaanza kupiga pesa kupitia pete aliokuwa kaivaa, japo mpaka leo hajui kuwa pete ile ndio sababu ya biashara yake kuwa nzuri,...



    Mpaka sasa asha keshauza saluni yake yote kwani ndio sababu ya kunyooshewa vidole na watu juu ya ndugu yake. Mama yake alilaani sana kwa kitendo cha asha kuuza saluni yote ili kupunguza lawama ya kwamba saluni ile ndipo mdogo wake alipo pale,.. Mana asha alipiga pesa mpaka akanunua uwanja na kujenga Nyumba ambayo kwa sasa ipo kwenye lenta,... Na hapo ndipo ilipo ishia,... Maisha yao toka kuzaliwa kwake wameishi kwenye kota za serikali, hivyo akaona bora ajenge,.. Sasa katulia tu nyumbani ni mtu wa kulia...



    Lakini wakiwa bado wanazungumza... Ghafla mlango ulisukumwa....

    "heeeeeeeeeeeeeeeee"

    Mama alitahamaki kana kwamba kuna mtu kaingia bila kutarajia....



    "Heeeeeeee, baba asha haya nini tena, au wakimbizwa huko nje"

    Aliuliza mama asha, kumbe alio ingia kwa haraka hivyo ni mzew Rashidi ambaye ni baba yake surian au asha.

    "hapana mke wangu,... Kuna tangazo la kazi nimeliona na kesho ndio wanafanya usaili,... Sasa nimeona nimuwahishie asha akajaribu kazi pale, mana hapa wameandika wanataka wanaume 200 (miambili) na wanawake 300 (Miatatu)... Natamani kwenda, lakini kama mnavyojua mimi ni mbovu wa kifua, hivyo kazi za viwandani siziwezi... Asha mwangu, hebu kajaribu ili tupate chochote mama"



    Baba yake asha kumbe alikimbiza tangazo la kazi, ili asha ajiandae mapema, mana kesho ndio usaili (uchambuzi wa wafanyakazi)... Hivyo kawahi kumpelekea mana yeye ndio alikuwa mitaani huko...

    "baba, Utanisamehe sana... Kwa sasa sitaki kazi"

    Asha alikataa kupokea wito wa baba yake... Na yote hio ni hasira...

    "asha, unamkatalia baba yako"

    Mama aliingilia kati huku baba akisema kuwa

    "asha, hawahitaji vitu vingi, wanataka barua ya maombi ya kazi na vyeti vya shule tu"

    "baba na mama.... Mmeshindwa kunisomesha vizuri nipate kazi nzuri... Leo mnaniletea kazi zinazo tangazwa mitaani... Mimi sitaki, msubirini msomi wenu aje mumpe hilo tangazo"

    Asha aliwajibu wazazi wake hivyo huku akiondoka kwa hasira kali,...

    baba yake kuna kaulia alitaka kuitoa kama kumuachia laana kutokana na majibu yake lakini mama akamzuia mume wake asiongee lolote, kwani asha hapo alipo ana hasira sana kwa kashfa anayo pewa....

    "mama asha, hivi hapa tumezaa au tumemuokota huyu mtoto"

    "baba asha, huko unafika mbali sasa, ukumhuke huyu mtoto ana hasira kutokana na kashfa anayo pewa mitaani"

    "hata kama ana kashfa, haya sio majibu ya kutujibu sisi... Tumemkosea nini... Kufeli kwake ndio sababu ya kutulaumu kuwa hatujamsomesha... Mbona anataka kuniliza huyu mtoto"

    Aliongea mzew Rashidi huku akitaka hata kulia lakini mama anazuia machozi yasimtoke mzee Rashidi, kwani yakitoka ni laana kwa asha, mana kasababisha mzazi kalia kwa ajili yake... Hivyo mama alifanikiwa kuzuia machozi ya mume wake... Walikaa mahali yeye na mke wake wakiwa wanatulizana kama mke na mume....

    "sasa mama asha... Mimi naona niandike barua tu... Angalao nikawe hata dereva"

    Aliongea baba yake suria kuwa aandike barua akaombe kazi ya udereva

    "baba asha, hivi unaongea nini"

    "mama asha... Tulikua tukimtegemea mwenetu asha, leo asha hana kitu, tutakula nini humu ndani... Wacha niende nikaombe udereva, mana wana pia wanahitajika madereva"

    Aliongea baba yake asha huku akitoka kwenda kununua karatasi ili aandike barua ya kazi...

    "heeeee baba asha... Huo udereva ulijifunza lini? Au wataka ukafe huko kama mtoto wako suria alivyokufa... Hebu niachie hilo balaa... Wacha mimi nitakwenda, we niandike barua ya maombi ya kazi"

    Mama aliona ni bora aende akaombe kazi yeye kuliko mume wake, kwani hawezi udereva ila anataka kwenda tu, kuachilia hawezi pia anaumwa na kifua kwa miaka mingi, hivyo i Afadhali ya mama kidogo ana kajinguvu ka kufanya kazi

    "mke wangu... Ina maana wewe ufanye kazi mimi nile"

    "baba asha... Mbona uko hivyo... Mimi nimekula vyako vingapi, sembuse mshahara wangu?"

    "mmmhhh sawa, lakini nitakuwa nakusindikiza mpaka getini, na kuja kukuchukua"

    Aliongea baba yake suria huku akicheka

    "kwanini sasa ufanye hivyo"

    "heeee... Si namlinda mke wangu"

    "hehehehehe yaani baba asha wewe hukui, sasa na uzee huu nani anifuata"

    "weeeeeeeeeee.... Heeee we sema hivyo tu, mi ndio najua siri ilioko hapo"

    Aliongea mzee rashidi huku akitoka kwenda kununua karatasi ya barua, ili amuandikie mkewe barua ya kazi... Sasa mzee Rashidi ana wivu mana mama yake suria anazeheka nalo...





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog