Search This Blog

Thursday 24 November 2022

MKE JEURI - 2

 

     

     

     

    Chombezo : Mke Jeuri

    Sehemu Ya Pili (2)

     



    Sasa tukija huku kwa akina zai (zaituni na zainabu).. Leo mama kamueka chini mtoto wake zaituni na kumpa ukweli juu ya sheby,..

    "mwanangu zai,.. Yule kijana ana nia njema na wewe, na yupo tayari kuishi na wewe hata hivyo ulivyo"

    Aliongea mama zai huku akimshika mtoto wake

    "lakini mama, si unajua sheria za ndoa zilivyo, sasa nitawezaje kumtimizia mume wangu sheria kama hizo"

    "ni kweli zai, lakini hata yeye kakubali mwenyewe kuwa atajua ni jinsi gani atafanya"

    "kasema ananichukuwa lini"

    "kesho Jumapili mapemaa anakuja kukuchukuwa"

    "lakini mama... Nitawezaje kuishi na mwanaume na wakati hatujafunga ndoa mama"

    "najua hilo mwanangu, lakini dada yako zainabu keshajua hivyo ukiendelea kukaa hapa, atazidi kukudhuru, ni bora ukakae na huyo kijana huku mkiendelea kusubiri ndoa yenu"

    "mamaaaa, vijana wa sasa hivi... Sidhani kama ataniacha mama"

    "zaituni mwanangu... Huyo kijana keshakula kiapo mbele yangu kuwa, Hatokaa akuguse mpaka afunge ndoa na wewe"

    "kweli mama"

    "kweli, labda abadirike tu lakini kala kiapo juu yako mbele yangu namuona na kumsikia"

    Zaituni alijiskia raha sana mana hizi bahati za kuolewa alijua zimekwisha toka alipoupata upofu, lakini kumbe bado zinaendelea kuja,...

    "afu mama, huyo kijana anafanya kazi gani"

    "ni muuza viazi vya chipsi, anatembeza kwa mkokoteni"

    "sawa mama, mwambie aje anichukuwe nimeshakubali kiwa mke wake"

    "tena kijana mwenyewe hensamu huyo, yaani kakosa pesa, lakini kazuri"

    "mamaaaa usiniambie hivyo mama, nitalia bure, mana natamani kumuona mume wangu"

    Aliongea hivyo zaituni huku machozi yakimtoka kwa ukosefu wa macho.. Wakati huo akiwa kavaa miwani yake nyeusi na kifimbo chake kwa pembeni huku mama akimbembeleza mtoto wake ili kumpooza machungu.



    Sasa tukija huku kwa akina rose na mary, sheby akiwa ndani kwao akiwafundisha wadada hao jinsi ya kufanya kazi katika kampuni yao..

    Lakini ukumbuke mary kaenda toilet, afu huku sebuleni rose anapokea meseji kutoka kwa mary

    "jamani dada rose, anza basi ile kazi niliokuomba dada yangu"

    Rose aliposoma huo ujumbe alitabasamu sana huku akitikisa kichwa na kujisemea kimoyomoyo kuwa

    "mary mdogo wangu, rafiki yangu kipenzi, jua hata mimi ni binadamu kama wewe, na nimeumbiwa kupenda kama wewe,.. Ulichokipenda hata mimi nakipenda,.. Kukufanyia kazi yako itakuwa ngumu, mana hata mimi nampenda huyu mtoto wa kiume... Utanisamehe sana"

    Rose alijisemea maneno hayo katika moyo wake, kisha taaratibu alianza kazi ya kumsogelea kijana sheby... Sasa ona marafiki wawili wanavyogeukana kisa mapenzi... Sasa rose kabla hajaanza kufanya kazi yake.. Alishika simu na kumrudishia SMS kuwa...

    "chelewa chelewa huko huko nikufanyie mambo huku"

    Mary kuisoma ile sms alifurahi mno, hivyo akatoka chooni na kuingia bafuni ili aoge muda usogee, wakati rose anamtongozea kwa sheby...

    "vipi mbona unaniangalia hivyo"

    Aliongea sheby baada ya kuona vitendo vya rose vimezidi kipimo kuliko maneno, Mana rose alikuwa akimuangalia boss wake kwa jicho la huba,..

    "no boss,.. Sema una sura ya kutazamika kila mara.. Samahani boss kama nimekuudhi"

    Maneno yenyewe yalikuwa yakitokea puani kabisa,.. Maskini ya mungu ustaarabu wa kijana wetu utamuisha hivi punde tu, mana rose alikuwa kila dakika hafanyi makosa ya vitendo, yaani dakika moja inaisha kwa faida



    Sasa huku bafuni maskini mary anaoga kwa kujua kule rose anamseidia kumtongozea mana mary yeye ni muoga wa kumtongoza mwanaume kwa vitendo,...

    Maskini mary kapakalia sabuni yake vizuri lakini kila akijishika kifua chake anahisi ni sheby ndio anafanya hivyo, yaani kila anapojishika anahisi anashikwa na sheby...

    Sasa Wakati huo huku kwa sheby akiwa kuna kitu anaandika kwenye laptop yake, ili kumwonyesha rose jinsi inavyotakiwa kuandikwa,.. Sasa kamaliza kuandika akamgeukia rose huku akisema

    "sasa unaona hapa jinsi ya ku..... "

    Laaaaaa Haulaaaaaa, Sheby alistop kuongea baada ya kumwona Rose akiwa katika hali ya utofauti na mwanzo...







    Kijana sheby haamini kwa kuiona hali ya rose jinsi ilivyokuwa,... Mtoto wa watu alikuwa akitoa darasa ili wasichana hao wapate kazi katika kampuni yao, lakini kumbe wasichana hao wana hisia tofauti na kijana huyo, japokuwa ni kweli wana shida na kazi lakini mapenzi pia yana nafasi yake na hayahitaji bughuza hata kidogo, hivyo wadada walijikuta tu wanampenda kijana huyo bila kutegemea,... Na mwanaume ni mwanaume tu hata iweje...

    "sasa unaona hapa jinsi ya ku..... "

    Laaaaaa Haulaaaaaa, Sheby alistop kuongea baada ya kumwona Rose akiwa katika hali ya utofauti na mwanzo, Huezi amini mwanadada rose alikibinua kifua chake, yaani aliyatoa nje kidogo matiti yake walio madogo, yaliomfanya kijana sheby kuacha kuongea alichokuwa akiongea, kwani msisimko aliupata kama mtoto wa kiume,...

    Sasa rose alijishtukia na kujihisi kiwa kazidisha mbwembwe nyingi sana za mitego juu ya kijana huyo,.. Hivyo rose aliyarudisha matiti yake, kitendo kilichomfanya sheby kutikisa kichwa kama mtu aliolamba limau,... Pale pale sheby alifunga laptop yake na kuaga kuwa anaondoka,

    "heeeeee boss kwani lisaa limeisha"

    Aliuliza rose baada ya kumuona boss wake anakusanya vitu na kutaka kuondoka

    "aahhh najihisi kuchoka sana hivyo naomba niondoke kwa leo"

    Sheby aliongea hivyo huku akipiga hatua ya kuondoka

    "sasa mbona humuagi mary"

    "aahh utaniagia tu"

    Aliongea kijana sheby kisha akafungua mlango wa gari yake na kuondoka zake..

    Wakati huo mary yupo bafuni na hisia zake za kuhisi kama vile anaoga na sheby, na wakati huo alikuwa anajua kuwa rose anamseidia kumtongozea, mana mary anashindwa kufanya hivyo japo ana uzuri wa kuweza kumpagawisha mwanaume,.. Akiwa bafuni ghafla mlango uligongwa

    "wewe toka sasa heee"

    Aliongea rose huku akisukuma mlango kana kwamba alijua yupo bafuni, Mary alivaa nguo haraka haraka, mana alishajisuuza sema alikuwa anawaza kama vile yupo na kijana sheby, kumbe alikuwa peke yake bafuni,..

    "weeee dada rose boss umemuacha na nani kule ndani"

    Aliongea mary bila kujua kiwa boss wao alishaondoka muda tu

    "heeee kama ni nyumbani kwao keshafika"

    "we rose acha utani eti"

    "Aaaaahhhhhhh.... Kaondoka muda tu"

    "ok vipi, kimeeleweka"

    Mary aliuliza kuwa tayari sheby kakubali au?

    "waapi, boy mwenyewe mgumuu kama nini yani"

    Aliongea rose huku akiwa anacheka cheka

    "kwani ulimuambiaje"

    "mi nilimuambia mary ana maongezi na wewe, ili aniulize ni maongezi gani hayo nami nianze kuropoka... Lakini kakaa kimya yeye na kompyuta tuuu"

    "jamani dada rooose"

    "afu we mary siku hizi unaniita dada ili nikutongozee yule boy si ndio eee"

    "lakini ww si mkubwa kwangu wewe"

    "hata kama, lakini naona unanizeesha tuuu ebu tuachane na hayo"

    "jamani rose, kwahio hutaki tena kuniseidia"

    "sio kuwa staki... Ila boy ni mgumu"

    "jaribu hata kamwisho tuuu"

    "ok poa nitakujaribia tena siku nyingine"

    Rose aliongea hivyo huku moyoni mwake akisema kuwa

    "heee utasubiri sana nikuseidie,.. Kwaio mie ndio umeniona malaya wa kuwatongozea watu... Ukizubaa atakuwa shem wako bibie"

    Aliongea hivyo lakini ni katika moyo wake, huku mary alikuwa na furaha baada ya kuambiwa kuwa ataseidiwa kwa mara nyingine tena, bila kujuwa kuwa rose yeye amesha mgeuka rafiki yake kipenzi....



    Kesho yake ikiwa ni mida ya saa saba hivi mchana kweupeee,...

    Akiwa yupo nyumbani kwa akina zai, mama zai alishangaa sana kijana huyo kuja katika hali ya kimaskini ingali kwao ni tajiri na siri ya kijana huyo kuwa ni tajiri anaijua mama zai pamoja na zainabu, Sasa sheby kaja na bajaji hapo nyumbani na wakati huo mabegi ya zaituni yalikuwa zikitolewa na kupakiwa katika bajaji hio, mwisho na zaituni alipakia, wakati huo zainabu alikuwa hayupo maeneo ya nyumbani hivyo hatojua ndugu yake kaenda wapi,.. Sheby alimpatia mama huyo kiasi kidogo cha pesa, kisha bajaji ikaondoka, mama zaituni hakutaka kuipoteza tena bahati ya mtoto wake kutaka kuolewa, alikubali kwa moyo wote mtoto wake akaishi kwa mume na wala hakutaka kuuliza ni wapi mana mwanaume anajiweza kimaisha, lakini alishangaa sana kumuona sheby kaja kama maskini, yaani hata msukuma mkokoteni ana afadhali ya mavazi kuliko alivyovaa kijana sheby.. Ila hatujui sheby ana shida gani juu ya hilo, na hatujui nia yake ni ipi ya kuwa katika madhingira hayo ya kimaskini ingali ni mtoto wa kitajiri tena tajiri wa uhakika....







     





    Kwakuwa kijana kijana huyo alikuwa bado anaishi na wazazi wake hivyo hawezi kumpeleka zaituni nyumbani kwao na badala yake anampeleka katika kile chumba ambacho alipangisha kule uswahilini kabisa yani, tena nyumba yenyewe ni nyumba ya miti mabati yenyewe hayako vizuri, ukuta hauko vizuri lakini kaamua kumleta huku huku mtoto wa watu, na uwezo wa kupangisha hata jumba la kufahati anao, yaani hata akitaka kujenga nyimba sasa hivi anao,.. Lakini sijui ni kwanini kamleta mtoto wa watu katika nyumba hio tena ingali ni kipofu haoni..



    "karibu ndani... Mi bado naishi maisha magumu sana"

    Aliongea kijana huyo huku akimuingiza zaituni ndani ya chumba hicho,.. Zumuni lake haswa ni nini mana mtoto wa watu ni kipofu huyu kama ni kuona haoni sasa kwanini kamleta huku...

    Zaituni aliingia ndani ya nyumba hio, yaani hio nyumba ni mara kumi ya nyumbani kwao huyu zaituni kuliko hapo,.. Lakini sasa kijana sheby alipangisha chumba kikiwa hakina viti, lakini sasa hivi kina vitu lakini vimechakaa, makochi yamechakaa, kitanda chenyewe kidogo afu kigodoro chembamba mno.. Kila kitu kipo ndoo za maji masafuria yaliotumika, hata sijui kayapatia wapi, sheby alitoka nje mpaka kwa fundi cherehani ambae ni jirani yake aitwaye shadya,...

    "Samahani dada eti bafu ni lipi hapa"

    "lipo pale"

    Mungu wangu hilo bafu ni la matofali lakini juu halikuwa na paa la bati wala nini yaani kilikuwa wazi kabisaa

    "sasa shadi, kama nilivyokwambia, nitajitahidi kila siku nikulipe lakini naomba ukipika, umletee mchumba wangu, na pia uwe karibu nae sana"

    "we usijali kikubwa ni kwamba sio mbishi, mana vipofu wengi huwa ni wabishi sana"

    "No, No,  huyo sio mbishi."

    "sawa basi, lakini sasa kwenye swala la kuoga itakuwaje na kwenda msalani"

    "aahhhh kwenye swala la kuoga... Nadhani nitalifanya mimi, ila uwani unaweza kumpeleka na ukamuekea maji karibu na pia uhakikishe kakaa ndio uondoke, vingine atafanya mwenyewe"

    "mmmhhhhh huu mtahani huu lakini we kaka"

    "naomba niasidie dada yangu,.. Nitajitahidi kuuza viazi nikupatie hata elfu 10 kila siku ya mungu, na pia viazi nitawapatia mpike chakula shadi"

    "ok sawa basi.. Kwa sasa nataka nipike,.. Kwanini usimuogeshe kabisa ndio uondoke"

    "sawa wacha nifanye hivyo basi"

    Sheby alitoka hapo na kuingia ndani, ambako ndipo alipomuacha zaituni

    "Samahani, naweza kwenda kukuogesha"

    Alimuuliza kwanza kabla hajamwamsha katika kochi,...

    "hhhmmmmmm"

    Aliguna zaituni huku akiwa kama anataka afu hataki

    "lakini, mbona kama nitakupa kazi hapa.... Kwanini usingeniacha nyumbani"

    "usijali mke wangu... Kuna dada atakuwa akikuseidia mambo madogo madogo ila kukuogesha kasema hawezi"

    "hhhhhmmm sawa... Lakini we si mwanaume rijali jamani"

    "kwani mi nani wako"

    "mume wangu mtarajiwa"

    "kwanini unionee aibu"

    "sawa nimekubali"

    "afu, mimi siwezi kukugusa... Nimekula kiapo, mpaka utakapokuwa mke wangu rasmi"

    "hhhhmmmm nyie vijana nyie waongo kama nini"

    "usijali, sio wote ni waongo"

    Basi sheby alibandika maji haraka haraka yakapata moto, aliyapoza kisha akaenda nae bafuni,.. Kitimu timu ni pale kwenye kumvua nguo.... Maskini kijana sheby alikuwa akiteseka tu kwa maumivu, mana mtoto zaituni alikuwa ni msichana aliopewa shepu ya kuvutia,.. Ukiangalia figa lake, yaani hata chupi yake ilikuwa haimuenei vizuri kutokana na shepu yake ilivyokuwa nzuri, yaani umbo namba nane lakini sio kibwa, kifua kidogo kidogo kimechongoka, sheby alijikuta anamkagua mtoto wa watu, huku zaituni anajua anapozewa maji kumbe sheby kamtolea macho kweli kweli... Zoezi la kumuogesha lilianza vizuri na likaisha vizuri... Walipofika ndani sheby alifungua begi lingine ili kuchukuwa mafuta ya kupaka.. Sheby hakupenda mchumba wake aendelee kupaka mafuta ya baby care,.. Lakini alimpaka tu hivyo hivyo ila aliona hio ni mara ya mwisho kumpaka mafuta hayo.....  Sasa ilipofikia kwenye kupaka mafuta sheby alikuwa akiumia sana mana zaituni bado alikuwa mtupu, Shwby alijikuta anavua nguo za chini ili asiumize zakaria yake mana ilisimama mpaka ikawa inauma kwa udogo wa eneo, hivyo kavua nguo za chini ili asiumie.. Lakini sasa kumbe hata zaituni alikuwa akizipata hisia vile alivyokuwa akipakwa mafuta na na sheby, tena sheby alikuwa akifanya makusudi pale alipokuwa akifikia maeneo ya kifua,...

    "ivi we hujanitamani kweli"

    Zaituni alipata wasiwasi juu ya sheby, ina maana na uzuri aliokuwa nao na shepu yake yote, kweli huyo kijana hata hatetemeki,.. Zaituni alijihisi ana mapungufu ya kimwili, hivyo ndio mana kaamua kuuliza

    "kwanini nisikutamani, sema navumilia tu"

    "muongo wewe"

    "kweli vile"

    "yuko wapi huyo jamaa hebu nimshike"

    Aliongea zaitini huku akipapasa katika mwili wa sheby, ili aishike zakaria ya sheby,...

    "Yeuuuuuuuwiiiiii, basi baba vaa nguo mume wangu"

    Zaituni alifanikiwa kuishika zakaria ya sheby na kugundua kweli sheby alikuwa vizuri kiuwanaume... Mana alihisi ana mapungufu kumbe anamuumiza tu...

    Sasa zaituni alijikuta anamuonea sheby huruma, mana nanii ilisimama sana,...

    "sheby mume wangu.."

    Aliita zaituni huku sheby yupo bize kupaka mafuta katika mapaja ya zai,

    "sema mke wangu"

    "kwanini umekula kiapo kikubwa hivyo lakini"

    Aliongea zai huku akitamani kumruhusu sheby

    "nilikula kiapo ili kuleta uwaminifu juu yako"

    "Hapana, mimi sitaki tena.... naomba uvunje kiapo chako, siwezi kukuona unateseka kiasi hicho mume wangu... Kama ni bikra sina, sasa kwanini unilie kiapo kikubwa kiasi hicho???"

    Laaaaaa Haulaaaaaa sheby haamini maneno ya zaituni yaliokuwa yakimtoka kama kuku wa kutaga vile

    "lakini zaituni mke wangu... "

    Sheby kabla hajamaliza kuongea zaituni alidakia juu kwa juuu

    "lakini nini mume wangu??.... Mimi nilibakwa na wahuni, hivyo nilipoteza Bikira yangu, toka siku hio na sasa ni mwaka na zaidi umeisha... Kwa sasa sina Bikira tena,.. Kwanini ule kiapo choote hicho kisichokuwa na mbele wa nyuma"

    "usijali zaituni... Kuwa mpole basi"

    Sheby alikuwa anajifanya anakaza sana lakini ana hamu ile mbaya

    "afu mkononi umeshika nini?"

    Aliuliza zaituni baada ya kushika mkono wa sheby na kuukuta na nguo

    "si nimeshika chupi jamani zai wangu"

    "hebu weka hio chupi pembeni achana nayo,.. Kwanza umeifua wala staki kuivaa mbichi na sina nyingine"





    Zaituni ni msichana anejiheshim sana na hapendelei kufanya ngono kabla ya kuolewa, na hata hapo pia sio kuwa kataka, sema mwili wake umemsukuma kutaka mapenzi kwasababu kijana sheby alikuwa akimpaka mafuta kama vile alikuwa anamshika shika, hivyo hali hio ilimfanya zaituni kuamkwa na mashetani wa mapenzi,.. Kijana huyo alikula kiapo juu ya kumgusa zai mpaka pale atakapokuwa mke wake rasmi,

    "si nimeshika chupi jamani zai wangu"

    "hebu weka hio chupi pembeni achana nayo,.. Kwanza umeifua wala staki kuivaa mbichi na sina nyingine"

    Aliongea zai huku akimvuta kijana huyo kana kwamba hisia za kimapenzi zilimzidi...

    "hapana, siwezi kufanya hivyo"

    Sheby aliongea hivyo huku akiweka ile nguo mahali ili iweze kukauka... Kijana sheby alitoka na kwenda katika duka linalouza nguo za kike,

    "heeeee huyu mkaka ana akili kweli, anawezaje kuingia sehemu kama hii"

    Waliongea wahudumu wa kike ambao wao hawamfahamu,..

    Sheby alinyooka moja kwa moja kwenye nguo za ndani,..

    "huyu kaka vipi, mbona anaangalia nguo za kike"

    Waliongea kwasababu kijana huyo alikuwa katika mazingira ya kimaskini sana,..

    "tukuseidie nini kwenye duka la nguo za kike"

    "hizi nguo mnauzaje"

    "dazeni ni elfu 70 ila kwa reja reja moja ni elfu 10"

    "ok ebu nitolee hii dazeni"

    Wahudumu walishangaa kuona mtu mwenye hali ya kimaskini anawezaje kununua nguo za ndani za kike zenye gharama ya elfu 70,.. Walitoa nguo hizo kisha akachanganyiwa rangi tofauti huku akiziangalia kwa kumpima kiuno cha zai... Alipomaliza hapo aliingia upande mwingine wa nguo hizo hizo za ndani ila hizo ni zile ndefu ndefu kidogo tofauti na chupi, sijui wanaitaje wenyewe ila kwa macho yake aliona zinamfaa zaituni... Alipomaliza hapo aliingia upande mwingine wa ngu za kawaida tu, vitenge, magauni, sketi, na nguo za Kiislamu,... Kiufupi alifungasha sana tena nguo za gharama kubwa kweli

    "mmmhhhh huyu kaka anatania au ananunua"

    Aliongea mhudumu mmoja kana kwamba sheby asingeweza kuzilipia hizo kutokana na muonekano wake wa hali ya kimaskini sana..

    "sasa zote ni kiasi gani"

    Kwanza kabla hawajajibu Wadada hao waliangua kicheko kana kwamba walikuwa wakimuangalia tu na wakati hawezi kulipia...

    "unajua tunafurahai sana unampenda huyo mtu wako, na sisi tulitaka tu kufrai mana hutoweza kuzilipia.. Ila tutakupa nguo mbili za ndani umpelekee tu"

    Kijana sheby hakukasirika wala nini mana anajua hawajui atandalo

    "niambie ni kiasi gani basi nilipe niondoke"

    "ni laki nne"

    "boooooooooooo...... Mi nikajua imefika milioni kumbe bado ni laki nne tu"

    "sasa si utoe kama hio laki nne ndogo"

    Kijana sheby kumbe kavaa suruali mbili, hio ya ndani ndio yenye pesa.. Alitoa pochi yake amabayo hata haikuwa ikifunga kwa wingi wa pesa, wahudumu walibaki mdomo wazi huku wakitoa macho, inawezekanaje msukuma mkokoteni kama huyo awe na pesa za kutunisha pochi lake...

    "ooohhhh nikitoa hizi nitakosa pesa ya mfukoni,.. Ngoja niyoe hapa ATM sasa hivi"

    Yaani kwa mshangao hata kujibu walishindwa,.. Sheby alienda ATM na kutoa kiasi cha laki sita kisha akawapa laki tano badala ya laki nne,.

    "hio laki mtakunywa soda"

    Yaani mpaka sheby anaondoka wadada hawaamini kile kilichotokea eneo hilo... Sheby alichukiwa tax na kuondoka zake

    "ivi yule kaka, ana maana kuwa katika hali kama ile"

    "kiukweli ule msemo uliosema kuwa usimdharau usiemjua...ona sasa tulikuwa tunamuona chizi chizi tu kumbe ni mtu na pesa zake"



    Wakati huo huku kijana sheby anafikishwa na tax mbali na pale alipopanga mana watu wasije wakashangaa mpangaji kaletwa na tax,.. Alibebana na begi la nguo mpaka ndani, wakati huo shadya alikuwa akiangalia tu mafuko yaliokuwa yanaingia... Alipofika tu ndani alifungua begi ambalo lilikuwa na zile nguo za ndani, kisha akachagua rangi moja alioipenda yeye

    "ulienda wapi jamani"

    Aliuliza zaituni huku akiwa kajifunika shuka na hapo alikuwa hana kitu chochote mana hata kama kungelikuwa na nguo angewezaje kuziona na wakati ni kipofu, hivyo alichoweza ni kujifunika na shuka tu,

    "nilienda kukununulia nguo nyingine"

    Basi sheby alimvalisha mke wake mtarajiwa nguo hio ambayo ilimkaa vizuri sana... Saa ngapi sheby hajamtamani mana aleji yake ni nguo pale inapokuwa mwilini,.. Lakini alipiga moyo konde na kujizuia,..







     Zaituni alivalishwa nguo mpya mpya

    "lakini hela umepata wapi mara hii"

    "aahhhh hela nimekopa mahari, nitalipa kidogo kidogo kutokana na biashara yangu ya viazi"

    "angalia bwana mikopo sio mizuri eti"

    Ghafla simu ya sheby iliita, tena kalikuwa kasimu kadogo kabisa yani katecno, kucheki jina alikuwa ni baba yake

    "haloo mzee"

    "wewe upo wapi mbona ofisini haupo"

    "nakuja sasa hivi mzee"

    "fanya haraka afu ile safari ya india ni kesho ila tutakwenda wote"

    Sheby kuskia hivyo alifurahi lakini ghafla alinuna, kwasababu wanaenda na mzee wake india..

    "sawa mzee"

    "ndio, hebu njoo ofisini tuandae documents zake"

    "sawa mzee nakuja sasa hivi"

    Simu ilikata kisha zaituni akauliza

    "huyo ni baba mkwe"

    "hapana, ni boss wangu anasema gari la viazi limeshakuja hivyo niwahi nikachukuwe mzigo nianze kutembeza kwa mkokoteni"

    "wahi basi jamani"

    Aliongea zaituni kana kwamba anampenda sana mwanaume mchapa kazi

    Hajakaa vizuri mara shadya kaja na chakula,...

    "kaka chakula hiki hapa"

    "ooohhh sawa basi nyie endeleeni kula mimi nikachukuwe mzigo"

    "sawa wacha nile nae basi"

    Kiukweli kazi aliopewa shadya ya kuishi na kipofu ni ngumu sana kwa upande wake lakini anaifanya kwa moyo wake wote,...



    Sasa huku mjini katika hoteli moja hivi, kumbe kijana sheby kapangisha chumba kwenye hoteli hio ya kitajiri, yaani hoteli yenye hadhi yake ya kitajiri lakini,... Tunamuona sheby anatoka akiwa msafiii, tayari keshavaa nguo zake vizuri sasa anachukuwa gari yake na kurudi ofisini,...



    Sasa tukija huku kwa akina mary wakiwa wapo saluni wasichana watatu, akiwemo huyo rafiki yao aitwaye mwana, mana nasikia wakimwita mwana lakini hatujui kirefu chake,... Na huyo mwana alikuwa ni mtoto wa tajiri kama ilivyo kwa sheby, na ni mtoto wa pekee kwenye familia yao, bonge la toto umbo la hali ya juu, sura ya kutabasamu...

    "dada rose naomba leo usiniangushe mwenzio"

    Aliongea mary huku wakiwa wanaendelea kusukwa, mana saluni hio ilikuwa ni saluni ya mwana, hivyo walikuwa wakibadirisha nywele kila baada ya siku mbili mana hawalipiii..

    "heeeee siku hizi mary unamuita rose dada"

    Aliongea mwana huku akimwangalia mary, na hata mwana pia ni mkubwa sana kwa mary, mana mary hakosi miaka kama 22 hivi, na rose ana mia 25, mwana ana miaka kama 28 hivi, hivyo mwana ni mkubwa kwao ila wanapendana sana na hakuna mtu naemdharau mwenzie...

    "we acha tu shost, hata mimi nashangaa toka juzi"

    "heeeeeeee haya kulikoni"

    "mwenzangu Weeeeee, kuna kiboy kadata nacho ila mwenzio muoga huyo, sasa ananisukumia mimi tu nimtongozee"

    "mmmhhh mseidie tu kama inawezekana"

    "asijali"

    "kwaio ndio mana kakuita dada.. Hahahahahahahahaha mary anachekesha kweli kweli"

    "unajua nini dada mwana.... Mi nashangaa ghafla tu kaingia moyoni mwangu afu naona aibu kujipendekeza, na nikisema nisubiri mpaka anitongoze mwenyewe, mmhhhh itachukuwa muda au nisimpate kabisa"

    "kila kitu ni taratibu tu Mary, kuwa mpole na mapenzi, we bado mdogo"

    Aliongea mwana huku wakicheka sana,..



    Sasa tukija huku ofisini kwa akina sheby akiwa yupo na baba yake

    "kwahio kesho ndio safari mzee"

    "ndio, hivyo jiandae tuweze kwenda"

    "sawa"

    Lakini kitendo cha mzee kutaka waende wote, sheby hajakipenda kabisa, yaani hataki mana nia yake aende na zaituni...



    Ilipofika mida ya jioni sheby akiwa anatoka kwa akina mary, lakini alikuwa akiwasiliana na watu dulani wasiojulikana, kumbe sheby hakuwa mzuri kwa baba yake...

    "sikiliza gidi,.. Mshua bado hajarudi homu, sasa nataka tumvizie sehemu gulani, lakini hakikisha hadhuriki"

    "sheby usijali, lazima tufanye hivyo kwasababu yako"

    Maskini mida ilizidi kwenda mzee rashidi asijui hili wala lile kumbe mtoto wake mwenyewe anamfanyia kitu kibaya.....

    Ikiwa ni mida ya saa mbili kasoro usiku mzee huyo alikutana mawe njiani, hivyo hakuweza kupita ikabidi ashuke kujua kulikoni, na yeye alijua ni bijana wanataka pesa,.. Mzee rashidi hakuwa mtu wa mkono mfupi, yeye anatoaga pesa tu... Lakini ile anashuka kwenye gari alikutana na ngumi iliompiga shingoni na kudondoka chini,...

    "gidi vipi mi nimekwambja asidhurike bwana"

    Aliongea sheby baada ya kuona baba yake kanyamaza pale chini, wakati huo hata gidi alikuwa na wasiwasi mana nia yake ni kumfanya akae chini ili wamteke na kumfungia mahari, lakini cha ajabu kadondoka chini na kutulia kimya...

    "gidi umefanya nini sasa"

    "samahani sheby... Tumuwahishe hospitali"

    Sheby shida yake ni kwenda india peke yake na sii kwenda na mtu, lakini njia alioitumia imegeuka kuwa kilio kwao,..

    Mzee alifikishwa hospitalini mida ya saa tatu na nusu usiku,.. Machela zilikuwa zikipishana hospitali hapo, manesi walikuwa bize sana,...

    "dokta, dokta naomba umpime baba yangu"

    "subiri kwanza tumtundikie dripu"

    "sawa fanya hivyo basi"

    "kwani kafanya nini"

    "aagmhhhh kadondoka ghafla tu"

    Alidanganya kijana sheby

    Baada ya muda vipimo vilifanyika lakini dokta alikuja huku akiwa na huzuni juu ya vipimo vya baba yake

    "nione ofisini kijana"

    Aliongea dokta huyo huku sheby akimfuata kwa kukimbia sana, furaha imegeuka kuwa karaha, utani na ujinga wa kijana sheby umekwenda kuwa mbaya kwa mzazi wake huyo

    "kwanza pole sana kijana, mana inaonekana ni jinsi gani unampenda baba yako"

    Aliongea hivyo dokta huyo huku sheby akitaka kujua vipimo vya baba yake

    "dokta, tafadhali sana achana na maneno mengi... Mi nataka kujua baba yangu yupo hai"

    Ghafla dokta anatoa leso mfukoni, sheby akajua baaasi mambo yamekwisha, mana mpaka mtu kupewa leso basi unatakiwa ulie kisha ufute machozi...







    Sheby alilaani sana kitendo hicho alichomfanyia baba yake mzazi,... Na yote hayo ni kwasababu ya safari ya kwenda india ili aweze kwenda na zaituni mana kule kuna wataalam wa maswala ya macho, haswa haswa vipofu na kila kitu, na kama ataenda na baba yake basi nafasi ya kwenda na zai haitokuwepo mana baba lazima alete maneno ya hapa na pale,

    Wakati huo kijana sheby akiwa karibu na baba yake Dokta alikuja na kumtoa ili amfanyie vipimo mzee rashidi..

    Sheby akiwa yupo hapo nje ghafla anamwona dokta anatoka katika wodi aliolazwa baba yake

    "nione ofisini kijana"

    Aliongea hivyo dokta huku akiingia ndani, kijana sheby yupo nyuma ya dokta kujua hali ya baba yake,..

    Walifika ofisini hapo kwa dokta, lakini dokta alikuwa akianza na maelezo meengi sana yaliomfanya sheby kukasirika sana

    "dokta, tafadhali sana achana na maneno mengi... Mi nataka kujua baba yangu yupo hai"

    Aliongea sheby huku dokta akitoa leso katika koti lake,..

    Sheby kuona ile leso akajua anapewa yeye, kumbe dokta alikuwa anajifuta jasho lake ila hakuwa akimpa sheby..

    "usiwe na wasiwasi kijana baba yako ni mzima, wala hana alipodhurika"

    "dokta acha utani"

    "baba yako tayari keshaaka ila achwe kwanza apumzike"

    "naomba nikamwone mzee wangu"

    "nimekwambia kapumzika"

    Aliongea dokta, na hapo sheby akashusha pumzi kubwa sana kuashiria mwili wake umekuwa huru kwa tatizo la baba yake...

    "sasa dokta... Tafadhali sana, naomba..... Naomba umwambie haruhusiwi kutoka ndani ya siku tatu"

    "kivipi sasa, na wakati utatakiwa kuonfoka na mzee wako"

    "sikiliza dokta..."

    Sheby alitoa waleti na kumpa dokta kitu kama laki mbili hivi

    "fanya hivyo.. We mwambie kutokana na afya yako kuwa sio nzuri haruhusiwi kutoka hapa hospitalini"

    "sawa, hakuna shida.. Tena naandika na statement kabisaa"

    Baada ya lisaa limoja mzee wake sheby aliamka na alikuwa yupo vizuri tu hakuwa na tatizo,..

    Dokta huyo alikuwa karibu na mgonjwa

    "mzee hutakiwi kwenda popote, hali yako sio nzuri kiafya, hivyo utalazwa"

    "Whaaat, mbona mi najihisi nipo sawa"

    "ndio, ila kwa vipimo vyetu sisi madakatari tumegundua umepigwa sehemu mbaya sana na imeumia ndani kwa ndani"

    "eeeh mungu wangu wee, kijana wangu yupo wapi"

    "yupo nje mzee"

    "niitie mara moja"

    Sheby aliharakisha kufika kwa mzee wake,

    "baba? Vipi hali baba angu"

    "aahhhh mwanangu we acha tu, kumbe nimeumia ndani kwa ndani"

    "pole mzee,.. Pole sana, lakini kwani cha moto hukuwa nacho mzee"

    "aahh mimi nilijua tu ni bijana wanataka pesa hivyo nilishuka niwape chochote ili watoe mawe barabarani"

    "aaahhh pole sana mzee wangu"

    Sheby alikuwa anakazia sana, na yote hayo sababu ni yeye,

    "sasa kuhusu ile safari, nadhani sintoweza kwa mujibu wa madaktari"

    "haaaaaaa mzee sasa itakuwaje, na pesa ndefu kama tutaufikisha dubai salama... Mana ulikuwa uende congo lakini kwa sasa unakwenda dubai, ni pesa nyingi sana ni zaidi ya bilioni 5 mzee"

    "ni kweli, lakini sina maana ya kuziacha... Kifupi ni kwamba we jiandae uende, na mi najua documents zote unazo na tumeziandaa wenyewe hivyo kesho naomba upande ndege uondoke"

    "mzee, nilitamani twende wote mzee wangu"

    Sheby aliongea hivyo lakini moyoni mwake alikuwa na furaha ya hali ya juu mno, tena anasema ndio vizuri kabisa na ndivyo alivyotaka kijana huyo...

    "fanya hivyo, hakikisha mzigo unafika dubai, na usaini mkataba wa bilioni 5.7"

    "sawa mzee nitafanya hivyo"

    Sheby alifurahi sana kuskia hivyo..







     





    Usiku huo huo kijana sheby alikwenda kubadili nguo zake zile za kimaskini na kwenda kule kwa zaituni, uswahili sana huko..

    Lakini kwanza aliingia kwa shadya

    "asalam aleykh shadi"

    "waaleykh msalaam hali yako"

    "swalaama tu sjui weye"

    "aahhh kwa uwezo wa alah subuhanahu wataalah tupo salama kabisa"

    Sheby alikuja kwa shadi kumwomba kitu kimoja

    "sasa shadi, kesho kuna safari nataka kwenda, lakini sasa bado nahitaji msaada wako"

    Shwby wakati huo kavaa zile nguo zake za uswazi,

    "kitu gani, mbona kama ni kuishi na mchumba wako naishi nae vizuri tu au kuna kingine"

    "No, hakuna, ila nataka twende india"

    Shadi alicheka kuskia sheby anataka kwenda India,

    "ivi ulijua india ipo soko kuu kwenda kuchukuwa viazi"

    "nipo siriasi kweli"

    "wewe hizo hela za kuendea india umetoa wapi"

    "nimekopa..."

    Aliongea hivyo

    "ivi sheby ngoja nikuulize, ina maana benk siku hizi wanakopesha watu kama nyie"

    "ndio.. Haaaaa tena sasa hivi kwa taarifa yako kuna benki ya masikini na benki ya matajiri,.. Sasa nimekopeshwa na masikini wenzangu"

    "hio benki gani ambayo hata kuskia sijaisikia"

    "imeanza juzi tu kipindi cha huyu raisi wetu mpya huyu nani huyuuu aahh nimemsahau kidogo lakini ni benki ya juzi tu na inawahu mafukara na masikini wote nchini"

    "kwahio sheby, hata mimi naweza kukopa huko"

    "ndio ila sema wewe hujajiunga na uwanachama wetu"

    "mmhhhhhhh kumbe kuna kujiunga tena"

    "ndio"

    "ok sasa huko india unaenda kufanya nini"

    "nampeleka bibie kufanyiwa matibabu"

    "waaacha weeeeeee"

    "naomba ujiandae twende... Afu uje huku umuandae mwenzio ila usimwambie tunakwenda wapi sawa"

    "sawa, kwani hulali hapa"

    "hapana sintolala hapa... Ila nitakuja asubuhi mida ya saa mbili asubuhi"

    "sawa"



    Kesho yake mida ya saa moja hivi tunamuona kijana sheby kavaa vizuri sana na kuingia katika ile hoteli yake ya kubadili nguo,.. Alivaa nguo za kawaida kama vile ana safari, na wakati huo kwao alitoka akiwa smarti sana, lakini kaupunguza ule usmati wake, kavaa nguo za kawaida ila sio zile za kuuzia chipsi...

    Alipomaliza hapo alichukuwa tax mpaka uswahilini kwa baby wake,...

    "waaaaooo umependaza"

    Aliongea shadi baada ya kumwona sheby kavaalia, kavaa vibaya vibaya lakini shadi kamwona kama kapendeza...

    "ni nani huyo aliopendeza"

    Zaituni aliuliza huku akitamani hata kumuona mtu aliopendaza

    "ni mpenzi wangu"

    "aaahhhh hahahahaha hongera yako"

    Kitendo kile sheby alijiskia huruma sana, yaani mpenzi ni wake lakini kwakuwa haoni hata kuibiwa anaweza

    "wala usijali baby wangu.. Ni mimi sheby"

    "jamani shadi, kwanini unanifanyia hivyo, au kisa sioni jamani"

    Hata shadi roho ilimuuma na wakati alikuwa akifanya utani,

    "nisamehe sana zai, ilikuwa ni utani tuuu"

    "najua.. Wala usijali shadi"

    "sasa jamani twendeni"

    Aliongea sheby huku akibeba mabegi yao na kuyaingiza katika gari..



    Sasa tukija huku hospitalini ambako ndiko alipolazwa baba yake na sheby,

    "mzee mbona we ni mzima tu wa afya"

    Alikuwa ni dokta mwingine tofauti na yule alioongea na kijana sheby, sasa dokta huyu ndio kampima mzee rashidi na kugundua kuwa alikuwa ni mzima wa afya,

    "mbona kuna dokta kuniambia nimeumia ndani kwa ndani"

    "hapana mzee wangu, upo vizuri kiafya na unaweza hata kufanya shughuli zako"

    Mzee rashidi bula kuchelewa anaamka kitandani na kuchukuwa simu yake, namba ya kwanza kupiga ilikuwa ni nanmba ya sheby....

    Wakati huo namba ya sheby inaita kucheki jina anakuta ni baba yake

    "huyu mzee ana nini tena mungu wangu weeeee"

    Aliongea kijana sheby huku akitaka kuipokea simu hio... Hakutaka kuichunia, aliipokea na kuongea kwa wasiwasi mkubwa

    "haloo mzee, kuna nini tena"

    "subiri hapo hapo nakuja twende, nimepewa ruksa na dokta mkuu,.. Hivyo kuliko nibaki, ni bora twende wote"





    Sheby akiwa na furaha ya kwenda india peke yake, huku akianza kuwaandaa akina zaituni na shadi kwa ajili ya safari, na sababu ya kusafiri na shadi ni ili kwenda kutoa msaada mdogo mdogo kwa zai, pale atakapokuwa hospitali, hivyo ndio mana mpaka shadya kaombwa aende nae,...

    Wakati kijana huyo anapanga begi la nguo katika gari, ghafla simu yake ikaita, kuangalia jina alikuwa ni baba yake mzazi... Aliipokea na kumuuliza

    "haloo mzee, kuna nini tena"

    "subiri hapo hapo nakuja twende, nimepewa ruksa na dokta mkuu,.. Hivyo kuliko nibaki, ni bora twende wote"

    Sheby alishangaa nani kampa ruksa mzee wake, na hapo ndio kwanzaa hata Airport hawajafika, na akitangulizana na baba yake itabidi zai na shadi wabaki,...

    "sasa mzee, mbona mi nimeshaondoka na ndege ya saa 12,.. Yaani nipo mbali mno"

    "aaahhhhhh shit, kwanini uwahi kiasi hicho"

    "mambo ya kazi mzee, lazima ubembeleze kazi"

    "shit.... Aaahhhh"

    Simu ilikata, sasa sheby bila kuchelewa alipaki vitu haraka haraka katika gari,...

    Nusu saa mbele wapo Airport,.. Maskini shadi hajawahi hata kufika Airport, yaani licha ya kupanda ndege, bali hata kufika Airport hajawahi... Zaituni yeye ndio kwanza hata hajui hapo tupo wapi,.. Sheby bila kuchelewa alifanya taratibu zote za usafiri mana yeye ni mzoefu kiasi flani mana sio mara ya kwanza kusafiri kwa ndege,... Baada ya muda mfupi walikamilisha kila kitu,.. Mpaka hapo zaituni hajui yupo wapi, ila anajua kuwa tunasafiri lakini hajui ni usafiri gani wanaoutumia kwa wakati huo,....

    Shadya yeye ndio aliokuwa akiona kila kitu,.. Lakini katuliaaa, kama maji ya mtungi vile



    Tukija huku ofisini kwa akina sheby, na leo ndio siku ya kuanza kazi wale akina mary na rose, mana tayari walishafundishwa na kijana sheby wameiva vizuri ila wanaingia kazini pasina mwenyeji wao ambae ni sheby,... Mapokezi iliwapokea na kuwaonyesha vitengo vyao mana kazi walishapata wiki iliopita sema wakadanganyiwa na sheby kiwa walipata msiba, hivyo waende msibani kwanza misha warudi kuendelea na kazi,.. Lakini haikuwa msiba kweli, bali ilikuwa ni ujanja ujanja wa kijana sheby ili awafundishe kazi, hivyo mpaka sasa wadada hao wameshajua kazi na leo ndio siku ya kuanza kazi,

    "karibuni"

    Alikuwa ni Secretary ndie aliewakaribisha katika ofisi zao wanazotakiwa kufanyia kazi.. Secretary aliwapeleka mpaka kwa boss mkubwa ambae ni baba yake na kijana sheby

    "boss? hawa ni wale wasichana wa juzi"

    "ooohhh sawa sawa kabisa,.... Habari zenu"

    "salama boss shkamoo"

    "marahaba hamjambo"

    "hatujambo boss"

    "ok... Poleni sana na msiba"

    "tumeshapoa boss"

    Akina rose na mary walikuwa na heshima mno kwa baba yake na sheby, mana mzee huyo ni mkali sana katika kazi zake...

    "aaahhhh amina unaweza kuwapeleka katika ofisi zao,.... Na chumba ni kimoja ila chumba hicho kina patision (kimegawanywa) hivyo kila mtu na ofisi yake"

    "sawa boss, ahsante"

    "naombeni kazi ifanyike, sitaki mchezo na kazi"

    "sawa boss"

    Secretary aliwapeleka akina mary mpaka ofisini kwao, na kuwaelekeza baadhi ya vitu vidogo vidogo vya hapo ofisini... Mpaka hapo rose na mary wameshapata kazi







     





    Tukija huku kwa mama yake na sheby akiwa nyumbani kwake na mama yake mkwe aliomtembelea kwa siku hio,...

    "kweli mama kuna kitu kinaniuma sana katika moyo wangu"

    Aliongea mama yake sheby huku akitamani hata kulia

    "kuna nini tena mama"

    Aliingea bibi yake sheby ambae ni mama wa baba yake na sheby,..

    "baba sheby anataka kumpa mke sheby na umri huo kweli"

    Aliongea mama huyo huku akitamani hata kugombana kwa swala la mume wake kutaka Sheby aoe,..

    "lakini mbona mjukuu wangu ni mkubwa tu"

    "mama??.. Miaka 22 ni mkubwa kweli, mjukuu wako bado mdogo mama"

    Mwajabu hataki kabisa mtoto wake aoe na umri huo, mana anaona bado ni mtoto mdogo sana na umri wa kuoa bado haujafika,..

    "hata mimi sijapenda, lakini kumbuka baba ni baba mwanangu, kama kaamua hivyo sawa,.. Wacha mtoto azoee maisha ya ndoa mapema, mana kama ni pesa mnazo sasa mwahofia nini"

    "lakini mama, huyo mschana ni mkubwa, yaani hata mwanangu rehema ni mdogo kabisa yani"

    Rehema ni mtoto wa kwanza kwa huyu mama yake sheby... Na sheby ni mtoto wa pili, kisha anafuata Rajabu akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia hio...

    "mmmhhh kwanini lakini afanye hivyo"

    "mimi sijui,... tena nilitaka kuja nyumbani kukupa habari hizi, lakini mmhhh"

    "mwajabu, punguza hasira, ngoja nitaongea nae vizuri"

    "sawa mama"

    Moyo wa mama huyo ulitulia baada ya mama mkwe wake kusema kuwa ataongea nae vizuri



    BAADA YA MASAA 10 KUPITA



    Na sasa akina sheby wakiwa ndio wanaingia ndani ya hospitali hio yenye matibabu ya kimataifa,.. Walipokelewa vizuri sana lakini sasa sheby alikuwa anatafuta njia ya kuwakabidhi hapo hospitali ili atoke kufuata kazi iliomleta huku india, mana kuja hospitali ni ziada yake tu, lakini kikubwa ni kazi, na huko kwenye kampuni wanafunga mida ya saa 11 hivyo akichelewa tu, imekula kwake.. Zaituni alichukuliwa na kupelekwa katika wodi ya wagonjwa wa macho, alianza kufanyiwa vipimo na madaktari bingwa katika hospitali hio,

    "ivi dokta, kuna uwezekano wa kupona kweli?"

    "aahhh mbona hajaathilika sana huyu, kunaletwa wagonjwa hapa mpaka tunahaha, lakini nimempima huyu ni lazima apone"

    Aliongea dokta huyo huku akiahidi kupina kwa zai...

    Huku india kiukweli kila kona anayopita kinana sheby kulitakiwa kuandikwe kwa Kingereza, lakini ili nisiwachanganye mashabiki zangu katika kusoma.. Basi itabidi niandike Kiswahili, lakini ilitakiwa Kingereza kwa huku india, hivyo hata sheby anapoongea anaongea Kingereza lakini mwandishi kaifanya tu kama kiswahili tu....



    "itachukuwa siku ngapi"

    "wiki moja tu"

    "aahhh ok sawa"

    Wakati sheby anaendelea kuongea na dokta, ghafla simu yake iliita, kuangalia jina alikuwa ni mr mageshi, tajiri mwenye mzigo unaotakiwa kufika dubai

    "ndio mkuu"

    "mbona hufiki, muda unakwenda huu"

    "ok nafika hapo mara moja"

    Kijana sheby alimaliza kila kitu hapo hospitali, lakini ilikuwa ni kisiri siri hata shadi hajaona pesa ilivyotoka,.. Alipomaliza kulipa malazi ya wiki nnzima mpaka matibabu yote,.. Alimfuata shadya..

    "sasa mama, chukuwa hii laki moja kwa ajili ya kulinda mfuko.. Mana chakula malazi kila kitu ni hapa hapa, hivyo kaa karibu na mgonjwa"

    "sawa kaka... Sasa unaenda wapi.. Mana mi mwenzio sijui wanavyoongea hawa watu"

    Sheby ndio anastuka kuwa kumbe shadya hajui kuongea hata Kingereza, duu kazi ilikuwepo kwa kijana sheby

    "kwaioooo, dahh, lakini sio tabu mimi narudi sasa hivi"

    "sawa usichelewe basi"

    Aliongea shadya huku akiingia katika chumba cha kulala ambacho ni kama hostel humo humo kwa ajili ya wauguzi wanaowaseidia wagonjwa wao...

    Sheby aliingia mahari na kubadiri nguo zake za kawaida kisha akavaa nguo za asili yake,.. Mara moja anachukuwa tax iliomfikisha katika kampuni ya mr mageshi,..

    "yes boss"

    "umechelewa sana lakini hakuna shida"

    Aliongea mr mageshi huku wakielekea katika godown lenye mashine inayotakiwa kusafirishwa,..

    "sasa kama unavyoiona Mashine ni kubwa na itatakiwa kusafirishwa na ndege kubwa"

    "ookee na documents zote zipo tayari"

    Sheby aliuliza kana kwamba alitamani sana kuambiwa bado,

    "ndio, hapa ni wewe usaini, kisha niite ndege ije ipakie mzigo uondoke"

    Aahhh kijana alichoka baada ya kusikia kila kitu kipo tayari,..

    "ok nadhani kesho itatakiwa ifike dubai"

    "yes, yes,.. Tena ina haraka sana"

    "ok unaweza ita ndege ije kupakia"

    "malipo yao unayo kabisa"

    "ndio"

    Haikupita muda ndege kweli imefika mpaka katika kiwanda hicho kinachotengeneza injini za vyombo vyote duniani, hivyo kuna injini ya meli toleo jipya, ambayo ina injini nne ndani lakini zipo sehemu moja, mana ndege na meli hua zinakua na injini zaidi ya moja, lakini hii ni moja lakini imekusanya injini nne,.. Ina ukubwa wa nyumba yenye rumu mbili...

    "imeshalipiwa vibali vyote"

    Sheby alizidi kuuliza ili tu kimoja wapo kikosekane aweze kuendelea kuwepo karibu na hospitali...

    "kila kitu, yaani ni wewe kupanga unaondoka saa ngapi"

    "itabidi niondoke kesho"

    Sheby alikwenda kuongea na wahusika wa ndege kuhusiana na usafirishaji..

    "kiasi cha transporter kinakwenda vipi"

    "milioni mia mbili"

    "duuuuu... Mr mageshi.. 200 milion from here to dubai?"

    "tena hapo umefanyiwa fea sana, wanachajiwaga mpaka 300"

    "mmhhh ok, tutaondoka kesho saa mbili"

    Kila kitu kilienda sawa, malipo ya usafiri,.. Mashine yenyewe inauzwa bilioni 15 za kitanzania, na hapo ni tofauti na usafirishaji,.... Hivyo bilioni 5.7 watalipwa akina sheby kwa kufisha mzigo na kufanya kila kitu mpaka mzigo kufika eneo husika..



    Mara moja baada ya kila kitu kwenda sawa, sheby alisaini mikataba yote kila kitu, kasoro mkataba wa pesa ndio bado hajasaini...

    Baada ya kufanya hivyo kifuatacho ni kwenda hospitali,.. Alipofika alimkuta zaituni kafungwa mabandeji katika macho yake,..

    "usijali mgonjwa wako atatoka salama"

    Aliingea dokta huku akiendelea kufanya mambo yake ya kidokta,..

    "ok hakuna shida.... dokta, kuna yule mschana nilikuja nae hapa atakuwa kalala"

    Aliuliza hivyo kwasababu ilikuwa ni kagiza kameshaanza kutanda,..

    "kwani ulikuja na mschana mwingine"

    "ndio, mweupe mweupe hivi"

    Mara ghafla kuna nesi kaja na kusema kuwa

    "kuna mschana wa kiafrika yupo mochwari"

    "unasemaje wewe nesi??"

    Sheby alishtuka kwa kusikia hivyo, hata mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio

    "ndio.. Alidondoka baada ya kuona mtu kajeruhiwa vibaya, alifanyiwa vipimo vyote, lakini ameonekana keshapoteza maisha"

    "Mungu wangu shadya wa watu"

    Sheby alilalamika huku akipelekwa chumba cha watu waliokufa (mochwari)..

    "si ndio huyu hapa"

    Aliongea dokta mmoja huku akinyoosha kidole, kuashiria ndio huyo waliokuwa wakimsemea... Kijana sheby alitoa macho kama mjusi aliobanwa na mlango

    "mungu wangu... shadya wewe, nitakwenda kujibu nini kwenu mimi"

    Sheby aliongea hivyo huku akiinama chini, kumkagua vizuri.... Lakini sheby akiwa anaendelea kumkagua shadya pale chini, ghafla simu yake inaita, kucheki jina alikuwa ni baba yake..

    "haa... Ha... Haloo mzee"

    Kinana aliipokea na kusema haloo lakini huku akiwa na kwikwi za kulia

    "we una nini mbona unalia?? ... Afu mbona GPS yangu inanionyesha upo hospitali ya india, umefata nini huko"









    Kijana huyo alikuwa akilia mno kwa kilichotokea kwa shadi, yaani haamini kama shadi kafariki dunia kwa kuona mtu aliojeruhiwa vibaya, lakini wakati huo akiwa katika chumba hicho cha wafu, bado shadya kafunikwa na shuka jeupe, hivyo hata sheby hakumuona, lakini kwa maelezo ya madaktari aliamini kuwa huyo ni shadya baada ya kuambiwa ni mschana wa Kiafrika,..

    Ghafla baba yake anapiga simu, sheby aliipokea huku kwikwi za kulia zikimuandama..

    "haa... Ha... Haloo mzee"

    Kinana aliipokea na kusema haloo lakini huku akiwa na kwikwi za kulia

    "we una nini mbona unalia?? ... Afu mbona GPS yangu inanionyesha upo hospitali ya india, umefata nini huko"

    Aliongea baba yake huku sheby asijue ajibu nini, lakini papo hapo akapata wazo,.. Lakini kabla hajaliongea ghafla shadya alikohoa, na wakati huo bafo kafunikwa shuka jeupe mpaka usoni, na hata sheby hakumuona...

    "mfunueni bado ni mzima huyu"

    Aliongea sheby huku simu ya yeye na baba yake ikiwa bado ipo hewani.. Lakini sasa cha ajabu hakuwa shadya, yaani licha ya uzima wa huyo mtu, ila bado hakuwa shadya...

    "wewe aheby nani ni mzima hapo... Wewe huko hospitali umefata nini"

    Aliongea baba yake sheby

    "mzee, kuna mtu aligongwa na gari ambayo mimi nilikuwepo ndani, hivyo tumemleta hospitali"

    "ww ndio ulikuwa ukiendesha"

    "hapana ni tax za huku"

    "sasa kapona huyo mtu"

    "aahhh tulimleta hospitali lakini vipimo vilionyesha amekufa, lakini kumbe yupo hai"

    "aaahhhh afadhali... Vipi umeiona hio mashine"

    "ndio, na kesho saa mbili ndio naondoka"

    "hakikisha kazi inakwenda sawa sheby"

    "usijali mzee"

    "ok kazi njema"

    Simu ilikata huku sheby akizidi kumwangalia yule mgonjwa alioletwa kwa kusemekana kafariki dunia..

    Alikuwa ni mschana wa Kiafrika tena alikuwa ni Mtanzania kabisa...

    "habari yako dada"

    Sheby Alimsalimia dada huyo kwa kumpa mkono

    "salama... Huku nipo wapi... Uuuuuuuwwwiiiiiiiii jamani zile si maiti zile"

    Dada huyo alilia sana baada ya kuona maiti waliokuwepo hapo,.. Basi yule dada alitolewa pale na kuwekwa katika chumba cha matibabu mana hakuwa na ugonjwa wowote sema apimwe tu kwasababu alidondoka na kuzimia...

    "lakini ninyi madokta mna kesi kubwa sana ya kujibu.. Kwanini mtu ni mzima afu mnasaini kafa"

    "ni kosa lete boss, tunaomba ulinyamazie boss, tutamtibu bure hakuna shida... Ni mawazo tu"

    "mawazo kwenye maisha ya watu"

    "boss... Msamaha wako unahitajika boss"

    Madokta walikuwa wakimlilia sheby ili anyamaze, mana hio ishu ikivuja ni hatari kwao,..

    "ivi kwa hali hii, yule mgonjwa wangu atapona kweli"

    "bosiiiiii.... Hivi vipimo vilikosewa tu boss"

    "ok fanyeni juhudi na huyu awe salama"

    "sawa boss, lakini tunakuomba lisivuje hili jambo"

    "ok poa"

    Sheby alitoka hapo mbio mpaka kwenye chumba ambacho alitakiwa alale shadya,.. Alifungua na kumkuta shadi anabadili nguo..

    "ooohhh Sorry, Sorry mamy"

    Sheby alitoka mbio baada ya kumkuta shadya anabadili nguo,..

    "eeehhh uyu mtoto kaumbika, duuu"

    Sheby aliongea hivyo huku akitoka na kuelekea hotelini kwake ambako ndiko alipopangisha chumba chake,.. Alipofika alioga vizuri kisha akalala zake







     





    Kesho yake aliamkia hospitali ili kujulia hali wagonjwa wake, mana anamjua shadya hajui Kingereza hivyo sheby hatakiwi kuwepo mbali, na sijui itakuwaje pale sheby atakapoondoka,..

    Alianza kumjulia hali mpenzi wake zai ambae alikuwa bado ana mabendeji katika macho,..

    "za saa hizi shadya"

    "salama tu, hali yako"

    "nzuri... Vipi hali ya mgonjwa"

    "aahh tunamshukuru mungu anaendelea vizuri"

    "sasa shadya,... Samahani kwa kile kilichotokea jana"

    "kitu gani hicho"

    Sasa sheby alitaka kuongelea ile ishu ya jana kuingia chumbani bila hodi na kumkuta shadi anabadili nguo..

    Sasa baada ya kuona shadya kasahau ikabidi apotezee tu

    "au basi tu"

    Sheby Aliongea hivyo kisha akaondoka kwenda kumjulia hali na yule mwingine ambaye alisemekana kufa.. Lakini alioofika alimkuta kakaa mahari huku akiwa analia,..

    "za saa hizi dada"

    "salama tu"

    "vipi mbona haupo wodini afu unalia kuna nini"

    "aahhhh ni stori ndefu  kaka"

    "kwanini usiniambie tu kama naweza hata kukuseidia kwa mawazo tu"

    Dada huyo alikuwa mzuri sana na mwenye aibu za kipekee, na hakuwa mgumu wa kuongea na sheby..

    "tulikuja hapa hospitali toka juzi, lakini madaktari wakataka tuhamishwe hospitali nyingine,... Sasa katika kuondoka, mimi nikawa namalizia kukusanya vitu kule kwenye vyumba vya wauguzi.. Lakini nilipokuwa natoka, nikapishana na mtu aliopata ajali mbaya sana.. Sijawahi kuona nyama za binadamu,.. Kiukweli kitendo kile kilinifanya nizimie papo hapo.. Ndipo nilipozinduka nikajikuta nipo mochwari na ninyi mkiwa pembeni yangu... Hivyo mpaka sasa sijui wamekwenda wapi na sijui wanaendeleaje huko"

    "mmmhhh pole sana dada angu.. Naa ni nani wako hao"

    "ni shemeji yangu.. Yaani dada yangu kaolewa huko, sasa ndugu yake mume wa dada yangu, kaletwa kwa ugonjwa wa uvimbe tumboni"

    "ooohhh pole sana"

    "mpaka sasa sijui nawapata vipi ili niweze kurudi nyumbani"

    "ooohh pole sana dada angu,.. Lakini kwanini usiendelee kuwepo hapa, mana wanaweza kuja hapa"

    "sasa nitawezaje kukaa hapa na wakati mgonjwa alionileta hayupo, ulifikiri nitalipaje bili za watu"

    "kwani unadaiwa"

    "hapana, ila nikiendelea kuwepo hapa bila sababu"

    "sababu ipo..... Sikia nina mgonjwa hapa ndani, nilikuwa naomba ushirikiane na dada mmoja hivi"

    "una mgonjwa, mgonjwa gani"

    "twende ukamuone"

    Dada huyo ambae hata jina hatumjui alichukuliwa na kijana sheby mpaka kenye wodi ya macho na kumwonyesha mgonjwa wake

    "alikuwa haoni kabisa au"

    Dada huyo aliuliza

    "alikuwa kipofu kabisa"

    "hhhmmm pole sana.. Ni dada yako ee"

    "no, ni mpenzi wangu"

    "aahhhhhh wanaume kama ninyi ni wachache sana duniani,... Sijui kama wapo wengine, kwa jinsi wasichana tulivyo na akili mbovu, una moyo kaka angu"

    "nampenda sana mpenzi wangu"

    "I know"

    "Eeeeehhh we unajua kimombo kidogo"

    "yes, I know"

    "basi naomba ukae hapa na huyu hapa ni dada yangu, utakuwa nae hapa ili uongew na madaktari...... Dada shadi, huyu atakuwa mgeni wetu"

    "sawa...... Dada karibu"

    "Ahsante.... Naitwa Judith naishi Dar es Salaam"

    "ooohhh mi naitwa shadya, naishi arusha"

    "ooohhh napenda sana kuishi arusha"

    Basi shadya na Judith walianza kupendana ghafla tu na urafiki ukaanza.... Wakati huo madaktari wanaendelea na matibabu juu ya zaituni...

    "sasa naombni nitoke kidogo nitarudi nadhani"

    "sawa kaka"

    "aahhhh Judi, tayari nimeshalipa kila kitu, hivyoo.. Chukueni hii ikae ya mfuko kwa ajili ya vitu vidogo vidogo vitakavyohitajika"

    "sawa"

    Sheby aliondoka zake ikiwa ni saa mbili kasoro robo,... Alichukuwa tax ilimfikisha mpaka kwenye kampuni ya mr mageshi,.. Alimaliza mambo yote kisha safari ya kuelekea dubai ilianza...



    Huku hospitalini judi akiwa anaongea na shadi

    "kaka yako mkarimu eee, tena anaonekana anapenda kuseidia watu"

    "aahhhh waapi korofi hilo hapana chezea"

    "mi napenda wanaume wakorofi, mana mwanaume mkorofi basi lazima kuna mahari ni mzuri... Kuliko kupata mwanaume mzuri kila idara, basi jua kuna siku utalia mpaka ukome"

    "kwaio unamaanisha umeshapenda ivyo"

    "kupenda sio kazi, kazi kukubaliwa"

    "weeeeeeee shauri zako.. Mwenyewe yule pale kalazwa akikuskia huna bahati"

    Walikuwa wkiongea huku wakicheka,

    "hapana bwana,.. Huyu mkaka namueshim sana japo tumekutana kwa muda mfupi tu"

    "hata mimi mwenyewe namueshim weeee"

    "we kumueshim ni lazima... Si kaka yako"

    "mmmhhh"

    "mmmhhhh nini sasa"



    Baada ya masaa 9 kupita kijana sheby ndani ya dubai, wakati huo clan linafanya kazi ya kuitoa ile mashine katika ndege,.. Mashine yenyewe ina uzani wa tani 20

    "sasa jamani, nadhani mzigo wenu umefika salama"

    Sheby aliongea hivyo ili waamalizane aondoke zake...

    "kwahio watakaje"

    "mkataba wa pesa huu hapa, tusaini kisha mnilipe niondoke"

    "hapana, huezi ondoka bila mashine kuwekwa, mpaka mashine iwake ndio uondoke"

    "Ati nini we Mwarabu"

    Sheby alipanic ghafla kwa kusikia kuwa atatakiwa kukaa mpaka mashine iwake, laa sivyo hatolipwa..

    "hio ni moja ya kanuni zetu... Kulipwa utalipwa lakini mpaka mashine iwake, isipowaka utarudi nayo india"

    "ayaaaaaaaaaa"

    "sikia mr sheby.... Huku tutakugharamia kila kitu, yaani utachagua hoteli uitakayo utakula chakula ukitakacho, yaani maisha yako huku dubai tuachie sisi"

    "hamula lolote bwana mbwembwe tuuu"

    Sheby kwa hasira alimoigia baba yake

    "haloo mzee"

    "vipi, Nakuona hapa umeshafika bandarini, na nadhani mnapakua mashine"

    "ndio mzee... Lakini mbona wanasema siwezi kulipwa mpaka mashine iwake kwanini"

    "ndio kanuni zao, huwa hawatakagi biashara za kona kona"

    "sasa itachukuwa muda gani mzee"

    "mpaka waunganishe hio meli yao, yaweza chukuwa hata wiki nzima"

    "Whaaaat,... Mzee mi nilijua itachukuwa masaa, wiki nyingi mzee hebu ongea nao basi hata siku ziwe chache"

    "haiwezekani.. We kaa hapo uone na ulinde, tena ukikaa mbali itakula kwetu, kutatolewa kifaa hapo afu tuambiwe ni sisi wasafirishaji"

    "aaakhaaaaa"

    "ndio kazi hizo baba tulia"

    Sheby alikasirika kweli yani, afu unaambiwa hatakiwi kwenda mbali mpaka mashine iunganishwe kwenye meli,.. Iwake ndio alipwe,.. Sheby alikaa mahari huku akiwaza itakuwaje kule hospitali,... Yaani wasiwasi wake wote ni kule hospitali.



    Sasa tukija huku kwa mama yake zaituni, leo tunaiona nyumba ya akina zaituni inakarabatiwa yaani inakuwa nzuri, kwa muonekano wa haraka haraka inaonekana sheby keshainunua hio nyumba, hivyo hapo ilikuwa ikipigwa rangi,

    "mama, zaituni kaenda wapi mbona simuoni karibia siku ya tano hii"

    "we wamtakia nini mwananguc

    "heeeeeeee mamaa, kwani kuna shida gani kumuulizia pacha wangu"

    "pacha wako... Pacha wako ungemwagia tindikali kisa wanaume"

    "lakini mama si nimeomba msamaha, ilikuwa ni usichana tu"

    "mimi sijui hio, afu fanya uondoke kwenye nyumba yangu mshenzi wewe"

    "sasa nikiondoka nani atalipa kodi"

    "weeeeeeeeee, nyumba imeshanunuliwa hio,.. Mdogo wako ana nyota ya kupendwa, sio wewe mshenzi wewe... Tena staki hata kukuona, nilikuwa nakuchukua sana sema sikuwa na jinsi ya kufanya kwakuwa ulikuwa unalipa kodi lakini nilikuwa sikupendi hata kidogo"

    "mamaaaa.... "

    "tokaaaa"



    BAADA YA WIKI MOJA KUPITA



    "Ahsante sana mr sheby,.. Mashine imefanya kazi vizuri na umeifikisha salama"

    "sawa hebu tusaini kisha utume pesa kwenye akaunti ya mzee"

    "sawa njoo huku ndani"

    Kijana sheby alikuwa ana haraka ya hali ya juu, mana wiki nzima yupo dubai, licha ya kulipiwa kila kitu akiwa dubai,...Hali ya hewa ya dubai kwa sheby haikumpenda kiasi flani kwani alikuwa na mafua ya hapa na pale, hivyo hata sauti yake ilikuwa haitoki vizuri,... Basi Pesa zilitumwa katika akaunti ya mzee Rashidy kisha sheby akampigia simu baba yake

    "mzee B 5.7 zimefika"

    "aaahhhh ngoja niangalie kupitia akaunti ya simuuuuuuuu.. Yes, imefika"

    "ok poa... "

    "kazi nzuri, safi sana huo ndio ukubwa sasa"

    "sawaaaa"

    "rudi nyumbani sasa, au huna pesa nikutumie"

    "ninayo"

    Sheby alikuwa kakasirika sana hakua na raha hata kidogo, hata baba yake hakuwa akimjibu vizuri.. Yaani kakaa wiki nzima dubai bila sababu za msingi...

    Basi sheby alimaliza kila kitu kisha akawahi Airport na kupata usafiri wa private,.. Ndege iliokuwa na spidi kali kuliko za kawaida...



    Masaa matano tu yupo ndani ya india, hakutaka kuchelewa, mara moja akachukuwa tax, ilimpeleka mpaka hotelini alipopangisha chumba,.. Alibadiri zile nguo zake za kawaida za kimaskini japo zilikuwa safi safi kidogo lakini ni nguo za kimaskini sana... Bila kuchelewa sheby ndani ya tax mpaka hospitali, wakati huo alikuwa na haraka ya kwenda kuwaona wagonjwa wake,... Spidi aliokuwa nayo hata salamu alikuwa hatoi..

    "we kaka vipi, ina maana huoni au?"

    "Samahani da........ Haaaaaaa zaituni"

    "umelijuaje jina langu? ... We vipi wewe"

    Alikuwa ni zaituni, tena alimjibu huku akimuangalia juu mpaka chini...









    Tenda wema uende zako, ukisubiri shukrani kutoka kwa mtendewa, mwisho utapokea mateke ya punda, kijana sheby aliompenda mschana zaituni, mdada mrembo, mdada mwenye sura ya kuitwa mrembo, mdada mwenye umbo la kuitwa mrembo, lakini urembo wake wote ulifichwa na upofu wake,.. Mdada aliopatwa na upofu kutokana na bahati zake,... Lakini kijana sheby hakujali upofu wa dada huyo, alimprnda na kumjali bila kuuona upofu wa zaituni... Kijana sheby ni miongoni mwa watoto waliozaliwa katika familia za kitajiri, hivyo akaamua kumpeleka india ili aweze kuona tena,... Lakini sasa kipindi zaituni anafanyiwa operesheni ya macho, sheby alikuwa dubai, hivyo ile siku zaituni anaona hakukutana na sheby na wala hamjui kwa sura, wiki ikapita kijana ndio anakamilisha kazi aliotumwa na baba yake,.. Kijana huyo alipanda ndege ya haraka ili kumuwahi mgonjwa wake, ndege ilitua katika nchi hio sheby kaingia katika hoteli yake ya kubadirishia nguo...

    Bila kuchelewa sheby ndani ya tax mpaka hospitali, wakati huo alikuwa na haraka ya kwenda kuwaona wagonjwa wake,... Spidi aliokuwa nayo hata salamu alikuwa hatoi..

    "we kaka vipi, ina maana huoni au?"

    "Samahani da........ Haaaaaaa zaituni"

    "umelijuaje jina langu? ... We vipi wewe"

    Alikuwa ni zaituni, tena alimjibu huku akimuangalia juu mpaka chini...



    Kijana sheby anashangaa kuona zaituni anamwangalia kwa dharau ya hali ya juu,...

    "mmmhhhh samahani zai, yaani hata hunikumbuki"

    Sheby aliongea lakini ukumbuke kuwa kijana sheby alipatwa na mafua kule dubai, hali haikumpenda sana katika nchi hio,.. Sasa kijana huyo hakuwa akitoa sauti yake halisi bali ni sauti ya kubanwa na kifua

    "wala hata sikukumbuki"

    Sasa kabla sheby hajaongea, ghafla shadya katokea akiwa na judith

    "heeeeee sheby umerudi saa ngapi"

    Aliongea shadi huku akitamani kunikumbatia lakini kashindwa kutokana na zaituni kuona,...

    "nimerudi dada angu"

    "heeeeeee sauti yako imepatwa na nini tena"

    "we acha tu dada shdi, nimeenda kupigika kikazi huko nimebebana na mizigo mizito"

    "mmmhhh pole kaka sheby, lakini umewnda kufanya nini sasa"

    "sasa bila kufanya kazi tutapataje nauli ya kurudi Tanzania"

    Sheby aliongea huku akishika shingo kuashiria kabeba mizigo mizito, lakini sio kweli sema hataki kujulikana kama ni mtoto wa kitajiri,..

    "pole sana kaka"

    Aliongea judith huku akiwa na huzuni mana kweli kijana huyo alikuwa anahema kwa spiti afu katoka jasho kwa kukimbia....

    "kaka sheby.. Umemuona zai wako"

    "nimemuona, lakini yeye hanijui"

    "we zai,.. Huyu ndio sheby mwenyewe huyu"

    Aliongea ahadi huku akimsistizia zai kuwa huyo ndio sheby,

    "mbona sauti yake sio"

    "ina mana we hujaskia hapa nikimuuliza kuhusu sauti yake"

    Mara na judi na akaongea kuwa

    "ndio wewe zaituni, huyu ndio aliomileta huku india"

    Huezi amini zaituni alianza kulia kwa kile alichomfanyia sheby kabla ya kumjua,...

    "nisamehe baby wangu, sikujua"

    "najua sio kosa lako zai... Kwanza pole sana baby"

    "Ahsante"

    Basi walichukuwana mpaka katika chumba cha hapo hospitali,

    "unajua nini sheby... Zai alipoona tu, akaahidi kuanzia siku hio hatokaa kumjua mwanaume yeyote yule zaidi yako, yaani atamdharau kila mwanaume, sasa alipokuona wewe ndio akaanza dharau zake, ila haikumaanisha akudharau wewe"

    Aliongea shadya, huku wakiwa wamekaa wote kitandani

    "mimi mbona sijakasirika, nipo sawa na najua sababu ya yeye kuwa vile"

    Waliongea sana huku wakipanga mipango ya kurudi Tanzania,...



    BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA







     





    Na leo ni siku nyingine tena sheby akiwa anaburuza mkokoteni uliojaa viazi mbatata,.. Alifika mpaka pale alipo pangisha, ukumbuke kuwa walisharudi Tanzania na ni mwezi sasa umepita toka waliporudi nchini kwao,... Kijana sheby aliingia katika boma alilopangisha na kumkuta shdiya katika kazi yake ya ushonaji wa nguo,...

    "za saa hizi shadi"

    "salama tu kaka sheby habari yako"

    "safi tu... Vipi uyu mamsapu yupo"

    "nadhani atakuwa anachota maji hapo mbele"

    "ok.. Ngoja nimuachie viazi kidogo vya kupika mchana"

    "sawa"

    Sheby aliweka viazi ndani kisha akamfuata shadya...

    "we mwanamke, ivi kazi inaendelea"

    "ndio, inaendelea wala usijali"

    "ok poa"

    Waliongea maswala ya kazi lakini hatukujua ni kazi gani waliopeana baina ya shadi na sheby,... Kijana huyo akiwa anaondoka ghafla anakutana na mpenzi wake zaituni

    "waooo mume wangu, Asalam aleykh"

    "waaleykh msalam hali yako lakini"

    "mmmhh swalama tu"

    "upo freshi eee"

    "ndio, ila... Nina shida kidogo"

    "nini tena"

    "unajua toka nimefanikiwa kuona, lakini sijaenda hata kumsalimia mama yangu"

    "oooohhhh shit, sema bize nyingi.. Lakini kesho Jumapili lazima twende"

    "eti eeee"

    "Ahsante sana mume wangu"

    Basi sheby na zai waliagana, lakini huezi amini kijana huyo hajamgusa zai mpaka leo hiii.... Kiukweli ni ngumu sana kwa vijana wa sasa hivi kuishi na mwanamke bila kumgusa... Sasa sheby kumbe aliazima mkokoteni wenye viazi ili kuendelea kuimarisha uhusiano wao

    "Aisee asante sana bwana..."

    Kijana sheby alirudisha mkokoteni wa watu kisha akamlipa mhusika wa kago hilo,...

    "usijali kaka.... Ila umetoka jasho kwelikweli yani"

    "we acha tu,... I think mtakuwa mnapata tabu sana ndugu zangu.. Poleni sana"

    Sheby aliwapa pole wasukuma mikokoteni, mana yeye ni mara moja moja tu lakini kachoka ile mno..

     

     

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog