Search This Blog

Thursday 24 November 2022

THE DOM - 1

 

     

     



     IMEANDIKWA NA : MOONBOY



    *********************************************************************************

    Chombezo : The Dom

    Sehemu Ya Kwanza (1)

     

    SON OF PRESIDENT GU



    INAPOANZIA RASMI KATIKA SEHEMU YA KWANZA



    Simulizi yetu inaazia maeneo ya airport, tukiwa tunamuona kiongozi mkubwa akiandaliwa sehemu ya kukaa kana kwamba kuna mheshimiwa mwenzake aliokuwa akimsubiri eneo hilo, yaani kaja kwa mapokezi zaidi, lakini mapokezi hayo hayakuwa rasmi yaani nchi haina taarifa kuwa raisi kaenda Airport kwa mapokezi ya mgeni fulani, mana kila kiongozi wa nchi anapotoka basi nchi inapaswa kuwa na taarifa sahihi juu ya safari yake, lakini hapo tunamuona yeye na walinzi wake pamoja na makamu wake bila kusahau waziri mkuu na watu wachache sana ambao sio wa kujulikana sana katika nchi,... Kwa mbaaali rais alisema huku akinyoosha kidole

    "ndege toka korea Kusini hiooo"



    Aliongea mheshimiwa rais huku akinyoosha kidole, kitendo kilichofanya watu wote wa karibu yake kucheka,... Kweli kuna dege kuubwa liliokuwa likijiandaa kushuka katika uwanja wa JULIASI KAMBARAGE NYERERE (JK NYERERE) Dege linashuka na kufungua mlango taaratibu bila wasiwasi wowote..... Walishuka watu wengi sana hasa wa nchi za kigeni hususan Korea Kusini na wengine wengi,... Lakini kwa mtazamo hakukuwa na kiongozi yeyote aliokuwa ndani ya ndege hio, bali walikuwa ni abiria wa kawaida tu, wengine ni watanzania waliokuwa wakirudi kwao na wengine ni wageni kabisa wala hawafanani na watanzania,... Lakini watu wakiwa wanaendelea kushuka katika ndege hio ghafla kuna watu watano wakubwa waliojitokeza pembezoni mwa ndege hio, watu hao hawakuwa ndani ya ndege bali wapo nje ya ndege,,, kwa takwimu za haraka haraka walionekana kuwa ni majambazi watekaji, asilimia kubwa ya sehemu zisizoweza kuvamiwa ni Airport, mana kunakuwa na ulinzi wa hali ya juu sana, sio ulinzi wa askari wala sio ulinzi wa vyombo maalum, lakini ilishangaza majambazi wapatao watano tena waliokomaa kwelikweli, wakiwa wamesimama katika mlango wa ndege kana kwamba kuna mtu nao wanasubiri kwani hawakuhangaika na wale abiria wa kawaida waliokuwa wakishuka,.. Abiria walikuwa wakiishiria lakini waliokuwa wanamsubiri hatokei,... Lakini kati ya vijana hao kuna mmoja alipokea simu lakini haikujulikana alipokea simu ya nani na kaambiwa nini,.. Na uzuri wa majambazi hao hawakuwa na silaha aina yeyote ya moto ispokuwa visu tu ndivyo vilivyojaa katika miili yao, yaani hawa ni majambazi visu, sasa yule kijana mmoja alipomaliza kuongea na simu, alijikuta ananyoosha kidole juu ya ndege, kana kwamba mtu wao wamemuona,... Sasa kabla hajataka kusema ghafla kuna kijana mwingine kati yao, aliruka mithili ya Sungura na kumrukia mmoja wa abiria wale waliokuwa wanamalizikia kushuka



    Maskini alirukiwa kijana mmoja wa kitanzania ambaye alionekana kutoka nje ya nchi huku akiwa kubeba kabegi chake cha kushika mkononi, kijana huyo mdogo alidondoka chini mana hakutegemea kama angelirukiwa teke na njemba hilo,.. Sasa mbaya zaidi tukio linatokea mbele ya raisi, yaani hata rais yupo katika uwanja huo huo akiwa anamsubiri mgeni wake, sipati pocha majambazi hawa watafungwa miaka mingapo pindi wakiingia mikononi mwa polisi,... Na wakati huo mheshimiwa rais alikuwa akiona kila kitu tena alivua mpaka miwa ni huku akishangaa ujinga uliokuwa ukifanyika,....

    "ina maana hapa hakuna usalama wa aina yeyote"

    Aliongea mheshimiwa rais huku watu wake wakiwa kimya tu,....

    "nauliza ina maana hakuna usalama hapa,... Kwanini abiria wanatekwa hapa hapa Airport"

    "Kiukweli hatujui mkuu"



    Sasa pale kwenye ndege, Kumbe yule kijana wa kitanzania hakuwa mtu wa mchezo mchezo hata kidogo,... Kwani naye alikuwa ni kama wao, sasa ikawa ni sinema kwa abiria wengine, kuna waliokuwa wakipiga picha kwa ajili ya kiweka kama tukio ila wandishi wa habari hawakuepo eneo hilo, inaonekana hawakupewa nyeti nyeti za kuja kurekodi tukio zima



    Sasa kijana abiria alikaa sawa ili kuwakabili watu waliomzunguka wapatao kama watano tena ni wale walioshiba haswa, yaani ukiambia wabeba vyuma basi ndio hawa,.. Kijana abiria alikaa sawa kama vile mpiganaji mzuri lakini haijulikani kama atawaweza watu hao, na mbaya zaidi rais yupo eneo hilo la Airport,..







     





    Ama kweli udogo si tija, huezi amini mapigano yalipoanza hakuna jambazi alioweza kuingiza ngumi hata moja kwa kijana abiria, ilionekana dhahiri kijana abiria alikuwa na uwezo wa hali ya juu,... Sasa kibao kiliwarudia majambazi hao, kwani kila alietaka kukimbia hakupewa nafasi,... Sasa je, huyu kijana abiria ni nani,.. Watu watano walioshiba ameweza kuwashusha chini, sasa huyu ni nani??  Na kwanini walimkabili yeye tu??



    UKIIKOSA HII MIMI SIPO.... NI SIMULIZI YA ACTION AMBAYO MIMI MWANDISHI MoonBoy SIJAWAHI KUANDIKA ACTION, HIVYO KAMA KUTAKUWA NA MAKOSA, NAOMBA TUSAMEHEANE, MANA MIMI SIO MZOEFU WA ACTION STORY, BALI MIMI NI MZEE WA CHOMBEZO AU LOVE STORY... HII NI KWAMBA NIJARIBU KIPAJI CHANGU CHA UANDISHI KAMA NAWEZA AU SIWEZI... MNAPOONA PANA MAPUNGUFU NIKOSOENI KABISAA RUKSA NAWAPA...... SASA TUENDELEENI NA SIMULIZI YETU YA MAPIGANO....



    Sasa wakati wale majambazi wakiwa hoi na tayari wapo katika himaya ya kijana abiria, TAFADHALINI SANA NAITA KIJANA ABIRIA MANA BADO HATUJAMJUA JINA LAKE...



    Sasa pale pale polisi wanatokea na kumkamata kijana abiria,. Lakini sasa ilionekana kijana abiria ni mtu mkubwa kiasi fulani, mana alitoa waleti yake iliokuwa na vitambulisho vya kazi,.. Wakati huo bastola za polisi zikiwa zimemzingira katika uso wake, na hakuwa akiogopa,...

    Sasa ile anatoa tu kile kitambulisho ghafla kilinyakuliwa na askari wa rais,

    "unafanya ujinga gani... "

    Aliongea askari huyo huku akikificha kile kitambulisho, inaonekana huyu ndio mgeni wa raisi, lakini wale askari walitamani sana kujua kitambulisho cha kijana huyo, mana walikosa nguvu baada ya kumuona askari wa raisi akija kumchukuwa kijana abiria, hivyo kitambulisho hicho hakuna aliekiona zaidi ya askari wa rais peke yake mana alimuwahi asijitambulishe kwa kitambulisho hicho,.. Je? Huyo kijana ni nani, na katoka korea kufanya nini?



    Lakini sasa cha ajabu na cha kushangaza raisi anakuja huku akipiga makofi, yeye waziri mkuu, na makamu wa raisi... Hata wale askari waliotaka kumkama kijana abiria walishangaa kumuona raisi akiwa anafurahia mapigano,..

    "hahahahha, Kiukweli sihitaji kusema mengi, ila karibu sana kijana wangu... Kuwa huru na hao watu watano sio majambazi kama ulivyofikiria, nimewatuma wafanye hivyo, ili nijue kilichokupeleka korea umekipata?... Nashukuru sana na naomba tuingie katika gari kwa mapumziko zaidi"

    Aliongea raisi huku kijana huyo akiingia katika gari ya rais, yaani gari ya raisi hatakiwi kukaa mtu mwingine zaidi ya mlinzi wake tu, lakini leo kumkaribisha kijana huyo aingie katika gari, hivyo ndani ya gari la rais wapo watu wanne akiwemo, DEREVA, RASI, MLINZI WA RAIS, NA KIJANA ABIRIA..



    "mkuu, nimemwona mtoto wa General, yule wa kike na alionekana nae anatoka korea"

    Aliongea askari huyo huku safari ikiwa inaendelea,....

    "hakuna tatizo, hatojua lolote"

    Aliongea raisi huku safari ikizidi kwenda

    Lakini kijana abiria alionekana kutaka kuuliza lakini alinyamaza, kama vile hatojibiwa kwa usahihi....

    Gari iliingia mpaka Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo makazi makuu ya Mheshimiwa raisi,.. Kijana huyo hakiwa mgeni na mazingira ya uongozi kama hayo japo hujulikani yeye ni nani na alikuwa nchini kama nani,... Kijana anaingia Ikulu kama mheshimiwa fulani hivi, mana hatumjui ni nani,...



    "habari za safari kijana"

    Rais Alimsalimia kijana huyo,

    "salama tu, namshukuru mungu nimefika salama"

    "na uwezo ule, ivi ungepata misuko suko kweli"

    "kwa uwezo wa Mungu ningelipata, lakini kwa uwezo wa binadamu nisingelipata"

    Kijana huyo alionekana kumuamini mungu sana kila anapokwenda japo hatujajua ni dini gani mana hata jina hatulijui, na asilimia kubwa, Watanzania tunajuana kwa majina yetu, akiitwa Joseph basi tunajua huyo ni Mkristo, akiitwa juma basi tunajua huyo ni Muislamu kutokana na jina lake.. Lakini huyu hatulijui jina lake...

    "ok.... Mafunzo yaliendeleaje huko"

    "aaahhh Namshukuru Mwenyezi Mungu kajaalia nimesoma ulichonituma mkuu"

    "hata mimi nimekiona ulichokisomea"

    "aahh lakini mkuu, vp pale Airport, pale si kuna kamera za CCTV sasa inakuaje kwa rekodi zangu kuwepo"

    Aliongea kijana huyo na wakati wapo wenyewe tu katika chumba husika,  hata mlinzi wa rais hayupo eneo hilo

    "wala usihofu,.. Kabla ya wewe kufika kamera zote zilizimwa, vyombo vyote vya usalama vilizimwa... Na askari wa eneo lile wote walitolewa kwa muda kisha nikawaagiza makomando watano wakujaribu kama ulichokifuata huko ni chenyewe, kwa bahati nzuri umefanya vizuri"

    Kumbe wale majambazi ni makomando wa Tanzania, sasa iweje kijana mdogo kama huyu awazidi uwezo makomando wa Tanzania,.. Kweli hapa rais ana kijana bora na sio bora kijana

    "kwahio mkuu, wale vijana ni makomando wale"

    "ndio... Wale ndio moja wa vikosi vyetu vya kikomando"

    "aahhhh mbona ni wadhaifu kiasi kile"

    "kwasababu mafunzo yako wewe ni ya hali ya juu, na ndio mana umewaona ni wadhaifu"

    "Kiukweli hawaingii hata chembe katika mwili wangu"

    "nalijua hilo.... "

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya kijana huyo na Mheshimiwa rais, na walionekana kujuana kuliko kawaida

    "sasa, nataka ukapumzike... Lakini nataka utoe vitambulisho vyako vyote, vikiambatana na kadi zako za benki zoote, yaani kila kilichohusisha jina lako, naomba uviweke hapa mezani haraka sana, tena bila kufikiria"

    Aliongea mheshimiwa raisi huku kijana huyo akitafuta vitu hivyo katika begi lake, pamoja na waleti,... Baada ya Dakika mbili alikamilisha agizo la raisi, aliweka kadi na vitambulisho vyake vyote,...Tukianza na Vitambulisho vyake.. KITAMBULISHO CHA MKAZI... KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA... KITAMBULISHO CHA KITAIFA... KITAMBULISHO CHA JESHI... KITAMBULISHO CHA SHULE..... BILA KUSAHAU KITABU CHA KUSAFIRIA (PASPOT)..... Ikifuatiwa na kadi Za bank zifuatazo... CRDB BANK.... NMB BANK.... EQUTY BANK... KCB BANK... WESTERN UNION BANK... Vitu vilikuwa vingi mpaka rais akachoka.....

    "haaaaa... Kijana hivi VITANZI vyote ni vyako??"

    "Ndio."

    "nakagua kimoja baada ya kingine, angalia usije ukawa jipu"







    Aliongea mheshimiwa rais huku aki vikusanya vitanzi (Vitambulisho Vya kitanzania) (VITANZI) hivyo wakati huo kijana hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwasababu anakumbuka huyo ndiye aliemkatia vitanzi vyote hivyo, sasa iweje leo aje awe jipu,...

    "vitanzi vyote ulinikatia wewe, sasa sijui kwanini umesahau"

    Aliongea huyo kijana huku akiweka vitu vyake sawa baada ya kutoa vitanzi vyake vyote,..

    "kwani ulifikiri nakumbuka? Ata sikumbuki mana ni toka nilipokuwa waziri wa ujenzi, mpaka leo siwezi kushindwa kusahau"

    Aliongea mheshimiwa raisi, huku akiviweka vitanzi vile katika begi lake yeye rais,... Wakati huo kijana katulia tuli akisubiri mwongozo toka kwa raisi,.. Kuna kitu alibonyeza mheshimiwa rais pale pale kwenye meza kana kwamba anahitaji mtu aje hapo,.. Kweli alikuja askari wake na kumuamuru kuwa

    "mpeleke katika nyumba yake"

    Kijana alishangaa kuambiwa mpeleke katika nyumba yake, alitaka kuuliza lakini raisi alikunja sura kana kwamba alitakiwa kufata amri na sio jinsi alivyotaka,... Kijana alionekana kuwa na makazi tofauti na makazi ya serikali yaani kijana ana kwao lakini mheshimiwa hataki kusikia kijana akaishi kwao, na hapo ni aende akapumzike tu na mambo mengine kesho,... Kijana hakuwa na budi kwenda,

    "alafu sikiliza hutakiwi kutoka mpaka kesho"

    Aliongea mheshimiwa rais huku kijana akizidi kuingiza hofu juu ya swala hilo...

    "kwanini mzee"

    "nimeshasema hii ni amri na sio ombi"

    Roho ilimuuma sema tu hakuwa na uwezo wa kutenda kitu tofauti na rais



    Kijana alitolewa hapo kwa gari ya private, mana akitolewa na gari ya serikali, waandishi wanaweza kufuatilia ili kujua gari ya raisi au waziri inakwenda wapi,.. Na kitu kikubwa kijana huyu ni siri ya serikali haitakiwi mtu yeyote kufahamu uwepo wa kijana huyu, sasa hatujui ni kwanini ni siri kuwepo kwa mtu huyu,...

    "sikiliza kijana, najua bado hujapewa mwongozo wa kazi, lakini wewe ni mpelelezi wa siri, wewe ni askari wa siri, yaani anaetakiwa kukujua wewe ni sisi watu wa karibu wa raisi, na ndio mana mheshimiwa rais hataki serikali yoye ijue uwepo wako na ndio mana ukapelekwa kusoma kisiri siri"

    Aliongea askari aliokuwa anampeleka kijana huyo katika makazi yake,

    "sawa, mimi Sikatai lakini sio mpaka makazi nichaguliwe pakukaa"

    "weww tayari ni mfanyakazi wa serikali, hivyo lazima uwepo katika mazingira hayo"

    Kijana hakuwa na la kuongea zaidi ya kufuata kile kinachotakiwa, kijana alipelekwa mtaa wa Ostarbay jijini Dar es Salaam, mtaa wa watu wa hali nzuri kiasi fulani,.. Alishangaa anaingizwa katika jumba moja la kifahari ambalo geti lake tu linafunguka kwa rimoti kontroo, maana yake hakukuwa hata na mlinzi wala mfanyakazi,...

    "hapa ndio nyumbani kwako kuanzia leo,.. Kisheria kwa kazi yako haruhusiwi kuishi na mtu mwingine humu ndani, uwe wewe peke yako"

    "yaani jumba lote hili niishi peke yangu"

    "ndivyo inavyotakiwa, yaani hata mlinzi hatakiwi hapa"

    Aliongea askari huku akimzungusha nje ya nyumba hio, na hio nyumba haijawahi kukaliwa na mtu toka imejengwa,

    "alafu mbona kama hii nyumba haijawahi kuishi mtu"

    "ni kweli, nyumba hii ilijengwa spesho kwa ajili yako, kwasababu mheshimiwa raisi anajua kazi yako hivyo kujenga nyumba hii kutokana na kazi yako ya upelelezi wa siri"

    Kijana alizidi kuwa kimya,... Sasa kwenye milango, kila mlango una loku ya namba, yaani ukifika mlangoni kuna screen inakuangalia utie namba kisha mlango ufunguke,.. Nyumba nzima imezungukwa na kamera za siri yaani CCTV za siri, sio zile ukiingia tu umeziona hapana, hizo mpaka uzione yataka kutumia vyombo maalum vya kuangalia kamera kama zipo....

    "hii nyumba imezungukwa na kamera kote, kuanzia ndani mpaka nje"

    Aliongea askari, huku kijana akiangalia hio nyumba,...

    "usiangalie kijana, huezi kuziona.. Ni kamera za siri"

    Aliingea askari huku yule kijana akicheka sana

    "nisikilize mzee,.. Mimi nimekwenda korea kwa masomo haya ya upelelezi, jeshi, na mapigano... Katika masomo ya upelelezi tumesomea kamera aina zote,... Kabla hujanionyesha hizo kamera, mimi ndio nakuonyesha hizo kamera"

    Askari alishangaa sana kuona kijana anajua kila kitu

    "hebu Nionyeshe hata tatu za hapa nje"

    Aliongea askari huyo huku kijana akigeuka nyuma na kunyoosha kidole

    "moja hii hapa"

    Kiukweli kamera hizo bila vyombo maalum huezi kuona, lakini kijana huyo aliona..

    Askari alitulia kimya huku akizidi kuonyeshwa kamera hizo,...







     





    Basi baada ya mida kijana alibaki nyumbani hapo na uzuri zaidi kuna magari mapya hapo uwani, yaani mapaka magari kanunuliwa, sasa sijui huyu kijana ni nani zaidi ya upelelezi... Wakati huo askari keshaondoka hivyo kijana kubakia mwenyewe katika jumba hilo lenye ulinzi wa vyombo maalum na sio watu,.. Kijana alichukuwa begi lake na kutoa vitu vyake vya muhimu ana laptop maalum iliojaa systems za kamera na programu za upelelezi zaidi,.. Kwanza kabla ya yote aliisogelea kamera moja na kuitoa kisha kuna namba alizichukuwa katika kamera ile,... Alipomaliza aliirudishia mana ni kamera za kupachikwa tu katika sehemu za siri sana, yaani ni kadogo kama zile earphones ndogo za masikio,.. Alipochukuwa namba katika moja ya kamera, aliingiza katika mtambo wake wa kompyuta kisha akazisachi,.. Ghafla katika screen ikamwonyesha jumba zima hilo analo ishi kwa sasa.. Ghafla akazizima kamera zote,... Yaani uwezo aliokuwa nao huyu kijana sio wa kuigwa, yaani ukiiga hapa umeumia, elimu imekaa hapo, anacheza na kompyuta hata mzungu mjinga... Yaani utafikiri kuitengeneza yeye kumbe yeye ni mtumiaji tu,..

    Mara simu ikaita kucheki ni Mheshimiwa rais

    "haloo mzee"

    "kuna nini huko"

    "wapi"

    "naona kamera zimezima"

    Sasa kijana ndio anashangaa, ina maana systems nzima ya kamera hizo kumbe zimeunganishwa katika screen ya raisi, hivyo jengo hilo linaonekana na rais...

    "kuna waya niliugusa hapa hebu ngoja niuunganishe"

    Alidanganya, kisha akabonyeza mitambo yake kamera zikaendelea kufanya kazi,...

    "hapo vp"

    "acha hapo hapo usiziguse, afu pumzika kesho uje tukupe fomula nzima ya kazi"

    "sawa"



    Lakini kijana huyo naye ana familia lakini sasa haijulikani ni familia gani, sasa sijui kama huyu ndio mtoto wa raisi au vp,.... Kijana alitoa picha ya mwanamke mmoja hivi alionekana kumpenda sana mwanamke huyo, ila hatujui ni nani yake, mana ni mama mtu mzima, na sio mschana, inaashiria ni mama yake.... Mana aliikumbatia picha hio huku akisema

    "I love my mom"

    Aliongea huku akilia kiume, ilionekana mama yake amefariki dunia...



    Kesho yake akiwa yupo njiani kuelekea Ikulu, kwa ajili ya kupewa kazi yake, wakati huo alikuwa akiendesha gari yenye preti Namba ya usalama wa taifa, yaani ni ya serikali...

    Maramoja kijana alifika Ikulu na kuingia mpaka ndani,... Alimkuta waziri mkuu, pamoja na makamu wa rais, huku mlinzi wa rais akiwepo nyuma ya raisi, maana yake walikuwa watu wanne na kijana huyo alikuwa mtu wa tano,...

    "shkamoni"

    Alisalimia viongozi wote aliowakuta hapo lakini kabla hajakaa, alishangaa vitanzi vyake kumwagwa mezani,.. Lakini kumwagwa kwa vitanzi hivyo sio kitu, kitu ni kwamba vitanzi hivyo vilimshangaza sana kijana huyo, hivyo alishikwa na shauku ya kuuliza

    "kwanini imekuwa hivi"

    Aliuliza kijana, ambae mpaka sasa hatujalijua jina lake,.... Na hapa ndipo tutakapo lijua jina lake rasmi na kazi yake, bila kujua yeye ni nani na alikuwa nani hapa nchini.....





    Alipofika kijana huyo, mara moja rais alimmwagia vitanzi vyake ambavyo alivitoa kwa siku ya jana, na hio ilikuwa ni kwa ukaguzi tu na havikuwa na tatizo lolote, kwani hata kijana huyo alijitetea kwa kusema vitanzi hivyo alitengenezewa na yeye mwenyewe mheshimiwa rais,.. Hivyo havikuwa na tatizo lolote, lakini kijana alipofika ikulu na kuviona vitanzi vyake alishangaa na kuuliza

    "kwanini imekuwa hivi"

    Mheshimiwa raisi alitoa macho huku akimuuliza,

    "jana hujapigiwa simu"

    Ilibidi kijana akae kimya kutokana na majibu aliopewa na Mheshimiwa raisi, sasa haijulikani jana alipigiwa simu iliohusu nini mpaka kukubaliana na maneno ya raisi,... Kijana huyo ambae ndio leo tunaanza kumjua kupitia vitanzi hivyo, kwa jina la SALEHE RASHIDY KINGAZI (SAHI)



    "utakuwa na kazi mbili... Ila kazi hizo zitakuwa kama vile unajifunza"

    Aliongea rais huku Salehe au sahi akiwa tayari kwa kuuliza swali kwa raisi,

    "sababu ya kazi mbili ni nini"

    Aliuliza sahi huku akisubiri majibu toka kwa mkuu wa nchi

    "THE DISCATE OF MONEY IS LOST"

    Aliongea raisi kitu kilichomfanya sahi kushtuka sana, mana kifaa hicho ni kifaa maalum kama code ya kuchapishia pesa mpya iliotakiwa kutoka kimepotea,.... Yaani hicho kifaa ndio kina code za pesa mpya ya Tanzania, sasa hio discate inafungwa katika mashine ya kuchapishia pesa, ili itoke pesa ya kitanzania lazima hio discate iwepo,.. Tanzania wanataka kutengeneza noti moja ya shilingi Laki moja, na kila kitu kilishakaa sawa, kilichobaki ni kutangaza tenda katika makampuni ya kuchapisha pesa huko nchi za nje, na wakishakubaliana ndipo wanapewa hio discate ambayo ndio ina muongozo mzima wa pesa hio mpyq... Yaani ukiifunga katika mashine, ndio inatoa mfumo mzima wa laki moja ya Tanzania,.. Kama vile Computer bila Hard Disk ya Windows, basi computer haiwezi kuwaka maisha yako yote, mpaka uweke Hard Disk ya Windows na kama haina Windows utatakiwa kuweka CD ya Windows ili kuweka Windows computer ifanye kazi... Sasa ni sawa na mashine ya kuchapishia pesa.. Na mashine hizi zipo aina mbili, kuna mashine kubwa spesho kwa ajili viwandani kabisa yaani zile zinazopokea tenda za kuchapisha yaani kiwanda kinachojulikana dunia nzima... Afu kuna mashine ndogo, hii ni mashine binafsi, na haziuzwi tu hovyo hovyo na bei yake sio ndogo,.. Hizi mashine ndogo zinakuwa zipo spesho kwa nchi inayotaka kujichapishia wenyewe kutokana na maelewano na kampuni ya IMF, hivyo sio rahisi kuwa nayo mana inauzwa gharama kubwa afu ni mlolongo mpaka kuiweka katika nchi yako..



    Lakini sasa pia kuna matajiri ambao wanaweza kumiliki mashine hizo kupitia njia za kona kona, na wakaweza kuzipata, sasa kupata mashine sio kazi, kazi ni kuwa na hio Discate,.. Ukiwa na discate of money, Tayari wewe ni tajiri wa dunia na hakuna atakae kuweza,.. Sasa discate hio yenye ukubwa wa HARD DRIVE au HARD DISK, kwa wale wataalamu wa computer wanavijua hivi vifaa,.. Sasa hiki kifaa ndicho kilicho potea, na kilikuwa kimehifadhiwa BOT (Bank Of Tanzania)



    "mkuu, unachokiongea ni sahihi kweli"

    "tena hakukuwa na uvamizi wa aina yeyote, inaonekana kuna utaalamu wa uzimaji wa CCTV na aliochukuwa ni mtu anaefahamika na anaejua siri ya shelfu lililowekea Discate hizo"

    "kwahio, hizo discate zimebaki ngapi"

    "discate zilizobakia ni za Elfu kumi,  Elfu Tano, Elfu mbili, Elfu Moja, Na shilingi Mia tano... Hizo ndizo discate zilizobakia, ila hio discate mpya ndio iliopotea, na ni hatari sana mtu binafsi kuingiza pesa hio katika mzunguko, ni hatari sana pale atakapo pata code zake"

    Aliongea mheshimiwa rais, kana kwamba pamoja na upotevu wa discate hio bado kuna ugumu wa kuchapisha pesa, mana code number haikuchukuliwa.. Na code number ipo pale pale kwenye shelfu la kuhifadhia hizo discate, na kila discate imekaa pembeni na code number zake,... Sasa mtu aliochukuwa alichukuwa kwa pupa, kana kwamba akasahau kuchukua code zake, na code hizo zipo kwenye kifaa maalum, ambapo pale unapotoa discate, basi na code number zake zipo kwa chini, na sio za kunakili kichwani bali unachukuwa na kifaa chake chote, mana ni number nyingi sana zapata kama number 100 hivi zilizochanganywa na herufi mfano wa code za Facebook kuna wakati ukiingia Facebook kuna Codes wanazitaka na umewekewa juu ya kisanduku uziandike, sasa kwa hii discate zinafika numbers 100, zilizochanganywa na herufi, hivyo huezi kunakili kwa haraka kama unaiba, na hata wakati wa kupeleka hio discate kule Ujerumani ni lazima upeleke na codes number zote yaani unaikabidhisha kwenye kampuni hio ya uchapishaji wa fedha pamoja na codes zake, na wakimaliza kazi, unarudishiwa discate yako na codes zake,.. Usubiri kupeleka kwa wakati mwingine, na kila nchi ina discate zake na codes zake... Sasa huku BOT kilichobakia ni Codes za discate ya shilingi laki moja, yaani noti moja ya laki, sasa discate ndio ilioibiwa... Na urahisi wa kupata codes ni asilimia 90 kwasababu aliochukuwa anaweza kurudi na kuchukuwa zile codes,.. Mana unapofunga hio discate itakuonyesha kwenye screen ya mashine kuwa unahitajika kuweka codes ili discate hio ianze kazi, na wakati huo matirio ya fedha yapo tayari katika mashine...



    SAMAHANINI SANA WADAU, NIMETOA MAELEZO MENGI SANA LAKINI NI ILI MUELEWE VIZURI KINACHOFATILIWA NA KIKOJE NA KINA KAZI GANI NA KWANINI KINAFATILIWA,.. SIWEZI KUSEMA TU DISCATE WAKATI HUJUI DISCATE HIO INAKAA WAPI NA KAZI YAKE NINI, NITAKUWA SIJAKUTENDEA HAKI YA KUSOMA SIMULIZI HII.... HIVYO TUTAVUMILIANA TU ILI TUSIDANGANYANE SANA,







     





    "kwahio unataka kuniambia codes bado zipo"

    "ndio, mwizi hajaweza kuchukuwa codes, na ni lazima arudi"

    Aliongea rais, huku Waziri wa fedha akiwa ndio anaingia katika kiakao,..

    "shkamoo "

    Sahi Alimsalimia waziri wa fedha huku waziri huyo akivuta kiti na kukaa,... Lakini alipofika pale, ghafla mada ilibadirika, mana katika watu wanaohisiwa vibaya hata yeye yumo anatakiwa kufanyiwa upelelezi hivyo hapaswi kumjua sahi,...

    "Marahaba kijana.. Habari yako"

    "nzuri"

    "habari yako mheshimiwa rais"

    Waziri wa fedha alimsalimia raisi

    "salama tu hali yako"

    "aahh tunamshukuru mungu kwa newma zake, ila huyu ndie yule kijana uliosema anakuja"

    "hapana, huyu ni kijana wangu, wa yule mama yenu wa pili"

    Aliongea raisi, huku akimnyooshea sahi kidole,...

    "aaahhh kumbe una vijana wakubwa sana Mheshimiwa hongera zako"

    "aahhh ndio vijana wetu hawa"

    Waziri alisema kumbe mheshimiwa ana vijana wakubwa sana, hivyo inaonekana kuna mtoto wa raisi mwingine tofauti na huyu aliemtambulisha, na je huyu ni mtoto wa rais kweli au kazuga zuga tu..

    "haya, mimi nilikuwa napitia tu hapa nadhani wacha nielekee ofisini kwangu"

    "sawa kazi njema"

    Aliaga wazi huyo huku tukibakiwa na Waziri mkuu, na makamu wa rais, na sahi, pamoja na mlinzi wa rais,..



    "sasa basi, najua wewe hujamaliza masomo yako, nadhani bado miezi mitatu uweze kumaliza mafunzo yote, sasa tunataka uifanye kazi hii ndani ya mwezi mmoja, tuione discate ikiwa mikononi mwako"

    "sawa, nitaifanya kazi kadri ya uwezo wangu"

    "sasa, ili usitiliwe mashaka, tunakupeleka jeshini, na pale jeshini utakuwa kama mwanafunzi, tafadhali sana naomna usilete ujuaji mana watakushtukia,... Na Sababu ya kukupeleka jeshini yaani military ya kijeshi, ni ili wajue shughuli zako za hapa mjini... Na pia hutoishia jeshini tu, bali nitakupeleka katika kitendo cha usalama siri cha TSS (TANZANIA SECRET SERVICE) kitengo hiki, hakijulikani Tanzania ispokuwa viongozi wakubwa.. Na kitambulisho chake hiki hapa... Nadhani cha jeshi unacho kwa hapa Tanzania.. Hivyo utakuwa na kazi mbili kwa nyakati tofauti tofauti,.. Wiki moja jeshini, wiki moja mjini TSS, serikali imekukadiria bajeti ya Tsh milioni 500 mpaka pale kazi itakapoisha... Na ukishindwa ndani ya huo mwezi mmoja serikali itakuchagulia adhabu ya kukupa.... Wish you a good Luck"

    "ok.. Nimekuelewa mzee, ila napelekwa na nani katika vitengo hivyo"

    "ili usijulikane kuwa umeletwa na raiso, kuna raia wa kawaida tu atakupeleka military ya kijeshi, kama vile mzazi wako.. Na pia kule TSS atakupeleka vilevile kama mzazi wako.. Kikubwa hutakiwi kujulikana umeletwa na kiongozi gani"

    Aliingea raisi huku akiamka na kutaka kuondoka

    "afu nimesahau,.. Jina la misheni utatumia BB yaani (BLACK BOY) utavaa mavazi meusi mwanzo mwisho unapokuwa katika kitengo cha TSS na ukiwa military utavaa nguo za jeshi za kawaida... Lakini wiki ya mjini utavaa nguo nyeusi kuanzia juu mpaka chini.... Alafu hio kitu haruhusiwi kuvua na hutakiwi kujulikana wewe ni nani.. Umenielewa"

    "nimekuelewa mkuu"

    "nitakuwa nakupa misheni kwa kutumia Transmission ulio nayo katika skio... Jina langu la misheni nitatumia GU.... Hivyo utakaposikia neno GU, basi ujue ni mimi... Kama una swali uliza"

    "hapana, sina swali... Ila nilitaka kujua, kuna baadhi ya misheni utakuwa ukinipa, je nikiwa katika wiki ya jeshini itakuwaje na misheni itakuwa ya mjini"

    "tutajua cha kufanya pale litakapotokea swala kama hilo... Ila chunga sana huruhusiwi kuwa na wanawake... Mwanamke ni njia moja wapo ya kuvujisha siri zako... Kuwa makini na hawa watu... Na vitengo vyote, utakwenda kama mwanafunzi... Huku ukijua unachokifanya"

    "Yes Sir"

    Sahi alinyanyuka na kupiga saluti kwa raisi, wakati huo makamu wa rais na waziri mkuu wakitikisa kichwa kuashiria kijana yupo shupavu na makini zaidi..., alipoondoka raisi, kuna kijana alileta begi lililojaa vifaa maalum vya upelelezi.. Kama Rader, Computer ndogo, wireless network, na kuna kifaa kidogo cha satalaiti, bila kusahau miwani inayoweza kuscani mwili wa mtu na kugundua ameficha nini katika mwili wake,....



    Salehe aliondoka Ikulu na gari yake yenye usajili wa nymber za serikali, na gari hilo anaruhusiwa kuwa nalo ili usumbufu wa barabarani usitokee pale anapotakiwa kuwahi mahari fulani,..

    Sahi alifika nyumbani kwake majira ya saa tano za asubuhi, aliweka kila kitu chake,... Kisha akalikagua vizuri lile begi aina ya dranka maalum la kuwekea vifaa vya upelelezi,... Sahi alicheka sana huku akitoa kifaa kimoja kilichokaa mfano wa Hard drive,... Huku akisema

    "huu ndio utajiri unaotafutwa na serikali yangu,... The Discate Of Money,... Nazitaka hizo codes zake... AHahahahahahahah.."



    Sasa cha ajabu na cha kushangaza, kumbe discate of money anayo sahi, au BB,.. Tena anataka na hizo codes zake,... Wakati huo anacheka kwa mbwembwe nyingi sana huku akiiangalia hio Discate ya noti ya shilingi lakini moja,.....

    "How can get the codes?"

    Salehe au BB alijiuliza atazipataje cedes hizo?.... Wakati huo sahi anacheka kwa dharau huku akiiangalia ramani ya Jengo la BOT lilivyo..









    Ama kweli ukijua kula na kipofu, basi utafaidi vingi sana, mana sahi ndie alie kabidhiwa jukumu la kuitafuta discate hio, alafu kumbe yeye mwenyewe ndio anayo katika mikono yake, tena wakati huo akiwa anapiga mahesabu ya kuingia, BANK OF TANZANIA (BOT) Ili kukamilisha codes za hio discate,.. Sahi au BB kwa jina la kazi aliweza kurudisha discate hio katika kisanduku maalumu cha discate hio kisha akakiweka katika dranka la vifaa vyake,...



    Kesho yake asubuhi salehe akiwa na mtu mmoja hivi ambae kwenye uongizi hayupo, yaani ni mwananchi wa kawaida tu, huyo ndie aliekabiziwa jukumu la kumpeleka salehe katika kazi, na kitengo cha kwanza alipelekwa TSS kitendo ambacho kipo mjini kati lakini hakijulikani, hicho ni kitengo cha usalama wa taifa cha siri sana tena kinahusika na mambo mengi hususan upelelezi, na ndio mana salehe kaletwa huku mana kuna wapelelezi wenzake,... Na sio wapelelezi tu bali ni wapiganaji wazuri ila wao wamesomea Tanzania,



    Mzee huyo yupo spesho kama baba wa salehe, na salehe yeye hajui popote anapo pelekwa hata huko TSS hapajui hata kidogo... Gari iliingia katika ghorofa moja safi sana, juu ni makazi ya wao wao wenyewe, lakini kwa chini sasa ndio kuna kila kiti, kwanza gari ikiingia geti linafungwa, afu papo hapo baada ya kulipita geti, mbele kuna kibanda, kama cha sevisi za gereji hivi lakini sivyo,.. Gari ikifika pale, hua panabonyea chini, kwahio makazi ya TSS yapo chini ya ghorofa katika underground, yaani chini ya ardhi ndipo makazi ya TSS yalipo,... Na mlango mkuu ni hio sehemu iliokaaa kama sevisi za magari kumbe ndio mlango mkuu wa kuingilia huko ndani,







     





    Walipofika chini huko, yaani ni sehemu kubwa sana utafikiri ni nje, kumbe ni ndani,.. Hua mtu akishafika huko haulizwi sana kwasababu kama huhusiki huko, basi hata kwenye mlango mkuu pale hufiki, lakini kama umepita mlango mkuu basi unahusika,.... Sasa mzee ndio kipau mbele na hana wasiwasi, kwanza ni mtu mwenye pesa afu kaagizwa na kiongozi wa nchi, hivyo hakuwa na hofu kuingia ndani zaidi,.. Ukipita hapo kwenye maofisini kumejaa makompyuta ya kazi, na wakati huo watu wapo bize kana kwamba kila mtu kuna anchokitafuta au kuna kazi anaifanya, unaweza ukashirikiana na mwenzako lakini kila mmoja ana kazi iliomleta kama vile Salehe, kaletwa na kazi ya kutafuta discate na hapa sio kuwa discate ndio ipo ila awe na kazi ya kujizuia ili hata watu wanaomshtukia kuwa huyo ni nani, wakitafuta information zake wakute ni mwanafunzi wa TSS afu pia ni mwanafunzi wa TMA (TANZANIA MILITARY ACADEMY) Mana atakuwa anafanya kazi katika vitengo viwili kwa nyakati tofauti tofauti,... Lakini kazi hizo hazina maana kwake ispokua yupo kwa ajili ya kuitafuta discate,...

    Mzee huyo alietambulika kwa jina la mzee Rashidy, na hata hilo jina sio lake ni ili tu kujifanya amemleta mtoto wake asomee upelelezi kwahio kitengo hiki kipo kwa ajili ya kukufunza practically jinsi ya kupeleleza,... Na pia hapo hapo kinafanya kazi, yaani unafunzwa huku unafanya kazi mpaka unakuwa afisa mkubwa hapo hapo na haruhusiwi kuacha kazi kirahisi mana ni kitengo kinachoijua nchi kwa undani zaidi... Mzee alionana na ofisa mkuu wa TSS yaani yule General mwenyewe ambae anaagiza tu,... Mzee aliongea mengi sana na General wa TSS, wakati huo mzee anaongea kule ofisini, huku Salehe yeye anazungukia ofisi za watu, na hapo wafanyakazi bado hawajamjua kama atakuwa mwenzao nini, kila akipita kwenye kompyuta anakuta wafanyakazi wanafuatilia information fulani kwa kutumia satalaiti,.. Yaani walikuwa bize sana hata kumuona mgeni hawamuoni,... Salahe aliipenda sana ile bize iliokuepo pale, na hapo hajui mtu hata mmoja,...



    Huku ofisini mzee amemaliza kuongea na General wa TSS, sasa General anauliza huyo kijana yuko wapi, wakati huo sahi ndio kwanza yupo katikati ya maofisi ya watu,..

    Mzee alimpigia sahi simu

    "uko wapi wewe"

    "nakuja mzee"

    Sahi alitoka mbio mpaka ofisini, kwanza kaingia bila hata ya kupiga saluti, sio kwamba hajui ila kaambiwa aende kama mwanafunzi, hivyo ajifanye hajui ili ajue njia nyingi za kufanya kazi...

    "ataweza kazi kweli huyu? Mbona kama kalegea legea hivi"

    Aliongea general wa TSS, huku Salehe akijifanya kukakamaa kama mwanajeshi, lakini General akajua huyu kijana ni bure, hajui lolote...

    Mzee rashidi alimaliza kila kitu na Salahe akawa kapata kazi au shule ya kujifunzi, mana unajifunza kuitumia kompyuta kwa ajili ya upelelezi zaidi, kisha unapelekwa practically kufanya upelelezi wa vitendo,...



    Baada ya kumaliza hapo ikiwa ni mida ya saa sita za mchana,.. Sahi na mzee huyo aliekuwa kama baba yake wakiwa wanakwenda Airport kwa ajili ya kwenda Arusha kwenye chuo cha kijeshi, yaani anapelekwa zile sehemu nyeti za usalama wa taifa,... Walichukuwa ndege ya private kisha haooo, wakaondoka kuelekea TMA na huko ndipo atakapoanza kazi yake,.. Ilipofika saa nane ndege inatua arusha, kijijini munduli, ambako ndiko makao makuu ya jeshi,.. Hivyo katika mikoa yote mkiona kambi ya jeshi hayo ni matawi tu lakini makao makuu yapo arusha,.. Walipofika katika kambi hio au chuo hicho cha kijeshi, walishuka kama watu wakubwa fulani hibi, mana walikuja na private jet,



    "salama afande"

    mzee rashidi alisalimia kwa wakuu wa jeshi aliowakuta katika kambi hio, shamra shamra za mazoezi zilikuwa zikirindima, yaani kila kikosi na mazoezi yao, sahi sio mgeni na hivyo vitu tena kwa yeye anaona ni vitu vyepesi sana, mana ujeshi wake yeye kausomea korea, hivyo ana uwezo mkubwa kuliko mtu yeyote hapo kambini, na yupo kwa kazi maalumu..



    "afande, kuna mgeni anahitaji kukuona"

    "aingie"

    Mkuu wa majeshi Tanzania nzima ndio anamruhu baba yake SALEHE aingie ndani,... Mheshimiwa Nyange akiwa katika kiti chake cha heshima ya ukuu wa jeshi Tanzania nzima,... Sasa sahi kama kawaida yake ya kubaki nyuma, yaani mzee anaingia ofisini yeye kabaki nyuma,.. Saa ngapi asianze kuizunguka hio kambi ya jeshi, palikuwa na vijana wengi sana ni zaidi ya wanafunzi elfu moja ukijumlisha na walimu, wenye vyeo vyao.... Sasa wanajeshi bado hawajamjua sahi kuwa ni nani afu kavalia nguo zkisharobaro hivi, saa ngapi mwanajeshi mmoja hajamtamani sahi,... Yaani ilimradi kumkomoa mana alikuwa akiangalia amgalia mabogi ya magari ambayo ni magari ya kijeshi, sasa sahi alijifanya kuchungulia... Kwanza alishtukia kavutwa kisha kawashwa kofi,

    "umemueka baba yako uko chini ya gari"

    Aliongea mmoja wa makamanda huku makamanda wengine wakizidi kujaa eneo la tukio,.. Sahi kaambiwa awe mpole, ajifanye hajui, sasa kama unavyojua maonevu ya wanajeshi yalivyo... Kabla sahi hajajibu kasukumwa na mtu mwingine,... Papo hapo akaanza kupewa zoezi la kushusha giabox la gari peke yake, kitu ambacho hakiwezekani kushusha giabox la kalandinga la jeshi peke yako, eti kisa alikuwa anachungulia....

    "broo siwezi eti"

    Wakati huo sahi akiongea hayo tayari keshalioga vumbi jinga sana, nguo zake za usharobaro tayari zimekuwa kama nguo za kichaaa.... Sasa walipoona anazidi kukataa, likaletwa galeni la oili chafu, yaani hawana utani na hata sahi anajua yaani hata ni kuchomwa mwanajeshi akiamua anakuchoma kweli,... Lile dumu lenye oili lote lilimwagikia yeye, uso mzima kwa mweusi,.... Sasa huku mzee keshamaliza kuongea wanageuka nyuma hawamuoni kijana husika,... Nyange alijua tu tayari kimeshanuka huko nje, mana anawajua makamanda wake walivyo, yaani wakiona raia hapa kambini kama haeleweki wanampa adhabu,... Kweli walipotoka wanaona kuna mahari kuna watu wengi sana, yaani wanajeshi wamekusanyika sehemu moja wakimchezea mtu mmoja yaani wana hamu ya kutesa ile mbaya,...

    "waamuru basi vijana wako wamuache"

    Aliongea mzee huyo ili sahi aachwe, lakini Nyange hakutaka kufanya hivyo

    "kijana wako kaja kujifunza mafunzo ya kijeshi, na kisheria alitakiwa kuanzia JKT, lakini kwa kutumia shotkati zenu, umemleta huku.. Sasa tulia akaribishwe"

    "lakini imetosha afande, hebu ona alivyo kama chizi"

    Mzee rashidi anajua sahi sio mtu wa mchezo ila inabidi afiche siri,... Sasa mkuu wa majeshi mheshimiwa General Nyange, alipofika alimuuliza sahi,.. Na Wakati huo sahi hata kuona vizuri haoni kutokana na ile oili chafu aliomwagiwa, na hata sura yake haionekani vizuri kwasababu ya hio hio oili

    "huo ndio ukamanda kijana.... Karibu kambini kwetu"

    Aliongea general huyo, huku akitaka kuruhusu waendelee kumpa mazoezi

    "afande naombeni mnisamehe sirudii tena"

    Sasa ghafla general akasita kuondoka baada ya maneno hayo kutoka katika kinywa cha sahi,..

    "ebu rudia tena hio sauti yako"

    General alimuuliza sahi kwa mara nyingine,..

    "nisamehe afande"

    General alipatwa na kichaa,...

    "we mzee, huyu ni mtoto wako"

    Nyange alimuuliza mzee Rashidy feki,

    "ndio kwani vipi"

    "hapana.... Nyie Hebu muosheni huyu kijana nimuone"

    Heeeee kumbe general anamjua sahi, lakini sasa kumbe sio General tu, bali kuna vijana wengine wa kijeshi wanaijua sauti hio,....

    "muosheni nimuone,... Fanyeni haraka"







    Ilikuwa ni siku sahi anapelekwa jeshini na baba yake, ila tunajua kiwa sio baba yake mzazi bali ni mtu aliochaguliwa kwa ajili ya kazi hio, mana akipelekwa na mtu ambaye ni mtumishi wa serikali, watakuwa na maswali mengi juu ya mwanafunzi hiyo, hivyo wamemtumia raia ili wajue ni mtu wa kawaida sana, kumbe ndio jembe la tanzania tena linalotegemewa mno,.... Sahi alijikuta akizunguka zunguka katika kambi za watu akiwa bado ni mgeni, na kama unavyojua sifa za mwanajeshi zilivyo, walimshambulia kwa kumteda hawakujali alivyo vaa, Lakini mkuu wa majeshi mr Nyange, alikuja katika eneo la tukio na kuwataka wamuache mara moja tena wamuoshe ili amuone vizuri, kauli hio ilikuja baada ya kusikia sauti ya kijana huyo kuomba msamaha juu ya kosa la kuchungulia kwenye makalandinga ya kijeshi,....



    Pale pale wanajeshi walitii amri ya mkuu wao, walimchukuwa sahi na kumpeleka katika maji, nguo za jeshi zililetwa na hatimaye kuvalishwa, mana kakubaliwa kuingia jeshini, hivyo ana ruksa ya kuvaa nguo hizo pasina shaka, na alipewa kwasababu hakuwa na nguo zingine mana ndio kafika hata maandalizi vizuri hajafanya, hapo kama kaja kitambulishwa tu,...



    Sasa mr Nyange alikuwa kakaa katika mti fulani uliopo katika eneo hilo la kijeshi, mti uliotoa kivuli kizuuri sana kilichomvutia mr nyange, wakati huo sahi anatolewa ndani na kuletwa kwa mr Nyange,... Na wakati huo hata mzee rashidi wa muda alikuwepo,....

    Sahi alipendezwa sana na mavazi ya kijeshi aliokuwa kayavaa katika mwili wake, na hicho pia ni kitendo kilichozifi kumfanya nyange aamini huyo ni mtoto wake, na wakati huo sahi yupo mbali ndio anakuja kwa mr Nyange,...

    Yaani jinsi anavyotembea hizo hatua zake, ni mtoto wake mtupu, na wake nae alikuwa mwanajeshi sasa hatujui kwanini anamhisi sahi,... Sahi alifika kwa mkuu wa majeshi na kutoa saluti ile ya kujifanya hawezi, lakini ndio mwenyewe katika fani hio,.. Mr Nyange aliipokea saluti lakini machozi yalikuwa yakimtoka mfululizo,

    "mzee mwenzangu kuna nini tena"

    Mzee rashidi alimuuliza mr nyange kuwa kuna nini, mbona machozi kumtoka kwa kumuona kijana huyo

    "we acha tu... Kweli nimeamini duniani kuna watu wawili wawili,.. Yqani huyu kijana wako, anafanana na mtoto wangu kila kitu kasoro hio sura tu, lakini mwendo, sauti, hata hio saluti alivyopiga pia ni kama yeye jamani... Basi nimeamini sio mwanangu"

    "kwani mwanao ilikuwaje"

    "amefariki dunia, ila kijana wako kanikumbusha mbali sana"

    "pole sana mzee mwenzangu"



    Basi, hali hio iliishia hapo na hata sahi hakuweza kurudi nyumbani tena, mzee rashidi aliondoka zake na kumwacha sahi kambini hapo,.. Chumba chake alipatiwa kilicho cha nguo za kawaida lakini nazo ni za jeshi jeshi... Yaani ukiwa kambini kuvaa nguo za kiraia haitakiwi, hivyo nguo zao za kubadilisha zimekaa staili ya jeshi jeshi,... Sahi aliingia katika hicho chumba lakini kabla ya yote alijifungia ndani na kuanza kukikagua hakina kamera yeyote,... Sasa kumbe hata hio saa aliovaa sahi, ina miale ya kugundua kamera zilipo, na licha ya kazi hio pia saa hio ina rada maalum kwa ajili ya kazi yake, na licha ya kazi hio pia saa hio ina kamera ndani yake, na pia ina Voice recorder,.. Yaani kuna mahali ukibonyeza inakuja sistimu unayotaka, kisha unairudisha katika hali ya kawaida, hivyo hata mtu akiiona hawezi jua kama saa hio ina kazi kama hio, na pia ina kazi ya kupiga simu bila kutumia simu ya mkononi,... Hizo ni saa spesho kwa ajili ya wapelelezi kama hawa, na huku jeshini hakuna aliekuja kumpeleleza bali ni sehemu ya kujiweka ili akigundulika na hao wamiliki wa discate, wajue ni mwanafunzi wa kijeshi au wa TSS, lakini hakuja kulipeleleza jeshi na wala hana wazo hilo....

    Sahi alikagua chumba kizima na kugundua hakukuwa na kamera zozote zile, na yeye kama mpelelezi spesho ni wajibu wake kujua hilo, isije kuweka kazi yake matatani







     





    Tukija huku TSS jijini Dar es Salaam, ambako kuna makazi ya usalama wa taifa yaani wale wa siri zaidi,.. Mana kuna wale wa kawaida wanaojulikana na wananchi, lakini sasa kuna hao SECRET SERVICE hao ni zaidi ya hao wanaojulikana na wananchi,... Sasa hio TSS haijulikani mana ni usalama au jeshi la siri,.. Katika kitengo hicho yupo General mkuu wa kitengo hicho lakini kuna kijana mwingine mdogo mdogo hivi aitwaye JOSEPH JOHN POMBE MAGUFULI kwa jina hili tu ni dhahiri kuwa ni mtoto wa rais, ila ana nyota au cheo kikubwa katika kitengo cha TSS na ni kijana mdogo sana, nae ni mmoja wa wapelelezi walio hali ya juu zaidi,..

    General alimwita Joseph katika ofisi yake, yaani baada ya General anaefata kwa cheo ni Joseph ambae kwa jina la misheni wanamuita JJ (Joseph John)

    "habari yako"

    "salama mkuu, hali yako"

    Alijibu Joseph huku akipiga saluti kwa mkuu wake,...

    "aahhh salama,.. Kuna kijana kaja kujifunza zaidi katika kitengo chetu, ivi ulimkagua"

    "mmmhj nadhani sikuwepo wakati akiwasili hapa, ila naweza kumuona hata sasa hivi"

    "no, kwa sasa kaenda jeshini, mana anatakiwa kuchukiwa mafunzo ya TMA na TSS, hivyo atasoma wiki moja kule kisha atasoma wiki moja huku"

    "ok, kwahio atafika hapa tena baada ya wiki"

    "ndio"

    "sawa mkuu, nitamkagua pindi atakapokuja"

    "ni vizuri, ila unaweza kwenda kumwona kele Arusha"

    "hapana mkuu, Kiukweli toka nilipokuwa jeshini na rafiki yangu mtoto wa General Nyange na kupoteza maisha katika mazoezi, Kiukweli sitamani kabisa hata kuiona kambi ya jeshi"

    "inaonekana uliumia sana kwa hilo"

    "ndio, mana ni mpaka nimeachana na mafunzo ya jeshi baada ya rafiki yangu kipenzi kupoteza maisha... Yaani sitamani kuwa mwanajeshi"

    Aliongea Joseph huku akikumbuka tukio la zamani rafiki yake alipokuwa mazoezi na kulipuka na bomu wakati wakiwa mazoezi, kwa kawaida mabomu ya mazoezi hua hayaui lakini haikujulikana ni nani alileta bomu la kweli ndani ya jeshi,...



    Kesho yake asubuhi sana kama saa 11 hivi, tukiwa katika kambi ya jeshi kila mmoja alichukuwa begi lenye uzani wa kilo gramu 50 na kuliweka mgongoni, huku wakipiga kwata msituni katika sehemu zao za kufanyia mazoezi,... Wanafunzi walikuwa ni wengi sana huku walimu wao wakiwa kwa nyuma na mbele... Ndani ya wanafunzi kama kawaida wanawake hawakosekani kabisa, na kama unavyojua udhaifu wa wanawake,... Katika hali ya kukimbia hua wanashindwa kubeba lile begi lenye kilo gramu 50 na kukimbia nayo, hivyo wanabaki kuanguka,...

    "angalia chalii mgeni anavyoteseka kule"

    Aliongea mwanafunzi mmoja akimuongelea sahi au BB, sahi ni zaidi ya hao walimu wenyewe, lakini kaonywa aende kama mwanafunzi hivyo ajifanye hajui kitu, hivyo sahi alikuwa akianguka kila mara ili kuuonyesha uma kiwa kweli alikuwa hajui kitu

    "alijua kuna baga huku"

    "ahahahahahaha.... Anashindwa hata na baadhi ya wanawake"

    Kuna baadhi ya wanawake walikuwa wakijikaza lakini kuna wengine waliokuwa wakishindwa na mazoezi hayo, hivyo huambulia adhabu kali yoka kwa walimu wao,...



    Walifanya zoezi mpaka ilifika wakati wa saa mbili za asubuhi, na wakati huo tayari walishabadilisha mazoezi sasa ni kukroo chini huku wakiwa wameshika silaha ambazo hazikuwa na risasi,.. Na wakati huo mabegi yenye uzani yapo migongoni mwao..

    "mambo"

    Alikuwa ni dada mmoja hivi mrembo sana aliomsalimia sahi,

    Sahi hakuitika kwasababu ya kuchoka kwa mazoezi, na sio kuwa kachoka kweli laa bali yupo kikazi zaidi, anatekeleza maagizo alio pewa na wakuu wake,

    "haya mafunzo hayahitaji hasira kaka angu, utaumia"

    Aliongea yule dada huku wakiendelea kusota chinj, mana wapo wengi sana na kelele zilikuwepo, hivyo wawili wakiongea kwa mwingine kusikia ni ngumu, sahi hakumjibu yule dada chochiukile, waliendelea na mazoezi lakini dada wa watu alikuwa tu kwa ajili ya kufahamiana na kijana huyo, ila sahi kwa kujifanya kuchoka hakuweza kumwitikia,...

    Sasa walipokuwa wakiendelea kusota kimazoezi, ghafla sahi aliona baadhi ya wanafunzi kama saba hivi, wakiwa wanachepuka katika njia nyingine tena walimu wao ndio waliokuwa wakiwaamuru kufanya hivyo,.. Wakati huo hakukuwa na mtu alio ona zaidi ya wale wa mbele pale, hivyo watu wa nyuma au hata katikati hawawezi kuona kutokana na majani makubwa kutawala msitu,..

    "Samahani dada angu, eti wale wanapelekwa wapi"

    Sahi aliona bira avunje ukimya, japo hakuambiwa aipeleleze TMA yeye kaja ili kupata nguzo ya kazi yake, sasa alishangaa kuona baadhi ya wanafunzi wanapitishwa njia za pembeni na mwalimu wao

    "nilikusalimia ukanichunia, sasa waniuliza nini"

    "Samahani, nimechoka eti si unajua nimekuja jana tu"

    "hata salamu pia"

    "ok sorry kwa hilo"

    Ilibidi aombe radhi kwa kutomwitikia salamu yake,... Lakini sahi kila akipiga jicho, anaona wanazidi kwenda tu

    "sikiliza we mkaka, hapa jeshini fuata ulichokifuata, vinginevyo utapelekwa kua mpishi wa wenzako"

    "una maana gani dada angu"

    Aliuliza sahi huku wakizidi kupitwa na wenzao...

    "salehe na mwajuma, naomba msimame"

    Sahi na mwaju walionekana na mwalimu wao kuwa hawakuwa wakikroo bali walikuwa wakiongea huku wakiwa wamelala kama wanakroo kumbe laa,....

    "umeona sasa, mpaka tumeonewa, we makaka vipi... Haya sasa tutapewa adhabu kubwa hapa"

    Aliongea mwaju huku akitia hofu juu ya adhabu watakayo pewa na kamanda wao,

    "mumekuja kufanya mazoezi au mumekuja kuongea"

    Aliongea kamanda baada ya kuwatoa nje ya mstari,...

    "Samahani afande, mimi ni mgeni hivyo nilikuwa nahisi maumivu katika tumbo, baada ya kuburuzika, sasa ndio huyu dada akawa ananiambia nijitahidi, ndipo ukatuona"

    Aliongea sahi huku akishika tumbo kama vile anaumwa kweli,

    "sasa kwa adhabu yenu, mnatakiwa mrudi mwisho, yaani wale wa kwanzo kutoka mwisho, wawe wa pili kutoka mwisho.. Tena muende kwa kuruka ruka"

    Duuuu mwaju alishika kichwa mana hio mwisho yenyewe ilipo ni mbali sana afu uende kwa kuruka ruka kichura,... Hawakuweza kupingana na agizo la kamanda... Walitii japo kwa maumivu makali sana,..



    Sasa sahi alpofika eneo la tukio, pale walipokuwa wanachepuliwa wale wanafunzi wengine,... Sahi alitamani sana kupita kwenye hako kamchepuko, mana yeye kama mpelelezi ana haki ya kujua kinachoendelea huku kwenye njia hii tofauti na wengine,...

    "unataka ufanye nini"

    Aliongea mwaju, huku sahi akijiandaa kuruka,..

    Wakati huo mqaju anauliza yeye yupo mbali nae, mana wapo mwisho kabisa,..

    "nataka nikajue wameenda kufanya nini wale, usikute wenzetu wanapewa mafunzo mazuri zaidi"

    Sahi alisema hivyo, ili kumzuga mwaju asijue kama yeye ni mpelelezi,

    "wewe mkaka, umekuja jana tu... Na hicho Kiherehere chako kitakuponza... Mazoezi ni haya haya hakuna mazoezi mengine"

    Lakink wakati huo salehe wala hakutaka kumsikiliza mwaju, yaani kama kazi yake inavyomruhusu kufanya.... Sasa ile sahi anajiandaa kuruka ili kutua pembeni alishtukia kukamatwa mguu wake, na kujikuta anarudishwa katika line...

    "lazima tukuchunguze kwa undani zaidi... Na utasema wewe ni nani hapa TMA"

    Ilikuwa ni sauti ya mtu mwingine kabisa ambae hata hamjui, tena alivalia mavazi ya kiuwalimu, kana kwamba huyo ndio yule mwalimu aliowachepusha wanafunzi saba... Sasa sahi kaja na moto ambao hakutakiwa kuwa nao,.. Yaani kaanza kubainika akiwa na siku ya pili jeshini







    Sahi alikuwa hatamani hata kidogo kuona jambo linampita hivi hivi, yaani haitakiwi limpite,.. Sasa swala la wanafunzi wenzake kuchepuliwa katika mazoezi, hili lilimshangaza sana salehe, tena akiwa mwanajeshi aliofuzu mafunzo kule korea, na elimu yake ya upelelezi alioisomea kule korea, hawezi ona kitu kinakwenda tofauti akakinyamazia tu, sasa katika harakati za kutaka kujua kwanini wanafunzi kadhaa wamepitishwa huku, aligundulika na mwalimu wake,...

    "lazima tukuchunguze kwa undani zaidi.... Na utasema Wewe ni nani hapa TMA"

    aliongea kamanda huyo huku sahi akiwa hana hata wasiwasi juu ya swala hilo,....

    "afande, mimi nilijua wanafunzi wageni wanapita huku, hivyo nikaona ngoja niende bila kuambiwa"

    "afu wewe mbona unajifanya unajua kuongea sana, kwanini"

    "hapana afande, najitetea tu ili usije nihisi vibaya"

    "ujinga ujinga hautaki, nitakupa adhabu sasa hivi, mhuni wewe... Endelea na mazoezi, na ole wako tukio lijirudie tena"

    Aliongea kamanda huku sahi akiendelea na mazoezi kama kawaida



    Baada ya masaa kadhaa, wakiwa kambini wakati huo kila mmoja keshaoga na kutulia,... Unajua kuna JWTZ NA KUNA JKT... Kwahio hapa ni JWTZ.... Ukitoka JKT ndio uje JWTZ, ila kama kwenu kunasoma vizuri Basi unakuja moja kwa moja JWTZ, ila ni zamani lakini sio kwa serikali hii ya majipu...



    Sasa wakiwa kambini muda wa kupata chakula cha mchana, upande wa wanaume vyao na upande wa wanawake vyao,... Mwaju akiwa yupo ofisini kwa kamanda aliokuwa zamu ya mafunzo ya leo, aliulizwa kuhusu kijana huyo, na wakati huo mr Nyange alikuwepo akisikiliza swala hilo, kumbe jambo lile halikuishia pale mazoezini, bali kamanda kalileta kwa mkuu wa majeshi ili ajue kuna kijana anaruka ruka sana,...

    "we mwaju, unamjua yule kijana"

    Mwaju aliulizwa na kamanda tita, huku mr Nyange mkuu wa majeshi, akiwa anasikiliza tu,...

    "hapana afande, sifahamu na pale nilikuwa namuuliza tu jina lake, mana sauti yake inafanana sana na mtoto General"

    Aliongea mwaju na kumfanya General Nyange anyanyue mdomo

    "Enheeee, kumbe hata wewe umejua eee,... Kiukweli tita yule kijana tofauti yake ni sura pekee, yaani kila kitu ni mtoto wangu... Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi"

    Aliongea general Nyange kwa masikitiko makubwa sana,...

    "sasa, sisi tunakupa kazi,.. Mfuatilie yule kijana.. Fanya kila liwezekanalo ukiwa kama mwanamke, zijue taarifa zake, yeye ni nani, na kaja kufanya nini"

    Aliongea kamanda tita huku general akimuuliza tita kuwa

    "kwani wewe umejuaje kama sio wa kawaida"

    "General, unajua hata wewe unaweza kumjua mwanajeshi kwa kumuangalia jinsi alivyosimama... Na mimi nimejua pale alipotaka kiruka, nikajua tu huyu sio mtu wa kawaida,.. Alikuwa anaruka kiprofesheno sana, yaani sikutegemea.. Na sikutaka ajue kama swala hilo nimelijua"

    "ohoooo, basi binti, fanya kazi yako, na, mimi kama mkuu wa majeshi nitakupata nafasi muda wowote wa kuwa nae, lakini hakikisha unaleta taarifa zake hapa ndani"

    "sawa afande, nitaifanya kazi vizuri"

    Mwaju ana mwaka wa pili sasa toka aje hapa jeshini hivyo, ana kiwango kikubwa cha uelewa katika mafunzo, mana kabakiza miaka kadhaa tu kumaliza mafunzo na kurudi majumbani kwa ajili ya kupangiwa maeneo ya kazi... Sasa Mwaju anajikuta anaaza kazi nyingine ya upelelezi ambayo hajawahi hata kuiota katika ndoto zake,.



    Wakati huo sahi alikuwa anacheza gemu kwenye saa yake,.. Kumbe sio saa ni simu tosha, kwani kuna mahari ukibofya, inafunguka na kuwa kama simu ndogo ya tachi... Na ukibofya tena inarudi kujikunja kama saa, yaani ni hatari sana pale saa hii itakapogundulika hapa jeshini,.. Ila uzuri ni kwamba saa hio inaporudi katika hali ya saa, hua inakuwa na muonekano wa kawaida sana, yaani hata uichunguze vipi huezi jua.. Ila sasa saa hio inapofika sehemu yenye kamera inapiga alarm na kuwasha miale inayo muelekeza kamera ilipo, sasa ni hatari kwa mtu mwingine kuwa nayo...







     





    Basi sahi alikuwa akicheka na gemu, unajua uzuri ni kwamba jeshini hakuletwa kwa ajili ya upelelezi, bali jeshini kaja tu kama mwanafunzi wa kawaida ili kujiwekea nguzo katika kazi yake, usiku ulipofika sahi akiwa kalala zake, kama kawaida mwaju alipewa nafasi kubwa sana ya kutoka wakati wowote ule na hata wanajeshi waliopo lindo siku hio wanajua kuwa mwaju kapewa ruksa kutoka upande wa wanawake kwenda kwa wanaume, mana anakijua chumba cha sahi,.. Sasa ikiwa ni mida ya saa nane hivi za usiku, Sahi aliamka ili kwenda kupata haja ndogo, milango ni mingi sasa Sahi alitokea mlango wa nyuma na mwaju anakuja kwa mlango wa mbele, mana hana wasiwasi na hilo.. Lakini sasa sahi akiwa chooni, alishangaa kuona vitochi tochi vikimulika kwa mbaali sana kule nje ya uzio wa jeshi,...

    "wanafunzi gani wanajifunza usiku, tena nje ya jeshi?"

    Sahi alijiuliza na wakati huo mwaju ndio anafanikiwa kuingia katika chumba cha sahi,... Sasa sahi kuangalia vizuri, alishangaa geti la pembeni kuwa wazi, yaani kuna geti kuu, alafu kuna vile vigeti vya pembeni ambavyo vimezungushiwa waya ila hata karandinga la jeshi linapita bila wasiwasi,... Sasa mbaya zaidi vitochi hivyo vilikuwa vikielekea huku jeshini,.. Salehe hakuweza kulinyamazia jambo hilo, alitoka chooni kisha akaangalia walinzi wa kijeshi jinsi walivyo kaa... Alianza kukroo na ukuta, na uzuri wa sehemu za jeshi sio rahisi kuwekwa kamera,.. Huaga hakuna.. Sasa mwaju huku ndani alishangaa kukuta hakuna mtu wala nini, akatoka nje lakini pia hakumwona, alirudi katika kile chumba na kuanza kusachi,... Nia yake haikuwa kusachi, alikuwa aje kuanza kumteka hata kimapenzi usiku huu ili ajue kinachoendelea kwake, lakini kwa bahati mbaya hajamkuta mhusika, na hilo nalo ni tatizo la kutoka nje ya kambi usiku,.. Sasa uzio wa jeshi umezungushiwa waya tu, yaani zile wayameshi, sasa salehe alipoona walinzi wamekaa hovyo, aliruka juu, na kutua nje ya uzio wa jeshi,.. Hii ni hatari sana kwake, kwasababu mwanafunzi yeyote haruhusiwi kutoka nje ya jeshi bila ruhusa,....



    Sasa alitembea kwa utaratibu mkubwa sana, mpaka akafika eneo la tukio,.. Sasa kumbe zile tochi sio kuwa zilikuwa zikitembea, bali ni watu walikuwa wanapikia silaha, kutoka kwenye gari ya jeshi kwenda kwenye gari la kawaida aina ya fuso,.. Sahi alitega mahali na kuangalia mwanzo mwisho mpaka wakamaliza kupakia silaha,... Sasa cha ajabu na cha kushangaza, alionekana mkuu wa majeshi mr Nyange akiwa katika eneo hilo, sahi alishangaa mno,... Mara katokea mwarabu mmoja aliokuwa kashika briefcase ya pesa na kumkabidhi mr Nyange,... Baada ya kukabiziwa pesa hizo,.. Gari la jeshi lilisukumwa mpaka kambini, yaani sio kuwashwa, bali linasukumwa kimya kimya ili watu wasishtuke

    "usiondoke sasa hivi, mpaka tufike kambini ndipo nikuruhu uondoke"

    Aliongea mr nyange huku makamanda wengine wakianza kulisukuma gari hilo,.. Sasa kwakuwa ni mstuni na kiza kimetanda haswa hata vile vitochi vimeshazimwa hivyo wote wakajaa kwenye gari kusubiri ruksa ya mkuu wa majeshi aseme waondoke...



    Sasa kijana hajataka gari hio iondoke, alikroo mpaka chini ya gari,.. Kisha alitoa kisu kidogo sana, kisha akaanza kuchokonoa kufuli la Tools Box (box la supana).. Kweli alifanikiwa na kuingia chini ya gari, kitu cha kwanza kufungua ni propela, wakati huo majangili wapo kwenye ganasikiliza Music kwa njia ya hedifoni, hivyo hata kukuru kukuru hawawezi kuisikia....



    Ghafla simu ya muarabu inaita...

    "hello mr nyange"

    "yes mnaweza kuondoka sasa"

    Aliongea mr nyange, huku mwarabu akikubali na kusema

    "ok, see you next month"

    "ok, wish you a good luck"

    "ok... "

    Mwarabu aliwasha gari ikawaka, na hapo wapo tayari kwa kuondoka...



    Sasa huku chumbani, kumbe sahi aliacha simu, na huezi amini simu yake ilionewa na mwaju, na kama unavyojua simu ya sahi ilivyo beba siri nzito ambazo anawasiliana na Mheshimiwa rais, sasa mwaju keshaipata simu hio,....

    "yes, nimefanikiwa kupata simu,.. Sasa wacha nimpelekee General Nyange aichunguze"

    Lakini sasa cha ajabu na cha kushangaza, mwaju aliitupa simu kitandani baada ya kuona picha juu ya screen sever, mwaju alishangaa huku akiishika tena hio simu na kuangalia hio picha kwa makini...

    "huyu kijana, ana uhusiano gani na huyu mtu, mbona picha yake ipo hapa"

    Mwaju Alijiuliza swali hilo huku akisema tena kuwa

    "lazima General nyage mjue huyu kijana"







     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog