IMEANDIKWA NA :
MOONBOY
*********************************************************************************
Chombezo : Young Pastor
Sehemu Ya Kwanza (1)
Katika kanisa moja
kubwa ikiwa ni wakati wa saa nne hivi asubuhi… Kanisa kubwa lenye urefu wa
rosheni mbili kwenda juu.. Na rosheni zote zimesheheni waumini wa lika
mbalimbali kuanzia watoto wazee na vijana.. Wakati huo wapo mapasta ambao
walikuwa wakitoa sifa kwa Bwana Yesu kwa kutumia nyimbo za injili,… Floo ya
chini ya kanisa hilo ni sehemu ya kupaki magari, na floo ya katikati ni ukumbi
mkubwa yaani kama kuna ndoa basi hapo ndipo mahali pake, ila pia hio floo ya
katika imejaa waumini, mana sio siku zote watu wanaoa, na pia ina skrini kubwa
karibia ukuta mzima ule wa mbele, hio ni skrini ya kumuonyesha pasta akiwa floo
ya juu, yaani ni kama sinema vile,,.. Sasa hio floo ya juu na ya mwisho, ndio
kanisa lenyewe,.. Ukiangalia mazabauni yaani imeng’aa kwa maru maru maalum,
yaani pale ni sehemu ya pasta pekee. Na wakati huo pasta bado hajaja, hivyo
waumi waikuwa wakitoa sifa za bwana Yesu kwa kupitia nyimbo zilizoimbwa na
wasanii mahiri nchini,
Sasa huku chini ilionekana gari moja ya
bei mbaya… Ikiwa inapaki, tena ina sehemu yake maalum ya kupaki sio kila
mahali,… Ilikuwa ni familia moja iliokuwa ikija kanisani, na ilionekana
kuheshimika sana kanisani hapo,… Walikuwa ni wasichana watatu waliotofautiana
umri, akiwemo baba yao na mama yao,… Hatua za kuelekea kanisani zilianza
taratibu, na kila muumini aliiheshim familia hio,…
“tumsifu yesu
Kristo”
Ni waumini waliokuwa wakitoa salamu kwa bwana huyo, huku
akiwaitikia
“milele amina”
Yaani waumini wanapanda kwa ngazi,
lakini yeye ana lift yake maalum, yaani yeye na familia yake hutumia wao tu,…
Alipofika ndani ya kanisa waumini wote wa floo ya katikati na floo ya mwisho
walinyanyuka na kutoa salamu kwa pamoja…
“tumsifu Yesu Kristo alie hai
mbele za mungu”
Walisema waumini hao huku familia ikiwa ina viti vyao
pale mbele, yaani ule ule upande wa waumini, sasa viti vya mbele ni spesho kwa
ajili ya familia hio… Lakini pia katika viti hivyo kuna kiti kimoja hakikuwa na
mtu, na ni kiti cha mmoja wa familia hio na hakiruhusiwi kukaliwa…. Sasa hatujui
huyo aliosalia kukaa pale ni nani,…. Pale pale mr huyo alipanda
mazabauni,….
Kumbe huyo bwana ana kipawa cha UBISHOP yaani ni
Bishop Jacob… Ni kiongozi wa makanisa yake yapatayo 50 kwa idadi kamili…. Yaani
mzee huyu ana makanisa 50 makubwa kama hili na ni yakwake peke yake…
Anayasimamia mwenyewe, licha ya kuwa Bishop, bado pia ni tajiri mkubwa… Mana ana
makampuni mengi sana, ana viwanda… Huezi amini ni Bishop anaemiliki ndege
binafsi, ana magari ya kutembelea kama utitiri,…..
“tumsifu Yesu Kristo
kwa jina la baba”
Aliongea Bishop Jacob huku waumini wakipaza sauti zao
kwa hali na mali
“milele aminaaaaaa”
Raha sana ukiwa na imani ya
dini yako….
Wadada, wamama, wakaka, watoto, wazee…. Yaani malika yote
yalijaa hapo, na unambiwa akitoka hapo anakwenda katika makanisa mengine kutoa
neno la bwana… Yaani amekuwa mtu wa kutoa neno siku
nzima….
BISHOP ni kipawa au cheo kikubwa ambacho ni ukitoka
pasta sasa anaefatia kwenda juu,… Anakuwa ni Bishop, lakini pia Bishop ana
mkubwa wake ambaye ni ATBISHOP huyu ATBISHOP huyu sio mtu wa kawaida, huyu
anaweza kuwa ATBISHOP wa kidunia au wa kitanzania nzima…. Yaani anasimamia au
kuongoza makanisa yote Tanzania. Na sio kuwa ni yake lahasha bali anayasimamia
tu, na pia sio kuwa anasimamia yote, lahasha bali kuna matawi mengi sana juu ya
haya makanisa… Hivyo atasimamia makanisa ambayo ni tawi fulani pekee, hivyo
atakuwepo ATBISHOP mwingine wa kusimamia makanisa ya tawi lake husika… Hivyo
ATBISHOP ni mkubwa, tuchukulie mfano wa rais…. Afu huyu Bishop yeye tufanye ni
kama mbunge… Hivyo katika mkoa mmoja kunaweza kuwa na ma Bishop hata mia moja..
Kutokana na kila mtu kumiliki jimbo lake yaani makanisa yake…. Nakupa tu kwa
ufupi ujue vipawa vilivyo….
Sasa Bishop Jacob alianza kuhubiri
kama ilivyo kawaida yake, ni mchungaji aliojaaliwa kipawa na upako wa hali ya
juu katika kutoa neno la Bwana,…. Waumini walikuwa wakilia kutokana uzito
mahubiri aliokuwa akihubiri Jacob,… Machozi kila muuni, wengine kama kawaida yao
kudondoka chini wakati wa pepo kutoka,… Na yote hayo ni kwasababu ya mchungaji
Jacob au Bishop Jacob
Mahubiri yaliisha na hatimaye ibada ya
siku ya Jumapili inakwenda ukingoni,… Lift yake ni ile ile, hachanganyikani na
waumini hata siku moja,…. Akiwa na familia yake wanaingia katika gari,…. Lakini
wakati wanaingia alitokea mschana mmoja ambae nae ni muumini wa kanisa
hilo,..
“tumsifu yesu Kristo mama”
Alisalimia mschana huyo huku
akimpa mkono mke wa Jacob,….
“milele amina….. Eva mbona siku hizi huji
nyumbani, au kwasababu mwenzio hayupo”
Aliongea mama huyo aliokwenda kwa
jina la Rebecca,.. Sasa hatukujua huyo mwenzie ni nani haswa, lakini eva
alipokua akisalimiana na mwanamke huyo, ghawna wale wasichana nao wakaanza
kumsalimia eva….
“heee wifi hali yako”
Aliongea mtoto mkubwa wa
huyo mama aliokwenda kwa jina la Jessica mwenye umri wa miaka 28, ndio mtoto wa
kwanza kwenye hio familia, lakini sasa Jessica kamuita eva wifi kitu ambacho
hatujui kaolewa na ndugu yake nani, au ndio ile utani tu,… Mara mschana mwingine
kasalimia
“shkamo wifi eva”
Alisalimia mschana mwingine
aliokwenda kwa jina la martha, mwenye umri wa miaka 20…. Kuna mwingine hakutaka
kuachwa nyuma kwa salamu
“wifi eva shkamo”
Alisalimia mschana
mwingine wa mwisho, aliokwenda kwa jina la maria ana miaka
15…
“amarahaba mawifi zangu hamjambo”
“hatujambo… Hatukuoni
nyumbani”
“aahhh nitakuja Maria usijali”
Eva alikuwa ni mschana
mzuri sana na mwenye heshima kwa rika zote,
“mwanangu, kabla mwenzio
hajakwenda masomoni, ulikuwa unakuja, lakini sasa hivi huuuji
jamani”
Aliongea Rebecca au mama Jessica, au mama
mchungaji,…
“mama, hata mimi hua nakuwa na ubize sana… Sasa hivi nadili
sana maombi, sitaki mwenzangu anikute nipo nyuma, hivyo nami nakua bize na
mungu”
“yesu atakubariki eva,… Na naomba nikutaarifu, mwenzio anarudi
wiki ijayo”
Eva kusikia mwenzie anarudi wiki ijayo, alifurahi na kuruka
ruka, alimkumbtia mama mkwe wake karibu kudondoshana, mpaka baadhi ya waumini
walishangaa kwa furaha hio alionayo eva…
“eva utaniangusha
jamani”
“mama, nina furaha kiasi gani juu ya taarifa hio”
Eva
ana mdogo wake wa kike aitwaye HAPPINESS, mwenye miaka 15 alikuja pale baada ya
kuona dada yake ana furaha…
“tumsifu yesu Kristo
mama”
Alisalimia happy huku akiinama chini kuashiria ni heshima ya hali
ya juu mno,…
“milele amina,… Heew happy, umependeza Jumapili ya
leo”
“ahsante mama… Sifa kwa Yesu”
“amina mwanangu”
Basi
waliongea mengi sana na hatimae kila mmoja kuondoka baada ya ibada
kuisha,…
Kuanzia hapo Eva alikuwa ni mtu wa furaha siku zote,
mana sasa usingizi wake karibu kuja… Eva ni mschana aliolelewa katika mazingira
ya kidini na anaijua dini haswa, yaani humwambii kitu kuhusu Bibilia,… Eva
alipofika nyumbani alimkuta mama yake kesharudi, nyumbani… Ni familia ya kawaida
sana…
“mamaaaa….. Yesu kajibu maombi yangu mama”
Aliongea eva
huku akimkumbatia mama yake,…
“ni nini eva… Afu leo sijakuona kanisani
ulikaa wapi”
“mama… Leo niliamua kukaa nyuma sana”
“enheee, yesu
kajibu maombi yako kivipi… Mana una furaha kweli yani”
Aliongea mama
huyo huku mama akiwa anaandaa ratiba zake za jumuiya,..
“mama njoo ndani
nikwambie”
Mama eva aliingia ndani ili kumsikiliza mtoto
wake…
“haya Niambie”
“mama…. Wiki hii mkwe wako
anakuja”
Mama alishangaa kusikia mkwe wako anakuja….
“ina maana
umeachana na adam unataka uniletee mwanaume mwingine, eva mwanangu ni mawazo
gani unayo”
Mama alikuwa hajamuelewa mtoto wake ana maana
gani…
“mama sio kuwa naleta mwanaume mwingine,…. Namaanisha huyo huyo
Adam, anarudi toka masomoni”
“weeeee…. Unasema kweli”
“ndio,..
Nilikuwa na mama mkwe pale kanisani ndio kaniambia”
“jamani eva
mwanangu”
“nini mama…. “
Familia hio ni familia fukara sana ila
wengi wao wanaona wivu kwa mtoto Bishop Jacob, kuoa katika familia hio, na ni
kila muumini anajua uhusiano wa Adam na Eva,… Lakini kwakuwa Eva anaishi katika
maisha ya kimasikini hivyo kwao ni kama bahati kuolewa na mtoto wa kitajiri,
tena mtoto wa Bishop, yaani sio pasta ni Bishop… Kwa wale waikristo nikisema
Bishop nadhani mnanielewa..
“mara paaap adam anashuka kwenye ndege na
mke wa kinaigeria… Utafanyeje sasa”
Mama alimwambia mwanae hivyo mana
adam yupo Lagos nchini Nigeria, katika vyuo vya dini ya kikristo, japo adam ana
nguvu na miujiza kuliko hata baba yake, lakini akaamua kwenda kujiongeza, sasa
akirudi huko ni moto wa kuotea mbali, Sasa baada ya mama eva kusema hivyo, eva
alianza kulia huku akisema kuwa….
“mamaaaaaa….. Usiseme
hivyo”
“sikuombei umkose mwanangu… Ila wanaume wa siku hizi…. Siwawekei
mia kwa mia… Hawakawiii kubadirika”
“ni kweli mama… Lakini sio kwa mtu
mwenye imani kama adam”
“eva mwanangu, mimi ni mama yako… Nimekuficha
mengi sana kuhusu adam…. Na nikisema nikuambie nitakupoteza mwanangu… We mpende
tu”
Eva alitoa jicho kuskia mama yake anasema maneno
hayo…..
“unasemaje mama”
“una kifua cha kubebea jambo mwanangu,
tusije kuanza kupepeana na kanga hapa”
Aliongea mama yake eva huku
wakikaa vizuri kitandani
“mama… Nipo tayari kumwacha adam kama ana tabia
chafu”
“heeeeee wewe ndio wa kusema hivyo”
“mamaaaaa Niambie
basi nijue”
Eva alikuwa na wasiwasi
mno kuhusu mchumba wake ambaye mama anasema ana siri nzito sana juu ya adam..
Sasa eva kakaa kwa umakini ili kuweza kujua ni siri gani hio ambayo mama
anaijua… Eva alitamani hata kutoa chozi, lakini ghafla mama anacheka kweli mpaka
machozi yanamtoka kwa kucheka,..
“kumbe mwanangu unampenda sana adam…
Mimi nikajua utakuwa umemsahau kabisa kutokana na muda aliokaa masomoni sana…
Kumbe bado unampenda… Kiukweli hakuna lolote mwanangu, nilikuwa nakutisha
tuuu”
Hapo eva akashusha pumzi nzito kisha akachukuwa Biblia na kuanza
kusoma kama vile kamkasirikia mama yake…
“mwanangu usinune basi jamani…
Yesu hajafundisha umnunie mama yako eva”
Eva kweli anajua sheria na
mafundisho alio yaacha bwana yesu
“mama, sijakununia mama
angu”
Aliongea eva huku akimkumbatia mama yake,…
“najua
nimekuuzi mwanangu”
Mara bite kaja mpaka chumbani,.. Yaani watoto wa
huyu mama ni wazuri, mpaka basi sema hali ya maisha kwao ni ngumu mno, na
wanaishi hivyo hivyo kwa nguvu za mungu….
Tukiachana na familia
ya akina eva sasa turudi huku kaisani, walikuwepo waumini waliosikia fununu za
kuwa mtoto wa bishop jacob yukaribuni kuja Tanzania kutoka masomo, hivyo hizo
ndio atori zilizo zagaa katika kanisa hilo… Inaonekana ni jinsi gani adam
anapendwa na waumi sasa hatujui adam ana lika gani na ana rangi gani, na yupoje
yupoje.. Bali sifa zake ndio huongelewa zaidi….
“ester, iv umesikia za
chini chini kuwa adam yukaribuni kuja”
Aliongea dada mmoja ambaye ni
muumini wa kanisa hilo la mr Jacob
“adam gani tena…. Au adam yule wa
karne ya 5”
“aaahhh we ester huelewi kwanini”
“sasa Janet, mi
namjuaje huyo adam”
“si adam wa Bishop Jacob”
Ester kusikia ni
adam wa bishop Jacob nae alitahmaki, walikuwa wasichana wengi na wao pia
walitahamaki….
“we janet muongo… Adam si yupo Nigeria kimasomo
wewe”
“sasa anakuja.. Nimeskia za chini ya kapeti… Wiki hii ndani ya
Arusha”
“eeeeh bwana weee…”
“alafu sasa…. Umeona kanisa
lake”
Alizidi kuongea janet huku wengi wakiwa hawajui…
“weeee,
ina mana mchungaji Jacob ana kanisa lingine”
Aliuliza mmoja wa marafiki
wa janet
“sio la mchungaji Jacob ni la adam”
Aliongea janet tena
kwa kujiamini haswa….
“we janet wewe, unajua bwana yesu hajafundisha
uongo”
“sasa huu ni uongo au ukweli”
“skia adam, hana mke, adam
bado anaishi kwa baba yake… Adam bado ni mdogo, hawezi kabidhiwa kanisa… Kwanza
huo upako wa mpaka apewe kanisa kautoa wapi”
“heeeeeee Cecilia,… Ivi
hujui kuwa uchungaji ni wito toka kwa mungu.. Uchungaji aio lazima awe……
“
Ghafla janet alinyamaza baada ya kumuona mzee wa kanisa akipita maeneo
hayo, mana wanacho kiongea ni siri, bado hakikuwekwa wazi kuwa kijulikane, ni
nyepesi nyepesi tuuuu…. Baada ya mzee wa kanisa kupita janet aliiacha ile mada
mana ni hatari sana kwa midomo yao
“ester, unajua mimi nawadokezeeni
tu.. Sasa tuachane na hii mada”
“ok, afu… Leo nimemwona eva karuka ruka
pale alivokutana na mama mchungaji”
Aliuliza ester mana jenet kwa fununu
hajambo
“hapo ndio hata mimi nikajua kuwa adam anakuja wiki hii… Mana
baada ya pale nikamfuata bite mdogo wake eva ndio nikamuuliza mbona dada yako
amekuwa na furaha sana.. Ndio akaniambia kuwa mchumba wake
anakuja”
Aliongea hivyo janet huku akina Esta na wengine
wakacheka….
“ivi janet, eva anajidanganya kabisa kuwa ataolewa na adam….
Aache kutafuta mtoto wa Bishop kama yeye, aje aoe maskini kuliko hata
mimi”
“we ester wewe, chunga mdomo wako huo… Ukisikiwa unaongea huo
ujinga, mi simo”
Aliongea janet huku akishika mkoba wake na kuanza hatua
kana kwamba hawahitaji maongezi yanayo muhusu eva…
Baada ya
masaa kadhaa kupita sasa tukiwa huku nyumbani kwa Bishop Jacob, wakiwa mezani
wanapata chakula cha usiku…. Na hapo walikuwa wakiomba kabla ya kula,… Kama
kawaida wa wakristo lazima waombe maombi marefu tena wengine huchukua hata
dakika 10 kwa maombi tu… Familia yenye watu watano, baba na mama na wasichana
watatu… Baada ya kuomba walianza kula huku vikisikika vijiko tu vikigongana
katika sagani, yaani hawaruhusiwi kuongea wakati wa kula… Ukweli walikuwa ni
matajiri sana, yaani haikuwa mboga saba kama tunavyojua… Hata mimi mwandishi,
naona kuna vibakuli zaidi ya kumi… Yaani, yaani walizidisha hata sio ile mboga
saba… Walimaliza kula hatimae mfanyakazi anapata kazi ya kuwaandalia maji kila
mmoja wao, japo wasichana hao wana malezi bora hivyo hawahitaji kuletewa maji..
Wanayafuata wenyewe,…. Baada ya hapo watoto wote waliondoka na kuingia kwenye
vyumba vyao, mana kila mschana ana chumba chake… Jumba lenyewe kubwa kama
kanisa…
“haya baba mtoto…. Mwanao ndio huyo anakuja….umemuandalia nini
mana sasa akija ni kazi moja hapa mtashindana weeeee”
“ahahahahahaha….
Mama Jessica,.. Mimi nina tabu gani… Kanisa lake limeshafaa, akija nitawaita
wazee wa makanisa yangu yote… Kama anafaaa kuwa mchungaji
aendelee”
“kama anafaa?.. Kivipi.. Kwani huko shule kaenda kufanya nini
kama sio kujiongeza… We si unamjua mwanao, yaani kabla hajaenda huko, akishika
tu mtu kichwa anadondoka chini na hapo hajaenda Nigeria, je akirudi
itakuwaje”
“na ndio mana nikampeleka kwa rafiki yangu, yaani najua
makanisa yote ni ya mwanangu.. Sina pingamizi juu ya hilo”
“mmmmhhh
angalia msije mkaanza ushindani, mana kazi ya mumgu yahitaji uvumilivu toka kwa
bwana yesu… Tumuombee mtoto wetu huko aliko”
“milele
amina”
Walikuwa wakiongea huku wakipata juis kwa
mbali,…
Baada ya siku hio kupita na leo ni siku ya jumatatu, mr
Jacob amiwa katika shughuli zake, mana unaambiwa tii wito wa mungu kisha
katafute kula… Hivyo siku za juma bishop Jacob yeye huwa bize na kazi zake, na
katika makanisa yake kuna wale mapasta wadogo wadogo ambao watakuwepo wiki yote
kwa ajili ya maombezi, na Jacob ana ofisi yake inayohusu kanisa… Hivyo ya
kanisani ni kanisani na kazini ni kazini… Bishop jacob ni mtu wa kumuomba mungu
kila wakati, yeye na Biblia, kwani hata kazini kwake ana Biblia aina zote,..
Wafanyakazi waliopo hapo ni wakristo wote, yaani kila mfanyakazi ana rozali yake
mezani, bwana Jacob akiingia ofisini kwake ni yeye na neno la mungu, hataki
kupitwa na lolote….
Akiwa hapo ofisini mara ghafla simu yake inaita,
alikuwa ni Bishop james, yaani huyo ni kipawa mwenzie mwenye kipawa cha
Bishop,…
“tumsifu Yesu Kristo james”
Alisalimia jacob huku
akitabasamu kwa mbaali
“milele amina… Naona kwenye kikao sikuoni huku
njiro”
“aahhh nimetingwa kidogo… Si unajua kijana wangu hayupo sasa hivi
nahangaika mwenyewe, mana angalau alikuwa anafuatilia miradi ya baba yake lakini
sasa hayupo”
“aaahhh lakini nadhani ni wito wa mungu juu ya kulitangaza
neno la bwana yesu alie hai”
“ndio, na hana muda atarudi”
“yesu
asifiwe bwana jacob”
“milele amina… “
“basi nilikuwa nakujulia
hali tu.. Mana sijakuona katika kikao cha leo”
“hakuna shida mtumishi wa
Mungu”
“haya siku njema na yesu akutangulie”
“milele amina… nawe
pia”
Simu ilikatika na mzee akaendelea kupata neno la mungu,… Na uzuri
wa wakubwa kama hawa hua wana vitabu vya mungu vya pande zote mana hata hapa kwa
Bishop jacob, ana kitabu cha Kiislamu, ni kawaida ya viongozi wakubwa hua lazima
ujue neno la upande wa pili ili kujua kama kuna utofauti na upande wao,.. Hata
papa mwenyewe ana kitabu cha Kiislamu,… Na ndivyo inavyotakiwa kujua upande wa
pili wa dini ya mwenzio… Na sio kuwa hawakiwezi kukisoma, wanakiweza haswa… Na
sio hao tu hata wale viongozi wa dini ya kiislamu kuna basdhi yao wanaijua
Biblia kuliko hata wewe Mkristo ambae ni kitabu chako
kotakatifu..
Tukija huku kanisani alionekana eva akiwa anaomba
sana… Na siku hio kulikuwa na maombi ya kawaida tu, na hakui na watu wengi kama
ilivyo Jumapili,… Eva ni mschana aliopendelewa kila aina ya mwili wake, yaani
kiukweli ana haki ya kuitwa mrembo wa kanisa, japo haitowahi kutokea lakini hio
nafasi inamfaa….
“eti yule, aje kuitwa mama mchungaji.. Inawezekana
kweli”
Aliongea Janet wakiwa katika mlango wa kuingilia, mana eva
alikuwa bize na maombi huku akiwa kafumba macho yake….
“nashangaa hata
mimi…. Ww ulizani adam ni wa mchezo mchezo”
“lakini janet? mbona familia
zao zinajuana”
“hata kama esta, ila sio rahisi adam kumuoa
eva”
“hebu kaone kanajifanya kanajua dini sanaaaaa”
“weeee janet
sio vizuri, huko tunapokwenda sasa ni unafiki jamani janet… Hebu tuyaache
hayo”
Lakini sasa kumbe walipokuwa wakiongea walikuwa wakisikiwa na mzee
wa kanisa… Kitu ambacho hajakipenda mzee huyo…. Lakini hakuwaambia kitu
chochote…
“huyu mzee katokea wapi”
Aliongea janet huku
wakimshangaa
Baada ya siku hio kuisha,… Bwana Jacob akiwa
kazini ikiwa ni siku ya Jumanne,.. Alikuwa na rafiki yake aliokuja kumtembelea
ofisini kwake,..
“yusi ni mkuu, madam tumekutana leo basi yesu katenda
miujiza”
“ni kweli bwana Jacob, yesu amefanya makubwa na nadhani
anakwenda kufanya makubwa”
“yesu asifiwe bwana
yohana”
“amina”
“haya nipe taarifa za jimbo
lako”
Aliuliza kumaanisha ampe taarifa ya makanisa yake yanaendeleaje…
Mana hata huyu bwana yohana ni Bishop kama alivyo bwana Jacob.. Hivyo vipawa
vyao ni sawa..
“bwana weee, nataka Yesu afanye miujiza juu ya vijana
wetu”
Aliongea bwana yohana…. Huku bwana Jacob asielewe maana ya maneno
ya yohana…
“ni kweli ila sijakuelewa”
“aaahhhh, juzi uliniambia
kijana wako yupo karibuni kuja… Na ulisema ana kanisa lake lipo tayari, nami
najua kabisa kijana wako baado hawezi kukabidhiwa kanisa bila kuoa… Nina binti
yangu, kwanini yesu asifanye miujiza juu yao”
Aliongea bwana yohana huku
bwana Jacob akitabasamu…..
Huku kanisani masikini eva ni mtu wa
maombi hataki kushindwa na shetani juu ya watu wanaomuandama kumbe jana mzee wa
kanisa alimtonya kuhusu akina janet… Sasa eva wa watu kila kukicha ni yeye na
maombi, anamuombea mchumba wake afike salama… Lakini sasa uchumba wao unaingia
dosari, bwana yohana nae ana binti yake, nae anataka waowane na mtoto wa Bishop
jacob…..
Sasa huku ofisini katika maongezi ya bwana Jacob na
bwana yohana, yanayo husu muunganiko wa watoto hao wawili, na ni kweli sheria za
kiwa mchungaji shariti uwe na mke… Japo wengi wanafosi tu.. Sasa leo bwana
yohana anakuja kuzima ndoto za eva mwenye tegemezi la kuolewa na adam, mtoto wa
mr Jacob……
Katika dunia hii, hakuna kitu
unachoweza kukiwekea mia kwa mia kuwa utakipa, na si katika simulizi kama hizi
bali wapo watu waliotamani kupata kitu fulani katika maisha lakini hawakukipata
kwa vizuizi tofauti tofauti… Sasa tukija katika upande wa mapenzi, unakuta wewe
mwanaume kuna mwanamke unatamani sana kumuona, lakini kuna vigezo au vizuiz
vitakavyo sababisha usimuoe.. Au wewe mwanamke una mwanaume unatamani akuoe
lakini kuna vizuiz vingi sana ambavyo vitasababisha
asikuoe..
Sasa kwa mwanadada eva, masikini ya mungu, wao hali
ya maisha kwao ni ngumu, yaani ni masikini lakini ni mcha mungu.. Kila kukicha
yeye na ibada yeye na kanisani, yeye na Biblia, hio yote ni kuiombea familia
yake na yeye mwenyewe apate mume bora katika maisha yake, na katika akili yake
tayari keshapata mchumba, tena wanapendana sana, na mchumba mwenyewe ni Adam,..
Na Adam huyo huyo ndio anapigiwa debe na Bishop yohana kuwa amuoe mtoto
wake….
Sasa tuje huku ofisini kwa mr Jacob
“kwanza
tumsifu yesu Kristo mr yohana”
Aliongea mr Jacob huku akitabasamu kwa
mbaali kuonesha kiwa ombi la bwana yohana ni zuri sana ila litakuwa na
mashaka…
“milele amina”
“umeleta jambo zuri sana tena katika
wakati muafaka… Lakini katika uwepo wangu pale nyumbani, nasikia sikia kuhusu
mchumba wa adam, ila sijafuatilia sana kwa ukaribu mana mimi sikutambulishwa
lakini mke wangu analifahamu hilo… Sasa huoni katika hali hii tunaweza
kuwavurugia”
Aliongea mr Jacob, mana kweli anasikiaga habari za Eva kuwa
ni mchumba wa adam… Lakini hakutambulishwa…
“ni kweli bwana Jacob,..
Hata mimi mtoto wangu nilizisikia habari kuwa na mchumba.. Ni mwinjilisti mmoja
hivi sasa kwa hadhi ya familia yangu, mtoto wangu hawezi kuolewa na mwinjilisti…
Mimi kama baba nilikataa hilo na kakubali… Kwanini usitumie nguzo ya uzazi..
Mana wakijichagulia wenyewe tutaonekana sisi hatuna malezi bora.. Na istoshe
mtoto wangu nimemlea katika imani.. Yaani sijui niseme nini… Atukuzwe bwana
yesu”
Aliongea mr yohana huku akimsifu yesu Kristo kwa neema
zake
“amina”
Aliitikia mr Jacob huku kweli akiingiwa na maneno
ya Bishop mwenzie kama yeye…
“mr Yohana… Kweli mwanangu a DC am
ananisikiliza sana, lakini kwenye hili swala… Hahahahaha, sina
hakika”
“basi inaonekana mtoto wako hujamlea vyema”
“tena hakuna
mtoto mwenye heshima kwangu kama adam”
“najua na ndio mana nimekufata
rafiki yangu wa zamani sana”
“basi wewe niache hilo.. Nitalifanyia
kazi”
“bwana yesu ni mkuu… Hakika hawezi shindwa jambo jema mbele za
mungu”
Saa hio hio maombi yalishuka, yaani hapo hapo kanisani..
Wafanyakazi kusikia maombi nao wakafumba macho na kuanza kuyapokea maombi toka
kwa watumishi hao wa mungu….
Tukija huku kanisani eva akiwa
anatoka kanisani baada ya maombi, alikuwa akipita pita katika paking za magari,
ikiwa ndio ngazi ya kupandia juu, hivyo akiwa kushika Biblia yake tayari kurudi
nyumbani… Akiwa njiani alikutana na akina Janet…
“shalom”
Alitoa
sifa kama salamu kwa akina janet,
“shalom eva”
“yesu asifiwe
kwakweli”
Aliongea eva kutoa sifa ya bwana wake mwokozi alie
hai,…
“unatoka wapi eva”
Aliongea janet lakini ni kama
kumkebehi, mana njia wanayokwenda ndio hio hio anayo toka eva, hivyo hakukuwa na
haja ya kumuuliza sana
“natoka kanisani janet… Esta hali
yako”
“safi tu”
Aliitikia huku akiangalia pembeni, lakini eva
alishaambiwa na mzee wa kanisa kuwa watu hao hawana ahueni nae, hivyo hilo
analijua vizuri yu na hana shaka nalo
“sawa safari njema
kwako”
Aliongea janet huku wakipishana,.. Wakati huo yapata saa 10 za
jioni katika misa ya saa 10 ila akina janest wao walichelewa kidogo hivyo eva na
waumini wengine walishamaliza ibada ya maombi ya siku hio…
Sasa
ikiwa masaa yamekwenda sana na sasa ni saa mbili za usiku,… Tukiwa katika nyumba
ya bwana yohana, nae ana familia kubwa tu kama ya Bwana Jacob,… Ila bwana Yohana
yeye ana watoto wanne.. Wakiume wawili na wakike waili.. Ila bwana Jacob yeye
ana wakike watatu na wakiume mmoja… Sasa wakiwa wapo mezani wanapata chakula
kama vile ilivyo kwa mr Jacob wakati wa kula hakuna kuongea,.. Na watoto walipo
maliza kula, kila mmoja alishika kona yake ya kwenda chumbani kwake…. Na hapo
baba ana jambo la kuongea na mama na ndio mana watoto wamesambaratika kila mmoja
kona zake…
“Mama Catherine…. Unajua tayari nimeshaongea na mtumishi
jacob kuhusu watoto wetu”
Aliongea bwana Yohana… Lakini mke wake
alionekana kutopendezwa na hili mana kama vile atawauzi watoto
“lakini
baba Catherine… Huoni kuwa utamnyima mtoto raha ya maisha… Mana umeuvunja
muelekeo wake”
Aliongea Melissa ambae ndio mama wa familia ya mzee
Yohana…
“mimi ni mzazi ni lazima nifanye maamuzi kama mzazi…. Catherine
ni lazima aolewe na mtoto wa mr Jacob”
“nitafanya nini sasa… Sina cha
kufanya juu ya maamuzi yako mtumishi wa mungu”
“hayo ndio majibu sasa
sio kupingana”
Mama alikubali lakini ni ile kishingo upande… Sasa pendo
ambae ndio mtoto wa pili akitoka Catherine mwenye miaka 21 anakuja huyu pendo
mwenye miaka 16 hivi au 17..sasa alisikia yale maongezi ya baba na mama… Saa
ngapi hajakimbilia chumbani kwa dada yake….
“dada… Dada…
“
Aliita pendo huku dada akiitikia kwa hasira, mana alikuwa usingizini
tayari keshalala…
“nini we pendo, hujalala tu jamani mdogo
wangu”
“nimesikia kitu kwa baba”
Aliongea upendo huku Catherine
akiamka kwa hofu… Mana baba yake kawa mkali sana kwa sasa…
“kitu gani
tena”
“baba kamwambia mama… Utaolewa na yule mkaka hensam”
Sasa
upendo kumbe anamjua Adam vizuri sana…
“mkaka hensam??? Mkaka hensam
ndio nani”
“dadaaa…. Unakumbuka mwaka uliopita, tulikwenda kwenye harusi
ya rafiki yako wanjiku… Sasa yule aliokuwa akifungisha ndoa ya wanjiku,… Mtoto
wake sasa ndio anatakiwa kukuo wewe”
“unamaanisha mtoto wa mchungaji
jacob”
“haswaaaa”
“anaitwa adam”
“ndio huyo huyo… Japo
naskia hayupo”
“ndio hata mimi najua hayupo… Ila baba ndio
kasema”
Aliuliza kwa umakini mkubwa sana Catherine huku akionekana kama
kuipenda taarifa hio…
“ndio.. Na mama kakubali… Dada yule mkaka ni
hensam afu kwao kuna hela”
“Peleka ujinga huko.. Kwani siai hatuna
hela”
“sawa ila wao wametuzidi ai tuseme ukweli tu”
“ondoka
nenda kalale”
Upendo aliondoka lakini huku nyuma, Catherine alionekana
kushika kifua chake na kuanza kutabasamu… Kumbe nae anampenda adam sema alisikia
kuwa adam ana mchumba wake, hivyo akakata tamaa ya kumpenda, sasa ile ndoto yake
ni kama imerudi tena kivingine…. Catherine alikuwa ni mzuri.. Mweupe, ana umbo
la kipekee, yaani tuseme uzuri wa eva na Catherine ni sawa sema tofauti ni
rangi… Catherine ni mweupe, na Eva ni maji ya kunde,.. Ila wote wana maumbo ya
kuvutia… Ila Catherine yeye, kidogo anapenda mavazi ya kisasa, hapo ndipo
atakapomshinda eva..
Catherine aliingia Google na kuanza kumtafuta adam
katika mitandao ya kijamii,…. Alipomuona roho ilimpasuka na kujikuta
anamuita..
“mume wangu… Mungu kajibu maombi yangu,.. Nilikuwa nikikuota
usiku na mchana lakini leo ndoto zinakwenda kuwa kweli”
Aliongea hivyo
kwa sauti huku akiiangalia ile picha….
Mara mama yake kaingia
hapo chumbani, kumbe mama alikuwa akilia jinsi mtoto wake alivyochaguliwa mume…
Lakini mama alipoingia hakujulisha kama alikuwa akilia…
“hujalala
tu”
“ndio mama… Hata usingizi hauji”
Aliongea Catherine huku
akiificha simu yake ili asionekane kama kakubali sana kuolewa na
adam..
“au umesikia wazo la baba ako ndio mana hujalala”
“wazo
gani tena hilo mama”
Catherine alijifanya hajui chochote kuhusu wazo la
baba yake
“amesema eti uolewe na mtoto wa mchungaji
Jacob”
“mmmhhhh mamaaaa… Sasa na mwinjilisti wangu
je”
“Catherine, ina maana bado hujaachana na huyo
mpumbavu”
“yesu wangu mama… Ina maana keshakuwa mpumbavu
tena”
Kumbe mama aliongea vile kwasababu baba alikuwa akipita huko kwa
nje, sasa hakutaka kujulikana kuwa yupo tofauti na mumewe,…
“mamaaaaaa
jamani”
“ah ah… Sikia sasa… Mimi sipo tayari uolewe na mtoto wa jacob,
mana yule ana mchumba wake, afu istoshe yule kijana katembezwa sana na baba yake
nchi mbalimbali, anajua starehe za kila aina… Mi sitaki uolewe
nae”
Catherine alinuna ghafla, mana hata huyo mwinjilisti sio kuwa
alimpenda sana,…
“mama mbona mimi nimekubali”
Mama kusikia hivyo
alishtuka na kumwangalia mwanae kwa hasira
“unasemaje
wewe”
“mama, nilikuwa nikimpenda sana adam, nilikuja kupoteza mawazo juu
yake baada ya kusikia ana mchumba”
“ivi Catherine nikuulize
swali”
Mama alibadirika kabisa na kua na hasira…..
“swali gani
tena mama”
“ivi usichana wako unao wewe…. Mana ile familia ni ya
kitajiri haswa, na haitaki mschana ambae hana bikra…. Sasa kama huyo mwinjilisti
wako umeshampa…. Jua adam sio wako mama.. We jishaue
tu”
Katika maisha ya kuoa kuna
wanaume hawajali uthamani wa mwanamke, nikimaanisha BIKRA… Na wengi wetu hua
tunaoa wanawake wasio na bikra, lakini kuna mahali mwanamke akukosa bikra tu,
basi hata kuolewa kwake ni kwa tabu, hususan Zanzibar… Mzanzibari akikosa bikra
ataolewa sawa lakini ataishi kwa masimango sana, na hata familia haitompenda
sana mana wanahisi kaleta nuksi katika familia yao… Au kama hana bikra pia
huenda akaolewa mke wa pili… Kule wanajali sana bikra tofauti tanganyika yetu..
Hua tunaoa tu… Lakini kama na sisi tungelikuwa na mikakati kuwa bila bikra
mwanamke haoleki,.. Walahi nakuapia ungekuta kila mschana ana bikra huko mtaani…
Lakini sasa hakuna.. Na pia Tanzania wapo ambao bila mwanamke asie na bikra
haoi….
Sasa tukiwa katika simulizi hii ya YOUNG PASTOR, kumbe
mr Jacob hataki mtoto wake aoe mwanamke asie na bikra,… Sasa hapa Catherine
alikuwa akiulizwa na mama yake kuhusu usichana wake upo au keshampa yule
mwinjilisti wake…
“ivi usichana wako unao wewe…. Mana ile
familia ni ya kitajiri haswa, na haitaki mschana ambae hana bikra…. Sasa kama
huyo mwinjilisti wako umeshampa…. Jua adam sio wako mama.. We jishaue
tu”
Aliongea mama huyo aitwaye Melissa, ambaye ndio mke wa mr Yohana au
Bishop yohana..
“niambie, mbona wantumbulia macho mimi”
Mama
alikuwa mkali sana juu ya mtoto wake, mana yeye roho ilikuwa ikimuuma kwa
kitendo cha mtoto wake huyo kuchaguliwa mchumba ingali ana mchumba
wake,….
“mama, toka nizaliwe… Simjui mwanaume wa aina yeyote ile… Kama
huamini nikague uone”
Aliongea Catherine huku akiamka na kuanza kufunua
ahumizi lake ili mama amkague
“nitolee ujinga wako apa”
Aliongea
mama yake Catherine huku akiondoka na kufunga mlango kwa hasira,… Sasa swali
linakuja je? Mbona mama hataki mtoto wake aolewe na adam, kwanini??… Hapo kuna
jambo zito hatulijui tu…
Wakati Catherine bado anaendelea kuangalia
picha ya Adam katika mitandao ya kijamii, akiwa anahubiri katika moja ya
makanisa yao mwaka uliopita, mana mwaka huu wote hakuwepo Tanzania, hivyo hizo
ni picha za awali tena katika tovuti ya kanisa lao, mana adam hata mitandao ya
kijamii hajawahi kujiunga… Sasa Catherine alichukuwa picha kadhaa katika tovuti
moja inayomiliki makanisa yote, yaani makani yote ya Bishop Jacob, habari zake
hupatikana katika tovuti moja… Hivyo Catherine alichukuwa picha kadhaa na
kuziposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kuandika maneno kadhaa katika
picha hizo.. Na wakati huo ni usiku yapata kama saa 4
hivi
Kesho yake ikiwa ni siku nyingine tena,… Catherine aliamka
akiwa na furaha sana kwa swala lile, sasa inashangaza kuwa kwanini Catherine
alimpenda huyo mwinjilisti ingali alikuwa akimpenda adam… Hapo napo kuna
maswali…. Catherine hata kuoga kwake, alikuwa akimuwaza tu adam, yaani sijui
ampe nini baba yake kwa kufikiria jambo kama hilo… Hivyo Catherine yupo tayari
Eva amkose adam…. Wakati huo mzee yohana nae alikuwa akijiandaa kwenda katika
shughuli zake za kawaida, mana ukishatoa wito ulioagizwa na mungu wako juu ya
watu wake basi hakuna shida hata ukienda kutafuta kula…
Wakati
huo huku nyumbani kwa akina Eva,… Msichana mpole mtaratibu, akiwa anafanya usafi
huku akiimba kwaya za kumsifu bwana yesu…
“yeeeesuuu alinitendea weema,
na kila siku nipo naeeee”
Sasa akiwa anaimba mara ghafla mama yake
katoka…
“heee eva mwanangu hujaenda kanisani”
Aliongea mama huyo
wakati huo anatoka nae kuelekea kanisani,..
“mama, bite hayupo kaenda
shule… Sasa nani atafanya usafi”
“sawa.. Hebu hakikisha misa ya pili
haikosi sawa mwanangu”
“sawa mama… Tumsifu Yesu Kristo”
“milele
amina”
Mama alibeba Biblia yake huku akielekea
kanisani…
Sasa huku kanisani, kuna wale wasichana ambao hawapo
kwa ajili ya kumwomba Mungu wao, kazi ni kufuatilia maisha ya watu, hususan ya
mwanadada Eva,…
“heheheheeeee, Yesu kafanya miujiza kwakweli
janet”
Alikuwa ni esta aliomkuta janet akiwa katika bustani ya hapo
kanisani anajisomea Biblia,…
“wewe esta.. Hebu tulia kuna ukurasa
unanipa ashki ya kuusoma”
Aliongea Janet ambae ndio mbea mkubwa lakini
cha ajabu umbea aliokuja nao esta Janet haujui…
“ivi janet, ulijuaje
kuwa eva hatoolewa na adam”
Sasa wakati wanaongea hilo, na mama yake eva
ndio anatokea na kusikia hilo neno, japo eva wako wengi, lakini aliposema na
adam… Huyu mama ikamjia tu huenda ni eva wake,..
“una maana gani
esta”
“iv unamjua yule mschana wa mtumiahi yohana”
“yuleeee…
Ndio ana wasichana wawili.. Catherine na Pendo”
“sasa huyo Catherine…
Ona alichoandika juu ya picha ya adam”
Esta alifungua simu yake na
kumwonyesha janet…..
yalikuwa ni maneno yalioandikwa
katika picha alioipost Catherine katika akaunti yake ya Instagram,… Sasa janet
alivyo hakaushi kaamka kwa furaha na kupiga kelele
“nilisema mimi….
Masikini na tajiri wapi na wapi… Mi najua tajiri kwa tajiri masikini na masikini
mwenzie”
Sasa mama eva ndio anasikia hizo habari na kushindwa kuelewa
inakuwaje hapa, mana kasikia kila kitu kasolo tu hayo maneno yalio andikwa
katika picha ya adam huko Instagram,…
Mama roho ilianza kumuuma, mana
mtoto wake atakuwa katika hali gani endapo atasikia taarifa hizi..
“Eehh
mungu wangu… Pokea maombi ya mwanangu”
Aliongea mama huyo huku
akinyoosha mikono juu katika msalaba uliopo mlango hapo ikiwa na sanamu la Yesu
katika msalaba huo…. Mama aliingia ndani lakini akina janet hawakujua kuwa mama
eva aliwasikia wakiongea jambo hilo.. Mama alitamani kumwambia mwanae kupitia
simu, asije kanisani lakini sasa alisita mana ni sehemu ya kila mja kumwomba
Mungu wake…
Sasa huku nyumbani kwa akina adam, au Bishop
Jacob,.. Akiwa anafungiwa tai na mke wake…
“sisi leo hatutofika mana
tunakwenda kumpokea mtoto…. Na wewe pia usichelewe huko”
Aliongea mama
huyo huku akimkaba mtumishi tai yake…
“nyie kampokeeni tu…. Ila
nitamjulisha mr Yohana kuwa, amtaarifu mtoto wake kuwa adam
anakuja”
Sasa mama adam yeye bado hajagusiwa kuhusiana na habari za adam
kumuoa mtoto wa mr yohana..
“sasa huyo mtoto wa mr yohana na adam
wanahusiana vipi”
“heeeeeeee, mama Jessica, ivi
sijakwambia”
“umeniambia lini mimi jamani baba Jessica”
“Mr
yohana, kasema yupo tayari mtoto wake aolewe na adam… Na sasa adam anatakiwa
kuwa mchungaji rasmi, na kama ulivyosema kuwa hawezi kupewa uchungaji bila kuoa…
Sasa sio vibaya kumuoa mtoto wa yohana”
Mama kusikia hayo maneno, kwanza
alishika kifua chake kuashiria hio habari kwake sio sahihi kabisa… Mana huyu
mama anamjua mtoto wa kike mkubwa wa mzee Yohana, ni mschana mzuri sana na ana
tabia nzuri lakini… Mama adam anamjua kiwa Catherine havaagi nguo za heshima
japo sio mhuni lakini nguo zake ni za kisasa mno, kitu ambacho mama adam sidhani
kama atakubaliana nacho…
“sasa hapa tunapoteza muelekeo wa mtoto
wetu”
Aliongea mama Jessica huku akiwa hana hata nguvu, mana mume
akiamua kitu, basi hata mke kuzuia ni asilimia chache sana….
“kwanini
mama Jessica….. Mtoto wa mr Yohana si unamjua wewe…. Sio mbaya akiwa mwali wako…
Nipe koti langu niende kanisani”
“baba Jessica…. Adam ana mchumba wake
lakini”
“sikutambulishwa, hivyo simjui… Aoe mwanamke ninaemjua mana mr
Yohana ana maadili mazuri hivyo najua hata watoto wake watakuwa kama baba
yao”
Mzes Jacob alichukuwa koti lake kisha huyo kaelekea katika gari
yake.. Na wakati huo mr Jacob anampigia aimu mr Yohana kuwa amwambie mtoto wake
Catherine aelekee Airport mana adam anawasili leo katika uwanja wa ndege wa KIA
(Kilimanjaro International Airport)
Mama alikuwa akisikia taarifa hio
ikotolewa kwa njia ya simu.. Lakini mama akiwa na huzuni juu ya mtoto wake
kuozeshwa mwanamke ambae ana tabia ya kisasa, japo kwa namna moja ama nyingine
ni mschana mstaarabu, lakini mavazi yake tu ndio shida kwa jamii.. Mana hata
kanisani kwao yeye hajali anachokivaa…
“mama, mbona umekuwa mnyonge
hivyo, na ulisema leo unapika chakula kizuri kwa ajili ya kaka
adam”
Alikuwa ni Jessica mtoto wa kwanza katika familia hio, ana miaka
28 na adam ana miaka 24,… Kisha anafuatiwa na martha 20 na maria 15, yaani mama
kawapangilia vyema watoto wake, wasipishane sana….
“Jessica, ivi
umelisikia wazo la baba yako”
Aliongea mama huyo kama vile anataka kumpa
taarifa hio…
“taarifa gani tena mama”
“kasema, Adam atatakiwa
kumuoa mtoto wa mr yohana”
“Whaaaaat???…. Yule mvaa vimini au
yupi”
“huyo huyo”
“baba kawaza nini lakini”
“mimi hata
sijui”
“ila mama, yule mschana ni mzuri haswa”
“mimi sihitaji
uzuri wa sura au umbo… Nataka mwanamke mwenye tabia nzuri”
“sasa mama…
Na eva wa watu maskini kama namuona vile”
“mimi hata sijui nitamwambia
nini yule mtoto, mana anavyoniheshim… Mana anajua fika tayari mimi ni mama mkwe
wake… Na nimeahamkubali eva kwa asilimia zote”
“sio wewe tu…. Hata mimi
nampenda sana eva… Ila kwa jinsi adam anavyompenda Eva… Heeee patachimbika hapa
mjini”
“kwanza… Mpigie simu eva aje nyumbani… Twende naye
Airport”
“sawa”
Sasa huku nyumbani kwa akina Catherine,
baada ya kupata taarifa kuwa adam anakuja leo na ndege ya saa kumi jioni… Huezi
amini Catherine katoka kanisani mpaka nyumbani, hapo kitandani kwake kumejaa
nguo na hajui avae ipi ili aende Airport kumpokea mtarajiwa wake… Na taarifa hio
kapewa na baba yake live bila chenga, japo alianza kuisikia toka jana… Sasa hapo
hajui avae nguo gani,.. Mama vimini…..
Sasa huku kanisani mzee
Jacob akiwa yupo kwenye lifti kuelekea ibadan… Alishika simu yake na kumpigia
mtoto wake….
“halooo, shalom”
Huyo ni mzee Jacob, lakini sauti
ya adam haisikiki hapo
“habari ya safari mwanangu”
Ni huyo huyo
Jacob ama Bishop Jacob
“ok sasa…. Katika watu watakao kupokea hapo
Airport, mmoja wapo ni mtoto wa mr Yohana”
Aliongea mzee Jacob huku kama
vile adam kamuuliza kitu mzee wake
“najua hujui baba…. Ila ndio atakuwa
mkeo, baba yako nakuchagulia mke mwenye heshima bora.. Anaeijua dini na ana
wlimu kama ulivyo mwanangu”
Aliongea mzee huyo kwa kumsifia
Catherine…
“nimeshasema mimi baba yako.. Na hakuna wa kupinga hilo… Huyo
mchumba wako mimi simtambui… Na usipofanya hivyo lile kanisa nitalibinafsisha
kwa watu wengine”
Adam alionekana kukataa swala hilo, lakini mzee
akachimba mkwara wa hali ya juu kwa mtoto wake
“adam, hata wazee wa
kanisa hawawezi kukubalia kuwa mchungaji endapo hutakuwa na mke… Mchumba wako
yupo hapo Airport anakusubiri.. sawa”
Aliongea mr Jacob huku akiwa kama
anamlazimisha mtoto wake amuoe Catherine…
“hayo sasa ndio maamuzi
mwangu… Hongera kwa kunielewa baba yako”
Mzee Jacob alionekana kuwa na
furaha juu ya adam kukubali wazo la baba yake…
Baada ya masaa
kadhaa kupita, familia ya mr Jacob ikiwa imejaa katika uwanja wa ndege mkoani
Kilimanjaro,…. Lakini kati yao mtoto wa mr yohana yupo hapo hapo.. Na pia Eva
nae yupo hapo hapo.. Lakini sasa Catherine yeye anajua tu kuwa adam ana mchumba
lakini hamjui huyo mchumba mwenyewe, hivyo hapo EVA NA CATHERINE hawajuani
kabisa, ila wanajuana tu ile kiumini umini, Eva anamjua Catherine kama mtoto wa
Bishop Yohana, lakini hajui kama ni mchumba mwenzie….. Huo ni ubabe alioufanya
mama yake adam, na wakati huo masikini eva hajui lolote kuwa kuna taarifa za
kitoolewa na Adam…. Eva alikuwa anaruka ruka kwa furaha…. Masikini ya mungu,
laiti angelijua kuwa hapo hana chake, basi hata hapo Airport asingetakiwa kuja,
sasa mama Jessica au mama adam hakumwambia kitu eva…
Dege kubwa
liliokuwa linatua katika uwanja huo, yaani eva alitamani hata kuifuata ile ndege
kabla haijasimama, lakini kapoozeshwa na mama mkwe wake, mana ni mwaka sasa
umepita hajamuona mchumba wake,.. Walishuka abiria wote,… Na Adam alikuwa ni
abiria wa mwisho kushuka
Laaaa haulaaaa…..
SHARBIN RASHIDI
KINGAZI ndio mwenye jina la Adam katila simulizi hii, na ndio yeye akiwa
kapigilia suti yake saafi… Kweli mwenye mali ni mwenye mali tu… Eva ndio mtu wa
kwanza kumuona adam wake,… Yaani hivyo alivyoanza kukimbia, utapenda yani…. Sasa
Catherine nae anashangaa huyu anaeanza kukimbia kwa kujiua ua ni nani… Hakuta
kujua sana, ila nae alianza kumkimbilia adam… Wakati huo adam kashika kibegi
chake.. Mana begi kubwa linabuluzwa na wahudumu wa hapo uwanjani…. Maskini Adam
kasimama na asijue amkumbatie yupi kati ya wawili hao
PATAMU
APO……
Katika maisha ya sasa tunasema mwanaume kama
mwanamume lazima uwe na maamuzi ya kiume,.. Adam ni kijana mpole sana na
kalelewa katika mazingira ya dini.. Na katika kukua kwake kote hajui undani wa
mwanamke hata mmoja, yaani haijui siri ya mwanamke ikoje, mana yake ni kwamba
hajawahi kutembea na mwanamke, na mwanamke alioapa kumuoa ni eva pekee ambaye
nae ni vivyo hivyo hamjui mwanaume,.. Adam kabla hajaamua maamuzi yake
alikumbuka siku anapanga safari ya kwenda Nigeria kimasomo
zaidi..
KABLA YA KWENDA NIGERIA
“eva… Mimi
kesho nasafiri.. Naomba uwe makini na mapepo wachafu juu yako”
kitendo
cha Eva kusikia kuwa Adam anasafiri, moyo ulimpasuka huku akishika kifua
chake,…
“baba mtumishi, unakwenda wapi.. Na unarudi lini… Hivi kuna
usalama kweli huko”
Aliongea eva huku akimshika adam bega
lake,..
“nakwenda kimasomo,… Si unaona kanisa langu linajengwa… Hivyo
wacha nikajiongeze angalau”
“lakini baba mtumishi, upasta siokusoma,
upasta ni wito toka kwa mungu… Sasa kwanini lakini”
“ni kweli,.. Wito
numeshaupata na nimeupokea… Na hata sasa naweza kukabidhiwa kipawa hicho, lakini
kuna njia ambazo natakiwa kupitia.. Kwa mfano mwanamke anaetaka kuolewa,.. Kabla
hajaolewa wanasema lazima awekwe ndani, sasa ule wakati yupo ndani, kuna mambo
mengi anafundishwa jinsi ya kuishi ndani ya ndoa yake… Hivyo mimi nakwenda
kupewa makatazo yasiofaa nikiwa ndani ya kipawa changu,.. Au yanayo faa, hivyo
sina shaka na kipawa changu eva.. Nipo makini sana”
Adam aliongea adam
mtoto wa mr Jacob,…
“sawa, ila utarudi lini… Siamini kama nitabaki
mwenyewe”
“eva, niruhusu kwa moyo mmoja,.. Itanichukuwa mwaka
mmoja”
“yesu wangu na maria, Uuuuuuuuuwiiiiiiii, baba mtumishi, mbona
unakaa sana”
“ndio wakati unaotakiwa”
“sawa, sina jinsi juu ya
hilo… Naomba uape kwa jina la yesu na mungu wake.. Kuwa utanioa
mimi”
Aliongea Eva kana kwamba haamini kama kweli atamuoa, mana anajua
Nigeria kumejaa wasichana warembo na wanaojua dini yao kuliko hata eva, na Adam
anapenda msichana anaeijua dini na kuitumikia dini yake vilivyo, sasa huko
Nigeria ndio wamejaa wasichana wa aina hio
“naapa kwa jina la na la yesu
na mungu wangu alie hai… Sintokaa kukuwcha eva,… Na endapo umeshindwa kujitunza
eva, naomba siku narudi usinisogelee”
Adam aliapa kisha hapo hapo
akamwambia kabisa,… Mana uhusiano wao una miaka lakini hajawahi kumuomba mpaka
waoane
“baba mtumishi wangu… Kama sijajitunza, basi hata kanisani kwenu
siji.. Mimi ni mali yako, mshukuru mungu, nakuoenda sana baba mtumishi wangu..
Nitajitunza kama alivyonitunza mama yangu… Nenda urudi baba nakusubiri wewe
tu”
“hata mimi nakuapia, sintokaa kujigusa ispokuwa kwako
tu”
“tumsifu Yesu Kristo alie hai”
“milele amina”
“baba
mtumishi, unaondoka lini na saa ngapi”
Eva alimuuliza
adam…
“naondoka kesho, ila itakuwa asubuhi baada ya misa ya kwanza
kuisha.. Ila nitapelekwa na baba”
“lazima nikuone mpaka unavyopanda
ndege.. Nikusindikize mpaka mwisho”
“lakini nitakuwa na
baba”
“nitapanda gari tofauti na yakwenu, lakini nikuone
tu”
Kwaho yake sasa adam na baba yake wakiwa ndio wanafika
uwanjani, lakini kumbe eva alishafika kabla yao, shida ya eva amuone baba
mtumishi wake anaondoka salama, alitamani kwenda kumuaga lakini iloshindikana,
kwasababu mwanamke anaejieshim hatakiwi kujionyesha kwa baba mkwe mpaka
utambulishwe, sasa anaejua utambulisho huo ni mama yake adam peke yake, ila baba
bado haja tambulishwa,… Adam alimwona eva akampungia mkono kwa mbali… Lakini
huezi amini eva aliona liwalo na liwe, hawezi kumpungia kwa mbalimbali kisa
hajatambulishwa.. Huezi amini eva alitoka pale alipo na kumkimbilia adam au baba
mtumishi wake.. Adam nae hakutaka kujua yupo jirani na baba yake…. Alinyanyua
mikono yake kuashiria kumkumbatia eva,… Baba yake rajabu, alishangaa, japo huyo
msichana si mgeni katika macho yake, mana pia ni muumini wa kanisa lake…
Hakumuwazia sana mtoto wake,… Wakati huo mzee anasonga mbele huku nyuma adama na
eva wanaendelea kuagana… Mpaka wanaachana eva anageuka nyuma na adam anaguka
mbele kuuelekea mlango wa ndege husika…..
MWISHO WA KUMBUKUMBU
YA ADAM, KABLA YA SAFARI…..
Sasa adam alipokumbuka hilo,…
Lakini pia alikumbuka muda mchache uliopita alipigiwa simu na baba yake kuhusu
Catherine,… Adam alitabasam kidogo kisha akaweka brifkesi yake chini na kuamsha
mikono kuashiria mapokezi mazuri kwa anaekuja…. Adam alimkumbatia huku akiskia
sauti ikisema
“Ahsante sana mungu baba…. Umenirudishia baba mtumishi
wangu”
Alikuwa ni eva baada ya kukumbatiana na adam wake…. Sasa
Catherine anashangaa mbona huyu mschana kakumbatiwa badala yake,.. Catherine
hakuwaza mengi sana alijua labda ni muumini wa kanisa lao, hivyo Catherine yeye
nguvu zake zote ziliishia kubeba kile kibegi kilichokuwa chini na pia alijiskia
vibaya sana, mana kakimbia bure bila mafanikio yeyote… Haikupita muda na familia
yote ikamzunguka adam
“mwanangu, umenenepa wewe, haaa.. Yaani unataka
kusema mimi mama yako nilikuwa sikupendi mwanangu”
Aliongea mama yake
adam huku akiwa na furaha ya kumwona mtoto wake tena,.. Dada yake adam nae
hakuwa nyuma
“shalom kaka D”
“shalom…. Asa d ndio nini, umeanza
uhuni dada eti ee”
“amna bwana,… D nimehisi ni kifupi cha
adam”
“najua dada yangu una maneno mengi kweli wewe”
Aliongea
adam huku wadogo zake wakimsalimia kaka yao, ilikuwa ni furaha kuanzia kwa eva
mpaka kwa familia yote, kasoro Catherine pekee,
Gari ya familia
iliandaliwa kisha wakapanda gari lao… Kisha haooo wakaondoka, ndani ya gari
furaha iliyokithiri, eva ndio kabisa usiseme, ana furaha ya ajabu kuliko mtu
yeyote hapo ndani,…
Walifika nyumbani, maandalizi ya kupika
yalianza,…
“mama, naomba nimpikie adam”
Eva aliomba nafasi ya
kumpikia adam na wakati huo adam kakaa katika meza, sasa kuna kakitabu chake
anapenda kukasoma pale anapokuwa mwenyewe,…
“martha….
Martha?”
Adam alimuita mdogo wake ambae ni martha,
“Abee
kaka”
Aliitika Martha huku akimjia kaka yake
“ebu niletee kibegi
changu kipo katika gari”
Aliongea adam huku martha akiharakisha agizo la
kaka yake, wakati huo eva yupo jikoni, yaani eva keshakubalika na familia yote,
swma ubabe wa mr Jacob kutaka mtoto wa rafiki yake aolewe na mtoto wake,.. Mama
alikuwa karibu na mtoto wake akimuuliza habari ya masomo mana ni mwaka sasa toka
aende Nigeria… Lakini sasa adam alisahau na sio adam tu bali wote walisahau kuwa
pale uwanja wa ndege walikuwa wa9 na Catherine,… Hivyo Catherine ndio alibeba
kibegi au briefcase ya adam ambayo ina vitabu vya mungu karibia kibegi
kizima…
“kaka sioni mbona”
“aahhh we nawe akuizi huna
macho”
Wakati huo eva ndio analeta chakula, tayari keshapika, mama
alimtabasamia eva kwa chakula alichopika… Na leo ndio mara ya kwanza eva kuingia
kwenye hii nyumba, lakini kazoeleka ghafla tu na hapo yeye hajui kama kipo
kinachoendelea juu yake..
“unatafuta nini wifi
nikakusaidie”
“kaka kantuma kibegi chake”
Sasa eva yeye ndie
alipata kumbukumbu ya pale uwanjani…
“kuna yule dada nilimwona pale
uwanjani na ndie aliekibeba, kwani sio ndugu yenu yule”
Aliongea eva,…
Sasa mama ndio anafungukwa na akili,..
“afu kweli, ivi Catherine alipita
njia gani saa ile”
Aliuliza mama yake adam, kisha adam akamuuliza mama
yake kuwa
“kwani si mlikuja nae”
“hapana, alikuja kivyake na
gari yake”
“aahhhh… Afu mama, kuna taarifa nimepewa na baba kuhusu yule
msichana, mi sielewi mama”
Mama sasa roho ikamshuka, hayo maneno
yalimkuna sana eva, na kutaka kujua kinaga ubaga cha huyo
Catherine,..
“mwanangu, hata mimi sielewi, ni asubuhi tu hapa baba yako
ananiambia kuwa eti ndio mwanamke unaetakiwa kumuoa”
Heeeeee Eva alikuwa
nyuma ya mlango, anasikia, yaani ilibaki kidogo tu adondoke,.. Akajikaza
kisabuni ila wakati huo alikuwa yupo na Martha, mana hata watoto sio wote
wanajua hilo,.. Martha alimshika wifi yake mana anamjua kuwa anampenda sana kaka
yake… Martha ni mschana mkubwa ana miaka 20,…
“lakini mama, ina maana
umeshindwa kumwambia baba nina mchumba… Au hajui hilo”
“nimemwambia
lakini akasema mimi sijatambulishwa”
“sasa ngoja aje… Na eva asiondoke
hapa amkute”
“sasa unaenda wapi mwanangu”
“nakwenda kuchukuwa
kibegi changu”
Sasa wakati adam anatoka, Martha akamwambia wifi yake
kuwa
“ambatana nae, mana najua huyo Catherine katumia akili kwasababu
anajua ni lazima kaka adam atakwenda kule, hivyo nenda nae”
Aliongea
martha, mana anampenda eva kuliko Catherine,..
“njoo kula kwanza
baba”
Mama Jessica alikuwa akimlazimisha adam ale kwanza, lakini
hakutaka kufanya hivyo… Mana hasira zilishamjaa…..
Wakati huo eva
anatetemeka, ivi atamwambia nini mama yake, familia yake yote inajua ataolewa na
adam, baadhi ya makanisa yao yanajua uhusiano wa adam na eva,..
“baba
mtumishi, naomba niongozane nawe”
Aliongea eva huku akihisi kukataliwa
na adam
“yes, ni sawa twende, tena familia yao yote
ikakujue”
Eva hakuamini kumbe adam hakubaliani na swala la baba yake,…
Eva aliingia kwenye gari na adam.. Kisha haoo wakaondoka,.. Kweli familia ya mr
jacob ni tajiri mno..
Sasa huku kwa mr yohana, Catherine akiwa
kakumbatia begi la adam, yaani kusema kweli hata yeye anampenda sana
adam..
Mama aliingia chumbani kwa mtoto wake, alimkuta kashikilia begi
dogo
“wewe una nini… Mana ulitoka kwa furaha sasa mbona umekiwa hivyo
mwanangu”
Aliongea mama huyo, au mama mchungaji kwa mzee
Yohana
“mama, nimekwenda uwanja wa ndege, nimeambulia kubeba hiki kibegi
tu”
“aaahhhh ina mana adam hajakuona”
“kaniona sana tu, ila kuna
msichana ndio kamkumbatia badala yangu”
“lakini Catherine mwanangu,
nilikuambia adam ana mchumba lakini husikii”
Aliongea mama huyo na hata
yeye huyu mama hataki mtoto wake Catherine aolewe na adam, sasa hatujui ni
kwanini
“mama mimi nampenda hivyo hivyo tu, na nilikuwa sina nguvu
kwasababu ni moyo wangu tu, lakini sasa hata baba kaingilia kati hivyo nina
nguvu na lazima niolewe na Adam”
Catherine hakutaka kukata tamaa, na
kweli jambo likiingiliwa na wazazi, sidhani kama mtoto atapinga, tena haswa
wazazi wa kiume… Hatari sana.. Lakini wakiwa wanazidi kuongea ghafla honi
ilisikika nje ya geti lao, mlinzi alifungua geti kisha gari inaingia ndani…
Alikuwa ni adam
“haya si ndio huyo anaingia”
Aliongea mama yake
Catherine huku akifunua pazia…
“nilijua tu lazima aje…. Mama twende
ukanisaidie kuongea nae”
“ati nini…. We ulifikiri napenda uolewe nae,
sipendi hata kidogo.. Umuache mkaka wa watu mpole kiasi kile,.. Mwanangu… Kwani
John kakufanya nini lakini”
“mama tuachane na mambo ya
John”
Catherine aliongea hivyo huku akitoka nje na kile
kibegi,…
Wakati huo adam anashuka katika gari kwa hasira sana,.. Tena
kwa dharau anakwenda kumfungulia eva mlango, na wakati huo Catherine anaona live
bila chenga…
“unamuona mchumba wake,… Kwanza ona nguo alizovaa… Pili
muangalie juu mpaka chini, kama kuna kitu cha kisasa alichokitia mwilini, hebu
jiangalie na wewe mwanangu, kila kitu mwilini mwako ni kitu cha kisasa… Haya
Adam huyo hapo, mwambie kuwa unampenda”
Melissa alimchana mtoto wake
live bila chenga,… Kweli Catherine akijiangalia, uzuri anao, shepu anayo. Labda
na tabia anayo… Lakini sasa mwili wake umejaa udigitali mwingi
mnoo….
“baba, karibu”
Alimkaribisha mama kwa
shangwe
“Ahsante mama… Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina
mtumishi”
Adam alimgeukia Catherine
kisha…
Wanasema huezi lazimisha maji
kupanda mlima hata siku moja, mzazi wa adam ambae anataka mtoto wake huyo kuoa
mtoto wa rafiki yake mr yohana,… Lakini kwa upande wa mtoto wa mr jacob
hakuridhika na matakwa ya baba yake,…
Wakiwa uwanja wa ndege
baada ya Catherine kukosa kumbatio toka kwa Adam, alifanikiwa kuondoka na begi
dogo la Adam, na aliondoka nalo makusudi ya kwamba ni lazima angelikuja kule
nyumbati ili alipate kumbatio kwa uzuri akiwa kwao,.. Kweli akili yake ilizaa
matunda kwa kitendo cha adam kufika kwao, ila kupata kumbatio kama alilopata eva
pale Airport, hakuweza kulipata…
“baba,
karibu”
Alimkaribisha mama kwa shangwe
“Ahsante mama… Tumsifu
yesu Kristo”
“milele amina mtumishi”
Adam alimgeukia Catherine
kisha akamsalimia kwa kumpa mkono
“shalom dada”
Aliongea adam
huku akimpa mkono Catherine….
“shalom”
Catherine aliupokea mkono
kiunyonge sana tena ni kwakuwa anamuheshim sana, mana kitendo cha adam kumwita
Catherine DADA, alijiskia vibaya sana….
“Samahani mtumishi… Iv huna
taarifa zangu zozote”
Catherine aliona bora kuongea tu, mana kama mtu
mwenyewe hata haonyeshi kuwa na upendo juu yake
“nimekuja kuchukuwa vitu
vyangu, hio ndio taarifa niliokuja nayo”
Aliongea adam huku akinyoosha
mkono wake kuashiria anataka begi lake,….
“Catherine, unamchelewesha
mtumishi”
Aliongea mama yake Catherine huku Catherine akilitoa begi hilo
aliokuwa kalikumbatia,… Mtumishi adam alilipokea begi hilo na kumgeukia mama
take
“mama, asifiwe bwana yesu”
“milele amina
baba”
“basi mimi naona niwaache”
“mungu akutangulie mtumishi
wangu”
Aliongea mama yake Catherine huku adam akimpa eva lile begi,…
Adam alimfungulia eva mlango, Catherine anaona live bila chenga…. Baada ya
kumaliza akaja katika upande wake wa dereva, lakini kabla hajaingia
aliita
“Catherine…. Taarifa zako ninazo, lakini umechelewa… Nina mchumba
na nakwenda kumuoa hivi karibu, ndio huyu hapa Eva… Bwana yesu akutangulie
Catherine… Ahsante”
Adam aliingia katika gari kisha huyooo,… Lakini
alipokuwa anatoka getini akakutana na baba yake Catherine akiwa katika gari
yake, Adam alishusha vioo na kumsalimia
“Shalom baba
mchungaji”
“shalom mtumishi, habari ya uzima”
“aahhh
Tunamshukuru mungu.. Anatenda miujiza”
“basi tumsifu yesu
Kristo”
“milele amina”
Mzee anajua fika labda adam kamleta
Catherine mara baada ya kutoka airport, kumbe kilichofatwa huku ni begi tu… Mzee
Yohana anaingia nyumbani kwake, anamkuta Catherine kuvimba haswa…
“raha
gani hii mwanangu, unaolewa na kijana mwenye heshima zake,.. Umeletwa mpaka
nyumbani upewe nini mwanangu”
Aliongea Bishop yohana bila kujua lolote,
wakati huo mama yake Catherine yupo ndani anakaukia kucheka tu… Ile kimoyo moyo,
mana kweli hapendi mtoto wake aolewe na mtumishi adam
“baba,… Adam kaja
na mchumba wake hapa”
Aliongea Catherine huku machozi yakimlenga
lenga,
“Unasemaje?”
“ndio, tena kaniambia kuwa huyo ndio mchumba
wake na anatarajia kumuoa wiki hizi… Hivyo hahitaji usumbufu na
mtu”
Aliongea Catherine, wakati huo maongezi yakiendelea, tayari simu
ilishawekwa maskioni siku nyingi sana,..
“hello mr Jacob… Tumsifu yesu
Kristo”
“milele amina”
“habari ya siku mbili
tatu”
“aaahh bwana yesu ashukuliwe sana”
“Samahani mr Jacob,
kijana wako hujampa taarifa juu ya kinachoendelea”
Mr Yohana alimuuliza
bwana Jacob
“kwanini Unauliza hivyo ingali anajua kila kitu,.. Namuamini
kijana wangu hana shida”
Aliongea bwana jacob bila kujua kilichoendelea
huku
“numepishana nae getini kwangu hapa sasa hivi tu”
“si
unaona sasa, umbe kaja? Hawa ni watoto wetu bwana”
“lakini nadhani
hayupo tayari kwa hilo mana nimemkuta binti yangu kanuna na istoshe kaja na huyo
anaesemekana ni mchumba wake”
“unasemaje?.. Amekuja na huyo binti
mwingine”
“inavyosemekana”
“hebu nipe hii siku ya leo…
Tutayamaliza, wewe ni rafiki yangu toka utotoni, mpaka sasa tupo pamoja.. Nataka
tuwe ndugu sasa, hahahahaha.. Bwana yohana kiwa huru bwana”
Aliongea mr
Jacob huku akiwa na furaha sana juu ya kutaka kumpa mtoto wake mke ambae ni
mtoto wa rafiki yake
“sawa mr jacob, staki binti yangu aolewe na vijana
wa ajabu ajabu… Mimi ni mtu na heshima zangu”
Aliongea mr yohana wakati
huo Catherine ndio anazidi kujiskia raha na kupata nguvu zaidi mana swala hilo
limeshikiliwa na wazazi,…
“usijali kabisa ndugu yangu… Bwana yesu
atuongoze”
Aliongea bwana Jacob kisha simu
ikakata,
Huku nyumbani kwa akina adam akiwa ndio anaingia
nyumbani kwao, Jessica aliwahi kumpokea mdogo wake, na anamheshimu sana mdogo
wake,.. Jessica ndio mtoto wa kwanza katika hii familia,..
“imekuwaje
huko wifi”
Aliongea Jessica huku akiingiza kibegi ndani,
“wala
hakuna lolote, alimwambia tu kuwa ana mchumba wake”
Wakati huo
wakiulizana hivyo adam hakuwepo hapo, kumbe alishatoka kitambo tu, na Wakati huo
ni mida ya saa 11 za jione kwenda saa 12,… Adam alifikia kwenye nyumba moja
mpyaaaa, ila imeshaisha ujenzi, kumbe adam ana nyumba kabisa yaani akirudi huko
sio mtu wa kukaa tena kwa baba yake,… Ilikuwa ni nyumba kubwa mno na haistahili
aishi pekee bali mke.. Katika nyumba hio kila kitu kilisha wekwa, yaani hapo ni
kuhamia tu,…
“ondoa hofu, lazima uilewe na kaka
yangu”
Ni huku kwa akina Adam, Jessica akiwa anamhakikishia eva kuwa ni
lazima aolewe na adam,…
“sawa wifi yangu, ila kama hili jambo
wamelishika wazazi, huoni itakuwa ni hatari kwangu”
“ondoa shaka, mimi
namjua vizuri adam… Nimemkuza mwenyewe.. Namjua haoi mtu pale”
Aliongea
Jessica, lakini wakati huo eva anataka kirudi nyumbani,… Haraka haraka Jessica
anampigia adam simu..
“we subiri upelekwe mpaka nyumbani unaogopa
nini”
Aliongea Jessica huku simu ikiwa
sikioni
“sawa”
“haloo mtumishi… Njoo basi umpeleke
mwenzio nyumbani”
Aliongea Jessica kwa kumuita mtumishi,.. Ni jina
ambalo wamelizoea kwa watu wengi na pia kutokana na kipawa chake..
“sawa
nafika hapo sasa hivi”
Kweli haikuchukuwa muda adam alifika nyumbani
kwao na kumchukuwa eva,….
Sasa huku kazini baba yake Adam
anatoka kazini, anawaza cha kumwambia mtoto wake, kwanini kaenda kuleta fujo
katika nyumba ya watu,
Wakati huo mama yake eva alikuwa hana
raha mana toka mchana hajamwona mtoto wake,… Bite ambae ndio mdogo wake na eva
pia alikuwa ni mtu wa wasiwasi, tena mama ndio kabisa kwasababu asubuhi kuna
maneno aliyasikia toka kwa akina janet,.. Mama na mtoto wake bitw wakiwa wamekaa
hapo nje kila mmoja kashika tama, na tayari kagiza kameshaanza kutanda,..
Waliona taa za gari zikiwaelekea huku waliko…, taa iliwakera mno mana walikuwa
katika dimbwi la mawazo,…. Ghafla gari inasimama karibu yao na adam anashuka na
kumsalimia mama mkwe
“mama, shikamoo mama”
“marahaba baba,
ooooohhh mtumishi? Tumsifu yesu Kristo”
“milele amina”
“karibu
ndani”
Wakati huo eva nae ndio anatoka ndani, bite akamkimbilia dada
yake baada ya kusalimiana na shemeji yake,… Mama haamini kama leo mwanae kaletwa
na gari japo aio mara moja kuletwa na gari, ila kwa sasa kuna changamoto kidogo
hivyo lazima kuwepo na mshangao kiasi,…
“karibu baba
mtumishi”
“Ahsante sana….”
“biteeee, we bite… Hebu kalete
maandazi haraka mtumishi apate chai”
Aliongea mama kwa kumtuma bite,
lakini adam alikataa kupata chai kwa maana ya kuwahi nyumbani,… Kweli kwa akina
eva maisha si mazuri, yaani ni watu wanaomtegemea mungu vibiashara vidogovidogo
ambavyo mama huyo huweka nje ya kanisa ili apate kuuza angalau hata juisi,… Na
ukiwaona huezi jua kama ni watu wa dhiki, mana wahenga walisema kuwa, UMARIDADI
HUFICHA UMASIKINI,… Ghafla simu ya adam iliita, kuangalia jina, alikuwa ni baba
yake
“haloo mchungaji”
Aliita adam huku simu ikiwa
sikioni
“sijakukuta nyumbani upo wapi usiku unaingia huu”
“aahh
nakuja sasa hivi baba”
“hebu wahi nina maongezi na
wewe”
“sawa”
Adam hakutaka kuchelewa, alimuaga mama yake eva
kisha akatoka zake nje… Aliingia katika gari lakini ghafla eva kaja nae kaingia
katika gari,
“nimeona sms yako, kuwa ukitoka nikufuate”
Aliongea
eva, kumbe hakutaka kumuita mbele ya mama yake…
“ndio, kwani ni vibaya
kumuita mama mchungaji wangu”
“hahahahaha hapana si vibaya”
“ok…
Shika hiki kiasi, kitawasaidia”
“lakini baba mtumishi”
“lakini
haitakiwi,… Ashukuliwe baba muumba kwa riziki kupatika…. Kwaheri, tuonane kesho
kanisani.. Afu, naomba hio pesa ikiisha unipe taarifa,… Staki mama mkwe akakae
juani tena, kuleni vizuri muombeni mungu sana.. Mwezi huu huu naweza
kuoa”
Aliongea adam huku akiwasha gari
“Catherine
au”
Aliongea eva huku akiwa kashika tama
“sina uwezo huo, naoa
nilichokipenda.. Hata vitabu vya mungu viliandika, Mpende
anaekupenda”
Adam aliongea mengi sana,… Kumbe hata kabla ya adam
kuondoka, yeye ndio alikuwa akitegemewa na familia ya eva,.. Mana baba yake eva
alikuwa ni mzee wa kanisa moja wapo kati ya makanisa ya mr Jacob, hivyo baada ya
kifo cha baba yake eva,… Adam aliamua kubeba jukumu zima la familia hio, mana
mzee yule alikuwa akiishi kwa sadaka za waumini, sasa hayupo, nani achukue
sadaka.. Hakuna…. Hivyo adam kachukuwa jukumu hilo peke yake…. Na anajua
waliteseka sana kipindi yupo masomoni,.. Japo aliwaachia kiasi kikubwa cha
fedha,..
“mtumishi jacob kaniita, hivyo wacha nimuwahi”
Aliongea
adam kumaanisha baba yake kamuita….
“sawa,… Naomba bwana yesu aingilie
kati mahusiano yetu, mana tuna nia njema na huu ulimwengu”
Aliongea
eva,.. Na wakati huo ibada ikadondoshwa hapo hapo kwenye gari,… Mama na mtoto
wake bite kusikia ibada inadondoshwa, nao wakaungana nao kwa kupiga magoti kisha
kuomba sambamba na wao,..
Baada ya maombi, adam aliondoka
zake…. Sasa eva anakwenda kukagua kapewa kiasi gan,…
“yesu wangu, kakupa
pesa zote hizi”
Aliongea mama yake eva huku wakizimwaga
mezani,…
“mama, unajua kweli mtumishi adam anaona mbali sana… Hivi
kajuaje kuwa humu ndani tunaishi kwa uwezo wa mungu pekee… Kajuaje kuwa hatuna
kitu.. Mama?? Ashukuliwe baba Muumba mbingu na ardhi”
Kiukweli pesa
walizopewa zilikuwa ni nyingi, kwa haraka haraka, labda ni kitu kama laki tano
hivi, ila inazidi zaidi ya hapo…… Walifurahi sana na kuzidi kumuombea mtumishi
adam
Huku kwa mzee jacob akiwa kaketi Katika sofa la uvivu,
yaani lile la kulala,… Ghafla alisikia honi ya gari,.. Alijua tu ni mtoto wake
adam ndio anakuja… Kweli alikuwa ni adam, au mtumishi
adam
Wakati huo mzee Jacob baada ya kumsikia
mtoto wake adam akiingia, basi aliitisha kikao cha dharura hapo ndani akiwemo
mama na dada mkubwa wa adam,... Huku katika paking adam alipaki gari vizuri
lakini hakushuka, sasa akawa anawaza ni jinsi gani ataongea na baba yake kuhusu
swala la kuoa kwake,.. Lakini akiwa ndani ya mawazo, alikumbuka kitu fulani na
kutoa simu yake na kumpigia mtu fulani ambae anajuana
nae,..
Baada ya kuongea na huyo mtu, adam alishuka katika gari,
lakini kidogo alikuwa na tabasamu, sasa hatujui aliongea na nani na maneno
gani,.. Adam aliingia ndani moja kwa moja mpaka mezani, mana alijua tu kukaa kwa
watu hao mezani na hakuna hata mtoto wala mfanyakazi, alijua tu kuna maongezi
yanaendelea hapo
"asifiwe bwana yesu Kristo"
Alitoa salamu ya
kumsifu bwana Yesu Kristo...
"milele amina"
Waliitikia wote watu
watatu,.. Lakini kabla hajakaa, ghafla simu yake inaingia meseji... Aliifungua
na kuisoma kimya kimya kisha akaendelea kukaa...
"ndio mchungaji,
ulisema niwahi nyumbani"
Aliongea adam huku anamwomba Mungu wake kwa
lolote litakalotekea liwe zuri katika maisha yake,....
"nyumbani kwa mr
yohana ulifika saa ngapi"
Aliuliza mr jacob
"nilikwenda time za
jioni hivi... Kuchukuwa begi langu"
"begi?? Begi gani
tena"
"aahh wakati nashuka pale Airport,.. Alikuwepo mtoto mchungaji
yohana, na yeye ndie aliepokea begi langu"
"kwanini ulipokwenda huko
ulikwenda na mwanamke, ingali nilishakupa taarifa kuhusu mtoto wa mr
yohana"
Aliongea bwana jacob, huku akihitaji jibu la kueleweka toka kwa
adam
"ndio baba... Kwanza samahani kama nitakukosea baba yangu,... Ni
kweli ulinipa taarifa juu ya binti yule, lakini baba huoni utakuwa hunitendei
haki kwa kunichagulia mke... Hapo utakuwa umenikosea baba... Kweli nataka kuoa
lakini sikumtazama Catherine na pia hata kwenye akili yangu haipo kwa
Catherine.... Baba, tafadhali sana, sijawahi kukutambulisha, ila nadhani
ulishawahi kusikia, sasa mimi nataka kumuoa Eva na sio Catherine"
Adam
aliongea huku mama na Jessica wakitikisa kichwa kumaanisha sawa kabisa kwa kile
anacho kiongea bwana adam...
"yaani eva huyu mtoto wa marehemu
paulo"
"ndio"
"nipe sababu saba za kumwoa eva"
"sasa
mzee... Nitakuja kuongea sababu hapa, mwisho utaniona nimetusi sasa... Naomba
unipe nafasi ya moyo wangu mzee.. Yule msichana mimi simjui, tunakutana tu
kwenye kumbi mbalimbali na makanisani, sijui tabia yake sijui ni mzima au
naniii.. Eeeeeee babaaa"
Sasa alipomaliza tu kuongea adam, mara mama nae
akaingilia kati na kusema
"ni kweli.. Kwanza yule mschana anavaa nguo za
ajabu sana, yule msichana hata kanisani kwao utamkuta kavaa nguo za ajabu,..
Kwanini tumpe mtoto wetu mwanamke wa ajabu jamani baba Jessica"
Aliongea
mama tena kwa msisitizo mkubwa ili aeleweke,....
"mimi nimeshasema....
Taka asitake lazima umuoe Catherine... We ulizani utabarikiwaje na mungu usipo
oa?? Lazima uoe ili mungu akubariki"
"sijakataa kuoa baba, tatizo ni
mke"
"nasema hivi napiga simu mwanamke aandaliwe wiki hii uoe na kanisa
lako"
"baba... Samahani sana.... Kama ni kanisa aitaki,... Wacha niwe
mwinjilisti wa mitaani nikaitangaze injili kwa waumini waliokosa nafasi ya
kufika makanisani... Sitaki kuoa iwe eva ama Catherine... Alafu kesho nahamia
nyumbani kwangu"
Aliongea adam kisha akaondoka,.. Wakati huo simu
imeganda skioni kwa mr Jacob,
"umeona sasa unamvunjia heshima mtoto wetu
baba Jessica"
Aliongea mama huku nae akiamka kumfuata mtoto wake kule
alipo elekea, na Jessica nae huko huko... Mara mr yohana anapokea
simu
"haloo bwana jacob"
"ahahahahah bwana yohana... Habari ya
masaa mawili matatu"
"aahh salama tu bwana jacob vp hali"
Yohana
alikuwa na furaha mana alijua anapewa jibu zuri juu ya adam kukubali
kuoa
"bwana hapa ndio nimemaliza kikao na bwana mdogo... Lakini kiukweli
bwana yohana nguvu zangu zimeishia hapo, namuheshim sana kijana wangu... Na kitu
ambacho nikiweza mpaka sasa... Sintokubali amuoe mwanamke anaemtaka yeye.. Ila
sasa naomba umpe nafasi mtoto wako, awe karibu na kijana wangu, ili angalau
wazoeane... Kwasababu hapa kwenye kikao kalalamika sana kuwa, hamtambui
Catherine... Kwani wao hukutana katika kumbi mbalimbali na makanisani, sasa
hawatambuani, hebu mpe nafasi binti yako awe karibu nae, angalau wajenge hata
mazoea.."
Alimaliza kuongea bwana jacob huku bwana yohana akijibu
kuwa
"aah hilo mbona halina shaka.. Mimi nataka tuwe ndugu kabisa... Sio
urafiki tena, na undugu wetu utaunganishwa na watoto wetu"
"sawa
kabisa... Mwambie tu ajitahidi kiasi, mana bwana mdogo ana msimamo huyo, namjua
mwenyewe"
Aliongea bwana jacob wakati huo yupo peke yake hapo
sebuleni,..
"ondoa shaka, hapo watakutana, mana hata Catherine hana
mchezo mchezo kabisa"
Lakini mr Jacob kuna swali alimuuliza
bwana Yohana kuhusu binti yake, na wakati huo huo adam ndio anakuja sebuleni kwa
ajili ya chakula... Lakini adam aliposikia hilo swali alisita kuja sebuleni
kwanza ili asikie vizuri, mana lilikuwa ni swali la siri... Na hata sisi
wasomaji hatutakiwi kulijua.... Adam alisikiliza umakini mzee wake akimuuliza
bwana yohana kuwa.....
Hatujui kamuuliza nini lakini adam
alisikia peke yake, na hata kuja sebuleni hakuja tena akaishia mlangoni na
kurudi chumbani kwake
Maongezi ya mr jacob na mr yohana yaliisha baada
ya kupata vyema, hivyo kwa sasa Catherine ni yeye na juhudi zake za kuwa karibu
na adam, kazi ipo hapo...
Baada ya siku kadhaa kupita na leo ni
siku ya Jumapili,.. Familia ya mr Jacob ikiwa katika maandalizi ya kuwahi
kanisani katika misa ya kwanza, ikumbukwe kuwa adam toka arudi Nigeria katika
chuo cha Biblia, alikwenda kuabudu katika makanisa mengine ya baba yake, mana
kuna kanisa kuu na kuna makanisa ya kawaida, na hayo makanisa ya kawaida yana
mapasta wengine, mana huyu mr Jacob yeye ni Bishop, hibyo kateua mapasta kwa
ajili ya malanisa mengine, sasa kuna kanisa kuu ambalo Bishop mwenyewe
hilitumikia kutoa huduma kwa waumini wake,... Sasa kanisa hilo kuu adam hajawahi
kufika toka aliporudi masomoni,.. Sasa leo Jumapili ndio anakwenda katika kanisa
hilo, wote walikamilika walikuwa kama watu saba hivi skose.. Baba, mama, watoto
wanne, na mfanyakazi wa ndani wa kike.. Walipanda katika usafiri tofauti
tofauti,... Bishop Jacob alipanda yeye na mtoto wake wa mwisho na mke wake,.. Na
adam alipanda yeye na mfanyakazi na dada zake wawili,.. Kanisa wanalo lielekea
ni moja..
Katika kanisa hilo wapo waliokuwa wakiabudu kwa
mapambio,.. Na walikuwepo viongozi wenye vipawa kwa ajili ya kutoa huduma kwa
waumini wao, na hapo ni katika hatua za kumsubiri mchungaji Jacob ama Bishop
jacob kuja kutoa huduma ya neno la mungu,...
"dada, sjui
niwawahishe kwanza, mana nahitaji kwenda kumchukuwa eva ili awahi misa ya
kwanza"
Aliongea adam wakati huo walikuwa njiani...
"twendeni tu
kwani gari si inatosha"
Aliongea Jessica huku adam akikata kona katika
njia ya akina eva, mana eva na mama yake na mdogo wake hua wanachelewa misa ya
kwanza, na misa ya kwanza ni bora zaidi kuliko hata misa zinazifuatia... Uzuri
aliwakuta wakiwa tayari wamejiandaa, mara moja walipanda gari ili kuwahi misa ya
kwanza...
Huku kanisani, Bishop Jacob akiwa tayari keshafika
kanisani na huduma ilianza mara moja, lakini sasa katika waumini wa mbele,
alionekana Catherine,... Hii siri ya Catherine kuwepo hapa anaijua mzee peke
yake.. Mana aliambiwa kuwa aanze kujenga ukaribu na adam,.. Sasa ndio kaanza
kuja kanisani kwao, na hata huyu Catherine wana makanisa mengi kama ilivyo
Bishop jacob... Hivyo huku kaja kwa kazi maalumu,.. Bishop Jacob alianza
kuhubiri kwa kishindo kama ilivyo kawaida yake,..
Huku katika
lifti ya kupanda juu akiwemo Jessica, Martha, sekwa, Eva, Bitris na mama yao,...
Lifti ilifika mahala husika na walitoka ili kwenda katika ukumbi wa maombi,
sauti ya Bishop Jacob inasikika ikitoa mahubiri yake mazuri sana.. Lakini ghafla
simu ya adam inapata meseji, hivyo kitendo hicho kilimfanya asimame na kuisoma
mesji,.. Sasa yeye aliposimama wale aliokuja nao wakatangulia
mbele,...
"mwanangu, namuona Catherine hapa kanisani"
Adam
alishtuka, ilikuwa ni meseji iliotoka kwa mama yake,...
Lakini hakujali,
aliendelea na safari ya kuingia kanisani,...
Sasa waumini
walikuwa wakisikia tu mtoto wa Bishop Jacob karudi, lakini hawakuwahi kumwona
kwasababu alikuwa hasalii kanisa hilo,...
Sasa ile adam anaingia tu,...
Hata baba yake alishangaa, waumini walinyanyuka wote na kusema
"tumsifu
yesu Kristo mtumishi adam"
Hata adam alishangaa, yaani waumini
wanampenda kupita maelezo,... Hata Catherine haamini kuwa kanisa zima
limenyanyuka kwa ajili ya adam... Mzee jacob haamini, yaani mtoto wake
anakubalika kuliko yeye,
"asifiwe bwana mwokozi wetu"
Aliongea
adam huku akipunga mkono,.. Lakini sasa vile alivyokuwa akipunga mkono, waumini
wengi walikuwa wakitetemeka,.. Adam anashangaa mbona baadhi ya wingi wa waumini
hutetemeka... Akajaribu kupungia tena... Sasa kumbe adam hajajua kuwa sio
waumini peke yao,.. Mana ndio alikuwa akiwapungia mkono,.. Ghafla ilisikika
sauti ikisema
"adam acha, inatosha, hebu chukua kiti na
ukae"
Kawaida ya kanisani au
msikitini hapatakiwi kuwa na mapendo, mana pamejaa maombi na dua za kila aina
kila siku,…. Hivyo hata pepo au shetani hana nafasi katika nyumba hizi mbili,…
Lakini inashangaza ya kwamba katika kanisa kubwa la ROHO MTAKATIFU liliotakaswa
kwa damu ya yesu, leo ninaonekana kuwa na mapepo,… Kivipi na wakati linaongozwa
na Bishop Jacob, yaani ni wito ulio mkubwa kwa mungu baba
Adam
aliingia na waumini wote kunyanyuka katika viti vyao kisha wakamsalimia adam kwa
furaha, mana ni mtu aliojaa upako, aliotakaswa kwa damu ya Yesu na akatakasika,
na ni kweli sio uongo, adam hakutaka kukaa kimya kwa salamu ya waumini hao,
ilibidi nae kwa furaha kuamsha mkono wake juu na kupungua huku
akisema
“asifiwe bwana mwokozi wetu”
Lakini sasa cha ajabu na
cha kushangaza, aliona watu wakitetema kila anapopunga mkono wake,.. Hio
iliashiria kwamba waumini wote hawakuwa sawa,.. Lakini sasa kumbe sio waumini
pekee, hata mr Jacob pia ilikuwa ikimtetemesha ile hali ya mkono ukipungwa, huku
akitaja jina la mungu… Sasa kwakuwa adam yeye alikuwa haoni nyuma kuwa baba yake
nae alikuwa akitetema, ndipo mama yake adam akapaza sauti kwa nguvu na kumfikia
adam..
“adam acha, inatosha, hebu chukua kiti na
ukae”
Aliongea mama yake adam huku akivutwa na mama yake,… Adam
alishangaa hili kanisa limevamiwa na nini? Mbona limejaa mapepo kiasi hicho na
baba yake akiwa mhudumu mkuu wa kanisa hilo….. Sasa adam alimsikiliza mama yake
na kuketi katika kiti, lakini bado kulikuwa na waumini waliokuwa wakipiga
kelele, mana wengine walikuwa wakitokwa na mapepo pale adam alipokuwa akipunga
mkono,… Na adam mpaka hapo hajui kuwa hata baba yake alikuwa akitetemeka,….
Baada ya muda waumini walitulizwa na huduma ya kutoa neno la bwana ikaanza
rasmi, mana palitokea mvurugano kidogo baada ya adam
kuingia,…
“tumsifu yesu Kristo”
Aliongea mr Jacob
lakini mpaka hapo ana wasiwasi sana mana kakutana na mtoto wake ni moto wa
kuotea mbali, yaani hafai katika swala la kutoa huduma kwa waumini wake,…. Ibada
ilifanyika vizuri na hatmae ilikwisha,.. Vipindi mbalimbali vilifanyika, misa
misa zote ziliisha na kuna wale wa maombi ya chain player, waliingia na kuanza
maombi yasiokatika…
Sasa leo ni siku adam anahamia nyumbani
kwake,.. Ni nyumba ya kifahari mno,.. Ukizingatia ni kuwa jana mdogo, ndio
anaendea miaka 24 sasa,…
“lakini adam mwanangu,… Wewe bado hujaoa,
unahamia huko utaishi vipi,.. Utapikiwa na nani, nani atafua nguo zako, nani
atafanya usafi wa nyumba yako mwanangu”
Alikuwa ni mama yake adam,
wakati huo adam alikuwa akipaki nguo zake katika begi, mana kila kitu kule kipo
ni yeye kubeba nguo zake na vitu vyake vya thamani,…
“mama, wacha
nihamie kwangu,… Bwana yesu yupo nami,.. Kama mkate mmoja uliwatosha kundi la
watu wa bwana Yesu, sembuse mkate mmoja usinitoshe mimi,
kwanini”
Aliongea adam huku akimalizia kupaki nguo zake
“Kwahio
unataka kusema kuwa utakwenda kushindia mkate si ndio”
Aliongea mama
Jessica, mana hataki mtoto wake ahame hapo nyumbani, ingali anatakiwa
kuhama..
Lakini wakiwa bado wanazozana na mama yake mara dada yake
kaingia
“Jessica,.. Mdogo wako ndio anakwenda hivyo”
Aliongea
mama huku akimuonyeshea Jessica kwa kidole
“anakwenda wapi? Zimbabwe
au”
Jessica alileta utani mbele ya jambo la usiriasi
“staki
utani wako Jessica… “
Mama aliongea huku akiwa hataki kweli
utani
“mama, mi naona kweli akae peke yake, mana akizidi kukaa huku,
baba atazidi kumbana na kushindwa kufanya mambo yake”
“kumbuka kuna
usafi kule, kumbuka atatakiwa kupika huyu”
Aliongea mama
Jessica
“mama, mimi nitajitolea kumfanyia usafi kila baada ya siku
tatu”
Jessica alivunja ukimya na kusema kuwa yupo tayari kufanya usafi
kila baada ya siku tatu,…
“iv Jessica kwanini unataka twende tofauti na
mimi lakini”
“mama,… Adam keshakuwa mtu mzima, wacha akae mbali na baba
ili kidogo heshima ije”
Walikuwa wakibishana lakini ilikuwa ni kazi
bure,… Adam alimaliza kukusanya nguo zake kisha akazitupia katila gari yake…
Mana kama ni mali keshapewa nusu ya mali na baba yake… Hivyo hamtegemei baba
yake kwa lolote lile, hata kanisa na hio nyumba pia hakujenga kwa pesa za baba
yake, ispokuwa zakwake… Baba alishiriki tu kusimamia ujenzi wa kanisa lakini
hana asilimia yeyote katika kanisa hilo
“labda niwatakie siku
njema, mana ndio nakwenda hivi ili niwahi kuandaa vitu vingine”
Aliongea
adam huku akitoka zake
“adam mwanangu… Usije ukaajiri msichana wa kazi,
utakosa sifa za kuchaguliwa na wazee wa kanisa”
Aliongea mama yake kwa
msistizo mkubwa sana
“mama, najua kila kitu kuhusu hilo.. We ondoa
shaka… Baba yangu ananionea sana… Lakini bwana Yesu yupamoja
nami”
“milele amina baba”
Waliongea ongea kwa kiasi fulani kisha
adam huyoo, lakini alisindikizwa na dada zake na mama pia,… Walifika katika
nyumba hio mama akamtangulia mtoto wake kuingia katika nyumba hiyo,… Maombi
yalianza mara moja ili kama lipo baya basi liweze kutakaswa kwa damu ya Yesu,
maombi yalichukuwa muda kiasi fulani, kisha wakaingia ndani,… Basi dada zake na
mama wao walianza kufanya usafi, mana si unajua nyumba mpya, lazima kidogo kuwe
na usafi japo ilishafanyiwa Usafi muda mrefu, sema hapo ni kama kufuta futa yu…
Adam yeye alikuwa akizunguka zunguka huko nyuma ya nyumba kama vile anakagua
baadhi ya mambo, wakati huo anaimba nyimbo za kumsifu bwana Yesu Kristo,….
Lakini ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni mzee wa
kanisa
“haloo mzee shalom baba”
“shalom… Tumsifu yesu
Kristo”
“milele amina baba”
“unahitajika huku kanisa nitajitolea
haraka sana”
Simu ilikata ghafla na kushindwa kuelewa kwanini kaambiwa
anahitajika haraka sana,.. Adam hakutaka kujiuliza mara mbili,
“bwana
yesu kuwa nami kila hatua”
Alinuia baadhi ya maneno kisha akapanda
gari
“baba mtumishi, unakwenda wapi tena”
Aliuliza mama yake
mzazi
“nimehitajika kanisani mara moja”
“sawa, uwahi kurudi basi
mana hatutochukuwa muda”
“sawa mama”
Adam aliondoka kwa usafiri
wake, yote hio ni kuwahi alipoitwa na mzee wa kanisa….. Sasa huku ndani sasa
mama alimuuliza mtoto wake ambaye ni Jessica kiwa
“hiv Jessica, umeona
kilichotokea asubuhi wakati adam anaingia”
Aliongea mama huku Jessica
nae pia akishangaa
“mimi pia nilishangaa,.. Kwasababu hata baba
nilimwona akitetema kwa maneno machache tu ya adam”
“sasa lile kanisa
linaongozwa na nini, kwasababu sio waumini pekee mpaka mchungaji nae ana hali
mbaya”
“mama, hapa kuna kitu, lakini bwana Yesu Kristo atajafa miujiza
na atatakasa kila pembe ya njia yetu”
“amen”
Huku
kanisani sasa adam akiwa katila lift kuelekea kanisani, na hio ni siku ya
Jumapili ambapo asubuhi ndio alifanya kile kituko,… Sasa ile anafika tu ndani ya
kanisa, alikutana na viongozi mbalimbali wa makanisa hapa jijini Arusha,..
Lakini alipoangalia vizuri alimwona Catherine na baba yake, ghafla akamwona hata
baba yake mr jacob, lakini mr Jacob alikuwa katika moja ya jasira mno,… Adam
alijua sasa hapa kumekucha, akiangalia vizuri mpaka wale wanaohusika na mambo ya
ndoa wapo, hapo tumbo la adam likaanza kuwaka moto,… Mana hakuutegemea huu wito
utakuja kuwa hivyo,
“asifiwe bwana mwokozi wetu alie hai”
Alitoa
salam huku akivuta kiti akae,
“milele amina baba mchungaji”
Adam
alikuwa na hofu, mana hapo hakukuwa na muumini mdogo mdogo hata mmoja, yaani
wote hapo ni viongozi wakubwa wa makanisa mbalimbali hapa jijini, yaani muumini
mdogo mdogo ni Catherine peke yake, sasa haijulikani pana kikao
gani
Adam alikuwa haamini kama leo
anafungishwa ndoa ya lazima lazima, mana kama ni kanisa lake tayari
limeshakamilika kila kitu, ni yeye kuchaguliwa kuwa mtoa huduma katika kanisa
hilo, mana kama ni wito anao na tayari keshapokea wito kuwatumikia kondoo wa
bwana,.. Adam alianza kukusanya hasira, na hapo ni mbele ya viongozi mbalimbali
wa makanisa yote hapa jijini Arusha… Mabishop wote wamejaa hapo, na haijulikani
kuna nini… Lakini wakati adam akiendelea kuwaza kuhusu kikao hicho, ghafla
lililetwa joho la rangi nyeusi mchanganyiko na nyeupe,.. Tena joho jipyaaaaa….
Hajakaa vizuri mara yliletwa maji ya baraka,.. Mpaka hapo adam aifurahi sana, na
hapo hapo Mabishop wakaanza kufurahi na kupiga
makafiri,…
“haleluyaaaaaaa”
“ameeeeeeen”
“nasema
haleluya”
Alisifu Bishop mmoja mkubwa hapo jijini, huku viongozi wengine
wakipokea sifa hio,…
“aaaameeeen”
“bwana asifiwe
sanac
“ameeen”
Maji ya baraka yaliletwa kisha akamwagiwa adam,…
Yaani hapa sasa ndio anaupokea wito wa kuwa mchungaji rasmi, mana mchungaji wa
kanisa ni lazima uchaguliwe na wakuu wa makanisa, sio lazima Mabishop wawepo,
hata pasta wa kawaida anaweza kukuchagua kuwa pasta.. Ila sema mr Jacob yeye
anajulikana sana na hakupenda mtoto wake apokee wito kwa kusua
sua,..
“mpaka sasa umeshapokea wito, sasa unaweza kuliendesha kanisa
lako… Bwana yesu
asifiweeeeeeee”
“aaaaaaaaaaaaaaameeeeeeeen”
Zilikuwa ni shangwe
japo hapakuwa na waumini wengi zaidi ya hao hao viongozi,.. Yaani muumini
anatakiwa kusikia tu kuwa tayari mambo yamekuwa mambo,… Mwanamke wa kwanza
kumrukia adam alikuwa ni Catherine,… Adam alitamani sana kumkwepa lakini
ilishindikana kwasababu kuna baba yake binti, kuna baba yake huyo adam… Afu watu
wakubwa walikuepo, na hapo ndio kwa mara y kwanza Catherine analipata kumbatio
la adam.. Kumbe Viongozi wote wameshajuzwa kuhusu adam na Catherine, saaa ngapi
hawajaanza kusema
“inapendeza sana… Watoto wa viongozi kuoana,
inapendeza sana”
Aliongea Bishop mmoja ambae nae ni mualikwa, adam
hakutaka kuonyesha nidhamu mbaya mbele ya viongozi wakubwa wa
makanisa,..
“kuanzia leo… Sasa una kanisa lako.. Sasa hata
ukianza na waumini 10.. Utajua mwenyewe, ni wewe na juhudi zako”
Ilikuwa
ni kauliza ya baba yake adam, ikiongea nae…
“ni kweli… Hata sisi usione
sasa tuna wito wa Bishop, sisi tumeanza na muumini mmoja, mpaka sasa tuna
makanisa meeengi sana.. Tena huyu mtoto ana bahati nzuri sana… Sisi enzi zetu
tulikuwa na makanisa… Yaani hata halijapauliwa… Lipo wazi kabisa… Lakini wewe
unakwenda kuanza uchungaji ukiwa na kanisa la kifahari”
Yalikuwa ni
maneno ya pasta mmoja aliohusika katika swala zima la kumbariki katika kulitoa
au kulitangaza neno la Mungu,… Na uzuri adam amekwenda chuo cha Biblia na
kuyasoma yote yaliostahiki.. Mana kusoma Biblia kila mmoja anajua,.. Tatizo ni
kuifafanua maana zake…
“bwana Yesu asifiwe”
Aliongea adam huku
akinyoosha mikono,..
“milele amina”
“kwanza niwashukuru wote kwa
ujioni wenu, naamini yoye hayo ni kwa neema za mungu…. Bwana yesu awatangulie
viongozi wangu”
“ubarikiwe kijana…. Umri wako ni mdogo, ila wito
unapoupata huna budi kuufanyia kazi”
“ni kweli mchungaji… Nashukuru sana
kwa kunidhihirishia wito huu… Yesu awabariki saaaana”
Aliongea adam kwa
furaha ya hali ya juu mno, huku akiketi katika kiti,…
“unajua sisi
tunapomchagua mtu kuwa kiongozi wa kanisa fulani,.. Kwanza hata wakati wa
kumwita haambiwi, na pia anapokuja hatutakiwi kuonyesha sura za furaha, ispokuwa
huzuni mwanzo mwisho”
Aliongea Bishop mmoja mwenye asili ya kizungu,
huku Mabishop wengine wakipokea maneno hayo, kana kwamba ndio torati yao ya kila
wanapomteuwa kiongozi mpya wa kanisa fulani,…. Adam alifurahi sana mana alijua
kutokana na kukataa kuoa huenda asipate nafasi ya kupata wito wa kuchunga kondoo
wa bwana… Lakini pia hakuwa na wasiwasi sana kwasababu siku ile anawekwa kikao
na baba, mama na dada, kuna mtu alimpigia simu akiwa yupo nje tena ndani ya
gari,… Kama unakumbuka kuna sehemu aliongea na mtu fulani ila sisi hatukujua
aliongea na nani… Sasa adam alipokuwa akitoka nje alikutana na mzee wa kanisa
lao hilo alipokuepo muda sio mrefu,…
“ukawachunge vyema kondoo wa
bwana…. Hakikisha unakwenda na junsi hali inavyotakiwa. Sawa bwana
mchungaji”
Aliongea mzee wa kanisa na wakati huo Catherine keshapata
nafasi ya kumganda adam, yaani siku moja yu kupata nafasi ya kumbatio la adam
basi kamganda moja kwa moja…
“mzee ndio mana juzi nilikupigia simu, kuwa
ivi ukikataa kuoa unaweza kweli kukabidhiwa kanisa.. Uliposema ndio… Kiukweli
nilifurahi sana mana napenda kuwa mchungaji katika roho, yaani nimejikuta tu
napenda, sasa sikutaka ndoto zangu kuishia njiani, au wito wangu kuishia
njiani”
“basi baba mchungaji.. Kilichobaki sasa ni kiteuwa wasaidizi
wako katika kanisa lako… Wazee wa kanisa, waalimu, nabiii, na wengine wengi
wenye vipawa vyao”
Aliongea mzee wa kanisa huku Adam akitoa mkono wa
Catherine kwenye bega lake,…
“kama ungelikuwa ni mwanamke mwenye adam,
basi huu uzungu wako ulitakiwa uwe mkiwa wawili na mumeo, sio huku kwenye nyumba
za ibada”
Adam alimwambia Catherine, mana Catherine ile nafasi ya
kumbatio ndio kapata dezo, kaganda kabisaa… Yaani adam anamchukia sema ni
mtumishi wa mungu, hivyo hatakiwi kumchukia mtu kiasi hicho….
“mtumishi
adam… Lakini kwanini unanifanya kuwa mdhaifu kwako.. Eti baba”
Adam
hakutaka kumjibu chochote kile zaidi ya kuagana na mzee wa kanisa… Kisha akawa
analielekea gari lake,… Na Catherine nae yupo nyuma yake
“huna
pakwenda”
Adam alimuuliza Catherine…
“baba mtumishi… Hata yesu
alikuwa na wafuasi wengi sana mpaka wanawake,.. Lakini hakuambiwa awaoe, sasa
siwezi kulazimisha kitu ambacho hakitakiwi,… Mimi ni kondoo wako, nipe nafasi
kwenye kanisa lako… Hata ukiniweka kwa waimba kwaya, nitashukuru sana baba
mtumishi”
Catherine aliongea mengi, yaani kama unamuona ungelimuonea
huruma, lakini kweli hapo anafunika riziki ya mwenzie ambaye ndio mwenye nafasi
ya kuolewa na adam,
“siwezi kuteuwa mwimbaji wa kwaya anaevaa nguo
fupi”
“nipo tayari kubadirika kwa njia yeyote ile, na pia nitamheshim
mama mchungaji mtarajiwa”
Hapo adam kidogo akapata timaini juu ya maneno
ya Catherine
“apo sasa kidogo umeongea pointi… Nipe muda nitakuchagulia
nafasi kanisani kwangu”
Aliongea adam wakati huo Catherine alitamani
hata kupiga magoti kwa kukubaliwa nafasi yeyote ya kanisani kwa pasta adam… Na
hivyo ndivyo alivyotaka,.. Sasa mambo yanaiva taratibu, maskini eva wa watu
sijui atakaza buti kwa staili gani, mana ndio taratibu anaanza kunyang’anywa
mume… Basi adam alipanda gari yake na hata Catherine nae alipanda gari yake
kisha kila mtu akapita njia yake… Ukumbuke adam aliwaacha mama yake na dada yake
kule nyumbani kwake wakiendelea kufanya usafi mana adam ndio alikuwa anahama
siku hio….. Moja kwa moja mpaka nyumbani kwake, lakini kwa bahati mbaya
hakuwakuta walikuwa wameshaondoka muda tu, lakini mezani alishaandaliwa kila
kitu, sasa maisha ya ubachela ndio anayaanza…. Hapo anawaza kanisa lake litakuwa
na vipawa vya aina gani, yaani alikuwa akipanga mengi sana juu ya kanisa lake,….
Lakini ghafla simu yake inaita, kuangalia alikuwa ni mama yake.. Alipo pokea tu
akakutana na sauti ya mama yake
“haleluyaaaaaaaaaa….. Bwana Yesu Kristo
atukuzwe kwa kupambana juu yako mwanangu.. Hongera, nimepata taarifa sasa hivi
tayari umeshaupokea wito ulioitwa na baba muumba”
Aliongea mama adam
huku akionyesha kuwa na furaha ya hali ya juu, na aliamini mpaka hapo adam
hawezi muoa Catherine, mana ilikuwa bila kuoa hapewi wito huo, sasa
keshapewa….
“tumsifu yesu Kristo, baba alie hai”
“milele amina
mwanangu”
“mama… Kesho nahitaji kwenda kulifungua kanisa na nyimbo za
kuabudu,… Siku nzima waumini wajue tayari kanisa limeshafunguliwa.. Mama..
Kanisa langu litakuwa kanisa la kipekee katika huu ulimwengu.. Litakuwa kanisa
la uokovu kwa kila muumini”
“baba nakuunga mkono… Dada yako huyu hapa
nae anaruka ruka”
“mpe simu dada Jessica”
Adam alitaka kuongea
na dada yake, mana alipo waacha, hakusema anakwenda wapi,
“YOUNG PASTOR
in the church… Thanks Jesus, for your power to my brother”
Alikuwa ni
Jessica akiyaongea hayo maneno kwa furaha ya hali ya juu
“sasa ndio nini
hivyo… YOUNG PASTOR ndio maneno gani dada”
“mtumishi adam… Haijawahi
tokea kwa kijana mdogo kumiliki kanisa, tena kwa kishindo… Hata wewe unajua ni
kanisa gani linamilikiwa na kijana? Hakuna, yaani wewe ndio wa
kwanza”
“basi sawa lakini hilo jina si sahihi, nitakushtakia kwa
mungu”
“basi baba mtumishi… Ila nina furaha sana juu ya jambo hili,
kesho nakuja kushinda kanisani kwa ajili yako kaka yangu”
Yalikuwa ni
maneno ya Jessica, yaani familia nzima ipo nyuma ya adam, yaani inapendeza zaidi
kwa hali kama hio…..
Baada ya masaa kadhaa ikiwa ni usiku, Adam alifanya
maombi kabla ya kulala kisha akalala zake ikiwa ndio siku ya kwanza kulala
katika jumba hilo kubwa
sana…..
**********************************
Ghafla
alishtuliwa na ngurumo za ajabu, akiangalia saa ni saa nane za usiku, na ngurumo
hizo zinatokea humo humo ndani, adam alisali kabla hajafuatilia ngurumo hizo,
ilikuwa ni usiku tena tena umeme ulikuwa umekatika,.. Hakuna kitu kibaya kama
umeme ukatike afu jumba kubwa tena yupo pekee,…. Alichukuwa simu yake na kuwasha
tochi kisha akaanza kuzunguka ndani ya jumba hilo… Alipita vyumba vyote lakini
muumgurumo bado ipo kama vile kuna watu wanasali kwa imani ya kishetani,… Lakini
kuna chumba kimoja hicho hajawahi kukifungua toka kuzaliwa kwake, yeye hukiona
tu.. Hakutaka kukiacha, na kweli katika hicho chumba kulisikika sauti za wati
kadhaa wakifanya ibada,.. Wakati huo adam nywele zake
zinamchemka.
Kiukweli ni sauti zilizokuwa zikitisha sana…. Lakini adam
ni mtumishi wa Mungu, yupo tayari kufa kwa ajili ya kondoo wake, kama alivyokufa
Yesu Kristo kwa niaba ya wakristo wote,.. Adam alikibonyeza kitasa cha mlango na
kwa bahati nzuri hawakufunga mlango, hivyo adam akasukuma mlango ule kisha
akaingiza kichwa…. Ilisikika tu sauti
ikisema
“haaaaaaaaaaa”
Ilikuwa
ni siku nzuri kwa mchungaji adam kukabidhiwa fimbo zidi ya kondoo atakao
wachunga, lakini siku hii hii ya leo, ilikuwa na balaa katika upande wake, kwani
siku ambayo anahamia katika nyumba yake hio, na ndio siku anapewa wito dhidi ya
kipawa chake,.. Na siku hio hio mishale ya usiku alianza kusikia ngurumo za
ajabu katika nyumba hio, sauti hizo zilimfanya ashtuke na kuanza kutoka taratibu
ili kubaini ni sauti gani na ni akina nani… Adam alizunguka ndani ya jengo hilo
kubwa ambalo kwa wakati huo umeme ulishakatika hivyo alikuwa akitumia simu kama
tochi,… Bila uoga aliweza kuzunguka jengo lote,… Sauti zili zilinyamaza wakati
akiwa anazunguka.. Lakini sasa katika pita pita, alikipita chumba kimoja, hicho
chumba hua anakionaga tu na hajawahi kuingia katika chumba hicho toka kuzaliwa
kwake,… Adam alisali pale pale kisha akashika kitasa cha mlango, tayari kwa
kufungua… Ndani yake zilisikika sauti za kusali kwa njia ya shetani…. Adam bila
kuogopa alifanikiwa kufungua huo mlango na kuingiza kichwa chake,.. Sauti
iliyosikika ni ya adam akiwa
katahamaki
***********************************
“haaaaaaaaaaaaaa”
Alikurupuka
kitandani huku akifikicha macho yake, kana kwamba alikuwa usingizini, na hio
ilikuwa ni ndoto na haikuwa kweli,… Mana umeme ulikuwepo, na pia nyumba alio
iota sio hio ya kwake, bali ni nyumba ya familia yao kule alipotoka, yaani
alipokuwa akiishi na wazazi wake.. Na ndio mana kuna mahari paliandikwa kuwa,
chumba hicho hajawahi kuingia toka kuzaliwa kwake, maana yake ni kule kwa wazazi
wake na sip hapo kwake…
“shindwa kwa jina la Yesu…. Pepo mchafu
tooookaaaa”
Kesho yake adam aliamka asubuhi sana akaingia
jikoni kutengeneza chai, mana ikumbukwe kuwa adam ana kampuni ambayo ni mali
aliopewa na baba yake ili aendelee maisha yake, na hapo bado hajakabidhiwa mali
vizuri, hio aliopewa ni moja ya kampuni za mr Jacob, na mtoto wa kiume ni yeye
pekee,.. Adam si mvivu wa kupika, na haruhusiwi kuishi na mwanamke wa aina
yeyote yule, hata mchumba haruhusiwi kuishi nae ispokuwa kusalimiwa tu… Au kama
anataka kufanyiwa usafi wa nyumba na mmoja kati ya waumini, basi yeye hatakiwi
kuwepo pale usafi unapofanyika, anaeruhusiwa kufanya usafi humu au hata kulala,
ni dada zake na mama yake tu basi… Ndio wana ruhusa ya kuja kuishi hapa, ila
mwanamke yeyote yule haruhusiwi kuishi hapa ispokuwa mkewe tu, hivyo kama pasta
hujaona… Basi haruhusiwi kuishi na mwanamke ambaye hujamuoa,… Hata mchumba
hairuhusiwi… Wakati akiwa jikoni alikuwa akiikumbuka sana ile ndoto, haijawahi
kutokea katika maisha yake
Sasa huku kanisani kwa adam,… Kumbe
taarifa za ufunguzi wa kanisa hilo zilishasambaa kila kona, hivyo palikuwa
pakipambwa vizuri kwa ajili ya kuabudu siku nzima kwa furaha,.. Waumini walikuwa
wengi sana ingali kanisa ni jipya, hata adam atashangaa sana kuona siku ya
kwanza tu ana waumini wengi sana,.. Lakini sasa mwanamke wa mbele sana alikuwa
ni Catherine, na inaonekana waumini wengi alikuja nao yeye,… Mapambo ya kila
aina yalipambwa katika kanisa hilo lililojengeka kwa vioo vitupu,… Wengine
walikuwa wakifanya usafi, wengine walikuwa wakifunga majukwaa, vinywaji
mbalimbali kasoro vilevi pekee ndivyo vilivyo kosa nafasi ya kuletwa
hapo…
Huku kwa adam akiwa anakunywa chai baada ya kumaliza
kupika, simu yake ilikuwa katika sikio
“haloo…. Tumsifu yesu
Kristo”
“milele amina baba mtumishi… Hali ya kuamka
waionaje”
Alikuwa ni Eva ndie aliepigiwa simu
“bwana Yesu ndie
kila kitu katika usingizi wangu… Ashukuriwe na bwana muumba mbingu na
ardhi”
“amen, vp baba mtumishi…. Kiukweli sijalala kwa furaha… Nimepata
habari kuwa, tayari umeupokea wito toka kwa Bwana wetu”
“ndivyo
ilovyo”
“Ashukuriwe bwana yesu”
“amen…. Uko wapi sasa
eva”
“nipo nyumbani najiandaa kwenda kanisani”
Eva alikua hana
taarifa yeyote kuhusu ufunguzi wa kanisa la mchumba wake,
“mama
mchungaji”
“ndio, baba mchungaji”
“ina mana huna taarifa juu ya
kanisa lako”
Adam alimuuliza eva, lakini eva kweli hakuwa na
taarifa
“sina taarifa… Na kwanini usingeniambia”
“Samahani,
huenda furaha ilinizidi mpaka kusahau jambo jema kama hili”
“enhee, nipe
taarifa”
“kuna maombi ya kufungua kanisa, na sasa kila mmoja mbona
anajua”
Aliongea bwana adam huku eva akifurahi sana na kuairisha kwenda
kanisani kwa baba yake adam, ili aende kwenye kanisa la mchumba
wake,
“upo wapi sasa baba mchungaji”
“nipo nyumbani, namalizia
kunywa chai”
“utatoka na familia yako”
“hapana, nadhani wao
wameshatangulia, na hata hivyo mimi sipo kule tena, nimeshahama”
“weeee
baba mtumishi, unasema kweli”
“ndio, mbona nimehama jana na hapa
nakunywa chai”
“nani kapika hio chai”
“nimepika mwenyewe, si
unajua sheria na taratibu za mchungaji mbae hajaoa”
“nazifahamu na ndio
mana sijatamani nije nikupikie… Ila utateseka sana baba mchungaji,… Nipo tayari
kwa hali yeyote baba mchungaji sitaki uteseke”
“hebu ngoja tutaongea
vizuri… We jiandaa nakupitia hapo nyumbani”
“sawa baba
mchungaji”
Adam alimaliza kunywa chai haraka iwezekanavyo, kisha
akatafuta suti nzuri na kuanza kuinyoosha nyoosha na pasi mara moja… Kisha huyoo
kapanda gari yake.. Uzuri wa geti yake inafunguka kwa rimoti, hivyo hakuwa na
shida ya mfungua geti,..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment