Chombezo : Pete Ya Kike
Sehemu Ya Nne (4)
Tukija
huku dukani kwa faima
"sasa umerudi kazini, chezea
tena..."
Aliongea zamina dada yake na faima akiwa dukani anapouza mdogo
wake
"dada, mimi nakuelewa ila Kiukweli suria hatoki kichwani mwangu,..
Sijui kama huko alipo kama ananisikia"
Aliongea faima huku zamina
akisema
"wewe acha ujinga, suria, suria kila siku suria... Mtu
keshauwawa na dada yake wewe unateseka tu"
Mara zamina alitulia kwani
simu yake iliita...
"halo shem mambo"
Alipokea simu hio huku
akisema shem, lakini sauti ya huyo shem haikusikika
"eeeh
umefika"
Aliongea faima kana kwamba huyo shem yupo maeneo
hayo...
"ok njoo kwenye duka moja hivi, ulizia IC (ISLAMIC CLOTH) ndipo
nilipo"
Alimuelekeza mtu huyo
"umepaona eee?"
Alijibu
mwenyewe kisha akamalizia kusema
"sawa njoo chap basi"
Zamina
alikata simu kisha akamwambia mdogo wake kuwa
"acha na wanaume wasio na
mbele wala nyuma... Tariki unamkataa bure tu lakini ana hela, acha ufala.. Na
ndio huyo anakuja, ongea nae vizuri"
Aliongea zamina kisha akaamka pale
kwenye kiti,.. Alikuja jamaa mmoja sharobaro mno, na pia alionekana kuwa nazo
kutokana na nguo kali alizo vaa...
"ooohhh shem Riki,
mambo"
"poa shem nambie"
"safi tu... Kumbe we mwenyeji hapa
IC?"
"ndio, mbona ndio mitaa yetu hii"
"wacha
Weeeee"
"ndio"
"ok karibu,.. Mwenzio uyo apo.... Sasa faima mi
naenda kwa tizo"
"sawa dada"
Zamina aliondoka zake hivyo faima
akabaki na Tariki, ikiwa wateja wamepungua kidogo....
"mambo
fai?"
Tariki alimsalimia faima, lakini faima hakuwa na muda nae tena
anatamani wateja waje ili asiongee na Riki....
"nakusalimia tu jamani
fai"
"shida yako nini riki,.. Sitaki kuongea na wewe"
"lakini
fai,... Moyo ndio unanipeleka puta juu yako,.. Mimi ni mtu na pesa zangu,
inakuwaje nakosa mtu wa kutumia nae"
Aliongea Tariki, huku faima ndio
kwanza hata habari hana....
"pesa ni zako na familia yako, hazinihusu
hizo"
"fai ina maana bado unampenda mtu aliokufa.... Umekuwa mkali mpaka
nimeamua kumtumia dada yako"
"tariki tafadhali sana naomba
usinichefue"
Faima alimjibu tariki huku tariki akituma sms kwa zamina
mana ndio msaada wake...
Ghafla simu ya faima inaita.. Kucheki ni dada
yake...
"halloo"
Aliipokea faima na kuita haloo"
"acha
ujinga wewe, kupenda gani huko mpaka kwa watu waliokufa... Acha ujinga, wanaume
siku hizi hakuna sasa potezea hio bahati endelea kupenda mtu aliokufa, na
ukumhuke umri wako unazidi kwenda na utahitaji ndoa.. Sasa jifanye unapenda
utaolewa na mizimu ya suria"
Aliongea zamina kisha akakata
simu
Faima alihema kwa nguvu kisha akamuangalia
tariki...
"naomba uondoke na staki uje tena"
"nini tena
faima"
"nasema tokaaa"
"ok poa, ila siku ukijiskia... Utanicheki
kwenye simu, namba yangu hio hapo"
Tariki aliacha karatasi yenye namba
za simu yake, ili siku faima akifikiria vyema basi amtafute kwa namba
hio
Hivyo tariki aliondoka zake, lakini alipofika mahali alikutana na
rafiki yake wa kiume ambaye alikuja naye lakini hakutaka afike nae pale IC,
hivyo alimuacha mbali na hata rafiki huyo anajua leongo la
tariki...
"riki vipi"
Aliuliza rafiki yake huyo, huku riki
akijibu
"mmmhhh ebana mtoto ni mgumu... Nimejigamba nina hela lakini
wapi mtoto hajali wala nini"
Aliongea tariki, kana kwamba hana pesa wala
nini sema ilikuwa mikwara ya kutongozea tu....
"unajua tariki
unakosea,.. Na ndio mana mademu hukai nao... Mana unajinadi sana kuwa na pesa
wakati hata kazi huna"
"sasa jumbe kama unavyojua, mademu wa sasa hivi
ni wakali kinoma ila kuwapata ni mkwanja, ukumhuke samaki bila chambo humpati
ujue"
"ni sawa, lakini kumbuka yule sio samaki"
"wacha nijitape
tu... Akichomoa poa kwani kwsho si tunakwenda kupata kazi kule
kiwandani"
"na usipo pata je"
"fresh tuuu"
"afu sitaki
kuamini kuwa hata dada yake anajua una hela"
"sasa je? Anajua ninazo...
We ulizani kwa pamba hizi ataachaje kuamini"
"duuuuuu, yaani wewe ni
zaidi ya Jambazi aiseee"
Tukiachana na hao tuje huku kwa akina
surian na mke wake maimuna waliokuwa ofisini, na msichana mmoja hivi ambae yeye
ni jirani yao, baada ya kuskia anatafuta kazi,... Na dada huyo alisomea
usekretari, hivyo imekuwa rahisi sana kwake kupata kazi,... Wakiwa hapo ofisini
dada alianza kuonyeshwa sehemu yake ya kazi,...
"sasa wewe ndio
sekretari wa kampuni hii, haruhusiwi mtu yeyote kumuona boss bila wewe kuleta
taarifa zake kwangu"
Aliongea surian na hapo alikuwa na mke wake
maimuna,
"sawa boss, nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu ni sitakiuka
kanuni na taratibu za kampuni hii"
"ok... Nadhani kwa siku ya kesho
utapata changamoto kubwa na kazi kubwa pia kwasababu kwsho ndio siku ya usaili,
hivyo wataingia watu watano watano, utamkagua mmoja baada ya mwingine kisha
unaniletea barua yake ikiwa na vyeti vyake... Nitakapo ona vyeti ya mhusika,
basi mimi ndio nitajua namuweka nafasi gani kitokana na elimu
yake"
"sawa boss,. Naaa... Mfanyakazi anaruhusiwa kuingia ofisini
kwako"
"hapana... Haruhusiwi mtu yeyote kuingia ofisini kwangu, ispokuwa
wewe na mke wangu tu... Hivyo ofisi itaingiliwa na watu watatu... MIMI NA MKE
WANGU PAMOJA NA WEWE na wewe utaingia kwa kuleta document au taarifa za kitu au
mtu fulani, sio kuingia mara kwa mara kwakua unaruhusiwa, na hata awe boss wa
kampuni gani, mwambie anisubiri chumba cha meeting (mikutano)... Nadhani
umenielewa"
"nimekuelewa boss... Hivyo kesho, nakagua barua za
mtu kisha nakuletea"
"yes, na uhakikishe barua imekamilika vigezo vyote
ndio uilete kwangu kama naipitisha au laa, na kama haijakamilika sitaki
usumbufu, mtu huyo arudi akakamilishe vigezo vyote... Sawa
Cecilia"
"sawa boss"
"ok, nipo ofisini kwa wale watakao tokea
leo wapokee tu"
"sawa boss"
Ilikuwa ni mipango ya kazi
ambayo anatakiwa kufanya sekretari huyo, ikiwa ni kampuni mpya katika mkoa wa
tanga, na inahitaji watu takribani 500 (miatano) ikiwa na lengo la kusaidia watu
kwa njia ya kuwaajiri, kampuni ya MOON ISLAMIC CLOTH COMPANY, Ipo tayari kwa
wafanyakazi kuleta maombi ya kazi
Kesho yake asubuhi mida ya
saa mbili, ndani ya geti la kampuni hio kulifulika watu wengi mithili ya soko,
kweli hapo kazi ipo... Watu walikuwa ni wengi mno na uchambuzi huu hautakiwi
kufanywa na maimati, mana yeye hutumia nguvu za asili yake, hivyo asije
kupitisha watu Ilimradi tu......
Katikati ya watu zaidi ya
miambili alionekana mama yake surian akiwa kashika bahasha yake, naye kaja
kuomba kazi kwenye kampuni hio, na watu woote walikuwa na umri usiopungua miaka
18 mpaka 35 lakini mama kajikaza tu kuka mana haoni lika lake kati ya
wafanyakazi aliosimama nao... Mama suria au mama asha anachungulia tu kama
angalao hata atamuona boss ampe kipaumbele kwakua ni mtu mzima,.. Lakini kwa
bahati mbaya au nzuri boss keshaingia ndani na haruhusiwi kutoka wala kuingia
mtu...
"heeee we mama vipi mbona unanisukuma"
Aliongea dada
mmoja huku kama wakimcheka mama yakw suria,.. Yaani laini wangelijua kuwa huyo
ndio mama wa bosa wanaye muomba kazi sijui ingelikuwaje, na mama nae hajui kama
anakwenda kuomba kazi kwenye kampuni anayomiliki mtoto wake, na hata mtoto hajui
kuwa mama yake kaja kuomba kazi,...
Usaili Ulianza, na vigozo
visipo timia unarudishwa ukatimize vigezo, na kama huezi basi usirudi tena...
Hivyo kuna wale ambao hawana vigezo basi wanarudi lakini namba zao zimeachwa
kwamba watachukuliwa kama masalia tu... Hivyo hata akiondoka namba inaachwa kwa
sekretari, siku akihitajika mtu aitwe...
Wasichana walikuwa
wakimcheka mama asha, kwani alikuwa na umri mkubwa sana
"huyu mama
jamani ananikanyaga"
"we mama ulikuwa wapi ujanani
kwako"
Walikuwa ni wasichana waliokosa heshima ndio walikuwa wakimsema
mama huyo, mpaka mama asha akakata tamaa na kukaa pembeni mana alikuwa kwenye
nafasi ya kuitwa lakini akajikuta karudi nyuma ili asichekwe na watoto kulingana
na umri wake..
Pamoja na uvumilivu wake wote, zamu yake ilifika
akiwa na furaha kwa kupata nafasi, wengine walicheka sana... Na hata sekretari
alishtuka kumuona mama mwenye umri mkubwa amekuja kuomba kazi za
viwandani...
"heeeee mama.... Hata wewe"
Alikuwa sekretari ndio
mwenye kuongea
"ndio mwanangu, nitafanya kazi usinione hivi
tuuu"
Aliongea mama asha au mama surian na mama huyu anasikia tu mtoto
wake kafa lakini hana imani hio mana yapata miezi miwili hamjui alipo wala
hajawahi kuwasiliana nae
"mama, umri wako hauruhusu kufanya kazi hapa...
Na hata karatasi ya matangazo ilisema ni kuanzia miaka 18 mpaka 35 ndio
mwisho... Kwani mama una umri gani"
Aliuliza sekretari huyo huku mama
akiwa mshapu kujibu ili aonekane yupo shapu hata kwa kufanya kazi
"nina
miaka 58"
"haaaaaaaaaa mama, haiwezekani"
"jamani nipeni hata
kufagia fagia tu"
"labda ingekuwa hio lakini hata vyeti vya shule huna,
hapa naona barua na paspoti saizi tu"
Aliongea Cecilia huku akisoma
barua ya mama huyo
"nisaidie mwanangu... Ina mana nife njaa na nina
uwezo hata wa kudeki vyoo"
"mama, tatizo ni umri wako ni mkubwa sana...
Kwani huna watoto wasomi waje tuwape nafasi"
Aliongea Cecilia bila kujua
boss wake ndio mtoto wa huyo mama lakini hakuna anaejua hilo... Sasa Cecilia
aliposema hivyo, mama akakumbuka mtoto suria ambaye ni msomi mpaka
basi,....
"usinikumbushe yaliopita mwanangu, nisaidie
kazi"
"mama, kweli naogopa kufokewa na boss kama nitaipeleka hii
barua"
"jaribu tu, nitasafisha hata vyoo tu"
"mmhhh mama angu
unanipa mtihani"
Mara ghafla simu ya mezani kwa Cecilia inaita...
Alipokea
"hallo boss"
"eeehh vipi watu
wameisha??"
"hapana boss bado wapo"
"sasa mbona huleti document
zao"
"naleta boss.. Ila kuna"
Cecilia alitaka kusema lakini
akasita,.. Sasa alipomwangalia yule mama anatia huruma sana
"ila nini
ceci? Lete document muda unakwenda huu"
"boss?"
"nini Cecilia?
Lete"
"boss... Kuna mama mtu mzima hapa, hana vyeti, ana miaka 58..je
tunamsaidiaje"
Aliongea Cecilia, huku akisubiri jibu toka kwa boss
surian....
"hivi we Cecilia una akili kweli,.. Vigezo ni kuanzia miaka
18 mwisho 35, sasa huyo mwenye miaka 58 aliambiwa hapa ni kituo cha watoto
yatima kuwa aje kulea watoto??... Lete documents za vijana na nikiona documents
kuanzia miaka 36 huna kazi Jinga kabisa wewe"
Simu ilikata na Cecilia
akawa hana jinsi tena zaidi ya kumpa mama karatasi zake...
"mama,
nimejitahidi sana kukusaidia.. Lakini nimetukanwa kama mtoto... Shika bahasha
yako mama angu, ila pole sana mama..."
"boss wako ni mkali
kumbe"
Aliongea mama huyo bila kujua boss huyo huyo ndio mtoto wake wa
kumzaa ila anasikia sikia tu kua kafariki dunia...
Lakini sasa ikumbukwe
kuwa maimuna ni jini,.. Sasa kule ndani ofisini maimuna yupo, na hapa kwa
sekretari kivuli chake kipo, kwahio kule ni mwili na huku ni kivuli,... Sasa
alishangaa kuona Qarina wa surian na Qarina wa huyu mama wanaongea, na yeye kama
jini ndio mwenye uwezo wa kuongea na hao Qarina,.. Sasa leo maimuna ndio anajua
kumbe huyo mama hapo mapokezi ndio mama yake surian, Yaani ndio mama mkwe wake
kabisaa..
Ama kweli usilo lijua ni usiku wa
giza, kwani surian angelijua kuwa anaye mkatalia ni mama yake mzazi kabisa,
sijui ingelikuwaje hapo, mana ana uchungu na wazazi wake, anatamani sana
kusaidia wazazi wake nao wale raha, lakini mke alio muoa ni jini na kawaida ya
majini hua na masharti yao, na moja ya masharti hayo ni kuto isaidia familia
yake ispokuwa kwa kufanya kazi, sasa baada ya asha kukataa kuja ku apply
(kuomba) kazi, mama aliamua kuja mwenyewe baada ya mtoto wake kukataa,... Sasa
boss au kanuni ya kampuni hio haitaki wafanyakazi wenye umri mkubwa, wanahitaji
vijana wachapa kazi na sio wazee wasinziaj,....
Sasa maimuna
kutokana na asili yake ya ujini, aliweza kugundua kuwa mama aliopo mapokezi ni
mama mkwe wake, na keshaikosa kazi... Maimuna aliumia sana mana hata yeye
hakuipenda hali hio, na laiti kama wangeruhusiwa kufanya hivyo, basi angemruhu
surian aisaidie familia yake,... Pamoja na maimuna kujua kuwa huyo ni mama yake,
lakini hakuna msaada wowote alio ufanya zaidi ya kitulia na hakumgusia surian
kuwa huyo mama ni mama yake mzazi kabisa...
Sasa huku mapokezi,
hata kile kivuli cha maimuna kilirudi ndani kwani hakutaka kuyaona machozi ya
mama yake surian yakimwagika kwa kukosa kazi, na mbaya zaidi ni umri wake ndio
ulimtupa mkono... Basi mama akawa anaondoka huku baadhi ya wasichana wakimcheka
kwani aliziba riziki za vijana..
Lakini Cecilia ambaye ndie
sekretari wa kampuni hio naye ni msichana aliojawa na huruma juu ya huyu
mama,
"mama Samahani kaa pale Kwanza"
Aliongea Cecilia huku mama
akikubali mana hajui kwanini kaambiwa akae pembeni Kwanza,
Muda
wa kupokea barua uliisha kwani ilikuwa ni saa 11 za jioni, lakini wameahidiwa
waliobaki warudi kesho kwa ajili ya usaili,... Cecilia alimwita mama yule na
kuchukua zile karatasi zake,...
"nipe namba zako za simu, ili siku kazi
ikianza nikupigie uje"
Aliongea Cecilia huku mama akitaka kuuliza lakini
akaona wacha aende tu
"sawa mwanangu, ahsante.. Namba zangu ni hizi
hapa"
Cecilia alichukua namba za mama yake surian lakini sio kuwa
Cecilia anajua kuwa huyo ni mama yake surian, hapana hajui... Na Cecilia kaamua
kufanya kitu yeye kama yeye ili amsaidie mama huyo..
Kila mmoja
alishaondoka sasa surian ndio anatoka, lakini wakati huo mama yake alisha ondoka
baada ya kuachiana namba na sekretari...
"pole na kazi"
"ahsante
boss, pole na wewe"
"ahsante... Aahh nadhani ni muda wa kutoka,
hakikisha unafunga vizuri... Na ufunguo wa hii ofisi utakaa nao wewe kwasababu
mimi nitakuwa wa kwanza kabla yako ila wewe ndio utakuwa wa kwanza kufungua
ofisi na kuifanyia usafi na kila kitu,.. Kasoro ofisini kwangu nitabaki na
ufunguo wangu pamoja na ufunguo wa mlango mkubwa ili niingie ofisini
kwangu"
Surian aliongea sana kwa kumuachia maagizo Cecilia
"sawa
boss nimekuelewa na ahsante kwa kunipa nafasi hio"
"ok sawa... Tukutane
kesho"
"sawa boss, niwatakie jioni njema"
"nawe
pia"
Alijibu maimuna ambaye ndio mke wa surian, mana saa ya kutoka
hutoka wote na huingia wote lwani wao hutumia gari moja
tu...
Baada ya nusu saa, Cecilia alipanda daladala mpaka mjini
ambapo aliingia katika duka moja la nguo za Kiislamu, na duka hilo ni ICC
(Islamic Clothing Centre) ambapo ndipo anapouza faima mchumba wa
surian,
"heeeeee anti, Asalam Aleykh"
Faima alifurahi na
kumsalimia Cecilia kwa furaha kana kwamba wana undugu fulani hawa
watu,..
"waaleykh msalam habari yako fey"
"ah namshukuru Mungu
kwa rekhma zake"
"mguu huu wako mdogo wangu..."
Aliongea Cecilia
huku faima akiwa makini kumsikiliza anti wake
"enhee, najua wewe huja na
vya maana wewe"
Aliongea faima kuwa Cecilia hua anakujaga ma mambo ya
maana
"sasa skia, tusipoteze muda.... Kuna kampuni fulani hivi ya nguo
za Kiislamu, inaanza kazi jumatatu ijayo, sasa hivi tupo kwenye usaili na mimi
nimepata kazi nafasi ya Secretari"
Aliongea Cecilia huku faima akifurahi
mno
"waaaaooo! Jamani anti hongera, mana ulivyokaa mtaani mpaka basi..
Mungu kakujaalia anti wangu"
"ahsante sana, ila nina shida na wewe, tena
kubwa tu"
"shida gani hio anti ceci"
"kama unavyojua, katika
kazi hua kuna majaribu sasa kuna mama mmoja kaja kuomba kazi kwenye hio kampuni,
na huyo mama ana miaka 58, hana cheti chochote kile... Na pia umri wake umemtupa
mkono... Sasa mimi nataka tumsaidie huyo mama"
Aliongea Cecilia huku
faima akishtuka kwa hilo
"mmhh sasa anti shadya... Mimi nitatoa msaada
gani ingali sifanyi kazi huko"
Aliuliza faima, tena kwa kumuita shadya,
kwani Cecilia hua sio jina lake halisi, ni jina alilopewa chuoni na rafiki zake,
sasa mwenyewe anapenda kulitumia mana lina muonekano wa
kisekretari,...
"swali lako zuri sana faima... Lakini msaada wako ni
vyeti vyako, na paspoti saizi zako... Hivyo tu basi ili yule mama akapate kazi,
mana mpaka analia maskini ya mungu... Tumsaidie jamani faima"
Aliongea
shadya au Cecilia, na laiti kama Cecilia angelimuonyesha faima paspoti saizi ya
yule mama.. Basi faima angemjua mana ni mama wa mchumba wake,.. Patamu
apo...
"mmmhhh lakini anti, hii si hatari sana, mana huyo mama akiharibu
huko kazini kwenu, si nitafuatwa mimi jamani"
"hapana faima...
Nikishakua kopi ya vyeti vyako, nakwenda kubadili majina yote yanakua ya jule
mama"
"mmmmhhhh, sawa.... Lakini huyo mama ane hana watoto, si apumzike
tu alishwe na watoto wake"
"mmmhh mdogo wangu, mimi hata sijui... We
tutoe msaada tu"
"kwahio tunaanzaje, mana vyeti vipo
nyumbani"
"sasa hivi twende tukapige paspoti saizi kabla jua
halijazamia"
Aliongea shadya huku wakiamka na kuingia mlango wa pili
ambapo kuna kajistudio ka kupigia picha za paspoti saizi kwa dakika tatu...
Walipiga kisha wakatoka, na uzuri ni kwamba ilikuwa ni mida ya kufunga, hivyo
faima alifunga duka kisha wakapanda majaji mpaka huko kwao, ambako alikwenda
kumpa Cecilia kopi ya vyeti vyake ili kwenda kutoa msaada kwa yule mama... Siku
hio Cecilia hakulala, kwani alikwenda kila mahali kuhakikisha anabadili majini
ya vile vyeti ili kesho apeleke kwa boss kama mfanyakazi, sasa hapo ile ishu ya
vyeti hewa, anaye fanya kazi ni mwingine, na mwenye vyeti ni
mwingine,...
"ZUWENA RASHIDI SURIA... Hahahahahh safi
sana"
Shadya alilisoma jina hilo katika vyeti ambavyo keshavibadilisha
majina, na kama unavyoona hayo majina hapo juu, iko hivi
Ndoa
za zamani ilikuwa mwanamke akishaolewa hata jina la ubini wa familia yake
hubadilika, yaani atatumia jina la mume wake kama baba yake, lakini wakiachana
anatumia jina la baba yake kama kawaida,.. Huu mpangilio upo lakini kwa sasa
haufuatiliwi, unakuta mwanamke kaolewa lakini bado anatumia ubini wa baba yake
mzazi, ingali inatakiwa ubini unakuwa wa mume wake... Sasa kwenye vyeti hivi
ubini ni wa mume wake,.. Babu yake surian anaitwa SURIA... Na baba yake surian
anaitwa RASHID, na mama yake anaitwa ZUWENA,... Sasa kwenye vyeti yamewekwa hayo
majina yote matatu,....
Wakati huo huku kwa akina surian, yaani
kwa mama yake,.. Mama alikuwa akisali na kumuomba mungu afanikiwe kupata kazi,
kwani hali ya maisha yao yamekuwa mabaya mno, kula kwao kumekuwa kwa shida,
mtoto waliokuwa wakimtegemea ndio huyo kauza saluni, naye yupo nyumbani kawa mtu
wa kulia siku zote, mana kila anapo pita huambiwa kamuua ndugu yake ndio mana
anapata pesa nyingi... Mzee Rashidi naye kwenye maombi mana kiuhalisia kule kazi
imebuma, sasa shadya au Cecilia kaamua kupita chocho ili kumsaidia mama
huyo,..
"kazi leo imeendaje mume wangu"
Sauti nzuri ya
mwanadada maimuna au maimati kwa jina la uasili wake
"aah namshukuru
Mungu, kazi sio mbaya japo documents ni nyingi lakini zitaisha
tu"
Aliongea surian huku wakiwa kitandani katika hali ya
kupapasana,
"weeee mungu unantia kidole jamani, acha izo
baaasi"
Aliongea muna huku wakichezeana baadhi ya sehemu
zao,
"sasa chupi ya nini saa hizi jamani mke wangu"
"kwani
nimekataa kuivua?, kwanza kuvua chupi ni kazi yako sio yangu"
"mmmhhh
niache nilale mimi"
"jamani mume wangu, nina hamu ujue"
"si una
vidole wewe"
"duuuuuu, sasa vidole na hio nanii wapi na
wapi"
"niache nilale nimechoka eti mamuu"
"basi mume wangu, lala
tu... Najua leo umefanya kazi kubwa sana"
Kesho yake saa 12
kamili asubuhi surian pekee akiwa katika gari, kana kwamba leo kamuacha mkewe
nyumbani, sasa kaja kazini peke yake, ikiwa yeye ndio wa kwanza kuingia ofisini,
na akiingia yeye moja kwa moja anaingia ofisini kwake, na hayo ni masharti
ambayo kapewa na maimuna kuwa hahitajiki kuonekana na wafanyakazi wa kiwandani
mpaka siku saba ziishe ndipo aonekane, kwahio Cecilia ndio mfanyakazi wa kwanza
kuja ofisini kabla ya wote, kwani yeye ndio mapokezi kwa kila kitu na ndio wa
kufanya usafi wa ofisi nzima, hivyo katika wafanyakazi wanaomjua boss, ni
Cecilia peke yake,
Saa moja kamili Cecilia ndio anaingia
kazini,.... Alianza kufanya usafi katika ofisi mbalimbali ambazo bado hazijapata
wafanyakazi, hususan vitengo vya mameneja na wengine wengi ambao watapata vyeo
vya kukaa katika ofisi,... Mana kuna wafanyakazi wa ofisini na wafanyakazi wa
viwandani,
Saa tatu na madakika eneo la kiwanda lilijaa
waombaji wa kazi, yaani waliokuja kuomba kazi, walikuwa wengi sana wake kwa
waume,... Na hapo utachaguliwa kutokana na sifa za vyeti vyako,... Basi kazi ya
kuchukua vyeti na kupeleka kwa boss ilianza,... Cecilia hakutaka kuanza na vyeti
feki ambavyo mfanyaji kazi ni mwingine na vyeti ni vya mwingine,... Ilipofikia
kundi la kumi, hapo hapo Cecilia akaunganisha na zile documents za ZUWENA RASHID
SURIA,.. Sasa hatujui kama surian ataweza kutambua lolote kuhusu documents
hizo,..
Suria baada ya kupewa documents za watu watano, alianza
kukagua moja baada ya nyingine,...
"heeeeee faima kaja kuomba
kazi"
Surian alitoa macho huku akisema faima kaja kuomba kazi,.. Hio ni
baada ya kuona picha ya faima na ni kweli ni faima ambaye ni mchumba wake, na
wanapendana mno,... Ila wamepoteana baada ya surian kupelekwa ujinini na kukaa
zaidi ya miezi mitatu huko chini ya bahari ambako ndiko majini walipo,.. Sasa
toka arudi hajawahi kumuona wala kuwasiliana naye kwani yupo ndani ya ndoa, sasa
atawezaje kumpigia simu wakati ana ndoa.. Na anampenda faima kupita maelezo,..
Sasa baada ya kutahamaki picha, alikuja kutahamaki kwenye jina...
"eehh?
Kumbe sio faima... Lakini mbona hili jina ni la mama yangu,.. Inakuwaje
hapa"
Aliongea surian kwani jina la ZUWENA sio la mtu mmoja lakini
ukiunganisha na ubini wake, lazima likupe mashaka jina hilo
Alijiuliza
mwenyewe bila kupata majibu sahihi.... Aliangalia mara mbili mbili lile jina
pamoja na picha,.. Majina ni ya mama yake, na picha ni ya mchumba wake,.. Sasa
akaamua kuangalia barua ya mtu huyo,... Sasa alipoangalia kwenye sehemu ya namba
za simu, laaaa haulaaaa.... Surian aliamka katika kiti chake na kutaka kutoka
nje, wakati ni kosa la jinai kutoka nje, mana ataharibu masharti ya jini
maimuna.. Na nia yake ni kwenda kumuona huyo mtu mwenye documents hizi, ni
nani??????
Hakuna binadamu ambaye hampendi
mama katika hii dunia, hata wanyama hupenda mama zao,... Hata uwe jambazi kiasi
gani, huezi kumkaba mama na kumuua kikubwa tu labda amuibie hela, ila kumuua
hawezi, na ukiona binadamu kamuua mama yake, basi jua huyo hakuwa mama yake wa
kumzaaa... Kwasababu pindi unapotaka kufanya hivyo unashindwa,. Lakini mama yako
kabisa huezi kumuua...
Surian ni mtoto wa mwisho katika familia
yenye watoto wawili, akiwemo asha ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia hio,
wazazi wa surian waliwekeza pesa nyingi sana kwenye elimu ya mtoto wao ambae ni
surian, na ni kweli surian kasoma kwelikweli, yaani mpaka makampuni binafsi
yanaogopa kumuajiri kwani kutokana na elimu yake, anatakiwa kulipwa mshahara
mkubwa kuliko hata boss mwenyewe anavyo jilipa,.. Unajua mtu unasoma mpaka
unaogopwa kuajiriwa,... Surian akienda kuomba kazi huambatanisha vyeti visivyo
pungua kumi, ambavyo kasoma katika vyuo mbalimbali hapa nchini,.. Surian ana
madigrii mengi, mana kasoma baadhi ya vyuo vikubwa tu... Hivyo hapo kichwani
madigrii yamelala....
Sasa wazazi Waliwekeza Pesa zao katika
elimu ya mtoto wao,... Kwa bahati mbaya alikosa kazi nzuri, lakini kwa bahati
nzuri kapata mke mwenye asili ya ujini,... Mali zimekuwa nyingi mno, lakini
mbaya zaidi anapewa masharti ya msaada juu ya familia yake,.... Hivyo
anaruhusiwa kuiajiri familia yake ili ipate pesa ila sio
kuwapa,...
Sasa leo amefanikiwa kuliona jina ambalo mama yake
hulitumia, japo koo zipo nyingi lakini kwa mazoea yake alijua fika kuwa huyo
aliokuja kuomba kazi ni mama yake,... Lakini pia kama ni mama yake mbona picha
ni ya mpenzi wake, sasa inakuwaje hapo... Aliona wacha asome barua ya mtu
huyo,... Sasa katika kusoma akaona sehemu ya namba za simu haikujazwa, mana kama
ingejazwa angelimpigia simu mtu huyo,... Sasa surian kanyanyuka kwenye kiti kwa
hasira ili amwambie Cecilia kuwa kwanini huyo mfanyakazi hakuandika namba za
simu,... Sasa ile anataka kutoka nje,.. Akakumbuka kuwa haruhusiwi kuonekana nje
mpaka siku saba ziishe ndipo aweze kutembelea wafanyakazi wote, hivyo hapo
atawaajiri wafanyakazi kupitia vyeti vyao, na vipicha vyao, lakini sio kuwaona
hivi uso kwa uso...
Surian alirudi katika kiti chake baada ya
kukumbuka hilo,.. Alishika simu yake na kumpigia Cecilia
"hallow Ceci?
Njoo ofisini"
"sawa boss"
Alimuita Cecilia, na ceci alijua fika
kuwa anaitiwa zile documents za ZUWENA,...
"yes boss"
"huyu mtu
vipi huyu... Kaja mpaka hapo ofisini"
"ndio boss, kaja ila katoka kasema
anakwenda hospitali mtoto wake anaumwa"
"eeehh ana mtoto huyu
mtu"
"ndio, kwani vipi boss"
"hapana, nimeona hajaandika namba
za simu hapa kwanini hajafanya hivyo"
Suria Aliuliza hivyo lakini hapo
anatamani amuone huyo dada, sasa kuambiwa ana mtoto, akapunguza munkari, mana
faima yeye hana mtoto, tena ni bikra kabisaaa....
"aaahh samahani boss,
huyu msichana kasema hana simu"
"aaahh, sawa.... Ila akipata simu alete
namba ofisini kama zilivyo andikwa kwa wenzie... Na huyu nampa nafasi ya
kusimamia upande wa wanawake... Atakua supervisor (msimamizi). Jina lake ni zuri
sana... Hata sura yake pia, na hii ni sababu ya kumpa hio nafasi
sawa"
"sawa boss"
"ok kaendelee na kazi"
Basi surian
alilipenda hilo jina na kulipa nafasi nzuri ya kazi kwani lipo kama jina la mama
yake,.. Nzuri zaidi sura yenyewe pia ni kama ya mchumba wake, japo ni yeye
lakini surian hajui mana hio sura hapo ni ya faima,.. Na jina ni la mama yake
kweli
"duuuuu watu wanafanana, yaani kama faima vile... Ila
yote tisa.. Kumi ni hili jina, kama jina la mama yangu vile"
Surian
aliendelea kudiskasi hivyo vyeti na kufanya mfananisho
Huku kwa
Cecilia, sasa kichwa moto, yule mama kapata nafasi kubwa kama ile na istoshe
yeye alikuwa amsaidie amuweke mama wa usafi chooni,.. Mana akimuweka huko
kiwandani atagundulika mapema kwani boss lazima atembelee maeneo
hayo...
"sina jinsi, wacha nilinde ugali wangu, na niulinde ugali wa
mama yule... Atakaa nafasi ya usafi na mshahara wake atachukua ule wa
kiwandani"
Aliongea Cecilia kuwa mama huyo atafanya kazi ya usafi wa
vyoo vya kiwanda, mana huko chooni bosa hawezi kwenda... Hivyo pamoja na kuwekwa
huko chooni, mshahara wake sio ule wa chooni, atachukua mshahara wa kule
alikotakiwa kukaa, halafu sasa yule atakaye kaa kule kama supervisor (msimamizi)
atalipwa mshahara wa chooni, hivyo hio ishu ceci kaamua kuicheza yeye kama
yeye,... Na uzuri ni kwamba secretari yeye ndio aliopewa dhamana ya kutoa
mishahara kwa wafanyakazi,... Yaani analetewa kitita kisha atakaye kuja anakula
mshahara wake kama inavyo takikana, kwani pale anapopeleka documents kwa boss,..
Bosa anaziingiza kwenye kompyuta na kuandika kitendo au cheo cha mtu na mshahara
wake,.. Hivyo siku mtu anakuja kuchukua mshahara anaangaliwa kwenye kompyuta
analipwa kiasi gani kisha anahesabiwa.... Hapo mama surian keshapa kazi tena kwa
mshahara mrefu sana,.. Kwani kaandikiwa laki nne,... Na Cecilia kaapa kumpa yote
kwani ndio kitengo chake kilivyo ruhusu mshahara huo,....
Siku
ilikwenda vyema na leo walimaliza usaili wa watu wote, japo wapo waliokosa
kutokana na vigezo kuto kamilika, lakini waliokamilisha wote walipata
kazi,...
"Cecilia? Hakikisha mpaka wiki ijayo, wafanyakazi wote wawe na
NSSF sawa?"
"sawa boss"
"ok nakwenda, hakikisha unafunga vizuri,
na afu ivi kila mfanyakazi umemwambia kuwa Jumatatu ndio kazi
inaanza"
"ndio boss, wanazo taarifa hizo"
"ok
sawa"
"sawa boss"
Surian aliondoka,.. Kafanikiwa kumuajiri mama
yake lakini hajui kama kamuajiri mama yake mzazi, na mama pia hajui kama boss
wake ndio mtoto wake wa kumzaaa...
Sasa huku kwa akina aisha,
au kwao akina surian, ikiwa ni jioni ya saa 12, mama huyo akiwa anasali nyumbani
kwake,... Ghafla simu yake iliita mpaka ikakata kwani alikua katika ibada,...
Iliita tena mpaka ikakata...
Alipomaliza ibada aliiendea simu
yake na kukuta kapigiwa zaidi ya mara moja na namba ni moja iliomtafuta,...
Masikini ya Mungu salio hana,... Ghafla mumewe anaingia
"eeh Afadhali
baba suri umekuja.. Hebu nipe miatano nikapate vocha,.. Kuna namba ngeni
hapa"
"mke wanguuu... Unaomba maiti damu wewe"
"oohhh samahani
mume wangu,.. Sasa sijui huyu atakuwa nani"
Mara simu ikaita tena kwa
mara ya tatu,...
"eehhh huyu hapa kapiga tena.... Hallooo"
"eeh
Shikamoo mama"
"marahaba, ni nani mwenzangu"
"oohh naitwa
Cecilia ni sekretari wa kampuni ya MICCO (Moon Islamic Cloth
Company)"
"Miko ndio kampuni gani"
"ehehehe, pale ulipoleta
barua jana"
"aaaaaaaaaa, nimekumbuka, kile kiwanda cha nguo za
Kiislamu"
"haswaaaa"
"enhee mwanangu mpendwa niambie
jamani"
"Jumatatu njoo uanze kazi... Japo sio nafasi nzuri lakini naomba
tufanye kazi mama angu"
"wooooo ahsante sana mwanangu,.. Kiukweli
nitafanya kazi yeyote wewe ondoa shaka mpendwa wangu"
"sawa mama, njoo
jumatatu"
"ahsante sana mwali wangu... Kiukweli natamani uolewe na
mwanangu jamani, mana kwa msaada huu"
"hahahahahahaha... Mama bwana,
usijali"
"ooohhh mwanangu suria uko wapi mwanamke nilio mpenda ndio
huyu... Ahsante sana mwanangu"
"usijali mama"
"haya jioni njema
mwanangu"
"haya nawe pia"
Simu ilikata, kumbe wakati huo alikuwa
pamoja na faima, kwani faima alimuuliza kiwa vitu alivyo mpa vimesaidia? Ndipo
Cecilia akaamua kupiga simu kwa mama huyo
"weee mama kashukuru
huyoo"
Aliongea ceci huku faima akiwa na shauku ya kujua alichokisema
mama huyo, yaani laiti kama faima angejua kuwa huyo mama aliopigiwa ndio mama wa
mchumba wake, na vyeti alivyo vitoa, hajui kama katoa kwa ajili ya mama wa
mchumba wake..
"enhee, kasemaje"
"nakwambia ametamani niolewe na
mtoto wake sjui nani kamtaja jina kabisa"
"Weeeee,... Wamama nao
wakifanyiwaga wema tu, utasikia uolewe na mtoto wangu... Duuuu haya kaolewe
anti"
"mmmhhh Mwenzangu wee, mali ina wenyewe hii"
"mmhhh
niambie anti... Siku izi unanene tu"
"kawaida tuuu"
"mmmhhh
kawaida gani hii unene huo, ona shavu hilo"
Sasa huku kwa akina
asha, mama kapata furaha mpaka analia, kwa kumkumbuka mtoto wake,... Mana kama
angelikuwepo naye angelikwenda kuomba kazi kwenye kampuni hio, mana kutokana na
elimu yake ana uhakika angechukuliwa,... Mama hajui kiwa surian ndio boss mkubwa
katika kampuni hio,...
"sasa mambo safi kabisa baba asha... Kazi
imepatikana"
"tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema
zake..."
Aliongea mzee huyo ambaye yeye anaumwa, na toka astaafu kazi
kazi katika shilika la reli mkoani tanga, mpaka leo hana kazi wala haruhusiwi
kufanya kazi yeyote ile kutokana na ugonjwa, kwani kafanya kazi katika shilika
la reli kwa muda mrefu hivyo amepata maradhi juu ya kazi yake, anaugua henia kwa
muda mrefu hivyo inamsumbua...
Tukija huku kwa faima akiwa
kamsindikiza dada yake mtoto wa mama yake mkubwa Cecilia au shadya, sasa alikuwa
akirudi nyumbani baada ya kufunga duka ambalo anauza yeye...
"fey
mambo"
Alisikia salamu ilio ambatana na jina
lake
"poa"
Alikuwa ni tariki mwenye kumfuatilia fey kwa ukaribu,
na nguvu hio hupewa na zamina,.. Tariki naye ni mmoja kati ya wafanyakazi
waliopata kazi kwenye kampuni ya MICCO (MIKO) ila kwa faima anajifanya mtoto wa
mashavuni, ili akubaliwe...
"mbona kama huna raha pindi unionapo, au
nakukera Fey"
"yes, kwa kiasi flani unanikera"
"samahani kwa
hilo... Ila mtoto mzuri kama wewe sidhani kama una roho ya kumchukia mtu.. Mi
naona unasingiziwa tu"
"sema shida yako riki, kwani sihitaji kuongozana
na wewe usiku huu"
Aliongea faima kwani anamfahamu tariki ni mtu
anayetaka mahusiano na faima,..
"Kiukweli sina asili ya usanii, na
sihitaji kuwa msanii, ila neno langu kwako litakuwa wimbo kila
siku"
Wakati huo tariki akiongea hivyo safari ilikuwa ikiendelea, japo
fey hataki kuongozana, lakini kama vile kakubali flani hivi..
"enhee,
imba niskie"
Alionge faima kama kwa dharau, kwani anajua moyoni mwake
yupo aliojaa....
"najua neno nakupenda kwako umelisikia mara nyingi, ila
yote yana uzito wa tofauti tofauti... Je nakupenda yangu kwako ina uzito kiasi
gani Fey?? Nakupenda sana fey.. Niangalie basi, najua yupo umpendae, lakini kama
unavyosikia tetesi za hapa na pale kuwa mtu huyo kafariki dunia fey,...
Tumuombee huko aliko... Ila isiwe sababu ya kuninyima nafasi,.. Nahitaji kutulia
na mwenzi wangu... Nina pesa lakini sitaki kuliongelea hilo kwani wewe sio
mfanya Biashara kuwa tuzungumzie mambo ya fedha... Fey,.. Moyo unataka kuangua
huu.. Fanya jambo basi jamani... Mana pamoja na fedha zangu lakini haziwezi
kuzuia anguko la moyo wangu... Hebu ona... Ona sasa moyo huu hapa unachungulia..
Ona huo huo"
Tariki alibwabwaja maneno mia kidogo, ila hakuna aliopanda
mahindi akavuna mchicha... Kwa mara ya kwanza faima anatabasam kwa maneno mazuri
kutoka kwa tariki,...
Hakika wanaume ni watu wabaya
sana, wanaweza kumfanya mwanamke awe atakavyo, iwe kwa mapenzi motomoto au pesa
motomoto, mwanamke lazima ukae kwenye namba husika,... Faima aliokuwa mgumu kana
kwamba hata kuitika salamu kutoka kwa tariki, kwake ni ngumu, lakini tariki
kapiga domo mpaka fey katabasam kwa mara ya kwanza
"waalakhi
leo najipa ushindi japo sijafunga goli"
Aliongea tariki huku fey
akimuuliza riki kuwa
"wajipa ushindi wa nini"
"Kiukweli fey,
sikuwahi kuliona tabasamu lako, Kiukweli limenipa amani ya moyo na kuona kipo
kivuli katika moyo wangu, japo baado hakijasogea"
Aliongea tarikwa
maneno fulani ya uchombezaji,..
"mmhh una maneno riki,..."
"sio
maneno fey,... Ni moyo wangu hautulii kabisa bila kupata mwenza"
"bwana,
ebu niache niende nyumbani kwanza"
Aliongea fey kwani mahala walipofika
kuna njia ya panda ya kwenda kwao... Hivyo wata achana hapo,.
"ni sawa
fey, nipe imani juu ya makutano mengine"
"siwezi kukupa imani now coz,
siwezi kukuamini moja kwa moja... Nitakujibu swali lako"
Riki kusikia
maneno hayo moyo wake ulimpasuka na kuhisi bahati imemuelemea kuliko
wengine
"sawa madam fey,... Ila jua kwa sasa napata jua na hakuna
anayeweza kunipa kivuli, ispokuwa wewe fey... Wacha nikuache ili nikupe nafasi
ya moyo wako juu yangu... Bye, ulale salama"
"nawe pia"
Kwa sasa
fey hakuwa na majibu mabaya kqa riki, kwani keshajua ni mwanaume mwenye maneno
mazuri yaliomfanya kutabasamu kipindi kigumu kama hiki ambacho kampoteza mpenzi
wake,....
Baada ya tariki kuachana na fey, alikutana
na rafiki yake jumbe,
"we riki nini sasa"
"acha weweeeee....
Nani kasema mi nakataliwa... Mtoto keshaanza kuingia laini mpaka kalegea kama
papai"
"muongo riki"
"aahh... We baki na mineno yako, eti mi
muongo"
Aliongea riki akiwa na rafiki yake mr
jumbe,
BAADA YA SAAA.... SIKU.... KADHAA
KUPITA
Ikiwa leo ndio siku ya Jumatatu, ni siku rasmi ya
kufungua kampuni ya MICCO (Moon Islamic Cloth Company) Boss mkuu ambaye ni
surian akiwa katika ofisi yake, yaani yeye kuwa wa kwanza katika ofisi yake ndio
masharti ambayo kapewa ndani ya siku hizi za karibuni,.. Wafanyakazi walianza
kumiminika katika kampuni hio, walimu wa kufundisha wafanyakazi jinsi ya
kuzitumia mashine na kutengeneza mavazi maalum ya Kiislamu,.. Shadya au Cecilia
ambaye yeye ndio mwenye kujua nani akae wapi na nani akae wapi, kwani yeye ndie
alie wapokea na ndio mwenye kujua kila sekta ya mfanyakazi, hivyo walipangwa
wote na idara zote zikawa na watu,... Walifelea watu kadhaa tu, lakini
haikudhuru kitu chochote,
Walimu Walianza kazi ya kufundisha
wafanyakazi hao, jinsi ya kuanza kufuma uzi mpaka kuja kuwa nguo, ikiwa kiwanda
kimeanza na nguo za dini pekee,.... Surian akiwa ofisini kwake anaendelea kugawa
vitengo kwa wafanyakazi wa ofisini, yaani mameneja, wapokea oda, wahasibu na
wengine wengi ambao wana vigezo vya kukaa ofisini na sio
kiwandani,....
Mama yake surian akiwa kawekwa kwenye nafasi ya
chooni, na hio ni kwasababu tu asionekane kwakua umri wake hauruhusu kufanya
kazi katika kampuni hio,...
"samahani sana mama angu, Kiukweli nimefanya
juu chini niweze kujenga riziki yako,... Binafsi hata mimi Sitamani ufanye kazi
huku,.. Lakini nakuweka huku ili boss asikuone mana huku hawezi
kufika"
Aliongea shadya kama kumwelezea mama huyo ili asijiskie vibaya
kwakua umri wake hauruhusu kufanya kazi hapo
"usijali mwanangu, pia
nakushukuru sana kwa kunisaidia... Nitafanya kazi mpaka utajiskia raha
mwanangu.."
Aliongea mama yake surian huku shadya ama Cecilia akisema
kuwa
"usijali mama,.. Pia utakua ukijificha pindi unapohisi boss
anakuja, afu pia kwakua namba yako ninayo, basi pale nitakapo ona boss anakuja
huku nitakupigia haraka ili asikuone"
"sawa mwanangu, mimi nikiona tu
simu yako, nitajificha mwanangu... Mungu akuzidishie mama"
"usijali...
Na mshahara wako, utalipwa laki nne"
Aliongea shadya huku mama akibaki
mdomo wazi, mana anajua kazi ya kusafisha choo hua haina malipo mazuri sasa
anashangaa atalipwa laki nne ingali sio pesa kubwa lakini kwa maisha yao yalivyo
magumu kwa sasa, hio pesa kwao ni kubwa sana... Na kama unakumbuka huo mshahara
sio wa mfanyakazi wa chooni, bali jina la huyo mama lilipewa kipau mbele cha
kusimamia wafanyakazi huko idarani, lakini kwakua umri wake hauruhusu kufanya
kazi, hivyo ili boss asimuone ilibidi amueke huku chooni, kisha atafute msichana
mingine ampe nafasi ya idarani...
"mwanangu, ina maana nitalipwa pesa
yote hio"
"hehehehe mama bwana, Usijali hio ni pesa ndogo na pia
ukifanya kazi vizuri utaongezewa mshahara"
Aliongea shadya lakini mama
huyo bado haamini kwa malipo ambayo analipwa, ikiwa ndio mshahara wa Kwanza wa
kazi yake...
Mama alitaka hata kupiga magoti kwa
kushukuru,....
Shadya alikwenda idarani na kumweka msichana
mwingine kwenye idara aliotakiwa kukaa mama yake surian,
"kazi yako ni
kusimamia wafanyakazi na kuhakikisha wanatoa bidhaa bora na zenye uwingi unao
hitajika"
"sawa dada, nitafanya kazi kadri ya uwezo
wangu"
Aliongea dada huyo huku shadya akimtajia mshahara
wake
"utalipwa laki moja na themanini, ikiwa ndio mwanzo wa
mshahara"
"waoooo, ahsante sana dada... Nashukuru sana kwa kupata
mshahara mzuri"
Dada huyo alifurahi sana,.. Sasa mshahara huo ndio wa
mtu wa chooni, na ule wa kitengo chake ndio ule analipwa mama yake suria,...
Yaani hapo kuna mgeukano wa kazi na mishahara yao,...
Basi kazi
zilienda vizuri na kila mfanyakazi alishika kitengo chake huku akifundishwa
katika mashine yake,.. Kiwanda ni kikubwa sana kana kwamba mpaka sasa kina
wafanyakazi mia nne tu, hivyo bado wafanyakazi takribani mia moja ili kufikia
idadi ya wafanyakazi mia tano,
Ofisini wakiwa wamesha kamilika
wafanyakazi 21, akiwemo mmoja ambaye ni mfanya usafi katika ofisi na vyoo vya
ofisini,... Ila choo cha ofisi ya boss kipo ndani ya ofisi yake na hua mkewe
ndio kaamua kumfanyia usafi mume wake, hivyo ofisini kwa surian, atakuja kufanya
mkewe peke yake.... Kumbe hata majini wana wivu na wanaume kiasi hicho, kwani
hakutaka kutoa nafasi kwa mume wake afanyiwe usafi ofisini kwake,... Hivyo
mfanya usafi ataishia nje ya ofisi ya boss na hatakiwi kuingia ndani,.. Hio sio
masharti bali ni wivu wa jini maimuna
Jioni saa kumi na moja
mama asha akiwa nyumbani kwake anapiga stori na familia yake, wakiwa watu watatu
tu, mana walikuwa wanne pamoja na surian, lakini kwa sasa wapo watatu mana
surian katoweka nyumbani hivyo hawajui kama kafariki au yupo hai.. Lakini kwa
sisi wasomaji tunajua surian yupo hai na mama huyo anafanya kazi kwa mtoto wake
bila kujua,...
"yaani bana asha, nalipwa mshahara mkubwa jamani,
haaaaa... Yaani mpaka natetemeka"
Aliongea mama huyo huku mzee Rashidi
ambaye ndio baba yake surian akiuliza kuwa,
"kwani kitengo gani
wamekupa"
"baba asha, kwani mimi nimetaka Mashauzi, mimi nafanya usafi
wa chooni"
"haaaaaaaaaa, mama muongo... Ina maana mfanya usafi wa chooni
ndio alipwe pesa yote hio"
Aliuliza asha huku mzee rashid akianza
kuogopa kana kwamba labda mkewe kapendelewa kutokana na mwili wake, mana mama
surian pamoja na umri mkubwa alio nao lakini anazeheka na umbo
lake,...
"kwahio mama asha, unalipwa laki nne afu unadeki
vyoo"
"ndio baba, asha"
"uuuuufyuuuuuuuuuu"
Baba asha
alipumua kwa kuchoka na kujua mkewe keshajilipua na vijana mana, mama yake suria
kama ni wale wamama wasio jielewa, basi ndio ule wakati wa kuchukua vijana
wadogo, japo ana umri mkubwa lakini uzuri na umbo, ni kama bado anavyo,.. Na
yote hio ni kwasababu ya matunzo alio tunzwa na mume wake, kwa umri huo kijijini
ni mzee wa miaka 70, lakini kwakua yupo mjini basi anakuwa anakwenda na umri
wake....
"baba asha, mbona umepumua kwa nguvu hivyo"
"aaaaa
tutaongea usijali"
Aliongea mzee huyo huku mama asha akiwa na wasiwasi
kuwa mume wake anataka kusema nini,
"asha mwanangu, naskia nafasi bado
zipo, kwanini nawe usiende mwanangu..."
Aliongea mama huyo kuwa kwanini
asha asiende kuomba kazi,
"aahhh mama, hebu wacha kwanza nitulize akili
yangu kwanza mama... Mana sasa hivi hata simu yangu nimeuza na laini nimetupa
mana staki mawazo"
Aliongea asha huku mzes rashid akisema
"huyu
mtoto ana kichaa huyu, yaani kauza na simu afu laini katupa"
"baba asha,
huezi jua... Haya wewe asha kwanini ufanye hivyo"
"mama.... Yaani kwenye
group letu la wasapu nasemwa mimi tu, meseji zinakuja naambiwa mimi muuaji...
Sitaki kabisa mimi sitaki"
"lakini ni bora ungezima simu
tu"
"msijali, nitakwenda kuomba kazi ila sio leo"
"sasa kama sio
leo mwanangu, nafasi si zitajaa"
"kama sio riziki yangu baba, hata
nikienda sasa hivi sitapata"
"lakini ni vyema kuwahi"
"basi
nitakwenda wiki ijayo"
Aliongea asha kuwa kakubali kwenda kuomba kazi
wiki ijayo,.. Sasa lile agizo la maimuna kumtaka surian aajiri familia yake ndio
linakwenda kutimia,...
"habari za kazi mume
wangu"
Maimuna au maimati alimsalimia mume wake huku akimvua tai, mana
suria yeye ndio wa kwanza kuingia kazini na ndio wa mwisho kutoka kazini,
hatakiwi kuonwa na mtu yeyote yule ndani ya wiki hizi za karibuni,....basi suria
alikwenda kuoga kisha akapata chai ili kusubiri chakula cha jioni, wakiwa wawili
tu na mke wake,.... Sasa wakati surian kakaa kwenye sofa akipata chai, na mkewe
akiwa jikoni anafanya mambo ya chakula cha jioni,.. Ghafla alianza kushikwa
shikwa nyuma ya shingo yake....
"mke wangu acha utani... Hebu kapike mi
nataka kulala"
Aliongea surian,... Lakini na huku jikoni, maimuna naye
kuna kitu kahisi ndani ya nyumba yake,... Huku sebuleni, surian anazidi kushikwa
na anaemshika yupo nyuma ya sofa, na kwakua suria anajua ni mke wake hivyo
katulia na kusapoti kushika mkono wa huyo mwanamke ambaye anamshika,... Lakini
surian kuangalia huo mkono, laaaaaaa
haulaaaaaa
Kabla ya siku
hio nyakati za jioni katika himaya ya majini wema ndani ya bahari,.. Sio majini
wote wa ndani ya bahari ni wema, wengine ni wabaya, ila kundi hili la akina
shaimati na maimati, wao ni kundi la majini wema, ama wazuri, wasio na tabu na
mtu,....
Sasa siku hio shaimati alikuwepo nje akiwa kama
malikia wa eneo hilo baada ya murati Sabaha kukiuka masharti yalio wekwa dhidi
ya binadamu na majini, sasa malikia wa majini katika himaya hio ni Murati
shaimati (shamimu).... Sasa siku ya leo Aliweza kumkumbuka ndugu yake au jini
mwenzie ambaye kwa sasa anakula raha ndani ya ndoa yake, na hayupo tena katika
himaya hio, japo anaruhusiwa kwenda kusalimia....
"nimemmisi maimati
wangu jamani"
Ilikuwa ni sauti ya shaimati akiwa chumbani kwake, na
nyakati hizo zilikuwa ni za usiku wa saa sita, kulilindima baridi kwa kiasi
fulani,...
"naweza kwenda hata kumuona angalau kwa macho
tu"
Aliongea shaimati akiwa pekee hapo chumbani kwake, kwani hakua na
mtu wa Kuzungumza naye,.... Haikupita hata dakika moja shaimati kapotea katika
mazingira ya kutatanisha, kana kwamba kaelekea duniani kwa nduguye
maimati,...
Kama kawaida yao au kanuni na masharti yao wao
wenyewe kuja duniani kila saa nane za usiku, haijalishi unakwenda kwa ubaya ama
kwa uzuri,.... Majini karibu wote wamepewa uwezo mkubwa, ingali wanatofautiana
nyenzo kwa wale wazuri na wabaya,.... Shaimati hakuwa na muda wa kufikiri kuwa
maimati anaishi wapi, kwani wao wana uwezo wa kunusana popote pale walipo, na
mbaya zaidi nyumba ya maimuna au maimati haipo mbali sana na bahari ambayo wao
hutokea, hivyo ilikuwa ni rahisi sana kwa shaimati kujua wanapo
ishi....
Ikiwa ni saa nane usiku shaimati akiwa nje ya jengo la
ndugu yake ambaye ni maimuna,....
Na wakati huo huo maimuna
alikuwa akipata raha zake toka kwa mume wake,.... Na mbaya zaidi naye kagundua
kuwa shaimati yupo nje ya jengo hilo ambalo yeye yupo kwa ndani na wakati huo
alikuwa katika hali ya kufanya mapenzi na mume wake ambaye ni
surian....
Sasa maimati kumbe anapenda sana ndugu yake au jini
mwenzake aje kuolewa, mana mpaka sasa hajui hata raha ya mapenzi ipoje,... Sasa
maimuna akaanza kulia milio ya msisimuo ambayo inaweza kumfanya shaimati
kuyatamani maisha ya ndoa, hivyo maimuna akazidisha milio ya kimapenzi kwa
makusudi ilo shaimati asikie naye aitamani ndoa ili wote wawe wamesha olewa,
mana kule ujinini sio wengi ambao wana asili mbili, na shaimati na maimati ni
majini walio shibana...
Kweli zile sauti taamu ziliweza kupenya
kwenye masikio ya shaimati, hivyo akajikuta anaanza kutega sikio ili kusikia ni
utamu wa aina gani ambao ndugu yake huupata kila usiku wa saa nane,... Sasa
shaimati alikuwa akihisi baridi, lakini ghafla akaanza kuhisi joto, kana kwamba
sauti tu inampa joto, je kama angelikuwa shughulini ingelikuwaje,.. Na wakati
huo maimuna anazidi kulia milio ile ya hatari hatari, yaani ile ya kumtoa nyoka
pangoni... Shaimati alipotea pale nje haikujulikana kaelekea
wapi,
Kesho yake asubuhi sana nyakati za saa 12 na nusu, surian
ndio wakati wake wa kutoka nyumbani ikiwa anamaliziwa kufungwa tai na mke wake,
na siku hio mke hakuwa tayari kwenda kazini,... Na surian anawahi kazini ili
asionwe na wafanyakazi wake kwani kuna masharti kawekewa na mke
wake,...
Ilipofika nyakati za macha shaimati aliingia ndani kwa
maimuna, alimkuta anasoma kitabu cha dini, mana hana pakwenda kwa nyakati
hizo,
"heeeeee shamimuuuuu... Karibu"
Maimuna alimkaribisha
mwenzie kwa furaha na kujifanya jana hakumhisi kuja kwake,... Sasa kila mmoja
anajua kuwa usiku wa jana hakujulikana, hivyo ndivyo ilivyo kwa majini, huyu
kajua kuna jini mwenzie nje, lakini yule wa nje hajui kama kajulikana ndani, na
yule wandani kajua kuwa kuna jini nje lakini hajui kama kajulikana kule
ndani.... Hivyo ndivyo ilivyo kwa majini,
"ahsante, heeeeee
munaa umenenepa jamani"
Aliongea shaimati kama kumsifia maimuna kwani
ilionekana hali ya mwili wake kuwa mkubwa kiasi fulani,
"mambo ya ndoa
hayo"
"mmmmhhh kwa unavyo yasifia mhhh"
"sasa nisi yasifie
kwanini? Mana nipo ndani ya ndoa, na nimejua utamu wake na raha
zake..."
"mmmhhh hongera yako mwenzangu"
"haya niambie,
hawajambo huko kwetu"
Shaimati aliuliza hali ya ujinini kuwa
hawajambo
"aahh nadhani wote wamekumisi sana, ila mimi nimetoka kwa
kutoroka ujue"
"weeeeee, sasa wairati sarika akijua itakuwaje shaimati?
Hebu nenda bwana"
Maimuna alimtaka jini mwenzie aweze kurudi ujinini
kwani alitumia njia ya kutoroka usiku ule,
"nitakwenda,.. Lakini nami
nimejikuta nayatamani maisha ya duniani"
"sawa lakini unatakiwa upewe
ruksa ya kuja kuishi duniani"
Aliongea maimuna huku shamimu akiwa
hatamani kurudi ujinini....
"Kiukweli shamimu nahisi upo huru huku
duniani, Kiukweli nayatamani maisha yako ambayo unaishi...."
Aliongea
shamimu huku akiangaza macho huku na kule na kuiona picha ya surian iliopo
ukutani
"waooo shem wangu huyu"
Aliongea shamimu huku
akiisogelea ile picha na kuishika shika, kitu ambacho maimuna hakukipenda,
kwasababu alihisi shamimu angemtamani mume wake,...
"shamimu? Naomba
utoke tafadhali"
Aliongea maimuna huku akiwa kakasirika kwa kitendo cha
shamimu kuipapasa picha ya surian kimahaba
"unanifukuza nyumbani
kwako"
"sina maana hio, ila kuna hisia za ujinga mbele ya uso
wako"
Aliongea maimuna huku shamimu akijibu
"ni kweli, sikua
nikitamani mwanaume kamwe... Lakini sauti za jana, zimenifanya nami nivute hisia
kali na kujiuliza ni raha gani ambazo unazipata usiku wa saa
nane..."
Aliongea shamimu ambaye ni jini mwenzie na maimuna, na wote
binadamu kwa majini... Yaani wana asili mbili...
"ni sawa, lakini jaribu
kutafuta wako"
Aliongea maimuna jambo ambalo limemchekesha sana shamimu
huku akisema
"kwani wewe huyu ni wako"
"una maana
gani"
"mchumba wa mtu huyu... Hapa umempokonya mwanamke mwenzio tunda
lake... Sasa limekuwa lako, wakati ulilichuma kwenye mti wa
watu"
Aliongea shamimu huku maimuna akiwa hataki kuyajali maneno
yake
"ok sawa, hata mimi nililijua hilo... We nenda nyumbani kwetu... Na
pia nisingetamani kukuona kwa wakati mwingine"
Maimuna aliamua kama ni
mbwai iwe mbwai, lakini sio kwenye swala la mume....
"sawa, nakwenda,
lakini kaa ukijua kua, mti wenye matunda ndio hupigwa mawe"
Aliongea
shamimu kisha akapotea katika mazingira ya kutatanisha, kana kwamba tayari
wamesha anza ugomvi kati ya wawili hawa kisa ni mwanaume mmoja
tu,.....
Sasa ilipofika nyakati za jioni, surian akiwa kaketi
katika sofa akipata chai safi kabisa.... Na wakati huo katoka kuoga, lakini
katika kidole chake hakukua na pete,... Ghafla shamimu alitokea nyuma ya surian
na kuanza kumshika shingoni, tena ile kimahaba.. Surian kwa akili yake alijua ni
mke wake, mana wanaishi wawili tu na yeye hana nguvu au uwezo wa kujua kuwa kuna
jini mwingine kaja... Sasa surian akawa anaushika ule mkono kwa nia ya kusapoti
mshiko mshiko wa mkewe,.. Japo alikuwa akimharakisha akapike kwani anataka
kulala... Na wakati huo kule jikoni, maimuna naye keshajua kuwa shamimu yupo
mdani, sasa hakutaka kutoka mapema ili ajue shamimu kampenda mume wake kweli au
alitania... Hivyo akachelewa kutoka na kubaki kuchungulia kwenye upenyo wa
mlango,... Aliweza kuona jinsi surian anavyo shikwa shikwa kimahaba na wakati
huo suria anajua ni mkewe kwakua yupo nyuma ya mgongo
wake
Lakini surian kuangalia huo mkono, laaaaaaa haulaaaaaa,
kumbe hakuwa mkewe... Na aliujua vyema na kukumbuka, siku ile ya Kwanza
kupelekwa ujinini alishikwa mkono na huu mkono, hivyo alipo uona tu akastuka na
kuamka... Alikuwa ni shamimu,.. Na pale pale maimuna akatokea
"shaimati,
hivi ni tabia gani umeanza... Mbona asili yetu hatupo hivyo ndugu
yangu"
Aliongea maimuna tena kwa upole wa hali ya juu...
"yaani
kitendo cha kumshika mumeo, joto nililo pata... Sijawahi kulipata toka kuzaliwa
kwangu.... Ila narudia tena MTI WENYE MATUNDA NDIO WENYE KUPIGWA MAWE...
Nakwenda, lakini jua kuwa umedungua tunda la mtu, hivyi sio
lako"
Aliongea shamimu kisha huyoo akapotea,... Maimuna alikasirika sana
kwa kitendo ambacho shamimu kakifanya,
"surian mume wangu, kwanini
hujavaa pete yako...."
Muna alilia na mume wake kwanini hakuvaa pete
ambayo kapewa, mana kama surian angelikuwa na pete basi shamimu asingeliweza
kumsogelea kamwe,...
"samahani mke wangu,... Nami nilijua ni wewe ndio
upo nyuma yangu na ndio mana nikawa nimetulia... Basi nakwenda
kuvaa"
Aliongea surian kisha akaingia chumbani na kuivaa PETE YA KIKE,
ambayo ndio msaada wake juu ya viumbe vibaya na hata vizuri,.. Kwani shamimu ni
kiumbe mzuri lakini amekuwa na tamaa ya mapenzi ingali mwanzo hakuwa hivyo....
Ila jambo hilo analijutia sana maimuna kwa kuongeza milio ya mahaba ilio mfanya
shamimu kupata hamu
Kesho yake, kama kawaida surian akiwa
kazini ikiwa ni mida ya saa nne za asubuhi,... Kwa ukawaida hatakiwi kutoka
ofisini hapo mpaka siku 17 ziishe ndipo anaruhusiwa kuonwa na wafanyakazi
wake... Leo mkewe kaja kazini hivyo ndie mwenye kutembelea wafanyakazi
kiwandani,.. Wafanyakazi wenyewe wanabaki mdomo wazi kwani maimuna ni mzuri
mithili ya malaika, hata wanawake wenzie walikuwa wakimshangaa mwanamke huyo
ambaye ndio mke wa boss wao...
Tukija huku ICC ambako ndipo
faima anapo fanyia kazi kwa kufanya mauzo ya nguo za Kiislamu,... Baada ya
kufanya biashara na wateja alio kua nao, sasa katulia huku akiwa anafungua simu
yake,... Kuna namba ya simu alikuwa akiitafuta na kuipata
"RIKI, hivi
utakuwa mkweli kwangu... Kiukweli naogopa kuumizwa katika mapenzi,.. Sihitaji
pesa zako wala uzuri wako.. Nahitaji mapenzi ya kweli ila nahitaji
ubadilike"
Aliongea faima bada ya kuiona namba ya Riki ambaye ni
mwanaume aliotokea kumpenda sana hivyo hapo kaitafuta namba ili aweze kumpigia
simu amkubalie....
Lakini kabla hajapiga, alifungua upande wa
picha, zake na kuangalia picha ambazo alipiga akiwa na surian,.. Kitendo ambacho
kilimtoa machozi kwa mara nyingine tena, hivyo inaonekana anamkubalia tariki ili
ampunguzie tu mawazo, ila aliopo moyoni ni surian japo anasikia kafariki
dunia....
"mwaahhh,.. Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, sitokaa
kukusahau surian wangu... Nakupenda kuliko hata ninavyo jipenda... Sijakusaliti,
ila nakwenda kumpata mwenzangu atakaye nipotezea mawazo yangu... Nakupenda sana
mume wangu, japo nasiki umefariki dunia... Mungu akulaze mahali pema peponi...
Amen"
Aliongea faima baada ya kuangalia picha ambayo walipiga
pamoja,... Faima aliweka simu sikioni, alimpigia tariki ili amkubalie ombi
lake,... Na simu ilianza kuita.... Ilipokelewa
"hallow Riki Asalam
Aleykh"
"waaleykh msalam, vipi hali"
"salama tu"
"haya
niambie bibie, nina furaha sana kuiona simu yako nyakati hizi"
"ndio...
Vipi upo bize sana"
"hapana, hapana, hapana,... Sipo bize.. Nipo ofisini
hapa kuna baadhi ya documents nazi saini"
"basi nitakwambia baadae
Ukimaliza"
"nooooo niambie sasa hivi.... Usiutese moyo wangu kwa
madakika machache yajayo"
Aliongea tariki na kujifanya mtu wa busara na
mwenye pesa....
Lakini sasa faima kabla hajaongea, alishangaa
kusikia sauti ya kike hapo nje ikisema kuwa....
"surian wako yupo
hai"
Faima alikata simu haraka ili kuangalia hapo nje ni nani kataamka
maneno hayo,...
"waaaaaaoooooo.... Dada shamimu, ulienda
wapi"
Ikumbukwe kuwa shamimu na faima walijengaga urafiki wakati ule
walipokuja kutafuta MWANAUME MSAFI, na faima alitoboa siri ya yeye na surian
kuwa wao hawajawahi kufanya mapenzi, ndipo shamimu akaanza kumfuatilia mchumba
wa faima kwasababu ndio aina ya mwanaume waliokuja kumtafuta, hivyo faima
anatakiwa kumlaumu shamimu mana shamimu ndio kasababisha surian kwenda
ujinini
"mbona nipo jamani fey"
"hapana bwana dada,... Karibu
miezi mitatu minne hivi sijakuona"
"aahh si unajua mambo ya kazi
fey"
"ni kweli,... Haya niambie dada shuu"
"nipo... Mbona kama
ulikuwa unalia"
"we acha tu dada shuu,... Ni mwezi wa tatu kama sio wa
nne, surian wangu sijamuona, naumia sana..."
Aliongea faima huku akilia
na kumuegemea shamimu....
"mbona surian yupo na hata jana
nilimuona"
Shamimu katumbua jipu lililoiva....
"unasemaje dada
shuu"
"surian wako jana nilimuona... Na jinsi ya kumpata ni rahisi
sana... Ila unatakiwa kuwa mpole, mvumilivu, mnyenyekevu, na mwenye
utulivu..."
"sawa dada shuu... Nipo tayari kutii vigezo vyote,.. Hebu
niambie... Nampataje na yupo wapi kwasasa"
Faima aliuliza kwa umakini
huku akiwa katoa macho
"unaijua kampuni mpya inayotengeneza nguo za dini
hapa mkoani Tanga"
"ndio.... Si hii inayo itwa
MICCO"
"yeeees.... Mmiliki wa kampuni hio ni surian na mke
wake"
Faima kashtuka kwa kusikia neno SURIAN NA MKE WAKE
"hivi
umesema surian peke yake au surian na mke wake"
Katika
maisha haya hakuna kitu kinauma kama kusikia ya kwamba mtu umpendae ameoa au
kaolewa, inauma sana,....
Faima alipatwa na mshangao wa hali ya
juu baada ya shaimati kumpa ukweli wa mambo,.. Faima ametokea kumpenda surian
toka moyoni mwake, na kajitunza mpaka kesho kwa ajili ya suria, siku zote
husikia kuwa suria kafariki dunia tena kwa kuuwawa na dada yake,.. Leo anasikia
kuwa suria ndio mmiliki wa kampuni mpya iliofunguliwa hivi karibuni, shaimati
pia hakutaka kumficha kuwa suria keshaoa japo kaoa mwanamke ambaye sio asili
yake,...
"hivi umesema surian peke yake au umesema surian na
mke wake"
Faima aliuliza kwa mshangao wa hali ya juu,
"faima,
surian bado ni wako tu.. Ni kweli surian kaoa, lakini bado ni haki yako
kwasababu haki za kibinadamu zikiingilia kati, nina uhakika aliokuwa naye
atachukuliwa hatua za kisheria, japo hawato muweza"
Aliongea shaimati na
yote hio ni kwasababu ya wivu wa mapenzi, hivyo kaona kuliko maimuna afaidi
mwenyewe, bora tunda hilo lirudi kwa aliekua nalo awali,...
"una maana
gani dada shuu, ina maana nu kweli surian kaoa"
Aliendelea kulia
msichana faima huku shaimati akijihisi kua na raha sana kwani tayari
keshalitumbua jipu
"ndio, ila kuoa kwake sio tatizo, mana anamilikiwa na
kiumbe kama mimi"
Faima alishtuka sana kusikia kua suria anamilikiwa na
kiumbe kama huyu, kana kwamba rafiki yake huyo sio binadamu bali ni
kiumbe,...
"una maana gani? Ina maana wewe sio
binadamu"
Aliongea faima lakini shuu ama shamimu alimjibu
"mimi
ni nusu ya binadamu, ila ni mapema mno kunifahamu"
Shuu alijibu kisha
akaondoka zake kwa hatua za kawaida tu, wakati huo faima anamwangalia tu mpaka
akapotelea uchochoroni,...
"mbona sielewi, au naota
mie?"
Fey alijiuliza mara kadhaa kua huenda ni ndoto labda ndio imemjia
mchana huo... Lakini aliamini haikuwa ndoto bali ni ukweli
mtupu
Huku nyumbani kwa mzee Rashidi akiwa na mtoto wake asha,
mana mama kaenda kazini, sasa baba ana wasiwasi na mke wake kwasababu kitengo
alicho kipata hakiendani na mshahara ambao analipwa mkewe
"mwanangu
asha, hebu fanya hima ukaombe kazi pale... Mimi nina wasiwasi na mama yako...
Ina mana hata wewe inakuingia akilini hio.. Mfagia vyoo alipwe laki nne,..
Hapana.. Hebu kaombe kazi mama"
"baba, mi najua mama hana lolote ni
wasiwasi wako tu baba... Mimi nataka nikaombe wiki ijayo"
"aahhhh sawa
mimi sina wasiwasi sana, ila inawezekanaje Mfagia vyoo alipwe laki
nne"
"huezi jua baba.. Ni bahati ya mtu tu"
Wakati huo asha
akipika chakula cha mchana,.... Ghafla mlango unagongwa, asha akaacha safuria
ichemke, akaenda kufungua mlango..
Hakuamini kumuona
shamimu
"haaaaaaa jani shuu, mambo"
"poa, mbona umebadilika
hivyo, ulikuwa unavaa vizuri, unajisitili sasa mbona
umebadilika"
Aliongea shamimu mana alimuacha akiwa anapiga hela na
anajua kwanini alikuwa akipiga pesa....
"we acha tu shuu, yaani ulipo
niacha biashara yangu ilikuwa nzuri, lakini pia ilikuja kuwa mbaya baada ya
kusikia kuwa mimi nimemuua mdogo wangu, Kiukweli sikua na raha
kabisa"
"wewe umemuua mdogo wako? Kwani una ndugu
wangapi"
"mmoja tu"
"sasa umemuua yupi tena"
"aahh bwana
tuyaache hayo... Mambo mengine vipi"
"safi tu... Vp surian
yupo"
Shamimu aliuliza makusudi japo yeye ndio anajua surian
alipo
"aahh sasa shuu, si ndio nimekwambia hapa surian hayupo, yapata
miezi minne sasa na ndio mana nimeambiwa nimemuua ili nipate
pesa"
Aliongea asha huku akitaka hata kulia,
"sikiliza asha....
Ile pete, ndio ilikuwa sababu ya biashara yako kuwa nzuri, na kama ni surian
mbona yupo... Na hata jana nikua naye usiku"
Aliongea shaimati lakini
asha kwa hasira na ghazabu za kujua kua shamimu anaongea uongo, kwani surian
hawezi kuwepo mjini bila kuja nyumbani kwao, tena kwa jinsi surian anavyo mpenda
mama yake, hawezi kaa hata siku moja bila kuja,..sasa leo anasikia ya kua surian
yupo tena hata jana alikuwa naye....
"asha.... Asha... Njoo basi
rafiki"
Shamimu aliita lakini asha hakutaka kusikia kwani alichokisema
shuu ni uongo mtupu, na hatamani kuusikiliza tena,... Basi shaimati aliondoka
zake baada ya kujua kuwa asha kagoma kuongea naye... Nia ya shamimu ni kutangaza
uwepo wa surian, ili amkomeshe jini mwenzie ambaye anapata raha kupitia mtu
huyo,
Ilipofika mida ya jioni mama asha akiwa nyumbani baada ya
kurudi kazini, na kila akirudi kiuno humuuma kwa vile anavyo inama kila wakati
kwa kusafisha vyoo, mana vyoo hivyo huchafuka kila wakati,.... Mama asha akiwa
nyumbani akifanya maandalizi ya kupika chakula cha mchana, na hapo alikuwa
akimpa stori mtoto wake asha
"wewe ungekuja kuomba kazi mwanangu,...
Wasichana wenzio wapo wamejaa tele, yaani wamama hakuna kabisa"
Aliongea
mama huyo huku asha akiwa na msimamo wake kuwa atakwenda lakini ni wiki
ijayo
"nitaenda mama"
"tena naskia skia huyo boss ni
mtotoooo"
"heeeeee mama,.. Kumbe ndio mana baba ana wasiwasi, haya hivyo
umevijuaje"
"si wafanyakazi walio muona wanasema"
Mara fsima
kaingia huku akiwa na furaha kwa kitendo cha kusikia kuwa surian ndio mmiliki wa
kile kiwanda cha nguo za Kiislamu...
"heeee mwali wangu huyooo karibu
mama"
"ahsante mama, shkamoo"
"marahaba mwali
hujambo"
"sijambo, shkamo wifi asha"
"marahaba mambo
fey"
"poa...."
Lakini kabla faima hajaanza kusema, ghafla mama
asha kaanza kusema kuwa
"hivi faima mwanangu... Mbona hujaenda kuomba
kazi kwenye kile kiwanda kipya... Yaani wasichana weeengi wapo
humo"
Aliongea mama huyo huku faima akiuliza
"kwani wewe umepata
kazi"
"ndio"
"boss wa kampuni hio unamjua"
Faima
aliuliza makusudi tu mana kaambiwa kuwa boss wa kampuni hio ni
surian
"ndio tena ni kijana mdogo tu"
"aahhh nitakwenda kuomba
tu"
Sasa faima kajiuliza sasa kama mama mtu anafanya kazi huko na kamjua
boss, ina maana shamimu kamdanganya kuwa surian ndio mmiliki wa kiwanda
hicho,....
"nendeni, hata sasa hivi nilikuwa namwambia wifi yako hapa...
Aende ili tupate pesa nzuri"
"sawa mama nitakwenda"
Faima
alianza kupata huzuni tena mana kaja kutoa taarifa kuwa surian yupo pale, sasa
anakuja kujua kumbe mama mtu anafanya kazi hapo, sasa kama ni kumuona si
angemuona kabla,... Faima akatulia tu wala hakuongelea swala la surian tena mana
ataanza kuliza watu,... Ila katika moyo wake alimlaumu sana shamimu kwani
kamdanganya vikubwa sana kuhusiana na mchumba wake,....
Sasa
tukija huku nyumbani kwa akina surian akiwa jirani na mkewe wakiwa wamebanana
kwenye sofa moja,.. Surian kasahau kama anatakiwa kwenda kuiona familia yake,
kasahau kila kitu,...
"mme wangu,... Nina jambo nahitaji
nikwambie"
Aliongea maimuna huku surian akiwa
makini
"niambie"
"nina mimba"
"aaaaaacha utani
muna"
"kweli vile"
"umepima saa ngapi na wote tulikuwa kazini
leo"
"mimi sina cha kupima... Ina maana umenisahau"
"aaahh
hapana sijakusahau mke wangu, ila sikufahamu kwamba hata mimba mnaweza
kuzifahamu bila kupima"
"uwezo tulio nao ni mkubwa sana,.. Na hata hapa
baada ya miezi miwili tuna uwezo wa kujua hata jinsia ya mtoto
wetu"
"ole wako awe wakike, atakuwa sio wangu huyo"
Aliongea
surian huku wakifurahia swala hilo, mana ni muda mchache tu hata mwezi hakuna
toka kufunga kwao ndoa, lakini muna anadai kuwa na
mimba...
BAADA YA WIKI MBILI KUPITA
Ni siku
nyingine tena, na ni mwezi toka kampuni ya MICCO kufunguliwa, hivyo wafanyakazi
wameshakula mishahara ya kwanza kwanza,... Siku hio mke na mume wakiwa
kazini,... Mje alitamani kutoka na mume wake wakatembee mjini, kwa sasa masharti
yameisha kwani tayari ule wakati umekwisha,...
"we nenda
tu"
Aliongea surian kana kwamba hataki kutoka hata nje yaani mazoea ya
masharti yamekuwa kweli,
"jamani baba Rashidi, twende tukale hata chipsi
jamani, kila siku uletewe humu, noo bwana twendeee"
"mama chidi, naomba
uende wewe tu"
"hapana,..."
"lakini nipo bize, ona oda zinavyo
miminika, naondokaje sasa"
"ok... Shadya?, Shadya"
"abee
boss"
Aliitwa sekretari Shadya kupewa ile laptop ya
boss...
"fuatilia hizo oda zote hakikisha zinatoka, sawa"
"sawa
boss, nitaifanya kazi hii"
"haya sasa upo bize tena"
"lakini mke
wangu,... Ile kazi yapaswa nifanye mimi"
"hapana, wewe ni boss now,
unahitaji kutuma tu, hebu twende bwana ukanitembeze kwenye mji
wenu"
Aliongea mwanamke huyo huku surian akikubali kishingo upande,...
Gari yao hua wanaipaki pembeni kidogo ya ofisi yao hivyo hata wakitoka hakuna
mfanyakazi ambaye atawaona,.. Basi surian aliingia na kupandisha kioo cha gari,
kwani tayari tabia ya kuto onekana na watu imeanza kumzoea, yaani hataki kuonwa
na watu kabisa... Kasahau kuwa kuna familia yake,...
MLINZI WA
GETI alifanya kazi yake kisha mke na mume wakatoka, lakini ile wanatoka tu na
asha nae ndio anaingia, yaani kiduchu kiduchu waonane, na asha hana tetesi
zozote kuhusu mdogo wake ndani ya kampuni hio,... Asha akiwa kashikilia vyeti
vyake kaja kuomba kazi kama alivyokuwa akilazimishwa na wazazi wake,... Asha
anafika ofisini boss hayupo,
"yaani boss katoka sasa hivi
tu"
Aliongea shadya huku akiwa bize na kazi ambayo
kapewa
"kwahio unanisaidieja dada angu"
"mmhhhh, hebu ngoja
nijaribu kumpigia simu"
Shadya alichukua simu ya mezani kisha akampigia
simu boss wake...
"umeona sasa, nimetoka sasa hivi tu, na simu
napigiwa, ndio mana staki kukaa mbali na ofisini"
Aliongea surian baada
ya kuona simu ya shadya
"Enhee sema kuna nini tena"
"aahhh
boss... Kuna msichana kaja kuomba kazi"
"documents zake
zimekamilika"
"mmmhh ndio, ziko sawa"
"ok mwambie sadiki
amsajili na aanze kazi kesho... Afu pia akampange mahali penye upungufu wa
wafanyakazi"
"ok sawa boss ahsante"
"ok"
Shadya alikata
simu kisha akampeleka asha kwa sadiki,... Sadiki ndio meneja mwajiri wa kampuni
hio, hivyo yeye ndio anajua kila kitu kuhusu wafanyakazi, na ni kijana mdogo
lika na surian,...
"boss,... Kuna mgeni hapa"
"ni nani na katoka
wapi"
"samahani boss,.. Kaleta barua ya maombi ya kazi"
"aaaoo
ok mwambie aingie"
Huku mjini surian akiwa na mke wake walipaki
gari mahali fulani, kisha wakaingia sehemu moja iliokwenda kwa jina la TANGA
SPECIAL BITES, waliingia hapo lakini surian alitaka kukaa ndani, japo kwa nje
kuna nafasi, yaani surian kwa sasa keshakua mtu wa kujificha ficha kwani
keshazoea yale masharti na kayatamani yaendelee vile vile...
"ndani kuna
joto mume wangu, tukae hapa nje"
Aliongea maimuna huku baadhi ya wanaume
wakitoa macho kwani muna ni mwanamke mrembo sana, wakijua ni mwanamke wa kawaida
tu
Surian alikubali kukaa pale nje lakini hajapenda kabisa kukaa hapo
nje, kakaa kwa niaba ya mke wake tu,... Basi waliagiza vyuku vipsi na vitu vingi
hususan vinywaji safi,... Midomo yao ilianza kuchangamka, lakini ghafla
ilisikika sauti ikisema
"jamani, ona ule sio mzimu wa surian
ule?"
Aliongea dada mmoja ambaye ni mpita njia eneo hilo,.. Lakini muna
aliisikia hio sauti peke yake....
"heeeeee afu mbona ni surian
kweli"
"wewe, sio surian, ule ni mzimu wa surian"
Walikuwa ni
rafiki zake na asha, kama unawakumbuka hawa ndio wale kimbelembele
waliomtangazia kuwa kamuua mdogo wake,.... Mara moja walipiga simu kwa
asha...
Wakati huo asha ndio anatoka kiwandani baada ya kuonyeshwa
kitengo ambacho kesho atakuja kufundishwa,...
"heeeeee we mnafiki
mzanditi, leo unanipigia simu ya nini"
Aliongea asha akiwa hata getini
hajatoka,
"asha Punguza jazba.... Wahi hapa Tanga Special Bites
ujioneee"
"nijionee nini, mlivyo nitangazia mimi nimemuua mdogo wangu,
mji mzima natengwa kwa ajili yenu..."
"sasa sikia, surian mdogo wako
tunamuona hapa anakula kuku kwa mrija,... Yaani ni tajiri, sasa sijui ni
mzimu"
"ati nini"
"mdogo wako.. Tunamuona
hapa"
"wapi"
"hapa Tanga Bites"
Lakini wakati huo huo
wakiongea, muna Aliweza kusikia kila neno kwani yeye anatumia hisia za asili ya
pili ambayo ni jini,....
"ok nisubiri hapo hapo nakuja"
"chukua
toyo jamani asha"
Wakati huo asha anatamani amtafute mama yake hapo
kazini ili ampe habari hizi, lakini mbaya zaidi hajui mama anafanyia kazi upande
gani hapo ndani,... Hivyo asha aliamua kuondoka lakini kazini keshasajiliwa
tayari,...
Punde sii punde TANGA SPECIAL BITES asha anafika,
kwa haraka haraka akawaona rafiki zake ambao ni fatuma, na amina...
"we
Fatuma, haya yuko wapi surian mdogo wangu"
Aliongea asha huku akiwa na
shauku ya kumuona ndugu yake, ingawaje mwanzoni alikuwa akimchukia kwakua
kapendelewa elimu.. Wakati huo surian na mke wake wanakula vyuku kwa kwenda
mbele na ila surian hajui kama kaonwa na rafiki zake asha...
"mdogo wako
yule pale"
Asha anatamani sana amuone mdogo
wake ambaye anashutumiwa kumuua kisa ni pesa,... Sasa ili jambo hilo liwe safi
katika maisha yake ni lazima surian aonekane,... Amina na Fatuma ni marafiki wa
asha ambao walikuwa karibu naye toka kufungua kwa saluni yake,... Lakini
walikuja kumwonea wivu baada ya asha kuanza kukusanya pesa nyingi, lakini wakati
akikusanya pesa nyingi kutokana na wateja,... Mdogo wake alipotea katika
mazingira ya kutatanisha,.. Hii leo rafiki zake wanamwita asha aje kumwona mdogo
wake....
"mdogo wako yule pale"
Aliongea fatuma huku
akinyoosha kidole, lakini ghafla hawakuwa wakiona mtu, hata wao wenyewe
walijikuta hawaoni mtu,...
"yuko wapi"
Aliuliza asha huku
akiangaza macho katika eneo husika
"walikuwa pale na mwanamke mmoja
mzuri sana"
"sasa wako wapi"
"walikua pale karibu na meza ile
pale"
Asha aliona rafiki hao walikuwa wakimzingua na kuendelea kumtania
au kumchokoza kutokana na kashfa alio nayo,...
Lakini surian na
maimuna, walikuwa pale pale wakiendelea kula kuku maeneo hayo, ila maimuna
kamshika surian sikio na ndio sababu hawaonekani, na surian anajua kashikwa
kikawaida tu kumbe hapo alipo haonekani,.... Asha aliondoka zake kwa hasira,
mana rafiki zake ndio wenye kumchezea akili,... Hata akina Fatuma na Amina
waliona ni kama maajabu, kwani sekunde chache waliwaona pale, sasa iweje
wasiwaone kwa mara nyingine,... Waliona kweli surian kauwawa kwani ni lazima ule
utakuwa ni mzimu wake
"amina, hii sio bure... Kweli surian sio
binadamu"
Aliongea fatuma huku wakiwa wanarudi majumbani
mwao,
"ni kweli, mana dakika ile ile walikwenda wapi"
"na
kwanini alivyokuja asha tu,.. Wakatoweka, ni kweli asha kamuua ndugu
yake"
Walizidi kuongea mengi sana, lakini hawajui
lolote
Baada ya wiki kadhaa kupita, siku zilizidi kwenda na
kiwanda kilizidi kuzalisha bidhaa na kuzisambaza mikoani, na ubora wa bidhaa
hizo kutoka MICCO, ilifanya hata wafanyabiashara wa nguo aina hizo wasiagize
kutoka dubai au maskati, ama oman,.. Hivyo wamiliki wa maduka ya nguo za
Kiislamu walihamia katika kiwanda cha nyumbani,... Kiwanda kulipwa kipaumbele
kwani kiliajiri Watanzania 500 na wote wanalipwa kwa mishahara mikubwa kutokana
na viwango vya elimu zao,....
Asha akiwa ndani ya kiwanda na ni
wiki kadhaa zimepita toka kuanza kazi hivyo sio mgeni tena katika kiwanda
hicho,... Mpaka sasa ni miezi miwili toka Kuanzishwa kwa kiwanda hicho lakini
boss mkuu hajulikani sura wala sauti, kwani alipewa masharti ya kuto onekana na
wafanyakazi, lakini licha ya siku hizo kuisha surian kawa mzoefu wa kuto onekana
na wafanyakazi, na hata hakumbuki umuhimu wa kwenda kuiona familia
yake,....
Wakiwa ndani ya idara yake na rafiki zake ambao
aliwakuta kabla yake,...
"nyie fanyeni kazi boss huyo"
Aliongea
asha huku wakiwa wameshika vitambaa wakiwa tayari kwa kuviweka mapambo kwa niaba
ya kutengeneza kanzu,...
"nani boss?"
Aliuliza rafiki yake mmoja
huku asha akijibu
"si huyo hapo anakuja"
"heeeeee nani kakwambia
huyo ni boss?.. Huyo ni Meneja anaitwa sadiki"
Siku zote za asha
alizokaa hapo alijua sadiki ndio mkurugenzi mkuu wa kampuni hio, kumbe huyo ni
Meneja,....
"sasa boss wa hii kampuni, ni nani"
Aliuliza asha
huku akitamani sana kumjua boss, mana anakumbuka mama yake alisema boss wao ni
mdogo mdogo, sasa asha akadhani labda ni sadiki, kumbe boss ni mtu wa familia
yao lakini hawajui na hata boss hajui kama familia yake ipo
humu,
"mmmhhh mwenzetu, hata sisi hatumjui, ni mwezi wa pili huu
tunalipwa lakini boss hatumjui"
Sasa sadiki alifika katika eneo husika
ambalo asha yupo,...
"asha?, nakuhitaji ofisini mara
moja"
Aliongea sadiki huku akiendelea kuzungukia baadhi ya idara kama
zinazalisha vyema, au wanapiga stori tu....
"afu mbona meneja
anapenda sana kumuita asha, au ndio wameanza nini mahusiano"
Aliongea
msichana mmoja baada ya kumwona asha anaitwa itwa kila siku na
Meneja
"kwani hukumbuki ndio aliokuja kumfundisha
mwenyewe"
"mmmhhh, haya watu na bahati zao"
Aliongea dada mmoja,
na wakati huo asha anaelekea ofisini,... Kaitwa na Meneja,... Mama akiwa
anafanya usafi alimwona mtoto wake akielekea ofisini,.. Mama huyo haruhusiwi
kujionyesha kwani kawekwa kwa kificho, ili apate
riziki
"asha,.. Mbona upo kimya toka juzi Nasubiri meseji
yako... Nimekununulia simu ili tuwasiliane"
Aliongea sadiki huku asha
akijing'ata vidole, kana kwamba watu hawa wana mpango wa kuwa na
mahusiano...
"lakini boss, mimi nitakujibu... Alafu sasa boss akijua una
mahusiano na mfanyakazi, itakuwaje"
"boss nani tena... Mimi ndio mwenye
kauli ya juu, na sitaki kujulikana mimi ndio boss mkuu kwasababu watu sio wazuri
hapa mkoani tanga... Najiita meneja ili nionekane wa kawaida
tu"
Aliongea sadiki kama vile kujipa nafasi ya uboss mana anampenda sana
asha, lakini sasa asha yeye anatamani uzuri wake autumie kwa boss mkuu, hio ndio
nia yake, mana maisha yalisha watupa mkono, na kama tunavyomjua asha mwanzoni
alikuwa ni msichana wa kudanga danga sana hivyo hata kuja hapa kwenye hii
kampuni shida yake apate mwanaume wa kumchuna,.... Sasa aliposikia kuwa boss wa
kampuni hii ni kijana mdogo akajua uzuri alio nao ataweza kumteka awe naye ili
maisha yaendelee,.. Sasa alipokutana na sadiki akajua huyo ndio boss mwenyewe,
kumbe sadiki ni Meneja na boss ni kaka yake kabisa baba mmoja mama mmoja, ila
hajui kama kaka yake ndio mmiliki wa hapa...
"mbona nilisikia kuna boss
mwingine"
"ndio, ni ili mimi nisijulikane"
"ok, lakini daki.. Mi
naomba vuta subra kidogo nitakujibu tu"
"asha, mtoto mzuri kama wewe,
yanini nikukose... Nataka mke, ona nina maisha mazuri lakini sina
mke"
"ni sawa diki, lakini nipe nafasi ya kufikiri, tatizo ninyi wanaume
hamuaminiki"
"sio wote asha,... Please naomba kesho unipe furaha ya moyo
wangu, kama ni mshahara mimi nitaupandisha mara dufu"
Aliongea sadiki na
kujigamba sana kuhusu nafasi yake....
"kweli diki"
"ndio, kwani
we watakaje... Sema lolote nifanye"
"usijali, ila kikubwa nataka mama
yangu ahamishwe kitengo kutoka kusafisha vyoo kuja kiwandani au hata awe mpishi
sio mbaya"
Aliongea asha akiwa na nia ya kumsaidia mama yake asiende na
kazi ya usafi wa vyoo kwa haipendi
"kumbe yule ni mama
yako"
"ndio"
"ok ni hilo tu?... Au una Lingine"
"ni hilo
tu, na mshahara wangu sio mbaya kama utapanda
kidogo"
"usijali"
"mimi shida yangu ni kukumiliki wewe na uwe
mke wangu, wala sitaki kukuchezea asha"
Asha ni msichana mzuri sana sema
aliutumia uzuri wake vibaya, na mpaka sasa bado ni kisu, na ndio maana meneja
kanasa mwenyewe
Wakati huo huo suria akiwa ofisini kwake, oda
zilikuwa zikiingia nyingi kwa njia ya simu ya secretary, kisha secretary
anamtumia boss wake kule ndani na boss anamtumia meneja masoko ili afanye kazi
na watu hao, asha anatoka ofisini kwa sadiki, akiwa haamini kama anapendwa na
boss, na hapo anapopita ndipo mlango wa boss mkuu ulipo, na ni ndugu yake
kabisaaaa, ila hajui
Ilipofika jioni mida ya saa 12 na nusu,
suria akiwa ndio wa mwisho kabisa kutoka,... Na ni ili asionekane na watu, sasa
haijulikani ni kwanini mana siku za masharti ya jini maimuna zilisha isha,
lakini suria bado haihitaji kuonwa na watu kana kwamba kesha zoea kujificha
ficha...
Sasa huku nyumbani kwa akina asha, akiwa na mama yake
jikoni wanapika, kwa sasa maisha yao sio mabaya mana mama keshapokea mshahara
wake wa kwanza wa laki nne, sasa hawana ziki za hapa na pale... Wakati huo baba
yao akiwa msikitini wao wapo jikoni wanaongea, kama unavyojua mama na mtoto wa
kike walivyo...
"wewe asha,.. Mchana ule niliogopa kukuona na Meneja
unakwenda ofisini, nikajua unafukuzwa kazi"
Aliongea mama yake asha huku
asha akitabasamu tu,...
"mama, ina maana kila nikienda ofisini nakwenda
kufukuzwa"
"ndio, mana juzi tu kuna wasichana wawili walifukuzwa kwa
kuvaa nguo fupi, nikajua na wewe pia"
"hapana mama... Afu mama yule sio
meneja ni boss mwenyewe"
"weeeeeeeeee, usikute kakupenda ndio mana
kakudanganya... Yule ni meneja pwiiiii, hata siku nakwenda kuomba kazi,
nilimuona kwenye foleni na vyeti vyake"
"haaaaaaaaa mama unasema
kweli"
"ndio, yule ni Meneja.... Kwani kuna nini"
"basi mi
nikajua ni boss"
"we asha, hebu niambie ukweli mwanangu, nini
kinaendelea wewe na Meneja sadiki"
"mmmhhh mama bwana tuyaache
hayo"
"najuaaaa,... Najua keshakupenda yule"
"ni kweli mama, ila
mi namtaka boss mwenyewe..."
"asha mwanangu, umefuta kazi fanya kazi....
Ina mana unataka kurudia ujinga wako wa zamani"
"mama... Ina maana mimi
nikiwa na mahusiano na boss mkuu ni vibaya"
Aliongea asha huku mama
akiangalia chini kama anawaza na kumjibu kuwa
"sio vibaya mwanangu,
lakini kumpata boss mkuu sio mchezo mchezo, ni sawa na kwenda kumuona raisi uso
kwa uso"
"sasa nifanyeje mama.... Ina mana uzuri wangu ipotee bure
tuuu"
"asha... Kama sadiki ana nia nzuri, mlete atujue wazazi wako...
Achana na huyo boss mkubwa mwanangu, na pia boss mkubwa naskia ana
mke"
"mke?? We ai umesema ni mdogo"
"ndio, ila ana
mke"
"ila mama kwani si muislamu, nitakubali niwe hata mke wa pili...
Nataka tukiwa kwenye mahusiano, atujengee nyumba"
Aliongea asha bila
kujua boss huyo huyo ni mdogo wake kabisa tumbo moja, lakini kwakua hajawahi
kumuona, sio rahisi kujua....
"ni kweli, lakini hata sadiki
anaweza"
"sitaki bwana..."
"tatizo lako mwanangu unapenda pesa
za haraka jamani... Hebu ngoja nitajaribu kupeleleza ili hata nipate namba ya
huyo boss mkubwa"
Aliongea mama huyo bila kujua boss huyo ni mtoto wake,
yaani anataka kumpigania mtoto wake wa kike aolewe na boss ambaye ni mtoto wake
wa kiume, ila hawajui wote na hata surian hajui kama familia yake ipo hapo
ndani...
Tukija huku kwa akina surian na mke wake, wakiwa
jikoni wote wanapika..
"mke wangu, nataka nikuletee mfanyakazi wa
ndani"
Aliongea surian huku mke akianza kununa, mana naye ana
wivu
"kwa kazi gani sasa ulete mfanyakazi, kwani ni lini ukakuta nadeki
humu ndani... Mana nyumba inajideki wenyewe kila siku... Inajifuta vumbi
yenyewe, nguo zinajifua zenyewe, sasa mfanyakazi wa nini"
Aliongea mke
huyo mana ikumbukwe maimuna ni jini, ila ni jini mwenye asili
mbili,
"mimi sipendi uwe unatumia nguvu zako za kijini kufanya usafi, na
hii asili siitaki, nataka uwe wa kawaida tu"
"ni sawa mume wangu, ila
mimi ni jini na nitabaki kuwa hivyo.... Kwanza mtoto wako ananipiga
mateke"
Aliongea maimati kana kwamba mtoto alioko
tumboni
"mmmhjh wa juzi tu"
"hapana... Kwenye asili yetu ya
majini hua hatukai miezi tisa kama binadamu wa kawaida... Tunakaa miezi minne na
nusu... Na shetani anakaa miezi miwili na nusu"
"heeeeee... Kwahio
keshokutwa tu nina mtoto"
"sanaaaaa"
"waooooooo.... Nakupenda
jamani mke wangu"
"nakupenda pia baba watoto wangu"
Suria
alinogewa na penzi la jini huyo na kufumbwa macho asione
popote
Kesho yake ikiwa ni siku nyingine tena, asha akiwa ndani
ya kiwanda lakini alionekana kukasirika sana kwasababu mwanaume aliojipendekeza
sio yule aliomtaka yeye,... Asha Alishika simu yake ambayo kanunuliwa na sadiki,
kwani asha hakuwa na simu baada ya kuiuza,...
"hallo diki
mambo"
"poa mzima asha jamani"
"mzima... Nipo kiwandani, nataka
tutoke kidogo nikakujibu ombi lako"
"sawa mama... Toka nikukute nje ya
geti hapo kuna hoteli moja nzuri sana nakuja"
"ok sawa, uwahi mana
nataka nirudi kazini"
"usijali asha wangu"
Sadiki aliongea hayo
kana kwamba kweli kampenda sana asha, lakini asha alikuwa hamtaki sadiki kwani
hakuwa boss alio mkusudia,... Asha alitoa laini zake kwenye simu ili akampe simu
yake huko nje...
Huku ofisini sadiki anafurahi kwani anajua
anakwenda kupewa utamu wa mwili, ikiwa ni mpenzi mpya kwake, kumbe anakwenda
kupewa simu yake.... Sadiki alitoka nje ya kampuni akiwa kama meneja, hivyo
hakukua na wa kumuuliza, asha alisha toka nje ya geti kwa kisingizio cha kwenda
kununua dawa kwani hajiskii vizuri kiafya.... Walikutana nje kisha sadiki
akachukua taxi, kwani angelitoka na gari yake labda angeulizwa anakwenda wapi
kwani ilikuwa ni majira ya saa tisa alasiri,
Sasa huku kwa
surian kashika simu yake ya mezani na kumpigia shadya au Cecilia aliopo
mapokezi....
"hallo boss"
"shadya"
"abee
boss"
"mwambie sadiki akakague products kabla muda wa kazi
haujaisha"
"aaahh sorry boss, sadiki katoka kidogo nadhani kafuatilia
oda"
"ok basi, nitakwenda mwenyewe"
Aliongea surian kisha
akakata simu,.. Sasa shadya kaka akijiuliza anakwenda mwenyewe yeye au nani,
mana toka kampuni kuanza surian hajawahi kwenda kukagua kiwanda wala kuangalia
wafanyakazi wake,... Sasa kwa mara ya kwanza surian anatoka kwenye upande wa
kiwanda ambako kuna wafanyakazi takribani 500, na wote hao hawamjui
boss....
Shadya alishangaa kweli boss anatoka kwenda
kiwandani,... Shadya haamini macho yake, yaani ni kama ndoto, afu mbaya zaidi
ile ile idara ambayo asha alikuwepo ndio surian anaingia kuanza ukaguzi wake,
kana kwamba kama asha angelikuwepo, basi angemuona ndugu yake, lakini
hakuwepo... Wasimamizi walikuwa kipaumbele kumwelekeza boss, kwani shadya
alitangulia kuja kutoa taarifa kuwa boss anafika hivi punde,.. Sasa wafanyakazi
kila mmoja anasema yakwake...
"kumbe ni katoto tu... Mi nikajua
kuubwa"
Mmoja kati ya wasichana aliongea hivyo...
"ila ni hensam
jamani,.. Hivi ana mke kweli"
"heeee mwenzangu mi najuaje kama ana mke
au hana"
"waaoooo kazuri kweli.... Asha yuko wapi si alikuwa anataka
kumjua boss mwenyewe"
"asha atakuwa kaenda uwani"
Wafanyakazi wa
kike walikuwa wakimuwazia sana boss surian... Sasa katika pitapita yake kwenye
ukaguzi, akakuta sehemu moja ni chafu...
"hapa vipi hapa... Mbona idara
hii sio safi"
Aliongea hivyo huku wafanyakazi na wasimamizi wakitetemeka
mno
"hapa palimwagika maji boss"
"nani kaingia na maji... Na
toka wakati wote kwanini msipakaushe"
"samahani boss..... Nyie, hebu
chukueni dekio kausheni hapo"
huyo ni msimamizi mwenye kutoa sauti
hio..
"sjapenda kabisa... Mabwana usafi wakija hapa ni tatizo kubwa
sana... Hivi kama kiwandani ni hivi, je huko chooni
kutakuaje..."
"hapana boss, chooni ni kusafi kila wakati
boss"
"hapana.... Lazima nikakague usafi wa vyoo, mana mtafanya kampuni
ipigwe faini au kufungiwa kwasababu ya uchafu"
Aliongea surian huku
akielekea chooni, na vyoo hivyo vinafanyiwa usafi na mama yake mzazi, na hajui
kuwa mama yake naye anafanya kazi kwenye kampuni yake, na hata mama naye hajui
kama mwanaye ndio mmiliki wa kampuni
hio,...
Hakuna kitu kinauma kama kumkuta mama
yako anafanya kazi za ajabu ingali una uwezo wa kuwapumzisha nyumbani, yaani
wawe wanakula matunda yako tu,... Lakini kwa upande wa surian alitamani sana
kuwasaidia wazazi wake lakini kutokana na masharti ya jini maimuna, anatakiwa
awasaidie kwa njia ya ajira, yaani awaajiri, kitu ambacho surian alikataa
kabisa, hawezi kuwatumikisha wazazi wake kisa pesa,... Lakini bila kujua hali za
wazazi wake, zilikua mbaya na waliona matangazo na kuja kuomba kazi,... Lakini
surian hajui kama mzazi wake mmoja yupo hapa kazini pamoja na dada yake... Na
mbaya zaidi mzazi kapangiwa sekta moja mbaya sana, yaani mama wa tajiri akafanye
kazi chooni??? Haiwezekani
Wasimamizi mbalimbali na viongozi
wakiwa wanamuongoza kwenda katika vyoo hivyo ili kuhakikisha usafi unakuwa
mzuri,.. Sasa shadya alishangaa kumuona boss anaelekea kule chooni,... Na mfanya
usafi wa kule chooni amewekwa kwa siri kwasababu umri wake hauruhusu kufanyakazi
kwenye kampuni hiyo,. Shadya haraka haraka alimpigia mama yake surian
simu....
"samahani, namba ya mteja unayempigia haipatikani, tafadhali
jaribu tena baadaye"
Ilikuwa ni sauti ya vodacom ikimjulisha shadya kuwa
namba ya mteja haipatikani,.. Sasa shadya kichwa kinapata moto kwani yeye ndie
alie fanya ujanja mpaka mama huyo akapata kazi, na umri wa mama huyo hauruhusu
kabisa.... Shadya alijaribu na kujaribu, lakini wapi simu haipatikani,....
Surian anafika katika eneo la vyoo, wapambe wakaanza kuongea...
"boss??
Angalia vyoo ni visafi kila wakati"
Aliongea kiongozi mmoja ambaye ni
kama mpambe tu... Na kweli palikuwa pasafi kabisa,... Sasa mama huyo alikuwa
anafanya usafi ndani ya choo, hivyo hana taarifa kuwa boss mkuu yupo nje ya vyoo
bavyo anavifanyia usafi kila wakati,.. Sasa boss karidhika kuona usafi ambao
unafanyika hapo chooni,. Na karidhika nao kwa asilimia zote,... Bila kujua anaye
fanya usafi ni mama yake mzazi,.. Aiseee surian anageuka na kuondoka, na mama
naye anatoka chooni baada ya kumaliza kufanya usafi,... Mama alishangaa tu kuona
kundi la watu wakimalizikia kuondoka, lakini hakujua kama boss wake alikuwepo
hapo,... Yaani ilikuwa kiduchu tu aonwe na boss.... Sasa surian hakuwa na haja
tena ya kutembelea idarani, alirudi zake ofisini,... Wakati huo shadya
anatetemeka kwani anajua tayari kimebumburuka huko chooni,... Alishangaa boss
kaingia ofisini kwake bila tabu na mtu.... Shadya alihema kwa nguvu kuashiria
labda hakuna kitu,... Lakini hakuamini alitoka kwenda mpaka chooni
kuhakikisha...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment